Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

MWAUWASA WAPIGWA MSASA NA JUMUIYA YA KIMATAIFA YA MAJI

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga (kulia) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uandaaji wa Mpango wa Usalama wa Maji yanayotolewa kwa wafanyakazi wa MWAUWASA na Jumuiya ya Kimataifa ya Maji (IWA).
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa Mpango wa Usalama wa Maji yanayotolewa na Jumuiya ya Kimataifa ya Maji (IWA) wakimsikiliza Mhandisi Anthony Sanga (hayupo pichani). Wa pili kulia ni Mkufunzi kutoka IWA, Kizito Masinde.
Washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa Mpango wa Usalama wa Maji yanayotolewa na Jumuiya ya Kimataifa ya Maji (IWA) wakifuatilia mafunzo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa Mpango wa Usalama wa Maji yanayotolewa na Jumuiya ya Kimataifa ya Maji (IWA) wakimsikiliza Mkufunzi Kizito Masinde (hayupo pichani).
Washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa Mpango wa Usalama wa Maji yanayotolewa na Jumuiya ya Kimataifa ya Maji (IWA) katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Anthony Sanga (mbele katikati) mara baada ya ufunguzi wa mafunzo.


Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA) wametakiwa kuzingatia Mpango wa Usalama wa Maji kila wanapotekeleza shughuli zao ili kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama kwa ubora unaotakiwa.

Wito huo umetolewa Novemba 12, 2018 na Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uandaaji wa Mpango wa Usalama wa Maji yanayotolewa kwa wafanyakazi wa MWAUWASA na Jumuiya ya Kimataifa ya Maji (IWA). Mhandisi Sanga alisisitiza umakini kwenye usimamizi wa mnyororo mzima wa utoaji huduma ya maji kuanzia kwenye chanzo, uzalishaji hadi yanapomfikia mtumiaji ambapo alisema ni wajibu wa kila mtumishi kuhakikisha maji yanayozalishwa yana ubora unaokubalika Kitaifa na Kimataifa.

Aliongeza kuwa suala la usalama wa maji ni nyeti na linapaswa kupewa kipaumbele cha kipekee na kila mtumishi ili kutimiza wajibu wa kuwapatia wananchi huduma wanayostahili kupata. “Watumishi mliopata nafasi ya kuhudhuria mafunzo haya, mkitoka hapa hakikisheni mnawaelimisha na wale ambao hawakufanikiwa kushiriki,” alisema Mhandisi Sanga.

Aliwataka waliohudhuria mafunzo hayo kuuliza maswali na kufuatilia kwa umakini ili mara baada ya mafunzo hayo waboreshe Mpango wa Usalama wa Maji uliopo. Mafunzo hayo ya siku Tano yameanza Tarehe 12 na yatamalizika Tarehe 16 Novemba, 2018 lengo likiwa ni kuwawezesha wataalam wa Mamlaka kuhakikisha ubora wa maji wanayosambaza kwa wananchi kuanzia mahala yanapozalishwa hadi yanapofika kwa mtumiaji.

Kwa mujibu wa Mkufunzi kutoka IWA, Bwana Kizito Masinde alisema MWAUWASA ndiyo Mamlaka pekee miongoni mwa Mamlaka za Maji Nchini ambayo imepewa kipaumbele cha mafunzo hayo. Kizito aliongeza kwamba matarajio ya IWA ni kuona wataalam wa MWAUWASA wakitoa mafunzo ya namna hiyo kwa Mamlaka zingine kote nchini.

UPATIKANAJI WA DAWA MKOANI MTWARA NI ASILIMIA 97

$
0
0
Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Florida Sianga (kushoto), akiwaelekeza Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Naliendele iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani Abdallah Njee (katikati) pamoja na Mtunza Dawa wa Zahanati hiyo, Pili Makota (kulia), jana, mfumo maalum wa kieletroniki unaojulikana kama“MSD-Customer Portal” unaweza kutumika na wateja wake popote walipo nchini jinsi ya kuagiza dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na bei zake, taarifa za akaunti zao na taratibu za maombi ya bidhaa wanazo hitaji kutoka MSD. Wa pili kutoka kushoto ni Afisa Huduma kwa Wateja wa MSD Mkoa wa Mtwara, Larisa Manyahi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Jully Maleko akizungumzia upatikanaji wa dawa katika mkoa huo.
Mganga Mkuu wa Halmshauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani, Joseph Kisala, akizungumzia upatikanaji wa dawa katika halmashauri hiyo.
Jengo la Halmshauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Jengo la Zahanati ya Kijiji cha Rwelu
Muuguzi Msaidizi wa Zahanati ya Kijiji cha Rwelu, Shadida Rashidi (katikati), akimuonesha moja ya kopo lenye dawa Afisa Huduma kwa Wateja wa MSD, Florida Sianga. Kulia ni Mfamasia wa Hospitali ya Mkoa ya Ligula Mtwara, Boniface Magige.
Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kijiji cha Rwelu, Edwin Manyama akizungumzia upatikaji wa dawa.
Mkazi wa Kijiji cha Rwelu, Lukia Matipa (kushoto), akizungumzia jinsi anavyopata dawa anapokwenda kutibiwa katika Zahanati ya Rwelu.
Mjumbe wa Kamati ya Afya wa Kijiji cha Rwelu, Salum Chimbiaka, akizungumzia upatikanaji wa dawa katika zahanati hiyo.
Mtunza Dawa katika Zahanati ya Naliendele, Pili Makota akielezea namna wanavyo nunua dawa kutoka MSD. Kushoto ni Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Abdallah Njee.
Mkazi wa Kijiji cha Naliendele,Hamisi Chikambu akizungumzia upatikanaji wa dawa katika zahanati ya kijiji chao. Kushoto ni mtoto wake Kauthari aliyempeleka kutibiwa kwenye zahanati hiyo.
Afisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Florida Sianga (kulia), akimuelekeza, Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Likombe, Nuru Namkuna, mfumo maalum wa kieletroniki/kidigitali unaojulikana kama“MSD-Customer Portal” unaweza kutumika na wateja wake popote walipo nchini jinsi ya kuagiza dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na bei zake.
Mkazi wa Mtwara mjini, Furaha Masanja akizungumzia huduma nzuri alizopata wakati alipofikishwa kujifungua katika Kituo cha Afya cha Likombe.





Na Dotto Mwaibale, Mtwara

IMEELEZWA kuwa upatikanaji wa dawa vifaa tiba na vitendanishi vya maabara mkoani Mtwara ni asilimia 97 ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo ilikuwa chini ya asilimia 40.

Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Jully Maleko, wakati akizungumza na waandishi wa habari na maofisa wa Bohari ya Dawa (MSD) ambao wapo mkoani humo kuwatembea wateja wao na kujua changamoto walizonazo ili kuzifanyia maboresho.

"Hivi sasa hali ya upatikaji wa dawa katika mkoa wetu ni nzuri tumefikia asilimia 97 ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo tulikuwa chini ya asilimia 40" alisema

Mfamasia wa Hospitali ya Mkoa ya Mtwara Ligula, Boniface Magige alisema changamoto kubwa waliyonayo ni ukusanyaji wa fedha vituoni baada ya kupelekewa dawa pamoja na kada ya wafamasia kuwa wachache.

Katika hatua nyingine MSD imetambulisha mfumo wa upatikanaji wa taarifa muhimu kwa wateja wake, ambazo ni pamoja na taarifa za upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na bei zake, taarifa za akaunti zao na taratibu za maombi ya bidhaa wanazo hitaji kutoka MSD.

Taarifa hizo zinapatikana kwenye mfumo maalum wa kieletroniki unaojulikana kama“MSD-Customer Portal” unaweza kutumika na wateja wake popote walipo nchini na kuwaondolea usumbufu waliokuwa wakiupata awali wakati wakuagiza dawa, ambapo ili walazimu kusafiri ofisi za Kanda ya MSD inayowahudumia au kupiga simu ili kupata taarifa hizo na nyinginezo.

Akizungumzia mfumo huo Afisa Huduma kwa Wateja wa MSD, Florida Sianga alisema kupitia mfumo huu, MSD imedhamiria kuongeza ufanisi katika kuhudumia vituo vya kutolea hudumaza afya nchini ili kuhakikisha adhma ya serikali ya awamu ya tano ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi inatimizwa kwa vitendo.

“Mfumo huu unalenga kurahisisha na kuharakisha upatikanaji wataarifa muhimu zihusuzo dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara vinavyotolewa na MSD kwa vituo vya kutolea huduma za afyanchini, kwa kuviwezesha vituo hivi kupata taarifa muhimu zihusuzo dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa wakati popote walipo nchini hata kupitia simu zao za mkononi” alisema, Sianga.

Aliongeza kuwa mfumo huu, utawawezesha wateja wa MSD kupata taarifa za upatikanaji wa dawa ghalani (stock status) iliiwerahisi kwao kuagiza mahitajiyao MSD kulingana na matakwayaokwawakatihusikahata pale wanapokuwa na mahitajiya dharura.

“Mfumo huu utawasaidia wateja wa MSD kupata taratibu za maombi ya dawa (order processing status) kutoka Makao Makuu, Ofisi za Kanda, Vituo vya mauzo vya MSD,jambo ambalo litawaondolea usumbufu wa kusafiri kupata maelekezo, kwa kuwa mfumo huu unataarifa zote muhimu juu ya namna ya kupata mahitaji yao kutoka MSD” alisema.

Sianga aliongeza kuwa watejawa MSD wataweza kufahamu bei ya dawa (item price) mbalimbali zinazopatikana kwa wakati husika katika maghala ya MSD, kwani taarifa hizi ni muhimu kwao wakati wakupanga bajeti zao za manunuzi, na kufanya nakisi ya kiasi gani kitumike kununulia dawa husika.

Pamoja na hayo, alidokeza kuwa mfumo huo utawawezesha wateja wa MSD kupata taarifa za miamala yao (customer statement) ili wafahamu kiasi cha pesa kilichopo kwenye akaunti zao MSD na kiasi cha fedha kilichotumika kununulia dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na kwa wakati gani ambapo kupitia mfumo huo utakuwa unaondoa sintofahamu zilizokuwa zikijitokeza kipindi cha nyuma,kwa kuwa mfumo huu ni wa wazi na rahisi kutumia.

Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Afya ya kijiji cha Rwelu, Salum Chimbiaka alisema hivi sasa kila wanapokwenda kutibiwa dawa zimekuwa zikipatikana tofauti na zamani hivyo wanaishukuru serikali kwa kuwaondolea wananchi changamoto hiyo.

"Hivi sasa katika zahanati zetu wananchi wanaokwenda kutibiwa wamekuwa wengi kutokana na huduma nzuri wanayopata ukilinganisha na miaka ya nyumba ambapo walikuwa wakikimbilia kwenye zahanati za watu binafsi" alisema Chimbiaka.

Katika siku ya kwanza ya ziara hiyo mkoani humo maofisa hao wa MSD walitembelea Zahanati ya Rwelu, Naliendele na Kituo cha Afya Likombe.

MAGAZETI LEO JUMANNE NOVEMBA 13,2018

TIMU YA WIZARA YA KILIMO YATUA LINDI NA MTWARA KUANZA NA KOROSHO, WAZIRI HASUNGA AONGOZA MSAFARA

$
0
0
Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo, Mtwara

Ikiwa ni siku moja tu mara baada ya kuapishwa kuongoza wizara ya kilimo katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam Jana Jumatatu Novemba 12, 2018, Waziri wa kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Mb) Leo Tarehe 13 Novemba 2018 ameongoza viongozi wakuu wa Wizara yake kutembelea katika Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kwa ajili ya kuhakiki Korosho zilizopo katika maghala makuu.

Katika msafara huo Waziri Hasunga atatembelea Mkoani Mtwara ambapo ameambatana na Naibu Waziri wa kilimo Mhe Innocent Lugha Bashungwa na Katibu Mkuu Mhandisi Mathew Mtigumwe watakaotembelea Mkoa wa Lindi, na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Prof Siza Tumbo atakayetembelea Mkoa wa Ruvuma.

Katika ziara hiyo viongozi hao wakuu watahakiki usimamizi wa maghala ambao kwa sasa unasimamiwa naBodi ya usimamizi wa stakabadhi ya ghala na Usimamizi wa ziada wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko.

Vilevile watahakiki taarifa za Ubora wa maghala kama zilivyopitishwa na Bodi ya usimamizi wa Stakabadhi ya ghala (Warehouse Receipt Regulatory Board-WRRB) pamoja na Ubora wa ghala.Watahakiki uwezo wa maghala na kiasi kilichopo ghalani, na kuhakikisha taarifa ya umiliki wa Korosho zilizopo kwenye ghala.

Aidha, viongozi hao watahakiki kiasi cha Korosho kwenye ghala kwa kupitia nyaraka za mapokezi ya Korosho kwenye ghala ambazo zinawasilishwa na Vyama vya msingi (AMCOS) na kuoanisha taarifa hizo na taarifa zilizomo kwenye taarifa za stakabadhi ya ghala (Warehouse Report).

Katika ziara hiyo timu ya viongozi wakuu kutoka wizara ya kilimo wataambatana pia na Ofisini za Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Bodi ya Mazao Mchanganyiko, Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI)-Naliendele, na Bodi ya usimamizi wa Stakabadhi ya ghala (WRRB).
Waziri wa kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Mb) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe Evod Mmanda leo Novemba 13, 2018 mara baada ya kuwasili Mkoani humo kwa ziara ya kikazi kwa ajili ya kuhakiki Korosho zilizopo katika maghala makuu kabla ya kuanza ununuzi. (Picha Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)
Waziri wa kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Mb) akijadili jambo na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Byakanwa leo Novemba 13, 2018, mara baada ya kuwasili Mkoani humo kwa ziara ya kikazi kwa ajili ya kuhakiki Korosho zilizopo katika maghala makuu kabla ya kuanza ununuzi.
Naibu waziri wa kilimo Mhe Innocent Lugha Bashungwa (Mb) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi kwa ajili ya kuhakikisha Korosho zilizopo katika maghala makuu kabla ya kuanza ununuzi. Mwingine pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe Evod Mmanda, leo Novemba 13, 2018.
Kulia ni katibu Mkuu wa wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe na Naibu Katibu Mkuu wizara ya kilimo Prof Siza Tumbo walipowasili Mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi kwa ajili ya kuhakikisha Korosho zilizopo katika maghala makuu kabla ya kuanza ununuzi leo Novemba 13, 2018.

MBIO ZA NAMTUMBO SELOUS MARATHON ZAFANA, DC KIZIGA ATOA NENO LA SHUKRANI KWA WATANZANIA ,WANARIADHA

$
0
0
Na Ripota Wetu ,Globu ya jamii 

WILAYA ya Namtumbo mkoani Ruvuma imefanya Mbio za Namtumbo maarufu kama Namtumbo Selous Marathon ambapo wanariadha mbalimbali akiwamo Godefrey Masaki wa JKT Arusha walishiriki. 

Katika mbio hizo Masaki alishinda kwa kushika nafasi ya kwanza baada ya kushinda mbio za kilometa 21 huku akimuacha Mohemed Dule kutoka kikosi cha KG Songea aliyesgika nafasi ya pili wakati nafasi ya tatu ikishikiliwa na Ostin Kinyunyu kutoka mkoani Njombe.

Pia kwa upande wa wanawake katika mbio hizo Magdalena Crispin kutoka Arusha ameibuka mshindi wa kwanza wa mbio za Kilometa 21 huku mkimbiaji machachari Fabiola John kutoka Jeshi la Polisi Dar es Salaam akiibuka mshindi wa pili na kumwacha Adelina Irasias kutoka Dar es Salaam akishikilia nafasi ya tatu. 

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mbio hizo Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Sophia Mfaume Kizigo aliyeshiriki mbio za kilometa 2.5 akivalia nambari 021 amewashukuru Watanzania hasa wanariadha walioshiriki mbio hizo kwa kujitokeza kwao kushiriki na kuhamasisha malengo ya mbio 

“Nashukuru Mungu kuwa miongoni mwa walioshiriki mbio hizi na kumaliza kilometa mbili na nusu.Nawashukuru sana washiriki na Watanzania wote kwa kuja kutuunga mkono katika safari yetu ya kujenga maendeleo ya sekta ya afya,” amesema Kiziga. Pia amepongeza jitihada za wadhamini wa mbio hizo Mantra Tanzania na Uranium One kwa ushirikiano mzuri wanaouonesha kwa wana namtumbo na watanzania kwa ujumla. 

Kwa upande wake Katibu wa Afya Wilaya ya Namtumbo Yusuph Mwaipalu amesema sekta ya afya nchini na kote duniani na moja kati ya viungo muhimu sana katika ujenzi maendeleo ya kiuchumi katika jamii yoyote hivyo kuwaasa wana namtumbo na watanzania kwa ujumla kujenga tabia ya kujali afya zao kwanza ili kutengeneza taifa imara na yenye kujihami hapo baadae. 

“Kwa niaba ya wana namtumbo na watanzania wote napenda kuwapongeza sana washiriki kwa kujitokeza kwa wingi lakini pia nawapongeza sekta zote husika kwa kujitokeza kushiriki katika harakati hizi ambazo lengo lake kubwa ni kuleta maendeleo .chanya katika nchi yetu” alisema katibu huku akiwataka watanzani kujali mazoezi ya miili yao kama tiba ya kwanza. 

Amesema mbio hizo zimeshuhudiwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali pamoja na wageni wengine kutoka Urusi na mataifa mbalimbali duniani.
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo akimvalisha medali ya dhahabu mshindi wa kwanza KM21 wa Namtumbo Marathon Godfrey John Masaki kutoka JKT Arusha,wemgine ni washindi wa pili na wa tatu
mkuu wa wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza KM21 wa Namtumbo Marathon Godfrey John Masaki kutoka JKT Arusha,  wengine ni washindi wa pili na wa tatu ambao pia walijinyakulia zawadi ya Fedha, Simu ya kisasa pamoja na medali.

Mshindi wa kwanza wa kike KM21 Magdalena Crispin (katikati) baada ya kukabidhiwa zawadi ya ushindi na Andrei Shutov(kulia) mwakilishi kutoka Uranium One Urusi, wa pili kutoka kulia ni mshindi wa pili Fabiola John na wa kwanza kushoto ni mshindi wa tatu Adelina Irasias. 

Picha ya baadhi ya Wanariadha mbalimbali walioshiriki Namtumbo Marathon.

WAZIRI KAMWELWE KUFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA WADAU WA BARABARA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, anatarajiwa kufungua mkutano wa kimataifa kuhusu mapinduzi ya sekta ya usafirishaji na mabadiliko ya kiuchumi katika nchi zinazoendelea, jijini Arusha. 

Mkutano huo wa siku mbili (2) ulioandaliwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kushirikiana na Shirikisho la Barabara Duniani (World Road Association-PIARC), utafanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC. 

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Joseph Nyamhanga, amesema maandalizi kwa ajili ya mkutano huo yamekamilika ambapo takribani washiriki zaidi ya 200 kutoka nchi 25 duniani watashiriki mkutano huo. 

Mkutano huo ambao lengo lake kuu ni kuangalia matokeo ya uwekekezaji katika mundombinu ya usafirishaji utajadili kwa kina mada mbalimbali zinazohusu changamoto zinazozikabili nchi zinazoendelea ikiwemo rasilimali chache za kuimarisha miundimbinu ya usafirishaji wakati huohuo kuboresha huduma nyingine za kijamii kama vile maji, afya, elimu na nishati. 

"Tutajadili namna ya kuimarisha miundombinu ya kisasa ya usafiri na usafirishaji inayoendana na teknolojia inayopatikana katika nchi zinazoendelea", amesisitiza Mhandisi Nyamhanga. 

Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Barabara Tanzania (TARA), Bw. Joseph Haule, ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo amezitaja nchi zitazoshiriki kuwa ni Bangladesh, Botswana, Canada, Jamhuri ya Czech, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ethiopia, Ufaransa, Ujerumani, Ghana na Japan. 

Nyingine ni Kenya, Liberia, Madagaska, Msumbiji, Nepal, New Zealand, Nigeria, Rwanda, Seirra Leone, Afrika Kusini, Korea kusini, Sudan Kusini, Sri Lanka, Uturuki,Uganda, Uingereza na mwenyeji Tanzania. Kwa upande wake, Katibu mkuu wa PIARC. Bw. Patrick Mallejacq, amesema kufanyika kwa mkutano huo Tanzania kutafungua fursa za kiuchumi, kijamii na kiteknolojia katika ukanda wa Afrika Mashariki. 

Tanzania ilijiunga na PIARC mwaka 1992 na mwaka huu TARA imekubaliwa kuwa kamati ya kitaifa ya PIARC katika mkutano uliofanyika Yokohama nchini Japani mwishoni mwa mwezi Oktoba, 2018. 

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, akisisitiza jambo kwa wadau wa Mkutano wa Kimataifa wa Shirikisho la Barabara Duniani (PIARC), hawapo pichani, Mkutano huo unaanza kesho mjini Arusha.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Barabara Duniani (PIARC), Bw. Patrick Mallejacq, akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama cha Barabara Tanzania (TARA) Bw. Joseph Haule, hati ya makubaliano baada ya TARA kukubaliwa kuwa mwakilishi wa PIARC nchini Tanzania, katikati ni Katibu Mkuu wa Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Joseph Nyamhanga, akishuhudia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Shirikisho la Barabara Duniani (PIARC) utakaoanza kesho katika ukumbi wa AICC, mjini Arusha.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Barabara Duniani (PIARC), Bw. Patrick Mallejacq (kulia), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu Mkutano wa Kimataifa wa Shirikisho la Barabara Duniani (PIARC), unaoanza kesho mjini Arusha. Katikati ni Katibu Mkuu wa Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Joseph Nyamhanga na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Barabara Tanzania (TARA) Bw. Joseph Haule.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Dkt. Ndumbaro Ajibu Maswali Bungeni

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akijibu maswali Bungeni kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb).

Dkt. Ndumbaro alianza kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Dkt. Ndumbaro akijibu swali kuhusu sababu zinazofanya hadi sasa Tanzania kutoridhia Mkataba wa Afrika kuhusu Demokrasia, Chaguzi na Utawala Bora uliopitishwa mwaka 2017.Mhe. Naibu Waziri alieleza kuwa Tanzania inachelewa kuridhia kutokana na baadhi ya ibara za mkataba huo kukinzana na Katiba na Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Salma Kikwete akiuliza swali la nyongeza kwa Naibu Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani). 
Dkt. Ndumbaro akiendelea kujibu maswali mbalmbali ya nyongeza yaliyokuwa yakiulizwa na Waheshimiwa Wabunge. 
Mkutano wa Bunge ukiendelea 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga akimpongeza Naibu Waziri, Mhe. Damas Ndumbaro mara baada ya kumaliza kujibu Maswali Bungeni. 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi akimpongeza Dkt. Ndumbaro mara baada ya kumaliza kujibu maswali.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA WAGENI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mfanyabiashara Rostam Aziz Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mfanyabiashara Rostam Aziz Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mfanyabiashara Rostam Aziz mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mfanyabiashara Rostam Aziz mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa TCD ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia aliyefika Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Mazungumzo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Mwenyekiti wa TCD ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia kabla ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa TCD ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwanasiasa mkongwe John Shibuda ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mwanasiasa Mkongwe wa Chama cha UDP John Cheyo Ikulu jijini Dar es Salam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwanasiasa Mkongwe wa Chama cha UDP John Cheyo Ikulu jijini Dar es Salam.

WAZIRI MKUU ASIKITISHWA WIZI KWENYE MRADI WA NSSF DEGE

$
0
0
*Aagiza wakurugenzi wakuu wa NSSF, AZIMIO, Kamishna TRA wakutane

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa nyumba unaojengwa kwa ubia kati Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kampuni ya Azimio Housing Estate Limited katika eneo la Dege Beach Kigamboni na kutamka kuwa amesikitishwa na uharibifu wa mali na wizi unaendelea kwenye eneo hilo.

Amewaagiza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio na Mkurugenzi wa Mkuu kampuni ya Azimio Housing Estate Limited, Mohammed Iqbal wakutane na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere ili wajadiliane namna ya kudhibiti wizi na kuimarisha ulinzi. 

Waziri Mkuu alitembelea eneo la mradi huo jana jioni (Jumatatu, Novemba 12, 2018) ambapo baada ya kufika katika eneo ambalo linajengwa nyumba zaidi ya 7,000 alionesha kusikitishwa na uharibifu wa mali na wizi unaoendelea na kutoa maagizo kwa wahusika.

“Kuna mpango gani wa ulinzi wa mali hapa, mali zinaendelea kuibiwa, tutakuja kuanza ujenzi hapa na kukuta hakuna mali hata moja. Ulinzi lazima uimarishwe pande zote mbili za mradi huu eneo la ujenzi na eneo la kuhifadhia vifaa vya ujenzi.”

Kwa upande wakeMkurugenzi Mkuu wa NSSF, Erio alimuahidi Waziri Mkuu kwamba atahakikisha wanakutana na Kamishna wa TRA na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya AZIMIO ili kujadiliana na namna ya kuimarisha ulinzi na kutatua changamoto ya wizi wa mali unaoendelea katika eneo hilo.

Mkataba kati ya NSSF na Azimio Housing Estate Limited (AHEL) ulisainiwa mwaka 2012 na kuanzisha kampuni ya hodhi ya “Hifadhi Builders” ambapo AHEL ilikuwa na asilimia 55 na NSSF asilimia 45. Katika asilimia 55 za AHEL, asilimia 20 ni ardhi iliyotoa kwenye mradi na asilimia 35 angetakiwa kuweka fedha taslimu.

Mradi ulihusisha ujenzi wa nyumba 7,460 ambapo jumla ya gharama za mradi zilikadiriwa kuwa Dola za Marekani 653,436,675 ambazo kati yake ujenzi ungegharimu Dola 544,530,562 wakati gharama za ardhi zingekuwa Dola 108,906,113. Kwa fedha za Tanzania mradi pamoja na ardhi ungegharimu sh. trilioni 1.5.

Hadi kufikia Juni 2018 NSSF walishailipa kampuni ya Hifadhi Builders Dola 133,838,662.2 kama mchango wake kwenye ujenzi wa mradi huo ambazo ni sawa na sh. bilioni 305.8 wakati kampuni ya Azimio ikitoa Dola 5,500,000 sawa na sh. Bilioni 12.6 tu.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, NOVEMBA 13, 2018.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia Majengo ya  DEGE ECO- VILLAGE  mradi wa   ubia kati ya Shirika la hifadhi ya Jamii NSSF na Azimiao wa Nyumba 7,4460 zilizopo  Wilaya ya Kigamboni Dar es salaam .jana  Novemba 12/2018 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa . katikati mwenye Tai nyekundu   atembelea DEGE ECO- VILLAGE  mradi wa   ubia kati ya Shirika la hifadhi ya Jamii NSSF na Azimio wa Nyumba 7,4460 zilizopo  Wilaya ya Kigamboni Dar es salaam .kulia  ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF .Wiliam Erio na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Azimio. Mohammed Iqbal. Waziri Mkuu ametembelea mradi huo jana  Novemba 12/2018.PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa . katikati mwenye Tai nyekundu   atembelea DEGE ECO- VILLAGE  mradi wa   ubia kati ya Shirika la hifadhi ya Jamii NSSF na Azimiao wa Nyumba 7,4460 zilizopo  Wilaya ya Kigamboni Dar es salaam .kulia  ni Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF Balozi Ali Siwa.na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Azimiao. Mohammed Iqbal. Waziri Mkuu ametembelea mradi huo jana  Novemba 12/2018

MBAO FC YAALIKWA KWENYE MICHUANO YA SPORTS PESA SUPER CUP

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Globu ya jamii.

KLABU ya Mbao FC inayoshiriki Ligi kuu Tanzania Bara imealikwa kwenye michuano ya Sports Pesa Super Cup inayotarajiwa kuanza Januari 22 mwaka 2019.

Ikiwa ni mara ya tatu ya michuano hiyo tangu ianzishwe hapa nchini ambayo inazikutanisha timu za Tanzania na Timu za Kenya zinazo dhaminiwa na Kampuni hiyo ya Kubashiri ( Sports Pesa)

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Mkurugenzi Mtendaji wa Sports Pesa Tarimba Abas amesema kuwa sababu ya kuialika Mbao FC kwenye michuano hiyo ni kutokana na Klabu hiyo kuonesha ushindani mkubwa kwenye Ligi kuu Tanzania Bara.

Kwa upande wa uongozi wa Klabu ya Mbao FC kupitia kwa Mwenyekiti wa Klabu hiyo Solly Zephania Njash amesema anaishukuru Kampuni ya Sports Pesa kwa kuialika timu hiyo kwaajili ya kushiriki michuano hiyo na wanaamini watafanya vizuri kwenye michuano hiyo.

"Naishukuru Sports Pesa kwa kutupa heshima hii ya kutualika katika michuano hiyo na mualiko huu kwetu sisi ni Challenge kubwa kwa sababu tutakutana na timu za kigeni ambazo hatujawahi kucheza nazo, hivyo ni jambo jema kwetu na nazikaribisha pia timu za Simba,Yanga na Singida katika michuano hii.Michuano hiyo itashirikisha timu nane kutoka Tanzania na Kenya ambapo kwa Tanzania timu hizo ni Simba,Yanga,Singida United na Mbao FC kwa upande wa Kenya ni Gor Mahia,Kariobangi Sharks,Bandari FC na AFC Leopards.

Mshindi wa michuano hiyo atajishindia kitita cha Dola za Marekani 30000 na pia atacheza na timu ya Everton FC kutoka Uingereza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Sports Pesa Tarimba Abas akizungumzia michuano ya Sports Pesa Super Cup inayotarajiwa kuanza Januari 22 mwaka 2019.

MASHINDANO YA SPORTPESA MSIMU WA TATU KUANZA JANUARY 22, MBAO FC YAALIKWA...

Wataalam wa Afya Muhimbili Wanaendelea kuwajengea Uwezo Wataalam wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Lindi

$
0
0

Daktari Bingwa wa macho kutoka Muhimbili Judith Mwende akimpima macho mgonjwa kwa kutumia mashine maalum ya kuangalizia Retina, kushoto ni Dkt. Mwita Machage wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Lindi Sokoine.
Dokta Willybroad Massawe ambaye ni Dkt. wa upasuaji, pua, koo na masiko (kushoto) kwa kushirikiana na watalaam wengine wa MNH pamoja na wa hospitali ya Sokoine akimtoa mgonjwa matezi ya koo na matezi ya nyama ya pua (mafindofindo) upasuaji ambao huwa haufanyiki katika hospitali hiyo kutokana na ukosefu wa wataalam.
Daktari Bingwa wa Patholojia kutoka MNH Innocent Mosha akifanya uchunguzi wa vivimbe ili kujua tatizo alilokuwanalo mgonjwa kwa ajili ya kuwasaidia Madaktari wa upasuaji kuendelea na tiba sahihi.
Wataalam wa Muhimbili wakimfanyia upasuaji mgonjwa ambaye alikua akisumbuliwa na uvimbe.
Mtaalam wa Radiolojia Dkt. Maria Mtolera wa MNH (kulia) akimuelekeza Dk. Idrisa Chande wa hospitali ya Sokoine jinsi ya kusoma X-Ray ya kifua.
Mtaalam wa Maabara kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Scholastica Mdete akimuelekeza mtaalam wa maabara wa Hospitali ya Sokoine Mwanaidi Kudra jinsi ya ku stain sampuli za wagonjwa.

Wataalam wa afya wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na wataalam wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Lindi Sokoine wakiendelea kutoa huduma kwa wagonjwa na kuwajengea uwezo wataalam wa hospitali hiyo ili kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa Muhimbili, endelea kufuatilia habari katika picha.

MAKAMU WA RAIS AENDELEA NA ZIARA YAKE WILAYA SIHA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Siha Dkt. Andrew Method (kulia) wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa wodi ya mama na mtoto katika hospitali ya Wilaya ya Siha. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa hospitali ya Wilaya ya Siha. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Pichani Hospitali ya Wilaya ya Siha inavyoonekana baada ya kufunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
 Sehemu ya Wakazi wa Kijiji cha Matabi wilayani Siha wakiwa wamejitokeza kwenye mkutano wa hadhara ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Sehemu ya Wakazi wa Kijiji cha Matabi wilayani Siha wakiwa wamejitokeza kwenye mkutano wa hadhara ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa kijiji cha Matabi wilayani Siha.
 Sehemu ya Wakazi wa Kijiji cha Matabi wilayani Siha wakiwa wamejitokeza kwenye mkutano wa hadhara ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Tanzania kupokea Watalii 10,000 kutoka Shanghai mwaka 2019

$
0
0


Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imesaini makubaliano na kampuni ya Touchroad International Group ya China kwa ajili ya kusafirisha watalii 10,000 kutoka jiji la Shanghai kutembelea Tanzania mwaka 2019 kwa kutumia ndege Maalum (chartered flights).

Makubaliano hayo yalisainiwa sambamba na mikutano ya kutangaza utalii katika soko la China- Tourism Roadshow katika miji mitano ya China iliyoanza katika jiji la Shanghai tarehe 12 Novemba 2018.

Mikutano hiyo ni matokeo ya jitihada za Ubalozi wa Tanzania nchini China kwa kushirikiana na TTB ambapo katika mkutano wa kwanza uliofunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki, washiriki mbalimbali zaidi ya 200 walijitokeza wakiwemo makampuni ya utalii (tour operators), mawakala wa usafirishaji (travel agents), mashirika ya ndege (airlines), na vyombo vya habari.

Katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii, Bi. Devotha Mdachi alitoa mada maalum kuhusu vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania pamoja na fursa za uwekezaji katika sekta ya utalii. Aidha, makampuni ya utalii kutoka Tanzania yalipata fursa ya kuelezea packages zao za utalii mahsusi kwa soko la China. Kadhalika, Shirika la Ndege la Tanzania lilitumia fursa hiyo kutangaza juu ya mpango wake wa kuanza safari za moja kwa moja kutoka Tanzania hadi China katika mji wa Guangzhou mwezi Februari 2019.

Mikutano ya kutangaza utalii itaendelea kufanyika katika miji mingine ikiwa ni pamoja na Guangzhou tarehe 14 Novemba 2018, Hong Kong tarehe 16 Novemba 2018, Chengdu tarehe 19 Novemba 2018 na Beijing tarehe 20 Novemba 2018.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 
Dodoma, 13 Novemba 2018



Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki akitoa neno la ukaribisho katika mkutano wa kutangaza vivutio vya utalii uliofanyika Shaghai, China tarehe 12 Novemba 2018. 

Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania, Bi. Devotha Mdachi, Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki, Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania, Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo na viongozi wa kampuni ya Touchroad International Group wakiwa katika furaha baada ya kukamilika uwekaji saini wa makubaliano ambapo kampuni hiyo italeta watalii 10,000 nchini Tanzania mwaka 2019. 

Wajumbe wameshika shuka la kimasai ambalo linaonesha utamaduni wa kabila hilo maarufu kutoka Tanzania. 

Baadhi ya Washiriki wakiwemo viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, TTB na Balozi wa Tanzania nchini China wakiwa katika mkutano huo. 

REGIONAL INTEGRATION KEY TO BUILDING MASS OF QUALIFIED SCIENTISTS – HON. MUTIMURA

$
0
0

Kigali, November 13, 2018 - The Eastern and Southern Africa Higher Education Centers of Excellence Project (ACE II) is holding its sixth Technical and Advisory meeting at the Serena Hotel in Kigali, Rwanda, from November 12th to 14th, 2018.

The ACE II project is strengthening 24 competitively selected Africa Centers of Excellence (ACEs) to deliver quality, market relevant post graduate education, and building collaborative research capacity in five regional priority areas of industry, agriculture, health, education and applied statistics. Sixteen universities in eight countries are participating in the ACE II Project.

The five year project is financed by the World Bank to a tune of $140 million in form of credit to the eight countries which include Ethiopia, Kenya, Malawi, Mozambique, Rwanda, Tanzania, Uganda, and Zambia. Burundi, which does not host any ACE, is eligible to access services offered by the ACEs in other countries and regional capacity-building activities under the project.

The first phase, ACE I, was launched in 2013 in West and Central Africa with 22 ACEs and the second phase in Eastern and Southern Africa with 24 ACEs so as to create a collaborative movement across the continent to steer higher education towards science and technology. Combined, ACE I, ACE II and ACE III projects have a total investment of $600 million. 

The Minister of Education, Republic of Rwanda, Hon. Dr. Eugene Mutimura expressed his passion for the ACE II project “because of the potential benefits and outcomes we expect this project to bring to the region.” 

“We cannot develop as islands. Many of the pillars that we are talking about in terms of developing science must be linked to regional integration,” he said. For example, Carnegie Mellon University Africa Center in Rwanda and other ACEs in Rwanda have offered scholarships to several students from the region.

“It would be good to think about regional integration in terms of developing human capital resource required for our region as a bloc,” said Hon. Mutimura. Prof. Alexandre Lyambabaje, the Executive Secretary of Inter-University Council for East Africa (IUCEA), the Regional Facilitation Unit of ACE II, said that the main aim of countries joining the ACE II Project was to create a conducive environment for training highly skilled and competent scientists at Masters and PhD degree levels in identified key strategic areas.

“Trained scientists are expected to help address the huge deficit of qualified human resources in higher learning institutions in the region and provide high level expertise to our industries, private sector and public sector,” he said. He added, “I am confident that ACEs will produce great scientific results out of their research activities.” He disclosed that IUCEA and the World Bank are in the process of establishing “Regional Incubators”. “The Centers that will host the Regional incubators will be selected competitively before end of the first quarter of the year 2019,” he said.

Dr. Sajitha Bashir, the Practice Manager, Education Global Practice at the World Bank said that the World Bank adopted a regional approach for higher education in 2014 to build capacity in Science and Technology. “The regional approach was adopted by the World Bank because we felt that to really create a critical mass of high quality scientists and to be able to do applied research of the kind of quality that is required, it would be difficult to do this country by country and a regional approach would be appropriate.” Dr. Bashir noted that it is important that Africa’s young population is equipped with skills.

“By 2040 our estimation shows that about 85% of the world’s young people will be in Sub Saharan Africa. It is important that a good proportion of these young people have high quality higher education and that there is a critical mass of highly qualified scientists and engineers and technologists who can adapt, assimilate and adopt technologies and also create new technologies to address the challenges of Africa,” she said. “I hope that this project and the other initiatives will make a contribution to equipping these young people and motivating them to contributing to Africa’s transformation.”

Rwanda, the host of the meeting, has four Centers of Excellence: the African Centre of Excellence in Energy for Sustainable Development (ACEESD) and the African Centre of Excellence in Internet of Things (ACEIoT) both hosted at the College of Science & Technology, the African Center of Excellence for Teaching and Learning Mathematics and Science (ACEITLMS), College of Education and the African Centre of Excellence for Data Sciences (ACE-DS), College of Business & Economics. These four Centers will get a total of $20 million over five years to implement their projects

As with the other ACEs, the funds will be used to develop new programs, expand enrollment, provide world class research facilities, build capacity among faculty and strengthen partnerships with leading regional and global institutions as well as the private sector. For example ACEESD has established a state of the art micro-grid research laboratory and a high performance energy computing unit. The Center will also work with the private sector for curriculum development, student internships and manufacturing of components for its micro grid systems.

Over the project’s duration of five years, the 24 ACEs are expected to enroll more than 3,500 graduate students in the regional development priority areas, out of which at least 700 would be PhD students and more than 1,000 would be female. By the end of the project in 2022 it is envisioned that the centers will have developed sufficient capacity to become sustainable regional hubs for training and research in their specialized fields.

DC TANGA AWATAKA WAANDISHI WA HABARI MKOANI TANGA KUWAFICHUA WAFANYABIASHARA WANAOPITISHA BIDHAA KWA NJIA ZA MAGENDO

$
0
0

MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati akifungua semina ya kodi kwa waandishi wa Habari mkoani Tanga iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Mkoani Tanga (TRA) kushoto ni Meneja wa TRA mkoani Tanga Masawa Masatu
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati akifungua semina ya kodi kwa waandishi wa Habari mkoani Tanga iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Mkoani Tanga (TRA) kushoto ni Meneja wa TRA mkoani Tanga Masawa Masatu na kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Tanga (TANGA PRESS CLUB) Hassan Hashim semina hiyo ilifanyika kwenye Ukumbi wa Bandari Jijini hapa

Meneja wa TRA mkoani Tanga Masawa Masatu akizungumza katika semina hiyo
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Tanga (TANGA PRESS CLUB) Hassani Hashim akizungumza katika semina hiyo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa Afisa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi TRA mkaoni Tanga Salim Bakar akizungumza katika semina hiyo kulia ni Meneja wa TRA Mkoani Tanga Masawa Masatu
Mratibu wa Tanga Press Club Neema Omari akiwa kwenye semina hiyo kulia ni Mwandishi wa gazeti la Uhuru mkoani Tanga Sophia Wakati
Makamu Mwenyekiti wa Tanga Press Club Lulu George akifuatilia semina hiyo
Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia mada mbalimbali kwenye semina hiyo
Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia semina hiyo katikati ni Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania na kulia ni Mbaruku Yusuph wa Tanzania Daima
Sehemu ya maafisa wa TRA wakiwa kwenye semina hiyo
Mratibu wa Tanga Press Club Neema Omari kulia akiteta jambo na Mwandishi wa Habari wa TBC Tanga Bertha Mwambela na kushoto ni Sussan Uhinga wa Gazeti la Mtanzania

Mwandishi wa gazeti la Uhuru mkoani Tanga Sophia Wakati kushoto akiwa na Mwandishi wa TBC Tanga Joachim Kapembe wakichukua dondoo kwenye semina hiyo n
Sehemu ya waandishi wakifuatilia matukio
Mwandishi wa Gazeti la Habari leo mkoani Tanga Cheji Bakari kulia akiwa na Amina Kingazi
Mwandishi wa Habari wa Azam TV mkoani Tanga Mariam Shedafa akiwa kwenye semina hiyo





MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa amewataka waandishi wa habari mkoani Tanga kusaidia kuwafichua wafanyabiashara wanaopitisha bidhaa kwa njia ya magendo ili waweze kuchukuliwa hatua na kukomesha vitendo vya namna hiyo kwenye jamii badala ya kuendelea kuzikalia.

Mwalipwa aliyasema hayo leo mjini hapa wakati akifungua semina ya kodi kwa waandishi wa habari mkoani Tanga ambapo alisema waandishi wa habari wana mchango mkubwa sana katika suala la kuhakikisha wanapambana kwenye vita ya biashara kwa wanakuwa mstari wa mbele katika kuwatoa taarifa kwa mamlaka husika kuwepo kwa vitendo vya namna hiyo kwenye jamii.


“Ndugu zangu waandishi wa habari wasidie kuwafichua wafanya biashara wanaopitisha biashara kwa njia ya magendo saidieni kufuichukua hili kwa kutoa taarifa kwa yoyoye anayehusika na uingizaji bidhaa haramu za magendo nawaombeni acheni kuzikalia toeni taarifa kwa mamlaka husika hatua za kisheria zichukuliwe”Alisema DC Mwilapwa.

Aidha alisema kwamba kwa mwanahabari ambaye atakakuwa ameikalia habari hiyo atakuwa ameitendea dhambi kubwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu atakuwa hajatusaidia katika mapambano ya kuhakikisha tunakomesha tabia hiyo kwenye jamii.

“Lakini pia niwaambie kwamba watu ambao ninaamini wakiingia kwenye vita hii kushirikiana na vyombo mbalimbali watasaidia sana itakuwa wanahabari naombeni sana mshirikiane na serikali kupeana taarifa na kuelimishana lakini pia mtembee na hisia ya serikali kuchukia vitendo hivyo kwani madhara yake ni makubwa kwani vinaikosesha serikali mapato “Alisema DC Mwilapwa

“Pia licha ya mapato lakini Taifa linakosa kitu muhimu ambacho kingekuwa cha manufaa kwa maendeleo yao…kuingiza bidhaa inayopita kwenye milango isiyokuwa rasmi inawezekana bidhaa iliyopita na wakati, feki, lakini pia ni bidhaa duni”Alisema.

Awali akizungumza kwenye semina hyo Meneja wa TRA Mkoani Tanga Masawa Masatu alisema kwamba wameamua kuandaa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari ili watambue magendo ni nini na sheria inayosimamia bidhaa zinazoingia nchini inavyoeleza ili watakapotoka wawe mabalozi wazuri kuwaelimisha watu kupitia kwenye milango sahihi kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

“Siku ya leo tumeandaa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari mojawapo ni juu ya masuala ya vita dhidi ya magendo kama TRA tunatambua changamoto ya magendo inayoikabili mkoa wetu na Mkuu wa mkoa ameunda kamati maalumu ya mkoa ambayo itakuwa na jukumu la kukomesha vitendo vya magendo kwa mkoa wetu wa Tanga”Alisema

“Lakini namshukuru RC kwa kusimamia suala hilo naamini kwamba litakapotekelezwa kwa ukamilifu suala la magendo litapungua kwa asilimia kubwa sana”Alisema Meneja huyo.

LONGIDO KUPATA MAJISAFI NA SALAMA KWA ASILIMIA 100-PROFESA MBARAWA

$
0
0
Waziri wa Maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) amesema hali ya upatikanaji majisafi na salama katika mji wa Longido wenye idadi ya wakazi 16, 712 inaongezeka kutoka asilimia 15 ya sasa inayowafikia wananchi 2, 510 hadi kufikia asilimia 100.

Waziri Mbarawa akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo amefafanua kuwa hatua hiyo inamaanisha wananchi wote katika mji huo watapata huduma ya majisafi na salama kupitia mradi mkubwa wa maji wa Longido unaoanzia mto Simba katika wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro wenye uwezo wa kuzalisha maji kiasi cha Mita za ujazo 2,160 kwa siku wakati mahitaji halisi katika mji wa Longido ni Mita za ujazo 1,462.

Waziri Mbarawa ameainisha mradi wa maji Longido unaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 15.7 tayari mabomba yenye urefu wa kilometa 94 yamelazwa kutoka katika chanzo cha maji cha mto Simba wilayani Siha na mkandarasi kampuni ya ujenzi ya STC anatakiwa kukabidhi mradi mwezi ujao Tarehe 15 Desemba 2018. 

Waziri Mbarawa amesema ili kuhakikisha wananchi wa Longido wanapata maji huduma ya maji haraka na kujikita katika shughuli nyingine za maendeleo, Serikali iliamua kandarasi ya mradi huo itekelezwe na Wakandarasi waliopewa kazi tofauti; kazi hizo ni pamoja na kujenga matanki, ujenzi wa mifumo ya kusambaza maji, na ujenzi katika chanzo cha maji.

Waziri Mbarawa amesema Serikali imejipanga kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma ya majisafi na salama kama ambavyo Sera ya Taifa ya Maji ya mwaka 2002 inavyoelekeza kuwapatia wananchi waishio vijijini majisafi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao. 

Aidha, ameongeza nia hasa ni kufanikisha asilimia 85 ya wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama katika maeneo ya vijijini ifikapo mwaka 2020 na asilimia 95 katika miji. Pamoja na hilo amewataka wananchi kutunza mazingira na kuotesha miti kulinda vyanzo vya maji. 
Waziri wa Maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) akitoa maelekezo katika kizimba cha kupunguza msukumo wa maji (BPT) katika eneo la mto Simba, wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro. Mradi wa maji wa Longido chanzo chake kipo mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa akiangalia ubora wa kizimba na bomba zilizotumika katika kizimba cha kupunguza msukumo wa maji (BTP) katika eneo la mashamba la Simba. BTP moja ya kazi yake ni kuzuia mabomba kupasuka. Mradi wa maji wa Longido mabomba yamelazwa kwa umbali wa kilomita 94 na thamani ya mradi ni kiasi cha Shilingi bilioni 15.7.
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa (Mb) akishiriki kazi ya kuunga mabomba kabla ya kulazwa eneo la Mbugani, katika mradi wa maji wa Longido . Waziri Mbarawa amemtaka mkandarasi kampuni ya Ujenzi ya STC kukabidhi mradi ifikapo Tarehe 15 Desemba 2018. 

KAMATI YA BARAZA LA WAWAKILISHI INAYOSIMAMIA OFISI ZA VIONGOZI WAKUU ZANZIBAR YAVUTIWA NA MAFANIKIO YA TASAF.

$
0
0








NA Estom Sanga- TASAF.

Wajumbe wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wamepongeza hatua ya Serikali ya Muungano na ile ya Mapinduzi kwa usimamizi thabiti wa utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF.

Wakizungumza jijini Dar es salaam baada ya kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Shughuli za TASAF mwanzoni mwa ziara ya siku NNE ya kutembelea miradi ya Mfuko huo, Wajumbe hao wameeleza kuridhishwa kwao na namna Mfuko huo ulivyoleta hamasa ya wananchi kujinasua na tatizo la umaskini uliokithiri.

Wamebainisha kuwa miradi iliyotekelezwa na TASAF nchini inaonyesha taswira nzuri ya uwajibikaji na utekelezaji wa maagizo ya serikali yenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi na kuondoa kero ya umaskini.

Wametolea mfano wa miradi ya Shule ,Afya,Maji na hata uanzishaji wa miradi ya midogo midogo ya kiuchumi kwa wananchi kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa shughuli za kujiongezea kipato .

Aidha Wajumbe hao wameiomba serikali kupitia TASAF kuhakikisha kuwa inatoa fursa nyingine ya Wananchi wanaokabiliwa na umaskini ambao hawakupata fursa ya kuandikishwa kwenye shughuli za Mpango huo unaohudumia takribani Kaya Milioni MOJA na Laki Moja Tanzania Bara ,Unguja na Pemba.

Awali akiwakaribisha Wajumbe hao Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga amesema maandalizi ya awamu ya pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambayo italenga zaidi katika kuwashirikisha Walengwa kufanya kazi katika kutekeleza miradi ya maendeleo yako katika hatua za mwisho na inatarajiwa kuanza mwezi Aprili mwaka ujao.

Amezishukuru Serikali ya Muungano na ile ya Zanzibar na wadau wa Maendeleo kwa kuendelea kuunga mkono utekelezaji wa Shughuli za TASAF jambo ambalo amesema limewezesha kupatikana kwa mafanikio huku akipongeza hatua ya Walengwa kuanza kutumia huduma za TASAF katika kuleta mabadiliko kwenye maisha yao.

Akitoa taafa ya utekelezaji wa shughuli za TASAF, Mkurugenzi wa miradi wa TASAF,Amadeus Kamagenge amesema kwa kiwango kikubwa Mfuko huo umetekeleza miradi yake kwa ufanisi mkubwa na hivyo kutekeleza azma ya serikali ya kuwaondoa wananchi kwenye dimbwi la umaskini.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bw. Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akizungumza kwenye kikao cha Wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa Zanzibar wa liotembelea taasisi hiyo kuona utekelezaji wa shughuli zake.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia Ofisi za watendaji wakuu wa kitaifa katika baraza la wawakilishi Mhe. Ali Suleimani Ali akizungumza kwenye kikao na Watendaji wa TASAF baada ya kupokea taarifa ya miradi ya TASAF.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais –Zanzibar Mhe. Mihayo Juma N’hunga akizungumza wakati wa kikao cha pamoja katika wajumbe na menejimenti ya TASAF juu ya utekelezaji wa shughuli za mfuko huo.
Mkurugenzi wa Miradi wa TASAF ,Bw. Amadeus Kamagenge(aliyesimama ) akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za TASAF kwa wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa kitaifa Zanzibar.
Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa kitaifa akichangia taarifa ya utekelezaji wa shughuli za TASAF kwenye kikao kilichofanyika kwenye ofisi za TASAF jijini Dar es salaam.
Wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa kitaifa wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TASAF baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya taasisi hiyo jijini Dar es sdalaam.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO NOVEMBA 14,2018

TBL YAZINDUA 'KAMATA USUKANI WA MAISHA YAKO, KUNYWA KISTARAABU'

$
0
0
Kamishina Msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Operesheni Kikosi cha Usalma barabarani Makao Makuu ,Abdi Issango,akiongea wakati wa uzinduzi huo,wengine pichani ni Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL, Irene Mutiganzi (katikati) na Mrakibu wa jeshi la Polisi na Mkuu wa Kitengo cha elimu Tanzania, Abel Swai.
Mkurugenzi wa Udhibiti Usafiri wa barabara (SUMATRA), Johansen Kahatano ,(Kushoto) akiongea kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ( hawapo pichani) katikati ni Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL Group Irene Mutiganzi na Kamishina Msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Operaresheni Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu ,Abdi Issango.
Meneja Masuala Endelevu wa TBL Irene Mutiganzi akielezea kampeni hiyo kwa waandishi wa habari.
Mkurugenzi wa Udhibiti Usafiri wa barabara (SUMATRA) Johansen Kahatano, akikabidhiwa Stika kuhusiana na kampeni hiyo na Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL ,Irene Mutiganzi (wa pili kulia) wakati wa uzinduzi Kushoto ni Mrakibu wa jeshi la Polisi na Mkuu wa Kitengo cha elimu Tanzania, Abel Swai na Kamishina Msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Operesheni Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama barabarani ,Abdi Issango.
Mmoja wa waandishi waliohudhuria uzinduzi huo, Felister Massae akikabidhiwa stika zenye ujumbe wa kuhamasisha Unywaji wa kistaarabu *Inashirikiana na Polisi, SUMATRA, TANROAD NA UBER Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) kupitia bia yake chapa ya Kilimanjaro imezindua kampuni ya unywaji wa pombe kistaarabu inayojulikana kama ‘Kamata Usukani wa Maisha Yako,Kunywa Kistaarabu.

 Akiongea wakati wa uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam,Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL,Irene Mutiganzi,alisema katika kufanikisha kampeni hii itakayodumu katika kipindi cha miezi miwili kampuni imeshirikiana na wadau mbalimbali ambao ni Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, SUMATRA, TANROADS na kampuni ya usafirishaji abiria ya UBER. “Kama kampuni tunajali wateja wetu na pia tunatambua kuwa ni jukumu letu kuelimisha jamii yetu kuhusu madhara ya unywaji pombe kupita kiasi. Elimu hii itatolewa kwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari”,alisema Mutiganzi. 

Aliongeza kuwa pia itatolewa elimu kwa madereva 150 wa UBER wa mkoa wa Dar es Salaam ili kuwakumbusha kuhusu usalama wao na abiria wao wakati wanapokuwa barabarani na madereva watakaopata mafunzo wataweka stika za ‘Shika Usukani wa Maisha Yako,Kunywa Kistaarabu’ kwenye magari wanayoendesha kama ishara ya kuonyesha ushiriki wao na ahadi yao ya kuzingatia elimu waliopewa.

 “Katika siku za karibuni nchi yetu imekumbwa na matukio ya ajali za barabarani na sisi, ndugu zetu, marafiki zetu na wateja wetu tukiwa kama watumiaji wa barabara ni vema kukumbushana jukumu hili la usalama barabarani na kulitafutia ufumbuzi. TBL kwa kushirikiana na wadau wetu tunapenda kuwahamisisha wateja wetu kutokuendesha chombo cha moto pindi wanapokuwa wamelewa na badala yake kutumia usafiri wa UBER au njia nyingine mbadala”,alisisitiza. 

Kwa upande wake Mkuu wa Operesheni kutoka Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi Abdi Issango, alipongeza jitihada hizo zinazolenga kupunguza matukio ya ajali. 

“Suala la kupunguza matukio ya ajali nchini hususani za barabarani ambazo zimekuwa zikisababisha vifo vingi na hasara sio jukumu la serikali na jeshi la polisi pekee bali ni jukumu la kila mtanzania,hivyo tunaendelea kushirikiana na wadau wote kuhakikisha tunafanikisha kupunguza ama kuondoa tatizo hili la ajali hususani zinazotokana na uzembe wa madereva wanaoendesha vyombo vya moto wakiwa wamelewa” alisema Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Abdi Issango. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa usafiri wa barabara kutoka SUMATRA,Bw.Johansen Kahatano alisema, “Kama wadau wa usafirishaji abiria,tunayo furaha kushirikiana na TBL na wadau wengine katika kampeni hii ya kupunguza ajali nchini nasi tutakuwa mstari wa mbele siku zote tutakuwa mstari wa mbele kushiriki katika uhamasishaji wa jamii kuhusu matumizi salama ya vyombo vya usafirishaji ili kukomesha matukio ya ajali hususan zinazotokana na uzembe wa madereva”.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images