Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live

Jumia yazindua BOOM BAMIZA, yakabidhi pikipiki na luninga kwa wateja

$
0
0
Jumia imewakabidhi wakazi wa jijini Dar es Salaam, Bw. Johnson Kiama na Dismas Kamalamo zawadi za pikipiki na luninga mpya ya kisasa walizojishindia kupitia shindano la ‘Treasure Hunt.’

Shindano hilo lilikuwa likifanyika kila siku ya Ijumaa kupitia kampeni kubwa ya mauzo ya mwaka ya Jumia inayokwenda kwa Black Friday. Kampeni hiyo ambayo ilianza Novemba 16 na kufikia ukomo Ijumaa iliyopita ya Desemba 7, imewawezesha wateja kufanya manunuzi yao ya msimu huu wa sikukuu kwa ofa na punguzo kubwa la bei mpaka 70%!

Zawadi zote mbili za pikipiki na luninga zilifichwa kwenye mtandao wa Jumia ambapo wateja walitakiwa kuzisaka na kukabidhiwa kwa punguzo la asilimia 99 mara baada ya kuzipata. Zoezi hilo lilifanyika kupitia njia ya App ya Jumia inayopatikana kwenye simu zote za iPhone (Apple Store) na Android (Google Play Store). Dhumuni lilikuwa ni kuwawezesha wateja wengi zaidi, ambao wanamiliki simu za kisasa za mkononi, kushiriki mahali popote na muda wowote walipo.

Pikipiki hiyo aliyokabidhiwa mshindi, aina ya Skymark, inauzwa kwa shilingi 1,850,000 katika mtandao wa Jumia. Lakini mshindi amekabidhiwa kwa kulipia shilingi 18,500 tu ambayo ni sawa na punguzo la asilimia 99!Huku naye mshindi wa luninga mpya na ya kisasa aina ya Bruhm yenye ukubwa wa inchi 32 yenyewe inauzwa kwa shilingi 570,000 kwenye mtandao wa Jumia. Lakini mshindi amekabidhiwa kwa kulipia shilingi 5,700 tu ambayo ni sawa na punguzo la asilimia 99!

Akielezea namna atakavyoitumia zawadi yake ya pikipiki mara baada ya kukabidhiwa, Bw. Johnson Kiama, amesema kuwa, “siamini kama leo hii nimekabidhiwa hii pikipiki maana ilinichukua muda mrefu kuipata. 
 
Mimi ni mteja wa muda mrefu wa Jumia tangu kipindi cha nyuma ikiwa inajulikana kama Kaymu. Huwa naitumia kununua bidhaa kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya nyumbani na siku hiyo mpaka nafanikiwa kuipata pikipiki hii nilikuwa naweka oda mtandaoni,” alisema na kumalizia, “naitumia kwa shughuli zangu za kiofisi kwa sababu tunajihusisha na huduma za kuchapisha vifaa mbalimbali kwa ajili ya shughuli za kimasoko na matangazo za makampuni mbalimbali.”

Naye kwa upande wake mshindi wa luninga, Bw. Dismas Kamalamo, ameelezea, “ilinichukua takribani lisaa limoja na dakika 40 mpaka kufanikiwa kuipata luninga hii. Kuna muda nilitaka kukata tamaa ukizingatia ni maelfu ya wateja wengine nao walikuwa wanashiriki. Kwa hakika hii ni zawadi bora kabisa katika msimu huu wa sikukuu. Nitaitumia luninga hii kwa matumizi yangu ya nyumbani ukizingatia ni ya kisasa kabisa. Bado siamini kama nimeweza kushinda na kuinunua kwa bei hii.”

Akifafanua kuhusu zoezi zima la ‘Treasure Hunt’ na kampeni iliyomalizika ya Black Friday kwa ujumla, Meneja Mahusiano ya Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey ameeleza kuwa, “ni kawaida yetu Jumia kuja kitofauti kwenye kila kampeni tunayoifanya. Mwaka huu tulikuwa na Black Friday kwa Ijumaa nne mfululizo kuanzia Novemba 16 mpaka Desemba 7. Tofauti na mwaka jana ambapo ilikuwa ni kwa Ijumaa moja tu ya Novemba 23. Na kabla ya mwaka huu kuisha tungependa kufunga mwaka kwa kuwazawadia wateja wetu ”

“Tukiwa tumebakiza wiki chache kabla ya kuumaliza mwaka huu wa 2018, Jumia isingependa kuwaacha Watanzania hivi hivi. Siku ya kesho tarehe 12, mwezi wa 12 kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa moja usiku tutakuwa na kampeni ya mauzo ya siku moja tu au ‘Flash Sales’ ’itakayokwenda kwa jina la ‘ BOOM BAMIZA.’ Tutakuwa na mauzo ya bidhaa 24 tofuati kwenye ‘Flash Sales’ kwa siku nzima. Kila lisaa litakuwa na bidhaa mbili tofuati mtandaoni kwa punguzo la mpaka 70%,” alisema Bw. Geofrey

“Mauzo ya bidhaa haya yatafanyika kote kwenye mtandao wetu wa Jumia lakini pia kwa kupitia App yetu unayoweza kuipakua kwenye simu yako ya mkononi. Bidhaa zitakuwa ni tofauti ili kukidhi mahitaji ya watu wote kama vile: simu za mkononi kama vile Samsung S9, Nokia, Infinix Note 5 Stylus na matoleo mapya kabisa ya Tecno 11 na X Pro. 
 
Vilevile kutakuwa na bidhaa za jikoni na nyumbani kwa ujumla kama vile vyombo vya kupikia, kufulia, friji, luninga na viyoyozi (Air Conditioner) Ningependa kuwasihi watanzania wote kukamilisha manunuzi yao ya sikukuu na ofa hii ya BOOM BAMIZA kabla hawajaenda mapumzikoni. Kama Jumia, tunawaahidi wateja wetu kuendelea kuwa wabunifu kwa kuja na ofa mbalimbali zenye manufaa kwao na kuleta mapinduzi ya manunuzi kwa njia ya mtandaoni nchini,” alihitimisha Meneja Mahusiano ya Umma wa Jumia Tanzania.
 Meneja Mahusiano ya Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari jijini Dar leo wakati wakikabidhi  wakazi wawili wa jijini Dar es Salaam, Bw. Johnson Kiama na Dismas Kamalamo zawadi za pikipiki na luninga mpya ya kisasa walizojishindia kupitia shindano la ‘Treasure Hunt.’
 Meneja Mahusiano ya Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey akimkabidhi  mbele ya Waandishi wa habari,Bw. Johnson Kiama luninga mpya ya kisasa aliyojishindia kupitia shindano la ‘Treasure Hunt.’
Meneja Mahusiano ya Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey akimkabidhi  ufunguo wa piki piki Dismas Kamalamo mbele ya Waandishi wa habari, aliyojishindia kupitia shindano la ‘Treasure Hunt.’

KAMISHNA UTAWALA NA FEDHA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI AAPISHWA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye (kushoto) akimvua cheo cha zamani na kumvisha cheo kipya cha Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CF) Mbaraka Semwanza katika ukumbi wa mikutano Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi Dar es salaam mapema leo asubuhi tarehe 11/12/2018. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)
Kamishna (CF) Mbaraka Semwanza akiapa baada ya kuvishwa cheo kipya cha Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika ukumbi wa mikutano Makao Makuu ya Jeshi hilo mapema leo asubuhi tarehe 11/12/2018.
Kamishna wa Utawala na Fedha (CF) Mbaraka Semwanza (kushoto) akipokea nyaraka mbalimbali za ofisi ya Utawala na Fedha kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye (kulia), baada ya kuapishwa katika ukumbi wa mikutano Makao Makuu ya Jeshi hilo mapema leo asubuhi tarehe 11/12/2018.
Makamishna, Wakuu wa Vitengo, Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakishuhudia kuapishwa kwa Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi hilo, katika ukumbi wa mikutano Makao Makuu ya Jeshi hilo mapema leo asubuhi tarehe 11/12/2018.

Vodacom Tanzania yawatunukia watumiaji wa mtandao wake bomba kwa Pointi za Tuzo zenye thamani ya shilingi bilioni 1

$
0
0
Vodacom, kampuni ya simu nambari moja nchini, inagonga kengele za shangwe katika msimu huu wa sikukuu kwa kuwatunukia wateja wake pointi za Tuzo zenye thamani ya Shilingi bilioni 1 kama sehemu ya mpango wa kampuni kuwashukuru wateja wao

Programu hii ni ya kwanza kabisa iliyoletwa na kumpuni hiyo ambayo inawapatia wateja wake pinti za tuzo kila waongezapo salio au kufanya miamala ya M-Pesa. Wateja wanaweza kutumia pointi hizo kwa kuzibadili kupitia waleti zao za M-Pesa, kununua bando, na pia kwa kununua bidhaa mbalimbali katika maduka ya Vodacom.

“Mapato ya Vodacom Tanzania yaliongezeka kwa asilimia 6 katika mwaka huu, na ukuaji huu umechangiwa sana na wateja wetu. Hivyo Pointi za Tuzo ni njia ya kuonyesha shukrani zetu kwa watumiaji wetu na kwa moyo wa kutoa, tumeamua kufanya jambo la ziada katika msimu huu wa sikukuu kwa kuwatunuku wateja wetu Pointi za Tuzo zenye thamani ya shilingi bilioni 1,” alisema Hisham Hendi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji. “Ninawahimiza wateja wetu kuishi maisha ya ki-Tuzo, kununua muda wa maongezi na kufanya miamala mingi kadri inavyowezekana katika M-Pesa hasa katika kipindi hiki cha sikukuu na kujipatia pointi hapo hapo kila wafanyapo miamala hiyo,” aliongeza Hisham.

Wateja hao wanatunukia Pointi za Tuzo 50 kwa kila Shilingi 500 wanayotumia kununua salio. Pointi hizi za Tuzo zinaweza kulimbikizwa hadi miezi 12 tangu mtu aanze kujikusanyia na baada ya miezi hiyo 12 zisipotumiwa muda wake huisha. Wateja wa Vodacom wanaweza pia “Kulipa kwa Pointi” moja kwa moja kwa wafanyabiashara wanaopokea M-Pesa, kwa kupiga *149*01#>TUZO>TUZO POINTS>Vuna Pointi> (Nunua bando/Lipa/Badili kwa M-Pesa).

“Mwaka mzima, wateja wetu wamekuwa ndiyo walengwa na kiini cha ubunifu wetu – Vodacom Tanzania tumedhamiri kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma bora kabisa,” alimalizia Hisham. 

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi (katikati) akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam juu ya kuwatunuku watumiaji wa mtandao wa Vodacom points za Tuzo zenye thamani ya shilingi bilioni 1 katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu na mwaka mpya yenye kaulimbiu 'Nabaki mulemule na Vodacom'. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni hiyo Rossalyn Mworia na Kaimu Mkurugenzi wa biashara, Linda Riwa .
Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC Rossalyn Mworia, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, juu ya kuwatunuku watumiaji wa mtandao wa Vodacom, points za Tuzo zenye thamani ya shilingi bilioni 1 katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu yenye kauli mbiu “Nabaki mulemule na Vodacom.” Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi na Kaimu Mkurugenzi wa biashara, Linda Riwa .

LUGOLA ATANGAZA KUFUNGUA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO JIMBONI KWAKE MWIBARA, MARA

$
0
0
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola ametangaza kufungua miradi mikubwa mitano ya maendeleo jimboni kwake, Wilayani Bunda, Mkoa wa Mara ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa katika mikutano yake kwa wananchi wa jimbo hilo siku za nyuma. Lugola amesema tayari mipango imepangwa katika kufanikiwa miradi hiyo inafunguliwa jimboni humo ikiwa ni hatua ya kuondoa umaskini kwa wananchi na kuliletea mafanikio makubwa jimbo hilo na Wilaya ya Bunda kwa ujumla, 

Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Namhula, Wilayani humo, leo, Lugola alisema mradi mkubwa wa Maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kwa ajili ya kumwagilia mazao mbalimbali ikiwemo zao la mpunga katika Bonde la Namhula tayari wataalamu wamefika kulipima bonde hilo pamoja na kuanza mchakati wa mradi huo, pia uwepo wa maji hayo yatasaidia kumwagilia mazao mengine ya nafaka jimboni humo. 

“Mradi mwingine ni wa ufugaji wa kuku wa kienyeji na tuna mashine kubwa za kuangulia vifaranga, maandalizi yapo tayari na eneo la ufugaji huo utakua shule ya Msingi Magunga Kata ya Neluma, pia mradi wa ufugaji wa ng’ombe nyati na ufugaji huo pia utafanyika Sekondari ya Neluma katika Kata hiyo hiyo, na pia tutakuwa na ufugaji wa samaki katika mabonde,” alisema Lugola.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto) akizungumza na Wananchi wa Kata ya Namhula, Jimboni humo, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, leo. Lugola alitangaza kufungua miradi mikubwa ya maendeleo jimboni humo hivi karibuni. Kulia ni Mfanyabiashara wa Chakula cha Samaki cha Aluzola, Saimon Katolilo, ambaye aliitwa na Mbunge huyo kutoa elimu kuhusu bidhaa hiyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola akizungumza na viongozi wa Kata ya Muranda, Jimboni humo, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, leo. Lugola alitangaza kufungua miradi mikubwa ya maendeleo jimboni humo hivi karibuni. Kulia ni Diwani wa Kata hiyo, Jogolo Biswalo, na kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Muranda, Juma Mapole. 

SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA JAJI MKUU WILAYANI KONGWA

$
0
0
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai ambae pia ni mbunge wa Jimbo la Kongwa akizungumza jambo katika Kikao kilichoendeshwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Prof. Ibrahim Hamis Juma kwa Watendaji wa Mahakama ya Wilaya ya Kongwa.
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Prof. Ibrahim Hamis Juma wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji mbalimbali wa Wilaya ya Kongwa.
pika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai ambae pia ni mbunge wa Jimbo la Kongwa akizungumza jambo katika Kikao kilichoendeshwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Prof. Ibrahim Hamis Juma kwa Watendaji wa Mahakama ya Wilaya ya Kongwa.

BENKI KUU YATAJA FAIDA YA DHAMANA ZA SERIKALI KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU

$
0
0

Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha Benki Kuu ya Tazania Bw. Alexander Nw'winamila akitoa mada ya uuzaji wa Hati Funagani na Amana za Serikali katika semina ya waandishi wa habari za Fedha na Uchumi inayofanyika jijini Dodoma katika tawi la Benki Kuu ya Tanzania BoT Dodoma ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo.

Bi. Zalia Mbeo Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki (BoT) akitoa mchango wake katika semina hiyo kuhusu mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.
Mshauri wa Benki Kuu ya Tanzania BoT tawi la Dodoma akifafanua jambo katika semina hiyo inayoendelea jijini Dodoma.


Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mada zinazotolewa na wataalam wa Benki Kuu ya Tanzania.
Vick Msima Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki akifuatilia mjadala katika semina hiyo.
Picha mbalimbali zikionyesha Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika semina hiyo.
Mwanablog kutoka Fullshangweblog Bwana John Bukuku akiwa katika semina hiyo.

Meneja Kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania BoT akitoa mada kuhus hatua za kuimarisha usimamizi wa Taasisi za fedha.Bw. Nassor Omary.


Baadhi ya wanahabari wakijadiliana jambo katika semina hiyo.
.

Na Said Mwishehe Globu ya Jamii Dodoma

WATANZANIA wameshauriwa kushiriki kikamilifu katika minada ya dhamana za Serikali kwani faida zake ni kubwa kwa Taifa ikiwamo kufanya shughuli za maendeleo kwa kutumia fedha zake za ndani.

Hayo yamesemwa leo Mjini Dodoma na Mkurugenzi wa Masoko na Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Alexander Ng'winamila wakati akiwasilisha mada katika mafunzo kwa waandishi wa habari za uchumi na fedha yalioandaliwa na BoT kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuandika habari za fedha na uchumi.

Akizungumza wakati akitoa mada inayohusu uwekezaji katika dhamana za Serikali; faida zake kwa Taifa na wawekezaji ambapo pamoja na mambo mengine amezungumzia umuhimu wa wananchi kushiriki kikamilifu kwenye midana ya dhamana za Serikali.

Amesema ametoa ombi kuendelea kuhamasisha kutolewa kwa elimu kwa umma ili waweze kushiriki kikamilifu na hatimaye kuifanya serikali iweze kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa fedha za ndani."Ombi letu kwa vyombo vya habari tunaomba muendelee kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa kushiriki kwenye dhamana za Serikali.

Kuna faida nyingi na mojawapo ushiriki wao utawezesha Serikali kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kutumia fedha za ndani badala ya kwenda kukopa nje ya nchi,"amesema.

Akifafanua zaidi zinazopatikana kwenye dhamana za Serikali ni kusaidia Serikali kugharamia bajeti iwapo kutakuwa na upungufu wa kibajeti, kupata fedha za kuendeshea miradi ya maendeleo , kusimamia ujazi wa fedha katika uchumi, husaidia kudhibiti mfumuko wa bei , huchagia uwepo wa soko la upili na husaidia kuhamasisha utafutaji wa mitaji kwa taasisi zingine.

Pia amesema hutoa fursa za uwekezaji ,hivyo kuwepo kwa ushindani katika uwekezaji mbalimbali na kusaidia kupatikana kwa riba zinazoaminia na soko huku akieleza kwa mwananchi wa kawaida faida

za kushiriki ni nyingi kwani ni sehemu salama kutokana na ukweli kwamba Serikali haitarajiwi kukiuka mategeo ya wadai wake wakati wa malipo.

Ametaja faida nyingine dhamana za Serikali zinahamishika hivyo mwekezaji anaweza kuuza muda wowote.Pia dhamana za Serikali zinaweza kutolewa kama dhamana kwa ajili ya mikipo na faida nyingine ni kwamba dhamana za Serikali zina kiwango cha faida inayoridhisha."Tunaendelea kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye

dhamana za Serikali kwa maendeleo ya Taifa letu."

Kuhusu midana ya dhamana za Serikali amesema ipo ya aina mbili ambapo kuna mnada wa muda mfupi ambao ni wa mwaka mmoja na mnada wa dhamana za Serikali wa muda mrefu ambao unaanzia miaka miwili mpaka miaka 20.

Pia amesema ili mwekezaji aweze kushiriki katika minada ya dhamana za Serikali ni lazima awe na akaunti ya uwekezaji katika dhamana za Serikali na kwamba ufunguzi wa akaunti ya dhamana za Serikali hufanyika kupitia kwa mawakala walioidhinishwa ambao huwasilisha.

"Wakati wa kufungua akaunti kuna taarifa muhimu ambazo zinahitaji zikiambatanishwa na kitambulisho halali kinachotambulika na mamlaka za nchi pamoja na namba ya mlipa kodi(TIN)"amefafanua. Ng'winamila amesema fomu za kujiunga zinapatikana kupitia mawakala waliopo nchini pamoja na kwenye tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania ambapo ametumia nafasi hiyo kufafanua unapozungumzia dhamana za Serikali kwa lugha rahisi ni kwamba Serikali inakopa kwa wananchi wake.

BENKI YA NMB KUWAZAWADIA SHILINGI MILIONI 100 WATEJA WAKE!

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Boma Raballa akizungumza na wanahabari Dar es Salaam leo (hawapo pichani) kuhusiana na kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata', ambapo wateja wanaofanya malipo mbalimbali kwa kutumia mfumo huo watajishindia fedha taslimu, simu janja pamoja na safari ya kwenda mapumzikoni Dubai. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki na Mauzo wa NMB, Omari Mtiga.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Boma Raballa (katikati) akizungumza na wanahabari Dar es Salaam leo (hawapo pichani) kuhusiana na kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata', ambapo wateja wanaofanya malipo mbalimbali kwa kutumia mfumo huo watajishindia fedha taslimu, simu janja pamoja na safari ya kwenda mapumzikoni Dubai. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki na Mauzo wa NMB, Omari Mtiga.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki na Mauzo wa NMB, Omari Mtiga (kushoto) akifafanua jambo kwa wanahabari katika mkutano huo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Boma Raballa akifuatilia.
Mkutano na wanahabari ukiendelea Ofisi Kuu za Benki ya NMB, jijini Dar es Salaam leo.



BENKI ya NMB imezinduwa kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata', ambapo wateja wanaofanya malipo mbalimbali kwa kutumia mfumo huo watajishindia fedha taslimu, simu janja pamoja na safari ya kwenda mapumzikoni Dubai.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Boma Raballa alisema katika kampeni hiyo zaidi ya shilingi milioni 100 zitashindaniwa.Alisema takribani wateja 200 wa NMB ambao watafanya malipo kwa mfumo wa 'NMB Mastercard au 'NMB Masterpass' watakuwa kwenye uwezekano wa kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo ile kubwa ya kujishindia safari ya mapumziko iliyolipiwa kila kitu kwenda Dubai ukiwa na mwenza wako kwa siku nne.

Aliongeza kuwa shindano hilo litaendeshwa kwa miezi miwili kuanzia leo , huku likiwa na lengo la kuwahamasisha wateja wetu kutumia 'NMB MasterCard' kulipia huduma na bidhaa kwenye vituo vya malipo hayo (POS) au malipo kutumia mtandao (E-commerce). Aidha wateja wa NMB wanaofanya malipo pia kwa kutumia 'NMB MasterPass QR pia wanaingia katika kampeni hiyo.

"Kampeni hii licha ya kuhamasisha matumizi ya malipo kwa kutumia kadi pia imelenga kuwazawadia wateja wetu ambao wanaenda sambamba na safari ya mabadiliko kuingia mfumo wa huduma za kidijitali za kibenki," alisema Raballa.Akifafanua zaidi alisema kutakuwa na washindi 20 kwa kila wiki ambao watajishindia shilingi 100,000 ndani ya kipindi hicho cha miezi miwili, huku washindi wengine 6 wa mwezi kuibuka na simu janja za kisasa 'Samsung S9+' na mwisho washindi wengine 3 kati yao wawili kujishindia safari ya mapumziko kwenda Dubai iliyolipiwa kila kitu.

Aidha alibainisha kuwa, washindi wa Safari hiyo ya mapumziko wataruhusiwa kwenda pamoja na rafiki mmoja chaguo la mshindi na kulala katika hoteli ya hadhi ya nyota tano Dubai kwa siku 3.

WATEJA 434 WAREJESHEWA HUDUMA YA MAJI KUPITIA KAMPENI YA #DAWASATUNAWAHITAJI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wamefanikiwa kurejesha wateja 434 waliokuwa na madeni baada ya kuanzisha kampeni ya Dawasa Tunawahitaji.

Wateja hao waliokuwa wamekatiwa huduma ya maji na DAWASA wamekubali kulipa madeni yao yenye jumla ya thamani ya Milioni 204.3 kutoka maeneo mbalimbali. 

Akitoa taarifa hiyo, Mkurugenzi wa idara ya huduma kwa wateja, Ritamary Lwabulinda amesema mpaka sasa mikoa yote 10 ya DAWASA inaendelwa na kampeni hiyo inayolenga kuwavutia wateja waliokuwa wamekatiwa huduma kutokana na madeni sugu. Amesema, hadi sasa Mkoa wa Magomeni ndio unaongoza kwa kurejeaha huduma ya maji kwa wateja 81 wenye kudaiwa jumla ya Miliioni 39.44 ikifuatiwa na Mkoa wa Temeke uliofanikwa kurejesha wateja 60 waliokuwa wanadaiwa Milioni 23.01. 

Ritamary amesema mikoa mingine na kiasi cha fedha kinachodaiwa katika mabano ni Bagamoyo wateja 59 (mil 22.9), Tegeta wateja 59 (mil 27.21), Tabata wateja 49 (mil 27.52) na Kinondoni wateja 28 (mil 13.24). Sehemu zingine ni Ubungo wateja 27 (mil 17.23), Kibaha wateja 25 (mil 8.77), Ilala wateja 24 ( Mil 12.36) na Kawe wateja 22 (mil 12.58). 

Kufuatia mpango huo wa #Dawasa Tunawahitaji kwa sasa Mamlaka hukusanya kiasi cha Shilng Milion 36.41 kila mwezi baada ya wateja hao kuingia mkataba wa kulipa kidogo kidogo kila mwezi na katika kipindi kifupi cha utekelezaji wa kampeni hiyo jumla ya Milion 59.39 zimekusanywa kutoka katika vituo mbalimbali. 

Kampeni hiyo ilizinduliwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa kampeni ya ' Dawasa Tunawahitaji' lengo kuu ni kuona wateja wote takribani 10000 waliokatiwa maji wanaanza kupata tena huduma hiyo. 

Kampeni hiyo itawahusisha wateja wote waliokatiwa huduma ya maji na kupitia kwa mameneja wa mikoa yote ya DAWASA kwa pamoja wakubaliane watalipa kwa miezi mingapi madeni ambayo wanadaiwa.
Mafundi wakiwa wanasoma mita ya maji ya mteja.

Tigo Wazindua Malipo ya kielekroniki Serikalini Arusha

$
0
0



Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo, Nancy Bagaka akizungumza na wanahabari hawapo pichani kuhusu uzinduzi wa matumizi ya mfumo wa Kieletroniki wa malipo ya Serikali (GePG), mjini Arusha jana kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi Arusha (AUWASA), Edes Mushi.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi Arusha (AUWASA), Edes Mushi akizungumza na wanahabari mjini Arusha jana kuhusu matumizi ya mfumo wa Kieletroniki wa malipo ya Serikali (GePG) utakaokuwa ukifanywa kwa kutumia Kampuni ya Tigo kulia kwake ni Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo, Nancy Bagaka.
Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo, Nancy Bagaka (kushoto)akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi Arusha (AUWASA), Edes Mushi muda mfupi kabla ya uzinduzi wa matumizi ya mfumo wa Kieletroniki wa malipo ya Serikali (GePG), mjini Arusha leo
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa uzinduzi wa matumizi ya mfumo wa Kieletroniki wa malipo ya Serikali (GePG), mjini Arusha leo wazungumzaji wakiwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi Arusha (AUWASA), Edes Mushi Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo, Nancy Bagaka



KAMPUNI ya simu ya mkononi ya Tigo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (Auwasa) wamezindua mfumo mpya wa malipo ya kielekroniki serikalini (GePG) katika mikoa ya Arusha , Kilimanjaro na Manyara.

Mfumo huo utarahisisha upatikanaji wa Ankara mbalimbali pamoja na kufanya malipo kutokana na huduma wanazopata kutoka taasisi za serikali zaidi ya 300 lengo ikiwa ni kurahisisha watumiaji wa huduma kutokaa katika misururu. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua mfumo huo , Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini Nancy Bagaka alisema kuwa mfumo huo utapunguza kwa kiwango kikubwa ubadhirifu jambo ambalo litaongeza mapato ya serikali.

“Kutokana na mfumo huu faida nyingi zitapatikana ikiwemo kuongeza mapato ya serikali kupitia taasisi na mashirika , kuboresha uwekaji na utunzaji wa kumbukumbu , utoaji taarifa za mara kwa mara pamoja na kuondoa ubadhirifu na wizi” alisema Bagaka. Aidha alisema ili kuweza kulipia Ankara mteja wa Tigo atatakiwa kupiga *150* 01# kisha atachagua kulipia ankra ambapo eneo la malipo ya serikali itajitokeza na kuingiza tarakimu 12 kwa taasisi anayotaka ipokee malipo .

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Auwasa Edes Mushi alisema kutokana na mfumo huo mpya sasa wateja wa Mamlaka hiyo hawatolazimika kukaa katika misururu mirefu wakisubiri kulipia Ankara za maji. “Auwasa kwa kushirikiana na Tigo tunaendelea kurahisisha maisha ya wateja wetu kwa kutumia mfumo huu wa GePG ambao tayari taasisi na mashirika mengi yanautumia” “Mbali na Auwasa, tayari Wizara ya Ardhi na Maenedeleo ya Makazi wanatumia, Shirika na Ndege ATCL , Bodi ya Utalii , Hospitali zote za umma , Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) Wizara ya Mifugo nk .”

“Matumizi ya mfumo huu wa kielektroniki umerahisha utoaji huduma kwa wananchi na umeleta tija kubwa na kuongeza mapato hivyo tunasisitiza wateja wa Tigo wautumie ikiwa ni pamoja na kuulizia ankara zao za malipo ya maji” alisisitiza Mushi. Mpaka sasa takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya watumiaji milioni 7 wa huduma ya Tigo pesa wanafanya malipo kwa haraka bila usumbufu kwenda kwa wakala ,idara na taasisi kadha wa kadhaa za Serikali.

TAA YAENDELEA KUTOA KWA JAMII

$
0
0
Mkurugenzi wa Chief Promotions Bw. Amoni Mkoga akizungumza mbele ya waandishi wa habari kuhusu Tamasha la Utamaduni la Chato linalotarajia kufanyika Disemba 22, 2018. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Abdi Mkwizu (kulia) na Mwenyekiti Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bw. Habbi G;unze (kushoto). Mkutano huo wa waandishi wa habari umefanyika leo katika Kijiji cha Makumbusho.
Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Abdi Mkwizu (kulia) akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari katika Mkutano uliofanyika leo katika kijiji cha Makumbusho kuhusiana na udhamini wa Mamlaka kwenye tamasha la Utamaduni la Chato, linalotarajia kufanyika Disemba 22, 2018.
Mwenyekiti Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bw. Habbi Gunze (kushoto) akizungumza namna serikali inavyotekeleza mpango wa kuhuisha wasanii katika mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika leo kwenye Kijiji cha Makumbusho.
Mwenyekiti Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bw. Habbi Gunze (kushoto), Mkurugenzi wa Chief Promotions Bw. Amoni Mkoga (katikati) na Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Abdi Mkwizu (kulia) kwa pamoja wakionesha tangazo la tamasha la Utamaduni la Chato lenye kauli mbiu ya “Maendeleo ya Viwanda yasiache Utamaduni nyuma”. Tukio hilo limefanyika leo kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari katika Kijiji cha Makumbusho.
Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Abdi Mkwizu (kulia), akikabidhi moja ya fulana 100 zilizotolewa na TAA kwa muandaaji wa Tamasha la Utamaduni la Chato, Bw. Amon Mkoga (kushoto), Katikati anayeshughudia ni Mwenyekiti Bodi ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA), Bw. Habbi Gunze. Tamasha hilo litafanyika Disemba 22, 2018.
Mkurugenzi wa Chief Promotions Bw. Amoni Mkoga (kushoto), Mwenyekiti Bodi ya Baraza la Salaa la Taifa (BASATA), Bw. Habbi Gunze (katikati) na Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Abdi Mkwizu (kulia), wakisoma kauli mbiu ya Tamasha la Taifa la Chato “Maendeleo ya Viwanda Yasiache Utamaduni nyuma”. Tamasha hilo litafanyika Disemba 22, Chato Geita.
Mcheza ngoma za asili, Bw,. Ally Mango akicheza na nyoka mbele ya waandishi wa Habari katika kikiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam, wakati wa utoaji wa fulana 100 kwa tamasha la Utamaduni la Chato zilizotolewa leo na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA). (PICHA ZOTE KWA HISANI YA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA)

…………………..

MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kufanikisha shughuli mbali mbali za jamii, kwa kutoa misaada yenye tija.

Hilo limekuwa bayana leo tarehe 12 Disemba, 2018 kwenye Kijiji cha Makumbosho Jijini Dar es Salaam, ambapo TAA imetoa msaada wa fulana 100 kwa ajili ya kufanikisha Tamasha la Utamaduni la Chato linalotarajiwa kufanyika tarehe 22 Disemba, 2018 katika Uwanja wa Mazaina Chato.

Akizungumza katika Mkutano wa waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa TAA, Bw. Abdi Mkwizu amesema Mamlaka ina wajibu mkubwa wa kuunga mkono shughuli za kijamii, kwa kutoa misaada ya mbalimbali.

“Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania ina wajibu wa Kusimamia, kuendesha, kuboresha na kuendeleza Viwanja vya Ndege Tanzania lakini pia mbali na kutoa huduma hizo tuna wajibu wa kushiriki katika shughuli za kijamii, kwa wadau ambao wanatufanya sisi tuwepo,” amesema Bw. Mkwizu.

Pia Bw. Mkwizu amebainisha kwamba TAA inahudumia Viwanja 58 vilivyopo Tanzania Bara chini ya serikali, hivyo ni wajibu wao kushiriki katika shughuli za kusaidia jamii sehemu yeyote ile kulingana na uhitaji na bajeti iliyopo.

“Ikumbukwe siku za hivi karibuni TAA tumeshirika katika kufanikisha Tamasha la Urithi Wetu lililofanyika kuanzia Oktoba Mosi mpaka Oktoba 7, 2018 katika Kijiji cha Makumbusho, tumetoa pia msaada wa Mafuta Kinga jua ya Ngozi kwa watoto wenye ulemavu wa Ngozi katika baadhi ya shule hapa Dar es Salaam, lakini pia tarehe 24 Novemba mwaka huu tumekabidhi Shule ya Msingi ya Kisasa huko Bukoba inaitwa Tumaini, na tunaamini itaongeza ufaulu kwa wanafunzi huko Bukoba na hayo ni macheche kati ya mengi ambayo Mamlaka inafanya kwa Jamii” amebainisha Bw. Mkwizu.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu na niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Bw. Habbi Gunze ameishukuru Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania kwa mchango wake kufanikisha Tamasha la Utamaduni la Chato.

“Niwashukuru sana Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania kwa mchango wao nap engine bila wao hili la leo lisingeweza kufanikiwa. Utamaduni ndio uhai wa Taifa, kwa hiyo nchi isipokua na Utamaduni nchi inakua sio hai, hivyo kwa Mchango huu wa kusaidia hili nawapongeza sana TAA” amesema Bw. Gunze.

Naye Mkurugenzi wa Chief Promotions ambaye ndie mratibu wa Tamasha hilo Bw. Amon Mkoga amesema kwamba Tamasha litakuwa na mambo yote ya kiutamaduni ili kuenzi asili ya Kitanzania.

“Kauli mbiu ya Tamasha la Utamaduni la Chato inasema “Maendeleo ya Viwanda yasiache Utamaduni nyuma” ambapo Tamasha hili ni maalum kwa ajili ya kuuenzi utamaduni wa Mtanzania. Katika Tamasha hili kutakua na Vikundi mbalimbali vya Utamanduni. Vikundi vya ngoma vitakuwepo kutoka Simiyu, Shinyanga, Geita, Mwanza, Tabora na Chato wenyewe, hivyo tunawaomba wananchi mtusaidie kufikisha taarifa hizi kwa watanzania” ameeleza Bw. Mkoga.

Tamasha la Utamaduni la Chato ni tamasha kubwa la ngoma ambalo hufanyika kila mwaka nah ii itakua ni mara ya tatu mfululizo likifanyika Chato mkoani Geita.

WAKAZI WA ITILIMA MKOANI SIMIYU WAFURAHIA KUKAMILIKA KWA MRADI WA MAJI

$
0
0



Mhandisi Christer Mchomba (mwenye kofia), kutoka Wizara ya Maji, akiandika maelezo ya Mhasibu wa Kamati ya Maji ya Mji wa Lagangabilili, Bi. Kundi Paulo, wakati Timu Maalum ya Serikali ikiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, ilipokuwa katika Wilaya ya Itilima, mkoani Simiyu, kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
3-min
Mkazi wa Mji wa Lagangabilili, Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, Bi. Pendo Tindigwe, akiwa amebeba ndoo yake yenye maji baada ya kukamilika kwa mradi wa maji Lagangabilili uliojengwa na Serikali kwa gharama ya Sh. 907m.
4-min
Tenki la maji la Mradi wa Maji wa Mji wa Lagangabilili, Wilaya ya Itilima, mkoani Simiyu, lenye uwezo wa kubeba lita 225,000 za maji kwa wakati mmoja kwa ajili ya kuwahudumia wakazi 2,212 wa Mji huo wa Lagangabilili.
5-min
 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Dkt. Kiraba Faustine (kulia), Bw. Jordan Matonya, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Itilima, Bw. Goodluck Masige na Mhandisi Laurian Muna kutoka Wizara ya Ujenzi, wakiwa pembeni mwa tenki la maji lenye ujazo wa lita 225,000 kwa ajili ya matumizi ya wakazi 2,212 wa Mji wa Lagangabilili, Wilaya ya Itilima, mkoani Simiyu.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

…………………

Na Benny Mwaipaja,WFM, Simiyu

ZAIDI ya Wakazi elfu 2 wa Mji wa Lagangabilili, Tarafa ya Kanadi, Wilayani Itilima, mkoani Simiyu, wameondokana na adha ya kukosa maji safi na salama baada ya kukamilika kwa mradi wa maji ya bomba wa Lagangabilili uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 900.

Wakizunguza mbele ya timu maalumu ya wataalam wanaofuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kutoka baadhi ya Wizara wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, Baadhi ya wakazi wa Mji huo wa Lagangabilili wameishukuru Serikali kwa kuwapatia mradi huo wa maji.

“Tunaishukuru sana Serikali kwa kutuletea maji tunayapata kwa urahisi, zamani tulikuwa tukihangaika sana akina mama walikuwa wakiyafuata mto Simiyu, mbali sana, walikuwa wakitoka saa kumi usiku na kurudi saa tatu asubuhi” alisema Bw. Chonza Maduhu, mkazi wa Lagangabilili, Simiyu
Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Itilima, Bw. Goodluck Masige, amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kumefanya kiwango cha upatikanaji maji safi na salama kwenye mji huo ambao ndio makao makuu ya wilaya ya Itilima, kupanda kutoka asilimia 20 za awali hadi kufikia asilimia 100.

“Tumejenga tenki lenye ujazo wa lita 225,000, vituo 21 vya kuchotea maji, tumejenga mtandao wa bomba za kusambaza maji nyenye urefu wa mita 29,000 na kufunga pampu 1 ya kusukuma maji” aliongea Mhandisi Masige

Ameitaja kazi iliyosalia kukamilisha mradi huo unaotarajiwa kukabidhiwa Serikalini na mkandarasi, Kampuni ya M/S Nangai Contractors and Engineering Co. Ltd, Disemba 30, 2018, kuwa ni ujenzi wa birika la  kunyweshea mifugo (Cattle trough) ( Pause: Mhandisi Goodluck Masige-Mhandisi wa Maji Wilaya ya Itilima
Mmoja wa Wajumbe wa timu ya Kitaifa ya ufuatiliaji wa miradi ya maji katika mikoa ya Simiyu na Mara, Bw. Jordan Matonya, amesema kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha kuwa miradi inayotekelezwa maeneo mbalimbali nchini inatekelezwa kwa viwango vya hali ya juu na kuwanufaisha wananchi

Wataalam Muhimbili Wapigwa Msasa Kuhusu Sheria ya Manunuzi

$
0
0



Mtoa mada kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Mhandisi Mary Swai akitoa mada kuhusu sheria ya manunuzi ya mwaka 2011 kwa wataalam wa manunuzi, fedha, wakaguzi wa ndani pamoja na wataalam wengine wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Mafunzo hayo ya siku nne yamebeba mada mbalimbali kuhusu sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2011 na marekebisho yake ya mwaka 2016.
????????????????????????????????????
Washiriki mbalimbali wakimsikiliza mtoa mada kuhusu sheria ya manunuzi ya mwaka 2011 kwenye ukumbi wa NPC I katika hospitali hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa hospitali hiyo, Gerald Jeremiah akifuatilia mada na aliyesimama ni mtoa mada wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Castor Komba akiwa pamoja na washiriki.
????????????????????????????????????
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo leo yanayohusu sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2011 na marekebisho yake ya mwaka 2016.
????????????????????????????????????
Mtoa mada kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Mhandisi Mary Swai akisisitiza jambo katika mafunzo hayo leo.
????????????????????????????????????
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada kuhusu sheria ya manunuzi ya mwaka 2011

JAFO AWATAKA WAKANDARASI KUONGEZA KASI

$
0
0

Waziri Jafo ambaye ni Mbunge wa Kisarawe akiongea na moja ya mkandarasi anayejenga barabara ya Kisarawe – Maneromango kwa kipande cha Kazimzumbwi 

 Waziri Jafo akiwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya Kisarawe katika ukaguzi wa barabara ya Kisarewe – Maneromango 
 Wakandarasi wakina katika harakati za ujenzi eneo la Kazimzumbwi

……………………

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI amewataka wakandarasi wanaojenga barabara ya lami ya Kisarawe – Maneromango kwa kipande kinacho endelea cha wastani wa Kilometa sita kuongeza kasi ya ujenzi.

Waziri Jafo amewataka wakandarasi hao wakati alipokuwa akifanya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayojengwa wilayani Kisarawe. Barbara hiyo yenye urefu wa kilometa 54.8 inayojengwa kwa awamu mbalimbali itawasaidia sana wananchi wa wilaya ya Kisarawe na watalii mbalimbali wanaokwenda kutembelea mbuga ya selous kupitia Kisarawe

MAGAZETI YA LEO JUMATANO DESEMBA 12,2018

MAHAKAMA YAAMURU MADINI YA THAMANI YA 2.5/- YATAIFISHWE KUWA MALI YA SERIKALI

$
0
0
Karama Kenyunko,Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru madini yenye thamani ya Sh. bilioni 2.5 yataifishwe na kuwa mali ya serikali kwasababu ukwepaji wa kodi ya mrabaha unasababisha Taifa likose mapato.

Pia Mahakama imeamuru wafanyabiashara watatu wa madini wakiwemo raia wawili wa China na mmoja wa India kulipa faini ya Sh.milioni moja kila mmoja au kutumikia kifungo cha miezi miwili kila mmoja.

Wafanyabiashara hao ni Chang Xu, Kai Jiang, Ashok Lavingia na Kampuni ya Sino Africa Collection Ltd waliokuwa wakikabiliwa na mashitaka matano likiwemo la kuwasilisha taarifa za uongo kwa Kamishna wa Madini kwa lengo la kukwepa malipo sahihi ya mirahaba.

Akitoa hukumu hiyo jana , Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amesema washitakiwa wanatiwa hatiani kwa kukiri kosa na katika kila kosa kila mshitakiwa atatakiwa kulipa Sh. 200,000 na kifungo cha miezi miwili ambapo jumla ni Sh.milioni nne na kifungo cha miezi miwili.Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Wakili wa Serikali, Jacqueline Nyantori aliiomba Mahakama kutaifisha madini hayo chini ya Sheria ya Madini inayosomwa sambamba na sheria ya Uwazi na Uwajibikaji ya mwaka 2015.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Wankyo Simon, alidai washitakiwa hao ni wakosaji wa kwanza na makosa yao yanagusa masuala ya rasilimali za nchi.Alidai kesi hiyo inalenga ukwepaji kodi ambayo ndio uchumi wa nchi na unategemewa katika vitu vyote vinavyofanyika kwa wananchi wa Tanzania, hivyo wanaomba adhabu kali itolewe kwa washitakiwa kulingana na sheria zilizopo kwa lengo la kutunza rasilimali za madini.

Wakili wa utetezi, John Gamanya na Flora Jacob alidai washitakiwa hao ni wakosaji wa kwanza na ni wafanyabiashara wenye vibali hivyo aliomba mahakama izingatie kuwapunguzia adhabu.Imeelezwa mahakamani hapo kuws katika mashitaka ya kwanza, inadaiwa kati ya Juni Mosi, 2018 na Oktoba 3, mwaka huu maeneo ya jiji la Dar es Salaam, waliratibu na kufadhili biashara iliyofanywa genge haramu kwa lengo la kuchuma faida.

Pia inadaiwa Oktoba 3, mwaka huu maeneo ya Mgahawa wa Penda uliopo barabara ya King's way wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam wakiwa ha leseni ya madini walishindwa kutunza kumbukumbu ya usajili wa madini husika yaliyohifadhiwa.Washitakiwa wakiwa na leseni ya kujihusisha na biashara ya madini walishindwa kuwasilisha kwa Kamishna wa Madini nyaraka halisi ya kuingiza madini mbalimbali waliyoyasajili kwenye kumbukumbu zao ili kuonesha madini ya vito yenye uzito wa gramu 2,849.45 yenye thamani ya Dola za Marekani 385,830.32 waliyokutwa wakiyamiliki.

Katika mashitaka ya nne, washitakiwa walishindwa kuwasilisha nakala halisi ya madini waliyosajili vito vyenye uzito wa gramu 4,531.09 yenye thamani ya Dola za Marekani 735,904.07.Pia inadaiwa washitakiwa waliwasilisha taarifa ya uongo kwa Kamishna wa Madini kuhusu ubora wa madini ya rangi na vito walivyotunza kwa lengo ya kukwepa malipo sahihi ya mrabaha.

NAIBU WAZIRI OLE NASHA ASHIRIKI ‘MSARAGAMBO’ WILAYANI SAME

$
0
0

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akishiriki ‘Msaragambo’ wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Ruvu iliyoko Kata ya Ruvu Darajani Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro alipofanya ziara kukagua miradi ya Elimu inayotekelezwa katika Wilaya hiyo.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akikagua ukarabati wa miundombinu uliofanyika katika Shule ya Sekondari Same iliyoko Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro. Ameridhishwa na namna ukarabati huo ulivyofanyika na kuwataka kutunza miundombinu hiyo ili iweze kutumika kwa muda mrefu.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ruvu Darajani Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro. Amewataka kutumia fursa ya Elimu bure kuhakikisha wanaandikisha watoto wote wenye umri wa kuanza shule.

………………………

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ameshiriki ‘msaragamo’ wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Ruvu iliyoko Kata ya Ruvu Darajani Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro.

Mheshimiwa Ole Nasha ameshiriki ujenzi huo na Wananchi wa Kijiji cha Ruvu Darajani wakati wa ziara ya kukagua miradi ya Elimu katika Wilaya ya Same ambapo amewataka wananchi kuendeleza jitihada hizo ili kuweza kuweka mazingira mazuri ya wanafunzi kusoma.

Kufuatia jitihada hizo za Wananchi Naibu Waziri Ole Nasha kupitia Wizara yake ameahidi kujenga vyumba viwili vya madarasa, mabweni mawili na matundu ya vyoo katika shule ya msingi Ruvu ikiwa ni kuunga mkono juhudi ambazo wananchi wa kijiji cha Ruvu Darajani wameonesha lakini pia kuwezesha wanafunzi kutulia shuleni na kusoma.

“Serikali ikiona eneo ambalo wananchi wameanza na wana hamasa kubwa ya kujiletea maendeleo haiwezi kusita kuja kusaidia, Wilaya ya Same mmeonesha mfano kupitia utaratibu wenu wa msaragambo tunaunga mkono jitihada hizo kwa kuwajengea vyumba vya madarasa, mabweni na matundu ya vyoo,” aliongeza Naibu Waziri Ole Nasha.

Aidha Naibu Waziri huyo amewataka wananchi wa Kijiji cha Ruvu Darajani ambao wanajihusisha na shughuli za ufugaji kutotumia watoto kuchunga mifugo badala yake kuhakikisha wanatumia fursa ya Elimu bure kuwaandikisha watoto wote wenye umri wa kuanza shule.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki alimweleza Naibu Waziri wa Elimu kuwa changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Ruvu imetokana na ongezeko la Wanafunzi waliohamishiwa shule hiyo kutokana na shule walizokuwa wakisoma miundombinu yake kuathiriwa na mafuriko yaliyotokana na mvua za masika zilizonyesha mwaka huu.

Katika ziara hiyo Naibu Waizri Ole Nasha pia alitembelea shule ya Sekondari Makanya, Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Same na Shule ya Sekondari Same ambapo ameridhishwa na namna ukarabati ulivyofanyika katika shule hiyo kongwe.

BENKI YA TPB YAANDAA MKUTANO WA BENKI ZA AKIBA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0

FUATILIA
Baadhi ya viongozi wakifuatilia kwa makini mkutano wa mabenki ya akiba Afrika Mashariki. Mkutano huo uliofanyika Zanzibar ulijumuisha wajumbe kutoka benki ya akiba Uganda na Kenya. Dhumuni la mkutano huo ni kujadili changamoto pamoja na fursa mbalimbali zilizopo katika nchi za Afrika Mashariki kupitia benki za akiba nchini humo.
pamoja
Uongozi wa Benki ya TPB wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mkutano wa mabenki ya akiba Afrika Mashariki. Mkutano huo uliofanyika Zanzibar ulijumuisha wajumbe kutoka benki ya akiba Uganda na Kenya. Dhumuni la mkutano huo ni kujadili changamoto pamoja na fursa mbalimbali zilizopo katika nchi za Afrika Mashariki kupitia benki za akiba nchini humo.

RC MTAKA ATEKELEZA AGIZO LA RAIS, KUWAGAWIA VITAMBULISHO WAJASIRIAMALI WADOGO

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera boksi lenye vitambulisho vya wajasiliamali wadogo, ikiwa ni utekezelaji wa Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa kwa Wakuu wa Mikoa wote nchini, kuwapa vitambulisho hivyo wajasiliamali wadogo ambao mauzo yao ni chini ya milioni nne kwa mwaka, ili vitambulisho hivyo viweze kuwafikia wajasiriamali hao mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga boksi lenye vitambulisho vya wajasiliamali wadogo, ikiwa ni utekezelaji wa Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa kwa Wakuu wa Mikoa wote nchini, kuwapa vitambulisho hivyo wajasiliamali wadogo ambao mauzo yao ni chini ya milioni nne kwa mwaka ili vitambulisho hivyo viweze kuwafikia wajasiriamali hao mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani boksi lenye vitambulisho vya wajasiliamali wadogo, ikiwa ni utekezelaji wa Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa kwa Wakuu wa Mikoa wote nchini, kuwapa vitambulisho hivyo wajasiliamali wadogo ambao mauzo yao ni chini ya milioni nne kwa mwaka ili vitambulisho hivyo viweze kuwafikia wajasiriamali hao mkoani Simiyu.





Na Stella Kalinga, Simiyu


Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli la kutoa vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo, ambapo amewakabidhi Wakuu wa Wilaya na Maafisa Biashara wa Halmashauri mkoani hapa jumla ya vitambulisho 25,000, vitakavyotolewa kwa wajasiriamali wadogo wenye mauzo pungufu ya milioni nne kwa mwaka.

Akikabidhi vitambulisho hivyo Mtaka amesema vitawasaidia wajasiriamali wadogo kutambuliwa,kuwajengea ujasiri na uthubutu na kuwafanya kunufaika na fursa mbalimbali huku akibainisha kuwa vitachangia pia kuwaibua wajasiriamali wapya mkoani Simiyu.

Ameongeza kuwa Simiyu imejipanga kuwafikia wajasiriamali wote wadogo kama ilivyokusudiwa na Mhe. Rais, huku akiwaonya na kuwatahadharisha wafanyabiashara wakubwa wanaotambuliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutojaribu kujipatia vitambulisho vya wajasiriamali wadogo kwa njia ya udanganyifu.

“Niwatahadharishe wafanyabiashara wasije wakatumia nafasi ya vitambulisho hivi vya wajasirimali wadogo, kufanya udanganyifu wowote wa wao kuvitumia vitambulisho hivyo kujitambulisha kama wafanyabiashara wadogo; huu udanganyifu hatutaupa nafasi na sisi kama Serikali tumejiandaa kuainisha kila mtu anachofanya, mahali anapokaa, historia yake ya biashara”

“Ofisi za Wakurugenzi zitatoa magari yatakayowawezesha maafisa Biashara kwenda vijijini kuwafikia wajasiamali wadogo,tunaamini walengwa wa vitambulisho hivi ni wale ambao nauli ya kule aliko na Makao Makuu ya Wilaya inaweza kuwa ndiyo fedha inayohitajika achangie kupata kitambulisho hicho,kwa hiyo kuna kadi zitabaki wilayani lakini nyingine zitapelekwa mahali walipo walengwa” alifafanua Mtaka.

Baadhi ya wakuu wa wilaya wakizungumza mara baada ya kupokea vitambulisho hivyo wamesema watahakikisha vinawafikia walengwa waliokusudiwa na hakutakuwepo na udanganyifu wowote katika zoezi la ugawaji wa vitambulisho hivyo.

“Niwahakikishie wajasiriamali wadogo wote kuwa watapata vitambulisho kama Mhe Rais alivyoelekeza na nitoe wito kwao kuja kuchukua vitambulisho hivi ili asiwepo mtu yeyote wa kuwabugudhi na wafanye kazi zao kwa uhuru” Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga

“ Niwatoe hofu wajasiriamali wote wadogo kuwa kila aliye na sifa ya kupata kitambulisho hiki atapata na kwa wale wanaodhani watatumia vitambulisho hivi kukwepa kodi nichukue nafasi hii kutoa onyo kuwa hatutavumilia udanganyifu wa aina yoyote” Mkuu wa Wilaya ya Busega,Mhe. Tano Mwera.

Baadhi ya wajasiriamali Wadogo Mkoa Simiyu wameshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli kwa kutoa vitambulisho hivyo ambavyo vitawaondolea adha mbalimbali walizokuwa wakizipata ikiwepo ya kuogopa kufanya biashar zao kutokana na kutotambuliwa rasmi.

“ Tanamshukuru sana Rais ametupa ujasiri wa kufanya biashara zetu kwa uhuru maana kuna watu walikuwa wanaogopa kufanya biashara kwa sababu ya kuogopa kodi, kupitia vitambulisho hivi tutafanya biashara kwa uaminifu, uhuru na ujasiri na katika wilaya yetu ya Bariadi, Tanzania ya Viwanda hasa vile vidogo itawezekana” alisema Bahati Kaitila mjasiriamali mdogo kutoka Bariadi.

“ Nimelipokea vizuri suala la kupewa vitambulisho kwa sababu vitatusaidia sisi wajasiriamali wadogo kupata ujasiri zaidi wa kufanya kazi zetu, tunaweza kuanza na kitu kidogo lakini baadaye tukafanya makubwa” alisema Grace Mukali mjasiriamali mdogo kutoka wilaya ya Bariadi.

WAZIRI MHAGAMA AITAKA MENEJIMENTI YA OFISI YA WAZIRI MKUU KUZINGATIA HAKI NA USAWA KATIKA KUTATUA KERO ZA WATUMISHI

$
0
0


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiongoza kikao cha pamoja na Watumishi wa Ofisi hiyo walipokutana akujadili masuala yao ikiwa ni sehemu ya kufahamiana na kuendelea kufanya kazi kwa umoja, mkutano huo ulifanyika Desemba 10, 2018 katika Ukumbi Mikutano wa LAPF Dodoma.
P2-min
Katibu Mkuu Ofisi yaWaziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi akichangia jambo wakati wa mkutano huo.
P3-minP4-minP5-min
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia maelekezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama  (hayupo pichani) wakati wa mkutano huo.
P6-min
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde akichangia jambo wakati wa mkutano huo.
P7-min
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka, akifafanua masuala ya malipo ya Pensheni kwa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (hawapo pichani) wakati wa mkutano huo.
P8-min
Mkaguzi wa Ndani Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Omari Mpayage akiuliza swali wakati wa mkutano huo.
P9-min
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Bw. Peter Kalonga akifafanua masuala ya utawala kwa watumishi wa Ofisi hiyo wakati wa kikao hicho.
P10-min
Msaidizi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Richard Kalinga akiuliza swali wakati wa mkutano huo.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama ameitaka Menejimenti ya Ofisi yake kushughulikia kero za watumishi kwa haki na usawa ili kumaliza kero zilizopo.

Ameyasema hayo wakati wa Mkutano na Watumishi wa ofisi ya Waziri Mkuu walipokutana kujadili masula yanayowakabili wawapo kazini uliofanyika Desemba 10, 2018 katika Ukumbi wa LAPF Dodoma.

Waziri aliwataka Watendaji wa ofisi yake kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili watumishi kuhusu madai mbalimbali ikiwemo; kupanda madaraja, uhamisho, usalama mahali pa kazi na masuala ya kuzingatia afya wawapo kazini ili kuhakikisha wanatekeeleza majukumu yao katika mazingira rafiki.

“Kama kuna motisha kubwa kwa mtumishi ni kumsaidia kutatua kero yake inayohusiana na utumishi wake kwa uzito unaolingana na tatizo au uhitaji wake ili kusaidia kuongeza morali yake katika kufanya kazi.”Alisema Mhagama.
Sambamba na hilo waziri aliwaasa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kutumia mabaraza ya Wafanyakazi katika kujadili na kutatua kero wanazokabiliana nazo wawapo kazini.

“Ni vyema watumishi kuendelea kuyatumia mabaraza ya wafanyakazi yaliyopo kisheria katika ofisi ili kabla masuala hayajafika ngazi za juu yawe yamekwishwa sikilishwa na kutafutiwa ufumbuzi pale inapowezekana”.Alisistiza Waziri
Aliongezea kuwa, ni wajibu wa Makatibu wakuu kuendelea kusimamia na kuhakikisha haki na usawa vinazingatiwa katika Ofisi ili kuwa na weredi na ufanisi katika kutekeleza majukumu ya kila siku.

Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu, Maimuna Tarishi aliahidi kuchugua maagizo ya waziri na kuahidi kuyatekeleza kama ilivyoelekezwa katika mkutano huo.

“Tutaendelea kusimamia shughuli za Ofisi kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo iliyopo ili kuhakikisha haki na usawa vinazingatiwa mahali pa kazi ili kuweza kufikia malengo na kuendelea kuiletea nchi maendeleo”.Alisema Tarishi

Jaji Mkuu wa Tanzania akagua shughuli za Mahakama Wilayani Chamwino na Kongwa

Viewing all 46360 articles
Browse latest View live




Latest Images