Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1748 | 1749 | (Page 1750) | 1751 | 1752 | .... | 1896 | newer

  0 0

   Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd akimkabidhi madawati 52 Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. John Rwegasha kwa ajili ya wagonjwa na ndugu wa wagonjwa wanaofika kupatiwa matibabu hospitali hapo. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akishuhudia tukio hilo. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura wa Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga. Msaada huo una thamani ya Tsh. 10 milioni.
   Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akikagua madawati hayo. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba wa Muhimbili, John Rwegasha, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura wa Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga.
   Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na waandishi wa habari kabla ya NMB kukabidhi msaada wa madawati hayo kwa uongozi wa Muhimbili.
   Mkazi wa Kurasini jijini Dar es Salaam, Mariam Shaban akiishukuru Muhimbili pamoja na NMB kwa kuwapatia madawati hayo ambayo watayatumia kusubiri ndugu na jamaa  wakati wakipatiwa matibabu na wataalam wa afya. Pia, Bi. Mariam amemweleza Naibu Waziri jinsi wataalam wa Muhimbili walivyompokea vizuri mgonjwa wake na kuanza kumpatia matibabu kwa wakati.
  Dkt. Ndugulile akizungumzia huduma za afya zinazotolewa na Muhimbili baada ya kukagua madawati hayo leo.


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akipokea ngao kutoka kwa Dkt. Jameel Alata ambaye ni mkuu wa msafara wa wataalamu wa afya kutoka mradi wa Little Heart wa nchini Saudi Arabia ambao walikuwa katika Taasisi hiyo kati ya tarehe 2-8 Desemba, 2018 kwa ajili ya kambi maalum ya matibabu ambayo iliandaliwa kwa pamoja na Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Taasisi ya misaada ya MUNTADA ya Uingereza, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation ya Tanzania.
  Baadhi ya madaktari kutoka mradi wa Little Heart kutoka Saudi Arabia ambao ni mradi wa afya ulioko ndani ya Taasisi ya Msaada ya Muntada yenye makao makuu yake mjini London nchini Uingereza wakifuatilia hotuba zilizokuwa zinatolewa wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza madaktari hao baada ya kumalizika kwa kambi maalum ya matibabu ya moyo ya kuzaliwa nayo iliyofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Madaktari hawa walikuwa katika Taasisi ya Magonjwa ya Moyo ya Jakaya Kikwete kati ya tarehe 2-8 Desemba kwa ajili ya kambi maalum ya matibabu ambayo iliandaliwa kwa pamoja na Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Taasisi ya misaada ya MUNTADA ya Uingereza, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation ya Tanzania.
  Mufti Abubakari bin Zuberi akimkabidhi Katibu Mkuu wa Taasisi ya Dhi Nureyn Bw. Shams Elmi Obsiye ngao ya kuipongeza Taasisi hiyo kutokana na kuwa kiunganishi kati ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na mradi wa Little Heart wa nchini Saudi Arabia ambao walifanya kambi ya matibabu ya moyo na kutibu watoto 70 na watu wazima wawili wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo kuanzia tarehe 2-8 Desemba, 2018. Kambi hii ya matibabu ya hisani iliandaliwa kwa pamoja na Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Taasisi ya misaada ya MUNTADA ya Uingereza, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation ya Tanzania.

  0 0

  Mtumishi wa Wizara ya Afya kitengo cha maabara na mkazi wa Mpwapwa mkoani Dodoma Mbwana Saidi Mbela , ameibuka mshindi wa zawadi ya shilingi milioni 10 za Tigo Jigiftishe na kukabidhiwa zawadi yake jijini Da es Salaam.

  Mbela anakuwa ni mshindi wa tatu wa zawadi ya shilingi milioni 10 ambayo hutolewa kila wiki kwa mshindi mmoja kupitia Promosheni inayoendelea ya Tigo Jigiftishe. Milioni 10 ya kwanza ilichukuliwa na David Mmuni huku ya pili ikienda kwa Iyaka Seifu Muinga.

  Mbela aliungana na washindi wengine wanne ambao ni washindi wa kila siku ambao walikabidhiwa shilingi milioni moja moja .Akiongea muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake katika hafla iliyofanyika eneo la Chamazi jijini Dar es Salaam, Mbela alisema alipigiwa simu kuwa ameshinda akiwa likizo jijini Dar es Salaam ambapo alikuja kumtembela shangazi yake.

  “Niliamua kutumia likizo yangu kuja jijini Dar es Salaam kumsalimia shangazi yangu. Nilipofika tu nyumbani kwake Chamazi, nikapigiwa simu ya kuambiwa kuwa nimekuwa mshindi wa zawadi ya shilingi milioni 10,” anasema. Mbela aliishukuru kampuni ya Tigo kwa zawadi hiyo na kusema kuwa atatumia fedha hizo kumalizia nyumba yake.

  “Nawashauri watu watumie huduma za Tigo ili waweze kushinda. N rahisi sana kushinda haya mamilioni, mimi nimefanikiwa kushinda baada ya kuwa natumia huduma za tigo kama kutuma pesa, kununua muda wa maongezi, kununua umeme,” alisema .Akiongea wakati akimkabidhi mshindi huyo zawadi yake, Shadya Bakari kutoka Tigo aliwataka wateja kuendelea kutumia huduma mbali mbali za Tigo ili kujishindia mamilioni ya shilingi yaliyotengwa kwa ajili ya kuwazawadia katika msimu huu wa sikukuu

  Promosheni ya Jigiftishe inayoendeshwa na kampuni ya Tigo inalenga kuwazawadia wateja wanaotumia huduma za mtandao huo katika kipindi hiki cha sikukuu na mwaka mpya. Promosheni itaongeza idadi ya mamilionea katika msimu huu wa sikukuu kwa kutoa zawadi kumi za shilingi milioni moja kila siku, zawadi moja ya shilingi milioni kumi kila wiki na zawadi kwa washindi wa jumla za shilingi milioni 15, milioni 25 na milioni 50 itakayotolewa mwisho wa promosheni. 
   Mshindi wa zawadi ya wiki ya shilingi milioni 10 katika promosheni ya Jigiftishe na Tigo, Mbwana Saidi Mbela (wa kwanza kulia) akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi kutoka kwa Shadya Bakari (kulia) wa Tigo katika hafla iliyofanyika Chamazi jijini Dar es Salaam. Katikati ni Verykeys Julius kutoka Kitengo cha Biashara Tigo
   Mshindi wa zawadi ya wiki ya shilingi milioni 10 katika promosheni ya Jigiftishe na Tigo, Mbwana Saidi Mbela (wa tatu kulia) akipongezwa na washindi wa kila siku wa shilingi milioni moja moja pamoja na wafanyakazi wa Tigo muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake katika halfa iliyofanyika Chamazi jijini Dar es Salaam 
   Mmoja wa washindi wa zawadi ya kila siku ya shilingi milioni moja kwenye promosheni ya Jigiftishe na Tigo, Theresia Philipo (wa kwanza kulia) akilia kwa furaha wakati akikadihiwa  mfano wa yenye thamani ya shilingi milioni moja na Shadya Bakari (wa kwanza kushoto) kutoka Tigo katika hafla iliyofanyika Chamazi jijini Dar es Salaam. Katikati ni Verykeys Julius kutoka Kitengo cha Biashara Tigo
   Washindi wa zawadi za kila siku za shilingi milioni moja moja katika Promosheni inayoendelea ya Jigiftishe na Tigo wakiwa na nyuso za furaha muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi zao katika hafla fupi iliyofanyika Chamazi jijini Dar es Salaam

   Mmoja wa washindi wa zawadi ya kila siku ya shilingi milioni moja katika promosheni inayoendelea ya Jigiftishe na Tigo, Hanifa Hassani Rashidi (kulia) akipokea mfano wa hundi kutoka kwa wanyakazi wa Tigo Shadya Bakari (kusho) na Verykeys Julius katika haflaya kuwakabidhi washindi zawadi  iliyofanyika Chamazi jijini Dar es Salaam
  Mmoja ya washindi wa kila siku wa shililingi milioni moja katika promosheni ya Jigiftishe inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Khaled Miraji Sabuni (katikati) akipokea mfano wa hundi kwa wafanyakazi wa Tigo, Shadya Bakari (kushoto) na Verykeys Julius (kulia) katika hafla iliyofanyika Chamazi jijini Dar es Salaam

   

  0 0

  Makamu Mwenyekiti wa Ulingo Nancy Mrikaria akishiriki kufanya usaifi na wanachama wenzake kwenye soko la Mawananyamala kama maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake ambapo kilele chake kitafanyika Desemba 10 mwaka huu.
  Mjumbe wa Sekretarieti ya Ulingo Bi Saumu Rashid akibandika kipeperushi chenye ujumbe wa kuhamasisha wanawake kujiunga katika vyombo vya maamuzi na kupinga ukatili dhidi ya wanawake katika moja ya kuta za soko la Mwananyamala wakati wanachama wa taasisi hiyo walipofanya usafi sokoni hapo leo.
  Picha mbalimbali zikionyesha baadhi ya wanachama wa Taasisi ya Ulingo wakishiriki kufanya usafi katika soko la Mwananyamala ambapo pia wamewahamasisha wanawake kujiunga katika vyombo vya kufanya maamuzi.
  Mjumbe wa Sekretarieti ya Ulingo Bi Saumu Rashid akishiriki kufanya usafi katika soko la Mwananyamala pamoja na wenzake.
  Mmoja wa wanachama wa Taasisi ya Ulingo Salma Masoud akibadika kipeperushi chenye ujumbe wa kuhamasisha wanawake kujiunga katika vyombo vya maamuzi na kupiga vita unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake katika moja ya bajaji katika soko la Mwananyamala.  Na Said Mwishehe Globu ya Jamii

  TAASISI Ulingo ambayo inajihusisha na kusimamia wanasiasa wanawake wa vyama vyote nchini imefanya usafi kwenye Soko la Mwananyamala jijini Dar es Salaam huku ikitumia nafasi hiyo kuwahimiza wanawake wanaofanya kazi katika shughuli mbalimbali kuhakikisha wanashiriki kugombea nafasi zenye maamuzi.

  Mbali ya kuhimiza wanawake kushiriki kugombea nafasi zenye maamuzi, pia wamekemea tabia ya vitendo vya rushwa ya ngono ambapo wamesema wanaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano ambayo imekuwa mstari wa mbele kukomesha vitendo vya rushwa ikiwamo rushwa ya ngono.

  Wakizungumza leo mapema asubuhi wakati wa kufanya usafi kwa kufagia maeneo yanayozunguka soko hilo la Mwanayamala ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake, wadau mbalimbali wa taasisi hiyo wakiongozwa na viongozi wao wamesema wao kama taasisi inayosimamia wanasiasa wanawake wamekuwa na jukumu la kuendelea kuhamasisha wanawake nchini unapotokea uchaguzi washiriki ili wawe sehemu ya nafasi za maamuzi.

  Makamu Mwenyekiti wa taasisi hiyo Nancy Mrikaria amesema pamoja na kufanya usafi sokoni hapo wamepata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya viongozi wa soko na moja ya kitu ambacho wamebaini bado kuna idadi ndogo ya wanawake kwenye nafasi za uongozi katika soko hilo , hivyo wameendelea kuwahamasisha ili utakapotokea uchaguzi mwingine wajitokeze kugombea nafasi za uongozi kwa maendeleo ya soko na Taifa kwa ujumla.

  "Moja ya jukumu letu ni kuwahamasisha wanawake kujitokeza kuwania nafasi za uongozi na hasa ambazo zinahusu maamuzi ili kufikia asilimia 50 kwa 50 katika ngazi ya maamuzi.Kwa mfano ndani ya nafasi za uongozi katika Soko hili la Mwananyamala idadi ya wanawake iko chini , hivyo ni kazi yetu kuwakumbusha wanawake wote kwenye maeneo yote kutambua wanayo nafasi ya kugombe nafasi za uongozi,"amesema Mrikaria na kuongeza uongozi ni haki ya watu wote.

  Kwa upande wa Mjumbe wa Sekretarieti ya Ulingo Saum Rashid amesema taasisi yao imeamua kufanya usafi kwenye soko hilo kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhimiza usafi wa mazingira nchini ambapo ameelezea namna ambavyo wameitumia siku hiyo kusambaza vipeperushi vinavyozuia rushwa ya ngono.

  "Tumefanya usafi kwenye soko la Mwananyamala leo hii, tukiri tu ni jukumu letu sisi wadau wa taasisi ya Ulingo kushiriki kikamilifu kwenye kuweka mazingira yetu safi.Tunajua tunalojukumu pia la kusimamia wanasisa wanawake kutoka vya vyama vyote nchini kuhakikisha wanagombea nafasi zenye maamuzi.Kwetu sisi ni fahari kubwa kufanya usafi soko la Mwananyamala, tumezungumza mengi na viongozi wa soko hili lakini tumeelezea namna ambavyo kuna umuhimu wa kuendelea kukomesha rushwa ya ngono,"amesema.

  Ameongeza kuwa kwenye maeneo mengi yakiwamo ya sokoni , kumekuwa na lugha nyingi ambazo zinatolewa za kumdhalilisha mwanamke, hivyo wanaiomba jamii kumheshimu mwanamke kokote aliko."Tunaomba wanawake wanaofanya kazi kwenye maeneo yoyote yale waheshimiwe, ukifika kwenye masoko utasikia baadhi ya watu wanavyotoa lugha za kumdhalilisha mwanamke. Wapo wasichana ambao wanafanya biashara ya mama lishe lakini baadhi ya watu wanaona kama vile wapo kwenye biashara hiyo kwa ajili ya kujiuza.Hii si sawa hata kidogo na tunaikemea vikali,"amesema Rashid.

  Wakati huo huo Mwenyekiti wa Soko la Mwananyamala Mbaraka Salum amewashukuru wanawake wa Ulingo kufanya usafi sokoni hapo na kwamba wamefurahishwa na uamuzi wao wa kuchagua soko lao.Hata hivyo amesema changamoto kubwa iliyopo taka hizo ambazo zimekusanywa baada ya kufanyika usafi hawana pa kuzipeleka kwani gari ya manispaa kwa wiki inafika mara moja na hivyo taka kuzagaa.

  "Changamoto yetu kubwa hapa ni gari la taka , kwa wiki linakuja mara moja tu.Hivyo taka zinajazana na kama uavyojua kuna taka zikikaa zaidi siku moja zinaanza kuharibika na kutoa harufu kali, hivyo tunaomba manispaa waje wachukue taka kwa wakati.Tunafirikia kubeba taka hizi na kuzipeleka manispaa kwani wao ndio watajua wapi wanatakiwa kuzipeleka na Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam alishawahi kusema kama taka hazizolewi na zinarundikana sehemu moja basi zibebebwe zipelekwe ofisi ya mazingira,"amesema Salum.

  Kuhusu usawa kwenye nafasi za uongozi katika soko hilo, Salum amesema wamekuwa wakihamasisha wanawake kugombea uongozi lakini changamoto iliyopo idadi ya wanaojitokeza ni ndogo ambapo amefafanua uchaguzi uliopita sokoni hapo walijitokeza watatu na hivyo wawili wakachaguliwa "Kati ya viongozi tisa wa soko la Mwananyamala wanawake wapo wawili tu na wanaume saba, sababu kubwa wanawake wenyewe hawajitokezi kugombea pindi uchaguzi unapotangazwa lakini tunaendelea kuwahamasisha."

  0 0


  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akielezea kuhusu taaluma ya Uhasibu kuwa nia muhimu katika maendeleo ya Viwanda na kutimiza ndoto ya Serikali ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 wakati wa kuhitimisha mkutano wa mwaka wa Wahasibu na kugawa tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa washindi wa mwaka 2017, katika Kituo cha Uhasibu na Ukaguzi eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akimkabidhi tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2017 Mhasibu Mkuu wa Serikali Msaidizi Fungu 23, Bw. Aziz Kifile, katika Kituo cha Uhasibu na Ukaguzi eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  hasibu mwandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango fungu 50, Bw. Mwita Wambura (katikati) akiwa amenyenyua tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2017 iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) eneo la Bunju, Nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mhasibu Mkuu wa Serikali, CPA. Francis Mwakapalila (katikati), Mhasibu Mkuu wa Fungu 50 Bw. Christopher Nkupama (wa pili kushoto), Mhasibu Mkuu wa Serikali Msaidizi Fungu 23, Bw. Aziz Kifile, na maafisa wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiwa na furaha baada ya kupokea tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2017 iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) eneo la Bunju, Nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

  Washindi wa wa makundi mbalimbali ya Tuzo ya taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2017 zinazotolewa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) wakiwa katika picha ya pamoja na Meza kuu baada ya kukabidhiwa tuzo hizo eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  (Picha na Peter Haule- Wizara ya Fedha na Mipango)

  Na, Peter Haule. WFM, Dar es Salaam


  Wizara ya Fedha na Mipango Fungu Hamsini (Vote 50) linalohusika na masuala ya utawala, na Fungu ishirini na tatu (Vote 23) la Mhasibu Mkuu wa Serikali yamepata tuzo ya mshindi kwa nafasi ya pili na tatu katika utoaji wa Taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2017 katika kundi la Wizara na Idara za Serikali inayoandaliwa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA).

  Tuzo hizo zimetolewa kwa washindi na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, katika Kituo cha Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu kilichopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa Mkutano wa mwaka wa Wahasibu nchini uliofanyika katika eneo hilo.

  Dkt. Kijaji alisema kuwa, taaluma ya Uhasibu inamchango mkubwa katika kukuza uchumi wa viwanda na kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 kwa kuwa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu wanahusika moja kwa moja katika suala la utawala na uongozi kupitia mipango, kudhibiti matumizi ya fedha za Serikali na pia kuweka mazingira bora ya uwekezaji kuelekea katika maendeleo ya uchumi wa viwanda hivyo kuwa na tija katika agenda hiyo ya Taifa.

  “Ni wazi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, inafanya kazi kwa bidii kuhakikisha Tanzania inakua na uchumi wa kati ifikapo 2025, jambo hili haliwezi kufikiwa na Serikali pekee bali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ambao wanaweza kutumia taaluma yao na kuishauri Serikali kwa njia mbalimbali, ikiwemo mijadala inayotokana na mikutano ya mwaka ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu”, alieleza Dkt. Kijaji.

  Alisema kuwa, ni vema Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu kuhakikisha wanaandaa taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu maendeleo ya viwanda ili wawekezaji wasipotoshwe kuhusu uhalisia wa maendeleo ya Sekta hiyo, kwa kuwa taarifa za fedha huwasaidia walipa kodi, wawekezaji na wadau wengine kufanya maamuzi.

  Aidha alisema kuw,a Serikali inaendelea kupambana na wararushwa na watumiaji wabaya wa fedha za umma, kwa kuwa bado wapo Wahasibu ambao sio waaminifu ambao wanacheza na hesabu kupitia taaluma hiyo kupotosha ukweli, alisema kipindi cha kufanya mambo hayo kimepita na yeyote anayeendelea na tabia hiyo awe na uhakika hatabaki salama kama hata badilika.

  Alibainisha kuwa suala la maadili ni muhimu sana kwa wahasibu kwa kuwa wao wanaweza kufanya Serikali ikapata mapato au kupoteza na kufanya ndoto za kuwa na uchumi wa viwanda kufikiwa au la

  Hata hivyo kufikiwa kwa uchumi wa Viwanda kunategemea uimara wa Sekta ya Umma na Binafsi kwa kuwa wote wanajukumu la msingi la kufikia maendeleo hayo kwa kuwa na taarifa za soko, taarifa za kihasibu na kutafuta suluhisho kwa masoko ya fedha.

  Naibu Waziri huyo amefurahishwa na kuongezeka kila mwaka kwa idadi ya washiriki katika ushindani wa taarifa bora ya fedha kutoka Sekta binafsi na umma, hasa Mamlaka ya Serikali za Mitaa na Taasisi za Serikali, kwa kuwa ni hatua kubwa kuelekea katika uwajibikaji na uwazi katika Sekta ya umma na kuongeza imani ya wananchi katika utendaji wa sekta hiyo.

  Naibu Waziri Kijaji, amewapongeza washindi wote kwa juhudi walizozifanya na kuwataka waendelee kufanya hivyo kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla. Aidha amewapongeza wahasibu kwa kuamua kukaa pamoja na kujadili taaluma ya uhasibu katika maendeleo ya Sekta mbalimbali ikiwemo ya viwanda ambayo ni ajenda ya kipaumbele kwa Serikali ya awamu ya tano.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA. Pius Maneno, alisema kuwa tuzo zinazotolewa na NBAA zinalengo la kuhamasisha uwajibikaji na kuandaa taarifa ya fedha zilizo na viwango vya kitaifa na kimataifa.

  Alisema kuwa washindi wa tuzo hizo wanapatikana kupitia mchakato uliosheheni weledi wa hali ya juu kutoka kwa wabobezi wa taaluma ya uhasibu nchini ambao wanaangalia vigezo kadhaa vikiwemo taasisi kusajiliwa nchini, kuwasilisha hesabu kwa wakati na pia kufikisha kiwango cha ubora wa taarifa kuanzia asilimia 75.

  Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Fungu 50, Bw. Christopher Nkupama na Mhasibu Mkuu wa Serikali Msaidizi Fungu 23, Bw. Aziz Kifile, walisema kuwa tuzo hizo walizopata zinawapa morali ya kufanyakazi kwa umahili zaidi na kuwapongeza watumishi walioko katika idara hizo kwa kufanyakazi kubwa na bila kuchoka kuhakikisha kuwa wanazingatia kanuni na taratibu za uhasibu wanapotekeleza majukumu yao.

  Mshindi wa Jumla katika tuzo hizo kwa taarifa bora ya fedha kwa mwaka 2017 ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Tanga Cement Plc na kwa upande wa Wizara na Idara za Serikali ni Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya

  Washiriki wa Tuzo hizo ni pamoja na Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Wakala wa Serikali, Wizara na Idara za Serikali na Sekta Binafsi.

  0 0


  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakionyeshwa ramani ya ofisi na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro inayojengwa katika mji wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakionyeshwa mipaka ya kiwanja na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro ya eneo linalojengwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika mji wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakipewa maelezo kuhusu ujenzi wa ofisi na Msanifu Majengo wa TBA, Bw. Kileo Yusuph wakati viongozi hao walipotembelea mji wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma kujionea maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.


  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakiangalia msingi uliochimbwa kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika mji wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma mara baada ya kutembelea eneo hilo ili kujionea maendeleo ya ujenzi wa ofisi.

  0 0

  MKUFUNZI wa Riadha kutoka Japan, Ayane Sato, anatarajiwa kushuhudia Mashindano ya Riadha ya Taifa ya Wazi ya Ngorongoro ‘Ngorongoro National Athletics Open Championship 2018’ yanayotarajiwa kurindima Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha, Ijumaa Desemba 14 mwaka huu.

  Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Msaidizi wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Ombeni Zavala, mkufunzi huyo ambaye yuko nchini kwa miaka miwili akijitolea, atashuhudia mashindano hayo ikiwa ni sehemu ya majukumu yake ya kikazi, ikiwamo kuwanoa wanariadha mbalimbali hapa nchini.Zavala, alisema itakuwa ni fursa pekee kwa Sato kujionea vipaji mbalimbali vya wanariadha kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani, jambo litakalomrahishia majukumu yake.

  Ujio wa Sato ni kutokana na mahusiano mazuri kati ya Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Kimataifa la Maendeleo (JICA), na RT.Mashindano ya wazi ya Taifa ambayo yamewezeshwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), yatashirikisha mbio za Mita 100, Relay 100×4, 200, 400, Relay 400×4, 800, 1,500, 5,000 na Mita 10,000, Kuruka Juu, Kuruka Chini, Miruko Mitatu, Kurusha Mkuki, Tufe na Kisahani kwa wanaume na wanawake.

  Washindi watakaofanya vizuri watazawadiwa zawadi za fedha na medali, ambako mshindi wa kwanza atapata Medali ya Dhahabu na kitita cha Sh. 150,000 wa pili Medali ya Fedha na Sh. 100,000 huku wa tatu akiondoka na Medali ya Shaba na Sh. 50,000.Pia watapata fursa ya kushiriki mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwamo Japan, kusaka viwango vya kufuzu mashindano ya kimataifa ikiwamo World Championship na Olimpiki.

  Sato katikati siku akitambulishwa kwa waandishi wa habari. Kulia kwake ni Katibu Msaidizi RT, Ombeni Zavala na Mjumbe RT, Tullo Chambo
   

  0 0

  Na.Imma Msumba Arumeru

  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro amefanya ziara ya kustukiza usiku wa manane katika Hospitali mbili za Wilaya na kujionea hali ya utoaji wa huduma za Afya nyakati za Usiku , ziara ambayo alianza saa Saba na nusu Usiku mpaka saa kumi na moja alfajiri.

  Hatua ya Mhe Muro kufanya ziara ya kushtukiza nyakati za Usiku katika hospitali imekuja Kutokana na kuwepo Kwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi ambao wameonyeshwa kukerwa na huduma duni za Afya zinazotolewa nyakati za Usiku ikiwemo kutokuwepo Kwa wataalamu katika maeneo yao ya kazi kama inavyotakiwa Kwa mujibu wa sheria, Kanuni na taratibu.

  Akiwa katika Hospitali ya Halmashauri ya wilaya (ARUSHA DC) Hospitali ya Oltrumet Mhe. Muro Alifika katika Eneo la mapokezi ambalo mbali na milango kuwa wazi pamoja na nyaraka na baadhi ya Madawa na vifaa tiba lakini hapakuwa na mtu yoyote katika eneo hilo na badala yake kazi ya mapokezi aliachiwa Askari mgambo anaelinda hospitali hiyo ambapo huwapokea wagonjwa na kisha kwenda KUWAAMSHA WAHUSIKA AMBAO MUDA MWINGI WANAKUWA Wamelala tukio ambalo limeshuhudiwa na Mhe Muro ambae alilazimika kwenda katika Hospitali hiyo akiwa na Usafiri Binafsi wa pikipiki na gari lingine la kawaida moja.

  Pia Dc Muro alitembelea katika jengo la upasuaji na kukuta tukio la kukera ambapo wauguzi na wahusika wa chumba hicho walikuwa wamelala uku wamejifunika mablanketi hatua iliyomlazimu Mhe Muro kuwaamsha jambo ambalo liliwafanya wakimbie wakihisi wamevamiwa na Mzimu.

  Pamoja na kuwepo Kwa changamoto hizo, Mhe Jerry Muro alioonyeshwa kufurahishwa na kitendo Cha muuguzi wa zamu katika jengo la kujifungulia kina mama ambae mbali na kuwa mwenyewe lakini alikuwa akitimiza wajibu wake wa kuendelea kuwahudumia kina mama ambao baadhi walikuwa katika hatua za kujifungua.

  Baada ya kumaliza ziara katika Hospital ya Halmashauri ya Arusha ya Oltrumet Mhe Muro alitembelea hospital ya Halmashauri ya Meru ya Tengeru kujionea pia huduma za matibabu nyakati Za Usiku ambapo akiwa katika hospital hiyo aliwakuta baadhi ya wataalamu wakiwajibika ikiwemo muuguzi wa zamu katika eneo la mapokezi , pamoja na wauguzi wa wodi za kina mama , kina baba, watoto na pamoja na eneo la jengo la wazazi ambapo alikuta huduma zikiendelea kama kawaida uku Mganga wa zamu akiwa amelala, ambapo hata hivyo alikerwa na kitendo Cha kutokuwepo katika eneo la kazi kwa Dereva wa gari la wagonjwa ( Ambulance ) ambapo walitumia zaidi ya nusu saa kumtafuta pasipo kupatikana.

  Wakizungumzia ziara hiyo ya aina yake , baadhi ya wagonjwa na ndugu waliokuwa wakipatiwa huduma katika Hospital hizo mbali na kupongeza hatua ya Mhe Muro kuzunguka usiku kujionea hali ya utoaji wa huduma wamesema kitendo hicho kitaisaidia kuwazindua wafanyakazi waliokuwa wakifanya kazi Kwa mazoea.

  Mhe Muro amemaliza ziara yake kwa kutoa maelekezo kwa wakurugenzi wa Halmashauri za Meru na Arusha kuchukua hatua stahiki kwa watendaji wa sekta ya Afya ambao wamekuwa wakidumaza mfumo wa utoaji wa huduma za afya nyakati za Usiku na kuagiza kila mtu anaepaswa kuingia zamu ya Usiku anatakiwa kuwa katika eneo lake la kazi hata kama hakuna wananchi wanaofika kupata huduma kwa wakati huo.

  Dc Muro amefafanua kuwa nyakati za Usiku matukio mengi ya dharura hutokea japo sio mara kwa mara lakini akawatahadharisha kuwa lazima watu wawe katika maeneo yao ya kazi ili kukabiliana na dharura hizo kwa ajili ya kuokoa maisha ya wananchi .

  Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru
   Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro Akizungumza na Waaguzi walikuwa zamu katika hospital ya Halmashauri ya Meru ( Tengeru) baada ya kufanya ziara yake ya kushtukiza usiku wa manane katika hospital hiyo.
   Dc Muro Akizungumza na moja ya wagonjwa walikuwa wamelazwa katika hospital ya Halmashauri ya Arusha Dc ( Oltrument) usiku wa kuamkia leo
   Dc Muro akipakua moja ya Nyaraka za Hospital ya Halmashauri ya Arusha Dc ( Oltrument ) alipozikuta katika chumba cha mapokezi kilichokuwa wazi na hapakuwa na mhudumu kwa muda huo.

  0 0

  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kushoto akitoa maagizo kwa Meneja wa Temesa mkoa wa Shinyanga Mhandisi Margareth Mapela wakati wa ziara yake ya kukagua karakana ya wakala mkoani humo.
  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia akikagua mojawapo ya mtambo wa kuchongea vipuri vya mashine mbalimbali katika karakana ya Temesa mkoa wa Shinyanga wakati wa ziara yake mkoani humo, watatu kulia ni Meneja wa TEMESA mkoani humo Mhandisi Margareth Mapela.
  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kushoto akimpa maelekezo Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo wa wakala huo Mhandisi Sylvester Simfukwe wakati akikagua karakana ya Temesa mkoani Dodoma.
  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia akikagua mojawapo ya kilainishi kinachotumika katika injini za magari wakati akikagua chumba cha kuhifadhia vipuri na mafuta ya vilainishi vya magari katika karakana ya wakala mkoani Dodoma. Kushoto ni Meneja wa Temesa mkoani Dodoma Mhandisi Liberatus Bikulamchi.
  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kushoto akiwapa maagizo viongozi waandamizi wa wakala huo mkoani Shinyanga wakati akikagua baadhi ya mitambo katika karakana hiyo, kulia ni Meneja TEMESA wa mkoa Mhandisi Margareth Mapela.

  0 0   Waziri wa Nchi Ofis ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Kapteni Msaafu George Mkuchika akimkabidhi Tuzo, Bw.Vita Kawawa aliyeambatana na mwanafamilia mwenzake Bibi. Zamaradi Kawawa kwa niaba ya Waziri Mkuu wa zamani Hayati Rashid Mfaume Kawawa ikiwa ni kuthamini mchango wake katika kukuza lugha ya Kiswahili kupitia sanaa ya maonesha na michezo ya kuigiza wakati wa hafla ya kilele cha Kamapeni ya Uzalendo na Utaifa leo jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bibi Susan Mlawi akimkabidhi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kwa niaba ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli zawadi ya Kamusi Kuu ya Kiswahili iliyotolewa na Baraza la Kiswahili Tanzania (Bakita) wakati wa Kilele cha Kampeni za Uzalendo na Utaifa mwaka 2018 leo jijini Dodoma. Kauli mbiu ya Kampeni hizo kwa mwaka huu ni ” Kiswali Utashi Wetu, Uhai Wetu”. Anayeshuhudia ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza.
  UZ3b
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa CD za makala ya uzalendo wakati wa hafla za Kilele cha Kampeni za Uzalendo na Utaifa mwaka 2018 leo jijini Dodoma. Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bibi Susan Mlawi. Kauli mbiu ya Kampeni hizo kwa mwaka huu ni ” Kiswali Utashi Wetu, Uhai Wetu”.
  UZ3c
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza (kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bibi Susan Mlawi wakionyesha CD za makala ya uzalendo mara baada ya kuzinduliwa rasmi wakati wa hafla za Kilele cha Kampeni za Uzalendo na Utaifa mwaka 2018 leo jijini Dodoma. Kutoka kulia ni. Kauli mbiu ya Kampeni hizo kwa mwaka huu ni ” Kiswali Utashi Wetu, Uhai Wetu”.
  UZ3d
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi Kitabu cha Uzalendo wakati wa hafla za Kilele cha Kampeni za Uzalendo na Utaifa mwaka 2018 leo jijini Dodoma. Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bibi Susan Mlawi. Kauli mbiu ya Kampeni hizo kwa mwaka huu ni ” Kiswali Utashi Wetu, Uhai Wetu”.

  UZ5b
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akimkabidhi Tuzo mmoja  ya wasanii wakongwe kwa kutambua mchango wake katika kukuza lugha ya Kiswahili kupitia sanaa ya muziki wakati wa hafla ya kilele cha Kamapeni ya Uzalendo na Utaifa leo jijini Dodoma.
  UZ5c
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Masuala ya Ulemavu na Bunge, Stella Ikupa akimkabidhi cheti Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita), Dkt. Selemani Sewangi kwa kutambua mchango wake katika kukuza lugha ya Kiswahili wakati wa hafla ya kilele cha Kamapeni ya Uzalendo na Utaifa leo jijini Dodoma. Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe. (Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO)
  UZ7UZ8 
  UZ0a
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa hafla za Kilele cha Kampeni za Uzalendo na Utaifa mwaka 2018 leo jijini Dodoma. Kauli mbiu ya Kampeni hizo kwa mwaka huu ni ” Kiswali Utashi Wetu, Uhai Wetu”.
  UZ0b
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bibi Susan Mlawi akizungumza wakati wa Kilele cha Kampeni za Uzalendo na Utaifa mwaka 2018 leo jijini Dodoma. Kauli mbiu ya Kampeni hizo kwa mwaka huu ni ” Kiswali Utashi Wetu, Uhai Wetu”.
  UZ0c
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza akitoa neno la shukrani  wakati wa hafla za Kilele cha Kampeni za Uzalendo na Utaifa mwaka 2018 leo jijini Dodoma. Kauli mbiu ya Kampeni hizo kwa mwaka huu ni ” Kiswali Utashi Wetu, Uhai Wetu”.
  UZ1b
  Msanii Mrisho Mpoto akitumbuiza mbele ya washiriki wa hafla ya Kilele cha Kampeni ya Uzalendo na Utaifa mwaka 2018 leo katika ukumbi wa DCC jijini Dodoma. Kauli mbiu ya Kampeni hizo kwa mwaka huu ni ” Kiswali Utashi Wetu, Uhai Wetu”.
  UZ2
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Dkt. Ayoub Ryoba akielezea jambo wakati wa mdahalo kuhusu Uzalendo na Utaifa wakati wa Kilele cha Kampeni ya Uzalendo na Utaifa mwaka 2018 leo jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Tanzania (Bakita), Dkt. Seleman Sewangi.
  UZ4a
  Baadhi ya washiriki wa hafla ya Kilele cha Kampeni za Uzalendo na Utaifa mwaka 2018 wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa DCC jijini Dodoma leo. Kauli mbiu ya Kampeni hizo kwa mwaka huu ni ” Kiswali Utashi Wetu, Uhai Wetu”.
  UZ4bUZ4c


  0 0
  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

  Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) imekabidhiwa tuzo kwa kuwa Taasisi katika kundi la Wakala bora ya Serikali ulioandaa na kuwasilisha taarifa za kifedha zenye kiwango cha Kitaifa na Kimataifa kwa mwaka 2017.

  Tuzo hizo zimekabidhiwa na Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt Ashantu Kijaji  mwishoni mwa wiki Desemba 8, 2018 katika ukumbi wa APC Bunju Jijini Dar es Salaam.

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji akihutubia na kufunga mkutano wa mwaka wa Wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu NBAA, amezitaka taasisi nyingine za Serikali kuiga mifano hiyo kwani awamu hii ya tano chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli inahimiza matumizi sahihi ya fedha za umma ili zitumike katika utoaji wa huduma bora sambamba na kulifikisha Taifa katika uchumi wa Kati wa kilimo na viwanda. 

  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Emmy Hudson amesema kuwa kwa tuzo waliopata inawapa moyo katika kuendelea kuchapa kazi kwa katika kuandaa vitabu vya mahesabu kwa viwango vya kitaifa na Kimataifa.

  Amesema kuwa ushindi huo ni kutokana na kufanya kazi kwa ushirikiano na wahasibu na ndio matokeo yake taasisi inaibuka na ushindi ambao kila mtu anafurahi.Hudson amesema kuwa hata mwakani watafanya vizuri zaidi kutokana na ushindi huo ambao watu wengine wanakosa.
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akikabidhi tuzo kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bi Emmy Hudson kwa Taasisi yake kuwa Wakala ya Serikali iliyoandaa taarifa bora ya kifedha yenye kiwango cha Kitaifa na Kimataifa kwa mwaka 2017, sherehe za makabidhiano ya tuzo hizo yaliyofanyika katika ukumbi wa APC Bunju Jijini Dar es Salaam. 
  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bi Emmy Hudson akionesha tuzo ya kuwa uwa Wakala ya Serikali iliyoandaa taarifa bora ya kifedha yenye kiwango cha Kitaifa na Kimataifa kwa mwaka 2017, sherehe za makabidhiano ya tuzo hizo yaliyofanyika katika ukumbi wa APC Bunju Jijini Dar es Salaam. 
  Picha ya pamoja ya wadau waliotunukiwa tuzo katika zinazotolewa na NBAA zilizofanyika katika katika ukumbi wa APC Bunju Jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Azania , Charles Itembe (kulia) akipongezana na  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya Watumishi wa Umma (PSSSF) Bw Eliud Sanga wakati wa kikao kifupi  kilichofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma ili kutathmini mwenendo wa benki hiyo  ikiwemo ufunguzi wa tawi lake jipya jijni humo. Mfuko wa PSSSF ni moja ya wanahisa wakubwa wa benki hiyo.
   Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Azania , Charles Itembe (kulia) akimkabidhi zawadi kwa Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya Watumishi wa Umma (PSSSF) Bw Valerian Mablanketi wakati wa kikao kifupi  kilichofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma ili kutathmini mwenendo wa benki hiyo  ikiwemo ufunguzi wa tawi lake jipya jijni humo. Mfuko wa PSSSF ni moja ya wanahisa wakubwa wa benki hiyo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Azania , Charles Itembe (wa tatu kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya Watumishi wa Umma (PSSSF) Bw Eliud Sanga (kulia kwake) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi waandamizi wa Benki ya Azania pamoja na Mfuko wa PSSSF wakati wa kikao kifupi  mara baada ya kumaliza kikaohicho.

  0 0

  *Naibu Gavana ahimiza uwajibikaji kwa waandishi wa habari nchini

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  BENKI Kuu ya Tanzania(BoT) ,imesema imeamua kuanzisha utaratibu wa kuendesha semina kwa waandishi wa habari wa vyombo vya habari nchini kwa lengo la kukuza uandishi wa habari za uchumi na fedha.

  Pia lengo la semina hiyo kwa waandishi wa habari nchini ni kuelimisha na kufafanua masuala yanayohusu majukumu na kazi za Benki Kuu , kujenga uwezo wa kutafsiri na kuchambua taarifa za uchumi na fedha, kuboresha na kudumisha uhusiano mzuri wa kikazoi kati ya vyombo vya habari na BoT.

  Malengo mengine ya semina hiyo ni kupata mrejesho kutoka kwa waandishi wa habari kuhusu utendaji wao wa kazi na njia bora ya kudumisha mawasiliano baina ya taasisi zao.
   
  Hotuba ya Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) upande wa Uchumi na Sera Dk. Yamungu Kayandabila ambayo imesomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Tawi la Benki Kuu Dodoma Richard Wambali amesema benki hiyo inatambua mchango wa vyombo vya habari nchini katika kuufahamisha umma wa Watazanzania na dunia
  kwa ujumla.

  "Mara kadhaa mmekuwa msaada mkubwa sana katika kutufikishia taarifa zetu kwa umma, na wakati mwingine baada ya kupokea mwito wa muda mfupi.Pia kupitia kazi zenu mnatuwezesha kujua ni nini wananchi wanasema au kutarajia kutoka katika taasisi zetu."Benki Kuu ya Tanzania imekuwa ikiendesha semina kama hii, tumeshuhudia kuimarika kwa uandishi wa habari za uchumi na fedha katika vyombo mbalimbali vya habari.Matokeo haya mema yametupa uthibitisho kwamba mafunzo tunayotoa kwa wadau wetu wakuu yana manufaa makubwa,"amesema.

  Pia amesema wameshuhudia kuendelea kukua kwa ushirikiano kati ya BoT na vyombo vingi vya habari zikiwemo redio, televisheni , magazeti na mitandao ya kijamii na kwamba uhusiano huo unadhirihishwa kupitia maswali mengi na ya mara kwa mara wanayoyapata kutoka kwa mwandishi mmoja mmoja au kupitia idara yao ya uhusiano wa umma na itifaki.

  Ametumia nafasi hiyo kusisitiza umuhimu wa kuzingatia maadili na kauni zinazoongoza tasnia ya habari kwa sababu wajibu wa wanahabari katika kuchangia maendeleo ya ustawi wa jamii ni mkubwa ambapo amesisitiza uandishi wa habari unaozingatia uwajibikaji pamoja na kuandika habari za usahihi.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO)Zamaradi Kawawa ameipongeza BoT kwa kutoa mafunzo yanayohusu habari za uchumi na fedha hasa kwa kuzngatia mafunzo hayo yameendelea kuwajengea uwezo waandishi wa habari nchini kuandika kwa usahihi na weledi.

  Wakati huo huo waandishi wa habari waliokuwa kwenye semina hiyo wameipongeza BoT kwa kuendelea kuandaa semina hizo kwani zimekuwa zikiwajengea uwezo hasa wa kuandika habari za biashara na uchumi kwa ufasaha zaidi. Pia wamesema kutokana na semina hiyo kumekuwa na uhusiano mzuri kati ya BoT na waandishi wa vyombo vya habari nchini

  Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania tawi la Dodoma Bw. Richard Wambali aliyemwakilisha Dkt. Yamungu Kayandabila Naibu Gavana anayeshughulikia Uchumi na Fedha akifungua semina ya siku tano ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kuhusu masuala ya uchumi na fedha inayofanyika kwenye ukumbi wa (BOT) jijini Dodoma.

  0 0

  Una mpango wa kusafiri? Zingatia haya

  Ni wakati mwingine tena wa msimu wa sikukuu za Krismasi na mapumziko ya mwisho wa mwaka. Katika kipindi hiki tunashuhudia pilikapilika za hapa na pale watu wakijiandaa namna watakavyosherehekea.

  Kuna baadhi ya watu wanafikiria kusafiri nje ya mikoa waliyopo kwa ajili ya kusherehekea. Watu wengi wana kawaida ya kusafiri kurudi waliko zaliwa na kukulia ili kujumuika pamoja na ndugu na jamaa zao. Wengine hupanga kwenda kutembelea vivutio vya kutalii kwenye mikoa tofauti na walipo.

  Kipindi cha nyuma kidogo usafiri wa umma ndio ulikuwa tegemezi ukilinganisha na sasa ambapo baadhi ya wasafiri wanamiliki usafiri wao binafsi. Kusafiri kwa usafiri binafsi kuna faida lukuki hususani kama mko wengi na wote mnakwenda sehemu moja. Hupunguza gharama lakini mnakuwa huru kuamua msafiri namna gani, muda wa kuondoka na kufika, kupumzika njiani nakadhalika.
  Pamoja na faida lukuki za kusafiri kwa kutumia usafiri ubinafsi, yafuatayo ni masuala ya msingi kuyazingatia kabla ya kuanza safari yako.

  Jipange mapema. Kabla ya kuanza safari yako hakikisha kuwa chombo chako cha usafiri kipo kwenye hali salama. Hali ya hewa inatofautiana kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine hivyo huna budi kuhakikisha gari lako linakuwa na uwezo wa kuhimili hali yoyote itakayokutana nayo safarini. Wasiliana na fundi wako ambaye huwa analihudumia gari lako mara kwa mara ili kukusaidia katika hili.

  Pumzika vya kutosha. Miongoni mwa sababu iliyotajwa kusahaulika kuwa inachochea kutokea kwa ajali nyingi za barabarani ni madereva kutopumzika vya kutosha kabla ya safari. Hivyo basi kama dereva ambaye unatarajia kuendesha chombo cha usafiri kwa umbali mrefu hakikisha kuwa unapata muda wa kutosha kupumzika. Hii itakusaidia mwili kuwa katika hali nzuri na kupelekea umakini mkubwa barabarani.

  Kuwa makini na mwendo kasi. Hakuna haja ya kushindana kwa mwendo kasi na madereva wengine barabarani. Zingatia umbali wa kutosha baina yako na chombo kingine cha usafiri ili kuweza kuepuka ajali pindi itakapotokea. Takwimu tofauti duniani zinaonesha kuendesha gari kwa mwendo kasi kunapelekea ajali nyingi, majeruhi wengi na hata vifo zaidi. Unashauriwa kuendesha kwa kuzingatia alama za barabarani.

  Epuka vishawishi. Kumekuwa na kawaida ya baadhi ya madereva kuendesha gari huku wakiwa wanazungumza na simu, kusoma au kuandika jumbe za maneno, pamoja na kuperuzi kwenye simu zao za mkononi. Kuendesha chombo cha usafiri kunahitaji umakini wako wote. Endapo kutakuwa na ulazima wa kutumia simu yako ya mkononi hakikisha unaegesha gari pembeni ya barabara ili kukidhi haja yako halafu uendelee na safari.

  Endesha kwa kujihami. Barabarani kunaweza kuwa na sababu tofauti ambazo zinaweza kukuondolea umakini wako. Barabara zinaweza kuwa katika hali mbaya hivyo kupelekea kupata ajali kwa urahisi. Au kunaweza kuwepo na madereva wenye kuendesha kwa kasi kuwahi huko waendapo. Wapuuze madereva wa aina hii wala usishindane nao. Hakikisha unaweka usalama wako na wa abiria uliowabeba kwanza.

  Usiendeshe ukiwa umelewa. Kama una mpango wa kunywa pombe, achana na mpango wa kuendesha. Pombe ni miongoni mwa sababu kubwa inayopelekea ajali nyingi za barabarani. Kama una mpango wa kuendesha chombo cha usafiri hakikisha hautumii kilevi cha aina yoyote na endapo utafanya hivyo basi hakikisha unakabidhi usukani kwa mtu mwingine.
  Mbali na kujiandaa mapema kwa ajili ya kusafiri, pia unashauriwa kupanga mapema masuala ya malazi. Unaweza kukamilisha mipango ya safari yako kwa kujihakikishia malazi kupitia Jumia Travel. Katika msimu huu wa sikukuu huduma ya malazi huwa na uhitaji mkubwa kutokana na watu wengi kusafiri sehemu mbalimbali. Unaweza kuokoa kiasi kikubwa cha fedha, kuepuka usumbufu wa dakika za mwisho kwa kufanya huduma zako mapema pamoja na kuwa na uhakika wa malazi huko uendako

  0 0

   Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania tawi la Dodoma Bw. Richard Wambali aliyemwakilisha Dkt. Yamungu Kayandabila Naibu Gavana anayeshughulikia Uchumi na Fedha akifungua semina ya siku tano ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kuhusu masuala ya uchumi na fedha inayofanyika kwenye ukumbi wa (BOT) jijini Dodoma. 

  Katika semina hiyo wanahabari watapata ufafanuzi wa masuala yanayoshughulikiwa na benki hiyo pamoja na mabenki ya biashara ya kifedha nchini Tanzania kwa kufuata sheria kanuni na taratibu zinazosimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa na kushoto ni Bi. Zalia Mbeo Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki (BOT) 
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa akizungumza katika semina hiyo inayofanyika kwenye tawi la Tenki Kuu jijini Dodoma katikati ni Mkurugenzi wa Benki Kuu Tawil la Dodoma Bw. Richard Wambali na kulia ni Bi. Zalia Mbeo Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki (BOT).
  Bi. Zalia Mbeo Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki (BOT) akizungumza katika semna hiyo inayofanyika kwenye tawi la Benki Kuu jijini Dodoma katikati ni Mkurugenzi wa Benki Kuu Tawil la Dodoma Bw. Richard Wambali na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa.
  Kaimu Meneja wa Idara ya Uhusiano na Itifaki, BoT, Bi. Vicky Msina akitoa maelezo ya utangulizi wa semina hiyo kabla ya kufunguliwa rasmi na Mkurugenzi wa Benki Kuu Tawi la Dodoma Bw. Richard Wambali.
  Dkt. Suleiman Missango, Meneja Msaidizi-Idara ya Utafiti, Kurugenzi ya Sera za Uchumi na Utafiti, BoT akizungumzia mambo mbalimbali yatakayojadiliwa katika semina hiyo.
  Mwenyekiti wa Semina hiyo Bw. Nurdin Suleiman akiteta jambo na katibu wa semina hiyo Bi Dorcas Raymos kabla ya kuanza kwa semina hiyo.
  Dkt. Suleiman Missango, Meneja Msaidizi-Idara ya Utafiti, Kurugenzi ya Sera za Uchumi na Utafiti, BoT akiwa na watoa mada wengine kutoka benki kuu tayari kwa kutoa mada katika semina hiyo.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika semina hiyo.
  Kaimu Meneja wa Idara ya Uhusiano na Itifaki, BoT, Bi. Vicky Msina akiwa pamoja na wanahabari wanaohudhuria semina hiyo.
  Beatrice Lyimo kutoka Idara ya habari Maelezo katikati akiwa pamoja na baadhi ya wanahabari wanaohudhuria katika semina hiyo.

  0 0

  *Shahidi asema Kiluwa alipata viwanja hivyo kwa utaratibu wa kawaida
  *Akana kuomba wala kupokea rushwa...aeleza namna hati zilivyomfikia

  Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

  MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam imeelezwa kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Steal Group. Co.ltd na Kiluwa Free Processing Zone, Mohamed Kiluwa (50)  alipata hati za viwanja 70 
  kihalali kwa kufuata taratibu zote za ardhi.

   Kamishna Msaidizi wa Ardhi, Mathew Nhonge ambaye ni shahidi wanne wa upande wa mashtaka, ameyasema hayo leo  mbele ya Hakimu Mkazi Samweli Obas, alipokuwa akitoa ushahidi dhidi ya kesi ya kutoa rushwa Sh.milioni 90 kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi

  Akijibu maswali ya Wakili wa utetezi Imani Madega, shahidi huyo amedai Kilua alipata viwanja hivyo kutoka Halmashauri kwa utaratibu wa kawaida na viwanja hivyo vyote vilipimwa na ardhi.

  Anadai hati zote zilizosainiwa kila kitu katika hati hizo kilikuwa sawa sawa na aliridhika nazo ndio sababu alisaini. Alipohojiwa kama katika mchakato wote huo walimuomba fedha mshtakiwa au alipewa fedha yoyote, shahidi alikana kuwa hajapewa fedha wala kuomba hela kwa Kilua. Pia amedai hakuona wakati rushwa hiyo ikitolewa, hati za mshtakiwa alizipata kihalali na endapo Mahakama itaamua vinginevyo Wizara haitabisha .

  Wakati akitoa ushahidi wake, shahidi huyo akiongozwa  na Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Maghela Ndimbo, shahidi Mathew amedai Kampuni ya Kilua iliomba kumiliki ardhi maeneo ya Kikongo wilayani Kibaha, hati za kumiliki 
  viwanja 73 zilimfikia kwa ajili ya kuzisaini. 

  Amedai katika hati hizo, hati 70  zilisainiwa kisha kupelekwa kwa Msajili wa hati na hati tatu hazikusainiwa kwa sababu zilikuwa na mapungufu.Shahidi huyo amedai, baada ya kusainiwa kwa hati hizo, Julai 13 mwaka huu alipigiwa simu na Waziri Lukuvi akimuelekeza amfahamishe Kilua aende ofisini kwake akiwa na hati zake. 

  Pia amedai alimpigia mtu aliyemtaja kwa jina la Shabani na kumtaka amfikishie taarifa Kilua ambapo Julai 16 mwaka huu, Kilua alienda 
  ofisini kwa Waziri aliyetaka hati hizo ziongezewe masharti kudhibiti hasa katika uwekezaji wa viwanda. Mathew ameendelea kudai, Kilua alifika kwa Waziri baada ya kukutana naye mapokezi ya kwenda ofisini kwa Waziri lakini amedai hakujua kilichondelea mpaka aliposikia kwa watumishi wa wizara kwamba Kilua kakamatwa kwa rushwa. 

  Amedai, kutokana na kuwepo kwa taarufa hizo za suala la rushwa hati zote 70 zilifutwa katika usajili chini ya kifungu namba 178 cha sheria ya ardhi namba nne,"alidai. Katika kesi hiyo, inadaiwa Julai 16, mwaka huu kati ya saa sita na saa nane mchana akiwa Mkurugenzi wa kampuni hizo mbili alitoa rushwa ya Dola za Marekani 40,000 ambazo ni sawa na Sh.milioni 90 kwa Waziri Lukuvi.

  Mshtakiwa anadaiwa kutoa fedha hizo kwa lengo la kwamba asiwasilishe hati ya umiliki wa kiwanja namba 57 Block B Kikongo na D Disunyura kilichopo eneo la viwanda lililopo Kibaha mkoani Pwani.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  katika Kilele cha Maadhimisho ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa  kwenye Kiwanja cha Nyerere Squre jijini Dodoma, Desemba 10, 2018. 
   Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika  Kilele cha Maadhimisho ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa kwenye Kiwanja cha Nyerere Square jijini Dodoma, Desemba 10, 2018. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni  (mstaafu), George Mkuchika katika Kilele cha Maadhimisho ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa kwenye  Kiwanja cha Nyerere Square  jijini Dodoma, Desemba 10, 2018.

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi (katikati ) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni  (mstaafu), George Mkuchika baada ya kuhutubia katika Kilele cha Maadhimisho ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa kwenye Kiwanja cha Nyerere Square jijini Dodoma, Desemba 10, 2018. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi  baada ya kuhutubia katika Kilele cha Maadhimisho ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa kwenye Kiwanja cha Nyerere Square jijini Dodoma, Desemba 10, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania.(UWT) Thuwaiba Editon Kisasa, kulia Katibu Mkuu wa UWT, Queen Mlozi na kushoto Mwenyekiti wa UWT Gaudensia  Kabaka, walipofika Ikulu Zanzibar kumtambulisha Mwenyekiti wa UWT Taifa  Kabaka.10-12-2018.
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania,(UWT) Gaudensia Kabaka,alipofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar,akiwa na Ujumbe wake wa Viongozi wa UWT.kulia Makamu Mwenyekiti wa UWT  Thuwaiba Editon Kisasa na Katibu Mkuu wa UWT. Queen Mlozi.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ukiongozwa na Mwenyekiti wa Umoja huo Gaudensia Kabaka,Makamu Mwenyekiti wa UWT Thuwaiba Editon Kisasa na Katibu Mkuu wa UWT.B. Queen Mlozi, wakiwa katika ukumbi wa mkutona Ikulu leo wakati wa mazungumzo yao walipofika kujitambulisha.kwa Rais wa Zanzibar.(Picha na Ikulu)

  0 0

  Na Veronica Simba - Dodoma
  Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen leo Desemba 10, amemtembelea Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma na kufanya mazungumzo kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta ya nishati nchini.

  Balozi Jacobsen amemweleza Naibu Waziri kuwa kampuni mbalimbali nchini mwake zina nia ya kuwekeza katika sekta ya nishati nchini na baadhi yake ziko katika hatua nzuri kwani tayari zimewasilisha serikalini mchanganuo wake unaoainisha sifa walizonazo wakisubiri zoezi la kushindanishwa na kampuni nyingine ili kupata zabuni husika za uwekezaji.

  “Mojawapo ya kampuni hizo ina nia ya kuwekeza katika uzalishaji wa umeme wa upepo eneo la Makambako, ambapo ni ubia baina yake (52%) na wazawa (48%),” amesema Balozi. Kwa upande wake, Naibu Waziri Mgalu amemshukuru Balozi Jacobsen ambaye ni mwakilishi wa Serikali ya Norway kutokana na ushirikiano ambao nchi hiyo imekuwa ikiuonesha kwa Tanzania ikiwemo uwekezaji nchini na pia kufadhili wanafunzi katika masomo ya fani za gesi na mafuta.

  Aidha, amemweleza Balozi huyo kuwa bado zipo fursa nyingi za uwekezaji katika sekta ya nishati nchini na hivyo ametumia fursa hiyo kuendelea kukaribisha kampuni mbalimbali za Norway kuja kuwekeza.
   Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) akifafanua jambo kwa Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen wakati Balozi huyo alipomtembelea mapema leo, Desemba 10, 2018 ofisini kwake Dodoma, kujadili fursa za uwekezaji katika sekta ya nishati.
   Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen baada ya mazungumzo yao kujadili fursa za uwekezaji katika sekta ya nishati mapema leo, Desemba 10, 2018 Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma.
  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto) akiagana na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen, baada ya mazungumzo yao kujadili fursa za uwekezaji katika sekta ya nishati mapema leo, Desemba 10, 2018 Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma.

older | 1 | .... | 1748 | 1749 | (Page 1750) | 1751 | 1752 | .... | 1896 | newer