Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46200 articles
Browse latest View live

NMB YAFANYA KONGAMANO LA MAFUNZO KWA MAWAKALA WAKE

0
0


Sehemu ya mawakala wa NMB waliohudhuria kongamano hilo wakionesha vyeti vyao mara baada ya kukabidhiwa.


Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd akizungumza na mawakala wa Benki ya NMB walioshiriki kwenye kongamano la mawakala wake wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd (kulia) akimkabidhi mmoja wa mawakala wa Benki ya NMB cheti kwenye semina ya mawakala wake wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd (kulia) akimkabidhi mmoja wa mawakala wa Benki ya NMB cheti kwenye semina ya mawakala wake wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Mawakala wa Benki ya NMB, Ericky Willy (wa pili kulia) akimpongeza kabla ya kukabidhiwa cheti mmoja wa mawaka aliyehudhuria semina ya mawakala wa Benki ya NMB wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.


Mawaakalaa wakiwa katika kongamano hilo.

Mada mbalimbali zikiwasilishwa na maofisa wa Benkli ya NMB

Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Mawakala wa Benki ya NMB, Ericky Willy akizungumza kwenye semina ya mawakala wa Benki ya NMB wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd na Meza kuu kwenye semina kwa mawakala wa Benki ya NMB wa jijini Dar es Salaam wakipiga picha ya pamoja na mawakala bora kwa mwaka 2018 wa Benki hiyo kwa kanda ya Dar es Salaam.



BENKI ya NMB leo imefanya kongamano la mafunzo kwa mawakala mbalimbali wanaotoa huduma za kibenki kwa wateja wa benki hiyo, lengo likiwa ni kuboresha huduma zake na kuwajengea uwezo wa kibiashara mawakala hao.

Akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika Sinza jijini Dar es Salaam, Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd alisema benki hiyo itaendelea kuwajengea uwezo mawakala hao kwani wao ni sehemu ya benki hivyo huduma zao zinatakiwa kufafana na zinazotolewa kwenye matawi yao.

Aliwataka kuendeleaa kutoa huduma kwa uaminifu kwa wateja na kuzingatia taraatibu walizopewa na Benki ili wateja wanaowahudumia waendelee kuiamini benki yao. Aliongeza NMB itaendelea kuboresha huduma zake na kuendelea kuwa kinara katika sekta ya fedha nchini.

Katika kongamano hilo la kuwajengea uwezo mawakala wa NMB ikiwa ni muendelezo wa semina hizo nchi nzima, NMB imetoa zawadi na vyeti kwa mawakala wanaofanya vizuri katika kutoa huduma kwa wateja ili kuwapa motisha ya kuendelea kufanya vizuri.

Akitoa mafunzo kwa mawakala, Meneja Mwandamizi wa NMB Wakala, Tito Mangesho alisema mikakati ya NMB ni kuongeza idadi ya wateja huku ikitumia njia rahisi na salama ya kuwahudumia kiufanisi zaidi.Aidha aliongeza kuwa malengo mengine ni pamoja na kuongeza unafuu wa gharama zake na uharaka wa kuwahudumia wateja, kupunguza msongamano na kuboresha kamisheni kwa mawakala wake.

Naye, Meneja wa NMB Wakala Kanda ya Dar es Salaam, Kisamo Edwin aliongeza kuwa miongoni mwa matarajio ya NMB hapo baadaye ni kuleta mashine mpya za kisasa kwa mawakala zitakazo kuwa na wigo mpana wa kutoa huduma na kumuongezea kipato.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU NOVEMBA 12,2018

0
0
















Benki ya Stanbic yazindua huduma ya soko la fedha za kigeni kidijitali iitwayo eMarket Trader

0
0
Benki ya Stanbic Tanzania imezindua mfumo utakaoruhusu mauzo na manunuzi ya fedha za kigeni kimtandao uitwao ‘eMarket Trader’. Hii ni jitihada ya benki hiyo kuwapatia wateja wao huduma mahususi katika kubadilisha fedha za kigeni, huduma hii inajumuisha wateja binafsi pamoja na makampuni makubwa na madogo. Kupitia mtandao huu, wateja wanaweza kujua taarifa za thamani ya fedha za kigeni kwa wakati husika pia kupata taarifa juu ya mwenendo wa soko.

Huduma hii ni ya kwanza na ya kipekee nchini Tanzania na inapatikana mtandaoni. eMarket Trader inawawezesha wateja kubadilisha fedha zao kwa urahisi zaidi na kuwapatia zaidii ya aina 64 za fedha zilizopo sokoni kwa wakati huo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Meneja wa Masoko ya fedha kutoka Benki Kuu (BoT), Bw Lameck Kakulu alisema “Tunafuraha kuona benki ya Stanbic, moja ya wadau muhimu katika sekta ya fedha nchini wakijikita katika teknolojia. Kupitia uboreshaji huu wenye vipengele muhimu vya kidijitali kama kupata taarifa za soko katika muda halisi na upatikanaji wa tafiti za Benki ya Standard Bank.”

“Hapo zamani wateja wetu walihitaji kupiga simu kitengo cha ubadilishaji fedha kwa ajili ya kununua au kuuza fedha zao, na huduma hii iliwezekana tu wakati wa saa za kazi za benki. Hivyo basi, kupitia e-Market Trader, wateja wetu wanaweza kubadilisha fedha zao na kupata taarifa juu ya soko kwa wakati” alisema Mkuu wa Kitengo cha Masoko ya Fedha za kigeni wa Benki ya Stanbic, Bw Erick Mushi.

Bidhaa hii imelenga kuhakikisha wateja wote wa Benki ya Stanbic ambao biashara zao zinahusiana na masoko mbali mbali ya kimataifa wanapata maendeleo ya kifedha. Mpaka sasa miamala inayofanyika katika mtandao huu kwenye benki za Stanbic Africa ni dola za Kimarekani bilioni 18 na watumiaji zaidi ya 5,000 huwepo mtandaoni kila siku. Uzinduzi huu unaashiria utekelezaji wa ahadi iliyowekwa na Benki ya Stanbic ambayo ni kuchochea maendeleo ya wateja wake na Tanzania kwa ujumla.

Meneja wa Masoko ya fedha kutoka Benki Kuu (BoT), Bw Lameck Kakulu akizindua huduma ya soko la fedha za kigeni kidijitali ya Benki ya Stanbic iitwayo eMarket Trader jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko ya Fedha za kigeni wa Benki ya Stanbic, Bw Erick Mushi (kulia) na Mkuu wa Huduma za kibenki za mashirika na uwekezaji wa Benki ya Stanbic Bw Manzi Rwegasira. 
Meneja wa Masoko ya fedha kutoka Benki Kuu (BoT), Bw Lameck Kakulu akipeana mkono na Mkuu wa Kitengo cha Masoko ya Fedha za kigeni wa Benki ya Stanbic, Bw Erick Mushi (kulia) baada ya uzinduzi wa huduma ya soko la fedha za kigeni kidijitali ya Benki ya Stanbic iitwayo eMArket Trader jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Katikati ni Mkuu wa Huduma za kibenki za masharika na uwekezaji wa Benki ya Stanbic Bw Manzi Rwegasira.

WATUNGA SERA, WAWEKEZAJI NA WABUNIFU KATIKA SEKTA YA AFYA KUJADILI FURSA ZILIZOPO KUELEKEA TANZANIA YA UCHUMI WA VIWANDA

0
0
Zaidi ya wataalamu 600 katika sekta ya afya nchini Tanzania and kwingineko duniani wanakutana jijini Dar es Salaam kwenye kongamano la 5 la afya (Tanzania Health Summit) linaloanza Novemba 13(kesho). Litahitimishwa Jumatano Novemba 14. Kwa mara ya kwanza, kongamano hili lilifanyika nchini mwaka 2014.

Kongamano la mwaka huu linakuja na fursa mbalimbali kwa wadau wote walioko katika mfumo mzima wa afya nchini. Viongozi wa serikali, wawekezaji, watafiti na wabunifu watakutana kujadili mada kuu kuhusu dira ya Tanzania katika kuelekea uchumi wa viwanda. Kaulu mbiu ya mwaka huu ni, Ukuaji wa viwanda nchini Tanzania: Tathmini ya ukuaji na jinsi ya kutatua changamoto zilizokithiri.

Waandaaji na waratibu wa kongamano hili ni TAMISEMI), Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Afya ya Zanzibar, BAKWATA na Tume ya Kuratibu Huduma zitolewazo na makanisa (CSSC), Tindwa Medical and Health Services na Wasimamizi wa Hospitali za Binafsi(APHFTA).

 Wataalamu wa afya kunufaika
 Kwa mara ya pili, wataalamu wa afya nchini watakao hudhuria kongamano na watakaowasilisha machapisho yao watapewa alama za kufuzu viwango vya kitaaluma. Hii itawasaidia kukuza taaluma zao na kuongeza alama za ujuzi katika kile kinacho itwa Continuing Professional Development (CPD).

Kongamano la afya la Tanzania (THS) limepewa ithibati ya kutoa alama hizo na Chuo kikuu ya tiba na sayansi shirikishi(Muhas). Hii ni baada ya serikali, kupitia wizara ya afya, kutoa mwongozo kwamba wataalu wa afya ni lazima watafute njia za kujiendeleza kitaaluma wawapo makazini ili kukuza ujuzi na weledi katika taaluma zao.

Rais wa Kongamano la Afya Tanzania, Dkt Omary Chillo, amesema, “Wataalamu wa afya wasibweteke baada ya kupata na kuanza kufanya kazi. Utaalamu huwa unapotea taratibu na baada ya muda. Bila kuongeza ujuzi kitaaluma wataalamu wengi wanaweza kujikuta wakibaki nyuma. Haijalishi kama wana uzoefu kiasi gani. Kuna mabadiliko makubwa katika teknolojia za tiba na utandawazi. Kongamano hili ni fursa pekee kwa hivi sasa kujieongezea alama kitaaluma.”

Zaidi ya taasisi 100 kushiriki, watoa mada 40
Zaidi ya taasisi 100 zinashiriki katika kongamano hili. Katika majukwaa yaliyoandaliwa katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), taasisi ya JHPIEGO itaonyesha mbinu maalumu ya kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi usio salama hapa nchini.

 Lakini pia, taarifa mbalimbali kuhusu sera za afya na miradi ya maendeleo katika sekta ya afya zitatolewa na majukwaa ya Wizara ya afya, Tamisemi na Wizara ya Afya ya Zanzibar.Kutakuwepo na majukwaa ya wasimamizi wa hospitali za binafsi(APHTA), tume ya kuratibu huduma za kijamii zitolewazo na makanisa(CSSC), Chuo Kikuu cha Mt Joseph, Hospitali ya Aga Khan na ShopsPlus.Zaidi ya machapisho 100 yatawasilishwa na yatahusu waswala nyeti katika maendeleo ya sekta ya afya nchini. Mada kuu sita zaitawasilishwa na watoa mada 40.

Wajumbe kutoka mataifa mbalimbali, kitakacho zungumziwa
Wawekezaji katika afya, mahospitali mbalimbali, wasambazaji wa vifaa vya afya na madawa, watafiti katika nyanja ya afya, mashirika yasiyo ya kiserikali n.k, wanategemewa kuhudhuria katika kongamano hili muhimu ambalo kwasasa linatimiza miaka mitano baada ya kuonyesha mafanikio katika sekta ya afya.
Mazungumzo ya hali ya juu ya kitaalamu yatatawala. Kutakuwepo na fursa za uwekezaji katika sekta ya afya zitakazojionyesha wazi wazi katika machapisho ya kisayansi, mijadala ya kitaaluma na maonyesho ya kibiashara (exhibitions).

 Kwanini ukuaji wa sekta ya viwanda?
Kwa miaka kadhaa sasa, sekta ya afya imekuwa ikipitia katika hatua za ukuaji hasa tukizingatia mabadiliko yake katika ukuaji wa uchumi wa viwanda. Lakini, hapakuwepo na jukwaa mahususi la wazi kutathmini mabadiliko hayo na namna nzuri ukuaji huu unavyoweza kuleta tija na kujadili namna ya kuepuka hatari zitokanazo na haya mabadiliko.

“Tunataka kutafuta changamoto zilizopo katika sekya ya viwanda vya afya, na kuzitatua. Huu ni muda mwafaka kwa watanzania wenyewe kubuni mbinu za kuendeleza sekta hii na ili kujenga uwezo wa kuanzisha viwanda vya kuzalisha dawa hapa hapa nchini,’’ amesema Dkt Chillo.Katibu wa Umoja wa wamiliki wa Viwanda vya kuzalisha dawa nchini(TAPI), Abbas S. Mohammed, amesema, “Tanzania iko katika nafasi nzuri ya kuanzisha viwanda vya kuzalisha dawa nchini. Na hivi sasa bado viwanda vilivyopo havijatosheleza soko. Katika kongamano hili, mambo kadhaa yatazungumzwa zikiwamo mbinu za kufikia malengo kama taifa.”

Dkt Ntuli A. Kapologwe, Dr Ntuli A. Kapologwe, ambaye ni Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe(DHSWNS)—TAMISEMI, amesema, “Sekta ya viwanda ikichukuliwa kwa uzito mkubwa, haswa katika mutktadha wa ukuaji wa sekta ya afya italifanya taifa letu kuwa imara zaidi na kuliwezesha hata kuwavutia watu kufanya utalii katika maswala ya afya nchini(medical tourism).”

Mwenyekiti wa THS, Dkt Chakou Halfani, amesema, “Katika kongamano hili, tutajadili haya mambo kwa kina na kwa jicho la uchambuzi huru.Tuone tumefanikiwa wapi mpaka sasa, na tunakwenda wapi. Tutafute ufumbuzi wa pamoja.”

Majadiliano haya yana maana gani kwa taifa? Mapendekezo yatakayotolewa katika kongamano hili yatawekwa katika vitabu vya mpango kazi na kila mchangiaji atapendekeza mambo ya muhimu ya kufanya kama suluhu ya namna ambavyo yatasaidia katika kusaidia Tanzania kufikia uchumi wa viwanda.  
Kwa taarifa Zaidi: Barua pepe: info@ths.or.tz, admin@ths.or.tz Tovuti: www.ths.or.tz Simu ya mkononi: +255 684 244 377 & +255 683 907 080 Simu ya mezani: +255 22 171 555 Fax: +255 22 217 558

Hivi ndivyo Tamasha la Tigo Fiesta lilivyoacha gumzo jijini Arusha

0
0
-Whozu apanda stejini na Briefcase lililojaaa mishkaki
-Roma, Stamina waangusha bonge moja la show

JIJI la Arusha, jana lilishuhudia show za kufunga mwaka zilizojaa ubunifu na vituko vya aina yake kutoka kwa wasanii mbali mbali waliopanda jukwaani kutumbuiza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyilka katika  uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Msanii Whozu alikuwa ni kivutio kikubwa kutokana na staili aliyotumia kupanda jukwaani na madensa wake wakiwa  wamevalia  nguo za wapishi  huku akiwa na briefcase lililojaa mishkaki.Mashabiki wengi walipigwa na butwaa baada ya kuona Whozu akifungua briefcase ambalo lilionekana ni la thamani na kutoa mishkati kisha kutuimbuiza na simbo wa Ita Boda boda Twende Kwa Mromboo ambao ulikuwa ni kivutioa Whozu na madensa wake, walifanikiwa kuliteka vyema jukwaa ambapo wakitumbuiza huku wakiwa wanatafuna mishkaki.

Wasanii wengine ambao walifanikiwa kuteka nyoyo za mamia ya mashabiki waliofurika kwenye tamasha la  hilo  ni pamoja na Roma, Stamina ambao walipanda jukwaani  pamoja na mwanadada Maua Sama anayetamba na kibao chake cha Iokote.Wasanii wengine walipanda sjejini ni pamoja na Dogo janja, Lulu Diva, Rich Mavoko, Fid Q, Weusi na wengine.

Ikiwa ni sehemu ya Vibe la Tigo Fiesta 2018, kampuni ya simu za Simu za mkononi ya Tigo imewaletea promosheni bab-kubwa inayojulikana ya Data Kama Lote inayowapa wateja bonasi ya hadi mara mbili kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#.

Tigo pia inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Wateja wanapaswa kupiga *150*01#  na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika cha bei ya tiketi kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.

Wateja wa Tigo pia wanaweza kujaribu umahiri wao wa kujibu maswali yanayohusiana na msimu wote wa vibes kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia.  Washindi wanajinyakulia zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla.

Msanii Whozu na madensa wake wakitumbuiza katika Tamasha la Tigo Fiesta 2018 lilofanyika katika kiwanja cha Sheikh Amri Abeid jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
Wasanii wanaounda kundi la Weusi wakiongozwa na Joh Makini wakiwapagawisha mamia ya mashabiki walioshiriki katika tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018 lililofanyika katika uwanja Sheikh Amri Abeid jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
Msanii Maua Sama anayetamba na kibao chake cha Iokote akitoa burudani ya aina yake kwa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya walioshiriki katika tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018 lililofanyika katika uwanja Sheikh Amri Abeid jijini Arusha mwishoni mwa wiki.
Rich Mavoko Msanii Rich Mavoko akitoa burudani kwa maimia ya mashabiki waliofurika katika Tamasha la Tigo Fiesta mwaka 2018 lililofanyika katika uwanja Sheikh Amri Abeid jijini Arusha mwishoni mwa wiki.

MAHAKAMA YAELEZWA UPELELEZI KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI MFANYABIASHARA AKRAM AZIZI HAUJAKAMILIKA

0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa upelelezi dhidi ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyabiashara Akram Azizi ambaye ni mdogo wa mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Azizi bado haujakamilika.

Wakili wa Serikali Elia Athanas ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile kesi hiyo ilipoitwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa."Mheshimiwa keai hii leo imekuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika, tunaimba ipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa" amedai wakili Athanas.

Kufuatia malezo hayo, Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 26 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.Katika kesi hiyo, Mshtakiwa Azizi anakabiliwa na mashtaka 75 yakiwemo mashtaka 71 ya kukutwa na Silaha za aina mbali mbali mbali, utakatishaji wa fedha kiasi cha USD 9018.

Pia anakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na nyara za serikali zenye thamani ya sh milioni 108, risasi 6496 na pia anakabiliwa na kosa la kukutwa na nyama ya Nyati, Kilogramu 65 yenye thamani ya Shilingi Mil 4.35 bila kuwa na kibali, ambalo anadaiwa kulitenda Oktoba 30,2018 huko Oysterbay Kinondoni Dar es Salaam.

Katika shtaka la utakatishaji mshtakiwa anadaiwa, kati ya Juni 2018 na Oktoba 30. 2018 katika eneo la Osterbay, alijipatia jumla ya USD 9018 huku akijua kuwa kiasi hicho cha fedha ni zao la kosa tangulizi la kujihusisha na biashara haramu ya nyara za serikali pamoja na kukutwa na silaha bila kibali.

Katika mashtaka ya kukutwa na risasi mshtakiwa anadaiwa, Oktoba 30. 2018 (Jana) huko Osterbay, alikutwa na risasi 4092 bila ya kuwa na kibali kutoka kwa mrajisi wa kibali cha silaha.

Pia Imedaiwa Oktoba 31.2018 (leo) huko huko Osterbay mshtakiwa alikutwa na risasi 2404 bila ya kuwa na kibali kutoka kwa mrajisi wa silaha.
Mfanyabiashara Akram Azizi ambaye ni mdogo wa mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Azizi akiwasili leo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza kesi yake ya uhujumu uchumi inayomkabili .

NEWZ ALERT: Waziri wa Nishati avunja Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini

0
0

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani leo tarehe 12 Novemba, 2018 amevunja rasmi Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) iliyokuwa ikiongozwa na Dkt. Gideona Kaunda.

Uamuzi huo ameutoa katika Mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dodoma. Alisema kuwa, Bodi hiyo iliundwa mwaka 2017, kwa mujibu wa Sheria ya Wakala Vijijini Na.8 ya Mwaka 2005 (The Rural Energy Act. No.8 of 2005). 

“ Bodi hii imetekeleza majukumu yake kwa takriban mwaka mmoja (1) sasa na katika kipindi hicho ambapo Bodi hii imekuwepo, ninapenda kuwajulisha kwamba kwa ujumla sijaridhishwa na utendaji wake,” alisema Dkt Kalemani.Hivyo alieleza kuwa, kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu 9(3)(b) cha Sheria Na. 8 ya Nishati Vijijini ya 2005, ameamua kuivunja Bodi hiyo kwa kutengua uteuzi wa Mwenyekiti pamoja na Wajumbe wa Bodi.

Aliongeza kuwa, Bodi nyingine mpya itaundwa baadaye kwa mujibu wa Sheria ya Nishati Vijijini ya mwaka 2005. Bodi hiyo ilizinduliwa mwezi Aprili mwaka 2017 na ina wajumbe Saba.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuivunja Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua.

WAKUU WA MAGEREZA NCHINI WATAKIWA KUWA WABUNIFU UTATUZI WA NYUMBA ZA ASKARI

0
0
Na Lucas Mboje, Njombe

WAKUU wa Magereza yote nchini wametakiwa kuwa wabunifu ili kutatua changamoto ya uhaba wa makazi ya askari kwa kutumia nguvukazi ya wafungwa na rasilimali nyinginezo zilizopo katika maeneo yao.

Wito huo umetolewa leo Novemba 12, 2018 na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua magereza yote ya Mkoa wa Njombe ambayo yanaendeshwa na Jeshi hilo. Kamishna Jenerali Kasike amesema kuwa lazima wakuu wa magereza wawe wabunifu katika kutatua tatizo hilo la uhaba wa nyumba kwani Jeshi hilo linazo fursa nyingi ikiwemo nguvu kazi ya wafungwa.

“Mkoa wa Njombe na mingineyo nchini haipo sababu ya kuwa na tatizo la uhaba wa nyumba za askari kwani kuna fursa ya kutosha ya kufyatua tofali za kuchoma kwa kuwatumia wafungwa ili kumaliza tatizo hili nchini”. Amesisitiza Jenerali Kasike. Aidha, Kamishna Jenerali Kasike amewataka mafisa na askari wote kuendelea kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia maadili, sheria na kanuni mbalimbali za uendeshaji wa Jeshi hilo.

Awali, akisoma taarifa ya Gereza la Wilaya Njombe, Mkuu wa Gereza hilo, SP. Charls Mihinga amesema kuwa tayari wameanzisha mradi wa ufyatuaji wa tofali za kuchoma katika kambi ya mdandu ili kumaliza tatizo la uhaba wa nyumba za watumishi wa gereza hilo. “Katika msimu huu tumeweza kufyatua tofali kubwa zipatazo 30,000 ambazo tayari zimeshachomwa, tofali hizi zitatumika katika ujenzi wa nyumba za askari pamoja na ujenzi wa Ofisi mpya ya Mkuu wa Magereza Mkoani Njombe”. Alisema SP. Mihinga.

Pia, ameongeza kuwa malengo ya baadaye ni kuifanya kambi hiyo ya Gereza Njombe kuwa na taswira ya uzalishaji wa matofali kwa wingi kwa ajili ya kufanya biashara na hivyo kuongeza maduhuri serikalini.

Jeshi la Magereza linakabiliwa na uhaba wa nyumba za kuishi za Maafisa na askari hapa nchini, mkakati uliopo hivi sasa chini ya uongozi wa Kamishna Jenerali wa Magereza ni kuhakikisha kuwa tatizo hilo linatatulika kwa kutumia njia ya ubunifu pamoja na fursa mbalimbali zilizopo ndani ya Jeshi hilo.
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Njombe ambaye pia ni Katibu Tawala wa Mkoani Njombe Bw. Erick Shitindi akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP) Phaustine Kasike walipokutana  Mkoani Njombe alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa huo kabla ya kuendelea na ziara yake ya kikazi Mkoani Njombe, leo Novemba 12,  2018.
 Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Njombe wakimsikiliza  Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini (CGP) Phaustine Kasike(hayupo pichani) alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa kabla ya kuendelea na ziara yake ya kikazi Mkoani humo.
 Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini (CGP) Phaustine Kasike(wa kwanza kulia) akizungumza jambo alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Njombe. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo.
 Mkuu wa Gereza Njombe, SP. Charles Mihinga(kushoto) akimtembeza Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini (CGP) Phaustine Kasike(kulia) alipotembelea gereza hilo leo Novemba 12, 2018.
 Baadhi ya Askari wa Gereza la Wilaya Njombe  wakifuatilia maelekezo katika Baraza lililoongozwa na  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike ambapo askari hao wameelezea changamoto zao kiutendaji leo Novemba 12, 2018.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa na askari wa Gereza Njombe( Picha na Jeshi la Magereza).



BENKI YA BIASHARA YA DCB YAZINDUA UUZWAJI WA HISA ZAKE KUANZIA LEO

0
0
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tano, Benjamin William Mkapa (kulia), akipokea hundi kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka baada ya kununua hisa za benki hiyo muda mfupi baada ya DCB kuzindua zoezi la uuzaji wa hisa kwa mwaka 2018, jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa.Uzinduzi huu unawalenga wanahisa waliopo, wawekezaji wapya na umma wa watanzania ikizingatiwa kuwa kwa mara ya mwisho DCB ilitoa fursa kama hiyo mwaka 2012.

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena leo wakati alipotangaza uuzaji rasmi wa hisa za benki hiyo wakati DCB ilipozindua zoezi la uuzaji wa hisa kwa mwaka 2018, jijini Dar es Salaam . Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa. Uzinduzi huu unawalenga wanahisa waliopo, wawekezaji wapya na umma wa watanzania ikizingatiwa kuwa kwa mara ya mwisho DCB ilitoa fursa kama hiyo mwaka 2012.



Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa uuzaji wa hisa za benki hiyoleo ambapo DCB imezindua zoezi la uuzaji wa hisa kwa mwaka 2018, jijini Dar es Salaam. kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Prof. Lucian Msambichakakulia , Uzinduzi huu unawalenga wanahisa waliopo, wawekezaji wapya na umma wa watanzania ikizingatiwa kuwa kwa mara ya mwisho DCB ilitoa fursa kama hiyo mwaka 2012.



Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Prof. Lucian Msambichakakulia na Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi mara baada ya uzinduzi wa uuzaji wa hisa za benki hiyo leo jijini Dar es salaam.

........................................................................................

UONGOZI wa Benki ya DCB umetangaza rasmi kuanzia leo Novemba 12 mwaka huu kuanza hisa zake kwa wanahisa wa sasa na umma wa Watanzania kwa ujumla na kwamba uuzaji wa hisa hizo umegawanyika kwenye awamu mbili.

Wakizungumza leo wakati wanatangaza uuzaji wa hisa hizo jijini Dar es Salaaam uongozi wa benki hiyo umesema hiyo ni fursa ya kipekee ambayo wanahisa na watanzania wote wanatakiwa kuichangamkia na kwamba hisa moja itauzwa kwa bei ya Sh.265 ambayo ni cheni ya bei iliyopo kwenye Soko la Hisa Dar es Salaam(DSE).

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Biashara ya DCB Godfrey Ngalahwa amesema kuwa "Nachukua nafasi hii kuwataarifu kuwa uuzaji wa hisa za DCB unatarajia kuanza leo 12 Novemba 12, 2018. na kwamba Novemba 5, 2018, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) ilitoa idhini ya uuzaji wa hisa kwa wanahisa wa sasa na umma wa Watanzania kwa ujumla.

"Dhana kubwa ni kuwaruhusu wanahisa waliopo kununua hisa na kutoa nafasi kwa wawekezaji wengine kununua hisa zitakazobaki. Uuzaji hisa za DCB umegawanywa katika awamu mbili, awamu ya kwanza itaanza leo hadi Desemba 3, 2018, ambapo hisa zitauzwa kwa wanahisa waliopo katika daftari la wanahisa. Aidha, kuanzia Desemba 4 hadi Desemba 18, 2018, hisa zote zitakazobaki zitauzwa kwa wanahisa waliopo na kwa wawekezaji wengine wasio wananhisa wa DCB. Kwa sasa, daftari limefungwa na mauzo ya hisa za DCB zilizopo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) yamesimamishwa kuanzia November 7 kupisha uuzaji wa hisa,"amesema.

Kuhusu utaratibu wa kushiriki kwa wanahisa Profesa amesema wanahisa watakaoshiriki ni wale walioorodheshwa katika Rejista ya Wanahisa baada ya kufungwa kwa jalada ili kupata idadi ya hisa stahili, Novemba 7 mwaka huu na kusisitiza mwanahisa ana haki ya kununua hisa moja kwa kila hisa mbili anazomiliki.

Aidha amesema wawekezaji wengine wanatakiwa kujaza fomu kuonesha idadi ya hisa watakazonunua na baada ya awamu ya pili kukamilika, watagawiwa kwa mujibu wa utaratibu utakaowekwa na uongozi wa benki na maelekezo ya waraka wa matarajio.Hivyo basi, wanahisa waliopo na wawekezaji wapya, wote wanaruhusiwa, kwa mujibu wa taratibu, kununua hisa zitakazobaki baada ya awamu ya kwanza kukamilika. Amefafanua malipo ya kununua Hisa za Haki yatafanyika kupitia matawi yote ya Benki ya Biashara ya DCB na mawakala wa Soko la Hisa la Dar es Salaam.

Akizungumzia mpango mkakati wa biashara ameseama kuwa kwa njia ya mashauriano, mwishoni mwa mwaka 2017, Benki ilikaa na kufafanua mpango wake wa biashara wa miaka mitano ambao utatekelezwa kwa awamu tatu na kwamba mafanikio yaliyopatikana kati ya Januari na Juni mwaka 2018 yametokana na kuweka msisitizo kwenye mabadiliko ya kiutendaji na kuhakikisha benki inapata faida.

"Kazi hii imekamilishwa ipasavyo na matokeo yake hadi Septemba 2018 benki imefanikiwa kupata faida ya TZS 1.4 bilioni. Mafanikio haya yametokana na kupungua kwa gharama za uendeshaji na kupunguza uwiano wa mapato na matumizi kutoka asilimia 104 mwaka 2017 hadi asilimia 81 mwaka 2018.Aidha, benki ilianzisha utaratibu wa kuboresha mtandao wa matawi na kutanua wigo wa bidhaa zilizopo na huduma kwa wateja ili kukuza mizania. Mikopo chechefu imedhibitiwa kwa kuanzisha mpango thabiti wa makusanyo ikiwa ni pamoja na kusuka upya idara ya mikopo,"amesema Ngalahwa.

Ameongeza benki hiyo inatarajia kufikia tarakimu moja ya mikopo chechefu mwishoni mwa mwaka 2019.Pia kuhakikisha benki inakuwa na wafanyakazi wenye maadili, utekelezaji wa programu ya mafunzo umefanyika na mchakato wa kuimarisha utamaduni wa utendaji unaendelea ambapo wafanyakazi wote wanahusika.Ameeleza mipango ya benki yao imekuwa kupata faida kabla ya kodi ya Sh.bilioni 1.8 ifikapo Desemba 2018. Katika kipindi hiki, mtaji wa benki unasimamiwa kwa uangalifu na ufanisi, huku hatua madhubuti za kukusanya mkopo na ufuatiliaji zinaendelea ili kupunguza mikopo chechefu huku tukizidi kukuza biashara.

"Mpango wa biashara uliorekebishwa wa miaka mitano unathibitisha matarajio ya benki kukuza mali zake kutoka Sh.bilioni 154.88 hadi Sh.bilioni 363.20 na amana za wateja kutoka Sh.bilioni 119.20 hadi Sh.bilioni 304.83. Kuhusu idadi ya wateja benki yetu imedhamiria kukuza mara mbili wateja wake mpaka 300,000 ifikapo mwaka 2022 huku ikiongeza masoko yake katika maeneo muhimu ya kimkakati,"amesema.

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya DCB Profesa Lucian Msambichaka amesema anayo furaha kubwa kuzindua rasmi uuzaji wa hisa leo Novemba 12, 2018 na kusisitiza . Uzinduzi huo unawalenga wanahisa waliopo, wawekezaji wapya na umma wa Watanzania kwa ujumla na kwamba hiyo ni fursa hii ni adimu kwa kuwa haitokei mara kwa mara ikizingatiwa kuwa mara ya mwisho, Benki ya DCB ilitoa fursa kama hii mwaka 2012.

"Kuhakikisha wananchi wengi wanapata fursa ya kuwekeza katika benki yetu, hisa hizi zitauzwa kwa bei punguzo ya Sh.265 sawa na punguzo la asilimia 22 ikilinganishwa na bei yake halisi iliyopo katika soko la hisa la Dar es Salaam ambayo ni TZS 340 kama ilivyonukuliwa tarehe 9th Novemba, 2018. Kila mwanahisa atapewa stahiki ya kununua hisa moja kwa kila hisa mbili alizonazo na mwekezaji mpya atatakiwa kuomba kununua hisa zitakazobaki. Uuzaji hisa za DCB umegawanywa katika awamu mbili, awamu ya kwanza itaanza leo hadi Desemba 3, 2018, ambapo hisa zitauzwa kwa wanahisa waliopo katika daftari la wanahisa. Aidha, kuanzia Desemba 4 hadi Desemba 18, 2018, hisa zote zitakazobaki zitauzwa kwa wawekezaji wengine wasio wanahisa wa DCB,"amesema.

Pia Profesa Msambichaka amesema Benki ya DCB inatarajia kuuza jumla ya hisa 33,913,948 ili kuongeza mtaji wa Sh. bilioni 8.9, mtaji huo utasaidia kuongeza uwezo wa benki sambamba na kuchochea ukuaji na mageuzi ya kibenki yatakayoifanya ijiendeshe kibiashara kikamilifu. Amesema benki ya DCB mpaka sasa ina jumla ya hisa 67,827,897 ambazo tayari zimeishanunuliwa na kulipiwa kikamilifu na kiasi cha mtaji uliolipiwa kuhusiana na hisa hizo ni Sh.bilioni 16.96. Utoaji huo wa hisa mpya utafikisha idadi ya hisa kwa ujumla kuwa 101,741,845.Bodi ya wakurugenzi itapitia kwanza maombi ya wanahisa waliopo kabla ya kugawa hisa kwa wengine walioomba kwa mujibu wa sheria na utaratibu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA).

Amesema wanahisa wa sasa na watarajiwa watafaidika na uwekezaji huu kutokana uuzaji wa hisa kwa bei pungufu ukilinganisha na bei ya soko huku wakiwa na kumbukumbu kuwa ni miongoni mwa fursa adimu zinazoweza kuwaongezea umiliki katika benki kwa kununua hisa mpya. Aidha, thamani ya kila mwanahisa inaweza kuongezeka kutokana na ukuaji wa bei ya hisa unaosukumwa zaidi na ukuaji wa biashara na nguvu ya hisa za benki katika soko la hisa. Vilevile mwanahisa atapata gawio kila mwaka kulingana na mwenendo wa kibiashara wa benki.

WATALAAM KUTOKA MUHIMBILI WAWASILI LINDI KUTOA HUDUMA ZA AFYA

0
0
Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Lindi Sokoine kwa ajili ya kutoa huduma za afya na kuwajengea uwezo watalaam wa hospitali hiyo.
Madaktari Bingwa wa MNH pamoja na Madaktari wa Hospitali ya Sokoine wakiwa katika kikao cha asubuhi cha kiutendaji kabla ya kuanza kutoa huduma.
Wauguzi wa hospitali hiyo wakiwa katika kikao cha asubuhi kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali ya utoaji huduma za afya.

Daktari Bingwa wa magonjwa ya kike na uzazi Geofrey Marandu akizungumza na mgonjwa ambaye amefika leo katika Hospitali ya Sokoine kwa ajili ya kupata huduma.

Dokta Willybroad Massawe ambaye ni Dkt. wa upasuaji , pua , koo na masiko  (kushoto) pamoja na muuguzi Monica Mngoya (kulia) wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakimpatia maelezo mgonjwa ambaye amefika kwa ajili ya kupata huduma za afya.

Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Lindi ambao wamejitokeza katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Lindi Sokoine wakisubiri kupatiwa huduma hii leo.




LIND, MADAKTARI 


Madaktari Bingwa 11 pamoja na wataalam wengine wa afya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH) wamewasili katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Lindi Sokoine kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali za afya kwa wananchi wa mkoa huo sanjari na kuwajengea uwezo wataalam wa hospitali hiyo.

Daktari Bingwa wa magonjwa ya kike na uzazi kutoka MNH Geofrey Marandu amesema lengo la ujio wao katika hospitali hiyo ni kuwaongezea ujuzi watalaam wa hospitali za rufaa za mikoa nchini kupitia madaktari bingwa wa Muhimbili lakini pia kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa Muhimbili.

‘’Hospitali imeweka mkakati wa kuzitembelea hospitali mbalimbali za rufaa za mikoa nchini ili kushirikiana nao katika kutoa huduma za afya na kuwajengea uwezo , lakini pia kama Muhimbili tunatekeleza agizo la serikali linaloelekeza kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibwa nje ya nchi hatua ambayo tayari MNH inaitekeleza hivyo utoaji wa huduma za fya kwa njia ya mkoba utasaidia kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda Muhimbili endapo wangepewa rufaa ya kwenda kutibiwa huko’’.amesema Dkt. Marandu.

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine Dkt. Jumanne Shija amesema ujio wa watalaam wa afya wakiwemo Madaktari Bingwa utainufaisha hospitali hiyo kwakua watalaam wake watajengewa uwezo kiutendaji na kupata ujuzi wa kutosha.

Ametaja maeneo ambayo wataalam wa hospitali ya Sokoine watanufaika na kujengewa uwezo ni upasuaji, magonjwa ya kike na uzazi, meno, macho, watoto, magonjwa ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya koo ,pua na masikio pamoja na masuala ya maabara.

‘’Hii ni neema imetufikia watu wa Lindi natoa wito kwa wananchi wa mkoa huu na wale wa maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi kuja kupata huduma, madaktari bingwa wamekuja ni lazima tuwatumie ili na tunufake na huduma za kibingwa zitakazotolewa kwa kipindi cha wiki moja watakachokuwepo hapa ‘’. amesema Dkt.Shija.

Kwa upande wao wananchi ambao wamejitokeza kupata huduma wameelezea kufurahishwa na ujio wa watalaam wa afya kutoka Muhimbili na kueleza kuwa ujio wao ni faraja kwa wananchi wa Lindi kwani watapata huduma za afya wakiwa katika maeneo yao na itawapunguzia gharama endapo wangepata rufaa kwenda Muhimbili kwakua ingewalazimu watumie gharama kubwa za usafiri na mahitaji mengine muhimu.

Lawrence Masha Ateuliwa Kuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Fastjet Tanzania

0
0

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Fastjet Tanzania, Capt. Arif Jinnah(kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo kuhusu uteuzi mpya wa Mwenyekiti Mpya wa Fastjet Tanzania Lawrence Masha. Pichani wengine ni Mwenyekiti Mtendaji Mpya wa Fastjet Tanzania, Lawrence Masha na Mkuu wa Mahusiano ya Kiserikali wa Fastjet Tanzania, Eng. August Kowero.
Mwenyekiti Mtendaji Mpya wa Shirika la Ndege Fastjet Tanzania, Lawrence Masha akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo kuhusu uteuzi wake wa kuwa mwenyekiti wa shirika hilo. Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Fastjet Tanzania, Capt. Arif Jinnah na kushoto ni Mkuu wa Mahusiano ya Kiserikali wa Fastjet Tanzania, Eng. August Kowero.

……………

Kati ya mashirika ya ndege yanayokua kwa kasi zaidi, Fastjet Airlines Ltd, Tanzania, leo imethibitisha mikakati ya kumiliki shirika hilo yanaenda vizuri.

Tarehe 6 Novemba Fastjet ilimteua Ndugu Lawrence Masha kuwa Mwenyekiti Mtendaji wa kwanza wa shirika hilo. Uteuzi huu umedhibitisha nia ya kuendelea kuhudumia soko la ndani na nje ya nchi kama kampuni inayomilikiwa na Watanzania pamoja na masoko ya talii za nje.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam Ndugu Masha alisema, “ tumejikita zaidi kwa watanzania ambao wamefaidika kutokana na huduma zetu kwa miaka sita sasa. Tunatarajia kuongeza kuongeza safari za ndani na pia kuongeza idadi ya ndege ambazo zinakidhi mahitaji ya soko”. 
 
Tunaona fursa kufanya kazi na kushirikiana na mashirika ya ndege za ndani na nje ya nchi pamoja na Air Tanzania kutimiza mikakati ya serikati ya utalii.Ndugu Masha ataendeleza vizuri na mikakati ya kubadilisha shirika hilo pamoja na uongozi kuhakikisha wanatoa huduma kwa watanzania.

Fastjet imetoa huduma kwa miaka sita ambapo imesafirisha zaidi ya abiria milioni 2.5 ndani ya Tanzania pekee.Shirika hili lenye bei nafuu lina hudumia usafiri wa ndege katika miji ya Dar es salaam, Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro, Lusaka na Zimbabwe. Na linarekodi ya kusafirisha wastani wa abiria 30,000 kwa mwezi.

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI SABA (7) IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya kuwaapisha Viongozi saba wakiwemo Mawaziri wawili, Naibu Mawaziri wanne, pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mwita Waitara kuwa Naibu Waziri  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Joseph Kakunda kuwa Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Mary Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri wa ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Constantine Kanyasu kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Japhet Ngailonga Hasunga kuwa Waziri wa Kilimo Ikulu jijini Dar es Salaam huku Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma wakishuhudia tukio hilo. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Innocent Bashugwa Naibu Waziri wa Kilimo Ikulu jijini Dar es Salaam huku Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma wakishuhudia tukio hilo. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Mstaafu January Msofe kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria.
 Viongozi mbalimbali waliopishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakila Kiapo cha Uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam. Wakwanza kulia ni Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda, Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga, Naibu Waziri wa ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Mary Mwanjelwa, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu, Naibu Waziri wa Kilimo Innocent Bashugwa, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mwita Waitara pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Mstaafu January Msofe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ngugai, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Kamishna wa Maadili Tume ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela pamoja na Viongozi mbalimbali waliopishwa pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU

MWENYEKITI UVCCM AFUNGUA SEMINA YA KIMKAKATI KWA VIONGOZI NA WATENDAJI WAKE

0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chma Cha Mapinduzi Ndg Kheri Denis James akizungumza wakati akifungua Semina ya Kimkakati ya Siku Saba kwa Viongozi na Watendaji wa UVCCM Ngazi ya Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa UVCCM akizungumza wakati wa Kumkaribisha Mwenyekiti kufungua Semina hiyo
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mwl Raymond Mwangwala akitoa Ufafanuzi kuhusu lengo la Mafunzo haya.
Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Comred Peter Kasera akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Comred Kheri James akizungumza jambo na Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Comred Hassan Bomboko katika Ufunguzi wa Semina ya Kimkakati ya Siku Saba kwa Viongozi na Watendaji wa UVCCM Ngazi ya Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dodoma.
Sehemu ya Wakuu wa Idara wakifuatilia Katikati ni Comred Hassan Bomboko Mkuu wa Idara ya Uhamaishaji na Chipukizi,(Kulia)Comred Khamana Juma Simba Mkuu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Pamoja na Comred Nelson Lusekelo Mkuu wa Idara ya Uchumi na Uwezeshwaji.
 Baadhi ya Watendaji waliohudhuria Semina wakifuatilia
 Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanao tokana na Vijana wakifuatilia
 Sehemu ya Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi wakifuatilia semina
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Comred Kheri Denis James (kulia|) pamoja na Makamu Mwenyekiti Comred Thabia Mwita  wakifurahia jambo pamoja na Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Comred Hassan Bomboko leo mara baada ya Ufunguzi waSemina ya Kimkakati ya Siku Saba kwa Viongozi na Watendaji wa UVCCM Ngazi ya Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dodoma.(Picha zote na Fahadi Siraji wa Uvccm)
Picha ya Pamoja ya Viongozi washiriki wa Semina ya Kimkakati ya Siku Saba kwa Viongozi na Watendaji wa UVCCM Ngazi ya Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani leo jijini Dodoma. (Picha zote na Fahadi Siraji wa Uvccm)

MAHAKAMA YAMPA NAFASI YA MWISHO MBUNGE MSIGWA KUTAFUTA WAKILI WA KUMTETEA

0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa nafasi ya Mwisho kwa Mshtakiwa Peter Msigwa ambaye in Mbunge wa Iringa Mjini kutafuta wakili wa kumtetea katika kesi ya uchochezi inayomkabili pamoja na viongozi wenzake nane wa Chadema ma sivyo, Mahakama itaendelea na usikilizwaji wa kesi hiyo bila uwepo wa wakili wake.

Msigwa pia ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa anatukanwa Kisheria na mawakili wa upande wa mashtaka kwa sababu mawakili wake wanajitoa kumtetea.Hatua hiyo imefikwa leo Novemba 12. 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuanza kwa usikilizwaji wa upande wa mashtaka ambao walidai mahaka
mani hapo kuwa wako tayari kwa kuendela na hatua hiyo na kwa leo walikuwa na shahidi mmoja.

Msigwa amepewa nafasi hiyo ya mwisho baada ya wawakili wake wawili waliokuwa wawili waliokuwa wakimtetea kujitoa kwa madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa kesi.Mchungaji Msigwa ameeleza hayo baada ya wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi kudai kuwa inaonekana Msigwa amepanga njama ili mawakili wake wajitoe.

Kutokana na hatua hiyo, Msigwa alisimama na kueleza kuwa anaona Wakili wa Serikali kama anamtukana kisheria na kumnyanyapaa."Hakimu wewe ni shahidi mawakili wangu wamejitoa kwa sababu ya kutoridhishwa na mwenendo wa kesi, wakili wa serikali hana haki wala haimuhusu kuhusu mawakili wangu,"ameeleza.Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Mashauri amesema ni haki ya Kikatiba kwa mshtakiwa kuwakilishwa na Wakili, lakini anatoa nafasi ya mwisho kwa Msigwa na akishindwa ataonekana amefanya makusudi na kesi itaendelea bila ya yeye kuwa na wakili

.Kesi imeahirishwa hadi November mshtakowa 23 2018. Msigwa ametakiwa siku hiyo kuwa na wakili.Mbali na Msigwa, washtakiwa wengine ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya, na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji, Esther Matiko na mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari 1 na 16, 2018, Dar es Salaam.

AccessBank yazindua akaunti maalum kwa mwanamke inayoitwa Lulu

0
0

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Bi. Jokate Mwegelo akizungumza wakati wa uzinduzi wa akaunti ya akiba ya wanawake inayoitwa LULU iliyozinduliwa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye ukimbi wa Kisenga Makumbusho jijini Dar es salaam, LULU ni akaunti mahsusi kwa mwanamke anaejua malengo yake ya kimaisha iliyoanzishwa na AccessBank Tanzania.
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Bi. Jokate Mwegelo akiwa jukwaani mara baada ya kuwasili ukumbini kutoka kulia ni Bi. Maida Waziri Mkurugenzi wa Kampuni ya Ibra Constructiors Limited, Grace Metta kutoka AccessBank Tanzania na kushoto ni Jennifer Bash Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Alaska Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa AccessBank Tanzania Bw.Armando Massimiliano Sirola akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa Akaunti ya Lulu iliyozinduliwa mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa Kisenga jijini Dar es salaam.
Bi. Maida Waziri Mkurugenzi wa Kampuni ya Ibra Constructiors Limited akitoa mada wakati wa uzinduzi wa akaunti hiyo.
Namala Rwebandiza MC wa uzinduzi huo akizungumza na waalikwa.
Baadhi ya wafanyakazi wa AccessBank Tanzania wakiwa katika uzinduzi huo

Grace Metta Company Cecretary kutoka AccessBank Tanzania akizungumza na akina mama na akina dada waliofika kwenye uzinduzi wa akaunti ya LULU.
Jennifer Bash Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Alaska Tanzania akitoa mada kwa akina mama waliofika kwenye uzinduzi huo.
Mkuu wa Huduma AccessBank Tanzania Bw.Andrea Ottina akigawa fulana kwa akina mama waliokuwa tayari kufungua akaunti ya LULU wakati wa uzinduzi huo.
Baadhi ya akina mama na akina dada waliofika kwenye uzinduzi wa akaunti ya LULU iliyoanzishwa na AccessBank Tanzania uliofanyika kwenye ukumbi wa Kisenga jijini Dar es salaam.



Katika kuendelea kuwajali wateja wake AccessBank Tanzania imezidi kuboresha huduma zake, kwa kuongeza akaunti ya akiba ya wanawake inayoitwa LULU . Akaunti hii ilizinduliwa na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo jumamosi tarehe 10 Novemba 2018 ukimbi wa Kisenga International Conference Centre.

Akizungumza katika uzinduzi huo DC Mwegelo amesema "LULU ni akaunti mahsusi kwa mwanamke (anaye jithamini) anaejua malengo yake ya kimaisha, anaeona mbele na kupanga kwa ajili ya baadae yake. Akaunti hii imebuniwa ikiwa na mpango mzuri wa kujiwekea akiba na kumfanya mwanamke kutimiza malengo yake, hivyo kumsaidia kusonga mbele kiuchumi".

Mh. Jokate Mwegelo amesema LULU ambayo ni maalumu kabisa kwa mwanamke. ni akaunti maalum kwa akina mama na pia itakua mkombozi kwao kwani wanawake waliowengi wataweza sasa kujiwekea akiba kwa muda maalumu hivyo kusaidia kutimiza malengo waliyojiwekea.

Lengo la akaunti hii ni kumwezesha mwanamke kufikia malengo yake,kama tunavyojua mwanamke ndio kila kitu katika jamii na anapofanikiwa na pia Jamii nzima itafanikiwa. Mwanamke anapokua na uwezo wa kutatua matatizo yakifedha, basi familia au Jamii husika inakua imeondokana na kadhaa nyingi. Niwapongeze AccessBank Tanzania kwamba moja wapo ya faida ya akaunti hii ni; Mtapata fursa ya kuhudhuria mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali yatakayokuwa yakitolewa na benki hii kupitia wakufunzi mbalimbali ambao benki itawaandaa kama hawa waliopo leo. Mwisho kabisa nirudie kuwapongeza tena AccessBank Tanzania kwa kua miongoni mwa mabenki machache nchini yenye huduma maalumu kwa ajili ya Wanawake. Jambo hili linaonyesha jinsi gani Wanawake tulivyo na umuhimu katika Jamii yetu. Baada ya kusema hayo machache, basi nitangaze rasmi kwamba akaunti hii ya LULU imezinduliwa rasmi leo hii siku ya Jumamosi, tarehe 10 November 2018

Akizungumzia maendeleo ya Akaunti hiyo Mkuu wa Idara ya Opereshani wa AccessBank Tanzania Ndugu Andrea Ottina alisema, “AccessBank Tanzania kwa kua miongoni ya Taasisi yakifedha ambayo imekuwa ikiwajali na kuwathamini wananchi, hasa wale wenye kipato cha chini pamoja na wafanya biashara wadogo na wakati, ambao wengi wao wanaonekana kuwa hawana vigezo na hivyo kutengwa na taasisi za kifedha. 
Jambo hili AccessBank Tanzania wameliona, na wao kuwa miongoni mwa Taasisi inayowakumbuka na kuwawezesha wananchi wa aina hii kwa kuwaletea huduma zakifedha kulingana na maitaji yao. Na pia haijawaaacha akina mama na vijana wakike ambao miongni mwao wamekuwa wakijihusisha na biashara ndogo ndogo ili kukidhi maisha yao ya kila siku.”

AccessBank Tanzania ni taasisi ya kifedha inayolenga kutoa huduma za kibenki kwa wajasiriamali wadogo na wa kati kupitia wanahisa wake wa kimataifa ambao ni AccessHolding, International Finance Corporation (Word Bank), KfW, African Development Bank na MicroVest, maono ya benki ni kujidhatiti katika uanzishaji wa mifumo ya kifedha inayochochea maendeleo ya jamii kwa kutoa huduma zilizobora kwa watu wote.

RAIS DKT MAGUFULI AHUDHURIA MISA YA SHUKURANI YA UHAI YA RAIS MSTAAFU BENJMANIN MKAPA KUTIMIZA UMRI WA MIAKA 80

0
0



Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimpa zawadi ya kadi na kisha kumpongeza Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa akiwa na mkewe Mama Anna Mkapa kwa kutimiza umri wa miaka 80 katika Misa ya Shukurani ya uhai iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Imakulata jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2018
Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa pamoja na Maaskofu wakati wa Misa ya Shukrani kwa Mhe. Mkapa kutimiza umri wa miaka 80 katika kanisa la Mtakatifu Imakulata jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2018
Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiongea kwa furaha na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa baada ya Misa ya Shukurani kwa Mhe. Mkapa kutimiza umri wa miaka 80 katika kanisa la Mtakatifu Imakulata jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2018
Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakishiriki katika Misa ya Shukurani ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa kutimiza umri wa miaka 80 katika kanisa la Mtakatifu Imakulata jijini Dar es salaam leo Novemba 12, 2018. Kulia kwa Mhe. Mkapa ni mkewe Mama Anna Mkapa

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA WILAYA YA SAME NA MWANGA LEO

0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Cleopa David Msuya (kulia) muda mfupi kabla ya mkutano wa hadhara na wananchi wa Wilaya ya Mwanga. Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Kilimanjaro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Cleopa David Msuya (kulia) muda mfupi kabla ya mkutano wa hadhara na wananchi wa Wilaya ya Mwanga. Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Kilimanjaro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Cleopa David Msuya (katikati) muda mfupi kabla ya mkutano wa hadhara na wananchi wa Wilaya ya Mwanga kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira . Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Kilimanjaro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Cleopa David Msuya (katikati) muda mfupi kabla ya mkutano wa hadhara na wananchi wa Wilaya ya Mwanga. Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Kilimanjaro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Clelia Felician wa kampuni ya M.A Kharafi & Sons wakati alipotembelea mradi mkubwa wa maji wa Same – Mwanga – Korogwe ambao awamu ya kwanza imekamilika kwa asilimia 76%. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Sehemu ya Miundombinu ya Mradi wa Maji Same-Mwanga-Korogwe ambao asilimia 76% imekamilika.
Sehemu ya Miundombinu ya Mradi wa Maji Same-Mwanga-Korogwe ambao asilimia 76% imekamilika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji Same-Mwanga-Korogwe. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema hakuna Maendeleo pasipo Utawala bora.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mwanga mkoani Kilimanjaro.

“Viongozi wa Halmashauri, Viongozi wa Wilaya wasipokuwa na Utawala bora, wasiposhirikiana, Chama, Serikali, Wilaya, Halmashauri tusitegemee kuwa na maendeleo tutalalamika siku zote” alisema Makamu wa Rais. Leo katika ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo Makamu wa Rais alitembelea miradi mbali mbali katika Wilaya ya Same na Mwanga.

Akiwa Wilayani Same, Makamu wa Rais aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari ya New Dawn, Shule ambayo itakuwa ya mchepuo wa masomo ya sayansi na ni maalum kwa Watoto wenye mahitaji maalum na Yatima pamoja na kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa ofisi za Wakala wa Misitu Wilaya ya Same.

Makamu wa Rais amewahimiza Wakala wa Misitu nchi kuwapa wananchi miche ya kutosha na kuimarisha ulinzi katika hifadhi ya misitu. Akiwa Wilayani Mwanga, Makamu wa Rais aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji Same-Mwanga-Korogwe ambao awamu ya kwanza imekamilika kwa asilimia 76%.

Akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa amesema kwa sasa awamu ya kwanza ambayo ni Miundombinu ya mradi huo imekamilika kwa asilimia 76% na umegharimu bilioni 94.65 ambapo awamu ya pili itakuwa usambazaji wa maji Same na awamu ya tatu itakuwa usambazaji wa maji Mwanga. “Serikali imejipanga kila eneo ambalo maji yanapita wananchi watafaidika na maji hayo” alisema Waziri wa Maji.

Kwa upande wake Makamu wa Rais alisema Serikali imedhamiria kutatua tatizo la maji nchi na kuwataka wananchi kutambua kuwa miradi hii ya maji ina gharama kubwa hivyo inabidi wawe walinzi wazuri wa miundombinu ya maji.

Katika ziara hiyo Wilayani Same na Mwanga Makamu wa Rais ameongozana na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Wiliam Lukuvi.

MATUKIO YA PICHA KUTOKA BUNGENI JIJINI DODOMA LEO

0
0

Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Andrew Chenge akiongoza kikao cha tano cha Mkutano wa 13 wa Bunge leo jijini Dodoma. (Picha na: Frank Mvungi –MAELEZO)
Baadhi ya mawaziri wakijadiliana jambo Bungeni wakati kikao cha Bunge kikiendelea leo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akifafanua jambo wakati akijibu swali la Mhe. Asha Jecha(hayupo pichani) kuhusu ukatili wa watoto leo katika kikao cha tano cha Mkutano wa 13 wa Bunge jijini Dodoma leo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akijibu swali kuhusu mikakati ya Serikali kuimarisha sekta ya michezo nchini wakati wa kikao cha tano Mkutano wa 13 wa Bunge leo jijini Dodoma.
Mbunge wa Hanang’I Mhe. Mary Nagu akichangia hoja kuhusu Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa mwaka 2019/2020 katika kikao cha tano Mkutano wa 13 wa Bunge leo jijini Dodoma.
Baadhi ya wageni waliotembelea Bunge wakati wa kikao cha tano cha Mkutano wa 13 wa Bunge wakifuatilia michango ya wabunge leo jijini Dodoma.

Msaada wa Tshs. 86 Mil kunufaisha Wagonjwa wa Saratani ya Koo Muhimbili

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Hopitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akipokea kifaa tiba cha aina ya STENTS kwa ajili ya wagonjwa wenye tatizo la saratani ya koo la chakula kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Boston Scientific ya Marekani, Troy Lengel. Wengine kushoto ni wawakilishi kutoka hospitali ya Muhimbili, Mayo Clinic ya Marekani na Chuo Kikuu cha San Francisco nchini Marekani na kulia ni wawakilishi kutoka MUHAS na Hospitali ya Muhimbili.
Pichani ni vifaa tiba aina ya STENTS ambavyo wagonjwa wenye tatizo la saratani ya koo la chakula wameanza kuwekewa ili kuwasaidia kumeza chakula kutokana na mfumo wa koo kuharibiwa na ugonjwa huo. 

…………………. 

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa vifaa tiba aina ya Stents vyenye thamani ya Tshs. 86.2 milioni kutoka kampuni ya Boston Scientific ya Marekani kwa ajili ya wagonjwa wenye tatizo la saratani ya koo la chakula. 

Stents ni vifaa maalum mithili ya springi ambavyo vinaweza kuwa vya plastiki au chuma vyenye uwazi katikati wanavyowekewa wagonjwa wenye uvimbe kwenye koo lililoziba ili kupanua sehemu hiyo na kuruhusu kupitisha chakula. Kuna stents za aina mbalimbali kutegemeana na mgonjwa ana shida ya aina gani. 

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini, Dkt. Masolwa Ng’wanasayi amesema kampuni hiyo imetoa stents 25 ambazo zitatumika kwa wagonjwa 25 wenye satarani ya koo la chakula ili kuwasaidia kumeza chakula na kuendelea na matibabu ya mionzi. 

“Mgonjwa mwenye tatizo la saratani ya koo la chakula, anakuwa hawezi kumeza chakula na hali hii inasababisha mgonjwa kupungua uzito na kushindwa kuendelea na matibabu mengine, hivyo vifaa hivi vitawasaidia kumeza chakula na kuendelea na matibabu mengine,” amesema Dkt. Ng’wanasayi. 

Amesema kifaa tiba (Stent) kimoja hivi sasa kinauzwa Tshs. 3.4 milioni na kwamba kampuni hiyo imeahidi kupunguza bei hadi kufikia dola 100 za Marekani kwa kifaa tiba kimoja sawa na Tshs. 230,000. 

“Wameahidi kwamba watapunguza gharama za vifaa tiba hadi kufikia dola 100 za Marekani. Lengo ni kuhakikisha wagonjwa wengi wenye tatizo la saratani ya koo wanapatiwa matibabu,” amesema Dkt. Ng’wanasayi. 

Leo wagonjwa tisa wenye tatizo la saratani ya koo la chakula wamepatiwa matibabu ya kuwekewa kifaa hicho na baada ya matibabu hayo wameweza kumeza chakula vizuri na hivyo kurejea kwenye hali zao za kawaida. 

Kwa muda wa miaka miwili, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) na Hospitali ya Ocean Road kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani ya Marekani, Chuo Kikuu cha San Francisco nchini Marekani na Kampuni ya Boston Scientific ya Marekani wamekuwa wakifanya utafiti wa kutumia kifaa tiba hicho kwa wagonjwa wenye tatizo la saratani ya koo la chakula. Utafiti huo, umebainisha kwamba matumizi ya kifaa hicho kimekuwa msaada mkubwa kwa wagonjwa wenye tatizo la saratani ya koo la chakula.

WATUHUMIWA WA MAUAJI WAWILI, WANAODAIWA KUMUUA KWA KUMPIGA RISASI MFANYABIASHARA VICENT KISHA KUMPORA MALI ZAKE WAKAMATWA -WANKYO

0
0
 NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 

JESHI la polisi mkoani Pwani, limewakamata watuhumiwa wawili wa mauaji ya Vicent Paulo mkazi wa Lugoba, Chalinze ambao walimvamia na kumpiga risasi kichwani kisha kumpora mali za dukani kwake. 

Aidha jeshi hilo limekamata madumu 30 ya mafuta ya kula aina ya mico gold ambayo hayakulipiwa ushuru kupitia bandari bubu zilizopo Bagamoyo. 

Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo, kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Wankyo Nyigesa ,alieleza majina ya watuhumiwa wanaodaiwa kufanya mauaji hayo yamehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Alisema, mnamo july 31 mwaka huu walimvamia Vicent ambae sasa ni marehemu akiwa dukani kwake na kumpiga risasi na kupora baada ya tukio walitoroka kwenda kujificha Handeni Tanga. 

“Jeshi la polisi lilipata taarifa kutoka kwa wasamalia wema na kufanikiwa kuwakamata wote wawili usiku wa kuamkia novemba 12 na wenzao ambao wanaendelea kuhojiwa “baadhi tayari wamekubali kuhusika na mauaji hayo na wizi “alieleza Nyigesa. 

Kuhusu kukamatwa kwa magendo mafuta aina ya mico gold dumu 30 yalikutwa yamepakiwa kwenye gari lenye namba za usajili T. 946 DFX aina ya nissan ambae dereva wake alikimbia baada ya kubaini kuwa askari waliokuwa doria katika mwambao wa bandari bubu na kumsimamisha. Nyigesa alifafanua, ghafla alisimamisha gari lake na kukimbia kusikojulikana na akalitelekeza gari hilo na mafuta. Alielezea jeshi hilo linamsaka dereva huyo la sivyo ajisalimishe mwenyewe kituo chochote cha polisi. 

Kamanda huyo alitoa wito wafanyabiashara kuacha kujihusisha na biashara za magendo na ukwepaji wa ushuru, kwani kwasasa ndani ya mkoa huo watambue kwamba hawapo salama na wamejipanga kutindua mitandao ya wafanyabiashara wa aina hiyo.
Maofisa wa Jeshi la Polisi wakichunguza madumu  30 ya mafuta ya kula aina ya mico gold ambayo yanadaiwa kutolipiwa ushuru kupitia bandari bubu zilizopo Bagamoyo. 
Viewing all 46200 articles
Browse latest View live




Latest Images