Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live

WAZEE WASTAAFU 2000 MKOANI TANGA WANUFAIKA NA MIKOPO KUTOKA BENKI YA POSTA.

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta (TPB) Noves Moses kushoto akimkabidhi vifaa vya ofisi Mwenyekiti wa Chama cha Wanajeshi Wastaafu mkoani Tanga (MUWAWATA) Stepheni Mponji vifaa vya ofisi kwa ajili ya Chama cha Muungano wa Wanajeshi wastaafu mkoa wa Tanga (MUWAWATA) venye thamani ya milioni 1.5
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta (TPB) Noves Moses kushoto akimkabidhi vifaa vya ofisi Mwenyekiti wa Chama cha Wanajeshi Wastaafu mkoani Tanga (MUWAWATA) Stepheni Mponji vifaa vya ofisi kwa ajili ya Chama cha Muungano wa Wanajeshi wastaafu mkoa wa Tanga (MUWAWATA) venye thamani ya milioni 1.5
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta (TPB) Noves Moses kushoto akimkabidhi vifaa vya ofisi Mwenyekiti wa Chama cha Wanajeshi Wastaafu mkoani Tanga (MUWAWATA) Stepheni Mponji vifaa vya ofisi kwa ajili ya Chama cha Muungano wa Wanajeshi wastaafu mkoa wa Tanga (MUWAWATA) venye thamani ya milioni 1.5
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta (TPB) Noves Moses kushoto akimkabidhi feni kwa ajili ofisi Mwenyekiti wa Chama cha Wanajeshi Wastaafu mkoani Tanga (MUWAWATA) Stepheni Mponji vifaa vya ofisi kwa ajili ya Chama cha Muungano wa Wanajeshi wastaafu mkoa wa Tanga (MUWAWATA) juzi ambapo benkio hiyo ilitoa vifaa venye thamani ya milioni 1.5.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta (TPB) Noves Moses kushoto akimkabidhi meza kwa ajili ya matumizi ya ofisi Mwenyekiti wa Chama cha Wanajeshi Wastaafu mkoani Tanga (MUWAWATA) Stepheni Mponji juzi ambapo benki hiyo ilitoa vifaa venye thamani ya milioni 1.5


WAZEE Wastaafu 2000 mkoani Tanga wamenufaika na mikopo kutoka Benki ya Posta (TPB) wenye thamani ya sh.bilioni 6.7 kupitia pensheni zao ambao umeweza kuwasaidia kukidhi mahitaji yao na kuwakwamua kimaendeleo wao na jamii zao. 

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Benki ya Posta (TPB) Noves Moses wakati wa halfa ya kukabidhi vifaa vya ofisi kwa ajili ya Chama cha Muungano wa Wanajeshi wastaafu mkoa wa Tanga (MUWAWATA) zenye thamani ya milioni 1.5. 

Vifaa vya ofisi ambavyo vilikabidhiwa ni viti sita, meza moja na feni mbili ambavyo vitawawezesha wazee hao kuweza kutekeleza majukumu yao ya kila siku ya kiofisi hali itakayowasaidia kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa ambapo mikopo hiyo bado inaendelea. 

Alisema kwamba huo ni mwanzo hivyo wataendelea kushirikiana na wazee wote nchini wa taasisi mbalimbali ili kuweza kuwasaidia kukidhi mahitaji yao hivyo kuwataka wastaafu kuchangamkia fursa hiyo ikiwemo kuwapa elimu namna ya kutumia fedha husika. 

“Lakini niwaambie kwamba sisi TPB tunawaambiwa wazee wastaafu nchi nzima tunawajali kwa kutoa mikopo na huduma za kibenki wao wamekuwa wa kwanza kuweza kutoa mikopo kwao kabla ya hapo wastaafu walikuwa wanaonekana kama ni kada ambayo haikopesheni tulianza kutoa mikopo kwa wastaafu kupitia pensheni zao “Alisema. 

Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wanajeshi Wastaafu mkoani Tanga (MUWAWATA) Stepheni Mponji aliishukuru benki ya Posta kwa kuwawezesha na kuwathamini kuwapatia vifaa vya ofisi ambavyo vitakuwa chachu ya kutekeleza shughuli zao kwa ufanisi mkubwa. 

“Kwa kweli ofisi yetu ilikuwa na changamoto ya thamani hivyo tulipowaomba TPB hawakusita kutusaidia hivyo tunawaomba tuendelee kuwasaidiana lakini pia niwaombe waliangalie suala la riba kwa wazee“Alisema Alisema wanashukuru sana kutokana na kwamba hapo awali walikuwa hawakopesheki kutokana na kwamba kila mahali walipokuwa wakienda walionekana kama hawawezi kupata fedha za mikopo lakini wao waliamua kuwakopesha.

Dkt.Shein awasili Jijini Nairobi Kuhudhuria Mkutano wa Blue Economy.

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Aliu Mohamed Shein, akimsikiliza Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Balozi Dan Kazungu kulia na kushoto Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dkt. Pindi Chana,baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Nchini Kenya.akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Magufuli katika Mkutano wa Blue Economy unaotarajiwa kufanyika kesho Jijini Nairobi. katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mr. Dan Kazungu, wakiwa katika chumba cha VIP Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta,leo jioni 26/11/2018, akihudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Blue Economy, utakaofanyika kesho Nchini Kenya.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiutambulisha Ujumbe wake kwa Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mr. Dan Kazungu,wakiwa katika chumba cha VIP baada ya kuwasili leo jioni.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika chumba cha VIP katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Nchini Kenya akiwa anahudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Blue Economy,kulia Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Mr. Dan Kazungu na kushoto Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dkt. Pindi Chana. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dkt.Pindi Chana na anayefuata ni Balozi wa Kenya Nchini Tanzania Balozi Dan Kazungu, alipowasili katika hotelini.Jijini Nairobi. 

Na.Suzan Kunambi. Nairobi..

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein amewasili nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa uchumi endelevu wa bahari(Sustaniable Blue Economy Confrence) utakaoanza kesho katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta Jijini Nairobi Nchini Kenya.

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Nairobi, Dk.Shein amepokelewa na viongozi mbali mbali wakuu wa Serikali ya Kenya wakiongozwa na balozi wa Kenya nchini Tanzania Dan Kanzungu pamoja na Balozi wa Tanzania nchini humo Dk. Pindi Chana.

Katika ziara hiyo, Dk. Shein amefuatana na viongozi mbali mbali wa SMT na SMZ, akiwemo Waziri wa Kilimo Maliasili Mifungo na Uvuvi Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma,Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mhe.Dk.Sira Ubwa Mamboya,Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais Mazingira na Muungano Mhe January Makamba.

Mkutano huo Mkubwa unaohusu sekta ya uchumi wa bahari ni wa kwanza kufanyika nchini Kenya, ambao utawakutanisha wadau kutoka sekta mbali mbali kutoka nchi zilizoendelea na sinazoendelea kujadili namna bahari,maziwa na mito vinavyoweza kutumika katika kuimarisha uchumi wa nchi na dunia kwa ujumla.

Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamuhuri ya Watu wa Kenya Mhe.Uhuru Kenyatta, ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein atatoa tamko la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu Uchumi Endelevu wa Bahari, akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muunhano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Magufuli.

Mkutano huo utajadili maswala mbali mbali ya uchumi endelevu wa bahari na mchango wake katika kutekeleza Agenda ya 2030 ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa.vile vile washiriki wa mkutano huo watajadili hatua za utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa katika ,mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa wa mwaka 2015 wa Paris Ufaransa pamoja na mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari wa mwaka 2017 kwa ajili ya maendeleo endelevu pamoja na usalama na ulinzi baharini.

MUFTI WA TANZANIA AZINDUA MAANDALIZI YA IJITIMAI YA KIMATAIFA ITAYOFANYIKA T ZANZIBAR

$
0
0

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Fiy Sabilillahi Tabligh Markaz Zanzibar Alhaji Shekh. Mwalim Hafidhi Jabu akimkaribisha Mufti wa Tanzania Shekh. Abubakari Zubeir Ali katika viwanja Markaz Kidoti Mkoa Kaskazini Unguja.
Mufti wa Tanzania Shekh. Abubakari Zubeir Ali akiwa na mwenyeji wake, Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Vuai Mwinyi Khamis wa kwanza (kulia) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Fiy Sabilillahi Tabligh Markaz Alhaji Mwalim Hafidhi Jabu kukagua Mskiti unaotarajiwa kufanyika Ijitimai ya kimataifa huko Kidoti.
Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Vuai Mwinyi Khamis akimkaribisha Mufti wa Tanzania Shekh. Abubakari Zubeir Ali katika uzinduzi wa maandalizi ya Ijitimai ya kimataifa itayofanyika tarehe 22/02/2019 huko kijiji cha Kidoti Mkoa Kaskazini Unguja.
Mufti wa Tanzania Shekh. Abubakari Zubeir Ali akizindua rasmin maandalizi ya Ijitimai ya kimataifa itayofanyika tarehe 22/02/2019 katika Kijiji cha Kidoti Mkoa Kaskazini Unguja uzinduzi huo umefanyia Msikiti wa Jumuiya ya Fiy Sabilillahi Tabligh Markaz Kidoti.
Mufti wa Tanzania Shekh. Abubakari Zubeir Ali akimsalimia Bii. Mwajuma juma mkaziwa Kidoti alietoa kiwanja kwa ajili ya kujengwa Mskiti huo.Picha na Makame Mshenga.

Amber Rutty na Mpenzi wake waendelea kusota rumande,upelelezi wa kesi yao bado haujakamilika

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Wakati Msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama 'Amber Ruty na mpenzi wake Said Kitomali wakiendelea kusota rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana, katika kesi inayowakabili ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile upelekezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Amber Ruty na Said wanashtakiwa pamoja na James Charles maarufu kama 'James Delicious' ambaye yeye yupo nje kwa dhamana.kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, Amber Rutty alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Augustine, Rwizile kuwa mdhamini wake mmoja amefika mahakamani hapo lakini mwingine bado hajafika.

Hata hivyo, Hakimu Rwizile  amemwambia Amber Rutty kwamba dhamana ipo wazi na shughuli za mahakama zinaisha saa 9 alasiri hivyo wadhamini wake wakikamilika atadhaminiwa.Kesi  hiyo imeahirisha hadi Decemba 10,2018.

Katika kesi hiyo, Amber Ruth,  anadaiwa kufanya mapenzi kinyume na maumbil kosa analodaiwa kulitenda kati ama baada ya October 25, 2018 ambapo alimruhusu Said Bakary kumuingilia kinyume na maumbile, 

Pia kosa jingine la kufanya mapenzi kinyume na maumbile, linamkabili mshtakiwa wa pili Said Bakary ambapo anadaiwa kati ama baada ya October 25,2018 jijini Dar es Salaam alifanya mapenzi na Amber Ruth kinyume na maumbile.Kosa la tatu la kuchapisha video ama picha za ngono, ambapo linamkabili James Charles ama James Delicious akidaiwa kati ya October 25,2018 alisambaza video za ngono kupitia magroup ya Whatsapp.

Katika shtaka la nne ambalo ni kusababisha kusambaa kwa picha za ngono linamkabili Amber Ruth na Said Aboubakary ambapo wanadaiwa kati ya 25,2018 walisababisha kusambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp. Kosa ambalo wamesema si kweli.Amber  Rutty na mpenzi wake ili waweze kuwa nje kwa dhamana wanatakiwa kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini 2 ambapo kila mtu atasaini bondi ya Shilingi Milioni 15.

Pia wadhamini wawe na vitambulisho vya taifa pamoja na kuwasilisha hati zenu za kusafiria na msitoke nje ya Dar es Salaam bila ruksa.
Pichani kati Msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama 'Amber Ruty akirudishwa rumande huku upelelezi wa kesi yao bado haujakamilika

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU BABA ASKOFU EVARISTO CHENGULA WA JIMBO KUU LA MBEYA . NOVEMBA 26,2018

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe akisainib kitabu cha maombolezo mara baada ya kuwasili Makao makuu ya Baraza la Maaskofu wa kanisa Katoliki Tanzania (TEC) kuaga mwili wa Marehemu Baba Askofu Evaristo Chengula wa Jimbo kuu la Mbeya,Ibada iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Immakulata Makao Makuu ya Baraza hilo Kurasini Jijini Dar es Salaam Novemba 26, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe akitoa salamu zake za mwisho kwa mwili wa Marehemu Baba Askofu Evaristo Chengula wa Jimbo kuu la Mbeya,Ibada iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Immakulata Makao makuu ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini Jijini Dar es Salaam Novemba 26, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe akizungumza wakati wa Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Baba Askofu Evaristo Chengula wa Jimbo kuu la Mbeya,Ibada iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Immakulata Makao makuu ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini Jijini Dar es Salaam Novemba 26, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe akiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa,Mama Anna Mkapa pamoja na Maaskofu, Mapadre, Masista na Waumini wenginne wakati ibada ikiendelea ya kuaga mwili wa Marehemu Baba Askofu Evaristo Chengula wa Jimbo kuu la Mbeya, iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Immakulata Makao makuu ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini Jijini Dar es Salaam Novemba 26, 2018. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe akipongezwa mara baada ya kutoa salamu za rambirambi na Makamu wa Rais wa baraza la Maaskofu wa Kanisa katoliki Baba Askofu Dkt.Flavian Kasalla wakati wa Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Baba Askofu Evaristo Chengula wa Jimbo kuu la Mbeya,iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Immakulata Makao makuu ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini Jijini Dar es Salaam Novemba 26, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe akipongezwa mara baada ya kutoa salamu za rambirambi na Makamu wa Rais wa baraza la Maaskofu wa Kanisa katoliki Baba Askofu Dkt.Flavian Kasalla wakati wa Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Baba Askofu Evaristo Chengula wa Jimbo kuu la Mbeya,iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Immakulata Makao makuu ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini Jijini Dar es Salaam Novemba 26, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe akipongezwa mara baada ya kutoa salamu za rambirambi na Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam Mhadhama Polycapy Kadinali Pengo wakati wa Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Baba Askofu Evaristo Chengula wa Jimbo kuu la Mbeya,iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Immakulata Makao makuu ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Kurasini Jijini Dar es Salaam Novemba 26, 2018.

PICHA NA IKULU.

WATATU WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI

$
0
0
Na. VERO IGNATUS, MANYARA

Jeshi la polisi Mkoani Manyara, linawashikilia watu watatu kwa kudaiwa kukutwa na nyara za serikali ikiwemo vipande vitatu vya jino la Tembo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Augostino Senga akizungumza jana alisema watu hao walikamatwa kwenye nyumba ya kulala wageni ya Top In One iliyopo mtaa wa Oysterbay mjini Babati.

Kamanda Senga aliwataja watu hao kuwa ni Anthony Paschal (28) na Juma Ingi wote wakazi wa Endasak wilayani Hanang' na Tluway Gosi mkazi wa Simbay wilayani Hanang'. Alisema mbinu waliyotumia ni kuficha vipande hivyo ndani ya mfuko wa sulphate kisha kuweka chini ya uvungu wa kitanda ili wakaiuze.

Alisema baada ya timu ya makachero kwa kushirikiana na maofisa wanyamapori wa shirika la hifadhi ya Taifa ya Tarangire kupata taarifa walifika eneo hilo na kuwakamata watu hao. "Watuhumiwa hao wote wanashikiliwa na polisi na tunaendelea na upelelezi kabla ya kuwafikisha mahakama kwa ajili ya kujibu mashtaka yanayowakabili," alisema kamanda Senga.

Katika tukio lingine, kamanda Senga alisema watu watatu wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na lita 40 za pombe haramu ya moshi maarufu kama gongo. Alisema watu walikamatwa juzi kwenye kijiji cha Kazamoyo kata ya Kisangaji wilayani Babati wakiwa wamebeba kwenye pikipiki aina ya Skygo yenye namba za usajili MC 970. Aliwataja watu hao kuwa ni Daniel Hewasi (47) mkazi wa Magugu, Hussein Athuman (50) mkazi wa kijiji cha Kazaroho na Idd Hamis (35) mkazi wa kijiji cha Magugu.

Alisema watu hao walikuwa wamebeba pombe hiyo haramu kwenye pikipiki hiyo wakiwa wamehifadhi kwenye madumu mawili ya lita 20 kila moja.Alisema pikipiki hiyo iliyokuwa imebeba pombe hiyo haramu ni mali ya Idd Hamis na lengo lao ilikuwa ni kwenda kuuza ili kujipatia kipato.

Alisema polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kuwafikisha mahakamani wakajibu mashtaka yanaoyowakabili.


Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Augostino Senga

WAWEKEZAJI WA LIGANGA MCHUCHUMA WAOMBA KUKAA MEZA MOJA NA SERIKALI

$
0
0
*Kampuni ya Sichuan Hongda Group ya China yaomba kukaa meza moja na Serikali ili kufikia muafaka wa mradi wa uchimbaji  Liganga  Mchuchuma, ambapo yasubiri  hatima ya mradi huo kutoka Serikalini.

FCS YAJITOLEA KUCHANGIA DAMU HOSPITALI YA MUHIMBILI, KITENGO CHA MOI

$
0
0
Taasisi inayojihusisha na kutoa ruzuku kwa asasi za kiraia hapa nchini ya Foundation for Civil Society mapema jana imeendesha zoezi maalum la kujitolea damu kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa mbalimbali wenye uhitaji wa damu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha MOI.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema jana katika zoezi hilo la uchangiaji wa damu Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Bw. Francis Kiwanga amesema kuwa, wao wameamua kuchangia damu kwa wagonjwa ikiwa ni kama njia moja wapo ya kurudisha kitu kwa jamii.

Aidha Mkurugenzi huyo aliendelea kusisitiza umuhimu wa wananchi kuchangia damu nakuwataka wajitokeze kwa wingi katika zoezi hilo hasa vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa.

“Tumekuja hapa kuchangia damu kwa kuwa ni hospitali ya Taifa na ni sehemu yenye uhitaji mkubwa sana wa damu. Tunawaomba watanzania wengine wajitokeze kuchangia ili kuwaokoa watanzania wenzetu lakini pia kuunga mkono jitihada za shirika la damu salama ambalo kila kukicha wanaelezea umuhimu wa wananchi kuchangia damu ili kunusuru maisha ya wananchi wenzetu ” Alisema Kiwanga

Ameongeza kuwa mbali na kujitoa kwao katika zoezi la kuchangia damu lakini pia wamejipanga kwenda kuwasaidia wasichana wanaoishi katika mazingira magumu wa kituo cha New Hope for Girls kilichopo Kimara jijini Dar es salaam Tarehe 27/11 mwaka huu katika siku ya Jumanne ya kutoa.
Mmoja wa wachangiaji wa damu katika Kampeni hiyo iliyoendeshwa na Taasisi ya Foundation for Civil Society, Gloria Wangeleja(Mwenye nguo ya Rangi Nyekundu) akitoa damu mapema jana katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

KWA upande wake Mkuu wa Kitengo cha Maabara Moi Dokta Mbuta Jakckson alisema kuwa licha ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na makundi ikiwamo wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali, vikundi vya dini lakini bado changamoto hiyo haikuweza kumalizika na kusema kuwa kwa mahitaji ya kaiwada ya damu kwa siku ni unit 70 lakini zinazopatikana ni unit 40 mpaka 50 peke yake.

Amesema hospitali ina wataalamu wa kutosha wa kukusanya damu, watu hawana haja ya kutia shaka na uwezo wa taasisi hiyo katika kukamilisha zoezi hilo. 

“Tumekuwa tukienda hata nje ya kituo hiki, kwa mfano tulikwenda temeke katika msikiti mmoja hivi jina nimelisahau, lakini pia tulifika kwenye makampuni mbalimbali kuchukua damu. Tunachohitaji ni utayari wa raia, tuko tayari wakati wote kufika mlipo ili tuchukue damu itakayowasaidia wagonjwa” alisema.

Aliendelea kusisitiza kuwa hapo mwanzo wagonjwa walikuwa wakichangiwa damu kutoka kwa ndugu na jamaa zao, lakini kwa sasa hali imebadilika na wanaochangiwa na ndugu zao ni wachache sana ukilinganisha na wasio na watu wa kuwachangia, hali inayosababisha kuchelewa kwa huduma kutokana na kutokuwepo na damu katika benki hiyo.
Wachangiaji wakiendelea kujitolea damu.

Naye Shabani Mwin’juma Shekihenda, Mlemavu wa macho ambaye alijitokeza katika zoezi hilo la uchangiaji damu, ameshindwa kutimiza azma yake hiyo baada ya kupimwa na kugundulika kuwa damu yake ni ndogo na asingeweza kuhimili kama angetolewa.

Akizungumzia tukio hilo, Mwin’juma anasema amesononeshwa sana na kushindwa kuchangia damu kwani aliamini chupa ya damu yake ndogo ingeweza kunusuru maisha ya kiumbe mwingine.

Amesema Licha ya ulemavu wake lakini anauwezo wa kutembea sehemu yoyote ile, hivyo haina maana kuwa hana wajibu wa kusaidia wengine, ameguswa na tukio hilo na kuamua kutoka nyumbani kwakwe Buza kwa lengo la kutoa damu.

“KASI YA UMEME MIJINI NA VIJIJINI NI ILE ILE’’- WAZIRI KALEMANI

$
0
0
NA YASINI SILAYO, GEITA

Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dkt. Medard Matogolo Kalemani akiwa Mkoani Geita, jana Novemba 25 amesema kuwa, kasi ya utekelezaji wa jukumu la kusambaza na kuunganisha wananchi na huduma ya umeme kwa maeneo ya Mijini na Vijijini kote Nchini ni ile ile ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha kuwa huduma ya Nishati ya umeme inatumika kuchochea na kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na huduma za kijamii Nchi nzima. 

Sisi Kama Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) na Wakala wa Usambazaji Nishati ya Umeme Vijijini (REA) tumeendelea kusimamia na kutekeleza jukumu la kusambaza na kufikisha huduma za umeme kila pembe ya Nchi ikiwa ni Mijini na Vijijini” Alisema Waziri Kalemani. 

Aliongeza kuwa hivi sasa Wizara kupitia TANESCO na REA wanaendelea kutekeleza miradi ya usambazaji umeme Vijijini, lakini umeme huo unasambazwa kwa kasi ile ile maeneo ya mijini ikiwemo mitaa yenye makazi mapya na ile ya zamani ambayo ilikuwa bado hayajafikiwa na huduma za Umeme kupitia TANESCO yenye jukumu la kusambaza huduma hiyo katika maeneo ya Mijini. 

Alibainisha pia katika kuimarisha zaidi mpango wa usambazaji umeme vijijini serikali imeanza maandalizi ya kutenga fedha maalumu zitakazotumika kuchochea kasi ya usambazaji umeme maeneo ya mijini.

 Akiwa katika mji mdogo wa Katoro eneo la Bulengahasi Mkoni Geita, alitoa Rai kwa TANESCO na Wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme kuongeza kasi ya kusambaza na kuunganisha wateja na huduma ya umeme ambapo alitoa siku kumi kwa TANESCO kuhakikisha mitaa na vitongoji vingi zaidi vya eneo la katoro vinaunganishwa na umeme hivyo kuimarisha huduma za kijamii pamoja kuchochea maendeleo ya wakazi wa maeneo hayo. Aidha waziri Kalemani, mbali na kuagiza Wakandarasi, TANESCO na REA kuharakisha shughuli za usambazaji umeme. 

Pia aliwasisitiza na kuwahamasisha wananchi kuunganisha umeme pindi miundombinu hiyo inapofika katika maeneo yao. Waziri alieleza kuwa serikali imekuwa ikitenga mabilioni ya fedha kila mwaka katika kuhakikisha umeme unasambazwa na kuwafikia wananchi wote na kwa bei nafuu, hivyo ni vyema wananchi wakachangamkia fursa hiyo kujikwamua kiuchumi kwa kuunganisha umeme na kubuni miradi mbalimbali inayotumia umeme kujiingizia kipato.

Kwa upande wa mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO aliyeambatana na Waziri katika ziara hiyo, Mhandisi Theodory Bayona, alielezea kupokea na kutekeleza maelekezo na maagizo yote kulingana na ilivyoelekezwa na Waziri katika ziara hiyo lakini aliongeza pia mbali na kufikisha umeme mapema, TANESCO Itaendelea na juhudi za kuelimisha na kuhamasisha wananchi kuunganisha umeme pindi miundombinu inapofika katika maeneo yao na kuhakikisha wananchi wote wanaostahili kuunganisha umeme wanaunganishwa ili kuongeza idadi ya wateja wa Shirika na hivyo kuongeza zaidi mapato ya Shirika kupitia mauzo ya umeme. 

Naye Mwananchi mmoja Mkazi wa Kijiji cha Mapinduzi kilichopo kata ya Buseresere Wilayani Chato aliyehudhuria katika mkutano wa Waziri kijijini hapo na aliyejitambulisha kwa jina moja la Vedasto, aliishukuru Serikali kwa kuwajali wananchi na kuwafikishia huduma ya umeme mpaka kijijini hapo. Alisema kuwa umeme umekuja na matumaini mapya ya kimaendeleo kijijini hapo na tayari wameanza kujipanga kubuni na kuanzisha shughuli mbalimbali za kimaendeleo zinazotegemea umeme kujiingizia kipato tofauti na hapo awali ambapo walikuwa wakitegemea zaidi shughuli za kilimo, uvuvi na ufugaji pekee.
Waziri wa Nishati Mheshimiwa Dkt. Medard Kalemani, kulia akiongea na Wananchi pamoja na kutoa maelekezo kwa viongozi wa TANESCO na REA katika eneo la Bulengahasi lililopo Kata ya Katoro Mkoani Geita baada ya kukagua na kujionea maendeleo ya shuguli za usambazaji umeme eneo hilo. Kushoto kwake ni Meneja wa TANESCO Mkoa wa Geita Mhandisi Joaquim Ruweta.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (katikati) akiendelea na kazi ya ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya kusambazia umeme katika kijiji cha mapinduzi kilichopo kata ya buseresere Wilayani Chato Mkoani Geita. Kushoto ni Meneja wa TANESCO Mkoa wa Geita Mhandisi Joaquim Ruweta na Kulia ni Diwani wa Kata ya Buseresere Bw. Godfrey Fulko

WAZIRI MKUU AZINDUA VIZA NA VIBALI VYA UKAAZI VYA KIELEKTRONIKI

$
0
0
*Yawataka watakaopewa kufanya shughuli zilizoelekezwa kwenye vibali vyao
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezindua huduma za viza na vibali vya ukaazi vya kielektroniki na amewataka watu wote watakaopewa vibali hivyo kutii sheria kwa kufanya shughuli ambazo wameelekezwa kwa mujibu wa vibali vyao na si vinginevyo.

Amesema utoaji wa huduma hizo ni miongoni mwa jitihada za Serikali katika kuvutia uwekezaji, hususan katika sekta ya viwanda kwani hatua hiyo itarahisisha upatikanaji wa vibali hivyo kwa raia wa kigeni na kuchochea kasi ya maendeleo ya kiuchumi.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Novemba 26, 2028) wakati akizindua huduma za viza na vibali vya ukaazi vya kielektroniki katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na kwamba hatua hiyo itasaidia kuondoa urasimu na ucheleweshwaji wa huduma pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi.

Amesema Idara ya Uhamiaji inatarajia kuanza kutoa huduma tajwa kwa raia wa kigeni muda wowote kuanzia sasa na kwa kupitia huduma hiyo, raia wa kigeni wataweza kuomba vibali hivyo kwa njia ya kielektroniki wakati wowote na mahali popote walipo.Waziri Mkuu amesema watakaopewa vibali wanatakiwa kufanya shughuli zao kwa mujibu wa vibali vyao kwa sababu kufanya shughuli tofauti na ilivyoainishwa kwenye kibali ni kosa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Uhamiaji.

Amesema matumizi ya mtandao katika utoaji wa huduma za viza na vibali vya ukaazi ni hatua ya mfano, kwani inakwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia na sera ya Serikali ya matumizi ya TEHAMA katika shughuli za Serikali (e-government).Amesema Serikali inatarajia kuwa, matumizi ya mifumo hiyo itaongeza ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali kwa kuwa mteja ataweza kulipia huduma hizo mwenyewe moja kwa moja pasipo kupitia kwa mawakala au mtu yeyote.

“Natoa wito kwa Maafisa, Askari pamoja na Watumishi wote wa Idara ya Uhamiaji kuhakikisha kuwa mifumo hiyo inatunzwa pamoja na kuendeleza miundombinu yote ya kiutendaji.” 

Waziri Mkuu amesema kwa kuzingatia ahadi ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli ya kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi na raia wa kigeni, Maafisa Uhamiaji wanatakiwa kutoa huduma hiyo kwa wakati, weledi na kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Uhamiaji.

Amesema mfumo wa huduma hizo utaunganishwa na mifumo mingine ya Serikali, ambayo inatoa huduma kwa wananchi na wageni kama vile Mifumo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Idara ya Kazi – Ofisi ya Waziri Mkuu, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Mfumo wa Malipo ya Serikali Kimtandao (GePG). 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Kamishina Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Nchini, Dkt. Anna Makalala wakati alipowasili kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius  Nyerere jijini Dar es salaam  Kuzindua  Viza na Vibali vya Ukaazi vya Kielektroniki , Novemba 26, 2018.  Katikati ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Viongozi wa Idara ya Uhamiaji wakati alipowasili kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius  Nyerere jijini Dar es salaam kuzindua Viza na Vibali vya Ukaazi vya Kielektrtoniki,  Novemba 26, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua  Viza na Vibali vya Ukaazi vya Kielektroniki kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius  Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 26, 2018. 
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga akizungumza katika uzinduzi wa Viza na Vibali  vya Ukaazi vya Kielektroniki  kwenye Kituo cha Mikutano cha  Kimataifa cha Julius  Nyerere jijini Dar es salaam,  Novemba 26, 2018. 
 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde akizungumza katika uzinduzi wa Viza na Vibali  vya Ukaazi vya Kielektroniki  kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa  cha Julius  Nyerere jijini Dar es salaam,  Novemba 26, 2018.
  Kamishina Jenerali wa Idara ya Uhamiaji, Dkt. Anna Makalala akizungumza katika uzinduzi wa Viza na Vibali  vya Ukaazi vya Kielektroniki  kwenye Kituo cha  Mikutano cha Kimataifa  cha Julius  Nyerere jijini Dar es salaam,  Novemba 26, 2018.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi, Hamamad Masauni akizungumza katika uzinduzi wa Viza na Vibali  vya Ukaazi vya Kielektroniki  kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa  cha Julius  Nyerere jijini Dar es salaam,  Novemba 26, 2018. 
 Baadhi  ya Washiriki wa Uzinduzi wa  Viza na Vibali vya Ukaazi vya Kielektroniki  wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza kabla ya uzinduzi huo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam , Novemba 26, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizindua Viza na Vibali vya Ukaazi vya Kielektroniki  kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius  Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 26, 2018.  Kulia ni  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni na wapili kulia ni Kamishina Jenerali wa Idara ya Uhamiaji, Dkt. Anna Makalala.  
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde baada ya Kuzindua Viza na Vibali vya Ukaazi vya Kielektroniki  kwenye Kituo cha  Mikutano cha Kimataifa cha Julius  Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 26, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  Nchini (TAKUKURU)  Kamishina wa Polisi, Diwani Athumani baada ya Kuzindua Viza na Vibali vya Ukaazi vya Kielektroniki kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius  Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 26, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mstaafu, Augustino Ramadhani baada ya Kuzindua Viza na Vibali vya Ukaazi vya Kielektroniki kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius  Nyerere jijini Dar es salaam, Novemba 26, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SPIKA NA MAMEYA WA MANISPAA ZA JIJI LA DAR ES SALAAM WAIPIGA JEKI DCB KWA KUNUNUA HISA

$
0
0

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndungai ( wa pili kushoto) akipokea nyaraka za ununuzi wa hisa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa, baada ya kununua hisa za benki hizo ofisini kwake Jijini Dodoma hivi karibuni, huku Meneja wa Tawi la DCB la Dodoma Joseph Njile (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Rahma Ngassa (kulia) wakishuhudia. Alijefichika kidogo ni Mkurugenzi wa Mikopo Isidory Msaki.
Mheshimiwa Spika, Job Ndugai (kushoto), akisalimiana na Ofisa Mauzo wa DCB tawi la Dodoma, Nuru Ashraf wakati akiwakarbisha yeye, Mkurugenzi Mtendaji, Godfrey Ndalahwa (wa pili kushoto, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Rahma Ngassa na Mkurugenzi wa Mikopo, Isidory Msaki, ofisi kwake mjini Dodoma hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kushoto), akifurahi pamoja na mameya wa manispaa za Jiji la Dar Salaam baada ya kila mmoja kujitokeza kununua hisa za benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kutoka kushoto kwake ni; Mstahiki Meya Ilala Charles Kuyeko, Mstahikli Meya wa Kigamboni Mbadi Hoja, Maya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita , Mstahiki Meya wa Ubungo Boniface Jacob na Mstahiki Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta. Kulia ni Mkurugenzi wa Mikopo wa DCB, Isidory Msaki. Hisa moja inuzwa kwa bei pungozo ya shs 265.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigamboni, Mabadi Hoija akijaza fomu kwa ajili ya kununua hisa. Kushoto ni mfanyakazi wa DCB Brino Londo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB Godfrey Ndalahwa (kushoto) akimshukuru Mstahiki Meya wa Ubungo Jacob Boniface baada ya kununua hisa za benki hiyo. Kulia ni mfanyakazi wa DCB Catherine Ngassa.

Mshindi wa nyumba na sh Milioni 20 Mbeya akabidhiwa fedha zake

$
0
0
Mshindi wa pili wa nyumba na sh Milioni 20 wa bahati nasibu ya Biko, Alex Nyoka, amekabidhiwa fedha zake jana mkoani Mbeya, ikiwa ni siku moja baada ya kuibuka kidedea kutoka kwenye droo ya 158 ya Biko, iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki.

Makabidhiano hayo yamefanyika jana Lujewa, Mbalari mkoani Mbeya na kuongozwa na Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, huku mshindi huyo akizungumzia mkakati wake wa kujikwamua kimaisha baada ya kuibuka mshindi wa Biko.mechelewa kuamini kama ni kweli anaweza kuwa mshindi wa fedha nyingi na nyumba kutoka kwenye bahati nasibu pendwa ya Biko nchini Tanzania.

"Bado siamini kama ni kweli nimeshinda bahati nasibu ya Biko, ingawa nimeshika fedha hizi kwa sababu nilikuwa natamani nishinde ingawa najua waliokuwa wanataka ushindi huu sipo peke yangu."Kwakweli namshukuru Mungu kwa zawadi hii kubwa, huku nikiwataka Watanzania wengine wacheze Biko ili washinde kwa sababu sijawahi kuona bahati nasibu inayochezeshwa kwa uwazi na hata fedha zinaingizwa bank moja kwa moja, hivyo hakuna dalili ya unganyifu," Alisema.

Naye Grace Kaijage, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, alisema wimbi la mamilionea na wamiliki wapya wa nyumba linaendelea, huku akisema popote atakapoibuka mshindi wa nyumba atapata fedha na nyumba yake, akisema wanaoshirikiana nao Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wana miradi ya nyumba katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.

"Tumekuja Mbeya kumkabidhi mshindi wetu fedha zake ambapo jana tulimkabidhi fedha, lakini pia hatuondoki hadi leo apewe nyumba yake kutoka NHC ambayo hununuliwa na Biko kwa ajili ya washindi wetu popote walipo, hivyo naomba waendelee kucheza Biko ili waibuke mamilionea na wamiliki wapya wa nyumba kutoka Biko," Alisema.

Grace alisema zawadi za papo kwa hapo za Biko kuanzia sh 5,000, 10,000, 20,000 hadi sh Milioni moja zinaendelea kutolewa kwa kupitia Biko inayochezwa kwa kufanya miamala kwenye simu za mikononi ya Tigo Pesa, Mpesa na Airtel Money kuanzia sh 1,000 na kuendelea, namba yao ya Kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456.Droo kubwa huchezeshwa kila Jumatano na Jumapili, huku kuanzia Jumatano na Jumapili, watanzania wanaocheza Biko wakitarajiwa kushinda nyumba na sh Milioni 20.
 Mshindi wa nyumba na sh Milioni 20 wa Biko, Alex Nyoka, mkazi wa Mbalari mkoani Mbeya, akiwa na furaha tele baada ya kukabidhiwa fedha zake jana mkoani Mbeya.
Mshindi wa nyumba na sh Milioni 20 wa Biko, Alex Nyoka, mkazi wa Mbalari mkoani Mbeya, akiwa na furaha tele baada ya kukabidhiwa fedha zake jana mkoani Mbeya. Kulia kwake ni Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage. 

Watanzania wajengewa uwezo wa kupata ajira kwenye Umoja wa Mataifa

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhani Mwinyi Muombwa amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi kutoka Umoja wa Mataifa, Bi. Huda Hanina ambaye yupo nchini kwa ajili ya kutoa Semina ya kuwajengea uwezo Watanzania kuhusu mbinu za kuomba ajira kwenye Umoja wa Mataifa. Balozi Mwinyi alipongeza hatua hiyo kwa kuwa Tanznaia licha ya kuwa ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kuchangia vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa duniani, lakini idadi ya Watanzania waliojairiwa katika Sekretarieti ya umoja huo ni ndogo mno. 
Sehemu ya Uongozi wa Jeshi la Ulinzi wa Tanzania pamoja Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Hellen Maduhu wakifuatilia mazungumzo .
Sehemu nyingine ya watumishi wa Serikali wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Balozi Mwinyi na Bi. Hanani 
Mazungumzo yakiendelea. 
Balozi Mwinyi na Bi. Hanani wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi kutoka serikalini na Umoja wa Mataifa. 

Majadiliano katika Meza Duara






Bi. Hanani akielezea mambo mbalimbali kwenye Mkutano na Viongozi wa Serikali na Jeshi la Ulinzi Tanzania, kabla ya kufunguliwa kwa semina za kuwajengea uwezo Watanzania ili kuweza kuchangamkia fursa zinazotolewa na Umoja wa Mataifa. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ - Zanzibar, Mhe. Radhia Haroub Rashid (wa kwanza kulia) akichangia jambo katika semina ya kuwajengea uwezo wa Watanzania wa kuomba nafasi za ajira kwenye Umoja wa Mataifa. 
Juu na Chini sehemu ya viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini wakimsikiliza kwa makini Bi. Hanani 
Mazungumzo yakiendelea.

DJ MKONGWE ZAIDI DUNIANI

$
0
0
SUMIKO Iwamura mwanamke(83) kutoka nchini China ndiye Dj mzee zaidi duniani ambaye hadi sasa anafanya shughuli hiyo.

Sumiko Iwamura maarufu kama Dj Sumirock alizaliwa Januari 23, 1934 na alikuwa na ndoto za kuwa mtu maarufu duniani kote lakini baada ya baba yake kufungua mgahawa alienda kusaidia hapo mara baada ya kumaliza shule.

Dj. Sumirock alienda shule na kujifunza fani hiyo akiwa na miaka 77 na kuanza kufanya kazi hiyo mara mbili kwa mwezi huku akiendelea na kazi ya kuuza mgahawa.

Akiwa na ndoto za kusafiri duniani kote Dj. Sumirock amesafiri katika nchi mbalimbali zikiwemo Paris na Newzealand huku akieleza kupendezwa za muziki wa Jazz na Rock.

Alipoulizwa na jarida la Guiness World Report kuhusiana na fani hiyo alieleza kuwa, "Ninafikiri nilizaliwa na kipaji hiki na huwa sifanyi mazoezi kwa ajili ya afya ila ninapopiga muziki naona nafanya kitu cha tofauti, nahisi nna nguvu" ameeleza Dj. Sumirock.

Kuhusiana na vijana wanaopambana kutimiza ndoto zao Dj. Sumirock alinukuliwa akisema kuwa, "Nafasi zipo kila siku, wasikate tamaa na daima wasisite kujaribu kitu" alieleza.Dj. Sumirock ana ndoto za kusafiri duniani kote kwa kazi yake ya kupiga muziki.
Dj. Sumirock akifanya mambo yake

TFS YAWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI 11 KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO

$
0
0
Serikali kupitia Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imewasimamisha kutekeleza majukumu yao watumishi 11 wa TFS walioonekana kutenda makosa mbalimbali. Kati yao watatu wamefikishwa mahakamani kwa makosa ya uhujumu uchumi sambamba na watu wengine wawili.

Aidha, Serikali imezuia biashara ya mti wa Mkurungu kwa matumizi ya ndani au kusafirishwa nje ya nchi hadi hapo itakapotolewa taarifa nyingine.

Kusimamishwa kwa watumishi hao kunafuatia kubainika kwa uwepo wa magogo yaliyovunwa kinyume cha sheria na kutelekezwa katika maeneo mbalimbali kwenye vijiji na msituni kufuatia

va na Kikosi kazi cha kuzuia ujangili kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na kubaini baadhi ya watumishi kuonekana kushiriki katika uhalifu huo.

Kufuatia uchunguzi uliofanywa, gari moja lilikamatwa likiwa na mbao (slippers) 382 za mti wa Mkurungu na kuzuiliwa kwa uchunguzi ambapo watuhumiwa wawili walikamatwa. Aidha, mbao 825 zilikamatwa zikisafirishwa kwa treni katika stesheni ya Usule, Shinyanga na watuhumiwa 6 ambao ni watumishi wa shirika la reli kukamatwa kwa mahojiano.

Ili kudhibiti tatizo hili, uongozi wa Kikosi cha Taifa cha kuzuia Ujangili (NTAP), Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ulikutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Tabora (KUU) na kufikia maamuzi yafuatayo:

i.Kuzuia Halmashauri za Wilaya kupokea fedha au kuuza miti bila kuwa imeamriwa kwenye vikao vya uvunaji hali inayochochea wafanyabiashara kufadhili uvunaji haramu wa misitu.

ii.Kuhuisha kikosi cha kanda ya Magharibi cha kupambana na Ujangili

ii.Kamati ya Ulinzi na Usalama Tabora (KUU) kufuatilia mienendo ya wafanyabiashara wanaohisiwa kushirikiana na baadhi ya wageni kufadhili uvunaji haramu wa miti na uhalifu mwingine wa Maliasili mkoani humo.

Wizara ya Maliasili na Utalii ilipokea taarifa za uvunaji haramu wa miti hususani aina ya mkurungu katika kanda za Magharibi hususan katika wilaya za Urambo, Kaliuwa, Sikonge, mkoani Tabora na kutuma kikosi cha kufuatilia undani wa taarifa hizo.

Kwa sasa timu ya upelelezi inaendelea na kazi ili kuweza kubaini wahusika wote na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote watakaobainika kuhusika na uhalifu huo.

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK. SHEIN AHUDHURIA MKUTANO WA BLUE ECONOMY KENYA LEO

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Rais wa Jamuhuri ya Watu wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta leo Mjini Nairobi, katika ukumbi wa Jengo la Mikutano ya Kenyatta Nairobi baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Uchumi Endelevu wa Bahari, leo Jijini Nairobi.
 RAIS wa Jamuhuri ya Watu wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Uchumi Endelevu wa Bahari (Sustainable Blue Economy Conference) uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta Jijini Nairobi Nchini Kenya leo 26/11/2018 na kuwashirikisha Marais mbalimbali wa Nchi za Afrika.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa kuhusiana na Uchumi Endelevu wa Bahari (Sustainable Blue Economy Conference ) uliofanyika katika ukumbi wa Kmataifa wa mikutano wa Kenyatta, akiwasilisha Tamko la Serikala ya Jamuhuri ya Muungano, akimuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli.katika mkutano huo uliofanyika leo 26/11/2018, jijini Nairobi Kenya.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akifuatilia hutuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi Endelevu wa Bahari, (Sustainable Blue Economy) wakati Rais wa Jamuhuri ya Watu Kenya Mhe. Uhuru Kenyataa akihutubia na kuufungua Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Kenyatta Nairobi.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Marais wa Nchi mbalimbali akiwemo Rais wa Jamuhuri ya Watu wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta, wakielekea katika eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya upandaji wa miti kwa Marais waliohudhuria Mkutano huo.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akipanda mti katika viwanja vya Majengo ya Ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa ya Kenyatta Jijini Nairobi Nchini Kenya baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi Endelevu wa Bahari, uliofanyika leo.26-11-2018.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Marais wa Nchi mbalimbali waliohudhuria Mkutano wa Uchumi Endelevu wa Bahari (Sustainable Blue Economy ) uliofanyika Jijini Nairobi katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta leo, 26-11-2018. 
Picha na IKULU

ITUMIENI FURSA YA MSAADA WA KISHERIA KUTAMBUA HAKI ZENU- PROF. KABUDI

$
0
0

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akimpa mkono msanii Afande Sele baada ya kumaliza kutumbuza katika hafla ya ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria nchini uliofanyika mkoani Morogoro
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiangalia kitabu katika moja ya mabanda yaliyohudhuria uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria mkoani Morogoro , Prof. Kabudi alitembelea mabanda hayo baada ya kuzidua maadhimisho hayo mjini Morogoro
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza katika banda la Mahakama ambalo linashiriki maadhimisho ya wiki ya Msaada wa kisheria nchini ambayo ufunguzi wake kitaifa ulifanyika mkoani Morogoro uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria mkoani Morogoro
Wananchi waliofika kupata huduma ya msaada wa kisheria wakati wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria nchini katika picha ya pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe wakati wa uzinduzi wa wiki hiyo mjini Morogoro.
Wanasheria wa kujitegemea mkoani Morogoro katika picha ya pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe wakati wa uzinduzi wa maadhimisho y awiki ya msaada wa kisheria nchini uliofanyika mkoani Morogoro .
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe wakasalimia wananchi waliofika kuhudhuria uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria nchini uliofanyika mjini Morogoro.katika viwanja vya Shule ya Sekondari Morogoro

………………..

Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi amewataka wananchi kutumia fursa ya huduma za msaada wa kisheria ambayo inatolewa nchini ili kutambua haki zao na kuzipata kwa wakati.

Amesema wananchi wakiitumia huduma ya msaada wa kisheria itawawezesha kutambua haki zao na kuzipata kwa wakati , kufahamu sheria mbalimbali ikiwa ni pamoja na utaratibu unaotumiwa na Mahakama na hivyo kusaidia harakati za kupunguza msongamano Mahakamani. “Wananchi niwaombe mtumie fursa ya msaada wa kisheria ambayo Serikali imeridhia itolewe kwa wananchi wenye uhitaji, hii itasaidia kutambua haki zenu, kufahamu sheria na utaratibu unaotumika na Mahakama na hivyo kusaidia kupunguza msongamano Mahakamani” alisema Prof. Kabudi.

Prof. Kabudi amesema hayo mjini Morogoro alipokuwa akizindua maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria nchini ambayo inafanyika katika mikoa ya Morogoro, Singida, Tabora, Kagera na Kigoma kuanzia tarehe 26 Novemba hadi tarehe 30 Novemba ,2018. Amesema Wizara itaendela kutenga wiki moja kila mwaka kwa ajili ya kutoa msaada wa kisheria nchini ili kuhakikisha wananchi wengi wanafikiwa na huduma za msaada wa kisheia na hivyo kutimiza lengo la kutungwa kwa Sheria Na. 1 ya Msaada wa Kisheria ya Mwaka 2017.

Awali akizungumza katika ufunguzi hu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro DKt. Stephen Kebwe aliomba kupatiwa Mahakama mpya katika baadhi ya wilaya kama Mvomero na kupandishwa hadhi kwa baadhi ya Mahakama katika wilaya za mkoa huo ili kuwaondolea wananchi adha wanayoipata ya kufuata huduma hiyo kwa umbali mrefu. “Mhe. Waziri niombe kuongezewa Mahakama katika baadhi ya Wilaya kama Mvomero na Mahakama nyingine hasa za mwanzo zipandishwe hadhi na kuwa Mahakama za Wilaya ili ziweze kuwahudumia wananchi katika wilaya hizo,” alisema Dkt. Kebwe.

Maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria 2018 yanafanyika kwa kutoa huduma ya msaada wa kisheria kwa wananchi wenye uhitaji katika maeneo mbalimbali nchini, katika magereza , kutoa elimu ya sheria kwa umma ana kwa ana na kupitia machapisho.

TUMEKUSUDIA KUFANYA MAGEUZI MAKUBWA KWENYE SEKTA YA KILIMO-MHE HASUNGA

$
0
0


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza umuhimu wa sekta binafsi nchini wakati akifungua warsha ya Wadau wa Baraza la Kilimo na Mifugo Tanzania (ACT) katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es salaam tarehe 26 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya Wadau wa Kilimo na Mifugo nchini wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akifungua warsha ya Wadau wa Baraza la Kilimo na Mifugo Tanzania (ACT) katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es salaam tarehe 26 Novemba 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua bidhaa zilizoongezwa thamani ndani ya nchi wakati wa hafla ya warsha ya Wadau wa Baraza la Kilimo na Mifugo Tanzania (ACT) katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es salaam tarehe 26 Novemba 2018. Kulia ni Maryam Issa mtendaji wa Kampuni ya NatureRipe.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza wakati akifungua warsha ya Wadau wa Baraza la Kilimo na Mifugo Tanzania (ACT) katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es salaam tarehe 26 Novemba 2018.





Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam


Serikali imedhamiria kufanya mageuzi makubwa katika Sekta ya Kilimo ambapo Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Wizara za Sekta ya Kilimo (ASLMs) na wadau wa kilimo inatekeleza Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (Agricultural Sector Development Programme Phase Two-ASDPII).

Katika utekelezaji wa ASDP II serikali imelenga kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo (mazao, mifugo na uvuvi) ili kuongeza uzalishaji na tija, kufanya kilimo kiwe cha kibiashara na kuongeza pato la wakulima wadogo kwa ajili ya kuboresha maisha na usalama wa chakula na lishe.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo tarehe 26 Novemba 2018 wakati akifungua warsha ya Wadau wa Baraza la Kilimo na Mifugo Tanzania inayofanyika katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es salaam.

Alisema Utekelezaji wa lengo hilo ni kuhakikisha kuwa Taifa linaendelea kujitosheleza kwa chakula; kuimarisha uchumi; kuwa kichocheo cha kukua kwa viwanda; na kuongeza ajira ambapo ili kufikia malengo hayo; Utekelezaji wa ASDP II utazingatia mnyororo wa thamani wa mazao ya kipaumbele ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Mhe Hasunga alisema kuwa Serikali itaendelea kuboresha mifumo ya upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakulima na wafugaji na kwa bei nafuu.

“Tumeanza na mbolea ambapo kwa sasa inaagizwa kwa pamoja na tumeondoa kodi na tozo nyingi katika mbolea ili ipatikane kwa bei nafuu. Kwa sasa changamoto kubwa imebaki kuwa gharama kubwa ya usafirishaji hasa kwa maeneo ambayo hakuna usafiri wa reli ambapo Serikali bado inalifanyia kazi suala hili” Alikaririwa Mhe Hasunga na kuongeza kuwa

“Changamoto nyingine kama nilivyozitaja hapo awali tutaendelea kuzifanyia kazi na tunaomba wadau kupitia vyama vyenu na taasisi kilele kama Baraza la Kilimo, muendelee kutupa maoni yetu ya namna bora ya utatuzi na sisi tunaahidi kufanyia kazi maoni yenu”.

Kuhusu Masoko ya mazao ya kilimo Mhe Hasunga alisema kuwa serikali inatambua changamoto za masoko, usindikaji, miundombinu ya umwagiliaji na miundombinu mingine kwa ajili ya mifugo na uvuvi, upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakati na kwa bei nafuu, uhaba wa maafisa ugani, kero za kodi na tozo mbalimbali, wingi na mwingiliano wa taasisi za udhibiti huku akiahidi kuendelea kuzitafutia ufumbuzi.

“Baadhi ya kero hizi zimeshaanza kufanyiwa kazi. Mifano michache ni kuhusu tozo na kodi ambapo Serikali imeondoa kodi na tozo nyingi katika sekta ya Kilimo na bado tunaendelea kufanya maboresho katika eneo hilo.” Alisema
Aidha, alisema kuwa Wizara ya Kilimo inatambua mahusiano ya moja kwa moja kati ya Sekta ya Viwanda na ile ya Kilimo na pia changamoto zilizopo.

“Pamoja na dhamira ya Serikali iliyokuwepo katika kuweka mazingira mazuri ya biashara, ACT kama sehemu ya timu ya Kikosi Kazi Cha Taifa Cha Kuishauri Serikali Kuhusu Masuala ya Kodi, imekuwa ikitekeleza jukumu hilo bila kuchoka ambapo kwa kupitia ushauri huo, katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 na 2018/2019 Serikali imepunguza kodi na tozo nyingi sana katika sekta ya kilimo” Alisisitiza Mhe Hasunga

Alisema kutokana na jitihada hizi za ACT katika kuona kuwa kilimo kinakuwa moja ya ajenda kubwa kitaifa, Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imekubali kuwa na makubaliano maalumu na ACT (Memorandam of Understanding – MoU) kwa lengo la kuifanya sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya sekta ya kilimo nchini.

Warsha ya Wadau wa Baraza la Kilimo na Mifugo yenye kauli mbiu isemayo“Kilimo na Maendeleo ya Viwanda Tanzania” itafanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 26-27 Novemba 2018 ambapo wadau wa sekta ya Kilimo katika maeneo mbalimbali ya mnyororo wa thamani yaani kuanzia wazalishaji (wakulima, wafugaji na wavuvi), wasindikaji, watoa huduma mbalimbali kama wasafirishaji na wauza pembejeo, wafanyabiashara ya mazao, wasindikaji ikiwa na mada mbalimbali zenye kuakisi juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya Kuwa na Uchumi wa Viwanda ifikapo 2015.

Waziri Kamwelwe aomba subira kwa TBA

$
0
0


Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo ya Serikali Tanzania (TBA) mkoa wa Kagera, Mhandisi Herico Bahati (mwenye shati la batiki) akimpa maelezo mbalimbali Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kushoto) kuhusiana na ujenzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Ihungo, waliyoijenga baada ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mwaka 2016. Mbele ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bw. Philip Boniventura.
Waziri Mkuu wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (mwenye suti ya bluu) akimsikiliza Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo ya Serikali Tanzania (TBA) mkoa wa Kagera, Mhandisi Herico Bahati (mwenye shati la batiki) akimpa maelezo mbalimbali ndani ya moja ya vyumba 96 vya mabweni ya shule ya sekondari ya wavulana ya Ihungo, waliyoijenga baada ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mwaka 2016.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Wavulana ya Ihungo na wa shule ya sekondari Bukoba, wakinawa mikono katika mabomba ya kisasa, ambayo yamejengwa na Wakala wa Majengo ya Serikali Tanzania (TBA) baada ya shule hiyo kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mwaka 2016.

……………………………………………………………………………

Na Mwandishi Wetu, Bukoba
Aridhishwa ujenzi wa Ihungo Boys

WAKATI Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe ameomba taasisi za serikali, Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wizara, ambazo zimeipa kazi Wakala wa Majengo ya Serikali Tanzania (TBA), kuwa na subira kwa kuwa inaupungufu wa wafanyakazi, lakini ameridhishwa na ujenzi wa shule ya sekondari ya Wavulana ya Ihungo ya mkoani Kagera iliyojengwa na taasisi hiyo.

Akifafanua Mhe. Kamwelwe amesema TBA wanakumbwa na changamoto kubwa ya upungufu wa wafanyakazi, ambapo kwa Tanzania nzima wanawafanyakazi 300 pekee, ambao wanajitoa kwa kufanya kazi kwa bidii, ambapo idadi kamili inayotakiwa ni wafanyakazi 1700.

Hatahivyo, ameipongeza TBA kwa kufanya kazi nzuri za ujenzi mbalimbali za majengo ya serikali kwa kutumia thamani halisi ya fedha tofauti na wakandarasi binafsi wamekuwa na gharama kubwa.

“Utendaji wa TBA bado unaleta mashaka nchi nzima na nimefanya nao kikao nikabaini wapo wafanyakazi 300 pekee na wanatakiwa angalau 1000 ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi, hivyo nashauri pamoja na kusikia malalamiko kila upande kutoka kwa Wakuu wa Wilaya, Mikoa, Bungeni na Watendaji wengine wa serikali, ninayafanyia kazi likiwemo la uhaba wa wafanyakazi,” amesema Mhe. Kamwelwe.

Baadhi ya kazi za ujenzi wanazofanya na walizofanya TBA ni pamoja na ujenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma mkoani Dodoma; ujenzi wa hospital ya Mkoa wa Simiyu na Ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma mikoa mbalimbali.

Akizungumzia ujenzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Katika hatua nyingine, Mhe. Kamwelwe ameipongeza TBA kwa ujenzi wa shule ya kisasa ya sekondari ya wanaume ya Ihungo iliyoathirika na tetemeko la ardhi lililotokea Kagera 2016.

“Nawapongeza sana kwa kujenga shule nzuri tena kwa gharama nafuu ya Bil. 10.4, ukiangalia wengine walitaka kujenga kwa Bil. 36, hivyo TBA wameokoa fedha nyingi sana za Watanzania na kiwango chao cha kazi ni kizuri,” amesema Mhe. Kamwelwe.

Naye Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Kagera, Mhandisi Herico Bahati amesema ujenzi wa shule hiyo ulianza Oktoba 5, 2016, ambapo kuna majengo matatu ya ghorofa ya madarasa yenye vyumba 24, ofisi 12 za walimu, jengo la vyoo 80, mabweni matatu yenye vyumba 96, nyumba 30 za walimu, upanuzi wa bwalo la chakula na wamechimba kisima cha maji.

Shule hiyo inawanafunzi 600, ambapo sasa pia imeongezewa wanafunzi 751 wa shule ya Sekondari ya Bukoba waliohamishiwa hapo kwa muda baada ya shule yao kuezuliwa paa na upepo mkali uliotokea Oktoba 2018.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Muleba, ambaye pia anakaimu wilaya ya Bukoba Mjini, Mhandisi Richard Ruyangu ameishukuru serikali kwa kuijenga tena shule hiyo na sasa wanafunzi wanaendelea na masomo.

“Tunaishukuru serikali ya Awamu ya Tano ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa kutujengea tena shule nzuri na tunaimani kwa mazingira haya watoto watasoma kwa bidii, na hata walimu hali kadhalika watafundisha kwa moyo tumeona wamejengewa nyumba nzuri na za kisasa tena zipo maeneo ya karibu na shule itakuwa hawatoki mbali kuja kufundisha,” amesema Mhandisi Ruyangu.

Kiranja mkuu wa shule hiyo, Bw. Athuman Mohamed kwa niaba ya wanafunzi wenzake, ameishukuru serikali kwa kuwajengea tena shule yao na wameahidi kusoma kwa bidi ili kufanya vizuri katika masomo yao.

MKAZI WA MBEYA AJISHINDIA NYUMBA NA SH MILIONI 20 ZA BIKO,AKABIDHIWA.

Viewing all 46379 articles
Browse latest View live




Latest Images