Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 173 | 174 | (Page 175) | 176 | 177 | .... | 1897 | newer

  0 0

  BINGWA wa dunia wa mbio za marathon, Edna Ngeringwony Kiplagat wa Kenya amejitokeza kushiriki zile za Uhuru Marathon zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar ers Salaam Desemba 8, mwaka huu.
   
  Katibu wa Kamati ya Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema, wamefarijika kwa kiasi kikubwa kwa Edna mwenye sifa lukuki katika mbio za marathon kujitokeza kushiriki.
   
  “Kwetu tumefarijika mno kutokana na ushiriki wa Edna, kwani ni mwanariadha wa kimataifa mwenye rekodi nyingi za kuvutia na hasa hii ya ubingwa wa dunia kwa upande wa wanawake,” alisema.
   
  Edna,34, alitwaa ubingwa wa dunia kwa upande wa marathon mwaka 2011 katika mashindano yaliyofanyika Daegu, Korea Kusini na akafanya hivyo tena mwaka huu katika mashindano ya dunia yaliyofanyika Moscow, Urusi.
   
  Pia alishinda katika mbio za Los Angeles Marathon na New York Marathon zilizofanyika mwaka 2010 na muda bora zaidi kupata kuuweka katika mbio hizo ni wa saa 2:19:50 katika mbio za London Marathon mwaka jana.
  Pia ametwaa medali mbalimbali katika mashindano ya vijana wakati anaanza kukimbia mwaka 1996, pale alipoonyesha uwezo wake katika mashindano ya dunia kwa vijana.
   
  Melleck alisema, umuhimu wa mbio hizo unaonekana zaidi kwani watu wengi wanazidi kujitokeza kushiriki nab ado fomu za usajili zinaendelea kutolewa. Alisema, katika usajili huo, mshiriki wa kilomita 3 atalipa Sh 100,000 yule wa kilomita 5 Sh 2,000 na washiriki wa kilomita 21 na 42 watalipia Sh 6,000.
   
  “Pia tunapenda kuchukua fursa hii kuziomba kampuni au taasisi mbalimbali zinazotaka kudhamini mbio hizo zijitokeze na kufanya hivyo, kwani nafasi bado ipo na tukumbuke bila amani hakuna chochote kinachoweza kuendelea, hivyo hata wao pia wanatakiwa kuipigania amani kwa nguvu zote.”
   
  Mbio hizo zinatarajiwa kuanza na kumalizikia katika Viwanja vya Leaders, vilivyopo Kinondoni.

  0 0

  Mmmiliki wa kampuni ya 2 Eyez Production na aliyewahi kuwa mtangazaji wa kituo cha television cha channel ten Bw. Frank Mtao, jumamosi iliyopita ya tarehe 23/11/13 alifanikiwa kunyakua kiti cha uenyekiti wa chama cha jumuiya ya watanzania waishio New South Wales nchini Australia.

  Katika kinyang'anyiro hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Lethington uliopo kitongoji cha Summer Hill, mjini Sydney, Frank alifanikiwa kumshinda mpinzani wake ambaye ni mkazi wa muda mrefu katika jiji la Sydney Bw Christopher Banda kwa kura 55 dhidi ya 6 alizozipata Chriss.

  Baada ya ushindi huo mzito, Frank aliwashukuru wanachama wote kwa kujitokeza kwa wingi na kufanikisha sherehe hizo za kufunga mwaka na uchaguzi na pia aliwapongeza wengine waliochagulia katika bodi yake ya chama hicho na kuhaidi watafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na kuwahaidi kuongeza jitihada za kuwakutanisha Watanzania hao na kusaidiana kwa kila hali!

  Kwa upande wa msaidizi wa Frank yaani nafasi ya ukatibu ilikwenda kwa Louis ambaye ni mtoto wa mfanyabiashara mkubwa Tanzania Bw. S.H Amoni.

  Ifuatayo ni orodha ya matokeo rasmi ya kura yalivyokuwa

  MWENYEKITI (RAISI WA JUMUIYA)
  Frank Mtao                 55
  Christopher Banda     6

  KATIBU
  Louis Amoni               42
  Halima Haule             13
  Christopher Banda      6

  MWEKA HAZINA
  Halima Haule             35
  Nadhifa M. Mwinyi     10

  WAJUMBE 5 WA KAMATI KUU
  Andrea Mburuja        23
  Nadhifa M. Mwinyi    22
  Fina Nyongo              22
  Shomari Abdallah     21
  Attu Mwakyusa          19 Waliopita

  Henry Maembe         18
  Farida P. Banda        12 

  Kwa habari zaidi zinapatikana kupitia Facebook ya jumuiya hiyo 

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea mbele jopo la Marais wastaafu wa Afrika kuhusu linaloongozwa na Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe Joaquim Chissano anayefuatana na Rais Mstaafu wa Botswana Mhe Festus Mogae leo Novemba 25, 2013 Ikulu jijjini Dar es salaam. Mhe. Chissano, ambaye ni mwenyekiti wa Jopo hilo pamoja na Mhe Mogae, walifika Ikulu kusikiliza upande wa Tanzania kuhusu mgogoro wa mpaka na nchi ya Malawi, baada ya kufanya hivyo hivi karibuni huko Blantyre. PICHA NA IKULU


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Majadiliano na Wiki ya Sera za kuondoa Umaskini, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo.
  Naibu Waziri wa Fedha Saada Salum,akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais kwa ufunguzi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na baadhi ya Viongozi na wadau katika na Mkutano wa Majadiliano na Wiki ya Sera za kuondoa Umaskini, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo.
  Baadhi ya wadau walioshiriki katika mkutano huo wa majadiliano.Picha na OMR

  0 0


  0 0

  Mkuu wa mapato wa Airtel, Bw. Hoolass Lochee akiwafundisha kompyuta baadhi ya watoto wa shule ya msingi ya Kiromo iliyopo wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani ikiwa ni baada ya wafanyakazi wa Airtel kuitembelea shule hiyo kwa dhumuni la kutoa mafunzo ya kompyuta.
  Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya sekondari ya Kiromo, Bw. Joseph Ngunangwa akiwaelezea wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel jinsi ambavyo kiwango cha ufaulu kimepanda shuleni hapo tangu Airtel ilivyoamua kuiendeleza shule hiyo kuanzia ujenzi hadi kwenye vifaa vya kufundishia ikiwa ni baada ya wafanyakazi wa Airtel kuitembelea shule hiyo iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani kwa dhumuni kubwa la kutoa mafunzo ya kompyuta kwa wanafunzi.
  Mkurugenzi wa Idara ya Fedha wa Airtel Tanzania, Bw. Kalpesh Mehta akiwafundisha matumizi ya kompyuta baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kiromo iliyopo wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani. Wanafunzi wa shule hiyo walipata nafasi ya kujifunza kompyuta katika hatua za awali baada ya wafanyakazi wa Airtel kuitembelea shule hiyo leo.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Airtel mwishoni mwa wiki wameitembelea shule ya msingi ya Kiromo iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani na  kutoa mafunzo ya awali juu  ya matumizi ya kompyuta kwa wanafunzi wa shule hiyo.

  Wafanyakazi hao wamedai kuwa kujitolea kwenda kutoa mafunzo katika shule hiyo ambayo ilijengwa na kampuni yao kupitia mradi wa shule yetu sio jambo la msimu tu kwani wana mpango wa kuendelea kutoa huduma hiyo mara kwa mara katika shule mbalimbali nchini.

  Mkurugenzi wa idara ya Fedha ya Airtel, Bw. Kalpesh Mehta alisema Airtel inaelewa wazi ni jinsi gani matumizi ya vifaa kama kompyuta hurahisisha kazi nyingi katika jamii na hivyo imeamua kwenda kutoa mafunzo ya ujumla kwa wanafunzi wa shule hiyo kwa dhumuni la kuleta mchango chanya kwenye jamii.

  “Kompyuta ni kifaa muhimu sana ambacho hurahisisha kazi mbalimbali zinazofanywa kwa ajili ya maendeleo ya jamii hivyo inabidi wanafunzi waanze kujifunza juu ya umuhimu wa kifaa hiki mapema katika kusaidia maendeleo ya jamii huko mbeleni.” Alisema Mehta.

  Kwa upande wake Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya Kiromo, Bw. Joseph Ngunangwa alisema masomo hayo yametoa hamasa kubwa sana kwa wanafunzi wa shule hiyo kwa sababu yamewafanya wahisi masomo hayo yana urahisi na sio magumu kama walivyokuwa wakifikiria.

  “Wanafunzi walikuwa na mitazamo kwamba wanaojifunza kompyuta ni tabaka flani tu la watu na walikuwa wakihisi kwamba kompyuta ni somo gumu lakini leo  wametiwa moyo na wafanyakazi wa Airtel na wameanza kuona kuwa somo hilo ni rahisi na yeyote anaweza kulisoma na kufaulu vyema,” alisema Pangahela.

  Mwalimu huyo aliongeza kuwa kupitia masomo hayo idadi ya wanafunzi watoro imepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na sababu kuwa wengi huja shule kwa ajili ya kujifunza kompyuta.

  Kwa upande wao wanafunzi wa shule ya Kiromo waliwashukuru wafanyakazi wa Airtel kwa kuonesha ukarimu mkubwa sana na kusema kuwa wanatamani masomo hayo yangekuwa yanafanyika kila siku.

  Si mara ya kwanza kwa wafanyakazi wa Airtel kuzitembelea shule na kutoa mafunzo kama hayo vile vile Kampuni hiyo hutoa misaada ya vitabu mbalimbali vya kiada nchini na kuchangia katika ujenzi wa taifa hususani katika sekta ya elimu.

  0 0

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Zamani wa Ireland ambaye sasa ni mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa UN eneo la maziwa makuu,Bibi Mary Robinson ,wakati akimkaribisha ikulu jijini Dar es Salaam leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa karika mazungumzo na Rais wa Zamani wa Ireland ambaye sasa ni mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa UN eneo la maziwa makuu,Bibi Mary Robinson aliemtembelea leo Ikulu jijini Dar es Salaam.(picha na Freddy Maro)

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea mbele jopo la Marais wastaafu wa Afrika kuhusu linaloongozwa na Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe Joaquim Chissano anayefuatana na Rais Mstaafu wa Botswana Mhe Festus Mogae leo Novemba 25, 2013 Ikulu jijjini Dar es salaam. Mhe. Chissano, ambaye ni mwenyekiti wa Jopo hilo pamoja na Mhe Mogae, walifika Ikulu kusikiliza upande wa Tanzania kuhusu mgogoro wa mpaka na nchi ya Malawi, baada ya kufanya hivyo hivi karibuni huko Blantyre. PICHA NA IKULU


  0 0

  Hi Friends and Supporters of Evans Bukuku's Comedy Club,
  Introducing the BIGGEST STANDUP COMEDY SHOW EVER right here in the heart of Dar es Salaam. Featuring Joey Lee from The USA, The Nigerian Pastor from Nigeria, Eric Omondi from Kenya and a whole host of local talent from Tanzania including Saganda, Enika, Sidestory, Dogo Pepe, MC Pilipili and Evans Bukuku.

  Corporates book your VIP tables early. .  they're going quickly!!
  You definitely don't want to miss this!! 
  Please support on your respective platforms.
  Best Regards,
  Evans.

  0 0

   Ndugu Kinana na Ujumbe wake wakipita kukagua jengo la Maabara katika shule ya  sekondari ya Mwakaleli,katika halmashauri ya Busokelo,Wilayani Rungwe mkoani Mbeya.Mradi huo wa ujenzi wa madarasa na maabara ni  mpango serikali  wa kuboresha shule za sekondari zilizopo kwenye kata na Taifa kwa ujumla kwa kushirikiana na benki ya Dunia.
   Pichani chini, Ndugu Kinana akiwa amebeba tofali ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa ujenzi wa madarasa katika  shule ya  sekondari ya Mwakaleli,katika Halmashauri ya Busokelo,wilayani Rungwe.

    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba za Walimu wa Shule ya Sekondari ya Mwakaleli.

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Katende,katika halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe,mkoani Mbeya,Kinana aliwaeleza kuwa CCM inatekeleza ilani yake ya uchaguzi na kuongeza kuwa ahadi zilizoahidiwa zitatimizwa. Aidha Kinana alikazi pia kuwa kama chama Imara lazima kihoji serikali juu ya  pesa za ujenzi maendeleo ya wananchi,kwa nini hazitolewi kwa wakati. Ndugu Kinana yupo mkoani Mbeya kwa zaiara ya siku 11 katika kutekeleza Ilani ya CCM,kukagua miradi mbalimbali ikiwemo na kujua matatizo ama kero za Wanachi.
    Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Katende  ndani ya halmshauri ya Busokelo wilayani Rungwe mkoani Mbeya,ambapo Nape aliwatahadharisha wakaji wa mji huo kuwa makini na vyama vinavyojita vya siasa,kutokana na kuanza kupoteza dira na muelekeo.
   Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akikata ubao akiwa pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya maabara na madarasa ya shule ya Sekondari ya Mwakaleli.

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na wazee wa kijiji ambao leo walimpa heshima ya kuwa Mzee wa Katende na kumvisha mgolole kama heshima ya mtu mzima.
   Katibu wa NEC Siasa na Mahusiano ya Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwa ameketi kwenye mkeka unaojulikana kama Kalili aliopewa zawadi na wakina mama wa Katende,Wilayani Rungwe mkoani Mbeya.
   Mzee Issa Simion akitoa salaam kwa niaba ya wazee wa Kijiji cha Katende na pia kushukuru kwa Serikali na Chama Cha mapinduzi na pia kuelezea kero zinazohusu wakazi wa kata ya Katende.
  Mbunge wa Wanawake Mkoa wa Mbeya  Dk.Mary Mwanjelwa akiwasalimia wakazi Katende.katika halmashauri ya Busokelo,wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

  0 0

   Wahitimu wa Shahada mbalimbali kutoka Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya kutunukiwa shahada zao Mwisho mwa wiki katika mahafali ya nne ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) yaliyofanyika katika Viwanja vya Chimwaga.Kutoka Kushoto ni Mdau Isabela, Hashim, Hashim Mzule na Rafiki yao wakiwa na furaha mara baada ya kuhitimu masomo yao ya shahada ya kwanza
   Kutoka Kushoto ni Victor Mengi akiwa na rafiki yake (katikati) na Josephat Mwanaziche mara baada ya kutunukiwa shahada zao katika mahafali ya nne ya chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki chuoni hapo
   Wahitimu wa shahada mbalimbali wakijipongeza mara baada ya kuhitimu rasmi safari yao ya masomo ya shahada za kwanza ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) mara baada ya kutunukiwa shahada zao mwishoni mwa wiki
   Happy Mengi (katikati) akifungua shampeni pamoja na wadogo zake waliohitimu masomo yao ya Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) wakati wa tafrija fupi ya kuwapongeza. Kutoka Kushoto ni Mariam na Wa Kwanza kulia ni Victor Mengi
  Wahitimu wakikata Keki wakati wa tafrija fupi ya kuwapongeza wahitimu hao waliotunukiwa shahada zao mwishoni mwa wiki katika mahafali ya nne ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) yaliyofanyika katika viwanja vya chimwaga mkoani Dodoma

  0 0

  DSC_0022

  Hyatt Regency The Kilimanjaro Hotel General Manager Trevor Saldanha speaks to invited guests during the business partner celebrations hosted by The Kilimanjaro Hotel to his customers in Dar es Salaam.

  By MOblog Team
  HYATT Regency the Kilimanjaro Hotel has set aside USD 50,000 as part of the hotel’s Corporate Social Responsibility (CSR) efforts to foster the development of education sector in the country. It has been learnt.

  Speaking to invited dignitaries during the dinner party hosted by the Kilimanjaro hotel to its customers yesterday in Dar es Salaam, General Manager Trevor Saldanha said the funds would be used to repair and rehabilitate Mtoni Primary school in the Temeke municipality.

  “Equally important when in business is to give back to the community one operates in and I would like to mention here that “The Kilimanjaro” as part of its corporate social responsibility has kept aside 50,000 dollars that is being used to repair & maintain the Mtoni School,”

  “ We have already begun working with the school principal on the areas that are in urgent need of repair and while some work is being done with the help of outside contractors a lot of this project is being completed with the help of hotel employees who donate their free time to this important cause,”

  “We are also partnering with His Worship The Lord Mayor of Ilala, Jerry Silaa on his project for 2013 which is to ensure that every child attending a public school has a bench to sit on,” says Saldanha

  He said that the hotel will always remain the iconic “Kilimanjaro Hotel”; all team members will work hard to live up to the name and represent the brand to the best of theory collective abilities.

  Saldanha added that the hotel continues to be the preferred residence of Kings, Queens, Presidents, Prime Ministers, Entrepreneurs and Entertainers when they visit Dar es Salaam (some of you may have already caught a glimpse of some of our famous guests on the screens).

  He further said that the aim of any company is to expand and increase its enterprise value and Hyatt is currently constructing a 77 room hotel in historic Stone Town, Hyatt will commission the new “Park Hyatt Zanzibar” next year. This spectacular property will set the tone for hospitality on the island.
  DSC_0088
  Mr.Timoth Mlay The Hyatt Regency The Kilimanjaro Hotel, Front Office Manager along side with Sam Sarin Sales Executive Manager conducting a draw where by invited guests wins various Hampers.
  DSC_0135
  Sam Sarin Sales Executive Manager of the Kilimanjaro Hotel display a bottle of Hennessey from Q Way International.
  DSC_0532
  An Employee from Commercial Bank of Africa (CBA) Rehema Mashayo in a happy mood when she was announced as a lucky winner of the Business Class return Ticket from Dar to Instanbul whenHyatt Regency The Kilimanjaro Hotel conducted a draw on behalf of Turkish Airline.
  DSC_0533
  Turkish Airlines Director, Tanzania Alper KUCUK congratulate Ms. Rehema Mashayo from CBA Bank for being one of the lucky winners during Business Partners celebrations hosted by The Kilimanjaro Hotel Hyatt Regency.
  DSC_0535
  Turkish Airlines Director, Tanzania Alper KUCUK hands over an example of the return ticket Ms. Rehema Mashayo from CBA Bank.
  DSC_0556
  Turkish Airlines Director, Tanzania Alper KUCUK display an example of the returning ticket of Ms.Rehema Mashayo.
  DSC_0247
  His worship Lord Mayor Hon. Jerry Silaa shares a light moment with Jacqueline Kombe (left) from High Commissioner of Canada and Jully Urio (right) during the Business Partner Celebrations hosted by The Kilimanjaro Hyatt Regency Hotel.For more pictures click here

  0 0


  0 0

    Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Wadau mbali mbali walioshiriki kwenye Warsha ya Kamata Fursa Twenzetu,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam.Mh. Rais ameupongeza uongozi wa Kampuni ya Clouds Media Group kwa ubunifu wao wa Kampeni ya Fusra inayowakutanisha na kuwahamasisha vijana mbali mbali nchini kujituma na kufanya kazi ili kutokomeza swala zima la ukosefu wa ajira,Pia Rais Kikwete ameahidi kuwasaidia waendeshaji wa Warsha hiyo.Picha zote na Othman Michuzi. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi,Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,ili aweze kuzungumza na Wadau mbali mbali walioshiriki kwenye Warsha ya Kamata Fursa Twenzetu,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.
  Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Maxcom Africa,Ahmed Lussasi akizunguma katika Warsha ya Fursa namba alivyo
  Mwanamuziki wa Muziki wa Kizazi Kipya,Nasseb Abdul a.k.a Diamond akitoa ushuhuda wake wa namna alivyoanza na mpaka alipofikia sasa,ambapo ameweza kuiona Fursa na kuweza kugawana fursha hiyo na vijana wenzake anaofanya nao kazi kila siku.Kushoto ni Mwanafursa Mwingine,ambaye pia ni Msanii wa Mashairi,Mrisho Mpoto.
  Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Bi. Fatma Ally akielezea namna alivyoipata Fursa kwa kupitia Ufugaji wa Nyuki.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasikiliza vijana mbali mbali walopata Fursa na kuweza kufanikiwa katika maisha yao.
  Mrisho Mpoto akizungumzia Fursa yake.

  Wadau mbalimbali wa Warsha ya Kamata Fursa Twenzetu wakimsikiliza kwa makini Mwenyeshaji wa Kampeni hiyo ya Fursa,Ruge Mutahaba.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Naseeb Abdul a.k.a Diamond.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati akiwapongeza vijana walioiona Fursa.
  Wadau mbali mbali wakiwa kwenye Warsha ya Kamata Fursa Twenzetu iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam leo.
  Picha ya pamoja.

  0 0

  Tamasha la Krismas likikaribia, muimbaji nguli wa muziki wa Injili wa Afrika Kusini, Solly Mahlangu ‘Obrigado’ ni mmoja wa waimbaji ambaye anatarajia kuimba kwenye tamasha hilo linalotarajia kuanza Desemba 25 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions ambao ni waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama mwimbaji huyo ataimba live siku hiyo pamoja na waimbaji wake wengine 14.

  Msama alisema mwimbaji huyo anatarajia kushiriki katika tamasha hilo jijini Dar es Salaam, tamasha ambalo litafanyika pia katika mikoa ya Morogoro (26), Tanga (28), Arush(29) na Dodoma (1).

  Aidha Msama alisema bado wanaendelea kufanya mazungumzo na waimbaji wengine yameshakamilika kwa waimbaji wa ndani na nje ya Tanzania ikiwa ni pamoja, Solomon Mukubwa (Kenya), Ephraim Sekeleti (Zambia), Liliane Kabaganza (Rwanda).

  Waimbaji wa Tanzania ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Edson Mwasabwite, New Life Band na John Lissu.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la Nchi Wanachama wa Shirikisho la Viwanda vya Utengenezaji Nguo kwa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola Barani Afrika,lililoanza leo katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Kinyago kutoka kwa Makamu wa Mwenyekiti wa CAPA wa Kanda ya Afrika Magharibi, Prof. Daniel Nyarko, baada ya kufungua rasmi Kongamano la Nchi Wanachama wa Shirikisho la Viwanda vya Utengenezaji Nguo kwa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola Barani Afrika,lililoanza leo katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa nne kushoto), Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya CAPA,John Kondoro (kushoto kwa Makamu) na baadhi ya viongozi wa CAPA, wakifurahia kwa pamoja baada ya kuzindua rasmi Jarida la Wanachama wa Shirikisho la Viwanda vya Utengenezaji nguo kwa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola Barani Afrika (CAPA Journal), wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo lililoanza leo katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.


  0 0

  Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimesema kimewaandikia barua aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zitto Kabwe na Mjumbe wa kamati Kuu Dk Kitila Mkumbo ambazo wanapaswa kujieleza kwa siku kumi na moja, kisha watapata fursa kujieleza mbele ya kamati kuu maalumu kwa nini wasifukuzwe kutoka Chamani. 

   Akizungumza katika makao makuu ya chama hicho, Mkurugenzi wa habari na Uenezi John Mnyika alisema barua hizo zipo tayari na wahusika watapatiwa wakati wowote kuanzia leo. Mnyika alikuwa akitoa taarifa ya kikao cha Utekelezaji cha sekretarieti ya chama hicho iliyoketi baada ya mkutano wa kamati kuu iliyoketi tarehe 20 – 22 Novemba mwaka huu. 

   Ni katika Mkutano huo, Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho, Tundu Lissu alisema kuwa mkutano uliofanywa na Zitto na Dk Kitila mbele ya waandishi hawajazungumzia tuhuma zinazowakabili, badala yake walichofanya ni kujitungia tuhuma ambazo kimsingi sizo zilizo wavua nafasi zao. 
   Lissu alisema, Zitto na Dk Kitila hawakusimamishwa nyadhifa zao kwa masuala ya PAC, Uchaguzi wa mwaka 2010, wala kutoshiriki kwenye operesheni za chama au sababu zingine, na walitaja hizo sababu ili kupotosha tuhuma zinazowakabili kwa jamii: 
  “Walichokifanya kina Zitto na Kitilla ni "Diversion" (kubadili mwelekeo) wa mashtaka yao yanatokana na waraka wa kihaini wa mabadiliko ambao ni kinyume na katiba, kanuni na maadili na itifaki ya Chama. anawaambia waandishi, "wamevuliwa nafasi zao na kamati kuu kwa sababu ya waraka wenye nia ovu" alisema Lissu. 
   Aliongeza kuwa CHADEMA kina mwongozo wa uchaguzi uliopitishwa na kamati kuu, Zitto na Kitila wanaufahamu ingawa haijulikani ni kwanini wao walienda kinyume na mambo yanayojadiliwa katika kamati kuuu Aidha Lissu alieleza kuwa Dk Kitilla anapotosha umma na wanachaka kwa kauli yake kuwa kamati kuu haina mamlaka ya kumvua yeye nafasi yake ya ujumbe wa kamati kuu maana amechaguliwa na baraza kuu, alimtaka Kitila na Zitto waangalie vema katiba ya chama hasa majukumu ya kamati kuu, pale yanaporuhusu Mwanachama yeyote kusimamishwa au kufutiwa uachama harka kama kamati kuu itaona kuna umuhimu wa kufanya vile.
   Kigaila alisema, Kamati kuu iliyoketi Novemba 20-22/2013 ilipitisha ratiba ya uchaguzi wa ndani ya chama kama ifuatavyo:- 22/11/2013-14/12/2013 ni kukamilisha zoezi la usajili wa wanachama, 15 Desemba hadi 15 Januari uchaguzi ngazi za vitongoji, 16 januari 30 Januari 2014 Rufaa naukaguzi, ambapo tarehe 01 Februari hadi 15 Februari ni uchaguzi wa matawi. 

  CHADEMA pia ilisema 16 Februari hadi 29 mwezi huo huo ni kusikiliza rufaa na ukaguzi, ambapo uchaguzi wa majimbo utaanza rasmi 1 Aprili hadi Aprili 10, huku uchaguzi ngazi ya Wilaya ukitarajiwa kufanyika 25 Aprili hadi mei 5 mwaka 2014, na ngazi ya Mikoa ni 20 Mei hadi 25 Mei. 
   Huku uchaguzi wa kanda ukitarajiwa kufanyika Julai 9, na haada ya hapo Julai 23 hadi Julai 30 utakuwa ndio muda wa uchaguzi ngazi ya Taifa, utakaoanza na baraza la Wazee, Baraza la Vijana, Baraza la Wanawake kisha uchaguzi wa ndaniya chama. Source: 

  0 0

  Mwili wa Mtanzania Jerry Isaack Mruma  aliyekuwa akisoma Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Marekani (USIU) tawi la Nairobi nchini Kenya akichukua Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara (MBA) aliuawa wakati akitoka kwenye hafla ya usiku wa Mtanzania mjini Nairobi. Mwili  wake ulipatikana mwishoni mwa wiki iliyopita. Amezikwa leo katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
   Familia ya Isaack Mruma ikiwa katika ibada maalum ya kumuombea marehemu iliyofanyika katika Kanisa la KKKT, Usaharika wa Mbezi Beach Dar es Salaam.
  Kutoka kushoto ni Mama mzazi wa Jerry, Bi Joyce Mruma, Khan Mruma ambaye ni kaka wa marehemu, baba mzazi wa Jerry, Isaack Mruma na mdogo wake Kelvin Mruma wakiwa katika ibada hiyo. PICHA ZAIDI FATHER KIDEVU BLOG

  0 0

    Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kujenga moja ya nyumba ya waalimu katika shule ya sekondari ya Ikuti iliopo katika kata ya Ikuti,Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya mapema leo,akiwa sambamba na Ujumbe wake hawapo pichan,Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Asharose Migiro.Kinana na Ujumbe wake wako ziarani Wilayani Rungwe Magharibi mkoani Mbeya,ambapo kesho watakuwa wilaya ya Ileje kutekeleza Ilani ya chama,kukagua miradi ya chama na wanachi sambamba na kujua na kutatua matatizo yao kwa namna moja ama nyingine.
  Wakienda kukagua moja ya bweni la kulala wanafunzi wa shule hiyo ya Ikuti
  Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa ,Asharose Migiro wakielekea kuonana na balozi balozi wa shina la Kitonga,ndani ya kijiji cha Ikuti,Bwa.James Mbasi ,pichani nyuma anaefuatia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnaupe
  Katibu Mkuu wa CCM,pili kushoto,Ndugu Abdulrahman Kinana na wajumbe wake  wakielekea kuonana na balozi wa shina la Kitonga,ndani ya kijiji cha Ikuti,Wilayani Rungwe mapema leo.
  Pichani ni Katibu Mkuu wa CCM pichani kati,Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa kituo cha kuzalisha umeme kilichopo kwenye zahati ya Ikuti,katika kijiji cha Ikuti wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

  Kada maarufu wa CCM,Richard Kasesela akipiga ngoma ya asili ya kinyakyusa iitwayo Lipenenga.
  Baadhi ya vijana mbalimbali wakiwa juu ya miti wakifuatilia mkutano wa hadhara,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia jioni ya leo kwenye kijiji cha Ikuti.
  Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya kimataifa,Asharose Migiro akizungumzaa mbele ya wakazi wa kijiji cha Ikuti mapema leo.
   Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnaupeakizungumzaa mbele ya wakazi wa kijiji cha Ikuti mapema leo,Wilayani Rungwe.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na wakazi wa kijiji cha Ikuti mapema leo,kwenye mkutano wake wa hadhara .
  Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya,Dkt Mary Mwanjelwa akifafanua jambo kwa wakazi wa kijiji cha Ikuti mapema leo,Mbunge huyo pia aliwataka akina mama kujiunga katika vikundi vya ujasiliamali,ili kurahisishiwa kupata mikopo ya kuendeleza miradi yao ambayo wataianzisha katika suala zima la kujikwamua na ugumu wa maisha,
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na wafanyabiashara wa ndizi katika soko la Iponjora,Wilayani Rungwe,Kinana aliwaasa wafanyabiashara hao kutokuwa na tamaa ya kuuza biashara yao hiyo ya ndizi kwa bei ya kutupa,badala yake waachane na watu wa kati,wafanye biashara yao kwa faida na si kuwanufaisha wafanyabiashara wakubwa,ambao hawajui ugumu wa kilimo cha zao hilo,Kinana katika kuwaongezea kasi ya biashara yao ya ndizi aliwachangia kiasi cha shilingi laki moja
  Katibu NEC,Siasa na Mahusiano ya kimataifa,Dkt Asharose Migiro akizungumza na wafanyabiashara wa ndizi katika soko la Iponjora,Wilayani Rungwe,mkoani Mbeya.
  Wakazi wa kijiji cha Ikuti wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe mara baada ya kuusimamisha msafara wake.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na wakazi wa kijiji cha Lupando,Kata ya Masoko Wilayani Rungwe mapema leo,Kinana alizungumza mambo mbalimbali ikiwemo namna ya kutatua tatizo sugu la Maji na Barabara katika kijiji hicho,alichozaliwa Mbunge wa jimbo la Rungwe Magharibi,Mh.Dkt David Mwakyusa.Aidha kinana aliitahadharisha Serikali katika suala zima la kuitaka Serikali iache urasimu na umangimeza katika mipango ya maendeleo kwa Wananchi,kwa sababu Urasimu na umangimeza huo huwanufaisha zaidi wanaoshikilia fedha za miradi hiyo wakati wananchi Wanaumia na kuteseka kwa kukosa huduma muhimu mbalimbali.
  Mbunge wa jimbo la Rungwe Magharibi,Mh.Dkt David Mwakyusa,akizungumza na wakazi wa kijiji cha Lupando,Kata ya Masoko Wilayani Rungwe mapema leo kuhusiana na kero mbalimbali zinazowatatiza wakazi hao,ikiwemo suala la maji na barabara sambamba na tatizo la bei ya zao la ndizi kutoka kwa wakalima kwenda kwa wafanyabiashara.
  Mbunge wa jimbo la Rungwe Magharibi,Mh.Dkt David Mwakyusa akisalimiaa na Katibu NEC,Siasa na Mahusiano ya Nje,Dkt Asharose Migiro mara baada ya kukutana katika kijiji cha Lupango,Wilayani  Rungwe,ambapo Ndugu Kinana aliwahutubia wakazi wa kijiji hicho.
   Pichani shoto ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya,Dkt Mary Mwanjelwa akiwa na Katibu NEC,Siasa na Mahusiano ya kimataifa,Dkt Asharose Migiro walipokuwa wakielekea kukagua jengo la bweni la kulala wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ikuti,Wiayani Rungwe mkoani mbeya leo.

   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na wakereketwa wa shina la vijana waendesha boda boda katika soko la Kiwira,ambapo Ndugu Kinana aliwachangia kiasi cha fedha shilingi milioni tano kwa ajili ya kujiendeleza na kuwapa uwezo wa kujikopesha wenyewe katika suala zima la kujikwamua na suala zima la umasikini,hasa ikifahamika kuwa tatizo la ajira kwa vijana limekuwa kubwa.
   Pichani shoto ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya,Dkt Mary Mwanjelwa akiwa amepozi na mdau.

  0 0

  Mwanamuziki wa mtindo wa Bongo Flava , Mwana FA azungumzia juu ya changamoto na hadhi ya muziki huo mashuhuri unaopenda kote Afrika Mashariki alipokuwa mgeni wa kipindi cha Live Talk

older | 1 | .... | 173 | 174 | (Page 175) | 176 | 177 | .... | 1897 | newer