Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

MWENYEKITI WA CCM DKT MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU JIJINI DAR ES SALAA LEO

$
0
0
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Kamati Kuu (CC) ya CCM kilichokutana jijini Dar es salaam leo Desemba 17, 2018.PICHA NA IKULU

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI ZANAKI WATEMBELEA HIFADHI ASILI YA MAGAMBA LUSHOTO, TANGA

$
0
0
Afisa Utalii wa Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba iliyopo Lushoto, Tanga Samiji Mlemba (katikati) akitoa maelezo kwa wanafunzi wa Sekondari ya Zanaki jijini Dar es Salaam waliopata ufadhili wa kutembelea hifadhi hiyo waliopewa na Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kupitia mradi wa Uwezo Award uliendeshwa na Shirika lisilo la kiserikali la Great Hope Foundation. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG - Lushoto.
Afisa Utalii wa Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba iliyopo Lushoto, Tanga Samiji Mlemba akiwa ameongozana na kuwapa maelezo wanafunzi na wanahabari waliokuwa katika ziara hiyo.
Moja ya bango linalowakaribisha wageni katika hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba iliyopo Lushoto, Tanga na kuwapa maelezo machache.
Wanafunzi wakiendelea na safari ambayo iliwachukua saa 3 kufika katika kilele kwa km 2.2.
Wanafunzi wakifurahia katika kituo cha kwanza ambacho kilikuwa ni Chanzo cha Maji.
Pichani ni wanahabari wa vyombo mbali mbali Msungu wa ITV (kwanza kulia) na Said Makala (wa pili toka kulia) wakifurahia pamoja na maofisa wa GHF Noela na Maria wa TTB... Juu ni Mwanahabari Cathbert Kajuna -Kajunason/MMG akiwa na wanafunzi wakifurahia katika kituo cha pili ambacho ni Mshai.
Afisa Utalii wa Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba iliyopo Lushoto, Tanga Samiji Mlemba akitoa maelezo machache wakati wanafunzi hao walipofika kituo cha Mshai wakielekea katika kilele cha mlima Kigulu Hakwewa.
Safari ya kuelekea katika kilele cha mlima wa Kigulu Hakwewa.
Safari ilikuwa ni ndefu ambapo wengine waliamua kupumzika ili kuweza kuvuta pumzi katika miti yenye umri wa miaka 40.
Muonekano wa miti mikubwa yenye kuvutia iliyoishi umri wa miaka 40 mpaka sasa.
Kila mmoja alikuwa na furaha kufika katika kituo cha tatu cha Kwesimu ambapo historia ya sehemu hiyo ilikuwa ni kupatikana kwa huduma za simu. Hapo ndipo mawasiliano ya simu yakipatikana yani namaanisha kila mtu mwenye simu alikuwa akifika hapo ili aweze kupata nawasiliamo (Network ilikuwa ikipatikana eneo hilo).
Eneo hilo la Kwesimu ndipo mkondo wa maji ulikuwa ukipita.
Wanafunzi wakifurahia katika mlango wa pango la Wajerumani walilolitumia katika vita vya kwanza vya dunia vilivyotokea mwaka 1914 - 1918.
Wanafunzi wakifurahia na mwalimu wao walieambatana nae katika mlango wa pango la Wajerumani walilolitumia katika vita vya kwanza vya dunia vilivyotokea mwaka 1914 - 1918.
Meneja Uhusiano wa Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) nae aliweza kupata wasaa katika lango la pango la Wajerumani lililotumika katika Vita vya kwanza vya Dunia 1914-1918.
Ndani ya pango la Wajerumani walilolitumia katika vita vya kwanza vya dunia vilivyotokea mwaka 1914 - 1918.
Wanafunzi wakifurahia na Afisa Utalii, Samiji Mlemba (katikati) wakiwa kwenye geti la kuingia kilele cha mlima Kigulu Hakwewa.
 Kilele cha Mlima Kigulu Hakwewa ambapo ni (1840 A.M.S.L) Usawa wa Juu wa Kiwango cha Bahari.
Kila mmoja akifurahia...
Makulaji kidogo!
Kila mmoja akiwa na uso wa furaha baada ya kutoka kilele cha Mlima Mgulu Hakwewa.
Baada ya wanafunzi kutembelea kilele cha mlima Kigulu Hakwewa waliweza kufika katika Msitu wa Asili wa Mkusu unaolimilikiwa na Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) ili kujionea maporomoko ya maji ya Mvueni.
Wanafunzi wakifurahia katika maporomoko ya maji ya Mvueni yaliyopo katika Msitu wa Asili wa Mkusu uliopo Lushoto, Tanga.
Maporomoko ya maji ya Mvueni yaliyopo katika Msitu wa Asili wa Mkusu uliopo Lushoto, Tanga.
Wanafunzi wakifurahia katika Maporomoko ya maji ya Mvueni. 

 Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba iliyopo Lushoto, Tanga ni moja ya vivutio vya hifadhi 12 za mazingira asilia vinavyosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS). Watu wengi wamekuwa wakisahau kuwa utalii wa ikolojia nao unafaida kwa jamii yetu ili iweze kujifunza mambo mbali mbali kuhusu misitu na viumbe hai. 

Wakizungumza kwa wakati tofauti mara baada ya kutembelea hifadhi ya mazingira ya Magamba, Mfaume Salehe Msasa amesema “Kuwa Coordinator wa ni bahati kwangu na furaha pia kwa kuwa nimejifunza vitu vingi sana tangia nimeaza kuvolunteer @greathopetz pia naendelea kujifunza kwamaana kuwa kujifunza hakunaga mwisho," Kwa kwaida kila mwaka @greathopetz hua tunatoa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi pamoja na shule zinazofanya miradi bora zaidi. Mwaka huu tulikua na shule 100 ambazo zimefanya mradi na shule ambayo imefanya mradi bora zaidi nakuweza kuwa mshindi wa kwanza ni Shule ya Sekondari Zanaki.

 “Miradi ya mwaka huu imekua ni ya tofauti kubwa kwa mshindi wa mradi wa Uwezo Award kupata zawadi nyingi na wamepewa safari ya kitalii ya kwenda msitu wa Magamba kwa kudhaminiwa na Wakala wa huduma za misitu Tanzania na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Nae Meneja wa Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) ameshukuru jinsi wanafunzi walikuwa na moyo wa kujifunza kuhusu mazingira na kuomba shule pamoja na wazazi waweze kujitokeza kuwapeleka watoto wao katika vivutio mbali mbali vya utalii wa ikolojia ambao watu wengi wamekuwa wakiusahau.

 "Unajua watu wengi wamekuwa wakikimbiali kuangalia wanyama ila huku napo ni zaidi ya kule maana wale wanaopenda kuona mazingira yanavyotunzwa basi hawana budi kufika bila kukosa, tunawakaribisha watanzania wote hasa kipindi hiki cha likizo kwa wawalete watoto wao wajionee vivutio mbali mbali mbali," amesema Tulizo Kilaga Great Hope Foundation - GHF ni shirika lisilo la kiserikali lililojikita katika kuwasaidia vijana kutambua na Kuendelea uwezo wao katika maeneo mbalimbali. Shirika hubuni na kuendesha miradi katika muktaadha wa kuwajengea uwezo Vijana.

WAZIRI PROFESA MAKAME MBARAWA AKAGUA MRADI WA MAJI KIMARA BONYOKWA

$
0
0








Waziri wa Maji Mh. Profesa makame Mbarawa akishiriki kuchimba mtaro wa kupitisha mabomba wakati alipokagua maeneo ya mradi wa maji Kimara Bonyokwa Manispaa ya Ubungo jijini Dar es salaam leo.
Baadhi ya mabomba yanayotumika katika mradi huo.
Waziri wa Maji Mh. Profesa makame Mbarawa akikagua maeneo mbalimbali katika mradi wa maji unaoendelea Kimara Bonyokwa.
Waziri wa Maji Mh. Profesa makame Mbarawa akiangalia mabomba hayo.
Moja ya matenki ya kuhifadhia maji yaliyojengwa katika mradi huo.



Na Stahmil Mohamed

Dawasa wametakiwa kufanya kazi kwa weledi na uaminifu ili kufanikisha malengo ya miradi kama ilivyopangwa na serikali ili kufanikisha malengo iliyojipangia.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maji Proffesa Makame Mbarawa alipokuwa katika ziara yake ya kukagua maeneo mbalimbali yanayojengwa miradi ya maji iliyoanzishwa ikiwemo Kimara Bonyokwa,Kinzudi ,Salasala na Saranga ambako amebaini chamgamoto mbalimbali zinazosababishwa na wafanyakazi wenyewe wa Dawasa ikiwemo kuchelewesha kufungia wateja mabomba,kuandikisha wateja hewa pamoja na,kuwalipisha gharama zisizostahili

Hata hivyo Prof Mbarawa amemtaka Meneja mradi Mhandisi Ramadhani Mtindasi kushughulikia dosari zilizojitokeza kwa muda wa siku tatu na ikiwa hajatekeleza maagizo yake atawasimamisha kazi kutokana na uzembe wa kuwacheleweshea wananchi huduma.

Pia Professa Mbarawa amewataka wananchi kutoa taarifa mara moja iwapo watatakiwa kulipa gharama kwani huduma ya ufungaji mabomba ni bure .Professa Mbarawa ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa wahandisi katika maeneo yote yanayochimbwa mitaro kwa ajiri ya kupitisha mabomba kutowawekea vikwazo ili mradi ukamilike kwa wakati.

Kwa upande wake Meneja Mradi Mhandisi Ramadhani Mtindasi ameahidi kuzifanyia kazi dosari zote zilizobainishwa haraka iwezekanavyo pia amewataka wananchi kutolipia gharama yeyote ile kwani huduma ya uwekaji maji majumbani hutolewa kwa mkopo .

Wakizungungumzia ujio wa Mradi huo wakazi mbalimbali wa kata ya Wazo Hill Kinzudi wamesema wanafurahia ujio wa maji katika kata yao kwani wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu nr wamekuwa wakichota maji maeneo ya mbali pia gharama kwa ndoo moja ilikuwa ni shilingi 400 Pia wamemtaka waziri kuboresha mradi kwa kuwasimamia watendaji hao ili usije kukwama.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE DESEMBA 18,2018

JHIKOMAN, CHUO CHA TaSUBa WAZINDUA RASMI ALBAM YA SAFARI YA GITAA BARIDI

$
0
0

Msanii Jhikoman wa Afrikabisa akishirikiana na Wanafunzi wa TaSUBa wakiimba baadhi ya nyimbo zilizopo kwenye albam ndogo ya Safari ya Gitaa Baridi iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa TaSUBa na Afrikabisa wakati wa uzinduzi huo Usiku wa Ijumaa ya 14 Desemba 2018.

……………………

Na Andrew Chale, BAGAMOYO

MWANAMUZIKI nguli wa miondoko ya Afro reggae, Jhikolabwino Manyika maarufu Jhikoman kwa kushirikiana na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Ijumaa ya 14 Desemba, 2018, amezindua rasmi albam yenye nyimbo sita tukio lililofanyika mjini Bagamoyo,Mkoani Pwani.

Jhikoman ambaye anatoka kwenye lebo ya AfriKabisa ameweza kuonesha ukongwe katika muziki huo kwa kufanya kazi pamoja na vijana wadogo ambao ni wanafunzi wa Chuo cha Sanaa TaSUBa na kukonga nyoyo mashabiki waliojitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi huo.

Albam hiyo ina beba nyimbo kama: Mara ya kwanza, Ndotoni, Safari, Bad mind,Time to love na Kuagana zilizo kwenye mtindo wa regge.

Katika uzinduzi huo, Msanii Vitalisi Maembe na wengine wakiwemo Sinaubi Zawose, Voice of Revolution, K’Gwana Shija pamoja na Bocka T waliwez kupamba jukwaa katika kusindikiza uzinduzi huo kwa kuimba nyimbo zao mbalimbali.

Jhikoman ameshukuru uongozi wa TaSUBa kwa ushirikiano wa kutayarisha albam na kuirekodi kupitia studio ya chuo hicho.

“Wasanii waliopiga vyombo na kuimba na mimi hapa jukwaani ndio nilioshirikiana nao katika albam hii ni wa TaSUBa. Nashukuru kwa Uongozi kuwapa fursa ya kufanya kazi hii. Lakini pia nawashukuru Watanzania kuendelea kutuunga mkoni katika kazi zetu na kwa sasa albam itakuwa inapatikana pale Afrikakabisa hapa Bagamoyo na maeneo mengine tutaendelea kuwatangazia” alieleza Jhikoman.

Na kuongeza albam hiyo imebeba ujumbe mbalimbali hivyo itakuwa inaburudisha na pia kufundisha Jamii.

“Hii ni hatua moja. Kwa sasa nimeanza na vijana hawa wanafunzi wa chuo cha Sanaa Bagamoyo. Muziki una ishi hivyo tunawarithisha vijana ili uendelee miaka na miaka kwa muda mrefu muziki wetu” alieleza Jhikoman.

Aidha, Jhikoman amesema kwa sasa anatarajia kufanya ziara maalum kwa vyombo vya habari kwa lengo la kutangaza albam sambamba na kufanya shoo fupi katika vyuo na nyumba za tamaduni.

“Nimezindua albam ya safari ya gitaa baridi, lakini pia nimezindua na documentary yake ambayo yenyewe itaoneshwa sehemu mbalimbali ikiwemo kwenye tamasha la Kimataifa la filamu za nchi za majahazi (ZIFF 2019), Kwenye tamasha la Sauti za Busara, (Busara Extra 2019).

Lakini pia nitafanya shoo fupi ya kuitangaza albam katika nyumba za tamaduni: Alliance francaise de dar es salaam na Goethe-Institut Tanzania zote za Dar es Salaam pamoja na Vyuo vikuu vikiwemo UDSM, Mkwawa na vingine vingi” alimalizia Jhikoman.

Safari ya Gitaa baridi ni Extended playlist (EP) ikiwa na maana albam yenye ujazo mdogo. Nyimbo zote sita ameandika mwenyewe huku lakini pia katika uimbaji ameimba mwenyewe kwa kushirikiana na wanafunzi hao wa TaSUBa.

Katika uzinduzi huo mashabiki walifurika kwa wingi katika ukumbi wa TaSUBa ambapo muda wote wakati wa mwanamuziki huyo akiwa jukwaani walilipuka kwa shangwe za mara kwa mara.

Nae Mtendaji Mkuu wa TaSUBa, Dkt. Herbert Makoye alieleza kuwa, Taasisi iliamua kushirikiana na Jhikoman kwa kuwa ni msanii mkubwa anayefanya kazi vizuri na kwa maadili, hivyo anaamini kwa kushirikiana naye wanafunzi wa TaSUBa watajifunza vitu vingi kutoka kwake ambavyo vitakuja kuwasaidia baada ya kuhitimu na kuanza shughuli zao za muziki hapo baadae.

Katika historia ya muziki, Jhikoman mbaye ni msanii maarufu wa muziki wa regge nchini, ndiye msanii wa kwanza kufanya wimbo na mwanamuziki Peetah Morgan wa kundi la Morgan heritage la nchini Marekani mnamo mwaka 2015, Morgan hertage ni nyota wa muziki wa raggie wanaoishi Marekani lakini asili yao ni Jamaica.

Wimbo wa Africa arise ndio uliowaunganisha jhikoman na Peetah mogan, wimbo uliofanya vizuri katika anga za muziki duniani,kwa hiyo Jhikoman anaandika historia ya kuwa mwanamuziki wa kwanza Tanzania kushirikiana na mwanamuziki huyo wa Marekani, ambapo miaka miwili baadaye naye Diamond platnumz alifuata nyayo za Jhikoman kwa kushirikisha Morgan hertage kwenye wimbo wake wa Hallelujah.

NEWS ALERT: NDEGE MPYA AIRBUS A220-300 IKIWA TAYARI KULETWA TANZANIA KUTOKA CANADA

$
0
0
 Ndege mpya aina ya Airbus A220-300 ikiwa kwenye matayarisho ya mwisho mwisho kabla ya kuanza safari kutoka Montreal, Canada, kuja Tanzania tayari kuanza  kazi ikiwa imebatizwa jina la Ngorongoro
 Ndege mpya aina ya Airbus A220-300 ikiwa kwenye matayarisho ya mwisho mwisho kabla ya kuanza safari kutoka Montreal, Canada, kuja Tanzania tayari kuanza  kazi
 Mmoja wa wajumbe wa Tanzania akipata maelezo ya Ndege mpya aina ya Airbus A220-300 ikiwa kwenye matayarisho ya mwisho mwisho kabla ya kuanza safari kutoka Montreal, Canada, kuja Tanzania tayari kuanza  kazi
 Ujumbe wa Tanzania ukiwa na Ndege mpya aina ya Airbus A220-300 ikiwa kwenye matayarisho ya mwisho mwisho kabla ya kuanza safari kutoka Montreal, Canada, kuja Tanzania tayari kuanza  kazi
Ndege mpya aina ya Airbus A220-300 ikiwa kwenye matayarisho ya mwisho mwisho kabla ya kuanza safari kutoka Montreal, Canada, kuja Tanzania tayari kuanza  kazi

TAEC YAFUNGA VITUO 69 VYA AFYA TANZANIA BARA

$
0
0
Na Vero Ignatus, Arusha 


Tume ya nguvu za Atomic Tanzania (TAEC) imefungia vituo 69 vya afya Tanzania bara kwa kutotimiza vigezo vya kuendesha vituo hivyo

Hayo yameelezwa na kaimu mkurugenzi wa tume ya nguvu za atomic Tanzania Dkt. Wilbard Muhogorawakati akifungua mafunzo hayo ya kitaifa ya kinga ya mionzi kwenye uchunguzi wa magojwa kwa madaktari kutoka Tanzania bara ambayo yamefanyika jijini Arusha 

Amesema sheria ya nguvu za atomic inatoa vipengele ambavyo vinataka mafunzo kwa wafanyakazi wote waliopo kwenye sehemu ya mionzi yaweze kufanyika kwa kuwa kinga ya mionzi itatolewa kwa watu wrote."Mpaka sasa tumefungia vituo 69 kwa kutokuwa na leseni na mafunzo kwa wafanyakazi wanaotumia vipimo vya diology, na kutokuwa na ubora wa maamshine na majengo hiyo ndo sababu iliyofanya tukafungia vituo hivyo" alisema Dkt. Wilbard

Amewataka waajiri kuwapeleka wafanyakazi wao kwenye mafunzo ya kinga ya mionzi ili kuweza kupata elimu na hiyo imewekwa kila baada ya miezi mitatu kwa kila mkoa.Kwa upande wake Bakari Msongamwanja kutoka taasisi ya mifipa na mishipa ya fahamu Moi amesema umuhimu wa mafunzo hayo yatawasaidia kujua umuhimu wa kumlinda mgonjwa na waliowazunguka na kupitia elimu hiyo watawalinda wagonjwa

Aidha amesema kupitia mafunzo hayo ataenda kuisaidia jamii hasa katika kutoa elimu kwa jamii na kupunguza changamoto zinazotokana na madhara ya mionzi.Kelvini James ni mmoja wa mshiriki ambaye ametokea hospital ya Ikonda amesema umuhimu wa mafunzo hayo yatasaidia kuwalinda wao kujikinga na madhara ya mionzi ambapo changamoto ambayo imekuwepo ni wagonjwa wanaokwenda hospitali kutokujua namna ya kujikinga na mionzi

Hata hivyo amewataka waajiri kutimiza wajibu hasa kwa wafanyakazi kuwa na elimu ya kinga ya mionzi ambayo imekuwa ni changamoto kubwa kwa baadhi ya vituo vya afya hapa nchini.Hata hivyo mafunzo hayo ni kwa ajili ya vituo vya afya na yataendelea kufanyia na watu wa migodini na viwandani pamoja na kufanya ukaguzi maeneo mbalimali hapa nchini.

WAZIRI MKUU AZUNGUMZIA UONGOZI WA SHEIKH MKUU ALIVYOZIMA MIGOGORO KATIKA MISIKITI, AGUSIA MCHANGO WAO

$
0
0
Na Said Mwishehe ,Globu ya jamii

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amempongeza Mufti wa Tanzania kwa namna ambavyo uongozi wake umemaliza migogoro ambayo ilikuwa inaibuka kwenye misikiti mbalimbali nchini na kwamba kwa sasa Waislamu ni wamoja.

Pia Waziri Mkuu Majaliwa ametumia nafasi hiyo kuzungumzia hali ya amani nchini ambayo msingi wake unatokana na viongozi wa dini zote ambao wamekuwa wakihimiza umoja na mshikamano.

Majaliwa amesema hayo jana mbele ya Rais Dk.John Magufuli aliyekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za BAKWATA kufikisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake Desemba 17 mwaka 1968 ambapo amesema dini zote zimekuwa mstari wa mbele katika kushiriki katika maendeleo nchini.

Ametumia nafasi hiyo kuelezea namna ambavyo Mufti wa Tanzania ambavyo chini ya uongozi wake ambavyo amesaidia kuwafanya Waislamu nchini kuwa wamoja na kushiriki kwenye maendeleo ya nchi yao.

"Leo hii tunashudia chini ya Mufti wa Tanzania,hatusikii migogoro ambayo tulikuwa tunaisikia siku za nyuma.Kumetulia na mambo yanakwenda vizuri.Hongera Mufti Sheikh Aboubakary Zubeiry kwa uongozi wako mahiri.Tangu uwe kwenye nafasi hiyo sasa ni mwaka wa tatu,umetuunganisha ," amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Wakati huo huo amezungumzi mchango wa viongozi wa dini zote pamoja na waumini wa dini hizo kwa namna ambavyo wamekuwa wakishiriki katika kuleta maendeleo ya nchi yao na kuunga mkono juhudi za Rais Dk.John Magufuli katika kuleta maendeleo.

Amesema" Mchango wa viongozi wa dini zote wamekuwa mstari wa mbele katika kushiriki kwenye maendeleo ya nchi yetu, kupitia taasisi zao mbalimbali wamekuwa wakisaidia sekta ya afya, maji na utoaji wa huduma nyingine za kijamii.Kabla ya Waziri Mkuu kuzungumza Mufti wa Tanzania Sheikj Zubeiry alieleza namna ambavyo sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi wa ngazi mbalimbali BAKWATA ambao wamefika hapo.

Pia amesema Mufti Zubeiry amesema BAKWATA limefurahishwa na uamuzi wa Rais Dk.John Magufuli kukubali wito wao wa kuhudhuria sherehe za baraza hilo kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.

Amesisitiza kwamba viongozi wote wa BAKWATA nchini zima wako kwenye sherehe hizo za kutimiza miaka 50, pamoja na viongozi wengine wa taasisi ya dini,mabaraza ya dini pamoja na maimamu mbalimbali wamehudhuria sherehe hizo.

"Viongozi wote wako hapa kuqnzia ngazi ya wilaya hadi Taifa.kwa idadi ya waliokuwepo leo tungeweza kusema ni kama mkutano mkuu kutokana na idadi ya walioshiriki na nafasi zao," amesema Mufti Zubeiry wakati anazungumzia sherehe hizo na aina ya viongozi waliohudhuria

Tamasha la Tigo Fiesta 2018 ‘kuipagawisha’ Dar Jumamosi

$
0
0
Zaidi ya wasanii 40 ‘Machampioni ‘kutoa burudani ya kufunga mwaka.

Mkuu wa Kitengo cha  Huduma za  Masoko wa Tigo William Mpinga (wa pili kulia) akiwa na mratibu wa Tamasha la Tigo Fiesta 2018 Gardner Habash (wa tatu kulia) pamoja na baadhi ya wasanii watakaotumbuiza katika Tamasha la Tigo Fiesta 2018 litalaofanyika katika viwanja vya Posta jijini Dar es Salaam Jumamosi.
????????????????????????????????????
Msanii  Nedy Music (wa kwanza kushoto)  akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa kutangaza Tamasha la Tigo Fiesta litakalofanyika katika viwanja vya Posta jinjini Dar es Salam Jumamosi.  Wa pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za  Masoko wa Tigo Masoko William Mpinga akifuatiwa na Mratibu wa tamasha hilo Gardner G Habash kutoka Clouds Media Group akifuatia na msanii Chege

PIC 3
Msanii Dogo Janja (wa kwanza kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa kutangaza Tamasha la Tigo Fiesta litakalofanyika katika viwanja vya Posta jijini Dar es Salam Jumamosi. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za  Masoko wa Tigo William Mpinga akifuatiwa na Mratibu wa tamasha hilo Gardner G Habash kutoka Clouds Media Group
PIC 4
Msanii wa muziki wa kizazi kipya TID, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo picha kuhusu ushiriki wake kwenye Tamasha la Tigo Fiesta 2018 litakalofanyika katika viwanja vya Posta jijini Dar es siku ya Jumamosi. Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za  Masoko wa Tigo William Mpinga

Wananchi waaswa kuwafichua Wahamiaji Haramu

$
0
0
Serikali imewaasa wananchi kutoa taarifa za kuwepo wahamiaji wanaoishi maeneo mbalimbali  nchini kinyume na sheria  za nchi ili raia wema waweze kufanya shughuli za maendeleo kwa amani na salama huku ikiwaasa watumishi wa Idara ya Uhamiaji kuwa waadilifu katika maeneo yao ya kazi.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji Duniani, yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja yenye kauli mbiu ya Uhamiaji Unaozingatia Utu

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Naibu Waziri Masauni amesema ni lazima wananchi washirikiane na vyombo vya ulinzi na usalama kufichua wahamiaji haramu wanaoishi maeneo mbalimbali nchini.

“Serikali ya Tanzania inaheshimu haki za kila mtu na ndio maana tumeingia mikataba mbalimbali ya kimataifa yenye kulinda utu wa kila raia awe raia au mgeni aliyepo nchini, lakini hatutokuwa tayari kuona wahamiaji wasiofuata sheria za nchi wakiingia nchini kinyume na  taratibu zilizowekwa,” alisema Masauni

“…. Nawasihi wananchi watoe ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama kufichua wageni wanaoingia nchini kinyume na utaratibu kwani wakiwaacha wanaweza kuvuruga amani na utulivu uliopo nchini.” Aliongeza Masauni.

Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala amesema Idara yake itaendelea kutumia teknolojia katika kuendesha shughuli za uhamiaji lengo ikiwa kudhibiti uhalifu na kuiongezea mapato serikali huku akiahidi kuzuia na kudhibiti wahamiaji wanaoingia nchini kinyume na taratibu

Siku ya Maadhimisho ya Wahamaji Duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo Disemba 18 huku Kauli Mbiu ya Mwaka huu ni “Uhamiaji Unaozingatia Utu”
 Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi, Mhandisi  Hamad Masauni, akisikiliza  maelezo  juu  ya  historia  ya  mabadiliko  ya  Pasi za Kusafiria  kutoka kwa mtaalamu wa pasi hizo,  Sajini  wa  Uhamiaji, Vedasto  Rweikiza(kulia), wakati  wa  Maadhimisho  ya  Siku  ya  Kimataifa  ya  Wahamiaji  Duniani, ambayo  kwa  hapa  nchini  yamefanyika  leo, katika  Viwanja  vya  Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.Kauli  mbiu  ikiwa  Uhamiaji  Unaozingatia Utu. Kushoto ni Kamishna Jenerali  wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi, Mhandisi  Hamad Masauni, akipokea zawadi  kutoka  kwa  Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Salma Panja(kulia),  baada ya kutembelea mabanda ya maonyesho  wakati wa Maadhimisho  ya  Siku  ya  Kimataifa  ya  Wahamiaji  Duniani, ambayo  kwa  hapa  nchini  yamefanyika  leo, katika  Viwanja  vya  Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kauli  mbiu  ikiwa  Uhamiaji  Unaozingatia Utu. Kushoto ni Kamishna Jenerali  wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala.
 Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi, Mhandisi  Hamad Masauni na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala (kushoto), wakiangalia pasi ya kusafiria walipotembelea mabanda ya maonyesho wakati  wa  Maadhimisho  ya  Siku  ya  Kimataifa  ya  Wahamiaji  Duniani, ambayo  kwa  hapa  nchini  yamefamyika  leo, katika  Viwanja  vya  Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.Kauli  mbiu  ikiwa  Uhamiaji  Unaozingatia Utu.
 Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi, Mhandisi  Hamad Masauni, akizungumza wakati  wa  Maadhimisho  ya  Siku  ya  Kimataifa  ya  Wahamiaji  Duniani, ambayo  kwa  hapa  nchini  yamefamyika  leo, katika  Viwanja  vya  Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.Kauli  mbiu  ikiwa  Uhamiaji  Unaozingatia Utu.
Kamishna Jenerali  wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala, akizungumza wakati  wa  Maadhimisho  ya  Siku  ya  Kimataifa  ya  Wahamiaji  Duniani, ambayo  kwa  hapa  nchini  yamefanyika  leo, katika  Viwanja  vya  Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.Kauli  mbiu  ikiwa  Uhamiaji  Unaozingatia Utu..Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA), Dkt. Anold Kihaule, akisikiliza  maelezo  kutoka kwa mtaalamu wa pasi za kusafiria,  Sajini  wa  Uhamiaji, Vedasto  Rweikiza (kulia), wakati  wa  Maadhimisho  ya  Siku  ya  Kimataifa  ya  Wahamiaji  Duniani, ambayo  kwa  hapa  nchini  yamefanyika  leo, katika  Viwanja  vya  Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.Kauli  mbiu  ikiwa  Uhamiaji  Unaozingatia Utu.

MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifungua kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM jijini Dar es Salaam leo Desemba 18, 2018
  Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally akiongea kabla ya ufunguzi wa  kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM jijini Dar es Salaam leo Desemba 18, 2018.
 Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiendesha  kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM jijini Dar es Salaam leo Desemba 18, 2018

PICHA NA IKULU

MKAZI WA MOSHI AJISHINDIA BAJAJI KWENYE PROMOSHENI SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA

$
0
0


Zuberi Maeda wa Kiterini, Moshi mkoani Kilimanjaro baada ya kukabidhiwa Bajaji yake

Zuberi Maeda (19) alibahatika kuibuka kuwa mshindi wa droo ya 71 ya promosheni ijulikanayo kama Shinda Zaidi na SportPesa inayoendeshwa na kampuni ya michezo ya kubashiri SportPesa.

Timu ya SportPesa ilifika mpaka jiji la Moshi kwa ajili ya kumkabidhi kwani mpaka kukabidhiwa bajaji yake mshindi hapaswi kutumia kiasi chochote cha fedha.Akizungumza wakati wa makabidhiano Bwana Zuberi alisema “Kupata bajaji hii kutakuwa kumetatua sana matatizo yangu kwa maana nina bustani ya mboga mboga, nitakuwa nikiifanyia biashara huku nikihudumia shamba langukwa maana nilikuwa nampango wa kuanza biashara ya mifugo..

Nategemea kuwa mfanyabiashara mkubwa hapo baadaye na namshukuru sana mwenyezi Mungu kwa maana kupitia bajaji hii ndoto zangu zitatimia, nitaanza kufuga kuku wa kisasa au wa mayai na kutunza faida wakati bustani yangu na bajaji vikiniingizia kipato hadi pale nitakapoanza kujitengenezea faida kubwa ili nifungue biashara kubwa” alisema Zuberi

Baba mzazi wa Zuberi bwana Saidi Zuberi Maeda alisema ” Nilivyosikia mwanagu kashinda kiukweli sikuamini, nilifurahi sana hadi nilishindwa kula, kwa sababu mwanangu kama mnavyomuona kuwa ni kijana mdogo mwenye ndoto za kuwa mfanyabiashara mkubwa kupitia miradi mbalimbali, kupitia bajaji hii ninaimani haya mambo yatakamilika”

“Nimejisikia vizuri mjukuu wangu kujishindia bajaji hii kwakweli, nikiugua nitakuwa na uhakika wa usafiri wa kunipeleka hospitali pamoja na babu yake, sasa huyu mjukuu wangu ndiyo miguu yangu na tumepata ahueni kama familia” alisema Bi Chausiku Zuberi ambaye ni Bibi wa Zuberi Maeda.

Kutoka SportPesa Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania alisema Zuberi ni kijana mdogo sana na kama kampuni tumefurahi kuona anajishindia bajaji itakayomuwezesha kubadili nakuinua maisha yake kiuchumi.Familia yake inamtegemea na ikiwa anandoto za kuwa mfanyabiashara mkubwa tungependelea kumuona baada ya mwaka mmoja amepiga hatua kwani uwezo huo anao na kitendea kazi ambacho ni bajaji”

“Promosheni yetu bado inaendelea na ningependa kuwahamasisha watumiaji wa mitandao yote ya simu yani (Zantel, Tigo, Vodacom, Airtel pamoja na Halotel) kupitiahuduma zao za kuhamisha fedha kupitia simu ya mkononi wanaweza kujishindia zawadi mbalimbali kutoka SportPesa.

“Kucheza piga namba * 150 *87# na uweke pesa kwenye akaunti yako ya SportPesa ili kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo Jezi ya Simba na Yanga pamoja na tiketi ya kwenda Uingereza na Hispania kuangalia mechi za ligi hizo zinazoendelea” alisema Tarimba.

Waziri wa Afya apokea Hati ya TFDA ya Ubora wa Mifumo ya Udhibiti Dawa

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii .

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa TFDA ni Taasisi ambayo inafanya vizuri na kufanya nchi kuwa kifua mbele katika masuala ya udhibiti wa Mifumo ya Dawa katika kulinda wananchi. Mwalimu ameyasema hayo wakati akipokea Hati TFDA ya Ubora wa Udhibiti wa Mifumo ya Dawa iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO), iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa TFDA baada ya kufanyiwa tathimini na Shirika la Afya Duniani (WHO) imepanda ngazi ya Tatu ya  Udhibiti wa Mifumo ya Dawa na kuwa nchi ya kwanza kwa nchi Afrika kufikia ngazi hiyo. Ummy amesema kati asilimia 100 ni asilimia 30 ndizo zimefikia ngazi ya Tatu na zilizofikia ngazi  ya Nne ni nchi zilizoendelea. Amesema kubuniwa kwa kufanyika kwa  tathimini taasisi za udhibiti duniani ili ziwe na mifumo inayowezesha kudhibiti dawa inayopaswa na hivyo kuhakikisha dawa zinazosambazwa kwenye soko na zilizo bora, salama na zinazotibu watu.

Aidha amempongeza TFDA kwa hatua waliyofikia katika kuweka Tanzania kwenye ramani kwa kufikia ngazi ya Tatu kwa nchi Afrika kuwa taasisi bora.
"TFDA ni Taasisi ambayo inafanya vizuri katika suala la udhibiti wa dawa na hiyo ni kulinda watumiaji dawa" Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu Adam amesema kuwa mchakato wa kufikia hatua hiyo ulikuwa mrefu na kuahidi kuendelea kufanya vizuri na kupanda ngazi ya Nne
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikata Utepe ya Hati TFDA ya Ubora wa ngazi ya Tatu ya Udhibiti wa Mifumo ya Dawa iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza wakati hafla ya kupokea Hati ya  Mamlaka ya Chakula  na Dawa (TFDA)kufikia ngazi ya Tatu ya Ubora wa Mifumo ya Udhibiti wa Dawa iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Adam Fimbo akizungumza kuhusiana na TFDA kufikia ngazi ya Tatu ya Udhibiti wa Mifumo ya Dawa iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TFDa wakati wa hafla ya kupokea Hati ya TFDA ya Ubora wa Udhibiti wa Mifumo ya Dawa iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

MBUNGE NA MWAKILISHI WA JIMBO LA TUNGUU WAKABIDHI SETI ZA JEZI KWA MICHUANO YA JIMBO CUP

$
0
0

 MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, akizungumza na Vijana wa Jimbo la Tunguu Zanzibar wakati wa hafla ya kukabidhi Vifaa Vya Michezo kwa ajili ya Michuano ya Kombe la Jimbo hilo vilivyotolea na Mbunge na Mwakilishi kufanikisha michuano hiyo, hafla hiyo imefanyika katika Kituo cha Vijana Dunga Bweni.(Picha na Othman Maulid)
IMG_4067
MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akikabidhi Seti 10, zilizotolewa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo hilo,kwa ajili ya Michuano ya Vijana ya Mpira wa Miguu wa  Jimbo la Tunguu Zanzibar. hafla hiyo imefanyika katika Kituo cha Vijana Dunga Bweni.(Picha na Othman Maulid)
IMG_4071
MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, akimkabidhi Seti ya Jezi Mwenyekiti wa Vijana wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Ndg. Said Hassan, kwa ajili ya Michuano ya Vijana Mpira wa Miguu Jimbo la Tunguu, vilivyotolewa na Mbunge na Mwakilishi. kushoto Katibu wa Vijana wa Jimbo la Tunguu Ndg. Ali Khatib Kisu, hafla hiyo imefanyika katika Kituo cha Vijana Dunga Bweni.(Picha na Othman Maulid)
IMG_4080
MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, akipata maelezo ya Bidhaa zinazotengenezwa na Vijana wa Kikundi cha Maendeleo cha Vijana Ubago Bi. Hawa Ali Mzee, akitowa maelezo ya bidhaa zinazotengenezwa na Vijana hao, akiangali Shampoo wakati akitembelea kikundi hicho,kushoto Mwenyekiti wa Vijana Jimbo la Tunguu Ndg.Said Hassan.(Picha na Othman Maulid)
IMG_4081
MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said, akiangalia Shampoo inayotengenezwa na KIkundi cha Vijana cha Maendeleo Ubago, akipata maelezo kutoka kwa Katibu Hamasa wa Kikundi hicho Bi. Hawa Ali Mzee, wakati alipotembelea kikundi hicho Dunga Bweni Wilaya ya Kati Unguja.(Picha na Othman Maulid)
IMG_4085
IMG_4100
MWAKILISHI wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said, akiangalia moja ya nguo zinazozonwa na Kikundi cha Vijana na Maendeleo Ubago, wakati alipowatembelea Vijana hao katika Kituo chao kuangalia shughuli wanazozifanya za utengenezaji wa Shampoo, Sabuni. Lotion na mafuta ya mgando na ushoni wa nguo.(Picha na Othman Maulid)

CCM YAWASAMEHE NA KUWAREJESHEA UANACHAMA RAMADHANI MADABIDA NA WENZAKE WATATU

$
0
0
Kwa kauli moja Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imepokea maombi na kukubali kusamehewa adhabu ya kufukuzwa uanachama kutoka kwa waliokuwa wana CCM wanne ambao walitenda makosa hayo wakiwa Wenyeviti wa CCM ngazi ya Mikoa na Wilaya. 

Waliosamehewa na kurejeshewa uanachama ni; 
1.   Ndg. Ramadhani Rashid Madabida (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam).
2.   Ndg. Erasto Izengo Kwirasa (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga).
3.   Ndg. Christopher Mwita Sanya (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara).
4. Ndg. Salum Kondo Madenge (aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni). 
 Pichani ni wanachama hao waliosamehewa wakiwa wamesimama mbele ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu Mwenyekiti wake Ndg. Philip Mangula na Katibu Mkuu Dkt. Bashiru Ally na mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) wakati wa  Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa leo tarehe Desemba 18, 2018 Jijini Dar es Salaam 
Pichani ni wanachama hao waliosamehewa wakimshukuru Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu Mwenyekiti wake Ndg. Philip Mangula na Katibu Mkuu Dkt. Bashiru Ally  mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) wakati wa  Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa leo tarehe Desemba 18, 2018 Jijini Dar es Salaam 
PICHA NA IKULU

PROF. MSANJILA AKUTANA NA UJUMBE WA SERIKALI YA INDIA

$
0
0



Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akieleza jambo katika kikao kati yake na ujumbe wa Serikali ya India na Kampuni ya National India Development Corporation  (NMDC)
INDIA 2-min
Sehemu ya ujumbe kutoka Serikali ya India na Kampuni ya NMDC pamoja na watendaji wa wizara wakifuatilia kikao hicho.
INDIA 3-min
Sehemu ya Watendaji kutoka TUme ya Madini, Taasisi na Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Maafisa kutoka Wizarani wakifuatilia kikao hicho.
INDIA 4-min
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akiongoza kikao baia yake na ujumbe kutoka Serikali ya India kilichoshirikisha pia Watendaji kutoka Wizarani, Tume ya Madini na GST.
………………………….

Na Asteria Muhozya, Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila amekutana na Ujumbe   wa Serikali kutoka nchini India pamoja na Kampuni ya National India Development Corporation (NMDC) jijini Dodoma, katika kikao ambacho pia kimeshirikisha watendaji kutoka Wizarani, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Tume ya Madini.

Ujumbe huo umefika wizarani kwa lengo la kuonana na uongozi wa Wizara kwa ajili ya kufanya majadiliano juu ya nia yao ya kufanya uwekezaji kwenye shughuli za uchimbaji wa madini na kupata maeneo mapya ya uchimbaji. Awali kampuni hiyo ilikutana na Shirika la STAMICO na kufanya majadiliano kuona ni kwa namna gani wanaweza kushirikiana katika utekelezaji wa malengo yao kupitia fursa mbalimbali zilizopo katika sekta ya madini nchini.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Desemba 18, Katibu Mkuu Prof. Msanjila amewakaribisha na kuwapongeza kwa nia yao ya kufanya uwekezaji nchini na kuueleza ujumbe huo kuwa, kampuni ya NMDC inayo fursa ya kuchagua kuwekeza ikiwa kama kampuni inayojitegemea ama kwa kuingia ubia na Shirika la Madini la Taifa la (STAMICO).

Aidha, ameuleza ujumbe huo kuwa, wizara inazo taasisi ambazo zinasimamia masuala yanayohusu leseni na shughuli za utafiti na kuusisitiza kujadiliana na Kamishna wa Madini, Mkurugenzi wa Sheria na Tume ya Madini kwa ajili ya kupata taratibu zinazotakiwa kisheria kuhusu masuala ya leseni na mahitaji mengine wanayotakiwa kutekeleza kabla ya kuwasilisha mpango huo kwenye ofisi yake. Aidha, aliutaka ujumbe huo kujadiliana na GST kwa masuala yanayohusu shughuli za utafiti wa madini.

Pia, Prof. Msanjila ameishauri kampuni husika kukata leseni ya utafiti kwanza ili kufanya utafiti katika maeneo waliyoyakatia leseni na kuwasilisha taarifa hizo katika ofisi ya GST ndipo waendelee na utaratibu wa kupata leseni ya uchimbaji. Vilevile, ameutaka ujumbe huo kuwa tayari kuwasiliana na wizara pindi unapohitaji kupata ufafanuzi wa masuala yote ya yanayohusu uwekezaji katika sekta husika.

Kampuni ya NMDC inajishughulisha na shughuli za uchimbaji wa madini ya chuma na iko chini ya Wizara inayoshughulikia madini ya chuma ya India.  Pia kampuni hiyo pia inajishughulisha na utafiti wa madini mbalimbali kama vile madini ya chuma, shaba, phosphate, nk.katika nchi mbalimbali na barani Afrika.

Shonza awataka wanafunzi wa vyuo vikuu vya Afrika Mashariki kuimarisha Umoja wa Jumuiya

$
0
0

 Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akiwataka wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki waliyoshiriki Mashindano ya Michezo ya Umoja huo kuimarisha Umoja na Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki alipokuwa akifungua Mashindano Kumi na Moja ya vyuo vya nchi wanachama leo jijini Dodoma(kushoto ) Rais wa Shirikisho hilo la Michezo kwa Vyuo Vikuu Vya Afrika Mashariki Cyriaco Kabagambe.
PIX 2
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (aliyevaa tisheti ya kijivu na koti nyeupe) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Timu ya Chuo Kikuu cha Dodoma pamoja na wataribu wa mashindano hayo leo jijini Dodoma mara baada ya ufunguzi wa mashindano ya Kumi na Moja ya Michezo kwa Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki,aliyevaa track suit nyeusi  ni Naibu Waziri wa Elimu ya Juu na Tafiti za Kisayansi Burundi Mhe.Theophile Ndarufatiye.
PIX 3
Wanamichezo ambao ni wanafunzi  kutoka  Vyuo Vikuu nchini Burundi wakipita kutoa heshima kwa mgeni rasmi Mheshimiwa Naibu Waziri  wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza (hayupo pichani) wakati ufunguzi wa mashindano ya Michezo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Afrika Mashariki yaliyofanyika leo jijini Dodoma.
PIX 4
Wanamichezo ambao ni wanafunzi  kutoka  Chuo Kikuu cha Moi nchini Kenya wakipita kutoa heshima kwa mgeni rasmi Mheshimiwa Naibu Waziri  wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza hayupo pichani wakati ufunguzi wa mashindano ya michezo kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki yaliyofanyika leo jijini Dodoma.
PIX 5
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wanasomea masuala ya Sanaa na Habari wakiimba kwaya mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri  wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mashindano ya kumi na moja ya michezo kwa Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki leo jijini Dodoma.
PIX 6
Naibu Waziri  wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza akipiga mpira wa miguu kuelekea golini kuashiria ufunguzi wa mashindano ya kumi na moja ya Michezo kwa Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki leo jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………….
Na Anitha Jonas,Dodoma

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amewataka wanafunzi wa vyuo vikuu vya Afrika Mashariki wanaoshiriki Mashindano ya vyuo vikuu Kanda ya Afrika Mashariki kuzingatia Sheria Kanuni na Taratibu katika Michezo.

Mheshimiwa Shonza ametoa tamko hilo leo jijini Dodoma alipokuwa akifungua mashindano hayo yatakayo dumu kwa wiki mbili nchini ambapo mashindano hayo yamehusisha vyuo takribani ishirini huku lengo la mashindano likiwa ni kuimarisha Umoja na Ushirikiano kwa wanachama wa umoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

‘’Ninaimani na waamuzi watakaosimamia michezo yote katika mashindano haya kuwa watatenda haki na pale mtakapoona mwamuzi hakutenda haki basi kateni rufaa badala ya kuleta migogoro katika Jumuiya ya Afrika Mashariki,’’alisema Mhe.Shonza.Kwa upande wa Mlezi wa Umoja wa Shirikisho la Michezo kwa Vyuo Vikuu Tanzania Prof. Elifas Bisanda aliupongeza uongozi Chuo Kikuu cha Dodoma kwa maandalizi mazuri waliyofanya ili kufanikisha mashindano hayo ya Kimataifa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Kanda Afrika Mashariki.

Pamoja na hayo nae Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo Prof.Ahmed Ame aliwataka wanamichezo hao pamoja na kuja kushiriki mashindano hayo mara badaa ya mashindano wasisite kutembelea vivutio mbalimbali vilivyoko nchini hapa ikiwemo kutembelea vivutio kama mbuga za wanyama pamoja na Michoro ya Kondoa Irangi.

‘’Serikali ya Mkoa wa Dodoma imetuhakikishia usalama kwa washiriki wote michezo hii na katika kipindi chote watakacho kuwepo hapa watalindwa na kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu kwa uhakika bila shida yoyote na pia kwa washiriki wote pale wanapokuwa na tatizo basi milango ya ofisi yangu ipo wazi karibuni nitahakikisha nawapa ushirikiano na kutatua kero zenu,’’alisema Prof.Ahamed.

Halikadhali katika msimu huu wa kumi na moja wa mashindano haya tangu ya anzishwe nchi ya Zambia nayo imeshiriki kwa mara ya kwanza kwa kuwasilisha baadhi ya wanafunzi wa vyuo vyake kushiriki mashindano hayo ikiwa ni kwa lengo la kuongeza ushirikiano na umoja.

SERENGETI BOYS KUSHIRIKI MASHINDANO NCHINI UTURUKI

$
0
0
TIMU ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys inatarajia kushiriki mashindano maalumu ya maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) U17 mjini Antalya nchini Uturuki Februari mwakani.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka Miguu Afrika (CAF) kwa ushirikiano na Shirikisho la Soka Ulaya UEFA yataanza Februari 22 hadi Machi 2, mwakani na yatashirikisha jumla ya timu 12 kutoka Afrika na Ulaya. 

Mbali na Serengeti Boys nchi nyingine za Afrika zitakazoshiriki katika mashindano hayo ni pamoja na Angola, Morocco, Cameroon, Uganda, Nigeria, Senegal na Guinea ambazo zitaungana na timu 4 kutoka Bara la Ulaya. ‬Serengeti Boys itakwenda kwenye michuano hiyo ikitoka kutwaa ubingwa wa michuano ya U17 Kusini mwa Afrika (COSAFA) baada ya ushindi wa penalti 6-5 dhidi ya Angola kufuatia sare ya bao 1-1, kwenye mchezo wa fainali juzi mjini Gaborone nchini Botswana. 

Katika dakika 120 za mchezo huo, Angola walitangulia kwa bao la Morais kabla ya Tanzania kusawazisha kupitia kwa Kelvin Pius dakika ya 78.Na baada ya mchezo huo, Nahodha wa Tanzania, Michael Morice alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa mechi. Tanzania iliyo chini ya kocha Oscar Milambo ilifika hatua hii kwa ushindi wa matuta pia, ikiitoa Zambia kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 1-1 pia. 

Awali, katika mechi za Kundi B, Serengeti Boys ilizifunga Malawi 2-1 na Afrika Kusini 2-0 baada ya kufungwa 2-0 na Angola, hivyo kufanikiwa kuingia Nusu Fainali. Kikosi cha Serengeti Boys kinachojiandaa kwa fainali za Afrika za U17 Mei mwakani ambazo watakuwa wenyeji katika Jiji la Dar es Salaam. 
Nahodha wa timu ya Vijana Serengeti Boys Michael Morice akikabidhi kombe kwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe baada ya kutwaa ubingwa wa michuano ya U17 Kusini mwa Afrika (COSAFA) walipowasili Uwanja wa ndege jana. 
Wachezaji Michael Morice na Kelvin John wakiwa na tuzo zao.

RC Wangabo Atoa Tahadhari Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kalambo

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametoa tahadhari kwa uongozi wa wilaya ya Kalambo juu ya matumizi na ubora wa hospitali inayotarajiwa kujengwa katika wilaya hiyo ili kusijirudie makosa yaliyofanyika wakati wa ujenzi wa vituo vya afya vinavyoendelea ikiwemo kuchelewesha malipo kwa mfundi pamoja na kuachana na mafundi wasumbufu wanaochelewesha ujenzi.

Akitolea mfano wa ujenzi wa kituo cha afya cha Legeza Mwendo kilichopewa Shilingi milioni 700 na hatimae kufanikiwa kujenga majengo tisa, hivyo kumtaka Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kwa usimamizi wa mkuu wa Wilaya hiyo kuhakikisha wanazitumia vyema Shilingi bilioni 1.85, fedha ambazo zimetengwa na serikali kwaajili ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya.

“Utoaji wa fedha ofisi yako Mkurugenzi mmekuwa mnasuasua, malipo mnasingizia sijui mifumo mifumo, watu hawalipwi kule (kituo cha afya) Mwimbi imekuwa tabu karibu mwaka mzima, hata kule (kituo cha Afya) Legeza mwendo ilikuwa hivyo hivyo, nisingependa hili litokee, malipo lazima yaende vizuri, hata wale mama lishe walikuwa wanadai hawalipwi,” Alisisitiza.

Alisema kuwa kutokana na fedha hiyo iliyotengwa angependa kuona majengo mazuri yenye viwango ili kuupendezesha mji wa Matai ambao ni makao makuu ya wilaya hiyo.Maeyasema hayo katika ziara yake ya kuona maazimio ya eneo la ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Kalambo ambapo kumekuwa na mvutano juu ya eneo la kuijenga hospitali hiyo huku maeneo kadhaa yakihitaji fidia wakati maelekezo ya fedha hizo si kwa nia ya kulipa fidia bali ni ujenzi huku zikiwa zimebaki siku chache Ofisi ya Rais TAMISEMI kurudisha fedha zake endapo fedha hizo zitakuwa hazijaanza kutumika kwaajili ya ujenzi uliokusudiwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Mh. Daudi Sichone alimshukuru Mkuu wa mkoa kwa msukumo wake wa kusimamia miradi hiyo ya maendeleo pamoja na kuwasukuma wafanye haraka kutafuta ufumbuzi wa ujenzi wa hospitali hiyo ya wilaya ili wananchi waweze kupata huduma bora na kwa wakati.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo (aliyetupa mgongo) akiangalia eneo ambalo linatarajiwa kujengwa hospitali ya Wilaya ya Kalambo.

BONDIA RAMADHANI SHAURI AJIFUA KUMKABILI AZIZI ULIZA DESEMBA 31 KINESI

$
0
0
Msimamizi wa mazoezi Abdallah Seif 'Kamanyani' akimfanyika mazoezi ya kukaza misuri ya tumbo bondia Ramadhani Shauri anaejiandaa kuzipiga na Azizi Uliza Desemba 31 katika uwanja wa Kinesi Shekilango maeneo ya Urafiki.
Msimamizi wa mazoezi Abdallah Seif 'Kamanyani' kushoto akimsimamia bondia Ramadhani Shauri kupiga beg wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kuzipiga na Azizi Uliza katika mpambano wao utakaofanyika katika uwanja wa Kinesi Shekilango maeneo ya Urafiki.
Bondia Ramadhani Shauri kushoto akipiga beg uku akiwa kasimamiwa na Abdallah Seif 'Kamanyani' wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kuzipiga na Azizi Uliza katika mpambano wao utakaofanyika katika uwanja wa Kinesi Shekilango maeneo ya Urafiki.
Msimamizi wa mazoezi Abdallah Seif 'Kamanyani' kushoto akimwelekeza bondia Ramadhani Shauri kupiga ngumi iliyonyooka wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kuzipiga na Azizi Uliza katika mpambano wao utakaofanyika katika uwanja wa Kinesi Shekilango maeneo ya Urafiki. Picha na Super D Boxing News'
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images