Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

WAZIRI LUGOLA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UINGEREZA JIJINI DODOMA LEO

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Uingereza na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Lugola, jijini Dodoma leo.

Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke (kushoto) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Lugola, jijini Dodoma leo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimkaribisha ofisini kwake jijini Dodoma, Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke kwa ajili ya mazungumzo ya kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
………………..

Na Felix Mwagara, MOHA 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amefanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini, Sara Cooke na kumuakikishia ushirikiano zaidi kati ya Wizara yake na Ubalozi huo nchini. Mazungumzo hayo ya zaidi ya saa moja yalifanyika ofisini kwa Waziri Lugola, jijini Dodoma leo ambayo yalijadili masuala mbalimbali ikiwemo uimarishaji wa ushirikiano kati ya Wizara na ofisi ya Balozi huyo nchini. 

Waziri Lugola alimuakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa Wizara yake imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio nchini. “Mheshimiwa Balozi nashukuru sana kwa kunitembelea, najisikia furaha kwa ujio wako na karibu sana wakati wowote, Wizara yangu pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” alisema Lugola. 

Hata hivyo, Balozi Sara alimpongeza Waziri Lugola kwa kuteuliwa na Rais John Magufuli kuiongoza Wizara hiyo na pia alimuakikishia ushirikiano zaidi kati ya Uingereza na Tanzania. “Hongera sana mheshimiwa Waziri kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani na pia nimefurahi kuja katika ofisini yako kufanya mazungumzo nawe,” alisema Balozi Sara.

WAZIRI MKUU AZINDUA MKAKATI NA MPANGO KAZI WA KUJUMUISHA MASUALA YA JINSIA NDANI YA BUNGE

$
0
0
 Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akikata utepe katika hafla ya uzinduzi wa Mkakati na Mpango Kazi wa Kujumuisha Masuala ya Jinsia Ndani ya Bunge iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. Shughuli hiyo imeshudiwa na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, Naibu Spika, Mhe. Tulia Ackson,  Katibu wa Bunge Ndugu Stephen Kagaigai na mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Ndugu Godfrey Mulisa.
 Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akimkabidhi Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai kitabu cha Mkakati na Mpango Kazi wa Kujumuisha Masuala ya Jinsia Ndani ya Bunge mara baada ya kuzindua Mkakati huo leo katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. Anayefuata ni Naibu Spika, Mhe. Tulia Ackson na Katibu wa Bunge Ndugu Stephen Kagaigai, wa kwanza kushoto ni mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Ndugu Godfrey Mulisa.
 Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai wakifurahia uzinduzi wa Mkakati na Mpango Kazi wa Kujumuisha Masuala ya Jinsia Ndani ya Bunge uliofanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. Wengine ni Naibu Spika, Mhe. Tulia Ackson, Katibu wa Bunge Ndugu Stephen Kagaigai na wa kwanza kushoto ni mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Ndugu Godfrey Mulisa.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa mara baada ya uzinduzi wa Mkakati na Mpango Kazi wa Kujumuisha Masuala ya Jinsia Ndani ya Bunge uliofanyika leo katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma wengine ni Naibu Spika, Mhe. Tulia Ackson, Katibu wa Bunge Ndugu Stephen Kagaigai, mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Ndugu Godfrey Mulisa (wa kwanza kushoto), wengine nyuma ni watendaji mbalimbali wa Mradi wa kulijengea Bunge Uwezo (LSP). PICHA NA OFISI YA BUNGE.



WAZIRI MKUU AWAONYA WAAGIZAJI WA TAULO ZA KIKE
*Ni wale wazaoziuza kwa bei ya juu licha ya Serikali kuziondolea kodi
*Asisitiza kwamba Serikali haitasita kuwafutia leseni zao za uagizaji

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewatakabaadhi ya waagizaji wa taulo za kike ambao wanaziuza kwa bei ya juu licha ya kufutwa kwa kodi, waache mara moja na Serikali haitasita kuwafutia leseni zao za uagizaji mara watakapogundulika kutotekeleza maelekezo hayo.

Waziri Mkuu ametoa onyo hilo leo (Jumatano, Novemba 7, 2018) wakati akizindua mkakati wa Bunge wa masuala ya kijinsia, Bungeni jijini Dodoma. Amesema Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha kuwa wanawake wanawekewa mazingira mazuri yatakayowawezesha kupiga hatua zaidi.

Amesema hatua hizo ni pamoja na kuondoa kodi ya taulio za kike ili kuwezesha wanafunzi wa kike ambao walikuwa wanaacha masomo kutokana na changamoto ya kununua taulo za kike kwa ajili ya kujisitiri wakati wa hedhi wazipate kwa gharama nafuu.Waziri Mkuu amesema hatua nyingine ni mpango wa Serikali wa kujenga zahanati kila kijijina kituo cha afya katika kila kata kwa lengo la kupunguza vifo vya wanawake na watoto vilivyokuwa vinasababishwa na uhaba wa huduma za afya ya mama na mtoto.

Amesema mpango huo wa Serikali unatarajiwa kuongeza tija kwa wanawake hususan katika kuwapunguzia muda ambao wamekuwa wakiutumia katika kutafuta huduma hizo ambazo zilikuwa zinapatikana kutoka umbali mrefu.“Imethibitika kupitia tafiti za kitaifa na kimataifa kwamba uzazi wa mpango huweza kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa hadi asilimia 44 na vifo vya watoto kwa hadi asilimia 35.

Pamoja na kulinda afya ya mama na mtoto, huduma hizi zinawasaidia wanawake na wasichana kupata nafasi za kujiendeleza zaidi pamoja na familia zao na kuongeza ushiriki wao katika shughuli za kiuchumi, kijamii, na kimaendeleo.”Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kuwahamasisha wanafunzi wa kike kusoma masomo ya sayansi sambamba na kuwawekea mazingira wezeshi. Amesema hatua nyingine ni mpango wa Serikali wa kuwasomesha wanawake katika ngazi ya uzamili ili waweze kushika nafasi nyingi zaidi za uongozi Serikalini na mahali pa kazi. Zoezi hilo linaratibiwa na Idara Kuu ya Utumishi.

Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu amesema mifumo yetu, mila na historia vimewafanya wanawake na wasichana wabaki nyuma kwa kujiajiri kwenye sekta isiyo rasmi na isiyo na kipato cha uhakika wala maslahi na kubaki wakiwa wategemezi kiuchumi. Amesema hivi karibuni Serikali imeanza kutekeleza kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani. Kampeni hiyo inalenga kuwaondolea wananchi hususani wanawake tatizo la upatikanaji wa haraka wa huduma ya maji safi na salama.

Kwa upande wake, Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema Bunge linaendeshwa kwa kuzingatia uwiano wa kijinsia kwa kiwango cha kuridhisha. “Hata tunapoteua baadhi ya wabunge kwa ajili ya kutuwakilisha katika mikutano mbalimbali huwa tunazingatia uwiano wa kijinsia.Amesema atahakikisha Bunge linaendeleza azma ya Serikali ya kujenga Taifa lenye usawa wa kijinsia inatimia, ambapo amewataka mawaziri wanapowasilish hotuba za makadirio ya mapato na matumizi ya wizara zao waeleze namna walivyotekeleza jambo hilo.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 – Dodoma
JUMATANO, NOVEMBA 7, 2018.

MATUKIO YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA BUNGENI LEO JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Jenista Mhagama, Bungeni jijini Dodoma Novemba 7, 2018.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza Mbunge wa viti maalum Salma Kikwete, Bungeni jijini Dodoma. Novemba 7, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mbunge wa Malindi Ally Saleh, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma. Novemba 7, 2018

MAGAZETI YA LEO AL HAMISI NOVEMBA 8,2018

DTB-TANZANIA YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA AMANA.

$
0
0
Diamond Trust Bank (T) Ltd, (DTB-Tanzania) leo hii, imekabidhi vifaa tiba kwa uongozi wa hospitali ya rufaa ya Amana, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa shughuli za kijamii. DTB-Tanzania kila mwaka hutenga asilimia 2% ya faida yake kwa ajili ya utekezaji wa shughuli za kijamii. Fedha hizi huelekezwa katika kuboresha huduma katika sekta za Afya, Elimu na Mazingira.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na baiskeli za wagonjwa, magodoro, plasta na vifaa vingine vinavyotumika kwenye upasuaji. Vyote hivi vikiwa na thamani ya Tshs 10,000,000.00.

Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Hospitali ya rufaa ya Amana, Dk.Kilomoni alishukuru uongozi wa DTB-Tanzania kwa urafiki uliopo kati ya taasisi hizi mbili ambapo kila mwaka, DTB-Tanzania hutoa msaaada kama huo kwenyeb Hospitali hiyo.

Naye Mkurugenzi wa fedha wa DTB-Tanzania, Ndg. Joseph Mabusi, akiongea na waandishi wa habari wakati wa makabidhiano alisema, “kama taasisi ya kifedha kamwe hatuwezi kusahau jamii. Ni Dhahiri kwamba faida yetu hupatikana katika kufanya biashara na jamii inayotuzunguka. Kwa mtizamo huo, kila mwaka DTB-Tanzania hutenga fedha ambazo hutumika kwenye shughuli kama hii ya leo”.

Ngd, Mabusi alieleza kwamba DTB-Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo, wamekuwa wakilipa ada ya shule kwa watoto yatima watano kutoka kituo cha Kurasini katika shule ya sekondari ya Sullivan Provost iliyopo Kibaha, pia wamukuwa wakichangia miche ya miti katika Wilaya ya Nyamagana -Mwanza, ikiwa na mtizamo wa kuboresha mazingira katika milima iliyoharibiwa na shuguli za kibinadamu.

DTB-Tanzania kwa sasa ina matawi 28 nchini, 14 kati ya hayo yakiwa jijini Dar es Salaam kama ifuatavyo (Mtaa wa Jamaat, Masaki, Morocco, Magomeni, Mbezi, Mbagala, Nyerere, Kariakoo, Tawi la Nelson Mandela, Upanga lililo barabara ya Umoja wa Mataifa na Tawi la CBD lililo kwenye makutano ya barabara za Samora na Mirambo) jingine ni Tawi Mbezi Chini lililo Kata ya Kawe na tawi jipya kabisa la Mlimani City. Matawi mengine yakiwemo matawi mawili kwa miji ya Mwanza na Arusha na tawi moja katika miji ya Dodoma, Kahama, Mbeya, Morogoro, Moshi, Mtwara, Mwanza, Tabora, Tanga na visiwa vya Zanzibar.

DTB-Tanzania ni kampuni tanzu ya makampuni ya DTB (DTB Group) yanayoendesha shughuli za kibiashara katika ukanda wa Africa Mashariki nchini Kenya, Uganda na Burundi. DTB Tanzania pia ni kampuni tanzu ya Mfuko wa Aga Khan wa Maendeleo ya Kiuchumi (The Aga Khan Fund for Economic Development – AKFED) ambayo ni tawi la Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (Aga Khan Development Network -AKDN)
Mkurugenzi wa fedha wa DTB Tanzania, Joseph Mabusi (wa tatu kushoto) akimkabidhi Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dkt. Amim Kilomoni baiskeli za wagonjwa ambapo pia walikabidhi vifaa tiba mbalimbali ikiwemo ni pamoja na magodoro, plasta na vifaa vingine vinavyotumika kwenye upasuaji vyote vikiwa na jumla ya thamani ya Shilingi 10,000,000/= leo jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Kaimu Muuguzi Mkuu wa hospitali ya Amana, Anna Musa (wan ne kushoto) na wa wafanyakazi wa benki hiyo.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali Ya Amana, Dk. Amim Kilomoni (wa pili kushoto) na Kaimu Muuguzi Mkuu wa hospitali hiyo, Anna Musa (kushoto) wakisalimiana na wafanyakazi wa DTB Tanzania, Joseph Mabusi (wa pili kulia) na Sylvester Bahati (kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano ya msaada wa vifaa tiba mbalimbali toka Benki hiyo ikiwemo;-Baiskeli za wagonjwa, magodoro, plasta na vifaa vingine vinavyotumika kwenye upasuaji vyote vikiwa na jumla ya thamani ya Shilingi 10,000,000/= katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam.
Kaimu Muuguzi Mkuu wa hospitali ya Amana, Anna Musa, akitoa maelezo kwa wafanyakazi wa DTB Tanzania baada ya wafanyakazi hao kufanya ziara fupi katika hospitali hiyo ambapo pia walikabidhi msaada wa vifaa tiba mbalimbali ikiwemo;-Baiskeli za wagonjwa, magodoro, plasta na vifaa vingine vinavyotumika kwenye upasuaji vyote vikiwa na jumla ya thamani ya Shilingi 10,000,000/= leo jijini Dar es salaam.
Kulia ni Mkurugenzi wa fedha DTB Tanzania, Joseph Mabusi akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wa makabidhiano ya msaada wa vifaa tiba mbalimbali toka DTB-Tanzania ikiwemo;-Baiskeli za wagonjwa, magodoro, plasta na vifaa vingine vinavyotumika kwenye upasuaji vyote vikiwa na jumla ya thamani ya Shilingi 10,000,000/= katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali Ya Amana, Dk. Amim Kilomoni akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wa makabidhiano ya msaada wa vifaa tiba mbalimbali toka DTB-Tanzania ikiwemo;-Baiskeli za wagonjwa, magodoro, plasta na vifaa vingine vinavyotumika kwenye upasuaji vyote vikiwa na jumla ya thamani ya Shilingi 10,000,000/= katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa fedha wa DTB Tanzania, Joseph Mabusi na Kaimu Muuguzi Mkuu wa hospitali ya Amana, Anna Musa (kushoto).
 

Punguzo mpaka 70% msimu huu wa Jumia Black Friday 2018!

$
0
0
Ni Black Friday kila Ijumaa kuanzia Novemba 16 mpaka Desemba 7.

Ukiachana na punguzo la mpaka 70%, zawadi za bure ikiwemo pikipiki kutolewa bure kwa wateja!

Zimesalia wiki kadhaa kabla ya kuanza kwa msimu wa sikukuu, mapumziko, na shamrashamra za mwisho wa mwaka. Kipindi hiki huwa na pilikapilika nyingi za manunuzi ya mahitaji mbalimbali kama vile vyakula, mavazi, zawadi kwa ajili ya familia, jamaa na marafiki pamoja na vitu vingine kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Ni kipindi ambacho endapo haukujipanga awali au usipokuwa makini unaweza kujikuta unatumia gharama nyingi kwa kununua vitu mbalimbali.

Jumia kama kawaida yake huwa na tukio kubwa kabisa la mauzo la mwaka linalojulikana kama Black Friday. Katika msimu huu wa mwaka 2018 wateja wataweza kunufaika na manunuzi ya bidhaa lukuki kwa Ijumaa nne mfululizo kuanzia Novemba 16 mpaka Desemba 7. Katika kipindi hiki chote kutakuwa na ofa na punguzo kwenye bidhaa tofauti mpaka 70%. Pia kutakuwepo na ofa ya mauzo ya bidhaa za ndani ya muda mfupi (Flash Sales), zawadi (Treasure Hunts), vocha za manunuzi pamoja na huduma kwa wateja kupelekewa bidhaa walizonunua mpaka walipo bila ya malipo.
Lakini pia inajivunia katika kuleta mapinduzi ya biashara kwa njia ya mtandao na kuongeza thamani miongoni mwa wafanyabiashara nchini Tanzania. Ni bure kujiunga kwenye mtandao wake, husaidia kuwatangaza nje ya mipaka ya sehemu zao za biashara, huongeza na kuwafikia wateja wengi hivyo faida huongezeka. Kwa kuongezea, huduma ya kupeleka bidhaa kwa wateja huwa ni jukumu la Jumia, hivyo wafanyabiashara hawana wasiwasi kuhusu namna wateja watakavyofikishiwa bidhaa zao.

Imezoeleka wateja kutembea umbali mrefu kufuata yalipo maduka kwa ajili ya kufanya manunuzi kitu ambacho huwapotezea muda na gharama. Kupitia Jumia wanaweza kununua chochote wakitakacho kutoka kwa wafanyabiashara tofauti kupitia mtandaoni iwe kwa kutumia kompyuta, tabiti (tablet) au App ya Jumia kupitia simu zao za mkononi.

Sekta ya biashara za mtandaoni bado ni ngeni miongoni mwa watanzania hivyo wengi huwa na hofu ya ubora na usalama wa bidhaa zao. Bidhaa zote zinazopatikana kwenye mtandao wa Jumia ni halisi na zenye ubora wa juu kwasababu ni kutoka kwa wauzaji na wafanyabiashara walewale ambao wateja wanawatambua, wamewazoea na kuwatumia siku zote. Utofauti ni maduka yao kuwepo kwenye mfumo wa mtandaoni.

Jumia ina sera ya malipo kufanyika mara baada ya baada ya mteja kupokea na kujiridhisha kuwa bidhaa alizoziona mtandaoni na kuziagiza ndizo zenyewe. Na endapo mteja atakuwa ameletewa bidhaa ambayo siyo aliyoiagiza (ni mara chache kutokea kwa jambo hili) anao uwezo wa kuomba kubadilishiwa bila ya gharama zozote. Mteja anao uhuru wa kufanya malipo aidha kwa njia ya pesa taslimu au kwa kutumia Tigo Pesa.

Black Friday ni msimu mkubwa na maarufu kwa wafanyabiashara duniani hususani kwenye nchi za Marekani na Ulaya ambapo umeanza mnamo karne ya 19. Tukio hili huwa linafanyika katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi Novemba kuashiria kuanza kwa msimu wa sikukuu za Krisimasi. Wafanyabiashara hutoa ofa na punguzo kubwa la bei katika huduma na bidhaa wanazozitoa kwa wateja ili kuwarahisishia kufanya manunuzi kwa unafuu.

Katika msimu huu wafanyabiashara hufanya mauzo ya bidhaa kwa kiasi kikubwa na kupata faida pengine kuliko kipindi chote cha mwaka. Hii ni sababu inayopelekea wafanyabiashara kujiandaa vya kutosha na kuuheshimu msimu huu kwani wanakuwa na uhakika wa kunufaika kwa kiasi kikubwa.

Kwa upande wa wateja wao hunufaika na ofa za bidhaa na huduma, mapunguzo makubwa, vocha za manunuzi pamoja na zawadi kemkem ili kuwarahisishia na kuwashawishi kufanya manunuzi. Baadhi ya wateja werevu husubiria na kujipanga kwa kufanya manunuzi katika msimu huu kwa sababu chochote walichokuwa wanakitamani huuzwa kwa punguzo kubwa ukilinganisha na kipindi chochote cha mwaka.

Jumia ni sehemu pekee ambayo unaweza kupata huduma na bidhaa mbalimbali (sehemu moja) mtandaoni. Unaweza kununua maelfu ya bidhaa mbalimbali halisi na bora kutoka kwa wafanyabiashara wanaoaminika ndani na nje ya nchi, kupata huduma za malazi na usafiri, pamoja na huduma ya chakula kutoka kwenye migahawa tofauti jijini Dar es Salaam.


SADAKA NETWORK YAWAOMBA WATANZANIA KUCHANGIA FEDHA KUFANIKISHA UPASUAJI WA WANAWAKE NA WATOTO

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

TAASISI isiyo ya kiserikali ya SADAKA Network imeunga mkono juhudi za Hospitali ya Aga Khan, Muhimbili na Taasisi ya Women to Women katika kufanikisha upasuaji wa urekebishaji (upasuaji wa urembo) kwa wanawake na watoto utakaofanyika 27 November mwaka huu. 

Hospitali ya Agha Khan, Muhimbili na Taaisis ya Women to Women ziko kwenye harakati za kuweka tabasamu kwenye nyuso za wahanga wa ukatili wa nymbani uliosababisha wahanga hao kuathirika. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mwanzilishi wa SADAKA Network Dkt Ibrahim Msengi amesema kuwa SADAKA Network umeamua kuunga mkono kwa kuchangisha fedha kupitia programu yake ili kufanikisha mpango huo, wameamua kutumia viongozi wa jamii na watu maarufu ndani ya Tanzania kuhabarisha wananchi wote ili waweze kuchangisha fedha ili kwa pamoja waweze kusaidia kurejesha tabasamu kwenye uso zao. 

Dkt Ibrahim amesema kuwa, ukatili wa nyumbani na ajali unaweza ukasababisha mauti au majeraha yanayoweza kubadilisha muelekeo wa maisha ya yao, watu wameshuhudia, kusikia au kuona kupitia luninga wanawake na watoto ambao muonekano wao umebadilika kisa ajali au ukatili wa nyumbani au watoto wenye maisha yaliybadilishwa kisa wazazi waliowakatili. 

Amesema kuwa, Kwa pamoja wanatumia kauli mbiu ya "Kurudisha tabasamu usoni mwao" ili kuweza kurejesha utu watu, wanawake na watoto wanakuwa wamejeruhiwa sana na imewapelekea kuwa na aibu hata wanashindwa kuendelea na shughuli zao na majeraha haya yanawabadilisha, yanawafanya wajihisi kuwa tahamani yao kama binadamu imeshuka. 

Meneja Masoko na Mahusiano wa Agha Khan Hospital Olayce Steven Lotha amesema, kwa mwaka huu wamepana kuwafanyia upasuaji wanawake na watoto 40 kutoka kwenye Mikoa tofauti nchini ila uhitajiw a watu katika upasuaji huo ni mkubwa sana. 

Lotha amesema, "katika awamu ya kwanza ya mwaka 2016 tuliwafanyia upasuaji watu 36 na awamu ya pili wakiwa 35, na kwa mwaka 2017 ulihusisha wanawake na watoto 30 ila kwa 2018 lengo letu kuu ni 40 na tayari tumeshawapata kutoka Bunda, Kagra, Mwanza, Iringa, Mbeya, Dodoma na Tanga," 

Upasuaji huo utahusisha Madaktari bingwa wa upasuaji 16, 10 wakitoka kwenye taasisi yaWomen to women, watatu wakitoka Agha Khan na watatu Muhimbili, na timu ya manesi 10 pamoja na wataalumu wa dawa za usingizi. 

Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum pamoja na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Jackson Jackosn , Balozi wa Rejesha tabasamu usoni mwao Yvyone Cherry kwa pamoja wameungana kuwaomba watanzania wachangie na kuuna mkono juhudi za SADAKA Network ili kuweza kuanikisha upasuaji huo na kurejesha tabasamu usoni mwao na kila mmoja achangie kwa uwezo wake. 

Mtendaji Mkuu wa SADAKA Nwtwork Viola James, ili kufanikisha upasuaji huu kinahitajika kiasi cha Shiling Milion 268 kwa gharama zote na tunatambua kuwa Hospitali ya Muhimbili haiwezi kugharamikia peke yake na ndio maana SADAKA tukaamua kushirikiana kwa pamoja kuweza kuchangisha fedha itakayosaidia kurejesha tabasamu usoni mwao. 

Viola ametaja namba za kuchangia kwa kiasi chochote kwa Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum kupitia namba *150*92# halafu unaandika namba A0002, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Jackson Jackosn *150*92# halafu P0002 na kwa Balozi Yvyone Cherry ni *150*92# Y003. 
Mwanzilishi wa SADAKA Network Dkt Ibrahim Msengi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na taasisi yake kuunga mkono juhudi za Hospitali ya Aga Khan, Muhimbili na Taasisi ya Women to Women katika kufanikisha upasuaji wa urekebishaji (upasuaji wa urembo) kwa wanawake na watoto utakaofanyika 27 November mwaka huu, kushoto ni Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum na Meneja Masoko na Mahusiano wa Agha Khan Hospital Olayce Steven Lotha .
Meneja Masoko na Mahusiano wa Agha Khan Hospital Olayce Steven Lotha akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na upasuaji wa urekebishaji (upasuaji wa urembo) kwa wanawake na watoto utakaofanyika 27 November mwaka huu. 
Balozi wa Rejesha tabasamu usoni mwao Yvyone Cherry akiwa anawahisi jamii kuchangia kwa kiasi chochote ili kufanikisha upasuaji wa wanawake na watoto waliofanyika ukatili majumbani. Kushoto ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Jackson Jackson, Mwanzilishi wa SADAKA Network Dkt Ibrahim Msengi na Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum. 
Waandishi wa habari na wadau mbalimbali wakifuatilia mkutano huo.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA TIMU YA WATAALAMU WA MATIBABU YA MOYO IKULU JIJINI DAR

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wataalamu mbalimbali wa Afya wakiwemo Madaktari bingwa wa Moyo kutoka nchini Israeli, pamoja na Madaktari wawili kutoka nchini Marekani, Ikulu jijini Dar es Salaam.  
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Uti wa mgongo ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji Ubongo kutoka Hospitali ya Weil Cornell New York nchini Marekani  Profesa Roger Hartl akizungumza katika kikao kilichowajumuisha Wataalamu mbalimbali wa Afya wakiwemo Madaktari bingwa wa Moyo kutoka nchini Israeli, pamoja na Madaktari wawili kutoka nchini Marekani, Ikulu jijini Dar es Salaam.  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia zawadi ya Kitabu alichopewa Dkt. Akiva Tamir Mwakilishi  wa Madaktari hao kutoka Taasisi ya Save a Child’s Heart kutoka Israel kama Heshma Maalumu ambayo Taasisi hiyo huitoa kwa watu Maalum.

Madaktari hao kutoka Taasisi ya Save a Child’s Heart ya Israel pamoja na Madaktari kutoka Marekani wakiwa Ikulu jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza mazungumzo yao na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi mara baada ya mazungumzo ujumbe wa Madakatari kutoka Taasisi ya Save a Child’s Heart ya Israel pamoja na Madaktari kutoka Marekani Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa Barua ya Shukrani Balozi wa Israel hapa nchini Noah Gal Gendler ili aiwasilishe kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwa ajili ya kushukuru kutokana na mchango wa Taasisi hio ya Save a Child’s Heart.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wataalamu mbalimbali wa Afya wakiwemo Madaktari bingwa wa Moyo kutoka nchini Israeli, pamoja na Madaktari wawili kutoka nchini Marekani, Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuzungumza nao na kuwashukuru kwa huduma wanayoitoa nchini. Wengine katika picha ni Balozi wa Israel hapa nchini Noah Gal Gendler wanane kutoka (kushoto) waliosimama mstari wa mbele Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Dkt. Faustine Ndungulile watisa kutoka kulia mstari wa mbele.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Uti wa mgongo ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji Ubongo kutoka Hospitali ya Weil Cornell New York nchini Marekani  Profesa Roger Hartl mara baada ya Mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Uti wa mgongo ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji Ubongo kutoka Hospitali ya Weil Cornell New York nchini Marekani  Profesa Roger Hartl mara baada ya Mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

SERIKALI KUTAFUTA SOKO LA UHAKIKA ZAO LA KOROSHO

$
0
0

SERIKALI imewataka wananchi hususani wakulima wa korosho nchini kuendelea kuwa wavumilivu na watulivu wakati ikiendelea kuzungumza na wanunuzi wakubwa wa korosho kutoka maeneo mbalimbali duniani ili kupata masoko ya uhakika ya zao hilo. 

Kauli hiyo imetolewa leo (Alhamisi, Novemba 8, 2018) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akijibu swali la mbunge wa Mtwara Mjini, Maftaha Nachuma katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma.

Mbunge huyo alitaka kupata kauli ya Serikali kuhusu bei ya korosho ambayo imeshuka katika msimu wa mwaka huu hadi kusababisha wakulima kugomea baadhi ya minada, ambapo Waziri Mkuu amesema suala hilo linafanyiwa kazi na Serikali.“Tunaendelea kuzungumza na wanunuzi wakubwa ili tujue ni nani atanunua korosho na kwa kiasi gani, hivyo tunawaomba wakulima waendelee kuwa watulivu, Serikali inajitahidi kuhakikisha zao hilo linatafutiwa masoko. Korosho zitanunuliwa tu.”

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema Serikali imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo ya ujenzi wa viwanda vya mbolea, ambapo inatoa wito kwa wawekezaji kuja kuwekeza katika viwanda vikiwemo vya pembejeo.Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu, Neema Mgaya aliyetakakujua Serikali ina mpango gani katika kuwahamasisha wawekezaji kuja kuwekeza katika viwanda vya mbolea ili wakulima waweze kuipata kwa gharama nafuu.

Amesema viwanda vya mbolea vilivyopo nchini ni vichache na havitoshelezi mahitaji, hivyo kwa sasa kuna utaratibu wa kujenga viwanda vingine viwili kimoja kitajengwa Kilwa mkoani Lindi na kingine kitajengwa Mtwara. Kukamilika kwa viwanda hivyo kutaongeza uzalishaji wa mbolea na kupunguza uagizaji kutoka nje ya nchi.Kadhalika, Waziri Mkuu amefafanua kuhusu suala la wakulima wa mahindi kukosa masoko, ambapo amesema ruhusa ya kuuza mahindi nje ya nchi ilishatolewa. Amesema jambo hilo lilitolewa ufafanuzi na Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba.

Waziri Mkuu amesema licha ya kuwepo kwa kibali cha kuuza mahindi nje ya nchi ni lazima Serikali itambue kiasi gani kinachotolewa kwa ajili ya kuuza nje ya nchi, hivyo muuzaji anatakiwa awasisilishe taarifa zake kwa wakuu wa wilaya. “Tunahitaji kuwa na takwimu za mauzo na bei ili kujua kiasi kilichouzwa pamoja na kiasi cha fedha kilichopatika.”

Kuhusu upatikanaji wa pembejeo kwa gharama nafuu ikiwemo mbolea, Waziri Mkuu amesema suala hilo linaratibiwa vizuri na Wizara ya Kilimo na tayari asilimia 60 ya mahitaji ya pembejeo tayari imeshaingia nchini, hivyo Serikali itahakikisha zinawafikia wakulima kwa wakati.

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Lucia Mlowe, Mbunge wa Viti Maalumu aliyehoji Serikali inatoa tamko gani kuhusu tatizo kubwa la wakulima wa mahindi kukosa masoko ya uhakika.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980
 41193 – Dodoma
ALHAMISI, NOVEMBA 8, 2018.

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA UKUMBI WA MIHADHARA NA BWENI

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Ukumbi wa Mihadhara na Bweni la Wanafunzi katika chuo cha Misitu, Olmotonyi, Arusha. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya Bweni jipya la Wanafunzi wa Kike litakalochukua wanafunzi 150 kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki Dkt. Ezekiel Mwakalukwa wakati wa hafla ya ufunguzi wa Ukumbi wa Mihadhara na Bweni la Wanafunzi katika chuo cha Misitu, Olmotonyi, Arusha. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Balozi wa Nchini Mhe. Elisabeth Jacobsen, Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki Dkt. Ezekiel Mwakalukwa, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Japhet Hasunga (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo mara baada ya kukagua Bweni jipya la wanafunzi wa kike 150 waati wa hafla ya ufunguzi wa Ukumbi wa Mihadharaa na Bweni la Wanafunzi katika chuo cha Misitu, Olmotonyi, Arusha. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia baadhi ya kazi za wanafunzi wakati wa hafla ya ufunguzi wa Ukumbi wa Mihadhara na Bweni la Wanafunzi katika chuo cha Misitu, Olmotonyi, Arusha.

MAKAMU WA RAIS AANZA ZIARA YA SIKU SABA MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Kilimanjaro tayari kwa ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Anna Mghwira akisoma taarifa ya Mkoa mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ameanza ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani humo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MKUU WA JESHI LA MAGEREZA NCHINI, CGP PHAUSTINE KASIKE AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI IRINGA

$
0
0
 Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP) Phaustine Kasike (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Iringa,  Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Hassan Mkwanda na Maafisa wengine wa Magereza Mkoani Iringa, muda mfupi alipowasili leo Novemba 8, 2018 Mkoani humo. CGP Kasike yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kukagua magereza yote ya Mkoa wa Iringa na kuzungumza na Maafisa na askari pamoja na kujua chamgamoto mbalimbali wanazokutana nazo wakati wakitekeleza majukumu yao.
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Mhe. Richard Kasesela akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP) Phaustine Kasike walipokutana  Mkoani Iringa alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa kabla ya kuendelea na ziara yake ya kikazi, leo Novemba 8, 2018.
 Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Iringa wakisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini (CGP) Phaustine Kasike walipokutana  Mkoani Iringa alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Mkoa kabla ya kuendelea na ziara yake ya kikazi.
  Mkuu wa Magereza Mkoa wa Iringa,  Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Hassan Mkwanda  akimkaribisha Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini (CGP) Phaustine Kasike(katikati meza kuu) ili azungumze na baadhi ya Maafisa na askari wa Gereza Iringa(hawapo pichani, leo Novemba 8, 2018 . Kulia ni  ACP. Josephine Semwenda ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa Mkuu wa Magereza Mkoa  wa Lindi.
 Baadhi ya Askari wa Gereza la Wilaya Iringa wakifuatilia maelekezo katika Baraza lililoongozwa na  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike ambapo askari hao wameelezea changamoto zao kiutendaji leo Novemba 8, 2018.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Mhe. Richard  Kasesela(watatu toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(wa tatu toka kulia) pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Iringa ( Picha na Jeshi la Magereza).

SPIKA WA BUNGE AZINDUA KIKUNDI CHA WABUNGE CHA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

$
0
0
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akizungumza wakati akizundua Kikundi cha Wabunge cha Malengo ya Maendeleo Endelevu (Parliamentary Group on Sustainable Development Goals-SDGs) Jijini Dodoma.
Katibu wa Kikundi cha Wabuge wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (Parliamentary Group on Sustainable Development Goals-SDGs) Mhe. Salome Makamba akizungumza wakati wa uzinduzi wa kikundi hicho Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Wabuge wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (Parliamentary Group on Sustainable Development Goals-SDGs) Mhe. Augustine Vuma akizungumza wakati wa uzinduzi wa kikundi hicho Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge katika picha ya pamoja na Kikundi cha Wabunge kinachojishughulisha na Malengo ya Maendeleo Endelevu (Parliamentary Group on Sustainable Development Goals-SDGs) Jijini Dodoma.
PICHA NA BUNGE

CHIRWA ASAINI RASMI AZAM, AAHIDI KUIFANYIA MAKUBWA AZAM

$
0
0
Na Agness Francis, Globu   ya Jamii.

Uongozi wa klabu ya soka ya Azam fc umefanikiwa  kuinasa saini ya mshambuliaji Obrey Cholla Chirwa kwa mkataba wa mwaka mmoja. Ni baada ya dili lake la kurudi Yanga kugonga mwamba.

Uongozi  wa Azam FC umesema kuwa usajili wa Chirwa ni sehemu ya mapendekezo ya benchi la ufundi la Azam chini ya kocha mkuu Hans Van der Plujim katika kuboresha eneo la ushambuliaji la  kikosi hicho. 

Chirwa amejiunga na Azam baada ya kuvunja mkataba na klabu ya Nogoom El Mostakbal inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Misri ambayo alisajiliwa hivi karibuni.Mshambuliaji huyo ametua Azam akiwa ameshawahi pia kuichezea Yanga na kisha baadaye kukimbilia huko Uarabuni baada ya mambo ya kifedha na mabingwa hao wa kihistoria kutokuwa sawa.

Baada ya kurejea nchini, awali ilielezwa Chirwa angeweza kurudi Yanga lakini mambo yamekwenda tofauti.Kupitia ukurasa wa Istagram wa klabu ya Yanga,  Uongozi huo umebainisha  kuwa awali mshambuliaji  huyo alikuwa arejee klabuni  licha ya kocha mkuu wa  klabu hiyo mwinyi Zakhera kupinga usajiri wake."Kilichomkwamisha Chirwa kurudi Jangwani ni dau la mshahara alilotaka kulipwa alitaja kiasi kikubwa  cha fedha ambacho Yanga hawakukubali"

Licha ya Octoba 20  mwaka huu Chirwa  alionekana  uwanja wa Taifa katika uchezo uliopigwa na Yanga dhidi ya Alliance  akiwa na kaimu katibu Mkuu wa Yanga Omary  Kaya pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Husein Nyika na Mdau mkubwa  Yanga  Abbas Tarimba, ambapo pia aliingia vyumba vya kubadilishia nguo na kusalimiana na wachezaji wa Yanga

Chirwa sasa ataanza rasmi kuitumikia Azam kuanzia Novemba 15 2018 ambapo dirisha dogo la usajili litakuwa limeshafunguliwa.Na baada ya kutambulishwa, Chirwa amesema kwamba amejiunga na Azam FC kukiongezea nguvu kikosi ambacho tayari ni bora ili wafanikishe azam ya kutwaa mataji.Kwa upande wake, kocha Pluijm ambaye alifanya kazi na Chirwa katika klabu ya Yanga, alisema kwamba  amefurahi sana kumpata mchezaji huyo anayejituma na mwenye bidii kubwa uwanjani.

Chirwa sasa anakwenda kukutana na mshambuliaji raia wa Mzimbabwe, Donald Dombo Ngoma aliyewahi kufanya naye kazi FC Platinums ya Zimbabwe na Yanga.Kama ilivyokuwa Yanga, Ngoma alianza kuja na baadaye akamvuta Chirwa akimshawishi Pluijm aje kuongeza nguvu na kwa Azam hivyo pia, inaaminika Donald amemshawishi tena Pluijm kumsajili mchezaji huyo. .
Mshambuliaji Obrey Cholla Chirwa akikabidhiwa Jezi ya timu ya Azam fc na Kocha Mkuu wa Kikosi hicho Hans Van De Plujim mara baada ya kusaini kandarasi za kutumikia  klabu hiyo  kwa mwaka mmoja leo Jijini Dar es Salaam.

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO TOKA KWA MABALOZI WAPYA WA UAE, CANADA NA SPAIN IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Spain nchini Mhe. Maria Pedros Carrtero  kwenye sherehe iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 8, 2018  

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi kwenye sherehe iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 8, 2018.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Canada nchini Mhe. Pamela O'Donnel  kwenye sherehe iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 8, 2018  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Canada nchini Mhe. Pamela O'Donnel  kwenye sherehe iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 8, 2018 

YALIYOJITOKEZA KWENYE MAGAZETI YA LEO IJUMAA NOVEMBA 9.2018

TAASISI YA SADAKA NETWORK,HOSPITALI YA MUHIMBILI,AGA GHAN NA WOMEN TO WOMEN FOUNDATION KURUDISHA TABASAMU USONI KWA WATU WALIOHARIBIKA MAUMBILE YAO.

$
0
0
Watanzania wameombwa kwa pamoja kushirikiana na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya SADAKA NETWORK , Hospitali ya Muhimbili na Aga Ghan kwa kushirikiana na Women to women foundation kuchangia kurudisha tabasamu usoni  kwa wakina mama na watoto waliopata matatizo hayo kwa  bahati mbaya, kupata ajali,kwa ukatili wa kijinsia, kupigwa au matatizo yoyote yaliyopelekea wao kuharibika maumbile yao ikiwa ni usoni ama sehemu nyengine ya mwili. 

Mwanzilishi wa taasisi hiyo Dkt. Ibrahim Msengi akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa gharama za kuwatibu watoto na akina mama ni kubwa na haziwezi kubebwa na Muhimbili au Aga Ghan peke yake wala Women to women foundation,bali ghalama hizi zitafanikiwa endapo wananchi wataungana kwa pamoja ili kutoa michango yao ili kufanikisha zoezi hilo.

"Upasuaji huu utafanyika katika Hospitali ya Muhimbili na Aga Ghan na tunatarajia kuwafanyia upasuaji watu 40 kutoka sehemu zote Tanzania,hivyo pesa inayohitajika ni Tsh Milioni 268" alisema Dkt. Msengi.
Dkt. Ibrahim Msengi(wa kwanza kulia) Muasisi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya SADAKA Network, alisema lengo la kuwaita waandishi wa Habari ni kutaka  kusaidiana katika kutoa huduma kwa jamii "SADAKA Network ikishirikiana na Aga Khan, Muhimbili wakishirikiana na Women to women Foundation ambao kazi yao kubwa ni kuwasaidia akina mama na watoto katika afya, wanakuja kuona akina mama na watoto pamoja na akina baba na watoto ambao wameharibiwa maumbile yao kwa sababu mbalimbali ambayo inaweza ikawa ni kwa bahati mbaya, kupata ajali,kwa ukatili wa kijinsia kwa kupigwa, kwa hiyo hawa ndugu wakishirikiana na sisi watakuja kurudisha kile kilichoharibika kirudi katika hali yake" alisema Dkt. Msengi. Alimalizia kwa kusema kuwa wataalam hao wanauwezo mkubwa wa kufanya upasuaji na kumrudisha mtu katika hali yake hata  kama atakuwa aliharibika kwa kiasi gani.
 Baba Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosis ya Dar es Salaam  Jackson Sostenes Jackson, alisema kuwa SADAKA Network ni jukwaa ambalo linaunganisha watu kwa umoja wao kama watanzania,kuacha itikadi na tofauti tulizonazo, amewashukuru Women to Women Foundation kutoka Marekani kuja kuungana na watanzania katika hali na majanga ambayo yamewakumba ndugu ambao wameathirika kutokana na unyanyasaji wa kijinsia. alimalizia kwa kusema kuwa "Mtu yeyote anaweza kuchangia kwa M-Pesa ama Tigo Pesa piga namba *150*92# kisha ingiza Code number yangu  ambayo ni P0002  kisha utachangia kile unachoweza kuchangia"
Sheikh Alhad Mussa Salum Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mwenyekiti wa kamati ya Amani wa viongozi Dini,alisema kuwa anaungana na watanzania wote kusapoti mradi huu unaoratibiwa na SADAKA Network  wa kurudisha tabasamu usoni muhimu wenye lengo la kuwasaidia wale wote wanaoathirika kwa njia moja au nyengine majumbani, alisema ili kuwachangia kwa kadili ya mtu na uwezo alionao, "Ukiwa na M-Pesa ama Tigo Pesa piga namba *150*92# kisha ingiza Code number yangu  ambayo ni A0002 kisha utachangia kile unachoweza kuchangia" alisema 
Alhad Mussa Salum Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Balozi wa Rudisha Tabasamu lao  Msanii Maarufu wa kuigiza Filamu za Kitanzania Yvone Cherry maarufu kwa jina la Monalisa,alisema kwamba kuna changamoto nyingi ambazo wanapitia wazazi katika kulea watoto ambapo watoto hawa hukumbwa na majanga mengi hasa wakiwa majumbani ikiwa ni pamoja na kuungua kwa maji,chai, chakula ama moto hii inapelekea watoto kuharibika kwa moto. 
aliongeza kuwa kuwa wanaume wanawanyanyasa wakezao kijinsia kwa kuwapiga na hata pengine kuwachoma na moto na baadhi ya watu kumwagia wenzao tindikali jambo linalopelekea watu kuharibika miili yao. Hali hii inapelekea watu kukosa amani,furaha na kuishi vizuri kutokana na majeraha waliyoyapata. Ameishukuru taasisi ya kiraia ya SADAKA Network kwa kushirikiana na Women to Women Foundation kwa kuamua kurudisha tabasamu usoni kwa wote waliopatwa na majanga hayo. 
Mwisho aliwaomba watanzania kuungana pamoja kuwachangia watu hao .  "Ukiwa na M-Pesa ama Tigo Pesa piga namba *150*92# kisha ingiza Code number yangu  ambayo ni Y0002 kisha utachangia kile unachoweza kuchangia" alisema 
Alhad Mussa Salum Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Olai Stephen Ndota Mkuu wa idala ya masoko na mawasiliano  akiwakilisha  Hospitali ya Aga Khan, alisema kuwa shirika la Women to Women Foundation linaundwa na madaktari bingwa wa upasuaji wanawake wanaotoka katika nchi za Canada, Uingereza pamoja na Marekani, "Zoezi hili la upasuaji lilianza mwaka 2016 na hii itakuwa ni awamu ya nne, katika awamu ya kwanza 2016  tuliweza kuwahudumia watu 37, awamu ya pili 2016 tuliwahudumia watu 35 na mwaka 2017 Novemba tuliwahudumia watu 30" Alisema Ndota.
 Viola Massawe Meneja Miradi kutoka taasisi ya SADAKA Network, alisema kuwa SADAKA Network ni mtandao unaopatikana 'Online' na 'Offline'"Jukumu letu kubwa ni kuweza kuwa karibu na jamii na kuwaweka viongozi wa kijamii karibu na jamii ili kuweza kutatua matatizo ya kijamii kwa kutumia miradi" alisema Viola. aliongeza "Tunawaomba watanzania sote kwa pamoja tuungane kuchangia ili tuweze kurudisha tabasamu usoni mwa akina mama hawa." alimalizia kuwa unaweza kuchangia kile ulichonacho kwa kuingia katika Tovuti ya SADAKA Network ambayo ni www.sadakanetwork.com kisha bonyeza miradi ya kijamii
Wanahabari na wadau na wadau wakiwa katika katika mkutano huo.
(PICHA NA FREDY NJEJE)

TPDC YAWEZESHA WANAFUNZI ZAIDI YA 1000 KUNUFAIKA NA VYOO BORA

$
0
0
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limewezesha ujenzi wa vyoo bora kwa shule ya Msingi ya Kivinje yenye jumla ya wananfunzi 1320 iliyopo katika Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi. 

Akiongea wakati wa kuikabidhi mfano wa hundi na kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyoo hivyo Meneja Mawasiliano wa TPDC Bi. Marie Msellemu ameweka wazi kuwa TPDC inatambua kuwa inawajibika kwa jamii ambayo inaendesha shuhguli zake mbalimbali na hivyo maendeleo ya jamii hizo ni suala la msingi kwa Shirika hilo. 

 “Sisi kama Shirika la Umma tunaowajibu kurudisha sehemu ya kile tunachopata kwa jamii zetu hizi ili kuweza kuboresha maeneo mbalimbali ya huduma haswa Afya, Elimu, Maji na utawala bora na hivyo ujenzi wa vyoo bora kwa wanafunzi wa Shule hii ya Kivinje inaangukia katika maeneo yote mawili ya elimu na afya.” Alisisitiza kuwa suala la vyoo bora kwa wanafunzi ni muhimu sana haswa katika kuwapa faraja na kujiamini zaidi wawepo shuleni na hivyo kupelekea umakini zaidi katika masomo yao ambapo huwafanya wafanye vizuri zaidi kwenye masomo yao. Bi Marie Msellemu Meneja wa Mawasiliano akikabidhi hundi ya milioni 16 kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa Ndugu Ramadhani Hatibu mara baada ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa vyoo vya Shule ya Msingi Kivinje Aidha akielezea maendeleo ya ujenzi wa vyoo hivyo, Bi Msellemu aliwahimiza Watendaji wa shule hiyo pamoja na Kamati ya ujenzi kuongeza kasi ya ujenzi wa vyoo hivyo ambavyo kwa sasa vilitakiwa kuwa vimekamilika kwa asilimia kubwa ili kuepuka kipindi cha mvua kubwa ambayo inatarajiwa kunyesha katika mwezi ujao. 

 Akizungumza wakati wa makabidhiano ya mfano wa hundi hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa Ndugu Ramadhani Hatibu alisema, ameridhishwa namna ambavvyo TPDC inavyoshirikiana na Halmashauri hiyo katika kusaidia katika uboreshwaji wa huduma mbalimbali za jamii. Hapa Kaimu Mkurugenzi anaeleza zaidi “kwakweli TPDC mmekuwa mstari wa mbele katika kutushika mkono sisi kama Halmashauri ya Kilwa katika maeneo mbalimbali ambapo katika kumbukumbu zetu zinaonyesha mmefanya mengi tu yakiwemo mchango mlioutoa kawa ajili ya uboreshwaji na ujenzi wa maabara katika Shule zetu za Sekondari, ujenzi wa nyumba za walimu katika Shule ya Sekondari ya Songo Songo, usambazaji wa huduma ya maji kwa Kijiji cha Songo Songo pamoja na Shule ya Sekondari Songo Songo pamoja na uendeshaji wa zoezi la upimaji wa afya na kukabidhi vifaa vya upimaji wa afya katika Kijiji cha Songo Songo” 

Akiweka msisitizo Mkurugenzi huyo aliongezea kuwa “leo hii tunapokabidhiana rasmi kiasi cha milioni 16 lakini pia tunapokagua kwa pamoja utekelezaji wa ujenzi wa vyoo vya Shule ya Msingi Kivinje inazidi kuleta faraja na matumaini katika uhusiano tulioujenga miaka mingi iliyopita na hivyo kwanza ni himize Kamati ya Ujenzi wa Shule hii kuhakikisha ujenzi huu wa vyoo unatekelezwa kwa kasi na weledi ili kutendea haki thamani ya pesa ambayo TPDC wametoa kwa ajili ya uboreshwaji wa shule yetu ili watoto wetu wawe na mazingira rafiki ya kujisomea ambayo yatapelekea ufaulu mzuri kwenye mitihani yao.“ Meneja Mawasiliano akisikiliza muhtasari wa maendeleo yahusuyo maendeleo ya ujenzi wa vyoo toka kwa Kamati ya Ujenzi wa Shule ya Msingi Kivinje. Aidha akisoma taarifa ya ujenzi wa vyoo hivyo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kivinje Ndg. Ngabuba alieleza kuwa, “Shule yetu ina jumla ya wanafunzi 1320 kati yao wakiwa Wasichana 696 na Wavulana 624 na jumla ya Walimu 17 ambao kwa ujumla wetu tulihitaji kuwa na vyoo bora situ kwa kujisitiri lakini pia kuhakikisha suala la afya bora linazingatiwa na hivyo basi kwa kubahatika kupata msaada ktuoka TPDC kwakweli sasa tunaenda kuwa na vyoo bora ambavyo vitasaidia wanafunzi wetu kuwa na amani na kujiamini zaidi wawepo shuleni hapa” “Kwakweli ujenzi umechelewa tofauti na ilivyopangwa nahii ni kutokana na mambo mbalimbali ya kiutawala na kiutaratibu lakini pia uhaba wa seruji ulitokea katika kipindi cha mwezi Juni lakini hivi sasa tuna ahidi kundelea na ujenzi kwa kasi na ufanisi zaidi ili tufikie thamani halisi ya pesa ambayo Shirika letu la TPDC limetoa” aliongezea Mkuu huyo wa shule.

ACP ABDI ISANGO AWAPA SOMO MADEREVA KUHUSU USALAMA BARABARANI NA KUPIMA AFYA

$
0
0
Mgeni Rasmi katika wiki maadhimisho ya Usalama na Afya Barabarani ACP Abdi Isango Kamishna msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Oparesheni Kitengo cha Usalama Barabarani Taifa, anamuwakilisha kamanda wa kikosi cha usalama wa barabarani Taifa akizindua rasmi shughuli hizo za upimaji wa afya kwa madereva wasafirishao mizigo masafa ya mbali iliyoandaliwa na North Star alliance kwa kushirikiana na Puma Energy Foundation , Impala Terminals na Trafigura Foundation.
Ndg. Henry Mgala Bantu mtaalam wa usafirishaji na uchukuzi na mbobezi wa usalama barabarani na Mjumbe wa Balaza la taifa la usalama barabarani na mwenyekiti wa elimu mafunzo na uenezi katika balaza hilo, akiwakumbusha madereva mambo mbalimbali muhimu yahusuyo Sheria za barabarani na somo muhimu la madereva kujitambua.
Mrakibu Msaidizi  wa Polisi Abben Swai Mkuu wa Kitengo cha Elimu Mafunzo na Uenezi wa kikosi cha Usalama wa barabarani Tanzania, akiendesha chemshabongo fupi kwa madereva wa magari ya mizigo yaendayo safari ndefu lengo ni kuwakumbusha tu kuendelea kuwa makini pindi wawapo safarini.
Mrakibu  Msaidizi wa Polisi Yoronimo Kwesibaga Saimon Mkuu wa kituo cha Polisi Bandari, akitoa salam zake wakati wa wiki ya maadhimisho ya siku ya usalama na afya barabarani
 Dkt. Sist Agustino Mosha  Kaimu Mganga Mkuu Manispaa ya Temeke akitoa elimu wa madereva wasafirio safari za mbali kuhusu umuhimu wa kutambua afya zao kipindi chote wawacho safarini, pia kuwakumbusha kutazama afya zao mara kwa mara kabla hawajaanza safari, mwisho aliwakumbusha madereva kuhusina na UKIMWI. 
Mratibu wa Taasisi ya Mabalozi wa Usalama wa Barabarani(RSA) kanda ya Mashariki Bw. David Shao akielezea kwa ufupi umuhimu wa kuwa Balozi wa maswala ya Usalama barabarani na kuwaomba madereva wengi zaidi na watu wengine kujumuika kwa pamoja na kuwa mabalozi ili kusaidia kupunguza ajali. 
Bw. Mohamed Sharif Mwenyekiti Chama cha Madereva Tanzania na Mkufunzi wa Masomo ya usalama barabarani, akisisitiza kuwa kongamano hilo ni muhimu  sana kwa kuwa watu mbalimbali wakiwemo askari wa usalama barabarani, madaktari na watu wengine wameungana na madereva ili waje kuwapa elimu na kuwakumbusha mambo muhimu yahusuyo usalama wa barabarani na kujua afya zao maana ni mambo muhimu na yanayoendana kwa ukaribu. 
Mwakilishi kutoka Impala Terminals akitoa salam zake wakati wa mkutano huo, amewashukuru North Star Alliance pamoja na wahusika wa Usalama kwa ajili ya kuhakisha madereva wanasafiri wanapata huduma ya afya kila wawapo safarini na ndio maana katika yard mbalimbali hata mikoani kuna ofisi za North Star alliance, aliomba ushirikiano huo uendelee zaidi.
Mrakibu Msaidizi  wa Polisi Abben Swai Mkuu wa Kitengo cha Elimu Mafunzo na Uenezi wa kikosi cha Usalama wa barabarani Tanzania(kulia) akisikiliza majibu ya chemsha bongo kutoka kwa mmoja wa madereva 
Madereva pamoja na wageni wengine waalikwa wakiwa katika wiki ya kuelekea siku ya Usalama na Afya barabarani katika viwanja vya Impala Terminals 
Mgeni Rasmi katika wiki maadhimisho ya Usalama na Afya Barabarani ACP Abdi Isango Kamishna msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Oparesheni Kitengo cha Usalama Barabarani Taifa, akijiandaa kuendesha Scania ikiwa ni sehemu ya wiki ya maadhimisho ya siku hiyo.
Mgeni Rasmi katika wiki maadhimisho ya Usalama na Afya Barabarani ACP Abdi Isango Kamishna msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Oparesheni Kitengo cha Usalama Barabarani Taifa, akiwa anaendesha Scania hilo.
Mrakibu Msaidizi  wa Polisi Abben Swai Mkuu wa Kitengo cha Elimu Mafunzo na Uenezi wa kikosi cha Usalama wa barabarani Tanzania (kushoto) akiwa ndani ya Scania kupata maelezo namna ya kuendesha Gari hilo kutoka kwa mtaalam wa magari hayo Bw. Patric.
Mgeni Rasmi katika wiki maadhimisho ya Usalama na Afya Barabarani ACP Abdi Isango Kamishna msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Oparesheni Kitengo cha Usalama Barabarani Taifa akiwa anaungana na madereva wengine kupima afya zao.
 Madereva wa Magari ya mizigo yaendayo safari za mbali pamoja na baadhi ya watumishi wa makampuni ya usafirishaji wakipima afya katika mahema ya North Star Alliance.(Picha zote na Fredy Njeje)

DC DAQARRO ATAKA WADAU WA ELIMU KUHAKIKISHA MPANGO WA LANES UNAENEA ARUSHA NA KULETA MATOKEO CHANYA

$
0
0

Mkuu wa wilaya Arusha mjini Gabriel Daqarro akifungua wiki ya usomaji iliyofanyika kwenye maktaba ya mkoa Arusha pembeni ni mkutubi mkuu wa maktaba hiyo Bi Rafiki Mvamba na kushoto ni Afisa elimu Vielelezo Godfrey Augustino wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi mkuu huyo wa wilaya
Afisa elimu Vielelezo Godfrey Augustino akitoa hotuba kwenye ufunguzi wa wiki ya usomaji Lanes kabla ya kumkaribusha mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro
Meza kuu wakiwa wanajadiliana mkuu wa wilaya na mkutubi mkuu wa maktaba bi Rafiki Mvamba ambapo afisa elimu akiendelea kutoa hotuba yake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi
Pichani juu na chini ni sehemu ya wanafunzi wa shule sita za wilaya ya Arusha walioshiriki mashindano mbali mbali ya kusoma kuandika na kuhesabu wanaoonekana pichani ni wanafunzi wa shule ya msingi Mwangaza na sombetini wakifuatilia kwa makini matukio mbali mbali yalioendelea kwenye hafla hiyo

MAONYESHO YA VITABU MBALI MBALI NAYO YALIKUWEPO KWENYE WIKI YA USOMAJI KATIKA JIJI LA ARUSHA ILIYOADHIMISHWA KWENYE MAKTABA KUU YA MKOA WA ARUSHA
Mwanafunzi wa shule ya Msingi Uhuru Jaquline Abrogast akisoma kitabu mbele ya mkuu wa wilaya kwenye maadhimisho ya siku ya Usomaji iliyoadhimishwa kimkoa kwenye maktaba ya mkoa jijini Arusha

Picha juu ni igizo la wanafunzi wa shule ya msingi Naura wakionyesha masuala mbali mbali ya safari ya kusoma kwenye maonyesho ya wiki ya usomaji mbele ya mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Arusha

Wanafunzi wa shule ya msingi Arusha School wakiimba wimbo mbele ya mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Arusha
Mkutubi mkuu wa maktaba ya mkoa akiwa na majaji wenzake wakifuatilia mashindano ya kusoma kwa wanafunzi wa shule sita za Naura,Sombetini,Meru,Mwangaza,Uhuru na Arusha School

Baadhi ya wanafunzi wakioshiriki mashindano ya kusoma vitabu wa darasa la kwanza wa shule hizo sita zilizoshiriki maadhimisho hayo ya wiki ya Usomaji

Na Ahmed Mahmoud Arusha .

Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro amewataka waalimu na Afisa elimu kuhakikisha mpango wa KKK (LANES) unatiliwa mkazo sanjari na kuhakikisha wanafunzi wanajua kusoma kuandika na kuhesabu ili kuleta matokeo chanya na kufikia malengo ya serikali ya wananchi wote kujua kusoma. 

Akiongea wakati akifungua wiki ya kusoma na stadi za kukuza kusoma kuandika na kuhesabu (LANES) iliyofanyika katika Maktaba ya mkoa Dc Daqarro amesema kuwa wajibu huo ni wetu sote kuanzia nyumbani hadi mashuleni kuhakikisha kila moja wetu anatimiza wajibu wake. 

Amesema kuwa wiki kama hiyo ni ya kujitathmini tumefika wapi na tunaelekea wapi kama taifa kwa ajili ya kukuza uelewa wa vijana wetu kujua kuhesabu kusoma na kuandika ili kuwa na taifa linalopiga hatua kwa wananchi wake kujua kusoma. 

“Taifa limejipanga kuondoa wananchi wasio jua kusoma na kuandika ndio maana ilikaja na mkakati wa kkk hivyo kila mmoja wetu anawajibu kuhakikisha tunafikia malengo ya mkakati huu”alisema Daqarro
Kwa Upande wake Afisa elimu vielelezo Godfrey Augustino amesema kuwa wajibu wa wazazi ni kufuatilia maendeleo ya watoto wao na wao kama waalimu watahakikisha kila kijana anayepata nafasi anajua kusoma kuandika na kuhesabu lengo ni kuondoa vijana wanaomaliza elimu wakiwa hawajui kusoma na kuandika. 

Amesema kuwa hatavumilia kuona wilaya hiyo ikiwa ina vijana ambao hawajui kusoma wala kuandika na amejipanga kuhakikisha wanafikia malengo yalioanza kuonekana kwenye ufaulu kwa wilaya kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika ufaulu wa Darasa la saba mwaka huu. 

Awali mkutubi mkuu wa maktaba ya mkoa Rafiki Mvamba amesema kuwa analishukuru shirika Kwa kufadhili wiki hiyo na kuwataka watanzania kupenda kujisomea na kufuatilia watoto wao ili kujua kusoma na kuandika itakayopelekea taifa kuwa na wananchi wenye elimu ya kuweza kufikia malengo endelevu .

Amesema kuwa mpango huo LANES wa wiki ya kusoma ni kujitathmini na kuwafikia wanafunzi kujua uelewa wao katika kukuza stadi za kusoma kuandika na kuhesabu kuanzia watoto wa awali hadi vyuo vikuu kupenda kujisomea kwani elimu haina mwisho. 

“sisi kama maktaba tumejipanga kuhakikisha wanafunzi wote wanaofika hapa wanapata vitabu vyote wanavyohitaji sanjari na kuwapa nafasi na kuwaongoza pale wanapohitaji ili lengo ya kuwa na taifa lenye watu wanaojua kusoma na kuandika linafikiwa”alisema Mvamba
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images