Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1737 | 1738 | (Page 1739) | 1740 | 1741 | .... | 1897 | newer

  0 0  Na Ferdinand Shayo,Arusha.

  Benki ya ABC tawi la Arusha imeendelea na juhudi za kuwekeza kwenye maendeleo ya jamii kwa kutoa mikopo kwa wajasiriamali ,kusaidia jamii kupata bima za afya ili kuharakisha maendeleo ya jamii ya Kitanzania.

  Meneja wa Benji hiyo tawi la Arusha Magabe Nyambuche amesema kuwa kwa mwaka 2019 Benji hiyo imejipanga kutoa mikopo kwa Vikundi maalumu ikiwemo Vicoba na Sacco's ambao wamekua wakipewa mafunzo na Maafisa Wa Ustawi wa jamii ili waweze kunufaika na mikopo kwa kufanya shughuli za uzalishaji Mali.

  Magabe alisema kuwa benki hiyo limekua karibu na jamii na kuwafikia wananchi walioko vijijini kupitia ubunifu wa kutoa huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ambapo benki hiyo ilipewa tuzo ya Ubunifu.

  "Kwa sasa tuna mawakala 250 ambao wanahakikisha kuwa wateja wetu wanafikiwa na huduma za kifedha popote pale walipo" Anaeleza Meneja hiyo

  Hata hivyo benki hiyo imedhamini mkutano mkuu wa Wadau wa maendeleo ya jamii unaondelea jijini Arusha ikiwa ni juhudi mojawapo ya kuisaidia jamii ambayo hunufaika na Utaalamu wa Maafisa wa Maendeleo katika Vijiji na Mjini.

  Pia  wamejizatiti katika kuendelea kushirikiana na serikali kuharakisha maendeleo ya jamii kwa kutuma dhana ya uwezeshaji wa mikopo yenye masharti nafuu


  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Kilosa

  ujenzi wa reli ya kisasa kwa kipande cha pili kuanzia eneo la Morogoro hadi Makutupora Singida, unazidi kushika kasi baada ya wakandarasi wa ujenzi wa reli hiyo kumaliza kazi muhimu.

  Kazi hizo ni pamoja na uchukuaji wa sampuli za udongo, miamba kwenye milima itakayapasuliwa, kuchonga, kupasua na kujaza udongo kwenye njia za reli ya mwendokasi pamoja na kumalizia ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza mataluma ya reli.

  Hayo yalibainika kwenye ziara ya maalumu iliyoandaliwa na kampuni ya Ador Tanzania kwa waandishi mbalimbali nchini, ili kujionea ufanyaji kazi wa ujenzi wa reli hiyo kuanzia Morogoro hadi Makutupora.

  Ujenzi wa reli hiyo kwa kipande hicho, unajengwa na Kampuni ya Yepi Merkezi kwa gharama ya dola bilioni 2, ambapo Meneja Mradi huo katika Lot 2 inayotoka Morogoro Mpaka Makutupola, Dk. Husnis Uysa amesema wamekamimilisha mambo ya Msingi katika ujenzi huo.

  Amesema tayari wameshaleta vifaa ambavyo zaidi ya magari 3,085, ambayo ipo katika eneo la mradi, huku pia kambi za mafundi na wafanyakazi kujengwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo Mkata, Kilosa na Makutupora.

  "Malengo yetu ifikapo Januari mwakani au mwishoni mwa mwezi Desemba, kazi rasmi itaanza ya kuanza kuweka vifusi vya zege ili shughuli zingine za utandazaji wa reli uanze" amesema.

  Dk. Husnis amesema reli hiyo yenye kilometa zaidi 422, itakuwa na vituo vya kisasa nane huku kati ya hizo vituo vikubwa vikiwa viwili, ambazo ni Kilosa, na Dodoma Mjini.Amesema licha ya kuwepo kwa vituo hivyo, ambavyo vitajengwa kulingana na tamaduni za kila eneo na uasili wake, pia maandalizi ya njia ya kupita reli hiyo chini ya milima tayari imeanza kufanya kazi."Tuna milima kama minne ambayo tutaichonga hasa katika eneo la Kilosa kwenye mto mkoandoa, ambapo kwa muda mrefu lilikuwa eneo korofi, ambapo sasa tutaipitisha reli hiyo chini ya mlima," amesema.

  Vituo hivyo ni Mkata, Kilosa(itakuwa stesheni kubwa),Kidete, Igandu, Dodoma Mjini(ambapo kitakuwa stesheni kubwa), Bahi, Makutupora, ambazo zote zitajengwa kulingana na maeneo yao ya asili jinsi yalivyo.
  Kwa mujibu wa Dk. Husnis, milima ya Kilosa, reli hiyo itajengwa kwenda chini kwa mita 30 hadi mita 90, huku ikitarajia kutembea chini ya ardhi kwa zaidi ya kilometa 2.7.

  "Maandalizi yote ya mlima utakaopita treni tayari unajulikana na sasa tunaanza kupima miamba ya hapo ili tuweze kujua aina ya udongo uliopo kabla ya kuanza kuuchoronga," amesema.Kwa upande wake, Meneja mradi wa Stardand Gauge kipande cha Morogoro hadi Makutupora kwa upande wa Shirika la reli nchini(TRC), Injinia Faustin Kataraia alisema wanaendelea na usimamizi madhubuti.

  Amesema mradi huo ni mkubwa na ndio maana kama TRC imejipanga kikamilifu kuwa pamoja na mkandarasi, ambapo sasa katika hatua zote za awali walikuwepo pamoja na wadau wengine."Tupo na mamlaka ya maji Morogoro, shirika la umeme nchini(TANESCO) na wadau wengine muhimu ambao kwa namna moja au nyingine hii stardand gauge ina wahusu kwa ukaribu zaidi,' amesema.

  Aidha, amesema katika mradi wa pili wa ujenzi wa reli hiyo zaidi ya watanzania asilimia 79 wanashiriki kwenye ujenzi huo kwenye kazi mbalimbali sawa na wafanyakazi 1533 kati ya 1924 waliopo kwenye mradi huo.
  Meneja mradi wa Standard Gauge kipande cha Morogoro hadi Makutupora kwa upande wa Shirika la reli nchini(TRC), Injinia Faustin Kataraia akiwaeleza Waandishi wa Habari namna mradi huo utakavyoungana na ule wa kutoka Dar mpaka Ngerengere.
  Meneja Mradi wa SGR katika Lot 2 inayotoka Morogoro Mpaka Makutupola, Dk. Husnis Uysa akizungumza na Waandishi w ahabari juu ya hatua zilizochukuliwa katika kutekeleza Mradi huo. 
  Sehemu ya Waandishi wa Habari waliotembelea mradi wa SGR Kutoka Morogoro mpaka Makutupora wakiangalia mashine ya kusagia kokoto
  Sehemu ya Makandarasi wakiendelea na ujenzi wa tuta kutoka Morogoro mpaka Makutupora Singida.
  Mtambo wa kusagia Kokoto ukiwa umefungw akatika moja ya vituo vya kazi katika tuta la Morogoro kama unavyoonekana.
  Mashine ya kuchimba Miamba kwa ajili ya kukagua ubora wa Ardhi katika eneo ambalo Reli ya SGR itapita katika eneo la Mpwapwa.

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akimsikiliza kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Hamis Issah (kushoto), wakati alipofanya ziara ya Ukaguzi katika eneo la mafunzo ya mbinu za medani Kilelepori wilayani Siha mkoani Kilimanjaro leo 28/11/2018. Picha na Jeshi la Polisi.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akizungumza na wanafunzi wanaopata mafunzo kwa ngazi ya Uofisa pamoja na Mkaguzi wa Jeshi hilo katika Shule ya Polisi Moshi eneo la Kilelepori wilayani Siha mkoani Kilimajaro leo 28/11/2018. Picha na Jeshi la Polisi.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akisalimiana na baadhi ya Wakufunzi wa Shule ya Polisi Moshi mkoani Kilimanjaro wakati alipofanya ziara ya Ukaguzi Leo 28/11/2018. Picha na Jeshi la Polisi.

  0 0

   Mbunge wa jimbo la Vunjo ,Mh James Mbatia akizungumza wakati wa mkutano wake uliofanyika katika Mji Mdogo wa Himo. 
   Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mh ,James Mbatia wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika jimboni hapo. 
   Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akifanya dua na baadhi ya viongozi mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Ghalani Mji Mdogo wa Himo.  Kilimanjaro.


  MWENYEKITI wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na Mbunge wa Vunjo, James Mbatia amewamegea siri wananchi wa mji mdogo wa Himo juu ya mazungumzo yake na Rais Dk. John Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

  Alidai alikwenda kumueleza malalamiko ya wananchi kuhusu amri ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi ya kusitisha ujenzi wa barabara na kusababisha hasara ya mabilioni ya shilingi.

  “Haya yote nimemueleza Mheshimiwa Rais (Magufuli) niwe mkweli, nilibahatika hapo katikati Mheshimiwa Rais akaniita akasema hivi, narejea sauti ya Rais aliniambia na ameshaagiza ofisi zake na wengine wameniita Dodoma, barabara za wana Vunjo atachangia yeye binafsi kama John Pombe Magufuli, pili serikali yake itachangia na tatu atakuja kama Amiri Jeshi Mkuu kufungua barabara hizi yeye mwenyewe kama John Pombe Magufuli,”alisema

  Mbatia alikuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Makuyuni katika Mamlaka ya Mji mdogo wa Himo, Wilaya ya Moshi wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya ghalani. 

  Mradi wa upanuzi na ujenzi barabara za vijijini kwa kiwango cha changarawe unaodaiwa kusisitishwa katika Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, unahusisha barabara zenye urefu wa kilometa 389.3 ambazo zilikuwa zigharimu Sh. bilioni 12.077 kutokana na utafiti wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura) wa mwaka huu.

  Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba anadaiwa kusimamisha kazi ya ujenzi wa barabara hizo na hivyo kusababisha hasara.

  Zaidi Mbatia alisisitiza: “Sasa tuone ni nani zaidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na maendeleo ya watanzania, maendeleo hayana itikadi za vyama. Kwa nini amefanya hivyo, kwa sababu Jimbo la Vunjo tumekuwa wa kwanza Tanzania kuweza kujipanga wenyewe mpaka hatua tuliyofikia ya kujiletea maendeleo yetu wenyewe na tujipongeze wana Vunjo.

  "Hizi barabara zikiwa vizuri si tunazitumia sote, barabara za Makuyuni zikiwa nzuri zitaendelea kutumiwa na watu wote hata kama Mbatia sitakuwa Mbunge…Mimi sijawahi kumtukana Rais, sasa atakuja yeye mwenyewe.”Mbatia alikutana na Rais Magufuli na kufanya mazungumzo naye Ikulu, Novemba 13 mwaka huu akiwa pamoja na wanasiasa wengine Mh. John Cheyo (UDP), John Shubuda na mfanyabiashara Rostam Aziz.

  Katika mkutano huo, Mbatia aliwaeleza wananchi hao kwamba amekopa fedha zaidi ya Sh. milioni 500 Benki ya CRDB kwa ajili ya kununua mitambo ya ujenzi wa barabara hizo.

  “Mimi nimenunua mitambo sawa, mingine tunakodisha sawa lakini tukasema wananchi waanze kuchangia mafuta kwenye hiyo mitambo hiyo, kwa mfano Kijiji cha Mshihiri mpaka leo hii wameshachangia takribani Sh. milioni 26 lakini ukichanganya zote pamoja na za Ashira ni zaidi ya Sh. milioni 30 na kitu huko,”alieleza

  Akijibu maswali ya wananchi kuhusu kukwama kwa ujenzi wa barabara za Samanga/Sembeti, Mbunge huyo alisema Mungu sio Athuman na akawataka wananchi hao kusubiri kwanza ili mdomo wake usiteleze kwa vile wana kesi mahakamani.

  Wakati anahitimisha mkutano huo, Mbatia aliipongeza Kamati ya Maendeleo ya wana Vunjo (VDF) chini ya Askofu Mstaafu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Dk. Martin Shao, mashekhe wetu, mapadri wetu na wachungaji na viongozi wote, akisema yeye binafsi toka sakafu ya moyo wake hana chuki na mtu yeyote na anamshukuru Mungu amesikia na Mheshimiwa Rais (Magufuli) amesikia dua zao.

  0 0


  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii, Dodoma

  Kazi inakwenda vizuri. Ndivyo unavyoweza sema juu ya mradi wa reli ya kisasa marufu ya Standard Gauge kutokana na Shirika la Reli(TRC) kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa ikiwemo kumsimamia mkandarasi Yepi Merkezi kwa ukaribu mkubwa.

  Michuzi Blog imetembelea mradi huo, kuanzia Dar es Salaam hadi Makutupora, ambako kuna vipande viwili vya mradi huo vinavyotekelezwa na mkandarasi huyo, kujionea kuna mabadiliko makubwa juu ya ujenzi huo tofauti na watu wanavyozungumza katika Mitandao ya Kijamii na Vijiweni.

  Hii inatokana na kuwepo kwa madai ya kuwa hakuna kazi inayofanyika, ambapo kumefichuka kuwa kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro kazi imefanyika kwa zaidi ya asilimia 36, ambapo sehemu zilizobakia ni ndogo na zinazowezwa kufanya kazi kwa uharaka na mkandarasi.

  Pia, inaelezwa hata baadhi ya malighafi nyingi zinapatikana kwenye eneo la mradi iwe kipande cha Morogoro hadi Makutupora au Dar es Salaam hadi Morogoro, ambapo imerahisisha upataji wa marighafi.Akizungumza na Michuzi Blog Meneja mradi wa SGR kwa upande wa Shirika la Reli nchini(TRC), Injinia Masanja Machibya, amesema hakuna malighafi yeyote inayozalishwa nje, bali mahitaji yote muhimu yanapatikana kwenye eneo la mradi.

  Amesema kwa upande wa kipande anachokisimamia cha Dar es Salaam hadi Morogoro, malighafi zote zinapatikana ikiwemo kuwa na kiwanda cha kokoto chenye uwezo mkubwa wa uzalishaji wa kokoto na kuondoa kabisa tatizo la kuagiza kokoto.

  amesema kuna kiwanda cha kutengeneza mataluma, ambapo mataluma 1080 yanazalishwa kwa siku na kazi yote inafanywa na vijana wa kitanzania, Mataluma hayo yanatengenezwa kwa kutumia Nondo, Saruji, Kokoto, Mchanga na Maji ambavyo vyote vinapatikana nchini.Amesema wameweza hata kutandaza nyaya za mawasiliano ili kuwasaidia waongoza treni pindi itakapoanza. hivyo ana matumaini makubwa mradi huo unakwenda kufanyika kwa ufanisi mkubwa kutokana na vitu vinavyofanyika.

  Akizungumza naye na Michuzi Media, Injinia Faustine Kataraia, ambaye ni msimamizi wa mradi wa SGR kwa upande wa Morogoro hadi Makutupora, amesema sasa wamemaliza kujenga kiwanda cha kokoto eneo la Morogoro, ambazo zitatumika kwenye kipande hicho na mradi utakapomalizika kiwanda kitaendelea kuwepo.

  "Huu si mradi pekee kiwanda tulichojenga hapa Morogoro tunaweza kuuza hata kwenye miradi mingine ya barabara au kwa watu binafsi, hapa tunaweza kusema tumeunga mkono jitihada ya rais Dk.John Magufuli ya viwanda," amesema.

  Amesema kila kitu kinakwenda vizuri hasa upande wa Morogoro hadi Makutupora, hivyo hadi ifikapo 2021 mambo yatakuwa mazuri na mradi utakuwa bora kwa kuwa kwa miundombinu iliopo itasaidia hata mwendesha treni alioko Dar es Salaam kuona kila kitu kinachofanyika

  Meneja mradi wa SGR kwa upande wa Shirika la Reli nchini(TRC), Injinia Masanja Machibya, akizungumza na Waandishi wa habari  kuhusu mradi huo unavyoendelea katika Lot 1 inayotoka Dar es Salaam mpaka Morogoro.
  Meneja mradi wa SGR kwa upande wa Shirika la Reli nchini (TRC), Injinia Masanja Machibya,akiwaonesha Wanndishi wa Habari mfano wa Reli ya SGR itakavyokuwa katika kiwanda cha kuzalisha Mataluma ya Reli hiyo.
  Mafundi Wakiendelea na Ujenzi wa Madaraja na karavati katika eneo la mradi wa SGR eneo la Lot 1 Kisarawe.

  Mataluma ya Reli yakiwa yameweka kwa ajili ya kutandikwa juu ili kujenga mradi wa SGR kwa upande wa Shirika la Reli nchini(TRC),
  Sehemu ya Wakandarasi wakiendelea na upandaji nyasi kwa ajili ya kuzuia Mmomonyoko wa udongo  kwenye tuta la kukatisha reli ya SGR.
  Mafundi chuma wa mradi wa SGR Kutoka Yap Markenz wakiendelea na kazi katika yard ya Shaurimoyo Jijini Dar es Salaam.
  Mafundi chuma wa mradi wa SGR Kutoka Yap Markenz wakiendelea na kazi ya kujenga Madaraja ya kupachika katika yard ya Shaurimoyo Jijini Dar es Salaam.
  Moja ya kituo cha Mfano kikiwa katika picha ya mfumo wa 3d na kikionesha namna ya kituo cha Pugu Station kitakavyokuwa.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya, Bw. Jestas Nyamanga (kushoto) akizungumza na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Mhe. Nikolai Astrup mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ziara ya kikazi ya siku nne. 
  Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Mhe. Nikolai Astrup amekutana na Kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) katika ofisi za Wizara hiyo leo. Mazungumzo yao yalihusu kukuza na kuimarisha ushirikiano hususan katika programu za kuboresha mifumo ya ukusanyaji fomu kodi Tanzania. 
  Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Mhe. Nikolai Astrup katikati akiendelea na mazungumzo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji hayupo pichani. kushoto ni Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Elisabeth Jacobsen 
  Watumishi walioshiriki mazungumzo hayo, kushoto ni Bi. Tunsume Mwangolombe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akisikiliza kwa makini hoja zilizokuwa zinajadiliwa katika mazungumzo hayo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Jestas Nyamanga. 


  Ziara katika Shirika la Reli Tanzania

  Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Mhe. Nikolai Astrup akiwa katika Shirika la Reli Tanzania. Mhe. Waziri alienda katika Shirika hilo kutembelea wahandisi wa kike wanaofadhiliwa na Serikali ya Norway. Katika programu hiyo Serikali ya Norway ishafadhili wahandisi wa kike 506 kwa gharama ya zaidi ya Dola za Marekani milioni 4.2 kwa kipindi cha miaka 8. Ufadhili huo umepunguza uwiano wa wahindisi wa kiume na wakike kutoka 1:27 kabla ya programu kuanza na kufikia 1:10 kwa sasa. 
  Wahandisi wa kike ambao wapo katika mafunzo ya vitendo wakitoa maelezo ya shughuli wanazofanya katika Shirika la Reli Tanzania. 
  Ziara katika Viwanja vya Gymkhanas
  Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Mhe. Nikolai Astrup akipiga mpira akiwa katika viwanja vya Gymkhanas. Mhe. Waziri alienda katika viwanja hivyo kujumuika na kuongea na watoto wa kike walioshindwa kumaliza masomo kwa sababu mbalimbali na kwa sasa Serikali ya Norway inatoa msaada wa fedha kwa ajili ya kuwafundisha watoto hao stadi za maisha. 
  Baadhi ya watoto waliopo katika programu inayofadhiliwa na Norway ya kuwapatia stadi za maisha ijulikanayo Bonga Programu inayoendeshwa na Mfuko wa OCODE.

  0 0


  Na Mwandishi Maalum, Dodoma

  Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt Evaristo Longopa amesema, Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya utendaji wa Kazi ( OPRAS) utasaidia sana katika kuwapima watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

  Dkt. Longopa ameyasema hayo hivi karibuni wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya uwezeshaji kuhusu mfumo wa OPRAS kwa watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

  Mafunzo hayo yaliwahusisha Manejimenti, Mawakili wa Serikali na watumishi wa kada nyingine na yalifanyika katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Jijini Dodoma.

  Katika mafunzo hayo, pamoja na watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kuelimishwa Sheria na Nyaraka mbalimbali zilizoanzisha OPRAS pia walielimishwa kuhusu umuhimu wa kila mtumishi katika utumishi umma wa kujaza fomu ya OPRAS kila mwaka kwa kushirikiana na Mkuu wake wa Kazi na kwamba zoezi hilo linatakiwa kufanyika kwa uwazi.

  “ Katika vikao vyetu vya menejimenti, tulikubaliana kwamba, upo umuhimu wa zoezi la upimaji na tathmini ya utendaji kazi kwa watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Zoezi hili litatusaidia sana katika kujipima na kuwapima walio chini yetu ilikufikia malengo ambayo Ofisi yetu imejiwekea na hatimaye malengo ya Serikali kwa ujumla”. Akasema Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali

  Akasisitiza menejiment na watumishi wote kuyazingatia mafunzo hayo kutokana na umuhimu wake na kwamba ni haki na wajibu wa kila mtumishi wa Ofisi yake kufanyiwa tathimini na kupimwa kuhusu namna anavyotekeleza majukumu yake kwa kile alichosema upimaji huo unamanufaa kwa mtumishi binafsi pia.

  Wawezeshaji wa Mafunzo hayo walitoka Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

  Katika mafunzo hayo watumishi walisisitizwa juu ya umuhimu na haja ya kuyafahamu majukumu yake ambayo ndiyo atakayopimwa nayo pamoja na kuwa na mkataba ambao mtumishi atakuwa ameingia na kiongozi wake kabla ya kuanza kutekeleza malengo ambayo Idara au Kitengo imejiweka kwa mwaka huo.

  Na kwamba upimaji na tathimini ya utendaji kazi pia husaidia kubainisha changamoto mbalimbali ambazo kwa namna moja zinakwamisha utekelezaji kwa ufanisi wa malengo ambayo Taasisi imejiwekea na hatimaye kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo.

  Kwa mujibu wa Bi. Zainabu Kutengezah . Ujazaji wa fomu ya OPRAS ni muhimu sana kwa mtumishi wa umma na zoezi hili ni la kisheria kwa kuwa linasimamiwa na sheria , Waraka na kanuni mbalimbali za utumishi wa umma. Na ni zoezi linalotakiwa kufanyika katika mazingira ya uwazi baina ya mtumishi na kiongozi wake.

  Wakati wa mafunzo hayo watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali ikiwa ni pamoja na zoezi la vitendo la namna bora na sahihi ya kujaza fomu ya OPRAS.

  Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Evaristo Longopa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya OPRAS kwa watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikakali. Mafunzo hayo yalihusisha Menejiment, Mawakili wa Serikali na Watumishi wa kada nyingine . Walioketi nyuma ni wawezeshaji kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Zainabu Kutengezah na Bi. Shomi Mongi.
  Bi. Susan S. Kalele ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi Raslimali watu Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali akitoa maelezo kwa Menejiment kuhusu mfumo wa OPRAS
  Wakili wa Serikali Bi. Juliana Mnisi akiuliza swali kwa wawezeshaji kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
  Bi Dorina Kalumna akitoa maelezo kwa watumishi wenzie jinsi ya kufikia ukokotoaji wa alama ambazo mtumishi na kiongozi wake wanakuwa wameafikiana wakati wa ujazaji wa fomu ya OPRAS.

  habari na picha kwa hisani ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

  0 0

  *Ni baada ya wanafunzi 72 wa kike kupewa ujauzito wilayani Nyang’hwale

  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amechukizwa na vitendo vya watoto wa kike kukatisha masomo yao kwa kupata ujauzito wilayani Nyang’hwale ambapo jumla ya wanafunzi 72 wamepata ujauzo katika kipindi cha miaka mitatu cha kuanzia mwaka 2016 hadi 2018.

  Kutokana na wilaya hiyo kuwa na idadi kubwa ya watoto wa kike wanaokatisha masomo kutokana na ujauzito, Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale Hamim Gwiyama kufanya operesheni katika kila kijiji na kubaini waliowapa wanafunzi ujauzito na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

  Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Jumatano, Novemba 28, 2018) alipozungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba, ,kijiji cha Kalumwawilaya ya Nyang’hwale, akiwa katika ziara yake mkoani Geita.

  “Jambo lingine litakalowawezesha kukabiliana na tatizo la ujauzito kwa wanafunzi wa kike ni kuanzisha miradi ya ujenzi wa mabweni ili watoto wa kike waweze kusoma bila ya kupata vishawishi vinavyosababisha wao kupata ujauzito.”

  Waziri Mkuu alisema Serikali haiwezi kuacha jambo hilo likiendelea, hivyo aliwataka wananchi washirikiane katika kuwalinda watoto wa kike na Serikali itawachukulia hatua watendaji wote ambao katika maeneo yao watoto wa kike watabainika kuwa na ujauzito.

  “Watoto wa kike lazima waheshimiwe waachwe wasome bila ya usumbufu na atakayekatisha masomo adhabu yake ni kali. Tukikukuta umesimama na binti katika kona isiyoeleweka tutakukamata. Ole wenumtakaobainika kuwapa ujauzito wanafunzi, adhabu yake ni miaka 30 jela.”

  Waziri Mkuu pia, alitoa onyo kwa wazazi au walezi watakaowaozesha watoto kike ambao bado ni wanafunzi na kwa upande wa wazazi watakaomsindikiza mtoto wao wa kiume kwenda kuoa mwanafunzi wote watachukuliwa hatua za kisheria.

  Katika kuoneshwa kuchukizwa na jambo hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mwita Waitara ambaye anashughulikia elimu, amemueleza Waziri Mkuu kwamba Novemba 30, 2018 yeye arudi wilayani hapo kwa ajili ya kuwashughulia wote wanaokatisha masomo wanafunzi kike. Ametoa namba ya simu ili wananchi waanze kumpa taarifa za wahusika.

  Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu alisemaSerikali imedhamiria kusambaza umeme katika vijiji vyote ambavyo bado havijaunganishiwa nishati hiyo nchini vitaunganishiwa katika awamu ya tatu ya Mradi wa Nishati Vijijini (REA).

  “Rais wetu Dkt. John Magufuli anataka kuona nyumba ya kila Mtanzania inapata umeme tena kwa gharama nafuu na ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme katika vijiji vyote nchini. Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni sh. 27,000 tu.”

  Kuhusu suala la gharama za kulipia nguzo, Waziri Mkuu alisema wananchi hawatowajibika tena katika kulipia gharama za nguzo pamoja na zile za fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme kwa sababu tayari gharama hizo zimeshabebwa na Serikali.

  Awali, Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Nyamigogo ambapo alikagua miundombinu ya kiwanda hicho na kisha aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda hicho, ambacho muwekezaji wake ni mzawa.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro ameendelea na juhudi zake Za utatuzi wa migogoro na safari hii amemuomba Mhe Jenista Mhagama ambae ni Waziri wa Nchi ofisi ya waziri Mkuu anaeshughulikia masuala ya kazi kuingilia kati mgogoro huo ili kunusuru hatima Za maisha ya wafanyakazi wanaodai mishahara Kwa miezi tisa sasa .

  Hatua ya Dc Muro imekuja Mara baada ya wafanyakazi hao kuvamia ziara ya Mhe Mhagama akiwa katika Wilaya ya Arumeru wakati wa Uzinduzi wa kongamano la maafisa Maendeleo ya jamii nchini ambapo Mara baada ya kutembelea mabanda ya maonyesho kundi la wafanyakazi wa chuo Cha Mount meru lilimvamia Mhe Waziri Mhagama wakiwa na mabango wakitaka kujua hatima ya madai yao ambayo Mhe Mkuu wa Wilaya ya Arumeru amekuwa akipambana kuwasaidia wafanyakazi hao pasipo kuchoka.

  Kutokana na tukio hilo, ilimlazimu Mhe Mhagama kutoa maelekezo kwa kamishna wa kazi nchini ambae alimtaka kuunda kamati ya wataalamu kutoka wizarani ambayo itaungana na Mhe Jerry Muro Mkuu wa Wilaya ya Arumeru katika kuhakikisha changamoto hiyo inatatulia haraka iwezakanavyo hatua ambayo ilipokelewa Kwa shangwe na wafanyakazi wa chuo kikuu Cha Mount ~Meru.
   Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro ameendelea na juhudi zake Za utatuzi wa migogoro na safari hii amemuomba Mhe Jenista Mhagama ambae ni Waziri wa Nchi ofisi ya waziri Mkuu anaeshughulikia masuala ya kazi kuingilia kati mgogoro huo ili kunusuru hatima Za maisha ya wafanyakazi wanaodai mishahara Kwa miezi tisa sasa .
   
   Baadhi ya Wafanyakazi wakiwa wamebeba mabango yao yenye jume mbalimbali.
   

  0 0

  NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 

  BAADHI ya wananchi wa kata ya Pangani ,Kibaha Mjini mkoani Pwani, wameitaka serikali ya wilaya na mkoa kuangalia namna ya kufuta umiliki wa mashamba makubwa ambayo hayaendelezwi na kusababisha kutumika kama vificho vya wahalifu na kuokotwa miili ya wafu na walionusurika kufa.

  Wameeleza kwa kipindi cha miezi sita miili zaidi ya kumi zimeokotwa kwenye mtaa huo ambapo kati yao wengine walinusurika kifo na kuokolewa na wengine wakiwa wamefariki dunia. 

  Diwani wa kata ya Pangani , Agustino Mdachi aliyasema hayo kufuatia mwili wa mtu mmoja mwanaume aliyekufa kuokotwa kwenye mtaa wa Pangani .Alieleza ifikie wakati wamiliki hao wasiangaliwe nyadhifa ama majina yao ili kunusuru maisha ya watu. "Miili ya watu imekuwa ikiokotwa mara kwa mara,wengine wanaookolewa wakiwa wametupwa hivyo tunaitaka serikali kuyafutia hati mashamba haya ili yagawiwe kwa wananchi waweze kuyaendeleza likiwemo shamba la serikali la mifugo la Mitamba", alisema Mdachi.

  Hata hivyo Mdachi alisema ,wameshachukua hatua ya kuwaita wamiliki wa mashamba hayo ili kuwaeleza vitendo vinavyotokea lakini baadhi yao wamekuwa hawajitokezi .

  Nae mwenyekiti wa mtaa wa Pangani Jitihada Ndiali alisema,eneo hilo kwa sasa limefanywa kama dampo au sehemu ya kutupia maiti pia madereva bodaboda kuporwa pikipiki zao kisha kutupwa .Mwenyekiti wa mtaa wa Miwale ,Amos Mkwawa alisema kuwa maeneo hayo pia ni changamoto kwa wanafunzi wa kike ambao wapo hatarini kubakwa.

  Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka aliwaomba wamiliki husika kujitokeza kwenda kuyaendeleza maeneo yao. Jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP )Wankyo Nyigesa ili aeleze ama kuthibitisha kuhusu maiti hiyo iliyookotwa hazikuzaa matunda kutokana na kuwa kikaoni.
   BAADHI ya wananchi wa kata ya Pangani ,Kibaha Mjini mkoani Pwani, wakiwa kwenye mkutano wao kuhusu serikali ya wilaya na mkoa kuangalia namna ya kufuta umiliki wa mashamba makubwa ambayo hayaendelezwi na kusababisha kutumika kama vificho vya wahalifu na kuokotwa miili ya wafu na walionusurika kufa.

  0 0

  0 0


  0 0

  Ben Pol feat. The Mafik - Sio Mbaya (Produced by Nusder & Daxo Chali, written by Lollipop, Mixing & Mastering By Marco Chali),


  0 0

  New Video #MLEVI By @kellahtz Produced by @daxochali @mjrecordstz Video imeandaliwa na bwana Papushka,


  0 0

   Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Happiness Kusekwa akipokea zawadi ya Daktari bora wa mwezi Oktoba kutoka kwa Mkurugenzi wa Tiba ya Moyo na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Peter Kisenge wakati wa hafla fupi ya utoaji zawadi kwa wafanyakazi bora iliyofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo. Zawadi hizo zilitolewa na kampuni ya dawa za binadamu ya Samiro

  Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma ya Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akimkabidhi zawadi ya mfanyakazi bora wa mwezi Oktoba Afisa Muuguzi Msaidizi Keyness Erasmus Mng’anya wa JKCI wakati wa hafla fupi ya utoaji zawadi kwa wafanyakazi bora iliyofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo. Zawadi hizo zilitolewa na kampuni ya dawa za binadamu ya Samiro. Picha na: Genofeva Matemu - JKCI

  0 0

   Mshehereshaji George Mulamula (kushoto) wa uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 akiitambulisha meza kuu wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma. Kutoka kulia kwenda kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie Bouckly, Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida pamoja na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa ESRF, Prof. Sylvia Temu.
   Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akisoma hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Waziri mwenye dhamana ya wizara hiyo Dkt. Phillip Mpango wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
    Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
   Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie Bouckly ambao ni wafadhili wa ripoti hiyo akitoa salamu za Umoja wa Mataifa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma. Kulia ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa ESRF, Prof. Sylvia Temu.
   Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida, Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu pamoja na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw. Irenius Ruyobya wakisikiliza salamu kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie Bouckly (hayupo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
   Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw. Irenius Ruyobya akitoa salamu NBS kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dkt. Albina Chuwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
   Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (wa nne kulia) akikata utepe kuzindua Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma. Wanaoshuhudia tukio hilo kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie Bouckly, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw. Irenius Ruyobya (kulia) pamoja na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa ESRF, Prof. Sylvia Temu (wa tatu kulia).
   Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie Bouckly, Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu, Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa ESRF, Prof. Sylvia Temu pamoja na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw. Irenius Ruyobya katika picha ya pamoja huku wakiwa wameshika nakala ya Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 mara baada ya kuzinduliwa rasmi katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
   Mtafiti mshiriki mwandamizi wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF),Prof Samuel Wangwe akiwasilisha ripoti kuhusu hali ya ustawi wa jamii Tanzania wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
   Mkuu wa kitengo cha Uwezeshaji na Utawala Bora wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango akizungumzia masuala ya kisera katika mabadiliko ya kiuchumi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
   Mtaalam na Mratibu wa Programu kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Amon Manyama akizungumzia utengenezaji wa ripoti hizo kwa siku za usoni ambapo ameahidi kufikisha ripoti hizo katika vyuo mbalimbali 
   Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa ESRF, Prof. Sylvia Temu akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa ESRF, Philemon Luhanjo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
   Washiriki wakiuliza maswali wakati wa kujadili maeneo mbalimbali ya wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
   Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw. Irenius Ruyobya akipitia nakala ya Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 mara baada ya kuzinduliwa katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma. Kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa ESRF, Prof. Sylvia Temu.
   Washiriki wakipitia nakala ya Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 mara bada ya kuzinduliwa katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
  Wadau kutoka taasisi mbalimbali za serikali bara na visiwani, ESRF, Umoja wa Mataifa pamoja na wanafunzi wa vyuo vikuu Dodoma walioshiriki kwenye hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Phillip Mpango amesema Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu nchini Tanzania ya Mwaka 2017 (THDR) inayozungumzia  “Sera ya Kijamii Katika Muktadha wa Mageuzi ya Kiuchumi”, ina mchango mkubwa katika kuchambua masuala yanayohusu maendeleo ya binadamu na nafasi yake katika uandaaji wa mipango ya maendeleo, utengenezaji wa bajeti, ufuatiliaji na tathmini.
  Alisema hayo katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Khatibu Kazungu wakati wa uzinduzi wa ripoiti hiyo mjini Dodoma jana.

  “Kwa mtazamo wangu, dhana hii ya kufungamanisha maendeleo ya watu na mageuzi ya kiuchumi sio tu kwamba ni dhana sahihi bali pia inaendana na Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/17 – 2020/21.’ Alisema Dk. Mpango .

  Aidha, alisema dhana ya kufungamanisha maendeleo ya watu na mageuzi ya kiuchumi ni dhana ambayo imekuwa ikizingatiwa katika mipango ya ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka mmoja mmoja pamoja na miongozo ya uandaaji wa bajeti za serikali.

  Dk. Mpango alisisitiza kwamba kwa kuzingatia umuhimu wa kujenga uchumi jumuishi, kutokuacha mtu yeyote nyuma katika mchakato wa maendeleo na kufungamanisha maendeleo ya watu na mageuzi ya uchumi, serikali ya Tanzania imetoa umuhimu mkubwa katika utoaji wa huduma za jamii ili kuinua hali za watu wake.Waziri Mpango alisema kwamba sekta ya afya, elimu na miradi ya kimkakati kama ujenzi wa reli ya kisasa ni sehemu ya juhudi zinazofanya kuwezesha uchumi jumuishi.

  Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kwamba kutokana na jitihada mbali mbali zinazofanywa na serikali ya Tanzania katika utoaji wa huduma za kijamii na kuinua maisha ya watu wake, kiwango wastani wa umri wa Mtanzania umeongezeka kutoka miaka 62.2 mwaka 2013 hadi miaka 64.4 mwaka 2017.

  Alisema ni matazamio ya Serikali ni kuendelea kuboresha huduma za jamii ili kwamba kiwango cha wastani wa maisha ya Mtanzania yawe ni miaka 66.1 ifikapo mwaka 2020.    Alisema ni mtazamo wa serikali ya Tanzania kutoa huduma za kijamii kama afya, elimu na maji kwa umuhumi sawa na uwekezaji katika misingi ya uchumi kama ujenzi wa reli na barabara kwani pande hizi mbili zinategemeana na kusaidiana katika mchakato wa ujenzi wa uchumi wa kisasa.   

  Akimkaribisha mgeni rasmi kuzindua Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 Mkurugendaji Mtendaji wa ESRF Dkt. Tausi Kida alisema kwamba ripoti hiyo ni ya pili kitaifa nchini Tanzania.
  Aidha alisema kwamba Mada kuu ya ripoti ya mwaka ya “Sera ya Kijamii katika Muktadha wa Mageuzi ya Kiuchumi” ilichaguliwa makusudi ili kuendeleza dhana zilizoibuliwa na Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania ya mwaka 2014, ya umuhimu wa mageuzi ya kiuchumi ambayo Tanzania imedhamiria kuyafanya kama inavyoelekezwa na Dira ya Maendeleo ya Taifa.

  Kwa mujibu wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2014 iliyobeba mada ya “Mageuzi ya Kiuchumi kwa Maendeleo ya Binadamu dhana kuu ilikuwa ni mageuzi ya kiuchumi yalete maendeleo ya binadamu.

  “Kiukweli mchakato wa mageuzi ni lazima uende sambamba na upatikanaji wa ajira, ongezeko la kipato na utoaji wa huduma za jamii. Hivyo, Ripoti hii ya mwaka 2017 imelenga kuendeleza fikra za ripoti iliyotangulia katika kuchambua nafasi ya sera ya kijamii na utoaji wa huduma za kijamii katika mchakato endelevu wa mageuzi ya kiuchumi nchini Tanzania, “ alisema
  Miongoni kwa matokeo muhimu katika utafiti uliofanyika katika ripoti hii ni pamoja na kuonesha kwamba Tanzania imepiga hatua kubwa katika maendeleo ya binadamu, maendeleo ambayo yanathibitishwa na kuongezeka kwa alama za Kipimo cha Maendeleo ya Binadamu (HDI) kutoka 0.371 mwaka 1985 hadi 0.531 kwa mwaka 2015 ambalo ni ongezeko la asilimia 43.1 kwa kipindi cha miaka 30 (UNDP 2016).

  Kwa kuzingatia alama za mwaka 2015, Tanzania imepanda daraja ambalo ni zaidi ya wastani wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ambayo ni 0.518.
  Aidha ripoti hii imeonesha pia kwamba kiwango cha umaskini kwa kutumia kipimo cha vigezo mbali mbali yaani MPI umepungua toka kiwango cha asilimia 64.0 mwaka 2010  hadi asilimia 47.4  mwaka 2015. Kwa mujibu wa utafiti huu, mafanikio haya yamesababishwa na kuboreka kwa maisha ya Mtanzania katika maeneo mbali mbali hususan elimu na afya pamoja na ongezeko kubwa la upatikaji wa huduma ya umeme miongoni mwa wananchi.

  Pamoja na mafanikio haya, ripoti hii imeonesha pia kwamba Tanzania bado ina safari ndefu kuelekea katika viwango vya juu vya maendeleo ya binadamu yanayokusudiwa na Dira ya Maendeleo ya Taifa.Mchakato wa uandaaji wa ripoti hii ulioratibiwa na taasisi ya ESRF ikishirikiana na kikosi kazi cha zaidi ya wataalamu thelathini (30) toka taasisi mbali mbali nchini ina sura nne pamoja na viambatanisho vya takwimu.

  Naye Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie Bouckly ameelezea kufurahishwa kwake na ripoti hiyo na kusema inaonesha juhudi za serikali ya Tanzania katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa lengo la kubadilisha hali ya wananchi wake na kuwa bora zaidi.

  Alisema ripoti hiyo inaonesha njia inayochukuliwa na Tanzania kuleta mabadiliko ya kweli kwa wananchi wake kupitia mipango mbalimbali ya kukabiliana na umaskini ikiwamo MKUZA na FYDP.

  Ripoti hiyo imeandaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) ikishirikiana Wakala wa taifa wa Takwimu (NBS), Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa serikali ya Zanzibar na kitivo cha uchumi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP .

  Ripoti hii inapatikana kwenye anuani zifuatazo
  http://www.thdr.or.tz/
  http://www.esrf.or.tz/
  http://www.tz.undp.org/

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa utetezi katika kesi ya kesi ya Uhujumu uchumi inayomkabili mfanyakazi mstaafu wa Shirika la Mafuta Tanzania na Zambia(Tazama), Samwel Nyakirang'ani(63) na wenzake 11 kukamilisha mapema upelelezi dhidi ya kesi hiyo ili kigundua nani anahusika na nani hausiki kwenye kesi hiyo.

  Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ameeleza hayo leo Novemba 29, 2018 wakati kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa.

  Kabla ya kueleza hayo Wakili wa Serikali Patrick Mwita alidai kuwa upelelezi katika shauri hilo haujakamilika, jalada bado lipo katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), kwa ajili ya kulichambua na kisha kulitolea maamuzi kuangalia washtakiwa gani washtakiwe na washtakiwa gani waachiwe huru.

  Kutokana na hayo, Hakimu Simba ameutaka upande wa mashtaka wajitahidi kumaliza shauri hilo mapema kwani shauri lenye watu wengi kama hili ni vema ikajulikana mapema kwani inawezekana baadhi yao hawahusiki.Nyakirang’anyi na wenzake wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kujiunganishia isivyo halali bomba la mafuta, mali ya Mamlaka ya Bandari Tanzania ( TPA), katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

   Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 10 kwa ajili ya kutajwa na kuangalia upelelezi kama utakuwa umekamilika ama la.Washtakiwa wote wapo rumande kutokana DPP kuwasilisha hati ya kuzuia dhamana.Mbali Samweli, washtakiwa wengine katika kesi  hiyo namba 1/2018 ni Nyangi Mataro( 54) Mwalimu wa Shule ya  Msingi Ufukoni na mkazi wa Kisiwani Mkajuni Kigamboni.

  Mfanyabaishara, Farijia Ahmed(39)mkazi wa Soko Maziwa Kigamboni, Malaki Mathias(39) mkazi wa Magogoni, Kristomsi Angelus(25) mkazi wa Soko Maziwa,  Fundi Ujenzi Pamfili Nkoronko(40) mkazi wa Tungi Kasirati na Henry Fredrick (38) mkazi wa Tungi Kigamboni.Wengine ni Audai Ismail (43) ambaye ni mkazi wa Kibaha, Chibony Emmanuel, Roman Abdon, Amina Shaban na Zubery Ally.

  Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka matatu ya uhujumu uchumi kwa  kujiunganishia isivyo halali bomba la mafuta, kinyume cha sheria  ya Uhujumu uchumi.Katika shtaka la kwanza, kati ya mwaka 2015 hadi Januari 8, 2018 katika eneo la Tungi Muungano wilaya ya Kigamboni, washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kujiunganishia bomba la mafuta ya dizeli lenye upana wa inchi moja kutoa katika bomba lenye upana wa inchi 24, bila kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Bandari nchini(TPA).

  Pia wanadaiwa kuharibu miundo mbinu ambapo wanadaiwa kutoboa  bomba la hilo, ambalo  lilikuwa likitumika kufirisha mafuta,  mali ya Mamlaka ya Bandari nchini( TPA).Aidha washtakiwa wanadaiwa kuharibu  bomba la mafuta mazito( Crude oil) lenye upana wa Inchi 28, ambalo lilikuwa likitumika kusafirisha mafuta ghafi, mali ya Mamlaka ya Bandari nchini( TPA).


  0 0


  Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Happiness Kusekwa akipokea zawadi ya Daktari bora wa mwezi Oktoba kutoka kwa Mkurugenzi wa Tiba ya Moyo na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Peter Kisenge wakati wa hafla fupi ya utoaji zawadi kwa wafanyakazi bora iliyofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo. Zawadi hizo zilitolewa na kampuni ya dawa za binadamu ya Samiro
  Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma ya Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akimkabidhi zawadi ya mfanyakazi bora wa mwezi Oktoba Afisa Muuguzi Msaidizi Keyness Erasmus Mng’anya wa JKCI wakati wa hafla fupi ya utoaji zawadi kwa wafanyakazi bora iliyofanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo. Zawadi hizo zilitolewa na kampuni ya dawa za binadamu ya Samiro.Picha na: Genofeva Matemu - JKCI

  0 0

  Wananchi wa eneo la Sogea, Wilaya ya Mjini Unguja wamemkabidhi Naibu Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani ya Nchi, Mhandisi  Hamad  Masauni, orodha ya watu  wanaoshukiwa  kujihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya Visiwani Zanzibar. Wananchi hao wamekabidhi orodha hiyo baada ya Naibu Waziri Masauni kuwataka waorodheshe majina ya watu wanaowafahamu wakituhumiwa kujihusisha na biashara hiyo ambayo imekuwa ikiaribu nguvu kazi ya Taifa na kusababisha  kuwepo  kwa  matukio ya uhalifu katika sehemu mbalimbali Visiwani humo.

  Awali  wakiwasilisha  kero zao kwa nyakati  tofauti wananchi hao waliiomba serikali  kudhibiti  biashara  hiyo  ya dawa za kulevya  kwani  imekua ikishamiri kwa kasi Visiwani humo na wakishangaa ukimya wa mamlaka husika kuacha biashara hiyo ikizidi kuleta madhara katika jamii.
  Akizungumza katika Mkutano huo wa hadhara, Naibu Waziri Masauni amewaahidi  wananchi  hao  kuchukua  hatua  madhubuti  kukabiliana  na  wauzaji wa dawa za kulevya huku akitoa maelekezo kwa  Jeshi  la  Polisi  kuwakamata watu  wote waliotuhumiwa  na  uchunguzi  uanze  mara moja.

  “Hatuwezi  kama  Taifa  tukawa  na vijana ambao hawana faida katika jamii, vijana  ni  nguvu kazi ya Taifa, tutahakikisha majina yaliyoletwa hapa tunayafanyia  kazi na natoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi kuhakikisha watuhumiwa hao wanakamatwa na nitahitaji ripoti hiyo ndani ya wiki mbili, haiwezekani watu wachache waharibu nguvu kazi ya Taifa kwa maslahi yao binafsi na familia zao,” alisema  Masauni
  Akizungumza katika mkutano huo , Kamishna Msaidizi, Saleh Mohamed Saleh, aliwaomba wananchi kuzifikisha  taarifa  za  uhalifu  katika  vituo  vya  Jeshi la Polisi au Serikali ya Mtaa  ili  hatua ziwe zinachukuliwa ili kuweza kudhibiti  uhalifu  katika  maeneo yao.
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad (kulia), akiangalia majina ya watu wanaotuhumiwa kujihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi hao ikiwa ni jitihada za Serikali kudhibiti matukio ya uhalifu  yaliyoanza kushamiri katika maeneo mbalimbali  Visiwani Zanzibar.Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Polisi Jamii Zanzibar, Emmanuel Lukula, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Saleh Mohamed Saleh na Katibu wa Naibu Waziri, George Mwansasu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 
   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad (kulia), akizungumza na wananchi wa eneo la Sogea, Wilaya ya Mjini Unguja (hawapo pichani), wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi hao ikiwa ni jitihada za Serikali kudhibiti matukio ya uhalifu  yaliyoanza kushamiri katika maeneo mbalimbali Visiwani Zanzibar.Wengine kutoka kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Polisi, Saleh Mohamed Saleh na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka Zanzibar, Masoud Mabalila. 
   Mwananchi wa eneo la Sogea, Wilaya ya Mjini Unguja, Ally Saleh Ally, akielezea kero ya uhalifu kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad (kulia),wakati wa Mkutano wa Hadhara uliokuwa na lengo la kujadili jinsi ya kukomesha matukio ya uhalifu yanayoanza kushamiri Visiwani Zanzibar.
   Mwananchi wa eneo la Sogea, Wilaya ya Mjini Unguja, Mariamu Said Ali, akielezea kero ya uhalifu kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad (kulia),wakati wa Mkutano wa Hadhara uliokuwa na lengo la kujadili jinsi ya kukomesha matukio ya uhalifu yanayoanza kushamiri Visiwani Zanzibar.
  Kamishna Msaidizi wa Polisi, Saleh Mohamed Saleh, akizungumza na wananchi wa eneo la Sogea, Wilaya ya Mjini Unguja (hawapo pichani), wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi hao ikiwa ni jitihada za Serikali kudhibiti matukio ya uhalifu yaliyoanza kushamiri katika maeneo mbalimbali  Visiwani Zanzibar.Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.

  0 0

  NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

  NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi', amesema CCM inasimamia Sera zake ipasavyo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii na kiuchumi.

  Kauli hiyo ameitoa leo katika mwendelezo wa ziara yake kwa siku ya tatu ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM Katika Baraza la Manispaa ya Magharibi 'A' Zanzibar.

  Amesema CCM inaamini kwamba suala la maendeleo kwa jamii halina itikadi za kisiasa bali linatakiwa kutekelezwa kwa wananchi wote bila ya ubaguzi, hatua ambayo imefikiwa kwa kiasi kikubwa na mfumo wa ugatuzi wa madaraka katika Serikali za Mitaa.

  Ameeleza kwamba fikra na dhana ya zanzibar kuwa 'Singapore' ya Bara la Afrika inaendelea kutekelezwa kwa vitendo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na CCM kupitia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

  Amesema sifa kuu ya viongozi wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi ni uadilifu, hekima, busara, ukweli, utu na uongozi bora katika kutatua kero za wananchi.Kupitia ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu huyo, Dk. Mabodi amewaonya baadhi ya wanasiasa wa vyama vya upinzani nchini kuacha tabia ya kupotosha umma kwa makusudi juu ya hatua kubwa za maendeleo zilizofikiwa na Serikali katika Sekta ya Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia na kueleza kuwa Sera hiyo ipo katika Ilani ya CCM na inaendelea kutekelezwa kwa kufuata matakwa ya kisheria.

  " Kuna baadhi ya watu wanaojiita wanasiasa hapa Zanzibar wao kazi yao kubwa ni kuisubiri Serikali itekeleze jambo lolote la maendeleo, na wao waibuke na kukosoa na kubeza bila ya hoja za msingi ili waweze kupata siku za kuishi kisiasa.

  Kwa hali hiyo nawambia kwamba hakuna wa kuzuia kasi ya CCM katika kuwaletea wananchi maendeleo tutaendelea kufanya mambo mbali mbali tunayoyaona yana tija kwa maslahi mapana kwa wananchi kwani CCM ndio Chama tawala tulioaminiwa na wananchi wakatupa ridhaa ya kuongoza dola.", amesema Dk.Mabodi.

  Dk. Mabodi amesema CCM haina mzaha wala haiwezi kuyumbishwa na wanasiasa waliochoka na kufilisika kifikra na kisiasa, bali itaendelea kuwa imara na kutekeleza kwa kasi maendeleo ya wananchi.Naibu Katibu Mkuu huyo, amesema kwa sasa wananchi wa maeneo mbali mbali hasa waliopo pembe zoni 'Vijijini' wananufaika sana na miradi mbali mbali ya kujikwamua kiuchumi kupitia mfumo wa ugatuzi hasa katika sekta za ufugaji,kilimo,uvuvi,afya,elimu na ujasiliamali.

  Pamoja na hayo Dk. Mabodi ameelezea kuridhishwa kwake na kasi ya utekelezaji wa Ilani ya CCM uliofanywa na Manispaa hiyo kupitia mfumo wa ugatuzi kwani umesaidia kupunguza kwa kiwango kikubwa changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi.

  Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Mhe. Ayoub Mohamed Mahmoud ameeleza kwamba kupitia mfumo huo wa ugatuzi wataimarisha huduma bora za kijamii na kupunguza hatua kwa hatua changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi.

  RC Ayoub ameweka bayana kuwa wananchi wanatakiwa kuendelea kutoa ushirikiano wa kudumu katika kulinda na kutumia vizuri miradi mbali mbali inayotekelezwa na ugatuzi ili iwe endelevu katika kuwasaidia wananchi wengi kwa mujibu wa mahitaji yao ya msingi.

  Naye Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa hiyo, Ndugu Amour Ali Mussa amesema Baraza hilo lililenga kukusanya shilingi bilioni 1,322,381,262 hadi kufikia Septemba 2018 na limefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi bilioni 1,510,357,388 sawa na asilimia 114 ambapo wamevuka malengo 
  yaliyokusudiwa.

  Amesema wameendelea kupiga hatua kubwa katika Sekta zilizogatuliwa zikiwemo elimu, Afya na kilimo ambapo wananchi wa shehia mbali mbali zilizomo katika Baraza hilo wamenufaika na fursa zilizomo katika mfumo wa ugatuzi.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya watendaji wanaohudumu katika mfumo wa ugatuzi ndani ya manispaa hiyo, pamoja na wananchi wanaonufaika na fursa zinazotokana na ugatuzi wamekiri kuwa utaratibu huo umeharakisha upatikanaji wa huduma bora za kijamii.

  Alizungumza Daktari Dhamana wa Kituo cha Afya cha Bumbwisudi Said Fadhil Abbass, amesema toka kuanzishwa kwa mfumo huo huduma za Afya zimeimarika sambamba na upatikanaji wa dawa ni kwa asilimia 99 na asilimia moja inayobaki dawa zinanunuliwa na Manispaa ya Magharibi 'A'.

  Ameitaja changamoto wanayokabiliana nayo ni upungufu wa wafanyakazi kwani wananchi wanaohitaji huduma wanakuwa wengi huku wafanyakazi wakiwa ni kidogo.Naye Afisa Mifugo wa Wilaya Magharibi 'A', Ahmada Ramadhan Nassor amesema wametoa mafunzo ya ufugaji wa kisasa kwa wafugaji mbali mbali pamoja na kujenga kituo cha kisasa kitakachotumika katika matibabu mbali mbali ya mifugo.

  Kwa upande wake Afisa Uvuvi Wilaya ya Magharib 'A' Khamis Bai amesema katika hatua za kuwawezesha wananchi ambao ni wajasiriamali wa biashara za kukausha na kuuza dagaa katika eneo la Bububu Kihinani wanaendelea kuwekewa mazingira rafiki ya kufanya kazi zao kwa ufanisi.

  Amesema kwa sasa wanatumia mashine ya kisasa ya kukaushia dagaa yenye thamani ya shilingi milioni 40 inayokausha ndoo tatu zenye kilo sitini kwa masaa matatu, ambapo bado wana mahitaji ya mashine nyingine kubwa kwa ajili ya kazi hiyo.

  Akizungumza Kaimu Mwalimu Mkuu wa skuli ya maandalizi ya Kihinani, Mwajuma Makame Issa amesema mfumo wa ugatuzi umesaidia kuimarisha miundombinu ya utoaji wa elimu, kwani kwa sasa wanapata kwa haraka vifaa mbali mbali vya kufundishia tofauti na utaratibu uliokuwepo zamani.

  Ameitaja changamoto iliyopo katika Skuli hiyo kuwa ni wingi wa wanafunzi unaosababisha vyumba vya madarasa kuwa kidogo, ambapo darasa moja linachukuwa wastani wa wanafunzi 100 kiwango ambacho ni kikubwa.
  NAIBU katibu Mkuu CCM zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla pamoja na Mkuu wa Mkoa Mjini MAGHARIB Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud wakikagua machine ya wajasiriamali wa kuuza dagaa huko Kihinani Wilaya ya Magharibi 'A' Unguja.

older | 1 | .... | 1737 | 1738 | (Page 1739) | 1740 | 1741 | .... | 1897 | newer