Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 172 | 173 | (Page 174) | 175 | 176 | .... | 1896 | newer

  0 0

   Mdau akiangalia kitambulisho cha Taifa cha mmoja wa maofisa alioongozana nao Rais Kikwete wakati alipokutana na Watanzania waishio Poland katika hoteli ya Bristol jijini Warsaw usiku wa kuamkia leo. Wengi wa wadau hawa walikuwa hawana habari kwamba vitambulisho vya Taifa vimeshaanza kugawiwa kwa wananchi
   Aliyewahi kuwa balozi wa Poland nchini Tanzania akijitambulisha
   Mwalimu Anna Paciorek akiuliza swali
   Padri akieleza jambo
   Mmoja wa wadau akiuliza swali
   Rais Kikwete akiongea na Watanzania hao
   Hotuba na ufafanuzi wa mambo mbalimbali vinaendelea
   Kila mmoja akimsikiliza Rais Kikwete kwa makini
   Hotuba ikiendelea
   Hapa ni kuhusu umuhimu wa ughaibuni kujenga nyumbani...
   Mwalimu Anna PAciorek akisoma risala ya Watanzania wa Poland
   Kaimu Balozi Mhe Christopher Mvula akifunua pazia la kikao hicho
   Rais Kikwete akipokea risala toka kwa Mwalimu Anna Pacoirek
   Wadau wakijitambulisha
  Mama Salma Kikwete akiongea na familia ya Mdau Wambura
  PICHA NA IKULU.

  0 0


  Picha ya pili, Abeid Semira wa kutoka Mwanza anapokea zawadi yake kutoka kwa Bi, Hytham Ahmed wa Masoko Ltd. kupitia promosheni iliyokuwa ikiendeshwa na Colgate Palmolive.  
  Valarie Urio wa Dar es Salaam, anapokea jiko la Gesi cooker kutoka kwa Bi, Hytham Ahmed wa masoko Ltd kupitia promosheni iliyokuwa ikiendeshwa na Colgate Palmolive. 
  =======   =======  =======
  Wakazi wa jijini Dar es salaam na mikoa ya Arusha, Mwanza na Mbeya waliokuwa wakinunua bidhaa za  Sta- Soft  na Axion (sabuni ya kuoshea vyombo) zinazosambazwa na Colgate Pamolive wamekabidhiwa zawadi zao kupitia promosheni iliyokuwa ikiendeshwa na Colgate Palmolive.

  Kampuni ya Colgate Pamolive imekuwa ikiendesha promosheni  maalum ya CLEAN HOUSE kwa muda wa miezi miwili iliyokuwa na lengo la kuwafahamisha watanzania jinsi bidhaa zao za Sta- soft ambazo ni maalum kwa kufulia nguo na Axion maalum kwa usafi wa vyombo vya nyumbani. Bidhaa hizi ni maalum  kwa kufanya usafi kwa ufanisi mkubwa.

  Akieezea bidhaa hizo Afisa Masoko wa Colgate Pamolive  Bw, Meshack Mdingi alisema “ Lengo la promosheni  hii ni kuwajulisha wateja wetu jinsi wanavyoweza kuepuka magonjwa ya ngozi kwa kufua nguo zao na Sta- soft inayotunza nguo zako na kuziweka laini  wakati wote na harufu nzuri na  kusafisha vyombo vya ndani.  Wateja wetu tunawashauri watumie  bidhaa yetu ya Axion inayofanya vyombo vibaki na mng’ao wake mzuri siku zote”

  Walioibuka washindi kwenye promosheni ya Clean House ni wale wote walionunua bidhaa hizi kati ya September na Oktoba ambapo walichaguliwa kupitia droo maalum iliyofanyika wiki iliyopita maeneo ya Mwenge jijini Dar Es Salaam.

  Baadhi ya walioibuka washindi  kupitia promosheni hiyo ni  Valeria Urio mkazi wa Dar Es Salaam, aliyejishindia Jiko la Gas cooker,  Abeid Semira mkaazi wa Mwanza aliyejishidia Jagi la Kuchemsha maji, Hassan Ibraim mkaazi wa Tanga kati ya wengine 50.

  Bw, Mdingi alisema hadi kufikia mwisho wa promosheni  wameweza kuwaelimisha watu wengi kuhusiana na Usafi wa jamii, pia kurudisha faida wanazopata kwa jamii kwa kutoa zawadi ambapo jumla ya Majiko ya Gesi 3,Seti za Masufuria 8,  Seti za jagi za maji 8, pamoja na  mashine za umeme za kukausha mkate (Toaster) 8 za  kisasa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na zawadi nyengine ndogo ndogo.

  Kupitia bidhaa zetu bado tutaendelea kuwafikia wateja wengi kwa kufanya promosheni kama hizi huku tukitoa elimu kuhusiana na usafi kwa jamii na kutoa zawadi tofauti tofauti ili kuwafaidisha wale wote wanatumia bidhaa zetu za Colgate Pamolive, alimazia Bw, Mdingi

  0 0

  GWIJI wa muziki wa dansi mstaafu Muhidin Maalim Gurumo (pichani) ameugua ghafla mapema leo na kulazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.  Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Gurumo, Juma Mbizo na Said Mdoe, waliokuwepo Muhimbili, wameiambia Globu ya Jamii kuwa mwimbaji huyo mkongwe alipatwa na tatizo la shinikizo la damu na hali ikawa mbaya kabla ya kukimbizwa hospitalini hapo. Wamesema kwa sasa hali yake inaendelea vizuri na amelazwa katika wodi ya Mwaisela namba 1.

  Wajumbe hao wamesema siku chache zilizopita Gurumo alikuwa kwenye afya njema na hata siku ya Jumanne alihudhuria kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Vijana Social Hall Kinondoni.  Aidha, wajumbe hao wamedai kuwa kwa mujibu wa mke wa Gurumo, Bi Pili, ni kwamba hata jana mwimbaji huyo alikuwa hana tatizo lolote na alifanya mizunguko yake bila ya mikwaruzo yoyote.  Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha la Gurumo, Bi Asha Baraka amewataka wapenzi wa muziki kuwa watulivu kwa vile hali ya mwanamuziki huyo aliyeitumikia fani kwa miaka 53, inaendelea vizuri. 

  Tamasha la Gurumo limepangwa kufanyika tarehe 14 mwezi ujao katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe. Tumuombee dua mzee wetu Gurumo.

  0 0

   Paul Okoye wa kwanza kulia, akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani) kuhusu tamasha watakalolifanya kesho Jumamosi. Novemba 23 katika viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Peter Okoye ambao kwa pamoja wanaunda kundi la P Square, wakiwa na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twisa ambao ni wadhamini wa wasanii hao pamoja na Lady Jay Dee mmoja wa wasanii watakaowasindikiza jukwaani wasanii hao.
    Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule akipeana mkono na wasanii, Peter na Paul Okoye, maarufu kama P Square wakati walipowasili kwenda kutoa msaada katika kituo cha watoto wenye ulemavu wa usonji “Autism” (utindio wa ubongo) cha Msimbazi Mseto, jijini Dar es Salaam.
   .Msanii Peter Okoye akimuweka vizuri katika bembea  mmoja wa wanafunzi wenye ulemavu wa usonji katika shule ya Msimbazi Mseto jijini Dar es Salaam. Wa kwa nza kutoka kushoto ni mwalimu Mkuu wa shule hiyo Reuben Gadi  na Mjumbe wa bodi ya shule hiyo Mtumwa Nindi, na wa kwanza kulia ni mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Precious Hughes ambao ni wadhamini waliofanikisha wasanii hao kutua nchini.
   Wasanii wa kundi la P Square (Peter na Paul Okoye) katikati wakimsikiliza Mtoto mwenye ulemavu wa Usonji,  Erick wa shule ya msimbazi Mseto walipokwenda kushiriki kutoa msaada kwa kituo cha watoto hao. Wa kwanza kushoto ni mwalimu mkuu wa shule hiyo Reuben Gadi na kulia ni Mkuu  wa kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule pamoja na wafanyakazi wengine wa kampuni hiyo.
   Wasanii wa kundi la P Square wakikabidhi misaada mbalimbali kwa watoto wenye ulemavu wa usonji  wa kituo cha Msimbazi Mseto cha jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule akishuhudia makabidhiano hayo, na katikati ni walimu wa shule hiyo wakipokea kwa pamoja misaada hiyo.
  Wasanii Peter na Paul Okoye Maarufu kama P square wakiwa pamoja na Mkuu wa Kitengo cha huduma za jamii Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule wakicheza pamoja na watoto wenye ulemavu wa usonji  wa shule ya msingi ya Msimbazi mseto, wakati waliposhiriki kutoa msaada katika shule hicho kwa watoto hao wenye mahitaji maalum.
  =========  =======  ==========
  ·        Waviomba kuwapa ushirikiano wasanii wa muziki nchini
  ·        kufanya onesho kwa masaa mawili mfululizo
  ·        Washiriki katika shughuli za kijamii
  Baada ya kuwasili nchini usiku wa jana wanamuziki mapacha Peter na Paul Okoye maarufu kama “P – Square” wametoa wito kwa  vyombo vya habari nchini kuwasaidia wasanii wandani na kuwa chachu ya mafanikio ya muziki kama vilivyo vyombo vya nchi nyingine, huku wakiahidi kufanya makubwa katika Shoo yao ya siku ya leo kwa mashabiki wao watakaojitokeza katika Viwanja vya Leaders Club.
  Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hotel ya Hyatt jijini Dar wasanii hao wamesema wamefurahishwa na mapokezi waliyoyapata kutoka kwa jamii ya Watanzania na waandaaji wa Tamasha hilo na kuahidi burudani ya kipekee kwa Watanzania.
  Peter Okoye ambaye ni mdogo wake na Paul alisema, vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kuwajenga wasanii huku akitoa wito kwa vyombo hivyo kuwa kichocheo cha kuwajenga wasanii na sio kuwabomoa.
  “Vyombo vya nchini kwetu vimetufikisha hapa tulipo wamejitahidi kutujenga na kutusaidia kusikika Afrika nzima., Tutaona fahari kama vyombo vya hapa nchini pia vitajenga uwezo wa kuwasaidia wasanii wa ndani nao waweze kufika au hata kuzidi hapa tulipo, Tutafurahi siku tukiwaona wasanii kama kina Jay dee na Ben Pol wakija Nigeria kama sisi tulivyokuja nchini kwao, alisema Paul.
  Paul Okoye ambaye ni kaka kwa Peter  amesema “Tumefurahishwa sana na mapokezi tuliyoyapata tangu jana usiku hadi kufikia sasa, tumejisikia faraja kuwa katika nchi hii ya Tanzania watu wake ni wakarimu sana sifa hizi tumezisikia kwa watu mbalimbali na tumeshuhudia wenyewe tunawaahidi Mashabiki wetu kufanya Shoo ya uhakika., alisema Paul Okoye.
  Kwa upande wa wadhamini wakuu wa Tamasha hilo Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa,alisema wamejisikia faraja kwa pamoja kufanikiwa kuwaleta wasanii hao ili watoe burudani kwa Watanzania na kuweza kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kama vile kutoa msada wa vyakula katika shule ya Msingi Msimbazi Mseto kwa kupitia mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom” Vodacom Foundation”.
   “Kwa upande wetu sisi kama waandaaji kila kitu kimekamilika kuanzia, masuala ya usalama na jukwaa vyote vimekamilika, Pamoja na mambo mengine tunatoa wito kwa Watanzania kuwai kufika maana onyesho litaanza saa 1 na kuwa sihii kuwa wastaarabu wakati wote wa Shoo hiyo na kujiepusha na vitendo vyovyote ambavyo vinaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
  Wasanii kutoka Bongo watakao toa burudani katika Tamasha hilo ni pamoja na wakongwe, Prof. Jay, Lady Jaydee, Jo Makini”mwamba wa kaskazini”pamoja na Ben Pol.

  Wakati huo huo wasanii hao na kitengo cha huduma za jamii cha Vodacom Foundation wameshiriki katika kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa  watoto wenye ulemavu wa akili cha Msimbazi Mseto kilichopo jijini Dar es Salaam. Huku wakitoa wito kwa jamii ya Watanzania kuendelea kuwasaidia watu wote wasio na uwezo ili kujenga jamii yenye maisha sawa kwa wote.


  0 0


  Bondia mkonwe Iraki Huddu aka "Simba asiye zeeka" juzi kati alionekana tena
  katika ukumbi wa Milimani City, kumsindikia bint yake Bi.Mkumwena Huddu ambaye amemaliza kuitimu na kupata shahada ya BA - Culture Heritage chuo kikuu cha UDSM ,Iraki Huddu anaonekana anawapandisha watoto.

  wake katika ulingo wa ELIMU ya juu sio ulingo wa ngumi, Bint huyo Mkumwena Huddu
  sasa anaenda UDOM -Dodoma kuchukua MA,Natural Resource.
  Ni miezi ya nyuma tu mtoto wake mwingine alichukua nondo kule UDOM....
  sasa Bondia Iraki Udu anasema Boxing for High Education....kwa familia yake

  0 0

  Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh. Freeman Mbowe (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) waliofika kwenye Makao Makuu ya Chama hicho leo,ambapo Kamati ya Chama hicho imeamua imeamua kuwavua nyadhifa mbali mbali baadhi ya viongozi wa Juu wa Chama hicho akiwepo Mh. Zitto Kabwe. Wengine pichani toka kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Udhamini wa Chama hicho, Sylvester Kanyansi Masinde, Katibu Mkuu, Dk Wilbroad Slaa, Mwanasheria Mkuu wa Chama, Tundu Lisu na viongozi wengine wa Kamati Kuu ya CHADEMA.

  Na Chadema Blog
  KAMATI kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA imewavua Uongozi Viongozi wake watatu baada ya Kugundua waraka wa Siri uliowahusisha na mpango wa kukipasua Chama vipande vipande.

  Viongozi waliovuliwa Uongozi ni Zitto Kabwe ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Dr Kitila Mkumbo na Samsoni Mwigamba aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini. Hatua hiyo ilichukuliwa katika kikao cha kamati kuu kilichokuwa kimefanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam.

  Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari Mh Tundu Lissu amesema katika Waraka huo kulikuwa na mtu anayejulikana kama MM ambaye ni Naibu Katibu mkuu Zitto Kabwe, M1 ni Dr Kitila Mkumbo, M3 ni Samsoni Mwigamba na M2 hajajulikana ambaye ni mtumishi wa makao makuu ya Chadema. Mh Lissu amesema Dr Kitila Mkumbo alikana kabisa kumfahamu M2.

  Mh Tundu Lissu amesema Waraka huo uliojulikana kama Waraka wa Ushindi unavunja katiba ya Chama kwa sababu umepandikiza chuki za kidini, majungu na kukashifu viongozi wa Chama kinyume na katiba ya CHADEMA. 

  Mh Tundu Lissu amesema tuhuma zote zilizoko katika waraka huo hazijawahi kuwasilishwa kwenye kikao chochote halali cha chama kinyume na matakwa na masharti ya katiba yetu. Mh Tundu Lissu Amesema Kamati Kuu imeamua kuwavua nyadhifa zao zote watu wote waliotajwa katika waraka huo ambao ni Zitto Kabwe, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba.

  Pia kamati kuu imeunda kamati ya kuchunguza na kufuatilia mhusika mwingine M2 ambaye anadaiwa ni Mtumishi wa Makao Makuu ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yake.

  Kamati Kuu imeagiza wahusika wote waandikiwe barua za kujieleza ni kwanini wasivuliwe uanachama kwa makosa hayo makubwa waliyofanya.
  Pia Kamati Kuu imeagiza mchakato wa kumvua Zitto nafasi yake ya Unaibu wa Kambi ya Upinzani Bungeni.

  Lissu amesema Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe na Dr. Kitila Mkumbo waliomba kujiuzulu nyadhifa zao zote baada ya waraka wao kukamatwa lakini Kamati Kuu iliwakatilia baada ya kuona kuwa kukubaliana na maombi yao hayo ilikuwa ni kama kuwaacha wajiuzulu kwa heshima ambayo hawaistahili hata kidogo.

  Wakati huo huo kamati kuu imemteua Mh Tundu Lissu kuwa Mwanasheria mkuu wa Chama.

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipungia wananchi wakati akirejea kijiji cha Lituhi kwa kuvuka mto Ruhuhu kwa mtumbwi,  baada ya kutoka kuwasalimu wakazi wa kijiji cha Kipingu wilayani Ludewa,wengine pichani ni Dk.Asha-Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho.
   
  Sehemu ya eneo la mto Ruhuhu,kivuko cha mto huo kimeshindwa kufanya kazi kutokana na kina chake cha maji kupungu,Ndugu Kinana alisema kuwa kivuko hicho hufanya kazi kwa muda wa miezi minne tu kwa mwaka,miezi mingine yote halifanyikazi kutokana na kina cha maji kupungua,hata hivyo Ndugu Kinana alieleza kuwa Serikali itajenga daraja kufuatia ahadi aliyoitoa Mh Rais Jakaya Kikwete kwa wakazi wa kijiji hicho.
    Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Lituhi wakiwa ndani ya Mtumbwi  wakitokea katika kijiji cha Kipingu wilayani Ludewa,shoto ni  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Ndugu Ernest Kahindi wakivuka kwa mtumbwi mto Ruhuhu kuelekea kijiji cha Kipingu wilaya ya Ludewa.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya jinsi ya kutumia vifaa vya maabara katika kufanikisha kutambua kemikali kutoka kwa wanafunzi wa kidato cha nne Erasto Ndumba na Stella Hyera wa shule ya sekondari ya Kata ya Mtakatifu Paul kata ya Liuli wilaya ya Nyasa.

  Wakazi wa kijiji cha Lituhi wakimsikiliza   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Lituhi ambapo wanachama zaidi ya 400 wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi nyumba za madaktari zilizochini ya mradi wa Taasisi Benjamini Mkapa katika kituo cha afya  Mkili kata Liundi wilayani Nyasa.
   Mbunge wa Mbinga Magharibi Kapteni John Komba akimtambulisha Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kama Ndugu yake wa karibu kwani mafanikio yake yametokana na mchango mkubwa wa Marehemu Mzee Nnauye ,Pia Komba alimuelezea Kinana kama mmoja wa walimu wake wazuri wa masomo ya kijeshi pamoja na siasa. 
   nyumba za madaktari zilizochini ya mradi wa Taasisi Benjamini Mkapa katika kituo cha afya  Mkili kata Liundi wilayani Nyasa. 

  0 0
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana, asubuhi hii amemaliza ziara yake katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma na kuanza safari ya kwenda Kyela mkoani Mbeya, ambako ataanza ziara rasmi ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzipatia ufumbuzi.Pichani, Kinana na wajumbe wake wa sekretarieti ya CCM, Nape Nnauye (Itikadi na Uenezi) na Dk. Asha-Rose Migiro (Siasa na Uhusiano wa Kimataifa), wakiwapungia mikono wananchi wa Nyasa, baada ya kupanda Mv Songea, kuanza safari ya kwenda Kyela. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Ernest Kahindi
  Kwaherini wakazi wa wilaya ya Nyasa,sasa tunaelekea wilaya ya kyela mkoani Mbeya.

  Baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM wakiwa na shamra shamra wakati wakiusindiza ujumbe wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana walipokuwa wakielekea Kyela mkoani Mbeya mapema leo asubuhi kuendelea na ziara yake.

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakilakiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik(kushoto) muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaaam leo jioni.Rais Kikwete amerejea nchini akitokea Warsaw Poland ambapo alihudhuria mkutano wa Mabadiliko ya Tabia nchi Duniani na awali wiki iliyopita alikuwa nchini Srilanka kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Madola.(picha na Freddy Maro).

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Krismasi, Alex Msama akifafanua jambo kuhusu maadalizi ya tamasha la Krisimasi ambapo kwa mara ya kwanza litafanyika kwenye uwanja wa Mao Tse Tung  mjini Zanzibar. (Picha na Francis Dande)

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Krismasi, Alex Msama akifafanua jambo kuhusu maadalizi ya tamasha la Krisimasi ambapo kwa mara ya kwanza litafanyika kwenye uwanja wa Mao Tse Tung  mjini Zanzibar. 
  ==============  ======  ==========
  Na Francis Dande
  WARATIBU wa Tamasha la Krismasi, Kampuni ya Msama Promotions ya Jijini Dar es Salaam, kwa mara ya kwanza wamesema kuwa watapeleka uhondo wa tamasha hilo katika mji wa Zanzibar.  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo linalotarajiwa kutikisa kwa mara ya kwanza katika mji wa Zanzibar, Alex Msama alisema kuwa mbali ya Zanzibar, mkoa mwingine ambao umeongezeka ni Tanga.

  Msama aliwataka wakazi wa Zanzibar na vitongoji vyake kuunga mkono kwa kujitokeza kwa wingi katika Tamasha, hilo litakalofanyika kwenye uwanja wa  Mao Tse Tung, ambapo sehemu ya fedha zitapelekwa katika kusaidia kuwalipia ada watoto yatima wa Tanzania Bara na Zanzibar.
  Hivyo, Msama aliwataka Wazanzibar kufika kwa wingi katika tamasha hilo ili kufanikisha malengo hayo, kama alivosisitiza kwa wakasi wa mikoa yote ambayo tamasha hilo litarindima.

  Katika kufanikisha mpango huo, Msama ambaye ni Mkurugenzi pia wa Msama Promotions, ametoa wito kwa wapenzi, mashabiki, wadau na wapendwa katika Kristo Yesu, wajitahidi kumuunga mkono kwa kufika kwenye Tamasha hilo litakalozinduliwa rasmi Desemba 25 jijini Dar es Salaa, kisha kufanyika katika mikoa saba.

  Alisema baada ya Dar es Salaam, litahamia mkoani Morogoro Desema 26 kabla ya kwenda Moshi, Desemba 28 kisha kuvamia jiji la Arusha  Desemba 29, na mjini Dodoma, mikoa mingine ni Tabora, Tanga, Mbeya na Mwanza.
  Alisema mbali ya malengo mengine, pia tamasha la hilo litakuwa na ujumbe wa kuhimiza amani  nchini chini ya kaulimbiu ya ‘Tuilinde na Kuidumisha Amani Yetu.’

  Kwa upande wa waimbaji watakaopamba tamasha hilo la kimataifa, ni kutoka Afrika Kusini, Nigeria, Zambia, DRC Congo, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na wenyeji Tanzania.

  Msama alisema kuwa maandalizi yote kuhusiana na tamasha hilo yanakwenda vizuri na kuwataka watu wajitoleze kwa wingi kupata ujumbe wa Neno la Mungu kwa njia ya sauti za waimbaji mahiri waliojitoa kumtumikia Mungu kwa njia hiyo. 


  0 0

  Sekretarieti kuu ya CCM,ikiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (pichani kati),Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt Asharose Migiro (kulia) pamoja na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye wakiwapungia wakazi mbalimbali waliofika kuwalaki mapema leo walipokuwa wakiwasili kwenye Bandari mpya ya Kiwila Wilayani Kyela Mkoani Mbeya, kwa ziara ya kikazi,wakitokea wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma kwa meli. 
   Pichani shoto ni Nahodha Mkuu wa Meli ya Mv Songea akitoa maelezo mafupi namna ya moja ya chombo cha meli kinavyofanya wakati ikisafiri majini, kwa Sekretarieti kuu ya CCM,ikiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC,siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt Asharose Migiro pamoja na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye mapema leo walipokuwa wakienda Wilayani Kyela Mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi,wakitokea wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma kwa meli.Pichani kulia ni Nahodha msaidizi wa Meli ya Mv Songea.Conrad Shauritanga akiongoza meli hiyo.
  Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt Asharose Migiro akiuliza jambo kwa Manahodha wa meli hiyo wakati ikiwa safarini kuelekea Wilayani Kyela Mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi,wakitokea wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma kwa meli.
   Mbunge wa jimbo la Kyela na Waziri wa Uchukuzi,Dkt Harrison Mwakyembe akimlaki kwa furaha kubwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake walipowasili mapema leo  kwenye Bandari mpya ya Kiwila, Wilayani Kyela Mkoani Mbeya, kwa ziara ya kikazi,wakitokea wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma kwa meli. 
  Mbunge wa jimbo la Rungwe Magharibi,Mh.David Mwakyusa akimlaki  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake waliowasilia mapema leo  kwenye Bandari mpya ya Kiwila Wilayani Kyela Mkoani Mbeya, kwa ziara ya kikazi,wakitokea wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma kwa meli. Pichani kati ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mbeya (CCM),Dkt Mary Mwanjelwa akishuhudia tukia hilo
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakipokelewa na Mwenyekiti Mkoa wa Mbeya,Bwa. Godfrey Zambi wakati wakishuka ndani ya meli ya Mv Songea mapema leo  kwenye Bandari mpya ya Kiwila, Wilayani Kyela Mkoani Mbeya, kwa ziara ya kikazi,wakitokea wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma. 
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na baadhi ya wanachama wa CCM waliofika kumlaki na ujumbe wake mara baada ya kupokelewa vyema katika  kwenye Bandari mpya ya Kiwila, Wilayani Kyela Mkoani Mbeya, kwa ziara ya kikazi,wakitokea wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma. 
    Mbunge wa jimbo la Kyela na Waziri wa Uchukuzi,Dkt Harrison Mwakyembe akitoa ufafanuzi  kwa Katibu Mkuu wa  CCM,Ndugu Kinana kuhusiana na kivuko cha Tungi ambacho kwa sasa hakifanyi kazi .Kinana na ujumbe wake tayari amewasili leo kwa meli ya Mv.Songea Wilayani Kyela mkoani Mbeya akitokea Wilayani Nyasa mkoani Ruvuma 
   Sehemu ya kivuko cha Tungi ambachao hakitumiki kwa sasa mara baada ya kujaa mchanga,kwa sasa hakitumiki tena kama kionekanavyo pichani mapema leo.
  "UMOJA NI USHINDI".! Mbunge wa jimbo la Songwe Mh.Phillip Mulugo, Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mbeya (CCM),Dkt Mary Mwanjelwa Mbunge wa jimbo la Kyela na Waziri wa Uchukuzi,Dkt Harrison Mwakyembe wakiwa wameshikana mikono kwa pamoja mara baada ya kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake

  0 0

  Mbunge wa Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo,wakati akitoa taarifa yake ya kuhusu kuvuliwa nyadhifa mbalimbali ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na aliekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Dkt. Kitika Mkumbo (kushoto),kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.
  Aliekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Dkt. Kitika Mkumbo akizungumza.
  Zitto Kabwe (kulia) na Dk. Kitilla Mkumbo, wakisikiliza kwa makini maswali yaliyokuwa yakiulizwa na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo.
   Sehemu ya Waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali wakiwa kwenye Mkutano huo,uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam leo.

  Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo wakiingia Ukumbini katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam,kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa habari.
  Zitto Kabwe, akiagana na baadhi ya waandishi wa habari wakati akiondoka ukumbini.

  Na Ripota wetu, Dar es Salaam.

  MBUNGE wa Chadema na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe amesema hawezi kufanya maamuzi magumu ya kutaka kujitoa ndani ya chama hicho kwa kile kilichotokea ndani ya chama hicho hivi karibuni. Amesema yeye atakuwa wa mwisho kutoka Chadema na si vinginevyo,kama wanavyofikiria watu wengine.

  Zitto ameyatoa maneno hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,wakati alikizungumzia maamuzi ya Kamati Kuu ya Chadema ya kumvua nafasi zake zote za uongozi yeye pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho Dk. Kitilla Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa  Arusha,Samson Mwigamba.

  Zitto amekana kabisa kuhusika na wala kuujua waraka wa siri ambao ndiyo uliosababisha kumvua madaraka baada ya uamuzi wa Kamati Kuu ya chama kuunasa waraka huo.

  "Mimi nimeusikia ule waraka kwa mara ya kwanza kwenye Kamati Kuu na nilisikitika sana kwanini haukunifikia haraka kwani ningeanza kutekeleza mara moja." alisema Zitto akizungumza.

  Zitto aliendelea kusema "Huenda leo watu walitegemea nitafanya maamuzi magumu ya kuondoka kwenye chama; "Mimi bado ni mwanachama wa Chadema na nitakaekuwa wa mwisho kutoka kwenye chama hiki kwa hiyari yangu, nitafanya taratibu zote za chama kuhitimisha jambo hili mimi sitoki ng'o kwenye chama hiki labda wanitoe wao," alisema Zitto.

  Zitto alisema anaumia sana anapotuhumiwa kwa kuwa yeye ni binadamu. "...ninapotuhumiwa naumia ninapoambiwa nahujumu chama hiki naumia kwa kuwa nakipenda chama na nimekitumikia muda mrefu. Aidha aliwataka viongozi wa Chadema kuacha siasa za uzushi ili kujenga chama imara na kuwakomboa Watanzania.

  "...Sisemi kama mimi sina makosa,kwani mimi ni binadamu na nimefanya mambo mengi kwa chama changu, lakini kinachoendelea kwa sasa ndani ya chama chetu ni mapambano ya kukuza demokrasia na ni mapambano ya wanaotaka mabadiliko na wasiopenda mabadiliko ndani ya chama...mapambano ya wawajibikaji na wasiopenda kuwajibika ni mapambano ya wanaopenda demokrasia na wanaokwaza demokrasia." alisema Zitto huku akionesha kusikitishwa.

  TAARIFA YA MH. ZITTO KABWE
  TAARIFA YA DKT. KITILA MKUMBO

  0 0


  Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka kulia akigawa sabuni za Twiga Soup ambayo nayo inasambazwa na kampuni hiyo kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam mwishoni mwa wiki ilyopita kampuni hiyo imetoa sabuni na baadhi ya nguo kwa watoto hawo
  Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka kushoto akimkabidhi sabuni aina ya Twiga  inayosambazwa na kampuni hiyo kwa Aisha Omari anaelelewa katika kituo cha Shule ya Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita
  Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka kushoto akimkabidhi sabuni aina ya Twiga  inayosambazwa na kampuni hiyo kwa Aisha Omari anaelelewa katika kituo cha Shule ya Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita
  Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka kushoto akimkabidhi sabuni aina ya Twiga  inayosambazwa na kampuni hiyo kwa Nassoro Hamisi kulia wengine ni Omari Saiki na Ramadhani Rashidi wanaolelewa katika kituo cha Shule ya Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita     

  Na Mwandishi Wetu.

  KAMPUNI ya usambazaji wa Filamu nchini Tanzania na bidhaa mbalimbali ya DJ Marketeng and promosheni chini ya mkulugenzi wake Daniel Haule mwishoni mwa wiki iliyopita walitoa msaada wa sabuni ya  unga ya Twiga  ambayo wanazisambaza  na kuwapatia  watoto wanaoishi katika mazingira magumu wa kituo cha Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam zawadi ya sabuni hizo

  mbali na sabuni hizo za twiga walitoa na baadhi ya nguo kwa watoto wanaoishi hapo mkurugrnzi huyo ambaye amewaomba watu mbalimbali kusaidi watu wenye maitaji maalumu kama hawo ambao wengine ni walemavu wa macho

  akielezea historia yake Haule ambaye ni mkurugenzi kwa sasa amesema unajua mie nimelelewa katika mazingila magumu sana kifupi mimi ni mtoto wa mtaani ambapo maisha mengi nimeishi kwenye mitaa nikiwa nalala nje
  hivyo nimefutika katika kidogo nilicho nacho leo nakula na wenzangu naomba watu wawe na moyo wa kujitoa ili kusaidia maisha ya watoto hawa ili waonge mbele

  nae Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka amesema huu ni mwanzo tu wa kujenga mahusiano hivyo tunajipanga ili mradi kila wakati tuwe tunawakumbuka mana maisha haya awajajitakia bali ni mungu ndie muweza wa kila jambo
  Kampuni hiyo ambayo kwa sasa inatamba na filamu zake mbili za Dasmila na Trouble Make ambazo zimeshirikisha wasanii mbalimbali wanaotamba katika tasnia hiyo

  0 0


  Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka kulia akigawa sabuni za Twiga Soup ambayo nayo inasambazwa na kampuni hiyo kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam mwishoni mwa wiki ilyopita kampuni hiyo imetoa sabuni na baadhi ya nguo kwa watoto hawo
  Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka kushoto akimkabidhi sabuni aina ya Twiga  inayosambazwa na kampuni hiyo kwa Aisha Omari anaelelewa katika kituo cha Shule ya Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita
  Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka kushoto akimkabidhi sabuni aina ya Twiga  inayosambazwa na kampuni hiyo kwa Aisha Omari anaelelewa katika kituo cha Shule ya Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita
  Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka kushoto akimkabidhi sabuni aina ya Twiga  inayosambazwa na kampuni hiyo kwa Nassoro Hamisi kulia wengine ni Omari Saiki na Ramadhani Rashidi wanaolelewa katika kituo cha Shule ya Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita     

  Na Mwandishi Wetu.

  KAMPUNI ya usambazaji wa Filamu nchini Tanzania na bidhaa mbalimbali ya DJ Marketeng and promosheni chini ya mkulugenzi wake Daniel Haule mwishoni mwa wiki iliyopita walitoa msaada wa sabuni ya  unga ya Twiga  ambayo wanazisambaza  na kuwapatia  watoto wanaoishi katika mazingira magumu wa kituo cha Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam zawadi ya sabuni hizo

  mbali na sabuni hizo za twiga walitoa na baadhi ya nguo kwa watoto wanaoishi hapo mkurugrnzi huyo ambaye amewaomba watu mbalimbali kusaidi watu wenye maitaji maalumu kama hawo ambao wengine ni walemavu wa macho

  akielezea historia yake Haule ambaye ni mkurugenzi kwa sasa amesema unajua mie nimelelewa katika mazingila magumu sana kifupi mimi ni mtoto wa mtaani ambapo maisha mengi nimeishi kwenye mitaa nikiwa nalala nje
  hivyo nimefutika katika kidogo nilicho nacho leo nakula na wenzangu naomba watu wawe na moyo wa kujitoa ili kusaidia maisha ya watoto hawa ili waonge mbele

  nae Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka amesema huu ni mwanzo tu wa kujenga mahusiano hivyo tunajipanga ili mradi kila wakati tuwe tunawakumbuka mana maisha haya awajajitakia bali ni mungu ndie muweza wa kila jambo
  Kampuni hiyo ambayo kwa sasa inatamba na filamu zake mbili za Dasmila na Trouble Make ambazo zimeshirikisha wasanii mbalimbali wanaotamba katika tasnia hiyo

  0 0

  .Watanzania watakiwa kujitokeza kwa wingi kumtukuza Mungu

  WAKATI maandalizi ya Tamasha la Krismas yakipamba moto, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mizengo Kayanza Peter Pinda amesema wazo la kuanzishwa kwa Tamasha la Krismas ni zuri lenye lengo la kuwakutanisha Watanzania mahali pamoja kuabudu na kuliombea Taifa lao dhidi ya mabalaa yanayoitesa dunia likiwemo suala la ugaidi, utekwaji wa viongozi na kuteswa kwa Watanzania.

  Waziri Mkuu Pinda ambaye ni maarufu kama mtoto wa Mkulima anasema kwamba Tamasha hilo ni zuri na litakata kiu ya mashabiki wa Muziki wa Injili nchini tanzania kwa sababu linawakutanisha kwenye uwanja mmoja waumini wa madhehebu mbalimbali.

  Waziri Mkuu anasema tamasha hilo ambalo wazo la Muandaaji maarufu wa Matamasha ya Injili nchini, Alex Msama linapewa baraka zote kwa niaba ya serikali kwa kuwa lengo lake kuu ni kuwafanya Watanzania kuwa na hofu ya Mungu katika maisha yao yote wanayoishi hapa duniani.

  “Mimi kama mwakilishi wa Serikali, kwa niaba ya serikali yangu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, natoa Baraka zote kwa Tamasha hili na ninaomba lifanyike kwa amani na utulivu ili lengo  la kuanzishwa kwake litimie,” anasema Pinda. Mbali ya Waziri Mkuu , Pinda baadhi ya  Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameiunga mkono kauli ya Waziri Mkuu inayowataka Watanzania kujitokeza kwa wingi katika Tamasha hilo la Krismas.

  Lengo la kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo maaskofu, wanasiasa na watu maarufu ambao wanaweza kulizungumzia ipasavyo Tamasha hilo ambalo lina nia ya dhati ya kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa njia ya muziki  kwa Jamii yote ya Watanzania. Mbunge wa Viti Maalum (CCM)  Mkoa wa  Mbeya Mary Mwanjelwa amesema Tamasha la Krismas ni ubunifu ambao umekwenda mbali zaidi kwa kueleza kwamba ni jambo la ubunifu kwa sababu Msama ameona kwamba kiu ya waumini haijakatwa hadi alipoamua kuandaa muendelezo wa Tamasha pendwa la Pasaka.

  Mwanjelwa anasema lengo la Tamasha hilo ni mkusanyiko wa watu wa aina mbalimbali ambao wanakusanyika kwa ajili ya kusahau yale yote mabaya ambayo yana dhamira ya kupoteza taswira ya Tanzania ambayo ni kitovu cha amani.

  Dhamira hiyo inatokana na sababu kwamba Tamasha hilo ni la Kijamii zaidi na pia ni takatifu kwani linashirikisha waimbaji na wadau mbalimbali wa Kimataifa ambao wanakutana kwa lengo la kuondosha tofauti zenye kuashiria uvunjifu wa amani.

  Mwanjelwa anasema ujio wa waimbaji mbalimbali kutoka nje ya Tanzania kunachangia kukusanya wananchi kutoka nchi mbalimbali ambao hujitokeza kwa ajili ya kupata neno la Mungu na kuburudika, mikusanyiko hii pia huondoa ubaguzi wa nchi kwa nchi. Mbunge huyo anasema kutokana na mipangilio ya kuigwa inayofanywa na Msama, Serikali inatakiwa kuchangia nguvu zake katika kufanikisha mikakati inayofanywa na Msama kwani mikusanyiko ya Amani kama hii ni muhimu sana kwa utengamano wa Taifa na bara letu la Afrika.

  “Serikali inatakiwa kumuongezea nguvu Msama kwa anayoyafanya, anawaunganisha watu wa mataifa mengi kwa lengo la kumtukuza  Mungu na kutoa michango yao kuwasaidia wanaoishi katika mazingira hatarishi,” alisema Mwanjelwa.  Mbunge wa Igalula (CCM), Athumani Mfutakamba anasema Tamasha hilo linaleta mshikamano, upendo pia linaunganisha waumini wa  imani tofauti  katika mikusanyiko ya kumwabudu Mungu.      

  “Kwa sababu waumini mbalimbali watapata elimu na burudani,ambayo itazidisha  upendo amani na  mshikamano miongoni mwao kama viumbe wa mwenyezi Mungu, aliwataka waumini wa dini zote wajiandae kwa ajili ya Tamasha hilo ambalo ni la aina yake. Mfutakamba alisema kwamba upendo huo na amani vitakavyotangazwa  kwenye mikoa yote litakapofanyika Tamasha hilo, waumini wajiandae vilivyo na Tamasha hilo ikiwa ni pamoja na kupata maonyo ya Mwenyezi Mungu kupitia Injili.

  Mfutakamba anasema hatua ya kuandaliwa kwa Tamasha hilo kunatokana na sababu kwamba dhamira ya dhati ya waasisi wa nchi hii waliweka sheria na haki ya kuabudu, kukusanyika  na kwenda kokote utakako pasi na kuvunja sheria.   
    
   Naye Mbunge wa Newala, Kapteni, Geroge Mkuchika amesema ni jambo la kheri kwa waandaaji wa Tamasha hilo kulifanikisha kwa sababu linakusanya waumini mbalimbali. Mkuchika anasema Tamasha hilo ni muhimu kwa Watanzania kwa sababu linazungumzia zaidi masuala ya amani, hivyo waumini wa dini mbalimbali linawahusu,alisema wadau wote wa muziki wa Injili wajitokeze kwa wingi siku hiyo uwanja wa Taifa kwa upande wa Dar es salaam na mikoa yote ambako matamasha yatafanyika.

  Mkurugenzi wa Msama Promotions ambaye ni muandaaji wa Tamasha hilo, Alex Msama anapongeza jitihada za Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao wanatambua mchango wake katika kufikisha ujumbe kwa jamii kupitia muziki wa injili  na mapambio.

  Msama anasema Tamasha hilo linalotarajia kufanyika kwenye mikoa mitano, Desemba 25 litafanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam siku inayofuata litahamia Morogoro, Dodoma, Tanga na Arusha.

  “Wadau wa Dar es Salaam na mikoani wakae mkao wa kula kwa sababu nimejiandaa vilivyo kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa kishindo, natarajia kushirikisha waimbaji wa nchi mbalimbali ambao wataimba ‘live’,” alisema Msama na kuongeza. “Tamasha la Krismas litazungumzia Amani zaidi baada ya matukio kadhaa ambayo yanatishia maisha, hali ambayo haimfurahishi Mwenyezi Mungu,” alisema Msama.

  Msama anasema Tamasha la Krismas litashirikisha waimbaji mbalimbali wa Tanzania na kutoka nje ya Tanzania, mfumo wa waimbaji utakuwa ni wa kuimba live tofauti na ilivyokuwa katika matamasha yaliyopita. Aidha Msama anawataja waimbaji waliothibitisha kushiriki katika Tamasha hilo ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro (Tanzania), Ephreim Sekereti (Zambia) na Solomon Mukubwa (Kenya).

  Msama anamalizia kwa kueleza kwamba, fedha zitakazopatikana kwenye Tamasha hilo zitasaidia ujenzi wa kituo cha wenye uhitaji maalum kama Yatima, wajane na wanaoishi katika mazingira hatarishi kinachotarajia kujengwa Pungu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Ipinda wilayani Kyela kwenye mkutano wa hadhara ambao ndio mkutano wake wa kwanza kama Katibu Mkuu wa CCM lakini pia ndio siku aliyowasili akitokea Ruvuma .
   Katibu wa NEC Siasa na Mahusiano ya Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimu wakazi wa Ipinda wilaya ya Mbeya na kuwasihi wakina mama wawe mstari wa mbele kuhakikisha mabinti zao wanapata elimu.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Ipinda na kuwaeleza mambo muhimu ya kutafakari kabla hawjakurukupia siasa na baadhi ya vyama vingi vipo kwenye mfumo na utawala binafsi.
   Mbunge wa Kyela Dk. Harisson Mwakyembe akihutubia wakazi Ipinda wa kwenye mkutano wa hadhara ambao mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amekaa Nyumbani kwa Balozi wa Nyumba 10 Ndugu Menas Ndoma .

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza  na Wananchi wa Shina namba 1 kata ya Walema,alipokwemda kumtembelea Balozi Menas Ndoma.

  Wananchi wa Shina namba 1kata ya Walema wakishangilia salaam za Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuja kumtembelea Balozi Menas Ndoma wa kata ya walema.

  0 0  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi mbalimbali wa chama hicho mara baada ya kuwasili mpakani mwa Wilaya ya Kyela na Rungwe mapema leo asubuhi,wakati ujumbe huo ulipokuwa ukiwasili wilayani Rugwe kwa ziara ya siku 11 ndani ya mkoa wa Mbeya.pichani shoto sambamba ni Katibu wa NEC,Itikasi na Uenezi ,Nape Nnauye akisalimiana na wanachama wa CCM.
  Kada Maarufu wa CCM,Bwa. Richard kasesela akisalimiana na Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro mara baada ya kuwasili mpakani mwa Wilaya ya Kyela na Rungwe mapema leo asubuhi,wakati ujumbe huo ulipokuwa ukiwasili wilayani Rugwe kwa ziara ya siku 11 ndani ya mkoa wa Mbeya.pichani shoto sambamba ni Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi ,Nape Nnauye akisalimiana na wanachama wa CCM.
  "Karibu sana nyumbani Kaka Nape"...Kada Maarufu wa CCM,Bwa. Richard kasesela akisalimiana  Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi ,Nape Nnauye
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake (haupo pichani) akizungumza na Wajumbe Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ndani ya ukumbi wa Halmashauri kuu ya Rungwe mapema leo.
  Msafara wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana na Ujumbe wake ukipokelewa mpakani mwa Wilaya ya Kyela na Rungwe mapema leo asubuhi,wakati ujumbe huo ulipokuwa ukiwasili wilayani Rugwe kwa ziara ya siku 11 ndani ya mkoa wa Mbeya.

  0 0

  Screen Shot 2013-11-25 at 6.40.09 AM
  Mwezi Novemba ni mwezi wa ugonjwa wa Kisukari ( diabetes) Kwa mujibu wa kalenda ya afya , Kwa kuzingatia Hilo hospitali ya Doctors plaza (MOROCO BRANCH ) ikishirikiana na Lancet Laboratories tuna punguzo la vipimo kwa wataopenda kufanya check up ya ugonjwa wa kisukari. Kuanzia Novemba 30 hadi Desemba 7

  0 0

  Karibu ule nyama ya bata... Special Bata choma iliyoandaliwa kwa utaalam wa hali ya juu
  Njoo na rafiki zako mle bata kwelikweli... Usingoje kusimuliwa
  NB: Bata hauzwi vipande vipande... anauzwa full so make sure you have a company otherwise itabidi ubebe T/Away..
  See you all there... The 1st Ever BATA Experience in town...
  Date: Saturday 30th November 2013
  Venue: GMB Executive - Mbezi Beach (Njia ya chini opp. njia panda ya kwenda Mediteranneo)
  Time: From 4PM
  For more Details please contact me on +255 784 55 77 55

older | 1 | .... | 172 | 173 | (Page 174) | 175 | 176 | .... | 1896 | newer