Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

MFANYAKAZI WA UDSM AJISHINDIA GARI KUPITIA PROMOSHENI YA 'TBL KUMENOGA, TUKUTANE BAA'

$
0
0
Meneja wa bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli, (kushoto)Meneja Udhamini na Mawasiliano wa TBL,David Tarimo (katikati) na Afisa Kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Humid Semvua wakifuatilia namba ya mshindi wakati wa droo ya kwanza ya mshindi wa gari iliyofanyika jijini Dar es Salaam
Meneja wa bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli, (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (Kulia) ni Meneja Udhamini na Mawasiliano wa TBL, David Tarimo.


Mkazi wa Dar es Salaam na mfanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Julitha Kilawe, ameibuka mshindi wa gari mpya aina ya Renault KWID kupitia promosheni ya TBL Kumenoga, Tukutane Baa’iliyozinduliwa mwezi uliopita itakayowezesha washiriki 3 wa promosheni hiyo kujishindia gari 1 kila mwezi katika kipindi cha miezi 3 ya promosheni hiyo. 

 Droo ya kuwapata washindi hao imefanyika jijini Dar e Salaam, chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Taifa na kushuhudiwa na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari. Mshindi huyo alipokea habari hizo kwa furaha baada ya kupigiwa na Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya wateja wa TBL, David Tarimo, ambapo alieleza kuwa amefurahishwa na kujishindia gari ambalo litamrahishia usafiri katika shughuli zake za kila siku.

 “Natoa wito kwa wateja wetu wazidi kujitokeza kushiriki, tumejipanga vyema ili kuwafikia wote nchi nzima. Tumewaletea wateja wetu promosheni hii kwa lengo la kuwashukuru kwa kuendelea kutuunga mkono”. alisema Tarimo. Tarimo, aliongeza kuwa, promosheni hii inafanyika kwenye mabaa katika siku za mwisho wa juma yaani Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kwa muda wa miezi mitatu kupitia bia za chapa za Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite na Balimi Extra Lager.

 Kwa muda wote huu washiriki wataweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi kubwa kabisa ya gari mpya. Kwa upande wake, Meneja wa Bia chapa ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli, alisema mbali na zawadi kubwa ya magari mapya zipo zawadi nyingi za kujishindia papo hapo kwenye promosheni ikiwemo bia za bure, fulana nakadhilika. Alisema promosheni itakuwa inafanyika kwenye mabaa zaidi ya 5000 nchini katika siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. 

‘Wateja wetu wazidi kuitafuta bendera ya TBL Kumenoga, kwani ilipo bendera hii ndipo wateja na TBL wanapokutana katika promosheni.’ Alisema ili kuingia kwenye droo ya magari mapya ya ‘TBL Kumenoga, Tukutane Baa’ wateja watatakiwa kununua bia tatu kati ya Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite au Balimi Extra Lager kwenye promosheni ambapo watapatiwa kuponi yenye namba, kisha watatuma namba hiyo kwa meseji kwenda 15451, hii ni kwa wale wenye mitandao ya VODACOM, TIGO na AIRTEL. Kwa wateja wa mitandao mingine watatuma namba iliyo kwenye kuponi kupitia tovuti ya www.tblkumenoga.co.tz.

WAHITIMU MAJENGO SEC. 2000 WASAIDIA YATIMA, DAR, MWANZA NA KILIMANJARO

$
0
0

Mmoja wa wakilishi wa Kundi la Wasapu la Wanafunzi wahitimu kidato cha nne mwaka 2000 katika Sekondari ya Majengo iliyopo mkoani Kilimanjaro, Eng. Willbard Gandu (kulia) akikabidhi sehemu ya msaada wa wanafunzi hao katika kituo yatima cha ‘Green Pastures’ cha jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa wakilishi wa Kundi la Wasapu la Wanafunzi wahitimu kidato cha nne mwaka 2000 katika Sekondari ya Majengo iliyopo mkoani Kilimanjaro, Injinia Eng. Maeda (kulia) akimkabidhi mmoja wa watoto wa kituo yatima cha ‘Green Pastures’ cha jijini Dar es Salaam sehemu ya msaada uliotolewa na wanafunzi hao.

Mmoja wa viongozi wa kundi hilo la wanafunzi waliohitimu Sekondari ya Majengo, Joachim Mushi (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha watoto yatima ‘Green Pastures’, Mchungaji Douglas Kiseu sehemu ya msaada uliotolewa na kundi lao.
moja wa wakilishi wa Kundi la Wasapu la Wanafunzi wahitimu kidato cha nne mwaka 2000 katika Sekondari ya Majengo iliyopo mkoani Kilimanjaro, Bw. Oswald (kulia) akimkabidhi mmoja wa watoto wa kituo yatima cha ‘Green Pastures’ cha jijini Dar es Salaam sehemu ya msaada uliotolewa na wanafunzi hao.
Mmoja wa viongozi wa Kundi la Wasapu la Wanafunzi wahitimu kidato cha nne mwaka 2000 katika Sekondari ya Majengo, Bi. Grace Minja (kulia) akimkabidhi mmoja wa watoto wa kituo yatima cha ‘Green Pastures’ cha jijini Dar es Salaam sehemu ya msaada uliotolewa na wanafunzi hao.
Mmoja wa viongozi wa Kundi la Wasapu la Wanafunzi wahitimu kidato cha nne mwaka 2000 katika Sekondari ya Majengo, Eng. Maeda akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika kituo yatima cha ‘Green Pastures’ cha jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wakilishi wa Kundi la Wasapu la Wanafunzi wahitimu kidato cha nne mwaka 2000 Sekondari ya Majengo akiwa na wanaye (kulia) akimkabidhi mtoto wa kituo cha ‘Green Pastures’ cha jijini Dar es Salaam sehemu ya msaada uliotolewa na wanafunzi wenzake wahitimu.
Sehemu ya viongozi na wawakilishi wa Kundi la Wasapu la Wanafunzi wahitimu kidato cha nne mwaka 2000 katika Sekondari ya Majengo iliyopo mkoani Kilimanjaro, wakipiga picha ya ukumbusho na watoto wa Kituo cha 'Hope Village For Orphans and Vulnerable Children' cha mkoani Kilimanjaro mara baada ya kukabidhi msaada katika kituo hicho.
Sehemu ya wawakilishi wa Kundi hilo mkoani mwanza wakipiga picha ya ukumbusho mara baadaa ya kukabidhi msaada katika kituo cha watoto yatima cha ‘Tanzania Childrens Rescue Centre (TCRC)’ jijini Mwanza.
Bw. Emmanuel Rimoy mwakilishi wa Kundi hilo mkoani Mwanza (wa pili kulia) akizungumza na watoto wa kituo cha watoto yatima cha ‘Tanzania Childrens Rescue Centre (TCRC)’ jijini Mwanza (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhi msaada wao.
Sehemu ya msaada uliokabidhiwa Kituo cha 'Hope Village For Orphans and Vulnerable Children' cha mkoani Kilimanjaro na wawakilishi wa Kundi la Wasapu la Wanafunzi wahitimu kidato cha nne mwaka 2000 katika Sekondari ya Majengo.
Sehemu ya msaada uliokabidhiwa na wawakilishi wa kundi mkoani Kilimanjaro Kituo cha 'Hope Village For Orphans and Vulnerable Children' cha mkoani Kilimanjaro.

KUNDI la Wasapu la Wanafunzi wahitimu kidato cha nne mwaka 2000 katika Sekondari ya Majengo iliyopo mkoani Kilimanjaro limetembelea vituo vitatu vya watoto wanaoishi katika maazingira maagumu na kutoa misaada mbalimbali ikiwa ni kuwafariji watoto hao.

Vituo vilivyonufaika na misaada hiyo ni pamoja na Kituo cha watoto yatima ‘Green Pastures’ cha jijini Dar es Salaam, Kituo cha watoto yatima cha ‘Tanzania Childrens Rescue Centre (TCRC)’ jijini Mwanza na Kituo cha 'Hope Village For Orphans and Vulnerable Children' cha mkoani Kilimanjaro.

Akizungumzia msaada huo mmoja wa viongozi wa kundi hilo la wanafunzi waliohitimu Sekondari ya Majengo, Joachim Mushi alisema wanafunzi hao walichanga fedha kwa ajili ya kuwatembelea wahitaji ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 4 tangu kuanzishwa kwa kundi hilo.

“…Wanakikundi waliamua kuchangishana fedha kwa ajili ya kuwatembelea wahitaji na kutoa chochote kwa lengo la kuwafariji yatima, na misaada kugawanywa katika mikoa mitatu yenye wawakilishi yaani Mwanza, Dar es Salaam na Mkoa wa Kilimanjaro…hii ni sehemu ya maadhimisho ya miaka minne ya kundi ambalo tulilianzisha 2014,” alisema Bw. Mushi.Msaada uliyotolewa ni mifuko ya unga wa sembe, mchele, sukari, maharage, sabuni za kufulia na kuogea, mafuta ya kupikia, madaftari, vyombo vya kutumia pamoja na peni.

Vingine ni pamoja na Dawa za meno, miswaki, biskuti, juisi, maji ya kunywa, mikate, majani ya chai, viatu pamoja na nguo mbalimbali za watoto vyote vikiwa na zaidi ya thamani ya zaidi ya milioni 1.8.
Eng. Willbard Gandu (aliyesimama) akizungumza na watoto wa kituo yatima cha ‘Green Pastures’ cha jijini Dar es Salaam kuwafariji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha watoto yatima ‘Green Pastures’, Mchungaji Douglas Kiseu (wa kwanza kulia) akiwatembeza wawakilishi katika kituo chake mara baada ya kukabidhi msaada wa kundi lao.
Picha ya pamoja ya wawakilishi wa Dar es Salaam wa kundi la Wasapu la Wanafunzi wahitimu kidato cha nne mwaka 2000 Sekondari ya Majengo iliyopo mkoani Kilimanjaro
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha watoto yatima ‘Green Pastures’, Mchungaji Douglas Kiseu akiwatembeza wawakilishi katika kituo chake kuangalia changamoto zilizopo katika kituo hicho. Pichani akiwaonesha tanki la kuhifadhia maji ya mvua ambalo kituo kimeshindwa kukifunika jambo amblo ni hatari kwa watoto kituoni hapo.

ZIARA YA JUKWAA LA WANAWAKE WILAYA YA MKURANGA YAJA NA FURSA YA MKOPO BILA RIBA

$
0
0
Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MWENYEKITI wa Jukwaa la wanawake Wilaya ya Mkuranga Mariam Ulega ameendelea na ziara yake iliyolenga kuhamasisha kuwainua wanawake kiuchumi kupitia jukwaa hilo.

Akizungumza na wanawake akiwa ziarani katika kijiji cha Mwandege bi. Mariamu amesema kuwa lengo la kufanya ziara hiyo kuwafahamisha wanawake kuhusiana majukumu yanayofanywa na jukwaa hilo tangu kuanzishwa kwake.

Amesema kuwa akiwa kama mweyekiti wa Wilaya hiyo atahakikisha fursa za kiuchumi zinawafikia ili waweze kuendeleza shughuli zao za kijasiriamali.Kuhusiana na mikopo kwa wanawake bi. Mariamu amesema kuwa wanachotakiwa kufanya ni kuendeleza miradi yao ili waweze kupata mikopo katika halmashauri zao bila riba.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Mwandege Adolf Kowero amesema kuwa amekuwa akifarijika na juhudi za akina mama hao na kuhusu ahadi ya eneo alilohaidi kwa ajili ya biashara lipo tayari na ramani imeandaliwa ambapo soko kubwa litajengwa kwa ajili ya wanawake na vijana.

Ameeleza kuwa frame zaidi ya 1000 zitajengwa na kuchukuliwa na vikundi au mtu mmoja mmoja kwa gharama nafuu kabisa.Aidha amesema kuwa amefanya mazungumzo na benki ya Amana kuhusiana na mikopo ambayo inatoa mikopo bila riba hivyo fursa hiyo wanawake wa Mwandege wasipoteze fursa hiyo ambayo itawasaidia kujikwamua na kuendeleza miradi yao.

Pia amemshukuru Mbunge wa jimbo hilo Abdallah Ulega kwa juhudi za kimaendeleo anazozileta katika jimbo hilo na ameomba apate maafisa maendeleo 2 pindi soko litakapokamilika.Katika ziara hiyo mwenyekiti wa jukwaa hilo amechangia kiasi cha zaidi ya shilingi laki nne na doti 20 za kanga kwa vikundi vya kijiji cha Mwandege na amewataka akina mama hao kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. John Magufuli na Mbunge wa jimbo hilo katika kujenga maendeleo ya taifa.
Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake wilaya ya Mkuranga,Mariam Ulega akizungumza na wajasiriamali wa kata ya Mwandege ,ambapo amewaomba kufanya kazi kwa waminifu ili waweze kunufaika na kazi zao na kuongeza pato la Taifa.
Diwani wa kata ya Mwandege wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani,Adolf Kowero akizungumza na wajasiriamali wa kata hiyo.
Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake wilaya Mkuranga,Mariam Ulega akiwakabidhi viongozi wa kata ya Mwandege laki nne na doti 20 za kanga kwajili ya mtaji wa vikundi mbalimbali vya kata hiyo.
Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake wilaya Mkuranga,Mariam Ulega akiwaunga mkono wajasiriamali wa kata ya Mwandege.(Picha na Emmanuel Massaka MMG)
Sehemu ya wajasiriamali wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika katika kata ya Mwandege wilayani Mkuranga Mkoani wa Pwani.

DKT. ABBASI: SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA MIFUMO YA UTENDAJI NA UWAJIBIKAJI KULETA TIJA KWA WANANCHI

$
0
0

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na waandishi wa Habari waandamizi wa Kituo cha Redio Times FM cha Jijini Dar es Salaam, wakati alipofika katika kituo hicho kwa ajili ya kuzungumzia tathmini ya miaka mitatu ya mafanikio wa Serikali ya Awamu ya Tano leo (Jumanne Novemba 6, 2018)

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza katika mahojiano ya kipindi ya maalum cha Redio Times FM, wakati wakati alipofika katika kituo hicho kwa ajili ya kuzungumzia tathmini ya miaka mitatu ya mafanikio wa Serikali ya Awamu ya Tano leo (Jumanne Novemba 6, 2018)

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali , Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari waandamizi wa Kituo cha Redio cha Times FM cha Jijini Dar es Salaam wakati alipofika katika kituo hicho kwa ajili ya kuzungumzia tathmini ya miaka mitatu ya mafanikio wa Serikali ya Awamu ya Tano leo (Jumanne Novemba 6, 2018)

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Kituo cha Redio cha Times FM cha Jijini Dar es Salaam wakati alipofika katika kituo hicho kwa ajili ya kuzungumzia tathmini ya miaka mitatu ya mafanikio wa Serikali ya Awamu ya Tano leo (Jumanne Novemba 6, 2018)
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Kituo cha Redio cha Times FM ch Jijini Dar es Salaam, Leule Nyaulawa wakati alipofika katika kituo hicho kwa ajili ya kuzungumzia tathmini ya miaka mitatu ya mafanikio wa Serikali ya Awamu ya Tano leo (Jumanne Novemba 6, 2018)

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akibadilishana mawazo na Watendaji wa Kituo cha Redio cha Times FM cha Jijini Dar es Salaam wakati alipofika katika kituo hicho kwa ajili ya kuzungumzia tathmini ya miaka mitatu ya mafanikio wa Serikali ya Awamu ya Tano leo (Jumanne Novemba 6, 2018) .(PICHA NA MAELEZO)


DAR ES SALAAM

MKURUGENZI wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amesema Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kutekeleza sera, programu na miradi ya maendeleo iliyopo nchini kwa kuhakikisha kuwa inajenga mfumo imara wa utendaji na uwajibikaji ili kuboresha kiwango cha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa Wananchi.

Akizungumza katika mahojiano ya kipindi maalum na Kituo cha Redio Times FM leo (Jumanne Novemba 6, 2018) Jijini Dar es Salaam kuhusu tathmini ya miaka mitatu ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Dkt. Abbasi alisema Serikali ya Awamu ya Tano ni Serikali ya vitendo na imekusudia kuleta mageuzi ya kweli ya haraka kwa wananachi.

Alisema kuwa tangu kuingia kwake madarakani mwaka 2015, Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake imejenga mfumo imara wa uwajibikaji kwa Watendaji na Viongozi mbalimbali katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo rushwa, ufisadi pamoja na ukosefu wa huduma bora za kijamii ikiwemo Elimu, afya na miundombinu.

Aidha Dkt. Abbasi anasema katika huduma za maendeleo ya jamii ikiwemo elimu na afya, anabainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeleta mageuzi makubwa katika mfumo wa uendeshaji na utoaji wa huduma hizo, hatua iliyowafanya wananchi wengi kuweza kumudu changamoto ya gharama katika sekta hizo katika hatua mbalimbali za upatikanaji wake.

“Serikali imeanzisha utaratibu wa utoaji wa elimu bure kwa ngazi ya Shule za Awali, Msingi na Sekondari, ambapo kwa kufanya hivyo tumeweza kuwaletea unafuu pamoja na kuokoa kiasi kikubwa cha pesa za wananchi zilizokuwa zikitolewa katika michango mbalimbali mashuleni” alisema Dkt. Abbasi.

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano imepiga hatua kubwa katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi, ambapo katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais John Magufuli, Serikali imefanikiwa kuanzisha Mahakama ya maalum ya ufisadi inayoshughulikia makosa makubwa ya rushwa, ambapo mpaka sasa jumla ya kesi 41 zimefunguliwa katika Mahakama hiyo iliyopo katika Mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya.

Anaongeza katika sekta ya usafiri wa anga, mwezi Desemba mwaka huu, Serikali inatarajia kuipokea ndege mpya mbili za Airbus na kufanya na kufanya idadi ya ndege kufikia s, na hivyo kuendelea kudhihirisha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kuboresha Shirika la Ndege Nchini (ATCL) katika kufanya kazi na kuleta mageuzi ya kiuchumi.

Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi anasema katika kipindi cha miaka mitatu ya utawala, Serikali ya Awamu ya Tano imefanikiwa kuweka mfumo imara wa usimamizi wa fedha za umma,ambapo makusanyo ya mapato kwa mwezi yameongeza na kufikia kiasi cha Tsh. Trilioni 1.3 kutoka Tsh. Bilioni 800 zilizokuwa zikikusanywa hapo awali ikiwa ni kongezeko la Tsh Bilioni 500.

Juhudi hizi zinatokana na mchango wa taasisi mbalimbali za umma ikiwemo wakala, mashirika na Mamlaka za Serikali za Mitaa, ambapo Serikali imeweka mfumo wa EFD ambao makusanyo yote ya fedha za Serikali yatapitia katika mfumo wa EFD” anasema Dkt. Abbasi.

Kuhusu mageuzi ya kiuchumi kupitia ujenzi wa viwanda, Dkt. Abbasi anasema hadi kufikia sasa Serikali imesajili viwanda vipya 3300, hatua itakayoifanya Tanzania kujitosheleza kwa bidhaa za ndani na kuwafanya wananchi wengi kutosafirisha nje ya nchi kwa ajili ya ununuzi wa bidhaa.

JUKWAA LA WAKULIMA ARUMERU LAPATA NEEMA

$
0
0
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akipata maelezo ya bidhaa kutoka kwa mmoja wa mkulima katika maonyesho ya wakulima wilayani hapo. 
DC Muro akizungumza na wakulima katika maonyesho hayo ya kilimo yaliyoanza tarehe 1-3 Novemba 2018 wilayani humo. 
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza na wakulima na wananchi wa wilaya hiyo katika maonyesho hayo ya wakulima
Mmoja kati ya mkulima. Wilayani humo akimpatia maeleza ya mbegu ya mahindi kama inavyoonekana katika picha Mkuu wa wilaya Jerry Muro katika maonyesho hayo
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro akiwa katika picha ya pamoja na wakulima katika maonyesho hayo ya wakulima Meru. 


Na. Vero Ignatus, Arumeru. 

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro amejitolea kuwasadia kuandika Maandiko ya kibiashara wananchi wanaotaka kufanya Kilimo na Ufugaji wa Kibiashara ili waweze kukopesheka na Ta asisi za kifedha 

Amesema hatua hiyo imefikia baada ya kubaini kuwepo kwa vikwazo katika maandiko katika hatua za awali kwani Taasisi hizo kabla ya kutoa msaada au mkopo huitaji mchanganuo, andiko la kibiashara kwanza kabla ya kuwawezesha wananchi ambao wanataka kuanza kilimo au ufugaji wa kibiashara.

Wanapoanza safari ya kutimiza ndoto zao za kuwekeza katika sekta hizo, ambapo baada ya kubaini uwepo wa vikwazo hivyo aliamua kujiongeza Kwa kutafuta wadau ambao atashirikiana nao katika kuwasaidia wananchi kuondoa Vikwazo hivyo.

Mhe Muro amesema tayari kampuni Binafsi ya Wawezeshaji wa wakulima (PASS)Private Agricultural Sector Support imekubali kuwaandalia na kugharamia Mpango kazi wa kibiashara zitakazowasaidia Wakulima na Wafugaji katika kupata Mkopo katika Taasisi za Kifedha hali ambayo itawasaidia katika uendelezaji wa Kilimo chenye tija na ufugaji wa kibiashara. 

Akifungua maonyesho ya jukwaa la wakulima Meru ambayo yamefanyika Kwa siku tatu na kuwaleta pamoja wakulima, wafugaji na wadau mbalimbali katika sekta ya kilimo na mifugo kwa pamoja wamekukubali kutoa msaada katika kuandaa, kuandika maandiko ya mchanganuo wa kibiashara 

Muro amewapatia chumba Cha ofisi ya kuratibu na kuendesha shughuli za kilimo na ufugaji Jukwaa hilo la Wakulima Meru ili kuwawezesha kufanya kazi zao Kwa haraka zaidi, na kuhaidi kuwatafutia kompyuta Kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu za taarifa za wakulima na wafugaji.

Kwa upande Meneja wa Tawi la kampuni ya ( PASS)amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkuu huyo wa wilaya kwa kuonyesha kuwajali wakulima na wafugaji ambapo amewataka wananchi hao Kujitokeza kwa wingi ili waweze kunufaika kupitia na Taasisi hiyo.

FURSA NYINGINE KWA VIJANA WA KITANZANIA KUSHINDA MPAKA $1500 NA FCS

$
0
0
Foundation for Civil Society ni miongoni mwa mashirika yanayowezesha AZAKI mbalimbali hapa nchini kwa kuzipatia ruzuku, Na leo wamezindua rasmi kampeni yao ya Jumaanne ya kutoa (Giving Tuesday Campaign) ambayo uadhimisha kila mwaka na kwa mwaka huu wamekuja na mpango kabambe wa kuwawezesha vijana wanaofanya kazi za kijamii.
Washiriki wakifuatilia mkutano.

Akielezea Kampeni hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Bw. Francis Kiwanga alisema kuwa kampeni hiyo imekuwa ikifanyika duniani kote na mpaka sasa mataifa kumi yanaadhimisha siku hiyo Tanzania ikiwemo na kuyataja mataifa hayo ni India, China, Brazil, Mexico, Afrika ya kusini, Hispania, Rusia, na Jamhuri ya Czech pamoja na Romania.


Huku kauli mbiu kwa mwaka huu ikiwa ni “Utoaji Wangu Hazina Yangu”


Aidha Mkurugenzi huyo alisema kuwa lengo la kampeni hii ni kuunga mkono na kuhamasisha utamaduni wa kujitolea hapa nchini, Na wameamua kulenga katika kundi kubwa ambalo ni vijana ili wawe na utamaduni huu wa kujitolea na kuweza kuifikia jamii yenye uhitaji kwa ukubwa zaidi.

Aliendelea kusema kuwa katika kampeni hiyo vitafanyika vitu vikubwa viwili cha kwanza ikiwa ni kampeni ndogo ya Kuchangia Damu itakayofanyika Novemba 24 katika Hospitali ya Muhimbili jengo jipya la Moi ghorofa ya nne kuanzia saa 3 kamili asubuhi mpaka saa 8 kamili mchana.


Na jambo la pili litakuwa ni kuchangia kwa ajili ya kituo cha New Hope Girls kilichopo Kimara jijini Dar es salaam, Hii ni asasi inayojihusisha na kuwalea watoto wa kike wanaoishi katika mazingira hatarishi wapatao 38 na mahitaji yao ni vitu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi za kitanzania Million tisa (9000,000/=) ambapo inabidi michango hiyo iwasilishwe Novemba 27 ambayo ni Jumanne ya mwisho kwa mwezi Novemba.

Akizungumzia fursa hiyo Bw. Kiwanga alisema kuwa kwa vijana wenye umri kati ya miaka 18 mpaka 35 wanachotakiwa ni kuandaa stori au hadithi za kazi walizowahi kuzifanya katika kusaidia jamii eidha kwa kutoa Fedha, Muda, Kupaza sauti kwa ajili ya Wanyonge nk. Na kuviweka vitu hivyo kwa njia ya andiko lenye maneno yasiyozidi 200 au video isiyozidi dk 2 na kutuma kupitia barua pepe ifuatayo.

givingtuesday@thefoundation­-tz.org Huku mtumaji akianza na Jina kamili, Mahali anapoishi na Namba ya simu.

Kwa upande wa zawadi zitatoka kwa washindi watano wa kwanza huku mshindi wa kwanza akipatiwa Dola za Kimarekani 1500 na wapili atapata Dola 800, wa tatu Dola 700, wa nne Dola 600 na watano atapata 500 na mwisho wa kutuma ni tarehe 20 ya mwezi huu novemba.


Ikumbukwe kuwa Foundation for Civil Society ilianza kuadhimisha jumanne ya kutoa tangu mwaka 2016 ambapo waliweza kutoa vitu mbalimbali katika Shule ya msingi ya watoto wenye ulemavu ya Uhuru Mchanganyiko ikiwemo Magodoro, Mipira ya kuchezea na Mashine za kuandikia (Braille Machine) pamoja na kufanya ukarabati wa Vyoo ili viweze kutumiwa na watoto wenye wenye mahitaji maalum.

Na kwa mwaka 2017 waliadhimisha kwa kugharamia watoto wapatao 91 wenye Vichwa Vikubwa na Mgongo wazi kufanyiwa upasuaji na kutoa Bima za afya kwa watoto 101, Pamoja na kuhamasisha wananchi Kuchangia Damu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Kitengo cha Moi ambapo watu wapatao 40 walijitokeza kuchangia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Francis Kiwanga akitoa ufafanuzi wa jambo mapema leo katika Uzinduzi wa Kampeni ya Jumanne ya Kutoa (Giving Tuesday Campaign) uliofanyika makao makuu ya shirika hilo Jijini Dar es salaam.
Meneja Biashara, Maendeleo na Ushirikiano wa FCS Martha Olotu akiendelea kutoa msisitizo kwa vijana kushiriki katika zoezi hili la jumanne ya kutoa.

Kijana Hussein Melele kutoka katika Taasisi ya Mulika Tanzania akiuliza maswali kuhusiana na kampeni ya Jumanne ya kutoa inayoendeshwa na Foundation for Civil Society.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dorcus Masha ambaye pia ni muwakilishi wa Taasisi ya YUNA akiwasilisha maoni yake katika kampeni inayoendeshwa na FCS.
Meza kuu ikijibu maswali ya washiriki wa mkutano.

Mkutano ukiendelea

Naibu Balozi wa Israel Nchini Mhe. David Eyal Atembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongea jambo na Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David alipotembelea Taasisi hiyo jana (5/11/2018) kwa ajili ya kuona kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart – SACH) la nchini Israel kwa kushirikiana na JKCI. Jumla ya watoto 85 wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi, upasuaji wa moyo wa kufungua na bila kufungua kifua. 
Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David akiongozana na mkuu wa kitengo cha ufundi na matengeneza cha Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mhandisi Abella Rwiguza akielekea kuangalia ukarabati wa jengo jipya la watoto la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati alipotembelea Taasisi hiyo jana (5/11/2018) kwa ajili ya kuona kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart – SACH) la nchini Israel kwa kushirikiana na JKCI. 
Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David akiangalia kipimo kinachoonyesha jinsi moyo unavyofanya kazi (ECHO Cardiogram) alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jana kwa ajili ya kuangalia kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto(Save a Child Heart – SACH) la nchini Israel kwa kushirikiana na JKCI. 
Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David akiongea na wazazi wa watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alipotembelea Taasisi hiyo jana kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart – SACH) la nchini Israel kwa kushirikiana na JKCI. Jumla ya watoto 85 wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi, upasuaji wa moyo wa kufungua na bila kufungua kifua
Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David akisalimiana na Mkuu wa kitengo cha wagonjwa walioko katika uangalizi maalum (ICU) ambaye ni daktari bingwa wa wagonjwa mahututi Vivienne Mlawi alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jana kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart – SACH) la nchini Israel kwa kushirikiana na JKCI. Jumla ya watoto 85 wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi, upasuaji wa moyo wa kufungua na bila kufungua kifua.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David pamoja na wafanyakazi wengine na JKCI na Israel wakimuombea Daktari bingwa wa usingizi kwa watoto na wagonjwa mahututi Marehemu Onesmo Mhewa aliyefariki mwanzoni mwa mwezi wa tano mwaka huu. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David pamoja na wafanyakazi wengine wa JKCI na Israel mara baada ya kumalizika kwa ziara yake ya kutembelea Taasisi hiyo jana kwa ajili ya kuangalia kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Shirika la Okoa moyo wa mtoto Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart – SACH) la nchini Israel kwa kushirikiana na JKC. 
Mkuu wa kitengo cha ufundi na matengeneza cha Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mhandisi Abella Rwiguza akimweleza Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David jinsi ukarabati wa jengo la watoto unavyoendelea. Mhe. David alitembelea Taasisi hiyo jana kwa ajili ya kuangalia kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart – SACH) la nchini Israel kwa kushirikiana na JKCI.
Picha na Anna Nkinda – JKCI



Na Genofeva Matemu – JKCI
Zaidi ya watoto 750 wenye matatizo ya moyo hapa nchini wamefaidika na matibabu ya moyo kutoka kwa wataalam wa Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) la nchini Israel tangu mwaka 1999.

Hayo yamesemwa jana na Naibu Balozi wa Israel hapa nchini mwenye makazi yake Jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. David Eyal alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kuangalia kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na madaktari bingwa kutoka SACH kwa kushirikiana na JKCI.

Mhe. Naibu Balozi Eyal alisema watoto hao kutoka Tanzania Bara na Visiwani walifanyiwa uchunguzi na kutibiwa hapa nchini wale ambao walikutwa na matatizo yanayohitaji utaalamu wa hali ya juu walipelekwa nchini Israel kwa ajili ya matibabu zaidi. Gharama za usafiri na matibabu ziligharamiwa na Serikali ya Israel.

“Kujitoa kwa wataalam kutoka Shirika la SACH kuja Tanzania kufanya uchunguzi na matibabu kwa watoto wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo ni ubalozi wa kweli wa kuitangaza nchi ya Israel kwa vitendo, ni matarajio yetu kuwa huduma hii itakuwa endelevu na kuendelea kuokoa maisha ya watoto wetu wengi zaidi”, alisema Mhe. Naibu Balozi Eyal.

Alisema Israel itaendelea kushirikiana na JKCI katika mambo mbalimbali ikiwemo kutoa matibabu ya kina kwa watoto na kutoa udhamini wa mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa wafanyakazi wa Taasisi hiyo.Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi alisema wataalamu kutoka Israel wanafika katika Taasisi hiyo mara mbili kwa mwaka kwa ajili ya kufanya uchunguzi na matibabu kwa watoto. Kuwepo kwa kambi hizo za matibabu ya pamoja kumewaongezea ujuzi madaktari, wauguzi, wataalam wa usingizi na mashine za moyo.

“Hivi sasa tuna kambi maalum ya siku sita ya uchunguzi na matibabu kati ya madaktari wetu bingwa wa moyo kwa watoto kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) la nchini Israel. Licha ya kutoa huduma ya matibabu kuwepo kwa kambi hii pia ni njia mojawapo ya kuimarisha mahusiano katika sekta ya afya kati ya Tanzania na Israel”, alisema Prof. Janabi ambaye ni Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo.

Jumla ya wataalamu 32 ambao ni madaktari, wauguzi na wataalamu wa mashine za moyo kutoka Israel wanashiriki katika kambi hiyo ya matibabu ya moyo ambapo watoto 85 wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi, upasuaji wa moyo wa kufungua na bila kufungua kifua.

NMB YATOA MSAADA WA VITANDA TISA VYA WAGONJWA KITUO CHA AFYA KIGAMBONI

$
0
0


Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Bw. Ng'wilebuzu Lubigija akimshukuru meneja wa NMB Tawi la Kigamboni mara baada ya kupokea msaada huo wa vitanda. 
Sehemu ya vitanda vilivyotolewa na Benki ya NMB kwa Kituo cha Afya cha Kigamboni jijini Dar es Salaam. Vitanda hivyo sita (6) vikiwa vya wagonjwa wa kawaida na vitatu (3) vikiwa maalum kwa ajili ya kujifungulia wajawazito vinathamani ya shilingi milioni tano. 

Sehemu ya viongozi wa Kituo cha Afya cha Kigamboni cha jijini Dar es Salaam wakifurahiaa sehemu ya msaada pamoja na viongozi wa NMB waaliokabidhi msaada huo. Vitanda hivyo sita (6) vikiwa vya wagonjwa wa kawaida na vitatu (3) vikiwa maalum kwa ajili ya kujifungulia wajawazito vinathamani ya shilingi milioni tano. 
Picha ya pamoja ya wageni waalikwa mbele ya vitanda hivyo vilivyotolewa na Benki ya NMB.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd (wa pili kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vitanda vya wagonjwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Bw. Ng'wilebuzu Lubigija (wa pili kushoto) vilivyotolewa kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Kigamboni jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni viongozi wa NMB. 
 
BENKI ya NMB imetoa msaada wa vitanda tisa vya wagonjwa katika Kituo cha Afya cha Kigamboni vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni tano. Vitanda hivyo sita (6) vikiwa vya wagonjwa wa kawaida na vitatu (3) vikiwa maalum kwa ajili ya kujifungulia kwa wajawazito, vimekabidhiwa leo kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Bw. Ng'wilebuzu Lubigija.

Akikabidhi vitanda hivyo, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd alisema msaada huo ni sehemu ya utaratibu wa kawaida wa NMB kurejesha faida kidogo kwa jamii. Alisema Benki hiyo, hutenga takribani bilioni moja fedha ambayo hurejesha kwa jamii kwa kusaidia sekta za afya, elimu na masuala mengine yanayoikumba jamii kama maafa na majanga.

Alisema Benki ya NMB inaunga mkono juhudia za Serikali za kuboresha huduma mbalimbali ikiwemo  afya kwa wananchi, ili jamii ambao ni sehemu ya wateja wa benki hiyo wawe na afya njema."..Kama tunavyojua afya ni huduma ya msingi kwa jamii wakiwemo wateja wetu, hivyo tuna kila sababu ya kuisaidia pale tunapopata fursa ya kufanya hivyo," alisema Bw. Badru Idd katika hotuba yake.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Bw. Ng'wilebuzu Lubigija akipokea msaada huo aliipongeza Benki ya NMB kwa juhudi zake za kuendelea kusaaidia sekta mbalimbali za huduma za kijamii. Aliziomba taasisi nyingine kuiga mfano wa Benki ya NMB kutoa sehemu ya faida yake kusaidia jamii ili kuchochea maendeleo ya taifa. 

Alisema Serikali inapambana katika kuhakikisha inaboresha huduma za afya kwa wananchi, lakini haiwezi kufanikiwa kwa kiwango kikubwa bila kushirikiana na wadau wengine kama ilivyofanya NMB kutoa msaada kwenye kituo hicho cha afya.

Naye Mganga Mfawidhi Kituo cha Afya Kigamboni, Dk. Julius Nyakazilibe alisema msaada wa NMB umefika wakati muafaka kwani kwa sasa kituo kinapanua huduma zake ikiwemo kuongeza majengo hivyo vitasaidia kuziba mapengo yanayojitokeza.

NSSF YASHIRIKI MAONYESHO YA VIWANDA VIDOGO MKOANI MTWARA

$
0
0
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) linashiriki maonyesho ya viwanda vidogo vidogo yanayoendelea mkoani Mtwara kuanzia Novemba 5 hadi 11,2018. Maonyesho hayo yalianzia mkoani Simiyu, na sasa yanaendelea mkoa wa Mtwara na yatamalizikia mkoani Tanga.

Maonesho haya yenye lengo kuu la kuwasidia wajasiriamali kupata masoko ya bidhaa zao, kujifunza kupitia wenzao na kujenga mahusiano baina ya taasisi moja na nyingine, yameshirikisha taasisi takribani 16 za kiserikali na zisizo za kiserikali pamoja wajasiriamali zaidi ya 278 kutoka mkoa wa mtwara na mikoa ya jirani.

NSSF kupitia maonesho hayo imepata fursa ya kuwafikia washiriki Mbalimbali na kutoa elimu kwa ukaribu zaidi juu ya huduma zitolewazo na shirika pamoja na hifadhi ya jamii kwa ujumla.Baada ya kupatiwa elimu wajasiriamali wanapata nafasi ya kusajiliwa na kuwa wanachama wa nssf ili nao waweze kunufaika na mafao yote yatolewayo na shirika hili ambayo ni pamoja na matibabu bure kwao na familia zao.

Meneja wa NSSF mkoa wa Mtwara,Ndugu
Stanley Millanzi  ametoa wito kwa wakazi wa Mtwara, mikoa ya karibu na nchi nzima kwa ujumla kutembelea banda la NSSF katika maonesho hayo ili kupata elimu na kujiandikisha, hususan baada ya Mabadiliko ya sheria yaliyofanyika mwaka 2018, ambapo NSSF ilipewa jukumu la kuwaandikisha na kuwapa hifadhi ya jamii wananchi wote waliopo katika sekta binafsi na sekta isiyo rasmi ikiwemo wajasiriamali. 
 Afisa uhusiano wa NSSF Rehema Urembo akimkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa viwanda Mhandisi  Stella Manyanya katika banda la NSSF kwenye maonesho ya viwanda vidogo yanayoendelea mkoani Mtwara
 Naibu Waziri wa viwanda Mhandisi  Stella Manyanya akiwa sambamba na Mbunge wa Mtwara Vijijini Mh Hawa Ghasi wakimsikiliza  Afisa uhusiano wa NSSF Rehema Urembo alipokuwa akitoa ufafanuzi wa baadhi ya huduma zitolowezo na Shirika hilo,kwenye maonesho ya viwanda vidogo yanayoendelea mkoani Mtwara
Meneja NSSF na PSSSF  mkoa Mtwara,Ndugu Stanley Millanzi  pamoja na Zaida Mhava wakimsikiliza Naibu Waziri wa viwanda Mhandisi  Stella Manyanya (hayupo pichani) kwenye  Banda la NSSF,wakati wa maonesho ya SIDO yakiendelea mkoani Mtwara

BALOZI MPYA WA KUWAIT NCHINI AJITAMBULISHA KWA MAKAMU WA RAIS LEO JIJINI DODOMA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kuzungumza na Balozi mpya wa Kuwait nchini Mhe. Mubarak Mohammed Faleh ALSEHAIJAN aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais Kilimani jijini Dodoma kwa lengo la kujitambulisha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi mpya wa Kuwait nchini Mhe. Mubarak Mohammed Faleh ALSEHAIJAN aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais Kilimani jijini Dodoma kwa lengo la kujitambulisha. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)  
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi mpya wa Kuwait nchini Mhe. Mubarak Mohammed Faleh ALSEHAIJAN aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais Kilimani jijini Dodoma kwa lengo la kujitambulisha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Balozi mpya wa Kuwait nchini Mhe. Mubarak Mohammed Faleh ALSEHAIJAN aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais Kilimani jijini Dodoma kwa lengo la kujitambulisha. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

BREAKING NEWZZZZZ: CGP KASIKE AFANYA MABADAILIKO MAKUBWA WAKUU WA MAGEREZA MIKOA TANZANIA BARA

$
0
0
Katika kuboresha utendaji kazi ndani ya Jeshi la Magereza Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Martin Kasike amefanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi kwa kuwateua Wakuu wa Magereza wa Mikoa Tanzania Bara(RPOs) 19 wapya na saba (7) kuwabakiza katika nyadhifa zao. 

Katika mabadiliko hayo Kamishna Jenerali Kasike ameteuwa na kuthibitisha maafisa sita (6) kuwa Wakuu wa Vyuo vya Magereza na kuwabadilisha maafisa wengine watatu (3) katika vitengo muhimu ndani ya Jeshi hilo. 

Aidha, Kamishna Jenerali Kasike katika mabadiliko hayo kwa mara ya kwanza amewateua Wakuu wa Magereza wa Mikoa katika mikoa ya Katavi, Songwe, Njombe, Simiyu na Geita ambayo ilikuwa haina uongozi wa kimagereza katika ngazi ya mikoa hiyo. 

Katika mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa RPO (DSM) SACP. Hamis Nkubasi ambaye amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza kitengo cha Ujenzi na nafasi yake kuchukuliwa na SACP. Julius Ntambala, SACP. Salum Hussein RPO (Dodoma) amebakia katika kituo chake na aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kiwira SACP. Luhende Makwaia anakwenda kuwa RPO (Mbeya) na nafasi yake kuchukuliwa na ACP. Mathias Mkama na aliyekuwa RPO (Mbeya) SACP. Kijida Mwakingi amehamishiwa Makao Makuu, Kitengo cha TEHAMA. 

Aliyekuwa RPO (Mtwara) SACP. Ismail Mlawa amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza Kitengo cha Mipango na nafasi yake kuchukuliwa na ACP. Varisanga Msuya aliyekuwa Kaimu Bohari Mkuu wa Jeshi ambapo nafasi yake inachukuliwa na ACP. Robert Masali ambaye anakuwa Boharia Mkuu wa Jeshi la Magereza. Aliyekuwa RPO (Mwanza) SACP. Athuman Kitiku amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza sehemu ya Utumishi na nafasi yake kuchukuliwa na SACP. Hamza Hamza aliyekuwa RPO Tabora. 

Aidha, ACP. Joseph Mkude anakuwa RPO (Tabora) na aliyekuwa RPO (Kagera) SACP. Boyd Mwambingu amehamishiwa Makao Makuu Kitengo cha Utawala na nafasi yake inachukuliwa na ACP. Rymond Mwampashe. Aliyekuwa RPO (Lindi) SACP. Rajabu Bakari amehamishiwa Makao Makuu Kitengo cha Mawasiliano na Usafirishaji na nafasi yake kuchukuliwa na ACP. Josephine Semwenda. 

Aliyekuwa RPO (Rukwa) SACP. Benno Hunja amehamishiwa Makao Makuu sehemu ya Kilimo, Mifugo na Mazingira na nafasi yake inachukuliwa na ACP. Jail Mwamgunda na aliyekuwa RPO (Kilimanjaro) SACP. Hassan Mkwiche amehamishiwa Makao Makuu kuwa Mkuu wa Kitengo cha Afya, Tiba na Lishe na nafasi yake kuchukuliwa na ACP. Rajab Igongi. Aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Afya, Tiba na Lishe ACP. Wilson Rugamba anakuwa RPO (Shinyanga). 

Pia, Aliyekuwa RPO (Morogoro) SACP. Mzee Nyamka amehamishiwa Makao Makuu kuwa Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na Takwimu na nafasi yake inachukuliwa na ACP. Stylvester Mrema. Aliyekuwa Kaimu RPO (Mara) ACP. Benezeth Bisibe amehamishiwa Makao Makuu kuwa Mdhibiti wa Fedha (FC) na nafasi yake inachukuliwa na ACP. Hospitius Adrian. Mkuu wa Mkuu wa Chuo KPF ACP. Lazaro Nyanga anabakia katika nafasi hiyo, ACP. Anthony Sogoseye anabakia kuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Bwawani. Aliyekuwa Msaidizi wa Mkuu wa chuo Ruanda SSP. Enock Mwanguku anakuwa Mkuu wa Chuo hicho. 

Aidha, waliokuwa Kaimu RPOs, Vyuo na maeneo mengine ambao sasa wamethibitishwa ni kama ifuatavyo:- ACP. Hasseid Mkwanda (Iringa), ACP. Anderson Kamtearo (Arusha), ACP. Emmanuel Lwinga (Tanga), ACP. Masudi Kimolo (Manyara), ACP. Joel Matani (Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji), ACP. Rehema Ezekiel (Pwani), ACP. Msepwa Omary (Singida), na SP. Ally Uwesu (Mkuu wa Kikosi Maalum cha Magereza). 

Walioteuliwa kuwa RPOs katika mikoa mipya ni ACP. Alexander Mmassy (Katavi), ACP. Lyzecky Mwaseba (Songwe), ACP. Festo Ng’umbi (Njombe), ACP. Robert Rumanyika (Geita) na ACP. Andulile Mwasampeta (Simiyu). Wakati huo huo ACP. Alexander Nyefwe anakuwa RPO (Ruvuma) na ACP. Leonard Burushi anakuwa RPO (Kigoma) kufuatia waliokuwa RPO katika mikoa hiyo kustaafu kazi kwa mujibu wa sheria. 

Maafisa wengine waandamizi walioko Makao Makuu ambao wamepangiwa majukumu mengine ni SACP. Bertha Minde anakuwa Mkuu wa Kitengo cha Parole na SACP. Chacha Jackson ambaye anakuwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Mahabusu. 

Kwa mujibu wa Kamishna Jenerali Kasike Maafisa wote waliohamishiwa Makao Makuu wanatakiwa kuripoti Makao Makuu ya Jeshi la Magereza jijini Dodoma.
   
Imesainiwa na; Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Deodatus Kazinja – Ofisa Habari,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM,
07 Novemba, 2018.

Mbunge Biteko achangia miradi ya maendeo jimboni Bukombe

$
0
0
Na George Binagi-GB Pazzo 

Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko (CCM), ameunga mkono juhudi za maendeleo za wakazi wa Kata ya Namonge jimboni humo kwa kuchangia utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyoanzishwa na wakazi hao.

Akizunguma kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Shilabela Novemba 03, 2018, Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini alichangia mifuko 30 ya saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa choo katika Shule ya Msingi Shilabela pamoja na shilingi laki nane kwa ajili ya ujenzi wa choo katika Shule ya Msingi Nyamagwangala.

Biteko alitumia mkutano huo kuwapongeza wananchi wa Jimbo la Bukombe kwa kubuni na kutekeleza miradi mbalimbali ya ya maendeleo na kwamba serikali itaendelea kuwaunga mkono kwani maendeleo ni ushirika baina ya serikali na wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Biteko (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini, akizungumza na wakazi wa Kata ya Namonge kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Shilabela.

WODI YA UZAZI KATIKA KITUO CHA AFYA CHALINZE CHAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA UFINYU WA JENGO,VITANDA NA WATUMISHI WA AFYA

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE

WODI ya uzazi katika kituo cha afya Chalinze,mkoani Pwani inakabiliwa na baadhi ya changamoto ikiwepo ufinyu wa jengo hali inayosababisha wakati mwingine akinamama wazazi kusongamana na kulazimika kulala wawili katika kitanda kimoja.

Aidha kina tatizo jingine la upungufu wa vitanda na watumishi wa afya hasa madaktari . Akikabidhiwa msaada wa vifaa vya akinamama waliojifungua kutoka kwa kikundi cha Pwani generation queens ,mganga mfawidhi wa kituo hicho Salama Masukuzi alisema kuwepo kwa mlundikano wa wagonjwa kunatokana na upungufu wa majengo ya wodi ya uzazi pamoja na vitanda .

Alieleza ,kwasasa wapo maafisa tabibu wanne ,madaktari wasaidizi wawili na daktari mmoja ambao bado ni wachache kutekeleza majukumu yao ya kutoa huduma bora ya kiafya . “Kituo hiki kinapokea wagonjwa mbalimbali na wengine wakitokea kwenye zahanati 44 zinazozunguka halmashauri ya Chalinze suala ambalo linawawia vigumu kutekeleza wajibu wao ” alifafanua Salama .

Alieleza wamepata manesi wanne kupitia ajira mpya, ameishukuru serikali lakini aliiomba kuwaboreshea zaidi huduma ya afya ili kuwahudumia wananchi. Kwa upande wa akinamama wa Chalinze,akiwemo Demertia Milichadesi pamoja na Mariam Muhoja walisema wanapata shida katika kununua drip,vifaa vya uzazi na kipimo cha kujua wingi wa damu ambacho hutakiwa kwenda nje wakati mjamzito akiwa tayari yupo wodini.

“Tumekuwa tukipata shida ya ukosefu wa vifaa kwa ajili ya kujifungulia na wakati mwingine inatubidi kwenda dukani kununua na uwezo wetu kifedha ni mdogo ,tunqshindwa kumudu gharama za matibabu” Demertia aliwashukuru Pwani generation queens kwa misaada waliyoipata na kuomba wadau na vikundi vingine vikumbuke kusaidia kituo cha afya Chalinze.

Akikabidhi msaada wa vifaa mbali mbali katika wodi ya uzazi kwenye kituo hicho cha afya , Mwenyekiti wa kikundi cha Pwani Generation Queens Betty Msimbe alisema wamesaidia kutokana na kubaini kuwepo kwa upungufu wa vifaa hasa kwa wanawake wajawazito ambao wanakwenda kupatiwa matibabu na kujifungua.

Betty alieleza,wapo wanawake ambao wamekuwa wakipata shida pindi wanapokwenda katika zahanati, vituo vya afya na hospitali kwa ajili ya kujifungua hivyo wakaona kuna umuhimu wa kutoa msaada huo

SERIKALI INAENDELEA KUIMARISHA USIKIVU WA TBC NCHI NZIMA:DKT.MWAKYEMBE

$
0
0

Na Shamimu Nyaki –WHUSM.

Katika kuimarisha usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Serikali imeendela kuweka mikakati mizuri ya kuongeza usikivu wa shirika hilo hapa nchini kutegemea na upatikanaji wa fedha.

Hayo yamesemwa leo Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alipokuwa akijibu swali la mbunge Mhe. Zaynab Matitu Vulli (Viti Maalum) aliyeuliza Ni chanagamoto zipi zinazopelekea TBC kutosikika katika baadhi ya maeneo ya Pwani ambapo Mhe. Waziri alieleza kuwa katika Bajeti ya mwaka 2016/17 maeneo mengi ya nchi yaliongezewa usikivu.

“TBC ina mitambo ya kurushia matangazo  ya redio ya masafa ya FM katika Wilaya ya Kisarawe ambayo hufikisha matangazo kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani katika masafa ya  87.8 MHz kwa idhaa ya TBC Taifa, 90.0 MHzkwa idhaa ya TBC FM na 95.3 kwa idhaa ya TBC International”.Alisema Dkt. Mwakyembe.Aidha ameongeza kuwa katika Bajeti ya mwaka 2016/17 TBC ilitekeleza mradi wa upanuzi wa usikivu katika Wilaya tano zilizopo mpakani ambazo ni Wilaya za Longido, Rombo,Tarime,Nyasa na Kibondo.

Vilevile katika Bajeti ya mwaka 2017/18 mradi wa usikivu katika mkoa wa Mtwara na Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga ulitekelezwa ambapo hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu TBC ilikua na vituo thelathini na tatu vya kurushia matangazo katika masafa ya FM kwenye Wilaya 102 kati ya 161 nchi nzima.

Dkt. Mwakyembe ameeleza kuwa Serikali inaendelea kuhakikisha kuwa TBC inapanua usikivu ambapo kwa mwaka huu wa fedha maeneo ya Unguja na Pemba,Simiyu,Njombe,Songwe,Lindi maeneo ya Nangurukuru  pamoja na Mkoa wa Morogoro maeneo ya Morogoro Vijijini,Bondwa na Mahenge yatafikiwa.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa bungeni Jijini Dodoma.

Rais Magufuli ateua Mwenyekiti wa Bodi ya Mzinga na Mkuu wa Chuo cha NIT


WAHITIMU WA MAFUNZO YA RDP YA TBL WATUNUKIWA VYETI

$
0
0
Mkurugenzi wa ukuzaji wa Masoko wa ABIn Bev,Kanda ya Afrika Mashariki, Carlos Bernitt,akiongea wakati wa hafla ya kutunuka vyeti wahitimu wa mafunzo hayo. Meneja Masoko na Ukuzaji Biashara wa TBL,Edith Bebwa, akiongea wakati wa hafla ya kutunuka vyeti wahitimu wa mafunzo hayo.

Baadhi wa wahitimu wa mafunzo wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo
Baadhi ya wahitimu wakionyesha vyeti vyao wakiwa na Maofisa wa TBL na ABIn Bev --- Washiriki wapatao 167 wanaofanya biashara kwa kushirikiana na kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) walioshiriki mafunzo ya ujasiriamali na mbinu za biashara yanayojulikana kama Retail Development Programme (RDP) wametunukiwa vyeti katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Wanufaika wa mafunzo haya ambao wengi wao ni wamiliki wa mabaa,mameneja wa baa na wafanyakazi wametokea katika wilaya za Temeke, Kinondoni, Kigamboni, Ilala Ubungo na yaliendeshwa na TBL chini ya kampuni mama ya ABIn Bev. Mkurugenzi wa ukuzaji wa Masoko wa ABIn Bev,Kanda ya Afrika Mashariki, Carlos Bernitt,aliwapongeza wahitimu wa mafunzo hayo “Nawapongeza kwa kuhitimu mafunzo haya na nina imani mkitumia vizuri maarifa mliyoyapata yatawasaidia kukuza biashara zenu na kuleta maendeleo ya kwenu binafsi na jamii nzima kwa ujumla”,alisema Bernitt. 
 
Akiongea kuhusu mafunzo hayo,Meneja Masoko na Ukuzaji Biashara wa TBL,Edith Bebwa,alisema mafunzo ya ujasiriamali yanayotolewa chini ya mpango unaojulikana kama Retail Development Programme (RDP), yanalenga kuwapatia mbinu za kufanya biashara kwa ufasaha wafanyabiashara wadogo wanaoshirikiana nao kibiashara ili kuwasaidia kukua kibiashara. “Mafunzo haya yameendeshwa na wataalamu wa masuala ya ujasiriamali na washiriki wamewezeshwa kujifunza mambo mbalimbali ya biashara ikiwemo urasimishaji biashara zao,tunaamini yatawasaidia kufanya vizuri sambamba na malengo yetu yaliyokusudiwa”.
 
Alisema Bebwa. Akiongea kwa niaba ya washiriki wa mafunzo haya,Damas Asenga,alisema kuwa mafunzo haya yamewasaidia kujua masuala mbalimbali ya kuendesha biashara hasa za kuuza vinywaji kama vile utunzaji wa hesabu,mbinu za kuongeza mauzo,huduma kwa wateja,nidhamu ya matumizi ya pesa,jinsi ya kukabiliana na ushindani wa kibiashara na umuhimu wa kufuata kanuni za biashara zilizowekwa na serikali. “Mafunzo haya ni mazuri na tunaiomba TBL iangalie uwezekano wa kuyafikisha kwa wajasiriamali wengi zaidi nchini kote “,alisema Asenga.

BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO (TADB) YAAHIDI MAKUBWA PANGANI

$
0
0

 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ndg. Japhet Justine akiungumza na viongozi wa wilaya ya Pangani wakati wa kikao chao cha pamoja kuhusiana ushirikiano
 Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah akizungumza katika kikao hicho kulia ni Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gibson George
 Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gibson George kulia akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ndg. Japhet Justine  kushoto akiangana na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah
Wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kufanya mazungumzo hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mh. Zainab Abdalah ametembelea uongozi wa Benki ya Maendeleo ya kilimo nchini kufanya kikao kilichomkutanisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Ndg. Japhet Justine na viongozi waandamizi ambao kwa pamoja wameahidi kuifanya Pangani wilaya ya mfano na ya kimkakati kwenye mipango yao.
..
Kikao hiki kimetoka na maazimio mazito kuelekea mapinduzi ya kilimo Pangani na moja kwa moja Mkurugenzi amekubali kua tayari kujenga kituo kikubwa cha ukusanyaji maziwa Pangani eneo la Madanga.

Aidha kikao kimeadhimia kuisaidia sekta ya uvuvi Pangani kuhakikisha inaleta mapinduzi ya uchumi kwa wavuvi.
..
Muhimu zaidi mazungumzo yamefanyika na kuweka misingi itakayowasaidia vijana wa Pangani hasa waliotayari kuungana na kunufaika na mipango ilioazimiwa na uongozi mzima kuahidi hivi karibuni kufika Pangani kuchagiza yaliopangwa na kujionea nini zaidi wanaweza kufanya na Pangani.
..
Mkuu wa Wilaya Pangani amemshukuru Kaimu Mkurugenzi Mtendaji kwa ufanisi wake na utayari aliounesha,kasi uwajibikaji na zaidi alivo tayari kujitoa kwa ajili ya Maendeleo ya nchi yetu.

MKUU WA WILAYA YA CHUNYA AAHIDI KUPAMBANA NA WAFUGAJI WANAOHALIBU VYANZO VYA MAJI

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Meryprisca Mahundi (katikati) akimkisikiliza kwa makini Afisa Mtendaji Kata ya Sangambi kijiji cha Igundu Joseph Nangale ,kuhusiana na namna ambavyo wafugaji wamefanya uhalibifu wa vyanzo vya maji katika kjiji hicho.Picha David Nyembe
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Meryprisca Mahundi akiwa katika harakati za kujionea maeneo ya vyanzo vya maji ambayo yamehalibiwa vibaya na baadhi ya wafugaji wa kijiji cha Igundu kutokana na kunywesha mifugo katika maeneo hayo .
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mh Meryprisca Mahundi (Katikati)akiteta jambo na viongozi wa vijiji vinavyo zunguka kata ya Sangambi ambako kumefanyika uhalibifu wa vyanzo vya maji kutokana na baadhi ya wafugaji wa vijiji hivyo kunywesha mifugo yao sanjali na kupitisha mifugo katika maeneo ya vyazno hivyo.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mh Meryprisca Mahundi akizungumza na wananchi wa Kata ya Sangambi (hawapo pichani) mara baada ya kukamilisha ziara ya kutembelea maeneo ya vyanzo vya maji ambako kumefanyika uhalibifu mkubwa kutokana na baadhi ya wafugaji kupitisha mifugo yao .
Wananchi wa kijiji cha Igundu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Chunya Merryprisca Mahundi (hayupo pichani) mara baada ya kukamilisha ziara ya kutembelea maeneo ya vyanzo vya maji ambako kumefanyika uhalibifu mkubwa kutokana na baadhi ya wafugaji kupitisha mifugo yao .


Na David Nyembe, Chunya

MKUU wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Maryprisca Mahundi, amewapa wiki tatu wafugaji wa Kijiji cha Igundu katika Kata ya Sangambi wilayani humo kuhamisha mifugo yao na kuipeleka katika Kijiji cha Paris ambacho kimetengwa kwa ajili ya wafugaji.

Ametoa kauli hiyo wakati wa Mkutano wa Hadhara uliofanyika kijijini hapo ambapo alisema lengo la kuondoa mifugo hiyo ni kumaliza mgogoro kati ya wakulima wa kijiji hicho na wafugaji pamoja na kuokoa chanzo cha maji ambacho wakazi wa eneo hilo wanakitegemea. Alimuagiza Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Joseph Nangale, kusimamia na kuhakikisha mifugo hiyo inahamishwa huku akimtaka kutumia nguvu iliyotumika kuwazuia wakulima kufanya shughuli zao karibu na chanzo cha maji.

Mahundi alisema amechoshwa na migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijji hicho cha Igundu na kwamba agizo lake hilo ni la mwisho na kwamba atakaporudi tena kwenye kijiji hicho na kukuta inaendelea hakutakuwa na majadiliano tena na kwamba wasije wakamlaumu.

“Mkae chini mjadiliane na mkubaliane idadi ya mifugo ambayo kila mfugaji wa kijiji hiki atatakiwa kubaki nayo hapa, nimewapa siku 10 viongozi wenu waniletee taarifa ya majidiriano hayo, lakini nimewashauri kila mfugaji abaki na mifugo 10,” alisema Mahundi.

Alisema idadi hiyo aliyopendekeza kila mfugaji abaki nayo kijijini hapo ni rahisi kuimudu ili isiingie kwenye mazao ya wakulima na kwamba itasaidia kumaliza migogoro. Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Nangale alikiri kijiji hocho kuwa na idadi kubwa ya mifugo kuliko uwezo wa eneo la kijiji hicho hali ambayo inapelekea migogoro ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji.

Alisema migogoro hiyo ilikuwa inaibuka baada ya mifugo kuwashinda wafugaji na kuingia kwenye mashamba ya wakulima na kuharibu mazao na hivyo kuwafanya wakulima waanze kutaka kulipiza kisasi. Aliahidi kushiriiana na halmashauri nzima ya kijiji hicho katika kutekeleza agizo la Mkuu wa Wilaya la kuondoa mifugo na kwamba watayashirikisha makundi yote ili kufikia mwafaka ambao hautaleta shida.

“Kijiji cha paris kina eneo kubwa kwa ajili ya mifugo na ni eneo rafiki kwa sababu hakuna mwingiliano na shughuli zingine za kibinadamu, tulikitenga maalumu kwa ajili ya wafugaji,” alisema Nangale. Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya aliwatahadharisha viongozi wa vijiji wanaopokea rushwa kutoka kwa wafugaji ili waingize mifugo kwenye vijiji vyao kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria endapo watabainika.

TANZANIA KUSHIRIKI MAONESHO YA CIIE YATAKAYOFANYIKA SHANGHAI NCHINI CHINA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KATIKA  kuendeleza mkakati wa kutangaza utalii wa Tanzania nchini China, Bodi ya Utalii Nchini (TTB) kwa kushirikiana na wadau wa Utalii wa Tanzania pamoja na Sekta ya Madini inashiriki onesho kubwa la biashara yaliyoandaliwa na Serikali ya China.

Maonesho hayo makubwa  yajulikanayo kama China International Impact Expo (CIIE) yatafanyika katika jiji la Shanghai kuanzia  5-10 Novemba, 2018 na  Kupitia maonesho haya, sekta ya madini itaudhihirishia ulimwengu kuwa Madini ya Tanzanite yanapatikana Tanzania tu. 

Akielezea safari hiyo ya nchini China, Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii  Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amesema kuwa safari hiyo ya nchini China imeandaliwa na bodi ya utalii kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini China na Shirika la Ndege la Tanzania ATCL, wameandaa ziara ya utangazaji nchini China ambapo pamoja na kushiriki maonyesho ya CIIE watafanya ziara ya utangazaji katika miji mbalimbali.

Amesema miji hiyo ni Shanghai (12 Novemba, 2018), Guangzhou (14 Novemba, 2018), Hong Kong (16 Novemba, 2018), Chengdu (19 Novemba, 2018) na Beijing (20 Novemba, 2018). Misafara hii itatuwezesha kukutana na wafanyabiashara wa utalii wakubwa katika miji hiyo na wawekezaji wakubwa katika sekta ya utalii pamoja na vyombo vya habari mbalimbali vya China.

 Aidha, Mihayo amesema Shirika  la N dege la Tanzania (ATCL) litatumia ziara hii kama fursa ya kutangaza kuzinduliwa kwa safari mpya kwa kutumia ndege aina ya 4 Dreamliner kwenda katika mji wa Guangzhou.

 "Tunaamini ziara hii itasaidia kuongeza idadi ya watalii kutoka China.na  Ujumbe utakaoshiriki katika ziara utaongozwa na Naibu katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii akiongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB,'amesema Mihayo.

"China ni miongoni mwa masoko mapya yanayokuwa kwa kasi sana kwa Tanzania, na ni soko la sita miongoni mwa masoko yanayotuletea watalii wengi ambapo kwa takwimu za mwaka 2017Tanzania ilipokea watalii 29,224 kutoka China. Nchi ya kwanza ni Marekani (87,238); ikifuatiwa na Uingereza (66,491); Ujerumani (58,390); Italia (49,909) na India (39,115),"

Mihayo ameeleza, Taasisi zitakazoshiriki ni Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Hifadhi za Taifa (TANAPA), Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Kituo Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), Mamlaka ya Wanyamapori (TAWA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA) na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS). Pamoja na Kampuni 15 za utalii kutoka Tanzania Bara na Viziwani.

Kwa upande wa Meneja Masoko na Usambazaji Edward Mkwabi amesema kuwa kuzinduliwa kwa safari za ndege hiyo kuelekea China kutatoa fursa kwa watalii, wafanyabishara pamoja na wanafunzi.

Mkwabi amesema kuwa, safari za ndege rasmi zitaanza mwezi Februari na ndege itapitia Bangkok kuelekea China, pia ili kuwapa fursa watumiaji wa ndege hiyo ya BOEING -DREAMLINER 787 itaondoka saa 7 usiku kwa siku za Jumanne, Alhamis na Jumamosi.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)  Jaji Mstaafu Thomas akizungumzia safari ya China na ushiriki wao wa Maonesho  makubwa  yajulikanayo kama China International Impact Expo (CIIE) yatafanyika katika jiji la Shanghai kuanzia  5-10 Novemba, 2018, Kushoto ni  Mihayo    Meneja Masoko na Usambazaji Edward Mkwabi.

MAHAKAMA KUU TANGA YAJIPANGA KUSIKILIZA NA KUMALIZA MASHAURI KWA WAKATI

$
0
0
Na Amina Ahmad, Mahakama Kuu-Tanga .

Mahakama Kuu Kanda ya Tanga imefanya kikao cha kusukuma mashauri (Case flow Management Meeting) na kujadili mikakati mbalimbali ikiwemo namna bora ya kuzuia mashauri kuwa mrundikano na kuondoa vikwazo visivyo vya lazima ili kurahisisha uendeshwaji wa mashauri. 

Akiongoza Kikao hicho Novemba 05, Mwenyekiti wa kikao ambaye pia ni Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Tanga, Mhe. Amiri Mruma aliwataka Wadau kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha lengo lililopo mbele yao.
“Wito wangu kwa Wahe. Majaji na Mahakimu wa Kanda hii ni kufanya vikao vya awali na Wadau (Pre – session meeting) ili kuweza kujadili masuala mbalimbali hususani changamoto za Mashahidi ili kurahisisha uendeshwaji wa mashauri pindi vikao vya Mahakama (Session) vitakapokuwa vinaendelea,” alieleza Mhe. Mruma. 

Akisoma taarifa katika kikao hicho, Katibu wa kikao ambaye pia ni Naibu Msajili Mahakama Kuu, Kanda ya Tanga, Mhe. Francis Kabwe alisema, tangu kuanza mwaka 2018 Mahakama Kuu Kanda hiyo imefanikiwa kufanya vikao vitatu (3) vya kesi za mauaji (criminal sessions) ambapo jumla ya mashauri 20 ya usikilizwaji wa awali (PH) yalipangwa kusikilizwa. Mhe. Kabwe alisema kati ya mashauri hayo, jumla ya mashauri 12 yaliisha na mashauri 8 yalitolewa maelekezo ya kupangwa katika vikao vijavyo ambapo kati ya mashauri 8, mashauri 6 pia yalimalizika. Kwa upande wa mashauri ya mrundikano, Mhe. Kabwe alisema, Mahakama Kuu Tanga ina mashauri 21 yenye umri kati ya miezi 13 – 24 yakiwemo mashauri ya Mahakama ya kazi. 

“Mashauri hayo 21yamewekewa mkakati madhubuti wa kuyaondoa ili kuzuia mrundikano (Back stopping) ambapo tayari kikao kimoja kimeshaanza kusikiliza mashauri hayo mbele ya Mhe. Jaji Mruma na kutarajiwa kumaliza Novemba, 15, 2018,” alisema Mhe. Kabwe. Aidha; Mhe. Kabwe aliwaeleza wajumbe kuwa kikao kingine kitafanyika kuanzia Novemba 12 hadi Novemba 15, 2018 mbele ya Mhe. Jaji Edson Mkasimongwa. Wajumbe waliohudhuria ni kutoka Ofisi ya mwanasheria wa Serikali, Mawakili wa kujitegemea, Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), CMA na Taasisi ya kutoa msaada wa kisheria (TAWLA). 

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Tanga, Mhe. Amiri Mruma (aliyesimama) akizungumza na Wadau waliohudhuria katika kikao cha kusukuma mashauri.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Mhe. Francis Kabwe akiwasilisha taarifa katika kikao hicho. Katikati ni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Mhe. Amir Msumi, wa pili kulia ni Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Tanga, Bw. Ahmed Ng’eni, wa kwanza kulia ni Kaimu Mwenyekiti chama cha Mawakili wa kujitegemea (TLS – TANGA CHAPTER), Bi. Linda Lugano na Kushoto niKaimu Mwanasheria wa Serikali Mfawidhi Mkoa wa Tanga, Mhe. Shose Naimani.

Pichani ni baadhi ya Wadau waliohudhuria kwenye kikao.
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images