Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live

WAZIRI DKT.KIGWANGALLA AWATUNUKU VYETI WAHITIMU 289 WA CHUO CHA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI-MWEKA

$
0
0

Waziri wa Maliasi na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akimtunuku cheti Mhitimu wa Shahada ya Usimamizi wa Wanyamapori, katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka katika mahafali ya 54 yaliyofanyika jana Novemba 24, 2018 chuoni hapo katika wilaya ya Moshi mkoani Kiliamanjaro. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Jafari Kideghesho. Jumla ya wahitimu 289, wa kozi mbalimbali walitunukiwa vyeti.
Waziri akicheza muziki wa Kwaito na wahitimu
Waziri akizungumza katika mahafali hayo

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi na Maliasili Nape Nnauye akizungumza katika tukio hilo.
Waziri wa Maliasi na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akipokea zawadi ya picha ya kuchorwa aliyochorwa na mwanafunzi wa chuo hicho (kushoto) anayemkabidhi. Wakati wa tukio la kukabidhi zawadi katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori-Mweka katika mahafali ya 54 yaliyofanyika jana Novemba 24, 2018 chuoni hapo katika wilaya ya Moshi mkoani Kiliamanjaro.



Na Andrew Chale,Moshi.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangalla amewataka watumishi walio kwenye Wizara yake hiyo kupitia mafunzo ya Jeshi Usu ili kujiimalisha zaidi katika kutokomeza vitendo vya ujangili wa Maliasili zilizopo sehemu mbalimbali hapa nchini.

Waziri Dkt. Kigwangalla amesema hayo Novemba 24, 2018 wakati wa kuwatunuku vyeti wahitimu 289 katika kozi mbalimbali ikiwemo Shahada, Stashahada na Astashada kwenye Usimamizi wa Wanyamapori na Utalii kwenye Mahafali ya 54 ya Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori- Mweka, Wilayani Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Akielezea suala la kupata mafunzo kwa watumishi hao, amesema suala hilo la uhifadhi ni la kudumu hivyo ni vyema watumishi hao kujiandaa katika ulinzi wa Maliasili za Taifa.Dkt Kigwangalla amesema mifumo wanayotengeneza ikiwemo Jeshi Usu lazima ifanye kazi imara na iwe madhubuti ili kusaidia kulinda Malisili zilizopo kwani hali ya uvamizi wa wananchi na waalifu wa Maliasili za taifa ni kubwa.

“Kama Serikali tuna nia na dhamira ya dhati ya kulinda na uhifadhi Maliasili tulizonazo ambazo ni urithi sio tu kwa watoto wetu hapa Tanzania, lakini ni urithi wa vizazi na vizazi vya Dunia yote” amesema Dkt. Kigwangalla.Aidha, Waziri Dkt. Kigwangalla ametoa wiki mbili kuanzia Novemba 24, kwa taasisi nne zilizo chini ya Wizara hiyo Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa kila kutoa Shilingi Milioni 100 ilikuchangia ujenzi wa jengo la Utawala na mafunzo chuoni hapo ili kuanza mara moja ujenzi wa jengo hilo jipya.

“Kwa mamlaka niliyonayo, Nawaagiza taasisi za TFS, NCAA, TANAPA na TAWA kwa kuanzia, ndani ya wiki mbili zinazofuata kabla hatujaenda likizo ya sikukuu za Christmass, Wawe wameleta shilingi milioni 100, kila taasisi hapa Mweka. Ambapo kwa taasisi hizo nne nilizozitaja tutakuwa tumefikisha shilingi milioni 400” amesema Dkt. Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo hayo ya kuchangia Chuo hicho ambacho kimetoa viongozi na watendaji wakuu wengi wa Serikali wakiwemo wa Wizara hiyo ya Maliasili na Utalii.

Aidha, Dkt. Kigwangalla ametoa wito kwa wahitimu baada ya dakika chache za kufurahia kutunukiwa cheti, waanze mawazo ya kujiajiri na kuwaajili wengine kwa kutumia elimu waliyopata chuoni hapo na kuachana na dhana ya kutembea na bahasha za kaki kutafuta kazi.“Chuo hiki kikongwe. Kina sifa ya kipekee hivyo fikiria zaidi kwenda kujiajiri na pia ukawaajiri wengine baadala ya kwenda kuzunguka kwenye maofisi na bahasha za kaki.. unakuta mtu anazunguka kila ofisi hata ambayo haijatangaza nafasi za kazi. Nendeni mkajiajiri wenyewe kwa elimu mulioipata hapa” amesema Dkt. Kigwangalla.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya kudumu Mheshimiwa Nape Nnauye (MB) amesema kamati yake imepokea changamoto ya miundombinu ya chuo hicho na watakaa kuona namna ya kupitisha bajeti ya chuo hicho.Nape ameongeza kuwa, kwa taasisi zote za Umma na binafsi zinazojihusisha na Utalii waanze kuchukua watumishi kutoka Chuoni hapo ilikupata watumishi wazuri na utasaidia kupata bora wa shughuli za Utalii na uhifadhi.

Naye Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Jafari Kideghesho amesema Chuo hicho kina ubora wa hali ya juu hivyo ni wakati sasa wa taasisi binafsi na za Kiserikali kuendelea kutoa ajira kwa vijana wanaopikwa Chuoni hapo.Mahafali hayo ya 54 yalihudhuriwa pia na Balozi wa Nigeria nchini, Balozi Sahabi Dada, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Chuo hicho, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Aaron Mbogho, na wengine wengi.

Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori, Mweka kilianzishwa mwaka 1963 baada ya azimio la Arusha mwaka 1961 ambalo lilitaka uwepo wa watu waliopewa mafunzo kwa ajili ya kulinda na kusimamia urithi wa rasilimali za Afrika.Chuo hicho ambacho huendesha mafunzo yake kwa vitendo kwa zaidi ya asilimia 60 kimepata ongezeko la wanafunzi kutoka 25 mwaka 1963/1964 hadi zaidi ya wanafunzi 550 mwaka 2016/2017 kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Malawi na Cameroon.

Aidha, katika kipindi cha miaka 54 iliyopita chuo hicho kimeweza kufundisha zaidi ya mameneja wa wanyamapori 8,000 kutoka nchi zaidi ya 50 duniani.Chuo hicho pia kimepewa tuzo na Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kama Kituo cha Ubora wa Taaluma ya Usimamizi wa Wanyamapori (Centre of Excellence).

WATANZANIA HAWABABAISHWI NA WANASIASA WENYE MAWAZO DUNI-SHAKA

$
0
0
Na Ripota Wetu, Morogoro

KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa morogoro, Shaka Hamdu Shaka amesema Watanzania hawana shauku wala ndoto ya kufanya mabadiliko ya utawala kwa kuwategemea wanasiasa wenye mtazamo na mawazo duni.

Amesema katika kipindi hiki ambacho Serikali ya CCM ikijibadili kimfumo na kisera kukidhi matakwa ya wananchi na wakati ni vigumu vyama vya upinzani kushika dola.

Shaka alitoa kauli hiyo wakati aliposhiriki mahafali ya kwanza ya Shule ya Sekondari Morogoro Open School, Mkoani hapa. “Tofauti ya kati ya viongozi CCM na wa vyama vingine, viongozi wa Serikali ya CCM hujikuta katika kujadili hoja na utekelezaji wa mipango na si kuishi kwa nadharia isiyo na tija.

Aliongeza: “Serikali ya CCM itabaki kuamini katika siasa ya ujamaa na kujitegemea. Tangu zama za sera za uchumi hodhi na ujio wa soko huria na utandawazi, CCM imekataa kushikilia ukale bali hufanya mabadiliko ya kisera,”alisema

Alisema anayefikiria siasa ya ujamaa na kujitegemea imekufa hawana uelewa kwani serikali inaposomesha wanafunzi bure, kutoa huduma bora za afya ni katika utekelezaji wa msingi ya ujamaa. Katibu huyo wa CCM mkoa, alisema wanasiasa hawapaswi kukosoa kwa pupa na jazba badala yake wawe na vipimo vya uhalisia wa madai yao kwani wananchi ni werevu, wanajua kutofautisha yaliyokuwepo na ufanisi wa mabadiliko yanayooneka.

Shaka aliwahimiza wanafunzi kuendelea kujenga matumaini kwa sera za CCM kwani ndicho chama chenye uwezo wa kufanyakazi kwa uhodari katika kuleta maendeleo. “Nawawatia shime wanafunzi mjipe jukumu la kusoma kwa bidii. Wale waliohitimu watambue wana jukumu la kujiandaa mwa kutumia fursa zinazotolewa na serikali pia mshiriki ushindanikwenye soko la ajira” alisema Shaka

MAMIA WAJITOKEZA KUJISAJILI KUSHIRIKI MBIO ZA MOROGORO MARATHON 2018 .

$
0
0
Mamia ya washiriki wa Mbio za Morogoro Marathoni zinazotarajia kufanyika Deseba 2 mwaka huu katika mkoa wa Morogoro wameendelea kujitokeza katka zoezi la uandikishwa linaloendelea katika vituo mbalimbali nchini .

Zoezi hilo lilioanza Novemba 10 mwaka huu linawashirikisha washiriki wa Mbio za Kilometa 21,kwa upande wa wanaume na wanawake ,kilometa 5 kwa mbiio za kujifurahisha pamoja na watoto na zile za kutumia Baiskeli .

Kampuni ya Itete Sport Agency ambao ndio waratibu wa mbio hizo wametenga baadhi ya maeneo kwa ajili ya kujiandikisha ambayo ni pamoja na .Kwa Morogoro ;Samaki Spot , Tengo Restaurant ,
Shani Sinema

Na Vyuo Vikuu mkoani Morogoro. Kwa Dar es Salaam ,Governos Pub Kinondoni .Mlimani City.(Chiken Hut Restaurant)Chuo cha IFM Stationary.Kimara Baruti (Hawaii Bar)Kwa mkoa wa Iringa.

Kalenga HotelChuo Kikuu cha Iringa (Bilionea Stationary)

Zanzibar .Sherry’s CollectionTangaMkwabi SupermarketPower and Sport Fitness club.

Dodoma .Mr HomangaMoshi /ArushaMr Wence Tarimo .Zoezi la uandikishaji linaendelea katika vituo tajwa.Kwa Mawasiliano zaidi piga simu naomba 0713172815

HALMASHAURI NA MIJI ILIYOFANYA VIBAYA KATIKA MASHINDANO YA AFYA NA USAFI WA MAZINGIRA ZATAKIWA KUJITATHMINI

$
0
0

NA WAMJW-DODOMA

Halmashauri za Miji, Majiji, Wilaya, Vitongoji na Vijiji zilizofanya vibaya katika mashindano ya afya na usafi wa mazingira zimetakiwa kujitathmini na kuhakikisha zinaweka mikakati madhubuti ya utunzaji wa mazingira.

Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa kilele cha wiki ya usafi wa mazingira ulioenda sambamba na mkutano uliojumuisha Maafisa Afya nchini na Wadau mbalimbali wa maendeleo kilichofanyika jijini Dodoma.

Waziri Ummy alisema hayo wakati akitaja washindi waliofanya vizuri katika Halmashauri za Miji, Majiji, Wilaya, Vitongoji na Vijiji viliyofanya vizuri katika mashindano ya afya na usafi wa mazingira ambayo Wizara imekuwa ikitekeleza tangu mwaka 1988.

“Mashindano hayo huanza katika ngazi ya Kitongoji na kuhitimishwa kwa kupata washindi wa kitaifa. Kila mwaka tumekuwa tukiboresha mashindano haya ambapo kwa mwaka huu tumeongeza makundi manne kutoka sita ya awali. Makundi yalioongezeka ni; Hospitali za Rufaa za Binafsi, Shule za Msingi za Vijijini, Shule za Sekondari za Bweni za Serikali, na Shule za Sekondari za Bweni za Binafsi”. Alisema Waziri Ummy.

Aidha, waziri huyo alitaja makundi ya washindi waliofanya vizuri na makundi ya Halmashauri, Majiji na Mikoa iliyofanya vibaya.

Katika kundi la Halmashauri za Manispaa na Majiji lilihusisha Manispaa 25, ambapo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ilikua kinara kwa asilimia 92.7, ikifuatiwa na mshindi wa pili Halmashauri ya Jiji la Arusha asilimia 90.5 na mshindi wa tatu ikiwa ni Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kwa asilimia 89.7.

Kundi la pili lilikua la Halmashauri za Miji ambapo lilihusisha Halmashauri za miji 22 nchini. Mshindi wa kwanza ni Halmasahuri ya mji wa Njombe asilimia 93.4, Halmashauri ya Mji wa Kahama ikishika nafasi ya pili kwa asilimia 75.0 na Halmashauri ya Mji wa Tunduma ikiwa nafasi ya tatu kwa asilimia 73.5.

Kundi la tatu la Halmashauri za Wilaya, ambapo lilishirikisha Halmashauri za Wilaya 25. Mshindi wa kwanza ni Halmasahuri ya Njombe ikiongoza kwa kupata asilimia 98.3, ikifuatiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Meru Asilimia 88.0 na mshindi wa tatu ni Halmasahuri ya wilaya ya Mufindi Asilimia 80.2.

Kundi la nne lilihusisha Halmashauri za Vijiji ambapo vilishiriki vijiji 47 kwa wastani wa vijiji viwili kwa kila Halmashauri ya Wilaya iliyoshiriki. Kiongozi wa kundi hili ni Kijiji cha Ikuna, Kata ya Ikuna, Halmashauri ya Wilaya ya Njombe asilimia 97.3. Mshindi wa pili ni Kijiji cha Kidegembye, Kata ya Kidegembye, Halmashauri ya Wilaya ya Njombe asilimia 97.0. Na kijiji cha cha Kikwe, Kata ya Kikwe, Halmashauri ya Wilaya ya Meru kilishika nafasi ya tatu kwa asilimia 86.5.

Kundi la Tano lilihusisha shule za msingi za vijiji, ambapo Shule za msingi 47 za serikali zilishiriki. Katika kundi hili shule iliyoongoza ni Shule ya Msingi Ikuna, Kata ya Ikuna, Halmashauri ya Wilaya ya Njombe kwa asilimia 98.7. ikifuatiwa na Shule ya Msingi Kidegembye, Kata ya Kidegembye, Halmshauri ya Wilaya ya Njombe kwa asilimia 97.8 na mshindi wa tatu ilikua Shule ya Msingi Kikwe, Kata ya Kikwe, Halmashauri ya Wilaya ya Meru ikiwa na asilimia 89.7

Katika kundi la sita lilimujuisha shule za sekondari za bweni kutoka katika mikoa 25 nchini. Shule iliyoibuka kidedea ni Shule ya Sekondari Njombe, iliyopo Halmashauri ya Mji wa Njombe kwa asilimia 91.7. Ikifuatiwa na Shule ya Sekondari ya Ufundi Tanga, Halmashauri ya Jiji la Tanga asilimia 90.9, na mshindi wa tatu ni Shule ya Sekondari ya Wasichana Ifakara, Halmashauri ya Mji wa Ifakara yenye asilimia 90.5.

Kundi la saba lilihusisha Shule za Sekondari za Bweni za Binafsi ambapo Shule ya Sekondari St. Francis, Halmashauri ya Jiji la Mbeya iliongoza kwa asilimia 99.0, ikifuatiwa na Shule ya Sekondari ya Wasichana St. Monica, Halmashauri ya Jiji la Arusha iliyokua na asilimia 97.6 huku msahindi wa tatu ikiwa Shule ya Sekondari ya Savannah Plain, Halmashauri ya Mji Kahama yenye asilimia 97.0.
Kundi la nane lilikua linajumuisha Hospitali za Rufaa za Mikoa za Serikali ambapo Hospitali 25 za Rufaa za Mikoa za Serikali zilishiriki. 
 
Mshindi katika kundi hili ni Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro iliyokua na asilimia 89.8, ikifuatiwa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara yenye asilimia 88.3 na mshindi wa tatu ni Hospitali ya Rufaa ya Mt. Meru yenye asilimia 88.0.

Kundi la tisa lilishirikisha Hospitali za Rufaa za Binafsi ambapo washiriki walikua tisa (9). Kundi hili lina washindi wawili kutokana kuwa na washiriki wachache. Ambao ni Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center yenye asilimia 95.4 na Hospitali ya Dodoma Medical Center iliyokua na asilimia 80.6.

Kundi la kumi na la mwisho lilihusisha Hoteli ambapo washiriki walikua 26 ikiwa ni hoteli moja kwa kila mkoa. Hoteli ya Melia Mkoa wa Mara imeibuka mshindi wa kundi hili kwa asilimia 98.5, ikifuatiwa na Hoteli ya Ruhuwiko Hunt Club iliyoko Mkoa wa Ruvuma kwa asilimia 96.3 na Hoteli ya Mt. Meru ya Mkoa wa Arusha ilishika nafasi ya tatu kwa kuwa na asilimia 93.3.

Waziri Ummy alitaja mgawanyo wa zawadi zilizotolewa ni pamoja na Tuzo Maalum, Trekta yenye Tela, Gari (FWD) Ford Ranger, Vyeti vya ushindi, pamoja na Pikipiki. Zawadi hizo zilitolewa kulingana na makundi kumi yaliyoshindanishwa kuanzia ngazi za Vijiji hadi Halmashauri za Majiji na Manispaa.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa kilele cha wiki ya usafi wa mazingira ulioenda sambamba na mkutano uliojumuisha Maafisa Afya nchini na Wadau mbalimbali wa maendeleo kilichofanyika jijini Dodoma.Waziri Ummy amezitaka 
Halmashauri za Miji, Majiji, Wilaya, Vitongoji na Vijiji zilizofanya vibaya katika mashindano ya afya na usafi wa mazingira kujitathmini na kuhakikisha zinaweka mikakati madhubuti ya utunzaji wa mazingira.

Kalogeresi atoa vigezo vya kuwapata wagombea 2020

$
0
0
Na Ripota Wetu, Morogoro

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro kimesema kupatikana kwa wagombea wa udiwani na ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kutatokana na kuthibitika kwa vigezo vya ushiriki wao katika shughuli za maendeleo ya chama hicho.

Pia, kimesema hadhi wanaoyopata ama wabunge ambao baadhi yao huteuliwa na kuwa mawaziri au manaibu waziri huku madiwani wakiwa wenyeviti wa halmashauri na mameya ni kutokana na heshima ya CCM kukubalika kwa wananchi.

Hayo yalielezwa jana Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Innocent Karogelesi alipokuwa akifunga mafunzo ya siasa, itikadi na maadili kwa vijana wa chama hicho huko Kilosa mkoani Morogoro.Kalogelesi alisema chama ndicho kinachowapa tiketi wanachama wake kugombea ubunge na udiwani hivyo wanapochaguliwa hawapaswi kujiweka mbali na shughuli za ujenzi wa CCM.

Alisema hakuna mwanafunzi anayeweza kujivunia kufanikiwa kwake kielimu ikiwa hawezi kutambua au kuheshimu mchango mkubwa uliotolewa na walimu wake ama katika masomo ya awali au shule ya msingi."Ili tuwapitishe wagombea wetu kwenye udiwani au ubunge mwaka 2020, tutampima kila mgombea kutokana na ushiriki wake katika kazi za chama bila kumtazama usoni. Sifa ya msingi na ya awali nje ya uanachama wake ni kujihusisha kwa kwake na maendeleo ya CCM," alisema Karogelesi.

Mwenyekiti huyo alisema chama cha siasa kitakachokosa kujijenga, kuimarika na kukubalika hakitapata madiwani na wabunge hivyo hata rais atashindwa kuteua mawaziri na manaibu wake pia kwenye majiji na halmashauri hakutakuwa na wenyeviti au mameya wa CCM.

Aliwataka wabunge wa kuchaguguliwa, madiwani na wale wa viti maalumu kutambua kuwa kufika kwao walipo sasa kumetokana na nguvu ya chama na sio uwezo wao binafsi.Kalogeresi aliwataka wanachama wa CCM na jumuiya zake kutambua kuwa wana wajibu na ulazmia wa kuishi kwa kuheshimu misingi ya chama kikatiba, kinidhamu na kimaadili ili kila kiongozi haiba yake iwe ni kioo kinachoakisi mema kwa chama na jamii. 

Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa alimuagiza Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka, kuwaandikia barua ya ukumbusho wabunge na madiwani wote juu ya ushiriki na wajibu wao ndani ya chama na kwenye jamii.Pia, makatibu wote wa CCM na jumuiya zake mkoani aliwataka kutoa maelekezo na kuwataka wanachama wao kujiweka mbali na vitendo vya udalali wa kisiasa na rushwa.

MKOA WA TABORA WAAINISHA MAENEO NANE YA UWEKEZAJI

$
0
0
Mkoa wa Tabora umeanisha maeneo ya vipaumbe vya uwekezaji katika kila Halmashauri nane za Mkoa huo ambayo yatajengwa viwanda vikubwa na uanzishaji wa ranchi kwa ajili ya ufugaji wa ng’ombe.

Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa majumuisho ya kikao cha Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani humo. Alisema kwa upande wa Wilaya ya Urambo wamepewa jukumu la kutenga eneo la ujenzi wa Kiwanda cha Kusindika Tumbaku, Halmashauri ya Kaliua wapewa jukumu la kujenga kiwanda cha mazao ya misitu.

Mwanri alisema Sikonge wenye wanatakiwa kuandaa eneo kwa ajili ya kujenga kiwanda cha kuchakata mazao ya nyuki ikiwemo asali na nta kwa ajili ya kuongeza ubora wake ili yaweze kupata soko kubwa ndani na nje ya Nchi .Alisema Halmashauri ya Mji wa Nzega imepewa jukumu la kuwa na eneo kwa ajili ya machijio ya nyama na Kiwanda cha kuchakata nyama ya ng’ombe na Halmashauri ya Wilaya ya Nzega inapewa jukumu la kuandaa na kuanzisha Rachi kwa ajili ya kunenepesha ng’ombe ili kuwezesha kuwa na nyama nzuri itakayopata soko ndani na nje ya Nchi.

Mwanri alisema Igunga wamepewa jukumu la kuimarisha kilimo kikubwa cha pamba kwa ajili ya viwanda Tabora na Manonga na kuongeza maeneo ya miradi ya umwagiliaji mpunga, ujenzi wa viwanda vya kukoboa mpunga ambavyo vitasaidia kuuweka katika madaraja. Alisema Uyui watahusika zaidi kutenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda cha kusindika mafuta ya alizeti na mazao mengine.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa Manispaa ya Tabora wanatakiwa kutenga eneo kwa ajili ya ukanda maalumu wa uwekezaji ambapo vitajengwa viwanda kama vile wa EPZA Ubungo Jijini Dar es salaam. Alisema Mkoa umefikia uamuzi huo ili kutogawanya nguvu na kufanya baadhi ya viwanda kushindwa kufanya kazi vizuri kwa sababu ya uchache wa malighafi kutokana na kuwepo kwa mrudikano wa viwanda vya aina moja katika eneo moja.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa ufafanuzi hivi karibuni wakati wa majumuisho ya kikao cha Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani humo.
 

OPERESHENI KOROSHO YAZIDI KUNUFAISHA WAKULIMA WA MIKOA YA KUSINI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi, Rukia Muwango (wa pili kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Market Watch Co. Ltd anayesimamia wa Ghala la kuhifadhia korosho la Lindi –Nachingwea Farmers Msafiri Zombe (wa pili kushoto) kuhusu hali ya upokeaji na usafirishaji wa korosho katika Ghala hilo wakati wa ziara yake aliyoifanya Ijumaa Novemba 23, 2018.

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi, Rukia Muwango (mbele) akizungumza na Uongozi wa Umoja wa Akina Mama wanaotoa huduma ya chakula kwa wabebaji na washushaji wa zao la korosho katika Ghala la Lindi-Nachingwea Farmers waliofika mbele yake kwa ajili ya kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili mara baada ya kufanya ziara katika Ghala hilo Ijumaa Novemba 23, 2018.

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Rukia Muwango akitazama orodha ya majina ya wabebaji na washushaji aliyopatiwa na Uongozi wa wapokeaji na washushaji wa zao la korosho katika Ghala la kuhifadhia zao la korosho la Lindi-Nachingwea Farmers wa waliofika mbele yake kwa ajili ya kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili mara baada ya kufanya ziara katika Ghala hilo Ijumaa Novemba 23, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi, Rukia Muwango akizungumza na watoa huduma ya ushushaji na upakiaji wa shehena ya zao la korosho katika Ghala la Lindi-Nachingwea Farmers waliofika mbele yake kwa ajili ya kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili mara baada ya kufanya ziara katika Ghala hilo Ijumaa Novemba 23, 2018.

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi, Rukia Muwango akizungumza na Viongozi Waandamizi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati alipofanya ziara katika Ghala la kuhifadhia zao la korosho la Lindi-Nachingwea Farmers Ijumaa Novemba 23, 2018 kujionea hali halisi ya zoezi la usafirishaji wa korosho kuelekea katika Maghala Makubwa yaliyopo Mkoani Mtwara.
Katibu Mtendaji Mkuu wa Chama cha Ushirika wa Msingi cha Makanjiro AMCOS kilichopo Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi, Rashidi Chihope akionesha nakala ya orodha ya majina ya wanachama wa Chama hicho wakulima wa zao la korosho waliolipwa na Serikali kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) sehemu ya taarifa ya kifedha kutoka Benki ya NMB Ijumaa wiki iliyopita.

MHE HASUNGA ATANGAZA KIAMA KWA WASAMBAZAJI WA MBEGU FEKI

$
0
0

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akikagua Maabara ya
Kutazama kiwango cha Uotaji wa Mbegu wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani
Morogoro alipotembelea Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), tarehe 24 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akikagua shamba la mahindi wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro alipotembelea Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), tarehe 24 Novemba 2018.

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) Ndg Patrick Ngwediagi akitoa taarifa ya Taasisi hiyo mbele ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga tarehe 24 Novemba 2018.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akikagua bustani ya nyanya wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro alipotembelea Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), tarehe 24 Novemba 2018.


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Morogoro

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga, 24 Novemba 2018 ametangaza kiama kwa wafanyabiashara wa mbegu nchini wanaouza Mbegu feki zilizopigwa marufuku na serikali.

Amewataka wafanyabiashara wote wa mbegu ambao wamekuwa wakifanya biashara hiyo kwa kuwauzia wakulima mbegu feki zilizopigwa marufuku na serikali kuacha haraka iwezekanavyo kwani serikali itawachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kukiuka maagizo ya serikali.

Ametoa agizo hilo akiwa ziarani Mkoani Morogoro ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Taasisi iliyopewa jukumu na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la usajili wa wafanyabiashara wa mbegu (Seed Dealers). “Serikali imepokea malalamiko mengi kwa wananchi kuhusu Ubovu wa mbegu jambo ambalo limepelekea kwa kiasi kikubwa kuwa na mavuno kidogo pasina kukidhi matakwa ya wakulima wetu nchini” Alikaririwa Mhe Hasunga

Waziri huyo pia ameiagiza Taasisi ya udhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) kutimiza majukumu yao kwa kuwabaini wafanyabiashara wanaokiuka maagizo ya serikali pamoja na taratibu na sheria za nchi. “Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuhusu mbegu feki jambo hili serikali haiwezi kukubaliana nalo hivyo TOSCI wanapaswa kusimamia kwa weledi ukaguzi na usajili wa Mbegu bora, pia ni lazima kuwabaini wasambazaji feki wa mbegu ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao” Alisisitiza Mhe Hasunga

Alisema Wizara ya Kilimo imepewa jukumu mahususi la kuhakikisha sekta ya kilimo inaimarika kwa usimamizi madhubuti wa sera, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali hivyo kunapokuwa na kelele za wananchi kuhusu mbegu feki ni dhahiri kuwa Taasisi zenye jukumu hilo hazitekelezi kazi yake kwa weledi.

Mhe Hasunga alieleza kuwa serikali imejipanga kuhakikisha kuwa inaongeza thamani ya mazao yote yanayozalishwa nchini, sambamba na kutafuta masoko mazuri. Vilevile, ameitaja Wizara ya Kilimo kuwa ina wataalamu wengi hivyo unaandaliwa mfumo mzuri wa kuwaunganisha watalaamu hao ili kujadili kwa pamoja namna ambavyo kilimo kinaweza kubadilika kutoka kilimo cha kujikimu na kuwa kilimo cha kibiashara ili kutoa malighafi za kutosha zitakazohuisha serikali ya viwanda.

DARAJA LA MTO MARA KUKAMILIKA JANUARI

$
0
0
Sehema ya chini ya daraja la mto Mara lenye urefu wa mita 94, mto Mara unaoanzia katika kijiji cha Masai Mara nchini Kenya maji yake huelekea na kuishia Ziwa Victoria upande wa Tanzania.

Muonekano wa daraja la mto Mara lenye urefu wa mita 94 na barabara ya maungio ambayo ni sehemu ya barabara ya Tarime-Mugumu ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea.



Mkuu wa Mkoa wa Mara Bw, Adam Malima (wa pili kushoto), akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa (wa pili kulia), eneo litakaloongezwa katika upanuzi wa njia ya kurukia ndege katika kiwanja cha ndege Musoma alipokagua kiwanja hicho (kushoto), ni Kaimu Meneja TANROADS Mara Mhandisi Reginald Masawe na (kulia) ni Meneja wa kiwanja cha ndege cha Musoma Bw, Shadrack Chilongani.


Naibu Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Elias John Kwandikwa ameutaka muungano wa Makampuni mawili ya kizalendo ya M/S Gemen Engineering Construction Co. Ltd na Mayanga Constractors Co. Ltd yanayojenga daraja la mto Mara kukamilisha ujenzi huo Januari mwakani.

Amesema Serikali haitawaongezea muda katika kazi hiyo hivyo wahakikishe daraja hilo pamoja na barabara za maingilio zinakamilika kwa wakati na ubora unaostahili. “Hakikisheni mnafanya kazi kwa bidii na weledi ili Serikali izidi kuwaamini na kuwapa miradi mingi zaidi wakandarasi wazawa na hivyo kukuza ujuzi na uchumi wa nchi”, amesema Mhe. Kwandikwa.

Daraja la mto Mara lenye urefu wa mita 94 ambalo linaunganisha Wilaya za Tarime na Serengeti ujenzi wake unagharimu zaidi ya shilingi bilioni 8.5 na ni miongoni mwa madaraja mawili makubwa yanayopitiwa na mto Mara unaoanzia katika kijiji cha Masai Mara nchini Kenya kuelekea Ziwa Victoria, daraja jingine ni Kirumi lenye urefu wa mita 223.3 lililojengwa mwaka 1985.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kwandikwa amekagua kiwanja cha ndege cha Musoma na kusisitiza kuwa Serikali itakijenga kiwanja hicho ili ndege nyingi zaidi ziweze kukitumia na kuhuisha uchumi wa mkoa wa Mara. Amesema ujenzi wake ukikamilika utafungua uchumi wa mji wa Musoma na mkoa wa Mara kwa ujumla kwani utavutia watalii wengi kufika katika vivutio vya mkoa huo ikiwemo hifadhi ya Serengeti.

Naye Mkuu wa mkoa wa Mara Bw, Adam Malima amemhakikishia Naibu Waziri Kwandikwa kuwa kufunguka kwa barabara, madaraja na uwanja wa ndege mkoani humo kutahuisha uchumi wa mkoa huo. Meneja wa kiwanja cha ndege cha musoma bwana Shadrack Chilongani amesema kiwanja cha ndege hicho ambacho kiko daraja la tatu C kina urefu wa mita 1,600 na upana wa mita 30 hivyo uboreshaji wake utakapokamilika utakipandisha daraja na kukiwezesha kuongeza miruko ya ndege na abiria na hivyo kukuza utalii wa mkoa wa Mara.

WFP Yakubali Kuipa Nguvu Wizara ya Kilimo

$
0
0
Naibu Waziri wa Kilimo Ndugu Innocent Bashungwa akijadiliana na wawakilishi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Michael Dunford na Riaz Lodhi katika ofisi za Wizara ya Kilimo jijini Dar es Salaam

Kutoka kulia: Riaz Lodhi (Mkuu wa Kitengo cha Mnyororo wa thamani WFP), Michael Dunford (Muwakilishi wa Shirika la WFP), Naibu Waziri Kilimo Mheshimiwa Innocent Bashungwa, Bi Vumilia Zikankuba na Elimpa Kiranga katika picha ya pamoja baada ya kikao

Naibu Waziri wa Kilimo nchini Mheshimiwa Innocent Bashungwa amekutana na muwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) Michael Dunford na mkuu wa usambazaji wa shirika hilo Riaz Lodhi katika ofisi za wizara hiyo jijini Dar es Salaam kujadili namna ya kuboresha ushirikiano baina ya Serikali na shirika hilo.  

Katika kikao hicho ndugu Michael Dunford alielezea namna WFP imekuwa ikishirikiana na serikali ya awamu ya tano katika kuboresha sekta ya kilimo kupitia miradi mbalimbali ikiwemo ya kuboresha lishe, kuongeza thamani ya mazao, utafiti na ubunifu katika kilimo na pia katika masoko.

Alimuhakikishia Mheshimiwa Bashungwa kuwa shirika la WFP lina nia ya dhati ya kumkomboa mkulima wa Tanzania ikiwa ni sehemu ya Malengo Endelevu ya Dunia (SDG) ya kutokomeza njaa ulimwengu ni kuishukuru Serikali kwa ushirikiano ambao imekuwa ikilipatia katika kutimiza majukumu yake. 

Nae Naibu Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Innocent Bashungwa amemueleza muwakilishi huyo nia ya Serikali ya kuhakikisha wakulima wanapata bei nzuri ya mazao ndani na nje ya nchi ambapo shirika la WFP limekubali kununua tani laki moja na nusu ya mahindi toka ghala la taifa na kuahidi kununua nyingine. Pia Mheshimiwa Bashungwa alimuhakikishia kuwa serikali itaendelea kurekebisha na kuboresha baadhi ya sheria ili kurahishisha biashara ya mazao nje ya nchi.  

Katika kikao hicho pia kilihudhuriwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba na Elimpa Kiranga (Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Chakula

DK. SHEIN ZIARANI KENYA

$
0
0










RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, wakati akielekea Nchini Kenya kwa ziara ya Kiserikali kuhudhuria mkutano wa Uchumi wa Bahari, ambapo anamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Salum Maulid Salum katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Abeid Amani Karume, wakati akielekea Nchini Kenya kwa ziara ya Kiserikali kuhudhuria mkutano wa Uchumi wa Bahari, ambapo anamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na wakuu wa Vikosi vya ulinzi na usalama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Abeid Amani Karume, wakati akielekea Nchini Kenya kwa ziara ya Kiserikali kuhudhuria mkutano wa Uchumi wa Bahari, ambapo anamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Abeid Amani Karume, wakati akielekea Nchini Kenya kwa ziara ya Kiserikali kuhudhuria mkutano wa Uchumi wa Bahari, ambapo anamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli.(PICHA NA HAROUB HUSSEIN

WACHORAJI JENGO LA ABIRIA MWANZA AIRPORT WAHARAKISHWA

$
0
0

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe jana akipata maelezo ya ujenzi wa Jengo la mizigo la Kiwanja cha Ndege cha Mwanza kutoka kwa Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Unetec ya Dubai, Geofrey Asulumenye (aliyenyoosha mkono. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri (MAB) ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Prof. Ninatubu Lema.
Baadhi ya vyumba katika jengo la mizigo la Kiwanja cha Ndege cha Mwanza ambalo linaendelea kujengwa, jana Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe alitembelea na kuridhika na maendeleo ya ujenzi.
Mhandisi Simon Makoye (mwenye kofia ngumu), akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (katikati), mchoro wa eneo linapojengwa rada, jana alipotembelea na kukagua maendeleo ya miradi inayoendelea kwenye Kiwanja cha Ndege cha Mwanza.
Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Unetec ya Dubai, Geofrey Asulumenye (kushoto) akimpa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe maelezo mbalimbali ya ujenzi wa Jengo la kuongozea ndege la Kiwanja cha Ndege cha Mwanza wakati alipofanya ziara jana.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri (MAB) YA Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Prof. Ninatubu Lema (kulia), akiongozana na Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Mwanza, Mhandisi Marwa Rubilya wakiambatana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe aliyetembelea kukagua maendeleo ya miradi kwenye kiwanja cha Ndege cha Mwanza. PICHA ZOTE KWA HISANI YA TAA


Na Mwandishi Wetu, Mwanza

WACHORAJI wa jengo jipya la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Mwanza, wametakiwa kuharakisha ili serikali itangaze zabuni ujenzi uanze haraka.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema jana mkoani hapa alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miundombinu ya kiwanja hicho ambayo ipo kwenye maboresho makubwa.

Mhe. Kamwelwe amesema kukamilika kwa michoro hiyo ya jengo la kisasa kutasaidia serikali kupitia wasimamizi wa ujenzi huo Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kutangaza zabuni na kupatikana kwa mkandarasi atakayejenga jengo hilo.

“Kiwanja cha ndege kinashughuli nyingi na jengo la abiria ni kituu muhimu sana, hivyo ninaharakisha hao wachoraji wajitahidi kufanya haraka ili kukamilisha michoro hiyo,” amesisitiza Mhe. Waziri.

Hatahivyo, amesema ameridhishwa na mradi wa ujenzi wa jengo la mizigo ambalo lipo mita chache kutoka eneo la abiria, ambapo ndege za mizigo zimejengewa maegesho yake rasmi tofauti na awali zilikuwa zikishusha upande wa ndege za abiria.

Halikadhalika ametembelea jengo la kisasa la kuongozea ndege, ambalo nalo limekamilika kwa asilimia 90 na kuridhishwa na utendaji wa Mhandisi Mkazi, Godfrey Asulumenye wa Kampuni ya Unetec ya Dubai, pamoja na eneo linapojengwa rada.

“Nimeridhika kuna maendeleo kwa kiasi kikubwa tofauti na nilivyopita awali, sasa kuna tofauti maboresho yamekamilika kwa asilimia kubwa na imebaki sehemu za kumalizia tu, ninaimani kwa kiasi kikubwa mkandarasi huyu atakamilisha kwa wakati na kuboresha zaidi sehemu ambazo wanaona hazijakaa sawa kabla ya kukabidhi,” Mhe. Kamwelwe.

Mhandisi Asulumenye amesema maboresho hayo yamehusisha ujenzi wa jengo la mizigo, jengo la kuongozea ndege, Kituo cha umeme, urefushaji wa barabara ya kutua na kuruka kwa ndege kwa mita 700 na ikikamilika itakuwa na urefu wa Km4.

Maboresho mengine kwa mujibu wa Mhandisi ni pamoja na uwekaji wat aa za kuomgozea ndege (AGL), mifereji mikubwa ya kupitisha maji ya mvua, maegesho ya ndege, mifumo ya maji taka na matenki ya maji safi.

Kiwanja cha Ndege cha Mwanza kwa sasa ni daraja la 4C kinauwezo wa kuhudumia ndege za abiria 300 na maboresho yakikamilika kitapanda na kuwa daraja la 4D. Takwimu zinaonesha kinahudumia abiria 500,000 kwa mwaka ila matarajio ni kufikia abiria milioni mbili (2) baada ya maboresho kukamilika.

MAJALIWA AZINDUA KAMPENI YA SIKU 16 YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA JIJINI DODOMA

$
0
0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Kampeni ya Siku 16 ya Kupinga Ukatili  wa Kijinsia kwenye  Uwanja  wa Jamhuri jijini Dodoma, Novemba  25, 2018.
PMO_8646-min
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozindua kampeni ya Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Novemba 25, 2018.
PMO_8638-min
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wapili kulia), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto)  na   Mratibu wa Kitaifa wa Shirika la  Wanawake Katika Sheria  na Maendeleo Barani Afrika ( WILDAF), Anna Kulaya  wakati alipowasili kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kuzindua Kampeni ya Siku  16 ya Kupinga Ukatili  wa Kijinsia, Novemba 25, 2018.
PMO_8829-min
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya  pamoja na  baadhi ya viongozi wa kitaifa na kimataifa walkishiriki katika Uzinduzi wa Kampeni ya Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia ulifanywa na Waziri Mkuu kwenye Uanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Novemba 25, 2018.Picha na Ofisi ya Waziri mkuu.

 

*Ni dhiri ya wanawake na watoto katika jamii kwa silimia 50 ifikapo 2022

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeandaa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kwa lengo la kupunguza kiwango cha ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika jamii kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022.

Amesema mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia (2000); Mkakati wa Taifa wa Maendeleo ya Jinsia (2005); Sera ya Maendeleo ya Mtoto (2008); Sheria ya Makosa ya Kujamiiana – SOSPA (1998).Ameyasema hayo leo (Jumapili, Novemba 25, 2018) wakati akizindua Kampeni ya siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsiakatika Uwanja vya Jamhuri jijini Dodoma. Amesema katika kukabialia na ukatili wa kijinsia Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imekuwa ikichukua hatua mbalimbaliza kuzuia na kutokomeza ukatili.

Waziri Mkuu amesema utekelezaji wa mpango huo utachangia katika utekelezaji wa mipango na Mikataba ya Kikanda na Kimataifa kuhusu usawa wa kijinsia, uwezeshaji wanawake na wasichana pamoja na haki na ustawi wa mtoto.Kadhalika Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaagiza Wakuu wa Mikoa wote wahakikishe wanasimamia uanzishwaji wa Kamati za Ulinzi wa Wanawake na Watoto za ngazi za Mikoa, Halmashauri, Kata na Vijiji kama inavyoelekezwa katika Mwongozo wa uratibu wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto.

“Vilevile, nawaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuanzisha Programu za Kijamii za kutokomeza ukatili wa kijinsia katika Halmashauri husika zitakazozingatia hali halisi na kuzitengea bajeti programu hizo kama inavyoelekezwa kwenye Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto. “

Pia Waziri Mkuu amesema watu wenye ulemavu wana mahitaji maalumu na ni wahanga wa ukatili wa kijinsia ameelekeza Jeshi la Polisi kuboresha Dawati lake la jinsia ili liweze kushughulikia kikamilifu masuala ya ukatili wa kijinsia dhidi ya watu wenye ulemavu. “Hivyo, kuanzia sasa Dawati hilo liitwe Dawati la Polisi la Jinsia, Watoto na Watu wenye Ulemavu.”

Akizungumzia kuhusu maana ya ukatili wa kijinsia amesema ni hali ya kutenda vitendo viovu, vinavyodhalilisha, vinavyotesa, vinavyonyanyasa, vinavyokandamiza, visivyojali haki za kuishi kwa binadamu anaweza kuwa wa kiume au kike.Kadhalika, Waziri Mkuu amesema ukatili wa kijinsia huja katika taswira nyingi. “Aidha, kwa uchache tunapozungumzia ukatili wa kijinsia tunamaanisha vitendo kama vile, vipigo, ubakaji, ukeketaji, ulawiti, matusi, lugha na vitendo vya udhalilishaji pamoja na kunyimwa fursa za kushiriki katika shughuli za kiuchumi.”

“Hivyo, ukatili wa kijinsia ni unyanyasaji wowote unaofanywa na mtu dhidi ya mtu mwingine bila kujali umri, maumbile, kabila, rangi, dini au mtazamo wa kisiasa. Unyanyasaji huu unahusisha mambo mengi kama kumpiga mwanamke au mwanamme, kumnyima mtoto elimu, kumlawiti mtoto wa kike au kiume, kumbagua mtu katika mahitaji ya msingi au kuwanyima urithi warithi wanaohusika.”

Aidha, taarifa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto (UNICEF) za mwaka 2017 zinaonesha kuwa wanawake na wasichana wapatao milioni 750 Duniani waliolewa wakiwa chini ya miaka 18. Halikadhalika, taarifa hiyo inakadiria kuwa wasichana milioni 120 (yaani mmoja kati ya wasichana 10) Duniani wamekumbana na vitendo vya kulazimishwa kufanya ngono bila ridhaa yao.

Waziri Mkuu amesema kama zilivyo nchi nyingine Duniani, Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zinakabiliwa na tatizo la ukatili wa kijinsia na kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu mwaka 2015/2016 kupitia inakadiriwa kuwa asilimia 40 ya wanawake wenye umri kati ya miaka 15 - 49 wamefanyiwa ukatili wa kupigwa au kingono katika kipindi cha maisha yao.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,JUMAPilI, NOVEMBA 25, 2018.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU NOVEMBA 26,2018

iStore Tanzania yazindua simu mpya hapa nchini

$
0
0
DUKA la istore nchini Tanzania imezindua simu mpya ya iPhone Xs na iPhone Xs max inayoanza kutumika nchini kuanzia sasa. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mtaalamu wa Bidhaa za simu za Apple, Salum Abdalla amesema kila nchi yenye bidhaa hiyo ina muda wake wa kuzindua simu mpya na kwa Novemba 23 imekuwa ni muda wa nchi ya Tanzania kuzindua simu ya iPhone Xs na iPhone Xs max.

Amesema wamezindua simu hiyo baada ya kukamilisha taratibu zote ikiwemo kuwasiliana na Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) ili kuitambulisha kwao na kuiruhusu kutumia mitandao ya hapa nchini.

 Abdalla amesema kila nchi ina taratibu zake na kwa Tanzania lazima wafike TCRA na iStore Tanzania imefanya jambo hilo na kwa hiyo sasa hivi iPhone Xs na iPhone Xs max rasmi zinaweza kutumika nchini.

Akielezea utofauti wa simu ya 
iPhone Xs na iPhone Xs max, amesema ni simu zenye uwezo mkubwa sana tofauti na simu zingine.
Mkurugenzi wa iStore Tanzania, Vipul Shah akizungumza na wanafamilia wa iStore Tanzania waliofika kwenye uzinduzi wa simu mpya ya iPhone Xs na iPhone Xs max uliofanyika katika dula la iStore Tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi na wateja wa iStore Tanzania wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati wa uzinduzi wa Simu mpya ya iPhone Xs na iPhone Xs max uliofanyika katika duka la iStore Tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa iStore Tanzania, Pareshi Gohil akitoa ufafanuzi kuhusu laptop kwa mmoja wa wateja waliofika kwenye uzinduzi  wa simu mpya ya iPhone Xs na iPhone Xs max ,duka la iStore tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi wa iStore Tanzania, Shamim Goliama(kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu simu mpya ya iPhone Xs na iphone Xs max kwa baadhi ya wateja waliofika kwenye tukio hilo la uzinduzi uliofanyika katika duka la iStore tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa iStore Tanzania, Vipul Shah(kushoto) akizungumza na mmoja wa wateja waliofika katika duka la iStore tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa simu mpya ya iPhone Xs na iPhone Xs max.
Afisa masoko na Mtaalamu wa Bidhaa wa iStore Tanzania, Salum Abdalla akizungumza na wandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa simu mpya ya iPhone Xs na iPhone Xs max ilinayoanza kutumika hapa nchini
Baadhi ya wateja wakiangalia bidhaa za iStore wakati wa uzinduzi wa simu mpya ya iPhone Xs na iPhone Xs max uliofanyika katika duka la iStore Tawi la Mlimani City jijini Dar es Salaam.


WAJASIRIAMALI MARANGU WAMKANA AFISA MAENDELEO YA JAMII

$
0
0

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akizungumza na wajasirimali kutoka Umoja wa Vicoba Marangu (UVIMA) na Shirika la Floresta wakati wa ziara yake kukagua shughuli zinazofanywa na vikundi hivyo mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akiangalia mkungu wa ndizi unaolimwana wajasirimali kutoka Umoja wa Vicoba Marangu (UVIMA) na Shirika la Floresta wakati wa ziara yake kukagua shughuli zinazofanywa na vikundi hivyo mkoani Kilimanjaro. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW


Na Mwandishi Wetu Marangu Moshi

Umoja wa Vicoba Marangu (UVIMA) wamemueleza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile kuwa ndani mwaka mzima hawajawahi kumwona Afisa Maendeleo ya Jamii wa mkoa wala Wilaya kuja kuwatembelea katika vikundi vyao.

Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo katika Shirika la Froresta linalojihusisha na utunzaji wa mazingira na Umoja wa Vicoba Marangu katika kujionea shughuli za uwezeshaji wananchi hasa wanawake kiuchumi. Naibu Waziri Ndugulile amewaagiza Maafisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Kilimanjaro na Wilaya ya Moshi Vijijini kuhakikisha wanawatembelea wajasiriamali na kuweka wazi vigezo vya uanzishaji vikundi na utoaji wa mikopo katika vikundi hivyo.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa ili kuwezesha kiuchumi hasa wanawake mamlaka husika zinatakiwa kutimiza wajibu katika kulifanikisha hilo. Aidha Dkt. Ndugulile ameziagiza Mamlaka za SIDO, TFDA, na TBS kutoa elimu kwa wajasiriamali ili kuwawezesha katika kupata elimu juu ya uanzishaji wa biashara na kutengeneza wa bidhaa bora. “Natoa agizo kwa kila ziara yangu wawepo SIDO, TFDA, na TBS waongozane na mimi ili kutatua changamoto na kero za wananchi kwa kila napoenda” alisisitiza Dkt. Ndugulile

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Floresta Mchungaji Winford Mosha amemshukuru Naibu Waziri kuwatembelea na kuahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza majukumu ya kuwawezesha kiuchumi wananchi hasa wanawake. Ameongeza kuwa uazishwaji wa vikundi na umoja wa Vicoba umewasaidia wanawake wengi kujipatia kipato kinachowawezesha kutekelza majukumu yao katika familiana jamii.

Naye mmoja wa wajasiriliamali Bi. Mary Mtei amesema kuwa wanamekuwa akikutana na changamoto mbalimbali katika kufikia malengo ikiweo unyanyasaji kwa wanawake ikiwa ni moja ya Ukatili wa Kijinsia unaowakandamiza wanawake. Naibu Waziri Ndugulile yupo mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya siku tatu kufuatilia shughuli za Afya na Maendeleo ya Jamii.

CHINA DASHENG BANK LIMITED YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM, KUSAIDIA UCHUMI WA VIWANDA

$
0
0
NA K-VIS BLOG

BENKI mpya ya China Dasheng Bank Limited, inaanza kutoa huduma leo Jumatatu Novemba 26, 2018, jijini Dar es Salaam, ikiwa na mtaji wa kuanzia wa dola za kimarekani milioni 40 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 92, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya benki hiyo Bw. Yu Jiaqin amesema.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa benki hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Bw. Yu Jiaqin amesema benki hiyo ni benki ya kibiashara inayomilikiwa na makampuni sita ya serikali ya China yakishirikiana na makampuni binafsi kutoka mji wa Shanghai na Jiangsu.

Benki hii inalenga kutoa huduma kwa makampuni makubwa ya kichina yanayofanya miradi mbalimbali hapa nchini, lakini pia watanzania wanaofanya biashara na China ikizingatia makundi yote ya watu wenye kipato cha chini, cha kati na cha juu, alisema Bw. Jiaqin.

“Tutatoa huduma za bidhaa zote za kawaida za kibenki kama vile akaunti za akiba, akaunti za kudumu na za muda maalum, mikopo ya muda mfupi na muda mrefu na mikopo hii itatolewa kwa shilingi za kitanzania pamoja na fedha za kigeni.” Alibainisha Mwenyekiti huyo wa bodi.

Aidha Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bi Nunu Saghaf alishukuru Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kutoa leseni ya kufanya biashara kwa benki yake na kuahidi kuisaidia serikali ya Tanzania katika kufikia malengo yake ya uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.

"Makao Makuu ya China Dasheng Bank Limited, yatakuwa hapa jijini Dar es Salaam kwenye jingo la Ex-telecom, makao makuu ya kampuni ya TCCL barabara ya Samora, tunawakaribisha sana watu wote wanaohitaji huduma za kibenki." Alifafanua Bi. Saghaf.

Kwa upande wake, Balozi wa China nchini Mhe.Wang Ke, alisema, kufunguliwa kwa benki hiyo hapa nchini ni ishara ya ushirikiano madhubuti na wa muda mrefu baina ya China na Tanzania na benki hiyo itaboresha huduma za kifedha na hivyo kuwa na manufaa makubwa kwa wafanyabiashara kutoka China na Tanzania.

China imefanya mageuzi makubwa sana ya kiuchumi kutoka umasikini na kufikia nchi ya pili kwa uchumi mkubwa duniani na hili pia linawezekana kwa Tanzania, alisema balozi Wang Ke.Balozi huyo alisema, anaimani kubwa na uongozi wa juu wa benki hiyo ukiongozwa na mwenyekiti Bw.Yu Jiaqin kwani anao uzoefu wa muda mrefu wa shuhhuli za kibenki.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda alisema, anayo furaha kubwa kuona benki hiyo yenye mtaji mkubwa inafunguliwa katika jiji la Dar es Salaam na hivyo itaongeza mitaji ya wawekezaji na wafanyabiashara wa kitanzania.

Alisema kuwa serikali ya Mkoa itaendelea kutoa ushirikiano unaotakiwa na taasisi hiyo kwa lengo la kufikia malengo yanayotarajiwa.“Mimi binafsi nimekwenda China ile dhana kuwa ni wajanja kibiashar ni dhana potofu cha msingi ni kuendelea kushirikiano katika sekta mbali mbali kwa manufaa ya nchi hizi ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa kujituma”, alisema

Katika kuimairisha ushirikiano na jamii ya wachina, Makonda alidokeza kuwa serikali ya mkoa wa Dar es Salaam itaandaa mkutano wa kubaini changamoto wanazokutana nao wafanyabiashara hao kwa nia ya kuzitatua.
Alisema kuwa nia na lengo la serikali ni kuona kuwa wafanyabiashara wa kigeni wanafanya biashara zao katika mazingira sawa na huru.
Balozi wa China nchini Tanzania Mhe.Wang Ke, (katikati), akiungana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, (wapili kushoto), Mwenyekiti wa Banki mpya ya China Dasheng Bank Limited, Yu Jiaqin, (wapili kulia), Afisa mwandamizi kutoka Banki Kuu ya Tanzania, Sadaat Mussa (wakwanza kulia) na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka China, Zhujin Feng, baada ya kukata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Benki hiyo imeanza kutoa huduma leo Jumatatu Novemba 26, 2018 ikiwa na mtaji wa kuanzia wa dola za kimarekani milioni 40 sawa na shilingi za kitanzania bilioni 92, Mwenyekiti wa benki hiyo amesema.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, akitoa hotuba yake.
Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Wang Ke akitoa hotuba yake.
Mwenyekiti wa Banki mpya ya China Dasheng Bank Limited, Yu Jiaqin, akitoa hotuba yake.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka China, Zhujin Feng, akitoa hotuba yake.
Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa China Dasheng Banki Limited, Bi. Nunu Saghaf (watatu kushoto mstari wa mbele akiwa na wageni mbalimbali kwenye hafla hiyo ya uzinduzi.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
 Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi benki ya China Dasheng ,Limited Bw.Yu Jiaqin, (kulia), akibadilishana hati na Mkurugenzi Mtendaji wa Star Times Tanzania, Bw.Wang Xiaobo, wa ushirikiano baina ya benki na kampuni hiyo, wakati wa uzinduzi wa benki hiyo mpya jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wik.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda (kushoto), akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi China Dansheng Bank Limited, Bw. Yu Jianqin huku Balozi wa China nchini, Mhe. Wang Ke, (wapili kushoto) na afisa mwandamizi kutoka Benbki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Saadat Musa wakishuhudia wakati wa uzinduzi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Wang Ke, (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, wakati wa uzinduzi wa benki mpya ya China Dasheng Bank Limited jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Benki hiyo inaanza kutoa huduma Jumatatu Novemba 26, 2018 ikiwa na mtaji wa kuanzia wa dola za kimarekani milioni 40 Sawa na shilingi za kitanzania bilioni 92, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya benki hiyo Bw. Yu Jiaqin amesema. Kulia ni afisa mwandamizi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Saadat Mussa. 
Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Wang Ke, (watau kushoto) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda,(wapili kushoto), wakati wa uzinduzi wa benki mpya ya China Dasheng Bank Limited jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Benki hiyo inaanza kutoa huduma Jumatatu Novemba 26, 2018 ikiwa na mtaji wa kuanzia wa dola za kimarekani milioni 40 Sawa na shilingi za kitanzania bilioni 92, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya benki hiyo Bw. Yu Jiaqin (pichani wakwanza kulia) amesema. Wakwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa China hapa nchini, Bw.Zhujin Feng. 
Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Wang Ke, (wapili kushoto), akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda,(wakwanza kushoto), wakati wa uzinduzi wa benki mpya ya China Dasheng Bank Limited jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Benki hiyo inaanza kutoa huduma Jumatatu Novemba 26, 2018 ikiwa na mtaji wa kuanzia wa dola za kimarekani milioni 40 Sawa na shilingi za kitanzania bilioni 92, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya benki hiyo Bw. Yu Jiaqin (pichani wapili kulia) amesema. Wakwanza kulia ni Afisa mwandamizi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Saadat Mussa.(PICHA/HABARI NA K-VIS MEDIA)

BARAZA LA WAHITIMU WA CHUO KIKUU ARDHI WAFANYA MATEMBEZI YA HISANI KWA AJILI YA HARAMBEE

$
0
0
Jumuiya ya wahitimu ya Chuo Kikuu Ardhi (Adhi University Convocation) jana imefanya matembezi ya hisani yenye lengo la kuwaita wanajumuiya wote wa chuo hicho (ALUMN) ili kukumbuka nyumbani (waliposoma) hivyo kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo za chuo. 

Maandamano yaliongozwa na Rais wa baraza la wahitimu la Chuo hicho, Haruna Masebu pamoja na Naibu makamu Mkuu wa Chuo Mipango Fedha na Utawala, Profesa Robert Kiunsi. Mbali na matembezi hayo kulikuwa na mazoezi ya ya pamoja na michezo mbalimbali kiwemo Aerobic, Soka na mbio.Miongoni mwa washiriki walikuwepo pia sehemu ya wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ALUMNI wakiongozwa Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. Maulid Bajani.Pia alikuwepo Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu Dkt. Moses Kusiluka ambaye ni mdau mkubwa wa chuo hicho.Wengine ni UCLAS Veteraniambao walicheza soka na wanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi na kuibuka kidedea. 
Sehemu ya wadau (ALUMN) na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) pamoja na wadau wao Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakifanya matembezi katika Barabara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Novemba 24, 2018 kwa ajili ya shughuli za chuo jijini humo. Chuo hicho kinatarajiwa kuwa na Kongamano la wahitimu (CONVOCATION) Ijumaa ya Novemba 30, 2018. (Imeandaliwa na Robert Okanda) 
Sehemu ya wana ALUMNI na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakifanya matembezi katika Barabara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Novemba 24, 2018.
Sehemu ya wana ALUMNI na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakifanya matembezi katika Barabara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Novemba 24, 2018.
 
Sehemu ya wana ALUMNI na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakifanya mazoezi ya viungo baada ya matembezi hayo.
Sehemu ya wana ALUMNI na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU) wakifanya mazoezi ya viungo baada ya matembezi hayo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dkt. Sophia Kongela (tisheti ya blue) akiwa katika picha pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo baada ya kushiriki matembezi ya hisani yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu Ardhi (ARU) Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Pamoja naye (wa saba kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dkt. Maulid Banyani.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dkt. Maulid Banyani akitoa agizo kwa wafanyakazi wa shirika hilo kuanzia sasa kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi pamoja mara moja kila mwezi baada ya kushiriki matembezi ya hisani yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu Ardhi (ARU). Mwenye (tisheti ya blue) ni Mwenyekiti wa NHC, Dkt. Sophia Kongela.

PANGANI JOGGING CLUB YAZINDULIWA KWA KISHINDO

$
0
0

 Mbunge wa PANGANI na naibu waziri wa maji na umwagiliaji Mh jumaa awesso akikata utepe ikiwa kama ishara ya uzinduzi wa PANGANI JOGGING CLUB
 Mbunge wa PANGANI na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe Jumaa Awesso (Wa tatu toka kushoto) akiwa na Kamati na wajumbe wa awali wa PANGANI JOGGING CLUB wakiwa katika picha ya pamoja
 Kamati na wajumbe wa awali wa PANGANI JOGGING CLUB wakiwa katika picha ya pamoja.
 Mbunge wa PANGANI na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe Jumaa Awesso akiwa na wana-PANGANI JOGGING CLUB wakiwa katika picha ya pamoja.
Mbunge wa PANGANI na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe Jumaa Awesso (Mbele) akiwa katika mazoezi na Wana-PANGANI JOGGING CLUB mara baada ya kumaliza uzinduzi.
Maulidi Kitenge wa Efm sambamba na afisa tawala wa Pangani ndugu Gibson George wakati wa uzinduzi wa PANGANI JOGGING CLUB walipokuwa wakikimbia katika mji huo wa kihistoria.
 Mbunge wa PANGANI na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe Jumaa Awesso akiwa katika mazoezi ya viungo na Wana-PANGANI JOGGING CLUB. 

 Zaidi ya watu mia tano wamejitokeza katika uzinduzi wa PANGANI JOGGING CLUB uliyofanyika asubuhi ya Jumamosi ya tarehe 24/11/2018 katika uwanja wa Bomani Pangani mjini. Uzinduzi huo umepambwa na mazoezi ya pamoja, yaliyoendeshwa na club ya mazoezi kutokea jijini Tanga, Power and Sports ambayo yalinogesha na kuongeza hamasa kwa umati mkubwa ulihudhuria uzinduzi huo wa kihistoria. 

Mbali na Power and Sport, club nyingine zilizoshiriki katika uzinduzi huo ni pamoja na TK Jogging club kutokea jijini Tanga, na EFM jogging club kutokea jijini Dar es salaam ambayo baadae ilicheza mchezo wa soka wa kirafiki dhidi ya wakazi wa Pangani. 

 Mgeni rasmi katika Uzinduzi wa PANGANI JOGGING CLUB alikuwa ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Na Mbunge wa Pangani Mh. Jumaa Awesso ambaye mbali na kushiriki mazoezi na wananchi wake, pia amekubali kuwa mlezi wa club hiyo,Pia katika kutambua umuhimu wa michezo na Mazoezi Mh Aweso alitoa zawadi ya mipira kwa klabu za soka wilayani Pangani Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kiserikali, waheshimiwa madiwani, wakuu wa idara halmashauri ya Pangani pamoja na wadau mbali mbali kutoka sekta binafsi PANGANI JOGGING CLUB imezinduliwa ikiwa na lengo la kuhamasisha mazoezi kwa ajili ya kuboresha afya, kwa mustakabali wa maendeleo ya Pangani, sambamba na kuhamasisha ushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii, kukuza mahusiano ya watu na kubadilishana mawazo, pamoja na kusukuma ajenda mbalimbali za kimaendeleo za serikali. 

 Afisa Tarafa wa Pangani mjini na Mwenyekiti wa club hiyo Bi. Zuhura Rashid, sambamba na katibu wake Bwana Midraj Msusa, wamemesema kuwa, club hiyo itakuwa endelevu, na itasaidia kwa kiasi kikubwa wanapangani katika mustakabali wa kupambana na afya zao.

POLISI IPO IMARA KUPAMBANA NA UHALIFU WA AINA YOYOTE NCHINI, USALAMA WA WANANCHI SERIKALI YA AWAMU YA TANO ‘HAUBIPIWI’-WAZIRI LUGOLA

$
0
0
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema Jeshi la Polisi lipo imara kupambana na uhalifu wa aina yoyote utakaojitokeza nchini hivyo wahalifu wasithubutu kulichezea, wala ‘kulibipu’.

Lugola pia amewataka wananchi kuendelea kuwapa taarifa za uhalifu Polisi ili ziweze kufanyiwa kazi haraka kwa kuwa Serikali ya Rais Dk. John Magufuli si ya kuchezewa na imejipanga kikamilifu kwa kuwalinda wananchi wake.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Ragati, Kata ya Kasuguti, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, Lugola alisema Jeshi la Polisi lipo imara na litaendelea kuwalinda wananchi pamoja na mali zao, ila Polisi ili waweze kufanya kazi zao kwa umakini zaidi, wananchi wanapaswa kuwasaidia katika kufichua uhalifu katika maeneo yao wanayoishi.

Lugola aliyazungumza hayo baada ya wananchi wa Kijiji hicho kumlalamikia kuwa kuna kundi la vijana ambalo linaongozwa mwananchi mmoja kijijini hapo wanahatarisha amani na kuwafanya kuishi kwa wasiwasi na kushindwa kufanya shughuli zao za maendeleo.

“Polisi wapo kwa ajili yenu hivyo kuweni huru muda wowote kutoa taarifa za kiuhalifu katika maeneo yenu, hivyo kutokana na viashiria hivyo vya uvunjifu wa amani katika Kata hii namuagiza mkuu wa polisi wilaya (OCD) kuwasaka, kuwakamata wale wote ambao wanahatarisha amani katika Kata hii ya Kasuguti,” alisema Lugola. Lugola aliongeza kuwa, yeye ni Mbunge wa Jimbo hilo na pia ni Waziri ambaye anasimamia usalama wa wananchi na mali zao, hivyo hatakubali wananchi waishi kwa wasiwasi katika maeneo yao na nchi kwa ujumla, na pia Serikali ya Magufuli haichezewi, haijaribiwi na wala haibipiwi na mtu yeyote.

Amesema licha ya polisi usiku na mchana wanalinda wananchi na mali zao lakini pia wananchi ni wadau wakubwa kwasababu wana mengi wanayaona mitaani kwao hivyo kwa baadhi ya wale wenye tabia ya kuficha matukio ya uhalifu ni hatari kwa usalama wao. Aidha, Lugola aliwataka wananchi wa Kata hiyo waendelee kufanya shughuli za kimaendeleo katika vijiji vyao na pia waanze maandalizi ya kilimo, naye atahakikisha anatoa misaada mbalimbali ikiwemo mbegu ili wananchi hao waweze kupata mazao yaliyo bora kwa hapo baadaye.

Lugola pia alijibu maswali mbalimbali ya wananchi hao, yakiwemo kuhusu maendeleo ya Jimbo lao na pia kuhusu Jeshi la Polisi pamoja na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kuhusu kuwapa vitambulisho. Hata hivyo, kwa upande wa wananchi kupata vitambulisho vya taifa, Lugola aliendelea kusisitiza kuwa, Vitambulisho hivyo vitatolewa kwa watanzania wenye sifa na haki yao kupata lakini ili waweze kupata vitambulisho hivyo lazima wapitie katika mchujo ili kuepusha kutoa kwa wasio raia.

Amesema mchujo huo unaofanywa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) upo makini ili kuhakikisha hakuna makosa yatakayofanywa wakati wa utoaji wa vitambulisho, hivyo wananchi wawe na uvumilivu wakati mchujo huo ukiendelea. Lugola anaendelea na ziara jimboni kwake akisikiliza kero za wananchi pamoja na kuhamasisha kilimo cha mazao ya pamba, mahindi, mpunga, viazi na mengineyo ambayo wakazi wa jimbo lake wanalima mazao hayo kwa wingi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kulia), akimsindikiza kumpeleka ndani ya gari Mkazi wa Kitongoji cha Songambele, Kata ya Kasuguti, Jimbo la Mwibara mwenye umri wa miaka 100, Mzee Mtatiro Silla, mara baada ya Waziri huyo kumaliza mkutano wake wa hadhara akizungumza na wananchi wa Kata hiyo, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, leo. Lugola aliwataka wananchi jimboni kwake watoe polisi taarifa za uhalifu nchini na pia Serikali ya Awamu ya tano ipo imara haichezewi na mtu yeyote. Pia Lugola aliwataka wananchi jimboni kwake waanze maandalizi ya kilimo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto), akimsikiliza Mkazi wa Kitongoji cha Songambele, Kata ya Kasuguti, Jimbo la Mwibara, mwenye umri wa miaka 80, Mzee Nyamuhanga Mtatiro Silla, wakati mzee huyo alipokua anamuuliza swali Waziri Lugola katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kitongoji hicho, leo. Wapili kushoto meza kuu ni Mzee mwenye umri wa miaka 100, Mtatiro Silla ambaye ni baba mzazi wa anayezungumza, na mtoto wake wa tatu katika kuzaliwa. Baba na mwana wote walihudhuria mkutano huo wa Waziri Lugola. Lugola aliwataka wananchi jimboni kwake watoe polisi taarifa za uhalifu nchini na pia Serikali ya Awamu ya tano ipo imara haichezewi na mtu yeyote. Pia Lugola aliwataka wananchi jimboni kwake waanze maandalizi ya kilimo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto), akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kasuguti, Kata ya Kasuguti, Jimbo la Mwibara, Mkoani Mara, akiwataka wananchi jimboni kwake watoe taarifa za uhalifu Polisi na iliwawe na amani na waendelee kufanya shughuli zao za kilimo, pia alisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya tano ipo imara haichezewi na mtu yeyote.

Viewing all 46360 articles
Browse latest View live




Latest Images