Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA BALOZI WA FALME ZA NCHI ZA KIARABU

$
0
0
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akizungumza na Balozi wa Falme za Nchi za Kiarabu Mhe. Khalifa Abdulrahman  Almarzooqi alipomtembelea Ofisini kwake  Jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Falme za Nchi za Kiarabu Mhe. Khalifa Abdulrahman  Almarzooqi akimuelezea jambo Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai alipomtembelea  Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai katika picha ya pamoja na Balozi wa Falme za Nchi za Kiarabu Mhe. Khalifa Abdulrahman  Almarzooqi mara baada ya kuzungumza naye Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. PICHA NA BUNGE

TAARIFA ZA MICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF).

$
0
0
MECHI ZOTE ZA LIGI KUU ZINAZOTUMIA UWANJA WA TAIFA KUCHEZWA SAA 10 JIONI 

Mechi zote za Ligi Kuu Tanzania Bara zitakazochezwa kwenye Uwanja wa Taifa,Dar es Salaam zitachezwa saa 10 jioni. 

Awali kulikuwa kuna mechi zilizopangwa kuchezwa saa 12 jioni na saa 1 usiku. 

Mechi zilizopangwa kuchezwa katika muda huo zimerudishwa saa 10 jioni kufuatia mmiliki wa Uwanja wa Taifa kutoa taarifa za kutowashwa taa za Uwanja ambazo zingehitajika kwa mechi hizo za jioni. 

Utekelezaji wa taarifa hiyo ya wamiliki wa Uwanja inaanza kutekelezwa leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Young Africans vs JKT Tanzania mchezo ambao awali ulikuwa uchezwe saa 12 jioni.

BARAZA KUU BODI YA LIGI KUFANYIKA TANGA DISEMBA 1,2018

Mkutano wa Baraza Kuu la Bodi ya Ligi (TPLB) unatarajia kufanyika Jumamosi Disemba 1,2018 Jijini Tanga. 

Mkutano huo utafanyika kwenye hotel ya Regal Naivera saa 3 asubuhi.

Aidha Mkutano huo utatumika kujaza nafasi zilizo wazi za Mwenyekiti na Mjumbe anayewakilisha klabu Ligi Daraja la Kwanza na Mjumbe anayewakilisha klabu Ligi Daraja la Pili.

Steven Mnguto ndiye mgombea pekee anayegombea nafasi ya Mwenyekiti wakati Azim Khan na Brown Ernest wakigombea nafasi ya Mjumbe anayewakilisha klabu Ligi Daraja la Kwanza na Michael Kadebe yeye akigombea nafasi ya kuwakilisha klabu Ligi Daraja la Pili. 

HATUA YA AWALI KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM KUPIGWA DISEMBA 3-4,2018


Hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)ASFC inatarajia kuchezwa kati ya Disemba 3-5,2018.

Hatua hiyo ya awali itashirikisha timu 36.

Raundi ya Kwanza itachezwa kati ya Disemba 8-9,2018 ikishirikisha timu 32.

Timu 40 zitashiriki katika raundi ya Pili itakayochezwa kati ya Disemba 14-16,2018

Bingwa mtetezi wa mashindano hayo ni timu ya Mtibwa Sugar ambayo ilicheza Fainali na timu ya Singida United kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha. 


Cliford Mario Ndimbo 
Afisa Habari na Mawasiliano,TFF 
Novemba 29,2018

NMB YAMWAGA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU ZA JWTZ, WANAJESHI WATOA TAMBO

$
0
0

Kaimu Mkuu wa Wateja Wadogo kutoka Benki ya NMB, Salie Mlay (kushoto) akimkabidhi moja ya jezi zilizokabidhiwa Kanali Damian M. Majare(katikati).

Kaimu Mkuu wa Wateja Wadogo kutoka Benki ya NMB, Salie Mlay (kushoto) akimkabidhi mipira Kanali Damian M. Majare (katikati).

TIMU za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zimepokea msaada wa vifaa vya michezo kwa ajili ya kuboresha timu zao mbalimbali zinazoshiriki katika Ligi Kuu Bara na michuano ya mbalimbali ya majeshi.

Msaada huo wenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 10 umetolewa na Benki ya NMB Tanzania, leo Jumatatu jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Kanali Damian M. Majare ambaye ni Kaimu Mwenyekiti wa Kanda ya Ngome.Akizungumza katika hafla hiyo, Kanali Damian M. Majare alisema vifaa hivyo vitawawezesha kujiimarisha kukabili michuano ya majeshi inayotarajiwa kuanza mapema mwakani.

Kwa upande wake, Kanali Erasmus Bwegoge ambaye ni Mkurugenzi wa Utimamu wa Mwili, Michezo na Utamaduni kutoka JWTZ amesema timu zitakazonufaika na msaada huo ni pamoja na timu za Ruvu Shooting, JKT Tanzania, Green Warriors, Mlale JKT ya Songea, Mgambo Shooting na baadhi ya timu ambazo zinashiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Naye Kaimu Mkuu wa Wateja Wadogo kutoka Benki ya NMB, ambao ndiyo wametoa msaada huo, Salie Mlay amesema kuwa wanalenga kuona Timu za JWTZ zikiongeza mwamko katika mashindano mbalimbali hususan mashindano ya majeshi ili waweze kuliwakilisha taifa kikamilifu.
Meza kuu ilivyoonekana mbele.

WAFANYAKAZI TISA TPA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA WIZI WA MALI,UTAKATISHAJI FEDHA

$
0
0
Na Karama Kenyunko,Blogu ya jamii 

WAFANYAKAZI tisa wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) leo Novemba 
29, 2018 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Mahakimu watatu tofauti kujibu tuhuma za wizi wa mali isafirishwayo na utakatishaji wa jumla wa zaidi ya sh. milioni 277.

Washtakiwa waliofikishwa Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile wametajwa kuwa ni Naushad Mohamed, Alfred Mhina, ,Joseph Mrema, Justine Mosha, Anuary Shampoo Pius Nyeregeti,ambapo imedaiwa na mwendesha mashtaka mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi kuwa, kati ya Agosti 30 na Sepemba 9 mwaka huu, washtakiwa walikula njama ya kuiba Mali iliyokuwa ikisafirishwa.

Imedaiwa katika shtaka la pili kuwa, Septemba 8 mwaka 2018 katika eneo la Geti namba tano la TPA lililopo wilayani Temeke, mshtakiwa Nyeregeti, alijitambulisha kama Nassoro Mohamed kwa Gaspa Swai ambaye ni Ofisa wa TRA huku akijua kuwa si kweli.

Katika shtaka la tatu, watuhumiwa hao waliiba kontena lenye nguo zenye thamani ya sh. 177,608,761 mali ya Nkonde Bright ambayo iliyokuwa ikisafirishwa kutoka Dar es Salaam kwenda Lusaka Zambia.Aidha washtakiwa hao wanadaiwa kujihusisha katika muamala uliohusiana na wizi wa nguo hizo huku wakijua mali hiyo ni zao la kosa la utangulizi la mali isafirishwayo.

Mbele ya Hakimu, Maira Kasonde imedaiwa na Wakili wa Serikali Eric Shija kuwa Septemba 18, 2018 washtakiwa Anuary Shapoo, Pius Nyeregeti, Athanas Nsenye, Yusuph Mkuja, na Ismail Hajji walikula njama ya kuiba mali iliyokuwa ikisafirishwa.Katika shtaka la pili imedaiwa washtakiwa waliiba contena lililokuwa na magunia 520 ya mahindi yenye thamani ya sh. 31,698,411 Mali ya Brian Mwacha ambayo ilikuwa ikisafirishwa kutoka Dar kwenda Zambia.

Pia washtakiwa hao wanadaiwa kubadilisha magunia hayo na na fedha kwa kuyauza huku wakijua kuwa kosa hilo ni zao la kosa la utangulizi la wizi wa mali isafirishwayo kwa dhumuni la kupotezea uhalisia wa mali.
WAFANYAKAZI tisa wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) leo Novemba 
29, 2018 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Mahakimu watatu tofauti kujibu tuhuma za wizi wa mali isafirishwayo na utakatishaji wa jumla wa zaidi ya sh. milioni 277.

WATEJA WA TIGO SASA KUFANYA MALIPO KWA KUTUMIA MFUMO WA KIELETRONIKI WA MALIPO SERIKALINI (GePG)

$
0
0
Fanya malipo ya haraka, urahisi na kwa usalama zaidi kwa zaidi ya idara 300 za serikali, mawakala na mamlaka za udhibiti kwa Tigo Pesa 

Wateja wa Kampuni ya Tigo, sasa wanaweza kufanya malipo kutumia mfumo wa Kielektroniki wa Malipo Serikalini (GePG) baada ya kampuni hiyo kuongeza malipo ya Serikalini kwenye App yake ya Tigo Pesa. 

Akiongea katika uzinduzi wa GePG kwa mtandao wa Tigo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Bernard Mabagala Afisa Mwandamizi wa TEHAMA – Wizara ya Fedha na Mipango alisema kuwa ubunifu na juhudi za Serikali katika kuanzisha mdumo huo wa Kieletronbiki wa Malipo Serikalini (GePG) umerahisisha upatikanaji wa ankara na kufanya malipo kwa wananchi. Pia imeleta faida nyinginezo ikiwemo kuboresha uwekaji wa kumbukumbu, utoaji wa taarifa, kupunguza uvuvaji na ubadhirifu pamoja na kuongeza mapato kwa idara mbali mbali za Serikali. na 

Kupitia mfumo wa GePG Serikali pia imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma kwa wananchi na kuongeza fursa za biashara kwa kampuni zinazotoa huduma za malipo kama Tigo. Wananchi wanaweza kupokea ankara zao moja kwa moja kutoka ofisi na mashirika ya Serikali au kwa njia mbali mbali za kimtandao, na kufanya malipo ya ankara kwa urahisi na mahali popote kwa njia ya simu za kiganjani, benki au kwa njia ya mtandao. 

“Kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili kufikisha huduma za kifedha kwa wananchi wengi ni moja kati ya malengo na mkakati wetu,” alisema Hussein Sayed, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za kifedha wa Tigo. 

“Zaidi ya wateja milioni 7 wanaotumia huduma yetu ya Tigo Pesa sasa wana uwezo zaidi wa kufanya malipo kwa haraka kwenda kwa taasisi, Wizara na wakala wa Serikali zaidi ya 300 kupitia Tigo Pesa USSD, Tigo Pesa App na QR Code,” alisema Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Serikali wa Tigo, Ally Maswanya. 

Baadhi ya taasisi za Serikali ambazo malipo yanaweza kufanywa kwa Tigo Pesa ni pamoja na Wizara ya Ardhi, Shirika la Kodi Tanzania (TRA), Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, Mamlaka za Miji, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Shirika la Hifadhi ya Mbuga za Taifa (TANAPA), Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Mamlaka ya Misitu (TFS), Wizara Malia Asili na Utalii, Bodi ya Utalii, Idara ya Uhamiaji, Mamlaka za Maji katika miji ya Mwanza (MWAUWASA), Tanga (Tanga UWASA), Dar es Salaam (DAWASA), Dodoma (DUWASA), Hospitali mbali mbali kama vile Muhimbili, Mwananyamala na idara nyingine zaidi ya 300. 

Ili kufanya malipo kwa kutumia Tigo Pesa App na QR Code, wateja wa Tigo wanahitaji kupakua App ya Tigo Pesa na kuscan QR code kisha kuingiza namba ya siri ili kufanikisha muamala. 


Ili kufanya malipo kwa kutumia menu ya Tigo Pesa, mteja anatakiwa kufuata hatua zifuatazo;. 

1) Kupiga *150*01# kisha kuchagua Lipa Bili 
2) Kuchagua namba 5 (Malipo ya Serikali) 
3) Kuingiza tarakimu 12 za mamlaka au taasisi anayotaka ipokee malipo 
4) Kuingiza kiasi cha fedha anachotaka kulipa 
5) Kuingiza namba ya siri kwa ajili ya kuruhusu malipo 

Kwa upande mwingine, wateja wanaweza kutumia App ya Tigo Pesa ambayo inarahisisha ufanyaji wa malipo kwa kiasi kikubwa. 

Baada ya kukamilisha malipo, wateja wa Tigo watapokea risiti ya kielektoniki kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi unaothibitisha kuwa muamala umefanyika kikamilifu. Risiti hiyo ya kielektroniki inakubalika kama uthibitisho tosha wa malipo na inaweza kusaidia kurahisisha kufuatilia malipo kwa kuwa ni rahisi kuhifadhi na kuipata pale inapohitajika ukilinganisha na risiti za karatasi ambazo ni rahisi kupotea au kuharibika. 

Tigo inawakaribisha wateja wake kuanza kutumia huduma hii ya Malipo ya Kieletroniki Serikalini (GepG) sasa. 


Mkuu wa Huduma za Biashara na Serikali wa Tigo, Ally Maswanya (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mfumo wa Malipo ya Kieletroniki Serikalini (GePG) ambao utawezesha wananchi kulipia ankara mbali mbali za kiserikali kwa urahisi na moja kwa moja kwa njia ya simu za mkononi kupitia huduma ya Tigo Pesa. Pamoja naye ni Afisa Mwandamizi wa TEHAMA katika Wizara ya Fedha na Mipango, Bernard Mabagala (kushoto) na Mkuu wa Huduma za Tigo Pesa, Hussein Sayed (kati). 
Afisa Mwandamizi wa TEHAMA katika Wizara ya Fedha na Mipango, Bernard Mabagala (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Mfumo wa Malipo ya Kieletroniki Serikalini (GePG) unaowezesha wananchi kulipia ankara mbali mbali SerikaliNI kwa urahisi na moja kwa moja kwa njia ya simu za mkononi kupitia huduma ya Tigo Pesa. Pamoja naye ni Mkuu wa Huduma za Tigo Pesa, Hussein Sayed (kati) na Mkuu wa Huduma za Biashara na Serikali wa Tigo, Ally Maswanya (kulia).
Baadhi ya wafanyakazi kutoka kampuni ya Tigo na Serikali wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya uzinduzi wa Mfumo wa Kielektroniki wa Malipo Serikalini (GePG) uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA BALOZI WA ITALIA NA BALOZI WA FALME ZA KIARABU NCHINI

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.  
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na kumkaribisha  Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MAJAMBAZI SITA SUGU WAUAWA DAR KWA KUPIGWA RISASI

$
0
0
*Wakutwa na mabomu ya kutupa kwa mkono, risasi 217,wamo Waburundi 
*Mambosasa ataja matukio ya kutisha yaliyofanywa na majambazi hayo

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limesema leo Novemba 29 mwaka huu maeneo ya Ubungo UFI jijini Dar es Salaam kupitia kikosi kazi maalum cha kupambana na ujambazi kimefanikiwa kuwaua majambazi sita.

Mbali na kuua majambazi hayo wamekamata silaha moja aina ya AK 47, risasi 11, kitambulisho chenye namba OP 0216239 kwa jina la Theophili Manirakiza mkazi wa Rukana Rugombo nchini Burundi na kitambulisho cha kazi kinachotumiwa na kikundi cha CNDD-FDD chenye jina hilo la Theopili Manirakiza katika majibizano ya risasi.

Kamanda Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amewaambia waandishi wa habari kuwa majambazi hao wameuawa baada ya mtego uliowekwa na askari kutokana na taarifa za watuhumiwa watatu waliokuwa wamekamatwa.

Amewataja watuhumiwa hao ni Willy Irakozes maarufu kwa jina la mandoo ambaye ni wa Burundi, Jean Mugisha raia wa Burudi na Mtanzania Omary Nassoro ambaye ni Mtanzania na kwamba walikuwa na bunduki tatu aina ya AK47 na magazine 8, risasi 217 na mabomu ya kutupa kwa mkono 8,ambao 

walipanga Novemba 29 mwaka huu saa 10 :30 alfajiri kufanya tukio la kumpora mfanyabiashara aliyekuwa akisafiri kuelekea Morogoro akisadikiwa kuwa na kiasi kikubwa cha fedha,Kamanda Mambosasa amesema watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kuwepo kwa matukio ya uhalifu yaliyotokea huko Mabibo External Novemba 3, mwaka 2018 ambapo 

mfanyabiashara wa Tigopesa/Mpesa aliporwa Sh.milioni 50 na huko Tegeta Novemba 15 mwaka huu mfanyabiashara raia wa China ambaye aliporwa 
Sh.milioni 10.

Pia imeelezwa kuwa jambazi Irakozes amekuwa akitafutwa kwa kufanya matukio mbalimbali ya unyang’anyi wa kutumia silaha hasa katika tukio la kuvamia Benki ya NMB Temeke ambapo aliua askari wawili .Pia Machi 15 mwaka 2011 akiwa anashikiliwa kituo cha Polisi Kagongwa Kahama kwa makosa mbalimbali yeye na wenzake walitoroka baada ya kuwaua askari 
polisi wawili na kutoroka na silaha mbili aina ya AK47. 

Mambosasa amesema matukio mengine waliyoshiriki ni pamoja na kuteka mgodi wa Tulawaka Geita mwaka 2011, kuvamia maduka ya kubadilishia fedha za kigeni huko Zanzibar.Pia mwaka 2012 walivamia kituo cha mafuta huko Kagera na kufanya mauaji, walivamia maduka yaliyopo karibu na kituo cha Polisi 

Chato na hivyo kukishambulia kituo ili kurahisisha uporaji ambapo walipora Sh.milioni tatu na mwaka 2010 walivamia mgodi wa Nyamongo na kufanya 
mauaji ya askari mmoja na kujeruhi wengine.
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kuwaua watu sita wanaosadikika kuwa Majambazi katika eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo huku miongoni mwa wahalifu hao akitambulika kuwa ni raia wa kutoka nchini Burundi akiwa na kitambulisho cha Chama cha CNDD-FDD.Pichani ni kamanda wa polisi wa kanda hiyo SACP LAZARO MAMBOSASA akizungumza na wanahabari.

Miaka Mitatu ya Rais John Magufuli-MSD yachaguliwa kuwa mnunuzi mkuu wa dawa ukanda wa SADC


Dkt. Ndumbaro atembelea Chuo cha Diplomasia

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (kulia) akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia, Dkt. Bernard Archiula mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika chuo hicho. Mhe. Naibu Waziri aliweza kutembelea maeneo mbalimbali ya chuoni hapo pamoja na kufanya mkutano na Uongozi wa chuo na Wakufunzi. Katika mkutano huo, uongozi wa chuo pamoja na Wakufunzi walitumia fursa hiyo kumwelezea Dkt. Ndumbaro changamoto wanazokabiliana nazo chuoni hapo ikiwa ni pamoja na ufinyu wa majengo kulingana na mahitaji ya chuo na uchache na uchakavu wa miundombinu ya kufundishia.

Aidha, Mhe. Naibu Waziri alitumia ziara hiyo kujua mikakati mbalimbali waliyojiwekea chuoni hapo ikiwa ni pamoja na dhamira ya kujenga majengo mapya ambayo ramani ya mchoro wa majengo hayo iliwasilishwa kwa Mhe. Naibu Waziri.

Kwa Upande wa Dkt. Ndumbaro alitumia fursa hiyo kuupongeza Uongozi pamoja na Wakufunzi wa chuo cha Diplomasia kwa kufanya kazi kwa bidii pamoja na changamoto wanazokumbana nazo. Aidha, alitoa rai kwa Uongozi wa Chuo pamoja na Wakufunzi wawe wabunifu zaidi. 
Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia, Dkt. Archiula akimwelezea jambo Dkt. Ndumbaro huku Naibu Mkurugenzi wa Masomo Prof. Kitojo Wetengere akisikiliza kwa makini. 
Balozi Charles Sanga akisalimiana na Dkt. Ndumbaro 
Dkt. Ndumbaro akisalimiana na mmoja wa wahasibu wa Chuo cha Diplomasia, Bw. Daniel Kaguo. 
Dkt. Ndumbaro akizungumza kwenye mkutanao na Uongozi pamoja na Wakufunzi wa Chuo cha Diplomasia hawapo pichani. 
Sehemu ya watumishi wa Chuo cha Diplomasia wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri, Dkt. Ndumbaro hayupo pichani alipokuwa akizungumza nao. 
Sehemu ya Wakufunzi wa Chuo cha Diplomasia, wa kwanza kulia ni Katibu wa Naibu Waziri, Bw. Charles Faini 
Mkutano ukiendelea 
Dkt. Ndumbaro akionyeshwa na kuelezewa ramani yenye mchoro wa majengo ya kisasa yatakayo jengwa katika eneo la Chuo cha Diplomasia kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam

BENKI YA NMB YATOA MAFUNZO KWA MAWAKALA WAKE SHINYANGA

$
0
0
Benki ya NMB imeendesha mafunzo kwa Mawakala NMB mkoa wa Shinyanga kwa ajili kuwajengea uwezo wa kiutendaji wafahamu mbinu za kudhibiti fedha haramu pamoja na mbinu za kukuza biashara zao kwa kuongeza wateja.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Alhamis Novemba 29,2018 katika ukumbi wa Empire Hotel Mjini Shinyanga ambapo mgeni alikuwa Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo,Melusori alisema mafunzo hayo yana lengo la kuwawezesha mawakala kukuza kipato chao lakini pia namna ya kudhibiti fedha chafu/haramu ‘Money laundering’.

“Lengo jingine ni kuwasilisha na kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili mawakala hawa,kuwapongeza/kutambua mchango wa mawakala wanaofanya kazi vizuri na kuwaeleza kuhusu maboresho yanayofanywa na NMB”,alisema Melusori.

Hata hivyo aliwataka mawakala wa NMB kufanya kazi kwa umakini na kuzingatia maadili katika utendaji kazi wao na kuhakikisha wanafuata taratibu na sheria halali za fedha.“Asilimia ya watanzania wanaotumia benki ipo chini ya asilimia 20 kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni hivyo shirikiane na benki kuhakikisha kuwa watanzania ambao hawajaanza kutumia huduma ya benki kwani benki ni sehemu salama zaidi”,aliongeza.

Kwa upande wake Meneja Mahusiano Wakala na Mauzo NMB Makao Makuu, Nehemiah Simba alisema benki ya NMB yenye matawi 228,ATM mashine 715 ina mawakala 7000 wa NMB nchini kati yao 75 ni wa mkoa wa Shinyanga.

“Nawapongeza mawakala wa Shinyanga kwa kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa NMB,tunajivunia sana kuwa na mawakala waadilifu,tumeamua kuwafikia kwani tunajali wateja wetu kwani lengo letu ni kutoa huduma bora,salama na zenye ufanisi”,alisema.

Alisema katika mafunzo hayo,miongoni mwa mada zilizotolewa ni pamoja na huduma zinazotolewa na NMB,Mawakala wa NMB,matumizi sahihi ya mashine za kutolea huduma,namna ya kupata mikopo na mbinu za kutambua na kudhibiti watakatishaji wa fedha ‘watu wabaya’.
 Picha ya pamoja baada ya mafunzo kumalizika. 
 Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori akizungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa Mawakala wa Benki ya NMB mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Novemba 29,2018 katika ukumbi wa Empire Hotel mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog  Meneja Mahusiano Wakala na Mauzo NMB Makao Makuu, Nehemiah Simba akizungumza wakati wa mafunzo kwa mawakala wa NMB mkoa wa Shinyanga.  Meneja wa Uwakala Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Tabora,Ngarami Urassa akizungumza wakati wa mafunzo kwa mawakala wa NMB mkoa wa Shinyanga.  Mawakala wa NMB wakiwa ukumbini.  Mawakala wa NMB wakiwa ukumbini.  Meneja Mahusiano Wakala na Mauzo NMB Makao Makuu, Nehemiah Simba akitoa mada kuhusu huduma zinazotolewa na benki ya NMB.  Mawakala wa NMB wakifuatilia mafunzo hayo.  Msimamizi wa Sheria,Taratibu na Kanuni benki ya NMB Kanda ya Tabora, Janeth Uiso akitoa mada jinsi ya kuzuia vitendo vya kutakatisha fedha na kuwezesha kifedha vikundi vya kigaidi.  Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori akimkabidhi zawadi ya cheti na fedha taslimu 100,000/- bi Juliana Shilatu aliyetangazwa kuwa Wakala bora wa NMB mkoa wa Shinyanga.  Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori akimkabidhi Saha Dachi and Company shilingi 75,000 mshindi wa nafasi ya pili ya wakala bora wa NMB.  Picha ya pamoja baada ya mafunzo kumalizika.  Picha ya pamoja baada ya mafunzo kumalizika. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

KAIRUKI KUWAKUTANISHA WAHITIMU WALIOSOMA CHUONI HAPO KUPITIA KONGAMANO KITAALUMA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

WATAALAMU wa afya ambao wamesoma katika Chuo kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU) wametoa mtazamo wao katika sekta ya afya huku wakijizatiti kupanua wigo wao katika kuimarisha sekta hiyo.

Wataalamu hao watakutana katika kongamano la kwanza la kitaaluma ambalo litafanyika kesho Novemba, 30 katika viwanja vya chuo kabla ya kufanyika kwa mahafali ya 16 yatakayofanyika mapema jumamosi wiki hii.

Akizungumza na waandishi wa habari Makamu mkuu wa chuo Profesa. Charles Mgone amesema kuwa kongamano hilo  litazinduliwa na katibu mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya ambapo wataalamu hao watajadili kuhusu  magonjwa yasiyoambukiza pamoja na UKIMWI. Aidha amesema kuwa kongamano hilo litawakutanisha wasomi waliosoma katika chuo hicho, wafanyakazi na wageni mbalimbali.

Kwa upande wake Naibu makamu mkuu wa chuo taaluma Profesa. Moshi Ntabaye amesema kuwa kuna vyuo vya afya 7 nchini na chuo chao kinachangia katika ufundishaji wa wataalamu wanaotakiwa kwenye sekta ya afya na kuhakikisha wanakuwa bora zaidi.

Aidha amesema kuwa wana mpango wa kujenga kampasi mpya katika eneo la Boko jijini Dar es salaam ili kuweza kuongeza uwezo wa kudahili wanafunzi wengi zaidi hasa madaktari na manesi ili kuweza kuimarisha sekta hiyo na wamewaomba wadau mbalimbali wa sekta afya kujitokeza kusaidia katika kufanikisha ujenzi wa kampasi hiyo ili kuweza kuimarisha sekta ya afya nchini.

Kwa upande wake Rais wa kongamano hilo Dkt. Leonard Malasa amesema kuwa kongamano hilo ni sehemu ya kusherekea zaidi ya miaka 20 ya hospitali hiyo huku wataalamu mbalimbali walisoma katika chuo hicho ambao wameanzisha taasisi mbalimbali za afya watatoa neno la kuwahamasisha wanafuzi chuoni hapo na hatimaye   zawadi kutolewa kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwa mwaka 2018.

Aidha amesema kuwa katika kongamano hilo wamiliki wa makampuni na taasisi za afya watapata fursa za kuonesha bidhaa zao na kutoa huduma kwa washiriki.Kuhusiana na mahafali yatakayofanyika jumamosi Makamu mkuu wa Chuo amesema kuwa jumla ya wanafunzi 230 watatunikiwa shahada za awali, uzamili, na stashahada uzamivu.

Amesema kuwa kati ya wahitimu 230 wanawake ni 126 na wanaume 
104 huku idadi ya madaktari ikiwa 153 idadi kubwa zaidi ukilinganisha na miaka iliyopita.

Pia Rais wa wanafunzi chuoni hapo Bernard Mutalemwa amesema kuwa wamefurahi sana kwa idadi kubwa ya madaktari watakaohitimu jumamosi kwa kuwa hitaji la madaktari ni kubwa zaidi.

Na kuhusiana na changamoto ya ajira Mutalemwa amesema kuwa madaktari wasibweteke kwani wanaweza kujiajiri kwa kuanzisha taasisi mbalimbali za afya na ametoa wito kwa Wizara na Serikali kuliangalia hilo ili kuweza kukuza na kuimarisha sekta ya afya nchini.
 Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki  profesa Charles Mgone katikati akizungumza na waandishi wa Habari wakati wakitambulisha kuwepo kwa kongamano la kwanza la kitaaluma la chuo hicho litakalifanyika kesho katika ukumbi wa chuo hicho jijini Dar ea Salaam. Mgeni rasmi katika kongamano hilo anatarijiwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee jinsia na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya. Kushoto kwake ni Ras wa Kongamano la kwanza la kitaaluma la Chuo cha Kairuki, Dr Leornad Malasa na kulia ni Rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho, Bernad Mutalemwa.
 Naibu Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki Dr, Moshi Ntabaye wa kwanza Kushoto akizungumza na waandishi wa Habari hawapo pichani wakati wakitambulisha kuwepo kwa kongamano la kwanza la kitaaluma la chuo hicho litakalifanyika kesho katika ukumbi wa chuo hicho jijini Dar ea Salaam. Mgeni rasmi katika kongamano hilo anatarijiwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee jinsia na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya. Kulia kwake  Rais wa Kongamano la kwanza la kitaaluma la Chuo cha Kairuki, Dr Leornad Malasa akifuatiwa na profesa Charles Mgone na wa mwisho ni Rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho, Bernad Mutalemwa.
Rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha kumbukumbu ya Hubert Kairuki  Benard Mutalemwa (kulia) akizungumza na waandishi wa Habari wakati wakitambulisha kuwepo kwa kongamano la kwanza la kitaaluma la chuo hicho litakalifanyika kesho katika ukumbi wa chuo hicho jijini Dar ea Salaam. Mgeni rasmi katika kongamano hilo anatarijiwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee jinsia na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya. Kushoto kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Kairuki profesa Charles Mgone, (Picha na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii)

TAASISI YA MIFUPA (MOI) YATAKIWA KUWASILIANA NA WATEJA KWA KWA NJIA YA SIMU

$
0
0
Na.WAMJW,Dar es Salaam

Taasisi ya mifupa (MOI) imetakiwa kuanzia leo kuwasiliana na wateja wao kwa njia ya simu pale panapotokea mabadiliko ya watoa huduma kutokuwepo mahali pa kazi ilikuepusha usumbufu wa kukaa hospitalini muda mrefu.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati alipofanya ziara katika taasisi hiyo na kukuta wagonjwa wakisubiri kwa muda mrefu kupata matibabu pamoja na vipimo.Dkt. Mpoki alisema alichokiona kwenye taasisi hiyo ni mawasiliano ambayo inasababisha wagonjwa wengi kutokupata taarifa za kutokuwepo kwa madaktari wao hivyo kufanya wagonjwa kusubiri kwa muda mrefu.

“kuanzia leo taasisi hii itawasiliana nanyi kila inapotokea changamoto inayofanya mabadiliko ya mida yenu na madaktari, mtapigiwa simu sasa wewe utafanya maamuzi yakuja au kusubiri hadi muda ulioambiwa ili uonane na daktari wako muda utakaombiwa”. Alisema Dkt. Mpoki.Aidha, aliwataka madaktari na wauguzi wawe wanawajulisha wagonjwa mapema wao kwa wale wenye simu kwani kwenye kila jarida la mgonjwa huwa wanaandika namba za simu za wateja wao.

Hata hivyo Dkt. Mpoki alisema hii ni kutokana na mkakati wa Serikali wakutatua changamoto za wananchi wanaofika kupata matibabu kwenye taasisi zake na hivyo kuboresha huduma kwa wahitaji kadri ya uwezo unavyopatikana.

Katibu Mkuu huyo alifanya ziara katika taasisi hiyo kwa kutembelea idara ya Mionzi, wagonjwa wa nje pamoja na kuongea na wagonjwa waliofika kupata matibabu katika hospitali hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiangalia mashine ya mionzi ya CT SCAN katika Taasisi ya mifupa (MOI) wakati alipoitembea ili kujionea hali ya utoaji wa huduma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Udhibiti wa Ubora wa Huduma kutoka Wizara ya Afya Dkt. Mohamed Mohamed na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya mifupa (MOI) Dkt. Samuel Swai kuhusiana na kuboresha utoaji wa huduma kwa wagonjwa wakati alipoitembelea Taasisi hiyo Leo Jijini Dar Es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na wananchi waliofika kupata huduma za uchunguzi na matibabu katika Taasisi ya mifupa (MOI) wakati alipotembelea Taasisi hiyo leo kujionea hali ya utoaji huduma.

WAZIRI ANGELA KAIRUKI, AZINDUA KITABU CHA MIAKA 10 CHA SIMULIZI ZA LUKUNDO

$
0
0
Waziri wa Madini Angela Kairuki Akikata Utepe Kuzindua Kitabu Cha Simulizi ya za Lukundo Kilichoandikwa na Mama Fatma Kange,Anayeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Same Rose Staki Pamoja na Salehe Njaa mume wa Mwaandishi wa kitabu hicho (Kushoto).Uzindui Huo Umefanyika Jijini Dar es salaam.Aidha Waziri Kairuki Amewataka Watanzania Kupenda vitu vya Nyumbani ili kuwapa Moyo watazania wenzetu katika Kazi nao na Ubunifu wao.Amepongeza Sana Mwandishi wa Kitabu Hiko Bi Fatma Kange ambaye katika Kitabu hicho amegusia Maisha na Malezi ya Kabila la Wapare..
Fatuma A. Kange, amefurahi kuzindua kazi yake kubwa “ KITABU CHA SIMULIZI ZA LUKUNDO” ambachoamekifanyia utafiti na kuelezea mambo mengi ya msingi kwa muda mrefu mno.. imemchukua takribanimiaka 10 kukamlisha kazi yake hiii kuntu! wakati wa ufunguzi Fatuma alisema amekuwa akitumia likizoyake kila mwaka anapokwenda kijijini kwao Makanya,Kimunyu Same kufanya utafiti. anasema alikuwaanaona raha kwenda kwao, kumsalimia babu yake Mzee Juma Kimomwe na bibi yake Kozaina naKorashid ambao kupita likizo hiyo, alijikita kufanya tafiti ndogondo za kitongoji cha kimunyu ambachoamelelewa na kutumia muda huo vizuri kuhifdha habari mbalimbali. maeneo aliyoyataja ni yale yoteambayo yanaizunguka kitongoji cha kimunyu kama yote ya Chome, Mwembe, Hekapombe,Mongoloma,Mnazi, Mzumura, Tae, Makuyuni, Makanya stasheni, Mgwasi na kimunyu.
Uzinduzi ulipata wafadhili wakutosha na kushukuru kwamba kazi aliyoifanya kumbe imekuwa ya faida!kitabu chake kimechambuliwa na maprofesa waliobobea katika kiswahili na kukipa kitabu hicho nguvuya kuthibitishwa na Mhe. mama Samia Suluhu Hassan-Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, ambaye amekipa heshima kubwa ya kukiandikia dibaji. 

Fatuma Kange amejionamwenye bahati kubwa sana.kikubwa katika kitabu hicho, Fatuma ameeleza masuala ya malezi kwa mtizamo wa kipare, dhana zakipare zote zililenga kumjenga mtoto wa kike, hivyo amezungumzia, kuratera, kuja ghwi, kirighi cha ngwina upendo kama ambavyo bibi yake Kozaina alimpa! mapenzi makubwa yaliyotukuka! hakuna kama bibikozaina na ndiyo maana ameona ahifadhi kumbukumbu zote alizolelewa na bibi yake katika kitabu hikikikubwa cha SIMULIZI ZA LUKUNDO. ambacho kimebeba jina la kozaina.

SERIKALI YA NORWAY YARIDHISHWA NA UKARABATI WA VITUO VYA KUZALISHA UMEME NCHINI

$
0
0


NAIBU Waziri wa Nishati wa tatu kutoks kushoto akiwa na Waziri wa Maendeleo ya Nchi ya Norway Nicolai Astrup wakimsikiliza kwa umakini Kaimu Meneja wa Pangani Hydro System Lewis Loiloi akieleza namna ya uzalishaji wao wakati wa kutembelea kituo cha New Pangani Falls, katika ziara yake ya kukagua miradi wanayoifadhili
Kaimu Meneja wa Pangani Hydro System Lewis Loiloi akieleza namna ya uzalishaji wao wakati wa kutembelea kituo cha New Pangani Falls, katika ziara hiyo kukagua miradi wanayoifadhili kushoto ni Waziri wa Maendeleo ya Nchi ya Norway Nicolai Astrup katikati ni Naibu Waziri wa Nishati Subiri Mgalu
Waziri wa Maendeleo ya Nchi ya Norway Nicolai Astrup kushoto akiteta jambo na Naibu waziri wa Nishati Subira Mgalu

Waziri wa Maendeleo ya Nchi ya Norway Nicolai Astrup kushoto akisaini kitabu cha wageni kulia ni Naibu Waziri wa Nishati Subiri Mgalu
NAIBU Waziri wa Nishati wa nne kutoka kushoto Subira Mgalu akiwa na Waziri wa Maendeleo ya Nchi ya Norway Nicolai Astrup wakimsikiliza kwa umakini Kaimu Meneja wa Pangani Hydro System Lewis Loiloi akieleza namna ya uzalishaji wao wakati wa kutembelea kituo cha New Pangani Falls, katika ziara yake ya kukagua miradi wanayoifadhili
Waziri wa Maendeleo ya Nchi ya Norway Nicolai Astrup kulia akiwa na Naibu Waziri wa Nishati Subiri Mgalu na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wakifurahia jambo wakati wakiwa eneo la Mradi
Wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kutembelea
Waziri wa Maendeleo ya Nchi ya Norway Nicolai Astrup katika akiwa na Naibu Waziri wa Nishati Subiri Mgalu kulia na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigellakushoto mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mkoani Tanga

Waziri wa Maendeleo ya Nchi ya Norway Nicolai Astrup wa pili kutoka kulia akiwa na mwenyeji wake Naibu Waziri wa Nishati Subiri Mgalu wakitazama ngoma mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege mkoani Tanga


SERIKALI ya Norway imefurahishwa na jitihada zilizofanywa na serikali nchini katika kusimamia fedha walizotoa mwaka 1995 kugharamia miradi ya ukarabati wa vituo vya kuzalisha umeme vilivyopo hapa nchini.

Akizungumza leo baada ya kutembelea kituo cha New Pangani Falls, katika ziara yake ya kukagua miradi wanayoifadhili, Waziri wa Maendeleo nchini Norway Nicolai Astrup, alisema walitoa fedha hizo kwa serikali kutokana na uhusiano uliopo baina ya mataifa hayo ikiwemo usimamizi mzuri uliofanywa na serikali ya awamu ya tano. Waziri huyo pia alisema kuwa serikali yake imeongeza mkataba wa kusaidia uwekaji wa nishati ya umeme katika maeneo ya vijiji kutoka mwaka 2020-2021 baada ya kuridhika na usimamizi mzuri uliofanywa katika ukarabati wa vituo hivyo.

“Nipo hapa Pangani Falls, Norway na Tanzania wanahusiano muda mrefu, nimekuja kufuatilia matokeo ya msaada tuliotoa mwaka 1995, kwa vituo vya kuzalisha umeme ‘Hydro Power Plants’,” alisema. Baadaye akizungumza na wananchi wa mji wa Bagamoyo wilayani Korogwe Waziri huyo alisema kwamba nishati ya umeme ni muhimu katika maendeleo ya wananchi katika kufanya shughuli zao za kiuchumi na kwamba serikali yao itanedelea kushirikiana na Tanzania kusaidia nishati hiyo.

Serikali ya Norway ilitoa kiasi fedha za Kimarekani dola milioni 126 awamu ya kwanza na kisha awamu ya pili ya ukarabati wa vituo vya kuzalisha umeme vya New pangani Falls, Kidatu, Kihansi, Nyumba ya Mungu na Mtera ukarabati uliomalizika Aprili mwaka huu walitoa jumla ya shilingi bilioni 21.

Awali akizungumza Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu alisifu juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Norway kuwekeza kwenye sekta ya nishati kwa nchi hatua ambayo imewezesha maeneo mengi kunufaika na huduma hiyo muhimu.
Licha ya kufanyia ukarabati lakini pia walishiriki katika ujenzi kwa kutoa zaidi ya asilimia 42 pamoja na Serikali ya Sweeden kwenye ujenzi wa kituo hicho hatua ambayo imesaidia kuweza kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.

Alisema serikali ya Norway ni wadau wakubwa kwenye utekelezaji wa umeme vijijini na mkoa wa Tanga ni miongoni mwa mikoa iliyopata fursa ya uwepo wa vijiji vinavyofadhiliwa na katika mradi wa umeme vijijini ujazilizi. “kwa kweli kama Naibu Waziri naishukuru sana Serikali ya Norway kwa jitihada kubwa wanazofanya kwa uwekezaji kwenye sekta ya nishati katika nchi yetu sio suala la kupeleka umeme vijijini pekee lakini wamekuwa wakiwekeza kwenye sekta za mafuta na gesi”Alisema Naibu Waziri Mgalu.

Aliongeza kuwa licha ya uwekezaji wao katika maeneo hayo lakini pia katika sekta ya nishati jadidifu kwa kuangalia maeneo yaliyopo mbali kuweza kuyawekea miundombninu ya umeme ambao umesaidia kuchochea kazi ya ukuaji wa maendeleo kwenye baadhi ya maeneo.

“Sisi tunaona katika hili wametupa fursa na wamehaidi kuendelea kushirikiana na serikali kwenye maeneo mbalimbali hasa ya vijijini kuhakikisha yanapata nishati ya umeme na wamefadhili mpaka 2021 kuona vijiji vinapata umeme”Alisema.

MABULA AZITAKA MAMLAKA ZINAZOHUSIKA NA MAJI PAMOJA NA UMEME KUFIKISHA HUDUMA KATIKA MJI WA SERIKALI IHUMWA JIJINI DODOMA

$
0
0
 Bw.Frank Mambo,mbunifu majengo kutoka Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) akimuonyesha eneo Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ,Angelina Mabula itakapojengwa ofisi za Wizara hiyo alipotembelea eneo hilo leo jijini Dodoma
Mafundi mbalimbali kutoka Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) wapo kazini katika eneo la ujenzi wa ofisa za Wizara ya Fedha na Mpango, Wizara ya Ardhi nyumba maendeleo ya makazi pamoja na Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto
Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ,Angelina Mabula akiangalia ramani ya ujenzi wa ofisi ya wizara yake katika ni Frank Mambo,mbunifu majengo kutoka Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) na kulia ni wa msimamizi mradi huo Hasani Bendera 
Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ,Angelina Mabula akiwa na Frank Mambo,mbunifu majengo kutoka Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) wakikagua maeneo ya ujenzi wa ofisi za Wizara ya Fedha na Mpango, Wizara ya Ardhi nyumba maendeleo ya makazi pamoja na Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifatilia kwa umakini maelezo ya Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ,Angelina Mabula (hayupo pichani) alipotembelea eneo zitakapojengwa ofisa za Wizara ya Fedha na Mpango, Wizara ya Ardhi nyumba maendeleo ya makazi pamoja na Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto

Msimamizi mradi huo Bw.Hasani Bendera kutoka shirika la nyumba Tanzania (NHC) akionyesha eneo itakapojengwa ofisi za Wizara ya Fedha na Mpango, Ardhi nyumba maendeleo ya makazi Mhe.Angelina Mabula alipotembelea eneo hilo leo jijini Dodoma.
Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ,Angelina Mabula akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipotembelea eneo zinapojengwa ofisi za Wizara ya Fedha na Mpango, Wizara ya Ardhi nyumba maendeleo ya makazi pamoja na Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto leo jijini Dodoma
Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ,Angelina Mabula,akimsisitizia jambo Kaimu meneja kutoka shirika la nyumba Tanzania (NHC) kutoka Dodoma kulia ni Frank Mambo,mbunifu majengo wa NHC 
Bango likionesha mji wa Serikali ambapo eneo hilo zitajengwa ofisi za wizara mbalimbali Ihumwa jijini Dodoma
Fundi kutoka NHC Yusuph Amir akizungumzia ujenzi wa ofisi ya wizara ya ardhi nyumba maendeleo ya makazi .PICHA NA ALEX SONNA WA FULLSHANGWEBLOG



Na.Alex Sonna,Dodoma

Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi imezitaka mamlaka zinazohusika na maji pamoja na umeme kufikisha huduma hizo mapema iwezekanavyo katika mji wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma ili kurahisisha ujenzi wa ofisi za Wizara kuanza.

Naibu waziri wa wizara hiyo Angelina Mabula ametoa maagizo hayo leo alipotembelea eneo zinapojengwa ofisi za Wizara ya Fedha na Mpango, Wizara ya Ardhi nyumba maendeleo ya makazi pamoja na Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto katika eneo hilo.

Mabula amesema kuwa kutokana na kasi walinayo Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) ambao ndio wanatekeleza ujenzi huo wanaweza kukwamishwa na changamoto ya maji .

“Shirika la Nyumba wako serius kweli na kazi hii maana walipewa kazi ya kujenga ofisi za Wizara tatu baada ya siku mbili tu wakaanza kufanyia kazi agizo hilo, ila changamoto inakuwa kwenye huduma ya maji na umeme ambazo hazipo katika eneo hili.

“Sasa ili kuhakikisha kuwa tunakamilisha ujenzi huu kwa wakati wa siki 30 ni lazima mamlaka husika wahakikishe wanafikisha huduma ya maji na umeme mapema iwezekanavyo, hasa maji ambayo ndio inahitajika katika hatua ya awali,” amesema Mabula.

Aidha Naibu amesema kuwa wakati wanasubiria huduma hiyo kufikishwa wataangalia namna ya kupata maji ya visima lengo ikiwa ni kukamilisha ujenzi huo kwa wakati huku akisema atatembelea tena eneo hilo baada ya wiki moja .

Kwa upande wake msimamizi wa mradi huo kutoka NHC Hasani Bendera amesema kuw wanatarajia kukamilisha mradi huo kwa muda uliopangwa bila kujali changamoto ambazo zitajitokeza.

“Tusiangalie changamoto, muda tuliopewa si tatizo kwetu kwani tumejipanga kuhakikisha kuwa tunafanya kazi hii kwa wakati, iwe usiku, mchana, kiangazi au mvua ikiwa inayesha, kazi Itafanyika na tutakamilisha kwa wakati,” amesema Bendera

Kuhusu gharama ya mradi huo Bendera amesema kuwa hadi siku ya jumapili Disemba 2, 2018 watapata jibu kamili kuwa mradi huo utagharimu kiasi gani cha fedha.

Naye fundi kutoka NHC Yusuph Amir amesema kuwa kazi ya kusafisha eneo hilo lenye ukubwa wa hekari zaidi ya 20 itafanyika kwa muda wa siku mbili huku akisema kupitia mradi huo Watanzania watapata ajira.

Katika eneo hili ambalo zitajengwa ofisi za Wizara hizo, tayari NHC wapo hatua ya kusafisha huku ujenzi ukitarajiwa kuanza rasmi jumatatu Disemba 3, 2018.

AUTOPRO YAWAPELEKA BEACH YATIMA WA 'GREEN PASTURES' DAR

$
0
0
Picha ya pamoja ya watoto yatima wa Kituo cha 'Green Pastures' cha Mapinga jijini Dar es Salaam na wadau wengine wa Kampuni ya Autopro mara baada ya kuwasili eneo la Kunduchi Beach kujumuika katika michezo anuai na watoto hao.
Sehemu ya watoto yatima wa Kituo cha 'Green Pastures' cha Mapinga jijini Dar es Salaam na wadau wengine wa Autopro wakimsikiliza Meneja Ufundi wa Autopro, Willbard Gandu (wa kwanza kulia) alipokuwa akizungumza na watoto hao mara baada ya kuwasili eneo la Kunduchi Beach kujumuika na watoto hao.
Sehemu ya watoto yatima wa Kituo cha 'Green Pastures' cha Mapinga jijini Dar es Salaam wakipata chakula Kunduchi Beach mara baada ya kujumuika na michezo mbalimbali ya watoto.

KAMPUNI ya Autopro imejumuika na watoto yatima wa Kituo cha 'Green Pastures' cha Mapinga jijini Dar es Salaam ikiwa ni tukio la kurejesha sehemu ya faida yake kwa wahitaji. Katika tukio hilo kampuni ya Autopro inayotoa huduma za 'Car service, tires, diagnosis, 3D wheel alignmnent na balance, accessories, brakes, suspension, batteries, bushes, autodetailing eneo la Goba mwisho jirani na Banki ya CRDB iliwapeleka Kunduchi Beach watoto wa kituo hicho pamoja na kujumuika katika chakula cha mchana.

Akizungumza katika tukio hilo, Meneja Ufundi wa Autopro, Willbard Gandu alisema waliamua kujumuika na watoto hao kwa pamoja na familia zao ili kuwafariji jambo ambalo ni jema katika jamii.

Muonekano wa ofisi za Autopro zinazotoa huduma za 'Car service, tires, diagnosis, 3D wheel alignmnent balance, accessories, brakes, suspension, batteries, bushes, autodetailing iliyopo eneo la Goba Mwisho jirani na Banki ya CRDB, Dar es Salaam.

Serikali Yaandaa Mtaala Utakaotumika Kuwanoa Wanasheria Wapya Katika Utumishi wa Umma

$
0
0









Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais; Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Mick Kiliba akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Dkt. Laurean Ndumbaro leo Jijini Dodoma wakati wa hafla ya ufunguzi wa kongamano la wadau kutoa maoni kuhusu mtaala wa mafunzo elekezi kwa wanasheria wapya kwenye Utumishi wa Umma.Kongamano hilo limeandaliwa na Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.
Mkuu wa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Mhe. Jaji Paul Kihwelo (PhD) akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa kongamano la wadau kutoa maoni kuhusu mtaala wa mafunzo elekezi kwa wanasheria wapya kwenye Utumishi wa Umma leo Jijini Dodoma.
Mkuu wa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Mhe. Jaji Paul Kihwelo (PhD) akisisitiza jambo kwa washiriki wa kongamano la wadau kutoa maoni kuhusu mtaala wa mafunzo elekezi kwa wanasheria wapya kwenye Utumishi wa Umma leo Jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wa wa kongamano la wadau kutoa maoni kuhusu mtaala wa mafunzo elekezi kwa wanasheria wapya kwenye Utumishi wa Umma leo Jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais; Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Mick Kiliba akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la wadau kutoa maoni kuhusu mtaala wa mafunzo elekezi kwa wanasheria wapya kwenye Utumishi wa Umma leo Jijini Dodoma.kulia ni Mkuu wa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Mhe. Jaji Paul Kihwelo (PhD).

Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) Chadhamiria Kuwajengea Uwezo waajiriwa wapya Serikalini wa Kada ya Sheria ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt . Laurean Ndumbaro wakati akifungua Kongamano la Wadau lililolenga kupitia na kutoa maoni kuhusu mtaala wa mafunzo elekezi kwa mawakili na wanasheria wa sekta ya umma, Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Mick Kiliba amesema kuwa lengo ni kuwajengeauwezo wanasheria hao ili waweze kujua mifumo ya uendeshaji wa shughuli za Serikali, Uongozi na Utumishi wa Umma.

“Lengo la kuwaandaa waajiriwa wapya wa Kada ya Sheria ni kujenga utumishi uliotukuka na bora katika Kada hii muhimu kwa maendeleo ya Taifa letu”; Alisisitiza Kiriba.Akifafanua Bw. Kiliba amesema kuwa waraka namba (5) Tano wa mwaka 2011 wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, unaoelekeza kutolewa kwa mafunzo elekezi kwa watumishi wapya katika Utumishi wa Umma.

Aliongeza kuwa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kimekasimiwa madaraka ya kuandaa na kutoa mafunzo ya awali na elekezi kwa waajiriwa wote wa kada ya Sheria katika sekta ya Umma nchini.

Aidha, Kuzinduliwa kwa mtaala huo ni utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka Mitano wa Chuo cha IJA wa 2018/19-2022/23. Katika kuandaa mtaala huo, Chuo cha IJA kilishirikiana na Wataalamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya Umma kama vile Mahakama ya Tanzania ya Tanzania na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) Mhe. Jaji Paul Kihwelo (PhD) amesema kuwa mafunzo kwa mawakili na wanasheria wa sekta ya Umma yamekuwa yakitolewa bila kuwepo kwa mtaala mahususi ambapo kwa sasa ni wakati muafaka kuwa na mtaala huo.Aliongeza kuwa kwa kuzingatia waraka namba 5 uliotolewa na Ofisi ya Rais; Utumishi na Utawala Bora kila Taasisi ya Serikali inatakiwa kuhakikisha kuwa waajiriwa wapya wa kada ya Sheria Serikalini wanapata mafunzo elekezi kupitia katika Chuo Uongozi wa Mahakama Lushoto.

Baadhi ya Mambo ya yanayoangaziwa katika mtaala huo ni pamoja na; kuwawezesha waajiriwa wapya kuelewa namna ya kuendesha shughuli za Serikali, Utumishi wa Umma, Sheria ya Utumishi wa Umma, Kanuni na taratibu, Namna ya kufanya mawasiliano ndani ya Utumishi wa Umma, kanuni na taratibu, namna ya kufanya mawasiliano ndani ya Utumishi wa Umma,pamoja na rasilimali watu.

DKT. NDUGULILE ASIKITISHWA NA UTENDAJI KAZI SEKTA YA AFYA NA MAENDELEO YA JAMII TANGA

$
0
0

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na watendaji wa Wilaya ya Lushoto wakati wa ziara yake mkoani Tanga kufuatilia utekelezaji wa utoaji huduma katika Sekta ya Afya na Maendeleo ya Jamii.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akipokea zawadi ya ua kutoka kwa mmoja wa mtoto anayeishi katika makao ya kululelea watoto yatima na wenye shida ya Irente yaliyopo Lushoto mkoani Tanga wakati wa ziara yake mkoani humo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiwa amembeba mmoja wa mtoto anayeishi katika makao ya kululelea watoto yatima na wenye shida ya Irente yaliyopo Lushoto mkoani Tanga wakati wa ziara yake mkoani humo. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW



Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amesikitishwa na utendaji kazi usioridhisha katika Sekta ya Afya na Maendeleo ya Jamii kwa mkoa wa Tanga kutokana na kutokuwa na usimamizi mzuri katika utekelezaji wa majukumu yao

Ameyasema hayo leo Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga alipofanya ziara ya kujionea shughuli zinazosimamiwa na Wizara yake katika Sekta ya Afya na Maendeleo ya Jamii na kukuta baadhi ya maafisa wahusika wakiwemo Waganga Wakuu wa Wilaya na Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Lushoto hawapo katika ziara yake..

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya Wilaya ya Lushoto amesema kuwa watendaji wa Wilaya hiyo hawako makini katika kutekeleza majukumu yao na hakuna usimamizi wa moja kwa moja katika kuhakikisha mambo yanaenda wilayani hapo.

“Nimesikiliza taarifa sijaona masuala ya Maendeleo ya Jamii na pia Afisa Maendeleo ya Jamii hayupo hapa na nimetembeela na Wilaya nyingine Waganga Wakuu wa Wilaya hawakuwepo hii inaonesha hamko makini katika kazi yenu” alisisitiza Dkt. Ndugulile

Dkt Ndugulile amesema usimamizi na uwajibikaji ni njia pekee itakayowezesha kuleta ufanisi katika kutekeleza majukumu katika Sekta zilizopo na hapo baadae itabidi kila awajibike katika ngazi yake ya uteuzi iwapo hatashindwa kutimiza majukumu yake ipasavyo.

Ametolea mfano katika taarifa ya Wilaya iliyosomwa kwake kuwa kuna baadhi ya vituo vya afya vilivyopokea hela ya ujenzi na ukatarabati wa vituo hivyo havijakamilika na vingine kutokuwa na milango ikiwa Wilaya ya Lushoto ni wazalishaji wa mbao na kusema kuwa taarifa aliyopokea imeegemea katika Sekta ya Afya na kusahau Sekta ya Maendeleo ya Jamii ambayo inasimamia masuala muhimu ikiwemo mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia, mimba na ndoa za utotoni.

Naibu Waziri Ndugulile ameupa uongozi wa Wilaya ya Lushoto mwezi mmoja kukamilisha kuweka milango katika majengo yote yaliyopo katika vituo vya Afya vilivyopokea fedha ya ujenzi na ukarabati jumla ya Shillingi Billioni 1.4.

Aidha Dkt. Ndugulile ameagiza kufanyika kwa marekebisho kasoro ndogo ndogo za kitaalam katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto ili kuongeza ufanisi katika utoaji huduma bora kwa wananchi wa Wilaya hiyo.

Akitoa maombi kwa niaba ya wananchi wa Lushoto mbele ya Naibu Waziri Ndugulile, Mbunge wa Jimbo la Lushoto Mhe. Shaban Shekilindi ameomba kupatiwa gari ya kubeba wagonjwa vifaa vya X Ray pamoja na kuogezewa watumishi ili kuendana na kasi ya utoaji wa huduma za afya katika Wilaya ya Lushoto.

Naibu Waziri Ndugulile amemaliza ziara yake ya Kikazi ya Siku kadhaa katika Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga katika kufuatilia utendaji kazi katika Sekta ya Afya na Maendelo ya Jamii.

NDITIYE: TAKUKURU FUTUATILIENI UJENZI WA GATI YA BANDARI YA LINDI

$
0
0

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye ameilekeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufuatilia na kuchunguza thamani ya fedha zilizotumika kujenga gati ya bandari ya Lindi ili kuweza kubaini kama gharama iliyotumika inaendana na ujenzi uliofanyika
 
Hayo yameelezwa na Nditiye wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa gati ya bandari ya Lindi mkoani humo ambapo amebaini kuwa kasi ya utendaji kazi kwenye gati hilo hairidhishi na kuongeza kuwa kazi ni ya mwaka mmoja ila imechukua miaka mitatu hadi sasa na bado haijakamilika. “Naielekeza TAKUKURU waje wafuatilie thamani ya fedha zilizotumika kujenga gati hili,” amesema Nditiye. 

Nditiye amesema kuwa kwa bahati mbaya miradi ya maendeleo ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) inayotekelezwa nje ya bandari ya Dar es Salaam haitekelezwi ipasavyo, tufike mahala tuheshimu fedha za Serikali na za wananchi. “Kwa bahati mbaya TPA hamfiki eneo la mradi wakati wa kuandaa nyaraka na hata ujenzi wa miradi husika inavyoendelea hivyo tunaingia hasara,”amesema Nditiye .

Mhandisi Ujenzi wa Bandari ya Mtwara Twaha Msita wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa gati hiyo kwa Nditiye amesema kuwa Kampuni ya Comfix & Engineering Ltd ilipewa kazi na TPA ya kujenga gati hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia mwezi Mei mwaka 2015 na kutakiwa kukamilika mwezi Mei mwaka 2016 kuendana na mkataba husika kwa gharama ya shilingi bilioni 3.1 ambapo baada ya muda ilionekana kazi zimeongeza na hivyo kuongezewa fedha hadi kufikia shilingi bilioni 3.5 .

Nditiye amesema kuwa tayari mkandarasi amelipwa shilingi bilioni 2.448 na kazi hiyo ilisimama kwa kipindi cha mwaka mzima mwaka 2017 na kuanza tena ambapo hadi sasa haijakamilika na imechukua kipindi cha miaka mitatu tofauti na mkataba wa awali ambapo ilitakiwa ijengwe kwa kipindi cha mwaka mmoja. “Serikali hatuwezi kuvumilia jambo hili kwa kuwa tunawatesa wananchi kwa kukosa huduma na kutumia vibaya fedha za Serikali,” amesema Nditiye
 
Naye Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga amesema kuwa bandari ya Lindi ni muhimu sana kwa uchumi wa watu wa Lindi kwa kuwa tuna korosho na kiwanda cha Jeshi cha kubangulia korosho. Amekiri kuwa kazi hairidhishi na kuna tatizo la kujaa kwa mchanga hivyo tuombe wahusika wakamilishe ili bandari hii iweze kutoa huduma kwa wananchi .

Katika hatua nyingine, Nditiye ametoa rai kwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Phillip Mpango kuwachukulia hatua watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania wa Mkoa wa Lindi wanaosimamia Bandari ya Lindi kwa kuikosesha Serikali mapato kwa kuwasaidia wafanyabiashara kukwepa kodi na kuvusha biashara za magendo. “Wafanyakazi wa TRA waliopo bandari ya Lindi wameoza, Waziri wa Fedha na Mipango tafadhali safisha uozo huo kwa kuwa wamepitisha madumu ya mafuta 650 mwezi huu Novemba yaliyopakiwa Zanzibar na kushushwa Lindi yakiwa madumu 30 tu na kusema kuwa yako tupu,” amesema Nditiye. Pia, amefafanua kuwa alimuagiza Mkuu wa Wilaya awaite ila wamedharau na hawakufika kwenye kikao na ziara yake mkoani humo. 

Vile vile, amemuelekeza Mkuu wa Wilaya hiyo kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilayani humo kudhibiti bandari bubu zilizopo na kuwachukulia hatua wafanyabiashara wasio waaminifu wanaokwepa kodi, hivyo kuikosesha Serikali mapato kwa kufanya biashara za magendo kwa kutumia bandari bubu na kushusha mizigo na bidhaa zao kwenye pori lililopo karibu na eneo la Uwanja wa Ndege wa Lindi ambapo unaweza kuhatarisha usalama wa uwanja huo
Nditiye pia amekagua uwanja wa ndege wa Mkoa wa Lindi na kuwaeleza kuwa uwanja huo umewekwa kwenye viwanja 11 na Serikali ambavyo vimepangwa kukarabatiwa na kuendelezwa na kiwanja hicho kimetengewa shilingi bilioni 2.95 na Serikali katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 za kuwezesha kuanza kwa ukarabati huo .

Vile vile, ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa gati ya bandari ya Nyamisati iliyopo Kibiti mkoani Lindi inayowawezesha wananchi kusafiri kwenda Mafia ambapo ujenzi huo ni pamoja na majengo ya ofisi, sehemu ya kupumzika abiria na vyoo na kubaini kuwa ujenzi huo unaendelea vizuri ambapo unagharimu shilingi bilioni 14.4 ambao ni wa kipindi cha mwaka mmoja ambao ulionza mwezi Machi 2018 na unatarajiwa kukamilika mwezi Machi, 2019. 

Meneja Mradi huo wa TPA, Mhandisi Erick Madinda amemueleza Nditiye kuwa mradi wa ujenzi huo unagharamiwa na TPA na tayari mkandarasi Alpha Logisitics Tanzania Ltd & Southern Engineering Company Ltd ameshalipwa shilingi bilioni 2.4 kati ya shilingi bilioni 14.4 ambazo ni gharama za ujenzi atakazotakiwa kulipwa mara kazi itakapokamilika. 
  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akitoa maelekezo kwa Mhandisi Ujenzi wa Bandari ya Mtwara, Twaha Msita (hayupo pichani) kuhusu kutoridhishwa na ujenzi wa gati ya bandari ya Lindi wakati wa ziara yake ya kukagua bandari hiyo mkoani humo. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga.

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyevaa fulana ya bluu) akikagua ujenzi wa gati ya bandari ya Lindi unaosuasua wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi huo mkoani Lindi. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia) akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa gati ya bandari ya Nyamisati wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi huo Kibiti, Lindi. Meneja Mradi wa TPA Mhandisi Erick Madinda akitoa maelezo

BENKI YA KCB TANZANIA YANDAA SEMINA ‘BIASHARA CLUB’ KWA WAFANYA BIASHARA WADOGO NA WAKATI (SME).

$
0
0
BENKI ya KCB nchini yaendesha kongamano la Biashara Club kwa mara ya pili mwaka 2018 jijini Mwanza,baada ya kongamano la kwanza likiwa na wafanyabiashara zaidi ya 200 jijini Dar es Salaam mapema mwaka huu.

Zaidi ya kutoa elimu ya usimamizi wa fedha, uendeshaji wa biashara na sheria za kodi, KCB Biashara Club pia inawawezesha wafanyabiashara kupanua wigo wa biashara zao kwa kuwakutanisha na wafanyabiashara wa nje na ndani ya nchi.

Tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2017, KCB Biashara Club imeendelea kuonyesha dhamira yake ya kukuza biashara katika sekta ya SME kwa kutoa huduma bora za kibenki kwa wafanyabiashara wadogo na wakati (SME) pamoja na kuwaonyesha mbinu za kukuza mitaji ya shughuli zao za kibiashara.

Semina hiyo iliyofanyika katika jijini Mwanza ilikusanya wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka nyanja tofauti, wakiwa na changamoto mbali mbali za kibiashara zikiwemo rasilimali, ushindani, uelewa finyu katika maswala ya kodi na nyinginezo. Nia kubwa ya KCB ikiwa ni kutaka kuwafundisha wafanyabiashara njia bora ya kukabiliana na changamoto zinazowakumba.

Akiongea katika warsha hiyo, Meneja wa Tawi Benki ya KCB Mwanza, Emmanuel Mzava aliwashukuru wafanyabiashara na wajisiriamali kwa Kujitokeza kwa wingi kuja kupata mbinu muhimu zitakazowasaidia katika kukabiliana na changamoto za kibiashara.

“Mtegemee semina kama hizi kwa siku za mbeleni kwani Mwanza ni jiji linaloonyesha kushamiri kibiashara” aliongezea Mzava.NayeSwetbert Thomas ambaye ni mtaalamu wa mswala ya kodi aliyealikwa na KCB kwa ajili ya kutoa mafunzo katika warsha hiyo aliwahimiza wafanyabiashara hao kuhusu muuhimu wa kuelewa mifumo ya kodi hapa nchini na ni kwa namna gani unagusa biashara zao.

Mbali na kufaidika na ujuzi wa mambo kupitia semina na safai mbalimbali zinazoandaliwa na kitengo cha “Biashara Club”, wanachama pia watafaidika kwa kujenga uhusiano wa kibiashara baina yao ambao utapelekea wao kuongeza si ujuzi wa kibiashara tu, bali pia kupanua wigo wa biashara zao. KCB Bank inatambua umuhimu wa wafanya biashara wadogo na wakati katika kukuza uchumi wa nchi lakini pia inatambua kwamba uchumi hautakuwa kama wafanya biashara hao hawatakuwa na nyenzo sahihi za kibiashara.
Mkuu wa Kitengo cha wafanyabishara wadogo na wa kati Abdul Juma akizungumza na wafanyabiashara wa jiji la Mwanza katika hafla ya Biashara Club Workshop iliyofanyika Gold Crest Hotel tarihe 29.11.2018. Hafla hiyo iliyohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 200 ilikuwa na lento la kutoa mafunzo katika maswala ya usimamizi wa fedha,uendeshaji wa biashara na sheria zinazohusu kodi.
Meneja wa Mauzo ya Kibiashara wa Benki ya KCB Lightness May kijibu maswali kutoka kwa wafanyabiashara wa jiji la Mwanza katika hafla ya Biashara Club Workshop iliyofanyika Gold Crest Hotel tarehe 29.11.2018 jijini Mwanza. Hafla hiyo iliyohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 200 ilikuwa na lengo la kutoa mafunzo katika maswala ya usimamizi wa fedha,uendeshaji wa biashara na sheria zinazohusu kodi.
Wafanyabiashara wakiwa wanaendelea kufuatilia semina.
Wafanyakazi wa Benki ya KCB wakiwa katika picha ya pamona wakati wa utambulisho.
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live




Latest Images