Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

Idris Sultan avunja rekodi nyingine tena

$
0
0


Mchekeshaji Idris sultan akiburudisha maelfu ya wakazi wa Dar es salaam na viunga vyake waliofika katika tamasha la Komedi maarufu kama SEX TOUR hivi karibuni katika ukumbi wa Club next door Arena Jijini Dar es salaam.

Mchekeshaji Deo Akiwaburdisha wakazi wa Jiji la Dar es salaam waliojitokeza kwa singe katika onesho la SEX tour Lilofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Club Next door Arena Jijini Dar es salaam.

Coy Mzungu akita burudani katika jukwaa la Sex Tour katika onesho hilo liliofanyika hivi karibuni hapa jijini Dar es salaam na kuvunja rekodi kwa maelfu ya watazamaji zaidi ya elfu 7 patika ukumbi mmoja.
Msanii wa Muziki wa Kijazi kipya Billnass akitumbuiza umati wa wakazi wa Dar es salaam waliojitokeza katika Tamasha la komedi maarufu kama SEx Tour lilofanyika hivi karibuni hapa Jijini Dar es salaam.

Jaymondy akiwavunja mbavu maelfu ya watazamaji waliojitokeza katika ukumbi wa Club next door katika Tamasha la Komedi maarufu kama Sex Tour liliofanyika hivi karibuni hapa jijni Dar es salaam.


Idris sultan akiendelea kuvunja mbavu za maelfu za wakazi wa Jiji la Dar es salaam katika jukwaa la Club next door Arena katika Tamasha la komedi maarufu kama Sex Tour liliofanyika hivi karibuni Jijini Dar es salaam.

Maelfu ya wakazi wa jiji wakifurahia burudani za wachekeshaji mbali waliotumbuiza katika onesho la Sex Tour lilofanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam.
Maelfu ya wakazi wa jiji wakifurahia burudani za wachekeshaji mbali waliotumbuiza katika onesho la Sex Tour lilofanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam.
Idris akiwa anapima afya yake katika madhimisho ya siku ya ukimwi duniani huku akiongozana na wachekeshaji wenzake kuhamasisha vijana kutokuwa na woga wa kupima na kujua hali zao.



Mchekeshaji Idris Sultan amealikwa kuhudhuria tamasha kubwa la Komedi litakalofanyika mwezi huu nchini Afrika kusini lililoandaliwa na Comedy Central , moja kati ya taasisi kubwa Duniani katika tasnia ya ucheshi na uchekeshaji.

Mualiko wa Idris unakuja baada ya msanii huyo wa tasnia ya uchekeshaji kufanya Tamasha la Sex Tour ambalo liliwavuta maelfu ya wapenzi wa comedy hapa nchini .Kwa mujibu wake mualiko wa huo ni sifa kubwa kwa Taifa, baada ya bongo flava kutoboa kimataifa, sasa ni zamu ya tasnia ya uchekeshaji wa Tanzania.

Akizungumzia kuhusu tamasha la Sex Tour Idris alisema lilikuwa na lengo kuu ya kuburudisha na kuelimisha watu katika ma swala mbali mbali ya kijamii kwa kutumia Sanaa ya uchekeshaji.“Tarehe 1 December Idris Sultan aliandaa tamasha la kwanza la Sex Tour katika ukumbi wa Next Door Arena. Watu zaidi ya 7,000 walihudhuria huku wengi wakilalamika kukosa ticket.

SexTour imekua tamasha kubwa zaidi la comedy kuwahi kutokea nchini Tanzania na kufananishwa na baadhi ya matamasha makubwa ya muziki” anasema.Likibeba ujumbe "Kutokupima hakubadili matokeo"tamasha hilo lilihudhuriwa na wachekeshaji mbali mbali akiwemo Jaymondy, Mkaliwenu, Dogo pepe, Coy Mzungu, Blackpass,kitenge,Nalimi ,Optalema Deo, Max, Young Unstopable ,D comic na wengine wengi huku upande ma muziki wa kizazi kipya ukiwalishwa vyema naa Whozu na Billnass

“Changamoto za maambukizi mapya kwa vijana wa umri 15-24 bado ni kubwa, hivyo Sex Tour ilikua inalenga zaidi kushauri vijana kujali afya zao, kutokuwa na hofu ya kupima afya zao lakini pia kubadili fikra potovu za kuwa nyanyapaa wenye maambukizi,”anasema Idris

Tamash la Sex Tour lilidhaminiwa na Mfuko wa dharura wa Raisi wa Marekani wa kupambana na maambukizi ya Ukimwi (PEPFAR) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani Tanzania

RAIS DKT. MAGUFULI AGAWA VITAMBULISHO 670,000 KWA WAKUU WA MIKOA KWA AJILI YA MATUMIZI YA WAJASIRIAMALI WADOGO WADOGO (MACHINGA) KATIKA MIKOA YOTE YA TANZANIA BARA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizingumza na Wakuu wa Mikoa, Mawaziri na Makatibu Wakuu wa baadhi ya Wizara, Mameneja wa Mikoa wa Mamlaka ya Mapato nchini TRA, Waakilishi wa Machinga kabla ya kutoa Vitambulisho kwa ajili ya Wafanyabiashara wadogo wadogo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Vitambulisho hivyo vitagharimu kiasi cha Shilingi 20,000/ kwa kila kimoja.
 Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakisikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyokuwa akiitoa katika ukumbi wa katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia wakati Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila alipokuwa akisaini hati ya makabidhiano ya vitambulisho vya wajasiriamali wadogo wadogo machinga kwa ajili ya mkoa wa Mbeya.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia wakati Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira alipokuwa akisaini hati ya makabidhiano ya vitambulisho vya wajasiriamali wadogo wadogo machinga kwa ajili ya mkoa huo wa Kiliamnjaro.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia wakati mkuu wa mkoa wa Njombe Cristopher Ole Sendeka alipokuwa akisaini hati ya makabidhiano ya vitambulisho vya wajasiriamali wadogo wadogo machinga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia wakati mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka alipokuwa akisaini hati ya makabidhiano ya vitambulisho vya wajasiriamali wadogo wadogo machinga .
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwandri kabla ya kusaini hati ya makabidhiano ya vitambulisho vya wajasiriamali wadogo wadogo machinga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia wakati mkuu wa mkoa wa Tabora Agrey Mwandri alipokuwa akisaini hati ya makabidhiano ya vitambulisho vya wajasiriamali.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Ardhi Wiliam Lukuvi wakati akiondoka kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia mkono wakati akiondoka kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Meneja wa Mamlaka ya Mapato TRA kwa mkoa wa Kilimanjaro Msafiri Mbibo ambaye alikataa rushwa ya Dola za kimarekani $2000. Rais Dkt. Magufuli ameagizwa kuandikiwa barua ya kupongezwa kwa Meneja huyo. PICHA NA IKULU

SERIKALI HAITOMVUMILIA KIONGOZI ATAKAYEKIUKA MAADILI-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kuenzi misingi ya utawala bora haitamvumilia kiongozi yeyote wa umma atakayekiuka misingi hiyo na kutanguliza maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma katika utendaji wake.

Amesema mgongano wa maslahi umechangia rasilimali za nchi kunufaisha watu wachache huku wananchi wengi kuendelea kuwa fukara, wakati wachache wakijitajirisha isivyo halali, hivyo Serikali itaendelea kuziba mianya, kwani ikiachiwa iendelee, itarudisha nyuma jitihada za Serikali katika kufikia Dira ya Maendeleo ya Taifa.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema mmomonyoko wa maadili umechangia sana kutozingatiwa kwa sheria, kanuni na miongozo mbalimbali katika utumishi wa umma, tatizo ambalo limesababisha mgongano wa maslahi.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Desemba 10) kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu yaliyofanyika Kitaifa jijini Dodoma, ambapo ametumia Napenda fursa hiyo kuwaasa viongozi wote kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika utendaji wao kwani hiyo ndio njia pekee itakayoepusha mgongano wa maslahi.

Waziri Mkuu amesema mgongano wa maslahi ni miongoni mwa mambo yaliyochangia kuisababishia hasara Serikali kwa muda mrefu, tatizo ambalo lazima lidhibitiwe kwani mara kadhaa baadhi ya viongozi au watumishi wa umma wamekuwa wakifanya maamuzi kwa mambo wanayojua wazi kuwa wana maslahi binafsi nayo.

”Mathalan katika Halmashauri zetu wapo madiwani au watumishi wanaoshiriki kutoa maamuzi yanayohitimishwa kwa kumpatia kazi mkandarasi au mzabuni wakati kampuni husika inamilikiwa na mwenza, rafiki, ndugu wa karibu au mtoa rushwa.”

Amesema mgongano wa maslahi ambapo amesema kuwa huwa unatokea pale mahitaji, manufaa na faida (maslahi) binafsi ya kiongozi yanapokinzana na yale ya umma katika utendaji wake wa kazi, jambo ambalo ni kinyume na misingi ya utawala bora ambayo Taifa letu linaiamini na kuifuata tangu lilipoanzishwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.”

Amesema Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli itaendelea kuunga mkono na kutekeleza Mikataba na Makubaliano ya Kimataifa ipasavyo. Mikataba hiyo ni pamoja na mkataba wa Kimataifa wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Makubaliano yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu.

”Sambamba na maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi katika ibara ya 145 (a), ambapo tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, mojawapo ya agenda yetu ilikuwa ni kuendeleza jitihada za kukuza, kulinda na kuhifadhi haki za binadamu na utawala wa sheria katika ngazi zote za uongozi.

Jambo hili tumelifanya kwa nguvu kubwa na kwa sasa tumeona kuna mabadiliko makubwa sana miongoni mwa watumishi wa umma katika kutoa huduma kwa wananchi kwa nidhamu, bila upendeleo na kuepuka vitendo vya rushwa.”

Waziri Mkuu amesema katika kipindi cha miaka mitatu yameshuhudiwa mafanikio makubwa nchini na kwamba hakuna muujiza uliofanyika kufikia hatua hiyo, bali ni usimamiaji wa nidhamu ya kazi, uadilifu na rasilimali za nchi.

Amesema kinachofanywa na Serikali ni kuchukua hatua stahiki dhidi ya vitendo vyote vinavyokiuka maadili na misingi ya utawala bora kadri inavyowezekana na sasa mafanikio ya jitihada hizo yanaonekana, ambapo baadhi ya watumishi wa umma waliishakuwa miungu watu  na  kusahau kabisa  kwamba  utumishi  wao  ni wa  kuwatumikia  Watanzania,

”Mafanikio ya hatua hizo ni kurejea kwa  nidhamu katika utumishi wa umma, kushuka kwa mfumuko wa bei za bidhaa, kuendelea kutekelezwa kwa miradi ya maendeleo na kuimarika kwa utamaduni wa kufanya kazi halali ili kupata kipato halali hivyo, kufuta maisha yaliyojaa ujanja ujanja.”

Hivyo, Waziri Mkuu amesema maadhimisho hayo ni muhimu kwa sababu yanatoa fursa ya Serikali kujitathmini kama imefanya juhudi za kutosha kuhakikisha maadili yamezingatiwa katika kila eneo na hivyo kupunguza vitendo vya rushwa, kuimarisha uwajibikaji katika kuutumikia Umma na misingi ya utawala bora kwa ujumla wake.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Spika wa Bunge Job Ndugai, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni MstaafuGeorge Mkuchika, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Paramagamba Kabudi.

Wengine ni Manaibu Mawaziri, Makatibu Wakuu Wakuu wa Taasisi zinazosimamia Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji na Mapambano dhidi ya Rushwa, Viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na Wawakilishi wa Washirika wa Maendeleo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi wakati alipowasili kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma kuzungumza na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Desemba 10, 2018. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nchil Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavinde na kulia ni  Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu, Profesa, Faustine  Kamuzora. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

LUGOLA AWAOMBA WANANCHI KUCHANGIA UJENZI VITUO VYA POLISI KUIMARISHA USALAMA NCHINI

$
0
0
Na Felix Mwagara, (MOHA) MARA.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka Watanzania wawe na utamaduni wa kuchangia ujenzi wa vituo vya polisi kama wanavyochanga katika michango mingine ya maendeleo nchini.

Lugola amesema ni mara chache sana kuona wananchi wanachangia ujenzi wa kituo cha polisi katika maeneo wanayoishi kutokana na baadhi ya Watanzania wanaamini vituo vya polisi ujengwa na serikali pekee jambo ambalo halina msingi la linakwamisha maendeleo ya nchi.

Akizungumza na mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Kibara B, Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, Lugola amesema ili usalama uzidi kuimarishwa katika maeneo mbalimbali nchini, wananchi wanapaswa kushirikiana na Serikali katika ujenzi wa vituo vya polisi.

Lugola alisema katika mikutano yake ya nchi nzima anayoendelea kuifanya, atazidi kuwahamasisha wananchi waweke utamaduni wa kuchangia kwa ajili wa ujenzi wa vituo hivyo ili ulinzi upatikane sehemu mbalimbali nchini na kupunguza au kuyaondoa kabisa matukio ya uhalifiu.

“Nimeona wananchi wakichanga ujenzi wa zahanati, shule pamoja na michango mingine ya maendeleo, lakini wanakua wazito kabisa katika kuchangia ujenzi wa kituo cha polisi katika eneolao wanaloishi,” alisema Lugola.

 Lugola aliwataka wananchi kuungana na Serikali ya Rais Dk John Pombe Magufuli ambayo inalenga kuleta maendeleo katika kuibadili nchi, hivyo ushirikiano na wananchi unahitajika ili nchi iwezwe kusonga mbele zaidi.

“Tunatarajia kujenga kituo cha Polisi cha kisasa cha ghorofa katika eneo hili la Kibara, lakini wananchi mnapaswa kutoa michango yenu ili kufanikisha hili, tuweke utamaduni wa kuchanga jamani, si hapa tu Kibara jimbo la Mwibara bali wananchi wote nchini jengeni utamaduni wa kutoa michango ujenzi wa vituo vyenu vya polisi pamoja na nyumba za makazi ya hawa walinda usalama wenu,” alisema Lugola.

Aidha, Lugola aliwataka wananchi hao waongeze kasi katika maandalizi ya kilimo kwasababu mvua tayari zimeanza kunyesha, hivyo waongeze nguvu za kulima mazao ya chakula na biashara ili kuithibiti njaa isitokee katika eneo hilo.  

Lugola anaendelea na ziara yake kwa kutembelea vijiji vyote zilizopo katika kata 14 zilizopo jimboni kwake akisikiliza kero za wananchi pamoja na kuhamasisha kilimo cha mazao ya pamba, mahindi, mpunga, viazi na mengineyo ambayo wakazi wa jimbo lake wanalima mazao hayo kwa wingi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Kibara B, Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, leo.  Lugola aliwaomba wananchi wa kijiji hicho wachangie ujenzi wa kituo vya polisi katika eneo hilo ili kuimarisha ulinzi wa raia na mali zao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimsikiliza Mkazi wa Kijiji cha Sikiro, Kata ya Iramba, Mwibara Wilayani Bunda, Mkoa wa Mara, Elia Majinge alipokua anatoa kero yake katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji hicho, jimboni humo, leo. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kibara B, Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, leo.  Lugola aliwaomba wananchi kijijini hapo wachangie ujenzi wa kituo vya polisi ili kuimarisha ulinzi zaidi nchini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MITANDAO YA KIJAMII YAELEZA INAVYOIONA BENKI KUU YA TANZANIA, YATOA USHAURI

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAANDISHI wa habari kutoka mitandao ya kijamii nchini hasa wanaondika habari za uchumi na fedha nchini wametoa mtazamo wao kuhusu namna ambavyo wanaitazama Benki Kuu ya Tanzania(BoT).

Mtazamo huo umetolewa leo Mjini Dodoma kwenye semina ya waandishi wa habari za fedha na uchumi ambayo imeandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania(BoT) kwa ajili ya kuwajengea uwezo waandishi wa vyombo vya habari nchini ambapo kabla ya kutolewa kwa mtazamo huo imefafanuliwa kwa kina nini maana ya mitandao ya kijamii na nguvu yake katika kuhabarisha umma.

Akitoa mada kwenye semina ya waandishi wa habari za fedha na uchumi leo Mjini Dodoma ambayo imeandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania(BoT),Mmiliki wa Blog ya K-VIS Blog Khalfan Said amesema mtandao wa kijamii ni aina ya tovuti au Application inayowaruhusu watumiaji kuwasiliana kwa kuchapisha jumbe kwa njia ya maandishi, picha au video kwa kutumia computer au Smart phones.

Amesema unapozungumzia mitandao ya kijamii inayofahamika sana na jamii yetu ni pamoja na Blogs, Youtube, Facebook, Instagram, Flicker, Tweeter, Whatsaap na LinkedIn na kwamba faida ya mitandao ya
kijamii inasaidia kutengeneza mahusiano mapya kati ya mtu na mtu, mtu na taasisi au taasisi na taasisi.

Khalfa Said amesema awali mitandao ya kijamii haikutiliwa maanani sana na ilichukuliwa kama majukwaa ya kupashana “umbea” tu, mfano nani kavaa nini, katembelea wapi, yuko na nani nk. Lakini kutokana na nguvu yake ya kufikia hadhira kwa haraka na kwa upana zaidi, (walaji) yaani hadhira ikaona iitumie pia katika kuhabarishana taarifa muhimu.

"Kwa mantiki hiyo mitandao ya kijamii imefungua mlango mpya kabisa wa chombo kingine cha habari chenye ushawishi na uwezo mkubwa wa kutawanya habari katika kipindi kifupi tangu tukio litokee na wakati mwingine (live). Na Serikali nayo kwa kutambua “nguvu” hiyo ya kufikia hadhira kubwa na kwa haraka imeweka sheria sasa, kwa mtandao wa kijamii unaobeba maudhui ya habari lazima usajiliwe na Mamlaka ya Udhibiti Mawasiliano Tanzania (TCRA) kama chombo rasmi cha kupashana habari,"amesema.

Baada ya utangulizi huo, Khalfan Said ndipo aliamua kuizungumzia namna ambavyo 'Social Media' inaionaje BoT katika utoaji wake wa taarifa ambapo amefafanua ifahamike taasisi fulani inaweza ikawa haina bureaucracy katika utoaji wake wa taarifa lakini ikawa na udhaifu mkubwa wa usahihi wa taarifa hizo katika kuandaa na kutawanya taarifa.



Mwakilishi wa Michuzi Blog Said Mwinshehe akiwa kama sehemu ya washiriki kwenye semina ya waandishi wa habari za fedha na uchumi ambayo imeandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania(BoT) kwa ajili ya kuwajengea uwezo waandishi wa vyombo vya habari nchini ambapo kabla ya kutolewa kwa mtazamo huo imefafanuliwa kwa kina nini maana ya mitandao ya kijamii na nguvu yake katika kuhabarisha umma.


Mmiliki wa Blog ya K-VIS Blog Khalfan Said akitoa ufafanuzi kuhusu namna mitandao ya kijamii inavyofanya kazi,wakati wa emina ya waandishi wa habari za fedha na uchumi ambayo imeandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania(BoT) kwa ajili ya kuwajengea uwezo waandishi wa vyombo vya habari nchini ambapo kabla ya kutolewa kwa mtazamo huo imefafanuliwa kwa kina nini maana ya mitandao ya kijamii na nguvu yake katika kuhabarisha umma.

Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) tawi la Dodoma Richard Wambali( wa nne kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa wengine wa Benki Ku wakiwa pamoja na waandishi wa habari baada ya kufungua semina ya waandishi wa habari za uchumi na fedha leo jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) tawi la Dodoma Richard Wambali akizungumza na waandishi wa habari wakati akifungua semina ya waandishi wa habari za uchumi na fedha.Semina hiyo imeanza leo.

BODI YA WAKURUGENZI WA MAMLAKA YA HIFADHI YA WANYAMAPORI TANZANIA-TAWA

Wateja wa Tigo kuvinjari na Chopper

$
0
0


Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tigo Simon Karikari (kushoto) , akipeana mkono wa pongezi na Meneja wa Uber Tanzania Alfred Msemo, muda mfupi baada ya kuzindua promosheni ambayo itawawezesha wateja wa Tigo wanaotumia Uber pamoja nabaadhi ya washindi wa promosheni ya Jigiftishe kupanda helkopta siku ya Ijumaa na kufurahia mandhari ya Dar es Salaam wakiwa angani.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tigo Simon Karikari ( kulia) akibadilishana mawazo na Meneja wa Uber Tanzania Alfred Msemo (wa pili kulia) na Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo Hussein Sayed muda mfupi kabla ya uzinduzi wa promosheni ambayo itawawezesha wateja wa Tigo wanaotumia Uber pamoja nabaadhi ya washindi wa promosheni ya Jigiftishe kupanda helkopta siku ya Ijumaa na kufurahia mandhari ya Dar es Salaam wakiwa angani 


Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tigo Simon Karikari (wanne kulia) na Meneja wa Uber Tanzania Alfred Msemo (wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Tigo na Uber muda mfupi baada ya kuzindua promosheni itayowawezesha wateja wa Tigo wanaotumia Uber pamoja nabaadhi ya washindi wa promosheni ya Jigiftishe kupanda helkopta siku ya Ijumaa na kufurahia mandhari ya Dar es Salaam wakiwa angani.

HOSPITALI YA MNAZIMMOJA YAFANYA UCHUNGUZI WA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

$
0
0

Mratibu wa Mradi wa Uchukuzi wa Saratani ya Shingo ya Kizazi Zanzibar Dkt. Omar Mwalim Omar akimkaribisha Naibu Spika Mhe. Mgeni Hassan Juma katika Tiba ya Uchunguzi wa Saratani ya Shingo ya Kizazi inayofanyika Hospitali ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.
Mratibu wa Mradi wa Uchukuzi wa Saratani ya Singo ya Kizazi Zanzibar Omar Mwalim Omar akimuonyesha jambo Naibu Spika Mhe. Mgeni Hassan Juma wakati alipowatembelea Madaktari wanaoendelea kutoa matibabu Hospitalini hapo.
Naibu Spika Mhe. Mgeni Hassan Juma akipata maelezo kutoka kwa Daktari wa Maabara Kibwana Omar Kibwana wakati alipotembelea Chumba hicho cha Maabara Hospitalini hapo (kulia) Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman.
Mtaalamu wa Magonjwa ya Saratani ya Shingo ya Kizazi Hospitali ya Mnazi mmoja Dkt. Abdalla Yusssuf Mohamed akimpatia maelezo Naibu Spika Mhe. Mgeni Hassan Juma wakati alipotembelea katika Hospitali ya Mnazi mmoja Mjini Zanzibar.
Naibu Spika Mhe. Mgeni Hassan Juma akizungumza na Wananchi waliojitokeza kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya Uchukuzi wa Saratani ya Shingo ya Kizazi (kulila) Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman.

Baadhi ya Vifaa vinavyotumika kwa ajili ya kufanyia Uchukuzi wa Saratani ya Shingo ya Kizazi Hospitalini hapo. Picha Na Miza Othman – Maelezo Zanzibar.


Na Ali Issa Maelezo Zanzibar

Jumla ya kinamama 1,339 wamejitokeza katika uchunguzi pamoja na kufanyiwa vipimo vya maradhi ya kensa ya shingo ya kizazi katika hospitali kuu ya mmanazi mmoja mjini Unguja.

Mratibu wa mradi wa uchunguzi wa kensa ya shingo ya kizazi,Dk. Omar Mwalimu Omar alitoa kakwim hiyo huko hospitali ya mnazi mmoja wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya ziara maalum ya kutembelea eneo linalo endeshwa zoezi hilo.

Amesema katika zoezi hilo lililoanza Jumatatu iliopita hadi leo (Jumatatu) watu 36 kati hao wametiliwa mashaka na kufikia maamuzi ya kuchukuliwa vinyama ili kuchunguzwa kwa hatua nyengine na baadaye yatatoka majibu rasm ya afya zao.“Mara baada ya kuwafanyia uchunguzi mwengine na pindi tukibaini kuna mwenye maradhi hayo , tutaanza naye kwa kumpata tiba kwa kutumia dawa kwa mujibu wa taratibu za kitaalam”alisema Dk Omar.

Naye mtaalamu wa magonjwa ya saratani katika hospitali ya mnazi maoja, Dk Abdalla Yussuf Mohamed alisema katika zoezi hilo wanachunguza vinasaba vyote vya akinamama hao ambavyo ni muhimu katika uchunguzi huo. Mapema Naibu Spika Mgeni Hassan Juma alisema ni vyema wakaongezwa wataalamu wazalendo katika kupata kujifunza kutoka kwa watalamu wakichina waliopo. Aidha aliwapongeza akinamama hao waliojitokeza katika zoezi hilo na kuwataka waendelee kuwahamasisha wenzao ili zoezi hilo lifanikiwe kama lilivyokusudiwa.

Hatahivyo aliomba wizara ya afya kuangalia uwezekano wa uchubguzi kama huo kupelekwa Pemba na haospitali za mikoa ili idadi ya uchunguzi wa akinamama uongezeke. Kwa upande wa Naibu waziri wa Afya, Harusi Suleiman alisema lengo la serikali ya mapinduzi Zanzibar ni kuona kinamama wanapewa matibabu bora ili kutatua changamoto za maradhi yanayowasibu.

Mradi huo wa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi unaendeshwa na serikali ya china kwa muda wa miaka minne, ikiwa ni jitihada za Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk Ali Muhamed Shein

MIL. 800 ZATAKIWA KUKAMILISHA MAKAZI MRADI WA STIGLERS GORGE

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, RUFIJI .

NAIBU Waziri wa Ujenzi ,Elias Kuandikwa amemuagiza mtendaji mkuu wa Wakala wa Majengo Nchini (TBA) awasiliane na wizara ya nishati ,kuharakisha upatikanaji wa sh.milioni 800 ili kumalizia ukarabati wa nyumba za makazi 34 zinazojengwa katika ujenzi wa mradi wa uzalishaji umeme wa stiglers gorge Rufiji mkoani Pwani. 

Aidha amemtaka msimamizi wa ujenzi wa nyumba hizo kuhakikisha wanamaliza ujenzi huo wiki nne zijazo. Kuandikwa alielekeza hayo, wakati alipotembelea ujenzi wa barabara kutoka Kibiti -Mkongo na upande wa Mkoa wa Morogoro kupitia Ngerengere hadi Ubena-zote kuelekea kwenye mradi wa stiglers gorge. 

Alisema,wizara kupitia TBA ilikuwa na jukumu la kukarabati maeneo ya makazi na kutakiwa kumaliza mwezi Novemba mwaka huu lakini kutokana na changamoto ya kifedha ujenzi upo hatua ya umaliziaji. ” Nyumba hizi ni muhimu na kuna haja ya kuzikamilisha mapema ili mkandarasi akifika kuanza kazi akute mazingira ya makazi yako vizuri.” 

Awali akitoa taarifa kwa naibu waziri msimamizi wa ujenzi wa nyumba hizo ,Peter Baltazar alifafanua, fedha hizo milioni 800 zikipatikana ndani ya wiki nne watakuwa wamekamilisha ukarabati huo. Meneja wa wakala wa barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Pwani Mhandisi Yudas Msangi alisema , barabara ya kutoka Kibiti hadi kwenye eneo la mradi ina urefu wa kilometa 201,inajengwa kwa kiwango cha changarawe ,imejengwa na wakandarasi saba kwa upande wa Pwani na upande wa Morogoro wako wakandarasi sita . 

Akielezea barabara toka Kibiti hadi kwenye mradi alisema, umekamilika kwa asilimia 95. Msangi alisema ,barabara hiyo ni ya kiwango cha changarawe ina thamani ya shilingi bilioni 7.9 kwa sasa iko kwenye hatua za mwisho. Alielezea, mbali ya ujenzi huo wa barabara pia wamejenga madaraja matano na makalavati

RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA UJUMBE WA UWT UKIONGOZWA NA MWENYEKITI WAKE

$
0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania.(UWT) Thuwaiba Editon Kisasa, kulia Katibu Mkuu wa UWT, Queen Mlozi na kushoto Mwenyekiti wa UWT Gaudensia Kabaka, walipofika Ikulu Zanzibar kumtambulisha Mwenyekiti wa UWT Taifa Kabaka.10-12-2018.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania,(UWT) Gaudensia Kabaka,alipofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar,akiwa na Ujumbe wake wa Viongozi wa UWT.kulia Makamu Mwenyekiti wa UWT Thuwaiba Editon Kisasa na Katibu Mkuu wa UWT. Queen Mlozi.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ukiongozwa na Mwenyekiti wa Umoja huo Gaudensia Kabaka,Makamu Mwenyekiti wa UWT Thuwaiba Editon Kisasa na Katibu Mkuu wa UWT.B. Queen Mlozi, wakiwa katika ukumbi wa mkutona Ikulu leo wakati wa mazungumzo yao walipofika kujitambulisha.kwa Rais wa Zanzibar.(Picha na Ikulu)

Naibu Waziri Viwanda Atembelea Eneo Litakalotumiwa Kubangua Korosho ya Serikali

$
0
0

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya, akiwaonyesha mtambo maalum wa kuchemsha korosho wataalamu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele. Wataalam hao wametembelea eneo la SIDO kujiridhisha kama linafaa kwa ajili ya kuanza kubangua korosho iliyonunuliwa na serikali.
Kaimu Meneja wa SIDO mkoa wa Mtwara, Zamla Dongwala, akimuonyesha mashine ya kukausha korosho Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji (hayupo pichani) wakati alipotembelea eneo la SIDO, mkoani Mtwara leo. Eneo hilo ni moja ya maeneo yaliyochaguliwa kuanza kutumiwa wa wabanguaji wa korosho wadogo kubangua korosho zilizonunuliwa na serikali.
Fundi umeme akiwa kwenye hatua za mwisho kukamilisha matengenezo ya mashine ya kuchambua korosho kama alivyokutwa na mpiga picha wetu eneo la SIDO mjini Mtwara leo. (Picha na Idara ya Habari-MAELEZO

Washiriki Miss Journalism World Watua Kwa Tambo

$
0
0

Baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la Miss Journalism World wakiwa na mwenyeji wao ambaye ni mratibu wa shindano hilo, Sam Chazi (mwenye fulana) nje ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), walipowasili nchini jana. (Picha na Mpigapicha Wetu).


YAMETIMIA! Hatimaye warembo kutoka nchi kadhaa wanaowania taji la Miss Journalism World 2018, ambalo litafanyika hapa nchini Ijumaa ya Desemba 14, mwaka huu wamewasili.

Warembo hao waliwasili nchini jana kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), huku wachache waliobaki wakitarajiwa kuwasili leo. Wengi wa warembo hao walitamba kufanya kweli katika shindano hilo, huku waandaaji wakisema kila kitu kmekamilika. Shindano hilo linatarajiwa kufanyika jijini Arusha, katika ukumbi wa Kimataifa wa Aim Mall, huku waandaaji wakisema yatakuwa ya aina yake.

Akizungumza na waandishji wa habari jana, mratibu wa shindano hilo, Samwel Chazi, alisema warembo 16 wanatarajia kuwasili kesho mchana wakipitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ajili ya mpambano huo unaosubiriwa kwa hamu. Mmoja wa warembo hao kutoka China, Chen Sitong, alisema ana uhakika mkubwa wa kushinda, kwani amejiandaa.

Mratibu wa shindano hilo, Sam Chazi, aliwataja warembo hao na nchi wanazotoka zikiwa kwenye mabano kuwa ni Pauline Murati (Ufaransa), Nina Yetvushenko (Ukraine), Linda Plaude (Latvia), Fatima Kahametova (Urusi) na Zainab Mkuwu (Malawi).

Wengine ni Wioletta Tupko (Poland) na Noelia Ovejo (Hispania), Juliana Nare (Zimbabwe), Arlette Akimana (Burundi) na Chen Sitong (China). Wapo Roseline Ogunyale (Nigeria), Gisele Umwiza (Rwanda), Cassandre Joseph (Haiti), Wendy Omanga (Kenya) na mwenyeji wao Witness Kavumo (Tanzania).

“Kila kitu kimekamilika, hili ni shindano la kimataifa nab ado nafasi za kudhamini zipo, hii pia ni fursa kubwa ya kuitangaza Tanzania katika sekta ya utalii,” alisema Chazi. Alitaja viingilio katika shindano hilo ni Sh 100,000 kwa viti vya hadhi ya juu (VVIP), Sh 50,000 kwa viti maalumu (VIP) na viti vya kawaida Sh 30,000

“Tumeshusha viingilio ili kuwapa fursa Watanzania wapate kushuhudia warembo hawa wa dunia pale Aim Mall kwa mara ya kwanza,” alisema Chazi.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU WA MASUALA YA KIMATAIFA WA CANADA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Bw. Marc-Andre Fredette Mkurugenzi Mkuu Masuala ya Kimataifa wa Canada alipotembelea na kuzungumza nae Ikulu Jijini Dar es salaam,Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt.Agustine Mahiga .Desemba 10,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Bw. Marc-Andre Fredette Mkurugenzi Mkuu Masuala ya Kimataifa wa Canada alipotembelea Ikulu Jijini Dar es salaam ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt.Agustine Mahiga alihudhuria mazungumzo hayo.Desemba 10,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Bw. Marc-Andre Fredette Mkurugenzi Mkuu Masuala ya Kimataifa wa Canada alipotembelea na kuzungumza nae Ikulu Jijini Dar es salaam.Mazungumzo ambayo pia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt.Agustine Mahiga alihudhuria.Desemba 10,2018. . PICHA NA IKULU

TANZIA

SERIKALI YA WILAYA YA SIMANJIRO YATAKIWA KUFUATA UTARATIBU UJENZI WA CHUO CHA VETA

$
0
0








Naibu Waziri Wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Yefred Myenzi kuhusu namna walivyojipanga kujenga Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Wilaya katika eneo la Mradi la Emboreet lililoko katika Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akitoa zawadi kwa mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Kitwai A aliyefanya vizuri katika mitihani ya kuhitimu darasa la saba mwaka 2018. Shule ya Msingi Kitwai A imefaulisha wanafunzi 25 kati ya 28 waliofanya mtihani mwaka huu.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiongea na wakazi wa Kata ya Kitwai A iliyoko katika Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara ambapo amewataka kuhakikisha wanaandikisha shule wanafunzi wote wenye umri wa kuanza shule bila kuwaacha nyumbani na kuwapangia majukumu mengine.


Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ameitaka Serikali ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kuhakikisha inahusisha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA katika ujenzi wa Chuo cha VETA Simanjiro ili miundombinu ya chuo hicho iweze kujengwa kwa utaratibu na viwango vinavyohitajika.

Naibu Waziri Ole Nasha ametoa agizo hilo Mkoani Manyara wakati akikagua eneo ambalo Serikali ya Wilaya hiyo inategemea kujenga Chuo cha Veta kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Hiari ECLAT.

Alisema ni vizuri Mamlaka husika zikahusishwa katika ujenzi wa Chuo hicho tangu hatua za awali na kumtaka Mkurugenzi wa VETA kanda na yule wa Mkoa kufika katika eneo la Emboreet ambako mradi utajengwa kwa lengo la kuongea na wananchi pamoja na wafadhili wa mradi huo ili wazo ambalo limeanza liweze kutekelezwa kwa utaratibu unaostahili.

“Ninyi Halmashauri mnataka kujenga chuo cha Ufundi ni wazo zuri lakini ni lazima kijengwe kwa utaratibu sio kiholela kwa sababu vilianza kuibuka vyuo ambavyo mtu anakuwa na jengo moja anasajili kinaitwa chuo, kuna viwango na masharti ambayo ni lazima yatimizwe kabla chuo kuruhusiwa kufanya kazi, fuateni taratibu hizo ili muweze kuanzisha chuo cha Ufundi,” aliongeza Naibu Wazizri Ole Nasha.

Mheshimiwa Ole Nasha amesema Serikali ya Awamu ya Tano imeweka mkazo mkubwa katika Elimu ya Ufundi kwa kuwa kuna vijana wengi wanaomaliza shule wanaishia kutokuwa na ajira kwa kuwa hawana maarifa yanayowasaidia kupata ajira hasa pale wanapokosa fursa ya kuendelea na elimu ya juu hivyo ujenzi wa vyuo vya ufundi vingi utasaidia kuwajengea vijana wengi uwezo wa kujiajiri

“Nchi nyingi ambazo zimeendelea hata zile zinazoitwa ‘Asian tigers’ waliwekeza katika vyuo vya ufundi na sisi sasa tumetambua kuna mahali tuliteleza lakini sasa tumerudi kwenye mstari na ndio maana tunasema lazima tuwe na vyuo vingi vya ufundi ili kuongeza fursa za udahili ili vijana wetu wengi waweze kupata elimu ya ufundi,” alisema Naibu Waziri Ole Nasha.

Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Yefred Myenzi alisema wazo la kuanzisha Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi katika Wilaya hiyo ni ili kuwawezesha vijana kuweze kupata maarifa ya kuweza kujiaajiri badala ya kusubiri kuajiriwa.

Kwa upande wake Meneja Mradi ya ECLAT Bakiri Angalia amesema pamoja na shirika hilo kushiriki ujenzi wa Chuo hicho lakini pia katika Wilaya hiyo imefadhili miradi ya Elimu yenye thamani ya zaidi ya sh bilioni 3.

Naibu Waziri Ole Nasha pia ametembelea shule ya Msingi Kitwai A iliyopo Kata ya Kitwai katika Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro ambapo ameongea na wakazi wa kata hiyo na kuwataka kuhakikisha wanawaandikisha shule watoto wote wenye umri wa kuanza shule na kuahidi kujenga vyumba vya madarasa viwili na nyumba moja ya walimu yenye uwezo wa kuchukua familia mbili katika shule hiyo.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE DESEMBA 11,2018

JAJI MKUU ATOA WITO KWA VIONGOZI KUELIMISHA WANANCHI TARATIBU ZA UPATIKANAJI WA HAKI

$
0
0
Na Lydia Churi- Mahakama Dodoma

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ametoa wito kwa viongozi wa Mahakama, Serikali pamoja na Dini kuwaelimisha wananchi taratibu mbalimbali za upatikanaji wa haki. 

Akizungumza na wakuu wa wilaya za Chemba na Kondoa mkoani Dodoma leo, Jaji Mkuu amesema wananchi wengi hawafahamu taratibu za upatikanaji wa haki hivyo viongozi hao wanao wajibu wa kuwaelimisha kwa lugha ya upole wanapofika kwenye maeneo yao ya kazi.

Alisema kutokana na kutokufahamu taratibu za upatikanaji wa haki, wananchi wengine wamejikuta wakipoteza haki zao na wengine kutumia muda mwingi kushughulika na kesi ambazo thamani yake hailingani na muda na mali iliyotumika. 

“Wengine hudhani kupata haki ni kushinda kesi hawajui kwenye kesi kuna kushinda na kushindwa, dhana hii ndiyo inayoibua migogoro hivyo wananchi hawana budi kuelimishwa kuwa haki kwa aliyeshindwa ni kukata rufaa”, alisema Jaji Mkuu. Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania imejiwekea vigezo ili kuhakikisha inaboresha huduma zake na wananchi wanapata haki kwa wakati. Vigezo hivyo ni pa moja na kuhakikisha kesi inamalizika ndani ya miaka miwili kwenye Mahakama Kuu, miezi 12 kwenye Mahakama za Hakimu Mkazi pamoja na Mahakama za Wilaya  na miezi sita kwenye Mahakama za Mwanzo.

Kigezo kingine ni mapambano dhidi ya rushwa ambapo alisema Mahakama imesambaza nchi nzima mabango yenye ujumbe wa mapambano dhidi ya rushwa, simu za mikononi na pia imewapatia watumishi wake wote vitambulisho. Alisema Mahakama inaimarisha vitengo vya usuluhishi kikiwemo kitengo cha usuluhishi na mabaraza ya kata hasa kwenye maeneo  yasiyokuwa na Mahakama za Mwanzo.  Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, Mahakama pia hutoa nakala za hukumu bure na kuhakikisha nakala hizo zinatoka ndani ya siku 21, kupatikana kwa mienedo ya kesi ndani ya siku 30 ili kuwafikia wananchi na kutoa haki kwa wakati. 

Akizungumzia ushirikiano na mihimili mingine, Jaji Mkuu alisema mihimili yote ya dola inategemeana hivyo Mahakama haina budi kushirikiana ili wananchi wapate haki kwa wakati. Naye Mkuu wa wilaya ya Chemba, Simon Odunga akimkaribisha Jaji Mkuu wilayani kwake alisema wilaya yake itaendeleza ushirikiano kati yake na Mahakama ya Tanzania.Jaji Mk u wa Tanzania ameanza ziara ya siku mbili katika mkoa wa Dodoma ambapo leo ametembelea wilaya ya Chemba pamoja na Mahakama ya wilaya ya Kondoa na kukagua shughuli za Mahakama.

ARIEL CAMP 2018 YAFUNGULIWA DAR...MSAADA WA KISAIKOLOJIA WATAKIWA KWA WATOTO NA VIJANA

$
0
0

Imeelezwa kuwa vijana na watoto wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI wanahitaji msaada maalumu wa kisaikolojia kwa ajili ya kukabiliana na athari za kimwili, kisaikolojia, kijamii na kiroho ili waweze kuishi maisha marefu, yenye furaha na matumaini hivyo kutimiza ndoto zao. 

Rai hiyo imetolewa leo Jumatatu Disemba 10,2018 na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mwitikio wa Kitaifa, Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Bi Audrey Njelekela wakati akifungua Kambi ya Watoto na Vijana ya Ariel 2018 katika hoteli ya Serene, jijini Dar es salaam.

Kambi hiyo ya wiki moja inayojumuisha watoto na vijana 50 kutoka mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Mara na Mwanza ambao pia ni wanachama wa klabu za vijana na watoto zinasimamiwa na asasi isiyo ya kiserikali ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) inayolenga kutokomeza VVU na UKIMWI kwa watoto na familia.

Bi Njelekela alisema kuwa kupata tiba za kupunguza makali ya VVU pekee hakutoshi. " Watoto na vijana wanahitaji msaada wa kisaikolojia utakaowaimarisha ili kupambana na changamoto wanazokabiliana nazo," alisema.

"Changamoto hizi ni pamoja na msongo wa mawazo, unyanyapaa, hofu ya kufa au kujulikana kuwa wanaishi na maambukizi ya VVU, magonjwa ya kila mara na mshtuko unaotokana na kutunza wagonjwa au kushuhudia vifo vya wazazi au ndugu wa karibu," alieleza.

"Mara nyingi vijana wanaoishi na maambukizi ya VVU huwa wamepoteza mzazi mmoja au wawili, hivyo kutokuwa na watu wa kuwasaidia changamoto hizo na nyingine nyingi kuathiri makuzi na afya zao", aliongeza. Aidha Bi Njelekela alisema ufuasi wa dawa za ARV ni mdogo sana miongoni mwa watoto ikilinganishwa na ufuasi wa dawa hizo kwa watu wazima. Alisema kuwa ili kukabiliana na hali hiyo msaada maalumu wa kisaikolojia ili kuwasaidia watoto ni muhimu.

“Ufuasi huo mdogo unaelezwa kusababishwa na watoto na vijana kutojua kwanini wanakunywa dawa na umuhimu wa dawa hizo kwa afya zao, shinikizo rika na kutokuwa na usimamizi wa kutosha,” alisema Bi Njelekela.

Bi Njelekela alitumia fursa hiyo kuipongeza na kuishukuru AGPAHI kwa kutoa elimu ya kisaikolojia kwa vijana na watoto na kuiomba pia itoe elimu hiyo kwa wazazi na walezi hasa ikizingatiwa kuwa wengi wao hawana elimu ya kutosha kuhusu VVU na UKIMWI. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa alisema wanaendelea kushirikiana na serikali ili kuhakikisha maambukizi ya VVU yanatokomezwa.

“Tumeanzisha vikundi vya vijana wa umri balehe kwani tunatambua kuwa vijana wana mahitaji maalumu yanayoendana na ujana. Tumekuwa tukiwafundisha kuhusu masuala ya shinikizo rika, kujikinga na maambukizi mapya ya VVU, mabadiliko ya mwili, afya ya uzazi na stadi za maisha ili kuwajenga waweze kutimiza ndoto zao na kuwa wanachotaka,” aliongeza Dk. Sekela.

"Tanzania bila UKIMWI inawezekana hivyo tunaendelea kushirikiana na serikali ili kuhakikisha tunawafikia watoto wengi waliozaliwa na maambukizi ya VVU tunawaanzishia huduma za tiba na matunzo," aliongeza Dk. Sekela.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mwitikio wa Kitaifa,Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Bi Audrey Njelekela akifungua Kambi ya Watoto na Vijana ya Ariel 2018 katika hoteli ya Serene iliyopo Dar es salaam.Watoto na vijana hao wanatoka katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara.

Bi Audrey Njelekela akifungua kambi ya Ariel. Kutoka kulia ni Afisa Habari NACOPHA, Bi. Mensia John na Meneja wa Huduma za mama na mtoto AGPAHI Dk. Akwila Temu. Kutoka kushoto ni Meneja wa Fedha wa AGPAHI, Bw. Gwamaka Nsekela na Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa.

Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa, akizungumza katika ufunguzi wa Ariel Camp 2018 katika hoteli ya Serene, Dar es salaam.AGPAHI inatoa huduma za kisaikolojia kwa watoto na vijana wa mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Mara na Mwanza kwa kushirikiana na serikali kupitia halmashauri za wilaya.

Vijana wakimsikiliza Dk. Sekela Mwakyusa.
Afisa Mradi wa Huduma za Jamii na Huduma Unganishi AGPAHI mkoa wa Mara, Madina Maduhu, akitoa historia fupi ya Klabu na Kambi za Watoto na Vijana. Alisema Kambi zilianza mwaka 2011 ambapo kikundi cha watoto 60 katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga kilianzishwa. Hadi Septemba 2018 kambi hizo zilifika 105 zikiwa na wanachama 4,320 katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Mwanza na Mara.

Vijana na watoto wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea ukumbini.

Kijana Agnes William akielezea faida za klabu za watoto na vijana. "Klabu za Ariel vinasaidia kuwajengea vijana na watoto uwezo wa kujieleza, kujitambua na ujasiri wa kuendelea na malengo yao ya maisha na kutimiza ndoto zao za baadae.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Babawatoto Centre, Bw. Mgunga mwa Mnyenyelwa akicheza na vijana na watoto.

Kikundi cha Taasisi ya Babawatoto kikitoa burudani ya sarakasi wakati wa ufunguzi wa Ariel Camp 2018.

Vijana wakifuatilia burudani.
Picha ya pamoja mgeni rasmi na washiriki wa Ariel Camp 2018.

Picha ya pamoja. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

PROFESA KABUDI ATEMBELEA IHUMWA KUKAGUA UJENZI WA OFISI ZA WIZARA

$
0
0
 Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palmagamba Kabudi (mwenye shati jeupe) akiangalia moja ya mipaka katika kiwanja cha kujenga jengo la Wizara hiyo eneo la Ihumwa Mkoani Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. sifuni Mchome na aliyepo  katikati ni fundi ujenzi.
 Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palmagamba Kabudi akiangalia ramani ya ujenzi wa Jengo la Wizara katiika eneo la Ihumwa Mkoani Dodoma.
 Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palmagamba Kabudi akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wakati alipotembelea eneo la kiwanja cha Wizara Ihumwa.
 Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palmagamba Kabudi akipanda excavator ili kuishuhudia namna linavyofanya kazi wakati akikagua eneo la kiwanja linapojengwa jengo la Wizara ya Katiba na Sheria Mkoani Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palmagamba Kabudi akijadiliana jambo na Mkandarasi na viongozi wa Wizara wakati akikagua eneo la ujenzi wa jengo la Wizara hiyo.

TAKUKURU YAELEZA ILIVYOKUTA BAHASHA YA KAKI MEZANI KWA WAZIRI LUKUVI

$
0
0
Na Karama  Kenyunko, Blogu ya Jamii

KAIMU Kamishna Msaidizi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maendeleo  ya Makazi Wilson Luge (39) ameieleza Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam kuwa fedha alizoenda kuhakiki katika ofisi  ya Waziri  wa  Ardhi   zinazodaiwa  kutolewa kama rushwa kwa Waziri William Lukuvi zilikuwa zimehifadhiwa katika mfuko wa kaki.

Luge ameyasema hayo leo  Desemba  11, 2018  wakati anajibu swali la  Wakili  wa utetezi Imani Madega dhidi ya kesi ya tuhuma za rushwa  ya Sh. Milioni 90 kwa Waziri wa Ardhi, William Lukuvi inayomkabili Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Steal Group Co.ltd na Kiluwa Free Processing Zone,Mohamed Kiluwa alipokuwa akitoa ushahidi  wake mbele ya Hakimu Mkazi Samwel Obasi.

Amedai mahakamani hapo kuwa Julia  16 mwaka huu akiwa kazini kati ya saa saba mchana hadi saa 10 jioni, walikuwa wanaangalia mfumo wa kielekroniki wanaoutumia kama unafanya kazi vizuri, Esquires na Kamishna Mkuu wa Ardhi Mary Makondo na kuwaelekeza waende ofisi ya Waziri Lukuvi.

Pia amedai walipoingia walikuta watu mbalimbali huku mezani kukiwa na mfuko wa kaki uliokuwa umefungwa ambao hakujua ndani  yake kulikuwa na nini na kwamba mfuko huo ulifunguliwa na maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru na kutoa fedha ambazo ni mabunda manne ya Dola za Marekani 40,000 ambapo waliwataka  yeye na Hellen Philipo walihakiki fedha hizo.

Mapema akiongozwa kutoa ushahidi na Wakili wa Takukuru Maghela Ndimbo, shahidi huyo wa sita amedai Julai 16, mwaka huu alikuwa ofisini kwake Kanda ya Dar es Salaam ambayo zamani ilikuwa Makao Makuu ya Wizara hiyo.Alidai kati ya saa saba hadi saa 10 jioni, walikuwa wanaangalia mfumo wa kielekroniki wanaoutumia kama unafanya kazi vizuri ambapo Kamishna Mkuu wa Ardhi, Mary Makondo aliwaita akiwaelekeza waende ofisi ya Waziri Lukuvi.

"Tulipoingia tulikuta baadhi ya watu ambao ni maofisa uchunguzi wa Takukuru, Waziri Lukuvi na Kiluwa. Tuliambiwa kuna bahasha ifunguliwe na sisi tuhakiki kilichomo.... ofisa uchunguzi alifungua na sisi kueka mezani mabunda manne yaliyofungwa," amedai Luge.Amedai baada ya kuzihakiki waliainisha fedha zote kwenye karatasi ya uchunguzi na kusaini na baada ya kukamilisha kazi hiyo waliruhusiwa kuondoka.

Akihojiwa na Wakili Madega kuhusu mahali walipozikuta fedha hizo, shahidi alidai kuwa walizikuta kwenye mfuko na kwamba ofisa uchunguzi ndiye aliyefungua na si Waziri Lukuvi wala mshitakiwa.Pia alidai hakushuhudia tendo lolote zaidi ya kuhakiki fedha isipokuwa alifanya kazi aliyoambiwa ya kuhakiki na hakujua fedha za nini.

Kwa upande wa Ofisa Uchunguzi wa Takukuru, Colman Lubisa (36)  alidai kuwa hakushuhudia wakati Kiluwa akitoa rushwa kwa Waziri Lukuvi bali walipoingia ofisini walikuta fedha mezani ndipo walizihakiki."Kama Kiluwa asingefika kutokana na mwito wa Waziri Lukuvi kwa taratibu za Wizara ni lazima angeandikiwa barua ya mwito au notisi yoyote ile. Tulipata taarifa baada ya Waziri Lukuvi kupiga  simu kwa Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Takukuru, Mbengwa Kasomambuto na kumueleza kuwa Kiluwa atafika ofisini akiwa na fedha Dola za Marekani 50,000," alidai Lubisa.

Pia alidai baada ya taarifa hiyo walikwenda kuandaa mtego ikiwemo kifaa cha kurekodia ili endapo mshitakiwa atafika na fedha hizo waweze kumkamata.Shahidi wa tano alidai baada ya kuandaa mtego walikaa nje kumsubiria mshitakiwa huyo na kati ya saa sita  hadi saba alifika akiwa na begi.

"Mara baada ya kutoa fedha ambazo ni mabunda manne ya dola za Marekani yenye noti 100 kila moja na kuziweka mezani tuliingia na kumuweka chini ya ulinzi mshitakiwa na tuliita mashahidi wawili kuhakiki fedha zote," alidai Lubisa.Akihojiwa na Wakili wa Utetezi, Imani Madega, kuhusu kuchunguza mazingira ya rushwa kati ya Lukuvi na Kiluwa, alidai kuwa kitendo cha Waziri Lukuvi kumpa  taarifa kwa njia ya simu mshitakiwa  ni sahihi na endapo asingekwenda na fedha wasingejua kama anataka kutoa rushwa.

Alidai lengo la Kiluwa kutoa rushwa ni kumtaka Waziri alitelekeze alichokitaka katika hati 57 za kiwanja kilichopo maeneo ya Mlandizi na bila Waziri Lukuvi kutoa taarifa wasingejua mazingira hayo.Alidai tangu hati kusajiliwa ilikuwa na siku mbili pekee licha ya kutakiwa kutumika kwa uwekezaji baada ya miaka miwili huku umri wa hati ni miaka 66.

Pia alidai hakuwahi kupata malalamiko ya rushwa dhidi ya Kiluwa zaidi ya taarifa iliyotoka kwa Waziri Lukuvi na kwamba hawakutaka kuthibitisha uhalali wa taarifa hiyo kwa sababu aliyeitoa ni mtu wa serikali.Hata hivyo upande wa mashtaka umefunga kesi yao na Mahakama imeamua kuwa,  mshtakiwa  amekutwa na kesi ya kujibu, hivyo ataanza kujitetea Desemba 17 mwaka huu.

Katika kesi hiyo Kiluwa  anadaiwa kuwa Julai 16, mwaka huu,  akiwa Mkurugenzi wa kampuni hizo mbili alitoa rushwa ya Dola za Marekani 40,000 ambazo ni sawa na Sh.milioni 90 kwa Waziri Lukuvi.Mshitakiwa anadaiwa kutoa  fedha hizo ili asiwasilishe hati ya umiliki wa kiwanja namba 57 Block B Kikongo na D Disunyura kilichopo eneo la viwanda lililopo Kibaha mkoani Pwani. Kiluwa yupo nje kwa dhamana.
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>