Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1732 | 1733 | (Page 1734) | 1735 | 1736 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku ameitaka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kutumia vifaa vilivyopo katika karakana zake kuchonga vipuli na kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa mahitaji mbalimbali nchini.
  Butiku alitoa ushauri huo wakati wa mahafali ya chuo cha VETA Dar es Salaam yaliyofanyika Novemba 23, 2018.
  Alisema baada ya kutembea kwenye karakana mbalimbali na kuhojiana na walimu na wanafunzi, amebaini kuwa VETA ina rasilimali na hazina kubwa ya mashine na ujuzi wa walimu na wanafunzi ambao ukitumiwa vyema unaweza kuzalisha vitu vingi ambavyo kwa kiasi kikubwa bado vinafanywa na watu binafsi au kununuliwa kutoka nje ya nchi.
  “nimejionea vifaa vingi ambavyo naamini vikitumika vizuri vinaweza kuleta manufaa makubwa sana kwa taifa, ifike mahali sasa vifaa mlivyonavyo katika karakana zenu viweze kutengeneza mashine nyingine kwa ajili ya matumizi mbalimbali ” Alisema
  Alitoa mfano wa karakana ya uchapaji ambayo alisema ikiimarishwa inaweza kufanya shughuli nyingi sana za uchapaji wa vitu mbalimbali kwa kuwa ina vifaa na wataalam muhimu vya kuweza kufanya shughuli hizo kwa ufanisi mkubwa.
  Sambamba na hilo, aliishauri VETA kuanzisha masomo ya sanaa kama vile nyimbo na ngoma za asili kwa kuwa sanaa hizo kwa sasa ni ajira kwa vijana na zikiwekewa utaratibu mzuri zitakuwa na manufaa makubwa kwa nchi huku akiwaasa wahitimu kutumia vyema ujuzi walioupata kujitengeneza ajira zao wenyewe kupitia vikundi.
  Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt Pancras Bujulu alisema mamlaka hiyo inaendelea na juhudi mbalimbali za kuhakikisha inazalisha mafundi stadi mahiri watakaoweza kukidhi mahitaji ya soko la ajira na kushiriki kikamilifu katika miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ikiwa ni pamoja na mwelekeo kwenye uchumi wa viwanda.
  Alivitaka vyuo vya ufundi stadi kuweka nguvu katika kuendeleza vipaji vya vijana kwa kuwa vijana wengi wanaosoma katika vyuo hivyo wana vipaji ambavyo vikiendelezwa vinaweza kuwanufaisha na kuendelea.
  Dkt. Bujulu alitumia fursa hiyo pia kuwatangazia na kuwataka wahitimu, wanafunzi na walimu wenye ubunifu kushiriki kwenye mashindano ya kitaifa ya sayansi, teknolojia na ubunifu yaliyozinduliwa Novemba 14, yakiwa na lengo la  kuibua vipaji na kuhamasisha uendelezaji wa teknolojia na ubunifu  utakaoweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo endelevu ya viwanda, kuongeza tija ya uzalishaji wa malighafi, kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa nchini pamoja na kuboresha shughuli nyingine za kiuchumi.
  Aliwasihi wafanyakazi wa VETA kutumia utaalam walionao kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika vyuo kwa kutumia rasilimali zilizopo na kuongeza kuwa VETA itaendelea na jitihada za kuhakikisha elimu na mafunzo ya ufundi stadi inawafikia wananchi wengi zaidi ili watanzania wengi wanufaike nayo .
  Awali, Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Dar es Salaam Violeth Fumbo alisema jumla ya vijana 536 wamehitimu ambapo 523 wamehitimu ngazi  za ufundi stadi daraja la pili katika fani 20 za ufundi na 13 wamehitimu Diploma ya Ubunifu wa nguo na mitindo ya mavazi.
  Alisema pamoja na wahitimu hao wa kozi za muda mrefu, chuo hicho kimeendelea kuboresha huduma zake ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya muda mfupi kulingana na mahitaji na kwamba kwa mwaka huu chuo hicho kimeweza kutoa wahitimu wa kozi za muda mfupi 10,300.
  Naye mwakilishi wa waajiri kutoka kampuni ya PLASCO Fidelis Mashauri alisema waajiri wamejenga imani kubwa kwa vijana wanaotoka katika vyuo vya VETA kwa kuwa wanaonekana  wamepikwa vyema na kuwa mahiri katika fani zao.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku akizungumza katika mahafali ya 48 ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Pili ya Chuo VETA Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt Pancras Bujulu akizungumza kuhusiana na mpipango ya VETA katika kutoa ujuzi bobezi katika kupunguza uhaba mafundi katika mahafali ya 48 ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Pili ya Chuo VETA Chang’ombe jijini Dar es Salaam. 
   Mwakilishi wa waajiri kutoka kampuni ya PLASCO Fidelis Mashauri akitoa maelezo ya mchango wa VETA katika mahafali ya 48 ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Pili ya Chuo VETA Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
   Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Dar es Salaam Violeth Fumbo akitoa taarifa katika katika mahafali ya 48 ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Pili ya Chuo VETA Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
  Wahitimu wakionyesha umahiri wao katika  katika mahafali ya 48 ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Pili ya Chuo VETA Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

  0 0


  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola, akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Kamulebya, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, wakati Mbunge huyo alipofanya ziara katika kijiji hicho kusikiliza kero za wapigakura wake pamoja na kuwahamasisha kuanza maandalizi ya kilimo kwa kuwa msimu wa kilimo umeshafika. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
  Mkazi wa Kijiji cha Kamulebya, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara akimuuliza swali Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (hayupo pichani), wakati Mbunge huyo alipofanya ziara katika kijiji hicho kusikiliza kero za wapigakura wake pamoja na kuwahamasisha kuanza maandalizi ya kilimo. Lugola aliwapa nafasi wananchi kutoa kero zao ndani ya Jimbo lake. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kulia), akimsikiliza Afisa Tarafa ya Kenkombyo, Rebeca Mdodo alipokua anatoa taarifa ya Tarafa yake kwa Waziri Lugola, kabla ya Mbunge huyo hajaanza kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Bulamba, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara. Lugola ameanza ziara jimboni humo leo akisikiliza kero za wapigakura wake pamoja na kuwahamasisha kuanza maandalizi ya kilimo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0


  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia ubora wa tofali linalotengenezwa na wafungwa ikiwa ni mpango wa uongozi wa gereza la Kwamngumi kukabiliana na changamoto ya makazi kwa askari, Kulia ni Mkuu wa Gereza hilo,Christopher Mwenda, lililopo Wilayani Korogwe, mkoani Tanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia ubora wa nyumba iliyojengwa na matofali yanayotengenezwa na wafungwa katika Gereza la Kwamngumi lililopo Wilayani Korogwe, mkoani Tanga. Kushoto ni Mkuu wa Gereza hilo, Christopher Mwenda. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia tofali ambazo zimetengenezwa na wafungwa wa Gereza la Kwamngumi, ambazo hutumika kujengea nyumba za askari ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli la kutaka wafungwa watumike katika shughuli za uzalishaji na kilimo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(aliyevaa Kaunda suti), na ujumbe alioongozana nao wakipita mbele ya nyumba iliyojengwa kwa kutumia matofali yanayotengenezwa na wafungwa katika Gereza la Kwamgumi lililopo Wilayani Korogwe, mkoani Tanga.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  Serikali imeteua jumla ya magereza kumi nchini ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli la kulitaka Jeshi la Magereza litumie rasilimali watu ya wafungwa kuzalisha mazao kwa ajili ya biashara na chakula badala ya serikali kuingia gharama ya kulisha wafungwa.

  Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa agizo hilo katika Gereza la Kwamngumi wilayani Korogwe ,mkoani Tanga, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alisema utekelezaji huo unaenda sambamba na uteuzi wa magereza kumi ya kilimo nchini na akiweka wazi uwapo wa mpango maalumu wa kutathmini na kupima mpango mkakati huo kwa kila gereza.

  Aliyataja magereza hayo kuwa ni Songwe (Mbeya), Kitai (Ruvuma), Ludewa (Njombe), Mollo (Rukwa), Kitengule (Kagera) ambayo yameteuliwa kulima mahindi, mengine ni Idete na Kiberege (Morogoro) yaliyoteuliwa kulima mpunga huku Kitete (Rukwa), Kitengule (Kagera) na Gereza la Arusha yakiteuliwa kulima maharagae

  “Tunahitaji matumizi sahihi ya rasilimali watu na ardhi tuliyonayo katika magereza yetu itumike ipasavyo kwa shughuli za uzalishaji ili tuweze kutekeleza amri ya Mheshimiwa Rais, huku lengo la wizara kupitia jeshi la magereza ni kuweza kuwekekeza fedha kwa kulitumia shirika la uzalishaji mali lililopo ndani ya jeshi hilo na ikiwezekana hapo baadae tuweze kutafuta wateja watakaonunua mazao yatakayozalishwa katika mashamba hayo,” alisema Masauni

  Akizungumza katika ziara hiyo, Mkuu wa Gereza la Kwangumi, Christopher Mwenda, alisema wao kama uongozi wa gereza hilo wamejipanga vizuri katika utekelezaji wa aguzo hilo huku akiiomba wizara kuongeza vifaa vya kilimo ili waweze kuzalisha kwa kiwango kikubwa zaidi.

  0 0


  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akipokea shukrani za Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Moa, Rambazo A. Mohamedi (wa kwanza kushoto) kwa kurasimisha bandari bubu ya Moa kuwa bandari rasmi. Wa pili kushoto ni Mkuu wa bandari ya Tanga, Percival Salama

  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akipokea taarifa ya utendaji kazi wa Bandari ya Tanga kutoka kwa Mkuu wa Bandari ya Tanga, Percival Salama (aliyesimama katikati) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua bandari hiyo

  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akisikiliza kwa makini maelezo kuhusu upakuaji wa mafuta melini kutoka kwa Nahodha Andrew Matilya wakati wa ziara yake ya kukagua bandari ya Tanga. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Bandari ya Tanga, Percival Salama
  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akipokea taarifa kuhusu bandari bubu ya Moa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Yona Mark wakati wa ziara yake ya kukagua bandari bubu mkoani Tanga. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Bandari ya Tanga, Percival Salama


  …………………………………………………………………………..


  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amerasimisha bandari bubu nne mkoani Tanga kati ya bandari bubu 48 zilizopo mkoani humo wakati wa ziara yake ya kukagua bandari bubu hizo na kupata taarifa ya utendaji kazi wa bandari ya Tanga. Nditiye amerasimisha bandari bubu ya Moa iliyopo Wilayani Mkinga, Kigombe (Muheza), Kipumbwi na Mkwaja zilizopo wilayani Pangani.

  Nditiye amesema kuwa amerasimisha bandari bubu hizo nne tu kati ya bandari bubu 48 zilizopo mkoani Tanga kwa kuwa zipo mbali na bandari ya Tanga, zipo mipakani na nchi za jirani, kusogeza huduma karibu na wananchi na kuiwezesha Serikali kukusanya tozo na kodi mbali mbali kwa ajli ya kutoa huduma kwa wananchi. “Naiagiza TPA kuhakikisha kuwa bandari bubu nne nilizorasimisha zinafanya kazi ifikapo mwishoni mwa mwezi Januari mwaka 2019 na wahakikishe kuwa watumishi wa TPA na TRA wanakuwepo kwenye bandari hizo pamoja na ofisi zote za Serikali zinazohitajika ikwemo Jeshi la Polisi,”.

  Pia ameitaka TPA kwa kushirikiana na TRA itoe elimu kwa wateja kuhusu umuhimu wa kulipa kodi ya Serikali kwa kuwa kiwango cha kodi kinachotozwa ni kidogo ukilinganisha na athari wanazopata wananchi na wafanyabiashara kwa kuhatarisha maisha yao kwa kukwepa kodi na kutumia bandari bubu kupitisha mizigo na bidhaa nje ya bandari rasmi zilizopo na kupita maporini. Nditiye amesema kuwa, “tunahitaji bandari zetu zifanye kazi, wateja ni wengi na wana imani na nchi yetu kutokana na hali ya usalama iliyopo na ndio maana Serikali inapanua bandari ya Dar es Salaam na kuboresha bandari ya Tanga, tusisikilize maneno ya watu wachache wasio itakia mema nchi yetu katika ukuaji wa uchumi,”.

  Nditiye amesema kuwa lengo la Serikali ni kudhibiti uwepo wa bandari bubu nchini ili kuhakikisha kuwa wananchi wanatumia bandari rasmi zilizopo bila kukwepa kodi ili Serikali iweze kukusanya mapato kwa ajili ya kukuza uchumi na kuongeza pato la taifa letu. 
   
  Amefafanua kuwa kodi inayotozwa na Serikali ni ndogo hivyo hamna haja ya wananchi kutumia bandari bubu kuhatarisha maisha yao kwa kusafirisha bidhaa na mizigo mbali mbali kwa njia ya magendo ambapo bidhaa nyingine zinakuwa zimepitwa na muda wa matumizi hivyo kuhatarisha afya ya watumiaji, zinakosa ubora na viwango vinavyohitajika kwa kuwa hazijakaguliwa na taasisi husika za Serikali kama vile Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA). Nditiye ametoa rai kwa watanzania kutoa taarifa za baadhi ya wavivu wasio waaminifu wanaohujumu uchumi kwa kujifanya wavuvi kwa kupakia, kushusha na kusafirisha bidhaa kwa njia ya magendo kwa kutumia bandari bubu.

  Naye Mkuu wa Bandari ya Tanga, Percival Salama amekiri uwepo wa bandari bubu 48 mkoani Tanga ambapo amebainisha uwepo wa bandari bubu 12 Wilayani Mkinga, Tanga (20), Muheza (1) na Pangani (15). Katika hatua nyingine, Salama ameiomba Serikali kupitia kwa Nditiye kuhakikisha kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya kazi ya ukaguzi kwenye magari ya mizigo yanayokwenda nje ya nchi kutoka ukaguzi wa kwenye vituo 37 hadi vituo vitatu tu vya barabarani ili kupunguza kero na kuathiri mnyonyoro wa thamani na uchumi wa taifa letu na kushauri kuwa ukaguzi ufanyike kwenye maeneo yenye mizani ili kupunguza ucheleweshaji wa safari za magari hayo na kero kwa wafanyabiashara. Ameongeza kuwa Bandari ya Tanga ni bandari yenye kina kirefu kuanzia mita 12 hadi zaidi ya mita 20 na ina uwezo wa kuhudumia nchi saba zinazopakana na Tanzania

  Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Mkinga, Mkuu wa Wilaya hiyo, Yona Mark ameishukuru Serikali kwa kurasimisha Bandari bubu ya Moa iliyopo wilayani humo na wananchi wa kijiji cha Moa wametoa eneo kwa ajili ya TPA kuendesha shughuli za bandari hiyo. Pia, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Moa, Rambazo A. Mohamedi amesema kuwa wananchi wako tayari kushirikiana na Serikali ya Wilaya hiyo, Mkoa, TPA na taasisi nyingine za Serikali kuanzisha na kuendesha bandari ya Moa kwa kuwa iko umbali wa kilomita 14 tu kutoka kijijini hapo na nchi jirani ya Kenya.

  Nditiye amewashakuru wananchi wa kijiji cha Moa kwa kutoa eneo lao kwa ajili ya bandari ya Moa na kuwaahidi kuwa watumishi wa TPA na TRA watakuwa Moa ifikapo mwezi Januari, 2019 na amewaomba wananchi wa kijiji hicho kuwapa ushirikiano. “Tanzania tuna eneo lenye ufukwe mrefu, kati ya vitu vinavyotupa changamoto ni kufidia ardhi, ila tunawashukuru wananchi wa Moa kwa kutoa eneo lenu ili litumike kuwa bandari,” amesema Nditiye

  0 0
  Mrakibu wa Polisi Joseph Charles Bukombe mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani mkoani Arusha


  Na. Vero Ignatus, Arusha

  Madereva wa mabai ya kubebea abiria katika mkoa wa Arusha wamepatiwa mafunzo ilihali wengine waki3ndelea na mafunzo

  Akizungumza Mrakibu wa polisi Joseph Charles Bukombe mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani mkoani Arusha amesema lengo kuu ni kuhakikisha kuwa madereva wote wanapata elimu na wanatoa huduma inayoendana na elimu waliyoipata

  Tangia kuanzishwa kwa mafunzo ya madereva miezi minne iliyopita madereva 1600 wamehitimu mafunzo wa magari ya kubeba abiria (PSV)kupitia chuo cha Veta pamoja na chuo rafiki wa NIT cha Moden driving vyote vya mkoa wa Arusha.

  "Pamoja na mapambano hayo ya ajali za barabarani ni lazima kuhakikisha kuwa wapo madereva wenye weledi" alisema Bukombe. Aidha amesema mafunzo haya yamesaidia sana kwani mkoa hapo pamekuwa salama bila Ajali ."Tangia tumeanzisha mafunzo takribani miezi minne iliyopita kwa mkoa wa Arusha tupo salama, na ukikuta ajali imesababishwa na bodaboda na siyo magari ya abiria" alisema Bukombe

  Mara baada ya kuona ajali zimeongezeka jeshi la polisi liliendesha ukaguzi wa leseni na kugundua kuwa madereva wengi wana leseni lakini hawana vyeti, kwahiyo yamkini wanazipata leseni kwa njia wanazozijua wao."Sisi tukasema hawawezi kuendelea na leseni walizonazo badala yake warudi darasani kwenda kusoma ili waweze kupata vyeti"alisema

  Akizungumza wimbi la Magari ya viongozi wa serikali kupata ajali Bukombe amesema hakuna aliye juu ya sheria kwani hata madereva hao wameshaanza kushughulikiwa,"Mara ya kwanza ulipita tu kama upepo wa kuwasaha ulakini sasa unapoaona kitu kinazidi kuleta shida ule upepo tumeshafutilia mbali na wao wanachukuliwa hatua "alisema

  Amesema Jeshi la polisi linafikiria ninamna gani wanaweza kushirikiana na wizara kuhakikisha madereva wao wanawapeleka mafunzoni.Aidha Bukombe ametoa wito kwa madereva wakaidi ambao hawaoni umuhimu wa kuingia darasani, wale ambao wanasubiri waone ninini hatima ya jambo hilo amewashauri kuw ni vyema wakarudi darasani kujisomea wasisibirie matokeo kwani jeshi la poisi hatitawafumbia macho.

  Bikombe amesema maelekezo hayo yalipoyolewa na serikali yalikuwa ni kwa minubu wa miezi mitatu ambapo zoezi hilo likikuwa limalizike tarehe 1 novemba 2018, ikaonekana vyuo vilelemewa na maderevya hivyo serikali ikaongeza hadi miezi miwili hivyo litamalizika januari mosi 2019

  Ukaguzi wa leseni na vyeti utaendeshwa rasmi januari mosi 2019 hivyo madereva ambao watakutwa hawana leseni na vyeti sheria itafuata mkondo wake.

  0 0


  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (wakwanza kulia)  akitizama mboga za majani zilizokaushwa na kuhifadhiwa  katika paketi kwa ajili ya kuuzwa alipotembelea leo banda la wajasiriamali kutoka kikundi cha Amka Group cha Tabora Mjini kushoto ni Mjasiriamali wa kikundi hicho Bi.Anna Shango ambao wameshiriki maonesho ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji  linaloendelea Mkoani Tabora (wapili kulia) ni Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe.Joseph Kakunda uwanja wa Jeshi.
  PIX 2
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe  akitizama uyoga uliyokaushwa na kuhifadhiwa  katika paketi kwa ajili ya kuuzwa alipotembelea leo banda la wajasiriamali kutoka Mwamko Women Group kutoka Halmashauri ya Sikonge anayetoa maelezo ni Bi.Joyce Robert ambao wameshiriki maonesho ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji  linaloendelea Mkoani Tabora uwanja wa Jeshi.
  PIX 3
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (katikati)  akitizama viungo vya mbalimbali vya chakula vilivyosagwa na kuhifadhiwa  katika vikopo kwa ajili ya kuuzwa alipotembelea leo banda la wajasiriamali kutoka Wilaya ya Uyui ambao wameshiriki maonesho ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji  linaloendelea Mkoani Tabora katika uwanja wa Jeshi.
  PIX 4
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (wakwanza kulia)  akitizama sabuni ya kuogea iliyotengenezwa na mjasiriamali  Bi.Neema Paulo na amempongeza  kwa kuweka picha yake  kuthibitisha ubora wa sabuni hiyo  alipotembelea banda la wajasiriamaliwa wa Wilaya ya Kaliua  leo kilichoshiriki maonesho ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji  yanayofanyika Mkoani Tabora katika uwanja wa Jeshi.
  PIX 5
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (wakwanza kushoto)  na Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe.Joseph Kakunda (katikati) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Aggrey Mwanri wakifurahia maziwa yanayotengenezwa na Neema Brand mjasiriamali mdogo wa Mkoa huo leo walipotembelea Maonesho ya wajasiriamali waliyoshiriki maonesho  ya Jukwaa la Fursa za Biashara  katika uwanja wa Jeshi linaloendelea Mkoani hapo,kushoto ni Bi.Sameera Sumar mmilikiwa biashara hiyo.
  PIX 6
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (kushoto)  akitizama kiatu cha kiume kilichotengenezwa kwa ngozi  kwa ustadi mzuri  na mmoja wa wajasiriamali  wa mkoa wa Tabora  Bw.Baraka Vuzuka leo alipomtembelea maonesho ya wajasiriamali  yanayoendelea  katika Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji katika uwanja wa Jeshi .
  PIX 7
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (kushoto)  akitizama  zulia lillofumwa kwa mikono na Mjasiriamali  Bw.Hassan Rashid (kulia) kwa kutumia mikono  na mifuko ya sandarusi iliyokwisha kutumika na nzuri  leo  alipotembelea maonesho ya wajasiriamali  waliyoshiriki Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji  linaloendelea Mkoani Tabora katika uwanja wa Jeshi.

  0 0
  Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga akikagua ghala la kuhifadhia mbegu la Wakala wa Mbegu (ASA) katika ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro tarehe 24 Novemba 2018. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa ASA Dkt Sophia Kashenge.(Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo).

  Mtendaji Mkuu wa ASA Dkt Sophia Kashenge akimuonyesha Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga mfuko wa mbegu za alizeti zinazozalishwa na ASA wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro tarehe 24 Novemba 2018.

  Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga akikagua ghala la kuhifadhia mbegu la Wakala wa Mbegu (ASA) katika ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro tarehe 24 Novemba 2018.  Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga akikagua mbegu mbalimbali zinazozalishwa na Wakala wa Mbegu (ASA) katika ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro tarehe 24 Novemba 2018.
  ………………………………………………………………………………


  Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo-Morogoro

  Imebainika kuwa malighafi nyingi zinazozalishwa kwa ajili ya viwanda nchini zinatokana na sekta ya kilimo ambayo inategemewa na watanzania kwa zaidi ya asilimia 75.

  Hayo yamebainishwa tarehe 24 Novemba 2018 na Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati akizungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Mbegu (ASA) katika ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro.

  Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imejipambanua katika usimamizi madhubuti wa ujenzi wa viwanda hivyo wananchi wanapaswa kuzalisha kwa wingi mazao mbalimbali katika sekta ya kilimo kwani uhai wa viwanda vingi vinategemea zaidi sekta ya kilimo.

  Alisema kuwa Wizara ya kilimo itasimamia kwa weledi uzalishaji wa mazao mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuzalisha mbegu bora na kwa wingi ili wakulima waweze kunufaika katika uzalishaji wenye tija ili kuondokana na uzalishaji wa mazao kwa ajili ya chakula pekee badala yake kuzalisha kwa tija kilimo cha kibiashara.

  “Katika viwanda tutakavyozalisha zaidi ya asilimia 60 ya malighafi zitakazotumika zinazalishwa hapa nchini, hivyo tunawajibu wa kutoa malighafi zinazotosheleza viwanda tunavyovianzisha” Alikaririwa Mhe Hasunga

  Alisema kuwa wafanyakazi wote wa Wakala wa Mbegu (ASA) wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa kwani ndio silaha pekee itakayowafanya waweze kuzalisha mbegu nyingi kwa manufaa ya mkulima mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla wake.

  Alisema kuwa serikali ina mpango kabambe wa kuimarisha sekta ya kilimo nchini kitakachopelekea kupata chakula cha kutosha, kuongeza tija katika uzalishaji na kuongeza thamani ya mazao hayo.

  “Huwezi kuwa na viwanda mpaka uanzie kwenye kilimo na kilimo hakiwezi kustawi bila kuwa na mbegu bora za mazao hivyo wakala wa mbegu ni Taasisi muhimu nchini kwenye sekta ya kilimo” Alisisitiza Mhe Hasunga

  Aidha, Mhe Hasunga alisema kuwa wakulima wengi wamekuwa wakilima bila kufuata taratibu za kilimo hivyo wataalamu mbalimbali wa kilimo nchini wanatakiwa kufanya kazi zaidi kwenye maeneo ya wakulima kwa kufika mashambani ili kuwaongezea weledi na ujuzi wakulima kote nchini.

  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokutana na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. Festus Limbu (watatu kulia) na baadhi ya Watendaji wa Baraza hilo, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Novemba 24, 2018. Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Maimuna Tarishi, wapili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Baraza, Suleiman Malela na kulia ni Mchumi wa Baraza, Erad Mushi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimina na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. Festus Limbu kabla ya mazungumzo yao yaliyowashirikisha, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mainuna Tarishi na Watendaji wa Baraza. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Novemba 24, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0  Mchezaji wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Bunge “Ndugai Boys”, William Ngeleja akiambaa na mpira wa kati wa mazoezi ya timu hiyo inayojiandaa na michuano ya Mabunge ya Jumuia ya Afrika Mashariki jijini Bujumbura Burundi mapema mwezi ujao. Ngela pia ni Mwenyekiti wa Bunge Sport


  Naibu Waziriu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, na mchezaji wa timu ya Mpira wa Pete ya Bunge , Dk. Angelina Mabula akimiliki mpira mbele ya wachezaji wa timu ya Chuo cha Mipango wakati wa mchezo wa kirafiki baina ya timu . Bunge Queens inajiandaa na michezo ya Mabunge ya Jumuia ya Afrika Mashariki itakayofanyika Bujumbura Burundi kuanzia Desemba mosi mwaka huu

  Wachezaji wa Bunge Sports Club, kutoka kushoto Massay, Venance Mwamoto na Angelina Mabula wakifanya mazoezi Uwanja wa Jamhuri leo.
  Mbunge wa Manyoni mashariki na Mkimbia wa timu ya Bunge Sports Club, Daniel Mtuka akifanya mazoezi Uwanja wa Jamhuri.
  Mchezaji wa timu ya Bunge ya Netbal, Agness Marwa akimiliki mpira wakati wa mazoezi ya timu hiyo leo.  Kocha wa timu Netiboli, Eleonora Mongi (mwenye mpira) akizungumza na wachezaji wake.
  Wachezaji wa mpira wa Miguu wa Bunge FC ‘Ndugai Boys’ wakifanya mazoezi Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo tayari kwa kushiriki michuano ya Mabunge ya Afrika Mahsriki Bujumbura Burundi mapema mwezi ujao.
  TIMU ya Bunge Sport Club imeendelea na mazoezi makali katika uwanja wa Jamhuri Jijini hapa kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya michezo ya Wabunge wa Afrika Mashariki yanayotarajiwa kuanza Desemba mosi mwaka huu Jijini Bujumbura nchini Burundi.

  Gazeti hili limefika katika uwanja wa Jamhuri jana asubuhi na kushuhudia timu hiyo ikiendelea na mazoezi makali ambapo kwa upande wa Soka ilikuwa chini ya Kocha Msaidizi ambaye ni Mbunge wa Wawi,Ahmed Juma Ngwali.Kwenye Netiboli timu hiyo ilikuwa ikicheza mchezo wa kirafiki na Chuo cha Mipango huku Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angelina Mabula akionesha ufundi mkubwa wa kufunga mabao.

  Aidha wakimbiaji wake, Daniel Mtuka, Yosepha Komba, Zubeda Sakuru nao walikuwa wakifanya maozezi ya kukimbia kujiweka sawa na mashindano hayo.Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini hapa,Kocha Mkuu wa timu ya Soka,Venance Mwamoto alisema wamejiandaa kufanya vizuri katika mashindano hayo na kuwatoa kimasomaso Watanzania.Mwamoto ambaye ni Kocha mchezaji na Mbunge wa Kilolo, alisema kwa sasa timu za Taifa zimekuwa zikifanya vibaya katika mashindano mbalimbali hivyo akawataka Watanzania kuamini kwamba timu ya Bunge la Tanzania itawafuta machozi kwa kufanya vizuri.

  “Hivi karibuni tumefanya vibaya kwa timu yetu ya Taifa kwa kufungwa na Lesotho pia timu ya Vijana nayo ilipoteza mategemeo yapo kwetu niwaahidi Watanzania hatutawaangusha,”alisema Mwamoto.Kuhusiana na maandalizi ya mashindano hayo,Mwamoto alisema wameweka kambi ya zaidi ya wiki tatu pamoja na kucheza michezo miwili ya kirafiki ili kuangalia mapungufu ya timu kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.

  Mwamoto ambaye amewahi kuzichezea timu za Majimaji ya Ruvuma,RTC Kagera na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ miaka ya nyuma,alisema kwa sasa timu hiyo ina majeruhi wawili ambao ni Mbunge wa Rufiji Mohammed Mchengerwa na Sixtus Mapunda ambaye ni Mbunge wa Mbinga Mjini .Kwa upande wake,Kocha wa timu Netiboli, Eleonora Mongi alisema maandalizi yanaendelea vizuri kwa mchezo huo lakini changamoto wanayokutana nayo ni kumkosa Mbunge wa Tarime Mjini,Ester Matiko kutokana na kesi inayomkabili.

  Alisema Matiko ni mchezaji muhimu katika kikosi hicho kutokana na kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani.Kocha huyo alisema wanauhakika wa kutetea ubingwa wa mashindano hayo kutokana na maandalizi ya kueleweka waliyoyafanya.Mbunge wa Viti Maalum,Agnes Marwa (CCM) aliwatoa wasiwasi Watanzania kwa kuahidi kwamba timu hiyo itarudi na ubingwa wa mashindano hayo.

  0 0


  Meli kubwa itakayotumika kurekodi taarifa za mtetemo kwa kina kifupi cha maji wakati wa zoezi la utafiti wa mafuta na gesi asilia katika maeneo ya Unguja na Pemba ya Stanford Bateleur ikiwa imefunga gati Bandari Malindi ikiwa tayari kuanza kazi hiyo wiki ijayo.
  Nahodha wa meli ya Stanford Bateleur Raul Mendoza akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu meli hiyo inavyofanyakazi ya kurekodi mtetemo wakati wa zoezi la utafiti wa mafuta na gesi asilia katika kina kifupi cha maji
  Mkurugenzi Uwezeshaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa utafutaji na Uchimabaji wa Mafuta na Gesi AsiliaOmar Zubeir Ismail akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya ujio wa meli ya Stanford Bateleur inayorekodi mtetemo katika kina kifupi cha maji.
  PICHA NA RAMADHANI ALI MAELEZO

  …………………..

  Na Mwashungi Tahir ,Maelezo

  Mkurugenzi wa Uwezeshaji Mamlaka ya Udhibi wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar Omar Zubeir Ismail alisema SeriKali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na utafiti wa mafuta na Gesi Asilia kwa njia ya mtetemo kwa kitalu cha Pemba Zanzibar.

  Hayo ameyasema leo huko Bandarini Malindi wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana kuwasili meli kubwa ya kurekodi mtetemo wakati wa zoezi la utafutaji wa mafuta na gesi asilia kwenye kina kifupi cha maji.

  Aidha alichukua nafasi kwa kuwajuilisha wananchi kazi ya utafiti wa mafuta na gesi Asilia kwa njia ya mtetemo bado inaendelea kwa upande wa kina kifupi cha maji (TRANSITION ZONE 2D SEISMIC SURVEY) katika maeneo ya visiwa hivyo.

  “Nachukua nafasi hii kuwajuilisha wananchi kwamba suala la uchimbaji wa mafuta na gesi asilia ni la muda mrefu na linaweza kufika hadi miaka kumi kukamilika nawaomba muendelee na kazi zenu za kawaida”. Alisema Mkurugenzi huyo.

  Alisema tumuombe Mungu tufanikiwe suala hili kwani likifanikiwa ni la wote kwa maendeleo ya nchi yetu na vizazi vyetu vya hapo baadae. Pia alisema meli zitakazotumika katika zoezi la mtetemo kwa kina kifupi cha maji tayari zimeshawasili nchini kwa ajili ya kuanza kazi hiyo.

  Mkurugenzi huyo alielzea meli zitakazotumika ni MV DP STANFORD yenye urefu wa mita 86 ambayo itatumika kwa ajili ya kurikodi taarifa za mtetemo.nyengine ni MV HAIBAO yenye urefu wa mita 25 ambayo tatumika kwa ajili ya kutoa mawimbi sauti na kutakuwa na CHASE BOAT NA FAST BOAT ambazo zitatumika kwa ajili ya kutoa ulinzi wakati wa zoezi hilo pamoja na boti ndogo ndogo zinazoitwa RUBER BOAT kwa ajili ya kubebea vifaa.

  Alisema zozi hili liko chini ya dhamana ya kampuni ya RAKGAS ya nchini RAS-AL KHAIMAN na linafanywa na Kampuni ya BGP INTERNATIONAL yenye makao Makuu yake nchini China na zoezi hilo linasimamiwa na taasisi za Serikali ambazo ni mamlaka ya udhibiti wa utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar (ZPRA) na kampuni ya maendeleo ya mafuta na gesi asilia ya Zanzibar (ZPDC).

  Vile vile alisema tarehe 27-Oktoba 2017 ilizinduliwa Meli utafiti wa mafuta na Gesi Asilia kwa kutumia meli maalum ya Kampuni ya BGP kutoka China kwa ajili ya kufanya zoezi la mtetemo katika kina kirefu cha maji baharini na kazi hiyo ilikamilika mnamo tarehe 28 Novemba 2017 katika visiwa vya Pemba na U nguja na kazi hiyo ya mtetemo kwa maeneo ya ardhini nchi kavu kwa visiwa hivi imeshakamilika.

  Nae Nahodha wa MV Stanford Bteleur Raul Mendoza alisema kazi ya utafitaji wa mafuta na gesi asilia katika kina kifupi cha maji itachukua kiasi ya miezi miwili kukamilika kwa Unguja na Pemba.

  0 0


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika Ibada ya Misa Takatifu Dominika ya 34 ya mwisho wa mwaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Ibada hiyo ni mwisho wa mwaka ya sherehe ya Kristo Mfalme iliyoongozwa na Padre Projestus Marko Kahitwa . Novemba 25,2018.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa sadaka yake wakati wa Ibada ya Misa Takatifu Dominika ya 34 ya mwisho wa mwaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Ibada hiyo ni mwisho wa mwaka ya sherehe ya Kristo Mfalme iliyoongozwa na Padre Projestus Marko Kahitwa . Novemba 25,2018.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakipeana mkono wa Amani na Masista na waumini walipojumuika na waumini wengine wakati wa Ibada ya Misa Takatifu Dominika ya 34 ya mwisho wa mwaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Ibada hiyo ni mwisho wa mwaka ya sherehe ya Kristo Mfalme iliyoongozwa na Padre Projestus Marko Kahitwa . Novemba 25,2018.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikomunika Ibada ya Misa Takatifu Dominika ya 34 ya mwisho wa mwaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Ibada hiyo ni mwisho wa mwaka ya sherehe ya Kristo Mfalme iliyoongozwa na Padre Projestus Marko Kahitwa . Novemba 25,2018.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoka kanisani mara baada ya kumalizika kwa Ibada ya Misa Takatifu Dominika ya 34 ya mwisho wa mwaka katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam. Ibada hiyo ni mwisho wa mwaka ya sherehe ya Kristo Mfalme iliyoongozwa na Padre Projestus Marko Kahitwa . Novemba 25,2018.PICHA NA IKULU

  0 0


  Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Singida Mhandisi Masige Matari, akitoa taarifa ya mradi kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja (One Stop Inspection Station), katika kijiji cha Muhalala, wilayani Manyoni, mkoani humo.
  Muonekano wa baadhi ya nyumba za watumishi wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Polisi watakaoishi mara baada ya ujenzi wa Kituo cha Ukaguzi wa Pamoja kukamilika katika kijiji cha Muhalala, Wilayani Manyoni, Mkoani Singida.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri Adel alkhateeb, anayesimamia ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami wakati alipoukagua mradi huo, Mkoani Tabora.

  Muonekano wa kazi zikiendelea za ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, mkoani Tabora. Ujenzi wa sehemu ya barabara hiyo utafungua mkoa huo na mikoa ya Katavi na kigoma.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, akikagua moja ya boksi kalvati iliyojengwa katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, Mkoani Tabora.
  Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Mhandisi Damian Ndabalinze, akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga (katikati), kuhusu hatua zilizofikiwa katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chanya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami wakati Katibu huyo alipokagua mradi huo, mkoani Tabora.


  Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Joseph Nyamhanga, ameagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kumuandikia barua mkandarasi wa Kampuni ya Impesa di Construzioni anayejenga kituo cha ukaguzi wa pamoja (one stop inspection station) eneo la Manyoni mkoani Singida na Nyakanazi mkoani Kagera kurejea eneo la kazi na kuendelea na ujenzi.

  Akizungumza katika kijiji cha Muhalala mkoani Singida wakati wa ukaguzi wa kituo hicho, Katibu Mkuu huyo amesema Serikali tayari imeshashughulikia madai ya mkandarasi huyo, hivyo hana sababu ya kutoendelea na ujenzi wa mradi huo. “Naagiza Mkandarasi huyu arudi eneo lake la kazi na kuanza kazi ya ujenzi wa mradi huu mara moja”, amesema Mhandisi Nyamhanga.

  Aidha, Mhandisi Nyamhanga, ameeleza kuwa jumla ya gharama za mradi wa vituo hivyo ni takribani shilingi bilioni 55, ambayo itahusisha gharama za ujenzi, usimamizi na fidia.Mhandisi Nyamhanga amefafanua kuwa ujenzi wa kituo hicho unaenda sambamba na ujenzi wa kituo kingine eneo la Nyakanazi mkoani Kagera ambapo kituo kingine cha vigwaza mkoani Pwani kimeshakamilika na hivyo kutafanya jumla ya vituo vikuu vitatu vya ukaguzi vyenye umbali wa kilomita 500 kutoka kwa kila kimoja.
  Amefafanua kuwa lengo la ujenzi wa mizani hizo ni kupunguza vizuizi barabarani na gharama za usafirishaji wa mizigo kupitia barabara ya ukanda wa kati.

  Kwa sasa magari ya mizigo husimama takriban katika vituo 31 ambapo kati ya hivyo vituo nane ni vya mizani, vituo 20 ni vya polisi na vituo 3 ni vya ukaguzi wa mapato ambavyo vyote viko kati ya Dar es Salaam hadi mipaka ya Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa umbali wa kilomita 1000.Awali, akitoa taarifa za maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho, Kaimu Meneja wa TANROADS mkoa wa Singida Mhandisi Masige Matari, amesema ujenzi wa kituo hicho umefikia asilimia 60 na kazi zinazoendelea kutekelezwa ni kama vile barabara zinazoingia na kutoka kituoni.

  Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu huyo amekagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Chaya hadi Nyahua mkoani Tabora yenye urefu wa KM 85.4 inayojengwa kwa kiwango cha lami na mkandarasi CHICO, ambapo ameridhishwa na maendeleo yake na kumtaka mkandarasi huyo kufanya kazi kwa bidii ili mradi huo ukamilike mapema zaidi ili kufungua mkoa huo kwa fursa za kibiashara na usafirishaji wa abiria na mizigo.

  Naye Meneja wa TANROADS mkoa wa Tabora Mhandisi Damian Ndabalinze, amemuhakikishia Katibu Mkuu huyo kuusimamia kwa ukamilifu mradi huo na miradi mingine inayoendelea kutekelezwa mkoani humo.Mradi wa ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya unagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (KFAED) na kukamilika kwake kutafungua mkoa wa Tabora na mikoa ya Katavi na Kigoma katika kukuza uchumi wa wananchi.

  Katibu Mkuu wa Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Nyamhanga, yupo katika ziara ya kikazi mkoani Tabora ikiwa ni lengo la kukagua miradi mbalimbali inayosimamiwa na sekta yake hususani barabara, madaraja na kiwanja cha ndege.

  0 0


  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wana Shirika la KWIECO lilichopo Wilaya ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro linaloshughulisha na utoaji wa masaada wa kisheria kwa wahanga waliofanyiwa vitendo vya ukatili wa Kijinsia.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenzwa na wanachama wa Shirika la Floresta Tanzania lililopo Marangu Mkoa wa Kilimanjaro wakati wa ziara ya kukagua kazi zinazofanywa na wanawake wajasiriamali mkoani humo
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia mua uliokuzwa vizuri kwa njia za kiasili bila kutumia mbolea za kisasa unaolimwa na wanawake wajasiriamali wa Umoja wa Vicoba Marangu (UVIMA) uliopo Mkoa wa Kilimanjaro wakati wa ziara ya kukagua kazi zinazofanywa na wanawake wajasiriamali mkoani humo
  Wanakikundi kutoka Shirika la Floresta na kutoka Umoja wa Vicoba Marangu (UVIMA) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo Pichani) wakati akizungumza nao mara baada ya kukagua shughuli wanazofanya
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akikagua taarifa katika kitabu kilichopo chumba cha Polisi katika Kituo cha kutoa Huduma za pamoja ( ONE STOP CENTRE) katika Hospitali ya Wilaya ya Hai. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW  Na Mwandishi Wetu Moshi

  Imesemekana kuwa vitendo vya Ukatili wa kijinsia kwa miaka hivi karibuni vimezidi kukithiri na kuathiri wanawake na Watoto nchini nahivyo kufikia hatua ya kufananishwa na ugonjwa wa Kansa.

  Hayo yamebainishwa wakati wa Ziara ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea Shirika lisilo la Kiserikali la Kilimanjaro Women Information Exchange Community Organization (KWIECO) na kujionea shughuli za huduma za kisheria zinazotolewa kwa wahanga wa Ukatili wa Kijinsia katika Mkoa wa Kilimanjaro.

  Naibu Waziri Ndugulile amesema vitendo vya Ukatili wa Kijinsia vimekuwa vinaongezeka sana na kwa mwaka 2017 vitendo 41,000 viliripotiwa na kati ya hivyo vitendo 13,000 vilifanywa dhidi ya watoto. “Kwa idadi ya vitendo hivi vya kikatili ingekuwa kwa ujambazi hali ingekuwa mbaya yani ukatili wa kijinsia ndio Kansa mpya nchini” alisisitiza Dkt. Ndugulile

  Dkt. Ndugulile amewataka Wataalam wa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii kutoka ofisini na kwenda kwa wananchi kusikikiza kero na kutatua changamoto zao ili kuwapa chachu ya kuboresha maendeleo na ustawi wao. Amesisitiza kuwa Serikali imeamua kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuanzisha Mpango Mkakati wa Taifa wa Kutokomeza vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watotokwa kipindi cha mwaka 2016/2017 hadi 2021/2022 ili kuondokana kabisa na vitendo hivyo dhalili.

  Pia Naibu Waziri Ndugulile ameyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kushirikiana na Serikali katika kupambana na Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kilimanjaro Women Information Exchange Community Organization (KWIECO) Bi. Elizabeth Maro Minde amesema Shirika lake limejikita katika kusaidia wahanga wa vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto na wamewasaidia wahanga hao na kufanikiwa kupata haki zao.

  “Vitendo hivyo vinafanywa na watu wa karibu na familia yake kama Baba, Mama, mjomba na majirani na hivyo kusababisha kuwepo kwa changamoto katika upatikanaji wa ushahidi stahiki kwa pande zote mbili.” alisisitiza Bi. Elizabeth

  Naibu Waziri Ndugulile yupo mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya siku tatu kufuatilia utekelezaji wa shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii katika mkoa wa Kilimajaro.

  0 0

  Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mhandu kilichopo katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga tarehe 24 Novemba, 2018 ikiwa ni sehemu ya ziara yake kwenye mkoa huo yenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

  Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Mhandu kilichopo katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga akiwasilisha kero yake kwa Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani ) kwenye mkutano wa hadhara.

  Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia mbele) akiendelea na ziara katika eneo la uchimbaji wa chini ya ardhi kwenye Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu uliopo katika eneo la Kakola Wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

  Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kushoto) akipata maelezo jinsi shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu zinavyofanyika chini ya ardhi katika eneo la Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu.

  Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na msafara wake pamoja na watendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu kabla ya kushuka chini ya ardhi ili kujionea uchimbaji wa madini unavyofanyika.

  Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati mbele) akiendelea na ziara katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu uliopo katika eneo la Kakola Wilayani Kahama mkoani Shinyanga.


  Ni baada ya kruhusu wananchi kijiji cha Mhandu kuendelea na uchimbaji dhahabu


  Na Greyson Mwase, Shinyanga

  Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameruhusu wananchi wa kijiji cha Mhandu kilichopo katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga kuendelea na uchimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo la utafiti wa madini hayo lililokuwa linamilikiwa na Menan Sanga kwa kushirikiana na kampuni ya Lion Town.

  Biteko aliyasema hayo leo tarehe 24 Novemba, 2018 katika mkutano wa hadhara ulioshirikisha wananchi wa kijiji cha Mhandu kilichopo katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mkoa huo yenye lengo la kusikiliza na kutatua changamoto za wachimbaji wa madini.

  Katika ziara hiyo, Biteko aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha, Mbunge wa Jimbo la Msalala, Ezekiel Maige, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Simon Berege, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Shinyanga, Wataalam kutoka Wizara ya Madini pamoja na waandishi wa habari.

  Biteko alisema kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Madini haiwezi kuruhusu mwekezaji kumiliki eneo pasipo kuliendeleza, kutokulipa kodi inayohitajika Serikalini huku wananchi wenye nia ya kuchimba katika eneo husika wakiendelea kuteseka.

  Alisema kuwa, Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli imeweka mikakati mbalimbali ya uboreshaji wa Sekta ya Madini ikiwa ni pamoja marekebisho ya Sheria ya Madini inayotambua madini kama rasilimali za watanzania wote.

  “Madini ni mali ya watanzania wote, na sisi kama Serikali tumejipanga katika kuhakikisha kila mwananchi anashiriki kwa kiasi kikubwa katika umiliki wa rasilimali za madini, hivyo ninawaomba endeleeni kufanya kazi ya uchimbaji katika eneo hili wakati taratibu nyingine zikiwa zinaendelea,” alisema Biteko huku akishangiliwa na wananchi.

  Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Biteko alimtaka Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Shinyanga kurasimisha wachimbaji wadogo wa madini waliopo katika eneo hilo pamoja na kuwapatia leseni za uchimbaji wa madini kwa kuzingatia sheria na kanuni za madini ili wawe na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa sekta ya madini.Pia alimtaka Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Shinyanga kuandaa orodha ya wachimbaji wote wa madini pamoja na taarifa za uzalishaji wa madini yanayozalishwa na wachimbaji wa madini ikiwa ni pamoja na kodi mbalimbali wanazolipa Serikalini.

  Aliwataka wachimbaji wadogo hao kufuata sheria na kanuni za madini ikiwa ni pamoja na ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali zinazohitajika Serikalini na kusisitiza kuwa, Serikali haitasita kufuta leseni za madini pale watakapokiuka sheria na kanuni za madini.Awali wakizungumza katika nyakati tofauti wananchi wa kijiji cha Mhandu kilichopo katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga walisema kuwa awali eneo hilo lilikuwa likimilikwa kampuni ya Lion Town tangu mwaka 1989 kabla ya kukabidhiwa kwa Menan Sanga ambaye amekuwa haendelezi uchimbaji katika eneo hilo huku akiwafukuza wananchi ambao wamekuwa wakichimba madini ili kujikwamua kiuchumi.

  Akizungumza kwa niaba ya wanakijiji hao Innocent Deus alisema kuwa wachimbaji wadogo wa madini wanaochimba madini katika eneo hilo wamekuwa wakitishiwa maisha ikiwa ni pamoja na kupigwa mara kwa mara na walinzi waliowekwa na mmiliki wa eneo hilo Menan Sanga

  Deus alisema awali kikundi kwa ajili ya uchimbaji wa madini hayo kijulikanacho kwa jina la BMS kiliundwa na kuomba leseni ya uchimbaji wa madini katika Wizara ya Madini kupitia ofisi yake iliyopo mkoani Shinyanga lakini walishangaa kuambiwa kuwa leseni husika imeshaombwa na kutolewa kwa Menan Manga.

  Aliomba Serikali kupitia Wizara ya Madini kuwapatia sehemu ya eneo hilo kwa ajili ya kuendelea na shughuli za uchimbaji wa madini huku taratibu nyingine zikiendelea ikiwa ni pamoja na urasimishaji na utoaji wa leseni ili waweze kuchangia kwenye pato la Taifa.

  Naye Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige mbali na kutoa pongezi kwa Naibu Waziri wa Madini kwa kutatua mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu aliiomba Wizara ya Madini kuwapatia maeneo yenye madini kwa ajili ya uchimbaji hususan katika eneo husika kwa kuwa madini ni tegemeo pekee kwenye uchumi wao.


  Alisema kuwa, wananchi wengi wanaishi katika maisha magumu huku wakiwa na rasilimali za madini ya kutosha ambazo zikitumiwa kikamilifu zinaweza kuwanufaisha na kuimarisha huduma nyingine za jamii kama vile miundombinu ya barabara, umeme na maji.


  Wakati huohuo, Naibu Waziri Biteko alifanya ziara katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu ulioko katika eneo la Kakola Wilayani Kahama mkoani Shinyanga lengo likiwa ni kuona shughuli za uchimbaji madini na kufuatilia utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Waziri wa Madini, Angellah Kairuki tarehe 24 Aprili, mwaka huu.


  Katika hatua nyingine, Biteko aliutaka mgodi huo kuhakikisha unamaliza mgogoro kati yake na wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa mchanga wa marudio ambao ni mali ya wananchi wanaozunguka mgodi huo waliouacha wakati wakipisha shughuli za uchimbaji kwa mgodi huo kwa kufuata sheria na taratibu.


  Aidha, aliutaka mgodi kuandika barua kwenda Tume ya Madini kwa ajili ya kuomba mwongozo wa namna ya kutoa mchanga wa marudio na kuwakabidhi wananchi ambao ndio wamiliki wa awali wa mchanga huo wakati wakiendesha shughuli za uchimbaji wa madini katika eneo hilo.


  Aidha, Naibu Waziri Biteko alikerwa na kitendo cha mgodi huo kutokulipa kodi ya mapato kwa takribani miaka 19 na kuendesha shughuli zake kwa kusuasua kwa kisingizio cha kuwa mgodi umeamua kupunguza gharama za uendeshaji.


  “Haiwezekani kama mgodi mnaamua kupunguza gharama za uzalishaji pasipo kushirikisha Serikali huku mkibadilisha umiliki wa leseni ya baruti wa kampuni nyingine na ni jambo ambalo halikubaliki kabisa,” alisisitiza Biteko.


  Alielekeza Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Sinyanga kuangalia iwapo kuna taratibu zimekiukwa ili taratibu za kisheria zichukuliwe.

  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma Bw. Jabir Shekimweri akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge wakati wa hafla ya kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF), hafla hiyo imetanguliwa na matembezi ya hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma leo yakishirikisha wananchi, wanafunzi na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko akizungumzia mambo yatakayofanyika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani ikiwemo wiki ya maonesho itakayoenda sambamba na kuanzishwa kwa jiji cha vijana ndani ya uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma ambapo vijana watajifunza masuala mbalimbali ikiwemo Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Upimaji wa Virusi vya UKIMWI, Ushauri nasaha, upimaji wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama shinikizo la damu na kisukari .

  Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko akiteta jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia UKIMWI (UNAIDS) hapa nchini Dkt. Leo Zekeng wakati wa hafla ya kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF), hafla hiyo imetanguliwa na matembezi ya hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma leo yakishirikisha wananchi, wanafunzi na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI.
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia UKIMWI (UNAIDS) hapa nchini Dkt. Leo Zekeng akizungumzia hali ya UKIMWI Duniani ambapo alibainisha kuwa takribani watu milioni 37 wameambukizwa virusi hivyo, hayo yamejiri leo wakati wa hafla ya kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF), hafla hiyo imetanguliwa na matembezi ya hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma leo yakishirikisha wananchi, wanafunzi na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI.
  Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma Bw. Jabir Shekimweri (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya wananchi walioshiriki katika wa hafla ya kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF), hafla hiyo imetanguliwa na matembezi ya hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma leo yakishirikisha wananchi, wanafunzi na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI.
  Kikosi cha Bendi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikiongoza matembezi ya hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma leo yakishirikisha wananchi, wanafunzi na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI kwa lengo la kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF).
  Sehemu ya washiriki wa matembezi ya hisani yaliyolenga kuhamasisha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF) , matembezi hayo ya hisani yamefanyika Jijini Dodoma.
  Mmoja wa wasanii walioshiriki katika hafla ya uchangiaji fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF) , Bi. Hadhara Charles akionesha umahiri wake katika kumiliki mpira wa miguu wakati wa hafla hiyo iliyotanguliwa na matembezi ya hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia UKIMWI na Madawa ya Kulevya Mhe. Oscar Mukasa ambaye ni Mbunge wa Biharamulo akizungumzia faida za wananchi na wadau mbalimbali kujitokeza kuchangia mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania leo Jiji Dodoma wakati wa hafla ya kuhamasisha na kuchangia mfuko huo, hafla hiyo ilitanguliwa na matembezi ya hisani.
  Msanii wa Jijini Dodoma Bi. Judith Jenaro akiimba wimbo wa kuhamasisha wananchi kujitokeza kupima virusi vya UKIMWI ili watambue hali zao ili waweze kuchukua hatua stahiki.

  Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma Bw. Jabir Shekimweri (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu wanafunzi walioshiriki katika hafla ya kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF), hafla hiyo imetanguliwa na matembezi ya hisani yaliyofanyika Jijini Dodoma leo yakishirikisha wananchi, wanafunzi na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia UKIMWI na Madawa ya Kulevya Mhe. Oscar Mukasa (Kushoto) ambaye ni Mbunge wa Biharamulo akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia UKIMWI (UNAIDS) hapa nchini Dkt. Leo Zekeng mara baada ya hafla ya kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF).(Picha zote na MAELEZO na TACAIDS)

  …………………………………………………………

  Wananchi na Wadau wa Maendeleo wamehamasishwa kujitokeza kuchangia fedha kwa ajili ya Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI Tanzania (ATF) ili kujenga uwezo na kuongeza mapambano dhidi ya ugonjwa huo ambapo takribani milioni 15 zimechangishwa katika hafla iliyofanyika leo Jijini Dodoma ikitanguliwa na matembezi ya hisani.

  Akizungumza leo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge , wakati wa hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri amesema kuwa kuna umuhimu Mkubwa wakuchangia mfuko huo ili Taifa liweze kujitegemea katika kuendeleza mapamabano dhidi ya UKIMWI.
  ” Tuwe wepesi kuchangia mfuko huu kupitia namba 0684909090 ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kupambana na UKIMWI hapa nchini”; Alisisitiza Mhe. Shekimweri

  Akifafanua amesema kuwa kuna haja ya kuweka mikakati ya pamoja katika mapambano dhidi ya UKWIMWI hapa nchini ikiwemo kuangalia namna bora yakuwaelimisha vijana hasa walio mashuleni kwa kutumia mbinu za kisasa. Aliongeza kuwa, Kwa sasa maambukizi ya Virusi vya UKIMWI katika mkoa wa Dodoma yameongezeka kutoka asilimia 2.5 hadi asilimia 5 mwaka 2017 hali inayotaka mikakati zaidi ikiwemo udhibiti wa nyumba za kulala wageni na elimu kwa makundi maalum kama wanafunzi wa Shule na Taasisi za elimu zilizopo katika mkoa huo.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibi Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko amesema kuwa matembezi yaliyofanyika ni sehemu ya matukio yatakayofanyika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani.Matukio menegine yatakayofanyika ni pamoja na wiki ya Maonesho ya UKIMWI itakayoenda sambamba na ushauri nasaha na upimaji, mafunzo ya ujasiriamali, Kongamano la wataalamu wa Sayansi na wiki ya Vijana.Aliongeza kuwa Vijana ni kundi ambalo linatakiwa kutumia fursa ya maadhimisho hayo kupata elimu kuhusu masuala ya UKIMWI.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia UKIMWI Dkt. Leo Zekeng amesema kuwa kwa sasa Dunia ina takribani watu milioni 37 wanaoishi na Virusi vya Ukimwi na sehemu kubwa wakiwa wanaishi katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.
  Akifafanua amesema kuwa Shirika hilo liko tayari kuendelea kushirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya UKIMWI.

  Siku ya UKIMWI Duniani inaadhimishwa kila Novemba Mosi kila mwaka ikilenga kuhamasisha wananchi na wadau kushirikiana katika mapambano hayo, ” Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni Pima Jitambue, Ishi”; Maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika Jijini Dodoma ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

  0 0


   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo(katikati) akiwasili katika kituo cha Afya Mpwayungu kilichopo katika Jimbo la Mtera Wilayani Chamwino ambacho ni miongoni mwa Vituo vilivyopokea Tsh Mil. 400 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Afya.
  2
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo(katikati) akikagua  ujenzi wa Kituo cha Afya Mpwayungu wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Chamwino.
  3   
        Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo(katikati) akizungumza na wananchi wa Mpwayungu(hawapo pichani) wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Chamwino.
  ……………………

  Nteghenjwa Hosseah, Mpwayungu. 

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameridhishwa na  miundombinu ya Afya inayoendelea kujengwa katika kituo cha Afya Mpwayungu kilichopo katika Jimbo la Mtwera Wilayani Chamwino.
  Jafo ameonyeshwa kuridhishwa  kwake alipokwenda kutembelea kituo hicho na kukagua ujenzi wa miundombinu ya Afya inayoendela ambapo kituo hicho ni miongoni mwa vituo vya Afya Nchini vilivyopokea Fedha Tsh Mil 400 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Maabara, Upasuaji, chumba cha kuhifadhia maiti pamoja na nyumba ya mganga.

  “Mmewatendea haki wananchi wa Mpwayungu kituo hiki mimejengwa kwa kiwango kinachostahili nina uhakika na huduma zitakazotolewa hapa ni za uhakika na ile adha waliyokuwa wanapata wananchi ya kutembea umbali mrefu wa kufuata huduma za upasuaji sasa wataweza kuzipata hapa hapa” alisema Jafo.
  Wakati huo huo Waziri Jafo alimuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino kutafuta Fedha kwa ajili ya kukamilisha vitu vidogo vidogo ambavyo havijakamilika katika majengo mapya yaliyojengwa.

  Naye Mbunge wa Mtera  Mhe. Livingstone Lusinde amesema anaishukuru Serikali ya awamu ya Tano kwa kuona na kujali shida za wananchi wa Mpwayungu kwa kuwapelekea fedha kwa ajili ya uboreshaji wa Kituo cha Afya.Kituo hiki kinahudumia wananchi wengi sana wa Mpwayungu na maeneo ya jirani hivyo kwa kupata  majengo haya mapya yatasaidia katika kutoa huduma ambazo hapo awali zilizkua hazipatikani kutokana na uhaba wa majengo na vifaa amesema Lusinde.

  Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Bi. Asteria Mpota amesema kuwa ujenzi wa miundombinu ya Afya imefikia asilimia 95 na kuwa ameshakamilisha mchakato wa kuleta watumishi wapya watakaongeza nguvu katika utoaji wa huduma za Afya.

  0 0

   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo  kwa wadau wa Wizara hiyo katika  hafla fupi  ya Uzinduzi wa Uzalendo na Utaifa iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam .
   Kaimu Mkurungezi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa  Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Leah Kihimbi akiongea jambo na wadau wa Wizara hiyo (Hawapo katika picha) katika  hafla fupi ya Uzinduzi wa  Kampeni ya Uzalendo na Utaifa leo Jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mawasiliano na Uhusinao wa Umma kutoka benki ya NBC Bw. William Kallage ambao  ndio Wadhamini Wakuu wa Kampeni ya Uzalendo na Utaifa mwaka  huu inayotarajiwa kufanyika tarehe 8  Disemba  2018 Jijini Dodoma, akieleza jambo kwa wadau wenzake waliofika kuunga mkono uzinduzi wa kampeni hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
   Kaimu Mkurungezi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa,  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Leah Kihimbi(kulia) akimvalisha nembo inayoashiria uzalendo Mkuu wa Mawasiliano na Uhusinao wa Umma kutoka benki ya NBC Bw. William Kallage ambao ndio wadhamini wakuu wa Kampeni ya Uzalendo na Utaifa mwaka  huu inayotarajiwa kufanyika tarehe 8  Disemba  jijini Dodoma.
   Wadau wa Sanaa kutoka katika sekta binafsi taasisi za Serikali wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea  katika  hafla fupi ya uzinduzi wa Kampeni ya Uzalendo na Utaifa leo Jijini Dar es Salaam.

  0 0


  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola, akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mwisenyi, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, wakati Mbunge huyo alipofanya ziara katika kijiji hicho kusikiliza kero za wapigakura wake pamoja na kuwahamasisha kuanza maandalizi ya kilimo kwa kuwa msimu wa kilimo umeshafika. Na pia aliwataka wananchi hao waondoe hofu ya kutopata vitambulisho vya taifa kwani Watanzania wote wenye sifa watavipata vitambulisho hivyo.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola, akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Kamulebya, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, wakati Mbunge huyo alipofanya ziara katika kijiji hicho kusikiliza kero za wapigakura wake pamoja na kuwahamasisha kuanza maandalizi ya kilimo kwa kuwa msimu wa kilimo umeshafika. Na pia aliwataka wananchi hao waondoe hofu ya kutopata vitambulisho vya taifa kwani Watanzania wote wenye sifa watavipata vitambulisho hivyo
  Mkazi wa Kijiji cha Kamulebya, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, Mzee Range, akimuuliza swali Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (hayupo pichani), wakati Mbunge huyo alipofanya ziara katika kijiji hicho kusikiliza kero za wapigakura wake pamoja na kuwahamasisha kuanza maandalizi ya kilimo. Lugola aliwapa nafasi wananchi kutoa kero zao ndani ya Jimbo lake. Pia aliwataka wananchi hao waondoe hofu ya kutopata vitambulisho vya taifa kwani Watanzania wote wenye sifa watavipata vitambulisho hivyo.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kulia), akimsikiliza Afisa Tarafa ya Kenkombyo, Rebeca Mdodo alipokua anatoa taarifa ya Tarafa yake kwa Waziri Lugola, kabla ya Mbunge huyo hajaanza kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Bulamba, Kata ya Butimba, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara. Lugola ameanza ziara jimboni humo leo akisikiliza kero za wapigakura wake pamoja na kuwahamasisha kuanza maandalizi ya kilimo. Pia aliwataka wananchi hao waondoe hofu ya kutopata vitambulisho vya taifa kwani Watanzania wote wenye sifa watavipata vitambulisho hivyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


  …………………….


  Na Felix Mwagara, MOHA.

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema vitambulisho vya taifa vitatolewa kwa watanzania wenye sifa ambao watapita katika mchujo ili kuepusha kutoa kwa wahamiaji haramu.

  Amesema mchujo huo unaofanywa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) upo makini ili kuhakikisha hakuna makosa yatakayofanywa wakati wa utoaji wa vitambulisho, hivyo wananchi wawe na uvumilivu wakati mchujo huo ukiendelea.

  Waziri Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara aliyasema hayo leo, wakati alipokua anazungumza na mamia ya wananchi wa jimbo lake katika Kijiji cha Mwisenyi, Kata ya Butimba, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara na kuwataka wapiga kura wake na Watanzania kwa ujumla wawe na subira wakati hatua za utambuzi na usajili zikiendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini.

  “Hakuna Mtanzania mwenye sifa atakayekosa kitambulisho cha taifa, lakini lazima muwe na subira wakati zoezi la utambuzi wa watu gani wanaweza kupata vitambulisho hivi, na pia katika utambuzi tunapaswa kuwa makini sana kwasababu tusije tukapenyeza wahamiaji haramu wasiostahili na wao wakaweza kupata vitambulisho na baadaye tukaja kupata shida,” alisema Lugola.

  Lugola alisema baada ya hatua ya utambuzi, inafuata hatua ya usajili ambayo pia hatua hiyo nayo inahitaji umakini mkubwa zaidi na ikimalizika hatua hiyo majina yaliyosajiliwa yanarudishwa tena kwa wananchi kuulizwa kama waliosajiliwa wanatambuliwa katika sehemu wanazoishi, hatua hiyo ikiwa na lengo la kupata taarifa sahihi ya waliosajiliwa wanatambuliwa au hawatambuliwi na wazawa katika eneo husika.

  “Endapo majina tulioyasajili na kuyaleta kwenu, nanyi mtayakataa basi hatutaweza kutoa vitambulisho kwa huyo au hao mliowakataa, na endapo mtayaridhia majina tuliyowaletea, basi tutaweza kuwatengenezea vitambulisho bila shaka yoyote, na endapo kuna mwananchi amekataliwa na Kijiji kuwa hatambuliwi, anayohaki ya kukata rufaa na kutueleza kwanini apewe kitambulisho,” alisema Lugola.

  Lugola ambaye alikua anaulizwa maswali mbalimbali na wananchi hao kuhusu Nida na idara zake nyingine zilizopo ndani ya Wizara yake, aliwahakikishia wapiga kura wake kuwa, hakuna Mtanzania atakayekosa kitambulisho cha taifa, kila mwananchi ana haki ya kupewa akiwa ana sifa ya kupewa.Aidha, Waziri Lugola aliwataka wananchi wa jimbo lake waanze maandalizi ya kilimo cha mazao ya chakula na biashara ili kuepuka janga la njaa lisije liwakumba endapo hawata lima. Hata hivyo, kijiji hicho alichokitembelea, kwa mujibu wa taarifa ya mipango yao ya kilimo walisema kuwa wana upungufu mkubwa wa mbegu za mazao mbalimbali hasa zao la pamba.

  “Nimeagiza maafisa ugani waje kuangalia upungufu wa mbegu za pamba na kutatua kero hii kutokana na taarifa yenu ya mpango wa kilimo ya mwaka 2018/2019, na pia nasisitiza zaidi mulime mazao ya chakula kwa wingi,” alisema Lugola.Pia Waziri Lugola alitoa shilingi milioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji hicho ambao ulisimama kwa zaidi ya miaka sita kutokana na ukosefu wa fedha, na pia aliendesha harambee kwa madiwani na maafisa alioambatana nao katika mkutano huo, na kufanikiwa kuchangisha shilingi milioni moja na elfu ishirini.

  Lugola ameanza ziara jimboni kwake akisikiliza kero za wananchi pamoja na kuhamasisha kilimo cha mazao ya pamba, mahindi, mpunga, viazi na mengineyo ambayo wakazi wa jimbo lake wanalima mazao hayo kwa wingi.

  0 0
  Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme wa pili kulia akiwa ameshika jembe pamoja na baadhi ya wananchi wa kata ya Mindu wilaya ya Tunduru kama ishara ya matumizi ya Ardhi kwa ajili ya kilimo endelevu ya kumkomboa mkulima katika umaskini,Kushoto kwake mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera.

  Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akishiriki maandamano ya Amani na wananchi wa kata ya Mindu wilaya ya Tunduru kwa ajili ya kumpongeza Rais Dkt John Magufuri kutokana na uamuzi wake wa kununua korosho katika msimu wa 2018/2019 kwa bei ya shilingi 3300.
  Mkazi wa kijiji cha Mtonya Issa Yasin aliyepiga magoti,aliyeuz tani 4 na kg 200 za korosho na kujipatia kiasi cha shilingi milioni 13.8 akimshukuru Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme kwa niaba ya Rais Dkt John Magufuri kutokana na uamuzi wa serikali ya awamu ya tano kununua zao la korosho katika msimu wa 2018/2019 kwa bei ya 3300.
  Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme kulia,akimpongeza mkazi wa kijiji cha Mtonya ambaye ni mkulima wa korosho Issa Yasin baada ya kujipatia zaidi ya shilingi milioni 13.8 kutokana na kuuza korosho tani 4.200 kwa bei ya shilingi 3,300.Picha na Muhidin Amri

older | 1 | .... | 1732 | 1733 | (Page 1734) | 1735 | 1736 | .... | 1897 | newer