Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1735 | 1736 | (Page 1737) | 1738 | 1739 | .... | 1898 | newer

  0 0
  0 0


  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiangalia moja ya tairi lilipo katika kiwanda cha Matairi cha General Tyre Arusha wakati wa ukaguzi wa Miradi yenye hisa NSSF tarehe 26 Novemba, 2018.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiweka saini katika kitabu cha wageni katika ofisi za kiwanda cha General Tyre alipotembelea kukagua miradi yenye hisa NSSF pamoja na kuona hali halisi ya kiwanda hicho.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiangalia malighafi zinazotumika kutengeneza matairi na zilizohifadhiwa katika chumba maalumu katika kiwanda hicho.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama pamoja na Watendaji kutoka NSSF na baadhi ya viongozi wa kiwanda cha Matairi cha General Tyre wakiangalia hali ya miundombimu katika kiwanda hicho.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiuliza jambo kwa Mkurugenzi wa Uwekezaji NSSF Bw.Gabriel Silayo (wa kwanza kushoto) wakati wa ziara yake katika moja ya mradi wenye hisa za shirika hilo
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (katikati) akiwa katika ziara yake katika kiwanda cha matairi cha General Tyre Arusha.wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji NSSF Bw.Gabriel Silayo.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akieleza jambo kwa watendaji wa NSSF wakati wa ziara yake katika kukagua sehemu ya miradi yenye hisa za shirika hilo ikiwemo kiwanda cha General tyre.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akisisitiz ajambo wakati wa ziara hiyo. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

  0 0


  Akikagua kituo binafsi cha kuzalisha umeme cha Mwenga ambacho kinazalisha megawati 4 na kuunganishwa umeme vijiji 32
  IMG_7991-min
  Naibu Waziri akicheza na wananchi wa kijiji cha Ikondosi wilayani mufindi
  IMG_7958-min
  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumzia mikakati ya serikali ya kuwafikishia wananchu umeme wa uhakika na kwa gharama nafuu, Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa iringa, Ally Happi

  0 0

  Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

  NAIBU Waziri wa Kilimo Omari Mgumba ametoa onyo kali kwa madalali wanaowauzia wakulima wa mazao ya chakula,biashara na mbolea kwa bei ya Sh.70,000 badala ya kufuata bei elekezi ya Sh.64,700 kwa mfuko mmoja .

  Akiwa Katika ziara mkoani Iringa  ya ukaguzi wa upatikanaji wa mbolea kwenye maghala ya  Serikali na wawekezaji  waliopo mkoani hapa.

  Naibu Waziri huyo was Kilimo amewataka madalali hao kuacha mara moja tabia hiyo kwani   Serikali ya Awamu ya Tano chini ya  Rais Dk.John Magufuli haina utani katika kuwasaidia watu maskini na wanyonge.Ameamua kutoa onyo hilo baada ya wananchi wa kijiji cha Ngulwe wilayani Kilolo kutoa malalamiko yao wakati wa kikao kilichowahusisha wakulima ,wadau pamoja na Naibu Waziri hugo.

  “ Wananchi nimeskia malalamiko yenu kuhusu bei ya mbolea, nitoe rai kwa wauzaji wa mbolea nchi nzi.a kufahamu atakeyeuza mbolea kwa bei tofauti na elekezi iliyopangwa na Serikali tutamchukulia hatua za kisheria,"amesema Mgumba.Aidha amewatoa hofu wakulima wote nchini kuhusu upatikaji wa mbolea katika  kipindi cha kuelekea msimu wa kilimo na kwamba Serikali imejidhatiti kikamilifu na mbolea ipo ya kutosha.

  Imeelezwa wakulima wengi nchini wamekuwa katika  changamoto ya upatikanaji wa mbolea ambapo hapo awali kulikuwa na  Mbolea waagizaji zaidi ya mmoja hali iliyosababisha usumbufu kwa wakulima  na kwa bei ya juu.Kutokana na hiyo Serikali kuingilia  kati kwa kuweka Wakala Maalum wa kuagiza  mbolea kutoka nje ya nchi na kutoa bei elekezi kwa wauzaji.


  Naibu Waziri Omari Mgumba akizungumza na Wakulima wa Kijiji cha Ngulwe.
  Naibu Waziri Omari Mgumba akipata maelezo mafupi kutoka mmoja wa wauzaji wa Mbolea.
  Naibu Waziri Omari Mgumba akikagua Maghara ya kuhifadhia Mbolea mkoani Iringa.

  0 0


  Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akiwa na Mhandisi wa Wilaya ya Kakonko (kushoto), Mbunge wa Jimbo la Buyungu, Mhandisi Christopher Chiza (kulia) pamoja na na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala kwenye Mradi wa Maji wa Gwanumpu katika Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma.
  Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wakazi wa Kijiji cha Muhange wakati alipofanya ziara kwa lengo la kujua hali ya upatikanaji wa maji katika kijiji hicho.
  Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (mwenye kofia) akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Buyungu, Mhandisi Christopher Chiza wakiwa pamoja na na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala kwenye Mradi wa Maji wa Nyagwijima katika Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma.
  Mbunge wa Jimbo la Buyungu, Mhandisi Christopher Chiza akimuongoza Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa wakitoka kwenye Chanzo cha Maji cha Mugembezi kinachotumika kwa ajili ya Mradi wa Maji wa Muhange wilayani Kakonko, mkoani Kigoma.
  Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akiwa na akina mama kijijini Kiga mara baada ya kujionea mradi wa Kiga na kuzungumza na Jumuiya ya Watumiaji Maji wa Mradi wa Maji wa Kiga katika Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma.

  ……………….

  Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa amefanya ziara katika Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maji kwa lengo la kuhakikisha lengo la Serikali kuwapatia wananchi huduma ya majisafi na salama linatimia.

  Akiwa wilayani humo Profesa Mbarawa amejionea changamoto mbalimbali zinazosababisha utekelezaji usioridhisha na kuwataka watendaji wa wilaya hiyo kuchukua hatua sahihi ili kuwezesha miradi hiyo kukamilika, ambapo baadhi yake imeanza mwaka huu na mingine ni ya muda mrefu.

  Profesa Mbarawa ametembelea miradi ya Kakonko Mjini, Muhange, Kiga, Gwanumpu na Nagwijima kwa lengo la kujionea hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi wa miradi hiyo. Akizungumza na watendaji wa Wilaya ya Kakonko, Profesa Mbarawa amewataka watendaji hao kuhakikisha wanachukua hatua, ikiwemo kuvunja mikataba ya wakandarasi wanaoonekana kukosa uwezo wa kutekeleza miradi hiyo kwa kufuata taratibu za kisheria na kutafuta wakandarasi wanaoweza kufanya kazi nzuri.

  Profesa Mbarawa amesema anataka kuona miradi yote wilayani Kakonko inakamilika kwa wakati ikiwa ni sehemu ya kutekeleza lengo la Serikali kutoa huduma ya majisafi na salama kwa wananchi kwa kuwa fedha za kutimiza lengo hilo zipo, hivyo haoni sababu ya kutokukamilika kwa miradi ya maji.

  Huku akitaka kuwe na mawasiliano mazuri kila baada ya miezi miwili kati ya watendaji, wabunge na viongozi wa Serikali kuhusu maendeleo ya miradi kwa kila hatua ya utekelezaji. Wakati huo, Mbunge wa Jimbo la Buyungu, Mhandisi Christopher Chiza amesema utendaji wa wataalamu umekuwa kikwazo kikubwa kwa Serikali, kutokana na kutokufuatwa kwa taratibu sahihi za manunuzi na usimamizi mbovu wa miradi ya maji.

  Mhandisi Chiza amewaasa watendaji wa Serikali wenye dhamana ya usimamizi wa miradi ya maji kutumia taaluma zao vizuri ili kupata matokeo chanya kwenye miradi ya maji.

  0 0  0 0

  Waziri wa kilimo Mh Japhet Hasunga akizungumza wakati wa ufunguzi wa Warsha ya Kitaifa ya wadau wa Kilimo iliyoandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania ambapo amewataka wakulima kulima Kilimo chenye tija.
  Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya baraza la kilimo Tanzania Dkt Sinare Yusuph Sinare akizungumza wakati muda mfupi kabla ya kumakribisha waziri waziri wa Mh Japhet Hasunga kufungua warsha ya kitaifa ya wadau wa kilimo, ambapo Dkt Sinare alisema ili sera ya viwanda ifanikiwe ni muhimu kilimo kikaunganishwa na viwanda.
  Mwenyekiti wa TPSF Bw Salum Shamte ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Baraza la Kilimo, Bi Jacqueline Mkindi Makamo Mwenyeki wa Bodi, na Mwenyekiti Dkt Sinare Yusuph Sinare wakifurahia jambo wakati wa ufunguzi wa Warsha ya Kitaifa ya wadau wa Kilimo, iliyoandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania.
  Baadhi ya washiriki wa warsha ya kitaifa ya Kilimo iliyoandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania wakifuatilia kwa umakini uwasilishwaji wa mada mbalimbali wakati wa warsha ya siku mbili inayofanyika Dar es Salaam. 
  M/kiti wa bodi ya wakurugenzi wa baraz la kilimo, bi Jacqueline Mkindi akiteta jambo na mwenyeki wa bodi dkt sinare yusuph wakati wa warsha ya kitaifa ya wadau wa kilimo iliyoandaliwa na baraza la kilimo Tanzania, anayefutia ni Waziri wa Kilimo Mh Japhet Hasunga.
  Sehemu ya washiriki wa warsha ya kitaifa ya wadau wa kilimo wakifuatilia mjadala kuhusu sera za kilimo, warsha hiyo ya siku mbili iliyoanza leo jijini dare s salaam imeandaliwa na abraza la kilimo Tanzania.

  0 0

   Katibu  Tawala  wa wilaya ya Kasulu aliyemuwakilisha Mkuu wa wilaya hiyo mkoani Kigoma, Titus Mguha (wa tatu kushoto) akipeana mkono na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu (kushoto) wakati wa kupokea sehemu ya msaada wa vifaa tiba maalumu kwa Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti) vilivyotolewa na Taasisi ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi Doris Mollel kwa wadi ya Hospitali inayohudumia kambi wakimbizi ya Nyarugusu, Kasulu mkoani Kigoma hivi karibuni. Wa pili kushoto ni Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel na katikati ni Afisa Msimamizi wa Kambi hiyo, Francis Chokola.
  Katibu  Tawala  wa wilaya ya Kasulu aliyemuwakilisha Mkuu wa wilaya hiyo mkoani Kigoma, Titus Mguha (wa tatu kulia) akizungumza wakati akitoa shukrani kwa Taasisi za Vodacom Tanzania na Taasisi Doris Mollel kwa msaada walioutoa kwenye hospitali hiyo.
  Katibu  Tawala  wa wilaya ya Kasulu aliyemuwakilisha Mkuu wa wilaya hiyo mkoani Kigoma, Titus Mguh, akiwa ameambatana na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu na Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel wakimjulia hali mama aliyejifungua mtoto Njiti katika Hospitali inayohudumia kambi wakimbizi ya Nyarugusu, Kasulu mkoani Kigoma hivi karibuni, ambapo pia walimzawadia khanga kama sehemu ya faraja kwake.
  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme katika kuhakikisha mkoa wake unawezesha wanafunzi wote watakaochaguliwa kuingia kidato cha kwanza mwaka 2019 wanapata nafasi ya kusoma kwenye madarasa ya kutosha,amesitisha likizo zote za watendaji wakuu wa mkoa na wilaya ili wasimamie ujenzi wa madarasa mapya kwenye shule za sekondari. 

  Mndeme ametoa agizo hilo jana wakati wa kikao chake na viongozi na watendaji wa taasisi za umma na binafsi kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea na kuwataja viongozi ambao hawapaswi kwenda likizo hadi vyumba vipya 142 vikamilike kujengwa/

  Viongozi walizuiwa likizo ni Katibu Tawala Mkoa,Wakuu wote wa wilaya,wakurugenzi wa Halmashauri ,Afisa Elimu Mkoa na wale wa wilaya zote pia wahandisi wa ujenzi wa halmashauri.“Nataka katika halmashauri zote zenye upungufu wa vyumba madarasa hakuna kiongozi kwenda likizo ya mwisho wa mwaka hadi madarasa mapya yakamilike kujengwa ili wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2019 waingie darasani ” alisema Mndeme.

  Awali akitoa taarifa fupi ya hali ya hali ya miundombinu ya madarasa Katibu Tawala Mkoa Prof Riziki Shemdoe alisema jumla ya wanafunzi wapya 1,556 watahitaji madarasa mapya ya kidato cha kwanza kwenye shule za sekondari . 

  Prof.Shemdoe amezitaja halmashauri zenye upungufu wa madarasa na idadi kwenye mabano kuwa Tunduru(35),Mbinga (18),Songea (09),Songea Manispaa (09),Namtumbo (26) Halmashauri zingine zenye upungufu ni Nyasa (32),Mbinga Mji (09) na Madaba (04).

  Aidha mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mndeme amezuia safari za mafunzo za madiwani wote katika halmashauri nane za Ruvuma hadi watoto wote watakaochaguliwa kuingia kidato cha kwanza hapo mwakani watakapoingia darasani.
  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akiongea na watendaji wa Mkoa na wilaya jana kuhusu maandalizi ya mapokezi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza 2019.Kulia aliyekaa ni Mkuu wa wilaya ya Songea 

  0 0
  Mratibu wa ASDP 2 Mhandisi January Kayumbe akiwasilisha Mada ya fursa ya Sekta binafsi katika utekelezaji wa ASDP 2 katika warsha ya siku mbili ya wadau wa Kilimo iliyoandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania, ambapo ameonyesha fursa nyingi zinazopaswa kutumiwa na sekta binafsi katika Mpango huo wa Pili wa Kilimo nchini.
  Mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya baraza la kilimo Tanzania Bw. Julias Nyabicha na Mh Jitu Soni ambaye ni Mjumbe wa Bodi Mstaafu wakifuatilia kwa karibu uwasilishwaji wa Mada mbalimbali katika Warsha ya wadau wa Kilimo iliyoandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania.
  Sehemu ya wadau wa Kilimo nchini wanaoshiriki Warsha ya Kitaifa ya wadau wa Kilimo inayofanyika Jijini Dar es Salaam wakifuatilia Warsha hiyo iliyoandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania yenye kauli mbili ya Kilimo na Maendeleo ya Viwanda Tanzania.
  Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya baraza la kilimo Tanzania Dkt Sinare Yusuph Sinare akiwa na wadau wengine wa kilimo wakifuatilia warsha ya wadau wa kilimo iliyoandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania.
  Makamo Mwenyeki wa SACAU Bi Doreen Hlatshwayo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania Bi Janeth Bitegeko wakifautilia uwasilishwaji wa mada za kilimo kwa wadau wa walioshiriki warsha ya siku mbili ya wadau wa kilimo iliyoandaliwa na Baraza la Kilimo Tanzania.

  0 0

  Nahodha wa timu ya mpira wa miguu ya Diamond Trust Bank (DTB), David Kikambako (mwenye jezi ya kijani) akiwaongoza wachezaji wake kusalimiana na timu pinzani ya Kumbukumbu FC kabla ya kuanza kwa mechi ya ligi ya daraja tatu kwa Wilaya ya Kinondoni iliyopigwa jana katika Uwanja wa Chuo cha Sheria jijini Dar es salaam. DTB iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kumbukumbu FC.
  Kocha msaidizi wa timu ya mpira wa miguu ya Diamond Trust Bank (DTB), Kambi Mzee Kambi akizungumza na wachezaji wake wakati wa mechi ya ligi ya daraja la tatu kwa wilaya ya Kinondoni iliyopigwa katika Uwanja wa Chuo cha Sheria jana jijini Dar es salaam. DTB FC ilishinda 4-0 dhidi ya Kumbukumbu FC.

  Kocha msaidizi wa timu ya mpira wa miguu ya Diamond Trust Bank (DTB), Kambi Mzee Kambi akiongoza dua kabla ya mechi ya ligi ya daraja la tatu kwa wilaya ya Kinondoni iliyozikutanisha Timu ya mpira wa miguu ya DTB na Kumbukumbu FC. Mechi hiyo iliyopigwa katika Uwanja wa Chuo cha Sheria jana jijini Dar es salaam ambapo DTB iliibuka na ushindi wa mabao 4-0.
  Mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Diamond Trust Bank (DTB), Hussein Khamis akiwania mpira na mchezaji wa Kumbukumbu FC, Shauri Abbas wakati wa mechi ya ligi ya daraja la tatu kwa wilaya ya Kinondoni iliyopigwa katika Uwanja wa Chuo cha Sheria jana jijini Dar es salaam. DTB iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kumbukumbu FC.
  Mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Diamond Trust Bank (DTB), Hussein Juma akiwania mpira na mchezaji wa Kumbukumbu FC, Musa John wakati wa mechi ya ligi ya daraja la tatu kwa wilaya ya Kinondoni iliyopigwa katika Uwanja wa Chuo cha Sheria jana jijini Dar es salaam. DTB iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kumbukumbu FC.
  Kocha msaidizi wa timu ya mpira wa miguu ya Diamond Trust Bank (DTB), Kambi Mzee Kambi akizungumza na wachezaji wake wakati wa mapumziko katika mechi ya ligi ya daraja la tatu kwa wilaya ya Kinondoni iliyopigwa katika Uwanja wa Chuo cha Sheria jana jijini Dar es salaam. DTB iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kumbukumbu FC. Anayeshuhudia kulia ni Kocha mkuu wa timu ya hiyo, Michael Lugalela.

  0 0

  *Ni wa Imalabupina/Ichwankima wenye thamani ya sh. bil. 8.28

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameweka jiwe la msingi mradi wa maji wa Imalabupina/ Ichwankima wilayani Chato ambao una thamani ya sh. bilioni 8.28 na amewaagiza viongozi wa wilaya hiyo wahakikishe unakamilika kwa wakati.
  Waziri Mkuu amesemaSerikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na maeneo yao ya makazi. Ameyasema hayo leo (Jumanne, Novemba 27, 2018) alipozungumza na wananchi kwenye kijiji cha Nyamirembe baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi katika mradi huo wa maji wakati akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Geita.

  Amesema Serikali imedhamiria kuhakikisha wananchi wote nchini wakiwemo na wa wilaya ya Chato mkoani Geita wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao, hivyo amewataka waendelee kuwa na imaji na Serikali yao. “Serikali ya Awamu ya Tano ina mikakati mizuri inayolenga kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwenye maeneo mbalimbali nchini vikiwemo na vijiji vya wilaya ya Chato ili kuwawezesha wananchi kupata maji.”

  Waziri Mkuu ameagiza mradi huo ukamilike kwa wakati kwa kuwa Serikali inahitaji kuona wananchi wakinufaika na huduma hiyo. Mradi huo ulianza kujengwa Mei, 2017 na ulitakiwa ukamilike Mei, 2018 ila kutokana na changamoto mbalimbali unatarajiwa kukamilika Februari 2019. Awali,Mkuu wa wilaya ya Chato Mhandisi, Mtemi Simeon alisema mradi huo unatarajiwa kuhudumia watu takribani 59,609 katika vijiji 11 vilivyopo kwenye kata nne za Nyamirembe, Ichwankima, Kachwamba na Kasenga.

  “Vijiji vitakavyonufaika na mradi huu ni Nyamirembe, Kalebezo, Nyambiti, Busalala, Imalabupina, Ichwankima, Kachwamba, Ipandikilo, Idoselo, Igagula na Mwangaza. Tayari vituo 240 vya kuchotea maji vimeshakamilika na matenki nane kati ya tisa yamekamilika pamoja na mabirika 10 ya kunyweshea mifugo.”
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Viongozi wa Dini wakati alipowasili kwenye eneo la Mradi wa Maji wa Imalabupina - Ichwankima kuweka jiwe la msingi la Mradi huo wilayani Chato, Novemba 27, 2018. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Mradi wa Maji wa Imalabupina - Ichwankima wilayani Chato Novemba 27, 2018. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwita Waitara na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandishi Robert Gabriel. (Picha na Ofisi ya Naziri Mkuu)

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 27 Novemba, 2018 amefungua maktaba mpya, kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam iliyojengwa katika Kampasi Mlimani                           (
  Mwl. Julius K. Nyerere) Jijini Dar es Salaam.
  Maktaba hiyo kubwa Afrika Mashariki na Kati imejengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 93.6 ikiwa ni msaada kutoka Serikali ya China na inakuwa maktaba kubwa kuliko maktaba zote ambazo China imezijenga barani Afrika.
  Katika taarifa yake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam               Prof. William Anangisye amesema majengo ya maktaba hiyo yenye ghorofa mbili yamechukua eneo lenye ukubwa wa meta za mraba 20,000 yakiwa na uwezo           wa kuhifadhi vitabu 800,000, kukalisha watumiaji 2,100 kwa wakati mmoja, yana kompyuta 160 zilizounganishwa na mtandao kwa ajili ya kusoma vitabu kwa njia     ya kielektroniki, ofisi za wafanyakazi, eneo la wanafunzi wenye mahitaji maalum na ukumbi wa kisasa wa mihadhara wenye uwezo wa kuchukua watu 600.
  Prof. Anangisye ameishukuru Serikali kwa mchango mkubwa uliosaidia kufanikisha ujenzi wa maktaba hiyo, ameishukuru Serikali ya China kwa kutoa msaada wa fedha za ujenzi huo na kampuni ya ujenzi ya Jiangsu Jiangdu ya China kwa kujenga majengo yenye ubora na hadhi ya hali ya juu.
  Ameahidi kuwa Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam itahakikisha majengo   ya maktaba hiyo yanatunzwa vizuri na maktaba inatumika kuwanufaisha wanafunzi wa chuo hicho pamoja na wanafunzi wa taasisi zingine za vyuo na wananchi            wa kawaida.
  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa namna anavyotoa kipaumbele kwa sekta ya elimu              na ameahidi kuwa wizara yake itaendelea kuhakikisha taasisi zote zilizo chini ya wizara hiyo zinaendeshwa kwa kuzingatia maadili na matumizi bora ya rasilimali, pia amemshukuru Balozi wa China hapa nchini Mhe. Wang Ke kwa kusimamia     na kufuatilia kwa ukaribu ujenzi wa maktaba hiyo na kwa Serikali ya China kutoa shilingi Bilioni 50.8 kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha elimu ya mafunzo ya ufundi stadi (VETA) Mkoani Kagera.
  Akizungumza katika sherehe hizo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania   Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemshukuru Balozi wa China hapa nchini Mhe. Wang Ke na kumuomba apeleke shukrani za Tanzania kwa Rais wa China Mhe. Xi Jinping kwa misaada ambayo China imekuwa ikiitoa kwa Tanzania, ikiwemo ujenzi wa Maktaba hiyo na Chuo cha VETA kitakachojengwa Mkoani Kagera.
  Mhe. Rais Magufuli amesema urafiki wa China na Tanzania ulioasisiwa na Baba    wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Mwenyekiti Mao Zedong umeendelea kuleta manufaa makubwa na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano       na itauendeleza na kuukuza uhusiano na ushirikiano huu mzuri.
  “Jambo la kufurahisha ni kwamba misaada yao haiambatani             na masharti. Wenyewe wakiamua kukupa wanakupa, walitujengea TAZARA, URAFIKI na pia wametusaidia katika maeneo mengine       ya maendeleo” amesema Mhe. Rais Magufuli na kumhakikishia Mhe. Balozi Wang Ke kuwa Serikali itahakikisha kila msaada unaotolewa unatumiwa vizuri.
  Aidha, Mhe. Rais Magufuli amempongeza Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne       Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mstaafu Prof. Rwekaza Mukandala kwa kuandaa mpango wa ujenzi wa maktaba hiyo, na pia amewapongeza Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kupata maktaba ambayo itawasaidia kuongeza kiwango cha ubora wa elimu.
  Amewataka wana Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuhakikisha maktaba hiyo inatunzwa vizuri na ametoa wito kwa Watanzania kujifunza lugha ya Kichina katika jengo mojawapo la maktaba hiyo litakalokuwa likifundisha lugha hiyo kwa kuwa kuna manufaa makubwa kwa Watanzania kujifunza lugha hiyo.
  Sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Balozi wa China hapa nchini Mhe. Wang Ke, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Mawaziri Wakuu Wastaafu Mhe. Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba           na Mhe. Edward Ngoyai Lowassa, Mawaziri, Mabalozi wa nchi mbalimbali na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda.

  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam
  27 Novemba, 2018
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke kuashiria ufunguzi wa Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2100 kwa wakati mmoja. Wengine katika picha wanaoshuhudia ni Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Mama Kate Kamba, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam Profesa William Anangisye
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea mfano wa funguo kutoka kwa Balozi wa China hapa nchini Wang Ke kuashiria ufunguzi wa Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2100 kwa wakati mmoja huku viongozi wengine wakipiga makofi.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika hafla hiyo ya ufunguzi wa Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya Vitabu kutoka kwa Balozi wa China hapa nchini Wang Ke kabla ya ufunguzi wa Maktaba hiyo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisoma moja ya kitabu kilichomo katika Maktaba hiyo mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kabla hajaifungua rasmi huku Balozi wa China hapa nchini Wang Ke akitazama.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akirudisha kitabu hicho kwenye shelfu la vitabu mara baada ya kukisoma huku Balozi wa China hapa nchini Wang Ke akiangalia. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia moja ya kompyuta zinazohifadhi vitabu (onlinebooks) ambazo wanafunzi watakuwa wakijisomea pamoja na kupata huduma ya mtandao internet.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Msataafu Edward Lowassa mara baada ya kuwasili katika eneo la Maktaba mpya katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


  0 0

  Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama akizungumza na Ujumbe Mkubwa wa Sekta Binafsi za mafuta na Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano kutoka nchini Uganda waliotembelea Bandari ya Tanga na  kuvutiwa kuitumia Bandari ya Tanga kupitisha bidhaa zao kutokana na uwezo wa kupunguza gharama kwa zaidi ya asilimia 30 mpaka 45 ikiwemo kutumia muda mfupi kuhudumia shehena.
   MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akizungumza na UJUMBE Mkubwa wa Sekta Binafsi za mafuta na Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano kutoka nchini Uganda waliotembelea Bandari ya Tanga na maeneo mengine
   MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akisalimiana na UJUMBE Mkubwa wa Sekta Binafsi za mafuta na Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano kutoka nchini Uganda waliotembelea ofisini kwake kabla ya kutembelea Bandari ya Tanga na maeneo mengine
   UJUMBE huo wa Sekta Binafsi za mafuta na Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano kutoka nchini Uganda waliotembelea Bandari ya Tanga na maeneo mengine wakitoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella mara baada ya kufanya naye mazungumzo
  Mmoja wa wajumbe wakitoa ufafanuzi kwa baadhi ya mambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
   Sehemu ya ujumbe huo wakifuatilia kwa umakini mazungumzo hayo
   Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama katika akiwa na baadhi ya wajumbe wakiwa eneo la  yatakapojengwa matenki makubwa ya mafuta ghafi yatakayotoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga eneo la Chongoleani.
  Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama kushoto akitoa maelezo kwa  wajumbe hao wakati  wakiwa eneo la  yatakapojengwa matenki makubwa ya mafuta ghafi yatakayotoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga eneo la Chongoleani.
  Wakipata maelezo kutoka kwa Viongozi wa Bohari ya Mafuta Mkoani Tanga GBP
   Ujumbe huo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kutembelea eneo la Chongoleani Jijini Tanga
   Wakipata maelezo kutoka kwa Viongozi wa Bohari ya Mafuta Mkoani Tanga GBP
   Wakipata maelezo kutoka kwa Viongozi wa Bohari ya Mafuta Mkoani Tanga GBP

  NA MWANDISHI WETU, TANGA.

  UJUMBE Mkubwa wa Sekta Binafsi za mafuta na Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano kutoka nchini Uganda leo wametembelea Bandari ya Tanga huku wakionyesha nia yao ya kutumia Bandari ya Tanga kupitisha bidhaa zao kutokana na uwezo wa kupunguza gharama kwa zaidi ya asilimia 30 mpaka 45 ikiwemo kutumia muda mfupi kuhudumia shehena.

  Hayo yalisemwa na Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama mara baada ya ujumbe huo kutembelea Bandari ya Tanga ikiwemo maeneo yatakapojengwa matenki makubwa ya mafuta ghafi yatakayotoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga eneo la Chongoleani.

  Alisema kwamba lengo la ujumbe huo kutua mkoani Tanga ni kuangalia fursa eneo gani ambalo wanaweza kupitisha bidhaa zao kutoka nchini Uganda kwenda kwenye soko la nje kwa gharama nafuu zaidi na kupelekwa pia eneo ambalo litapokelea mafuta, Bohari ya Mafuta Mkoani Tanga ya GBP na sehemu ambayo mafuta yanaposhushwa (Gati ya Meli za mafuta).

  “Kwa kweli tunawashukuru TPA makao makuu na Serikali kutuletea ujumbe huu mkubwa wa sekta binafsi za mafuta za Uganda wakiwemo Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano ya Uganda jambo ambalo linatusaidia kutangaza fursa kubwa tulionayo Bandari yetu ya Tanga “Alisema.

  Alisema msingi wake wa kutumia muda mfupi wakati wa upitishaji wa bidhaa msingi wake ni meli kwenye Bandari ya Tanga inakuja moja kwa moja inapata gati tofauti na maeneo mengine unalazimika kusubiri kwa kipindi cha wiki moja mpaka mbili ambapo kitaalamu wanasema dunia kwenye biashara za bandari na meli katika kila sh, mia moja mwenye meli anaingia gharama ya s h.65 akiwa bandarini.

  Aliongeza kwamba hivyo meli inapofika bandari na kuondoka gharama zake inashuka kwa kiwango kikubwa lakini pia inaweza kusababisha mambo ya kupigwa penati kutokana na kuchelewesha meli lakini kwa bandari ya Tanga hilo halipo.

  Meneja huyo alisema jambo la pili ni kwamba wamekuta na mji ambao barabara zake zipo wazi za kutosha hivyo kuingia na kutoka bandarini hakuna haja ya kukutana na foleni sambamba na kushuhudia mifumo ya utengenezaji wa nyaraka ya kwamba wadau wote wanakaa jengo moja hivyo utengenezaji wake unakuwa wa kasi kubwa sana

  Naye kwa upande wake Meneja wa Bohari ya Mafuta Mkoani Tanga (GBP) Amour Ally alisema wanashukuru sana kupata ugeni kutoka nchini Uganda ambao wanataka kupitisha mafuta yao kwenye Bandari ya Tanga waliokwenda kuangalia miundombinu na uwezo walionao kwa sasa ambapo waliwaambia kwa sasa wanafanya kazi ni lita milioni 122 na laki tano.

  Meneja huyo alisema wana uwezo wa kupeleka mzigo kwa njia ya reli kupitia Mwanza na wanaangalia uwezo wa kupakia mabehewa 20 kwenda Kigoma hivyo wana machagua mawili kutumia reli inayofanya kazi kwa sasa au kutumia magari 12 kwa wakati mmoja.

  Aidha alisema kwamba pamoja na hayo alitumia nafasi hiyo kuwashawishi kuitumia bandari ya Tanga kupitisha bidhaa zao huku akiishukuru Serikali kwa kuweka miundombinu ya kisasa na kuwezesha mazingira mazuri kwa wawekezaji ikiwemo kusifu juhudi za kubwa za Bandari na kuwawezesha kushusha tani elfu 40 kwa siku mbili na nusu.

  0 0
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama akiangali moja ya vitabu vya Sera mbalimbali zilizo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kabla ya kuzindua Kongamano la wataalam wa Maendeleo ya Jamii unaofanyika mkoani Arusha.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama akiangali moja ya vitu mbalimbali inavyotengezwa na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vilivyo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kabla ya kuzindua Kongamano la wataalam wa Maendeleo ya Jamii unaofanyika mkoani Arusha.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wataalam wa Maendeleo ya Jamii kutoka Taasisi za serikali Sekta Binafsi, Mashirika yasiyo ya Kiserikali waliojumuika katika uzinduzi wa Kongamano la Wataalam wa Maendeleo ya Jamii linaloendela Mkoani Arusha.
  Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akielezea jinsia umuhimu wa wataalam wa Maendeleo ya Jamii unavyoweza kuleta mabadiliko katika jamii wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Wataalam wa Maendeleo ya Jamii linaloendela Mkoani Arusha.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagamakiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Maendeleo ya Jamii mara baada ya kuzindua Kongamano la Wataalam wa Maendeleo ya Jamii linaloendela Mkoani Arusha.
  Picha na kitengo cha Mawasiliano WAMJW

  ……………………

  Na Mwandishi Wetu Arusha

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama amewapa somo Wataalam wa Maendeleo ya Jamii nchini kuwa mfano katika kuanzisha viwanda vidogo vidogo na kuwapa mwanga wananchi kuona mfano na kuiga na kuanzisha viwanda vidogo vidogo vitakavyowezesha kufikia azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kufikia Uchumi wa Kati ifikapo mwaka 2025.

  Ameyasema hayo leo mkoani Arusha alipokuwa akizindua Kongamano la Mwaka liliwakutanisha Wataalam wa Maendeleo kutoka Wizara husika, Taasisi za Serikali, Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri, Sekta Binafsi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.

  Waziri Jenista amesema kuwa katika maendeleo ya nchi yoyote Wataalam wa Maendeleo ya Jamii ni watu muhimu katika kuamsha ari ya wananchi katika kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla katika kulueta uchechembuzi katika utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo katika maeneo yao.

  Ameongeza kuwa Serikali imeweka mazingira wezeshi katika kuwawezesha wananchi kuchumi na kusema kuwa katika Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kuna jumla ya mifuko.. inayotoa mikopo kwa waananchi ili kujikwamua kiuchumi kwa kufanya biashara na kauanzisha viwanda vidogo vidogo katika maeneno yao na kuwataka Wataalam wa Maendeleo ya Jamii kuchukua mikopo hiyo na kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili kuwa mfano kwa jamii.

  “ Nataka mkutano wa mwaka 2019 kusiwe na mabanda ya maonesho tu bali kuwe na viwanda vidogo vidogo 350 zaidi katika maeneo mnayotoka ili tuiishi kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kufikia Uchumi wa Kati na wa Viwanda ifikapo mwaka 2025” alisisitiza Mhe. Jenista

  Aidha amempongeza Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu kwa kusimamia Sekta ya Maendeleo ya Jamii kwa ukaribu zaidi kwani ana uzoefu katika Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa muda aliokuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza hilo hivyo kama atatumia uzoefu huo ataipeleka Sekta ya Maendeleo ya Jamii mbele ili iweze kuwezesha wananchi kujikwamua kiuchumi hasa wananchi waliopo vijijini.

  Kwa upande wake Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema lengo la Kongamano la Wataalam wa Maendeleo ya Jamii ni kuwakutanisha Wataalam hao kujadiliana mambo mablimbali yahusuyo Taaluma hiyo ili kuja na njia na mbinu mpya za kuiwezesha Taaluma hiyo kuendelea kuwa chachu ya mabadiliko ya kiuchumi kwa wananchi na Taifa la Tanzania kwa ujumla.

  “Mhe. Mgeni rasmi Kongamano ni muhimu sana kwa ajili ya uhai wa Taalaum ya Maendeleo ya Jamii ambayo ni Njini ya Maendeleo yoyote”alisisitiza Dkt. Jingu

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro amesema kuwa Maafisa na Wataalam wa Maendeleo ya Jamii ni nguzi muhimu katika maendeleo na anashangaa kwanini mpaka sasa bado tupo nyuma katika taifa kwani kuna baadhi ya watu bado wanajivuta katika kujiletea maendeleo katika maeneo yao.

  “Mwalimu Nyerere alisema Maendeleo yanahitaji Siasa safi tunayo, Ardhi tunayo, Watu tuano,na Uongozi bora tuonao chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Joseph Magufuli na kwanini mpaka sasa tuko nyuma” alisisitiza Mhe. Muro.

  Pia Rais wa Mpito wa Chama cha Maendeleo ya Jamii (CODEPATA) Bw. Sunday Wambura amemuahidi mgeni rasmi kuyatekeleza yale yote ambayo amewaagiza na kuhakikisha wanatumia fursa zilizopo katika kuiwezesha jamii kuamka na kuanza kuona umuhimu wa kushiriki katika shughuli za maendeleo yao wenyewe.

  Kongamano la Wataalam wa Maendeleo Jamii kwa mwaka 2018 lina kauli Mbiu inayosema “ Wataalam wa Maendeleo ya Jamii ni chachu katika kufikia Uchumi wa Kati 2025” na linafanyika kwa siku nne mfululizo Mkoani Arusha.

  0 0


  Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya kwenye kikao na balozi wa Nigeria nchini Tanzania Mhe. Sahabu Isah alipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar-es-salaam. Mhandisi Manyanya na mgeni wake wamezungumza mambo mbalimbali yanayohusu uwekezaji baina ya nchi hizo mbili. Kushoto (suti ya blu) ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Joseph Bchweishaija.
  Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Stella Manyanya, kwenye picha ya pamoja na balozi wa Nigeria nchini Tanzania, Mhe. Sahabu Isah baada ya kumaliza mazungumzo yaliohusu uwekezaji wa nchi ya Nigeria nchini. Kushoto kwa Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Joseph Bchweishaija.

  …………………

  Naibu Waziri Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya leo amefanya mazungumzo na balozi wa Nigeria nchini Tanzania Mhe. Sahabu Isah kuhusu mambo mbalimbali ya uwekezaji nchini.

  Katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ofisi ndogo za wizara hiyo Jijini Dar-es-salaam, Naibu Waziri Manyanaya na mgeni wake wamezungumza masuala mbalimbali ya uwekezaji ikiwemo uwekezaji wa uliofanywa na kampuni ya kuzalisha saruji ya Dangote.

  “Tumefurahi kumuona balozi amekuja kututembelea na kufuatilia masuala ya uwekezaji yanayohusu nchi yake”. Amesisitiza Mhe. Manyanya. Mhe. Manyanya ameeleza kuwa kupitia kikao hicho wameweza kubalishana uzoefu katika masuala ya maendeleo ya nchi zote mbili.

  Mhe. Waziri amemuhakikishia balozi huyo wa Nigeria kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi ya Nigeria katika masuala ya Uwekezaji na pia wizara yake iko tayari muda wowote kumokea endapo atakutana na changamoto yeyote.

  Mbali ya kumhakikishia uhsirikiano, mheshimiwa Manyanya pia alitoa shukran za serikali kwa uwekezaji uliofanywa na nchi ya Nigeria “sisi tunafurahi kumuona Dangote amewekeza, na tungependa uwekezaji wake uendelee ili watanzania waendelee kufaidika na uwekezaji huo”, aliongeza mhandisi Manyanya.

  Kwa upande wake Mhe. Sahabu amehaidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina na nchi hizo mbili na amefurahishwa na hatua za serikali za kutatua changamoto za wafanyabiashara mbalimbali kutoka Nigeria waliowekeza nchini.

  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Geita ya Nzera, Novemba 27, 2018. Wapili kulia ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwita Waitara . Watatu kulia ni Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma na wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijadili jambo na Mbunge wa Geita Vijijini, Jioseph Msukuma wakati alipotembelea Wodi ya Wazazi katika Hospitali ya Wilaya ya Geita, Novemba 27, 2018.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nzera wilayani Geita, Novemba 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  Na Mwandishi wetu, Mihambwe 

  Gavana Mihambwe, Emmanuel Shilatu amesisitiza jukumu kubwa la viongozi wa Serikali ni kuhakikisha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi unafanyika kwa kuhakikisha miradi inayopokelewa ni ile iliyokamilika vyema. 

  Gavana Shilatu aliyasema hayo wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Sekondari Mkoreha ili kujionea hatua iliyofikiwa. *Tarafa ya Mihambwe tunatekeleza, Viongozi wote wa Serikali tuna jukumu kubwa la kuhakikisha tunasimamia na kutekeleza vyema ilani ya uchaguzi ya CCM kwa kuhakikisha miradi ya kimaendeleo inayokabidhiwa ina ubora unaolingana na thamani ya pesa. Hivyo mradi wa maendeleo usiokamilika vyema usipokelewe.”* alisema Gavana Shilatu. 
  Gavana Shilatu alisifu hatua iliyofikiwa ya mradi huo wa ujenzi na kusisitiza madarasa hayo yakamilike haraka ili yaanze kutumika mara moja. *”Napongeza hatua iliyofikiwa. Kuanza kutumika kwa madarasa haya yatakidhi mahitaji yaliyopo ambayo yameongezeka kutokana na fursa ya elimu bure na bora ambayo Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Magufuli inatoa. Hivyo Madarasa haya yakamilishwe vyema mara moja na yaanze kutumika mapema iwezekanavyo.”* alisisitiza Gavana Shilatu

  0 0
  0 0


  Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Paul Bura (kushoto) mara baada ya ya kuweka jiwe la msingi la Mradi wa Maji wa Mukabuye, wilayani Kibondo katika Mkoa wa Kigoma.
  Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akiwa kwenye kisima cha IOM kilichopo eneo la Kumwayi kinachotumiwa na Mradi wa Maji wa Kibondo Mjini, mkoani Kigoma.
  Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akikagua ujenzi wa tenki la Mradi wa Maji wa Mabamba/Mukurazi uliopo Wilaya ya Kibondo, mkoani Kigoma.
  Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akizungumza na viongozi na watendaji wa Wilaya ya Kibondo katika ofisi za wilaya, mkoani Kigoma.
  Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa akijibu maswali ya wakazi wa Kijiji cha Mukabuye kabla ya kuweka jiwe la msingi la Mradi wa Maji wa Mukabuye, wilayani Kibondo katika Mkoa wa Kigoma.

  ……………………

  Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa ameiagiza Kampuni ya KGG Investment Ltd & Tanafri Group Ltd inayojenga Mradi wa Maji wa Mukabuye kuhakikisha inakamilisha mradi huo ifikapo mwezi Disemba, 2018 ili wakazi wa Mukabuye na vijiji jirani wapate huduma ya majisafi na salama.

  Profesa Mbarawa ametoa maagizo hayo wakati akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Mradi wa Maji wa Mukabuye kwenye ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Kibondo, mkoani Kigoma. “Mradi wa Maji wa Mukabuye umeanza kutekelezwa Juni, 2018 na unategemewa kukamilika mwezi Aprili, 2019 kulingana na mkataba. Lakini mimi nataka mkandarasi akamilishe mradi huu mwishoni mwa mwaka huu ili wananchi hawa wapate maji haraka iwezekanavyo’’, amesema Profesa Mbarawa.

  “Hakuna sababu ya kusubiri mpaka mwakani mradi huu ukamilike, kama fedha zipo na tutamlipa mkandarasi kiasi kilichobaki. Sina mashaka na uwezo wa mkandarasi kwa sababu uwezo anao, kikubwa ni kuongeza bidii na kasi ya utekelezaji’’, aliongeza Profesa Mbarawa. Akisisitiza ziara yake imelenga kubaini na kutatua changamoto zote za miradi ya maji katika Wilaya ya Kibondo kwa kuwa Serikali imelenga kuwa karibu na wananchi na kutatua kero zao kwa wakati.

  Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo inatekeleza Mradi wa Maji wa Mukabuye kupitia Bajeti ya 2018/19 kwa gharama ya zaidi ya Shilingi Bilioni 1 unaohusisha vijiji vitatu vya Mukabuye, Kageyo na Nyakilenda.

  Vilevile, Profesa Mbarawa amekubali ombi la Mkuu wa Wilaya ya KIbondo la kuongeza mtandao wa bomba la maji la Mradi wa Mabamba/Mukurazi kwa umbali wa kilomita mbili mpaka kwenye Soko la Pamoja la nchi za Tanzania na Burundi lilipo mpakani mwa nchi hizo katika Kijiji cha Mabamba kwa ajili ya kutoa huduma ya maji kwenye soko hilo. Akizungumza kwa niaba ya wakazi wa Wilaya ya Kibondo, Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Paul Bura amemshukuru Waziri wa Maji kwa kukubali ombi lao kutokana na soko hilo kuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa halmashauri.

  Pia, ameishukuru Serikali kwa jitihada inazozifanya katika kuhakikisha inamaliza kero ya maji wilayani Kibondo, kitu ambacho kimekuwa tatizo kubwa Kibondo ikizingatiwa asilimia 29 ya wakazi wa wilaya hiyo ndio wanapata huduma ya majisafi na salama. Akisema kwa sasa Serikali imetoa zaidi ya Sh. Milioni 359 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Kibondo Mjini, ambapo awamu ya kwa

  nza ikikamilika itaongeza upatikanaji wa huduma ya maji mpaka asilimia 56. Huku awamu ya pili itakayohusisha uchimbaji wa visima vitatu kazi itakayofanywa na Wakala wa Uchimbaji wa Visima na Ujenzi wa Mabwawa (DDCA) inayotegemewa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2019, itafikisha huduma ya maji asilimia 90 katika Mji wa Kibondo.

older | 1 | .... | 1735 | 1736 | (Page 1737) | 1738 | 1739 | .... | 1898 | newer