Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1722 | 1723 | (Page 1724) | 1725 | 1726 | .... | 1898 | newer

  0 0


   Dereva wa Bohari ya Dawa (MSD), Mkoa wa Mtwara, Bonventure Chacha Magesa, akishusha maboksi ya dawa kwenye Zahanati ya Kijiji cha Minyembe kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara DC mkoani Mtwara jana.
   Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Minyembe, Seleman Ismail (kulia), akisaidia na Wajumbe wa Kamati ya Afya wa Kijiji cha Minyembe kubeba maboksi ya dawa wakati wakizipokea kutoka MSD. Katikati ni Afisa Mtendaji wa kijiji hicho, Salum Dalanga na Mstafa Chindutu.
   Afisa Mtendaji wa kijiji hicho, Salum Dalanga, akipanga maboksi yenye dawa.
  Afisa Huduma kwa Wateja wa MSD, Florida Sianga (kulia),akisaidia kupanga dawa kabla ya kuzikabidhi.

   Dawa na mikoba maalumu yenye vifaa vya kujifungulia wajawazito ikipangwa kabla ya makabidhiano katika Zahanati ya Minyembe.
   Afisa Huduma kwa Wateja wa MSD Mkoa wa Mtwara, Larisa Manyahi (kushoto), akikabidhi dawa kwa wajumbe wa kamati ya afya wa Kijiji cha Minyembe.
   Mkazi wa Kijiji cha Mkutimango, Mussa Nkala, akizungumzia upatikanaji wa dawa katika zahanati ya kijiji hicho.
   Muuguzi wa Zahanati ya Mkutimango, Farida Mchopa akisaidia kupokea boksi la dawa kutoka kwa Dereva wa Bohari ya Dawa (MSD), Mkoa wa Mtwara, Bonventure Chacha Magesa.
   Afisa Huduma kwa Wateja wa MSD Mkoa wa Mtwara, Larisa Manyahi (kushoto), akisaidia kuhesabu mifuko maalumu yenye vifaa vya kujifungulia wajawazito kabla ya kuikabidhi Zahanati ya Mkutimango.
  Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mkutimango, akizungumzia upatikanaji wa dawa katika zahanati hiyo.

  Na Dotto Mwaibale, Mtwara DC

  WANANCHI wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara DC wameipongeza Serikali kwa kuwapekea dawa, vifaa tiba na vitendanishi jambo ambalo limewaondolea usumbufu wa kupata matibabu wanapoumwa.

  Pongezi hizo walizitoa kwa nyakati tofauti wilayani humo jana wakati wakizungumza na waandishi wa habari pamoja na maofisa wa Bohari ya Dawa (MSD), katika vijiji vya Mkutimango na Minyembe ambao wanawatembelea wateja wao kujua changamoto zao ili kuzitafutia ufumbuzi.

  Mkazi wa Kijiji cha Mkutimango, Mussa Nkala alisema anaipongeza MSD na Serikali kwa kufanikisha kuwafikishia dawa kwa wakati tofauti na miaka ya nyuma ambapo walikuwa wakilazimika kwenda kuzinunua katika maduka ya watu binafsi.

  " Watu katika familia yangu wakiumwa huwa nawaleta kutibiwa katika Zahanati yetu hii Mkutimango na hakuna siku waliyokosa dawa ingawa mimi mwenyewewe nikiumwa natumia dawa za asili kujitibu" alisema Nkala.

  Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mkutimango alisema hapo awali waliweka utaratibu wa wananchi wakiumwa wanakwenda kumuita nyumbani kwake na yeye uwasindikiza kwenda kutibiwa kwenye zahanati hiyo kwa ajili ya usalama wa wauguzi na dawa na vifaa vingine.

  "Zamani tuliweka utaratibu huo lakini hivi sasa baada ya kupata mlinzi huwa wanaenda moja moja kutibiwa bila ya kupitia nyumbani kwangu" alisema.

  Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa yeye na familia yake wanapoumwa huwa wanaenda kutibiwa kwenye zahanati hiyo na kuwa miezi michache iliyopita alijikata kidoleni na panga ambapo alipatiwa matibabu kwa haraka na sasa amepona jereha hilo.


  Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Minyembe, Salum Dalanga alisema hivi sasa hakuna changamoto ya upatikanaji wa dawa kwenye zahanati hiyo dawa na mahitaji mengine yanayohusu afya yanapatikana.

  Mjumbe wa Kamati ya Afya ya Kijiji cha hicho, Mstafa Chindutu alisema mara kwa mara wamekuwa wakipokea dawa kutoka MSD na kuzipokea kwa utaratibu uliopo na orodha ya dawa zote wanazozipokea na thamani yake hubandikwa kwenye ubao wa zahanati hiyo ili kila mwananchi aweze kuona.

  Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo ya Minyembe, Seleman Ismail alisema dawa zote muhimu  wamekuwa wakizipata kwa wakati na hawajawahi kupungukiwa kutokana na utaratibu waliojiwekea wa kutoa oda pale wanapoona zinapungua na kuwa katika eneo hilo ugonjwa unaosumbua zaidi ni malaria.

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Jully Maleko alisema hivi sasa upatikanaji wa dawa vifaa tiba na vitendanishi vya maabara mkoani humo ni asilimia 97 ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo ilikuwa  chini ya asilimia 40.

  Ofisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka alitoa mwito kwa vituo vya afya, zahanati na Hospitali mkoani humo kujiunga na mfumo maalum wa kieletroniki utakao wasaidia kujua upatikanaji wa taarifa muhimu za upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na bei zake, taarifa za akaunti zao na taratibu za maombi ya bidhaa wanazo hitaji kutoka MSD. 

  Alisema mfumo huo unajulikana kama“MSD-Customer Portal” unaweza kutumika na wateja wake popote walipo nchini na kuwaondolea usumbufu waliokuwa wakiupata awali wakati wakuagiza dawa, ambapo ili walazimu kusafiri ofisi za Kanda ya MSD inayowahudumia au kupiga simu ili kupata taarifa hizo na nyinginezo.


  0 0


  Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akipokea mojawapo ya Mashine maalum ya kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya kufikisha miezi tisa iliyotolewa na Benki ya Diamond Tust kwa Hospitali ya Wilaya ya Kongwa jana. (Picha na Ofisi ya Bunge).
  Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akitoa shukrani kwa Benki ya Diamond Tust mbele ya Waandishi wa Habari mara baada ya kupokea Mashine maalum ya kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya kufikisha miezi tisa iliyotolewa na Benki hiyo kwa Hospitali ya Wilaya ya Kongwa.
  Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akisikiliza maelezo kutoka kwa mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation Ndg. Doris Mollel kuhusiana na picha inayoonyesha mtoto aliyezaliwa kabla ya muda wake. Taasisi hiyo ikishirikiana na Benki ya Diamond Trust walitoa msaada wa Mashine maalum ya kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya kufikisha miezi tisa kwa Hospitali ya Wilaya ya Kongwa hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Bibi Sifaeli Kundashuma ambaye ni mmoja walioshiriki katika tukio la kuchanganya mchanga wakati wa Muungano wa Tanzanyika  na Zanzibar.Makamu wa Rais yupo wilayani Hai kwa ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) .
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi mara baada ya kufungua wodi ya Wanawake katika hospitali ya wilaya ya Hai. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0

  Na WAMJW, Dar es Salaam.

  KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa moja ya sababu za ajali barabarani, ni uchovu wa madereva.

  Dkt. Mpoki ameyasema leo Novemba 13,2018 wakati wa kufungua mafunzo ya watoa huduma za tiba, uokoaji na usafirishaji wa majeruhi wa ajali na wagonjwa wenye dharura mbalimbali nje ya Hospitali nchini.

  Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo, Dkt. Mpoki amelitaka jeshi la Polisi nchini kuangalia namna ya kuweka utaratibu wa madereva kubadilishana kwani suala la uchovu linachangia kwa kiasi kikubwa ajali za barabarani.Aidha,akitolea mfano suala la uchovu, dereva kutoka Mwanza au Bukoba kwenda Dar es Salaam, basi ashuke Singida ili aingie dereva mwingine kumalizia safari na hiyo itasaidia kuepusha ajali.

  “Tumemuomba Mkuu wa Jeshi la Polisi atusaidie kama mchango wa Polisi katika kupunguza ajali kwa kuhakikisha kwamba wanaweka utaratibu wa madereva wanaendesha kwa muda maalum. Kuliko ilivyo sasa madereva wanaweza kuendesha siku nzima, Hivyo wanakuwa wachovu na kuchangia kwa kiasi kikubwa sana ajali mbalimbali barabarani” amesema Dkt. Mpoki.

  Hata hivyo ameeleza kuwa, mpango huo ni hatua ya kwanza ambayo Serikali imewekeza kuingilia kati pale watu wanapokuwa wameumia, ambapo huko nyuma maisha ya watu wengi yalikuwa yakipotea kwa sababu vifaa vilikuwa vinachelewa sana kufika mahali tukio na hivyo kushirikiana na Benki ya dunia kwa kutenga kiasi cha shilingi Bilioni 8 kwa ajili ya uwekezaji na shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya kuendesha shughuli za kila siku za wataalam.

  “Katika fani ya tiba, Tunazungumzia saa ya kwanza ni saa muhimu sana kusaidia mtu aliyepata changamoto ya ajali. Hawa watakuwa chachu ya kusaidia kati ya wale waliopata mafunzo.” Amesema Dkt. Mpoki

  Dkt. Mpoki ameongeza kuwa katika afua hiyo,itakuwa na vituo maalum vyenye miundombinu ya kutoa huduma hizo ambapo awamu ya kwanza itaanzia Dar e Salaam hadi Ruaha Mbuyuni na kwa kila kituo kutakuwa na gari la kubebea wagonjwa, vifaa vya zima moto na kuweka utaratibu wa kusafirisha majeruhi kwa kushirikiana majeshi yakiwemo la Jeshi la Wananchi (JWTZ), Polisi, Zimamoto pamoja na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD).

  Kwa upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma (MUHAS), Profesa Appolenary Kamuhabwa amesema mafunzo hayo ni muhimu sana kwani kutakuwa na mfumo thabiti wa kuwahudumia wagonjwa wa dharura watokanao na ajali na ni hatua muhimu kwani bila afya bora, wananchi hawawezi kutumikia nchi hususani ajenda ya Serikali ya viwanda.

  Profesa Kamuhabwa amesema katika mpanguo huo, utakuwa na vituo mbalimbali vya Afya vitakavyokuwa vikitoa huduma za dharura ikiwemo: Vituo vya Afya vya Kimara (Dar es Salaam), Tumbi, Chalinze (Pwani), Mikese, St, Kizito, Doma-Mikumi (Morogoro) na Ruaha Mbuyuni (Iringa).
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza leo jiji Dar es Salaam, katika kufungua mafunzo ya watoa huduma za tiba, uokoaji na usafirishaji wa majeruhi wa ajali na wagonjwa wenye dharura mbalimbali nje ya Hospitali nchini.(Picha na Emmanuel Massaka wa MMG)
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akizindua kitabu cha mafunzo ya watoa huduma za tiba, uokoaji na usafirishaji wa majeruhi Wa ajali na wagonjwa wenye dharura mbalimbali nje ya hospitali nchini Tanzania
  Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma (MUHAS), Profesa Appolenary Kamuhabwa akizungumza machache wakati wa ukufungua wa mafunzo ya watoa huduma za tiba leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa idara ya dharura hospitali ya Ta ifa ya Muhimbili Dkt.Juma Mfinanga akipokea kitabu hicho cha mafunzo kutoka kwa Katibu Mkuu Dkt.Mpoki Mara baada ya kukizindua
  Picha ya Pamoja ya watumishi toka wizara ya Afya,hospitali,Shirika la msalaba Mwekumdu,Chuo kikuu MUHAS Pamoja na majeshi ambao kwa Pamoja watatekeleza mpango huo nchini

  0 0

  Na Mathias Canal-Wizara ya kilimo, Mtwara

  Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga amesema kuwa wizara yake itatekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kuhakikisha kuwa korosho yote inabanguliwa hapa nchini.

  Ameyasema hayo jana tarehe 13 Novemba 2018 wakati akieleza malengo ya ziara yake mkoani Mtwara na Lindi alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kabla ya kuanza kukagua maghala ya kuhifadhia korosho.

  Hasunga alisema kuwa kuruhusu wafanyabiashara kubangulia nje ya nchi korosho za wakulima wa Tanzania ajira nyingi zilikuwa zikipotea huku watanzania wakisalia kuhangaika kutafuta ajira kwani ajira nyingi zilipelekwa nje ya nchi.

  “Baada ya kujiridhisha tumeamua sasa hahutasafirisha korosho ghafi tunataka korosho yote iwe inachakatwa nchini kwenye viwanda vyetu, kwa hiyo korosho zote zilizokuwa zinachukuliwa na wafanyabiashara kwenda kubanguliwa sijui wapi huko tumezuia” Alikaririwa Mhe Hasunga

  Alisema kuwa viwanda vya kubangua korosho nchini vingi vimekufa kwa sababu ya ubadhilifu wa wananchi wachache na baadhi ya hujuma za watu lakini serikali imedhamiria kuanza kubangua kwenye viwanda vilivyopo kabla ya hatua za kuanzisha viwanda vingi vya ubanguaji.

  “Tunamuwezesha mkulima kwa bei ya shilingi 3300 ili imsaidie kufanya kazi zake zingine ili aweze kuongeza uzalishaji katika msimu ujao wa mwaka 2018/2019 na kuepuka kushuka kwa uzalishaji” Alisisitiza Mhe Hasunga.Alisema baada ya kukamilika uhakiki wa maghala yote ya kuhifadhia korosho serikali itaanza kulipa malipo yote stahiki kwa wakulima yatakayotolewa na Benki ya kilimo Tanzania (TADB).

  “Na tumeshaandaa fedha zao tunataka wakulima walipwe haraka iwezekanavyo lakini tumeanza kumjali mkulima kwanza halafu taasisi zingine zinazofaidika na korosho zitafuata” Alisisitiza

  Mhe Hasunga amewapongeza wakulima kwa kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha mpito wakati serikali ilipokuwa ikitafuta ufumbuzi wa zao la korosho.
  Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga akieleza malengo ya ziara yake mkoani Mtwara na Lindi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kabla ya kuanza kukagua maghala ya kuhifadhia korosho jana tarehe 13 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)
  Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga akizungumza na waandishi wa habari kuelezea malengo ya ziara yake mkoani Mtwara na Lindi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kabla ya kuanza kukagua maghala ya kuhifadhia korosho jana tarehe 13 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)


  0 0

   Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na ugeni kutoka Benki ya NMB ulioongozwa na Ofisa Mkuu wa Mikopo wa Benki hiyo, Ndg. Tom Borghlos (wa pili kushoto) walipomtembelea leo tarehe 14 Novemba 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Wa tatu kushoto ni Mjumbe wa Bodi, Ndg. Jos Lange, Afisa wa Benki ya NMB, Ndg. Juliana muwanga (wa tatu kulia), Mkuu wa Biashara Benki ya NMB, Ndg. Donatus Richard (wa pili kulia) na Meneja kanda ya kati, Ndg. Nsolo Mlozi
   Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Ofisa Mkuu wa Mikopo wa Benki ya NMB, Ndg. Tom Borghlos (wa pili kushoto) pale ugeni kutoka Benki hiyo ulipomtembelea leo tarehe 14 Novemba 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Mjumbe wa Bodi NMB, Ndg. Jos Lange na Afisa wa Benki ya NMB, Ndg. Juliana muwanga
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (watatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Benki ya NMB ulioongozwa na Ofisa Mkuu wa Mikopo wa Benki hiyo, Ndg. Tom Borghlos (watatu kulia) walipomtembelea leo tarehe 14 Novemba 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
   Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akiagana na Mjumbe wa Bodi wa Benki ya NMB, Ndg. Jos Lange pale ugeni kutoka Benki ya NMB ulipomtembelea leo tarehe 14 Novemba 2018 Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Biashara Benki ya NMB, Ndg. Donatus Richard.

  0 0

  Na Saidina Msangi na Farida Ramadhani-WFM.

  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) amesema kuwa Serikali itazingatia maoni na ushauri wa wabunge wote katika Maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka 2019/2020.

  Waziri Mpango alitoa kauli hiyo Bungeni wakati akiahirisha mjadala wa Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2019/2020.

  Akitoa ufafanuzi wa baadhi ya maoni ya wabunge kuhusu kuboresha sekta ya kilimo ikiwemo kuongeza bajeti ya kilimo, Dkt. Mpango alisema kuwa uongezaji wa bajeti ya kilimo ni muhimu lakini lazima ufanyike kwa ulinganifu wa mahitaji ya kibajeti ya sekta nyingine muhimu.

  “Ni muhimu kukumbuka kuwa sekta ya kilimo ina mwingiliano mkubwa na sekta nyingine. Mwenendo bora wa kilimo unategemea sana uwekezaji wa sekta saidizi hasa miundombinu ya umwagiliaji, barabara vijijini, umeme kwa ajili ya kuendesha viwanda vya kuongeza thamani ya mazao, uzalishaji wa zana za kilimo, dawa, elimu na afya kwa wakulima” alisema Waziri Mpango.

  Aidha, waziri Mpango aliongeza kuwa ni muhimu kuvutia sekta binafsi kuwekeza katika sekta za kilimo na uvuvi, kuimarisha upatikanaji wa mikopo kwa wakulima, wafugaji na wavuvi pamoja na kutafuta masoko ya kikanda na kimataifa.Akizungumzia miradi mikubwa inayotajwa kukwama Waziri Mpango alifafafanua kuwa miradi iliyokwama imetokana na masharti hasi ya wawekezaji ambayo hayana maslahi kwa Taifa.

  “Serikali ina nia ya kuona nchi inaendelea haraka hata hivyo inayo dhamana ya kuhakikisha kuwa rasilimali hizo zinatumika vizuri kwa kulinda maslahi mapana ya Taifa” alisema Dkt. Mpango.Kuhusu kupungua kwa ukwasi katika uchumi waziri ameeleza kuwa madai hayo yanahusishwa na kupungua kwa fedha mifukoni kwa wananchi na kwa benki za biashara kwani upatikanaji wa fedha kwa mianya isiyo halali umedhibitiwa, ukwepaji kodi, madai hewa , ufisadi, rushwa, wizi, ubadhilifu wa mali ya umma vimekomeshwa.

  Ametoa wito kwa wananchi kujishughulisha katika shughuli halali na kufanya kazi kwa bidii na ufanisi ili kujenga Taifa na kufikia azma ya ujenzi wa uchumi wa viwanda.Pia, Waziri Mpango ametoa rai kwa wabunge kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano katika kuwaletea wananchi maendeleo.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akijibu hoja mbalimbali za wabunge kabla ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maadalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/2020, Jijini Dodoma.
   Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akijibu hoja mbalimbali za wabunge kabla ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maadalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/2020, Jijini Dodoma.
   Viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia mjadala wa wabunge, kabla ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maadalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/2020, Jijini Dodoma jana, Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban
   Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA- Bw. Charles Kichere (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (wa pili kushoto) na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia mjadala wa wabunge, kabla ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maadalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/2020, Jijini Dodoma jana.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati), wakiwa katika picha ya pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Dkt. Adelardus Kilangi (Mb) (kulia), baada ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maadalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/2020, Jijini Dodoma jana.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akipongezwa na Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Mhe. Dkt. Sware Semesi na Wabunge wengine akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Dkt. Adelardus Kilangi (Mb) (kulia), nje ya ukumbi wa Bunge baada ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maadalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/2020, Jijini Dodoma jana.
   Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Dkt. Adelardus Kilangi (Mb) (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), nje ya Ukumbi wa Bunge, baada ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maadalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/2020, Jijini Dodoma jana.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (kulia) akijadili jambo na Mbunge wa Witi Maalum Mhe. Mama Salma Kikwete (kushoto) na aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Saada Nkuya (Mb),  nje ya Ukumbi wa Bunge, baada ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maadalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/2020, Jijini Dodoma jana.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

  0 0

  Na Stella Kalinga, Simiyu.

  Kuelekea katika kipindi cha maandalizi ya  bajeti ya mwaka 2019/2020 wito umetolewa kwa  Wakurugenzi wa Halmashauri mkoani Simiyu na maeneo mengine kote nchini kuyapa kipaumbele masuala ya Lishe katika mipango na bajeti za Halmashauri zao, ili kukabiliana na tatizo la udumavu kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.

  Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi Sera, kutoka Ofisi ya Raisi TAMISEMI, Bw.Eleuter Kihwele wakati mafunzo maalum yaliyotolewa kwa baadhi ya viongozi na maafisa Lishe, katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018.

  Kihwele amesema takribani asilimia 34 ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano nchi nzima wana udumavu, hivyo ipo haja ya kutilia mkazo suala la lishe ili kutoathiri maendeleo ya ukuaji wa watoto, uwezo wao wa kufikiri na maendeleo yao kitaaluma(shuleni).

  “Asilimia 34 ya watoto wa  nchi nzima wenye umri chini ya miaka mitano wana utapiamlo, suala hili linaathiri sana watoto, mfano matokeo yao shuleni na uwezo wa kufikiri, ndio maana serikali imeweka lishe kama kipaumbele na Ofisi ya Rais TAMISEMI kama wasimamizi tunapita kwenye Halmashauri nchi nzima kuhamasisha uzingatiaji wa masuala ya lishe katika bajeti ya mwaka 2019/2020” alisema

  Ameongeza kuwa katika mafunzo yanayotolewa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa Viongozi pia yamelenga  kuwakumbusha juu ya utekelezaji wa vipengele vya mikataba ya afua za lishe iliyosainiwa katia ya  Wakuu wa Mikoa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI na kutenga shilingi 1000 kwa kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano katika bajeti zao.

  Naye Afisa Lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bi. Mariam Nakuwa ametoa wito  kwa Halmashauri kutenga  fedha kwa ajili ya masuala ya lishe kwa kuzingatia miongozo na kuhakikisha fedha zinazotengwa zinatumika katika shughuli zilizopangwa ili kuondokana na tatizo la utapiamlo

  Aidha, Bi. Mariam amesema pamoja na kukabiliana na tatizo la utapiamlo fedha hizo zielekezwe katika huduma za utoaji wa virutubisho vya nyongeza kama vile virutubisho vya Vitamini A na vidonge vya kuongeza wekundu wa damu kwa akina mama wajawazito.

  Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini aliwasisitiza Wakurugenzi wa Halmashauri mkoani Simiyu kuyachukulia masuala ya lishe kama kipaumbele, huku akiwataka kuhakikisha wanafanya vikao vya kamati za lishe za wilaya kila baada ya miezi mitatu kama ilivyoanishwa  katika miongozo.

  Diwani wa Kata ya Dutwa  Mhe.Mapolu Mkingwa akizungumza kwa niaba ya  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe.Richard Buyamba amesema maelekezo na mafunzo waliyoyapata watayapelekea katika Mabaraza ya madiwani na kuhakikisha mipango na bajeti zinazopitishwa zinazingatia umuhimu wa afua za lishe.

  Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe amesisitiza viongozi na watendaji wakiwemo wajumbe wa kamati za lishe kubadilika na kuachana na mazoea katika kufanya ufuatiliaji na kutekeleza mipango ya masuala ya lishe badala yake wafanye kazi kulingana na miongozo ili kuwa na matokeo mazuri katika masuala ya lishe.

  Timu ya Wataalam kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI ipo katika ziara ya kuhamasisha Viongozi katika Halmshauri na Mikoa kuzingatia vipaumbele kwenye maeneo ya lishe na kupanga mipango ya bajeti inayojibu changamoto za lishe, ili kufikia malengo ya  mikataba ambayo Wakuu wa Mikoa walisaini na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwenye usimamizi wa afua za lishe katika maeneo yao.
   Mkurugenzi Msaidizi Sera, kutoka Ofisi ya Raisi TAMISEMI, Bw.Eleuter Kihwele  akizungumza na baadhi ya viongozi  na Wataalam Lishe wa mkoa wa Simiyu, katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018.
   Afisa Lishe kutoka Ofisi ya Raisi TAMISEMI, Bi. Mariam Nakuwa   akiwasilisha mada kuhusu mipango na bajeti ya masuala ya lishe Mkoani Simiyu kwa baadhi ya viongozi  na Wataalam Lishe wa mkoa wa Simiyu, katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018.
   Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akisisitiza jambo katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018.
   Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Bw. Kai.B. Mbaruk akizungumza na baadhi ya viongozi  na Wataalam Lishe wa mkoa wa Simiyu, katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018 wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Simiyu.
   Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani akichangia hoja katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018 wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Simiyu.
   Diwani wa Kata ya Dutwa  Mhe.Mapolu Nunde Mkingwa akichangia hoja katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe Mkoani Simiyu kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018, ambapo alimwakilisha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe.Richard Buyamba.
  Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt.Seif Shekalaghe akichangia hoja katika kikao cha Maandalizi ya Mipango ya Bajeti ya Afua za Lishe kwa mwaka 2019/2020 Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi, Novemba 12, 2018.


  0 0

  Idara ya Uhamiaji mkoani Shinyanga imekamata wahamiaji haramu 110 wakiwemo raia wa kigeni 103 na Watanzania saba kwa kuishi nchini Tanzania kinyume cha sheria.

  Hayo yamebainishwa leo Jumatano Novemba 14, 2018 Msemaji wa idara ya Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga Godson Mwanawima, wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu Maendeleo ya Idara ya Uhamiaji mkoa wa Shinyanga kuanzia Agosti hadi Oktoba mwaka 2018. 

  Alisema wahamiaji hao haramu wengi ni kutoka katika nchi za jirani ambapo Burudi wamekamata 46, Rwanda wakiwa 13, pamoja na wengine kutoka nchi za Ethiopia, Kenya,India na China.

  "Katika kipindi cha miezi mitatu,tumekamata na kuhoji watu 110 kati yao raia wa kigeni wakiwa 103 na Watanzania saba,kati ya wageni hao 103, wahamiaji 43 wamerudishwa kwenye nchi zao na 60 walibainika kuwa na vibali halali hivyo kuwaruhusu kuendelea kuishi hapa nchini",alieleza Mwanawina. Aliyataja maeneo ambayo wamekamata wa hamiaji haramu wengi kuwa ni wilaya ya Kahama kwenye mashamba ya Tumbaku, Mpunga na migodi na kwenye mgodi wa Mwakitolyo uliopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 

  Naye Mrakibu msaidizi mkuu wa upelelezi na Operesheni Idara ya Uhamiaji mkoa wa Shinyanga Filemon Meena, aliwataka watanzania kuachana na tabia ya kuhifadhi wahamiaji haramu, ambao wamekuwa wakivuruga amani ya nchi. Katika hatua nyingine aliwahimiza watanzania kila mmoja ajitahidi kuwa na kitambulisho cha taifa (NIDA), ambapo itafikia kipindi bila ya kuwa na kitambulisho hicho watakosa huduma za kijamii ikiwemo matibabu, lengo likiwa ni kukomesha kuwepo kwa hawamiaji haramu hapa nchini. 
  Msemaji wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga Godson Mwanawima, akizungumza na waandishi wa habari mkoani Shinyanga leo ofisini kwake.
  Mrakibu msaidizi mkuu wa upelelezi na Operesheni Idara ya uhamiaji mkoa wa Shinyanga Filemon Meena akielezea kuhusu Operation wanazoendelea nazo kushughulika na wahamiaji haramu.Picha na Marco Maduhu Malunde1 Blog

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi na Watendaji wa mkoa wa Kilimanjaro kufanya kazi kwa kushirikiana, kuheshimiana na kupendana.

  Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani humo.“Mheshimiane, muwajibike wote tunajenga Tanzania mmoja tutangulize maslahi ya Taifa na si maslahi binafsi” alisema Makamu wa Rais.

  Makamu wa Rais aliwasili mkoani Kilimanjaro tarehe 8 Novemba 2018 ambapo alifanya ziara katika Wilaya ya Rombo, Wilaya ya Moshi, Same, Mwanga, Siha na Hai.Katika ziara hiyo Makamu wa Rais alikagua miradi mbali mbali na kuweka mawe ya msingi katika ujenzi na mengine ufunguzi.

  Pamoja na mambo mengine Makamu wa Rais aliwataka Viongozi wa Halmashauri kukusanya mapato na kubuni njia zingine za kupata mapato, pia alizihimiza kufanya mambo yao ambayo yapo kwa mujibu wa Sheria.Makamu wa Rais amezitaka halmashauri kutochukua ushuru wa mazao shambani na badala yake waanzishe soko maalum la mazao ambalo mkulima atapeleka mazao yake hapo.

  Aidha Makamu wa Rais alitoa maagizo kwa mkoa kuhakikisha wafanyakazi wa viwandani na msahambani wanapewa msaada wa kutambua na kupata haki zao za msingi.Kwa upande mwingine Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesema kuwa mkoa wa Kilimanjaro una migogoro mingi ya ardhi ambayo hatua zitachukuliwa karibuni haswa kwa waliojimilikisha mashamba ya Ushirika na pia upo nyuma katika kulipa kodi za ardhi.

  Waziri wa Ardhi amesisitiza watu wote waliouziwa viwanja kwenye eneo la kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools wasiendeleze kwani hati zote 39 zimefutwa na eneo litakabidhiwa kwa Kituo cha Wawekezaji.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi na Watendaji wa mkoa Kilimanjaro wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani humo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISIEMI Mhe. Selemeni Jafo wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani Kilimanjaro kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0

  Na Karama Kenyunko,blogu ya jamii

  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imekwama kuendelea na usikilizwaji wa kesi ya utakatishaji fedha na kumiliki mali zisizolingana na kipato chake inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Takukuru Godfrey Gugai na mwenzake, sababu shahidi wa upande wa mashtaka ana dharura.

  Wakili wa Serikali Mkuu kutoka Takukuru Vitalis Peter amedai leo Novemba 13, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kuwa kesi hiyo imepangwa kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa lakini wamepata taarifa kuwa shahidi waliyemtarajia kutoa ushahidi katika Kesi hiyo amepatwa na dharura.

  Kutokana na hiyo, Hakimu Simba alisema kwa mtindo huu hii Kesi haitomalizika, watakuwa wanacheza tu."Wasa muwe mnaleta mashahidi Wawili Wawili ili mmoja akipata dharura mwingine anaendelea kwani hali kama hii imekwisha jitokeza zaidi ya mara nne au tano" amesema Hakimu Simba.

  Wakati upande wa utetezi ukiwakikishwa na Wakili Alex Mgongolwa amewataka mashahidi wanaokwenda kutoa mashahidi katika Kesi hiyo wajulikane na kwamba upande wa mashtaka unapoona shahidi wanayemtafuta anahitilafu watafute mwingine.

  Aidha hakimu Simba ameusisitiza upande wa mashtaka kupeleka mahakamani hapo mashahidi wawili wawili.Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 27 na 28, mwaka huu ambapo utaendelea kusikiliza kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.

  Mbali na Gugai, washtakiwa wengine ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera.Katika kesi hiyo, Gugai na wenzake, wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, katika Mahakama hiyo.

  Miongoni mwa mashtaka yanayomkabili Gugai ni kosa la kumiliki mali zilizozidi kipato chake halali, ambapo anadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Januari 2005 na Desembea 2015.

  0 0

   Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasialiano wa Benki ya Exim Bw Stanley Kafu  (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dr Philip Mpango ( wa tatu kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk. Albina Chuwa ( wa pili kulia), Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Profesa Peter Msoffe (wa pili kushoto) katika maadhimisho ya siku ya takwimu duniani iliyoadhimishwa jijini Dodoma hivi karibuni ambapo Benki ya Exim ilitoa kiasi cha Sh Milioni 10 kufanikisha maadhimisho hayo kupitia chuo kikuu cha UDOM.
   Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasialiano wa Benki ya Exim Bw Stanley Kafu (katikati) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. Mil 10/-  kwa Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Profesa Peter Msoffe (wa pili kushoto) ikiwa ni mchango wa benki hiyo katika kufanikisha maadhimisho ya siku ya takwimu duniani iliyoadhimimishwa jijini Dodoma hivi karibuni.
   Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango,  akizungumza na waandishi wa habari alipohudhuria katika maadhimisho ya siku ya takwimu duniani iliyoadhimimishwa jijini Dodoma hivi karibuni.
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk. Albina Chuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho hayo.

  0 0


  0 0

  Na Neema Edwin

  Maelfu ya watu wamejitokeza kupima afya zao katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya kisukari duniani, huku Mkurungezi Mtendaji wa hospitali hiyo, Prof. Lawrence Museru akiwataka Watanzania kujenga tabia ya kuchunguza afya zao mara kwa mara ili kubaini kama wana tatizo la kisukari au matatizo mengine ya kiafya.

  Katika maadhimisho hayo hadi kufikia saa 7:30 mchana leo, watu 1,150 wamejitokeza kufanya uchunguzi wa macho, uchunguzi wa afya ya kinywa na meno, uchunguzi wa magonjwa ya kisukari, homoni pamoja na shinikizo la damu.  

  Akizungumza katika maadhimisho hayo, Prof. Museru amesema kati ya watu wazima 100 takribani watu 9 wana ugonjwa wa kisukari na kati ya watu wazima 3 mmoja ana shinikizo la damu. “Tatizo ni kubwa kwani takwimu zinaonyesha kliniki ya kisukari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ina wagonjwa zaidi ya 6000 wanaoudhuria kwa mwaka,” amesema Prof. Museru.

  Prof. Museru amesema kwamba moja ya vyanzo vinavyochangia kuongezeka kwa magonjwa yasioambukiza ikiwamo kisukari na presha ni ulaji usiofaa kama kula chakula kuzidi mahitaji ya mwili na hivyo kunenepa, kula mafuta na chumvi zaidi ya mwili, kutokula matunda na mbogamboga kiasi cha kutosha na kula nafaka zilizokobolewa.

  Mkurugenzi huyo amesema matumizi ya pombe kupita kiasi, tumbaku na dawa za kulevya, kutofanya mazoezi na msongo wa mawazo pia yanachangia kuongezeka kwa magonjwa yasioambukiza.

  Akizungumzia madhara ya kisukari, Prof. Museru amesema ugonjwa huo unasababisha kuharibika kwa macho, figo, moyo na mishipa ya damu.
  “Kwa mfano, mtu anaweza kuishi miaka mingi na shinikizo kubwa la damu bila kubainika kama ana dalili zozote hadi pale anapopata kiharusi, moyo au figo unaposhindwa kufanya kazi,” amesema Prof. Museru.

  Mkurugenzi huyo amewashauri watu kuchunguza afya zao mara kwa mara kwa lengo la kugundua magonjwa hayo mapema ili kuepuka matumizi ya mabilioni ya fedha za kudhibiti magonjwa yasioambukiza.Amesema inakadiriwa ugonjwa kisukari pekee umeathiri maisha ya watu takribani milioni 425 duniani kote hadi mwaka 2017, huku asilimia 80 ya idadi ya watu wakiishi kwenye nchi za kipato cha chini ikiwamo Tanzania.

   “Ukubwa wa tatizo la kisukari duniani kote linaendelea kuwa tishio la uhai wa watu mwaka hadi mwaka kwani wagonjwa wa kisukari wanaongezeka kwa kasi sana ukilinganisha na ongezeko la idadi ya watu duniani,”amesema Prof. Museru.

  Amefafanua kuwa magonjwa mengine yasioambukiza kama magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, figo, magonjwa ya mfumo ya hewa na kansa yanazidi kuongezeka kwa kasi na kuwa chanzo kikuu cha vifo duniani kote.
  Siku ya kisukari duniani huadhimishwa tarehe 14 Novemba kila mwaka ambapo Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila imeadhimisha siku hii kwa kutoa huduma bure mbalimbali za uchunguzi kwa siku tano kuanzia Novemba 12-16, 2018.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila, Prof. Lawrence Museru akizungumza katika maadhimisho ya siku ya kisukari ambayo huadhimishwa Novemba 14, kila mwaka. Maadhimisho hayo yanafanyika katika hospitali hiyo iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.
   Mmoja wa wananchi aliyejitokeza kuchangia damu katika maadhimisho ya siku ya kisukari duniani hospitalini hapo.
   Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Prof. Museru akionyesha umuhimu wa wananchi kuchunguza afya zao kwenye maadhimisho hayo.
  Wananchi wakiendelea kupatiwa huduma ya uchunguzi leo.
   Wananchi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila wakati akizungumza nao kwenye maadhimisho hayo.
   Mmoja wa wananchi akipata huduma katika hospitali hiyo leo.
   Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupata huduma za uchunguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila wakisubiri kupatiwa huduma hiyo leo.
   Pichani ni Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila, Dkt. Julieth Magandi (katikati), Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila, Sufiani Baruani (kulia) na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila Sr. Redemptha Matindi.

  0 0


   • Kwa shilingi 1,000 tu mchezaji anaweza kushinda hadi 10,000,000/- kila baada ya dakika 10

  Kampuni ya The Network inayosimamia michezo ya namba nchini Tanzania leo imezindua mchezo wa namba ujulikanao kama Supa Tano ambapo mshindi anaweza kushinda hadi milioni 10,000,000/- kila baada ya dakika 10.

  Huu unakuwa ni mchezo pekee kwa sasa nchini Tanzania ambapo mshindi anaweza kupata kiasi kikubwa ndani ya dakika kumi tu. Mchezo wa Supa Tano pia unakuwa ni mchezo pekee wenye kutoa fursa nyingi zaidi za ushindi hapa nchini.
  Meneja wa Fedha wa The Network,Bwana Jacob Millinga, amesema ‘Supa Tano ni mchezo mpya wa namba ambao wachezaji wanaweza kucheza viwango mbalimbali kati ya shilingi 1000 mpaka 20,000. Mchezo unatoa nafasi ya kushinda hadi mara 10,000 ya dau uliloweka, ambacho ni kiasi kikubwa kuliko mchezo wowote Tanzania’ anasema Kupitia Supa Tano mchezaji anapata nafasi nyingi zaidi za ushindi, kwani kila namba anayolinganisha analipwa kuanzia namba 2, 3, 4 au namba 5 kwenye droo za kila dakika 10, na wakati huo huo kila shilingi 1000 yake inampa nafasi ya kuingia kwenye SupaMzuka Jackpot siku za Jumapili na Jumatano.

  ‘Mchezaji anacheza kupitia simu yake ya mkononi kwa kutuma shilingi 1,000 kwenda namba ya kampuni ambayo ni 551551 ikifuatiwa na kumbukumbu namba ambazo zitakuwa namba zake 5 za bahati kati ya 0-9, na kama ameshinda anatumiwa kiwango cha pesa cha ushindi wake moja kwa moja kwenye namba yake ya simu’ alifafanua balozi wa Supa 5, Yvone Cherry maarufu kama Monalisa.

  Mchezo wa Supa 5 unaendeshwa kwa uwazi na usimamizi wa serikali kupitia Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania. Matokeo yote ya washindi na zawadi walizoshinda yatawekwa kwenye tovuti ya: www.supatano.co.tz.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mwakilishi wa Bodi ya michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), amesema mchezo wa Supa 5 unaongeza fursa nyingine za ushindi kwa watanzania lakini ni muhimu kwa wachezaji kucheza kwa ustaraabu bila kutumia pesa ya matumizi muhimu kwenye mchezo huu.
   Meneja wa Fedha wa kampuni ya The Network. Jacob Millinga akizungumza leo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani), wakati wa uzinduzi wa mchezo wa namba ujulikanao kama Supa Tano ambapo mshindi anaweza kushinda hadi milioni10,000,000/- kila baada ya dakika 10,uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar
  ‘Mchezaji anacheza kupitia simu yake ya mkononi kwa kutuma shilingi 1,000 kwenda namba ya kampuni ambayo ni 551551 ikifuatiwa na kumbukumbu namba ambazo zitakuwa namba zake 5 za bahati kati ya 0-9, na kama ameshinda anatumiwa kiwango cha pesa cha ushindi wake moja kwa moja kwenye namba yake ya simu’ alifafanua balozi wa Supa 5, Yvone Cherry maarufu kama Monalisa kwa Wanahabari leo jijini Dar.
   
   Balozi wa Supa 5 Adam Mchovu akitoa ufafanuzi mbele ya Waandishi wa habari namna ya kucheza mchezo huo wa namba ujulikanao kama Supa 5 kupitia simu ya mkononi,ambapo mshindi anaweza kushinda hadi milioni10,000,000/- kila baada ya dakika 10,uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar
  Uzinduzi wa Mchezo wa namba ujilikanao kwa jina la Supa 5 ukiwa tayari kuzinduliwa rasmi na wananchi kuanda kuucheza mchezo huo kwa njia ya simu zao za Kiganjani.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Novemba 14, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto  (katikati) na Mbunge wa Mufindi Kaskazini, Mahmoud Mgimwa (kushoto) kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Novemba 14, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  0 0

   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Uongozi wa Taasisi ya Habari ya MISA –TAN kuhusu maendeleo ya sekta ya Habari leo Jijini Dodoma.
   Mwenyekiti wa Taasisi ya Habari ya MISA – TAN Bibi.Salome Kitomary (Kushoto) akitoa maelezo mafupi kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) wakati Taasisi hiyo ilipokutana nae leo Jijini Dodoma.Kulia ni Mkurugeni Msaidizi Idara ya Habari Bw. Rodney Thadeus.
   Mkurugeni Msaidizi Idara ya Habari Bw. Rodney Thadeus akimkaribisha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) kuzungumza na  Uongozi wa Taasisi ya Habari ya MISA – TAN leo Jijini Dodoma.
   Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Habari ya MISA –TAN  Wakili James Marenga akizungumza wakati wa kikao kati ya taasisi hiyo na  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia) kuhusu maendeleo ya sekta ya Habari leo Jijini Dodoma.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Taasisi ya Habari ya MISA –TAN pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara yake.


  0 0

  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge na Huduma za Maendeleo ya Jamii Peter Serukamba Mwongozo wa ubunifu mara baada ya kuuzindua leo Jijini Dodoma.
  Wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizra ya Elimu na Teknolojia wakifurahia mara baada ya Mwongozo na Mashindano ya ubunifu kuzinduliwa.
  Waziri Wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge na Huduma ya Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba wakionesho mwongozo wa Ubunifu mara baada ya Kuzinduliwa leo Jijini Dodoma.
  Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako akimkabidhi mmoja wa wanafunzi kutoka shule ya Sekondari Dodoma Mwongozo wa ubunifu mara baada ya kuzinduliwa leo jijini Dodoma


  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako leo amezindua mwongozo na mashindano ya ubunifu kitaifa mkoani Dodoma.

  Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi Waziri Ndalichako amesema lengo la mashindano hayo ni kutambua na kuendeleza fikra za wabunifu kwa lengo la kuongeza ajira.

  Prof. Ndalichako amesema katika kuimarisha uchumi wa viwanda lazima matumizi ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu yaimarishwe kwa lengo la kuongeza tija viwandani na kwenye biashara.

  “Kutoka na umuhimu wa mashindano haya naielekeza Idara ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu kuhakikisha mashindano haya yanafanyika kila mwaka, ili kukuza ujuzi, wabunifu kwa maendeleo ya viwanda,” alisisitiza Waziri Ndalichako.Mashindano hayo yameshirikisha Makundi mbalimbali ya kijamii zikiwemo Shule za Sekondari, Vyuo vya Ufundi Stadi, Sekta isiyo rasmi, Vyuo vya ufundi wa Kati, Vyuo vya Elimu ya Juu na Taasisi za utafiti na Maendeleo.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba amesema kuwa kuzinduliwa kwa mwongozo huo ni jambo kubwa na la kihistoria ikizingatiwa kuwa nchi inaelekea kwenye uchumi wa viwanda.Serukamba amesema bila Sayansi, Teknolojia na ubunifu nchi haiwezi kufanikisha malengo yake, hivyo ameiomba Serikali ihakikishe inawekeza fedha nyingi.

  “Kama hatutawekeza fedha za kutosha kwenye Sayansi, Teknolojia na Ubunifu hatuwezi kufanya kitu, hivyo tuwekeze fedha za kutosha ili tujiletee Maendeleo kwa haraka,” amesema Mhe. Serukamba.Kauli mbiu ya mashindano hayo ni “Kukuza Ujuzi na Ubunifu kwa Uchumi wa Viwanda.”


  0 0


  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuripoti ofisini kwake mapema leo jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.


  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kushoto) akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) mara baada ya kuripoti ofisini kwake mapema leo jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.
  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi.Dorothy Mwaluko, akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) kuzungumza na watumishi, mara baada ya kuripoti ofisini kwake mapema leo jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.
  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya kuripoti ofisini kwake jijini Dodoma leo kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.
  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) akisalimiana na mmoja wa watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya kuripoti ofisini kwake jijini Dodoma leo kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.

  ………………………………………………………………..

  Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) ameahidi kushirikiana na watumishi wa ofisi yake kupanga mikakati endelevu itakayowezesha kutoa huduma bora kwa umma na kuhakikisha ofisi hiyo inakuwa na mtazamo chanya katika kuwahudumia wananchi.

  Dkt. Mwanjelwa ametoa ahadi hiyo leo wakati akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya kuripoti ofisini kwake jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kazi rasmi. Dkt. Mwanjelwa ameomba ushirikiano wa dhati kutoka kwa watumishi wa ofisi yake kwani kila mtumishi ana mchango na umuhimu wake katika kuboresha utuoaji wa huduma kwa umma.

  Aidha, Dkt. Mwanjelwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuwa Naibu Waziri mwenye dhamana ya utumishi na utawala bora.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alimteua Mhe. Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, tarehe 10 Novemba, 2018 na kumuapisha tarehe 12 Novemba, 2018.

  0 0   Meneja Mawasiliano wa TPB Bank, Chichi Banda (Kulia) akikabidhi jezi kwa Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa Habari za Michezo Nchini (Taswa SC), Majuto Omary katika hafla fupi iliyofanyika jana. TPB Bank imetoa msaada ikiwa sehemu ya shughuli zao za kijamii. PICHA na MPIGA PICHA WETU.
  ????????????????????????????????????
  Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa Habari za Michezo Nchini (Taswa SC), Majuto Omary (kulia) akitoa neon la shukrani mara baada ya kukabidhiwa vifaa vya michezo na Meneja Mawasiliano wa TPB Bank, Chichi Banda katika hafla fupi iliyofanyika jana. TPB Bank imetoa msaada ikiwa sehemu ya shughuli zao za kijamii. PICHA na MPIGA PICHA WETU.
  ………………………………………………………………..
  Na Mwandishi wetu
  Dar es Salaam. Benki ya TPB imeendelea kuisadia  klabu ya  Waandishi wa habari za michezo  nchini (Taswa SC) baada ya kuikabidhi vifaa vya michezo ambavyo vitatumiwa na timu hiyo katika michezo yake mbalimbali.
  Akizungumza katika makabidhiano hayo, Meneja  Mawasiliano wa  Benki ya TPB Chichi Banda alisema kuwa wamesaidia msaada huo ni sehemu ya shughuli za Benki na kutambua mchango mkubwa wa Waandishi wa Habari Nchini na muendelezo wao katika shughuli za kijamii ambapo mbali ya michezo, pia usaidia afya na elimu.
  Chichi alisema kuwa wamefariji kakutoa msaada huo kwaTaswa SC ambayo mara kadhaa imekuwa ikitwaa ubingwa katika mashindano maalum ya vyombo vya habari yanayofanyika kila mwaka mkoani Arusha.
  Alisema kuwa benki ya TPB ni wadau wakubwa wa michezo na mbali ya Taswa SC, pia usaidia timu nyingine.
  “Waandishi wa habari wameonyesha mfano mkubwa kwa kucheza soka na netiboli, wameamua kuhamasisha michezo katika jamii, kwa vitendo, hii imetupa faraja kubwa sana kwetu, ”alisema Chichi.
  Mwenyekiti waTaswa SC, Majuto Omary aliishukuru benki ya TPB kwa kuendelea kuwakumbuka na kuahidi kutumia vifaa hivyo  kwa umakini mkubwa na kushinda katika mechi zao mbalimbali.
  “Tunajivunia uwepo wa Benki ya  TPB kwa kuthibitisha kuwa ni benki halisi ya Watanzania, nachukua fursa hii kuwaomba Watanzania kufungua akaunti zao katika benki hii na vile vilekuomba wadau wengine kufuata  mfano  kwa kuisaidiaTaswa SC ili iweze kufanikisha shughuli zake,” alisema Majuto.

older | 1 | .... | 1722 | 1723 | (Page 1724) | 1725 | 1726 | .... | 1898 | newer