Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA

$
0
0
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza na Balozi wa China Nchini Tanzania Mheshimiwa Wang Ke aliyemtembelea Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa China Nchini Tanzania Mheshimiwa Wang Ke alipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa China Nchini Tanzania Mheshimiwa Wang Ke alipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Balozi wa China nchini Tanzania Mheshimiwa Wang Ke akiwa katika Picha ya pamoja na Wabunge ambao ni wajumbe wa Chama cha urafiki wa kibunge baina ya Bunge la Tanzania na nchi ya China alipokutana nao leo Bungeni Jijini Dodoma. Balozi wa China nchini Tanzania Mheshimiwa Wang Ke akizungumza na Wabunge ambao ni baadhi ya wajumbe wa Chama cha Urafiki wa Kibunge baina ya Bunge la Tanzania na Nchi ya China alipokutana nao leo Bungeni Jijini Dodoma.

Wabunge EALA Wacharuka ‘Dola Milioni 10 Zadaiwa kuyeyuka EAC’

$
0
0
Mjadala Mkali wa kujadili Ripoti ya kamati ya fedha katika Bunge la NNE la Afrika Mashariki,EALA umeendelea Jana huku wabunge mbalimbali wakiendelea kumtupia lawama katibu Mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki EAC,Liberat Mfumukeko kuwa ndo chanzo cha ubadhidifu wa fedha kiasi cha dola za Kimarekani Milioni 10 za jumuiya hiyo.
Katika kikao hicho Mbunge wa Kenya Simoni Mbugua alitishia kujihudhulu nafasi yake ya ubunge iwapo wahusika hawatachukuliwa hatua za kinidhamu.
“Katibu Mkuu kwa muda mrefu amekuwa akifuja fedha na si pesa kidogo ukijumlisha fedha ambazo zimepotea ni zaidi ya dola Milioni 10″Amesema.
Amesema fedha hizo zinatoka kwa wachuuzi wa nchi wanachama ili zitumike kwa watu wa EAC lakini zimekuwa zikipotelea Mifukoni mwa wachache bila sababu za msingi
“Fedha hizo zikitolewa zinakuja zinaporwa na Katibu Mkuu na watu wake, wanapora na kuweka kwenye mifuko yao  ,Kwenye Masoksi wanabeba pesa zote ,sasa mwananchi aliyeko kule anajua mambo yanaenda vizuri lakini sisi kama wabunge tunasema inatosha ,hatutakubali tena” Amesema Mbugua
Aidha alisema kuwa yeye kama Mbunge  afadhali atoke kwenye nafasi yake kuliko kuona jumuiya ikiharibiwa kwa kiasi hicho.
Aliongeza kuwa kulitaka Bunge hilo kuiga utendaji wa Rais  John Magufuli na Rais Kenyatta wa Kenya ambao wameonyesha uwezo mkubwa wa kupambana na ufisadi  kwa kuwafunga watuhumiwa wanaopatika na hatia.

MADIWANI URAMBO WAIOMBA SERIKALI KUINGILIA KATI TATIZO LA MBOLEA YA TUMBAKU KUCHELEWA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Magreth Nakainga akitioa ufafanuzi kwa Madiwani wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kilichokuwa kikipitia taarifa utekelezaji kwa kila Kata wilayani humo jana.
4a
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Adam Malunkwi akifungua kikao cha Baraza la Madiwani cha kupitia taarifa za utekelezaji wa kila Kata wilayani Urambo jana.
A
Mbunge wa Jimbo la Urambo Magreth Sitta  akichangia taarifa ya utekelezaji wa kila Kata wilayani Urambo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Urambo jana.

NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA.

UZALISHAJI na ubora wa tumbaku msimu ujao wa kilimo unaweza kushuka baada ya mbolea ya kukuzia zao hilo kuchewewa kuwafikia wakulima hadi hivi sasa.Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Adam Malunkwi kwa niaba ya Madiwani wenzake wakati wa kikao cha Baraza hilo.

Alisema hadi hivi sasa mbolea ya aina ya N.P.K bado hajifika kwa wakulima wakati msimu wa mvua umeshakaribia kuanza jambo linalotishia ubora na uzalishaji.Malunkwi alisema kitendo hicho sio tu kitamwathiri mkulima pekee pia mapato ya Halmashauri ya Urambo yataathirika kwa sababu sehemu kubwa inategemea tumbaku ili kupata mapato ya ndani kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.

Alisema kwa mujibu wa taarifa za Mzabuni ambayo amepewa jukumu la kusambaza mbolea kwa wakulima wa tumbaku, meli iliyobeba mbolea hiyo itawasili nchini tarehe 11 mwezi huu na inaweza kuchukua wiki mbili na kendelea kuwafikia wakulima jambo ambalo litafanya mazao ya wakulima yapitwe na wakati.

Malunkwi aliomba Serikali kuibana Kampuni ya Mbolea nchini(TFC) kuhakikisha wanaazima mbolea kutoka Kampuni binafisi ili kuziba pengo hilo na kuokoa mazao ya wakulima na hatimaye mbolea yao itakapowasili wazirudishie mbolea yao.

Naye Diwani wa Kata ya Itundu Ahmed Hamoud alisema tatizo hilo la ucheleweshaji wa mbolea ya tumbaku limeanza kuwa sugu kwani kwa kipindi cha miaka mitatu mfufulizo imekuwa ikichelewa kuwafikia wakulima na kuwafanya kuzalisha chini ya ubora na kiwango.

Alisema hatua hiyo imesababisha kushuka kwa makisio ya wakulima kutokana na kushindwa kufikia malengo waliyokubaliana na Kampuni za ununuzi wa tumbaku.Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Urambo Angelina Kwingwa alimtaka Mzabuni anayepewa zabuni ya kuagiza mbolea kwa ajili ya wakulima wa tumbaku kuzingatia kalenda ya zao hilo , kinyume cha hapo ni kumuumiza mkulima na kurudisha nyuma juhudi zake za kujiletea maendeleo.

Alisema kuwa Kitendo cha Mazabuni kuchelewesha mbolea kinakwenda kinyume na juhudi za Serikali za kumshika mkono mkulima mdogo mdogo ili hatimaye siku moja naye apige hatua.

SERIKALI YATOA SIKU NNE KWA WANUNUZI WA KOROSHO

$
0
0

*Yawataka waandike barua wakionesha tani wanazohitaji na lini watazichukua
*Yasema zaidi ya hapo haitoruhusu kampuni yoyote kununua korosho tena

SERIKALI imetoa siku nne kwa wanunuzi wote 35 waliojiandikisha kununua korosho wawe wamepeleka barua katika Ofisi ya Waziri Mkuu wakionesha  kiasi cha tani wanazohitaji na lini watazichukua.

“Hivyo wanunuzi waliojiandikisha wakiwemo na wale wote ambao wamekuwa wananunua kwenye minada lakini kwa kiasi kidogo, wahakikishe ndani ya siku hizo nne kuanzia leo Ijumaa hadi Jumatatu saa 10 alasiri wawe wameleta barua na ofisi yangu ipo wazi saa 24.”

Hayo yamesemwa leo (Ijumaa, Novemba 9, 2018) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akitoa tamko la Serikali kuhusu ununuzi wa zao la korosho, ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma.Baada ya kupita siku hizo Serikali italazimika kufuta usajili kwa wote waliojisajili kununua zao hilo kwa sababu walikubaliana kwenda kununua lakini hali inayoonekana sasa ni kama kumkomoa mkulima kitu ambacho imesema haitakubaliana nacho.

“Mwenye nia ahakikishe katika siku hizo nne iwe ndio mwisho wa kununua korosho na waandike barua kwani ofisi yangu ipo wazi saa 24 wana nafasi ya kuleta barua wakati wowote wakionesha nia yao na kiwango wanachokihitaji. Zaidi ya hapo Serikali haitoruhusu kampuni yoyote kununua korosho tena.”

Waziri Mkuu amesema kwenye msimu wa ununuzi wa korosho wa mwaka huu, walishuhudia kusuasua kwa minada, ambapo Serikali ilikutana na wanunuzi wa korosho katika kikao kilichoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli ambapo walikubaliana kununua kwa bei inayoanzia sh 3,000 na kuendelea.

“Mjadala ulikuwa wa wazi na wafanyabiashara wenyewe walipendekeza bei ambayo ilikuwa inaanzia sh. 3,000, hata hivyo baada ya kikao hicho ununuzi katika minada imeendelea kusuasua na hata tani zilizokuwa zikinunuliwa zilikuwa kidogo sana. Sisi tunaiona hali hii kama mgomo baridi ambao si sawa sawa sana kwani malengo yetu sisi na sekta binafsi ni kumfanya mkulima apate bei nzuri.

Hali hii haifurahishi kwa sababu Serikali imedhamiria kuboresha mazao yanayolimwa na wakulima kwa kuwasaidia kuanzia katika hatua za utayarishaji wa mashamba, upatikanaji wa pembejeo na masoko ili waweze kunufaika na kilimo na kupata tija katika mazao hayo.”Waziri Mkuu amesema baada ya kugundua bei imekuwa tatizo Serikali ilifanya jitihada za kupeleka wataalamu wake katika masoko makuu duniani na kupata bei halisi ambayo bado  inatosha kumlipa mkulima sh 3,000.

Hatua hiyo imekuja baada ya zao la korosho kuendelea kununuliwa kwa bei ya chini na idadi ya wanunuzi kuwa ya chini licha ya uzalishaji wa mwaka huu kuwa mdogo ukilinganisha na msimu wa mwaka jana.Amesema msimu wa mwaka jana uzalishaji ulikuwa zaidi ya tani 300,000 na mwaka huu zinatarajiwa tani zaidi ya 200,000 hivyo wafanyabiashara wanao uwezo kununua korosho zilizopo.

Hata hivyo Serikali imewataka wananchi hususani wakulima wa korosho nchini kuendelea kuwa wavumilivu na watulivu wakati ikiendelea kushughulikia suala hilo.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980
 41193 – Dodoma
IJUMAA, NOVEMBA 9, 2018.

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU WANUNUZI WA KOROSHO

PUMA ENERGY TANZANIA YAZINDUA MRADI WA SKY IS THE LIMID PROJECT KWA LENGO LA KUAMSHA MOYO WA UJASIRI NA KUJIWEKEA MALENGO KATIKA KUFANIKIWA

$
0
0
????????????????????????????????????
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo (wa pili kulia) na Meneja Masoko wa mafuta ya Ndege Puma Tanzania, Illuminata Yateri (katikati) wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Josephat Kagirwa (kulia) alipokuwa akizungumza na wanafunzi kutoka Shule za Msingi wilayani Kisarawe walipofanya ziara ya mafunzo uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni adhimisho la mradi ujulikanao kama Sky is the limit.
????????????????????????????????????
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo (wa pili kulia) akizungumza na wanafunzi wa shule za msingi kutoka wilaya yake wakati wa ziara ya kimafunzo kutembelea karakana ya ndege jijini Dar es Salaam jana kwa kushirikiana na Kampuni ya Puma Energy Tanzania katika kuhudumia utoaji wa mafuta ya ndege chini ya mradi ujulikanao kama Sky is the limit.
????????????????????????????????????
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, Meneja Masoko wa mafuta ya Ndege Puma Tanzania, Illuminata Yateri na wanafunzi wa Shule za Msingi wilayani Kisarawe, wakiingia kwenye Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), walipofanya ziara ya kimafunzo katika mradi wa Sky is the limit kwenye uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam (JNIA) jana.
????????????????????????????????????
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo akimfunga vifungo mmoja wa wanafunzi wakati walipofanya ziara katika uwanja wa ndege wa JNIA katika mradi mradi ujulikanao kama Sky is The Timit
????????????????????????????????????
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, Meneja Masoko wa mafuta ya Ndege Puma Tanzania, Illuminata Yateri na wanafunzi wa Shule za Msingi wilayani Kisarawe, wakimsikiliza Injinia wa Ndege kutoka Shirika la Ndege Tanzania (ATC), Nkhambi Salanga walipofanya ziara ya kimafunzo katika mradi wa Sky is the limit katika uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam jana.
????????????????????????????????????

KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Energy (T) LTD kwa kushirikiana na Kampuni ya Air Tanzania Limited imezindua mradi unaojulikana kama “Sky is the Limit Project”wenye lengo la kuwatambulisha na kuwapa uelewa wanafunzi wa shule za msingi wasio na fursa au uwezo wa kuufikia kwa urahisi ulimwengu wa anga ili kuwapa uelewa kuhusu sekta hiyo yenye kuvutia.

Imeelezwa lengo la mradi huo ni kuwahamasisha watoto wanaotoka mazingira ya kawaida sana ya vijijini kwa kuwatia moyo katika masomo yao ili wajue na kuvutiwa na sekta ya anga na maeneo mengine ya fursa za kazi za nje ya maeneo wanaoishi.

Katika kufanikisha mradi huo zaidi ya wanafunzi 40 kutoka Shule za msingi za wilayani Kisarawe wamepata fursa ya kutembelea Shirika la Ndege la Air Tanzania pamoja na kushuhudia namna Kampuni ya mafuta ya Puma inavyohifadhi mafuta ya ndege katika Uwanja wa Ndege Terminal One jijini Dar es Salaam.

Meneja Masoko wa Mafuta ya Ndege Tanzania kutoka kampuni ya Mafuta ya Puma Illuminata Yateri amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa kama neon linavyojieleza la Sky is the Limit , mradi huo unataka kuamsha moyo wa ujasiri na kujiwekea malengo ya juu katika kufanikiwa.

Amefafanua mradi huo wa Sky is the limit utawapa wototo kutoka shule za msingi waliochaguliwa kutoka kwa jumuiya zisizo na fursa na uzoefu wa sekta ya anga kwa ukaribu zaidi, kwa kufanya ziara ya elimu inayofanywa katika miundombinu ya uwanja wa ndege kama ugavi wa mafuta ya ndege,huduma zinazotolewa kwenye ndege ,udhibiti wa safari za ndege, kupata habari mbalimbali za ndege kupitia watalaam wa sekta ya ana wanaohusika.

“Watoto watajua shughuli za kampuni ya mafuta ya Puma kuhusu biashara ya mafuta ya ndege jinsi yanavyouzwa kwenye ndege za ndani na za kimataifa.Kampuni ya Puma Tanzania ambayo ndio inayoongoza katika soko la kuuza mafuta ya ndege nchini imekuwa mshirika wa muda mrefu katika sekta ya anga katika kuunga mkono maendeleo ya kiuchumi ya Serikali ya Awamu ya Tano.

“Pia watoto watapata fursa ya kujua biashara ya kampuni ya ndege Tanzania –Air Tanzania “The wings of Kilimanjaro” kwa kutembelea kituo cha matengenezo ,kupata habari na kufahamu vizuri kuhusu juhudi zake za kuchangia uchumi wan chi kwa njia ya usafiri wa anga,”amesema Yateri na kuongeza kuwa idadi ndogo ya wanafunzi watapata fursa ya kupanda ndege kwa safari fupi ambayo inajumuisha majadiliano kutoka kwa rubani na wafanyakazi wa ndege katika siku za mbele.

”Tunashukuru mamlaka ya Kisarawe chini ya uongozi wa Mkuu wa Wilaya hiyo Jokate Mwegelo,Ofisa elimu Wilaya ya Kisarawe pamoja na walimu husika kwa msaada wa kupata wanafunzi hawa ambao leo hii wamejifunza kwa vitendo.Puma tutaendelea kushirikiana na walimu wa shule mbalimbali nchini katika kuhakikisha tunashiriki kuwahamsisha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi na mwisho wa siku kuongeza wataalam wa mafuta ya ndege na mambo ya anga,”amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amesema kuwa anaishukuru Kampuni ya Puma kwa kushirikiana na Air Tanzania kwa kandaa mafunzo kwa vitendo kwa ajili ya wanafunzi hao na kwamba hatua hiyo inaonesha namna ambavyo wamedhamiria kuunga mkono juhudi za Rais Dk.Magufuli katika kubooresha sekta ya anga nchini.

“Tumeona juhudi za Rais wetu mpendwa katika kuboresha sekta ya anga.Kitendo cha kuleta wanafunzi kujifunza kwa vitendo kuhusu masuala ya anga na mafuta ya ndege maana yake ni moja tu tunakwenda kuhamasisha vijana wa Tanzania kupenda masomo yanayohusu mafuta na anga.Tumepata taarifa kutoka Puma kwa mhandisi wa mafuta ya ndege nchini Tanzania yupo mmoja tu na anakaribia kustaafu, hivyo ujio wanafunzi hawa ni fursa nyingine ya kuwahamasisha na hatimaye kuwa na wahandisi wengi wa mafuta ya ndege,”amesema Jokate Mwegelo.

MAKAMU WA RAIS AENDELEA NA ZIARA WILAYANI ROMBO

$
0
0

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungungumza na Watumishi wa Wilaya ya Rombo mara baada ya kupokea taarifa ya Wilaya hiyo. Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Kilimanjaro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
24
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu ya mradi wa ujenzi wa jengo la Utawala la Halmashauri ya Rombo kutoka kwa Mhandisi wa Halmashauri Mhandisi Boniface Vedasto. Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Kilimanjaro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
56
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wananchi wa Tarakea waliojitokeza kumsalimia wakati alipokuwa njiani kuelekea kwenye shamba la miti Rongai. Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Kilimanjaro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
810
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua kitalu cha miche wakati alipotembelea shamba la miti la Serikali lililopo Rongai Rombo. Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Kilimanjaro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
14


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Watumishi wa Serikali Wilayani Rombo kufanya kazi kwa kushirikiana.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo mara baada ya kupokea taarifa ya Wilaya hiyo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Mhe. Agnes Hokororo.

“Wote tunajenga nyumba inayoitwa Tanzania katika nafasi yako yoyote ulipo unajenga nyumba inayitwa Tanzania, kwa itikadi yako yoyote uliyonayo unajenga nyumba inayoitwa Tanzania tunatawaliwa na sheria moja, tunataliwa na miongozo hiyo hiyo ya Serikali, kanuni na mambo mengine na hiyo hiyo Serikali”.

Katika ziara yake Wilayani Rombo Makamu wa Rais alikagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Jengo la Utawala la Halmashauri ya Rombo, mradi wa maji Shimbi Mashariki,kukagua shamba la Miti Rongai.

Makamu wa Rais ambaye yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo pia alipata nafasi ya kuwasalimu wananchi wa Tarakea waliojitokeza barabarani kumsalimia na alihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya shule ya msingi Keni-Mengeni.

Kwa upande mwingine Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amesema kuwa Serikali hii inafanya jambo la kihistoria kwa kukamilisha ujenzi wa vituo vya Afya 350.

Mongella amtaka Mkurugenzi Ilemela kununua vifaa tiba katika Kituo cha Afya Karume

$
0
0
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe. John Mongella jana amefanya ziara katika Kituo cha Afya Karume, Manispaa ya Ilemela na kushtushwa na uhaba wa vifaa tiba kwenye majengo mapya yaliyojengwa na serikali kupitia utaratibu wa “Force Account”.Mhe. Mongella ametoa muda wa siku saba kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela na Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo kuhakikisha majengo hayo yanaanza kufanya kazi kama ilivyokusudiwa.

Tazama Video hapa chini


BALOZI WA JAPAN ATEMBELEA MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA

$
0
0
Balozi wa Japani nchini Sinichi Goto akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwini Kunambi alipotembelea ofisini kwake kabla hajaenda kukagua eneo ambapo zitajengwa ofisi za ubalozi wa Japan
Balozi wa Japani nchini Sinichi Goto akiangalia mchoro wa ramani wa eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za Ubalozi wa Japan Mkoani Dodoma baada ya kufanya ziara ya kukagua.
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwini Kunambi akisisitiza jambo kwa Balozi wa Japani nchini Sinichi Goto baada ya kufanya ziara ya kukagua eneo lililotengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Ubalozi wa Japani Jijini Dodoma
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwini Kunambi akiwa na Balozi wa Japani nchini Sinichi Goto na baadhi ya viongozi wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukagua eneo lililotengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Ubalozi wa Japani Jijini Dodoma
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwini Kunambi akizungumza na Balozi wa Japani nchini Sinichi Goto baada ya kukagua eneo lililotengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Ubalozi wa Japani Jijini Dodoma
Balozi wa Japani nchini Sinichi Goto atoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwini Kunambi walipotembelea eneo lililotengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Ubalozi wa Japani 
Hilo ndio eneo lililotengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Ubalozi wa Japani Jijini Dodoma
Baada ya kumaliza kukagua eneo lililotengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Ubalozi wa Japani Jijini Dodoma Balozi wa Japan akiwa na Mkurugenzi wanaelekea katika kupanda gari 
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa tanki kubwa la kuhifadhia maji kwenye eneo hilo ambalo litakuwa na ujazo wa lita milioni moja.
Fundi anayejenga tanki kubwa la kuhifadhia maji kwenye eneo hilo ambalo litakuwa na ujazo wa lita milioni moja akitoa maelezo kwa Balozi wa Japan nchini Sinichi Goto kwa upande wa (kushoto) Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwini Kunambi akisikiliza kwa umakini.
Balozi wa Japan nchini Sinichi Goto akisaini kitabu cha wageni baada ya kumaliza kukagua eneo lililotengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Ubalozi wa Japani Jijini Dodoma.
PICHA NA ALEX SONNA WA FULLSHANGWEBLOG 


Na.Alex Sonna,Dodoma

Balozi wa Japani nchini Sinichi Goto ametembelea eneo la mji wa Serikali kwa dhumuni la kuona maendeleo ya ujenzi wa miondombinu pamoja na kiwanja kilichotengwa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za ubalozi huo, jiji Dodoma.

Akizungumzia ziara ya balozi huyo, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwini Kunambi, amesema kuwa zaidi ya mabalozi 20 wameshafika Dodoma kujionea maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi zao.

“Balozi wa Japan amekuja kuona eneo ambalo ubalozi wa nchi yake utajengwa, pamoja hilo amekuja miondombinu ambayo inaendelea kujengwa," ameeleza Kunambi.Aidha Kunambi amesema kuwa Jiji la Dodoma lipo kwenye ujenzi wa tanki kubwa la kuhifadhia maji kwenye eneo hilo ambalo litakuwa na ujazo wa lita milioni moja.

Hata hivyo amesema kuwa ujenzi huo utakamilika Januari mwakani kwa lengo la kusambaza maji kwenye eneo la mji wa serikali kabla ya kufikiwa na miundombinu ya Mamlaka ya Majisafi ya Jiji la Dodoma (DUWASA).Mkurugenzi huyo aliwahakikishia watumishi wanaohamia Dodoma kuwa huduma muhimu zinapatikana ikiwemo maji kwani wanazalisha lita 61,000 kwa siku huku mahitaji yakiwa lita 48,000.

Kwa upande mwingine Kunambi amesema kuwa bado wanaendelea na utatuzi wa migogoro ya ardhi ambayo imeirithi kutoka Mamlaka ya ustawishaji Makao Makuu (CDA).“Tunaendelea na utatuzi wa migogoro ya ardhi ndani ya Jiji la Dodoma, naikumbukwe masuala ya ardhi yalikuwa chini ya CDA. Rais alipovunja CDA, sasa masuala ya ardhi yote yanashughurikiwa na Jiji la Dodoma, tunahakikisha tunamaliza migogoro hii ns kuwa historia,” amesema Kunambi.

Alieleza ili kuhakikisha migogoro hiyo inamalizika walianzisha mpango wa kufanya ziara katika kata zenye migogoro ya ardhi na kuitatua kwenye eneo husika ili kujionea uhalisia.AIizitaja kata hizo ni Kikuyu Kaskazini, kikuyu kusini, Ipagala na Dodoma Makulu ambapo sasa migogoro imepungua.

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia mpunga uliovunwa tayari wa Bw. Emmanuel Paschal(kushoto) wakati alipotembelea Skimu ya Umwagiliaji ya Lower Moshi katika eneo la Mabogini ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua na kuhimiza shughuli za kimaendeleo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
20
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia mpunga uliovunwa tayari wa Bw. Emmanuel Paschal(kushoto) wakati alipotembelea Skimu ya Umwagiliaji ya Lower Moshi katika eneo la Mabogini ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua na kuhimiza shughuli za kimaendeleo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
21
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi wa Uru Kusini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Polisi Uru. Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wakulima wa mpunga alipotembelea Skimu ya Umwagiliaji ya Lower Moshi katika eneo la Mabogini ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua na kuhimiza shughuli za kimaendeleo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wakulima wa mpunga alipotembelea Skimu ya Umwagiliaji ya Lower Moshi katika eneo la Mabogini ikiwa sehemu ya ziara yake ya kukagua na kuhimiza shughuli za kimaendeleo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia aina mbali mbali za kahawa wakati wa maandalizi ya kujaribiwa kwenye maabara ya shamba ya Kahawa la Kilimanjaro Plantation Ltd. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia aina mbali mbali za kahawa wakati wa maandalizi ya kujaribiwa kwenye maabara ya shamba ya Kahawa la Kilimanjaro Plantation Ltd. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
6
Sehemu ya Wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika uwanja wa Polisi Uru Kusini.Makamu wa Rais yupo mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za Maendeleo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
9
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Mhe. Anthony Komu wakati wa mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Polisi Uru, kulia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
1014
Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Anne Kilango Malecela akisalimia wakazi wa Uru wakati wa mktano wa hadhara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye yupo mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
16
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi wa Uru Kusini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Polisi Uru.Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAKUTANA NA KAMATI YA BUNGE YA BAJETI KUJADILI MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA JIJINI DODOMA

$
0
0

 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akiteta jambo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Frolens Luoga, nje ya viwanja vya Bunge, Jijini, Dodoma, baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, kujadili  Muundo na Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018, unaotarajiwa kuwasilishwa Bungeni siku chache zijazo.
2
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. David Silinde (Mb), akimwonesha Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), kijitabu cha Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha, wakati kamati hiyo ilipokutana na Waziri huyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Adelardus Kilangi (Mb)  na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga, kujadili Muundo na Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018, utakaowasilishwa kwa hati ya Dharura katika Bunge linaloendelea Jijini Dodoma
3
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Geroge Simbachawene (Mb), akizungmza jambo wakati kamati yake ilipokutana na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Dkt. Adelardus Kilangi (Mb) na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga, na wataalamu wa Sera na Uchumi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma, kujadili Muundo na Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018.
4
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Andrew Chenge (Mb) na Prof. Anna Tibaijuka (Mb) wakifuatilia kwa makini mjadala wa Muundo na Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018, unaotarajiwa kuwasilishwa na Wizara ya Fedha na Mipango, Bungeni, Jijini Dodoma, siku chache zijazo.
5
Baadhi ya viongozi waandamizi kutoka Idara ya Sera ya Wizara ya Fedha na Mipango, wakiongozwa na Kaimu Kamishna wa Idara hiyo Bw. Mgonya Benedicto (kulia) wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, ilipokutana na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Dkt. Adelardus Kilangi (Mb), na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga, Bungeni Jijini Dodoma, kujadili muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha unaotarajiwa kuwasilishwa na Wizara ya Fedfha na Mipango, Bungeni, Jijini Dodoma, siku chache zijazo
6
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Albert Obama na Mbunge wa Viti Maalum Dkt. Swale Semesi wakisikiliza hoja mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha Muundo na Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedfha ya Mwaka 2018, unaotarajiwa kuwasilishwa kwa Hati ya Dharura katika vikao vya Bunge vinavyoendelea Jijini Dodoma.
7
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akizungumza Jambo mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya  Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. George Simbachawene (Mb),  wakati wa kujadili Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha ya Mwaka 2018, unaotarajiwa kuwasilishwa Bungeni siku chache zijazo.
8
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Dkt. Adelardus Kilangi (Mb) (katikati) na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga, wakiandika hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, kuhusu Muswada wa Sheria Ndogo za Fedha unaotarajiwa kuwasilishwa Bungeni Jijini Dodoma, siku chache zijazo
9
Mjumbe wa Kamati ta Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hussen Bashe, akichangia hoja wakati kamati hiyo ilipokutana na Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kujadili Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha ya Mwaka 2018,  unaotarajiwa kuwasilishwa Bungeni wakti wa vikao vya Bunge vinavyoendelea Jijini Dodoma
10
Mjumbe wa Kamati ta Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. David Silinde (Mb),  akichangia hoja wakati kamati hiyo ilipokutana na Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kujadili Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha ya Mwaka 2018,  unaotarajiwa kuwasilishwa Bungeni wakti wa vikao vya Bunge vinavyoendelea Jijini Dodoma.
11
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Dkt. Adelardus Kilangi (Mb) akitoa ufafanuzi wa masuala kadhaa ya kisheria baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, kujadili Maudhui ya Muswada wa Sheria ya Huduma Ndogo ya Fedha ya Mwaka 2018, unaotarajiwa kuwasilishwa Bungeni siku chache zijazo.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Fedha na Mipango)

USHIRIKIANO WA ZUKU NA MOBISOL WALETA FURAHA MAENEO YASIYOFIKIWA UMEME

$
0
0
 Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Mobisol Tanzania , Seth Matemu (wa pili kushoto) akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa hafla ya Kuadhimisha miaka 2 ya ushirikiano wa kibiashara kati ya Zuku Satellite Tanzania na Mobisol Tanzania . Kushoto ni Meneja Mauzo wa Zuku Satellite Tanzania, Nicolaus Kizenga ,Watatu ni Meneja Mkuu wa wa Zuku Satellite Tanzania, Thomas Wenanga, na Meneja Bidhaa wa Mobisol Tanzania, Lynda Okolo na Meneja Chapa kutoka Zuku.Veneranda Raphael.
 Meneja Mauzo kutoka Zuku Satellite Tanzania, Nicolaus Kizenga( Kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari( hawapo pichani)kuhusiana na miaka miwili ya ushirikiano wa kampuni hiyo na Mobisol wa pili kushoto ni Mkuu wa Masoko wa Mobisol Tanzania, Seth Matemu ,Meneja Mkuu wa Zuku Satellite nchini Tanzania, Thomas Wenanga,Meneja Bidhaa wa Mobisol Tanzania, Lynda Okolo na Meneja chapa wa Zuku TV Veneranda Raphael.
 Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Mobisol Tanzania, Seth Matemu ( wa pili Kushoto ) na Meneja Mkuu wa Zuku Satellite Tanzania, Thomas Wenanga, wakipongezana wakati wa hafla ya Kuadhimisha miaka 2 ya ushirikiano wa kibiashara wa kampuni hizo . ( Kushoto) ni Meneja Mauzo wa Zuku TV Tanzania, Nicolaus Kizenga, Meneja Bidhaa wa Mobisol Tanzania, Lynda Okolo na Meneja chapa wa Zuku TV , Veneranda Raphael (kulia).
Waandishi wa habari wakifuatilia matukio wakati wa mkutano huo *Wananchi wafurahia umeme wa jua wa Mobisol na kuangalia Zuku TV Makampuni ya Mobisol Tanzania na Zuku Satellite Tanzania, yameeleza dhamira ya kuendelea kuboresha maisha wa wakazi wa maeneo ambayo hayajafikiwa na umeme wa gridi ya taifa kupitia ushirikiano wake . 

Mobisol imekuwa ikisambaza umeme wa jua maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji sambamba na kuuza vifaa vya kisasa vinavyotumia nishati hiyo, wakati kampuni ya Zuku Satellite Tanzania kupitia ushirikiano huu imekuwa ikiunganisha wateja wanaotumia umeme wa Mobisol na king’amuzi cha Zuku kwa vifurushi vya gharama nafuu vinavyowezesha kuona vipindi vya kielimu,burudani na michezo sambamba na kupatiwa vifaa na kupata huduma ya kufungiwa vifaa hivyo bure. 

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar e Salaam wakati wa kuadhimisha miaka miwili ya ushirikiano baina ya makampuni hayo, Mkuu wa Masoko wa Mobisol Tanzania,Bw.Seth Matemu, alisema 

“Tunajivunia kuendelea kuunganisha wateja katika umeme wetu sambamba na kuwapatia huduma ya vifaa bora vya kisasa vinavyotumia nishati hii.Tumeshirikiana na kampuni Zuku kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma mbalimbali wanazohitaji watumiaji wa umeme mahali popote wanapokuwa”. 

Matemu ,alisema kuwa televisheni hivi sasa imekuwa zaidi ya kifaa cha kuleta furaha na burudani bali ni chombo cha kuelimisha pia kuwezesha kupata mapato kwenye maeneo ya mijini na vijijini,pia inatumika kwenye mabaa,migahawa,vituo vya sinema vijijini na kwa matumizi ya familia “Wakazi wa maeneo ya vijijini wanayo haki ya kupata taarifa na burudani kama wenzao wa mijini,wanastahili kupata burudani na kuishi maisha ya kisasa nasi tumejipanga kukidhi mahitaji yao”. Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Zuku satellite Tanzania, Thomas Wenanga, alisema

 “Tunayo furaha kushirikiana na Mobisol kuweza kuwafikia watanzania kupata huduma ya kuona televisheni yetu ya kulipia ya Zuku.Katika kipindi cha miaka 2 ya ushirikiano tumepata mafanikio ya kuwafikia wananchi wanaoishi vijijini sambamba na kuwawezesha kupata burudani ya vipindi vyetu na tunawahakikishia wateja wetu kuwa tutaendelea kuwaletea mambo mazuri zaidi kupitia ushirikiano huu”. 

 Mobisol inawezesha kufunga umeme wa jua wenye nguvu ya 10 MW ambao umefikia kaya zaidi ya 500,000 katika ukanda wa Afrika Mashariki,pia inauza vifaa vya kisasa vinavyotumia nishati hiyo.

Lugola awaondoa madarakani Kaimu RPC, Mkuu wa Operesheni Mkoa, OCD, Mkuu wa Intelejinsia Uvinza

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Uvinza

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro kuwaondoa katika madaraka Mkuu wa Utawala wa Jeshi l aPolisi Mkoa wa Kigoma ambaye alikuwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa, Mkuu wa Operesheni wa Mkoa huo, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Uvinza na Mkuu wa Intelejinsia wa wilaya hiyo.

Pia Lugola ameagiza askari wote wa kituo cha polisi Mpeta na Nguruka wilayani vinza wwahamishwe haraka iwezekanavyo katika vituo hivyo.

Lugola ametoa kauli nzito kwa kuwaondoa katika nyadhifa zao maafisa wa juu wa jeshi hilo, kutokana na mapungufu aliyoyaona katika operesheni iliyofanyika mwezi uliopita ya kuwaondoa wakulima na wafugaji waliovamia ranchi za Taasisi ya NARCO ambao ipo chini ya Wizra ya Mifugo, ambayo katika operesheni hiyo askari polisi wawili na raia wawili waliuawa.

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kitongoji cha Mwanduhubandu, Kijiji cha Mpeta Wilayani Uvinza, leo, Waziri Lugola alisema viongozi hao wa Polisi wameshindwa kuifanya kazi hiyo kwa umakini ndio mana kulikua upungufu mkubwa katika operesheni hiyo, hivyo damu za waliouawa zinakua juu ya hao viongozi wa polisi mkoa na wilaya.

“Kutokana na hali hiyo, namuagiza IGP Sirro kuwaondoa kwenye madaraka hao wote niliowataja ifikapo kesho, na kesho Jumatatu nitakapo kuwa Dodoma nitakutana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ili kuona hatua nyingine za kinidhamu zitakazochukulia kwa hao niliowataja,” alisema Lugola. Waziri Lugola aliongeza kuwa, Jeshi la Polisi halina nia ya kuua mtu, kumuonea mtu, kudhulumu mtu lakini pale inapotokea jeshi hilo limeshindwa kutekeleza wajibu wake vizuri, lazima yeye Waziri achukue hatua.

Hata hivyo, Lugola alisema Jeshi la Polisi halipaswi kuvunjika moyo, litaendelea kufanya operesheni za mara kwa mara katika kuhakikisha linapambana na uhalifu, kwa hayo ambayo yanayojitokeza hayana nafasi ya kuwakatisha tamaa wala kuwavunja moyo.

“Mimi Waziri wa Wizara hii, dhamana yangu na haya ninayoyafanya, vyombo vyangu vya ulinzi na usalama ninavyovisimamia msinione mimi kama mwanasiasa, msichukulie maagizo yangu na matamko yangu kama ya mwanasiasa, atyakaye jidanganya hivyo, itakula kwake,” alisema Lugola.

Lugola alioagiza waondolewe madaraka ni Mkuu wa Utawala wa Jeshi l aPolisi Mkoa wa Kigoma ambaye alikuwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wakati operesheni hiyo ilipotokea, ACP Simon Ngowi, Mkuu wa Operesheni wa Mkoa huo, SP Msembele, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Uvinza, SSP Mwakisambwe, na Mkuu wa Intelejinsia wa wilaya hiyo, InspektaDotto Daudi.

ZIARA YA PROF.KAMUZORA KATIKA MRADI WA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA (LIC) KIGOMA

$
0
0


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora akizungumza jambo wakati wa kikao na uongozi wa Mkoa wa Kigoma alipotembelea katika ofisi hizo ili kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi wa kuboresha mazingira ya biashara  (Local Investment Climate -LIC) alipoambatana na uongozi wa Baraza la Taifa la Biashara nchini.
????????????????????????????????????
Afisa Uvuvi Mwandamizi Bw.Azizi Daudi akimuonesha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora namna dagaa wanavyoanikwa katika Chanja ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuwahifadhi kwa ajili ya kuuza wakati alipofanya ziara katika Mwalo wa Kibirizi Kigoma.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kutoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa LIC Kigoma wakinukuu maelekezo ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora (hayupo pichani) wakati wa ziara yake Kigoma.
????????????????????????????????????
Afisa wa Baraza la Biashara la Taifa na Mratibu wa shughuli za Mabaraza ya Biashara Kigoma Bw. Ano Mwamsiku akieleza kusuhu utekelezaji wa mabaraza ya biashara katika mkoa huo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora alipofanya ziara mkoani hapo mapema mwishoni mwa wiki hii.
????????????????????????????????????
Afisa Biashara na Mratibu wa Mradi wa LIC Bw.Festo Nashoni akitoa ufafanuzi kuhusu ujenzi wa Kituo Kimoja cha Biashara (One Stop Business Center) kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora alipofanya ziara kituoni hapo.
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mradi wa LIC pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji.
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora akiteta jambo na Msimamizi wa Mradi wa LIC Kigoma Bw. Flemming Oslen wakati wa ziara yake katika mradi huo.
????????????????????????????????????
Afisa Uvuvi Mwandamizi Bw.Azizi Daudi akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora kuhusu gati la wavuvi katika eneo la Mwalo wa Kibirizi alipofanya ziara eneo hilo.
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Kibirizi mkoani Kigoma alipotembelea ili kuona mazingira ya biashara ikiwa ni sehemu ya wanufaika wa mradi wa LIC.
????????????????????????????????????
Afisa Biashara na Mratibu wa Mradi wa LIC Kigoma Bw.Festo Nashoni akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora kuhusu ukarabati wa vyoo vya wafanyabiashara watakao tumia soko la usiku lililokarabatiwa na mradi wa LIC mkoa wa Kigoma.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Daraja la Wami Kukamilika ndani ya Miezi 24

$
0
0
Frank Mvungi- MAELEZO 

Serikali kutumia zaidi ya Bilioni 67 katika ujenzi wa Daraja la mto Wami na linatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 24 na hivyo kuchochea ukuaji wa sekta ya uchukuzi hapa nchini. 

Akijibu swali la kuhusu ujenzi wa Daraja hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Elias Kuandikwa amesema kuwa kwa sasa Mkandarasi yupo kwenye maandalizi ya kuanza ujenzi ambapo baada ya maandalizi hayo kazi ya ujenzi wa daraja utaanza ukigharimiwa na Serikali kwa asilimia 100. 

“ Wakati wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Mkandarasi Power Construction Corporation kutoka China walisaini mkataba wa ujenzi wa daraja hili tarehe 28/05/2018 hivyo tayari kazi ya ujenzi inatarajiwa kuanza wakati wowote”; Alisisitiza Mhe. Kuandikwa 

Akifafanua Mhe. Kuandikwa amesema kuwa Daraja jipya la Wami litakuwa na urefu wa mita 513.5 na upana wa mita 11.85 na litajengwa umbali wa mita 670 pembeni ya daraja la zamani upande wa kulia ukiwa unaelekea Segera. 

Aliongeza kuwa upana wa daraja hilo umezingatia sehemu ya barabara, waenda kwa miguu pamoja na vizuizi kwa ajili ya usalama. Daraja hilo litakuwa kichocheo cha maendeleo katika mikoa ya Kaskazini kwa kuchochea shughuli za usafirishaji na uchukuzi kwa njia ya barabara. 

Daraja la sasa la mto Wami lenya urefu wa mita 88.75 liko mkoa wa Pwani na lilijengwa mwaka 1959 na ni kiungo muhimu kutoka Chalinze kwenda mikoa ya ukanda wa Kaskazini mwa nchi yetu na nchi za jirani. 
Daraja la Wami

PUMA ENERGY TANZANIA YATUMIA KLABU YA WANAFUNZI USALAMA BARABARANI KUTOA ELIMU, ZAWADI ZA MADAFTARI,MABEGI NA KALENDA KWA MADEREVA

$
0
0
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania, Dominic Dhanah akishuhudia wakati wanafunzi kutoka Klabu ya Usalama barabarani ya Shule ya Msingi Bunge Raymond Chuwa kulia na Abbas Abdalla wa darasa la tano wakitoa elimu ya usalama barabarani na kugawa zawadi za madaftari na mabegi kwa dereva Mary Carneiro aliyefika kwenye kituo cha mafuta cha Puma Upanga jijini Dar es salaam ili kujipatia huduma ya mafuta aliyesimama nyuma katikati ni Boniface Mench Meneja Usalama Kazini Puma.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania, Dominic Dhanah akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari mara baada ya kushuhudia wanafunzi hao wakati wakitoa elimu ya Usalama barabarani kwa madereva.


Mwanafunzi Samira Jaffari akitoa elimu ya usalama barabarani na kugawa zawadi ya madaftari kwa mmoja wa Madereva waliofika kwenye kituo cha mafuta cha Puma Upanga ili kujipatia huduma ya mafuta.
Loveness Hoyange Meneja Rasilimali Watu Kampuni ya Puma Energy Afrika Mashariki na Boniface Mench Meneja Usalama Kazini Puma wakikabidhi zawadi mbalimbali za Mabegi, Madaftari na Kalenda kwa wanafunzi wa Kalabu ya Usalama Barabarani kutoka shule ya msingi Bunge ili kugawa kwa madereva wakati walipokuwa wakitoa elimu ya usalama barabarani katika kituo cha mafuta cha Puma Energy Upanga jijini Dar es salaam.
Loveness Hoyange Meneja Rasilimali Watu Kampuni ya Puma Energy Afrika Mashariki akiwaangalia wanafunzi Samira Jaffari na Ruqsaina Sultan wa klabu ya Usalama Barabarani shule ya Msingi Bunge wakati walipokuwa akitoa elimu ya usalama barabarani kwa madereva katika kituo cha mafuta cha Puma Upanga jijini Dar es salaam
Baadhi ya wanafunzi wa klabu hiyo wakiendelea kutoka elimu ya usalama barabarani kwa madereva na kutoa zawadi za Mabegi, Madaftari na Kalenda.
Madereva mbalimbali wakijaza mafuta katika kituo hicho na kupata elimu kutoka kwa wanafunzi hao.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania, Dominic Dhanah akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi na wanafunzi wa klabu ya usalama barabarani kutoka shule ya msingi Bunge jijini Dar es salaam.
....................................................................................

*Lengo ni kukumbusha na kusisitiza umuhimu wa wadau kuzingatia sheria za usalama barabarani, wanafunzi watoa neno

KLABU ya Usalama barabarani ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge wametoa elimu ya usalama wa barabarani kwa madereva wa magari na bodaboda kuzingatia sheria za usalama barabarani haswa vivuko vya watembea kwa miguu ili kuepusha ajali na vifo.

Pia wametoa elimu hiyo wanafunzi hao wametoa zawadi ya madaftari,kalenda na mabegi ya shule yenye jumbe mbalimbali zinahusu masuala ya usalama barabarani kwa madereva mbalimbali kama sehemu ya kuhakikisha elimu ya usalama barabarani inafika kila mahali.

Wanafunzi hao 18 ambao ni mabalozi wa usalama barabarani kutoka kwenye Klabu hiyo wametoa elimu hiyo na zawadi hizo Novemba 10, 2018 wakiwa kwenye Kituo cha Mafuta cha Puma kilichopo Upanga jijini Dar es Salaam ambapo madereva waliofika kuweka mafuta walikuwa wakipewa elimu hiyo inayohusu usalama barabarani.

Akizungumza wakati wa utoaji elimu kwa madereva, Rosenice Senyandumi ambaye ni Mwanafunzi wa shule hiyo amesema ajali za barabarani zimekuwa zikikatisha uhai wa binadamu wasio na hatia wakiwemo wanafunzi na mara nyingi huchangiwa na madereva wazembe.

"Ajali za barabarani zinapunguza nguvu kazi ya Taifa na kuathiri watoto kwa kuwa wengi hupoteza wategemezi wao na wakati mwingine watoto wenyewe kupoteza maisha au kupata ulemavu wa kudumu kutokana na ajali," amesema.

Mwanafunzi huyo amesema kutokana na athari na madhara yanayotokana na ajali Kampuni ya mafuta Puma nchini Tanzania kupitia programu yake ya Usalama Barabarani imeamua kutoa elimu ya usalama kwao kupitia Shirika ka Amend ambao jukumu lao kufundisha wanafunzi na wadau wengine kuhusu umuhimu wa usalama na kisha wao kama mabalozi wa elimu hiyo nao wanaitoa kwa wengine.

Amefafanua imebainika asilimia kubwa ya ajali za barabarani huchangiwa na uzembe wa madereva na visababishi ni pamoja na ulevi wakati wa safari, uchovu, matumizi ya simu wakati wa kuendesha na kutozingatia alama za barabarani, hivyo wameamua kutoa elimu hiyo kama wanafunzi ili kuhakikisha tatizo la ajali za barabarani linakoma.

Kwa upande wake, Kassim Juma ambae ni dereva aliyepatiwa elimu ya usalama wa barabarani na kupewa zawadi ya begi la shule na kalenda amesema wanafunzi hao wameonesha uzalendo na wanapaswa kuungwa mkono ili kuwafikia madereva wengi zaidi na kuwapatia elimu ya usalama wa barabarani.

"Nawapongeza hata walioanzisha wazo la kuwawezesha wanafunzi hawa kutoa elimu kwa kuwa tunafahamu kwamba misingi bora ya elimu huanzia chini, hivyo watoto hawa watakuwa ni mabalozi bora wa vizazi vijavyo," amesema.

Awali Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania, Dominic Dhanah amesema kampuni hiyo imedhamiria kuhakikisha inashiriki kikamilifu katika masuala ya usalama barabarani ili kudhibiti ajali.

Amesema mwaka 2013 baada ya kugundua kwamba watoto wapo hatarini zaidi walianza kutoa elimu ya usalama wa barabarani katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Geita na Ruvuma na mwaka juzi walianzisha klabu ya usalama wa barabarani katika shule ya msingi Bunge.

"Tunahitaji kuwa na jamii ambayo inaheshimu sheria za usalama barabarani, na kwa kupitia wanafunzi hao ambao wamepewa elimu ya usalama barabarani wamekuwa wakieneza elimu hiyo kwa wadau wengine kuhakikisha sote kwa pamoja tunapunguza ajali za barabarani," amesema.

Wakati huo huo Meneja wa Usalama Kazini wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Boniface Menchi amesema wamekuwa wakitoa elimu kwa shule ambazo zipo hatarini zaidi zilizopo pembezoni mwa barabara.

Maandalizi yakamilika, watoto 10 kupandikizwa vifaa vya usikivu Muhimbili

$
0
0









Mmoja wa wazazi akiwa kwenye kikao leo cha mwisho katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) cha maandalizi ya kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto 10 wenye matatizo ya kusikia.



Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Masikio, Pua na Koo kutoka nchini Misri, Prof. Lobna El Fiky akijadili jambo kwenye kikao cha maandalizi ya kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto wenye matatizo ya kusikia.



Kulia ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Masikio, Pua na Koo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Shaban Mawalla akitoa taarifa ya mmoja wa watoto wenye tatizo la usikivu kwenye kikao hicho. Katikati ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Masikio, Pua na Mkoo wa Muhimbili, Dkt. Edwin Liyombo, mtaalam wa usikivu, Fayaz Jaffer na kushoto ni wazazi wakiwa kwenye kikao hicho leo.



Wazazi wakifuatilia mjadala kwenye kikao hicho leo



Watoto nao hawakuwa nyuma kwani walifika kwenye kikao hicho cha maandalizi ya kupandikizwa vifaa vya usikivu.



Wataalam wakiwa katika picha ya pamoja na wazazi wa watoto ambao watafanyiwa upasuaji wa kupandikizwa vifaa vya usikivu kuanzia Novemba 12 hadi 16, 2018

………………………………………………………………………..

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),kuanzia Novemba 12 hadi 16, 2018 inatarajia kufanya upasuaji wa kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto 10 ambao wana matatizo ya kusikia baada ya kukamilika kwa maandalizi ya mwisho.

Watoto hao watapandikizwa vifaa vya usikivu baada ya wataalam kuwafanyia uchunguzi wa kina pamoja na wazazi kupatiwa ushauri wa kitaalamu. Baada ya watoto hao 10 kupandikizwa vifaa vya usikivu, jumla ya watoto watakaokuwa wamepandikizwa vifaa hivyo itafikia 21 tangu kuanza kwa upasuaji huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Daktari Bingwa wa upasuaji wa Masikio, Pua na Koo wa hospitali hiyo Dkt. Edwin Liyombo amesema maandalizi kwa ajili ya kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto hao yamekamilika.

Dkt. Liyombo amesema kwamba leo wamefanya kikao cha pamoja na wazazi wa watoto hao kwa ajili ya kuwaandaa na kuwapatia maelekezo jinsi ya kuwa karibu zaidi na watoto hao ili waweze kusikia vizuri na kuzungumza baada ya kupandikizwa vifaa vya usikivu.

“Wazazi wanatakiwa kuwafutilia kwa karibu watoto baada ya kupandikizwa vifaa vya usikivu. Zinahitajika nguvu za ziada ili watoto waweze kuzungumza vizuri na kusikia,” amesema Dkt. Liyombo.

Katika mkutano huo wazazi wa watoto hao wameonyesha imani kunbwa kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa za kuhakikisha Watanzania wanapatiwa huduma bora za kibingwa.

Upandikizaji wa vifaa hivyo utafanywa na timu ya wataalam 10 wa Muhimbili na wataalam wawili kutoka Misri akiwamo Prof. Lobna El Fiky, Mohamed El Disouky.

PANGANI MJINI KUANZISHA CLUB YA MAZOEZI

$
0
0

 Afisa Tarafa Pangani Mjini Bi. Zuhura Abdulrahmani wa pili kulia akiwa kwenye kikosi hicho leo amekutana na kufanya kikao na kamati ya awali kwa ajili kuanzisha Jogging Club ya Pangani mjini.
 Kikao kikiendelea 
 Afisa Tarafa Pangani Mjini Bi. Zuhura Abdulrahmani wa tatu kutoka kushoto aliyevaa kilemba akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau hao mara baada ya kumaliza kikao hicho leo kwa ajili ya kuanzisha Jogging Club ya Pangani mjini wa tatu kutoka kushoto ni Mohamed Hamie kutoka Pangani FM








Afisa Tarafa Pangani Mjini Bi. Zuhura Abdulrahmani leo amekutana na kufanya kikao na kamati ya awali kwa ajili kuanzisha Jogging Club ya Pangani mjini.

Lengo la kuanzishwa jogging Club hiyo ambayo itakuwa ni ya kwanza Pangani Mjini ni kuhamasisha mazoezi kwa ajili ya kuboresha afya, kwa mustakabali wa maendeleo ya Pangani. 

Kamati hiyo ambayo imejumuisha takribani wajumbe 13, imefanya kikao chake cha kwanza katika ukumbi wa halmashauri wa wilaya, ambapo mbali na kuwa na lengo kuu pia ilikubaliana kuwa na malengo mengine madogo madogo. Malengo hayo ni pamoja na kushiriki katika shughuli za kijamii, kuunganisha vijana pamoja na kubadilishana mawazo, pia kusukuma ajenda mbalimbali za kimaendeleo za serikali. 
 
Bi Zuhura ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho, amepokea mapendekezo kadhaa ya uanzishwaji wa jogging hiyo kuwa ni pamoja na vifaa vya mazoezi ikiwepo mipira, jezi, muziki, pamoja na mkufunzi. 

Jogging Club hiyo ambayo imepewa jina la PANGANI JOGGING CLUB inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni punde baada ya kukamilisha utaratibu wa usajili.

TAASISI YA IMETOSHA YATOA MSAADA KWA MWENYE UALBINO ALIYEPATA UPOFU WA MACHO SHINYANGA

$
0
0

Taasisi ya Imetosha ya Jijini Dar es salaam imemtembelea na kumpatia msaada bwana Charles Kulwa Jagadi (41) mwenye Ualbino mkazi wa kijiji cha Mhunze kata ya Kishapu wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ambaye amepata upofu wa macho kutokana na ugonjwa wa saratani ya macho unaomsumbua uliopelekea jicho moja kung’olewa.
Mtendaji Mkuu wa Imetosha Foundation,Henry Mdimu aliyefika nyumbani kwa Jagadi leo Jumapili Novemba 11,2018 amesema taasisi yake imeguswa na hali ngumu ya maisha anayopitia Jagadi hivyo kuamua kumjengea kibanda cha kufanyia biashara ya mkaa ili kumsaidia katika maisha yake.
Alisema Imetosha Foundation kwa kushirikiana na Dar Marathon Club ya jijini Dar es salaam wameamua kuchangishana fedha kwa ajili ya kumsaidia Jagadi ili aweze kuendesha familia yake yenye watoto sita wote wakiwa na ualbino.
“Niliona picha ya Jagadi mtandaoni,baada ya mmoja wa watu wenye mapenzi mema kuipost kuonesha jinsi ndugu yetu anavyopitia wakati mgumu baada ya kupata upofu wa macho,nimeamua kuja kumuona na tayari tumemjengea kibanda kwa ajili ya kufanyia biashara ya mkaa ambayo amekuwa akifanya ili kupata kipato kuendesha familia yake”,alieleza Mdimu.
“Nimetoka Dar es salaam kuja kumuona na kujionea hali halisi ya maisha yake,huyu ni baba mwenye mke na watoto sita,sasa haoni,tunaamini kibanda hiki kitamsaidia kuingiza kipato ili kuisaidia familia hii”,aliongeza Mdimu.
Alisema pia wamempatia magunia 18 ya mkaa kwa ajili ya biashara na kuahidi kuwasomesha watoto wawili kati ya 6 na kuahidi kutafuta kiwanja kwa ajili ya kuijengea nyumba familia hiyo ambayo inaishi kwenye nyumba ya kupanga.
Kwa upande wake,Jagadi aliishukuru taasisi ya Imetosha na Dar Marathon Club kwa msaada waliompatia na kubainisha kuwa banda hilo litamsaidia kupata pesa kwa ajili ya kuendeshea familia yake ambayo imekuwa ikikabiliwa na uhaba wa chakula na kusababisha wakati mwingine kushinda na kulala na njaa.
“Nawashukuru sana kwa ufadhili wenu,kutoa ni moyo,natambua wapo watu wengi wana pesa na ninavyopata watu wa kunisaidia Napata faraja,Mungu awabariki sana”,alisema Jagadi.
Charles Kulwa Jagadi (41) amesema alianza kusumbuliwa na upele kwenye jicho lake la kushoto mwaka 2005,mwaka 2015 akaanza kupatiwa matibabu katika hospitali mbalimbali ikiwemo KCMC,Bugando na Julai 22,2018 jicho lake liling’olewa katika hospitali ya taifa Muhimbili kwa kile alichoelezwa na Daktari kuwa ni Saratani ya Jicho.
Jicho lake jingine pia limepata upofu hivyo amejikuta hafanyi tena shughuli za uzalishaji mali kama ile kazi ya kuosha magari aliyokuwa anaifanya mwanzo ambayo ilikuwa inamsaidia kupata pesa kwa ajili ya kuendeshea familia yake.
Kulia ni Charles Kulwa Jagadi (41) mwenye Ualbino mkazi wa Kata ya Mhunze wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga akimpokea Mtendaji Mkuu wa Imetosha Foundation,Henry Mdimu leo Jumapili Novemba 11,2018 kumtembelea.Nyuma ni kibanda cha biashara ya mkaa kilichojengwa kwa ufadhili wa Imetosha Foundation na Dar Marathon Club kwa ajili ya Charles Kulwa Jagadi - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mtendaji Mkuu wa Imetosha Foundation,Henry Mdimu (wa pili kulia) akijitambulisha kwa Charles Kulwa Jagadi (kulia).Wa kwanza kushoto ni mke wa Jagadi Esther Shija akifuatiwa na Mratibu wa Imetosha Foundation Kanda ya Ziwa,Janeth Chijanga.
Charles Kulwa Jagadi (kulia) akieleza magumu aliyopitia hadi sasa amepata upofu wa macho.
Mtendaji Mkuu wa Imetosha Foundation,Henry Mdimu akizungumza na familia ya Charles Kulwa Jagadi.
Mtendaji Mkuu wa Imetosha Foundation,Henry Mdimu akimpatia fedha Charles Kulwa Jagadi kwa ajili ya kununulia mkaa na kununua mahitaji mengine ya familia.
Charles Kulwa Jagadi (kushoto) akimshukuru Mtendaji Mkuu wa Imetosha Foundation,Henry Mdimu kwa kumtembelea na kumjengea kibanda kwa ajili ya biashara ya mkaa.
Mtendaji Mkuu wa Imetosha Foundation,Henry Mdimu akipokea maelezo kutoka kwa fundi Paschal Manumbu John kuhusu ya ujenzi wa kibanda cha kuuzia mkaa cha Charles Kulwa Jagadi.
Muonekano wa kibanda cha kuuzia mkaa cha Charles Kulwa Jagadi kilichojengwa kwa ufadhili wa Imetosha Foundation kwa kushirikiana na Dar Marathon Club.
Muonekano wa kibanda cha kuuzia mkaa cha Charles Kulwa Jagadi.- Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

KATIBU MKUU CCM,DK.BASHIRU ATEMBELEA ENEO LA UWEKEZAJI LA UHURU MEDIA GROUP

$
0
0

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ali (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa jiji la Dodoma,Godwin Kunambi (kulia) alipotembelea shamba linalomilikiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG) inayosimamia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na redio Uhuru,ikiwa ni mkakati wa kuanza uwekezaji wa ambapo kutajengwa mji wa kisasa pamoja na makao makuu ya ofisi za vyombo vya habari vya chama.
Mlinzi wa shamba hilo Zebeayo Lemgoha (kushoto) akimueleza jambo Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ali alipotembelea shamba linalomilikiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG) inayosimamia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na redio Uhuru,ikiwa ni mkakati wa kuanza uwekezaji wa ambapo kutajengwa mji wa kisasa pamoja na makao makuu ya ofisi za vyombo vya habari vya chama.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ali ,akizungumza na Mlinzi wa shamba hilo Zebeayo Lemgoha (kushoto) ni Mkurugenzi wa jiji la Dodoma,Godwin Kunambi alipotembelea shamba linalomilikiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG) inayosimamia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na redio Uhuru,ikiwa ni mkakati wa kuanza uwekezaji wa ambapo kutajengwa mji wa kisasa pamoja na makao makuu ya ofisi za vyombo vya habari vya chama
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ali (kulia) akimuonesha Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi walipofanya ziara ya kutembelea shamba linalomilikiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG) inayosimamia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na redio Uhuru,ikiwa ni mkakati wa kuanza uwekezaji wa ambapo kutajengwa mji wa kisasa pamoja na makao makuu ya ofisi za vyombo vya habari vya chama
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ali akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kutembelea shamba linalomilikiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG) inayosimamia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na redio Uhuru,ikiwa ni mkakati wa kuanza uwekezaji wa ambapo kutajengwa mji wa kisasa pamoja na makao makuu ya ofisi za vyombo vya habari vya chama
Mlinzi wa shamba hilo Zebeayo Lemgoha (kushoto) akionesha alama ya Shamba linapokomea kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ali aliye upande wa kulia huku mwaandishi wa Uhuru Gazeti pamoja na Mzalendo,Mussa Yusuph (katikati) akifatilia kwa makini maelezo yanayotolewa wakati wa ziara ya kutembelea shamba linalomilikiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG) inayosimamia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na redio Uhuru,ikiwa ni mkakati wa kuanza uwekezaji wa ambapo kutajengwa mji wa kisasa pamoja na makao makuu ya ofisi za vyombo vya habari vya chama
Msimamizi Mkuu wa Vyombo vya Habari vya Chama, Ernest Sungura (katikati) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ali pamoja na Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi walipofanya ziara ya kutembelea shamba linalomilikiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG) inayosimamia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na redio Uhuru,ikiwa ni mkakati wa kuanza uwekezaji wa ambapo kutajengwa mji wa kisasa pamoja na makao makuu ya ofisi za vyombo vya habari vya chama
Baada ya kumaliza kukagua shamba linalomilikiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG) inayosimamia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na redio Uhuru,ikiwa ni mkakati wa kuanza uwekezaji wa ambapo kutajengwa mji wa kisasa pamoja na makao makuu ya ofisi za vyombo vya habari vya chama ,Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ali,akiwa na Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi wanamaliza ziara na kuanza safari ya kuondoka katika eneo hilo.
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Godwin Kunambi,akizungumza na waandishi wa habari hawapo (pichani) baada ya kumaliza ziara na atibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ali walipotembelea shamba linalomilikiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG) inayosimamia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na redio Uhuru,ikiwa ni mkakati wa kuanza uwekezaji wa ambapo kutajengwa mji wa kisasa pamoja na makao makuu ya ofisi za vyombo vya habari vya chama .PICHA ZOTE NA ALEX SONNA WA FULLSHANGWEBLOG,DODOMA



Alex Sonna,Dodoma


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ali, ametembele shamba linalomilikiwa na Kampuni ya Uhuru Media Group (UMG) inayosimamia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na redio Uhuru, ikiwa ni mkakati wa kuanza uwekezaji wa ambapo kutajengwa mji wa kisasa pamoja na makao makuu ya ofisi za vyombo vya habari vya chama.

Dk. Bashiru aliambatana na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, Msimamizi Mkuu wa Vyombo vya Habari vya Chama, Ernest Sungura pamoja na baadhi ya wataalam wa mipango miji.

Katibu mkuu alisisitiza umuhimu wa vyombo hivyo kuhamia Dodoma kuunga mkono uamuzi wa waasisi wa taifa pamoja na ule wa Rais Dk. John Magufuli, wa kuhamishia makao makuu ya nchi kwenye mkoa huo. "Nimekuja kuangalia eneo linalomilikiwa vyombo vya habari vya CCM kwa sababu sasa maeneo yanabadilika kuwa ya mipango miji. Tumekuja kuangalia usalama wa mipaka ili tuweze kupanga matumizi yake na vyombo vyetu viweze kuhamia Dodoma.

"Ni sehemu ya kuenzi mawazo na firka za viongozi, waasisi wa chama chetu na Baba wa taifa aliyeona mbali kwa kuichagua Dodoma kuwa Makao Makuu ya Chama na Serikali," Dk. Bashiru alisisitiza.Hata hivyo amesema kuwa tayari maombi ya kubadilisha matumizi ya eneo hilo kutoka shamba hadi kutumika kwa shughuli za kibiashara au viwanda, yameshafikishwa kwenye Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji ambaye ndie mwenye jukumu la kusimamia sheria kwani chama hakipaswi kuwa sehemu ya kuvunja sheria.

"Kwa bahati nzuri nimelikuta shamba letu lipo salama limelindwa vizuri na tumeonyeshwa mipaka kitaalam. Wito wangu kwa wananchi wa Dodoma wanaotaka kuwekeza kwa kufanya shughuli za kibiashara au makazi, waheshimu sheria za mipango miji na ardhi," amesema Dk.Bashiru

Aidha Dk. Bashiru alivitaka vyombo vinavyosimamia sheria vitende haki kwani maendelezo yote ya Jiji la Dodoma yanapaswa kufanyika kwa haki, amani na yawe kwa njia shirikishi."Naamini uongozi wa jiji na Serikali itazingatia misingi ya haki ili mipango miji ya Dodoma iwe ya mfano. Matarajio yetu ni kwamba usimamizi na utatuzi mzuri wa migogoro ya ardhi izingatie sheria na tusingepenga migogoro mingi ya ardhi kufikishwa mahakamani kwani inaweza kutatuliwa kwa njia za mazungumzo na kwa amani.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, amesema kuwa ziara ya Katibu mkuu kutembelea eneo linalomilikiwa na vyombo vya habari vya chama ni maandalizi ya awali kwa vyombo hivyo kuhama kutoka Dar es Salaam kuja Makao Makuu ya Nchi, Dodoma.Kunambi amesema kuwa Katibu mkuu alikwenda kujiridhisha kwa namna gani anaweza kuzihimiza vyombo hivyo kuhamia Dodoma. Eneo lile lipo salama lakini maeneo yanayolizunguka yana migogoro mikubwa ya ardhi.

Kunambi alifafanua kuwa migogoro hiyo imegawanyika katika makundi manne ambapo kundi la kwanza ni la wakazi waliokutwa wakiishi kabla ya mwaka 1983 lilipopimwa kwa matumizi ya mashamba na wengine walimilikishwa baada ya upimaji mwaka 1983.Alieleza kundi lingine ni la wavamizi waliongia kwenye maeneo hayo kwenye miaka ya 1990 ambao nao waliwauzia wengine ambao yatari wameshajenga makazi ya kudumu.

"Baada ya kubaini hili tumefanya mawasilianao na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kuomba kibali cha kubadili matumizi ya eneo lile kutoka mashamba hadi kuwa eneo la biashara, makazi na hoteli ili kutoa fursa kwa wananchi kuyaendeleza ambapo sasa tupo kwenye hatua za mwisho kuandaa ramani ya upimaji na mipango miji.

Mkurugenzi huyo wa jiji alifafanua hatua hiyo itasaidia kutatua migogoro iliyopo kwani vitapatikana viwanja vingi ambavyo makundi yote yatapata nafasi kwa kuzingatia sheria na taratibu za mipango miji.

Katika hatua nyingine Msimamizi Mkuu wa Vyombo vya Habari vya Chama, Ernest Sungura, amesema kuwa kazi iliyopo ni kuleta mageuzi makubwa kwenye vyombo vya habari vya chama kupitia kampuni ya Uhuru Media Group ambayo imeanza kwa mtindo wa kawaida wa kuboresha maudhui yaliyojikita kwenye ubora unaohitajika.

"UMG imejipanga kuwekeza na kuzalisha mapato yatakayotokana na huo uwekezaji ili tutumie uwekezaji huo na mapato kuvifanya vyombo vya habari vya chama viwe imara zaidi."Tumejipanga kuanzisha jiji la Uhuru Media. mipango ipo tayari tunafanya uwasilishaji kwenye vyombo hisika ndani ya chama na mara baada ya kukamilisha mchakato huo, tutaanza uwekezaji na hapo ndipo kutakuwa Makao Makuu ya Uhuru," Sungura, alibainisha.

Alieleza kuwa eneo hilo litakuwa na mitambo ya uchapaji, redio, televisheni, kumbi za mikutano, eneo la mafunzo ya namna ya kufundisha uendeshaji na usimamizi wa mikutano, biashara za hoteli na mahali ambako mandhari itabadilishwa kwa kuweka ziwa la kutengenezwa ili watu waweze kuburudika.

"Itakuwa aina ya Mlimani City iliyopo Dar es Salaam, ambayo sasa itakuwa Uhuru City iliyopo Dodoma. hilo ndilo jambo kubwa tunalokusudia kulifanya. Tutaanza mikakati ya kukusanya vyanzo vya mapato ili uwekezaji huo uanze mara moja.

Alisisitiza: "Mkakati utakuwa wa miaka 10 utakaofanyika kwa awamu ambapo tunataka tuache alama isiyofutika ndani ya miaka hiyo kwani tutakuwa na uwekezaji wa nguvu kwa ajili ya vyombo vya habari vya Uhuru.

Mlinzi wa shamba hilo Zebeayo Lemgoha,amesema kuwa amefurahishwa na viongozi wake kutembelea eneo hilo ambalo hadi sasa lipo salama na halijavamiwa. Eneo hili ni la kamapuni ya magazeti ya chama ambalo tangu mwaka 1992 nimekuwa nikililinda. Nitahakikisha litaendelea kuwa salama liweze kutumika kwa mipango iliyokusudiwa na chama chetu.

UMG kupitia magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Redio Uhuru ipo kwenye maboresho makubwa kimaudhui na kimenejimenti ikiwa ni mkakati wa kuviimarisha zaidi vyombo vya habari vya chama kupitia Msimamizi Mkuu, Sungura.

Maboresho hayo yanahusisha mageuzi ya kimuundo na kimfumo ili vyombo hivyo vitoe ushindani madhubuti katika tasnia ya habari ndani na nje ya nchi pamoja na kuimarisha vyanzo vya mapato na kusaidia vyombo vya habari kujiendesha kama taasisi kamili zinazopata faida Katika kipindi kifupi cha siku 100 tangu mkakati huo uanze kutekelezwa, tayari vyombo hivyo viimeanza kutoa ushindani mkubwa kwenye tasnia ya habari nchini.
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live




Latest Images