Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1747 | 1748 | (Page 1749) | 1750 | 1751 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Wajumbe wa ALAT wakipata ufahamu wa namna maji ya Ziwa Victoria yanavyovutwa na kusafishwa kasha kusambazwa kwa wananchi walipfanya zaiara wilayani Sengerema.
  Wajumbe wa ALAT wakiwa katika mtambo wa kusafisha maji kabla ya kusambaza kwa wananchi walipfanya zaiara wilayani Sengerema.
  Wajumbe wa ALAT waendelea kupata elimu katika mtambo wa kusafisha maji kabla ya kusambaza kwa wananchi walipfanya zaiara wilayani Sengerema.
  Wajumbe wa ALAT wakipanda tangi la kuhifadhi na kusambaza maji ya Ziwa Victoria walipotela ya kusambaza kwa wananchi walipfanya zaiara wilayani Sengerema.  ……………………….

  Na Robert Hokororo

  Wajumbe wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) Mkoa wa Shinyanga wamefanya ziara ya mafunzo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Wilaya ya Sengerema jijini Mwanza kujifunza namna ilivyofanikiwa katika miradi ya maendeleo.

  Miradi iliyotembelewa na wajumbe hao ni pamoja na urasimishaji na upimaji wa ardhi manispaa ya Ilemela pamoja na mradi wa maji ya Ziwa Victoria katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema. Ziara hiyo ilihusisha wajumbe wa ALAT kutoka Halmashauri za Wilaya za Kishapu, Ushetu Msalala, Shinyanga, Mji wa Kahama na Manispaa ya Shinyanga pamoja na baadhi ya wataalamu wake.

  Katika kikao kilichowakutanisha wataalamu wa Ardhi na ujumbe huo kutoka mkoani Shinyanga walipata taarifa kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na idara hiyo ambazo zimesaidia kutatua migogoro ya ardhi. Akielezea kuhusu miradi hiyo, Afisa Mipango Miji Manispaa ya Ilemela, Shukrani Kyando alisema katika mwaka uliopita walipanga kupima viwanja 16,000 na hadi sasa wamepima 33,200 huku matarajio ni kufikia 52,000.

  Alisema hadi sasa tayari wana michoro ya viwanja 52,000 ambapo wanaandaa michoro ya mipango miji baada ya kuchukua taarifa za kila nyumba ili kuweza kuwa na mji uliopangika vizuri. Kwa upande wao baadhi ya wananchi kutoka Kata ya Shibuda kuwa mradi wa urasimishaji wa ardhi wameupokea vizuri na kueleza kuwa umeweza kuondoa migogoro ya ardhi.

  Wakishukuru na kupongeza Idara ya Ardhi katika manispaa hiyo, wananchi hao walisema wamepimiwa vizuri viwanja kupitia upimaji shirikishi ambao umefanyika bila kuharibu mipango miji. Akitoa maoni kuhusu mradi huo Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Shinyanga, Ngasa Mboje aliupongeza na kusema kuwa hilo ni jambo zuri na linalofaa kuigwa na halmashauri za mkoa huo.

  Alibainisha kuwa wao kama wajumbe wa ALAT Mkoa wa Shinyanga wanayo mengi ya kujifunza kutoka katika mradi huo wa upimaji ardhi unaotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.

  “Tumeona tujifunze kutoka kwa wenzetu hawa wa Ilemela na na ni jambo zuri kwani unapima kulingana na eneo lilivyo na sisi kule kwetu (Shinyanga) tuna miji iliyoanza kupanga kwa mfano kule Mhunze (Wilaya ya Kishapu) na Old Shinyanga (Manispaa),” alidokeza Mboje.

  Wakiwa wilayani Sengerema wajumbe hao walitembelea mradi wa maji ya Ziwa Victoria na kujionea shughuli za uzalishaji maji kutoka chanzo hicho na kuyasambaza mji wa Sengerema.

  0 0

  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kuwa kesho tarehe 09 Desemba, 2018litaadhimisha Sikukuu ya miaka 57 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa kufanya shughuli mbalimbali na kutoa huduma za Kijamii kwa Wananchi.

  JWTZ litatoa huduma za tiba kwa kuwapima Wananchi magonjwa mbalimbali bila malipo.  Zoezi hilo la tiba litafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kesho Jumapili tarehe 09 Desemba 2018 kuanzia saa mbili (2.00) Asubuhi hadi saa nane (8.00) Mchana.

  Wananchi wanataarifiwa kujitokeza ili kupima afya zao. Huduma za tiba zitakazotolewa ni pamoja na Ushauri Nasaha na Upimaji wa Virusi vya Ukimwi, Huduma za Mama na Mtoto, Upimaji wa Uzito, Shinikizo la Damu na Kisukari, Afya ya Kinywa na Meno pamoja na Uchangiaji wa Damu Salama.
   Aidha, kutakuwepo na “Press Conference” na Waandishi wa Habari katika viwanja hivyo kesho saa 4:00 Asubuhi.JWTZ linakialika chombo chako cha habari wakati wa “Press Conference” hiyo.

  0 0

  Wananchi wa kijiji cha Ndunyungu kilichopo Wilayani Liwale Mkoani Lindi wamelazimika kusimamisha msafara wa Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso alipokuwa njiani kwenda kukagua mradi wa maji wa Barikiwa Wilayani humo.


  Wakiwa na mabango yaliyobeba ujumbe wa kumtaka Nambu Waziri awasaidie kupata maji, pia walieleza adha inayowakumba ya kusubiria maji kwa muda mrefu katika eneo wanalochetea maji jambo ambalo linawasababishia kuchelewa kufanya shughuli za kimaendeleo.


  Baada ya kuwasikiliza kero zao Mheshimiwa Aweso alilazimika kwenda kuona chanzo pekee ambacho wananchi hao wanapata huduma ya maji, ambapo alijionea kisima kinachotumia pampu ya kusukuma kwa mkono na kuongea na wananchi walijitokeza kwa wingi.


  Naibu Waziri Aweso alisema kuwa tayari mkandari anayejenga mradi kwa ajili ya kijiji hicho ameshalipwa pesa kiasi cha shilingi milioni mia moja na moja, hivyo hana sababu za kutokukamilisha mradi na kutokulipa vibarua waliochimba mitaro ya kufukia mabomba ya maji.


  Aidha, akiwa katika kijiji cha Barikiwa swala la kutokulipwa kwa vibarua waliojenga mradi pia liliibuka jambo ambalo lilimlazimu Naibu Waziri kumsimamisha Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Liwale kujibu hoja za wananchi.


  Mheshimiwa Aweso alimtaka Mkuu wa Wilaya ya Liwale awasimamie wananchi hao walipwe kabla ya mwisho wa wiki ijayo. Naibu Waziri bado yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi kwa kukagua miradi ya maji.  Naibu Waziri wa maji Juma Aweso akipampua maji katika kijiji cha Ndunyungu Liwale
  Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso akiwahutubia wananchi wa Barikiwa wilayani Liwale

  0 0

  Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza kwenye Mkutano wa wamiliki wa viwanda vya kubangua korosho katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo tarehe 8 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
  Kushoto ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akijadili jambo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Joseph Kakunda (Mb) wakati wa Mkutano wa wamiliki wa viwanda vya kubangua korosho katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo tarehe 8 Disemba 2018.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Joseph Kakunda (Mb) akizungumza kwenye Mkutano wa wamiliki wa viwanda vya kubangua korosho katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo tarehe 8 Disemba 2018. 
  Kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof Joseph Buchweshaija na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe wakifatilia Mkutano wa wamiliki wa viwanda vya kubangua korosho katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo tarehe 8 Disemba 2018. 
  Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo- Mtwara

  Serikali imeagiza korosho zote inazonunua kwa wakulima kupitia Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko kuanza kubanguliwa nchini.

  Agizo hilo la serikali limetolewa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 8 Disemba 2018 wakati akizungumza kwenye Mkutano wa wamiliki wa viwanda vya kubangua korosho kwenye ukumbi wa mikutano kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

  Hasunga alisema kuwa Mkakati wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Mhe Dkt John Pombe Magufuli ni kuwanufaisha wakulima nchini hivyo maamuzi ya kununua korosho ni sehemu ya maamuzi mema kwa manufaa ya wakulima wote.

  Alisema wakati serikali inaendelea kukamilisha uhakiki wa wakulima wa korosho pamoja na kuendelea na malipo ya wakulima mpaka hivi sasa tayari wakulima 77,380 wamekwishalipwa hivyo hakuna korosho itakayoruhusiwa kusafirishwa kwenda nje ya nchi bila utaratibu maalumu badala yake korosho zote zitabanguliwa nchini.

  Mhe Hasunga aliongeza kuwa Korosho zitakazoruhusiwa kwenda nje ya nchi ni zile Tani 2000 pekee zilizonunuliwa mnadani na kampuni mbili kwa utaratibu uliokuwa ukitumika awali.“Hakuna kampuni yoyote wala mfanyabiashara yoyote anayeruhusiwa kusafirisha korosho nje ya nchi baada ya tamko la serikali kutolewa” Alikaririwa Mhe Hasunga

  Aliongeza kuwa kutokana na uamuzi huo wa serikali imechukua takwimu zote za korosho zilizozalishwa mwaka jana ambazo zilikuwa bado hazijabanguliwa hivyo haitegemei kusikia wafanyabiashara wakisema wana korosho nyingi walizohifadhi badala yake kuwa wazalendo kwa kusema ukweli.

  “Tuwe na uwezo wa kubangua ama hakuna lakini korosho zote zitabanguliwa nchini, hivyo wito wangu kwa wafanyabiashara kuchangamkia fursa ya ubanguaji usiku na mchana” Alisema.Mhe Hasunga aliongeza kuwa serikali imeanza mchakato wa kuwafuatilia baadhi ya wafanyabiashara wenye uwezo wa kujenga viwanda kwa kufunga mitambo ndani ya muda mfupi.

  Kwa upande wake Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Joseph Kakunda (Mb) amesema kuwa serikali imedhamiria kuimarisha uchumi wa viwanda hivyo Serikali haitakubali kuhujumiwa inapoendelea kuboresha uwekezaji, uanzishaji na uendelezaji wa viwanda.

  Alisema kuwa Tanzania ni nchi yenye amani na upendo hivyo wafanyabiashara kote Duniani wana wajibu wa kujitokeza na kuanzisha biashara zao pasina kadhia yoyote.

  Aliongeza kuwa mawakala wanaotumiwa kuvuruga uchumi wa viwanda na serikali kwa ujumla wake watachukuliwa hatua zinazopaswa kwa mujibu wa sheria.

  0 0

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji (wa tatu kulia) akizungumza na wauzaji wa Duka la Vifaa vya Michezo lililopo Mtaa wa lindi – Kariakoo jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza ya kukagua matumizi ya Mashine za Kielektroniki za EFD.
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji (wa tatu kulia) akikagua Kitabu cha Risiti za Kawaida katika moja ya Maduka ya Vifaa vya Michezo lililopo Mtaa wa lindi – Kariakoo jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza ya kukagua matumizi ya Mashine za Kielektroniki za EFD. 
  Kaimu Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Abdul Mapembe (wa kwanza kulia) akiwasiliana na Kampuni ya Paragon ambayo ni moja ya mawakala wa Mashine za EFD. 

  Na Veronica Kazimoto

  NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji, amefanya ziara ya kushtukiza katika maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukagua matumizi ya Mashine za Kielektroniki za EFD.

  Akizungumza mara baada ya kukamilisha ziara hiyo katika maduka mbalimbali, Naibu Waziri huyo amesema kuwa, bado kuna wafanyabiashara ambao hawatoi risiti za EFD na wengine hawatumii kabisa mashine hizo.

  “Nimekuwa nikifanya uchunguzi wangu binafsi na wa kiofisi kujiridhisha kama wafanyabiashara wanatoa risiti za kieletroniki na nilichobaini ni kwamba bado kuna baadhi ya wafanyabiashara ambao hawatoi risiti na wananchi wengi hawaombi risiti za EFD,” alisema Dk. Ashatu.

  Dk. Ashatu amebainisha kuwa, alifanya uchunguzi binafsi ambapo alikwenda kama mnunuzi na alipoomba risiti za EFD aliambiwa mashine za kutolea risiti hizo ni mbovu na kupewa risiti za kawaida.Miongoni mwa wafanyabiashara waliotembelewa na Naibu Waziri huyo ni Faridi Mohamed ambaye ni muuzaji wa Vifaa vya Michezo katika Mtaa wa Lindi eneo la Kariakoo aliyemuuzia Dk. Ashatu bidhaa mbalimbali na kumpatia risiti isiyo ya kielektroni na alipoulizwa alidai kuwa mashine ni mbovu.

  Dk. Ashatu hakuridhishwa na majibu hayo na kuamua kufanya ziara kukagua maduka yaliyopo katika maeneo hayo ambapo ametoa wito kwa wafanyabiashara kutoa risiti kila wanapouza bidhaa na huduma mbalimbali na wananchi kudai risiti kila wanapofanya manunuzi.

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi huo wa vioski wa kampuni ya Sigara Tanzania (TCC). (Kushoto) ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughilikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughilikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa mradi huo.
  Mkurugenzi wa Masoko, Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) Bi. Awaichi Mawalla akifafanua jambo kwa kuhusu mradi huo uliobuniwa kuwawezesha wajasiriamali wadogo.
  Baadhi ya wafanyakazi wa TCC na wajasiriamali wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa mradi wa vioski uliobuniwa na kampuni ya Sigara Tanzania.
  Mkurugenzi wa Masoko, Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) Bi. Awaichi Mawalla akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama kuhusu matumizi ya Vioski mara baada ya uzinduzi wa hafla hiyo.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akikabidhi mkataba kwa mjasiriamali Bi. Pendo Godfrey wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa mradi wa vioski iliyofanyika Jijini Dodoma.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa pamoja na Naibu Waziri Mhe. Anthony Mavunde (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Patrobas Katambi (kushoto) wakimsikiliza Fundi Mkuu wa Vifaa Saidizi kwa Watu wenye Ulemavu Bw. Mwita Marwa.
  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughilikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu wa Viungo Dodoma, Bw. Hassan Hussein.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wajasiriamali walioweza kunufaika na mradi huo, mara baada ya uzinduzi wa hafla hiyo iliyofanyika Jijini Dodoma, Disemba 8, 2018.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amezindua mradi wa vioski tembezi wa kampuni ya Sigara Tanzania (TCC).

  Akizungumza leo Disemba 8, 2018 Waziri Mhagama amesema kuwa mradi huo utasaidia wajasiriamali wanaojihusisha na biashara ndogo ndogo kuweza kujiajiri na kupata kipato kitakacho wanufaisha kiuchumi.“Hii ni faraja kubwa kwetu kama Serikali kuona mnaunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua changamoto za ajira nchini kwa kuwawezesha wajasiriamali kuchangamkia fursa za kujiendeleza kibiashara”, alisema Mhagama.

  Aliongeza kuwa Serikali inatambua mchango wa wadau na kuwataka wawekezaji wengine waweze kubuni miradi kama hiyo yenye manufaa kwa wananchi.Aidha, Mhe. Mhagama aliipongeza kampuni ya Sigara Tanzania kwa ubunifu na kuwasihi waendelee kufanya vizuri katika nyanja nyingine kwa manufaa ya watanzania kwa ujumla.Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mhe. Patrobas Katambi amesema kuwa ni jambo la faraja mradi huo umezinduliwa Jijini Dodoma ikiwa ni fursa kubwa kwa wajasiriamali kuweza kunufaika kiuchumi.

  Naye, Mkurugenzi wa Masoko, Bi. Awaichi Mawalla amesema kuwa Vioski 400 vitagawiwa nchi nzima kwa wajasiriamali wadogo ambao wamekuwa wakifanya kazi na kampuni ya TCC na wataweza kuuza bidhaa mbalimbali.

  0 0

  NA MWAMVUA MWINYI, KIBITI 

  NAIBU waziri wa Ujenzi, Elias Kuandikwa amesema ujenzi wa gati, uliokuwa ukisubiriwa kwa kipindi kirefu na wakazi wa Nyamisati wilayani Kibiti mkoani Pwani umeanza ambapo shehena ya vifaa vya ujenzi vimeanza kuwasili tayari kwa ajili ya kazi. 

  Aidha amewatoa wasiwasi wakazi wa Mafia kuhusu gati la Kilindoni ,kwamba linatarajiwa kuboreshwa kwa kuondoa dosari ndogondogo zilizopo ili liwe la kisasa. 

  Akizungumza na wananchi wakati alipotembelea eneo litakapojengwa gati hilo, katika muendelezo wa ziara yake mkoani hapo, Kuandikwa alisema ujenzi utakuwa wa miaka miwili kwa gharama ya sh. bilioni 14 .

  Alimtaka , mkandarasi wa gati hilo kufanya kazi inayotakiwa kwa kuhakikisha, ujenzi unakamilika kwa wakati ikiwezekana kuukamilisha kabla ya miezi 24.
  Kuandikwa alisema, ujenzi umeshaanza na mkataba ulisainiwa tarehe 24,octoba mwaka huu, ombi lake ni kuona mkandarasi anamaliza kazi haraka.
  “Fedha zipo hatutaki kuona mkandarasi anasuasua, gati litasaidia kurahisisha usafiri kwani ndio kiu ya wakazi wa Nyamisati na Mafia”
  “Itakuwa gati la kisasa na sasa tunakwenda kufanya maboresho katika gati la Kilindoni wilayani Mafia ili kuwa na gati la uhakika ,kwa kuwa itazingatia ubora, teknolojia mpya kwa lengo la magati haya yaweze kudumu kwa miaka mingi “alisisitiza Kuandikwa. 

  Pamoja na hayo, alielezea ujenzi huo utakwenda pamoja na maboresho ya barabara ya Bungu -Nyamisati itakayosaidia kurahisisha usafiri .
  Akiwa barabara ya barabara ya Mkuranga -Kisiju kiwango cha lami, yenye urefu wa 1.8km alimpongeza meneja wa wakala wa barabara (TANROADS) mkoani Pwani, Yudas Msangi kwa kubana matumizi kwenye miradi na kuweza kutumia katika miradi mingine. 

  Msangi alisema kwasasa wanaendelea na kazi za kufungua na kuboresha baadhi ya barabara muhimu kuelekea katika miradi mikubwa mbalimbali.

  0 0

  0 0

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ( wa pili kushoto) akizungumza mara baada ya ibada iliyofanyika katika ya Kanisa la Wasabato la Geita kati wakati ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita

  Baadhi ya waumini ibada wa Kanisa la Wasabato la Geita kati wakifuatilia ibada kabla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita.

  Mchungaji na Mwenyekiti wa South Nyanza Conference, Sadoki Butoke akitoa mahubiri kwa waumini waliojumuika katika ibada ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu (katikati) akiwa na baadhi ya watendaji wa mkoa wa Geita pamoja na viongozi wa Kanisa la Wasabato la Geita wakisikiliza mahubiri kabla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita.

  Baadhi ya wanakwaya wakiimba wakati wa mahubiri kabla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akivishwa skafu na vijana wanafunzi wa Skauti kanisa la Wasabato la Geita Kati kabla ya Naibu Waziri huyo kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita.

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja na kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa wa Geita mara baada ya kusomewa taarifa ya hali ya uhifadhi wa misitu na wanyamapori kabala ya kushirikia harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo cha Afya. (PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA)  LUSUNGU HELELA-GEITA


  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu amesali katika Kanisa la Wasabato la Geita Kati mkoani Geita ambako ameendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo cha Afya.

  Lengo la kuendesha harambee hiyo ni kwa ajili ya kuchangisha pesa zitakazotumika katika ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kanisa la Wasabato kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo kitakachosaidia kuihudumia jamii.

  Katika harambee hiyo Naibu Waziri Mhe. Kanyasu aliambatana na wadau wake ambapo kwa pamoja waliweza kukabidhi Sh15 milioni zikiwa ni fedha taslimu kama mchango wao.Katika harambee hiyo, ahadi mbali mbali zimeweza kutolewa ikiwemo matofali, saruji pamoja na malori ya mchanga na mawe.

  Sambamba na hilo, Mhe. Kanyasu ameupongeza uongozi wa kanisa hilo kwa kuwa na mpango huo wa kuisaidia serikali katika kutoa huduma kwa jamii ambayo kimsingi ni kazi ya Serikali,”Suala la kujenga vituo vya afya ni jukumu la serikali lakini ninyi mmeamua kuisaidia serikali nawapongezeni sana na msisite kunishirikisha kwa lolote.

  Aidha, Mhe. Kanyasu amewataka waumini wa Kanisa hilo kuendelea kujitolea kukamilisha hatua za ujenzi wa kituo hicho cha AfyaKwa upande wake Mchungaji na Mwenyekiti wa South Nyanza Conference, Sadoki Butoke amesema kituo hicho cha Afya mara baada ya kukamilikwa kwake kitatumika kwa ajili ya kuwahudumia wananchi na sio kwa ajili ya kupata kitu

  Ameongeza kuwa kituo hicho kitawasaidia kitasaidia kuijenga jamii kiroho na kimwili na ili kukamilika kwake jumla ya sh 150 milioni zinahitajika.

  0 0

  Mbunge Wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde jana amezindua rasmi Taasisi ya Wasanii Dodoma na kukabidhi ofisi na studio kwa wasanii wa Dodoma.

  Uzinduzi huo umefanyika jana katika eneo la Mapinduzi Club-Bahi Road,Dodoma kwa kujumuisha wasanii wa ndani na nje ya Dodoma.Ofisi hizo na studio.Zitatumiwa na Wasanii wote kupitia umoja wa na Vilabu vya wasanii.

  Akizungumza katika hafla hiyo,Mbunge Mavunde amewataka wasanii wa Dodoma kuwa na UPENDO,MSHIKAMANO na UMOJA ili kufikia mafanikio na kuahidi kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanafika mafanikio ya juu katika sanaa.

  Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh Patrobas Katambi amempongeza Mbunge Mavunde kwa namna anavyowatumikia wana DODOMA na kuahidi kushirikiana nae kuwasaidia Vijana wakiwemo wasanii ili wapige hatua zaidi katika mafanikio ya kwenye sanaa.
  Mbunge Wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Wasanii Dodoma na kukabidhi ofisi na studio kwa wasanii wa Dodoma,hafla hiyo ilifanyika katika katika eneo la Mapinduzi Club-Bahi Road.
  Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini,Mh Anthony Mavunde pamoja na MKuuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Patrobas Katambi wakiwa samamba na baadhi ya wasanii waliokuwa wakitumbuiza jukwaani wakati wa uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Wasanii Dodoma na kukabidhi ofisi na studio kwa wasanii wa Dodoma,hafla hiyo ilifanyika katika katika eneo la Mapinduzi Club-Bahi Road
  Mbunge Wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde akishiriki kupiga ngoma kwenye moja ya kikundi cha ngoma za asili kwenye hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Wasanii Dodoma na kukabidhi ofisi na studio kwa wasanii wa Dodoma,hafla hiyo ilifanyika katika katika eneo la Mapinduzi Club-Bahi Road
  Mbunge Wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde akishiriki kucheza muziki jukwaani sambamba na baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya katika hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Wasanii Dodoma na kukabidhi ofisi na studio kwa wasanii wa Dodoma,hafla hiyo ilifanyika katika katika eneo la Mapinduzi Club-Bahi Road

  0 0

  Equinor Tanzania inaona fahari kusimamia sherehe za mahafali ya wanafunzi kumi na tatu miongoni mwa wanafunzi wake wengi inaowafadhili ambao wamekuwa wakichukua masomo ya shahada- ya pili (Uzamili) katika Geoscience and Engineering.

  Wanafunzi wanaohitimu wamekuwa wakifadhiliwa chini ya programu ya ufadhili wa Equinor Tanzania unaojulikana kama Angola Tanzania Higher Education (ANTHEI). Programu hii ya ufadhili ya ANTHEI kutoka kwa Equinor ni programu ambayo inatoa ufadhili kamili kwa hadi kufikia wanafunzi kumi kila mwaka kusomea shahada ya pili katika masomo ya (Utafiti wa Petroli) Petroleum Geoscience na Uhandisi wa Petroli (Petroleum Engineering) katika chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha Norway (Norwegian University of Science and Technology) (NTNU) kinachofanya kazi kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Da es salaam (UDSM).
   
   Programu hii imeandaliwa kwa namna kwamba mwanafunzi atatumia mwaka mmoja nchini Norway na kukamilisha mwaka wa mwisho wa masomo ya shahada ya pili katika chuo cha UDSM. Kwa mujibu wa hati ya makubaliano iliyosainiwa na Equinor, Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na NTNU mpango huu wa udhamini chini ya Equinor ulianza mwaka 2012 na utaendelea mpaka 2019. Jumla ya wahandisi wa Petroli wapatao 42 (Wahandisi wa Uzalishaji, Uhifadhi na wahandisi wa Uchimbaji) wahandisi 16 wa Utafiti wa Petrioli (Geology, Petrophysicis na Geophysics) na wahandisi 6 wa usimamizi wa miradi wameshasajiliwa mpaka sasa.

  Akiongea katika sherehe za mahafali Maneja Mkaazi wa Equinor nchini Dr. Mette Halvorsen Ottoy, amesema, “Equinor inaona fahari kufanya kazi kwa kushirikiana na vyuo mbalimbali katika kuweza kufikia lengo la kujenga uwezo ambalo ni kusudio katika kuendeleza sekta ya gesi na mafuta nchini Tanzania. Ni lengo letu kuona Watanzania wanapata mafunzo na wanavigezo vya kushiriki katika kuchangia katika ukuaji wa sekta hii moja kwa moja au vinginevyo”.

  Equinor inatilia mkazo sana katika uendelevu katika shughuli zake zote za uendeshaji duniani kote. Mwelekeo wa Equinor katika uendelevu una maana kuwa, tunachangia katika maendeleo endelevu kupitia shughuli zetu za msingi katika maeneo tunakofanya kazi, aliingeza Dr. Mette.

  Kupitia programu za kujenga uwezo pia Equinor imejenga ushirikiano na Vyuo mbalimbali kufanya utafiti na kufundisha uwezo ndani ya sekta ya Mafuta na Gesi kama vile programu za shahada ya pili (uzamili) katika fedha na utunzaji wa hesabu katika mafuta na gesi ( Master program in Finance and Accounting in Oil and Gas) (MFA-OG) ambayo imeanzishwa kwa ushirikiano kati ya Chuo cha Biashara cha Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (University of Dar Es Salaam Business School (UDBS) na Chuo kikuu cha Stavanger (University of Stavanger) mwaka huu wanafunzi 25 wamehitimu wakiwa na shahada za uzamili katika Fedha na Utunzaji wa Hesabu katika mafuta na gesi ambapo 10 kati yao walikuwa wamepata ufadhili kamili kutoka Equinor. 
   
  Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) pia kimesaidiwa kwa kupatiwa msaada wa kiufundi kutoka Chuo kikuu cha Barcelona kuandaa program ya shahada ya uzamili ya sayansi katika petroleum Geoscience kwa msaada wa Analog Modeling Labaratory iliyotolewa na Equinor.
  Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen akizungumza jana na waandishi wa habari na wanafunzi waliohitimu shahada ya pili (Uzamili) masomo ya Petroleum Geoscience and Engineering waliodhaminiwa masomo na Kampuni ya Equinor Tanzania kupitia mpango wa ANTHEI. Jumla ya wanafunzi kumi na tatu walihitimu ambao wataweza kufanya utafiti na kufundisha uwezo ndani ya sekta ya Mafuta na Gesi, na utunzaji wa hesabu na fedha katika sekta hiyo. 
  Mhitimu, Bertha Ngereja akitoa shukurani zake kwa niaba ya wenzake kwa wafadhili Equinor Tanzania, ANTHEI, UDSM na NTNU kwa kuwawezesha kupata shahada ya pili ya masomo mbalimbali yanayohusu Mafuta na Gesi. Sherehe za mahafali zilifanyika jana kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam.
  Meneja Mkazi wa Equinor Tanzania, Dr. Mette H. Ottoy akizungumza jana na waandishi wa habari na wanafunzi waliohitimu shahada ya pili (Uzamili) masomo ya Petroleum Geoscience and Engineering waliodhaminiwa masomo na Kampuni ya Equinor Tanzania kupitia mpango wa ANTHEI. Jumla ya wanafunzi kumi na tatu walihitimu ambao wataweza kufanya utafiti na kufundisha uwezo ndani ya sekta ya Mafuta na Gesi, na utunzaji wa hesabu na fedha katika sekta hiyo.
  Mhitimu, Masolwa Kasongi akipokea cheti cha kuhitimu shahada ya pili ya Geoscience and Engineering jana kwenye sherehe ya mahafali zilizofanyika Hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam.

  0 0

  Na.Khadija seif,globu ya jamii.

  BODI ya Uhasibu na Ukaguzi wa hesabu (NBAA) watoa Tuzo kwa Taasisi,Makampuni pamoja na mashirika yaliyofanya vizuri kwa mwaka 2018 Bunju jijini Dar es salaam.

  Akipokea Tuzo hiyo Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya ustawi wa jamii ATHUMAN SENZOTA amesema ni kwa Mara ya tatu wananyakua Tuzo hiyo ambapo vilikua vyuo viwili Kwenye kinyang'anyiro cha Vyuo vikuu na Taasisi za elimu ya juu na Taasisi ya ustawi kuwa washindi wa pili huku nafasi ya kwanza kushika chuo cha Mzumbe.

  Aidha,Senzota ameeleza kuwa Tuzo hiyo waliyoipata inaonyesha jinsi gani Taasisi yao ya ustawi wa jamii ni waadilifu na wachapakazi wa hali ya juu katika kutunza na kutumia pesa za Umma Kikamilifu kutokana na kuwasilisha vizuri mahesabu ya mwaka wa fedha 2018.

  Hata hivyo amefafanua kuwa Waliweza kufikia viwango ambavo viliwawezesha kushinda Tuzo ambapo ili uweze kushinda Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi ilizingatia viwango vya uwasilishaji kufikia 75% ya Mapato kwa mwaka wa fedha 2018 .

  Na Tuzo hiyo imekua chachu kwa Taasisi ya ustawi wa jamii inayofanya tuendelee kujituma zaidi katika ukusanyaji na utunzaji wa Mapato ili kusaidia jamii na maslahi kwa nchi kwa ujumla.

  Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Taasisi ya ustawi wa jamii Dr.Zena Mabeyo amesema TAASISI ya ustawi wa jamii imewatunuku vyeti wahitimu 1387 katika mahafali ya (42) ya chuo hicho katika ngazi ya astashahada ,stashahada na shahada ya Ustawi wa jamii katika gani ya mahusiano kazini, menejimenti ya rasilimali watu na Mahusiano kazini hii inaonyesha dhahiri kuwa Taaluma inakua kwa kasi na huku tukiendelea kuzalisha wataalam hasa Afisa ustawi kwani bado ni hitajika katika kila sekta hapa nchini.

  "Na Tuzo hiyo imekua chachu kwa Taasisi ya ustawi wa jamii inayofanya tuendelee kujituma zaidi katika ukusanyaji na utunzaji wa Mapato ili kusaidia jamii na maslahi kwa nchi kwa ujumla "alisema Mabeyo.

  Vilevile ametoa rai kwa Taasisi,Mashirika na Makampuni yaliyofanya Tuzo hizo waendelee kufanya kazi kwa bidii,uwajibikaji madhubuti kwa lengo la kuongeza pato la Taifa na ili kufikia uchumi wa kati.
   Kaimu Mkuu wa Taasisi ya ustawi wa jamii  Dr. Zena Mabeyo  akipokea Tuzo ya uwasilishaji wa Mapato ya fedha katika nafasi ya Taasisi ya elimu ya juu na Vyuo vikuu  zilizoandaliwa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa hesabu (NBAA) kwa mwaka 2018 jijini Dar es salaam
  Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya ustawi wa jamii CPA Athuman Senzota akizungumza na waandishi wa habari baada ya kushinda Tuzo ya uwasilishaji wa Mapato ya fedha kwa mwaka 2018

  0 0
  Dr. Hassan Abbas mkurugenzi wa idara ya habari maelezo Tanzania picha kutoka Maktaba


  Na. Vero Ignarus, Arusha

  Msenaji wa Serikali Dkt Abbas amesema serikaki inaendelea na ukarabati na ujenzi wa Zahanati na Vituo vya afya kwa nchi nzima kwani Mpango wa serikali ni kuhakikisha kila Wilaya ina hospitali

  Amesema upatikanaji wa dawa umeongezeka kwa rikali kuongeza bajeti ya madawa kutoka bill.31 hadi bil. 280,ambapo Serikali inanunua madawa moja kwa moja kutoka viwandani na sio kwa madalali tena. Tiba za kibingwa zimeimarishwa sana katika nchi yetu hasa magonjwa ya Moyo,kupandikiza figo na matatizo yakutosikia hii imepelekea kupungua kwa idadi ya wagonjwa wakutibiwa nje ya nchi.

  Kwa upande wa sejta ya Elimu Dkt Abbas anesema Serikali inatoa fedha kiasi cha bil.29 kila mwezi kuwezesha elimu bure katika nchi yetu.Dkt.Abbas.Amesisitiza kuwa Migomo ya elimu ya juu imeshaisha katika awamu hii ya tano kwani fedha zinapelekwa kwenye vyuo kwa wakati ambapo kwa mwaka huu kiasi cha bil 137 kimeshapelekwa kwenye vyuo mbalimbali nchini.

  Amesema kuwa kwenye sekta ya Kilimo Serikali imeanzisha mamlaka ya udhibiti wa masoko kwa bidhaa za Tanzania, hii itawasaidia wakulima, wafanyabiashara kupata masoko yenye uhakika.June mwaka huu Serikali lizindua mpango mpya wa kilimo cha kisasa cha umwagiliaji ili kumuwezesha mkulima kutotegemea mvua

  '' Mabalozi wetu katika nchi mbalimbali wanakazi kubwa yakuhakikisha wanaitafutia nchi masoko ya bidhaa zetu za ndani".alisema.Katika Sekta ya Utalii amesema kuwa Serikali inatarajia kupata watalii wengi kutoka China- Hii ni juhudi ya serikali katika kukuza utalii na kuongeza pato la serikali. '' Katika miaka 3 ya serikali ya awamu ya Tano watalii wameongezeka zaidi"alisema Dkt Abbas

  Amewataka Wananchi wasiogope kupisha miradi ya maendeleo kwani kwa faida yao na nchi pia'' Viongozi waendelee kutatua migogoro ya ardhi katika maeneo yao".Dkt. Abbas.Amesema viwanda vingi vimeanzishwa vikiwemo vya matrekta,juisi na tiles, hivyo bidhaa hizi zinapatika hapa hapa nchini sio zakuagiza nje tena.

  Amesema Sekta ya Viwanda imechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza ajira kwa wananchi wa Tanzania.'' Watumishi wanatakiwa kutekeleza majukumu yao kwa nafasi zao''alisema.Serikali ya awamu ya Tano imerudisha nidhamu na weledi kwa watumishi kwa kiasi kikubwa ambapo awamu ya Tano inaheshimu Uhuru na Demokrasia. Amesema kuwa Wananchi watumia Uhuru, demokrasia, utaratibu wa sheria za nchi walionao ila kwa kuzingatia mipaka yake

  0 0

  Bodi ya Maji Bonde la Wami/ Ruvu imefika na kufyeka mazao mbalimbali yaliyolimwa pembezoni mwa Mto Ruvu na ndani ya Mita 60 kutoka kwenye mto huo katika eneo la Ruvu Darajaji mkoani Pwani.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu, Simon Ngonyani amesema kuwa zoezi hilo ni muendelezo wa operation ya kuwaondoa watu wanaofanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo na kujenga makazi yao ndani ya Mita 60 kutoka Mto huo ili kulinda chanzo hicho cha maji. 

  "Sasahivi maji yamepungua katika Mto huu nilikuwa naongea na ndugu yangu CEO wa DAWASA aliniambia kwamba mitambo yake sasa inaungua kwasababu kina cha maji kimepungua sana na maji yanapungua kwasababu watu wanalima hivyo michanga inaingia kwenye mto kina kinapingua" -Ngonyani.

  Aidha amesema kuwa kutokana na wakulima hao wanaolima kando ya Mto kwa kutumia mbolea za chumvi chumvi kunapelekea usalama wa maji hayo kupotea kwa watumiaji hivyo watu wafuate sheria ili kulinda maji ya Mto huo.

  "Tumeamua kusimamia sheria hatutawabakisha, leo tunafyeka mazao yote yaliyopo ndani ya Mita 60 lakini kinachofuatia nyumba ambazo zipo ndani ya Mita 60 zenyewe pia tutazifanyia kazi"- Ngonyani.

  Afisa  Maji  Bodi ya Maji Bonde la wami/Ruvu Simon Ngonyani (wa kwanza kulia) akiongoza zowezi la kufyeka mazoo mbalimbali yaliyolimwa ndani ya mita 60 pembezoni mwa mto Ruvu leo mkoa wa Pwani..(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
  Muonekano wa mazoo yaliyolimwa ndani ya mita 60 pembezoni mwa mto Ruvu mkoa wa Pwani.
  Ufyekaji wa mazao yaliyolimwa ndani ya mita 60 pembezoni mwa mto Ruvu mkoa wa pwani ukiendelea.
  Muonekano wa mto Ruvu uliopo mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)

  0 0

  MASHABIKI wa Hamisa Mobetto  wa kundi la mtandao wa Kijamii la WhatsApp wanatarajiwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali na kujumuika pamoja na Watoto Yatima wa kituo cha Gosipol Revival Ophanage Centre cha Wilayani Kisarawe, Mkoani Pwani.

  Kwa mujibu wa Mratibu wa michango wa tukio hilo, Christina Mlekwa amesema shughuli za michango zinaendelea na zinatarajiwa kufikia tamati saa sita usiku wa leo Jumapili huku tukio la kuwasilisha ni siku ya Jumatatu Disemba 10.

  “Zoezi ili la kukusanya michango limeendeshwa kwa muda wa wiki mbili. Kwa mudauliobaki unaweza kutoa ‘support’ kwa kuchangia kidogo ulicho nacho kwenda namba za simu  +255742052959 jina Christina Mlekwa.” Alisema Christina.

  Kwa upande wake, msimamizi wa kundi hilo Bi. Helleni Eliasi ametoa wito kwa mashabiki wengine  wenye vitu kama nguo, fedha ama mchango wa aina yoyote wanaweza kuwasiliana na kwa njia ya simu hiyo ili kupata maelezo ya namna ya kupokelewa.

  “Mpaka sasa tuna watu zaidi ya 30, wameweza kuchangia fedha kiasi kidogo. Lakini pia  watakaokuwa tayari kuungana na ‘team Hamisa Mobotto’  wapige simu ya mratibu kwa maelezo zaidi na mavazi rasmi siku hiyo ni tisheti nyeupe ama nyeusi.” Amesema Hellen.

  Kundi hilo la ‘Hamisa Mobetto Fans’ ni kundi la mashabiki mbalimbali wanaounga mkono harakati na juhudi za Mwanamitindo, Msanii na  Mjasiriamali Mwanadada Hamisa Mobetto.

  Miongoni mwa mambo hayo ambayo kundi hilo linafanya ni pamoja na kusapoti kazi za Hamisa Mobetto pamoja na shughuli za kijamii ikiwemo kusaidia wasiojiweza na walio katka mazingira magumu.

  Hamisa Mobetto ametokea  kujizoelea umaarufu mkubwa nchini kwa mambo mbalimbali ikiwemo ya Mitindo, Ujasiriamli na Sanaa  rasmi mwaka 2010 baada ya kuibuka mshindi wa Miss XXL After School Bash.

  Pia  ameshiriki Miss Tanzania na baadae Miss New World Tanzania na kua first Runner Up 2012.

  Lakini safari yake ilikuwa zaidi na kuweza kushiriki mashindano kadhaa wa kadya ya ulimbwende  na baadae filamu kama Bongo Movie na vieo  Queen  mpaka kuwa Balozi wa makampuni binafsi na ya Serikali.

  0 0

  Bango lenye Kauli Mbiu,' HAKUNA NCHI ITAKAYOBAKI NYUMA' ikiwa ni ujumbe wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
  Wafanyakazi na wananchi walioungana katika kilele cha maadhimisho ya  Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Nderemo na vificho vilitawala katika kilele cha maadhimisho ya  Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Mbuttolwe Kabeta (wa piku kulia) akipokea maandamano katika Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Mbuttolwe Kabeta (wa kwanza kushoto) akipandisha bendera ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani katika Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
  Wakiimba wimbo wa Taifa.
  Wafanyakazi na wananchi wakimshangilia Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Mbuttolwe Kabeta katika Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Mbuttolwe Kabeta alisema kuwa Tanzania kama mwanachama hai wa ICAO, imeendelea kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu hiyo ili kukuza sekta na kuifanya itoe mchango wake kikamilifu. 

  Alisema jitihada za TCAA za kuboresha miundombinu pamoja na raslimali watu zimeanza kuzaa matunda. Matokeo mazuri ya ukaguzi uliofanywa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) mwaka 2017 kuhusu uwezo wa Tanzania katika kusimamia na kudhibiti usalama wa sekta ni udhibitisho tosha ambapo matokeo ya ukaguzi yaliyotolewa Septemba 2017 yalionyesha uwezo wa Tanzania wa kudhibiti sekta umeongezeka toka 37.8 (2013) hadi asilimia 64.35 (2017). Alama hizo zinaifanya Tanzania kuwa juu ya kiwango cha wastani wa asilimia 60 kilichowekwa na Shirika hilo.

  0 0

  Na Veronica Kazimoto ,Dar es Salaam 

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeibuka mshindi wa jumla katika tuzo za uandaaji wa hesabu bora mwaka 2017 zinazotolewa kila mwaka na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA). 

  Hafla ya utoaji wa tuzo hizo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika Kituo cha Mikutano cha NBAA Bunju jijini Dar es Salaam. 

  Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere, amewaasa wahasibu nchini kuwasaidia wateja wao kuandaa vitabu vya mahesabu kwa kufuata viwango vya kimataifa ili kuepuka kufanya marekebisho ya vitabu hivyo na kupotea kwa kodi. 

  Amesema taasisi nyingi zimekuwa hazijui kuandaa vitabu vya mahesabu na wakati mwingine hulipua katika kuviandaa ambapo matokeo yake vimekuwa vikikataliwa na kutakiwa kurudia mahesabu hayo hali ambayo inafanya kazi hiyo kuwa ngumu na wakati mwingine inaleta mashaka. 

  Kichere amesema siri ya ushindi wao ni ushirikiano mzuri walionao kama mamlaka ikiwa ni pamoja na kutoa muda wa ziada wa kazi ili kuweza kukidhi viwango vya kimataifa na kama taasisi ya kukusanya mapato lazima ifanye hivyo. 

  “Tumefurahi kupata tuzo hii inayoonyesha kuwa, tunatengeneza mahesabu yetu kwa kufuata taratibu na viwango vya kitaifa katika uandaji wa vitabu vinavyohusiana na fedha. Tumekuwa na ushirikiano mzuri na wahasibu wetu ambao mara zote wamejitolea muda wao ili kukidhi vigezo hivi vya kimataifa,” amesema Kichere. 

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji ambaye alikuwa mgeni rasmi katika utoaji wa tuzo hizo, aliwaambia wahasibu kuwa, imani yake ni kwamba, siku tatu walizokutana wamezitumia vizuri kwa kujadili masuala mbalimbali yanayowahusu kwa undani. 

  Amesema kuwa amefurahishwa na namba ya wahudhuriaji wa mkutano huo wa wahasibu ambayo imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka jambo ambalo limewawezesha kujadili kwa undani changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika utendaji wa kazi zao. 

  Kabla ya ushindi huo wa jumla, TRA ilipata ushindi wa kwanza katika kipengele ya kushindanisha Taasisi za Serikali ambapo Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) lilikuwa la pili na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) ilikuwa ya tatu.

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji akimkabidhi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere tuzo ya uandaaji wa vitabu vya hesabu kwa kuzingatia taratibu na kanuni za mahesabu katika Taasisi za Serikali zinazotumia Mfumo wa Uhasibu wa IPSAS ambapo TRA imeibuka mshindi wa jumla. Hafla ya utoaji wa tuzo hizo ilifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) jijini Dar es Salaam mwishoni wa wiki. 
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (wa tatu kulia) akiwa ameshikilia tuzo ya uandaaji wa vitabu vya hesabu kwa kuzingatia taratibu na kanuni za mahesabu katika Taasisi za Serikali zinazotumia Mfumo wa Uhasibu wa IPSAS ambapo TRA imeibuka mshindi wa jumla. Hafla ya utoaji wa tuzo hizo ilifanyika katika Kituo cha Mikutano cha cha Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) jijini Dar es Salaam mwishoni wa wiki.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere (wa tatu kulia) akiangalia kwa makini tuzo ya uandaaji wa vitabu vya hesabu kwa kuzingatia taratibu na kanuni za mahesabu katika Taasisi za Serikali zinazotumia Mfumo wa Uhasibu wa IPSAS ambapo TRA imeibuka mshindi wa jumla. Hafla ya utoaji wa tuzo hizo ilifanyika katika Kituo cha Mikutano cha cha Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) jijini Dar es Salaam mwishoni wa wiki. 


  0 0


  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatangaza nafasi za kuandikishwa Jeshini Madaktari wa Binadamu na fani nyingine za Tiba.
        Nafasi hizo zinatolewa ili kuongeza idadi ya wataalamu wa tiba watakaotoa huduma za afya katika Hospitali zetu, vituo vya afya na Zahanati kulingana na mahitaji  ya sasa na siku zijazo.
        Watakao andikishwa Jeshini ni wale wenye taaluma zifatazo:-
  a.           Daktari Bingwa wa Meno    -  Dental Surgeon
  b.          Daktari Bingwa     -       Specialist Neurasurgeon
  c.           Mkemia   (Chemisist)
  d.          Mteknolojia Msaidizi (Maabara) - Assistant Laboratory Technician.
  e.           Tabibu msaidizi     -  Assistant Clinical officer.
  f.            Katibu wa Hospitali  - 
  g.          Msaidizi wa kumbukumbu.  – Medical Records (Certificate)
  h.          Daktari           - Medical Doctors.
  j.      Afisa Muuguzi  -  Registered Nursing Officer. 
  k.     Fundi sanifu vifaa tiba  -  Bio Medical Engineer.
  l.      Tabibu   - Clinical Assistant  (Certificate).
  m.    Mteknolojia msaidizi -  Laboratory Assistant (Certificate)
  n.     Mfamasia -  Pharmacist  (Degree)
  o.     Mtoa tiba kwa vitendo  - Physiotherapist  (Diploma)
  p.     Afisa Muuguzi msaidizi  - Assistant Nursing officer

  Sifa za kuandikishwa Jeshini ni zifuatazo:-
  a.    Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
  b.    Awe na umri kati ya miaka 18 hadi 28 isipokuwa specialist
  c.     Awe na afya njema ya mwili na akili timamu.
  d.    Awe mwenye tabia njema na nidhamu nzuri
  e.    Awe hajawahi kupatikana na hatia ya makosa ya jinai Mahakamani na kufungwa jela.
  f.     Awe na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate), vyeti vya shule (Academic & School Leaving Certificates) na vyeti vya Chuo (Transcript & Academic Certificates).
  g.    Kama ni Daktari awe amemaliza mafunzo kwa vitendo (Internship) na kutunukiwa vyeti pamoja na kusajiliwa na Bodi.
  h.    Awe hajatumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo.

         Wenye sifa tajwa na kuhitaji kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania waripoti katika Kambi yaJenerali Abdallah Twalipo, Mgulani    Dar es Salaam tarehe              17, Desemba, 2018 kuanzia saa 1.00 Asubuhi kwa usaili.
  Waombaji wafike na vyeti halisi (Original Certificates) vya kuzaliwa na masomo pia wajitegemee kwa usafiri, chakula na malazi.
  Aidha, watakaochaguliwa na kuandikishwa Jeshini watapatiwa mafunzo mbalimbali ya Jeshi na yatakayo waendeleza katika taaluma zao. Wakiwa Jeshini majukumu watakayopatiwa ni yale yatakayowapa changamoto na fursa nzuri za kutumia taaluma zao. 
  JIUNGE NA JWTZ UJIFUNZE MENGI, UONE MENGI NA UFAIDI MENGI

  0 0
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimuuliza maswali Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Namalebe, Kata ya Chitengule, Jimbo la Mwibara, wilayani Bunda, Wilbard Malea, katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijji hicho, leo. Mtendaji huyo alikiri kutafuna fedha za wanakijiji hao na aliahidi kuzirudisha. Hata hivyo, Lugola alimsweka ndani Mtendaji huyo kutokana na kosa hilo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  Na Ripota Wetu, MARA.

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemsweka ndani Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Namalebe, Kata ya Chitengule, Jimbo la Mwibara, wilayani Bunda, kwa kosa la kutafuna fedha za wanakijiji wilayani humo.

  Waziri Lugola ambaye ni Mbunge wa jimbo hilo alitoa maamuzi hayo katika mkutano wa hadhara na wananchi hao uliofanyika kijijini hapo leo, baada ya kuwataka wananchi wenye malalamiko, maswali pamoja na ushauri watoke mbele ili aweze kuwasikiliza wananchi hao.

  Baada ya agizo hilo, zaidi ya wananchi kumi walijitokeza na kuuliza maswali pamoja na kutoa kero zao, ndipo watu saba kati ya waliotoka mbele wakiwa wamepanga foleni walitoa tuhuma mbalimbali kuhusiana na Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Wilbard Malea kutafuna fedha zikiwemo fedha za maendeleo ya kijiji pamoja na za faini kutokana na mashtaka yanayowasilishwa na wananchi kwake kwa ajili ya usuluhishi pamoja na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

  Mkazi wa Kijiji hicho, Simon Joseph alimtuhumu katika mkutano huo, Mtendaji huyo alimfuata katika kikundi chao cha Muungano cha kuweka na kukopeshana alisema anaomba kukopa fedha shilingi 91,000 na kijiji kitarudisha fedha hizo, lakini mpaka leo hajazilipa na hakutumwa na Serikali ya Kijiji bali alisema uongo ili ajipatie kwa njia ya udanganyifu.

  Pia Happyness Tabonwa mkazi wa kijiji hicho, alimlalamikia mtendaji huyo amechukua mbuzi wake watatu baada ya kushindwa kulipa shilingi 50,000, akaamua kuwakamata mbuzi hao na baada ya kumpeleka elfu 50 anayoidai Mtendaji huyo akashindwa kuwarudisha mbuzi hao kwa kuwa alishawauza na pesa kazitafuna.

  Wananchi hao pia walimlalamikia Waziri Lugola, kuwa Mtendaji huyo wanapopeleka mashtaka yao, watuhumiwa hupigwa faini lakini fedha ikitolewa haiendi mfuko wa maendeleo ya kijiji bali fedha hizo uzitumia mtendaji huyo.

  Pia mtendaji huyo analalamikiwa kuchukua simu ya mkononi ya Joseph Japhet ambaye alipohamia kijijini hapo aliambiwa alipe shilingi 50,000 ikiwa ni malipo kwa ajili ya maendeleo kijijini hapo, hata hivyo fedha hiyo hakuwa nazo ndipo Mtendaji huyo akamnyang’anya simu yake.

  Wakati wananchi hao wanatoa malalamiko hayo, mtendaji huyo alikuwa mbele katika mkutano huo baada ya kuitwa na Waziri Lugola ili aweze kujibu tuhuma hizo zikiwemo za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyi pamoja na kuwadhulumu wananchi mbalimbali wa kijiji hicho.

  Akijibu tuhuma hizo Mtendaji huyo, Malea alizikana tuhuma hizo na baada ya kubanwa huku wananchi hao wakielezea kwa mifano, ndipo akakiri kutafuta fedha za wananchi hao na akaahidi katika mkutano huo atawalipa wananchi wote wanaomdai.

  Baada ya kukiri ndipo Waziri Lugola akamwita Mkuu wa Kituo cha Polisi Kibara Wilayani Bunda, Mkaguzi Boniface Mwalupale, ili Polisi walipo katika mkutanon huo wamkamate Mtendaji huyo na akafunguliwe mashtaka endapo atashindwa kuwalipa wananchi mbalimbali wanao mdai kama alivyokiri.

  “Ndugu wananchi, kwanini hawa viongozi mnaowachagua wanakua sio waadilifu?, nimefanya mikutano katika vijiji mbalimbali nimekutana na changamoto kama hii, na pia katika kijiji ambacho tumetoka, Mtendaji wa Kijiji pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji hicho wametafuta fedha za mchanga zilizotolewa na kampuni inayojenga barabara ya Bunda hadi Kisorya, tunaenda wapi ndugu zangu, viongozi wadokozi kama hawa lazima tuwakamate, najua polisi mnahamu ya kukamata mhalifu, mkamateni ili akaeleze hizo fedha alizipeleka wapi na kwanini alizitafuna fedha za wanakijiji,” alisema Lugola.

  Akizungumza saa mbili baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo, Mkuu wa Kituo cha Polisi Kibara (OCS), Mwalupale alisema Mtendaji huyo anadaiwa zaidi ya shilingi 300,000 lakini mpaka sasa ameshatoa 206,000, hata hivyo hawajamuachia bado yupo polisi mpaka atakapomaliza kulipa madeni yote.

  “Bado hatujamtoa mtuhumiwa huyo ambaye amejipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utapeli, mpaka sasa tayari ametoa 206,000, bado mbuzi watatu hajalipa,” alisema OCS Mwalupale.

  Lugola anaendelea na ziara yake kwa kutembelea vijiji vyote jimboni kwake Mwibara akisikiliza kero za wananchi pamoja na kuhamasisha kilimo cha mazao ya pamba, mahindi, mpunga, viazi na mengineyo ambayo wakazi wa jimbo lake wanalima mazao hayo kwa wingi.

  0 0

  KAMATI ya Marekebisho ya Katiba ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA), imekamilisha Rasimu ya Kwanza ya Mapendekezo ya Katiba ya chama hicho na itaanza kutolewa kwa wadau mbalimbali leo Jumapili Desemba 9, 2018 kwa ajili ya kujadiliwa.

  Hatua ya kuandaa rasimu hiyo ya kwanza imefanywa na Kamati ya Marekebisho ya Katiba ya TASWA kwa kuangalia Katiba za vyama mbalimbali duniani vinavyohusiana na waandishi wa habari za michezo na pia kupitia muongozo kutoka Chama cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari za Michezo (AIPS), ambacho TASWA ni mwanachama.

  Pia Kamati imechambua Katiba ya sasa ya TASWA na kupokea maoni kutoka kwa waandishi wa habari za michezo kuhusu maeneo yenye upungufu kwa nia ya kuiboresha.Maeneo mbalimbali yamefanyiwa kazi katika rasimu hiyo baadhi yakiwa ni sifa za mwanachama, wajibu wa mwanachama, muundo wa uongozi, sifa za viongozi na pia ukomo wa uongozi.

  Pia kuna mapendekezo katika rasimu hiyo ya kuanzishwa kamati mbalimbali kwa nia ya kuisaidia Kamati ya Utendaji.Kutokana na hali hiyo, Kamati imepanga hatua ya kwanza baada ya kuitoa rasimu hiyo leo, itapokea maoni binafsi ya wadau kwa njia ya email (katibataswatz@yahoo.com), kisha itakutana na wahariri wa habari za michezo, waandishi waandamizi na waandishi chipukizi kwa kadri mtakavyotaarifiwa.

  Baada ya kupokea maoni kutoka makundi hayo, Kamati itafanya mikutano miwili, ambapo wa kwanza utakuwa wa wadau wote kuijadili kwa pamoja na kisha kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji ya TASWA utafanyika Mkutano Mkuu wa kuipitisha na kuiwasilisha kwa Msajili tayari kwa Uchaguzi Mkuu haraka iwezekanavyo.Ni matumaini ya Kamati ya Katiba kila mdau ataisoma vyema rasimu hiyo na kutoa mchango wake na mwisho wa kufanya hivyo ni Desemba 12 mwaka huu. Mapendekezo ya Rasimu hiyo nimeambatanisha katika email zenu.

  Kamati ya Katiba ya TASWA imeundwa kutokana na agizo la Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe aliyeitaka BMT isitishe uchaguzi wa TASWA uliokuwa umepangwa kufanyika Novemba 25 mwaka huu na badala yake BMT ikutane na viongozi wa TASWA pamoja na baadhi ya wanahabari wa michezo kuona namna ya kuifanyia marekebisho Katiba ya TASWA iendane na wakati.

  Kamati ya Katiba inayoongozwa na Mwenyeketi wa zamani wa TASWA, Boniface Wambura ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), viongozi wengine ni Katibu wa Kamati Amir Mhando ambaye pia ni Katibu Mkuu wa TASWA na mwanahabari, Gift Macha ambaye ni Katibu Msaidizi wa Kamati.

  Wajumbe ni Katibu Mkuu wa zamani wa TASWA, Abdul Mohammed, Mhazini wa zamani wa TASWA, Nasongelya Kilyinga na wanahabari Thabit Zacharia na Devotha Kihwelu.

  Nawasilisha,
  Amir Mhando
  Katibu wa Kamati ya Katiba/ Katibu Mkuu TASWA
  9/12/2018

older | 1 | .... | 1747 | 1748 | (Page 1749) | 1750 | 1751 | .... | 1897 | newer