Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

Lowassa asaidia Maendeleo ya Elimu katika Tarafa ya Mbagala,jijini Dar

0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikamilisha ahadi yake ya kuchangia Elimu kwa Shule za Sekondari Mbagala,kwa kumkabidhi Mchango wake wa Sh. Mil. 10,Mkuu wa Shule ya Sekondari Mbagala,Mwl. Marcelina Kimario (wa tatu kulia).Wengine pichani ni Walimu wa Shule mbali mbali za Sekondari zilizopo kwenye Tarafa ya Mbagala.Makabidhiano hayo yamefanyika leo ofisini kwake,Mwenge jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Mbagala,Mwl. Marcelina Kimario (aliesimama) akisoma taarifa fupi ya namna walivyoweza kuiendesha harambee ya kuchangia Maendeleo ya Elimu katika Tarafa ya Mbagala,iliyofanyika majuma kadhaa yaliyopita.wakati walipofika Ofisini kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa,kuwasilisha taarifa hiyo leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea taarifa hiyo kutoka kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Mbagala,Mwl. Marcelina Kimario.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na walimu hao mara baada ya kuwakabidhi mchango wake leo,Ofisini kwake.
Baadhi ya wakuu wa Shule mbali mbali za Sekondari katika Tarafa ya Mbagala jijini Dar es Salaam,wakimsikiliza Mh. Lowassa.

VIONGOZI WA DINI NCHINI WAJITOKEZA KUSHIRIKIANA NA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KATIKA UHIFADHI

0
0
picha ya pamoja ya viongozi wa dini pamoja na menejimenti ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe Balozi Hamis Kagasheki (katikati) akisisitiza jambo wakati wa mkutano na viongozi wa dini mbali mbali waliofika leo Ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Bw. Gesimba, kulia ni Mkurugenzi wa Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania, Bi. Devotha Mdachi.
Mhe Balozi Kagasheki akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa kamati ya Viongozi wa dini, Askofu Munga wa KKKT.

Viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali nchini, leo wamekutana na Waziri Khamis Kagasheki pamoja na timu ya menejimenti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kujadili nafasi ya viongozi wa dini katika kuhamasisha uhifadhi wa maliasili nchini.

Akiwakaribisha viongozi hao wa dini, Mhe Balozi Kagasheki amesifu uamuzi waliochukua wa kutambua umuhimu wao katika kubadilisha mitazamo ya wananchi kupitia mafundisho ya dini.

Askofu Munga wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ambaye ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa viongozi wa dini waliotembelea ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii alisema wameona umuhimu wa kujumuika pamoja na Serikali katika kulinda rasilimali za maliasili. 

Aidha alisisitiza kuwa viongozi wa dini wana jukumu kubwa la kushiriki katika vita dhidi ya ujangili kwani katika historia ya uumbaji, viumbe wote ni  sawa na hamna mwenye dhamana ya kutoa uhai wa kiumbe kingine bila utaratibu maalum.

Katika hotuba yake, Askofu Munga alisema suala la uhifadhi linahitaji  ushirikiano baina ya serikali na sekta nyingine. Hivyo, viongozi wa dini wako kwenye nafasi nzuri ya kutoa elimu ya uhifadhi kwa waumini wao. 

Alitoa rai ya kuunda mkakati utakaowezesha Wizara na Viongozi wa dini kubadilishana mawazo na elimu juu ya uhifadhi ili waumini wote waweze kupata elimu hiyo na hivyo kupunguza vitendo vya ujangili vinavyoendelea nchini.

Askofu Paul Shemsanga mwakilishi wa madhehebu ya Pentekosti naye aliongeza kuwa viongozi wa dini wana uwezo wa kubadili mitazamo na mawazo ya waumini wao kwa kuzingatia maadili ya kidini wanayofundishwa, jambo ambalo ni muhimu katika kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za uhifadhi.

Mhe Balozi Khamis Kagasheki alisema elimu ya uhifadhi ni muhimu kwa wananchi na aliwashukuru sana viongozi wa dini kwa kujitolea kusaidia katika hilo. Vilevile alisema sheria mbalimbali za uhifadhi zilizotungwa hazijitoshelezi iwapo wananchi ambao ndio walengwa hawazifahamu, hivyo kupitia viongozi wa dini na mikakati itakayoundwa, elimu ya sheria itawafikia wananchi wengi nchini.


Wizara ya Maliasili na Utalii imeridhia kuteua wajumbe watakaoungana na wajumbe kutoka kamati ya viongozi wa dini ili kupata timu itakayohusika na shughuli ya kuhakikisha ushirikiano wa elimu ya uhifadhi unafanyika baina ya pande hizo mbili.

MAADHIMISHO YA SIKU YA TAKWIMU AFRIKA YAFANYIKA LEO JIJINI DAR

0
0
Naibu Waziri wa Fedha Bi. Saada Mkuya akizungumza na wadau wa sekta mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika leo jijini Dar es salaam.
Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi nchini Thobias Andengenye ambaye alikuwa miongoni mwa wachangiaji wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini kuhusu mchango wa takwimu katika kufanikisha majukumu ya Jeshi la Polisi nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza kabla ya ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika. Amesema kuwa Ofisi yake pamoja na majukumu mengine inaendelea kuhimiza matumizi ya takwimu kutoka katika vyanzo sahihi kwa mipango ya maendeleo.
Muimbaji maarufu nchini Tanzania Bi. Stara Thomas akiwasilisha ujumbe kwa njia ya uimbaji kuhusu umuhimu wa matumizi ya Takwimu katika kupanga mipango ya Maendeleo leo jijini Dar es salaam.
Sehemu ya washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa leo jijini Dar es salaam.

GURUMO KUAGWA NA WASANII LUKUKI NDANI YA TCC CLUB DESEMBA 14, 2013

0
0
BENDI za Twanga Pepeta, Msondo Ngoma na wanamuziki kibao kutoka Sikinde ni sehemu ya wasanii watakaosindikiza tamasha kubwa la Gurumo 53 litakalofanyika mwezi huu.

Tamasha hilo ambalo ni mahsusi kwa ajili ya kumuaga mwimbaji mkongwe Muhidi Maalim Gurumo (pichani) litafanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe Jumamosi Desemba  14, 2013.

Kwa mujibu wa kamati ya watu sita inayoratibu tamasha hilo, Gurumo anaagwa baada ya kutangaza rasmi kuachana na muziki wa jukwaani baada ya kudumu kwenye kazi hiyo kwa miaka 53.



Mratibu wa kamati hiyo Juma Mbizo amesema kutakuwa pia na wasanii wa bongo fleva, vichekesho na sarakasi. Aidha Mbizo amesema tamasha litatanguliwa na bonanza la soka la maveterani.

Hadi kustaafu kwake Gurumo aliyezitumikia pia bendi za Kilimanjaro Chacha,Rufiji Jazz, Kilwa Jazz, Sikinde na OSS – Ndekule, alikuwa ni kiongozi na mmoja wa wamiliki wa Msondo Ngoma ambayo hapo awali ilijulikana kwa majina ya NUTTA, Juwata na OTTU. Gurumo ameitumika Msondo katika majina yote ya nyuma.



Wasanii waliowahi kuitumikia Sikinde ambao watakuwepo kumsindikiza Gurumo ni pamoja na Cosmas Chidumule, Abdallah Gama, Hussein Jumbe, Mashaka Shaaban, Kalamazoo, Henry Mkanyia na Karama Legesu. Wengine ni Ali Yahaya na Boniface Kachala, Benno Villa Anton, Tshimanga Kalala Assossa na Ibrahim Mwinchande.



Baadhi ya wasanii wengine watakaotumbuiza ni Komandoo Hamza Kalala, Kassim Mapili, Hafsa Kazinja na Waziri Ali.


Kamati ya Gurumo iko chini ya uenyekiti wa Asha Baraka, makamu ni Waziri Ali na katibu ni Said Mdoe huku mratibu akiwa Juma Mbizo, wajumbe ni Said Kibiriti na Richardson Sakala. 

PPF KUYAFIKISHA MAHAKAMANI BAADHI YA MAKAMPUNI YA ULINZI.

0
0
MFUKO wa Pesheni wa PPF Kanda ya Ziwa imeyaonya baadhi ya Makampuni mbalimbali yakiwemo ya Ulinzi kwa tabia na mazoea ya kuwaandikisha wafanyakazi wao na kushindwa kuwasilisha michango yao hali inayopelekea wafanyakazi kuangaika kupata fedha za michango waliyokuwa wakikatwa na kuchangiwa na waajiri wao mara wanapotoka katika ajira.


Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Meshack Bandawe Meneja wa Kanda ya Ziwa (PPF) alipokuwa mgeni rasmi wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya askari wa ulinzi 35 waliohitimu kati ya 40 Kampuni ya K.K Security walioanza mafunzo hayo kwenye uwanja mkongwe wa michezo wa Nyamagana jijini Mwanza. (ZAIDI BOFYA PLAY KUMSIKILIZA )

Bandawe alisema kuwa Kampuni ya K. K Security imekuwa ikithamini shughuli za Mfuko wa Pesheni wa PPF kama mdau muhimu katika sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa manufaa ya mwajiri na wafanyakazi kwa ujumla katika kuwakinga na majanga mbalimbali wawapo katika ajira ama nje ya ajira.



Mkurugenzi huyo, alisema kwamba PPF imedhamilia kutoa huduma bora kwa makampuni yanayo wasilisha michango yao kwa wakati huku baadhi ya makampuni yanayoshindwa kufanya hivyo yatachukuliwa hatua kali za kisheria ili kulinda maslahi ya wafanyakazi na katika kutekeleza hilo tayari Mfuko wa PPF umekwisha yafungulia kesi Mahakamani baadhi ya makampuni ya ulinzi yaliyoshindwa kutimiza wajibu wao.


Bandawe alisema kwamba baadhi ya makapuni yamekuwa yakikumbwa na changamoto kubwa na kuibuka migogoro na wafanyakazi wao kutokana na kuwalipa mishahara midogo , lakini mbaya zaidi mishahara hiyo midogo hailipwi kwa muda na wakati hali hiyo inawafanya baadhi ya wafanyakazi wamekuwa na maisha ya shida na familia zao huku wakikabiliwa kufanya kazi katika mazingira magumu.


Mkurugenzi huyo aliipongeza Kampuni ya ulinzi ya K.K.S kuwa mfano wa kuigwa na makapuni mengine nchini ambapo kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kuwa kampuni hiyo inajumla ya wafanyakazi 6285 walioandikishwa katika mfuko wa pesheni wa PPF na huwasilisha michango yao isiyopungua kiasi cha shilingi milioni 267,771,967.00 kila mwezi katika ofisi mbalimbali za PPF katika Kanda zote nchini.


Ukaguzi wa parade.
“Mwaka huu 2013 mmeandikisha askari wapya wa ulinzi 533 hongereni, PPF inapenda kuwahakikishia huduma bora ya mafao mbalimbali ikiwemo kulipwa mafao yenu kwa muda wa siku saba mara baada ya kutoka katika ajira huku PPF ndio Mfuko pekee unaotoa fao la elimu  kwa wanachama wake kwa kusomesha watoto wasiozidi wane kuanzia shule ya awali hadi kidato cha sita ikitokea mwanachama amefariki” alisema na kuongeza kuwa.


PPF itaendelea kutoa mikopo ya gharama nafuu kupitia SACOSS zilizopo kwenye sehemu za kazi pamoja na kushiriki katika ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazokopeshwa kwa wanachama wake ili kuwawezesha kumiliki nyumba kabla ya kustaafu, PPF pia inawasii wafanyakazi wapya watakaoajiriwa na makampuni na taasisi katika sekta ya umma , serikali kuu, serikali za mitaa, binafisi na zisizo za kiserikali na isiyo rasmi kujiunga wapate mafao bora na huduma bora zinazotolewa na Mfuko huo.

Kakakamavu wa wahitimu.


Mguu sawa.

Attention..!
Namna ya kujilinda.
Meza kuu ya wadau wa PPF na KK Security Mwanza.
Kwa umakini yanayojiri uwanjani kutoka jukwaa kuu.
Parade likitoa heshima kwa jukwaa kuu.
Naye Meneja wa Tawi la Mwanza wa Kampuni ya K.K.S Bi. Levina Beal (pichani) alisema kuwa kutokana na askari walioajiriwa kukubali kukatwa asilimia 10 ya mishahara yao kumesaidia wao kupeleka michango ya asilimia 10 kama mwaajiri kutokana na sheria za mfuko huo zinavyoelekeza kwa wakati ili kuondoa malalamiko yanayojitokeza baada ya wafanyakazi kuacha au kutoka kazini ili kukwepa malimbikizo jambo ambalo wamekuwa wakilitekeleza kila mwezi. (ZAIDI BOFYA PLAY KUMSIKILIZA)


Beal alisema kuwa kutokana na Kampuni yake kuwekeza katika sekta ya ulinzi imeamua kutenga fedha kwa ajili ya kugharamia mafunzo kwa askari wake inaowaajiri ili kuwa na weledi wa ulinzi wenye kiwango kinachokubalika ikizingatiwa kuwa Jeshi la Polisi pekee haliwezi kumudu kufika kila mahali kuweka ulinzi na badala yake sekta binafisi imekuwa mdau wa kutoa ulinzi kwenye makampuni, taasisi za umma, mashirika ya umma na yasiyo ya serikali na watu binafisi hapa nchini.

KINANA NDANI YA WILAYA YA MBIGA,ASEMA CCM HAIWEZI RUBUNIWA KWA SABABU YA KUPATA KURA

0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  (watatu kushoto) na baadhi ya viongozi katika msafara wake, wakishiriki Nov 20, 2013, kungoa magugu na visiki, kuandaa shamba la mfano la wanawake na vijana wajasiriamali katika kijiji cha cha Mkwaya Kata ya Kilimani wilayani Mbinga mkoani Ruvuma,  alipotembelea shamba hilo lenye ukumbwa wa ekari 500. Mbali na  kushiriki kazi hiyo Kinana alitoa mchango wa kiasi cha shilingi milioni nne kwa ajili ya mafuta ya trekta ya kulimia shamba hilo. Baadhi ya viongozi wengine ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kulia).
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) akikagua mradi wa mgodi wa makaa ya mawe wa kampuni ya Tancoal katika eneo la Mtunduwalo, Mbinga mkoani Ruvuma, Nov 20, 2013. Kinana alitembelea mgodi huo, kufuatia mgogoro uliopo kati ya wananchi na uongozi wa mgodi kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo malipo ya fidia kwa maeneo yalitochukuliwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya kukabidhi pikipiki 50 zilizotolewa na mbunge kwenda kwa watendaji wa vijijini.
Kijana Bonus Hyera wa kijiji cha Lusewa, akimsalimia kwa kumbusu mikono kwa shauku, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, baada ya Dk. Asha-Rose kukutana na kijana huyo, wakati wa shughuli ya uzinduzi wa tawi la CCM Kata ya Mbinga mjini, mkoani Ruvuma, Nov 20, 2013, uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Kijana huyo aliyeonekana kama aliyekuwa amelewa kiasi, alionyesha heshima kubwa kwa Dk. Asha-Rose, tofauti ilivyokuwa inadhaniwa na baadhi ya watu waliopomuona akimsogelea kwa shauku kiongozi huyo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na wanachama wa shina namba 9,katika tawi la Amani Makolo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Aman Makolo waliojitokeza nyumbani kwa Balozi Hilda Komba wa shina namba 9 ,Tawi la Amani Makolo wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma.
 Balozi Hilda Komba wa shina namba 9 Tawi la Amani Makolo akimkaribisha nyumbani kwake Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Wanachama wapya wa Tawi la Amani Makolo wilayani Mbinga wakila Kiapo cha Uanachama wa CCM mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  ambaye leo amefanya ziara katika wilaya ya Mbinga.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na wanachama wa Shina namba 9 Tawi la  Amani Makolo ambapo aliwapongeza kwa ushirikiano na mshikamano waliokuwa nao kiasi wameweza kuwa na wanachama hai 426.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakazi wa kijiji cha Mtundawalo wakati akiwasili kijijini hapo tayari kwa kufanya mkutano wa hadhara.Katika Mkutano wa hadhara Katibu Mkuu wa CCM alizungumzia mipango mbali mbali ya kutatua matatizo ya wananchi na kuwaeleza wananchi CCM haiwezi kurubuniwa  kwa sababu ya kupata kura,akasisitiza wananchi wawe wa kweli kwa serikali ili haki itendeke kwa haraka.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajasiriamali wa Mkwaya kata ya Kilimani ambao kwa pamoja wameamua kujishughulisha na kilimo.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akiwasalimu wakulima wa kata ya Mkwaya .
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia ngoma ya Mganda wakati akiwasili kwenye eneo la mkutano wilayani Mbinga.

 Katibu wa NEC Itikadi na uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mbinga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya michezo Mbinga mjni.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimueleza Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose uzoefu wake wa kuendesha  pikipiki,kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbinga  Ndugu Senyi Ngaga.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Mbinga mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanika kwenye viwanja vya michezo vya Mbinga mjini ambapo aliwaeleza wananchi kuwa chama cha Mapinduzi kitasaidia kutoa ushauri kwa mazao ambayo bei yake inashuka na kupanda.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa Wilaya wa zamani Ndugu Osmund Kapinga.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Mzee Osmund Kapinga Mkuu wa Wilaya mstaafu mara baada ya kukamilika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya michezo  vya Mbinga mjini mkoa wa Ruvuma.

KITUO CHA MSAADA WA MATIBABU KWA NJIA YA DAWA ZA MIMEA.

0
0

Habari  Njema  Sana  Kwa  Wagonjwa  na  Wenye  Kusumbuliwa  na Matatizo  Mbalimbali  Ya  Kiafya. 

Neema  Herbalist    Foundation  Ni  Kituo  Cha   Utafiti  wa  Tiba  Asilia  na   Msaada  Wa  Matibabu kwa   wagonjwa  na  wenye  kusumbuliwa    na  matatizo  mbalimbali  ya  kiafya  wasio  na uwezo  wa kumudu  gharama  kubwa  za  matibabu. Tunapenda  kuwatangazia  watu wote  kuwa , sasa  tunatoa msaada  wa  matibabu kwa  njia  ya    dawa  za  mimea   na  vyakula  lishe  kwa  watu  wanao  kabiliwa  na matatizo  mbalimbali  ya  kiafya  kama  vile
i.                   Presha  na  Kisukari
ii.                 Vidonda  Vya  Tumbo
iii.              Uvimbe  wa  Tumboni  Kwa  Wanawake(Fibroid)
iv.               Tatizo  la  Uzazi  Kwa  Wanawake  na  Wanaume
v.                 Tatizo  la  Ukosefu  wa  Nguvu  Za  Kiume,
vi.               Tatizo  la  Ukosefu  wa  Askhi  Ya  Tendo  La  Ndoa  Kwa  Wanawake
vii.            Kuongeza  CD 4  Kwa  watu  wanaoishi  na  Virusi  Vya  Ukimwi
viii.         Mzio ama  allergy
ix.              Pumu
x.                  Kupunguza  Uzito, Unene  na   KUONDOA  Vitambi 
xi.              Kutengeneza  shape  ya  tumbo  na  kulifanya  kuwa  flat
xii.            Kuondoa  harufu  mbaya  kinywa
xiii.         Matatizo    Yote  Ya  Ngozi
xiv.         Matatizo  Ya  Watoto pamoja  na   matatizo  mengineyo  mengi. GHARAMA   ZA  KUJIUNGA  NA   HUDUMA  HII  NI  RAHISI  SANA ! Tunapatikana  jijini  Dar  Es  Salaam  katika  eneo  la  CHANGANYIKENI  karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU .
xv.            Kwa   maelezo zaidi  wasiliana  nasi  kwa  Simu  namba : 0766538384  Au Tembelea  : www.neemaherbalist.blogspot.com

USIENDELEE   KUTESEKA!  WASILIANA   NASI   LEO,  UPATE  MSAADA  WA MATIBABU  YA  TATIZO  LINALO  KUKABILI.

PSPF YATAMBULISHA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI (PSS) KWA WAANDISHI WA HABARI

0
0
 Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji PSPF ambaye pia ni Meneja wa kumbukumbu, Chacha Nyaikwabe
 Kutoka kushoto ni Afisa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Hawa Kikeke, Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji PSPF ambaye pia ni Meneja wa kumbukumbu, Chacha Nyaikwabe na Frank Mvungi wa Maelezo wakati PSPF ilipozungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa habari maelezo

Waandishi wa habari wakisikiliza ufafanuzi kuhusu mfuko wa pensheni PSPF.




 Kutoka kushoto ni Afisa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Hawa Kikeke, Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji PSPF ambaye pia ni Meneja wa kumbukumbu, Chacha Nyaikwabe
 *********************
Waandishi wa habari nchini wameshauriwa kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSPF Supplementary Scheme PSS) katika Mfuko wa pesheni wa PSPF ili kujiwekea akiba yenye mafao bora na itakayowainua kiuchumi.

Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji PSPF ambaye pia ni Meneja wa kumbukumbu, Chacha Nyaikwabe wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa habari maelezo Novemba 19 mwaka huu.

Nyaikwabe amesema mpango wa uchangiaji wa hiari ni msaada mkubwa kwa watu wote walio na wasio katika sekta rasmi ambao kwa kujiunga na mpango huo watanufaika na mafao ya elimu, ugonjwa, ujasiliamali, fao la uzeeni, kujitoa na mkopo wa nyumba kwa wale watakaokidhi vigezo.

“PSPF sasa ni kwa watu wote walio kwenye sekta rasmi na wale ambao hawako kwenye sekta rasmi maana lengo letu ni kuwafikia watu wengi ndani na nje ya nchi kupitia mpango huu wa uchangiaji wa hiari PSS ambao kiwango chake cha chini cha uchangiaji ni sh.10,000 kwa mwezi” anasema Nyaikwabe.

Akizungumzia mwamko wa watu kujiunga na mpango huo wa hiari PSS, Nyaikwabe amesema kumekuwa na mafanikio makubwa kwani tangu kuzinduliwa kwake mapema machi 7 mwaka huu tayari wanachama zaidi ya 2000 wamejiunga na mpango huo.

Kwa upande wake Afisa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Hawa Kikeke watu wengi wanajiunga na mfuko huo kutokana na ubora wa mafao yake na mikopo inayotolewa kwa wanachama waliojiunga na mfuko huo kwa miaka mitano tofauti na wakati wa nyuma ambapo mikopo ya nyumba ilitolewa kwa wanachama waliobakiza miaka mitano ya kustaafu.


TAMKO LA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI KUHUSIANA NA HABARI ILIYOCHAPISHWA NA GAZETI LA RAI KUHUSIANA NA KIFO CHA DKT. SENGONDO MVUNGI

0
0
Awali ya yote Hospitali ya Taifa Muhimbili inapenda kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki wa Dkt. Sengondo Mvungi aliyefariki katika Hospitali ya Millpark, Johanesburg nchini Afrika Kusini.  Mwenyezi Mungu aiweke mahali pema peponi, roho ya marehemu Dkt. Sengondo Mvungi, Amina.

Katika gazeti la Rai Nguvu ya Hoja Toleo Na. 1092 la Jumatano Novemba 20, 2013 lilichapisha habari ukurasa wa tatu ikisomeka “Maisha ya Dkt. Mvungi yangewezwa kuokolewa”

Gazeti hilo lilidai kwamba baada ya marehemu Dkt. Mvungi kufikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ilichukua zaidi ya saa sita kabla ya kupatiwa  huduma ya dharura aliyokuwa akihitaji na kwamba ni jambo la kawaida katika Hospitali hii ya Taifa.

Tunapenda kuwafahamisha umma wa Tanzania kuwa Idara ya  Huduma za Dharura ya Hospitali ya Taifa (EMD) imeimarika sana na huchukua takribani kati ya dakika 30-45 tu kwa  mgonjwa wa ajali kuhudumiwa na kupelekwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa matibabu zaidi. Na hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Marehemu Dr. Sengondo Mvungi.

Tunaomba radhi kwa huduma ya kwanza ya CT Scan kutofanyika Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na tatizo lililosababishwa na mawasiliano. Hata hivyo, huduma ya CT Scan ya mara ya pili ilifanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na ilisaidia kwa kiwango kikubwa katika kuimarisha tiba aliyokuwa anapatiwa na madaktari wa MOI.

Tunaendelea kusisitiza kuwa uandishi wa habari za afya unahitaji kuzingatia maadili ya sekta ya afya ili kutosababisha usumbufu usio wa lazima kwa wananchi.

Ni matumaini yetu kuwa Waandishi wa Habari watazingatia maadili ya kazi zao kama tunavyoshauri mara kwa mara katika matoleo yanayohusu Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Imetolewa na;

Ofisi ya Uhusiano
Hospitali ya Taifa Muhimbili
Novemba 22, 2013

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AFANYIWA MAOMBI YA NGUVU OFISINI KWAKE LEO

0
0
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa sita kutoka kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava ( wa pili kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi kutoka madhehebu mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa kikao.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiwa amepiga magoti kama ishara ya unyenyekevu huku akiwa amewekewa mikono na viongozi kutoka madhehebu mbalimbali waliokuwa wakimwombea ofisini kwake.
Baadhi ya viongozi wa madhehebu mbalimbali wakisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kabla ya kuanza kwa kikao chao. Viongozi hao walifika kwa ajili ya kumpongeza Waziri Muhongo kwa kazi nzuri ikiwa ni pamoja na kumfanyia maombi maalumu.
Viongozi kutoka madhehebu mbalimbali wakiendelea kubadilishana mawazo mara baada ya kumaliza kikao chao na Waziri. Aliyesimama ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiagana na baadhi ya viongozi wa madhehebu mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa kikao.

MKEKA WA NGUVU KUTOKA WILAYA YA NAMTUMBO KUELEKEA WILAYANI MBIGA MKOA NI RUVUMA

0
0





BODI YA NBC YAFANYA MAZUNGUMZO NA WATEJA WAO JIJINI DAR

0
0
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NBC, Dk. Mussa Assad (kulia) akisalimiana na mmoja wa wateja wa makampuni ya benki hiyo, Ankush Shah katika hafla hiyo. Katikati ni Mujumbe wa Bodi ya NBC, Daniel Btits.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF) William Erio katika hafla iliyoandaliwa na bodi kwa wateja wa makampuni kubadilishana mawazo na kuwajulisha mipango na maendeleo ya benki hiyo. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sekta za Umma na Huduma za Kibenki kwa Taasisi wa benki hiyo, William Makoresho na kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mauzo Hazina, Burton Hamisi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Bi. Mizinga Melu (kulia), Mjumbe wa Bodi, Dk. Hussein Kassim (kushoto), wakifurahi pamoja na baadhi ya wateja wa benki hiyo katika hafla hiyo ambayo NMBC imesema huo ni mwanzo wa matukio ya kila mara ambapo viongozi watakuwa watakutana na wateja ili kujua mahitaji yao na kubadilishana mawazo.  Wa pili kushoto ni Rishad Karimjee na Farishta Kohli wote kutoka Toyota.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Akiba wa Mashirika ya Umma (PPF), William Erio (katikati) akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Wateja Wakubwa cha Benki ya NBC Tanzania, Andre Potgieter katika hafla. Kushoto ni Naibu Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa wa NBC, Minnie Adolf Kibuta.
Baadhi ya wateja wakibadilishana mawazo na maofisa wa NBC katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam.

MAPACHA WATATU KUADHIMISHA SIKU YA KUZALIWA LEO

0
0
Meneja wa bendi ya Mapacha Watatu, Khamis Dakota akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maadhimisho yao ya miaka minne tokea bendi yao imeanzishwa. Pembeni yake wanamuziki wajasiriamali, Khalid Chuma ‘Chokoraa’ na Joseph Michael Mponezya ‘Jose Mara’. 
Waandishi wa habari wakifuatilia Mkutano huo ndani ya kiota cha Etasi (zamani Business Park) uliopo Victoria jijini Dar.
---
 BENDI ya Mapacha Watatu inayoongozwa na wanamuziki wajasiriamali, Khalid Chuma ‘Chokoraa’ na Joseph Michael Mponezya ‘Jose Mara’ leo Ijumaa Nov 22 katika ukumbi wa letasi (zamani Bussines Park) uliopo Victoria jijini Dar inatarajia kuzindua albam yake ya pili waliyoipa jina la Yarabi Nafsi.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari meneja wa bendi hiyo Khamis Dakota alisema kuwa baada ya miaka mine yenye changamoto nyingi wameamua kusherehekea pamoja na wanamuziki wakongwe kutoka bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.

Bendi ya Mapacha Watatu ina albamu mbili ambazo ni Shika Ushikacho na Yarabi nafsi.

Dakota akizitaja nyimbo zilizomo katika albamu yao ya pili Yarabi Nafsi ni pamoja na Yarabi Nafsi uliobeba jina la albamu, Ujasiriamali, Naonewa, Chanzo Wanaume, Sumu Ya Mapenzi Remix, Usia wa Babu, Mpenzi Nenda na Wivu.

Naye Khalid Chuma Chokoraa alisema kwamba anawaalika mashabiki wa bendi hiyo waje kwa wingi leo kwani kutakuwa na burudani ya aina yake ambapo wakishuka FM Academia wakiingia Mapacha Watatu kazi itakuwa bubwa.

Akizuungumzia safari ya muziki ya bendi hiyo Meneja Dakota amesema kwamba wamepitia misukosuko mingi, kiingilio ni sh. 10,000.

P-SQUARE WAWASILI JIJINI DAR, KUTUMBUIZA JUMAMOSI VIWANJA VYA LEADERS CLUB

0
0
 Wanamuziki wa kundi la P- Square Peter na Paul Okoye wakisalimiana na Mtangazaji wa kiruo cha Televisheni cha EATV, mapema baada ya kuwasili katika Uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerer e jijini Dar es Salaam. Wasanii hao wameambatana na wasanii wengine 13 kutoka katika bendi yao. Tamasha hilo limeandaliwa naEast African Radio na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
 Mwanamuziki wa kundi la P- Square Peter Okoye akizungumza na waandishi wa habari, mapema baada ya kuwasili katika Uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerer e jijini Dar es Salaam. Wasanii hao wameambatana na wasanii wengine 13 kutoka katika bendi yao.  Pamoja nao katika picha ni pacha wa msanii  huyo Paul Okoye ambao kwa pamoja wanaunda kundi la P - Square Tamasha hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
 Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu akizungumza na wasanii Peter na Paul Okoye punde baada ya kuwasili katika Uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerer e jijini Dar es Salaam. Wasanii hao wameambatana na wasanii wengine 13 kutoka nchini Nigeria.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu  na Afisa Udhamini na Matukio wa kampuni hiyo  Ibrahim Kaude, wakiongozana na wasanii Peter na Paul Okoye punde baada ya kuwasili katika Uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerer e jijini Dar es Salaam. Wasanii hao wameambatana na wasanii wengine 13 kutoka nchini Nigeria.
 Mwanamuziki wa kundi la P - Square, Paul Okoye akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarake Nyerere, Tayari kwa ajili ya kutoa burudani kwa Watanzania, Msanii huyo aliambatana na Pacha wake Peter Okoye ambao kwa pamoja wanaunda kundi la P- Square. Wasanii hao wameambatana na wenzao 13 ambao watatoa burudani jumamosi ya tarehe 23 Novemba. Tamasha hilo limeandaliwa na East African Radio na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.

Airtel, Baraza la Taifa la Usalama barabarani waungwa mkono na wananchi

0
0
Naibu Waziri wa mambo ya ndani, Bw. Pereira Silima (wa kwanza kushoto)akizungumzia umuhimu wa kupambana na ajali za barabarani leo katika hafla fupi ya kumtangaza Athmani Hamisi (wa tatu kutoka kulia)kuwa balozi wa usalama barabarani iliyofanyika katika ukumbi wa habari maelezo jijini Dar es salaam. Kulia ni Meneja wa Airtel Money Asupya Nalingigwa akifuatiwa na Mjumbe wa baraza la taifa la usalama barabarani Bw. Yakubu Rajabu.
Naibu Waziri wa mambo ya ndani, Bw. Pereira Silima (katikati) akisisitiza jambo juu ya umuhimu wa kila mwananchi kutii sheria bila shuruti ili kuepusha ajali za barabarani wakati wa hafla fupi ya kumtangaza Athmani Hamisi (kulia)kuwa balozi wa usalama barabarani iliyofanyika katika ukumbi wa habari maelezo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Kamanda Mkuu wa Jeshi la Polisi DCP Mohamed Mpinga.
Aliyeteuliwa kuwa balozi wa kampeni ya nenda kwa usalama barabarani, Bw. Athmani Khamisi akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kutangazwa rasmi kuwa balozi wa kampeni ya nenda kwa usalama barabarani iliyofanyika katika ukumbi wa jengo la habari maelezo jijini Dar es salaam hivi karibuni.Kulia kwake ni Mjumbe wa baraza la usalama barabarani Bw. Yakubu Rajabu.

BAADHI ya wananchi wanaoishi jijini Dar es salaam wamesema uamuzi uliofikiwa na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani  kumtangaza aliyekuwa mpiga picha wa magazeti ya serikali Bw. Athmani Hamisi kuwa balozi wa kampeni ya usalama barabarani una maana kubwa sana.

Wananchi hao wameyasema hayo katika nyakati tofauti walipokuwa wakihojiwa na mwandishi wetu juu ya kampeni hii ya nenda kwa usalama barabarani inayodhaminiwa na Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi ya Airtel.

Wananchi wengi wamesema uamuzi huo wa kumteua Bw. Hamisi kuwa Balozi wa kampeni hiyo kwa dhumuni la kutoa elimu ya usalama barabarani utakuwa na matunda zaidi kwa sababu kupitia yeye watu watajifunza vyema juu ya athari za ajali barabarani.

“Kumtumia mtu ambaye alishakuwa muhanga wa ajali ni jambo sahihi kabisa kwa sababu ataweza kutoa ushuhuda wa wazi ni jinsi gani ajali zimemkwamisha hata kwenye shughuli zake za kimaendeleo na kuwaasa vyema watu wanavyotakiwa kujikinga na ajali hizo.” Alisema Calisti Mushi mkazi wa Temeke jijini Dar es salaam.

Kwa upande mwingine baadhi ya wakazi wa sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaam walisema ni kweli kuwa jukumu la kupinga ajali ni la kila mwananchi lakini elimu zaidi inapaswa kutolewa ili kuzitokomeza kabisa.

“Bado elimu inahitajika zaidi kwa watumiaji wa vyombo vya moto ili kuepusha ajali ambazo hutokea kila siku, na kwa kutumia wahanga wa ajali kama Bw. Hamisi watu wataelewa vizuri zaidi ni jinsi gani ajali hudumaza maendeleo ya taifa kiujumla” walisema baadhi ya wananchi waishio katika jiji la Dar es salaam.

Kwa upande wake Balozi huyo mpya wa kampeni ya usalama barabarani, Bw. Hamisi alisema atajitaidi kwa hali na mali kutoa elimu na kuwaasa wananchi kuwa makini wanapokuwa njiani kwani ajali zinazotokea hukwamisha maendeleo kwa kiasi kikubwa.

“Mimi binafsi nimepumzika kwa muda mrefu kutokana na ajali niliyoipata, nataka nitumie fursa hii kama balozi kuiasa jamii na kutoa elimu juu ya madhara ya ajali na nini tufanye ili tuweze kuziepuka” alisema Hamisi.

Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema Airtel haitoacha kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Baraza la taifa la usalama barabarani katika kuokoa maisha ya watanzania ambayo hupotea kutokana na ajali za barabarani.

“Tunatambua umuhimu wa kuepusha ajali za barabarani na ndio maana tunaiunga mkono kampeni hii ya nenda kwa usalama barabarani kwa dhumuni la kuepusha vifo na majeruhi ambavyo hupatikana mara nyingi kwa kutokuwa na elimu ya usalama barabarani,” alisema Mmbando.

Kampeni ya nenda kwa usalama barabarani ina dhumuni la kutoa elimu kwa wananchi juu ya sheria za barabarani na itafanywa katika mikoa mbalimbali nchini.

PRESIDENT KIKWETE AT THE UN CLIMATE CHANGE CONFERENCE (COP19/CM9) IN WARSAW, POLAND

0
0
President Jakaya Mrisho Kikwete addresses African Ministerial Conference on the Environment (AMCEN) Ministers and African Group of Negotiatiors (AGN) in the margins of the UN Climate Change Conference (COP19/CMP9) at the Warsaw National Stadium in Warsaw, Poland, November 21, 2013.
President Jakaya Mrisho Kikwete holds talks with the Commissioner of Agriculture and Rural Economy of the Africa Union in the margins of the UN Climate Change Conference (COP19/CMP9) at the Bristol hotel in Warsaw, Poland, November 21, 2013.
President Jakaya Mrisho Kikwete greets the Secretary General of the World Meteorological Organisation Mr Michael Jarraud as the Director General of the Tanzania Meteorological Agency Dr. Agnes Kijazi looks on in the margins of the UN Climate Change Conference (COP19/CMP9) at the Bristol hotel in Warsaw, Poland, November 21, 2013.
President Jakaya Mrisho Kikwete poses with the Secretary General of the World Meteorological Organisation (WMO) Mr Michael Jarraud, Assistant Secretary General pf WMO Ms Elena Manaenkova and the Director General of the Tanzania Meteorological Agency Dr. Agnes Kijazi when they met in the margins of the UN Climate Change Conference (COP19/CMP9) at the Bristol hotel in in Warsaw, Poland, November 21, 2013.

MAJARIBIO YA AWALI YA MATUMIZI YA "VIDEO CONFERENCE" YAFANYIKA KWA KUZIKUTANISHA OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA OFISI ZA MAKATIBU TAWALA NA WAKURUGENZI WA MAMLAKA YA SERIKALI ZA MITAA MIKOA YA RUKWA, LINDI, MARA, RUVUMA NA SHINYANGA

0
0
Pichani wajumbe mbalimbali kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa, Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri za Wilaya ya Sumbawanga, Kalambo, Nkasi na Manispaa ya Sumbawanga wakifuatilia Mkutano wa kwanza wa majaribio ya huduma ya Video Conference leo katika ukumbi wa "Video Conference" uliopo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Anayeonekana kwenye Luninga akiwasilisha mada ni Naibu Katibu Mkuu Utumishi Ndugu Hab Mkwizu ambao ndio walioandaa mkutano huo uliojadili mada mbalimbali.

KINANA NA UJUMBE WAKE AWASILI WILAYA YA NYASA MKOANI RUVUMA,APOKELEWA KWA KISHINDO.

0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Rudisha baada ya kumsimamisha na kumtaka asalimiane wananchi .
 Ujumbe unaomtaka Katibu Mkuu wa CCM Ndugu asimame kwenye kijiji cha Maganagana japo wamsalimi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na wananchi wa kijiji cha Makatani wakati akielekea wilaya mpya ya Nyasa.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Luhangarasi  wilaya mpya ya Nyasa.
 Katibu wa NEC  Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimia  wananchi wa kijiji cha Luhangarasi wilaya mpya ya Nyasa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kubeba  matofali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Kata ya Luhangarasi.
wananchi nao wakishiriki kubeba matofali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Kata ya Luhangarasi.



 Wanachama  wa shina namba 1 kwa Balozi Joseph Nduguru tawi la Luhangarasi wilaya ya Nyasa wakicheza kwa furaha wakati wa kumaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kata ya Kingerikiti wilaya ya Nyasa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la ofisi ya CCM  wilaya ya Nyasa kulia ni Mbunge wa Mbinga Kapteni Jonh Komba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Kilosa wakati wa  ukaguzi,timu ya Kilosa ilicheza mechi ya kujipima nguvu na timu ya Mbamba Bay.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga mpira kama ishara ya ufunguzi wa mechi kati ya timu za mpira za wanawake Kilosa na Mbamba bay
Mbunge wa Mbinga Magharibi Ndugu Kapteni John Komba akihutubia wananchi kwenye viwanja vya michezo Mbamba bay.

IF TANZANIA ELECTIONS WERE HELD TODAY: WHO WOULD YOU VOTE FOR? WHO WOULD YOU ADD TO THIS LIST?

0
0
Urais Tanzania 2015.jpg The next Tanzania's General Elections are almost two years away. To be exact, Tanzanians [registered voters of course] will be on hopeful long ques in October 2015 to elect the next President of The United Republic and Members Of Parliament.In a country where almost everything is attached to politics, that is an important month and year.   While two years seems to be such a long stretch, in politics days are counted differently. 365 days could as well mean 65. 

They say politics is a sneaky game. You need to be prepared, you need to know yourself and your potential opponents way ahead. That, of course, makes politics take the title of a dirty game as well. Before you realize, the streets knows you as Mr. Inappropriate. 

Your lights are punched out and all you can see is darkness. You are no longer in control. The scene of dirty games and dirty wars I am trying to explain above is already on. If you are not aware please raise your hands up and better be in a don't shoot pose because I know you are not telling me the truth. 

I believe you have heard how some politicians are already exchanging words[ in a war-like styles] whenever they get a chance or whenever they see cameras flashing and microphones are set. They aren't telling jokes. They mean it. Holly! They love the attention. 

 Now,we live in a different era. Nowadays, you can easily tell what is in someone's mind just from their status posted on their pages over social network platforms. You can see excitement, anger, frustrations, jealousy, hopelessness, craziness from those lines. You just gotta master the art of reading between the lines. 

Few people and certainly few politicians are going to survive against the power of social networks. You gotta be a social lion to survive or completely avoid to expose your true feelings and arguably your "agenda". 
The ugly part is; if you are a politician and you are not on social networks, your chances are cut in half or unless if the office you are aiming is just Mjumbe wa Nyumba Kumi Kumi. In that case, all you need is ability to walk and drink evening tea with watu wako wa kitaa. 

 Given some of the factors I am talking about above [political jabs, war of words, social networks expose etc] it has become a bit easier [ I said a bit easier because please never underestimate a Politician] to do some guess work on our politicians' [they want to be called Waheshimiwa] next move or the office and position they are aiming for. 

I could be wrong and I could be damn right! Long story short, the men and women[ sorry a woman] whose photos appear above, are mentioned [and some have openly mentioned themselves] to be potential Presidential Candidates for Tanzania's next General Elections come October 2015. And honestly speaking, given their credentials and experiences [good and bad] and the nature of our politics or political system, anyone can the next man/woman who keeps you in "foleni" for hours because he/she is going "out".[You know] 

 The list above is not final. It can change anytime. Politicians are known to attract scandals too. So we may wake up the day after tomorrow and hear some rape charges or sale of national treasure and boom,some dreams are shattered. 

Who do you think we missed in the list?[that's why we left rooms] And most important question; Who would you vote for if elections were held today? 
Your opinion matters.Speak! 
 Jeff Msangi is a Writer/Blogger and Owner of www.bongocelebrity.com. You can reach him at bongocelebrity@gmail.com

RAIS KIKWETE KUWA MIONGONI MWA VIONGOZI MBALIMBALI WATAKAOPEWA TUZO ZA KUTAMBUA MCHANGO WAO KATIKA KUBORESHA AFYA YA MAMA NA MTOTO

0
0

NOVEMBA 23, mwaka huu, viongozi mbalimbai watapewa tuzo za kutambua
mchango wao katika kuboresha afya ya mama na mtoto. 

Tuzo hizo zimeandaliwa na Taasisi ya Madaktari Waliosoma Vyuo Vikuu nchini (THPI), na miongoni watakaopewa tuzo ni Rais Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, mke wa Rais, Salma Kikwete na Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi

Kuhusu THPI, ilianzishwa mwezi Machi, 2009 na madaktari 12, na Mkurugenzi  wa taasisi hiyo, Dk. Telesphory Kyaruzi, anasema wanaamini wakiwa wengi, watahudumia watu wengi na jamii kubwa zaidi. Anasema, hadi sasa taasisi ina madaktari  wanachama zaidi ya 120 ambao wamesambaa nchi nzima. "Lengo kuu la taasisi yetu ni kushiriki katika kuhamasisha uboreshaji huduma za afya nchini na kushiriki kikamilifu katika kutoa huduma bora za afya kwa watanzania,"anaongeza. Madaktari hao ni wale walioamua kubaki nchini badalayakukimbilia nje
ya nchi kufanya kazi...kwa kifupi ni madaktari wazalendo.

"Tuliamua kubaki nchini badala ya kwenda nchi za nje kutafuta maslahi mazuri    zaidi kwa sababu ya uzalendo juu ya nchi yetu. "Dira ya taasisi yetu, tunaona watanzania wenye afya bora, huduma bora , na miundombinu bora katika kutoa huduma za afya nchini . Katika taasis yetu  nguvu yetu ni umoja;  wote ni sawa, kila mtu ni muhimu na kila mtu ni kiongozi.  Nguvu yetu ni matumaini,"anaongeza.


 
Dk. Kyaruzi anasema ili kuwa na madaktari wengi sehemu mbalimbali nchini wanaotoa huduma za afya,  taasisi imeanzisha Idara ya Uendelezaji Madaktari Vijana inayoratibu Mtandao wa Madaktari Vijana Nchini, ambao ni Madaktari Wanafunzi( Medical Students), Intern Doctors, na Madaktari wanaoanza kazi ili kuwajengea uwezo    kitaaluma. Aidha, katika kutatua matatizo ya afya nchini, anabainisha kuwa   wanaongozwa na mpango mkakati.



Katika mpango wa mwaka 2011/2014, taasisi imejielekeza katika kutekeleza malengo ya Milenia, lengo la nne na tano, afya ya mama na mototo. Na kufikia lengo la kupunguza vifo vya akina mama kwa 75% ifikapo mwaka 2015. Katika kutekeleza jukumu hili muhimu, taasisi imeanzisha kampeni ya kitaifa ya Saidia Mama Mjamzito Ajifungue salama, ili kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Kutokana na taarifa za jarida la umoja wa mataifa , Global Health and Deplomacy, duniani kina mama  wajawazito 368,000 wanafariki kila mwaka, nafasi ya mama mjamzito kufa ni mara 100 zaidi katika nchi zenye
idadi kubwa ya vifo vya akina mama vinavyotokana na ujauzito. Akifafanua hilo, Dk. Kyaruzi anasema kuwa ni nchi 21 tu duniani ziko kwenye hatua sahihi katika kufikia malengo ya millennia ifikapo mwaka
2015. "Vifo vya mama wajawazito nchini kwa mwaka 2005 vilikuwa ni  578, kwa vizazi       hai 100,000,  na kufikia 454 kwa  vizazi hai 100,000 kwa mwaka 2012.



"Pia vifo vya watoto chini ya miaka mitano vilikuwa 122 kwa watoto hai 1,000 mwaka 2004 mpaka 81 kwa watoto hai 1,000 mwaka 2012. Na vifo vya watoto chini ya mwaka mmoja ilikuwa 68 kwa watoto hai 1,000 kwa
mwaka 2004 mpaka 51 kwa watoto hai 1,000 kwa mwaka 2012,"anasema. Kutokana na juhudi kubwa za wadau, anasema wamefanikiwa kumepunguza idadi ya vifo vitokanvyo na ujauzito na vifo vya watoto wachanga,   lakini lazima jitihada za kupunguza vifo vya mama na watoto ziedelee kwa nguvu kubwa zaidi.

Ili kutekeleza kampeni ya Saidia Mama Mjamzito ajifungue Salama, anasema taasisi ilifanya utafiti wa awali,  na kubaini upungufu wa damu ni namba moja, ikifuatiwa na kifafa cha mimba,  Aidha ni asilimia 50 tu ya  wajawazito wanaorudi kujifungua katika vituo vya afya, upungufu wa mindombinu na maambukizi ya Kutoka kwa
mama kwenda kwa mtoto ni changamoto kwa uzazi salama. "Kupitia kampeni tunahamasisha  wananchi kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wajawazito wanaohitaji  kwa dharura na kuhamasisha kina baba
kushiriki katika afya ya uzazi ikiwa ni pamoja na kuwasindikiza  kliniki ili kujua dalili za hatari wakati wa ujauzito na kujiandaa kujifungua.

"Kuongeza uwezo wa miundombinu katika utoaji huduma kwa mama wajawazito ambayo ni matumizi ya simu kufuatilia mama mwenye dalili za hatari kupitia rafiki kliniki mpaka anajifungua salama, kujenga wodi na vyumba vya dharura (ICU) na Upasuaji (Theatres) pamoja na kuzuia maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto,"anaongeza. Akielezea kuhusu tuzo, Dk. Kyaruzi anasema ya Rais Kikwete inatokana   na jitihada mbalimbali, na wanatambua kwa kuipa  kipaumbele sekta ya afya.



Alipoingia madarakani mwaka 2005, bajeti ya sekta ya afya ilikuwa ya  sita, hivi sasa ni ya tatu ikifuatiwa na miundombinu na elimu ambapo sekta hizi zote zinategemeana huku afya ya mama na mtoto ni ya kwanza katika vipaumbele vya Wizara ya Afya. "Rais ameunga mkono kampeni ya malaria haikubaliki ili  kulinda afya ya mama wajawazito na watoto wachanga, katika kufanikisha malengo ya kupunguza vifo vya mama na mtoto duniani, Umoja wa mataifa uliunda tume ya kuratibu taarifa na uwajibikaji juu ya afya ya mama na  mtoto na kumteua Rais Kikwete  kuwa mwenyekiti mwenza  wa tume hii pamoja na Waziri Mkuu wa Canada .

"Hii ni heshima kubwa kwa nchi yetu, ni imani kubwa dunia iliyonayo  juu yetu watanzania. Tuzo hii kwake ni ujumbe kwa jumuia ya kimataifa kwamba na sisi watanzania tunamwamini Rais Wetu,  tunamuunga mkono,"anaongeza. Anaitaja tuzo ya Rais Mstaafu Mwinyi, kwamba imetokana na kazi nzuri
hasa  kupinga maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na jitihada zake za mara kwa mara kuunga
mkono  matembezi ya hisani, kuwezesha upatikanaji wa fedha kusaidia watoto wenye matatizo ya moyo  na saratani ili wapate matibabu ndani na nje ya nchi.


Mkapa naye anapewa tuzo kwa kazi nzuri anayoifanya kupitia taasisi yake ambapo Dk. Kyaruzi anasema, anafana kazi kubwa  kujali afya ya mama na mtoto. Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), nayo ni chanzo kikuu kilichosababisha Mama Salma kupata tuzo kutoka madaktari hao.


Kwa mujibu wadk. Kyaruzi, Mengi anapata tuzo kutokana na utayari wake
kuisaidia jamii,  kupitia vyombo vyake, Taasisi ya Madaktari Wanawake (MEWATA) wamefanya
kazi kubwa ya kuokoa maisha ya wakina mama kutokana na Saratani ya Matiti na Shingo ya
Kizazi. Tuzo za kitaaluma zinaenda kwa Dk. Faraja Nipwapwacha, Daktari  Msaidizi , wa Kituo cha afya Kilimarondo mkoani Lindi , wilaya ya Nachingwea, ambaye kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita hajapata
vifo vinavyotokana na uzazi.

"Uwezo wake wa kujituma na tabia yake ya kufanya  maamuzi sahihi kwa wakati na haraka katika kuokoa maisha ya mama na mtoto, ametoa hamasa kubwa kwamba tunaweza kuzuia vifo vinavyotokana na ujauzito ata sehemu nyingine nchini,"anasema Dk. Kyaruzi.  Anasema THPI inatambua kazi kubwa inayofanywa na wauguzi nchini katika jitihada za kuboresha afya ya mama na mtoto kupitia.

Muuguzi  ambaye amependekezwa na wauguzi wenzake kupitia chama chao  kitaifa cha TANNA ni Elia  Mwumbui kutoka kijiji cha Matongo, kitongoji cha Kimbiji, wilaya ya Ikungi, tarafa ya Ikungi Singida
vijijini kwa kuwa mfano wa wakina baba wanaoshiriki kusindikiza kliniki wake zao wajawazito.

Anasema lengo ni kuhamasisha kuhusu afyaya mama na mtoto, kwani  wanaamini wajawazito na watoto wao wakiwa salama, taifa litakuwa salama na tutajihakikishia ustawi kama Taifa. "Namshukuru  Dk. Mary Nagu, Waziri wa Uwezeshaji na  Uwekezaji  kwa kutuunga mkono, Dk. Asha Rose  Migiro kwa kuwa mlezi wa vijana wa THPI, taasisi na watu binafsi  walioonyesha nia ya kusaidia sehemu ya kampeni hii ya Saidia Mama Mjamzito  ajifungue salama inayoendeshwa na taasisi yetu ya THPI,"anaongeza.


Dk. Kyaruzi anasema wana mradi wa kujenga uwezo kwa vituo vya afya  katika kuzuia maambukizi ya Virusi vya  UKIMWI kutoka kwa mama kwenda  kwa mtoto katika Wilaya za Iringa Vijijini , Wangig'ombe na Mpanda na
umeandaliwa kwa weledi wa hali ya juu na  mshauri mkuu akiwa Dk. David Urassa, unasubiri uwezeshaji wa fedha ili utekelezaji uanze.

"Pia mradi wa ujenzi jengo la akina mama wajawazito kata ya Ikindilo, kituo  cha afya Ikindilo wilaya ya Itilima mkoa mpya wa Simiyu nao unasubiri uwezeshaji wa fedha kuutekeleza,"anamaliza.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images