Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1731 | 1732 | (Page 1733) | 1734 | 1735 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Mwanza Mhandisi Marwa Rubirya (katikati), akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa (kushoto) eneo litakapojengwa daraja jipya linalounganisha Kigongo-Busisi mkoani Mwanza, daraja hilo litakuwa na urefu wa KM 3.2 kulia ni mkuu wa kivuko cha kigongo-busisi mhandisi Abdala Atiki.
  Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Mwanza Mhandisi Marwa Rubirya (watatu kushoto), akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa (wapili kushoto) eneo litakapojengwa daraja jipya linalounganisha Kigongo-Busisi mkoani Mwanza, daraja hilo litakuwa na urefu wa KM 3.2 (kulia) ni mkuu wa kivuko cha Kigongo-Busisi mhandisi Abdala Atiki.
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa (mwenye miwani), akiwasikiliza wanafunzi ambao ni abiria wa kivuko cha Mv- Mwanza kinachotoa huduma kati ya Kigongo-Busisi mkoani Mwanza alipokagua shughuli za uendeshaji wa kivuko hicho.


  Naibu Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Elias John Kwandikwa amewataka wakazi wa mikoa ya Mwanza na Geita kuchangamkia fursa za kiuchumi na kijamii zitakazojitokeza wakati wa ujenzi wa daraja litakalounganisha eneo la Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza.

  Amesema maandalizi kwaajili ya ujenzi wa daraja hilo la aina yake hapa nchini yako katika hatua ya usanifu wa kina hivyo ujenzi wake utaanza mara baada ya mkandarasi wake kutangazwa na linatarajiwa kuwa na urefu wa kilomita 3.2, litakapokamilika. “Hakikisheni mnatoa ushirikiano kwa mkandarasi ili kazi ya ujenzi iwe nyepesi na wale watakaopata fursa za ajira fanyeni kazi kwa weledi, bidii na nidhamu” amesisitiza Naibu Waziri Kwandikwa.

  Amesema Serikali inatumia fedha nyingi katika miradi ya maendeleo ya muda mrefu hivyo ni jukumu la wananchi kujiandaa na kubaini fursa za kiuchumi na kijamii na kuzitumia. Naye Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Mwanza Mhandisi Marwa Rubirya amesema daraja hilo litakuwa na njia nne za kupitisha magari, njia ya waenda kwa miguu ambapo pia litakuwa na kina kitakachoruhusu meli kupita chini ya daraja hilo.

  Mhandisi Rubirya amesisitiza umuhimu wa wananchi wenye maeneo yatakayotumika kupisha ujenzi huo kutoa ushirikiano ili kuharakisha kazi hiyo. Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kwandikwa amekagua kivuko cha Kigongo-Busisi na kuagiza Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), kuhakikisha elimu inatolewa kwa wananchi kuhusu usalama na matumizi sahihi ya utumiaji wa vivuko.

  Amezungumzia umuhimu wa TEMESA kuweka mifumo ya kielektoniki ili kuwezesha waendesha vivuko, wakusanya mapato na wasimamizi kuwa na mawasiliano ya pamoja na hivyo kuwezesha vivuko kuwa na abiria na mizigo inayokubalika wakati wote. Mkuu wa kivuko cha Kigongo –Busisi Mhandisi Abdala Atiki amesema kivuko hicho kwa sasa kinahudumiwa na Mv- Mwanza na Mv- Misungwi ambapo zaidi ya abiria elfu sita na mia tano huvushwa kwa siku.

  Zaidi ya mikoa 12 nchini ina maeneo yenye mahitaji ya vivuko ambapo takriban vivuko 30 vinatoa huduma nchini kote.

  0 0


  Wachezaji mbalimbali chipukizi wa kuogelea wakiwa katika matukio tofauti

  Mashindano ya kuogelea kwa wachezaji yoso yamepangwa kufanyika Desemba 8 na 9 kwenye bwawa la kuogelea la shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) Upanga.

  Katibu Mkuu wa Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA), Inviolata Itatiro amesema kuwa mashindano hayo yatashirikisha waogeleaji chipukizi kuanzia miaka 12 kushuka chini, yana lengo la kuibua vipaji vya waogeleaji kwa ajili ya kushiriki mashindano mbalimbali nchini na ya kimataifa.

  Inviolata amesema kuwa TSA kwa sasa inatafuta wadhamini wa kufanikisha mashindano hayo. Mwisho wa kuthibitisha ni Novemba 30. “Mashindano haya ni ya kuibua na kuendeleza vipaji, na pia yameandaliwa kwa ajili ya kupima uwezo wa waogeleaji chipukizi ambao wameibuliwa katika mashindano yaliyopita, tunaomba wadhamini wajitokeze,” alisema Inviolata.

  Amefafanua kuwa wanatafuta wadhamini kwa ajili ya kusaidia gharama za uendeshaji kwani siyo kazi rahisi mashindano hayo kufanyika bila sapoti kutoka nje. Alisema kuwa kila klabu inatakiwa kuorodhesha majina ya waogeleaji wake wakiwa na umri na aina ya mashindano ambayo wanatakiwa kushindana ili kuwawezesha kuandaa programu kamili ya mashindano hayo.

  “Mashindano haya yatatoa fursa kwa waogeleaji ambao walishindwa kushindana katika mashindano ya wakubwa kutokana na kigezo cha umri, kwa vile TSA inatamnbua waogeleaji chipukizi, tumeamua kuandaa mashindano ambao yatawafanya waogeleaji wanaochipukia nao kujipima uwezo wao,”alisema.

  Alisema kuwa kutakuwa na makundi manne, kundi la waogeleaji waliochini ya miaka saba, waogeleaji wa miaka nane na tisa, 10 na 11 na 12. Washindi wa jumla katika kila kundi atazawadiwa kikombe wakati washindi wa kila shindano watapata medali.

  0 0

  Mkurugenzi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bw. Valency Mutakyamirwa akizungumza na washiriki wa warsha ya siku mbili kuhusu uwezeshaji wa wanachama wa Taasisi hiyo leo Jijini Dodoma ikilenga kuibua changamoto na kuweka mikakati ya pamoja yakuzitatua. 
  Meneja Mradi kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bi. Veneranda Sumila akisisitiza kuhusu umuhimu wa semina ya kuwajengea uwezo wanachama wa TPSF leo Jijini Dodoma wakati wa hafla yakufungua warsha hiyo. 
  Mratibu kutoka Taasisi ya Best Dialogue Bi. Manka Kway akizungumzia umuhimu wa Maktaba ya Mtandaoni inayoleta pamoja taarifa za wajasiriamali wa Tanzania ikiwemo tafifi mbalimbali zinazofanyika zikilenga kuchangia katika kukuza biashara hapa nchini. 
  Muwezeshaji wa masuala ya Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw. Patrokil Kanje akizungumzia namna wajasiriamali wa Tanzania wanavyoweza kukuza na kuendeleza biashara zao kwa kutumia mbinu za kisasa wakati wa warsha ya wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi. 
  Katibu Mtendaji wa Umoja wa Wachimbaji wa Madini na Nishati Tanzania (TCME) Bw. Gerald Mturi akizungumzia umuhimu wa semina hiyo kwa wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi. 

  Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini imedhamiria kuendelea kuwajengea uwezo wajasiriamali nchini ili waweze kuzalisha na kukuza biashara zao na kuchangia katika ujenzi wa uchumi wa viwanda. 

  Akizungumza leo Jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bw. Valley Mutakyamirwa amesema kuwa dhamira yao ni kuendelea kujenga uwezo kwa wajasiriamali hao ili waweze kuchangika katika kutatua changamoto zinazowakabili kwa kuweka mikakati ya pamoja kati ya wanachama wa Taasisi hiyo. 

  “ Wajasiriamali hawa ni wanachama wetu hivyo jukumu letu ni kuhakikisha kuwa tunashirikiana nao katika kuibua changamoto na kuweka mikakati ya pamoja ambayo tunashirikiana na Serikali katika kuona namna bora yakuzitatua “; Alisisistiza Mutakyamirwa 

  Akifafanua amesema kuwa, Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wajasiriamali ikiwemo kujenga miundombinu, kupunguza kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kutoka asilimia 20 hadi 18 hali inayoonesha dhamira ya dhati ya Serikali kuendelea kuimarisha mazingira ya wajasiriamali kufanya biashara. Aliongeza kuwa Warsha hiyo inawasaidia wajasiriamali hao kufanya tathmini ya shughuli wanazofanya na kuja na mikakati ya pamoja itakayoasaidia katika kuimarisha Biashara hapa nchini. 

  Kwa upande wake Muwezeshaji kutoka Taasisi ya Best Dialogue Bi. Manka Kway akizungumzia kuanzishwa kwa Maktaba ya Mtandaoni itakayokuwa na taarifa zote kuhusu masuala ya wajasiriamali zikiwemo tafiti, machapisho,fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo, Utalii, Biashara, Uwekezaji, Viwanda na miundombinu. 

  Aliongeza kuwa kuwepo kwa maktaba hiyo kutasaidia kuimarisha na kusaidia kuinua kiwango cha Biashara hapa nchini kwa kuvutia wawekezaji na wajasiriamali wa ndani na nje ya nchi kuongeza uwekezaji na kuchochea maendeleo. Pia aliwataka wajasiriamali kutumia fursa ya kuwepo kwa Maktaba hiyo kufuatilia taarifa mbalimbali zilizopo katika maktaba hiyo ya mtandaoni katika kutafuta fursa mbalimbali zinazoweza kuimarisha utendaji wa wajasiriamali hao na kukuza sekta husika. 

  Katika maktaba hiyo ya mtandaoni wawekezaji kutoka katika mataifa mbalimbali wanaweza kupata taarifa zitakazowawezesha kuja kuwekeza hapa nchini na hivyo kuchochea ukuaji wa sekta ya Biashara na uwekezaji hapa nchini. 

  Warsha ya kuwajengea uwezo wajasiriamali ambao ni wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi inafanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma ikilenga kuwajengea uwezo wajasiriamali hao ili kuongeza tija kwa wajasiriamali hao hapa nchini .

  0 0

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mgwira (kulia) katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huyo kuhusu kuwaelekeza wadau wa NGO kupanga utekelezaji wa miradi yao kwa kufuata vipaumbele na kuwapangia sehemu sahihi wadau hao kufanya kazi katika maeneo ya pembezoni ili kuleta usawa katika mgawanyo wa rasilimali kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Aisha Amour.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akimsikiliza Mzee wa miaka 98aliyejulikana kwa jina la Daniel Mzava alipotembelea Hospitali ya
  Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile  kimjjulia hali mmoja wa Mtoto aliyekuwa akipata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi wakati wa ziara yake Hospitalini hapo.  Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

    Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amezidi kuyasisitiza Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuzingatia vipaumbele vilivyowekwa na Serikali
  katika kutekeleza miradi ya Maendeleo nchini.

  Ameyasema hayo mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya siku tatu kutembelea na kukagua shughuli mbalimbali katika sekta ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.  Dkt. Ndugulile amesema kuwa nia ya Serikali sio kuyabana Mashirika hayo ila kuyaratibu ili yaweze kufanya kazi katika mazingira mazuri ambayo yatawezesha kuwa na mgawanyiko mzuri wa rasilimali katika maeneo mbalimbali nchini.

  Naibu Waziri Dkt. Ndugulile ameutaka uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kuweka vipaumbele na kuzielekeza NGOs sehemu za kwenda na sio kuziweka NGOs nyingi mahala pamoja.  Dkt. Ndugulile pia amezitaka NGOs kufanya kazi katika misingi ya uwajibikaji na kufuata Sheria na taratibu za nchi ili kuendeleza ushirikiano kati yao na Serikali katika kuchangia juhudi za wananchi kupata Maendeleo jumuishi.  “Unakuta sehemu moja zimerundikana NGOs nyingi na mkoa huo huo maeneo mengine hakuna NGOs hata moja” alisisitiza Dkt. Ndugulile.

  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mgwira amesema Mkoa wake unapambana na changamoto mbalimbali katika Sekta ya Afya na Maendeleo ya Jamii na kuiomba Wizara kushirikiana nao ili kutatua changamoto zinazoukabili mkoa wake.  “Nikushukuru Mhe. Naibu Waziri kwa kutukumbuka kuja kututembelea ila naomba mtuangalie kwa jicho la tatu katika kutatua changamoto zetu hapa mkoani” Alisisitiza Mhe. Anna.

  Naye Mganga Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Best Magoma amesema huduma za Ustawi na Maendeleo ya Jamii zinazingatiwa na kuangaliwa kwa ukaribu ili kuendelea kumuwezesha mwananchi kufaidika na huduma hizo.  Msisitizo huu kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kufuata vipaumbele
  vya taifa umekuja baada ya Serikali kuyataka Mashirika hayo kufanya kazi kwa kuzingatia uwazi na uwajibikaji katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo nchini.

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile yupo mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya siku tatu kufuatilia utekelezaji wa sera na programu katika Sekta ya Afya na
  Maendeleo ya Jamii.

  0 0

   Kaimu Mkurugenzi wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Bw Hisham Hendi akitoa mada kuhusiana na uchumi wa kidijitali katika mkutano wa mwaka wa Taasisi ya Usimamizi wa Miradi uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Nyuma ni Mkurugenzi wa Muendeshaji wa kampuni ya FSDT, Bi Irene Mlola na Mwenyekiti wa DTBi, Bw Mihayo Wilmore. 
   Mkurugenzi Mtendaji wa Universal Communication Service Access Fund (UCSAF), Peter Ulanga akizungumza katika mkutano wa mwaka wa Taasisi ya Usimamizi wa Miradi (PMI) uliofanyika jijini Dar es Salaam mapema jana. Mkutano huu umelenga kujadili ukuaji wa uchumi wa kidijitali. 
    Kaimu Mkurugenzi wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Bw Hisham Hendi akichangia mada kuhusiana na uchumi wa kidijitali kaatika mkutano wa mwaka wa Taasisi ya Usimamizi wa Miradi uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Universal Communication Service Access Fund (UCSAF), Peter Ulanga
   Mshauri wa Taasisi ya Usimamizi wa Miradi (PMI, Bw Anael Ndosa, akichangia mada kuhusiana na uchumi wa kidijitali kaatika mkutano wa mwaka wa Taasisi ya Usimamizi wa Miradi uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.


  0 0


  1
  Mkurugenzi Mkuu wa Samsung Afrika Mashariki Hong Seok na Mkurugenzi wa vifaa vya kieletroniki Happy Grayson wakikata utepe wakati wa uzinduzi wa duka jipya la vifaa vya Samsung Posta jijini Dar es salaam leo kulia ni Abraham Okore Mkuu wa Usambazaji Samsung na kushoto ni Suleiman Mohammed Meneja Mkazi wa Samsung.
  2
  Mkurugenzi Mkuu wa Samsung Afrika Mashariki Hong Seok na Mkurugenzi wa vifaa vya kieletroniki Happy Grayson, , Abraham Okore Mkuu wa Usambazaji Samsung na Suleiman Mohammed Meneja Mkazi wa Samsung wakiingia dukani mara baada ya kukata utepe wakati wa uzinduzi huo.
  3
  Mkurugenzi Mkuu wa Samsung Afrika Mashariki Hong Seok akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa vifaa vya kieletroniki Happy Graysonmara baada ya kuzinduliwa kwa duka hilo.
  4
  Mkurugenzi Mkuu wa Samsung Afrika Mashariki Hong Seok akifuatana na Mkurugenzi wa vifaa vya kieletroniki Happy Graysonwakati akitembelea duka hilo.
  5
  Mkurugenzi Mkuu wa Samsung Afrika Mashariki Hong Seok akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa vifaa vya kieletroniki Happy Grayson kuhusu mashine ya kufulia moja ya vifaa vya kielektroniki vinavyopatikana katika duka hilo kulia ni Abraham Okore Mkuu wa Usambazani Samsung.
  6
  Mkurugenzi Mkuu wa Samsung Afrika Mashariki Hong Seok akiangalia moja ya simu za Samsung zinazopatikana dukani hapo kulia ni Mkurugenzi wa vifaa vya kieletroniki Happy Grayson na katikati ni Bw. Abraham Okore Mkuu wa Usambazaji Samsung.
  7
  Baadhi ya wananchi mbalimbali wakiwa wamejitokeza katika uzinduzi wa duka hilo.
  8
  Suleiman Mohammed Meneja Mkazi wa Samsung akizungumza katika uzinduzi huo.
  9
  Mkurugenzi Mkuu wa Samsung Afrika Mashariki Hong Seok akizungumza wakati wa uzinduzi hui uliofanyika leo Posta jijini Dar es salaam.
  10
  Mkurugenzi wa vifaa vya kieletroniki Happy Grayson akizungumza katika uzinduzi huo.
  ....................................................................................................
  *Viongozi wazungumzia ubora wa bidhaa zao, waipongeza Serikali
  *Watakaonunua bidhaa kwao kuingia kwenye droo kila siku
  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii.

  DUKA kubwa la kisasa linaouza bidhaa za aina mbalimbali za Samsung zenye viwango vya hali ya juu katika ubora limefunguliwa Posta katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

  Uzinduzi wa duka hilo umefanyika leo Desemba 24 mwaka 2018 ambapo viongozi wa ngazi mbalimbali wa kampuni ya Samsung ndani na nje ya Tanzania pamoja na baadhi ya wananchi wa Jiji hilo wameshuhudia uzinduzi huo uliokwenda sambamba na punguzo la bei pamoja na droo mbalimbali za kujishindia zawadi kwa wanaonunua bidhaa zao.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka hilo lililopo jengo la Askari Posta Mpya jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa vifaa vya kieletroniki Happy Grayson amesema Samsung ni bidhaa kubwa duniani na yenye ubora wa uhakika.“Tumeamua kufungua duka hili eneo la Posta mpya jijini Dar es Saam kwa ajili ya kuhakikisha bidhaa zetu zinapatikana kwa urahisi na gharama nafuu.Hatutaki watu wanaohitaji bidhaa za Sumsung wasumbuke kuzipata.

  “Tunayo maduka mengi nchini ikiwemo jijini Dar es Saalam lakini umuhimu wa duka hili unatokana na ukweli kwamba kuna bidhaa zote za Samsung ambazo mteja anahitaji kununua kutoka kwetu,”amesema.Amefafanua uzinduzi huo unakwenda sambamba na punguzo la bei la asilimia tano kwa watakaonunua bidhaa kwa siku ya leo ambapo pia wataingia kwenye droo ambapo mshindi atashinda luninga ya Samsung yenye inchi 24 kila siku.Pia kutakuwa na droo ya kila wiki.

  “Ili kuingia kwenye droo hiyo mteja wetu baada ya kununua bidhaa ya Samsung atatakiwa kuhakikisha anasajili.Jinsi ya kusajili ;kwenye uwanja wa kutuma sms andika neno sajili *serial No#tuma kwenda 15685.Utapata tisheti ya buree pindi unaponunua na kujisajili na utaingia kwenye droo ya kushindania Samsung TV 24”,amesema.

  Kwa upande wake Meneja Mkazi Tanzania wa Samsung Suleiman Ahmed amewahakikishia Watanzania katika duka hilo bidhaa zote za Samsung zitapatikana.Kuhusu ubora wa bidhaa zao amesema wamekuwa wakiuza bidhaa ambazo ni bora na zenye uhakika na hiyo imewafanya bidhaa zao kuaminika na kukubalika.

  Ameelezea namna ambavyo Samsung wanafurahishwa na hatua ambazo Serikali inachukua katika kuhakikisha bidhaa zinazoingia nchini zinakuwa na ubora huku akishauri wanaotaka kununua bidhaa zao ni vema wakafika kwenye maduka yao.“Serikali imefanikiwa kudhibiti bidhaa zisizo na ubora kwa kiwango kikubwa.Hata hivyo nishauri ni vema wanaohitaji kununua bidhaa zetu wakafika kwenye maduka yetu likiwemo na hili ambalo tumelizindua leo,”amesema Ahmed.

  Wakati huo huo Mkurugenzi Mkuu wa Samsung Afrika Mashariki Hong Seok amesema wanayo maduka mengi lakini duka hilo la Posta Mpya jijini Dar es Salaam ni muhimu zaidi kutokana na aina ya bidhaa ambazo wanauza kwa ajili ya wateja wao.

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemfutia dhamana Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko kwa kukiuka masharti ya dhamana katika kesi ya uchochezi inayowakabili wao pamoja na viongozi wenzao saba wa chama hicho.

  Uamuzi huo umetolewa leo asubuhi Novemba 23, 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri.

  Akitoa uamuzi huo dhidi ya Mbowe na Matiko, Hakimu Mashauri amesema, kitendo cha washtakiwa hao kutokufika mahakamani bila ya kuwa na sababu za msingi ni kudharau amri za Mahakama kwa makusudi.

  Akitoa uamuzi kuhusu mshtakiwa Mbowe, Hakimu Mashauri amesema, sababu zilizotolewa na mdhamini wake Novemba Mosi mwaka huu kuwa mshtakiwa huyo aliugua ghafla na kupelekwa nje ya nchi akiwa mahututi huku Wakili wake Peter Kibatala akieleza kuwa alipelekwa Afrika Kusini kwa matibabu si za kweli kwa sababu zinakinzana na taarifa alizotoa mshtakiwa mwenyewe.

  Amesema, Mbowe katika maelezo yake alieleza kuwa alisafiri nchini Oktoba 28 mwaka huu kuelekea Washngton DC kuhudhuri mkutano wa Oktoba 30 na kwamba Oktoba 31, usiku alipotaka kusafiri kurejea nchini kwa ajili ya kesi hiyo iliyopangwa kuwepo Novemba Mosi, mwaka huu alishambuliwa na ugonjwa wa ghafla.

  Alieleza kulingana na ugonjwa wake, madaktari waliokuwa wakimtibu, walimshauri asisafiri umbali mrefu kwa ndege lakini hata hivyo hati yake ya kusafiria inaonesha alisafiri umbali mwingine mrefu kwa kwenda Marekani kwa ndege na kitu kinachoonyesha kwamba alikuwa anadharau amri za mahakama kwa makusudi kwa sababu amezungumza mambo ya uongo.

  Pia alisema licha ya Mbowe kueleza kuwa alitakiwa kupumzika, lakini nyaraka yake ya matibabu ilionesha kuwa Novemba 8, mwaka huu ndio alipata matibabu katika nchi za Falme za Kiarabu nchini Dubai, wakati akijua alitakiwa kufika mahakamani.

  "Haiingii akilini kwamba daktari alizuia mshitakiwa kuruka na ndege kutokana na ugonjwa wake lakini aliweza kwenda Ubelgiji ambako alikaa kuanzia Novemba Mosi hadi 6, mwaka huu na kusafiri tena kwenda Dubai kwa ajili ya matibabu," alisema Hakimu Mashauri.

  Akitoa uamuzi kuhusu Matiko, Hakimu Mashauri amesema nchi yetu inaongozwa na sheria na sheria inamtaka mshitakiwa akikabiliwa na makosa ya jinai pamoja na vyeo vyao bado wanatakiwa kuwepo mahakamani.Amesema maelezo aliyoyatoa mshitakiwa kwanini asifutiwe dhamana hayakidhi matakwa ya yeye kushindwa kuhudhuria mahakamani na wanaleta dharau.

  "Mahakama imeamua kuwa mshitakiwa wa kwanza na wa tano (Mbowe na Matiko), dhamana yao imefutwa," alisema.Baada ya Mahakama kutoa uamuzi huo, Wakili wa utetezi, Peter Kibatala alidai.Hivyo sababu alizotoa Matiko kuwa alihudhuria ziara ya kibunge nchini Burundi si za msingi na hadhikizi matakwa yaye kutofika mahakamani na kuonyesha kuwa hata yeye pia anadharau amri za mahakama.

  Baada ya uamuzi huo wakili Kibatala alitoa taarifa kwa kuieleza mahakama kuwa wataukatia rufaa uamuzi huo Mahakama Kuu na kudai kuwa hawatupo tayari kuendelea na usikilizwaji wa ushahidi wa kesi hiyo kwa leo.Hata hivyo, Wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi aliiomba mahakama kutupilia mbali ombi la wakili Kibatala la kutaka kesi hiyo iharishwe kwa kuwa hoja zilizowasilishwa na wakili Kibatala za kuomba ahirisho zinakosa msingi wa kisheria na hata kiutaratibu.

  Nchimbi alidai kuwa hoja hiyo kimsingi hauna mashiko, na kuhusu kukata rufaa Mahakama imekwishatoa maamuzi kutokana na mwenendo wa Shauri hilo.Kutokana na mabishano makali ya kisheria, shauri hilo limeahirishwa hadi saa saba mchana.

  Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwa chini ya ulinzi baada kufutiwa dhamana kwa kukiuka masharti ya dhamana katika kesi ya uchochezi inayomkabili yeye na viongozi wenzake nane wa Chadema baada ya kesi hiyo kuahirishwa hadi saa saba mchana kwa ajili ya mahakama kutoa uamuzi kama kesi hiyo iendelee katika hatua ya usikilizwaji leo ama la.


  0 0


  0 0

   Ofisa Miradi wa Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association, Saidi Simkonda, akizungumza na wadau wa kilimo ambao ni wanachama wa shirika hilo kuhusu mchakato wa uanzishwaji wa Jukwaa la Wakulima wilayani Kisarawe mkoani Pwani pamoja na kukabidhiwa hati miliki za ardhi. Kushoto kwake ni Diwani wa Kata ya Kurui, Musa Kunikuni.
  `Ofisa Ardhi wa Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association, Ivy Jamson Mwansepe, akitoa taarifa ya shirika hilo wakati wa mkutano huo.
  Ofisa Ardhi wa Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association, Ivy Jamson Mwansepe, akimkabidhi taarifa hiyo Diwani wa Kata ya Kurui, Musa Kunikuni.
   Wadau wakiwa kwenye mkutano huo.
  Viongozi wakiwa  meza kuu wakati wa mkutano huo. Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Nzenga, Mohammed Rubondo, Diwani wa Kata ya Mafizi, Yadhamen Nghonde, Diwani wa Kata ya Kurui, Musa Kunikuni, Ofisa Miradi wa Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association, Saidi Simkonda na Mwenyekiti wa shirika hilo, Isabela Luoga.
   Wadau wa kilimo wakiwa kwenye mkutano huo.
   Ofisa Ugani kutoka Shirika la Yara Tanzania LTD, Maulidi Mkima, akizungumza kwenye mkutano huo.
   Linda Byaba kutoka Kilimo Joint LTD, akizungumza.
   Wadau wa kilimo wakiwa kwenye mkutano huo.
   Shabani Maulidi Mataula, akichangia jambo.
   Diwani wa Kata ya Kurui, Musa Kunikuni, akizungumza kwenye mkutano huo.
   Mkazi wa Kata ya Kurui, Salumu Jaza, akichangia jambo.
   Mkazi wa Kijiji cha Zagero, Fatuma Mindu, akichangia jambo.
   Ofisa Ugani wa Kata ya Marui, Fadhil Mkomeka, akichangia jambo.
   Mdau wa kilimo, Charles Andrea Mattaka, akizungumza katika mkutano huo.
   Diwani wa Kata ya Nzenga, Mohammed Rubondo, akizungumza.
  Diwani wa Kata ya Mafizi, Yadhamen Nghonde, akielezea kuhusu hati miliki za ardhi.

  Na Dotto Mwaibale, Kisarawe

  VIKUNDI vya wakulima 750 vya Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani vinatarajia kukabidhiwa hati miliki za ardhi zitakazoweza kuwasaidia kupata mikopo katika taasisi za fedha.

  Hayo yalibainika wilayani humo juzi katika Kijiji cha Zegero wakati wa mkutano wa mchakato wa kuanzisha jukwaa la wakulima unaoratibiwa na Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association kwa kushirikiana na Ofisi ya mkurugenzi wa halmshauri hiyo.

  Akizungumza katika mkutano huo Ofisa miradi wa shirika hilo, Said Simkonda alisema kati ya vikundi hivyo vitakavyopata hati hizo vikundi 250 ni vya watu wenye ulemavu ambavyo vimepata mashamba kwa ajili ya kufanya kilimo.

  Akizungumzia kuhusu uanzishwaji wa jukwaa la wakulima alisema litakuwa ni chombo cha  kuwakutanisha wakulima wote waliomo wilayani Kisarawe na mikoa ya jirani ili kuleta kilimo chenye tija.

  Alisema mchakato huo umewahusisha wadau wa kilimo kutoka Kata ya Kurui, Mzenga, Mafizi, Vihingo, Marui na Chole na kuwa shirika hilo linaupongeza uongozi wa Halmshauri ya Wilaya ya Kisarawe kwa kulidhia kuupokea mradi huo wa kilimo mnamo mwaka 2016.

  "Tangu tuanze kushirikiana na Halmshauri ya Wilaya ya Kisarawe shirika letu limeweza kuwasaidia wakulima ambao ni wanachama wao 255 na kuwapatia mafunzo ya kilimo na kuwa linatarajia kuendeleza kutoa mafunzo ya kompyuta, scanner, intaneti na kuendesha huduma za ugani kwa wakulima.

  Alisema pamoja na mambo mengine wanatarajia kuanzisha soko la kimataifa la mazao mbalimbali wilayani humo ili mazao yote yanayolimwa wilayani humo yapatikane eneo moja kama lile la Kibaigwa.

  Diwani wa Kata ya Kurui ambaye aliongoza mchakato wa kuanzishwa kwa jukwaa hilo la wakulima, Musa Kunikuni  alisema jukwaa hilo ni muhimu sana kwao kwani litawasaidia kuwaweka pamoja na kuwa hizo hati miliki za ardhi wakizipata zitawasaidia kupata mikopo ya kuendeleza kilimo.

  Diwani wa Kata ya Mafizi, Yadhanen Nghonde alisema ni muhimu hati hizo zikatolewa haraka ili wakulima waliowanachama waweze kujipanga kwa kuomba mikopo itakayowasaidia msimu ujao wa kilimo.

  0 0

  Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

  NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI) Mwita Wairata amewasisitiza wafanyabiashara na wenye Viwanda nchini kulipa kodi ya maendeleo ili Serikali iwe na uwezo wa kufanya miradi ya kimaendeleo ambayo itasaidia wananchi wengi.

  Waitara ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa kuelekea katika kilele cha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo(TCCIA) ambapo amesema ili Serikali iongeze ufanisi katika kuhudumia jamii wafanyabiashara na wawekezaji katika maenneo mbalimbali wanapaswa kulipa kodi ya mapato ambayo pamoja na kusaidia uongezwaji wa miradi ya maendeleo pia itaboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.

  Amesema chama hicho kimekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha uchumi wa Taifa na kuunga mkono juhudi za Seikali ya Awamu ya tano ya Rais Dk.John Magufuli inayosisitiza uchumi wa Viwanda.“Wafanyabiashara lipeni kodi ya maendeleo, Kodi ndio itatufanya kuwawekea mazingira mazuri ya uwezeshaji na hatimaye mfanye biashara zenu kwa ufanisi mkubwa, sisi tutaendelea kuwawezesha kwani chama chenu ni muhimu sana katika kukuza ustawi wa kijamii,"amesema Waitara.

  Kwa upande wake Kaimu Rais TCCIA Octavian Mshiu amsema kwa muda wa miaka 30 Serikali imekuwa ikifanya juhudi za kuhakikisha wawekezaji waliopo katika chama hicho wanaongeza shughuli zao na kusababisha mafanikio makubwa.Amesema katika Serikali ya awamu ya tano kumekuwa na mwitikio mkubwa kwa wanachama wake wa kuanzisha viwanda na kufungua biashara kubwa na hivyo kuiomba Serikali kuzidi kuwashauri kwenye masuala mbalimbali ya kuwekeza ili kufikia uchumi wa kati.

  Pia TCCIA imefungua matawi yake katika Nchi za China na Uturuki ili kupanua shughuli zake na kuwawezesha Wafanyabiashara, Wakulima na wenye viwanda kufanya biashara zao kimataifa zaidi ambapo Mkurugenzi wa Chamber ya China Martin Rajabu amesema wanapata ushirikiano mkubwa katika suala zima la kibiashara na raia wa nchini humo.

  Chama hicho cha Wafanyabiashara, Wakulima na wenye Viwanda kilianzishwa rasmi mwaka 1988 ambapo kwa mwaka huu kinatimiza miaka 30 tangu kuanzishwa kwake na miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana na kuwaunganisha wafanyabiashara kimataifa,kuwajengea uwezo,kukuza mitaji yao na kuwawezesha kuimarisha viwanda,biashara na kilimo.
  Naibu Waziri TAMISEMI Mwita Waitara (wa pili kushoto) akisalimiana na  Mkuu wa Kitengo cha Biashara benki ya KCB Masika Mkulu.Wa kwanza kushoto ni Kaimu Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo Octavian Mshiu.

  0 0


  0 0

   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya Mkutano wa Tano wa Chama Cha Wataalamu wa Figo Tanzania, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar, leo 23/11/2018, na kuhudhuriwa na Wataalamu wa Maradhi ya Figo kutoka Tanzania na Nje ya Tanzania.
   WAZIRI wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed akizungumza wakati wa Mkutano wa Tano wa Wataalamu wa Chama Cha Figo Tanzania, kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika ukumbi wa Karume Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
   MWENYEKITI wa Chama Cha Wataalamu wa Figo Tanzania Dr. Onesmo Kisanga , akizungumza wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa mkutano huo  uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar, na kuwashirikisha Wataalamu wa Maradhi hayo kutoka Tanzania na Nje, uliofunguliwa na Rais wa Zanzibar Dk. Shein
   BAADHI Madaktari Bingwa wa Maradhi ya Figo wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua Mkutano huo, katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar leo 23/11/2018.
   BAADHI ya Washiriki wa Mkutano wa Tano wa Wataalamu wa Chama Cha Figo Tanzania wakifuatilia Mkutano huo wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
   WANAFUNZI wa Chuo Cha Afya Zanzibar wakifuatilia Mkutano huo wa Wataalamu wa Chama Cha Figo Tanzania wakati wa ufunguzi huo uliofanyika  ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar. 
   BAADHI ya Madaktari wa Magonjwa wa Maradhi ya Figo wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa Chama Cha Wataalamu wa Figo Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibae Beach Resort Mazizina Zanzibar leo.
   WAKWANZA  Mshauri  wa Waziri wa Afya Dr. Mohammed Jidawi , Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu,Waziri wa Ujenzi  Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mhe Ali Karume na Naibu Waziri Afya Zanzibar Mhe. Harusi Saidi Suleiman, wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein.
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mtaalam wa Kampuni ya Harsh Pharmaceuticals Limited ya Dar es Salaam,Ndg. Augustino Mbunda, akitowa maelezo ya Mashine ya kusafishia Figo, wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa Chama Cha Wataalamu wa Figo Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Karume Hoteli ya Zanzibar Beach Resout Mazizini Zanzibar kulia Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid na kushoto Mwenyekiti wa  NESOT. Dr. Onesmo Kisanga, wakati akitembelea maonesho hayo.

   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe Balozi Seif Ali Iddi na kulia Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamah Rashid Mohammed, wakimsikiliza Mtaalamu wa Kampuni ya Harsh Pharmaceuticals Limited Ndg. Augustino Mbunda, akitowa maelezo ya Dawa zinazotumika kwa Wagonjwa waradhi ya Figo wakati akitembelea monesho kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa Chama Cha Wataalam wa Figo Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Karume Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar
   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisoma Kijarida cha Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, wakati wa mkutano huo wa Wataalamu wa Chama Cha Figo Tanzania,uliofanyika katika ukumbi wa Karume Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete(JKCI) Profesa Mohammed Janabi,kulia wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano baada ya ufunguzi huo, na kushoto Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed na Dr. Mohammed Jidawi Mshauri wa Waziri Afya Zanzibar.(Picha na Ikulu )

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikata utepe kwenye ufunguzi wa mkutano wa Maafisa Afya wa mikoa nchini, katika ukumbi wa mipango jijini Dodoma Novemba 23, 2018.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimkabidhi funguo ya gari mshindi wa kwanza katika usafi Mkuu wa Wilaya ya Njiombe Ruth Msafiri, kwenye ufunguzi wa mkutano wa Maafisa Afya wa mikoa nchini, katika ukumbi wa mipango jijini Dodoma Novemba 23, 2018.

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimkabidhi kofia na funguo ya pikipiki Kaimu Afisa Afya Halmashauri ya Meru Mkoa wa Arusha Elipokea Nassary kwenye ufunguzi wa mkutano wa Maafisa Afya wa mikoa nchini, jijini Dodoma Novemba 23, 2018.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Mshauri wa maji na usafi wa mazingira kutoka Shirika la Kiholanzi la SNV Saul Mwandosya, wakati akikagua mabanda, kwenye ufunguzi wa mkutano wa Maafisa Afya wa mikoa nchini, jijini Dodoma Novemba 23, 2018.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akioneshwa choo cha gharama nafuu na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati akikagua mabanda, kwenye ufunguzi wa mkutano wa Maafisa Afya wa mikoa nchini, jijini Dodoma Novemba 23, 2018.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza Mratibu wa Mradi wa Usafi wa Mazingira Shirika la Plan International Dodoma Rachel Stephen, kwenye ufunguzi wa mkutano wa Maafisa Afya wa mikoa nchini, katika ukumbi wa mipango jijini Dodoma Novemba 23, 2018, kutoka kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Mohammed Bakari, , Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalim.
  Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, akizungumza na Maafisa Afya wa mikoa nchini, kwenye ufunguzi wa mkutano wa Maafisa Afya wa mikoa nchini, jijini Dodoma Novemba 23, 2018.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Maafisa Afya wa mikoa nchini, wakati alipofungua rasmi mkutano wa maafisa hao kwenye ukumbi wa mipango jijini Dodoma Novemba 23, 2018.


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ikishirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi na Ajira ifanye ukaguzi wa vyoo na mifumo ya kutiririsha maji katika viwanda vyote na vitakavyobainika na makosa hatua kali zichukuliwe. Pia, Waziri Mkuu amewaagiza maafisa afya na mazingira katika mikoa yote nchini badala ya kuzingatia maeneo ya hoteli, mabucha na migahawa waende kwa jamii na kutoa elimu ya matumizi ya vyoo bora pamoja na umuhimu wa usafi wa mazingira, hivyo watakuwa wameiepusha na maradhi.

   Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Novemba 23, 2018) kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Usafi wa Mazingira Kitaifa na Mkutano wa Maafisa Afya wa Mikoa, Halmashauri na Wadau wa Afya Mazingira Tanzania, uliofanyika jijini Dodoma. Amesema viwanda vina jukumu la kuhakikisha vinatunza afya za wafanyakazi wake kwa kufuata taratibu na sheria za afya kazini. “Ni jukumu la kila kiwanda kuhakikisha kwamba kinadhibiti uchafuzi wa hewa ili tuweze kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.”

   Amesema kwamba hivi sasa, madhara ya mabadiliko ya tabianchi yameanza kushuhudiwa  nchini na endapo jitihada za makusudi zisipochukuliwa ipo hatari ya kufifisha matarajio ya kesho na kesho ya watoto. Kufuatia hatua hiyo, Waziri Mkuu ametoa rai kwa wakuu wote wa mikoa, wilaya, wakurugenzi wa halmashauri na maafisa watendaji wa kata, mitaa na vijiji nchini kwamba wasimamie vizuri na kwa ukaribu kampeni ya usafi wa mazingira na matumizi ya choo bora.

  “Hakikisheni kuwa lengo la kila kaya nchini kupata choo bora kabla ya tarehe 31 Desemba, 2018 linafikiwa. Waziri mwenye dhamana, tambua kwamba baada ya tarehe husika kupita nitahitaji kupata taarifa kuhusu utekelezaji wa agizo hilo kutoka kwa kila mkoa na halmashauri nchini.” 

  Waziri Mkuu amesema ameelezwa kwamba, hadi kufikia tarehe 30 Septemba, 2018 kaya zenye vyoo bora zimefikia asilimia 51.4 kutoka asilimia 46.6 Julai, 2017 na katika kipindi hicho kaya zisizokuwa na vyoo kabisa imepungua kutoa asilimia 5.4 hadi asilimia 3.8. 

  Amesema iwapo watazidisha kasi katika utoaji wa elimu, usimamizi wa sheria na kuongeza ufuatiliaji, kaya zote zitakuwa na vyoo bora ndani ya muda mfupi ujao. “Nimedokezwa hapa kwamba, Halmashauri ya Wilaya ya Njombe wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika hilo. Sasa nitashangaa sana kwa nini wengine mshindwe?

  Sambamba na suala hilo la ujenzi na matumizi ya vyoo bora katika kaya, pia Waziri Mkuu amesisitiza uwepo wa huduma za vyoo bora kwa taasisi zote za umma na binafsi. “Ninaagiza shule zote, vituo vyote vya tiba, vituo vya abiria, masoko na nyumba zote za ibada ziwe na miundombinu bora ya vyoo na sehemu za kunawa mikono.” 

  Kadhalika, Waziri Mkuu amewagiza wakurugenzi wa halmashauri wahakikishe maeneo yote hayo yanakuwa na huduma hizo muhimu kabla ya tarehe 30 Aprili, 2019 ili itasaidia sana kuondokana na aibu ya kukosa miundombinu ya usafi katika taasisi zao. 

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameonya jamii dhidi ya tabia ya ya kuchimba dawa wakati wa safari. “Tabia hii imeota mizizi, imekuwa kama ni desturi ya baadhi ya watu licha ya Serikali pamoja na sekta binafsi imeweza kuweka huduma za vyoo kwenye stendi za mabasi, vituo vya kuuzia mafuta, pamoja na hoteli zinazotumiwa na wasafiri.” 

  Amesema haiingii akilini kuona basi la abiria linasimama porini ili watu wajisaidie wakati muda mfupi uliopita basi hilo lilisimama kwenye kituo kikubwa cha abiria au sehemu zinazotoa huduma ya chakula.

  “Katika kudhibiti hali hii ninaagiza Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani, SUMATRA na TABOA kuandaa mikakati ya kuondokana kabisa na tabia hii hatarishi kiafya. “

  Waziri Mkuu amewaagiza maafisa afya mazingira kote nchini watekeleze wajibu wao kwa kuwachukulia hatua za kisheria madereva na makondakta wote watakaobainika kusimamisha magari porini kwa lengo la kuchimba dawa.

  Katika mkutano huo halmashauri ya wilaya ya Njombe imeibuka kidedea kwenye kundi la utekelezaji wa kampeni ya Taifa ya usafi wa mazingira, ambapo imepewa zawadi ya gari aina ya ford ranger lenye thamani ya Dola za Marekani 35,700.

  Mbali na halmashauri hiyo kuibuka mshindi na kupata zawadi ya gari jipya pamoja na tuzo, ndiyo Halmashauri pekee nchini ambayo kaya zake zote zina vyoo bora na kwamba hakuna kabisa tabia ya kujisaidia vichakani. 

  Hivyo, Waziri Mkuu ametoa wito kwa halmashauri nyingine nazo ziige mfano huo wa Njombe. “Ni dhahiri kuwa endapo halmashauri zote zitafikia hadhi ya Njombe tutaokoa fedha nyingi ambazo zinatumika kugharamia matibabu ya wagonjwa pamoja na kuokoa muda mwingi unaohitajika kwenye shughuli za uzalishaji ambao unapotea kila siku kwa kuuguza watu wanaopata magonjwa yanayoenezwa kwa njia ya uchafu.”

  0 0

   Meneja wa PSSSF Zanzibar Issa Sabuni akitoa elimu kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi juu ya faida zinazopatikanwa katika  mfuko huo baada ya kuunganishwa na mifuko mengine na kua  mifuko mmoja wanye kuleta faida kwa  Wafanyakazi Wastaafu.
    Afisa Maendeleo PSSSF Hamza Msangi akitoa Mafunzo kwa Jeshi la Polisi faida zinazopatikanwa katika Mfiko huo katika ghafla iliofanyika katika ukumbi wa Polisi  Ziwani Mjini Unguja.
   Msaidizi Kamishna wa Polisi Zanzibar F C Shilogile  akitoa shukurani kwa Maafisa wa PSSSF kwa kuwapatia Mafunzo Wafanyakazi wake katika ghafla iliofanyika katika ukumbi wa Polisi  Ziwani Mjini Zanzibar,( kulia) ni Meneja wa PSSSF Zanzibar Issa Sabuni.
  Baadhi ya Askari wa jeshi la Polisi waliohudhuria katika Mafunzo hayo yaliofanyika katika  Ukumbi wa Polisi Ziwani Mjini Unguja.

  Picha na Abdalla Omar  Maelezo – Zanzibar.

  0 0


  Mhe. Waziri, mgeni rasmi (aliyeshika kipaza sauti) akiongoza sherehe za Mahafala ya ‘IJA’ Lushoto.
  Waziri wa katiba na Sheria akipewa maelezo ya jinsi mfumo wa Kielektroniki wa Menejimenti ya Mafunzo ‘Training Management Information System (TMIS)’ unavyofanya kazi, Mhe. Waziri alizingua rasmi mfumo huo ambao utakuwa ukitoa taarifa ya Mafunzo mbalimbali na kuwezesha kujua ni Watumishi wangapi wa Mahakama waliopatiwa Mafunzo na ambao hawajapata mafunzo.

  Meza Kuu katika picha ya pamoja na sehemu ya Wahitimu wa Astashahada ya Sheria.

  Meza kuu ikiongozwa na Mhe. Mgeni rasmi (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya Wahitimu wa Stashahada ya Sheria.


  Maandamano kabla ya kuanza rasmi kwa Sherehe za Mahafali zilizofanyika Novemba 23, 2018 katika Ukumbi wa Nyalali uliopo ndani ya eneo la Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto
  Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Jaji, Dkt. Paul Kihwelo akitoa neno katika Mahafali hayo.
  Sehemu ya Wahitimu wa Stashahada ya Sheria, katika Mahafali hayo jumla ya Wahitimu 345 wamehitimu katika ngazi ya Stashahada na Astashahada.
  Sehemu ya Wahitimu wa Astashahada ya Sheria.
  Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Jaji Dkt Gerald Ndika akitoa hotuba yake katika Sherehe za Mahafali ya 18 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.
  Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb), ambaye pia alikuwa Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 18 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto akitoa hotuba.
  Na Ibrahim Mdachi, Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto

  Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb) ameahidi kukisaidia Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kwa kuwa anatambua mchango wake katika utoaji mafunzo ya Sheria nchini.

  Waziri wa Katiba na Sheria ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za Mahafali ya 18 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Novemba 23 alisema kuwa Serikali inatambua mchango wa Chuo hiki katika kutoa mafunzo ya sheria kwa ngazi ya Stashahada na Astashahada na katika kutoa mafunzo endelevu katika fani mbalimbali za sheria.

  “Ninaahidi kutimiza wajibu wangu kwa kutoa msaada pale mtakapohitaji na nitakapoona sina budi nitatoa msaada huo hata kama hamjaleta rasmi hitaji lenu kwangu.” Alisema Prof. Kabudi.Akiendelea kuhutubia hadhara ya Wahitimu, Watumishi wa Chuo na Mahakama Wazazi na Walezi wa wahitimu, Prof. Kabudi aliongeza kuwa wahitimu wa chuo hiki wamekuwa mfano kwa jamii kwa uadilifu na maadili kutokana na malezi wanayopata chini ya usimamizi wa Mahakama ya Tanzania.

  Alipongeza Uongozi wa Chuo kwa jitihada unazozifanya katika kukabiliana na changamoto mbalimbali na namna unavyoweza kuzikabili na kuweza kutekeleza jukumu lake la utoaji wa mafunzo sambamba na utekelezaji wa miradi mbalimbali.Sambamba na hayo aliwaasa na kuwasisitizia Wahitimu na juu ya kujiendeleza katika fani ya Sheria ambayo huhitaji kusoma kwani sheria na kanuni hubadilika kila mara na kujiepusha na vitendo vya rushwa.

  Mhe. Prof Kabudi aliwataka Wahitimu hao kuendelea kusoma vitabu kwa wingi kwani itawasaidia katika utendaji kazi wao wa kila siku.Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Jaji, Prof. Paul Kihwelo alisema kuwa Chuo kimeendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa Watumishi wa Mahakama ili kuwajengea uwezo zaidi.

  “Kwa kutambua umuhimu wake kwa Mahakama ya Tanzania pamoja na kuwajengea uwezo wa utafiti watumishi wake, Chuo kimeendesha mafunzo yaliyowajumuisha Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo na Wajumbe wa Mabaraza ya Kata mkoani Tabora ili kuwajengea uwezo wa namna wanavyopaswa kusikiliza mashauri katika ngazi zao,” alieleza Mkuu huo wa Chuo.

  Naye Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Jaji Dkt. Gerald Ndika alitaja miongoni mwa mafanikio ya Chuo kuwa ni kuboresha utendaji kazi wa Kurugenzi ya Mafunzo Endelevu ya Kimahakama.

  “Nichukue fursa hii tena kwa niaba ya Baraza la Uongozi wa Chuo kutoa shukrani za pekee kwa Mhe. Jaji Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania kwa ushirikiano wanaotoa kwa Uongozi wa Chuo, kutoa kipaumbele kwa shughuli za Chuo hususani kutenga fedha za mafunzo kwa maafisa wa mahakama na wasaidizi wao na kuamua kuwa mafunzo yote ya watumishi wa mahakama yaratibiwe na Chuo,” alieleza Mwenyekiti.

  Aliongeza kuwa katika utoaji wa elimu bora chuoni hapo, Chuo kwa sasa kina jumla ya Wanataaluma (Wahadhiri) Ishirini na Tatu (23) ambao wameendelezwa na kuwezesha Chuo kupata mafanikio ya kitaaluma yaliyotajwa. Miongoni mwa Wanataaluma hao, watano (5) wana Shahada ya Uzamivu na kumi na nane (18) wana Shahada ya Uzamili. Kwa sasa kati ya hao 18 wenye Shahada za Uzamili wawili wanafanya Shahada ya Uzamivu na wapo katika hatua nzuri.

  Katika Mahafali hayo, Mhe. Waziri alizindua Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Chuo hicho, Mfumo wa Kielektroniki wa Menejimenti ya Mafunzo ‘Training Management Information System (TMIS)’ na Klabu ya utunzaji mazingira ijulikanayo kama ‘IJA Green Club’.

  0 0  Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizundua Kongani ya tatu ya Centre Limited (SCL) Sagcot-Kilombelo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Flomi mjini Morogoro tarehe 23 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)

  Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizundua Kongani ya tatu ya Centre Limited (SCL) Sagcot-Kilombelo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Flomi mjini Morogoro tarehe 23 Novemba 2018.

  Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT Ndg Geofrey Kirenga akieleza mwelekeo wa jinsi SAGCOT itakavyoendesha shughuli zake wakati wa uzinduzi wa Kongani ya tatu ya Centre Limited (SCL) Sagcot-Kilombelo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Flomi mjini Morogoro tarehe 23 Novemba 2018.

  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kongani ya tatu ya Centre Limited (SCL) Sagcot-Kilombelo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Flomi mjini Morogoro tarehe 23 Novemba 2018.

  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Kongani ya tatu ya Centre Limited (SCL) Sagcot-Kilombelo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Flomi mjini Morogoro tarehe 23 Novemba 2018.

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Albert Chalamila akitoa ushuhuda toka kongani ya Ihemi na Mbarali wakati wa uzinduzi wa Kongani ya tatu ya Centre Limited (SCL) Sagcot-Kilombelo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Flomi mjini Morogoro tarehe 23 Novemba 2018.


  Muwakilishi wa Benki ya Dunia Bi Emma Isinika Modamba akiwasilisha taarifa fupi toka kwa wadau wa Maendeleo wanaowezesha mpango wa SAGCOT wakati wa uzinduzi wa Kongani ya tatu ya Centre Limited (SCL) Sagcot-Kilombelo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Flomi mjini Morogoro tarehe 23 Novemba 2018.


  Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Morogoro

  Mageuzi ya kilimo nchini Tanzania yanapaswa kutiliwa mkazo na wadau wote wa sekta ya kilimo wakiwemo wananchi, wadau wa maendeleo na serikali kwa ujumla.

  Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo tarehe 23 Novemba 2018 wakati akizundua Kongani ya tatu ya Centre Limited (SCL) Sagcot-Kilombelo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Flomi mjini Morogoro.

  Mhe Hasunga alisema kuwa Sekta ya kilimo imeendelea kuwa uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania kwani imekuwa ikichangia kwa Kiasi kikubwa katika kutoa ajira, kuchangia karibu nusu ya mauzo yote ya nje na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta fedha za kigeni.

  Alisema kuwa Serikali imeendelea kuweka juhudi zake katika kuwezesha sekta ya kilimo kwa kufanya mabadiliko mbalimbali ya kisera yenye lengo la kuweka mazingira wezeshi kwa sekta ya kilimo kukua.Pia serikali imezindua Mpango wa pili wa Maendeleo ya Kilimo (ASDP II) wenye lengo la kuhakikisha sekta ya kilimo inakuwa na inachangia katika maendeleo ya uchumi na kuongeza kipato cha mkulima mdogo.

  Mhe Hasunga amesisitiza kuwa mpango wa SAGCOT ulianza toka mwaka 2010 kwenye mkutano wa Baraza la Uchumi la Dunia kwa Africa (World Economic Forum of Africa WEF-A) uliofanyika Jijini Dar es Salaam ambao utatekelezwa kwa miaka 20 mpaka mwaka 2030.

  Alisema mpango wa SAGCOT umepangwa kutekelezwa kwa awamu katika mgawanyo wa kongani sita. Kongani hizo Ihemi, Mbarali, Kilombero, Rufiji, Ludewa na Rukwa hivyo ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ameitaka SAGCOT kuongeza ufanisi na weledi katika kukamilisha kongani zote sita kama mtazamo ulivyo.

  Naye Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba akizungumza katika hafla hiyo alisema kuwa wizara ya kilimo ina ziada ya kutosha kwenye mazao ya chakula huku akisisitiza kuwa mkakati wa kutafuta masoko unaendelea ili kuwanufaisha wakulima nchini.Alisema nchi ina fursa kubwa kwenye sekta ya kilimo hivyo wananchi wanapaswa kujikita zaidi katika kilimo kwani ndio sehemu pekee yenye uwezo wa kuwanufaisha wananchi wengi kwa wakati mmoja.

  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa alisisitiza kuwa SAGCOT inapaswa kufanya haraka katika kuanzisha kongani ya nne na hatimaye mpaka ya sita ili kuajiri vijana na wananchi wengi.Ameongeza kuwa wataalamu wengi wa kilimo wamenufaika na elimu nchini lakini ajira zimekuwa chache hivyo kuongezwa kwa kongani nyingine ajira zitaongezeka na wananchi wengi watanufaika na kipato kwa ajili ya maendeleo ya kaya na Taifa kwa ujumla wake.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT Ndg Geofrey Kirenga alieleza kuwa malengo ya mpango wa SAGCOT yanakwenda sambamba na Dira ya maendeleo ya Taifa ya 2025, mpango wa maendeleo wa miaka 5, utekelezaji wa mpango wa pili wa maendeleo ya kilimo (ASDP II) na mpango wa uwekezaji kwenye kilimo kwa ajili ya usalama wa chakula na lishe (TAFSIP) ambao unatumika kutekeleza programu kabambe ya maendeleo ya kilimo barani Afrika (CAADP).

  Alitaja lengo kuu la mpango wa SAGCOT kuwa ni kuhakikisha kuwa kilimo katika maeneo ya SAGCOT kinachangia katika kuongeza tija, kuhakikisha kuna usalama wa chakula, kupunguza umaskini, kuhakikisha wakulima wadogo wanatoka kwenye kilimo cha kujikimu na kwenda kwenye kilimo cha kibiashara na kuhakikisha mazingira yanatuzwa kwa maendeleo endelevu ya kilimo.

  0 0

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  HALMASHAURI ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam imefuta kibali cha kufanyika kwa tamasha la Tigo Fiesta ambalo lilitarajiwa kufanyika leo Viwanja vya Leaders.

  Sababu za kufuta kibali cha kufanyika tamasha hilo kwenye viwanja hivyo imetokana na Ofisi ya Ofisa Utamaduni wa Halmashauri hiyo ya Kinondoni kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi na wagonjwa waliolazwa hospitalini kutokana na matangazo yaliyoambatana na muziki unaopigwa kwa sauti kubwa.

  Barua ya Ofisa Utamaduni wa Halmashauri ya Kinondoni ambayo nakala yake imekwenda kwa Mkurugenzi wa Clouds Media imeeleza kuwa kutokana na malalamiko hayo amefuta kibali kilichotolewa Novemba 22 mwaka huu cha kufanyika kwa Fiesta uwanja wa Leaders na kuihamishia uwanjwa Tanganyika Peakers-Kawe.

  Baada ya barua hiyo , uongozi wa Kamati ya maandalizi ya Tigo Fiesta 2018 umesema kwa masikitiko makubwa wanatangaza kusitisha tukio la kilele cha msimu wa Tigo Fiesta lililopaswa kufanyika leo Novemba 24 mwaka 2018 katika viwanja vya Leaders na kwamba sababu zilizotolewa kusitishwa kwa tamasha hilo zipo nje ya uwezo wao.

  "Tunaomba radhi kwa madhara yoyote yatakayosababishwa na hili.Tunaambua fika wapenzi wa Tigo Fiesta Dar es Salaam na nje ya Dar waishajiandaa vema na tukio hili na zaidi walishanunua tiketi.Kwa walionunua tiketi kwenye Tigo pesa watarudishiwa fedha zao na wale ambao walinunua vituo vya mauzo wafike kwenye vituo hivyo watarudishiwa fedha zao.

  "Mioyo yetu imejawa na shukrani,sisi Clouds Media Group ,Prime Time Promotions,Tigo Tanzania,TBL, na Tatu Mzuka tutazidi kuwashukuru Watanzania wote kwa kutuchagua na ahadi yetu ni kuendelea kuwatumikia.Pia tunatoa shukrani kwa Serikali na wadau wote ambao wamejitoa kwa hali na mali kufanikisha shughuli zote za Tigo Fiesta tangu kuanza kwa msimu hadi sasa,"umesema uongozi huo kupitia taarifa yao kwa vyombo vya habari.
   Taarifa kutoka  Afisa Utamaduni Manispaa ya Kinondoni
   Taarifa kutoka kwa Waandaji wa Tamasha la Fiesta.

  0 0

  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewasimamisha kazi watumishi watatu wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya Jiji la Arusha kwa tuhuma ya kushirikiana na matapeli wa viwanja katika jiji hilo.

  Aidha, Lukuvi ameagiza maofisa hao waliosimamishwa kazi kutokanyaga katika eneo la ofisi za Jiji mpaka hapo uchunguzi utakapofanyika na maamuzi dhidi ya tuhuma zao yatakapotolewa.

  Lukuvi alichukua uamuzi huo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Jiji la Arusha jana kufuatia kuwepo tuhuma nyingi za matapeli ya viwanja kushirikiana na baadhi ya maofisa wa ardhi wasiokuwa waaminifu kufanya utapeli kwa wamiliki halali wa viwanja.Maafisa ardhi waliosimamishwa kwa tuhuma hizo za kushirikiana na matapeli kudhulumu viwanja kwa wamiliki halali katika jiji la Arusha ni Elizabeth Mollel, Lassen Mjema na Zawadi Mtafikikolo.

  Mbali na kusimamishwa kazi kwa watumishi, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliagiza maafisa Ardhi wa Jiji la Arusha kuhakikisha matapeli wote wa viwanja wanaoshirikiana na watumishi hao wasipatiwe huduma katika masuala yoyote ya ardhi kufuatia kuonekana kujihusisha na mipango ya utapeli wa viwanja kwa kushirikiana na baadhi ya watumishi wa sekta ya ardhi katika jiji la Arusha.

  Katika ziara yake hiyo ya kushtukiza pamoja na kuelezwa na Afisa Ardhi Mteule wa Jiji la Arusha Dicley Nyato uwepo wa watumishi wawili Lassen na Zawadi huku Elizabeth akiwa katika likizo ya uzazi, watumishi hao walipotea ghafla ofisini bila taarifa mara baada ya kuelezwa wanahitajika kwa waziri na hata pale walipopigiwa simu za mkononi hazikupatikana.

  Kwa mujibu wa Lukuvi, watumishi hao wa sekta ya ardhi katika jiji la Arusha wamekuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na matapeli wa viwanja katika jiji hilo jambo linalotia mashaka utendaji wao wa kazi na kubainisha kuwa maafisa hao wamekuwa na tabia ya kufuatilia kesi zilizopo katika Mabaraza ya Ardhi kwa nia ya kuwasaidia matapeli.

  Kufuatia kadhia hiyo, Lukuvi ameagiza kuanzia sasa hati zote za wito wa Mahakama nchini kusainiwa na Afisa Ardhi Mteule au Msajili wa Hati ama Kamishna Msaidizi wa Ardhi wa Kanda na Mwanasheria wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi lazima afahamishwe uwepo wa kesi husika.

  "Kuanzia sasa summons zote zipokelewe na Maafisa Ardhi Wateule, Makamishna au Wasajili wa Hati wa Kanda na watumishi wengine wasipokee wala kujihusisha" alisema Lukuvi

  Lukuvi alisema matapeli wa viwanja wamekuwa wakifungua kesi katika Mabaraza ya Ardhi dhidi ya wamiliki halali na wakati mwingine matapeli hao hawawafahamu hata wamiliki lengo lao likiwa kuwakatisha tamaa pale kesi inapochukua muda mrefu hasa ikizingatiwa baadhi ya wamiliki hawana uwezo wa kuweka mawakili na hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kupoteza haki zao.

  Alisema, tabia hiyo haiwezi kuvumiliwa na kusisitiza kuwa mtandao wote wa matapeli wa viwanja katika jiji la Arusha ataukomesha kama alivyofanya katika jiji la Dar es Salaam ambalo huko nyuma lilishamiri sana kwa tabia hiyo ili kusaidia haki za wanyonge.

  Kwa upande wake Afisa Ardhi Mteule wa Jiji la Arusha Dicley Nyato alimueleza waziri Lukuvi kuwa wamekuwa wakisumbuliwa sana na matapeli wa viwanja katika jiji hilo na wakati mwingine matapeli hao huwashitaki lengo likiwa kujipatia viwanja kwa njia ya udanganyifu na kuviuza.

  Lukuvi alifanya ziara hiyo ya kushtukiza katika ofisi za jiji Arusha akitokea wilayani Babati mkoa wa Manyara ambako huko aliweza kutoa faraja iliyopotea kwa muda mrefu kwa wananchi wa vijiji vya Singu na Endasago kwa kuamuru kubaki katika maeneo yao kufuatia mgogoro wa muda mrefu wa takriban miaka hamsini kati ya wana kijiji na wamiliki wa mashamba ambao ni kampuni za Agric Tanzania Ltd na Endasago Co Ltd.

  0 0

  *Ammwagia sifa kutokana na utendaji wa kutukuka
  *Asema anaandika historia kuwa Rais mjenga nchi
  *Ahoji Watanzania wanataka nini tena zaidi ya ....

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  WAKATI Watanzania wa kada mbalimbali wakitoa maoni yao kuhusu utendaji kazi wa Rais Dk.John Magufuli ambaye ametimiza miaka mitatu kwenye nafasi hiyo, Spika wa Bunge Job Ndugai ameamua
  kuweka wazi kila kitu kuhusu Rais wetu.

  Spika Ndugai amesisitiza utendaji kazi wa Rais Dk.Magufuli pamoja na timu yake yote ya Serikali ya Awamu ya Tano ni wa mfano usiopatikana kirahisi katika Bara la Afrika.Akizungumza na Michuzi Blog kwenye mahojiano maalumu yaliyofanyika hivi karibuni ofisini kwake Mjini Dodoma,Spika Ndugai amesema Rais Magufuli pamoja na mambo mengi ambayo ameyafanya na kuleta heshima kwa nchi yetu ukweli ni kwamba uzalendo wake ni mkubwa na wa hali ya juu.

  "Uzalendo mkubwa na wa hali ya juu ameounesha kama kiongozi wa nchi.Tuliwahi kupata ahadi na awamu zilizopita na hasa kutokana na zuluma iliyokuwa inafanyika kwenye madini ,lakini Rais wetu Dk.Magufuli yeye aliahidi kupitiwa upya kwa mikakata ya madini na kweli yote imefumuliwa na imeshonwa upya."Na hili eneo la madini lilikuwa eneo gumu ambalo haligusiki lakini yeye ameweza.Ameonesha uzalendo wa hali ya juu katika kuhakikisha rasilimali za nchi yetu zinanufaisha Watanzania wote,"amesema Spika

  Ndugai wakati anazungumzia utendaji kazi wa Rais Magufuli katika kipindi cha miaka mitatu.Pia jambo moja ambalo Watanzania walikuwa wakililia sana kabla ya uchaguzi mkuu ambao umemuweka madarakani Rais Magufuli ni ilikuwa kupata kiongozi mwenye maamuzi."Tumepata Rais mwenye maamuzi, aidha unapenda au hupendi hiyo shauri yako lakini yeye ameshaamua.

  "Rais Magufuli ni kiongozi mwenye maamuzi.Ni kiongozi anayeamua kwa wakati na tunakumbuka huko nyuma kuna mambo yalikuwa yamenyooka na yanahitaji maamuzi kwa ngazi mbalimbali lakini hayakutolewa maamuzi.Sasa hilo limebaki historia,"amesema.Spika Ndugai amefafanua zaidi kuwa Rais Magufuli anapambana rushwa na ufisadi moja kwa moja."Katika hilo tunashuhudia hata baadhi ya viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) wakibadilishwa kwa kushindwa kwenda na kasi yake kulingana na taarifa alizonazo,"amesema.

  Amesisitiza pamoja na yote hayo kubwa ambali kwake Spika anaweza kulizungumzia kuhusu miaka mitatu ya Rais Magufuli ni kwamba "Rais huyu anaweka rekodi ya kuwa Rais mjenga nchi.Yeyey anapenda kujenga nchi hata alipokuwa Waziri wa Ujenzi na mpaka sasa hivi. "Utaona miradi mikubwa ya ujenzi wa nchi ambayo Watanzania tulikuwa hatuwezi kuamini kama itafanyiwa kazi leo inawezekana.Kwa mfano haikuwa rahisi kuamini kama tunaweza kujenga reli ya mwendo kasi kwa spidi hii tunayoiona sasa.Makandarasi wako saiti kati ya Dar es Salaam na Morogoro pamoja na Morogoro -Dodoma.Matarajio yetu baada ya hapo ujenzi utaendelea Mwanza kama mpango ulivyo,"amesema Spika Ndugai.

  Amesema nani angeamiani ndani ya miaka mitatu tu Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL) lingekuwa linashurusha ndege zake ndani ya nchi yetu na nchi jirani."Kwanza tulishajikatia tamaa lakini amelifufua shirika hilo na hili si jambo dogo kwani linahitaji moyo mkubwa na wa uzalendo." Ujenzi wa bwawa la Stigles George, hili hata awamu ya kwanza ya Mwalim Nyerere walijaribu lakini wakaachia njiani.Rais wetu Dk.Magufuli ametushawishi Bunge na sisi tukatenga fedha zetu za ndani kwa ajili ya kuanza ujenzi wa bwawa hili ambalo litatupatia umeme wa kutosha,"amesema Spika Ndugai.

  Ameongeza kuwa kuna mifano mingi ya miradi ya ujenzi wa nchi ambayo inaendelea maeneo mbalimbali huku akiutolea mfano mradi wa ujenzi wa mji mkuu wa makao makuu ya Serikali Dodoma na kwamba Rais anatarajia kuhamia Dodoma Desemba mwaka huu."Jambo kama hili lilishindikana kwa zaidi ya miaka 40 lakini yeye leo anafanya na ujenzi wa mji wa Dodoma unaendelea.Ndio maana nasema ataingia kwenye historia kama Rais mjega nchi.Tunataka nini Watanzania zaidi ya kumuunga mkono Rais wetu katika kujenga nchi tena kwa fedha zetu za ndani,"amesema Spika Ndugai.

  0 0  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph akiwasisitiza Wataalam wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kukamilisha ujenzi wa ofisi kwa wakati katika Mji wa Serikali ili iweze kutumika kuwahudumia wananchi.
  002
  Afisa Ugavi Mwandamizi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Deograsius Michael (kulia) akikabidhi hati ya makabidhiano ya kiwanja kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Dodoma, Mhandisi David H. Shunu (kushoto) kwa lengo la kuanza ujenzi wa Ofisi katika Mji wa Serikali. Anayeshuhudia ni Afisa Ugavi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Benard Makanda.
  003
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph (wa pili kushoto) akizungumza na Wataalam  wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mara baada ya kukabidhi kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi katika Mji wa Serikali uliopo Ihumwa jijini Dodoma.
  004
  Kaimu Mkurugezi wa Huduma za Ushauri wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Dodoma, akiahidi kutimiza jukumu lake ili kuhakikisha ujenzi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora unakamilika kwa wakati katika Mji wa Serikali uliopo Ihumwa jijini Dodoma.
  005
  Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi na Ugavi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Peter Mabale akisisitiza jambo kwa TBA ili kuhakikisha ujenzi wa ofisi katika Mji wa Serikali jijini Dodoma unakamilika kwa wakati.
   

  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imekabidhi kiwanja kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ili wakala hiyo ianze ujenzi wa Ofisi katika Mji wa Serikali jijini Dodoma.

  Akikabidhi kiwanja hicho kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Musa Joseph amesema ujenzi wa Ofisi hiyo ni muendelezo wa utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais, Dkt John Pombe Magufuli ya kuhamishia shughuli za Serikali Makao Makuu ya nchi Dodoma.

  Bw. Joseph amefafanua kuwa, kiwanja kilichokabidhiwa kina ukubwa wa ekari 5.7 na kuwataka TBA kuanza ujenzi mara moja ili kuwawezesha watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuwahudumia wananchi wakiwa katika mji wa Serikali.

  Bw. Joseph ameongeza kuwa, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora tayari imeshaingiza fedha kwenye Akaunti ya Wakala wa Majengo Tanzania kiasi cha shilingi 700, 000,000/=  ili kuiwezesha TBA kuanza ujenzi na kuongeza kuwa nia ya kufanya malipo mapema ni kuwezesha ukamilishaji wa ujenzi kwa wakati.

  Akipokea kiwanja hicho, Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania mkoani Dodoma, Mhandisi David H. Shunu ameishukuru Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kuiamini TBA na kuahidi kukamilisha ujenzi wa ofisi hizo kwa wakati na kwa kiwango bora.

  Naye, Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi na Ugavi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Peter Mabale ameitaka TBA kufanya mawasiliano haraka iwezekanavyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pindi kunapotokea changamoto yoyote itakayokwamisha shughuli ya ujenzi badala ya kusubiri vikao ili kutatua changamoto hizo.

  Makabidhiano ya Kiwanja hicho yamefanyika baada ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania, Arch. Elius Mwakalinga kusaini mkataba wa ujenzi wa Ofisi hizo Novemba 22, 2018 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli la kuhamishia Shughuli za Serikali makao makuu ya nchi Dodoma.

  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imekabidhi kiwanja kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ili wakala hiyo ianze ujenzi wa Ofisi katika Mji wa Serikali jijini Dodoma.

  Akikabidhi kiwanja hicho kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Musa Joseph amesema ujenzi wa Ofisi hiyo ni muendelezo wa utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais, Dkt John Pombe Magufuli ya kuhamishia shughuli za Serikali Makao Makuu ya nchi Dodoma.

  Bw. Joseph amefafanua kuwa, kiwanja kilichokabidhiwa kina ukubwa wa ekari 5.7 na kuwataka TBA kuanza ujenzi mara moja ili kuwawezesha watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuwahudumia wananchi wakiwa katika mji wa Serikali.

  Bw. Joseph ameongeza kuwa, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora tayari imeshaingiza fedha kwenye Akaunti ya Wakala wa Majengo Tanzania kiasi cha shilingi 700, 000,000/=  ili kuiwezesha TBA kuanza ujenzi na kuongeza kuwa nia ya kufanya malipo mapema ni kuwezesha ukamilishaji wa ujenzi kwa wakati.

  Akipokea kiwanja hicho, Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania mkoani Dodoma, Mhandisi David H. Shunu ameishukuru Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kuiamini TBA na kuahidi kukamilisha ujenzi wa ofisi hizo kwa wakati na kwa kiwango bora.

  Naye, Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi na Ugavi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Peter Mabale ameitaka TBA kufanya mawasiliano haraka iwezekanavyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pindi kunapotokea changamoto yoyote itakayokwamisha shughuli ya ujenzi badala ya kusubiri vikao ili kutatua changamoto hizo.

  Makabidhiano ya Kiwanja hicho yamefanyika baada ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania, Arch. Elius Mwakalinga kusaini mkataba wa ujenzi wa Ofisi hizo Novemba 22, 2018 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli la kuhamishia Shughuli za Serikali makao makuu ya nchi Dodoma.

older | 1 | .... | 1731 | 1732 | (Page 1733) | 1734 | 1735 | .... | 1897 | newer