Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1751 | 1752 | (Page 1753) | 1754 | 1755 | .... | 1898 | newer

  0 0


  NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso wa kwanza kulia akikagua mabomba yatakayotoa maji eneo la Kilapula ambayo yatapeleka maji wilayani Muheza kutoka Pongwe Jijini Tanga wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani Tanga kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maji kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Maji Tanga Uwasa Mhandisi Jofrey Gerald
  NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia wakati wa ziara yake
  NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso akikagua moja ya miundombinu ya maji wilayani Pangani
  Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akipanda juu kuangalia tanki ya kuhifadhiwa maji eneo la Ngomeni wilayani Muheza ambapo mradi huo unatoa maji katika eneo la Pongwe Jijini Tanga na kuyapeleka wilayani humo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
  Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza mara baada ya kufanya ukaguzi huo
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Maji Tanga Uwasa Mhandisi Jofrey Gerald wakati wa ziara hiyo.

  NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo wakati wa ziara yake
  NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiangalia moja ya miradi ya inayotekelezwa wilayani Pangani Mkoani Tanga wakati wa ziara yake
  NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza na wananchi wa Kata ya Madanga wilayani Pangani wakati wa ziara yake kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
  Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso kulia akisalimia na mmoja wa wananchi wa wilayani Pangani mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya maji
  NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso katika akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kutembelea mradi huo akiwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia na wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Maji Tanga Uwasa Mhandisi Jofrey Gerald
  NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Kitila Mkumbo kumtafutia kazi nyingine Mhandisi wa maji Wilaya ya Pangani Novath Wilson kutokana na kushindwa kusimamia ipasavyo miradi ya maji wilayani humo na kupelekea wananchi kushindwa kupata huduma hiyo muhimu kwa wakati.

  Ametoa agizo hilo wakati akiwa wilayani Pangani ikiwa ni ziara yake ya siku mbili mkoani Tanga alipotembelea miradi mbalimbali ya maji inayotekelezwa wilayani humo na kutokuridhishwa nayo kutokana na utekelezaji wake kuwa chini ya kiwango hatua iliyomlazimu kuzivunja baadhi ya kamati za usimamizi wa maji ambapo ziara hiyo alianzia wilayani Muheza

  Licha ya mhandisi huyo kutoa sababu mbalimbali ya baadhi ya miradi kukwama kutoa maji lakini Naibu Waziri huyo alionyeshwa kutokuridhishwa na majibu hayo kutokana na baadhi ya maelekezo aliyokuwa akimpa ili kuweza kukabiliana na changamoto juu ya miradi hiyo.

  “Nimekuita marangapi Wizarani ..tena nikakukutanisha na viongozi wengi labda watakusaidia na kila mara nakupigia simu lakini bado unaonekana si mtendaji wa kazi sasa nitamwambia Katibu Mkuu wetu akutafutie kazi sehemu nyingine lakini sio hapa Pangani”Alisema Aweso.

  Aidha alisema ni jambo la ajabu ikiwa Serikali inapambana kutenga fedha kwa ajili ya kuwakomboa wananchi na tatizo la maji huku baadhi ya watendaji wa Serikali wakishindwa kusimamia vema miradi hiyo na kupelekea wananchi kuichukia Serikali yao.

  Awali akijibu hoja za Naibu Waziri juu ya sababu za mradi huo wa Maji uliotekelezwa kwa zaidi ya shilingi Milioni 260 Mhandi huyo wa Wilya alisema mradi huo ulimalizika machi 2013 na unamiaka mitano tangu kukamilika kwake.

  Mhandisi huyo alisema mradi huo unaendeshwa na jumuiya ya watumia maji ambayo iliundwa kwa mujibu wa kishera na ndio inayoendelea kusimamia mradi huo ambao kunatakriban mita 1500 kuelekea Kijiji cha madanga ambapo mabomba yake yalionekana kuchakaa.

  “Mh:Naibu Waziri mradi huu unanjia mbili kuelekea Jaira na Madanga lakini kunauchakavu wa miundombinu ambapo jumuiya iliyopo haikukusanya fedha ili kuweza kufanya ukarabati na ndio sababu ya eneo hilo kukosa maji muda wote”Alisema Mhandisi Wilson.

  Naibu Waziri huyo alishangazwa na hitaji la mabomba hayo kwa urefu wa mita hizo 1500 ambayo ni kiasi cha shilingi milioni 3 kwa ajili ya bomba za nchi mbili huku jumuiya hiyo ikiwa haina hata shilingi kumi jambo lililomtia wasiwasi Waziri huyo wa mradi huo kufa.

  “Mradi wa shilingi milioni 260 na leo hakuna hata shilingi kumi na leo hakuna maji maana yake wananchi hawana maji na kila kitu mnatoa majibu ya hakuna mradi huu unaweza ukafa na wananchi wakakosa maji swala hili sitolivumilia”Alisema.Wakati huohuo amemuiagiza Katibu Mkuu huyo kuhakikisha Mkandarasi wa Kampuni ya Koberg Constraction Ltd anaetekeleza mradi mkubwa wa maji toka Pongwe Jijini hadi Wilayani Muheza analipwa fedha kwa wakati ili kumuongezea ufanisi wa kazi zake.

  Akizungumzia mradi huo Mhandisi toka Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira(Tanga Uwasa) Salum Hamisi alisema mkandarasi anasimamia mradi huo wenye thamani ya shilingi Bilioni 2.6 yupo katika asilimia 50 huku akikabilia na changamoto ya fedha ili kukamilisha mradi huo kwa wakati.

  Mhadisi Hamisi ambae ni msimamizi wa mradi huo alisema mradi huo unatarajiwa kumalizika mwezi Mei mwakani ikiwa Wizara itamlipa mkandarasi fedha zake kwa wakati mradi utakaosukuma maji katika matank matano na kutarajia kupunguza kwa kiasi kikubwa adha ya maji Wilayani Muheza.
  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Maji Tanga Uwasa Mhandisi Jofrey Gerald alisema ziara ya Naibu Waziri inamanufaa kwa wananchi hasa baada ya kutembelea baadhi ya miradi na kubaini baadhi ya chanagamoto huku baadhi ya kamati zikionekana kutofanya vizuri na kuchukuliwa hatua.

  0 0  Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

  UKUAJI wa uchumi wa Taifa kutojionesha katika  kuongezeka kwa kipato cha kila mwananchi ni jambo la kawaida ambalo halimaanishi kuwa takwimu za ukuaji huo wa uchumi ni za kupikwa.

  Hayo yameelezwa kwa Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dk. Suleiman Missango alipokuwa akitoa mada katika semina kwa waandishi wa habari za uchumi na biashara
  inayoendelea jijini Dodoma.

  Akifafanua Dk Missango alisema kuwa takwimu za ukuaji wa uchumi zinatokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa jumla katika taifa ambapo mapato yake yanatofautiana katika kumwendea kila mmoja kutegemeana na shughuli za uzalishaji.Akitoa mfano kuhusiana na suala hilo, alisema kuwa shughuli za uzalishaji za jamii moja zinaweza kuwa zimeongezeka kwa kuhesabu wastani wa ongezeko la uzalishaji, lakini haina maana kuwa kila mwanajamii atakuwa ameona ongezeko katika kipato chake, kutokana
  na shughuli za kiuchumi alizonazo.

  Katika siku za karibuni kumekuwa na malalamiko miongoni mwa wananchi wakihoji takwimu za ukuaji wa uchumi zinazoonekana kuimarika ilhali wananchi wengi wamekuwa hawana pesa. Uchumi wa Tanzania unakaridiwa kukua kwa kasi ya asilimia 7 kwa mwaka.Dk Missango alisema kuwa hali ya baadhi ya wananchi kupungukiwa fedha mifukoni inatokana na kupunguza matumizi yao ya kawaida na kuyaelekezwa katika matumizi ya maendeleo, ambapo athari za kushuka chini (trickledown effect) hupungua.

  “Kwa mfano kama fedha za sherehe za uhuru zingetumika kwa shughuli hiyo, kungekuwa na watu ambao wangepta fedha na kuzitumia kwenye jamii kwa matumizi mbalimbali, lakini zinapoelekezwa kwenye miradi ya maendeleo, kuna maumivu yanayoonekana lakini kuna kuwa na manufaa mbeleni…huwezi kwenda mbinguni bila kwanza kufa,” alisema.

  Akizungumza na gazeti hili, Mwenyekiti wa Chama cha Wazalendo Tanzania (CHAWATA) Eliud  alisema kuwa takwimu za ukuaji uchumi zinawezak ueleweka kuwa nitambo za kisiasa kwa kuwa Hakuna uchimu usioleta manufaa kwa wananchi wake.“Wataalam wetu wanatueleza namba wakati hali ya mwananchi wa kawaida inazidi kuwa mbaya. Uchumi unaokua unapaswa kujiakisi kwenye maisha ya watu kuwa bora zaidi,” alisema.

  Hata hivyo, Dr Missango alisema kuwa ni wajibu wa Serikali kutengeneza sera zinazowezesha kuleta manufaa kwka wananchi, hasa wa kipato cha chini kutokana na kukua kwa uchumi.Alisema dhana na ‘robbing Peter to pay Paul’ hutumiaka na serikali zote duniani kwa kutoza kodi mbalimbali ambnapo mwenye kipato zaidi hulipa kodi zaidi na fedha hizo kwenda kwenye huduma za jamii.

  “Mambo haya unaweza kusiyaone moja kwa moja lakini kunapo kuwa na barabara nzuri zaidi, hospitali zenye dawa na kadhalika, hii ndio dalili ya ukuaji uchumi ambapo sio lazima ujieneshe kwenye kutuna
  kwa mifuko,” alisema.

   Mkurugenzi wa Sera za Uchumi na Utafiti wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Suleiman Misango akifafanua kuhusu hali ya uchumi kwenye mafunzo ya waandishi wa habari za uchumi na biashara mjini Dodoma
  Meneja wa Idara ya Itifaki na Uhusiano wa Umma wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Zaria Mbeo (kushoto), akijadiliana jambo na wakurugenzi wa Idara ya uchumi wa BoT, Tawi la Dodoma
   Mwenyekiti wa mafunzo ya waandishi wa habari za uchumi na fedha, Nurdin Selemani kutoka Azam Media, akijadiliana jambo na mtunza muda wa mafunzo hayo, Bakari Kimwanga kutoka Gazeti la Mtanzania Bakari Kimwanga (aliyekaa)
   Baadhi ya maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) wakifuatilia mjadala wakati wa semina ya waandishi wa habari za uchumi na fedha inayoendelea mjini Dodoma


  0 0


  Ni baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na dawa za kulevya kilogramu 3.03

   Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

  MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Uhujumu Uchumi jijini Dar  es Salaam, imemuhukumu Mwanamke mmoja  wa Msumbiji Ana Moisie Chissano kifungo cha maisha  baada ya kupatikana na hatia  katika  shtaka  la kukutwa na kilogramu 3.03 za dawa za kulevya aina ya cocaine Hydrochloride.

  Mshtakiwa  amefungwa chini  ya kifungu cha sheria cha 15(1)(b) cha sheria namba 5 ya 2015 cha sheria Kuzuia na kusababisha na kupambana na dawa za kulevya.

  Hukumu  hiyo imesomwa leo Desemba 12, 2018 na Jaji Lilian  Mashaka baada upande wa mashtaka kuweza kuthibitisha mashtaka hayo pasipo Kuacha shaka baada ya kuridhika na ushahidi  wa mashahidi sita wa  upande wa mashtaka waliofika mahakamani  hapo kutoa ushahidi wao.

  Aidha Mahakama  imeamuru dawa hiyo za kulevya kuteketezwa kwa utaratibu unaostahili.
   Mshtakiwa Ana Moisie Chissano raia wa Msumbiji  aliyehukumiwa kifungo cha maisha  baada ya kupatikana na hatia  katika  shtaka  la kukutwa na Kg 3.03 za dawa za kulevya aina ya cocaine Hydrochloride.
  Pichani kati ni Mshtakiwa  akiwa  katika ukumbi wa wazi wa Mahakama Kuu Kitengo cha mafisadi akisubiri kusomewa hukumu yake


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  MRADI wa malezi na makuzi kwa watoto (Play lab Program) wamefanya maadhimisho ya mahafali ya pili ya watoto kwa mwaka 2018 uliotekelezwa na Shirika la Brac Tanzania na jumla ya watoto 1200 wamefanikiwa kumaliza mafunzo hayo.

  Mradi huo wa malezi na makuzi kwa watoto hujifunza kupitia elimu ya malezi kwa wazazi, ulinzi na usalama kwa watoto.

  Akizungumza wakati wa mahafali hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke John Bwana amesema elimu waliyoipata watoto hawa ni msingi mkubwa katika kuwaandaa na elimu ya awali na wenine shule ya Msingi ambapo imetia chachu katika kuwaimarisha watoto katika maendeleo ya kiakili , kimwili, kihisia na lugha.

  John amesema, kupitia mradi huu wazazi wa watoto wamepewa mafunzo ya malezi kwa watoto wao kwani ni muhimu sana kwa sababu msingi wa ukuaji  wa motto huanzishwa na mzazi mwenyewe.

  Pia. Amesema wazazi wamekuwa mstari wa mbele katika kushiriki kazi mbalimbali za mradi kama utenenezaji wa vifaa vya asili kwa ajili ya watoto kutumia katika mafunzo yao na hii imesaidia katika kuwajenga watoto wetu kuwa na ujasiri , ukakamavu, kujiamini, kuchangamana na watoto wengine , kuwa na nidhamu bora na hata kuwa na msaada kwa wazazi wake.

  Aidha, ameishukuru Brac Tanzania kwa kuleta mradi huu unaomalizika 2020 kwa kuweza kuwapatia fursa ya elimu ya makuzi nna malezi kama msini katika maandalizi ya elimu ya awali na msingi,.

  Kwa upande wa Mtathmini wa mradi wa malezi na makuzi unaosimamiwa na Brac Tanzania Lilian Josephat amesema kuwa jumla ya watoto 1200 wa miaka 3-5 wamefanikiwa kupata mafunzo hayo na wengine kuanza elimu ya awali au msingi.

  Amesema jumla ya michezo 232 imeweza kutumika kufundishia mafunzo hayo katika masomo ya sayansi, hesabu, kuandika, sanaa, kusoma na michezo huru kwa watoto hao ndani ya miaka miwili ya mafunzo.

  Lilian amesema, mradi huu ulianza mwaka 2016 na unamalizika 2020 ila mpaka kufikia sasa jumla ya wafaidikla wa mradi huo ni Miloni 3.4 katika Nyanja mbalimbali za mafunzo kwa vitendo.

  Aidha ameeleza kuw Brac imeweza kutoa elimu ya sekondari kwa wasichana 114 na kati yao 80 wamefaulu elmu hiyo, huku watoto 1050 wamemaliza elimu ya awali na 1024 kufanikisha kuingia darasa la kwanza.

  Wasichana 4282 wamefanikiwa kupatiwa elimu ya stadi za kazi na maisha kwa mkoa wa Tanga kupitia Shirika la Brac nchini, wasichana 1985 wakipatiwa elimu ya ujasiriamali na vifaa huku wasichana 4000 wakipata mafunzo ya elimu ya afya ya uzazi.

  Katika mahafali hayo Kaimu Mkurugenzi aliweza kukabidhi vyeti na zawadi ya madaftari kwa watoto waliomaliza mafunzo hayo na kuwataka waendelee kujifunza na kuacha matendo yasiyo mema. Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke John Bwana akitoa vyeti kwa watoto waliohitimu mafunzo ya malezi na makuzi (play lab) unaoratibiwa na Shirika la Brac Nchini wakati wa mahafali ya pili yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Mtathmini wa mradi wa malezi na makuzi (play lab) Lilian Josephat akitoa risali wakati wa maadhimisho ya mahafali ya pili ya watoto kwa mwaka 2018 uliotekelezwa na Shirika la Brac Tanzania na jumla ya watoto 1200 wamefanikiwa kumaliza mafunzo hayo.Watoto wakiwa katika matukio tofauti.

  0 0

  NA MWAMVUA MWINYI, MKURANGA 

  TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa ,Mkoa wa Pwani imemfikisha mahakamani Naziru Mwakangali aliyekuwa anafanya kazi kama kibarua katika mamlaka ya bandari Dar es salaam kwa makosa ya kuahidi kutoa rushwa ya sh.laki nne na kutoa rushwa ya kiasi cha shilingi  390,000,kinyume na kifungu cha 15(1)(b) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa na. 11 ya nwaka 2007. 

  Mwakangali alifunguliwa kesi ya jinai namba. 4 ya mwaka 2018 katika nahakama ya wilaya ya Mkuranga, Mkoani hapo.

  Akisoma mashtaka mbele ya hakimu wa wilaya ya Mkuranga Tumsifu Barnabas, mwendesha mashtaka wa TAKUKURU, Euphrazia Kakiko ,aliieleza mahakama kwamba mshitakiwa alitenda kosa la kuahidi kutoa rushwa laki nne kwa mtoa taarifa ili ampatie ajira katika kiwanda cha Knauf Gypsum Tanzania Limited wilayani Mkuranga.

  Aidha aliieleza ,mahakama kwamba nshitakiwa alitoa rushwa sh. 390,000 kwa mtoa taarifa, jambo ambalo pia ni kosa kisheria .Mshitakiwa alikiri kutenda makosa yote mawili, ambapo alitiwa hatiani na hivyo kupewa adhabu ya kutumikia kifungo jela kwa muda wa miaka mitatu kwa kila kosa ambapo mahakama iliamuru vifungo vyote viende pamoja ama kulipa faini ya sh. 500,000 kwa kila kosa kwa mujibu wa sheria ya kanuni za adhabu, sura ya 16 ya sheria za Tanzania.

  Vilevile, mahakama iliamuru fedha zilizokamatwa kwa lengo la kutolewa na mshitakiwa kama rushwa zitaifishwe kuwa mali ya umma kwa mujibu wa sheria.Hata hivyo ,mshitakiwa alilipa faini kama Mahakama ilivyoelekeza.

  Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani, Suzan Raymond anatoa wito kwa wananchi kuacha kujihusisha na vitendo vya rushwa na badala yake wafuate taratibu zinazotakiwa katika suala zima la utafutaji wa ajira .

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Bandari ya Tanga inaelezwa kuwa bandari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika inayoweza kuhudumia nchi saba kwa kutumia mpaka mmoja.

  Hayo yameelezwa na Meneja wa bandari hiyo, Percival Salama, ofisini kwake jijini Tanga wakati akizungunza na waandishi wa habari kuhusu maboresho mbalimbali yaliyofanyika katika kuhakikisha wanaongeza ufanisi wa bandari hiyo.

  Amesema mbali na kuwa na uwezo wa kuhudumia nchi saba bandari ya Tanga kijografia ina sifa ya kuwa bandari pekee ya asili kutokana na kuwa na kina cha maji cha asili cha kuanzia mita tano hadi 30 huku ikizungukwa na visiwa vya asili ambavyo husaidia kupunguza nguvu ya mawimbi.

  "Serikali ya awamu ya tano kwa kuona upekee wa bandari ya Tanga iliamua kutoa fedha za kuwekeza katika miradi ya uboreshaji ili kuongeza ufanisi," amesema.

  Salama alifafanua kuwa maboresho makubwa ya bandari hiyo ambayo kwa sasa inaongoza kuwa bandari inayohudumia mizigo kwa kasi Afrika Mashariki, yamefanyika katika nyanja ya ukatabati na ununuzi wa mitambo mipya, ujenzi wa miundombinu ya kuhifadhia mizigo, na uboreshaji wa mifumo ya teknolojka ya habari na mawasiliano.

  Amesema kwa upande wa mitambo tayari imeshaanza kuwasili ambapo kati ya mitambo 20 iliyonunuliwa mitano imeshawasili bandarini hapo na wanatarajia kupikea mingine miwili siku chache zijazo na kwamba hadi kufikia Julai mwakani mitambo yote itakuwa imewasili.

  Alitaja mitambo iliyowasili kuwa ni mashine mbili za kupakia na kushusha makontena yenye uwezo wa kubeba tani 45 kila moja, mashine moja ya kupakia na kushusha mizigo kwenye majahazi na yadi ya uwezo wa tani 30, Fork lift moja ya tani 16 pamoja boti moja ya doria.

  Aliongeza kuwa katika uboreshaji wa miundombinu ya kuhifadhia mizigo Disemba 3 mwaka huu wameanza mradi wa uboreshaji wa ujenzi wa maghala ya kuhifadhia shehena yenye mita za mraba 13,000, mnara wa kuongozea meli, uwekaji sakafu na sehemu ya kulia chakula na kwamba utakamilika Machi 2020.

  Aidha alisema serikali kwa kupitia TPA imenunua mdaki unaotembea (mobile scanner) ambao umerahisisha zoezi la uondoshaji mizigo bandarini ambao unaweza kuhudumia makasha 80 hadi 100 kwa saa.

  "Kutokana na kuwa na mdaki huu sasa hivi mzigo ukitoka kwenye meli unaingizwa moja kwa moja kwenye mdaki kukaguliwa na kisha unaenda kuhifadhiwa tayari kwa mteja kuja kuchukua baada tu ya kukamilisha nyaraka zake za uondoshaji," amesema Salama.Amesema kutokana na maboresho hayo ufanisi umeongezeka kwa kiasi kikubwa ambapo wamefanikiwa kuongeza shehena za mizigo baada ya kuvutia wateja waliokimbia baada ya kutetereka.

  "Mfano ni kampuni ya A to Z ya Arusha ambayo tulipotetereka walituhama lakini sasa wamerudi na inapitisha mizigo yake hapa takribani tani 91 kwa mwezi na tuna hakika hadi kufikia 2020/21 tutakuwa tumewarudisha wateja wote waliohama," amesema Salama.

  Alisema Bandari ya Tanga ambayo ina lango kubwa kuliko bandari yeyote Afrika Mashariki la mita 1200, inatarajia kuhudumia shehena ya mizigo tani 1,267,000 kwa mwaka 2018/2019 ikilinganishwa na tani 646,718 za mwaka 2017/2018.

  "Mteja anakuja anakaa siku tano anatoa mzigo, kesho hawezi kuja tena lakini sisi hapa mtu akija kuchukua mzigo anaondoka siku hiyo hiyo na meli ikija hapa haisubirishwi kwenye eneo la bahari kama kwenye bandari zingine bali inaingia moja kwa moja kushusha au kupakia mzigo," alisema Salama.

  Alifafanua kuwa ucheleweshaji wa meli bandarini ni moja ya vikwazo kwa wenye meli kwani anapochelewa anapigwa penati ambapo kwa siku moja ni dola 20,000 hivyo anaongeza gharama za uendeshaji."Sisi hapa mara nyingi tunawahisha meli kabla hata ya muda wa makubaliano ambapo tumekuwa tukipata zawadi mara kwa mara," aliongeza.

  Awali meli ya tani 40,000 ilikuwa ikihudumiwa kati ya siku sita hadi nane lakini kutokana na maboresho yaliyofanywa bandarini hapo hivi sasa inahudumiwa kwa siku mbili."Bandari chakula chake ni mzigo hivyo, jitihada zetu ni kupunguza muda wa kuhudumia na wateja wanaangalia ubora wa huduma na kazi kubwa iliyofanyika katika bandari yetu ni kuboresha eneo la vifaa kwa sababu shida kubwa ilikuwa kwenye mitambo iliyosababisha uondoshwaji wa mizigo kuchukua muda mrefu," alisema.

  Kuhusu mapato alisema kwa mwaka 2018/2019 bandari hiyo imepangiwa kukusanya zaidi ya Sh bilioni 25 hivyo wameweka nguvu kubwa kuboresha miundombinu na kununua mitambo ya kisasa kufanikisha malengo hayo.

  Akizungumzia kuhusu miradi mikubwa iliyopangwa kufanyika Salama alisema tayari wameanza kufanyia kazi agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuchimba na kuongeza kina cha bandari hiyo hadi kufikia kina cha mita 15.

  Alisema tayari wamefanya utafiti wa aina ya udongo uliopo ambapo kazi oliyofanywa na kampuni ya BIKO ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam."Tumegundua kuwa taarifa zilizokuwepo kwa miaka mingi kuwa kuna jiwe si za kweli na kwamba kilichopo ni mchanga na udongo aina ya mfinyanzi na sasa tunatarajia kufanya usanifu na kumtafuta mhandisi mshauri ili tuanze kuchimba," alisema.

  Mradi mwingine ni wa ujenzi wa matanki ya kuhifadhia mafuta kutokana na kuwepo kwa mradi wa bomba la maguta kutoka Ohima Uganda hadi bandarini hapo eneo la Chongoleani litajengwa gati ya mafuta itakayowezesha meli kubwa za kubeba tani 100,000 hadi 250,000.

  "Kwa kuweza kupokea meli za aina hii bandari ya Tanga itakua ndio yenye uwezo wa kupokea meli kubwa kuliko bandari yeyote Afrika na huku ni kuelekea kuwa Hub ya ukanda wa Mashariki na kati," alisema Salama.

  Alisema bandari ya Tanga ina fursa kubwa ya kufanyiwa upanuzi kutokana na kuwa na ghuba nne zenye eneo la maji la mita za mraba milioni 35."Eneo hili ni sawa na bandari 12 za nchi jirani hivyo unaweza kuona fursa iliyopo kwenye bandari yetu ya Tanga," aliongeza.

  Akizungumza kuhusu changamoto katika bandari hiyo alisema ni uwepo wa bandari bubu ambazo kwa mujibu wa tathmini wamebaini uwepo wa bandari bubu 48 kwenye wilaya nne, 12 zikiwa wilaya ya Mkinga, 20 Tanga mjini, moja Muheza, na 15 wilaya ya Pangani.

  Alisema uwepo wa bandari bubu unaikosesha mapato serikali pamkna na kuhatarisha usalama wa nchi."Bandari ni mipaka ya nchi hivyo kuwepo kwa uingizaji na uondoshaji wa mizigo usiosimamiwa ni kuhatarisha usalama wa nchi kwasababu wanaweza kuingiza bidhaa zisizo ruhusiwa ikiwemo silaha," alisema.

  Hata hivyo alisema wamefanikiwa kwa kiasi fulani kudhibiti bandari hizo baada ya kutoa elimu kwa wananchi na kufanya doria za mara kwa mara kwa kutumia boti yetu ambayo ni mpya.

  Alisema tayari wameanza kuona mafanikio ya udhibiti wa bandari bubu ambapo mapato yanayotokana na majahazi yameongezeka kutoka Sh milioni 26 kwa mwezi hadi Sh milioni 63 kwa bandari ya Tanga na kutoka Sh milioni 2.5 hadi Sh milioni 8 hadi 9 kwa bandari ya Pangani huku lengo likiwa ni kufikia Sh milioni 12.

  Aidha alitoa wito kwa wananchi kutumia bandari rasmi ambazo ni Tanga na Pangani kwasababu ni gharama za chini kabisa kuliko bandari bubu ambazo wanaweza kukamatwa na mali zao kutaifishwa.Alisema katika mpango wa kutaka kurasimisha bandari hizo zipo bandari nne ambazo zinaweza kurasimishwa ambazo ni Mkwaja, Kipungwi, Kikombe na Moha.
  Meneja wa bandari hiyo, Percival Salama,akizungumza na Waandishi wa habari juu ya mipango ya kuboresha bandari ya Tanga na mafanikio yaliyopatikana katika miaka mitatu ya Rais Magufuli.
  Meneja wa bandari hiyo, Percival Salama, akiwaonyesha waandishi wa Habri baadhi ya mashine mpya za kupakulia mzigo zilizoletwa katika Bandari ya Tanga
  Bandari ya Tanga ikonekana kwa juu kama ilivyopigwa na Mpiga picha wetu alipotemblea Bandari hiyo .
  Mdaki mpya wa kukagua mizigo uliopo katika Bnadari ya Tanga.

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

  Taasisi za Umma zimeshauriwa kuwa na akaunti za makusanyo kwenye benki zaidi ya moja kati ya benki zilizoungwa na Mfumo wa Serikali wa Ulipaji wa Kielektroniki (GePG) ili kuwarahisishia walipaji wa huduma za serikali.

  Ushauri huo umetolewa leo jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango wakati akifungua mkutano wa mwaka wa watumiaji wa mfumo wa GePG katika ukusanyaji wa fedha za umma uliozishirikisha taasisi za Umma zinazotumia Mfumo huo pamoja na timu ya GePG kwa ajili ya kujengeana uwezo wa namna bora ya kutumia mfumo huo.

  Dkt. Mpango amesema kuwa utaratibu wa malipo kupitia GePG unatoa fursa ya kuwa na njia nyingi za kulipia fedha za umma pamoja na kuwapa walipaji wa huduma za serikali utaratibu rafiki na machaguo mengi ya kufanya malipo.

  "Kwa kuwa malipo yote yanayopitia GePG hayatozwi ada za miamala na benki hizo hivyo kuongeza akaunti za makusanyo katika benki hakutoongeza gharama za miamala kwa taasisi za umma bali kufanya hivyo kutaondoa hatari ya Ofisi husika kukosa huduma ya malipo endapo benki inayotumika itashindwa kutoa huduma kwa sababu mbalimbali", alisema Dkt. Mpango.

  Dkt. Mpango ameongeza kuwa utaratibu huo wa makusanyo kupitia GePG unaenda sambamba na utekelezaji wa maelekezo mengine ya Serikali yanayohusu makusanyo ikiwemo yale yanayotaka akaunti kuu za makusanyo za taasisi za umma kuwepo benki kuu ya Tanzania (BoT).

  Aidha, Waziri Mpango amezitaja baadhi ya faida za mfumo huo zikiwezo za kuongezeka kwa uwazi na udhibiti katika ukusanyaji wa fedha za umma, kupata taarifa sahihi na kwa wakati zinazohusu makusanyo pamoja na kuwa na viwango na utaratibu unaofanana katika ukusanyaji wa fedha za umma kwa taasisi zote za umma.

  Vile vile, mfumo huo unachochea ubunifu katika ukusanyaji wa pesa za Serikali na sekta ya fedha kwa ujumla kwa kuweka mazingira rafiki na ya usawa kwa wakusanyaji, kutoa huduma bora na rahisi ya malipo ya fedha za umma pamoja na kusaidia fedha kufika haraka katika akaunti kuu za makusanyo za taasisi.

  Amezikumbusha taasisi ambazo bado hazijajiunga na mfumo wa GePG kuwa ifikapo Juni 30 mwaka 2019 hakutokuwa na fedha yoyote ya umma itakayokusanywa nje ya mfumo huo, hivyo wakati wa kujiunga na kuunganisha mifumo yao na mfumo huo ni sasa.

  Mnamo Juni 2017, Serikali iliifanyia marekebisho sheria ya Fedha za Umma (PFA) ya mwaka 2001 na kuiongezea kipengele kinachotaka fedha zote za umma zikusanywe kupitia Mfumo wa Government e-Payment Gateway (GePG), hadi sasa jumla ya Benki 11 na mitandao sita ya malipo kwa njia ya simu za kiganjani zimeunganishwa na mfumo huo.

  0 0

  Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii. 

  MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kitengo cha makosa ya rushwa na Uhujumu Uchumi jijini Dar es Salaam, imemuhukumu Mwanamke mmoja Ana Moisie Chissano (36)raia wa Msumbiji kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia katika shtaka la kukutwa na Kg 3.03 za dawa za kulevya aina ya cocaine Hydrochloride.

  Mshtakiwa aliyekuwa amefunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi namba 6/2016 amefungwa chini ya kifungu cha sheria cha 15(1)(b) cha sheria namba 5 ya 2015 cha sheria Kuzuia na kusababisha na kupambana na dawa za kulevya. 

  Hukumu hiyo imesomwa leo Desemba 12.2018 na Jaji Lilian Mashaka baada upande wa mashtaka kuweza kuthibitisha mashtaka hayo pasipo Kuacha shaka baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi sita wa upande wa mashtaka waliofika mahakamani hapo kutoa ushahidi wao.

  Aidha Mahakama Imeamuru dawa hizo za kulevya kuteketezwa kwa utaratibu unaostahili.Akitoa hukumu hiyo jana, Jaji Lilian Mashaka amesema ametoa adhabu hiyo kulingana na kifungu cha sheria namba 15 (1) (b) cha Sheria namba 5 ya 2015 ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya.

  Jaji Mashaka amesema sheria hiyo inaelekeza mtu yoyote anayejihusisha na dawa za kulevya anapopatikana na hatia anapaswa kutumikia kifungo cha maisha jela."Nimezingatia sababu zilizotolewa na mshitakiwa, lakini mahakama pia imezingatia sheria ambayo imeweka adhabu kwa mtu kupitia kifungu hicho inayosema mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa makosa ya dawa za kulevya basi adhabu yake ni jela maisha.

  "Kwa mamlaka hayo, nakuhukumu wewe Ana Moisie Chissano kutumikia kifungo cha maisha kwa kosa ulilolitenda na iwapo haujaridhika na maamuzi una haki ya kukata rufaa Mahakama ya Rufani," amesema Jaji Lilian.

  Pia amesema dawa za kulevya ni tatizo linaloikabili jamii hivyo kwa njia yoyote yanapaswa kuzuiwa na jitihada za pamoja zinatakiwa zitekelezwe ili kupunguza tatizo ikiwemo kuwaadhibu wote wanaojihusisha na dawa za kulevya.

  Kabla ya kutolewa adhabu, Jaji Lilian aliuliza upande wa mashitaka kama wanakumbukumbu zozote juu ya mshtakia, wakili Kakula alidai hawana kumbukumbu ya makosa lakini makosa hayo yamekuwa yakiongezeka na kusababisha kupotea kwa nguvu kazi kutokana na kutumia dawa za kulevya.

  Hivyo aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa watu wote wanaojihusisha."Tunaomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshitakiwa kwa sababu ni njia ya kuzuia wengine wanaotaka kujihusisha na vitendo hivyo," alidai Kakula.

  Naye, Mshitakiwa kupitia Wakili wake, Hassan Ruwhanya aliiomba mahakama impunguzie adhabu mshitakiwa kwa sababu ni kosa lake la kwanza na kwamba anategemewa na familia kwa kuwa ana watoto wawili wadogo.

  "Tunaomba mahakama izingatie kutoa adhabu nyepesi kwa sababu tangu mshitakiwa afikishwe mahakamani amekaa mahabusu miaka mitatu na ameonesha kujutia kosa lake na amejifunza," amedai wakili huyo.

  Awali, upande wa mashitaka ukiongozwa na wakili wa serikali Mkuu Paul Kadushi akisaidiana na wakili wa serikali, Constantine Kakula na Batlida Mushi walidai kuwa mshitakiwa aliwasili nchini Novemba 16,2016 kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na ndege ya Shirika la Ethiopia E 827 akitokea Addis Ababa Ethiopia.

  Kadushi alidai kabla ya kufika maofisa wa polisi walikuwa na taarifa kwamba mshitakiwa huyo atawasili na ndege hiyo na atakuwa amebeba dawa za kulevya.

  Alidai mshitakiwa huyo alikamatwa na alivyopekuliwa kwenye begi lake alikutwa na bahasha na ndani yake kulikuwa na unga uzaniwao kuwa ni dawa za kulevya.

  Pia alidai baada ya unga huo kupelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali alithibitisha kuwa ni dawa za kulevya aina ya Cocaine zenye uzito wa kilogramu 3.03.

  0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili la Taifa Zanzibar (BAKIZA) Dkt. Mohammed Seif Khatib, alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar, kwa ajili ya Ufunguzi wa Kongamano la Pili la Kimataifa la Kiswahili Zanzibar .(Picha na Ikulu)
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) Dkt. Mohammed Seif Khatib, (katikati) wakati akitembelea maonesho ya Vitambu mbalimbali katika viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil , akiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, wakiangalia vitabu hivyo.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Alim Mohamed Shein, akiangalia Vitambu mbalimbali vya Wachapishaji wa Vitabu kutoka Tanzani na Kenya wakati wa maonesho hayo yaliokwenda sambamba na Ufunguzi wa Kongamano la Pili la Kimataifa la Kiswahili LILILOFANYIKA Zanzibar katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
  BAADHI ya Washiriki wa Kongamano la Pili la Kimataifa la Kiswahili la BAKIZA Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Ufunguzi wa Kongamano hilo, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia na kulifungua rasmin leo katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
  MWAKILISHI wa Wachapishajhi wa Vitabu Ndg. Gabriel Kitua akitowa Salamu za Wachapishaji waVitambu mbalimbali walioshiriki Kongamano la Pili la Kimataifa la Kiswahili Zanzibar , lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar, wakati wa ufunguzi wake uliofanyika leo,12-12-2018.
  WAZIRI wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Pili la Kimataifa la Kiswahili lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil, kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kulifungua leo. 12-12-2018.
  BAADHI ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wakifuatilia hutuba ya Ufunguzi wa Kongamano la Pili la Kimataifa ka Kiswahili Zanzibar, lililoandaliwa na (BAKIZA )wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia na kulifungua leo ,katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.12-12-2018.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia katika hafla ya Uzinduzi wa Kongamano la Pili la Kimataifa la Kiswahili Zanzibar,lililoandaliwa na Baraza la Kiswahili Zanzibar BAKIZA katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar na kuwashirikisha Wadau wa Kiswahuli na Watunzi wa Vitambu kutoka Tanzania na Nje ya Tanzania. 
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Cheti Mtunzi wa Riwaya Mzee Yussuf Masauni kwa utunzi wake wa nyimbo mbalimbali, kulia Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaaa na Michezo Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Cheti Mtunzi wa Vitabu vya Kiu,Nyota ya Rehema , Ndg. Mohammed Suleiman, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pili la Kimataifa la Kiswahili Zanzibar, linalofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Cheti Mtunzi wa Vitabu vya Kuli, Vuta N’kuvute, Haini, Mbali na Nyumbani , Kasiri ya Mwinyi Fuad na Mtoto wa Mama kilichozinduliwa leo.Ndg. Shafi Adam Shafi na kulia Waziri wa Vijana Utamaduni,Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Balozui Ali Karume, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akinesha Kitabu cha Mtunzi Shafi Adam Shafi cha Mtoto wa Mama, baada ya kukizinduwa leo wakati wa hafla ya Kongamalo la Pili la Kimataifa la Kiswahili lililoandaliwa na Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil ,kulia Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume, Katibu Mtendaji wa BAKIZA Bi. Mwanahija Juma na kushoto Mtunzi wa Kitabu hicho cha Mtoto wa Mama Mzee Shafi Adam Shafi akipiga makofi baada ya uzinduzi huo, uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akikabidhiwa Vitabu mbalimbali vya Kiu na Nyota ya Rehema na mtunzi wa Vitabu hivyo Ndg. Mohammed Suleiman, wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Kongamano la Pili la Kimataifa la Kiswahili Zanzibar, lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idirissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.

  0 0

  Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

  UTITIRI wa kodi ambazo zinalipwa na wawekezaji nchini bado umeonekana kuwa changamoto kubwa kwao na hivyo kutoa ombi kwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli kuangalia namna ya kupunguza utitiri huo wa kodi ambao umekuwa mzigo kwao pamoja na wananchi kwa ujumla.

  Ombi hilo limetolewa Mjini Dodoma na Mkurugenzi wa Ushirikiano na Uhusiano wa Jamii wa Kampuni ya Cetewico Limited Katrin Boehl baada ya baadhi ya maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) pamoja na waandishi wa habari wa habari za fedha na uchumi kufanya ziara ya kutembelea kampuni hiyo kama sehemu ya mafunzo kwa vitendo.Waandishi hao wapo kwenye mafunzo ya kuandika habari za fedha na uchumi yaliyoandaliwa na BoT ikiwa ni muendelezo wa mkakati wa kuwajengea uwezo waandishi wa habari nchini.

  "Kwa upande wangu lazima niseme nimeona ushirikiano wa hali ya juu katika Serikali yangu Dodoma kwani nikiwa na tatizo lolote ninakwenda katika ofisi za
  Serikali yangu ya Dodoma, hivyo imeonesha uthamini wa kiwango kikubwa wa kazi tunazofanya" ameongeza Katrin.

  Amesema kampuni yao inapongeza juhudi za Serikali katika ujenzi wa Tanzania ya viwanda nchini ili kufikia uchumi wa kati na wamedhamiria kuunga mkono kwa vitendo kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu lakini changamoto kubwa ambayo wanakabiliana nayo ni uwepo wa kodi nyingi ambazo zinawafanya wanakuwa katika wakati mgumu kutekeleza majukumu yao ya uzalishaji kwai gharama ni kubwa.

  "Nampongeza sana Rais Dk.Magufuli pamoja na Serikali yake kwani tunaona dhamira njema katika kuhakikisha Tanzania inakuwa ya viwanda.Kampuni yetu tumekuwa tukipata ushirikiano mkubwa kutoka Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.Hata hivyo kilio chetu ni wingi wa kodi ambazo zinasababisha kutumia fedha nyingi kwenye uzalishaji na matokeo yake bidhaa zetu zinakuwa juu kiasi cha kushindwa
  kuhimili ushindani wa soko.

  "Kampuni yetu pamoja na kuzalisha maji ya kunywa , pia tunayo kampuni ambayo inahusika na utengenezaji wa mvinyo unaotokana na zabibu za Dodoma.Tunajitahidi kutengeneza bidhaa bora ambayo ipo kwenye ubora wa kimataifa lakini kilio chetu ni makodi mengi ambayo yanatufanya tuuze kwa bei kubwa ili kurudisha sehemu ya gharama zetu ambazo nyingi msingi wake ni wa kodi ambazo tunazozwa,"amesema.

  Kutokana na utitiri huo wa makodi ambapo alihesabu zipo zaidi ya 13 , ametoa ombi kwa Serikali kuhakikisha wanakaa na kuangalia kodi na ikiwezekana zipunguzwe ili kurahisisha mazingira ya uwekezaji nchini Tanzania huku akionesha kufurahishwa na kasi ya uwekezaji wa viwanda unaondelea nchini.

  "Ombi letu namba moja tunaomba hili la kodi kuangaliwa upya, ni nyingi na zimekuwa mzigo kwetu.Tunapofikia suala la kodi kichwa kinauma na hapa ndipo tunataka Serikali itupie jicho lake.Tunaamini waandishi wa habari ambao mmetutembelea tunaomba mtusaidie kutufikishia kiloo chetu .Kodi zikiwa rafiki
  tutapiga hatua na kufanikisha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano,"amesema
  Katrin.

  Kwa upande wa waandishi waliotembelea kiwanda hicho, wameahidi kutumia kalamu zao kuhakikisha wanafikisha ombi la muwekezaji huyo kwa niaba ya wawekezaji wengine ambao wamekuwa wakilalamikia suala la uwepo wa kodi
  nyingi.Hata hivyo tayari Rais Magufuli mara kadhaa amekuwa akizungumzia
  umuhimu wa kuwepo kwa kodi rafiki ambazo zitalipika kwa urahisi.

  Waandishi wa habari wakiwa pamoja na maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) wakimsikiliza Mkurugenzi wa Ushirikiano na Uhusiano wa Jamii wa Kampuni ya Cetewico Limited Katrin Boehl wakati anafafanua namna kampuni yao inavyotengeneza mvinyo unaotokana na zabibu ya Dodoma.Waandishi na maofisa hao wametembelea kampuni hiyo kama sehemu ya mafunzo kwa vitendo.
  :Mwenyekiti wa mafunzo ya waandishi wa habari za uchumi na fedha Nurdin Selemen (kulia) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Ushirikiano na Uhusiano wa Jamii wa Kampuni ya Cetewico Limited Katrin Boehl wakati wa waandishi wa vyombo mbalimbali walipotembelea kwenye kampuni hiyo.
  Mkurugenzi wa Ushirikiano na Uhusiano wa Jamii wa Kampuni ya Cetewico Limited Katrin Boehl akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari za fedha na uchumi na maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) baada ya kutembelea kampuni yake kuangalia shughuli za uzalishaji.
  Meneja Msaidizi Uchumi na Takwimu wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Kanda ya Kati, Dk. Zegezege Mpemba akizungumza mbele ya Mkurugenzi wa Ushirikiano na Uhusiano wa Jamii wa Kampuni ya Cetewico Limited Katrin Boehl() baada ya waandishi wa habari walioko kwenye mafunzo ya habari za fedha na uchumi kutembelea kampuni hiyo.


  0 0

  *Ni baada ya kukiri makosa ya kutakatisha fedha, kuongoza genge la kuiba mafuta bomba la bandari


  Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu mmiliki wa Kampuni ya mabasi ya Princes Muro Majid Kimaro kulipa faini ya Sh. milioni 115 au atatumimia kifungo cha miaka nane jela baada ya kukiri mashtaka yanayomkabili ya kutakatisha fedha na kuongoza genge la uhalifu ili kuiba mafuta katika bomba linalomilikiwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

  Pia Mahakama imeamuru gari aina ya Scania lenye namba za usajili T 856 ADH ambalo lilitumika kuiba mafuta hayo ambayo ni zaidi ya lita 26,875.25 ya dizeli na petroli litaifishwe na kuwa mali ya Serikali.

  Hukuumu hiyo imesomwa leo Desemba 12, 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba na kuhukumiwa na jopo la mawakili likiongozwa na Wakili wa Serikali Wankyo Simon akisaidiana na Jackline Nyantori, Patrick Mwita

  Alitoa Hukumu hiyo, Hakimu Simba amesema, Mahakama imemtia hatiani mshitakiwa kwa makosa mawili baada ya kukiri kutenda makosa hayo mwenyewe.

  Akisoma adhabu, amesema, katika shitakalLa kuongoza genge la uhalifu, Muro anahukumiwa kulipa faini ya Sh. milioni tano na iwapo akishindwa atatumimia kifungo cha miaka mitatu gerezani. Wakati katika shtaka la utakatishaji fedha, mshtakiwa ameamriwa kulipa faini ya Sh.milioni 110 au kutumikia kifungo cha miaka mitano gerezani.

  Mapema kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Wakili Wankyo ameiomba Mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa kwa sababu makosa hayo ya wizi husababisha kuathirika kwa uchumi na nchi kukosa mapato.

  Pia ameiomba gari hilo litaifishwe na kuwa mali ya serikali kwa sababu ndilo lililotumika kubeba mafuta baada ya kulitoboa bomba na kuiba mafuta hayo.

  Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 81/2018 inadaiwa kati ya Julai Mosi, 2016 na Januari 8, mwaka huu katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kigamboni, Dar es Salaam na maeneo mengine Muro akiwa pamoja na wenzake ambao hawako mahakamani, kwa kujua aliongoza genge la uhalifu kwa lengo la kutoboa bomba la mafuta la TPA na kuiba mafuta ili kupata faida.

  Mshtakiwa Muro pia anadaiwa adaiwa kujipatia lita 15,950.3 za mafuta ya diseli na lita 10,925.22 za mafuta ya petroli na kusambaza mafuta hayo kwenye vituo vyake vya mafuta na kuyauza kwa watu mbalimbali huku akijua kwamba wakati akipata mafuta hayo, yametokana na makosa ya uhalifu.
  Pichani mshtakiwa Majid Kimaro ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya mabasi ya Princes Muro akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kufanikiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 115 na kukwepa kutumikia kifungo cha miaka nane gerezani.

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Agustine Mahiga amesema kuwa wakati wa kuadhimisha Uhuru ni lazima kuwakumbuka viongozi waliopigania Uhuru huo. Mahiga aliyasema hayo wakati sherehe za Uhuru wa Nchi ya Kenya kwa Wakenya waishio Tanzania iliyofanyika katika ukumbi Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

  Amesema kuwa Kenya inaadhimisha miaka 55 ni kutokana na Baba wa Taifa wa nchi hiyo Jomo Kenyatta kupigana mpaka kupatikana kwa Uhuru ambao wa Kenya wanaendelea kuwa wamoja. Mahiga amesema Tanzania na Kenya zina uhusiano ambao ulitokana na aliyekuwa Rais wa kwanza wa Kenya Hayati Jomo Kenyatta na aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambapo mafanikio hayo ndio nchi mbili zinaendelea kufaidi. Aidha amesema miaka 55 ni mingi kwa Kenya kuendelea kulinda misingi iliyoachwa na viongozi waliopigania Uhuru.

  Nae Balozi wa Kenya nchini Tanzania Dan Kazungu amesema kuwa Tanzania na Kenya zimekuwa na historia na kufanya wananchi wa nchi mbili hizo kuwa na uchumi unaotegemeana katika biashara pamoja na Uwekezaji. Amesema kuwa Tanzania zimefungua Milango ya biashara kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Kenya kuwa na nia njema kurahisha biashara pamoja na kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Amesema Kenya zimefungua milango kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanya Uwekezaji pamoja na biashara bila vikwazo vyovyote. Katika sherehe za maadhimisho ya Uhuru wa Kenya viongozi mbalimbali walihudhuria wakiwemo Mabalozi wanaowakilisha nchi zao.
  Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa , Balozi Augostine Mahiga akizungumza kwenye hafla fupi ya kusherekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

  Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu akizungumza na wageni waalikwa kutoka Balozi mbalimbali pamoja na viongozi wa serikali ya Tanzania wakati wa hafla fupi ya kusherekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
  Mtangazaji wa KTN, Mark Masai akitoa historia jinsi nchi ya Kenya ilivyopata uhuru wakati wa hafla fupi ya kusherekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

  Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa , Balozi Augostine(wa kwanza kulia) pamoja na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu wakikta keki kwenye hafla fupi ya kusherekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.  Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla fupi ya kusherekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

  Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa , Balozi Augostine pamoja na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu wakiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali waliofika kwenye hafla fupi ya kusherekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

  0 0

     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly wakishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme megawati 2100 katika mto Rufiji kati ya Waakilishi wa Kampuni ya J.V Arab Contractors/El Sewedy Electric kushoto pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Wakilishi wa Shirika la Umeme nchini Tanesco Dkt. Tito Mwinuka wapili kutoka kulia akifatiwa na Mwanasheria wa Shirika hilo Isdori Nkindi
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly wakishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme megawati 2100 katika mto Rufiji kati ya Waakilishi wa Kampuni ya J.V Arab Contractors/El Sewedy Electric pamoja na Waakilishi wa Shirika la Umeme nchini Tanesco.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly, Waziri wa Nishati Medard Kalemani wakipiga makofi wakati waakilishi wa Kampuni ya J.V Arab Contractors/El Sewedy Electric kushoto pamoja na Waakilishi wa Shirika la Umeme nchini Tanesco wakionesha vitabu vya mikataba hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly akizungumza na wageni mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kushuhudia utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme megawati 2100 katika mto Rufiji.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi mara baada ya kushuhudia tukio la kihistoria la utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme megawati 2100 katika mto Rufiji ambao utagharimu zaidi ya kiasi cha Shilingi za kitanzania Trilioni 6.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly kabla ya tukio la la kihistoria la utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme megawati 2100 katika mto Rufiji ambao utagharimu zaidi ya kiasi cha Shilingi za kitanzania Trilioni 6.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally.


  0 0


  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) akiongoza kikao kazi kilichofanyika katika ofisi za wizara ya Kilimo maarufu Kilimo 1 Jijini Dar es salam leo tarehe 12 Disemba 2018 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi wa Afrika Mashariki wa kampuni (TBL) Ndg Gareth Da Gee.
  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) akiongoza kikao kazi kilichofanyika katika ofisi za wizara ya Kilimo maarufu Kilimo 1 Jijini Dar es salam leo tarehe 12 Disemba 2018 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi wa Afrika Mashariki wa kampuni (TBL) Ndg Gareth Da Gee.
  Kikao kikiendelea
  Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi wa Afrika Mashariki wa kampuni (TBL) Ndg Gareth Da Gee akifatilia kikao kazi kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) kujadili namna ya kufungamanisha Kilimo na Viwanda nchini.  Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam

  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi wa Afrika Mashariki wa kampuni (TBL) Ndg Gareth Da Gee kujadili namna ya kufungamanisha Kilimo na Viwanda.

  Amesema kuwa kampuni hiyo inazalisha bia kwa wingi nchini Tanzania hivyo mazungumzo hayo yataongeza chachu na tija katika kuongeza masoko ya wakulima nchini.

  Mhe Bashunwa ameyasema hayo leo tarehe 12 Disemba 2018 wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ofisi za wizara ya Kilimo maarufu Kilimo 1 Jijini Dar es salam na kuhudhuriwa pia na Kaimu Mkurugenzi wa sera na Mipango, Kaimu Mkurugenzi wa idara ya usalama wa chakula, Kaimu Mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya mazao.

  Wengine ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti Tanzania (TARI), Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Kilimo (TADB) na Benki ya Uwekezaji (TIB), Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko, na Muwakilishi wa Baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi.

  Katika kikao hicho Mhe Bashungwa amesema kuwa mazungumzo hayo yataongeza mtazamo wa jumla kwa wakulima nchini kujipatia masoko ya mazao ya mvinyo hususani mahindi, Shairi, Ngano, Sukari na Mtama.

  “Alisema kuwa kwa zao la mahindi pekee nchini wakulima wana ziada ya Tani 810,000 huku bei ikiwa chini hivyo Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko wanapaswa kukutana na TBL ili kuangalia mahitaji yao kwenye mahindi na kuzingatia ubora ili wakulima waweze kunufaika na fursa hiyo” Alikaririwa Mhe Bashungwa

  Alisema kuwa moja ya mikakati ya serikali ya awamu tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli ni pamoja na kutafuta masoko ya mazao ya wakulima nchini ili wakulima hususani wa mazao ya shairi, mahindi, ngano, sukari na mtama waweze kunufaika na kilimo.

  Vilevile ameipongeza kampuni ya Bia ya TBL kwa kuanza kufanya utafiti kwenye zao la muhogo na zabibu kwani wakulima wa mazo hayo wataongeza uzalishaji wa mazao hayo nchini.Bashungwa amesema kuwa serikali inaendelea na mkakati wake wa kuimarisha masoko ya wakulima nchini ambapo atakutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa viwanda vingine.

  0 0  0 0


  Kazi ya Usimikaji wa Nguzo za Umeme utakaotumika Kuendesha treni za Kisasa zitakazotumia Umeme na Reli ya kisasa - SGR imeanza eneo la Soga nje Kidogo ya Kambi ya Ujenzi wa Reli ya  Kisasa liyopo Soga   mkoani  Pwani  mapema  Desemba  2018. Nguzo hizo zinajengwa umbali wa Mita 500 kutoka nguzo moja hadi nyingine, urefu wa nguzo moja ni Mita 9.5 huku uzito wa nguzo Moja ukiwa Tani 2.4, zina uwezo wa kudumu kwa kipindi cha Miaka 120 pia zimewekewa madini ya Zinki kwa ajili ya kuzuia kutu.

  0 0


  Na Heri Shaban

  MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema jijini Dar es Salaam ameanza kukabidhi vitambulisho vya wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama Wamachinga waliopo Kariakoo.

  Mjema amegawa vitambulisho hivyo Dar es Salam ikiwa ni siku mbili tu zimepita baada agizo la Rais John Magufuli kuwagiza wafanyabiashara wote watambulike wakiwa na vitambulisho hivyo vinavyotolewa vya Wajasiriamali wadogo.

  "Katika Wilaya yangu ya Ilala leo(jana) nimegawa vitambulisho 5000 kwa Wamachinga wa Kariakoo ambao tulikuwa tunawatambua katika mfumo maalum, zoezi hili baadae litahamia kwa Mama lishe wote waliopo wilayani Ilala ambao mtaji wao chini ya shilingi milioni nne," alisema Mjema

  Amesema katika wilaya ya Ilala mchakato huo umekwenda vizuri kwani wamachinga walishawekwa pamoja katika mfumo maalum ambao wanatambulika rasmi na Serikali. Aliwataka Wamachinga na wafanyabiashara wote kufuata utaratibu na wote watapewa vitambulisho hivyo katika ofisi za Halmashauri zilizopo jengo la Anatogluo.

  Aidha amesema wote waliopewa vitambulisho wanatambulika na biashara zao na maeneo kama sio mfanyabishara hawezi kupewa.Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Elzabeth Thomas amesema Manispaa ya Ilala wamejipanga vizuri katika juhudi za kumsaidia Rais na tayari wameanza na Wamachinga wa Kariakoo wote.

  Thomas amesema mpango huo wa kugawa vitamburisho ni endelevu mpaka wote wapewe vitamburusho Watendaji wake wa Manispaa hiyo wanasimamia. Naye Makamu Mwenyekiti wa Wamachinga Kariakoo Yusuph Namoto amesema wao ni wazalendo wanaungana na Serikali yao tukufu katika juhudi za kumsaidia Rais katika kukuza uchumi.

  Yusuph amesema kwa sasa wanaitaji kukuza uchumi biashara zao kila wakati zinabadilika hivyo wanaitaji uwezeshaji ili waweze kupiga hatua. 
  Mkuu wa wilaya ya Ilala sophia Mjema akimkabidhi kitambulisho mfanyabiashara mmachinga Ramadhan Said Dar es Salam jana ,wengine OFISA Masoko Ilala na Ofisa Biashara wa Manispaa wakishudia tukio hilo.Picha na Heri Shaaban.
   Makamu Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wamachinga Yusuph Namoto akionyesha KITAMBURISHO chake mara baada kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema Dar es Salam

  0 0

  Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa amefika eneo la Ihumwa kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi za Wizara ya Maji katika mji wa Serikali kwa nia ya kujionea hatua iliyofikiwa ya ujenzi huo.

  Profesa Mbarawa amemsisitiza mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili kumaliza ujenzi wa ofisi hizo kwa wakati ifikapo Januari 31, 2019 kulingana na maagizo ya Serikali.

  Ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Maji Ihumwa ulianza rasmi Disemba 7, 2018 na unatarajiwa kukamilika ndani ya siku 60.Kwa sasa ujenzi upo katika hatua ya msingi na unatekelezwa na Mkandarasi SUMA JKT kikiongozwa na Mhandisi Juma Ibrahimu chini ya Mtaalam elekezi Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wakisaidiana na Wataalam kutoka Wizara ya Maji wakiongozwa na Mhandisi Tamim Katakweba.

  Profesa Mbarawa amesema Wizara ya Maji imejipanga kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya uhakika ya maji muda wote, ambapo Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jijini Dodoma (DUWASA) imeweka vituo maalum kwa ajili ya kusambazia maji wakati wote wa ujenzi unaoendelea kwenye mji wa Serikali.

  Aidha, amesema utekelezaji wa ujenzi wa Mradi wa Maji Ihumwa ambao utahudumia mji huo wa Serikali chini ya usimamizi wa DUWASA unaendelea vizuri, ambapo mpaka sasa ujenzi wake umefikia asilimia 75.

  Huku ujenzi wa tenki la maji litakalotumika kuhifadhi maji kwa ajili ya kusambaza maji katika maeneo ya mji huo lenye ujazo wa lita milioni moja ukiwa katika hatua nzuri na kazi ya ulazaji mabomba ikiwa imeanza. Mradi huo unatarajiwa kukamilika kufikia miwshoni mwa mwezi Januari, 2019.

  Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi akimpa maelezo Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa kuhusu ujenzi wa tenki la maji Ihumwa unaoendelea lenye ujazo wa lita milioni moja.
  Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akisikiliza maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa ofisi za Wizara ya Maji katika mji wa Serikali, Ihumwa kutoka kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi alipotembelea kuangalia hatua ya ujenzi wa ofisi za wizara yake.
  Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akionyeshwa ramani ya ujenzi wa ofisi za Wizara ya Maji katika mji wa Serikali, Ihumwa na Mratibu wa Mradi kutoka Wizara ya Maji, Mhandisi Tamim Katakweba alipotembelea kufuatilia maendeleo ya ujenzi wa ofisi za wizara yake.
  Mafundi wakiendelea na ujenzi wa ofisi za Wizara ya Maji katika eneo la mji wa Serikali, Ihumwa ambapo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Januari, 2019.

  0 0


  Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya, akisisitiza jambo kwenye kikao na wawakilishi wa Umoja wa Wabanguaji Wadogo wa Korosho Tanzania(UWWKT) kilichofanyika kwenye hoteli ya Lindi Sea View. Pembeni ya Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi, mhehsimiwa Shaibu Ndemanga, Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Profesa Sylvester Mpanduji na kulia ni Mwenyekiti wa UWWKT Tumpale Magehema
  Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Wabanguaji Wadogo wa Korosho Tanzania (UWWKT) wakimisikiliza mgeni rasmi (hayupo pichani) Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, mhandisi Stella Manyanya. Umoja huo wa wabanguaji wadogo wa korosho umeonesha nia ya kubangua korosho iliyonunuliwa na serikali.
  Mwenyekiti wa Umoja wa Wabanguaji Wadogo wa Korosho Tanzania (UWWKT) Bi. Tumpale Magehema akisoma risala mbele ya Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, mhandisi Stella Manyanya alipofanya kikao na baadhi ya wanachama wa umoja huo mjini Lindi.
  Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, mhandisi Stella Manyanya(katikati walioketi) kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa wanachama wa Umoja wa Wabanguaji Wadogo wa Korosho Tanzania (UWWKT). Wengine walioketi kuanzia kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Profesa Sylvester Mpanduji, Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga, Mwenyekiti UWWKT Tumpale Magehema na Mkurugenzi Mtendaji wa ANSAF, Audax Rukonge.

  …………………………..

  Na Mwandishi Wetu

  Uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kununua korosho za wakulima na kuzibangua nchini umepongezwa na Umoja wa Wabanguaji Wadogo wa Korosho Tanzania (UWWKT).

  Akisoma risala mbele ya Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya, Mwenyekiti wa umoja huo Bi. Tumpale Magehema amesema uamuzi wa Rais Magufuli una nia ya kuwapa ajira wanachama wake wapatao 2881, jambo ambalo ni la kupongezwa.

  Licha ya kutoa ajira Bi. Tumpale ameueleza uamuzi huo wa kijasiri uliofanywa na Rais Magufuli utaongeza ari ya kufanya kazi na kuchochea ukuaji wa uchumi hasa kwenye mikoa inayolima korosho kwa wingi.

  Akitoa taarifa kwa mgeni rasmi, Katibu wa umoja huo Bw. Audax Mkongi, alimueleza mhandisi Manyaya kuwa umoja huo ni asasi mwamvuli ya kitaifa ya wabanguaji wadogo yenye jumla ya vikundi 183 kutoka wilaya tisa za mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani na Morogoro. Baadhi ya wilaya hizo ni Ulanga, Tandahimba, Kisarawe, Liwale na Ruangwa.

  Kwenye taarifa yake Bw. Mkongi amesema tangu umoja huo uanzishwe mwaka 2015 umefanikiwa kumiliki mashine za kubangua korosho ghafi kwa kutumia mkono 117, mashine za kutumia miguu 317, mashine za kuchemshia (boiler) 23, mashine za kupanga madaraja 12, mashine za kukaushia (oven) 12, na za kufungashia 14 zenye uwezo wa kubangua korosho ghafi kg 25,370 kwa siku.

  Kwa upande wake mgeni rasmi kwenye hafla hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Lindi Sea View, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Stella Manyanya ameupongeza umoja huo kwa ari na nia ya kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ya uchumi wa viwanda.

  Licha ya kuupongeza umoja huo, mhandisi Manyanya pia amewahakikishia ushirikiano kutoka wizara yake na kwa kuanza serikali inaandaa utaratibu wa kuutumia ili kuingia nao mikataba ya kubangua korosho iliyonunuliwa na serikali msimu huu.

  Wakati huo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO), Profesa Sylvester Mpanduji amesema taasisi yake itaendelea kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele pamoja na wadau wengine wa korosho kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati ili kuongeza thamani na ubora wa zao hilo ambalo linaongoza kwa kuliingizia taifa fedha za kigeni.

  0 0


  Kutoka kushoto, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mtwara, Mhandisi Ephraim Mushi, Msaidizi wa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo, Mhandisi Noel Baraka wakipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Migodi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Madini ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mtwara, Mhandisi Aidan Mhando kwenye eneo la uchimbaji wa mchanga la Ziwani lililopo Wilayani Mtwara mkoani Mtwara.
  Afisa Tarafa wa Ziwani, Fransis Mkuti (kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) kwenye eneo la uchimbaji wa mchanga la Ziwani lililopo Wilayani Mtwara mkoani Mtwara.


  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akichimba mchanga pamoja na wachimbaji wa madini ya mchanga kwenye eneo la uchimbaji wa mchanga la Ziwani lililopo Wilayani Mtwara mkoani Mtwara.
  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akikagua madini ya chumvi katika ghala la kuhifadhi madini hayo kwenye shamba la chumvi linalomilikiwa na Jeshi la Magereza la Kiwanda Chumvi lililopo wilayani Mtwara mkoani Mtwara.
  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wazalishaji wa madini ya chumvi kutoka katika Chama cha Wazalishaji wa Madini katika Mkoa wa Mtwara (MTWAREMA) mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichofanyika katika Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mtwara.  Na Greyson Mwase, Mtwara

  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amezitaka halmashauri zote nchini kutokutoza kodi zilizofutwa kwenye madini ya chumvi ili wazalishaji wa madini hayo waweze kufanya kazi katika mazingira mazuri na kulipa kodi stahiki serikalini.

  Naibu Waziri Nyongo ameyasema hayo leo Desemba 12, 2018 kwenye mkutano wake na wazalishaji wa madini ya chumvi kutoka katika Chama cha Wazalishaji wa Madini katika Mkoa wa Mtwara (MTWAREMA) kilichofanyika kwenye Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mtwara mjini Mtwara ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili katika mkoa huo yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

  Alisema kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Wizara ya Madini iliamua kufuta baadhi ya kodi walizokuwa wanatozwa wazalishaji wa madini ya chumvi ambazo zilikuwa ni mzigo kwao na kushindwa kufikia malengo waliyojiwekea. “Ninaziagiza halmashauri zote nchini kutoza kodi kwa kuzingatia sheria zilizopo huku zikihakikisha kodi zilizofutwa kisheria hazitozwi tena.” Alisema Naibu Waziri Nyongo.

  Akielezea mikakati ya Serikali kupitia Wizara ya Madini katika kuwasaidia wazalishaji wa madini ya chumvi katika mkoa wa Mtwara, Naibu Waziri Nyongo alieleza kuwa ni pamoja na kuangalia namna ya uanzishwaji wa kiwanda cha chumvi katika mkoa wa Mtwara kwa ajili ya kuongeza ubora na thamani ya madini ya chumvi.

  Katika hatua nyingine akizungumza na kikundi cha Umoja wa Vijana wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini ya mchanga katika eneo la Ziwani lililopo wilayani Mtwara mkoani Mtwara, mbali na kupongeza kikundi hicho kwa kazi nzuri Naibu Waziri Nyongo aliomba Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kuendelea kukisaidia kikundi hicho kwa kuwapa mikopo ya fedha ili waweze kuzalisha zaidi.

  Aidha, aliwataka wakandarasi wanaopewa zabuni za ujenzi wa miundombinu ikiwa ni pamoja na majengo kununua mchanga na tofali kutoka katika vikundi vya wachimbaji wa mchanga katika mkoa wa Mtwara ambao wanaendesha shughuli zao kwa mujibu wa sheria kwa lengo la kuwainua kiuchumi. Pia aliagiza Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mtwara kuendelea kuwapa ushauri wa kitaalam wachimbaji wa madini ya mchanga ili kufanya uchimbaji uwe wenye tija na kuzingatia sheria na kanuni za madini zilizopo.

  Wakati huohuo Naibu Waziri Nyongo alifanya ziara katika shamba la chumvi linalomilikiwa na jeshi la magereza la Kiwanda Chumvi lililopo wilayani Mtwara mkoani Mtwara na kupongeza jeshi hilo kwa kazi nzuri.

older | 1 | .... | 1751 | 1752 | (Page 1753) | 1754 | 1755 | .... | 1898 | newer