Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1715 | 1716 | (Page 1717) | 1718 | 1719 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mnada wanne wa msimu wa uuzaji korosho 2018/2019 wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Mdimba Mkoani Mtwara jana tarehe 2 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
  Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mnada wanne wa msimu wa uuzaji korosho 2018/2019 wakimsikiliza kwa makini waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza katika kijiji na kata ya Mdimba Mkoani Mtwara jana tarehe 2 Novemba 2018.
  Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mnada wanne wa msimu wa uuzaji korosho 2018/2019 wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Mdimba Mkoani Mtwara jana tarehe 2 Novemba 2018.
  Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mnada wanne wa msimu wa uuzaji korosho 2018/2019 wakimsikiliza kwa makini waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza katika kijiji na kata ya Mdimba Mkoani Mtwara jana tarehe 2 Novemba 2018.

  Na Mathias Canal-WK, Mtwara

  Wakulima wa zao la korosho wa Wilaya ya Tandahimba na Masasi wamekubali kuuza korosho zao mbele ya Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) kutokana na kuridhia na kukubaliana na maamuzi ya serikali.

  Hayo yamejili katika mnada wa nne wa msimu wa uuzaji korosho 2018/2019 uliojumuisha kampuni za ununuzi 11 katika maghala tofauti uliofanyika katika kijiji na kata ya Mdimba Mkoani Mtwara.

  Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Mdimba, Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba alisema kuwa bei ya zao la korosho imeonyesha mwelekeo wa kushuka katika mwaka 2018/2019 tofauti na hali ilivyokuwa katika msimu wa mwaka 2017/2018 ambapo bei ya zao hilo ilifikia shilindi 4,128

  Katika mkutano huo wakulima wa korosho walikubali mbele ya waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Tizeba kuanza kuuza korosho zao kwa bei ya juu ya shilingi 3,016 huku bei ya chini ikiwa ni shilingi 3000.

  “Wafanyabiashara wasipangiwe muda wa kuchukua korosho ghalani kwa ajili ya usafirishaji na wasipangiwe kutumia bandari gani, wawe huru kulingana na maagizo yaliyotolewa na Rais Magufuli’’

  “Nitashangaa sana kuona mnunuzi mwenye akili timamu akitoa barua na kutaka kuuziwa korosho chini ya shilingi 3,000 au akitaka kwa shilingi 2,500” Alikaririwa Dkt Tizeba

  Kufuatia hali hiyo tarehe 26 Octoba 2018 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa alitangaza maamuzi ya serikali kusimamisha minada yote hadi suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi.

  Kufuatia uamuzi huo tarehe 28 Octoba 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli alikutano na wanunuzi wa zao la korosho katika mkutano uliokuwa ukiendelea kati ya wanunuzi hao na Waziri Mkuu na kutoa msimamo wa serikali kuhusu zao hilo kufuatia kuwepo kwa mvutano wa bei ya zao hilo kati ya wanunuzi na wakulima.

  Katika mnada huo wa nne uliohudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa, Waziri wa kilimo Dkt Tizeba alisema kuwa matokeo ya mnada huo hayakuwa mabaya ukilinganisha na minada iliyopita katika msimu huu wa 2018/2019 ambapo bei ilishuka.

  Alisema baada ya Rais Magufuli kutangaza msimamo wa serikali kuwa bei ya kiwango cha chini ya mnadani katika msimu wa 2018/2019 kuwa shilingi 3000 kwa kilo moja ya korosho, wafanyabiashara wameitikia wito kwa kuweka bei nzuri mnadani.

  Aidha, Waziri wa kilimo alisema kuwa katika vikao vingi vya serikali vilivyotuama kujadili mwenendo wa zao hilo kwa mujibu wa kifungu cha 8 cha sheria ya Tasnia ya Korosho Na 18 ya mwaka 2018 ameielekeza Bodi ya korosho kupata kibali cha waziri wa kilimo na waziri mkuu kabla ya kuyafanyia maamuzi.

  Alisisitiza kuwa mnunuzi akishalipa ushuru katika Halmashauri moja hapaswi kudaiwa kulipa ushuru huo katika Halmashauri nyingine, Bodi kutotoa bei elekezi, Tozo ya Bodi ya korosho ambayo iliongezwa kwa msimu wa mwaka 2018/2019 kufikia shilingi 17 kwa kilo irudi shilingi 10 kwa kilo kama ilivyotozwa msimu wa 2017/2018

  Wanunuzi wa korosho wana hiari ya kusafirisha korosho kwenda nje ya nchi kupitia bandari ya mtwara, Dar es salaam au Tanga huku wanunuzi wakiruhusiwa kwenda na magunia yao kununua korosho ya wakulima, Bodi ya korosho kuangalia utaratibu wa wabanguaji wadogo kupata/kununua korosho katika mfumo wa mnada, sambamba na dhamana ya mnada (Bill Security) kupungua.

  Dkt Tizeba alisema kuwa baada ya maelekezo ya serikali kuhusu mwenendo wa zao la Korosho katika hatua ya kwanza ya utekelezaji Wizara yake ilianza kutathmini kuhusu mfumo mzima wa uuzaji wa korosho hatimaye kufikia uamuzi huo.

  Aliwasisitiza wakulima kutokata tamaa na minada kwani ni kawaida kwa bei za mazao kupanda na kushuka kulingana na uzalishaji katika nchi zingine pamoja na soko la Dunia.


  0 0  *Ni baada ya kuhakikishiwa kipande Dar-Morogoro kitakamilika Aprili 2019 badala ya Julai

  WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na kasi na viwango vya ujenzi wa mfumo wa reli ya kisasa (SGR) inayojengwa na kampuni ya Yapi Merkezi.

  Amesema kipande cha kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro chenye urefu wa km. 300 ambacho kilitakiwa kukamilika Julai 2019, wataalamu wamesema watakamilisha Aprili 2019.Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Novemba 3, 2018) alipotembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kuanzia eneo la Shaurimoyo Dar esSalaam hadi Soga, Pwani.

  “Nimeridhishwa na viwango na maendeleo ya ujenzi kwa sehemu ulivyofikia pamoja na ushiriki wa Watanzania wengi katika mradi huu, tunataka muendelee kujenga kwa kasi hii.”Waziri Mkuu amesema Serikali inataka kuona malengo ya Rais Dkt. John Magufuli ya kutaka kuona SGR inakamilika na kuanza kutumika nchini yanatimia.

  Kuhusu suala la ajira, Waziri Mkuu amesema amefarijika kusikia asilimia 96 ya watu walioajiriwa katika mradi huo ni Watanzania, amewataka wawe mabalozi wazuri.“Watanzania mnaofanya kazi katika mradi huu hakikisheni mnawajibika kwa kufanyakazi kwa bidii, uaminifu na muwe mabalozi wazuri ili wengine waweze wapate ajira.”

  Awali,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa alisema awamu ya kwanza ya mradi huo wa reli kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora unagharimu sh. trilioni 7.1.Alisema mradi wa ujenzi wa reli hiyo yenye urefu wa km 1,219 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza umegawanyika katika vipande vitano, kipande cha kwanza ni kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro chenye urefu km 300 na kitagharimu sh. trilioni 2.7.

  “Kipande kingine ni kutoka Morogoro hadi Makutupora chenye urefu wa km. 422 ambacho kitagharimu sh. trilioni 4.4, Makutupora hadi Tabora km. 376.5, Tabora hadi Isaka km 162.5 na Isaka hadi Mwanza km. 311.25.”Mkurugenzi huyo alisema kukamilika kwa reli hiyo ya kisasa kutachochea mipango ya Serikali katika kutekeleza sera ya viwanda na kulifikisha Taifa kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

  Pia reli hiyo itachochea mapinduzi ya kiuchumi kwa kanda nzima ya Afrika Mashariki na Kati hususan kwa nchi zisizopakana na bahari kwani watasafirisha mizigo yao kwa haraka na uhakika.Akizungumzia mradi huo kwa ujumla, Kadogosa alisema maendeleo ya mradi huo ni asilimia 32 kwa kipande cha Dar es Salaam-Morogoro na asilimia 3. 31 kwa kipande cha Morogoro-Makutupora.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMAMOSI, NOVEMBA 3, 2018.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la reli Tanzania  (TRC), Masanja Kadogosa kuhusu ujenzi wa Reli ya SGR wakati alipotembelea kambi ya Kampuni ya Yapi Markezi inayojenga Reli hiyo,  katika eneo la Shaurimoyo jijini Dar es salaam, Novemba 3, 3018
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikagua maandalizi ya  ujenzi wa madaraja  ya  kupitisha treni  juu  wakati alipotembelea kambi ya Kampuni ya Yapi Merkezi inayojenga reli ya Kisasa ya SGR   Oktoba 3, 2018. Kambi hiyo ipo eneo la Shaurimoyo jijini Dar es salaam. Wapili kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kazi ya utengenezaji mataluma ya reli ya SGR wakati alipotembelea Kambi ya Kampuni ya Yapi Merkezi katika eneo la Soga mkoani Pwani, Oktoba 3, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua utandikaji wa  reli ya SGR katika eneo la Soga mkoani Pwani, Oktoba 3, 2018.  Wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua utandikaji wa  Reli ya SGR katika eneo la Soga mkoani Pwani, Oktoba 3, 2018.   Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe. 
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua utandikaji wa  Reli ya kisasa ya  SGR katika eneo la Soga mkoani Pwani, Oktoba 3, 2018.   Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isack Kamwelwe na kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkurugenzi Mkuu wa Shiraki la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na  wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Yapi Merkezi inayojenga reli ya kisasa ya SGR kati ya Dar es slaam na Morogoro baada ya kukagua ujenzi wa reli hiyo katika eneo la Soga mkoani Pwani,  Oktoba 3, 2018.  Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tamasha la Mvinyo lililofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali pamoja na wadhamini wa Tamasha la Mvinyo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Peter Mavunde  akizungumza na Waziri Wakuu wa Staafu Mhe. Peter Mizengo Pinda (katikati) na John Samuel Malecela (kulia) wakati wa halfa ya uzinduzi wa Tamasha la Mvinyo lililofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suuhu  Hassan akipata maelezo ya umuhimu wa zabibu ya Dodoma katika uzalishaji  mvinyo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Alkovintages Bw. Archard Kato (kulia)  wakati wa hafla ya uzinduzi wa tamasha la mvinyo Dodoma.
  (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


   akamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suuhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Mvinyo kwenye viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suuhu Hassan akimkabidhi zawadi ya picha Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni kwa mchango wa nchi yake katika kusaidia kilimo cha zabibu wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Mvinyo kwenye viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suuhu  Hassan akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wake katika sekta ya mvinyo na zao la zabibu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Alkovintages Bw. Archard Kato wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Mvinyo kwenye viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suuhu  Hassan akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wake katika sekta ya mvinyo na zao la zabibu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Dane Dane Holdings Mhandisi Danford Semwenda wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Mvinyo kwenye viwanja vya Mashujaa jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


  0 0

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa leo Novemba 3, 2018, amefunga wiki ya maonesho ya viwanda Kibaha, Mkoani POwani, yaliyokuwa yakifanyika kwenye viwanja vya CCM-Sabasaba, eneo la Picha ya Ndege.

  Moanesho hayo yaliyofunguliwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Oktoba 29, 2018, yalilenga kuwakutanisha wazalishaji bidhaa za wviwanda na wanunuzi (masoko), ambapo pia taasisi za serikali zinazohusika na utoaji huduma mbalimbali zilishiriki pia.

  Miongoni mwa taasisi hizo, ni Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi WCF, ambao kazi yake kubwa ni kutoa Fidia kwa wafanyaklazi walioumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi.Moja ya ujumbe mkubwa alioutoa siku anafungua maonesho hayo kwa waajiri kote nchini, Makamu wa Rais aliuagiza

  uongozi wa (WCF), kuendelea kuwafuatilia waajiri ambao bado hawajajisajili ili waweze kufanya hivyo.Makamu wa Rais alitoa wito huo leo Oktoba 29, 2018 alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya viwanda Mkoa wa Pwani kwenye viwanja vya CCM-Sabasaba, Picha ya Ndege Mkoani humo.

  Alisema viwanda vimeongezeka nchini na kwamba huduma za WCF zitahitajika sana kwa wakati huu na hivyo kuutaka uongozi wa Mfuko, kuhakikisha unaendelea na ufuatiliaji kwa waajiri wa zamani na wapya ambao bado hawajajisajili na kuwasilisha michango kwenye Mfuko watekeleze takwa hilo la kisheria ili mfanyakazi anapoumia aweze kupata haki yake ya fidia.

  “Waajiri wao muwabane wajisajili na mfuko na waweze kuwasilisha michango ili Mfuko uendelee kuwa na uwezo wa kulipa fidia, pale watoto wetu (wafanyakazi) wanapokatika vidole au kuumia waweze kupata haki zao.” Alisisitiza.

  Katika hatua ya kuimarisha Hifadhi ya Jamii, Tanzania, Serikali ilianzisha Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi kwa mujibu wa kifungu namba 5 cha sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, kipengele cha 263 kilichofanyiwa marejeo mwaka 2015 ili kuhakikisha kila mfanyakazi Tanzania Bara kutoka sekta ya umma na binafsi anapata fursa ya kuwekewa bima na mwajiri wake ili anapopata majeraha au magonjwa awapo kazini basi aweze kufidiwa kwa mujibu wa sharia. 

  WIZARA, MIKOA ONDOENI VIKWAZO UJENZI WA VIWANDA-MAJALIWA

  NA OWM, PWANI 
  WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka Wizara zinazohusika na masuala ya viwanda, Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na sekta binafsi watambue na waondoe vikwazo na urasimu dhidi ya ujenzi na ustawi wa viwanda nchini. 


  Pia, Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage ampelekee taarifa ya hatua iliyofikiwa juu ya kampuni ya Budget Motors walioomba kibali cha kutengeneza na kuunganisha bodi za mabasi tangu mwaka jana na hawajajibiwa. 


  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Novemba 3, 2018) wakati akifunga wiki ya maonesho ya viwanda yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Sabasaba katika kata ya Picha ya Ndege, Kibaha mkoani Pwani. Amesena uwepo wa viwanda nchini unatoa ajira nyingi. 

  “Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeamua kujenga uchumi wa viwanda utakaokuwa mhimili mkuu wa maendeleo ya Taifa na wananchi, hivyo itaendelea kutoa ushirikiano ili kuhakikisha ajenda ya ujenzi wa viwanda inafanikiwa.” 

  Amesema katika kupunguza vikwazo na kuboresha sera nchini, Rais Dkt. Magufuli ameweka msukumo wa kutosha ili kurahisisha na kuondoa ukiritimba kwenye shughuli zote za kibiashara, lakini pia katika kuboresha sera za Taifa za kodi ili kulinda viwanda vya ndani 

  Waziri Mkuu amesema umuhimu wa viwanda umetokana na Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015/2020 ambayo inaielekeza Serikali kuweka nguvu katika ujenzi wa viwanda ili kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025. 

  Amesema kwa msingi huo, Rais Dkt. Magufuli alitoa msukumo wa sekta binafsi nchini kuanzisha viwanda vinavyotumia malighafi zinazozalishwa nchini kutokana na mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na maliasili, vikiwemo viwanda vya nguo, sabuni, korosho na matunda. 

  Waziri Mkuu ameongeza kuwa uwepo wa viwanda nchini utasaidia kuongeza wigo wa mapato ya Serikali kupitia kodi na tozo mbalimbali. “Huu ndio mwelekeo wa Serikali ya awamu ya tano unaolenga kuifikisha nchi kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.” 

  Kuhusu suala la kampuni ya Budget Motors, Wiziri Mkuu amesema ifikapo Ijimaa (Novemba 9, 2018) Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji awasilishe taarifa kuhusu suala hilo la kibali. “Huu ni urasimu, ni bora apewe atengeneze na akikosea arekebishwe.” 

  Kampuni ya Budget Motors inadai kuwa iliomba kibali cha kuwa na uthibitisho wa kutengeneza na kuunganisha bodi za mabasi kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS), kwa takribani mwaka mmoja bila ya kujibiwa. Walitoa malalamiko hayo kwa Waziri Mkuu alipotembelea banda lao. 

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametoa rai kwa taasisi zenye miradi mbalimbali nchini pamoja na wananchi kuthamini na kuzitumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini zikiwemo na za viwanda vya mkoa wa Pwani kwani zina viwango vya ubora. 

  “Wakati natembelea mabanda kwenye maonesho haya nimeshuhudia bidhaa nyingi nzuri na zenye ubora. Nimeona wazalishaji wa saruji, mabati, nondo, marumaru, mabomba ya plastiki, chuma, zana za kilimo, vyakula, vinywaji na vifungashio.” 

  Waziri Mkuu amesema kupitia maonesho hayo ya viwanda vilivyopo katika mkoa wa Pwani vimeudhihirishia umma kuwa vina uwezo mkubwa wa kuzalisha bidhaa zilizo bora na hata kuzidi zile zinazoingizwa kutoka nje, amewahamasisha wananchi kutumia bidhaa za ndani. 

  Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo ameiagiza mikoa yote nchini kuhakikisha inatumia bidhaa zinatengenezwa na viwanda vya ndani katika miradi mbalimbali ya ujenzi wanayoitekeleza kama ujenzi wa hospitali za wilaya na vituo vya afya. 

  Amesema Wakuu wa Mikoa ni lazima wahakikishe bidhaa kama saruji, nondo, marumaru, mabati zinavyotumika katika ujenzi ziwe vimezalishwa na viwanda vya ndani kwa sababu vina viwango vya ubora unaotakiwa na pia itasaidia kuondoa tatizo la soko la bidhaa hizo. 

  Naye,Waziri Mwijage amewataka watendaji wanaohusika na masuala ya viwanda kutoweka vikwazo kwa wawekezaji ambao wanakwenda katika ofisi zao kwa ajili ya kutafuta maeneo ya kuwekeza kwenye viwanda au wanaohitaji vibali kwani jambo hilo halina tija. 
  Mkurugenzi wa Uendeshaji, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Anselim Peter, (kushoto), akitoa elimu kuhusu kazi za Mfuko huo kwa baadhi ya watumishi wa umma na binafsi waliotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonesho hayo leo Bovemba 3, 2018 
  Mkurugenzi wa Uendeshaji, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Anselim Peter, (kushoto), akitoa elimu kuhusu kazi za Mfuko huo kwa baadhi ya watumishi wa umma na binafsi waliotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonesho hayo leo Bovemba 3, 2018 
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bi. Laura Kunenge, (kulia), akitoa maelezo kuhusu kazi za Mfuko kwa wanafunzi hawa wa kidato cha sita na pili, Shule ya Sekondari Kibaha walipotembelea banda la Mfuko huo leo Novemba 3, 2018. 
  Mkurugenzi wa Uendeshaji, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Anselim Peter(kulia), akimsikilzia mwananchi huyo aliyetembelea banda la Mfuko aliyetaka kujua kazi za Mfuko huo. 

  Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akiungana na vijana wa bendi ya muziki wa dansi ya kambi ya JKT-Ruvu walipotumbuiza wakati wa hafla hiyo ya ufungaji maonesho ya viwanda Kibaha leo Novemba 3, 2018. 
  Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akiungana na vijana wa bendi ya muziki wa dansi ya kambi ya JKT-Ruvu walipotumbuiza wakati wa hafla hiyo ya ufungaji maonesho ya viwanda Kibaha leo Novemba 3, 2018. 
  Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, (kushoto), akimkabidhi cheti cha shukrani Kaimu Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Semu Mwakyanjala mwishoni mwa maonesho hayo leo Novemba 3, 2018. 
  Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Mawaziri na viongozi wengine wa juu serikalini, wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na wawakilishi wa taasisi za umma na binafsi waliowezesha kufanyika kwa maonesho hayo. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Bibi Florence Max Mambali wakati alipotembelea banda la Kampuni ya kufuga kuku na kuzalisha vifaranga vya kuku ya Mkuza Chicks katika Maonesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba uliopo katika eneo la Picha ya Ndege, Kibaha, Oktoba 3, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  Waziri wa Nishati, Dk.Medard Kalemani, (katikati) akipita katika mitaa ya kijiji cha Nsalaga kukagua Miundombinu ya usambazaji wa huduma ya Umeme, unaotekelezwa na Shirika la Umeme, nchini (Tanesco) ambapo ametoa siku 14,kwa wananchi hao kuunganishwa na huduma hiyo.
  Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani (katikati mwenye kipaza sauti) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Iduda, ambao bado hawajaungwanishwa na huduma ya Umeme Licha ya miundombinu kuwafikia.
  Waziri wa Nishati, Medard Kalemani akikagua miundombinu ya kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mwakibete, Jijini Mbeya na kuagiza mafundi na wahandisi katika Vituo vyote nchini kufanya ukaguzi wa kila siku kuepusha kukatika Umeme kutokana na hitilafu zinazojitokeza katika Vituo hivyo.
  Mafundo na wahandisi wakiendelea na Kazi za ukarabati wa machine na mitambo katika kituo cha kupoza na kusambaza Umeme cha Mwakibete jijini Mbeya.


  Na Zuena Msuya, Mbeya

  Mameneja wote wanaosimamia vituo vya kupoza na kusambaza umeme nchini wametakiwa kufanya ukaguzi ( checkup) wa kila siku asubuhi katika mitambo na mashine zilizopo katika vituo hivyo kuondoa adha ya kukatika umeme kutokana na hitilafu au uharibifu katika vituo hivyo.

  Licha ya kuwa vituo hivyo vinafanyiwa ukarabati na ukaguzi wa kila mara au hata baada ya miezi kulingana na utaratibu waliojiwekea.

  Hayo yameleezwa na Waziri wa Nishati ,Dkt. Medard Kalemani , wakati wa ziara yake ya kikazi katika Jiji la Mbeya, baada ya kutembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Mwakibete na kukagua miradi ya kusambaza umeme katika kijiji cha Nsalaga na Iduda inayotekelezwa na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO).

  Alieleza kuwa kumekuwa na changamoto ya kukatika umeme kwa muda mchache katika baadhi ya maeneo na sababu kuu ya ikielezwa kuwa ni hitilafu katika vituo au kuharibika kwa kifaa katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme.

  Alifafanua kuwa changamoto hiyo inaepukika na kutoweka kabisa endapo wahandisi na mafundi watakuwa na tabia ya kufanya uchunguzi wa mitambo na mashine zao kila siku asubuhi kubaini tatizo kabla ya kutokea.

  “ Mafundi na wahandisi muwe na tabia ya kufanya ukaguzi na matengenezo ya kila siku asubuhi badala ya kusubiri tatizo litokee, achene kufanya kufanya ukaguzi na matengenezo kwa mazoea, hii itasaidia kufahamu mapema tatizo linazoweza kutokea baadaye na kuondoa usumbufu wa kukatika umeme kwa wananchi hali ya kuwa kuna umeme mwingi nawa kutosha”, alisisitiza Kalemani.

  Alifafanua kuwa kwa sasa serikali haitaki kuona mtu yeyote anakosa huduma ya umeme kwa muda Fulani kwa sababu tu kumetokea ya hitilafu katika mitambo na mashine katika vituo vya kupoza na kusambaza umeme, badala yake inataka umeme upatikane saa 24 na siku saba kwa wiki kwa kuwa umeme upo wa kutosha na ziada.

  Aidha alisisitiza kuwa , pia Serikali haitaki kuona mwananchi wake anaingia gharama ya kutumia jenereta kwakuwa nchi inazalisha umeme mwingi, pia inataka kuondokana na matumizi ya majenereta kwa kuimarisha njia ya usafirishaji, usambazaji pamoja na uzalishaji wa umeme nchini

  “Mpango wa serikali ni kuachana na matumizi ya magenereta kwa watu wote, wakiwemo wafanyabiashara, Makampuni, Mashirika na pia kuwapunguza gharama za maisha na kurahisisha utendaji wa kazi kuwa na umeme mwingi, wakutosha na ziada”, alisema Kalemani.

  Hata hivyo alisema kuwa ni lazima katika kila kituo cha kupooza na kusambaza umeme kiwe na stoo ya kuhifadhi vifaa vya dharura vitakavyotumika endapo ikatokea kifaa kimeharibika au kupata hitilafu.

  Alisisitiza stoo hizo ni lazima ziwe na vifaa vizima na vya kutosha wakati wote, badala ya vifaa hivyo kuhifadhiwa katika ofisi za mameneja wa kanda au mikoa, hivyo kuleta usumbufu pindi tatizo linapotokea.

  Akizungumzia huduma ya umeme wa viwandani, Dk. Kalemani alisema kuwa viwanda vikubwa vipewe umeme wa peke yao wa kutosha na uhakika ili wazalishe kwa wingi waweze kulipa kodi za na kuiingizia nchi mapato.

  Alisema kwa kufanya hivyo kutaweza kuwabana wenye viwanda waokwepa kulipa kodi kwa kisingizo cha kutozalisha kutokana na kukosa huduma ya umeme.

  Hivyo ametoa siku 10, kwa Tanesco, kufunga huduma ya umeme wa peke yake kwenye kiwanda cha kuzalisha saruji cha Mbeya, ili kiweze kuajiri watu na wengi zaidi, kuzalisha kwa wingi na kulipa kodi za serikali.

  Katika hatua nyingine ametoa siku 14, kwa Tanesco kuhakikisha kuwa wanawaunganisha huduma ya umeme wakazi wa Kijiji cha Nsalaga na Iduda waliokidhi vigezo vya kupata huduma hiyo.

  Alitolea ufafanuzi kuwa wananchi hao waunganishiwe huduma hiyo kwa gharama ya shilingi 27,000 tu, tofauti na gharama za Tanesco kwa kuwa vijiji hivyo vipo pembezoni mwa jiji la Mbeya, hali ya kuwa vinaoneka vipo mjini.

  Akizungumzia kituo cha kuzalisha umeme cha jijini mbeya, Dk.Kalemani alisema ,kituo hicho kinauwezo wa kuzalisha megawati 130, ambapo mahitaji ya Mkoa mzima wa Mbeya, Songe pamoja na Makete ni Megawati 52, hivyo kunaziada ya megawati 78, hivyo wananchi wachamkie fursa ya kuunganishwa na huduma ya umeme.

  0 0


  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akionyesha moja ya nyumba ya askari wa Gereza la Mbigiri, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro, ambayo inahitaji matengenezo. Lugolo alifanya ziara ya kushtukiza katika Gereza hilo la Kilimo kwa lengo la kupata kero na kuimarisha uzalishaji wa kilimo na ufugaji. Kulia ni askari wa Gereza hilo, Sajenti Lubimbi Sayi. Lugola alifanya kikao na askari na Maafisa wa Gereza hilo na kuwataka kumpa kero zao bila kuwa na woga na hakuna atakaye wanyanyasa.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akimsikikiliza Mkuu wa Gereza la Mbigiri, Mvomero, Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Magereza, (ACP) Shija Fungwe (kulia) alipokua anatoa taarifa ya utendaji kazi wa Gereza hilo la Kilimo. Lugola alifanya ziara ya kushtukiza katika Gereza hilo kwa lengo la kupata kero na kuimarisha uzalishaji wa kilimo na ufugaji. Lugola pia alifanya kikao na askari na Maafisa wa Gereza hilo na kuwataka kumpa kero zao bila kuwa na woga na hakuna atakaye wanyanyasa.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na askari na Maafisa wa Magereza wa Gereza la Kilimo la Mbigiri lililopo Mvomero, Mkoani wa Morogoro, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika Gereza hilo kwa lengo la kupata kero na kuimarisha uzalishaji wa kilimo na ufugaji. Kushoto kwa Waziri huyo ni Mkuu wa Gereza hilo, Kamishna Msaidizi wa Magereza, (ACP) Shija Fungwe. Lugola aliwataka na askari na Maafisa hao kusema kero zao bila kuwa na woga na hakuna atakaye wanyanyasa.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akichungulia ndani moja ya nyumba ya askari wa Gereza la Mbigiri ambayo inahitaji matengenezo, wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kushtukiza katika Gereza hilo kwa lengo la kupokea kero na kuimarisha uzalishaji wa kilimo na ufugaji. Kushoto ni Mkuu wa Gereza hilo, Kamishna Msaidizi wa Magereza, (ACP) Shija Fungwe. Lugola pia alifanya kikao na askari na Maafisa wa Gereza hilo na kuwataka kumpa kero zao bila kuwa na woga na hakuna atakaye wanyanyasa. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  Na Felix Mwagara, MOHA-Morogoro

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amewataka askari pamoja na watumishi mbalimbali waliopo ndani ya Wizara yake wawe huru kuuliza maswali, kusema kero zao zinazowakabili katika vikao vyake na hakuna kiongozi yeyote atakaye wanyanyasa baada ya yeye kuondoka.

  Waziri Lugola amesema hayo baada ya kuona baadhi ya watumishi katika ziara mbalimbali anazozifanya nchini, wanakua na woga wa kusema kero zao wakihofia watapata matatizo baada ya yeye kumaliza kikao. , wakati anapata mambo mengi ambayo yanamsaidia kutatua kero za watumishi wake licha ya kuwa baadhi ya watumishi wanakua na woga wa kusema matatizo yanayowakabili.

  Akizungumza katika kikao na askari na Maafisa wa Jeshi la Magereza wa Gereza la Kilimo la Mbigiri, liliopo Wami-Dakawa wilayani Mvomero mkoani Morogoro, jana, Lugola alisema ili aboreshe utendaji kazi wa Wizara na Idara zake, anahitaji kujua matatizo mbalimbali ya watumishi wake, hivyo katika kikao chake ruksa watumishi kuuliza maswali kwasababu kupitia maswali hayo yanamsaidia sana kutatua kero zao.

  “Mimi ndio Waziri wenu, ulizeni swali lolote, toeni kero zenu na hakuna wakuwafuatilia baada ya kikao hiki, hiki ni kikao cha Waziri wenu mmepata nafasi hii ulizeni, niambieni matatizo yenu yanayowakabili ili tuyafanyie kazi,” alisema Lugola. Pia aliwaambia watumishi hao endapo watapata matatizo baada ya kusema kero zao katika kikao chake, wawe huru kumuambia japo anaamini hakuna chochote kitakacho wakuta maana kikao chake ambacho ni huru.

  Lugola aliyasema hayo baada ya baadhi ya askari wa Gereza hilo kuwa na hofu wakati walipokua wanauliza maswali ambapo mmoja wao akitoa kero yake huku akitahadharisha kuwa Waziri huyo amlinde endapo atapata matatizo mara baada ya kikao hicho kumalizika. “Hivi huwa mnakua karibu na viongozi wenu? Kwa mfano unakuta ukaribu huu wa kukaa hapa kwa kumkaribia Mkuu wa Gereza katika kikao hiki ni wa leo tu kwasababu nipo, lakini baada ya kikao hiki unakuta Mkuu wa Gereza au kiongozi yeyote mkubwa katika Jeshi hafikiwi na askari, hii haiwezekani kuweni karibu na viongozi wenu, waambieni kero zenu na pia nyie viongozi msiwatishe hawa askari wenu, sikilizeni kero zao,” alisema Lugola.

  Hata hivyo, Lugola aliutaka uongozi wa Gereza hilo kuacha malalamiko na badala kutafuta majibu ya changamoto zinazowakabili na pia wahakikishe wanasimamia nidhamu kwa askari na kutooneana, na pia waendelee kutumia vitendea kazi vilivyopo katika Gereza hilo ili waweze kuongeza uzalishaji katika shughuli mbalimbali za kilimo. Kwa upande wake Mkuu wa Gereza hilo, Kamishna Msaidizi wa Jeshi hilo, (ACP) Shija Fungwe, alimshukuru Waziri Lugola kwa kufanya ziara katika Gereza lake, na pia maagizo yake aliyoyatoa watayafanyia kazi likiwemo la kuongeza uzalishaji kupitia vitendea kazi walivyonavyo na pia yeye pamoja na askari na Maafisa mbalimbali wa Gereza hilo aliweka wazi kuwa wanaishi vizuri, kwa ushirikiano na pia wapo huru kuzungumza naye kuhusu jambo lolote la utendaji kazi.

  “Tunakushukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa kufanya ziara katika Gereza letu, tunakuahidi kufanyia kazi maagizo yako uliotupa na pia tutaendelea kutumia vitendea kazi tulivyonavyo ili tuzidi kuboresha, pamoja na kuimarisha uzalishaji wa Gereza hili,” alisema ACP Fungwe. Waziri Lugola alifanya ziara ya kushtukiza katika Gereza hilo ambalo linafanya shughuli za kilimo ya mazao mbalimbali pamoja na ufugaji wa ng’ombe, kondoo, mbuzi na kuku ambapo kwa ujumla wana mifugo zaidi ya 1000.

  0 0

  Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano wa 14 wa wadau wa sekta ndogo ya Pamba katika mkutano ulifanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu Jijini Mwanza, leo jumapili tarehe 4 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
  Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Shinya Mhe Zainabu Telack, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe Agrey Mwanri wakifatilia mkutano wa 14 wa wadau wa sekta ndogo ya Pamba kwenye ukumbi wa Benki Kuu Jijini Mwanza, leo jumapili tarehe 4 Novemba 2018.
  Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza wakati akifungua mkutano wa 14 wa wadau wa sekta ndogo ya Pamba katika mkutano ulifanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu Jijini Mwanza, leo jumapili tarehe 4 Novemba 2018. 
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya kilimo (TADB) Ndg Japhet Justine akifuatilia mkutano wa 14 wa wadau wa sekta ndogo ya Pamba katika mkutano ulifanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu Jijini Mwanza, leo jumapili tarehe 4 Novemba 2018.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba Dkt Joel Kabisa akizungumza wakati wa mkutano wa 14 wa wadau wa sekta ndogo ya Pamba katika mkutano ulifanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu Jijini Mwanza, leo jumapili tarehe 4 Novemba 2018.
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akifuatilia mkutano wa 14 wa wadau wa sekta ndogo ya Pamba katika mkutano ulifanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu Jijini Mwanza, leo jumapili tarehe 4 Novemba 2018.


  Na Mathias Canal-WK, Mwanza

  Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) amewapongeza wakuu wa mikoa yote nchini inayozalisha pamba, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kwa usimamizi bora uliopelekea uzalishaji wa zao hilo kuwa maradufu katika msimu wa ununuzi wa mwaka 2018/2019.

  Dkt Tizeba ametoa pongezi hizo leo jumapili tarehe 4 Novemba 2018 wakati akifungua mkutano wa 14 wa wadau wa sekta ndogo ya Pamba katika mkutano ulifanyika katika ukumbi wa Benki Kuu Jijini Mwanza na kusema kuwa Uzalishaji wa pamba katika msimu wa ununuzi wa mwaka 2018/19 umeongezeka kwa asilimia 67 kutoka tani 133,000 hadi tani 221,600. 

  Pamoja na pongezi hizo waziri huyo amewataka viongozi hao kuongeza ufanisi wa usimamizi wa zao hilo kwani pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji lakini bado matarajio ya uzalishaji hayakufikiwa kwa mujibu wa makubaliano.

  Alizitaja sababu zilizopunguza uzalishaji kuwa ni pamoja na Ukame mkali kati ya mwezi Januari na Februari ulipukutisha vitumba vichanga; Mripuko wa wadudu wakiwemo viwavi jeshi vamizi, vidung’ata, chawa jani, vithiripi, vidukari. Wadudu wanaofyonza miaka ya nyuma halikuwa tatizo kwenye pamba; Mvua kubwa kupita kiasi kati ya Machi na Mei ilizamisha pamba kwenye maeneo yote ya mbuga na mabondeni; sambamba na Ufahamu mdogo wa wakulima kuhusu matumizi ya viuadudu. 

  Alisema, mfumo wa kuzalisha mbegu bora za pamba umefufuliwa na unafanya kazi. Mbegu mama (Breeder seed) inazalishwa katika Taasisi ya Utafiti ya Ukiriguru na inakwenda kupandwa katika shamba la Nkanziga lililopo Wilayani Misungwi ili kuzalisha (Prebasic seed)

  Mbegu hiyo inakwenda kupandwa katika Kata ya Mwabusalu wilayani Meatu ili kuzalisha mbegu ya Msingi (Basic seed). Mbegu ikitoka Mwabusalu inakwenda kupandwa Wilaya ya Igunga ili kuzalisha mbegu iliyothibitishwa (Certified Seed). 

  “Katika kipindi cha miaka 2 tumefanikiwa kuzalisha mbegu mpya ya UKM08 kwa ajili ya wakulima wote wa pamba. Kuanzia msimu huu wa kilimo wa 2018/19 wakulima wote watapanda mbegu mpya ya UKM08. Nichukue fursa hii kuwapongeza Wadau wote mlioshiriki kufanikisha uzalishaji wa mbegu bora kwa ajili ya wakulima wetu” Alikaririwa Dkt Tizeba

  Aidha, alisema kuwa Kilimo cha pamba bado kina matatizo ya msingi ikiwemo huduma za ugani kutowafikia wakulima. “Hili ni tatizo kubwa la uendelevu wa kilimo nchini si pamba peke yake. Maelekezo mengi yametolewa kuhusu umuhimu wa kuboresha utoaji wa huduma za ugani, lakini utekelezaji wake ni hafifu. Nakitaka kikao hiki tulijadili suala hili na tuliwekee azimio linalotekelezeka ili tija katika kilimo cha pamba na mazao mengine iweze kuongezeka” Alisema 

  Pia ameiagiza Bodi ya Pamba kugawa kamba za kupandia kabla ya tarehe 10 Novemba 2018. 

  Alisema, Uamuzi wa Serikali kubadili mfumo wa ununuzi wa pamba ulipokelewa kwa hisia mbalimbali lakini Vyama vya Ushirika vya Msingi vimesimamia kwa weledi na ufanisi mkubwa zoezi la ununuzi wa pamba.

  “Natambua yapo mapungufu yaliyojitokeza katika shughuli ya ununuzi wa pamba ikiwemo AMCOS kupoteza fedha za makampuni ya pamba mfano Wilaya ya Maswa na kuchelewesha kulipa baadhi ya wakulima katika Wilaya za Bunda na Serengeti” 

  “Namuagiza Mrajis kuchukua hatua za haraka za kisheria kwa viongozi wote wa AMCOS waliofanya ubadhirifu ili haki itendeke na ionekane inatendeka. Taarifa ya hatua zilizochukuliwa niipate tarehe 30 Novemba 2018” Alisisitiza Dkt Tizeba

  0 0

  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, amewataka viongozi wa vikosi vya operesheni Nzagamba na Sangara, kusimamia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya ya kukusanya maduhuli ya serikali.

  Akiwa kwenye ziara yake kwa nyakati tofauti katika ukaguzi wa operesheni hizo kwa mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Mwanza, Ulega alisema wapo wanaokiuka taratibu na miongozo.

  Awali mkuu wa timu ya operesheni mkoa wa Singida, Nankondo Senzila, alisema wanaendelea katika kanda hiyo ambapo kazi kubwa ni kukagua mazao ya uvuvi yanayosafirishwa kwenda sehemu mbalimbali

  Akiwa Shinyanga, Waziri Ulega alikutana na kuzungumza na timu ya operesheni Nzagamba inayosimamia mikoa ya Tabora na Shinyanga, aliitaka timu hiyo kujijenga vizuri katika kila idara ili kuongeza ukusanyaji wa maduhuli na kuondokana na ujanjaujanja.

  Kiongozi wa timu hiyo, Rogers Shengoto alisema katika operesheni hiyo ya mifugo awamu ya pili .Akiwa Mwanza alikutana na timu ya operesheni Nzagamba ya mikoa ya Mwanza na Mara ikiwa kazini na kuwataka wafanye kazi kwa kufuata sheria na kuachana na njia za ujanja zitakazofikia kupungua kwa ukusanywaji wa mapato

  Kiongozi wa operesheni wa mikoa hiyo, Shilagi Masele alimweleza Ulega kuwa kwa wiki ya kwanza walipata changamoto ya baadhi ya Halmashauri kutokuwa na tozo mpya katika sekta ya mifugo ambapo walihakikisha wanazijua vizuri na kwa sasa kazi zinaenda vizuri.
   
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na viongozi wa vikosi vya operesheni Nzagamba na Sangara ,ambapo amewataka viongozi kusimamia sheria na miongozo ya  kukusanya maduhuli ya serikali.(Picha na Emmanuel Massaka wa MMG)
  Timu ya operesheni Sangara,Nzagamba wakiendelea na ukaguzi katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.(Picha na Emmanuel Massaka wa MMG)

  0 0

  Na Grace Semfuko-MAELEZO

  Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbas amesema Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt John Pombe Magufuli imeongeza kasi ya ujenzi wa Hospitali za Wilaya na vituo vya afya nchini ambapo kwa miaka mitatu pekee jumla ya vituo hivyo 67 vimejengwa ukilinganisha na 77 vilivyojengwa miaka 53 iliyopita tangu uhuru.

  Dkt Abbasi amesema hatua hiyo ya Serikali ya ujenzi wa kasi wa hospitali na vituo vya afya inalenga kuimarisha afya za watanzania ambapo hivi sasa idadi kubwa ya watanzania inatumia huduma za bima ya afya ya Taifa NHIF idadi ambayo awali ilikuwa milioni 9.9 mwaka 2015 mpaka kufikia zaidi ya milioni 16 Mwaka huu wa 2018.

  Akizungumza nkatika semina ya Waandishi wa Klabu ya waandishi wa Habari wa Mkoa wa Dar Es Salaam (DDCPC) iliyoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF iliyokuwa na lengo la kujengeana uwezo ili umma wa watanzania waweze kunufaika zaidi katika huduma za Afya Nchini, Dkt Abbasi amesema ipo haja kwa waandishi wa habari hao kupongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.

  “Unajua hata sisi waandishi wa habari tunayo haki ya kupongeza,pale unapoandika changamoto na zikafanyiwa kazi ni muhimu kupongeza pia sio kukosoa tu, juhudi za Serikali ya awamu ya tano kwa kipindi kifupi tu makubwa yamefanyika ukilinganisha na kipindi kingine chochote” alisema Dkt Hassan Abbasi Msemaji Mkuu wa Serikali.

  Aidha Dkt Abbasi amewataka waandishi wa Habari Nchini kutumia kalamu zao katika kuandika mafanikio makubwa ya miaka mitatu yanayofanywa na rais Dkt John Pombe Magufuli.

  Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Huduma za wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF Bw. Mbarouk Magawa amesema idadi hiyo ya wanachama iliyoongezeka inaufanya mfuko huo kuzidi kujiimarisha na kuhudumia wanachama wengi zaidi.

  Mbarouk amesema kuongezeka kwa idadi hiyo ya wanachama kunaifanya Juhudi za Serikali ya awamu ya tano kufikia malengo yake ya kuhakikisha huduma za afya nafuu zinapatikana nchini kote.

  “Mfuko wa Taifa wa Bima za Afya lengo letu ni kuhudumia wanachama wengi zaidi na kwa awamu hii chini Uongozi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli wanachama wengi zaidi wameongezeka tangu kuanzishwa kwa mfuko huu mwaka 2001” alisema Magawa Mkurugenzi wa Huduma za wanachama wa NHIF.

  Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya ulianzishwa kwa Sheria namba 8 ya Bunge ya mwaka 1999 na mfuko huo ulianza kufanyakazi rasmi mwaka 2001,hadi sasa mfuko huo una wanachama zaidi ya milioni 16 kutoka Milioni 9.9 waliokuwepo hapo awali.

  0 0

  Na Rhoda James - Geita

  Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameuagiza mgodi wa Nyati Resources ltd uliopo katika kijiji cha Ngula kata ya Bujula mkoani Geita kutolipa gawio Serikali ya kijiji cha Ngula kuanzia tarehe 2 Novemba, 2018 ili kutoa nafasi ya uchunguzi kujua ni nani mmiliki halisi wa eneo hilo la mgodi.

  Ametoa agizo hilo wakati wa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia tarehe 2 hadi 3 Novemba, 2018 iliyolenga kukagua machimbo ya madini katika Mkoa wa Geita.

  Pamoja na ukaguzi huo, Biteko ameeleza kuwa, ametembelea machimbo hayo ili kutatua mgogoro wa ardhi uliopo baina ya Kijiji cha Ngula na mkazi wa kijiji hicho Mindi Masasi. Akizungumza katika kikao hicho, Biteko ameutaka Mgodi huo wa Nyati Resources ltd kutolipa gawio kwa kijiji hicho kwa kuwa kuna malalamiko kutoka kwa mkazi wa kijiji hicho ambaye ni Mindi Masasi.

  Biteko ameeleza kuwa mgodi huo umeanza uzalishaji tangu Desemba, 2017 na umekuwa ukimlipa Mindi Masasi gawio kwa zaidi ya mwaka kwa kuwa wakati wanaanza uzalishaji wa dhahabu wamemkuta katika ardhi hiyo ambayo amekuwa akiishi tangu mwaka 1954 lakini sasa kijiji kinadai kuwa ardhi hiyo ni mali yao na wao ndio wenye haki ya kulipwa gawio hiyo.

  Pamoja na maswali mengi yanayojitokeza, Biteko amesema ni vyema tuachie mamlaka husika kufanya uchunguzi kuhusiana na suala hili “Zaidi ya mwaka Masasi amekuwa akilipwa gawio na mgodi huu, je serikali ya kijiji cha Ngula ilikuwa wapi, mbona serikali ya kijiji haizungumzii eneo lingine isipokuwa eneo la mgodi,” aliuliza Biteko.

  Wakati huo huo Biteko ameutaka Mgodi wa Nyati Resources ltd kutoa maelezo ni kwa nini tangu mwaka 2017 Desemba walipoanza uzalishaji wa dhahabu wamelipa Mrabaha wa kiasi cha Shilingi 200,000/- tu wakati mapato yao ni zaidi ya milioni 50.

  “Huo ni ukiukwaji wa ulipaji wa kodi za Serikali, haiwezekani tangu mwaka jana hadi leo mmefanikiwa kulipa Mrabaha wa laki mbili tu,” alisema Biteko. Aliongeza kuwa lazima wazawa kuonesha mfano mzuri wa kulipa kodi ili hata wawekezaji kutoka nje ya nchi wakija waone umuhimu wa kulipa kodi.

  Kwa upande wake Meneja wa Mgodi wa Nyati Resource ltd, Christopher Nilla amekiri kuwa kweli kumekuwepo na mapungufu katika ulipaji wa kodi za Serikali lakini na kuahidi kubadilika na kulipa sawasawa na sheria ya madini na kubainisha kuwa wanamiliki mgodi mwingine ambapo zaidi ya Tsh milioni kumi zimelipwa serikalini. 

  Mkazi wa kijiji cha Ngula, Mindi Masasi (kushoto) akimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko (hayupo pichani). Katikati ni Mtoto wa Mindi Masasi, Makanika Chalo pamoja na Mwenyekiti wa kata ya Bujula (jina halikupatikana)
  Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko akihutubia wananchi wa kijiji cha Ngula na wachimbaji wadogo wadogo wa mgodi wa Nyati Resources Ltd (hawapo pichani) katika mkoa wa Geita tarehe 2 Novemba, 2018
  Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ngula mara baada ya kukagua Mgodi wa Nyati Resources Ltd uliopo katika kijiji cha Ngula kata ya Bujula mkoani Geita.

  0 0

  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inapenda kuwajulisha wananchi na jumuiya ya kimataifa kupitia vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi kuhusu masuala ya ushoga yaliyoongelewa na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam hivi karibuni. 

  Katika mkutano wake na vyombo vya habari, Mhe. Mkuu wa Mkoa alitangaza kampeni ya kukabiliana na vitendo vya ushoga katika jiji la Dar es Salaam. 

  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ingependa kufafanua kwamba, hayo ni mawazo yake na sio msimamo wa Serikali. 

  Aidha, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ingependa kutumia nafasi hii kukumbusha na kusisitiza kwamba, itaendelea kuheshimu mikataba yote ya kimataifa inayohusu haki za binadamu ambayo imesaini na kuridhia.

  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea na itaendelea kuheshimu na kulinda haki hizo kama zilivyo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Imetolewa na:
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 
  Dodoma.
  04 Novemba, 2018

  0 0


  Na George Binagi-GB Pazzo.

  Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameitaka kampuni ya Nyati Resources inayofanya shughuli za uchimbaji dhahabu katika Kijiji cha Ngula wilayani Geita, kusitisha mara moja kutoa gawio la umiliki wa ardhi kwa serikali ya Kijiji hicho baada ya mjane mmoja kulalamika kunyang’anywa ardhi hiyo kwa madai kuwa ndiye mmiliki halali.

  Biteko ametoa zuio hilo Novemba 02, 2018 baada ya kufanya ziara katika mgodi wa Ngula kukagua shughuli za uchimbaji madini, kusikiliza na kutatua kero zinazohusiana na sekta ya madini pamoja na kuzungumza na wachimbaji wadogo katika mgodi huo.

  Akisikiliza mgogoro wa umiliki wa ardhi katika mgodi huo, mjane huyo Bi. Mindi Masasi anayekadiriwa kuwa na zaidi ya miaka 80 alieleza kuwa mmiliki halali wa ardhi hiyo tangu mwaka 1954, na kwamba kampuni ya Nyati Resources ilipoanza shughuli zake mwaka jana ilikuwa ikimlipa gawio la umiliki wa ardhi lakini mwezi April mwaka huu serikali ya Kijiji cha Ngula kupitia Mwenyekiti wake Symphorian Mchael ilidai kumiliki ardhi hiyo na hivyo kuanza kupokea gawio kutoka kwa kampuni hiyo.

  Kufuatia malalamiko hayo, Biteko alimwagiza Christopher Nilla ambaye ni Meneja wa kampuni ya Nyati Resources kusitisha utoaji wa gawio hilo hadi pale tume huru ya uchunguzi itakapoundwa na kutoa majibu sahihi nani mmiliki wa ardhi hiyo inayokadiriwa kufikia heka 350.

  Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Ngulla, Symphorian Mchael kuchukua maamuzi ya kuweka zuio kwa kampuni ya Nyati Resources kutoa gawio kwa Bi. Mindi Masasi anayedai kumiliki eneo hilo baada ya vikao vyote vya kutafuta mmiliki halali kukaa na kubaini kwamba eneo hilo ni la Serikali ya Kijiji.
  Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko (kushoto), akimsikiliza mjane Bi. Mindi Masasi (kulia) anayedai kuwa mmiliki halali wa eneo la mgodi wa Ngula uliopo katika Kijiji cha Ngula wilayani Geita. Eneo hilo limechukuliwa na Serikali ya Kijiji cha Ngula na hivyo kuibua mgogoro baina ya bibi huyu na serikali ya Kijiji.
  Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko (kushoto), akimsikiliza Habi Makanika (kulia) ambaye ni kijana wa Bi.Mindi Masasi (katikati) wakati akisikiliza mgogoro wa umiliki wa ardhi baina ya bibi huyo na serikali ya Kijiji cha Ngula wilayani Geita.
  Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko (kushoto), akizungumza na wachimbaji wadogo wa dhahabu katika mgodi wa Ngula wilayani Geita.
  Mwenyekiti Kijiji cha Ngula, Symphorian Mchael (kushoto), Mjane Bi.Mindi Masasi anayedai kuwa mmiliki halali wa eneo la mgodi wa Ngula (katikati) pamoja na Diwani Kata ya Bujula (kulia), wakisikiliza maamuzi ya Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko (hayupo pichani) baada ya kusikiliza mgogoro wa umiliki wa eneo la mgodi wa Ngula.
  Baadhi ya wachimbaji wadogo katika machimbo ya Ngula wilayani Geita, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko (hayupo pichani).
  Tazama Video hapa chini

  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waumini mbalimbali wa Kanisa Katoliki, Maaskofu pamoja na Wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi  katika Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu mara baada ya Misa iliyofanyika Bagamoyo Mkoani Pwani.
  3
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Muadhama Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Polycarp Kardinali Pengo wapili kutoka kushoto waliokaa, Muadhama Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Nairobi John Kardinali Njue wapili kutoka kulia waliokaa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu wa Majimbo mbalimbali ndani  na nje ya nchi mara baada ya Misa ya Maadhimisho ya Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.
  4
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Maaskofu wa Kanisa Katoliki mara baada ya Misa ya ya Maadhimisho ya Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.
  6
  Baadhi ya Maaskofu mbalimbali wa Kanisa Katoliki wakiwa wanawasili kwa maandamano katika eneo lililoandaliwa kwa ajili ya Misa takatifu ya Jubilei ya Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.
  7.
  78.89
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamini Mkapa pamoja na Spika Mstaafu Anne Makinda wakiwa katika Misa takatifu ya ya Jubilei ya  Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.
  10
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Muadhama Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Polycarp Kardinali Pengo wapili kutoka kushoto waliokaa, Muadhama Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Nairobi John Kardinali Njue wapili kutoka kulia waliokaa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu wa Majimbo mbalimbali ndani  na nje ya nchi mara baada ya Misa ya Maadhimisho ya Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.
  12
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Muadhama Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Nairobi John Kardinal Njue ambaye aliongoza Misa Takatifu ya Jubilei ya  Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani.
  13
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamini Mkapa kabla ya kuanza kwa Misa takatifu ya Jubilei ya  Miaka 150 ya Uinjilishaji, Afya na Elimu Bagamoyo mkoani Pwani. PICHA NA IKULU

  0 0
  0 0


  Na.Alex Sonna wa Fullshangweblog,Dodoma

  Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Jijini Dodoma,wametakiwa kutilia mkazo ulipaji wa mafao ya wastaafu kwa wakati.

  Akitoa maagizo hayo leo jijini hapa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana na Wenyeulemavu, Anthony Mavunde, alipotembelea ofisi za mfuko huo kusikiliza maoni ya wanachama na wadau wanaohudumiwa na PSSSF.

  Mhe.Mavunde amesema kuwa inatakiwa mlipe kwa wakati mafao kama ilivyo kauli mbiu yenu ya “Tunalipa Kuanzia jana” ili lengo la serikali la kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii, litimie .''Inatakiwa wastaafu wapewe umuhimu wa elimu kabla ya kuwalipa mafao ili waweze kujiandaa vyema kwa kuanzisha miradi na kutunza kumbukumbu za matumizi ya fedha''amesema Mavunde

  Aidha Mhe.Mavunde amewaagiza wafanyakazi wote kuhakikisha wanatoa huduma stahiki zenye ubora na kwa wakati ili kuisaidia serikali kusonga mbele katika huduma ya hifadhi ya jamii.“Matarajio ni kwamba mtatoa huduma kwa ufanisi na kwa ubora ili yale matarajio ya serikali yaweze kutimia, awali kulikuwa na malalamiko watu hawapati huduma stahiki lakini naimani hakutakuwa na malalamiko hayo,”amesema Mavunde

  Kwa Upande wake, Meneja wa PSSSF Mkoa wa Dodoma, Meshack Bandawe, amesema kuwa ofisi hiyo imeanza kufanya kazi zake Septemba mosi mwaka huu na kuna wanachama wanaochangia ni zaidi ya laki moja.“Tumejipanga kuwahudumia ipasavyo na hadi sasa tumekusanya Sh.Milioni 880 katika mkoa wa Dodoma na tutaendelea kusimamia na kutekeleza majukumu kwa mujibu wa sheria,”amesema Bandawe

  Hata hivyo amebainisha kuwa hadi sasa wanachama 2792 wameshapita kupata huduma na wamepokea madai 796 ya wanachama wa mifuko mbalimbali iliyounganishwa kwenye mfuko huo. Bandawe amesema kuwa madai 717 yameshughulikiwa na wanachama wamelipwa mafao yao na mengine 79 yapo kwenye hatua mbalimbali za kufanyiwa kazi katika mkoa wa Dodoma tu.

  Aidha amesema takribani wastaafu 1027 wanatarajiwa kustaafu katika kipindi cha 2018/19 ambapo mfuko huo umejipanga kutoa elimu ya kujipanga na ustaafu wao ikiwemo kubuni miradi ya kujiimarisha kiuchumi kwa mkoa wa Dodoma peke yake.
   Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana na Wenyeulemavu, Anthony Mavunde,akizungumza waandishi wa habari (hawapo pichani) alipotembelea ofisi za mfuko huo leo jijini Dodoma kusikiliza maoni ya wanachama na wadau wanaohudumiwa na PSSSF.
  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana na Wenyeulemavu, Anthony Mavunde,akizungumza na Meneja wa PSSSF Mkoa wa Dodoma, Meshack Bandawe, alipotembelea ofisi za mfuko huo kusikiliza maoni ya wanachama na wadau wanaohudumiwa na PSSSF.
  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana na Wenyeulemavu, Anthony Mavunde,akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa PSSSF Mkoa wa Dodoma leo alipotembelea ofisi za mfuko huo kusikiliza maoni ya wanachama na wadau wanaohudumiwa na PSSSF.

  0 0


  Tanzania kati ya nchi 10 zinazokua kiuchumi ni ya Tisa na Nchi za Kusini Tanzania ni ya Nne na Afrika Mashariki ni ya kwanza ukuaji huo wa uchumi ni kutokana na ripoti ya Benki ya Dunia.

  Akizungumza na waandishi habari wakati akitoa Salaam za Rais Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya habari Marketing Dkt. Hassan Abbas amesema kuwa katika miaka mitatu Tanzania imekuwa ikifanya vizuri.

  Amesema kuwa katika ukusanyaji mapato umepanda kutoka sh.bilioni 850 mwaka 2015 hadi kufikia sh.Trioni 1.3.Amesema kuna mashirika yameweza kufanya kazi na katika ukusanyaji wa mapato ikiwemo Dawasa , TPA pamoja shirika la Posta.

  Dkt. Abbas amesema zaidi ya viwanda 3000 vimesajiliwa na vingine kufanya kazi.Ajira zaidi ya 26000 zimepatikana kutokana na viwanda na kufanya
  Kazi ya mahakama ya mafisadi imeanza na kazi mbalimbali zinafanyika .

  Upande wa rushwa Tanzania ya pili kwa Afrika Mashariki ya pili katika mapambano ya rushwa.Tanzania imenunua ndege za saba na Nne tayari na Desemba ndege mbili aina ya air bus.

  Dkt. Abbas amesema kuwa kuna ujenzi wa reli ya kisasa na iko katika asilimia 35 pamoja na kujenga barabara ya juu ya Tazara huku zingine zikiendelea.Mardi wa stiglers Gorge kuondoa changamoto ya umeme.Amesema serikali imepeleka maendeleo kwa wananchi na sio kuwekea watu fedha mfukoni.

  0 0

  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai aongoza kikao cha kamati ya Uongozi kilicholenga kujadili na kupokea Shughuli za Mkutano wa kumi na Tatu wa Bunge pamoja na Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano, Pia Kupokea hati ya dharura ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha wa Mwaka 2018 (The Microfinance Bill, 2018); kilichofanyika leo tarehe 5 Novemba 2018 katika ukumbi wa Spika Jijini Dodoma. Ikiwa ni Maandalizi ya kuanza kwa Vikao vya Bunge vinavyotegemea kuanzia kesho Novemba 6, 2018 Jijini Dodoma.
  Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akizungumza jambo wakati wa kikao cha kamati ya Uongozi kilicholenga kujadili na kupokea Shughuli za Mkutano wa kumi na Tatu wa Bunge pamoja na Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano, Pia Kupokea hati ya dharura ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha wa Mwaka 2018 (The Microfinance Bill, 2018); kilichofanyika leo tarehe 5 Novemba 2018 katika ukumbi wa Spika Jijini Dodoma.
  Wajumbe wa Kamati ya uongozi kuanzia kushoto ni Mbunge wa Bukoba Vijijini, Mhe. Jason Rweikiza, Mbunge wa kibakwe, Mhe. George Simbachawene na Mbunge wa Jimbo la Chemba, Mhe. Juma Nkamia wakiwa katika kikao cha kujadili na kupokea Shughuli za Mkutano wa kumi na Tatu wa Bunge pamoja na Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano, Pia Kupokea hati ya dharura ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha wa Mwaka 2018 (The Microfinance Bill, 2018); kilichofanyika leo tarehe 5 Novemba 2018 katika ukumbi wa Spika Jijini Dodoma.

  0 0

   Mkurugenzi wa Ubora na Uhakiki wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr. Mohamed Mohamed akifungua kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu katika ukumbi wa Hospitali ya MOI jijini Dar es salaam leo.
  Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya MOI Prof Charles Mkonyi akizungumza katika kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu
  Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akitoa neno la ukaribisho katika kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na mishipa ya fahamu.
  Kiongozi wa jopo la wakufunzi kutoka chuo kikuu cha Weill Cornel cha marekani Prof Roger Hartl akiwasilisha mada katika kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo ,Mgongo na Mishipa ya fahamu


  Mkurugenzi wa Ubora na Uhakiki kutoka Wizara ya Afya Dkt Mohamed Mohamed (wa pili) kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa  kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu kutoka mataifa mbalimbali duniani. Wa kwanza kushoto ni Profesa Charles Mkonyi mwenyekiti wa bodi ya wadhamini MOI, watatu kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface na wa kwanza kulia ni Kiongozi wa jopo la wakufunzi kutoka marekani Profesa Roger Hartl.


  0 0


  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akionesha nakala ya Jarida la Nchi Yetu Tanzania linalotolewa na Ofisi yake, ambalo limeainisha mafanikio mbalimbali ya kijamii na kiuchumi yaliyofikiwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha miaka mitatu madarakani (2015-2018). Mkutano huo umefanyika leo Jumatatu Novemba, 2018.
  5.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akionesha nakala ya Jarida la Nchi Yetu Tanzania litatolewa na Ofisi yake, ambalo limeainisha mafanikio mbalimbali ya kijamii na kiuchumi yaliyofikiwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha miaka mitatu madarakani (2015-2018) Mkutano huo umefanyika leo Jumatatu Novemba, 2018.
  6.
  Baadhi ya waandishi wa vyombo vya habari nchini wakifuatilia Mkutano baina yao na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakati alipotoa taarifa kuhusu Mafanikio ya kijamii na kiuchumi yaliyofikiwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha miaka mitatu madarakani (2015-2018). Mkutano huo umefanyika leo Jumatatu Novemba 5, 2018.
  1.
  1. Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari nchini kuhusu Mafanikio ya kijamii na kiuchumi yaliyofikiwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha miaka mitatu madarakani (2015-2018). Mkutano huo umefanyika leo Jumatatu Novemba 5, 2018.
  2.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari nchini kuhusu Mafanikio ya kijamii na kiuchumi yaliyofikiwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha miaka mitatu madarakani (2015-2018). Mkutano huo umefanyika leo Jumatatu Novemba 5, 2018.
  3.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari nchini kuhusu Mafanikio ya kijamii na kiuchumi yaliyofikiwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha miaka mitatu madarakani (2015-2018). Mkutano huo umefanyika leo Jumatatu Novemba 5, 2018.
   

  0 0

  KAMPUNI ya uchakataji wa  asili ya Ruaha farm mkoani Iringa kupitia asali yake Ruaha Honey imeanza kuwaokoa kiuchumi wafugaji wa nyuki mkoani Iringa kwa kutoa mizinga na kuwaunganisha na soko la asali . 

  “kampuni ya Ruaha Farm imekuja kivingine baada ya  kufunga mashine za kisasa za kuchakata asali yenye ubora pasipo kutumia vifaa vya kienyeji kama moshi na vingine “ 

  Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Ruaha Honey Fuad Abri alisema kuwa kampuni yake imeendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli ya Tanzania ya viwanda . 

  Alisema ubora wa asali ya kampuni ya Ruaha Honey ni tofauti na asali nyingine zinazouzwa mitaani kwani sifa kubwa ya asali ya Ruaha honey ni asali halisi toka katika vijiji vinavyozunga hifadhi ya Ruaha national park. 

  Asali ya ruaha honey ni Asali bora inayozingatia usafi wa vyombo, usafi wa uchakatishaji pamoja na ufugaji wa nyuki kwa njia salama na rafiki kwa nyuki. Alisema Ruaha honey ni asali ya kampuni ya ruaha farm pamoja na wafugaji wa nyuki wa vijiji vinavozunguka hifadhi ya ruaha. Kampuni ya Ruaha honey inashirikiana na wafuga nyuki wa Iringa kwa kuwawezesha kupata mizinga ya kisasa na kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara ya ufugaji sahihi wa nyuki ili kulinda ubora wa mazao ya nyuki yanayopatikana kama asali na nta. 

  Ruaha honey pia inawapatia soko la asali wafugaji wa nyuki kwa lengo la kuinua kiuchumi kaya maskini kupitia ufugaji wa nyuki alisema Abri .Kuwa asali ya Ruaha ni asali halisi inayotokana na uoto asili wa miti ya Acacia, mibuyu na miti pori na maua pori hivyo ni asali bora zaidi . Alisema kupitia kampuni ya Ruaha farm inafugia nyuki katika shamba lake liliopo Tungamalenga ambayo ni hifadhi ya nyuki ya kwanza binafsi Tanzania na Afrika mashariki 

  Lengo ni kuinua ufugaji wa nyuki wa nyanda za juu kusini pia kuendeleza ufugaji wa nyuki kisasa kama sehemu ya kuwa na viwanda bora vya mazao yatokanayo na nyuki . Hifadhi ya nyuki ya Ruaha ni eneo linafanyika utafiti mbali mbali wa nyuki pamoja na mazao yake, pia ni shamba darasa kwa wafuga nyuki wengine wanaozunguka eneo hilo.

older | 1 | .... | 1715 | 1716 | (Page 1717) | 1718 | 1719 | .... | 1897 | newer