Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1716 | 1717 | (Page 1718) | 1719 | 1720 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Na. Vero Ignatus, Manyara.

  Kamishna wa Bima Tanzania Dkt.Abdallah Saqware Baghayo amewataka wafanyabiashara hapa nchini wanaoagiza bidhaa kutoka nje ya nchi kwa kutumia njia ya magari,ndege,meli ikatiwe Bima kutoka katika makampuni yaliyosajiliwa na mamlaka hiyo.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi Madarasa Mawili Ofisi Pamoja na Vyoo katika shule ya msingi Gedamar iliyopo Wilayani Babati Mkoani Manyara,Baghayo amesema ni kosa kwa mfanyabiashara kisheria kwa mfanyabiashara kunua bidhaa ambayo haijasajiliwa na mamlaka hiyo.

  Amesema ni tegemeo la serikali kuwa makampuni yaliyopewa leseni yatapata biashara ya uagizaji wa bidhaa huku akiwataka wananchi kutambua umuhimu wa bima na kufuata sheria.Dkt.Baghayo amesema mabadiliko ya sheria hiyo yalisainiwa na raisi Dkt.John Pombe Magufuli ili kuweza kutekelezwa na kuzuia wafanyabiashara kutumia bima kupitia makampuni yasiyo sajiliwa.

  Kwa Upande wake Mkuu wa Kitengo cha fedha kutoka Jubilee Life Insuarence Helena Mzena alisema kuwa kampuni hiyo inatimiza miaka 80 tangu kuanzishwa kwake, hivyo kuamua kurudisha faida kwa jamii kwa kuangalia changamoto mbali mbali zilizopo katika shule ya msingi hapa nchini.

  Aidha alisema kuwa mradi huo walipanga kutumia kiasi cha shilingi Milioni 200 kwa Ajili ya kukarabati Vyumba vya Madarasa,Ujenzi wa Vyoo,Ujenzi wa Nyumba mbili za walimu na Ujenzi wa Ofisi ya Walimu kulingana na mahitaji ya shule husika.Mzena alisema kuwa Kampuni hiyo mpaka sasa imetumia kiasi cha shilingi milioni 152 katika Shule saba katika Mikoa ya Morogoro,Manyara,Bukoba,Mbeya,Dar es Saalam,Dodoma na Zanzibar.

  Naye Meneja wa Kanda ya Kaskazini Sweetbert Lasway alisema kuwa kampuni hiyo imeweza kukarabati madarasa mawili,Kumalizia Ofisi ya walimu na Ujenzi wa Vyoo katika shule ya msingi Gedamar kwa gharama ya shilingi milioni 25.
  Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini Dkt. Abdallah Saqware Baghayo akizungumza na waalimu, viongozi wa kijiji cha Gedamar
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Bima ya Jubilee. Dipankar Acharya
  Meneja wa TIRA Kanda ya Kaskazini Eliezer RweikizaMkuu wa Kitengo cha fedha kutoka Jubilee Life Insuarence Helena Mzena akizungumza katika hafla hiyo
  Meneja wa Kampuni ya Bima Jubilee Kanda ya Kaskazini Sweetbert Lasway akizungunza na wazazi na wanafunzi katika shule ya msingi Gedamar
  Kamishana wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini Dkt.Abdallah Saqware
  akibadilishana mawazo na viongozi wa kijiji cha Gendemar pamoja na waalimu wa shule ya msingi Gendermar.
  Picha ya pamoja. Picha zote na Vero Ignatus

  0 0


  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile pamoja na Laigwenani wa Kimasai Mzee Maika Ngukuu (84) wakizindua Kituo cha Mtandao wa Kupambana na Ukeketaji cha Shirka la NAFGEM kilichopo Orkesumet Simanjiro mkoani Manyara.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akionesha kufuraishwa kwake na baadhi ya bidhaa za wanawake wajasiliamali wakimasai wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Mtandao wa Kupambana na Ukeketaji Orkesumet Simanjiro Mkoani Manyara .
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akipanda mti mara baada ya kuzindua Kituo cha Mtandao wa Kupambana na Ukeketaji Orkesumet Simanjiro Mkoani Manyara.

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akiwa na Wasichana waliokolewa na vitendo vya ukatili wa ukeketaji wanaopatiwa mafunzo ya ujasiliamali na Kituo cha Mtandao wa Kupambana na Ukeketaji Orkesumet Simanjiro Mkoani Manyara.
  Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

  Na Anthony Ishengoma – Manyara


  Jamii ya Wamasai nchini imetakiwa kuacha tabia ya kumtumia mtoto wa kike kama bidhaa na kuanza kuwapeleka watoto wakike shuleni badala ya kuwaozesha wakiwa wadogo kama mtaji wa kujipatia ng’ombe.

  Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile aliyasema hayo jana alipofanya ziara ya siku moja Wilayani Simanjiro kwa aijili ya kukagua hospitali lakini pia kuzindua Kituo cha Mtandao wa Kupinga Ukeketaji kilichopo Makao Makuu ya Wilaya ya Simajiro eneo la Orkesumet.

  Dkt. Ndugulile aliongeza kuwa ni muhimu kwa Wamasai kuanza kujenga jamii inayoelimika ili kuweza kutokomeza baadhi ya mila zisizofaa kwani jamii ikielimika baadhi ya mila na desturi katika jamii husika upotea zenyewe.

  Awali Mkurugezi Mtendaji wa Kituo cha Mtandao wa Kupambana na Ukeketaji Simanjiro Bw. Francis Selasini alimwambia Dkt. Ndugulile kuwa kituo chake kilimwokoa mtoto wa miaka minane ambaye alikuwa anakaribia kuolewa na mzee wa miaka 72 ambaye tayari alishakubaliana na wazazi wake kumuoa na mtoto huyo kwa sasa amemaliza darasa la saba kwa msaada wa kituo hicho.

  Dkt. Ndugulile aliwaambia Wazee wa Kimila kutambua kuwa ni kinyume na matakwa ya serikali na ni dhambi kubwa kuozesha watoto wadodo hususan watoto walio chini ya miaka kumi na nane akiitaka jamii hiyo kubadilika na kuelimisha watoto wa kike kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.

  Naibu Waziri Ndugulile pia amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mhandisi Zephania Chaula kuwezesha wanawake wa kimasai kiuchumi kwa kuwapatia mikopo ili waweze kuzalisha mali kama hatua ya kupambana na umasikini kwani wanaume wao mara nyingi uhama na mifugo yao na kuacha na mzigo mkubwa wa kutunza familia.

  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mtandao Kupambana na Ukeketaji cha NAFGEM Simajiro Bw.Francis Selasini katika ya hotuba yake kwa Naibu Waziri Ndugulile alisema wakeketaji kwa sasa wamebadili mbinu ya ukeketaji na kwasasa wanakeketa watoto wadogo kwa nyakati za husiku kwa sababu watoto hao hawana uwezo wa kutoa taarifa.

  Hii hii inatokana na serikali pamoja na wadau kupinga vitendo vya ukeketaji lakini Mkurugenzi huyo pia amepinga takwimu zilizopo zinazosema mkoa wa Manyara una asilimia 58 ya vitendo vya ukatili hapa Nchini.

  “Takwimu zinaonesha Mkoa wa Manyara una asilimia 58 ya vitendo vya ukatili hapa nchini lakini takwimu hizi hazioneshi uhalisia kwa kuwa Mkoa huu jamii zake zote zina mila ya ukeketaji na vitendo hivi vipo kwa wingi sana tunaomba serikali itoe njia bora ya utafiti ili tuwezo kujua kiuhalisia ukubwa wa tatizo.” Alisema Bw. Selasini.

  Akihitimisha hotuba yake kituoni hapo Naibu Waziri Ndugulile aliyataka Mashirika ya SIDO, TFDA, na mengine Wilayani humo kutoa elimu ya namna bora ya kutengeneza bidhaa zenye ithibati ili bidhaa za wajasliamali wanawake ziweze kushindana kwa ubora katika Soko.

  Kituo cha Mtandao wa Kupambana na Ukeketaji cha NAFGEM kilichopo Wilaya ya Simanjiro kimekuwa msaada Mkubwa kwa Jamii ya Kimasai kwani kwa sasa kinawatunza Wasichana wanaokimbia ukeketaji na kuwarudisha shuleni na wengine kuwafundisha ujasiliamali wa kutengeneza sabuni, batik na ushonaji pamoja na shule ya chekechea kwa watoto wadogo

  0 0

  Katibu tawala wa mkoa wa Pwani Theresia Mbando (wa pili kulia ) na mkurugenzi wa Astra Pharmacy Ranjiy Jha(wa kwanza kushoto ) wakitia saini mkataba wa usambazaji wa dawa ,vifaa tiba na vitendanishi kwa kupitia mfumo wa mshitiri mmoja (prime vendor system),wa kwanza kulia ni mfamasia wa mkoa Elias Mabonesho


  Katibu tawala wa mkoa wa Pwani Theresia Mbando (wa kwanza kulia ) akisaini mkataba wa usambazaji wa dawa ,vifaa tiba na vitendanishi kwa kupitia mfumo wa mshitiri mmoja (prime vendor system)

  Baadhi ya wakurugenzi na waganga wakuu wa wilaya ambao wameshiriki katika zoezi la utiaji saini wa mkataba wa usambazaji wa dawa ,vifaa tiba na vitendanishi kwa kupitia mfumo wa mshitiri mmoja (prime vendor system).(picha na Mwamvua Mwinyi )

  ……………………..
   
  NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

  MKOA wa Pwani,umefikia asilimia 90 ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ,hadi kufikia octoba 2018, hatua ambayo inaelekea kwenda kupunguza kero ya upungufu wa dawa na vifaa hivyo kwenye vituo vya afya.

  Hayo yalibainika ,wakati wa kikao cha mkoa cha zoezi la kusaini mkataba wa usambazaji wa dawa ,vifaa tiba na vitendanishi kupitia mfumo wa mshitiri mmoja (prime vendor system),zoezi ambalo limefanywa baina ya katibu tawala wa mkoa Theresia Mbando na mkurugenzi wa Astra Pharmacy Ranjiy Jha.

  “Kwa mujibu wa taarifa zinavyotolewa katika mfumo wa kukusanya na kuchambua data za afya (DHIS 2 ),hadi kufikia kipindi hicho wamefikia asilimia hiyo jambo ambalo limenifurahisha” alisema Theresia . Theresia alisema ,kwa hatua waliyofikia mzabuni huyo anatarajiwa atafikisha lengo la upatikanaji wa dawa kwenye vituo na halmashauri za mkoa kwa asilimia 100.

  “Wananchi wamekuwa wakilalamikia juu ya upungufu wa dawa na vifaa tiba katika vituo vyetu hivyo ni imani yangu kwa hatua hii ,itakuwa muarobaini wa malalamiko hayo “ Aidha alisema, kumekuwa na wastani wa utimilizaji wa oda kwa kiwango ambacho ni cha kubadilika badilika kutoka bohari ya madawa (MSD). “Kufuatia uwepo wa mshitiri huyu naamini kwa bidhaa ambazo hazijatimia utimilifu kama ziliombwa bohari ya madawa zitajaziwa na mshitiri na hilo ndilo lengo kuu “alifafanua Theresia .

  Kwa mujibu wa Theresia, baada ya kusaini mkataba huo halmashauri hazitakiwi kutumia wazabuni wengine na badala yake zitatakiwa kununua kwa mzabuni aliyepatikana kisheria kupitia mchakato uliofanywa na OR-TAMISEMI mwaka 2017. Nae mfamasia wa mkoa wa Pwani Elias Mabonesho ,alielezea mfumo huo ulianzia Dodoma kama majaribio na kwasasa uko katika mikoa ya Morogoro ,Shinyanga na sasa Pwani .

  Anasema ,mfumo utasimamiwa na ofisi ya katibu tawala wa mkoa kupitia ofisi ya uratibu wa mfumo wa mshitiri mmoja chini ya Mganga mkuu wa mkoa akisaidiwa na mfamasia ambae ndie mratibu huu . Kwa upande wa wakurugenzi na waganga wakuu wa wilaya ,akiwemo mkurugenzi wa Mafia ,Erick Mapunda alisema ,kwa mfumo wa Jazia tatizo la ukosefu wa dawa linakwenda kuwa historia.

  0 0


  Asasi ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Health Initiative (AGPAHI) inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia nchini Tanzania imetoa msaada wa magari mawili aina ya Nissan Patrol kwa halmashauri za wilaya za Buchosa na Misungwi mkoani Mwanza kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI katika halmashauri hizo.

  Magari hayo yenye namba za usajili DFPA 7015 na DFPA 7016 yana thamani ya shilingi milioni 186 yamenunuliwa na shirika la AGPAHI kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR) chini ya vituo vya Kudhibiti Magonjwa na Kinga (CDC).

  Hafla fupi ya Makabidhiano ya magari, imefanyika leo Jumatatu Novemba 5,2018 wakati wa kikao cha wadau wa afya na ustawi wa jamii mkoa wa Mwanza kilichofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa John Mongella.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi magari hayo kwa Mkuu huyo wa mkoa, Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa alisema msaada huo wa magari ni kwa ajili ya kuboresha utoaji huduma za afya hususani za VVU na UKIMWI kwenye vituo vya kutolea huduma.

  Dkt. Mwakyusa alisema, AGPAHI imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na halmashauri katika kuboresha huduma za VVU na UKIMWI kwa ajili ya ustawi wa wananchi na taifa kwa ujumla.

  “Magari tuliyokabidhi leo yana thamani ya shilingi milioni 186, na hii ni sehemu ya vyombo vya usafiri (magari,pikipiki na baiskeli) vyenye thamani ya shilingi milioni 900.2 tulivyonunua katika kipindi cha kuanzia Oktoba 2017 hadi Septemba 2018 kwa ajili ya kuleta tija kwenye utendaji kazi ili kuboresha huduma za VVU na UKIMWI katika halmashauri ambazo AGPAHI inafanya kazi,” alieleza Dkt. Mwakyusa.

  Aliongeza kuwa katika jitihada za kuboresha utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI, katika kipindi hicho, AGPAHI imefanyia ukarabati vituo 146 vya kutolea huduma vikiwemo 36 vya mkoa wa Mwanza. Pia imeweka mifumo ya umeme jua kwenye vituo 40 vya kutolea huduma kwenye halmashauri mbalimbali.

  Akipokea magari hayo, Mkuu wa mkoa, Mheshimiwa Mongella aliishukuru AGPAHI kwa kuwa mdau muhimu katika sekta ya afya na kuomba waendelee kushirikiana na serikali katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

  Mheshimiwa Mongella aliwataka watendaji wa halmashauri zilizopewa magari kutunza na kuyatumia magari hayo kwa kazi za afya na maendeleo ya halmashauri na siyo vinginevyo.
  Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa Mongella, akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa afya na ustawi wa jamii mkoa wa Mwanza katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza ambapo kikao hicho kimeenda sanjari na hafla fupi ya AGPAHI kukabidhi magari mawili kwa halmashauri ya wilaya ya Buchosa na Misungwi.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
  Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa, akizungumza wakati wa kukabidhi magari mawili kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa John Mongella kwa ajili ya halmashauri ya wilaya ya Buchosa na Misungwi ili kuboresha huduma za VVU na UKIMWI katika vituo vya kutolea huduma. Kushoto ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Dkt. Thomas Rutachunzibwa.
  Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Mheshimiwa John Mongella, akiishukuru AGPAHI kwa kutoa msaada wa magari huku akiahidi kuwa magari hayo yatatumika kwa lengo lililokusudiwa na kuboresha huduma za VVU na UKIMWI.
  Magari yenye namba za usajili DFPA 7015 na DFPA 7016 yenye thamani ya shilingi milioni 186 yaliyonunuliwa na shirika la AGPAHI kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR) chini ya vituo vya Kudhibiti Magonjwa na Kinga (CDC).
  Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa John Mongella, akikata utepe wakati wa hafla ya makabidhiano ya magari yaliyotolewa na AGPAHI kwa ajili ya kuboresha huduma za VVU na UKIMWI katika halmashauri ya wilaya ya Buchosa na Misungwi mkoani Mwanza.
  Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Buchosa,Crispin Luanda na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa John Mongella (wa tatu kulia) wakioneshana magari yaliyotolewa na AGPAHI.
  Muonekano wa magari yaliyotolewa na AGPAHI kwa ajili ya kuboresha huduma VVU na UKIMWI katika halmashauri ya wilaya ya Misungwi na Buchosa.
  Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa, akikabidhi ufunguo wa gari kwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa John Mongella.
  Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa John Mongella, akionesha ufunguo wa gari.
  Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa, akikabidhi kadi ya gari kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi, Mheshimiwa Anthony Bahebe.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Buchosa,Crispin Luanda akipokea ufunguo wa gari.
  Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Buchosa wakiangalia gari walilokabidhiwa.
  Dereva wa halmashauri ya wilaya ya Misungwi ,Nicholaus Mzee, akiwa ndani ya gari walilokabidhiwa.

  Muonekano wa magari yaliyotolewa na AGPAHI.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

  0 0

   Muonekano wa kivuko cha MV. Chato mara baada ya kukamilika kwa ukarabati wake. Kivuko hicho cha tani 75 kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 6 kinatarajiwa kurudishwa katika kituo chake kuendelea na kazi ya kuvusha abiria maeneo ya Ikumba Itale, Izumacherl, Muharamba, Senga, Bukondo na Bwina Mkoani Geita.
  Kivuko cha MV. Chato kikielea majini baada ya kukamilika kwa ukarabati wake .Kivuko hicho cha tani 75 kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 6 kinatarajiwa kurudishwa katika kituo chake  Wilayani Chato Mkoani Geita kuendelea na kazi ya kuvusha abiria.PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA).
   Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia akijadiliana jambo na Meneja wa kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Boatyard ya jijini Mwanza Major Songoro mara baada ya kukagua kivuko cha MV. Chato ambacho ukarabati wake umemalizika, kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba tani 75 sawa na abiria 200,na magari 6 kinatoa huduma Wilaya ya Chato, maeneo ya Ikumba Itale, Izumacheli, Muharamba, Senga, Bukondo na Bwina Mkoani Geita .
   Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle wa pili kulia akisisitiza jambo kwa Meneja wa kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Boatyard Major Songoro wa pili kushoto mara baada ya kukagua kivuko cha MV. Chato ambacho ukarabati wake umemalizika, tukio lililofanyika katika yadi ya Songoro iliyopo Ilemela mjini Mwanza. Kivuko hicho cha tani 75 kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 6 na kinatoa huduma katika Wilaya ya Chato, maeneo ya Ikumba Itale, Izumacheli, Muharamba, Senga, Bukondo na Bwina Mkoani Geita. Kushoto ni Mkurugenzi Huduma za Ufundi (WUUM) Mhandisi Lazaro Vazuri na kulia ni Meneja wa TEMESA mkoa wa Mwanza Mhandisi Hassan Karonda.
   Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (aliyevaa suti) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua kivuko cha MV. Chato ambacho ukarabati wake umemalizika, tukio lililofanyika katika yadi ya Songoro mjini Ilemela Mwanza. Kivuko hicho cha tani 75 kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 6 na kinatoa huduma katika Wilaya ya Chato, maeneo ya Ikumba Itale, Izumacheli, Muharamba, Senga, Bukondo na Bwina Mkoani Geita.  0 0

   Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia akijadiliana jambo na Meneja wa kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Boatyard ya jijini Mwanza Major Songoro mara baada ya kukagua kivuko cha MV. Chato ambacho ukarabati wake umemalizika, kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba tani 75 sawa na abiria 200,na magari 6 kinatoa huduma Wilaya ya Chato, maeneo ya Ikumba Itale, Izumacheli, Muharamba, Senga, Bukondo na Bwina Mkoani Geita .
   Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle wa pili kulia akisisitiza jambo kwa Meneja wa kampuni ya Kizalendo ya Songoro Marine Boatyard Major Songoro wa pili kushoto mara baada ya kukagua kivuko cha MV. Chato ambacho ukarabati wake umemalizika, tukio lililofanyika katika yadi ya Songoro iliyopo Ilemela mjini Mwanza. Kivuko hicho cha tani 75 kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 6 na kinatoa huduma katika Wilaya ya Chato, maeneo ya Ikumba Itale, Izumacheli, Muharamba, Senga, Bukondo na Bwina Mkoani Geita. Kushoto ni Mkurugenzi Huduma za Ufundi (WUUM) Mhandisi Lazaro Vazuri na kulia ni Meneja wa TEMESA mkoa wa Mwanza Mhandisi Hassan Karonda.
   Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (aliyevaa suti) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua kivuko cha MV. Chato ambacho ukarabati wake umemalizika, tukio lililofanyika katika yadi ya Songoro mjini Ilemela Mwanza. Kivuko hicho cha tani 75 kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 6 na kinatoa huduma katika Wilaya ya Chato, maeneo ya Ikumba Itale, Izumacheli, Muharamba, Senga, Bukondo na Bwina Mkoani Geita.
   Muonekano wa kivuko cha MV. Chato mara baada ya kukamilika kwa ukarabati wake. Kivuko hicho cha tani 75 kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 6 kinatarajiwa kurudishwa katika kituo chake kuendelea na kazi ya kuvusha abiria maeneo ya Ikumba Itale, Izumacherl, Muharamba, Senga, Bukondo na Bwina Mkoani Geita.
  Kivuko cha MV. Chato kikielea majini baada ya kukamilika kwa ukarabati wake ambao. Kivuko hicho cha tani 75 kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 6 kinatarajiwa kurudishwa katika kituo chake  Wilayani Chato Mkoani Geita kuendelea na kazi ya kuvusha abiria.
  PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA)


  0 0
 • 11/05/18--06:17: ZOEZI LA UHAKIKI WA WASTAAFU


 • 0 0

  Na Khadija Seif,Globu ya Jamii 

  Msanii wa Bongofleva Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platinumz ametangaza ramsi kuanza kwa tamasha la Wasafi Festival Novemba 24 mwaka huu. 

  Tamasha hlo linalotarajiwa kufanyika kwenye mikoa mbalimbali nchini litaanzia Mkoani Mtwara ikiwa ni mara ya kwanza toka kuanza kwa Tv na Redio.

  Akizungumza na wadau pamoja na wanahabari Leo Jijini Dar es salaam, Diamond amesema kuwa tamasha la Wasafi Festival lina lengo la kutoa burudani nchini na nje ya nchi ili kutangaza mziki wa kitanzania zaidi na kufundisha jamii jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii vizuri. 

  Diamond amesema kuwa, licha ya kutangaza mziki huo kwenye mikoa ambayo itapata kushuhudia burudani hiyo ni wataanzia tarehe 24 mwezi huu kwenye mkoa wa Mtwara katika viwanja vya Nangwanda na ikifatiwa na mkoa wa Iringa,Morogoro , Zanzibar na mikoa mingine na pamoja na nchi ya Kenya. 

  Amefafanua zaidi katika kila Mkoa utakaotembelewa pia watapata fursa kwa kukarabati shule , Wanafunzi kupatiwa sare za shule, madaftari na kupatiwa madawati huku kwa wakina mama wasiopungua 200 kupewa mitaji ya kibiashara ili kujikwamua kiuchumi . 

  Sambamba na hilo wasichana wasiopungua 20 watapewa mafunzo ya urembo wa uso pamoja na vifaa vya kupambia. Meneja wa msanii Daimond Platinum Hamis Tale maarufu kama Babu Tale amewaambia wazi kwa sasa radio ya wasafi iko hewani kupitia masafa ya 88.9 ambayo ipo kwa ajili ya kutoa fursa kwa ambao vipaji vyao havijapata nafasi ya kuvuma. 

  Tale ametoa rai kwa mashirika ,wadau na wanamuziki ambao wangependa kushiriki katika tamasha hilo nafasi zipo wazi wanakaribishwa.

  Msanii wa Bongofleva Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' akizungumza na waandishi wa habari wakati wakutambulisha rasmi tamasha la Wasafi Festival Nov 24 mwaka huu Mkoani Mtwara.

  0 0

  Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

  SHIRIKA la Kimataifa la Hifadhi la  World Wide Fund for Nature (WWF) limefanya ziara katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma kwa lengo la kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa mradi ujulikanao SECAD program ( Selous Eco-system Conservation and Development program).

   SECAD ni mradi ambao kwa jumla utatekelezwa kwa miaka mitano ikiwa ni awamu ya kwanza na ya pili ambapo umejikita kuhakikisha wanaongeza uhifadhi wa mazingira kwa maana ya kwenye hifadhi ya Selous pamoja na ushoroba (corridor) unaounganisha pori la akiba la Selous na hifadhi ya Niassa ipatikanayo nchini Msumbiji

  Mkuu wa Wilaya Namtumbo Sophia Kizigo jana kwamba ugeni wa shirika hili uliofika wilayani kwake ulitembelea na kujionea maendeleo ya mradi  na kutembelea jumuiya ya uhifadhi ya Mbarang'andu ambapo walipata taarifa ya mradi na kujionea mafanikio, mipango na changamoto kwa sasa. 

  Mkuu wa Wilaya huyo ameueleza ugeni wa shirika hilo kuwa moja ya mafanikio ni mradi wa ufugaji wa nyuki kwa ajili ya kurina asali ambao unaosimamiwa na jumuiya hiyo pamoja na mpango wa ujenzi wa kiwanda cha kuongezea thamani asali pamoja na mabwawa ya samaki.

  Kuhusu changamoto amesema moja ya changamoto ya mradi ni  wananchi kuvamia maeneo ya hifadhi na kufanya shughuli za kibinadamu kama kilimo na ufugaji

  Pia walitembelea Chuo cha Likuyu ambacho kinatumika kufundisha VGS (village scouts) wanaotumika kulinda hifadhi hizo. 
   Mkuu wa Wilaya Namtumbo Sophia Kizigo akipewa maelezo kuhusiana na maendeleo ya mradi wa wa SECAD program ( Selous Eco-system Conservation and Development program) wakati SHIRIKA la Kimataifa la Hifadhi la  World Wide Fund for Nature (WWF) likifanya zaira wilayani yumo kufuatilia mradi huo  
   Eneo la mradi wa ufugaji wa nyuki kwa ajili ya kurina asali
   Mkuu wa Wilaya Namtumbo Sophia Kizigo akiwa sambamba na Wadau wa  SHIRIKA la Kimataifa la Hifadhi la  World Wide Fund for Nature (WWF) wakionesha chupa ya asali ikiwa ni sehemu ya mafanikio ya mradi wa ufugaji wa nyuki kwa ajili ya kurina asali ,ambao unasimamiwa na jumuiya hiyo pamoja na mpango wa ujenzi wa kiwanda cha kuongezea thamani asali pamoja na mabwawa ya samaki. 
   Mkuu wa Wilaya Namtumbo Sophia Kizigo akikaribishwa mara baada ya kuwapokea wageni kutoka SHIRIKA la Kimataifa la Hifadhi la  World Wide Fund for Nature (WWF) llilofanya ziara katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma kwa lengo la kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa mradi ujulikanao SECAD program ( Selous Eco-system Conservation and Development program).

  0 0

  0 0


  ZAIDI ya wakulima 57,000 Mkoani Katavi wanatarajiwa kunufaika na mafunzo yatakayowasaidia kuongeza uzalishaji katika mazao yao, namna bora ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni pamoja na kujengewa uwezo wa namna ya upatikanaji wa masoko kwa mazao wanayolima.

  Aidha pia imeelezwa kuwa ili kuendelea kuinua kiwango cha uzalishaji kwa wakulima mkoani humo zaidi ya maghala 18 ya kuhifadhia mazao yanatarajiwa kujengwa hasa katika maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa mazao,

  Hayo yalielezwa na Afisa Biashara kutoka Baraza la Kilimo Tanzania Bw Alinanuswe Ambalile Mkoani Katavi na kusema kazi kubwa katika Mkoa huo imekwisha kufanyika hasa katika kuwajengea uwezo wakulima wadogo ili kuongeza thamani mazao yao.

  Bw Ambalile alisema kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2018/19 Baraza la Kilimo Tanzania kwa kushirikiana na Mradi wa TIJA TANZANIA wanatarajia kujenga mashamba darasa zaidi 42 kwa mazao ya Mahindi, Mpunga na Maharage,lengo ikiwa ni kuendelea kumjengea uwezo mkulima.

  “Baraza la kilimo Tanzania linafahamu msimu wa kilimo umekaribia na tayari tumekwisha kukarabati maghala 7 ya kuhifadhia mazao pia tumekwisha kuwajengea uwezo wakulima ili mazao wanayozalisha yaendane na mahitaji ya soko na tunaamini kupitia mabadiliko haya tunayoyafanya katika kuweka mashamba darasa hayo 42 wakulima watakuwa na uwezo mzuri zaidi wakulima kilimo chenye tija” alisema Bw Ambalile.

  Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Tija Tanzania Bw. Japhet Laizer alisema chini ya uratibu wa Baraza la Kilimo Tanzania mradi wa Tija umekuwa na manufaa makubwa kwa wakulima mkoani Katavi ambapo tayari wakulima 32,000 wamekwisha kujengewa uwezo wa njia bora za kilimo ambazo zimewasaidia kuanza kulima kilimo chenye manufaa kwao kwa kupata mazao ya kutosha.

  “Katika msimu huu wa kilimo tumejipanga sasa kuongeza nguvu katika kuhakikisha mkulima anayelima Mahindi, Maharage na Mpunga anapata soko la uhakika la mazao yake tunaamini kupitia washirika wetu tutapata masoko sahihi ya wakulima ili mkulima anapolima apate bei nzuri na hiyo ndio njia pekee ya kumuinua mkulima wa Katavi ” alisema Bw Lazier. 
  Muonekano wa Ghala la kuhifadhia mazao linalojengwa na Baraza la Kilimo Tanzania chini ya udhamini wa AGRA katika Kijiji cha Mnyagala Mkoani Katavi likiwa katika hatua za mwisho za kukamilika kwake ambapo baada ya kukamilika litakuwa na uwezo wa kuhifadhi zaidi ya tani 660. 
  Mafundi wakiendelea na hatua za uwekaji Kenki katika ghala hilo ambalo litawasaidia wakulima wa kijiji hiki cha Mnyagala ambao ni wakulima wakubwa wa Mpunga mkaoni Katavi kuwa na uwezo wa kuhifadhi mazao yao, ghala hili linatajwa kuwa la kisasa la kipekee katika kijiji hicho.
  Mafundi wakiendelea na hatua za mwisho za ukarabati wa Ghala la kuhifadhia mazao la kampuni ya Nondo Investiment iliyoko Mkoani Katavi, Ukarabati ambao unaratibiwa na Baraza la Kilimo Tanzania chini ya udhamini wa AGRA ambapo baada ya ukarabati huo kukamilika ghala hilo litakuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 10000.
  Muonekano wan je wa ghala hilo baada ya kufanyiwa marekebisho kwa kuongeza urefu wa ghala hilo ambapo awali lilikuwa na uwezo wa kubeba tani 7000 pekee lakini baada ya kukamilika kwake litakuwa na uwezo wa kubeba tani 10000, ukarabati wote huo unafanywa na Baraza la Kilimo Tanzania chini ya udhamini wa AGRA.
  Mafundi wakiwa katika hatua za mwisho za uwekaji wa kenki katika ghala jipya linalojengwa na Baraza la Kilimo Tanzania katika Kata ya Mishamo Mkoani Katavi ambapo baada ya kukamilika kwa ghala hilo litakuwa na uwezo wa kuhifadhi zaidi ya tani 660 za mazao.
  Muonekano wa ghala la kuhifadhi mazao linalojengwa na Baraza la Kilimo Tanzania chini ya udhamini wa AGRA katika Kata ya Mishano Mkoani Katavi, kukamilika kwa ghala hilo kunatajwa kutawasaidia wakulima wa kata hii yenye vijiji 16 kuweza kuhifadhi mazao yao na kuuza kwa bei yenye tija.
  Msiamizi mkuu wa ukarabati wa ghala la kuhifadhia mazao katika kijiji cha Bulamata akitoa ufafanuzi kuhusu hatua zilizokwisha kufikiwa katika ukarabati wa ghala hilo linalokarabatiwa kwa kuongeza urefu kwenda juu na Baraza la Kilimo Tanzania chini ya ufadhili wa AGRA ambapo mara baada ya kukamilika litakuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 300 tofauti na tani 250 za awali.
   

  0 0

  Wanariadha kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi wamejitokeza kwa wingi kushiriki Namtumbo Marathon inayotarajiwa kutimua vumbi wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma ambapo maelfu ya wakazi wa wilaya hiyo na vitongoji vyake wamekuwa wakizitazamia mbio hizo kuanza wakati wowote ili nao wapate fursa mbalimbali za kushiriki katika mbio hizo.

  Akizungumzia usajili unaoendelea katika hospitali ya wilaya ya Namtumbo, Dokta Chihoma amesema watu wengi wameitikia wito na wamejitokeza kwa wingi wao kujiandikisha tayari kwaajili ya kushriki mbio hizo ambazo zilianzishwa rasmi mwaka 2017 kwa malengo mengi lakini kubwa likiwa ni kuchangisha fedha kwaajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Namtumbo ambayo imefanikia kuanza kwa kiasi kikubwa. 

  Aidha Chihoma ameongeza kuwa nafasi bado zipo wazi kwaajili washiriki watakaojitokeza kujiandika kwaajili ya bio hizo. 

  Kwa upande wao wadhamini wa na waandaaji wa mbio hizo Mantra Tanzania au Uranium one wamesema kila kitu kipo sawasawa na kuwataka watanzania na wageni kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hizo ambazo zinalenga kuleta maendeleo ya kiafya katika eneo la Namtumbo na vitongoji vyake. 

  Mwakilishi wa Mantra Tanzania Bi. Khadija Pallangyo Kawawa amaesema maandalizi yanaendelea vizuri na kwamba watanzania watafurahia mbio za mwaka huu kutokana na jinsi zilivyopata hamasa kubwa katika maeneo mbalimbali “Nawaomba sana watanzania wajitokeze kwa wingi waje washiriki nasi katika kufanikisha awamu ya pili ya Namtumbo Marathon” 

  Alisema Khadija huku akiwaomba wana Namtumbo, Songea Ruvuma na vitongoji vyake hasa wafanya biashara na wenye makampuni katika maeneo mbalimbali nchini kujitokeza kwa wingi kuuchangia ujenzi wa hospitali ya wila ya Namtumbo akiitaja hospitali hiyo kuwa itakuwa msaada mkubwa wenye kuleta mafanikio na maendeleo katika eneo lote linalopakana na wilaya hiyo. 

  Nao waratibu na wasimamizi wa tukio zima Corporate Info Limited ya jiji Dar Es Salaam wamesema mbio hizo zinaandandaliwa kuja kuwa moja kati yam bio kubwa kabisa nchini huku wakijivunia kuwa wasimamizi wa mbio hizo kwa mara nyingine. 

  Wilaya ya Namtumbo imezungukwa na vivutio mbalimbali vya kiasili mojawapo ikiwa mbuga kubwa ya wanya ya Sloue ambayo imekuwa kivutio kikubwa sana kwa watalii kutoka mataifa mbalimbali na ndani nchi hivyo kufanyika kwa mbio hizo itakuwa sehemu mojawapo ya kuitangaza mbuga hiyo pamoja na vursa zingine kama madini aina ya Uranium ambayo yanapatikana kwa wingi wilaya Namtumbo.

  0 0


  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa jimbo la Gairo Mh. Ahmed Shabiby katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma mara baada ya bunge kuahirishwa kwa mapumziko ya mchana.PICHA NAJOHN BUKUKU-BUNGENI JIJINI DODOMA

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Arusha Mh. Amina Mollel.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akifurahia jambo na Mbunge wa jimbo Mufindi Mh. Mahmoud Mgimwa katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma leo.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa jimbola Dodoma mjini na Naibu waziri Ofisi ya waziri mkuu (kazi, Vijana na ajira) Anthony Mavunde na vijana wa UVCCM Dodoma walipotembelea bungeni.
  Mbunge wa jimbo la Mikumi Mh. Joseph Haule akibadilisha na mawazo na baadhi ya wageni waliotembelea bungeni leo.
  Mkuu wa mkoa wa Manyara Mh Alexander Mnyeti akizungumza jambo na Mbunge wa jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu katikati nia Mbunge wa jimbo la Nyamagana Mh. Stanslaus Mabula katika viwanja vya bunge leo jijini Dodoma.
  Mbunge wa jimbo la Mikumi Joseph Haule akiwa katika picha ya pamoja na vijana wa kazi kulia ni Hussein Manane kutoka MMG na kutoka kushoto ni Abdulatif Makbel kutoka ofisi ya Waziri mkuu Eric Pickson kutoka MMG.

  0 0


  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akimuapisha Mh. Julius Kalanga Laizer mbunge wa jimbo la Monduli leo Bungeni mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akimuapisha Mwita Mwikwabe Waitara mbunge wa jimbo la Ukonga leo Bungeni mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akimuapisha Mh Timotheo Paul Mnzava mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini leo Bungeni mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akimuapisha Mh Zuberi Mohamed Kuchauka mbunge wa jimbo la Liwale leo Bungeni mjini Dodoma.

  Mbunge wa jimbo la Monduli Mh. Julius Laizer Kalanga akipongezwa na baadhi ya wananchi waliofika bungeni kumpongeza.
  Mh Zuberi Mohamed Kuchauka mbunge wa jimbo la Liwale kushoto akiwa na wananchi kutoka Liwale waliofika kumpongeza.
  Mh Timotheo Paul Mnzava mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa bungeni jijini Dodoma leo.
  Mh. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mh. Mwita Mwikwabe Waitara pamoja na familia yake.


  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Dodoma

  Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo amewaapisha wabunge wanne ambao walishinda katika chaguzi ndogo zilizofanyika katika Majimbo ya Ukonga, Korogwe,Monduli na Liwale.

  Mara Baada ya kufungua kikao cha 13 cha Bunge la 11 Spika Ndugai alianza kwa kumwita Mh Julius Kalanga Laizer wa Monduli,Mh Mwita Mwikwabe Waitara Mbunge wa Ukonga,Mh Timotheo Paul Mnzava Mbunge wa Korogwe Vijijini na Mh Zuberi Mohamed Kuchauka amabao wote ni kutoka Chama Cha Mapinduzi.

  Mara baada ya kumaliza kuwaapisha wabunge hao spika aliendelea na shughuli za bunge kama zilivyopangwa ambapo mapendekezo ya mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020 .

  Pia aliomba alimtaka Mwenyekiti wa kamati ya bajeti kutoa taharifa kuhusu mapendekezo ya mipango wa Maendleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na serikali pamoja na mwongozo wa kuandaa mpango wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

  Mh Spika pia alimwita Msemaji Mkuu wa kambi ya upinzani wa Wizara ya fedha na Mipango kuhusu mapendekezo ya mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na mwongozo wa kuandaa mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa fedha 2019/2020.

  0 0


   Mwanamuziki Mkongwe nchini Kikumbi Mwanza Mpango 'King Kiki' akizungumza na maofisa  wa Jeshi la Polisi  waliopo katika mafunzo Chuo cha Polisi cha Kurasini jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuhusu haki za wanamuziki hapa nchini ambapo ameliomba jeshi la polisi kuendelea kusimamia sheria ya haki miliki za wanamuzi ili kazi zao zisiishie kwa maharamia. Mada katika mkutano huo zilitolewa na viongozi wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO)
   Maofisa wa polisi wa chuo hicho wakisikiliza mada.
   Katibu wa TAMUFO Stellah Joel Diana akizungumza na maofisa hao.
   Rais wa TAMUFO Dkt. Donald Kisanga akizungumza na makamanda hao.
   Maofisa hao wakiwa bize kuchukua mambo mbalimbali katika mkutano huo.
   Hapa ni kazi tu kwa kwenda mbele maharamia wa kazi za wanamuziki mkae mbali si mnawaona hao jamaa walivyo makini katika mafunzo hayo.
   Mshauri wa masuala ya kisheria wa TAMUFO, Mkaguzi wa Polisi Dkt. Ezekiel Kyogo akitoa mada katika mafunzo hayo. 
   Mkutano ukiendelea.
   Makamanda wakiwapashia makofi viongozi hao wa TAMUFO kwa utoaji wa mada nzuri.
   Mwanamuziki wa nyimba za injili Emmanuel Mbasha akizungumza na makamanda hao.
  Picha ya pamoja

  Na Dotto Mwaibale

  MWANAMUZIKI Mkongwe hapa nchini Kikumbi Mwanza Mpango 'King Kiki' ameliomba jeshi la polisi kuendelea kusimamia sheria ya haki miliki za wanamuzi ili kazi za wanamuziki hao zisiishie kwa maharamia.

  Ombi hilo alilitoa mwishoni mwa wiki wakati viongozi wa Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO), ukitoa mada kwa maofisa wa Jeshi la Polisi  waliopo katika mafunzo Chuo cha Polisi cha Kurasini jijini Dar es Salaam kuhusu haki za wanamuziki hapa nchini.

  "Ninyi wenzetu jeshi la polisi ndio tunaowategemea katika kusimamia sheria hii tunaamini mtatusaidia kazi zetu zisiibwe na maharamia" alisema King Kiki.

  Akizungumza na katika mafunzo hayo Rais wa TAMUFO, Dkt. Donald Kisanga alisema lengo la mafunzo hayo ya siku moja kwa maofisa hao ni kuwajengea  uelewa wa ulinzi wa kazi za muziki ikiwepo  kudhibiti na kuwakamata maharamia wa kazi muziki hapa nchini.

  Katibu Mkuu wa TAMUFO Stellah alisema umoja huo ulishatoa mapendekezo kupitia waraka maalumu kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt Harisson Mwakyembe ili mtu yeyote atakayebainika akihujumu kazi za wasanii ashitakiwe kwa makosa ya jinai.

  Alisema TAMUFO pia inaandaa mapendekezo ya kupeleka serikalini ya kuweka dawati la jinsia katika vituo mbalimbali vya polisi hapa nchini ambayo yatakuwa yakishughulikia wizi wa kazi za wanamuziki.

  Mshauri wa masuala ya kisheria wa TAMUFO, Mkaguzi wa Polisi Dkt. Ezekiel Kyogo akitoa mada katika mafunzo hayo yaliyowahusisha maofisa wa polisi zaidi 500 kutoka mikoa yote ya Tanzania alisema ni muhimu kwa maofisa hao kujua sheria hizo kwa kuwa wao ndio wanaozisimamia.

  "Changamoto kubwa tuliyonayo ni maofisa wetu wa polisi kutojua sheria zinazosimamia kazi za wasanii wetu ndio maana tumeona tuwapige msasa ili waijue na kuweza kuongeza nguvu ya kuwakamata maharamia wa kazi hizo za wanamuziki" alisema Kyogo.


  Alisema sheria ya mtandao ya mwaka 2015 sheria namba 14 mtu yeyote atakaye bainika akidurufu nyimbo na kumpa mtu mwingine bila ya ruhusa ya mmiliki wa wimbo husika adhabu yake ni kifungo kisicho zidi miaka mitatu au kulipa faini shilingi milioni tano.

  Aliongeza kuwa kwa mtu atakayebainika akidurufu nyimbo za wasanii kwa lengo ya kuziuza kifungo chake ni miaka mitatu au kulipa faini shilingini milioni 20 hivyo alitoa rai kwa wananchi kuacha kuchezea kazi za wasanii kwani sheria hizo zipo na zinafanya kazi.

  Alisema kazi za wasanii zikilindwa zitawanufaisha kwa kuziuza na zitatoa ajira hivyo ni muhimu jamii ijengewe uelewa ili waache kuiba kazi hizo ambazo zikilindwa vizuri zitaweza kutangaza utamaduni wetu na serikali itapata mapato kutokana na kodi watakazolipa wahusika baada ya kuziuza.

  Maofisa hao wa polisi waliitaka TAMUFO ijihimarishe zaidi katika kazi yao hasa kwa kusimamia mapato yote ya wanamuziki kama inavyofanyika katika nchi zingine jambo likatalosaidia kuyalinda maslahi ya wanamuziki badala ya kuwategemea polisi ambao wanamajukumu mengi ya kesi za jinai.

  "Tunawaomba TAMUFO mjiongeze wekeni utaratibu wa nyinyi kuwa wakusanyaji wa mapato ya wanamuziki jambo ili litasaidia wanamuziki kupunguza uharamia na pia litatupungizia kazi hata sisi wasimamizi wa sheria" alisema mmoja wa maofisa hao wakati akiuliza maswali.  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo kwa kila Mkuu wa Mkoa aifanye afya ya uzazi na mtoto kuwa ajenda ya kudumu katika vikao vya ushauri vya Mkoa (RCC).

  Makamu wa Rais ametoa maagizo hayo leo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya “Jiongeze Tuwavushe Salama” ya Kuongeza kasi ya Uwajibikaji Kupunguza Vifo Vitokanavyo na Uzazi na Watoto Wachanga.

  “Ili kuhakikisha suala la kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto katika nchi yetu linapewa kipaumbele cha juu katika shughuli za Serikali za kila siku” alisema Makamu wa Rais

  Tafiti zilizofanyika mwaka 2015/2016 zinaonyesha kuwa, kiwango cha vifo vitokanavyo na uzazi ni 556 kwa kila vizazi hai 100,000 ambayo ni sawa na vifo 11,000 kila mwaka ambayo ni sawa na wanawake 30 hufariki kila siku, kutokana na matatizo yatokanayo na uzazi na kwa uapnde wa watoto wachanga ni 25 kwa kila vizazi hai 1000 .

  Makamu wa Rais amesema jamii ina jukumu zito la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga kwa kuhakikisha kuwa inajiwekea mpango mahsusi wa rufaa wakati wa dharura na utambuzi wa dalili hatarishi kwa mama na mtoto mchanga.

  “Nitoe rai kwa wananchi, wanawake na wanaume na vijana kujitokeza kuchangia damu mara kwa mara kwa kuwa wakifanya hivi wanaokoa maisha ya mama mjamzito na watoto.” Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 80 ya damu salama inatumika kwa wakina mama wajawazito na watoto alisema Makamu wa Rais.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kampeni ya "Jiongeze Tuwavushe Salama" jijini Dodoma.wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya "Jiongeze Tuwavushe Salama" jijini Dodoma.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionesha taarifa inavyoonyesha hali halisi ilivyo sasa katika masuala yanayohusu uzazi salama wakati wa uzinduzi wa kampeni ya "Jiongeze Tuwavushe Salama" jijini Dodoma.
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya "Jiongeze Tuwavushe Salama" ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
   Sehemu ya Wageni kutoka Taasisi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kampeni ya "Jiongeze Tuwavushe Salama" ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.


  0 0

  Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB) imetoa matrekta 24 yenye thamani ya zaidi ya TZS 1.5 bilioni kwa Vyama vya Ushirika vya Msingi vya Masoko (AMCOS) 24 vinavyolima zao la pamba katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ili kuongeza tija na uzalishajji wa zao hilo.

  Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine amesema kuwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo inalenga katika kuwawezesha wakulima wa zao la pamba nchini ili waweze kuongeza tija na uzalishaji kama inavyobainishwa katika Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba nchini, Bw. Marco Mtunga amesema kuwa kupitia mkopo wa viua dudu uliotolewa msimu uliopita na TADB, ambapo uliwanufaisha zaidi ya wakulima laki sita wa zao la pamba ambapo uliwezesha kuongeza uzalishaji kufikia tani 221,600 ikiwa ni ongezeko la asilimia 67 ikilinganishwa na tani 133,000 zilizozalishwa msimu wa 2017/18.

  Bw. Mtunga ametoa wito kwa taasisi nyingine kushirikiana ili kuweza kuongeza tija katika uzalishaji wa pamba hapa nchini.

  Wakizungumza wakati wa makabdihiano hayo, baadhi ya wakulima walionufaika na matrekta hayo, waliishukuru serikali kupitia benki ya maendeleo ya kilimo kwa kuweza kuwakopesha matrekta hayo hali itakayochagiza tija na uzalishaji wa zao la pamba nchini.
   Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba (aliyevaa tai) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (katikati) wakikata utepe wakati wa kukabidhi matrekta 24 yaliyotolewa kwa vyama vya Ushirika vya Msingi na Masoko (AMCOS) za mikoa ya Kanda ya Ziwa. Matrekta hayo yenye thamani ya zaidi ya TZS 1.5 bilioni yaliyotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).
   Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kulia) akikabidhi ufunguo wa trekta kwa mmoja kati ya viongozi 24 wa vyama vya Ushirika vya Msingi na Masoko (AMCOS) za mikoa ya Kanda ya Ziwa waliokopeshwa matrekta yenye thamani ya zaidi ya TZS 1.5 bilioni yaliyotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB). Wanaoshuhudia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba (katikati) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Japhet Justine na baadhi ya viongozi wa AMCOS hizo.
   Pichani ni matrekta yenye thamani ya zaidi ya TZS 1.5 bilioni yaliyotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo kama mkopo kwa Chama cha Ushirika cha Msingi cha Masoko (AMCOS) 24 zinazolima pamba Kanda ya Ziwa. Mkopo huu umewezesha AMCOS hizo ‘kutupa‘ majembe ya mkono katika kilimo.

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango akiwasilisha Hotuba ya Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/2020 bungeni leo jijini Dodoma.


  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango akiwasilisha Hotuba ya Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/2020 bungeni leo jijini Dodoma.

  Na Jacquiline Mrisho

  Serikali imejipanga kuongeza kasi ya ukuaji wa Pato halisi la Taifa kufikia asilimia 7.3 mwaka 2019 ikiwa ni moja ya shabaha na malengo ya uchumi jumla.

  Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango wakati akiwasilisha Bungeni Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/20. Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Mwikabe Waitara (CCM), akila kiapo mbele ya Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai wakati wa kikao cha kwanza Bunge la 13 leo jijini Dodoma. Wabunge wanne wameapishwa baada ya kuchagulia kutokana na kuhama vyama vyao. Wabunge hao ni Julias Kallanga (Monduli – CCM), Mhe. Kuchauka (Liwale – CCM), pamoja na Thimotheo Mnsava ( Korogwe Vijijini –CCM) aliyechukua nafasi ya Stevene Ngonyani (Majimarefu aliyetangulia mbele za haki). Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimskiliza kwa makini Waziri wa Ardhi Nyumba na Maenddeleo ya Makzi, William Lukuvi (kushoto) wakati wa kikao cha kwanza cha Mkutano wa 13 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo jijini Dodoma.

  Waziri Dkt. Mpango amesema kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2018, Pato halisi la Taifa lilikua kwa asilimia 8.4 ikilinganishwa na asilimia 5.7 katika kipindi kama hicho mwaka 2017 ambapo shughuli za kiuchumi zilizokua kwa kiwango kikubwa ni ujenzi, habari na mawasiliano, usafirishaji na uhifadhi mizigo pamoja na kilimo.

  “Serikali yetu imejipanga kuongeza kasi ya ukuaji wa Pato Halisi la Taifa kufikia asilimia 7.3 kwa mwaka 2019 ikilinganishwa na matarajio ya asilimia 7.2 mwaka 2018 na kuongezeka kwa wastani wa asilimia 7.6 katika kipindi cha muda wa kati (2019/20 – 2021/22)”, alisema Dkt. Mpango.

  Dkt. Mpango ametaja shabaha na malengo mengine ya uchumi, yakiwemo ya kuendelea kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei na kuhakikisha kuwa unabaki kwenye wigo wa tarakimu moja ya wastani wa asilimia 5 katika kipindi cha muda wa kati pamoja na mapato ya kodi kufikia asilimia 12.7 ya Pato la Taifa mwaka 2019/20 kutoka matarajio ya asilimia 12.5 mwaka 2018/19. Kutoka kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga wakifuatilia kitabu cha Mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Mwaka 2019/2020 katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa 13 wa Bunge la Jamhuri la Muungano leo jijini Dodoma. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Khamis Kigwangallah (kushoto) wakati wa kikao cha kwanza cha Mkutano wa 13 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo jijini Dodoma. Katikati ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Janeth Massaburi. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde akijibu swali wakati wa kikao cha kwanza cha Mkutano wa 13 wa Bunge la Jamhuri la Muungano leo jijini Dodoma. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akifafanua jambo wakati wakati wa kikao cha kwanza cha Mkutano wa 13 wa Bunge la Jamhuri la Muungano leo jijini Dodoma. Kutoka kulia ni Waziri wa Mabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Joseph Kandege. Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akijibu swali wakati wa kikao cha kwanza cha Mkutano wa 13 wa Bunge la Jamhuri la Muungano leo jijini Dodoma. Baadhi ya wageni wakifuatili kikao cha kwanza cha Mkutano wa 13 wa Bunge leo jijini Dodoma.

  Vile vile, Serikali imejipanga kupunguza nakisi ya Bajeti kutoka matarajio ya asilimia 2.9 mwaka 2018/19 hadi wastani wa asilimia 1.1 katika kipindi cha muda wa kati pamoja na kuwa na akiba ya fedha za kigeni kwa kiwango cha kukidhi mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa kipindi kisichopungua miezi 4.5.

  Akiwasilisha hoja hiyo, Waziri Mpango amefafanua kuwa misingi iliyozingatiwa katika kuweka malengo ya uchumi jumla ni pamoja na uwepo wa amani, usalama, utulivu na umoja wa nchi na nchi jirani, kuimarika kwa viashiria vya uchumi jumla, kutengamaa kwa uchumi wa dunia, utulivu wa bei za mafuta katika soko la dunia na hali nzuri ya hewa.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, George Simbachawene amesema kuwa kuna baadhi ya miradi ya maendeleo ambayo iliainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2018/19 lakini haionekani katika mapendekezo ya Mpango wa Mwaka 2019/20 hivyo kamati imeshauri miradi hiyo ijumuishwe katika Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2019/20.

  Aidha ametoa rai kwa Serikali kuanza kutenga kiwango cha asilimia moja ya Pato la Taifa kwa ajili ya shughuli za utafiti na maendeleo.

  0 0

  NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

  KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) ndugu Humphrey Polepole amesema njia pekee ya CCM kulipa wema kwa wananchi ni viongozi wake kufanya kazi kwa bidii na ubunifu ili kuleta maendeleo endelevu nchini. 

  Amesema wananchi wamekiamini Chama na kukipa ridhaa ya kuongoza Serikali zote mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutokana na usimamizi na utekelezaji mzuri wa Sera zake kwa jamii. Rai hiyo aliitoa leo (jana) katika hafla ya kukabidhi mipira ya kusambazia maji safi na salama kwa wananchi wa Jimbo la Tunguu huko katika ukumbi wa T.C uliopo Dunga Wilaya ya Kati Unguja. 

  Akizungumza mara baada ya kukabidhi mipira hiyo kwa uongozi wa Jimbo la Tunguu kwa niaba ya wananchi, Ndugu Polepole amesifu juhudi za kuwatumikia wananchi zinazofanywa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo hilo.Polepole aliwataja viongozi hao ambao ni Mbunge wa Jimbo hilo Khalifa Salum Said na Mwakilishi wa Jimbo hilo Simai Mohamed Said kuwa wametoa mipira hiyo kwa lengo la kumaliza changamoto ya ukosefu wa huduma za maji. 

  Ndugu Polepole alisema Viongozi wa Chama na Serikali hasa Wabunge, Wawakilishi na Madiwani nchini wanatakiwa kuendeleza utamaduni wa kufanya kazi na kuwapelekea wananchi maendeleo na sio ahadi za uongo.Katibu huyo wa NEC,Polepole alifafanua kuwa maisha ya mwanadamu yeyote yanahitaji maji hivyo Kitendo cha kuwapelekea wananchi huduma hiyo ni kuharakisha maendeleo ya jimbo kwani wananchi watafanya shughuli za kujiingizia kipato kwa utulivu.

  Kupitia hafla hiyo, kiongozi huyo aliwataka viongozi wa majimbo mengine Zanzibar kuiga mfano huo wa kutatua kero za wananchi ili ifikapo mwaka 2020 CCM iwe imetekeleza ahadi zote zilizotolewa katika Uchaguzi Mkuu wa Dola uliopita. Katika maelezo yake Polepole,alitangaza rasmi kuwa kiongozi yeyote atakayeshindwa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 asitarajie kupewa tena nafasi ya uongozi kupitia Chama Cha Mapinduzi kwani anakuwa haitoshi kiutendaji. 

  Pia alisema suala la Serikali kufanya kazi kwa pamoja na Chama sio jambo la hiari bali ni lazima linalotakiwa kufuatwa na viongozi wa mamlaka hizo.Polepole alieleza kuwa CCM inaendeleza kuwa na mvuto kwa wananchi na mataifa mengine Duniani kutokana na kutawaliwa na dhana ya ukweli na uwajibikaji katika kutekeleza Sera zake. Polepole ameziagiza Halmashauri zote za Wilaya Zanzibar kuhakikisha zinatenga fedha ya mikopo isiyokuwa na riba kwa wanawake na vijana ili wajikwamue kiuchumi na kunufaika na matunda ya nchi yao. 

  "Wanawake na Vijana ni miongoni mwa walipa kodi hivyo kupewa mikopo ni moja ya fursa yanayostahiki kupata kwa lengo la kujikwamua kiuchumi",Alisema Polepole na kuongeza kuwa kila mwananchi ana haki ya kunufaika na matunda ya Zanzibar. Sambamba na hayo alisisitiza suala la maadili kwa viongozi, watendaji na wanachama wote wa CCM kwa lengo la kuendeleza misingi na Itikadi bora za kisasa ndani ya CCM. 

  Pamoja na hayo alitoa tahadhari kwa viongozi na wanachama wanaendeleza kampeni za kuwania Kiti cha Urais wa Zanzibar kuacha tabia hizo kwani bado nafasi hiyo ina mwenyewe ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.Akizungumzia namna CCM ilivyoimarika alisema taasisi hiyo inashinda kwa kishindo katika Chaguzi ndogo ndogo za Kata na Majimbo ya Tanzania bara, hatua inayoimarisha CCM na kudhoofisha upinzani.

  Aliwapongeza Marais wote akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kwa kutekeleza ipasavyo Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020.Kwa upande wake Mwakilishi wa Jimbo la Tungu ndugu Simai Mohamed Said,amesema ataendelea kuimarisha huduma mbali mbali za kijamii na kiuchumi ndani na maeneo jirani ya Jimbo hilo. Alisema anashirikiana vizuri na viongozi wengine wa Jimbo hilo ambao ni Mbunge, Madiwani na viongozi wa Kamati ya Siasa ya Jimbo kuhakikisha wananchi wananufaika na miradi mbali mbali ya maendeleo.

  Naye Mbunge wa Jimbo hilo ndugu Khalifa Salum Said, amesema viongozi hao wamejipanga kumaliza kero ya upungufu wa maji safi na salama katika Vijiji mbali mbali vilivyomo katika Jimbo la Tunguu. Mipira hiyo ya Maji Safi na Salama imegharimu kiasi cha shilingi milioni tano ambayo ni awamu ya tatu ya usambazaji wa miundombinu ya maji katika Jimbo hilo.
  KATIBU wa NEC, Idara ya Itkadi na Uenezi CCM Humprey Polepole akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM mara baada ya kukabidhi miundombinu hiyo ya kusambazia maji safi na salama katika vijiji vya Jimbo la Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
  KATIBU wa NEC, Idara ya Itkadi na Uenezi CCM Humprey Polepole akimkabidhi mipira ya kusambazia maji safi na salama Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Nd. Simai Mohamed Said kwa niaba ya wananchi wa Jimbo hilo.
  KATIBU wa NEC, Idara ya Itkadi na Uenezi CCM Humprey Polepole akifukia mipira ya maji safi na Salama katika Kijiji cha Bungi Jimbo la Tunguu.
  BAADHI ya wanachama na viongozi wa CCM wakimsikiliza nasaha za Katibu huyo Polepole mara baada ya kukabidhi mipira ya kusambaza maji iliyonunuliwa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu kwa ajili ya kutatua kero za wananchi.

older | 1 | .... | 1716 | 1717 | (Page 1718) | 1719 | 1720 | .... | 1897 | newer