Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

Halotel Wasaini Mkataba na UCSAF

$
0
0
(Halotel) Naibu Mkurugenzi wa Halotel, Trieu Tanh Binh, (Kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Eng. Peter Ulanga, wakitia saini mkataba wa makubaliano wa awamu ya tatu kwa ajili ya kusambaza mawasiliano vijijini, utakao wezesha kampuni hiyo kufikia Zaidi ya vijiji 300, anaeshuhudia ni Waziri wa Mawasiliano, Ujenzi na Uchukuzi Eng. Aisack. (Katikati)

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (ucsaf) Eng. Peter Ulanga (Kushoto) akipongezana na Naibu Mkurugenzi wa Halotel Trieu Tanh Binh (Kulia) mara baada ya kutia saini Mkataba wa wa Kusambaza mawasiliano vijijini utakao wezesha kampuni hiyo kufikia Zaidi ya vijiji 300, anaeshuhudia ni Waziri wa Mawasiliano, Ujenzi na Uchukuzi Eng. Aisack. (Katikati)

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAKUU WA MIKOA PAAMOJA NA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika kikao kilichowahusisha Wakuu wote wa Mikoa pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa. Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi, baadhi ya Mawaziri pamoja na Makatibu Wakuu wa baadhi ya Wizara, Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Mkuchika, Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo pamoja na Wakuu wa Mikoa yote mara baada ya kikao chao pamoja na Makatibu Tawala kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala bora George Mkuchika, Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa yote Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Mkuchika, Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo pamoja na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala mara baada ya Kikao chao Ikulu jijini Dar es Salaam.  PICHA NA IKULU

BENKI KUU TAWI LA DODOMA WAANIKA MAJUKUMU YAO ILI KUFANIKISHA SHUGHULI ZA UCHUMI KWA WANANCHI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Dodoma limefafanua kwa kina majukumu yake mbalimbali na miongoni mwa majukumu hayo ni kutunza na kusambaza fedha (noti na sarafu) safi za thamani mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha wananchi kutekeleza shughuli mbalimbali za uchumi katika Kanda ya kati. 

Tawi la BoT, Kanda ya Kati, Dodoma, ni tawi la tano kufunguliwa tangu nchi ipate uhuru; na ni moja ya matawi mawili ambayo yamefunguliwa miaka ya hivi karibuni.Wakati tawi la Dodoma limefunguliwa 15/10/2015, Tawi la Mtwara limefunguliwa Machi 2017. 

Awali Tawi la Dodoma lilitarajiwa kutoa huduma za benki kuu katika mikoa ya Dodoma, Singida Iringa and Tabora. Hata hivyo kutokana na kukamilika ujenzi wa tawi la Mtwara, na kama ilivyokuwa kwa matawi mengine ya awali, mgawanyo wa mikoa katika kanda za Benki Kuu ulibadilika. 

Meneja wa masuala ya Fedha na Takwimu kutoka Benki Kuu ya Tanzania(BoT) tawi la Dodoma Dk.Camilius Kombe ametaja baadhi ya majukumu ya tawi hilo wakati anazungumzia majukumu ya benki hiyo kwa waandishi wa habari waliokuwa kwenye mafunzo ya habari za fedha na uchumi.

Ambapo katika majukumu hayo yapo pia ya kukusanya fedha zilizotumika kutoka vituo maalum vya kusambazia fedha vilivyo katika baadhi ya mabenki ya biashara na kuondoa katika mzunguko fedha ambazo zimechakaa na hazifai kutumika tena.

Pia kukusanya takwimu na taarifa za uchumi na biashara katika mikoa ya kanda ya kati na kuandaa ripoti za vipindi tofauti ambazo zinajumuishwa katika maandalizi ya sera ya fedha na utekelezaji wake. Kutoa huduma za kibenki na malipo kwa Serikali zote mbili, taasisi za serikali na mabenki.

"Majukumu haya yote ni kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT Act, 2016, Vifungu 5, 6, 31 na 32 vinavyohusu kukusanya na kuchambua takwimu za uchumi, BOT kuwa benki ya serikali na benki ya mabenki mengine na kushiriki na kutoa huduma za malipo au kukamilisha malipo,"amesema.

Amefafanua ili kutekeleza majukumu haya makuu, Tawi la Dodoma linafanya kazi muhimu zifuatazo ambazo ni kupanga na kutekeleza taratibu za kusambaza fedha (kwa ujumla) katika kanda kupitia mabenki ya biashara na kupitia vituo maalum vilivyopo Tabora na Kigoma.

"Ili kuwezesha usambaji wa fedha katika mikoa iliyo mbali na Dodoma, Benki Kuu ina mkataba na benki ya biashara ya NMB (tawi la Tabora, Mihayo) na benki ya CRDB (tawi la Kigoma) kwa ajili ya kutunza fedha za Benki Kuu katika matawi yao ili mabenki mengine yahudumiwe kupitia vituo hivyo maalum kama mabenki yaliyopo hapa Dodoma au mikoa ya jirani yanavyohudumia na tawi letu hapa jijini Dodoma. 

"Kwa hiyo, vituo hivi vya fedha na ofisi ya tawi hapa Dodoma, kwa pamoja, ndio mhimili mkubwa wa usambaji fedha safi katika mabenki kwa ajili ya shughuli za uchumi katika kanda yetu, kama ilivyo katika matawi mengine ya Benki Kuu,"amesema Dk.Kombe.

Kuhusu mchango wa maalum wa Tawi la Dodoma katika kuimarisha huduma za Benki Kuu Dk.Kombe amesema katika kutekeleza dhiima ya taasisi yao licha ya uchanga wake, zimekuwa zikiimarika tangu kufunguliwa kwake Oktoba 2015 ambapo tawi hilo lilipofunguliwa Oktoba 15, 2015 kulikuwa na benki saba; na tano tu ndizo zilikuwa zinapata huduma ya kibenki na sarafu hapo tawini. Hivi sasa katika kanda hiyo ya kati kuna jumla ya mabenki 21 yaliyo na matawi 101.

Amefafanua pamoja na majukumu ya kawaida ambayo matawi yote yanafanya, tawi la Dodoma limepewa nafasi ya kutoa baadhi ya huduma za msingi kwa wadau wakuu, hasa Serikali na taasisi zake, huduma ambazo zimekuwa zikifanyika makao makuu, Dar es Salaam pekee. 

Amesema tangu serikali ilipoanza kuhamisha shughuli zake kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma, na hatimaye kuhamia rasmi, huduma zote za kibenki kwa serikali, taasisi zake na Bunge wanazipata kwenye tawi hilo."Kwasababu hii ongezeko la kazi ya kutoa huduma katika tawi letu ni kubwa na linaendelea. Hata hivyo tumeendelea kujipanga na wadau wetu wanaridhishwa sana na huduma zetu"amesema Dk.Kombe.
Meneja Msaidizi kutoka Kurugenzi ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania(BoT) tawi la Dodoma Nolasco Maluli akizungumzia majukumu ya tawi hilo wakati wa semina ya waandishi wa habari mjini Dodoma leo
Meneja Msaidizi wa Huduma za kibenki BoT tawi la Dodoma Lilian Silaa akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa semina ya mafunzo ya uandishi wa habari za fedha na uchumi
Mtangazaji na Mwaandishi wa redio Clouds FM akizungumza kwenye semina ya waandishi wa habari za fedha na uchumi

MAAGIZO YA NAIBU WAZIRI MIFUGO NA UVUVI KWA WATENDAJI HALMASHAURI YA KILOMBERO

$
0
0
Na Emmnuel Masaka,Globu ya jamii
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amewaagiza watendaji wa Halmashauri ya Kilombero kuhakikisha wavuvi wote wanasajiliwa na kuwa na vikundi ndani ya mwezi mmoja ili waweze kufanya shughuli zao na kuchangia pato la taifa.

Pia amewataka kuwaangalia wavuvi hao kama wanauhitaji wa kupata vitambulisho vya wajasiriamali alivyovitoa Rais John Magufuli wapewe ili wafanye kazi zao bila bugudha.

Akizungumza katika ziara aliyoifanya katika kijini cha Miwangani kata ya Idete wilayani humo na kutatua migogoro mbalimbali Ulega amesema kuwa wavuvi lazima wathaminiwe na kupatiwa haki zao hasa za kuwa na vikundi mbalimbali hivyo haina budi kufanya tathimini na kuwasajili ili waweze kutambulika kwani nao husaidia katika kuchangia pato la taifa.

Amesema kuwa kabla ya Januari mwakani atatembelea na kuzungumza na wavuvi hao ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kama maagizo hayo yametekelezwa vyema.

Kwa upande wao wavuvi na wafugaji wamempongeza Rais Magufuli kwa juhudi zake za kujenga Tanzania mpya na hasa kwa kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini na wamemshukuru Waziri na Naibu waziri wa mifugo na uvuvi kwa ushirikiano wanaoutoa katika kukuza na kuimarisha sekta hiyo.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wafungaji na wavuvi wa kijiji cha Miwangani wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro,wakati wa zaiara yake ya kuzisikiliza kero mbalimbali za wananchi hao na kuzitafutia ufumbuzi .
Sehemu ya Wananchi wa kijiji cha Miwangani wilaya ya Kilombero mkoa wa Morogoro wakimsikiliza Naibu wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega alipokuwa akizungumza nao.
Mmoja wa Wanakijiji cha Miwangani akimshukuru Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega kwa kufika katika kijiji hicho na kuwatalulia kero zao na muda mrefu.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG) 
Katibu Tawala wa wilaya ya Kilombero,Robert Sidasela akizungumza na wafungaji na wavuvi wa kijiji cha Miwangani wilaya ya Kilombero kuhusu kuheshimu mipaka ya wakulima na wafungaji iliyowekwa na Serikali.

TIGO YAANDAA HAFLA KWA MAWAKALA WAKE ,WATAKAOFANYA VIZURI KUNEEMEKA NA MAMILIONI

$
0
0

Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha kutoka Tigo Hussein Sayed, akimuuliza swali mmoja wa mawakala walihudhuria hafla ya chakula cha jioni ambapo Tigo ilitangaza promosheni ya mwisho wa mwaka inayojulikana kama Wakala Chief itakayotoa zawadi ya mamilioni kwa mawakala watakaofanya vizuri katika biashara zao.
Meneja wa Tigo Pesa, James Sumari akizungumza na baadhi ya mawakala wa Tigo Pesa katika hafla iliyofanyika jijjini Dar es Salaam ambapo Tigo ilitangaza promosheni ya mwisho wa mwaka inayojulikana kama Wakala Chief itakayotoa zawadi ya mamilioni kwa mawakala watakaofanya vizuri katika biashara zao.
Baadhi ya Wakurugenzi wa kampuni ya mawasiliano ya Tigo wakiwa katika picha ya pamoja na mawakala wa Tigo Pesa katika hafla ambapo Tigo ilitangaza promosheni ya mwisho wa mwaka kwa inayojulikana kama Wakala Chief itakayotoa zawadi ya mamilioni kwa mawakala watakaofanya vizuri katika biashara zao.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha kutoka Tigo Hussein Sayed, akitoa zawadi ya kofia lwa mmoja wa mawakala wa Tigo Pesa aliyefanikiwa kujibu kwa usashi swali alilouliza kuhusu Tigo Pesa wakati wa hafla ya chakula cha jioni ambapo Tigo ilitangaza promosheni ya mwisho wa mwaka kwa inayojulikana kama Wakala Chief itakayotoa zawadi ya mamilioni kwa mawakala watakaofanya vizuri katika biashara zao.

Wanawake Watajwa Kama Sehemu ya Hamasa, Toharakinga kwa Wanaume Geita

$
0
0
Wakazi wa Katoro wakisubiri kupata huduma ya Tohara ya bila malipo, inayotolewa na Taasisi ya Kimataifa inayojihusisha na masuala ya Afya ya IntraHealth katika kituo cha afya Katoro.

Madaktari wakimtahiri mmoja wa wakazi wa Katoro,wakati wa huduma hiyo ya bila malipo inayotolewa na Taasisi ya kimataifa inayojihusisha na masuala ya Afya ya IntraHealth katika kituo cha afya Katoro.

Msimamizi wa kituo cha Tohara cha Katoro Bw. Faustine Edward, akizungumza na wakazi wa Katoro waliojitokeza kupata huduma hiyo ya bila malipo, inayotolewa na Taasisi ya kimataifa inayojihusisha na masuala ya Afya ya IntraHealth katika kituo cha afya Katoro, ambapo wanatahiri watu 20 hadi 30 kwa siku. Hapa hupewa elimu kabla ya kufanyiwa tohara.


Ikiwa zimesalia siku chache kabla ya kumalizika kwa robo ya kwanza, ya Kampeni ya Toharakinga kwa Wanaume wenye umri kuanzia miaka kumi na kuendelea inayoendeshwa mkoani Geita, kundi la wanawake limebainika kuwa chachu ya kufanikisha mpango huo kutokana na wengi wao kuwahimiza wanaume wao na watoto kwenda kufanyiwa Tohara.

Hadi kufikia Sepetemba 2018, wanaume 115, 000 kati ya 119, 000 waliolengwa kufanyiwa tohara Mkoani Geita walikuwa wamefikiwa na kuhudumiwa katika kampeni inayoendeshwa na Serikali kwa ushirikiano na Shirika lisilo la kiserikali la IntraHealth International kwa ufadhili wa Mfuko wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) PEPFAR kupitia CDC,

Kituo cha Afya Katoro ni kati ya vituo 23 vya muda na 13 vya kudumu vinavyotoa huduma hiyo ambayo kabla ya kutolewa wanaume wanaofika kufanyiwa tohara hupitia hatua kadhaa ikiwemo kuandikishwa, kuelimishwa na kupimwa virusi vya UKIMWI kabla ya huduma.

Msimamizi wa Kituo hicho, Bw. Faustine Edward alisema muitikio wa wananchi umekuwa mkubwa kiasi cha kuwafanyia tohara wanaume kati ya 10 hadi 30 kwa siku.

“Mwitikio ni mkubwa sana, wateja ni wengi, hadi tunafikiria kuongezewa muda kwakuwa tulianza zoezi hili mwezi Novemba 15, 2018 na mwisho ni mwezi Desemba 15, 2018; Lakini pia niwapongeze akinamama, wamekuwa mabalozi wazuri kwa kuwaleta watoto wao lakini pia kuwashawishi waume zao kuja kufanya Toharakinga salama hadi kutuwezesha kupata watu 10 hadi 30 kwa siku,” alisema Bw. Edward

Pamoja na muitikio huo, Bw. Edward Alisema zipo baadhi ya changamoto zinazoikabili kampeni hiyo ikiwemo upungufu wa miundombinu ya jengo la kutolea huduma kwa sasa, imani potofu kutoka kwa baadhi ya wananchi kuhusu tohara na kutozingatia ushauri wa kitaalam kwa baadhi ya wanaofanyiwa tohara kutumia njia za asili za kutibu vidonda.

“Baadhi ya wanaotahiriwa wakirejea majumbani husikiliza na kutumia ushauri wa mitaani ikiwemo kutumia kinyesi cha Ng’ombe kupakwa kwenye kidonda wakiamini husadia kupona haraka, jambo linalosababisha madhara kiafya. Tunakabiliana na tatizo hili kwa kutoa elimu kwa wananchi na tiba sahihi tatizo linapojitokeza,”alisema Edward

Kwa upande wake Bi. Winfrida John, Mkazi wa Ludete Stooni amekuwa shuhuda wa kupitia mtoto wake kutosumbuliwa na maambukizi kwenye njia ya mkojo (UTI) baada kufanyiwa Toharakinga aliyosema inasaidia usafi na kuepusha magonjwa mbalimbali ya zinaa huku akiwaasa wanawake na wananchi kwa ujumla kujitokeza kuunga mkono kampeni hiyo.

Bw. Masunga Maduhu ni mmoja wa wanaume waliofanyiwa Toharakinga wakiwa na umri wa miaka 34, ambaye katika mahojiano alisema hakupata madhara wala kusikia maumivu wakati wa tohara na kuiomba Serikali na wadau wengine kuendeleza huduma hiyo hadi maeneo ya vijijini.

“Pamoja na faida ya kujiepusha na maambukizi ya UKIMWI kwa asilimia 60, tohara pia imeniongezea kujiamini kiasi cha kuweza kujisaidia haja ndogo bila hofu mbele ya watu wengine kulinganisha na awali nilipokuwa naona aibu nikijificha kwa sababu nilikuwa sijafanyiwa tohara,” alisema Maduhu

Naye Bw. Peter Ngaseba, Mkazi wa Katoro Stooni amesema, usafi na kuepuka maambukizi ya virusi vya UKIMWI kupitia hamasa inayoendelea kufanywa na wataalam mtaani wakiwapa elimu na vipeperushi ndiyo imempa msukumo.

Alienda mbali zaidi kwa kusema tohara imeongeza hamasa na uwezo wake katika tendo la ndoa kutokana na kujiamini.

Vilevile, tunatakiwa kuelewa kwamba Toharakinga salama inazo faida kemkem zikiwemo kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya zinaa ambayo nayo huchangia kwa kiasi kikubwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI, kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya kichwa cha Uume, saratani ya mlango wa kizazi kwa akina mama, kukosa uwezo wa kutungisha mimba, uvimbe wa kichwa cha Uume na magonjwa mengine ya zinaa

MAGAZETI YA LEO IJUMAA DESEMBA 2018

HOTUBA YA RAIS DKT. MAGUFULI HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA WA UJENZI MRADI WA UMEME WA RUFIJI


Maafisa Madini Watakiwa kuwa Wabunifu, Ukusanyaji Maduhuli

$
0
0

Mtaalam kutoka kiwanda cha kuzalisha saruji cha Dangote kilichopo mkoani Mtwara, Victor Kamuhabwa (wa kwanza kulia mbele) akimwonesha Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kushoto mbele) namna mfumo wa uendeshaji wa mitambo unavyofanya kazi kwenye ziara ya Naibu Waziri Nyongo kwenye kiwanda hicho tarehe 13 Desemba, 2018.
Mtaalam kutoka kiwanda cha kutengeneza vyombo vya ibada kwa kutumia madini ya mawe kinachomilikiwa na Shirika la Benedictine Abbey katika Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, Mhandisi Kassari Viater (kulia mbele) akielezea namna mashine ya kukata mawe makubwa inavyofanya kazi kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati mbele) kwenye ziara ya Naibu Waziri Nyongo kwenye kiwanda hicho.
Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Lindi, Sophia Omari (kulia) akibadilishana mawazo na Mhandisi Migodi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mtwara, Aidan Gumbo Mhando (kushoto) kwenye ziara hiyo.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akiangalia zawadi aliyokabidhiwa na mmoja wa watendaji wa kiwanda cha kutengeneza vyombo vya ibada kwa kutumia madini ya mawe kinachomilikiwa na Shirika la Benedictine Abbey katika Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, Paulo Gembe (hayupo pichani) mara baada ya kuhitimisha ziara yake katika kiwanda hicho. Kushoto ni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mtwara, Mhandisi Ephrahim Mushi na kulia ni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Lindi, Sophia Omari.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya watumishi wa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mtwara na Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Lindi mara baada ya kumalizika kwa ziara.



Na Greyson Mwase, Lindi

Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa Nchini wametakiwa kuongeza ubunifu kwenye ukusanyaji wa mapato ili kuweza kufikia lengo lililowekwa na Serikali hivyo Sekta ya Madini kuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 13 Desemba, 2018 na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo kwenye kikao chake na watumishi wa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Lindi iliyopo Wilayani Nachingwea mkoani Lindi ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili kwenye mkoa huo, yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini pamoja na kutatua kero mbalimbali.

Naibu Waziri Nyongo aliyekuwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Rukia Mhango alisema kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Madini imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa sekta nyingine kutokana na makusanyo ya kodi mbalimbali za madini.

“Ninawaagiza maafisa madini wakazi kuhakikisha wanafikia lengo lililowekwa na Serikali kwenye ukusanyaji wa kodi mbalimbali zitokanazo na Sekta ya Madini kwa kuwa wabunifu, na tupo tayari kusaidia pale itakapowezekana,” alisema Naibu Waziri Nyongo. Katika hatua nyingine, Nyongo aliwataka maafisa madini kujiridhisha na maeneo yanayoombewa leseni kabla ya kutoa leseni ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza kati ya wamiliki wa leseni na wananchi wanaozunguka maeneo ya uchimbaji.

Wakati huohuo akizungumza mara baada ya kuhitimisha ziara yake kwenye kiwanda cha uzalishaji wa saruji cha Dangote kilichopo mkoani Mtwara, Naibu Waziri Nyongo alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwenye sekta ya madini na kusisitiza kuwa Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano kwa wawekezaji ili waweze kuzalisha zaidi na Serikali kupata mapato yake stahiki.

Aidha, Naibu Waziri alifanya ziara katika machimbo ya kokoto yanayomilikiwa na kampuni za Drumax Construction na Said Seff na kiwanda cha kutengeneza vyombo vya ibada kwa kutumia madini ya mawe kinachomilikiwa na Shirika la Benedictine Abbey katika Wilaya ya Masasi na kuwahakikishia watendaji wake kuwa Serikali imejipanga katika kutatua changamoto zinazowakabili ili uwekezaji wao uwe na manufaa, hivyo kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.

SERIKALI KUZISHUSHIA RUNGU TAASISI ZISIZOJIUNGA NA MFUMO WA GePG IFIKAPO JUNI 30, 2019

$
0
0

1-min
Mkurugenzi wa Mifumo ya Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Sausi, akieleza kuhusu bidhaa mpya zitakazo wasilishwa kwa wadau wa mfumo wa ukusanyaji mapato (GePG) wakati wa Mkutano wa wadau hao uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage Jijini Dodoma.
2-min
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu ambaye ni mgeni rasmi akifungua mkutano wa wadau wa mfumo wa ukusanyaji mapato (GePG) wa uliofanyika katika ukumbi wa wa Wizara ya Fedha na Mipango (Kambarage) Jijini Dodoma.
3-min
Meza kuu ikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (katikati) wakifuatilia kwa makini maelezo ya wadau wa mfumo wa ukusanyaji mapato (GePG), Jijini Dodoma
4-min
Baadhi ya Washiriki wa mkutano wa mwaka wa mfumo wa ukusanyaji mapato (GePG), wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (hayupo pichani), uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage Jijini Dodoma.
5-min
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu ambaye ni mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mkutano wa mwaka wa watumiaji wa mfumo wa ukusanyaji mapato uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Kambarage Jijini Dodoma.

(Picha na Josephine Majura MoFP Dodoma)
…………………………
Na. Josephine Majura na Peter Haule WFM, Dodoma
Serikali imezitaka taasisi zote ambazo bado hazijajiunga na Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato ya Serikali (GePG) kuhakikisha wamejiunga na mfumo huo kabla ya  Juni 30, 2019.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James, wakati wa Mkutano wa mwaka wa  wadau wa utumiaji wa mfumo wa GePG Jijini Dodoma.  

Dkt. Kazungu, alisema kuwa hakutokuwa na fedha yoyote ya umma itakayokusanywa nje ya Mfumo wa GePG, hivyo wakati mwafaka wa kujiunga na kuunganishwa  na mfumo huo ni sasa.

“Napenda kusisitiza kuwa, ni lazima kutumia mfumo huu kwa kuwa unaongeza ufanisi na uwazi katika ukusanyaji wa Fedha za Umma na pia utaratibu wa matumizi ya  GePG unatoa fursa ya kuwa na njia nyingi za kulipia na kuwapa walipaji wa huduma za Serikali utaratibu rafiki wa kufanya malipo”, alieleza Dkt. Kazungu.

Utaratibu wa makusanyo kabla ya mfumo wa GePG haukua rafiki kwa kuwa ilikuwa ni vigumu kuthibitisha malipo na pia  kuwa na foleni ndefu kwenye Ofisi za Serikali zilizosababishwa na zoezi la kufanyiwa tathmini ya malipo ya huduma na kuthibitisha malipo.

Alisema ili kukabiliana na changamoto hizo katika ukusanyaji wa Fedha za Umma, Juni 2017, Serikali iliifanyia marekebisho Sheria ya Fedha za Umma (PFA) ya mwaka 2001 na kuongeza kipengele kinachotaka Fedha zote za umma zikusanywe kupitia Mfumo wa Government e-Payment Gateway (GePG).

Lengo la kuanzishwa kwa GePG ni kutatua changamoto zilizopo kwenye Mfumo uliokuwepo wa ukusanyanji wa fedha za umma ili kuongeza uwazi na udhibiti wa fedha za umma, kuboresha na kurahisisha namna ya kulipia huduma za umma na pia kupunguza gharama zinazoambatana na ukusanyaji wa fedha hizo ambapo mfumo huo ulianza kutumiwa rasmi na taasisi za umma mwezi Julai 2017 baada ya majaribio yake kukamilika.

Alisema kuwa utaratibu GePG unaenda sambamba na utekelezaji wa maelekezo mengine ya Serikali yanayohusu makusanyo ikiwemo yale yanayotaka akaunti kuu za makusanyo za taasisi za umma kuwepo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), hivyo ni lazima kuhakikisha akaunti za Taasisi za ummaa za makusanyo zilizoko Benki Kuu zimewasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha na mipango ili ziunganishwe na GePG.

Mpaka sasa takribani Benki kumi na moja (11) na mitandao sita(6) ya malipo kwa njia ya simu za kiganjani zimeshaunganishwa na mfumo huo.

Dkt. Kazungu alisema kuwa ni vyema taasisi za Serikali kuwa na akaunti za makusanyo kwenye benki zaidi ya moja kati ya benki zilizoungwa na GePG ili kuwarahisishia walipaji wa huduma za serikali kwa kuwa malipo yote yanayopitia GePG hayatozwi ada za miamala na benki hizo, hivyo kuongeza akaunti za makusanyo hakutoongeza gharama za miamala kwa taasisi za umma.

Alibainisha kuwa kutekelezwa kwa rai hiyo kutaondoa hatari ya taasisi ya umma kukosa huduma ya malipo endapo benki inayotumiwa itashindwa kutoa huduma kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuvunja makubaliano ya namna ya kuzihudumia akaunti zilizounganishwa kwenye mfumo wa

Naibu Katibu Mkuu Kazungu amewataka wajumbe wa mkutano huo kuwa chachu katika kuboresha utendaji kwa vitendo kwa kutoa huduma nzuri kwa wananchi zinazohusisha ukusanyaji wa Fedha za Umma katika maeneo yao ya kazi baada ya kumalizika kwa mkutano huo.

Kwa upande wake Mkurungezi wa Mifumo ya Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. John Sausi, alisema kuwa mfumo huo umekuwa na tija tangu ulipoanzishwa kwa kuwa Serikali kupitia Wizara ya Fedha inaweza kuona makusanyo yote yanayoingia hivyo kuongeza ufanisi wa upatikanaji wa mapato, uwajibikaji na uwazi.

Alisema kuwa, jumla ya Taasisi 326 zimeunganishwa na Mfumo wa GePG na miongoni  mwa Taasisi hizo ni Wakala wa Misitu, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)

Amezitaja changamoto za Mfumo huo kuwa ni pamoja na Benki 11 tu ndizo zinazotumia mfumo huo kati ya Benki zaidi ya 50, hivyo kuleta mkanganyiko kwa wadau wanaotumia  mfumo huo.

Mkutano wa wadau wote wanaotumia Mfumo wa GePG ni wa kwanza kufanyika nchini ukiwa na lengo la kubaini na kutatua changamoto za mfumo huo tangu ulipoanzishwa.

UJENZI BARABARA BARIADI HADI MASWA MKOANI SIMIYU WASHIKA KASI

$
0
0
Maafisa wa Serikali kutoka Wizara ya Maji, Wizara ya Ujenzi, miundombinu na Mawasiliano, wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, wakipata maelezo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ya Bariadi hadi Maswa, (km50) wakati wa ziara ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Simiyu, ili kujua mafanikio, changamoto na mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo.
Mchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Jordan Matonya, akitaka kupata ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Bariadi hadi Maswa, mkoani Simiyu, yenye urefu wa km 50, kutoka kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara mkoani humo, Mhandisi Mohamedi Athumani (Hayuko pichani).

……………………..

Na Benny Mwaipaja, WFM, Simiyu

UJENZI wa barabara yenye urefu wa kilometa 50 kati ya mji wa Bariadi na Maswa mkoani Simiyu kwa kiwango cha lami, inayojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 88, unaendelea kwa kasi ambapo hivi sasa umefikia asilimia 34.

Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini-TANROADS, mkoa wa Simiyu, Mhandisi Mohamedi Athumani, ameiambia timu ya maafisa wa Serikali inayoongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, inayofuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani humo kwamba mradi huo utakapo kamilika mwezi Oktoba mwakani, utafungua fursa za kibiashara na kiuchumi kwenye mkoa huo na mikoa jirani ya Mwanza, Shinyanga, Singida na nchi jirani ya Kenya.

Amesema kuwa kazi zilizofanywa na mkandarasi anayejenga barabara hiyo, Kampuni ya CHICO ya China, ni kuanza kwa ujenzi wa madaraja makubwa mawili ya Simiyu na Banhya na uinuaji wa tuta la barabara maeneo mbalimbli ya mradi.

“Kuna madaraja mengine madogo madogo (Pipe culverts 57) pamoja na makalvati madogo (Box culverts 12), kwenye kipande hiki cha Barabara chenye urefu wa kilometa 50 na mkandarasi, Kampuni ya CHICO inafanyakazi vizuri na tuna imani kwamba ujenzi wa barabara hii utakamilika ifikapo mwezi Oktoba, 2019 kama mkataba unavyoonesha” alifafanua Mhandisi Athumani.

Kwa upande wake, Mhandisi Mshauri Mkazi wa mradi huo, Mhandisi Swalihi Kazuvi amesema kuwa barabara ya Mwigumbi-Maswa-Bariadi na Lamadi, inayojengwa kwa kiwango cha lami, yenye urefu wa kilometa 172, itakapokamilika, italeta chachu ya maendeleo yanayopitiwa na barabara hiyo.

“Kipande cha barabara ya lami kutoka Mwigumbi mpaka Maswa na kile cha Bariadi hadi Lamadi vimekamilika kwa hiyo kipande kilichobaki ni hiki (Bariadi-Maswa), ndio maana unaona magari yanayopita barabara hii ni mengi licha ya kwamba kipande hiki cha kilometa 50 hakijakamilika, madereva wanaona afadhali wapite huku kwenda Musoma kuliko kupitia njia ya Mwanza” aliongeza Mhandisi Swalihi Kazuvi

Lengo la ziara hiyo ya maafisa wa Serikali ni kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezawa katika Mkoa huo ili kujua mafanikio, changamoto na mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo.

WAZIRI WA MADINI AELEZEA MCHANGO WA SEKTA YA MADINI KATIKA KUFIKIA UCHUMI WA KATI , TIC YAZUNGUMZIA MABORESHO YA SERA NA SHERIA

$
0
0
WAZIRI wa Madini Angela Kairuki amesema ili kufikia malengo ya mpango wa taifa wa maendeleo ambao unaelekeza kuwa ifikapo mwaka 2025 Tanzania iwe imefikia uchumi wa kati, sekta ya madini inalazimika kuongeza mchango katika pato la taifa kutoka asilimia 4.8 ya sasa kufikia asilimia 10 mwaka 2025. 

Ametoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa kongamano la uwekezaji katika sekta ya madini kati ya Tanzania na China lililofanyika jijini Beijing nchini China. 

"Ili kufikia malengo ya mpango wa taifa wa maendeleo ambao unaelekeza kuwa ifikapo mwaka 2025 Tanzania iwe imefikia uchumi wa kati, sekta ya madini inalazimika kuongeza mchango katika pato la taifa kutoka asilimia 4.8 ya sasa kufikia asilimia 10 mwaka 2025," amefafania Waziri Kairuki.

Wakati Waziri Kairuki anazungumza washiriki wa Kongamono la siku moja la uwekezaji katika sekta ya madini kati ya Tanzania na China walikuwa wakisikiliza kwa makini fursa zilizopo nchini Tanzania.

Pia mada mmbalimbali zilizowasilishwa katika kongamo hilo ambalo limelenga kuhamasisha ubia katika sekta ya madini ikiwemo kuvutia mitaji zaidi, teknolojia mpya kwenye utafiti, uchimbaji na uchakataji wa madini ili kuyaongezea thamani. 

Akifungua Kongamano hilo la kwanza la aina yake kuandaliwa na Wizara ya madini kwa ushirikiano na kituo cha uwekezaji Tanzania na ubalozi wa Tanzania nchini China, Waziri wa Madini Angela Kairuki, ametumia jukwa hilo kuelezea mipango ya wizara yake katika kukuza sekta ya madini nchini. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania(TIC) Geofrey Mwambe amesema nia ya Serikali katika maboresho ya sera na sheria ni kuhakikisha kuwa rasilimali za Tanzania zinawanufaisha watanzania pamoja wawekezaji. 

Ametumia nafasi hiyo kufafanua fursa mbalimbali zilizopo nchini Tanzania na kuwahamasisha wawekezaji kuwekeza katika maeneo mbalimbali hasa kwa kuzingatia mazingira ya uwekezaji ni mazuri na nchi yetu ni salama.

Akikaribisha washiriki wa kongamano hilo Balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki amesema Serikali ya awamu ya tano imejipanga kutumia fursa za uwekezaji wakati wa mkutano wa FOCAC uliofanyika Beijing mwezi Septemba mwaka huu 

Wakati huo huo kwa upande wao wawekezaji kutoka China ambao wamewekeza Tanzania na wawekezaji watanzania wameeleza kufurahishwa na mabadiliko yanayofanywa na Serikali katika sekta ya madini lakini zaidi kuhusu kongamano hilo ambalo wamesema ni la faida. 

Kwa kukumbusha tu miongoni kwa mada zilizowasilishwa ni pamoja na fursa na mazingira ya uwekezaji katika sekta ya madini nchini pamoja na marekebisho ya sheria ya madini ya mwaka 2017 na utafiti wa madini nchini Wadau wengine walihudhuria kongamano hilo ni kutoka STAMICO na Tume ya Madini nchini.
WAZIRI wa Madini Angela Kairuki akizungumza mbele ya wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa kongamano la uwekezaji katika sekta ya madini kati ya Tanzania na China lililofanyika jijini Beijing nchini China hivi karibuni. 
WAZIRI wa Madini Angela Kairuki akizungumza mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) kuhusu ufunguzi wa kongamano la uwekezaji katika sekta ya madini kati ya Tanzania na China lililofanyika jijini Beijing nchini China hivi karibuni.

PROMOSHENI YA TBL YAWEZESHA MKAZI WA IRINGA KUSHEREKEA KRISMAS NA GARI MPYA

$
0
0
Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya Wateja wa TBL, David Tarimo ( kushoto) akimuonyesha gari aina ya Renauld Kwid mshindi wa pili wa promosheni ya TBL Kumenoga Tukutane baa. Frank Nathan na mkewe ,Tumaini Patric,muda mfupi baada ya kumkabidhi gari katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya Wateja wa TBL,David Tarimo ( wapili kushoto) akimkabidhi kadi ya gari mshindi wa pili wa droo ya promosheni ya TBL Kumenoga,Frank Nathan mkazi wa Iringa wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam,wengine katika picha kutoka kulia ni Meneja chapa wa Konyagi na Wine Isaria Kilewo na Meneja masuala endelevu wa TBL Irene Mutiganzi na (wa kwanza kushoto) ni Tumaini Patric ,mke wa mshindi
Mshindi wa gari Frank Nathan na mkewe Tumaini Patric ndani ya gari lao.
Mshindi wa gari ,Frank Nathan na mke wake Tumaini Patric katika picha ya pamoja na maofisa wa TBL baada ya kukabidhiwa gari

--- Mkazi wa Iringa, Bw. Frank Nathan (38), ambaye wiki iliyopita alijishindia gari kupitia droo ya pili ya promosheni ya wateja ya kampuni ya TBL ijulikanayo kama ‘TBL Kumenoga, Tukutane Baa’ amekabidhiwa rasmi gari alilojishindia aina ya Renault KWID katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Akiongea kwa furaha baada ya kukabidhiwa gari alisema kuwa tangu apatiwe taarifa za kushinda, alikuwa anajiona kama anaota ila baada ya kukabidhiwa gari lake ndio ameamini kuwa amepata bahati ya kushinda zawadi kubwa ya gari mpya.

 “Nilipopigiwa simu nakufahamishwa kuwa nimeshinda sikuamini hadi niliposoma habari juu ya ushindi wangu kwenye vyombo vya habari na baadaye kupigiwa simu kutoka TBL, Ninayo furaha kubwa kwa ushindi huu, nitasherekea sikukuu ijayo ya Krismas na mwaka mpya nikiwa namiliki gari mpya, namshukuru Mungu ameniona kupitia promosheni hii”, alisema Nathan kwa furaha. 

Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya wateja wa TBL, David Tarimo, kwa niaba ya kampuni ya TBL alimpongeza mshindi huyo baada ya kumkabidhi gari na kutoa wito kwa wateja wote wa vinywaji vya TBL nchini, kuendelea kuichangamkia promosheni hii ili kuweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi kubwa ya gari mpya aina ya Renault KWID. 

“Tunayo furaha kubwa kumkabidhi zawadi yake mshindi wetu wa pili wa mwezi ambayo ni gari mpya, kwa sasa imebaki gari moja na zawadi nyinginezo nyingi kwa ajili ya wateja wetu watakaoshiriki promosheni hii hususani katika kipindi hiki tunachoelekea kwenye msimu za sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya” alisema Tarimo. Tarimo, na kuongeza kuwa, promosheni hii inafanyika kwenye mabaa katika siku za mwisho wa wiki yaani Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kupitia bia za Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite na Balimi Extra Lager. 

 Kwa upande wake, Meneja wa Ukuzaji wa Masoko wa TBL, Edith Bebwa, alisema promosheni inafanyika kwenye mabaa zaidi ya 5,000 nchini kote. “Wateja wetu wazidi kuitafuta bendera ya TBL Kumenoga, kwani ilipo bendera hii ndipo wateja na TBL wanapokutana katika promosheni. 

 Alifafanua zaidi kuwa ili kuingia kwenye droo ya kujishindia gari jipya kupitia promosheni hii ya ‘TBL Kumenoga, Tukutane Baa’ mteja atatakiwa kununua bia tatu kati ya Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite au Balimi Extra Lager kwenye promosheni, ambapo atapatiwa kuponi yenye namba, kisha anatakiwa kutuma namba hiyo kwa meseji kwenda 15451, hii ni kwa wateja wenye mitandao ya VODACOM, TIGO na AIRTEL. Kwa wateja wa mitandao mingine watatuma namba iliyo kwenye kuponi kupitia tovuti ya www.tblkumenoga.co.tz.

BENKI YA EXIM YANG'ARA TUZO ZA NBAA

$
0
0
Mkurugenzi Idara ya Fedha benki ya Exim, Bw Selemani Ponda (kulia) akipokea tuzo kwa niaba ya benki hiyo toka kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Bi Ashatu Kijaji baada ya benki kuwa miongoni mwa benki tatu bora kuwa na hati safi ya taarifa za fedha kwa upande wa mabenki nchini katika ukaguzi uliofanywa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa mwaka 2017. Tuzo hizo zilitolewa jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Air Tanzania's FIRST Airbus A220-300 (BCS3) in action in Montreal


WAZIRI UMMY ASHIRIKI MKUTANO MAALUM WA MAWAZIRI WA AFYA KUHUSU AFYA YA MAMA NA MTOTO NCHINI INDIA

$
0
0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza kwenye Mkutano Maalum wa 4 wa Mawaziri wa Afya kuhusu Afya ya Mama na Mtoto (Partnership for Maternal, Newborn and Child Health Forum 2018) uliofanyika New Delhi, India kuanzia tarehe 12 hadi 14 Desemba, 2018.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akisalimiana na Waziri Mkuu wa India, Mhe. Narendra Modi wakati wa ufunguzi wa Mkutano Maalum wa Mawaziri wa Afya uliofanyika katika jiji la New Delhi, India kuanzia tarehe 12 hadi 14 Desemba, 2018.
Picha ya pamoja ya Mawaziri wa Afya pamoja na Waziri Mkuu wa India, Mhe. Narendra Modi wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo
Picha ya pamoja ya Mhe.Waziri Ummy Mwalimu na ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mkutano Maalum wa Afya ya Mama na Mtoto jijini New Delhi, India. Wa pili kukia ni Mhe. Baraka Luvanda, Balozi wa Tanzania nchini India

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto, Mhe. Ummy Mwalimu akijadiliana jambo na Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda (kushoto} wakati wa Mkutano Maalum wa 4 wa Mawaziri wa Afya kuhusu Afya ya Mama na Mtoto

Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA, Marekani, Bibi Natalia Kanem wakati wa Mkutano Maalum wa Mawaziri wa Afya kuhusu Afya ya Mama na Mtoto uliofanyika New Delhi, India


WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO ASHIRIKI MKUTANO MAALUM WA MAWAZIRI WA AFYA KUHUSU AFYA YA MAMA NA MTOTO ULIOFANYIKA JIJINI NEW DELHI, INDIA KUANZIA TAREHE 12-14 DISEMBA, 2018.

Tanzania imeshiriki katika Mkutano Maalum unaojadili Afya ya Mama na Mtoto unaojulikana kama "4th Partnership for Maternal,Newborn and Child Health 2018" uliofanyika katika jiji la New Delhi, India kuanzia tarehe 12 hadi 14 Desemba,2018.

Katika Mkutano huu,Tanzania imewakilishwa na Mhe.Ummy Mwalimu,Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.Mkutano huu ulifunguliwa na Mhe.Shri Narendra Modi, Waziri Mkuu wa India tarehe 12 Desemba, 2018. Mkutano huu unawakutanisha pamoja Mawaziri wa Afya kutoka nchi mbalimbali duniani kwa lengo la kujadili changamoto zilizopo katika eneo la Afya ya Mama na Mtoto na kuweka mikakati ya pamoja ya kuzitatua changamoto hizo ili kuboresha upatikanaji wa huduma za Afya ya Mama na Mtoto.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Waziri Mkuu wa India alieleza mafanikio yaliyopatikana katika kupunguza vifo vya mama mjamzito na watoto wachanga kufuatia mikakati mizuri iliyowekwa na Serikali ya India na kuzitaka nchi washiriki kuweka mipango thabiti itakayotekelezeka katika kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Kwa upande wake, Mhe.Ummy Mwalimu alieleza hatua mbalimbali zilizochukuliwa katika kupunguza vifo vya mama na motto nchini Tanzania ikiwemo kuboresha utoaji wa huduma za afya katika ngazi za chini kwa kuboresha vituo vya Afya na kuajiri watumishi wapya kwenye maeneo yenye upungufu. Pia, ameeleza hatua nyingine zinazochuliwa na serikali ni kumlinda mwanamke kutokana na unyanyasaji wa jinsia ambapo madawati ya jinsia yamezinduliwa katika majeshi ya polisi na magereza ili kuhakikisha mwanamke analindwa wakati wote.

Kadhalika, Mhe.Ummy ameueleza mkutano huo mikatikati iliyopo nchini ya kuhakikisha uboreshaji na utoaji wa huduma za Afya ya Mama na Mtoto unakuwa endelevu, ambapo aliweka bayana mipango hiyo ni pamoja na Kuongeza bajeti ya fedha katika sekta ya Afya, kuimarisha huduma za afya ya Mama na Mtoto kuanzia ngazi ya jamii.

Mipango mingine ni kuimarisha huduma kwa kuboresha vituo vya afya na kuajiri watumishi wanaohitajika, kutoa elimu ya uzazi wa mpango kwa walengwa pamoja na kutoa huduma stahiki ili kupunguza na kumlinda motto kutokana na maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Suala jingine la msingi zaidi ni kuilinda jamii kwa kutoa elimu ya kutosha kuhusu magonjwa ya saratani hususani saratani ya mlango wa kizazi ambayo sasa ni tatizo kubwa kwa akina mama duniani kote.

AGPAHI ARIEL CAMP 2018 YAFUNGWA DAR

$
0
0
Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Habari wa TACAIDS Bw. Jumanne Issango akifunga Ariel Camp 2018 kwa niaba ya Mkurugenzi wa TACAIDS.

Kambi ya watoto na vijana inayosimamiwa na Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) maarufu kama Ariel Camp 2018’ iliyoshirikisha washiriki 50 kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara na Simiyu imefungwa leo Ijumaa Disemba 14,2018 jijini Dar es salaam.

Akifunga kambi hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI nchini (TACAIDS), Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Habari wa Tume hiyo Bw. Jumanne Issango aliipongeza AGPAHI kwa kuanzisha kambi hizo zinazolenga kuwapa watoto na vijana msaada wa kisaikolojia utakaowawezesha kukabialiana na changamoto zinazowakabili.

“Naishukuru AGPAHI kwa kutoa msaada huu wa kisaikolojia kwa watoto na vijana kwani huduma hiyo ni muhimu sana kwa afya na ustawi wao hasa ikizingatiwa kuwa changamoto hizo zinawaathiri  kimwili, kiafya, kijamii na kisaikolojia,” alisema Bw. Issango.

Aidha aliitaka jamii kubadilika na kuacha vitendo vya kunyanyapaa wanaoishi na maambukizi ya VVU huku akiwahamasisha watoto na vijana hao kutumia kwa usahihi dawa za kufubaza makali ya VVU ili kuimarisha afya zao.
“Ili kuishi maisha bora na kukamilisha ndoto zenu za baadaye nawakumbusha kuwa ARV ndiyo mpango mzima, Watu wasiotumia vizuri dawa hizi afya zao zimekuwa zikitetereka na kushambuliwa na magonjwa nyemelezi na hata kufa. Kamwe msiache kutumia dawa kwa sababu yoyote ile,” alisisitiza.

Pia aliiomba AGPAHI kwa kushirikiana na watoa huduma na wadau mbalimbali kuelimisha wananchi kuhusu VVU na maambukizi yake kwani imedhihirika kuwa bado jamii haina elimu ya kutosha kuhusu VVU na UKIMWI. "Kudhihirika huku kunatokana na unyanyapaa unaoendelea katika jamii."

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taarifa za Kimkakati wa AGPAHI, Dk. Boniface Idindili, aliziomba halmashauri za wilaya kutenga bajeti kwa ajili ya kuanzisha klabu za vijana na watoto wanaoishi na VVU na kupata huduma za tiba na matunzo katika vituo vya afya ili wengi zaidi waweze kupata msaada wa kisaikolojia.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Idindili alisema, “Tunaiomba serikali iweke madawati maalumu mashuleni na kwenye vyuo kwa ajili ya kusaidia watoto na vijana wanaoishi na VVU, Vijana wengi hulazimika kukabiliana na changamoto zao kimya kimya kwa kukosa msaada na wakati mwingine hushindwa kuzimudu.”

Pia alishauri vyuo vya ufundi stadi vya VETA kutoa upendeleo maalum kwa vijana wanaoishi na VVU kujiunga navyo ili kuwawezesha kujitegemea na kukidhi mahitaji yao ya kila siku.

Nao washiriki wa Kambi ya Ariel walisema kuwa kipindi chote wakiwa kambini wamefundishwa mambo mengi yaliyowasaidia kuwajenga kiakili na kimwili.

 Katika risala yao kwa mgeni rasmi, walitaja baadhi ya mambo hayo kuwa ni pamoja na ujasiriamali, matumizi sahihi ya dawa, ukatili wa kijinsia na unyanyapaa.

Mbali na kubadilishana mawazo na kupata marafiki wapya, washiriki wamecheza michezo mbalimbali na kutembelea Mji wa Kihistoria wa Bagamoyo ili kujifunza kiundani historia ya Tanzania. 
Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Habari wa TACAIDS Bw. Jumanne Issango akizungumza katika ukumbi wa Serene Beach Resort wakati akifunga Ariel Camp 2018 kwa niaba ya Mkurugenzi wa TACAIDS. Kushoto ni Mkurugenzi wa Taarifa za Kimkakati wa AGPAHI, Dk. Boniface Idindili,kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za mama na mtoto AGPAHI, Dk. Akwila Temu.
Washiriki wa Ariel Camp wakimsikiliza mgeni rasmi.
Mkurugenzi wa Taarifa za Kimkakati wa AGPAHI, Dk. Boniface Idindili akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI wakati wa kufunga Ariel Camp 2018.
Waliokaa ni washindi wa shindano la Mr & Miss AGPAHI Ariel Camp wakiwa katika picha ya pamoja na jaji Lugano Maclean (wa kwanza kulia) na kiongozi wa washiriki wa shindano la Urembo 'Mr & Miss Ariel Camp' Agnes William ( wa kwanza kushoto) na washiriki wa shindano hilo. 
Keki ya upendo kwa ajili ya washiriki wa Ariel Camp 2018.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Habari wa TACAIDS Bw. Jumanne Issango akimlisha keki mshiriki wa Ariel Camp 2018.
Miss Ariel Camp 2018 akimlisha keki Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Habari wa TACAIDS Bw. Jumanne Issango.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Habari wa TACAIDS Bw. Jumanne Issango akikabidhi zawadi ya begi kwa mshiriki wa Ariel Camp 2018. Mabegi hayo ya shule yamekabidhiwa kwa washiriki wote 50 wa Ariel Camp 2018.
Kijana akifurahia baada ya kupewa zawadi ya begi la shule.
Watoto wakiwa wamekaa na mabegi yao.
Washindi wa shindano la Mr & Miss Ariel Camp 2018 wakifuata zawadi kwa mgeni rasmi.
Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Habari wa TACAIDS Bw. Jumanne Issango akikabidhi zawadi ya saa za ukutani kwa washindi wa shindano la Mr & Miss Ariel Camp 2018.
Vijana na watoto wakiwa na walezi wao waliojichora rangi usoni.
Latifa Abdallah kutoka Taasisi ya Babawatoto akitoa burudani ya kuzungusha meza kwa miguu.
Kijana wa Babawatoto Debora  Dickson akitoa burudani ya sarakasi.
Mtoto akielezea kuhusu mchoro aliochora  kwa Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Habari wa TACAIDS Bw. Jumanne Issango na Mkurugenzi wa Taarifa za Kimkakati wa AGPAHI, Dk. Boniface Idindili.
Picha ya pamoja mgeni rasmi na washiriki wa Ariel Camp 2018.
Picha ya pamoja Mmiliki wa Hoteli ya Serene ambapo ndipo kambi ya vijana na watoto imefanyika, Dk. Moses Mkonye (wa pili kulia) na watoto wawili aliojitolea kuwasomesha na Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Habari wa TACAIDS Bw. Jumanne Issango (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Huduma za mama na mtoto AGPAHI, Dk. Akwila Temu (wa kwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Taarifa za Kimkakati wa AGPAHI, Dk. Boniface Idindili (wa kwanza kulia).  Vijana wakipiga picha ya kumbukumbu baada ya Ariel Camp 2018 kufungwa. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog.

Biteko afungua Ofisi ya Madini Mahenge mkoani Morogoro

$
0
0
Wachimbaji madini Mahenge mkoani Morogoro watakiwa kulipa madeni yao


Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Ofisi ya Afisa Migodi Mkazi Mahenge-Ulanga mkoani Morogoro, jana Disemba 14, 2018. Wanaoshuhudia ni viongozi mbalimbali wa Serikali, Tume ya Madini pamoja na wachimbaji madini.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akisaini kitabu cha wageni baada ya kufungua ofisi ya Afisa Migodi Mkazi Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro. Aliyesimama ni mbunge wa Jimbo la Ulanga, Goodluck Mlinga.
Mkuu wa Wilaya Ulanga, Ngolo Malenya akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Afisa Migodi Mkazi wilayani humo.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa tatu), Mkuu wa Wilaya Ulanga, Ngolo Malenya (wa pili kulia),  Kamishna wa Madini kutoka Tume ya Madini, Dkt. Athanas Macheyeke (wa kwanza kushoto), Mbunge Jimbo la Ulanga, Goodluck Mlinga (wa pili kushoto) pamoja na Afisa Migodi Mkazi Wilaya ya Ulanga, Tandu Jilabi (wa kwanza kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa ofisi hiyo.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo wa Serikali, Tume ya Madini pamoja na wachimbaji madini wilayani Ulanga.
Jengo la Ofisi ya Afisa Migodi Mkazi Mahenge-Ulanga mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza na wachimbaji madini katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mahenge wilayani Ulanga.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na Serikali.
Viongozi mbalimbali wakiwemo wa CCM pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ulanga.
Wananchi na wachimbaji madini Mahenge wilayani Ulanga wakifuatilia mkutano huo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

VIJIJI VILIVYOPAKANA NA MKUZA WA BOMBA LA GESI ASILIA VYAPEWA ELIMU YA ULINZI NA USALAMA WA BOMBA

$
0
0
Wananchi wa Kijiji cha Somanga Simu wakiwa katika mkutano wa hadhara kusikiliza masuala yahusuyo usalama na ulinzi wa bomba la gesi yaliyokuwa yakizungumzwa na wataalamu kutoka TPDC 
Wananchi wa Kijiji cha Kiwanga wakiwa katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka TPDC baada ya kupata elimu kuhusu masuala ya usalama na ulinzi wa miundombinu ya gesi asilia. Na Mwandishi Wetu.

Kutokea kusini mwa Tanzania katika mikoa ya Lindi na Mtwara, limelala bomba lenye kipenyo cha inchi 36 na urefu wa kilometa 551 kuelekea jijini Dar es Salaam. Bomba hili lina uwezo wa kupitisha gesi asilia futi za ujazo milioni 784 kwa siku na lina matoleo yapatayo 16 ambayo yamewekwa kimkakati kuruhusu uunganishwaji wa gesi kwa wateja maeneo bomba linapopita. Bomba hili linapita katika vijiji takribani 136 ambapo suala la ulinzi limefanywa kuwa ni la kushirikiana kwa kuwawezesha wananchi wa vijiji husika kutoa huduma ya ulinzi katika mkuza wa bomba. 

Kwa kuzingatia kwamba suala la elimu na uhamasishaji ni suala endelevu, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ambalo ndio msimamizi wa miundombinu hiyo limekuwa na utaratibu wa kutembelea vijiji husika na kutoa elimu juu ya umuhimu wa miundombinu hiyo kwa Taifa na namna ya kung’amua hatari na kutoa taarifa kwa mamlaka husika. 

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara na wanakijiji wa Somanga Simu, Afisa Uhusiano wa TPDC, Ndg. Malik Munisi alisema “TPDC inatambua mchango wa kizalendo unaotolewa na wakazi wa maeneo bomba la gesi linapopita, inatambua kwamba mlinzi wa kwanza wa miundombinu hii ni mwananchi na hivyo tutaendelea kushirikiana nanyi kila wakati kuhakikisha miundombinu hii inaendelea kuwa salama na kudumu kwa kipindi kirefu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho”. 

Nae Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka TPDC, Ndg. Oscar Mwakasege alieleza namna ambavyo TPDC hujihusisha na dhana ya uwajibikaji kwa jamii (Corporate Social Responsibility-CSR) na kusisitiza kwamba maeneo ya kipaumbele katika kuwajibika kwa jamii ni masuala yahusuyo afya, elimu, maji na michezo. 

Ndg. Mwakasege alitoa mfano wa maeneo ambayo tayari TPDC imewajibika kwa jamii kama vile ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Marendego, ujenzi wa matundu ya vyoo shule ya msingi Kilwa Kivinje, kisima cha maji safi kijiji cha Njia Nne na maeneo mengine lukuki ambayo miundombinu ya gesi ipo au inapita. 

Nae Mwenyekiti wa Kijiji cha Somanga Simu, Ndg. Athumani Mkumbaya alionyeshwa kufurahishwa kwa namna ambavyo TPDC na Songas wanavyojitahidi kuwashirikisha wanakijiji katika ulinzi wa bomba na pia kuwasaidia katika changamoto za kijamii zinazolenga kukuza ustawi bora wa jamii. 

Akizungumza wakati wa kikao cha hadhara, Ndg. Mkumbaya alisema “pamoja na michango mbalimbali tunayoipata kutoka kwa watu wa gesi, ombi letu kubwa kwao kwa sasa ni ujenzi wa shule ya sekondari, watoto wetu maeneo ya Somanga wanalazimika kwenda umbali mrefu kufika shule ya sekondari ambayo iko kata ya Muhoro”. 

Nae Ndg. Elias Muganda, Afisa Usalama Mwandamizi kutoka GASCO anasema “TPDC kupitia kampuni tanzu ya GASCO imeingia mikataba ya ulinzi baina yake na vijiji 136 linapopita bomba, katika mikataba hii, kijiji kina majukumu makuu matatu, kwanza kusafisha mkuza, pili kulinda mkuza dhidi ya hatari na wavamizi na tatu kutoa taarifa pale kunapokuwa na jambo linaloenda kinyume na taratibu”. Ndg. Muganda anaeleza kwamba zoezi la kupita vijijini na kuwakumbusha juu ya masuala ya usalama wa bomba na faida za miundombinu hiyo ni endelevu kwani bila kufanya hivyo binadamu husahau na yakitokea madhara hasara itakuwa ni ya Taifa zima. 

TPDC kupitia kampuni tanzu ya GASCO inasimamia miundombinu ya gesi asilia ambayo inajumisha mitambo ya kuchakata gesi iliyopo Madimba (Mtwara) na Songo songo (Lindi) pamoja bomba la kusafirisha gesi hiyo kutoka inapozalishwa hadi sokoni. 

Kwa mujibu wa taarifa kutoka TPDC, takribani megawati 831 za umeme katika gridi ya Taifa zinazalishwa na gesi asilia, hivyo suala la ulinzi wa miundombinu ya gesi ni suala ambalo linafanywa kwa ueledi wa hali ya juu kwa kuzingatia umuhimu wa kimkakati ambao mradi huu unabeba.

BENKI KUU KUHAKIKI WAFANYAKAZI WA BENKI ZOTE NCHINI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inatarajia kufanya uchambuzi na kuwakagua wafanyakazi wote wanaofanya kazi katika benki zote nchini.

Hayo yamesemwa na Gavana wa Benki Kuu Profesa Florens Luoga wakati akifunga semina ya waandishi wa habari za fedha na uchumi iliyoandaliwa na BoT Mjini Dodoma Profesa Luoga amesema uamuzi huo unalenga kulinda fedha za wananchi ambazo wameweka benki pamoja na kuondoa wafanyakazi wasio waaminifu.

"Benki Kuu tunao mkakati wa kuhakikisha tunafanya ukaguzi ambao lengo lake litakuwa kuhakikisha wanapatikana wafanyakazi waliowaamini na wenye uwezo wa kulinda fedha za wateja.Tunahitaji kuona wafanyakazi wa benki ambao wanatambua na kuheshimu misingi ya kaziza benki,"amesema Profesa Luoga na kuongeza ni muhimu kwa BoT kulinda za wateja.

Amefafanua siku za nyuma kulikuwa na baadhi ya fedha za wateja wadogo zilizohifadhiwa kwenye baadhi ya benki, ziliibwa kwa ujanja na wafanyakazi wa benki hizo jambo ambalo ni kinyume cha sheria. Ameongeza kiongozi mzuri wa benki lazima awe mwaminifu na ndio maana BoT wanataka kuhakiki wafanyakazi wa benki zote nchini.

Amefafanua huu ni wakati wa kuwa na wafanyakazi wa benki amabo ni sahihi kwa kazi hiyo, hivyo kupitia uchambuz wa kina ambao utafanyika watabaini wafanyakazi waliopo na uwezo wao na waamini kazini.

Profesa Luoga ameeleza namna ambavyo kuna baadhi ya wateja wa benki ambao si waaminifu walivyokuwa wanatengeneza mazingira ya kujipatia fedha ambapo walikuwa tayari kutafuta watu na kuwajazia fomu na kisha kuwapatia mkopo.

"Anakuja mfanyakazi wa benki fulani anakwambia fungua akaunti ili upate mkopo, baadae anakupa mkopo wa Sh.milioni 50 halafu yeye anachukua Sh.milioni 20 na kukuachia Sh.milioni 30.Lazima ifike wakati tuwe na wafanyakazi waamini katika sekta ya kibenki,"amesema. Amesema BoT imejipanga kwa kila hali kuhakikisha inalinda haki za wateja ikiwamo kulinda fedha zao kwenye benki huku akieleza kuwa wanataka huduma za kifedha zimfikie mwananchi kila mahali na bila kikwazo.
 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Profesa Florens Luoga akizungumza na waandishi wa habari za fedha na uchumi wakati akifunga mafunzo yaliyoandaliwa na BoT kwa waandishi hao
 Mtunza Muda katika mafunzo ya semina ya waandishi wa habari za fedha na uchumi Bakari Kimwanga(aliyesimama) akitoa shukrani kwa Gavana wa BoT pamoja na maofisa wengine wa benki hiyo kwa kuandaa mafunzo ya habari za fedha na uchumi
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga akiwa ameshikana mkono na Mwakilishi wa Michuzi Blog Said Mwishehe baada ya kufunga mafunzo ya uandishi wa habari za fedha na uchumi iliyofanyika BoT tawi la Dodoma.Wanaoshuhudia ni sehemu ya maofisa wa benki hiyo na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images