Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

RC MAKONDA APATIA UFUMBUZI KERO SUGU ZA WANANCHI WA BUGURUNI.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda jana amefanya ziara ya utatuzi wa kero na migogoro ya wakazi wa Buguruni ikiwemo ule wa Wananchi waliovunjiwa nyumba baada ya kujenga ndani ya eneo la reli.

RC Makonda amesema wananchi tunapaswa kuunga mkono juhudi za serikali za ujenzi wa Reli ya kisasa (standard gauge) ambayo inaenda kulifikisha taifa katika uchumi wa kati na kuitangaza Tanzania katika ramani ya Dunia hivyo amewasihi wananchi waliovunjiwa kuwa wavumilivu.

Aidha RC Makonda ameiomba kampuni hodhi ya rasilimali za reli RAHCO kuangalia uwezekano wa kuwapatia wananchi angalau njia za kupita ili kuwapunguzia mizunguko mirefu.

Katika ziara hiyo RC Makonda amemuagia Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa kumuhamisha kituo kingine mkuu wa kituo cha Polisi Buguruni kwakuwa watu anaowaongoza hawamuamini.

Hata hivyo RC Makonda ametoa siku Saba kwa kigogo wa Bodi ya Mikopo kumkabidhi bajaji kijana alietambulika kwa jina la Jafari Raphael aliegongwa na gari na kigogo huyo na kupelekea ulemavu wa kukatwa mguu mmoja pasipo kulipwa fidia yoyote na kumfanya kijana huyo kugeuka kuwa mtu wa kuomba misaada huku kigogo huyo akiendelea kula maisha na familia yake.

Pamoja na hayo RC Makonda amepatia ufumbuzi kero ya muda mrefu iliyokuwa ikiwakabili Umoja wa Madereva wa daladala buguruni Chama waliokuwa wamezuiwa kuegesha magari eneo la Buguruni station ambapo RC Makonda amewaagiza madereva hao kurudi katika eneo hilo.

Miongoni mwa kero zilizotolewa na wakazi wa buguruni ni pamoja na tozo kubwa ya uchafu, polisi jamii,ukamataji wa watu, watu kubambikiziwa kesi, migogoro ya mirathi na watu kudhulumiwa ambapo RC Makonda amezipatia majibu kero hizo papo kwa papo kwa kupigia simu kwa walengwa.


 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na Wakazi wa eneo la Buguruni jana,alipofanya ziara ya utatuzi wa kero na migogoro ya wakazi wa eneo hilo ikiwemo ule wa Wananchi waliovunjiwa nyumba baada ya kujenga ndani ya eneo la reli.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akisikiliza moja ya swali kutoka kwa mkazi wa Buguruni jana,wakati Makonda alipofanya  ziara ya utatuzi wa kero na migogoro ya wakazi wa Buguruni ikiwemo ule wa Wananchi waliovunjiwa nyumba baada ya kujenga ndani ya eneo la reli.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda  na ujumbe wake alipokuwa akiwasili maeneo ya Buguruni jana,katika ziara yake ya utatuzi wa kero na migogoro ya wakazi wa Buguruni ikiwemo ule wa Wananchi waliovunjiwa nyumba baada ya kujenga ndani ya eneo la reli.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda  akizungumza na mmoja wakazi wa Buguruni ,katika ziara yake ya utatuzi wa kero na migogoro ya wakazi wa Buguruni ikiwemo ule wa Wananchi waliovunjiwa nyumba baada ya kujenga ndani ya eneo la reli.

ARUMERU WAAZIMIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mh.Jerry muro akihutubia wananchi wa Kata ya singisi
 Dc Muro akiwa na ujumbe wake akiwa katika ziara ya utatuzi wa mgogoro wa Ardhi katika kata ya Selasi Sing’isi ambayo ina migogoro mikubwa ya Ardhi baina ya wananchi waliovamia Mashamba ya Wizara ya Kilimo pamoja na Mashamba ya wawekezaji ambayo yamesababisha madhara makubwa ya kuuwawa Kwa wananchi wawili huku mali zikiharibiwa vibaya pamoja kukosekana Kwa Amani Kwa muda wa zaidi ya miaka 5 .
 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akifafanuliwa jambo na  Afisa Mtendaji kata wa Singisi
 
Na Imma Msumba

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Cornel Muro anakusudia kupeleka Ombi Kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli la kufuta Hati za baadhi ya Mashamba makubwa ya ardhi ambayo wamiliki wake wamebainika kuwa chanzo cha kuvuruga Amani na Usalama Kutokana na kuwepo Kwa migogoro ya muda mrefu ambayo baadhi imegharimu maisha ya wananchi pamoja na uharibifu wa Mali.

Dc Muro Ametoa kauli hiyo wakati alipofanya ziara ya utatuzi wa mgogoro wa Ardhi katika kata ya Selasi Sing’isi ambayo ina migogoro mikubwa ya Ardhi baina ya wananchi waliovamia Mashamba ya Wizara ya Kilimo pamoja na Mashamba ya wawekezaji ambayo yamesababisha madhara makubwa ya kuuwawa Kwa wananchi wawili uku mali zikiharibiwa vibaya pamoja kukosekana Kwa Amani Kwa muda wa zaidi ya miaka 5 .

Mhe. Muro ambae alilazimika kutembea Kwa miguu katika Kata nzima ameshangazwa kuona wananchi wengi wenye Uwezo wa kulima wakishindwa kulima Kutokana na baadhi ya wawekezaji na wamiliki wa maeneo hayo kushindwa kuyaendeleza hatua iliyosababisha wananchi kuamua kuvamia Mashamba hayo na kulima kienyeji hatua ambayo imeibua Migogoro mikubwa ya ardhi, ambapo amesisitiza Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha Wawekezaji wanawekeza Kwa nia ya dhati na sio kuhodhi Mashamba makubwa ambayo wameshindwa kuyaendeleza na hatimae kutoa mwanya Kwa wananchi kuvamia na kisha kuibua migogoro.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara baada ya kukagua maeneo hayo katika viwanja vya chama cha Ushirika Sing’isi Mhe. Muro amesema katika hatua za awali ametumia Busara ya kumtaka Ndugu Aloyce Kimaro mmiliki wa Hotel ya Nakara kutokanyaga Eneo la Madira Sing’isi alilokuwa akitaka kubadilisha matumizi ya Ardhi hatua iliyosababisha Kuibuka Kwa vurugu kubwa zilizosababisha Vifo pamoja na uharibifu wa Mali katika Eneo hilo ambalo apo awali Ndugu Kimaro alipewa Eneo hilo na Wizara ya Kilimo Kwa ajili ya uwekezaji wa hotel Kubwa Kwa ajili ya Mkutano wa kimataifa ambapo amesema taarifa zinaonyesha kuwepo na viashiria vya uvunjifu wa Amani endapo Ndugu Kimaro atarejea katika Eneo hilo kwani taarifa za awali zinaonyesha kuwepo Kwa utata wa njia alizotumia kumilikishwa Shamba hilo na kuviagiza vyombo vya ulinzi na Usalama kuendelea kulichunguza jambo hilo Kwa umakini mkubwa

Mhe. Muro ambae aliongozana na viongozi wa kamati ya wananchi waliounda wakati wa ziara ya Mkuu wa mkoa wa Arusha ya kushughulikia migogoro ya ardhi katika kata hiyo,Dc Muro ameagiza wananchi kupewa hekari 66 kati ya hekari 92 walizokuwa wanapaswa kupewa na Halmashauri ikiwa ni sehemu ya Ardhi iliyotolewa na Wizara ya Kilimo na kuagiza mchakato wa kutafuta hekari zingine 25 zilizobaki uendelee Kwa haraka ili wananchi wapate maeneo ya Kulima hatua itakayoondoa Migogoro ya wananchi kuvuamia maeneo mengine ya Wizara ya Kilimo ambayo yanetengwa Kwa shughuli za kilimo.

Dc Muro pia amekiri kuwepo Kwa Utata wa Umiliki wa Eneo hilo kama ambavyo imejionyesha katika ziara yake na kuviagiza vyombo vya Usalama ikiwemo Takukuru kuendelea na uchunguzi ambao ulishaanza lakini safari hii ametaka uchunguzi uwe wa Kasi kidogo Kutokana na kuwepo Kwa Taarifa za awali zinaonyesha kufanyika Kwa Miamala ya Fedha kutoka Kwa Bwana Kimaro kwenda Kwa baadhi ya wananchi ambao wanatajwa kuwa vinara wa kuchochea Mgogoro huo wa ardhi ili kuondoa Amani katika kata ya Selasi Sing’isi ambapo Dc Muro alivitaka vyombo vya Usalama pia kuwachukua watuhumiwa hao wawili Kwa hatua za uchunguzi zaidi.

Akizungumza katika Mkutano wa Hadhara Diwani wa kata ya Sing’isi pamoja na viongozi wa kamati ya wananchi iliyoundwa kumaliza mgogoro huo ambao pia ulihusisha viongozi kutoka makao makuu ya Wizara ya Kilimo wote Kwa pamoja mbali na kupongeza juhudi zilizofanywa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro Kwa kumaliza mgogoro huo walikubaliana kutoa Azimio la kumaliza mgogoro huo baada ya mazungumzo ya Hekima na busara ya pande zote zinazovutana katika mgogoro huo yaliyoongozwa na kusimamiwa na Mkuu wa Wilaya Ya Arumeru Mhe. Jerry Muro ambapo wananchi walikubali kutoka katika maeneo waliyovamia ya Wizara ya kilimo, pamoja na kukubali kupokea mgao wa kwanza wa Ardhi yenye hekari 66 ambazo wamekubali kuanza kuzitumia kwa ajili ya kilimo na viwanja pamoja na viwanja vya kujenga nyumba na maeneo ya Huduma za Jamii ikiwemo shule, zahanati kituo Cha Polisi pamoja na Miundombinu ya barabara.

Mgogoro huo ambao umedumu Kwa zaidi ya miaka 10 umesababisha hasara kubwa ya Vifo vya wananchi waliokuwa na hatia, uharibifu wa Mali pamoja na maeneo hayo kutokutimika ipasavyo ambapo Kwa Wizara ya Kilimo peke yake umekata Hasara ya zaidi ya Bilioni 8, uku wananchi na mwekezaji wakipata Hasara ambayo hata hivyo tathimini ya awali inaonyesha ni zaidi ya Bilioni 3 na kusababisha jumla ya Hasara kuwa zaidi ya Bilioni 11.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru amemaliza ziara yake ya kata ya Selasi Sing’isi pia Kwa kutoa maelekezo ya baadhi ya wananchi zaidi ya elfu moja ( 1000 ) ambao walikuwa wameuziwa Viwanja na kupewa Hati za makazi katika maeneo ya chini Kujitokeza na kuanza kuendeleza maeneo yao Kwa Kuwa Mgogoro umemalizika na Amani imerejea tena .

WAZIRI LUKUVI AAGIZA WALIOKUWA WAFANYAKAZI WA USHIRIKA KUTOONDOLEWA ENEO LA LAMBO ESTATE NA KUPATIWA EKARI MBILI KILA MMOJA

$
0
0
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsikiliza Meneja wa Kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools Manufacturing Co Ltd cha eneo la Viwanda la Weruweru wilaya ya Hai Andreano Nyaluke wakati wa ziara ya kushughulikia migogoro ya ardhi katika mkoa wa Klimanjaro.
DSC_4440
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsikiliza Meneja wa Kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools Manufacturing Co Ltd cha eneo la Viwanda la Weruweru wilaya ya Hai Andreano Nyaluke wakati wa ziara ya kushughulikia migogoro ya ardhi katika mkoa wa Klimanjaro. 
DSC_4441
Baadhi ya wananchi wa eneo la Shamba la Lambo Estate katika wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro wakifurahia baada ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutoa maagizo wananchi hao wasiondoke katika eneo hilo sambamba na kila mmoja kupatiwa ekari mbili kwa ajili ya kufanyia shughuli zao.
DSC_4443
Baadhi ya wananchi wa eneo la Shamba la Lambo Estate katika wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro wakifurahia baada ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutoa maagizo wananchi hao wasiondoke katika eneo hilo sambamba na kila mmoja kupatiwa ekari mbili kwa ajili ya kufanyia shughuli zao.
DSC_4448
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akipata maelezo ya mashine iliyotengenezwa katika  Kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools Manufacturing Co Ltd cha eneo la Viwanda la Weruweru wilaya ya Hai kutoka kwa meneja wa kiwanda hicho Andreano Nyaluke wakati wa ziara ya kushughulikia migogoro ya ardhi katika mkoa wa Klimanjaro. 
DSC_4486DSC_4502
Baadhi ya nyumba za wananchi waliokuwa wafanyakazi wa Ushirika katika eneo  la Lambo Estates wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro ambao Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi aliamuru wasiondoke eneo hilo na kuwapatia kila mmoja ekari mbili kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao ikiwa ni utatuzi wa mgogoro wa muda mrefu
PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
……………………..
Na Munir Shemweta, WANMM Kilimanjaro
 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amekata mzizi wa fitna ambapo ameagiza waliokuwa wafanyakazi wa chama cha ushirika katika eneo la Lambo Estate Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro kutoondolewa katika eneo hilo na kila mmoja kupatiwa ekari mbili kwa ajili ya kuendesha shughuli zao za kimaisha.
 
Uamuzi  huo wa Lukuvi wa kutoa ekari mbili kwa wananchi hao 78 unafanya kutolewa kwa jumla ya ekari 156  kati ya ekari 1600 . Uamuzi huo unafuatia mgogoro wa muda mrefu baina ya waliokuwa wafanyakazi wa ushirika na uongozi .Mgogoro huo umeibuka baada ya wafanyakazi hao kutakiwa kuondoka katika makazi yaliyopo kwenye eneo la shamba  kutokana na utumishi wao kukoma.
 
Waziri Lukuvi alitoa maamuzi hayo leo katika wilaya Hai  ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya kutembelea wilaya za Hai, Moshi na Same kushughulikia migogoro ya ardhi katika wilaya hizo mkoa wa Kilimanjaro.
 
Mhe Lukuvi ameshangazwa na ushirika wa watu wachache kutaifisha ardhi na kuamuru watu waliokuwepo muda mrefu katika eneo la lambo estate kuondoka na kusema kuwa safari hii serikali itawanyoosha wale wote wanaofanya ujanja wa kuwaonea wanyonge.
 
*”Sijawahi kuona ushirika wa namna hii ambapo wenye rasilimali hawanufaiki na ardhi iliyopo katika  kijiji chao halafu ardhi hiyo inakodishwa kwa wanachama wa ushirika wanaotoka  vijiji vingine”*  alisema Waziri Lukuvi.
 
Huku akishangiliwa na wananchi wakati akitoa maamuzi hayo, Mhe. Lukuvi alisema  amekwenda katika eneo hilo la Lambo Estate kushughulikia mgogoro wa ardhi. Suala la ushirika litashughulikiwa na waziri mwenye dhamana na vyama vya  ushirika ambae ataamua iwapo ushirika huo unafaa. Waziri Lukuvi alisisitiza kuwa, serikali haiwezi kuwaondoa wazee  walioishi kwa muda mrefu.
 
Waziri wa Ardhi ametoa maagizo kwa wananchi watakaopewa ekari mbili kuwa maeneo watakayopatiwa ni kwa ajili ya kufanyia shughuli zao na hawaruhusiwi kuuza na kwa yeyote atakayeamua kuondoka eneo hilo basi eneo hilo litabaki kuwa la serikali.
 
Kufuatia maelekezo hayo Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai kuanza mara moja zoezi la kuwagawia  wananchi ekari hizo kama ilivyoagizwa na  mhe Lukuvi.
 
Awali Katibu wa jumuiya ya wanaushirika Edward Chedi alimueleza Mhe Waziri Lukuvi kuwa mgogoro wa eneo hilo ulianza mara baada ya shamba hilo kutaifishwa na ajira za walikuwa wafanyakazi wa ushirika kukoma mwaka 2001 na kuwepo mfululizo wa kesi uliofikia ngazi ya Mahakama Kuu na kuagizwa waliokuwa wafanyakazi kulipwa mafao na kukabidhiwa vyeti vya kutambuliwa pamoja na ekari hamsini za kujikimu kwa kipindi  watakachokaa hapo kabla ya kuondolewa.

WALENGWA WA TASAF WAFURAHIA MAONESHO YA SIDO MKOANI SIMIYU.

$
0
0
Na Estom Sanga- Simiyu

Walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF waliopata fursa ya kushiriki katika maonyesho yaliyoandaliwa na Shirika la Kuhudumia viwanda vidogo vidogo –SIDO yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu wamesema maonyesho hao yamekuwa ya manufaa makubwa kwao na kuishukuru serikali kupitia TASAF kwa kuwawezesha .

Maonyesho hayo yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassimu Majaliwa yanawashirikiwa Wajasiliamali wadogo na wakati ambao wamepata fursa ya kuonyesha bidhaa wanazozalisha na pia kujifunza teknolojia rahisi ya kutengeneza bidhaa mbalimbali kwa lengo la kutimiza azma ya serikali ya kukuza sekta ya viwanda nchini.

Bidhaa zilizoletwa na Walengwa wa TASAF kwenye maonyesho hayo hutengenezwa kwa njia ya vikundi baada ya kuwezeshwa na Mfuko huo wa Maendeleo ya Jamii kama njia mojawapo ya kuinua kipato cha Walengwa na kupunguza adha ya umaskini. Miongoni mwa bidhaa ambazo Walengwa hao wa TASAF wanaonyesha , ni pamoja na sabuni za vipande na maji, majani ya chai yaliyozalishwa kutokana na mmea wa mchaichai,vyungu,bidhaa za ususi ,nguo aina ya batiki,urembo na mafuta ya kupakaa.

Wakizungumza kwenye banda hilo la TASAF, Walengwa hao wamesema fursa waliyoipata imewawezesha siyo tu kuuza na kupata soko la bidhaa zao, bali pia wameweza kujifunza mbinu za kuendesha shughuli za uzalishaji mali wenye tija jambo ambalo wamesema litainua kipato chao. “tunashukuru sana TASAF kwa kutufungua macho tumeweza kujua namna bora ya kuendesha shughuli zetu za kuzalisha bidhaa na kupata soko “amesema mmoja wa Walengwa ambaye kikundi chake kinajishughulisha na uzalishaji wa mafuta ya kujipakaa na sabuni.

Wakizungumzia changamoto wanayokabiliana nayo katika utekelezaji wa shughuli za uzalishaji wa bidhaa zao, Walengwa hao wametaja tatizo la uduni wa vifungashio vya bidhaa ambayo wamesema ikipatiwa ufunguzi watakuwa wamepiga hatua kubwa kuelekea katika maendeleo ya uhakika. “tazama hivi sasa tunalazimika kuweka sabuni ya maji kwenye chupa za plastiki tunazookoteza baada ya kutumika na kutupwa na watumiaji wengine jambo hilo linapunguza sana ubora wa bidhaa zetu” amelalamika mlengwa huyo wa TASAF.

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF umekuwa na utaratibu wa kuwashirikisha baadhi ya Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko huo kwenye maonyesho mbalimbali ya Wajasiliamali ili kuwawezesha Walengwa hao kujifunza na kuonyesha bidhaa wanazozalisha kwa lengo la kupata pia soko la bidhaa zao.

Baadhi ya Walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF waliopata fursa ya kushiriki katika maonyesho yaliyoandaliwa na Shirika la Kuhudumia viwanda vidogo vidogo –SIDO yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu wamesema maonesho hayo yamekuwa ya manufaa makubwa kwao na kuishukuru serikali kupitia TASAF kwa kuwawezesha .
 Baadhi ya Walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF waliopata fursa ya kushiriki katika maonyesho yaliyoandaliwa na Shirika la Kuhudumia viwanda vidogo vidogo –SIDO yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu,wakiwa na baadhi ya bodhaa zao walizozitengeneza,aidha wamesema maonesho hayo yamekuwa ya manufaa makubwa kwao na kuishukuru serikali kupitia TASAF kwa kuwawezesha .

Dkt. Abbasi Kuhutubia Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Habari China

$
0
0

 Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na Ujumbe wake wakipewa  maelezo ya kiutendaji wa kazi za kila siku zinazofanywa na Shirika la Habari la CCTV na CGTN kutoka kwa mmoja wa viongozi wa juu wa Shirika hilo mapema Jana jijini Beijing, China.
IMG-20181026-WA0015IMG-20181026-WA0014IMG-20181026-WA0017
Picha mbalimbali za ziara ya Msemaji Mkuu wa Serikali  Dkt. Hassan Abbasi na Ujumbe wake alipotembelea vyombo vya habari vya CCTV na CGTN na China Redio Kimataifa Beijing China.
……………………

Na Beatrice Lyimo – CHINA
Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi ataendelea na ziara yake nchini China ambapo leo Ijumaa mchana atatembelea Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Habari cha China na kutoa mhadhara.

Katika mkutano huo, moja ya masuala anayotarajia kuzungumza na wahadhiri na wanafunzi wa chuo hicho ni kuhusu  diplomasia ya Tanzania na China iliyopelekea kuwa na ushirikiano wa karibu mpaka sasa.Aidha, Dkt. Abbasi pia atazungumzia wajibu wa wanahabari na namna wanavyotakiwa kuenenda ili kutekeleza wajibu wao katika sekta nzima ya habari na mawasiliano.

Mbali na hayo, akiwa msimamizi wa sekta ya habari nchini Tanzania Dkt. Abbas katika mkutano huo  ataeleza  hali ya sekta ya habari Tanzania ilivyo sasa na ijayo kwa maendeleo ya nchi.Dkt. Abbasi na ujumbe wake wa Maafisa Habari na Uhusiano Serikalini wapo mjini Beijing kwa ziara iliyolenga kujifunza, kubadilishana uzoefu na kuimarisha ushirikiano.

Ufungaji wa flow meters katika bandari zote nchini kukamilika hivi karibuni.

$
0
0


Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani( aliyesimama) akifafanua jambo wakati wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, iliyokuwa ikijadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hali ya miundombinu ya kupokelea mafuta katika Bandari Kuu, Maghala ya kuhifadhi mafuta, pamoja na Flow Meters. kilichofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya watendaji wa wizara na taasisi zilizochini yake wakiwa katika wakati wa Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, kilichofanyika jijini Dodoma na iliyokuwa ikijadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hali ya miundombinu ya kupokelea mafuta katika Bandari Kuu, Maghala ya kuhifadhi mafuta, pamoja na Flow Meters.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Serikali wa Uwagizaji Mafuta kwa Pamoja( PBPA), Mhandisi Erasto Simon (aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hali ya miundombinu ya kupokelea mafuta katika Bandari Kuu, Maghala ya kuhifadhi mafuta, pamoja na Flow Meters.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Danstan Kitandula,( katikati) akitoa maelekezo kwa watendaji wa Wizara ya Nishati, wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini,iliyokuwa ikijadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hali ya miundombinu ya kupokelea mafuta katika Bandari Kuu, Maghala ya kuhifadhi mafuta, pamoja na Flow Meters.


Na Zuena Msuya, Dodoma

Serikali imesema kuwa taratibu za ufungaji wa flow meter katika bandari zote nchini ziko katika hatua za mwisho baada ya taratibu zote kukamilika.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, jijini Dodoma wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini,iliyokuwa ikijadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hali ya miundombinu ya kupokelea mafuta katika Bandari Kuu, Maghala ya kuhifadhi mafuta, pamoja na Flow Meters.

Kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Danstan Kitandula, ambaye alihoji mambo kadhaa kubwa likiwa ni hatua gani zimefikiwa katika zoezi za ufungaji flow Meter katika bandari kuu nchini ili kudhibiti upotevu wa mafuta na kuongeza mapato ya serikali.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani alieleza kuwa tayari hatua mbalimbali zimekwisha kuchukuliwa ili kukamilisha zoezi hilo, baada ya Mawaziri wa wizara tano, zinazoshirikiana katika sekta hiyo kukutana pamoja na kuweka ratatibu za kuimarisha na kudhibiti upotevu wa mafuta na mapato ya serikali.

Dkt. Kalemani alieleza wazi kuwa, kwa sasa Flow Meters zipo kwenye mchakato wa Manunuzi, ambapo zoezi hilo linakwenda haraka na muda si mrefu litakamika na kulitolea taarifa.“ Zoezi la kununua Flow Meter linaendelea vizuri na kwa kasi, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, ndiyo ilipewa jukumu la kusimamia zoezi hilo, kwa kuwa sekta hii inahusisha Wizara tano, ikiwemo Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Viwanda na Wizara ya Nishati yenyewe:, ufungaji wa flow meter hizo utafanyika katika bandari zote nchini ikiwemo Dar es salaam, Tanga pamoja na Mtwara”, alisisitiza Dkt. Kalemani.

Kuhusu suala la upokeaji wa mafuta kwa pamoja, Dkt. Kalemani alisema , kupitia Wakala wa Serikali wa Uwagizaji Mafuta kwa Pamoja( PBPA) na Kampuni zinazofanya biashara ya mafuta nchini( OMCs) unaendelea kukamilisha taratibu za kuanzisha mfumo wa upokeaji wa mafuta sehemu moja unaofahamika kama Single Receiving Terminal (SRT).

Alisema kuwepo kwa utaratibu huo kutapunguza muda wa meli kusubiri kushusha mafuta hivyo kupunguza upotevu wa mafuta. Pia PBPA kwa kushirikiana na Taasisi za serikali ikiwemo Mamlaka ya Bandari Tanzania( TPA), Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji( EWURA) pamoja na OMCs unaendelea kuimarisha mfumo wa kitaalam ili mabomba yote yaunganishwe kwenye mfumo ulio rahisi kuuendesha kwa lengo la kuboresha sekta hiyo.

Akizungumzia wa kampuni ya kuhifadhi mafuta ya TIPPA, pamoja na Shirika la Maendeleo la Petroli Nchini( TPBD)Dkt. Kalemani alisema kuwa kinachofanyika sasa ni kuangalia uwezekano wa kupanua miundombinu ya kulingana na uhitaji wa mafuta .

Aidha aliwaeleza wajumbe wa kamati hiyo kuwa, wameweka mfumo wa kieletroniki ili kulinda mindombinu ya mabomba yanayotoka baharini kuelekea kwenye maghala ya kupokelea mafuta ili yasitobolewe.Mfumo huo wa kieletroniki utakuwa ukitoa taarifa iwapo msukumo wa mafuta utapungua wakati wote wa zoezi la kupakuaji wa mafuta.

TANAPA NA WADAU WA UTALIIFANYA KAMPENI YA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII KATIKA JIJI LA MWANZA

$
0
0
Kundi la Waandishi wa Habari wakiwa katika boti maalumu kwa ajili ya safari ya kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane .
Muonekano wa Mawe yaliyobebana ni miongoni mwa vivutio vilivyopo katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Sannane.
Muinekano wa lango la kuingilia katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane .
Baadhi ya Watalii wa ndani wakiwa katika Lango la kuingia ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiw acha Saanane kwa ajili ya kujionea vivutio vya utalii vilivyopo katika Hifadhi hiyo.  
Baadhi ya Wageni wakipumzika katika moja ya maeneo yaliyopo katika Hifadhi hiyo.
Baadhi ya Vivutio vilivyomo ndani ya Hifadhi hiyo ,akiwemo ndege aina ya Tausi na Mnyama Simba.
Katika Hifadhi hiyo lipo ene maalum kwaa ajili ya kuweka kambi wakati wa kfanya shughuli ya utalii katika Hifadhi hiyo.
Eneo hili linajulikana kama Kona ya Siri "Scret Corner " iliyipo katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saaanane ambayo imekuwa ikitumiwa na wanandoa kwa ajili ya kuombana msamaha.
Eneo hili linajulikana kama Jiwe la Kugusa "Touch Stone" ni moja la eneo ambalo watalii wa ndani wamekuwa wakitumia kupata Taswira .
Mti wenye muonekano wa mnyama Twiga "Giraffe Tree" ni kivutio kingine ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane kilichopo jijini Mwanza.
Eneo hili limo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane ambalo linajulikana kama jiwe la kuruka "Jump Stone" limekuwa ni kuvutio kwa wageni walitembelea hifadhi hiyo kwa ajili ya kuchukua Taswira wakati wakiruka.
Mmoja waMhadhiri wa Chuo Kikuu cha St ,Agustine kilichopo jijini Mwanza,Judith Wanda akizungumza na wanahabri kuhusu kampeni inayozinduliwa leo ya kutangaza Vivutio vya Utalii katika jiji la Mwanza.
Mkuu wa Idara ya Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane ,Ikwabi Koroso akizungumza kuhusu kuanza kwa kampeni hiyo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii.


WADAU wa Utalii kwa kushirikiana na Vyuo Vikuu katika jiji la Mwanza leo wameanza kampeni  ya siku tatu ijulikanayo kama “Discover the Treasures of Mwanza” itakayoshirikisha zaidi ya wanafunzi  800 waliojiunga na vyuo vikuu mwaka huu.

Lengo la kampeni hii inayotarajia kufanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane  linatajwa kuwa ni kutoa fursa  kwa wanafunzi  hao wa elimu ya juu kutambua umuhimu wa kutembelea rasilimali zilizopo nchini na kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa utalii wa ndani.

Akizungumzia tukio hili mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya tukio hilo ambaye pia  ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustine(SAUT),Judith Wanda,anasema kampeni hiyo inatarajiwa kuanza  leo oktoba 26  hadi 28 mwaka huu.

Wanda amefafanua kuwa kupitia kampeni hiyo wanafunzi hao ambao ni wa mwaka wa kwanza watapata fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu kuhusu masuala ya uhifadhi na utalii wa ndani pamoja na namna bora ya kutangaza vivutio vilivyopo nchini.

"Vyuo vinaanza udahili hivyo tumelenga wanafunzi wapya wanaojiunga na elimu ya juu na tunatarajia kutumia fursa hiyo kuwafundisha wanafunzi kutembelea vivutio na rasilimali zilizopo nchini kama njia ya kujifunza na tunaamini hawa wataenda kuelimisha jamii umuhimu wa uhifadhi na utalii wa ndani,"anasema na kuongeza

"Kampeni hii ya siku tatu imelenga kukutanisha wanafunzi 800 na kila mwanafunzi atajigharamia kiasi cha Sh 8,800 kwa ajili ya usafiri na shughuli nyingine hifadhini(Saanane),tulishawahi kufanya kampeni ya kwanza na tulikuwa tukihusisha wanafunzi wa maeneo ya Mwanza,"

Awali Mkuu wa Idara ya Utalii katika hifadhi hiyo ya Saanane,Ikwabi Koroso,anasema  hali ya utalii hifadhini humo imeimarika ambapo tangu ilipotangazwa Julai mwaka 2013 kuwa hifadhi ilikuwa na wastani wa wageni 4,000 kwa mwaka ila kwa sasa ni wastani wa wageni 15,000 kwa mwaka.

"Hali ya utalii imezidi kuimarika,kati ya wageni hao asilimia 96 ni wale wanaotoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) na mapato yanazidi kukua kulingana na idadi ya wageni hivyo tunatumai kupitia kampeni hii itaongeza idadi ya watalii katika hifadhi yetu ambayo ni ndogo kuliko hifadhi zote,"anasema

Kuhusu usalama kwa watalii,Mkuu huyo anawahakikishia watalii kuwa usafiri huo wa kwenye maji uko salama na kuwa wanachukua tahadhari kubwa ikiwa ni pamoja na ukaguzi wa vyombo vya usafiri.

"Tunashirikiana na wadau wengine kutangaza utalii na tunaamini kupitia kampeni hii tutaongeza idadi kubwa ya watalii katika hifadhi yetu na maeneo mengine yenye vivutio katika ukanda huu,"

Naye Mkuu wa TTB  Kanda ya Ziwa,Gloria Mnihambo,anasema awali kabla ya kuanzishwa kwa ofisi katika Kanda hiyo idadi ndogo ya watalii wa ndani walikuwa wakitembelea Hifadhi na vivutio mbalimbali.

Anasema kuwa hivi sasa mwamko umekuwa mkubwa kwa watalii ndani kutembelea vivutio hivyo baada ya kushirikiana na wadau wengine na kuwa kupitia kampeni hiyo wataendelea kutangaza vivutio mbalimbaliili kuongeza idadi hiyo.

BENKI YAJINASUA KWENYE HASARA,YATANGAZA KUPATA FAIDA

$
0
0
YAJIVUNIA FAIDA YA BIL 1.4/- ROBO YA TATU 2018

BENKI ya Biashara ya DCB imefanya juhudi za makusudi kuhakikisha inatoka kwenye hasara iliyopata mwaka 2017 ya Sh.bilioni 1.6 na kurudi kwenye faida na kwamba baadhi ya hatua zilizochukuliwa ni kuboresha mfumo wa endeshaji biashara ambapo gharama za uendeshaji zimeshuka na huduma mpya za kidigitali zimeanzishwa ambapo zimevutia wateja wengi zaidi kufungua account na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa gharama zitokanazo na amana za wateja.

Hayo yameelezwa na Benki ya DCB jijini Dar es Salaam wakati ikitangaza kufanikiwa kupata faida ya Sh. bilioni 1.4 katika kipindi kinachoishia Septemba mwaka 2018 huku ikiipiku hasara ya Sh.bilioni 1.6 iliyopatikana kipindi kama hicho mwaka 2017 ambayo inawakilisha ongezeko la asilimia 187.Faida hiyo ni kwa kipindi cha robo tatu ya mwaka 2018.

Taarifa ya DCB inaeleza kuwa moja ya huduma za kidigitali ambazo benki imezindua ni akaunti ya kidijiti (DCB Digital Account), DCB Kibubu Digital Account na DCB FDR Digital account.Hivyo akaunti hizo zinamuwezesha mteja wao kufungua akaunti na kufanya miamala yote ya kibenki, kutunza fedha na kuwekeza kwa kutumia simu yake ya mkononi.

Kuhusu kukua kwa faida ,benki hiyo imesema kukua huko kwa faida umechagizwa na ukuaji wa mikopo ghafi ya wateja kutoka Sh. bilioni 89.3 Septemba mwaka 2017 kufikia Sh. bilioni 91.3 mwezi Septemba, 2018. Ukuaji huo umechagizwa na utoaji wa mikopo ambapo mikopo ya jumla ya Sh.bilioni 50 imetolewa hadi kufikia Septemba mwaka 2018.

"Idadi ya wateja imeongezeka kutoka 144,445 Desemba mwaka 2017, kufikia wateja 157,366 Septemba mwaka 2018. Mapato halisi ya benki yatokanayo na riba yameimarika katika robo ya tatu ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita hali ambayo imechagizwa na mkazo wa benki katika kuongeza amana za gharama nafuu kupitia bidhaa za amana za kidijiti, usimamizi wa mizania wenye ufanisi na usimamizi wa gharama za uendeshaji wa benki. Uwiano wa mikopo ghafi na jumla ya amana za benki umeongezeka kwa asilimia 3.1 ikilinganishwa na robo ya pili ya mwaka huu.

"Ili kuhakikisha ufanisi wa mizania, benki imeendelea kulinganisha amana aghali na zenye unafuu, ili kuendana na hali ya amana katika masoko ya kibenki ambapo amana za wateja zimepungua katika robo ya tatu ya mwaka 2018 ikilinganishwa kipindi kama hicho mwaka 2017. Upunguaji huu wa amana aghali umechangia kupungua kwa gharama za riba za amana na kuiwezesha benki kutoa mikopo nafuu kwa wateja, kuongeza mapato halisi na faida kwa ujumla,"imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Pia uongozi wa benki hiyo umefafanua pamoja na ongezeko la mikopo ghafi, benki ya DCB imefanikiwa kupunguza kiwango cha mikopo chechefu kutoka asilimia 18.9 mwezi Desemba 2017 kufikia asilimia 17.8 Septemba mwaka 2018 (Juni 2018 asilimia 17.7). Upunguaji huo umechagizwa na ongezeko la ufanisi katika ukusanyaji wa madeni, utoaji wa mikopo kwa riba nafuu na kuboreshwa kwa huduma kwa waateja.

Pamoja na kujivunia faida hiyo imeelezwa kwamba DCB ilianzishwa mwaka 2002 ikiwa kama Benki ya Jumuiya ya Wananchi “community bank” na Manispaa za Jiji la Dar es Salaam kutokana a kilio cha wakazi wengi wa Jiji kutokuwa na njia rahisi ya kupata mitaji midogo midogo ya biashara. Katika miaka yake 16 ya utoaji huduma, benki imeongeza idadi ya wateja kufikia 157,366 Septemba mwaka 2018, idadi hii ni kubwa kwa sababu benki ya DCB inalenga zaidi wananchi wa kipato cha chini. Benki ya DCB ambayo ni ya kwanza kuorodheshwa kwenye Soko la Hisa, imeweza kukuza mtandao wake wa matawi kufikia matawi nane likiwepo tawi la Dodoma, na inatarajia kuongeza matawi mengine mikoani katika miaka ya mbeleni.

Pia benki hiyo imejiimarisha zaidi katika teknohama na mifumo mbalimbali ya utoaji huduma huku ikiwa mstari wa mbele katika utoaji wa mitaji midogo kwa wananchi wa kipato cha chini, ambapo hadi mwishoni mwa Septemba mwaka 2018, imeweza kutoa mikopo yenye thamani ya Sh.billioni 150 kwa wafanyabiashara wadogo wa vikundi, ikiwemo Sh.billioni 16 zilizotolewa kwa mfuko wa wanawake na vijana wa halmashauri za Jiji la Dar es salaam. 



TAARIFA KUHUSU TUKIO LA KUTITIA KWA CHOO KATIKA SHULE YA MSINGI SELIAN ARUMERU

$
0
0
Leo 26/10/2018 Majira ya Saa tatu na nusu asubuhi tumepata changamoto ya kutitia na kuanguka kwa Jengo la choo cha shule ya Msingi ya Seliani katika kijiji cha Olevolosi kata ya kimnyaki Wilaya ya Arumeru ambapo katika tukio hilo tumeweza Kuokoa Mwanafunzi Mmoja wa Kiume aliepata majeraha sehemu na bado tunaendelea na jitahada za kuondoa kifusi kilichochanganyikana na matofali ambacho kimezama katika Shimo la choo kilichokuwa na matundu 20

Katika kukabiliana na Changamoto Iliyotokea Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry Muro akiambatana na Katibu Katibu tawala wa Wilaya na viongozi wa Halmashauri ya Arusha walifika kwenye eneo la tukio na kuanza kazi ya kuratibu jitihada za uokoaji wakishirkiana na vikosi vya uokoji na Zimamoto pamoja na mamia ya wananchi wa kata ya kimnyaki ambapo walifanikiwa kumuokoa mwananfunzi Mmoja akiwa amejeruhiwa usoni na kukimbizwa katika hospital ya Seliani kwa matibabu zaidi ambapo mpaka sasa vikosi vya uokoaji vinaendelea na jitihada za kufukua kifusi pamoja na matofali yaliyozama katika choo hicho Cha shule chenye matundu 20 ambacho ndio choo pekee Kinachotumiwa na zaidi ya wanafunzi 1,121 wa shule hiyo.

Katika Eneo la tukio kwanza tulilazimika kurejesha hali ya Amani na kutuliza taharuki za wananchi ambao baadhi Wana watoto wanaosoma katika shule hiyo na kutoa nafasi kwa vikosi vya ukoaji kuendelea na zoezi la kutafuta wanafunzi wengine Kutokana na kutokupatikana kwa Taarifa za awali zinazoonyesha idadi ya Wanafunzi ambao huenda walikuwa kwenye choo hicho.

Kutokana na shule hiyo kuwa na choo kimoja chenye matundu ishirini ambacho ndicho kilikuwa pekee kwa shule hiyo ilimlazimu Mkuu wa Wilaya ya Arumeru kuchukua hatua za kuzungumza na Uongozi wa Kanisa la KKKT usharika wa seliani na kuomba shule kutumia vyoo vya Kanisani ombi ambalo lilikubaliwa na *Mkuu wa jimbo la Arusha Magharibi Mchungaji Philemon Joseph Mollel ambae aliungana na Mkuu wa Wilaya katika zoezi a uokoaji na hivyo kuondoa Mashaka ya kufungwa kwa shule.

Kutokana na kadhia hiyo ilimlazimu Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro kuzungumza na wananchi waliojitokeza ambapo katika mazungumzo yake aliwataka wananchi kutulia na kutoa fursa ya kuendelea kwa zoezi la utoaji wa kifusi ili kujirisha na madhara zaidi ambayo huenda yametokea.

Awali kwa upande wao baadhi ya wananchi waliungana na Mkuu wa Wilaya katika kuchanga Fedha kwa ajili ya kuanza Mikakati ya Ujenzi wa choo kingine ili kutokwamisha masomo ya wanafunzi kazi ambayo ilifanywa na Mkuu wa Wilaya pamoja na viongozi wa Kanisani na halmashauri na kuitikiwa kwa wingi na wananchi waliotoa Fedha zao.

Awali Mhe Muro alilazimika kumtembelea majeruhi ambae amelazwa katika hospitali ya seliani na kumjulia hali uku akiongozana na viongozi mbalimbali.

Imetolewa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru
26/10/2018
vikosi vya uokoaji vikiendelea na jitihada za kufukua kifusi pamoja na matofali yaliyozama katika choo hicho Cha shule chenye matundu 20 ambacho ndio choo pekee Kinachotumiwa na zaidi ya wanafunzi 1,121 wa shule hiyo.
vikosi vya uokoaji vikiendelea na jitihada za kufukua kifusi pamoja na matofali yaliyozama katika choo hicho Cha shule chenye matundu 20 ambacho ndio choo pekee Kinachotumiwa na zaidi ya wanafunzi 1,121 wa shule hiyo.
vikosi vya uokoaji vikiendelea na jitihada za kufukua kifusi pamoja na matofali yaliyozama katika choo hicho Cha shule chenye matundu 20 ambacho ndio choo pekee Kinachotumiwa na zaidi ya wanafunzi 1,121 wa shule hiyo.
vikosi vya uokoaji vikiendelea na jitihada za kufukua kifusi pamoja na matofali yaliyozama katika choo hicho Cha shule chenye matundu 20 ambacho ndio choo pekee Kinachotumiwa na zaidi ya wanafunzi 1,121 wa shule hiyo.
vikosi vya uokoaji vikiendelea na jitihada za kufukua kifusi pamoja na matofali yaliyozama katika choo hicho Cha shule chenye matundu 20 ambacho ndio choo pekee Kinachotumiwa na zaidi ya wanafunzi 1,121 wa shule hiyo. 
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro akizungumza na wananchi waliojitokeza kushuhutia tukio hilo,ambapo katika mazungumzo yake aliwataka wananchi kutulia na kutoa fursa ya kuendelea kwa zoezi la utoaji wa kifusi ili kujiridhisha na madhara zaidi ambayo huenda yametokea.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro akimjulia hali mmoja wa wanafunzi aliyejuruhiwa usoni na kukimbizwa katika hospital ya Seliani kwa matibabu zaidi kufuatia kutitia na kuanguka kwa Jengo la choo cha shule ya Msingi ya Seliani katika kijiji cha Olevolosi kata ya kimnyaki Wilaya ya Arumeru 
Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro alipokuwa akizungumza nao kufuatia tukio la kutitia na kuanguka kwa Jengo la choo cha shule ya Msingi ya Seliani katika kijiji cha Olevolosi kata ya kimnyaki Wilaya ya Arumeru
 

 

ALIYEKUWA MKURUGENZI PRIDE ASAKWA NA TAKUKURU, UKWEPAJI KODI SOKO LA KARIAKOO WABAINIKA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii.

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) imetoa ripoti ya matukio  ambayo ni mkakati wa kitaifa dhidi ya rushwa na mpango wa utekelezaji wa awamu ya tatu  unaoratibiwa na kitengo cha uratibu wa utawala bora ofisi ya Rais Ikulu katika kupiga vita vitendo vya rushwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Brigedia Jenerali John Mbungo amesema kuwa aliyekuwa mkurugenzi  mtendaji wa taasisi ya PRIDE  inayojihusisha na utoaji wa mikopo kwa wananchi hasa akina mama ili kuwainua kiuchumi Rashid Gergar Malima (60) anatafutwa kwa tuhuma za kughushi nyaraka na ubadhilifu wa fedha za umma.

Amesema kuwa taasisi hiyo iliundwa kwa lengo la kusaidia wananchi wenye kipato kidogo na ilipata mtaji wake wa kwanza wenye thamani ya dola za kimarekani 4,000  kutoka Norway  kupitia NORAD.

Mbungo ameeleza kuwa katika vipindi mbalimbali kati ya mwaka 2015/2017 Malima na wenzake walifanya ubadhilifu wa fedha za kampuni ya PRIDE za kiasi cha shilingi Bilioni moja na milioni nane  na kuandaa malipo hewa kwa watoa huduma mbalimbali yakiwemo Arusha Art, Antelop Safaries, Essence international na paperwork na pia waliandaa malipo ya salary advance ambayo hayakufuata taratibu na baadaye fedha hizo zote walizichukua na kuzitumia kwa matumizi yao binafsi.

Aidha amesema kuwa mtuhumiwa huyo anadaiwa kutoroka nchini punde tu uchunguzi wa tuhuma hizo ulipoanzishwa mwaka 2018 na taarifa zilizopo ni kwamba alitoroka kupitia eneo la Namanga, na inasemekana kuwa yupo nchini Marekani hivyo amewaomba watanzania nchini na wale wanaoishi Marekani kutoa taarifa za mtuhumiwa huyo ili sheria ifuate mkondo wake.

Watuhumiwa  wengine katika uchunguzi huo wapo na walishahojiwa  na ametoa rai kwa mashirika mengine kuhakikisha kuwa fedha zinazotolewa kwa lengo la maendeleo ya watanzania zinatumika kwa kadri ilivyokusudiwa.

Katika tukio jingine aliyekuwa Afisa Mikopo wa chuo kikuu cha Dar es salaam Ndaki ya Elimu (DUCE) Josephat Museti Machiwa (35) anatafutwa kwa tuhuma za kughushi nyaraka,  wizi na ubadhilifu wa fedha za umma kinyume na sheria.

Imeelezwa kuwa mnamo tarehe 12 Februari 2015 Josephat Machiwa akishirikiana na Mhasibu Lameck Makoye wakiwa watumishi wa Chuo kikuu kishiriki cha Elimu cha Chuo kikuu cha Dar es salaam (DUCE) waliandaa hundi  ya malipo yenye thamani kubwa ya fedha  ambazo zilitokana na fedha za mikopo ya wanafunzi kutoka bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB) na kuzilipa fedha hizo kwenye akaunti za watu wasiokuwa walengwa na baada ya kufanikisha hilo watuhumiwa hao walizichukua fedha hizo kutoka kwa watu hao kwa njia mbalimbali za udanganyifu.

Aidha katika tukio jingine mamlaka hiyo imefanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa zoezi la ukusanyaji kodi kupitia mfumo wa kieletroniki (matumizi ya EFD  mashine) katika soko la kariakoo na kubaini ukwepaji kodi  unaofanywa na baadhi wa wafanyabiashara   jambo linalopelekea kukosesha mapato kwa serikali.

Akifafanua tuhuma hiyo Mbungo amesema kuwa wafanyabiashara hao hukwepa kodi kwa kuuza bidhaa bila kutoa risiti na kutoa risiti yenye malipo pungufu ikilinganishwa na thamani halisi. Na hadi sasa wafanyabiashara wengi wakubwa na wadogo wamekamatwa kwa tuhuma hizo.

Mbungo amewataka wafanyabiashara hao kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.
Naibu Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kutafutwa kwa watuhumiwa waliokimbia baada ya kutenda makosa ya rushwa, wizi na ubadhilifu wa fedha za umma.

SERIKALI YAITAKA WIZARA YA KILIMO IJITATHMINI

$
0
0


*Yaagiza Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Koroshokurudishwa wizarani

RAIS Dkt. John Magufuli ameitaka Wizara ya Kilimo ijitathmini kutokana na suala la mauzo ya zao la korosho linavyoendelea pamoja na utendaji wa Bodi ya Korosho Tanzania.

Pia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo kumrudisha wizarani Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) Prof. Wakuru Magigi baada ya kutoridhishwa na utendaji wake.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Oktoba 26, 2018) katika kikao chake na wakuu wa mkoa ya inayolima korosho kilichofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.“Haturidhishwi na utendaji wa bodi ambao amekiuka maelekezo ya msingi ya Serikali katika kusimamia mfumo mzima wa zao la korosho uliopelekea kuvurugika kwa minada.”

Kutokana na hali hiyo Waziri Mkuu amesema Serikali imesitisha minada yote ya korosho nchini kuanzia leo na kuwataka wakulima wawe watulivu wakati ikishughulikia suala hilo.Kiongozi huyo wa Bodi ya Korosho analalamikiwa kwa kufanya kazi bila ya kushirikisha ushirika wa zao hilo na kutotambua mamlaka zilizowekwa kisheria kama mkuu wa mkoa.

Mbali na malalamiko hayo pia anadaiwa kuendesha operesheni kwa kutumia silaha na askari dhidi ya viongozi wa ushirika kinyume cha taratibu za nchi. 
Hivyo, Waziri Mkuu amemuagiza Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Lindi na wa Mtwara wahakikishe gari lenye namba T 814 DDM pamoja na dereva wake linatafutwa popote.

Waziri Mkuu amesema gari hilo ndilo linalodaiwa kutumika katika kuwakamata viongozi wa ushirika waliokuwa wanawasimamia wananchi waliokataa kuuza korosho kwa bei ndogo.Amesema baada ya dereva wa gari hilo kukamatwa ahojiwe na aeleze askari hao alikuwa anawatoa wapi na nani aliyemtuma. Ameagiza askari wote waliohusika watafutwe.

“Bodi imekuwa ikiwatisha na kuwalazimisha wakulima na viongozi wa ushirika kukubali kuuza korosho kwa bei ya chini jambo ambalo Serikali haiwezi kulikubali.”Waziri Mkuu amesema Serikali haiwezi kulifumbia macho suala hilo kwa sababu limekuwa likiipaka matope kwani mkurugenzi huyo alikuwa anaingiza askari katika mikoa hiyo bila ya mamlaka kuwa na taarifa.

Kadhalika Waziri Mkuu ameitaka Wizara ya Kilimo kutokaa kimya pindi zinapotokea changamoto kama hizo na badala yake watoe taarifa mapema. “Mambo kama haya yanatokea alafu wizara mmekaa kimya tu.” Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. Magufuli anawapongeza wakulima wa korosho kwa uamuzi wao wa kukataa kuuza kwa bei ndogo na kwamba yuko pamoja nao.

“Rais Dkt. Magufuli ameitaka Wizara ya Kilimo ijitathmini katika suala la mauzo ya zao la korosho linavyoendelea,” amesema Waziri Mkuu.Pia Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. Magufuli anataarifa kwamba kuna baadhi ya watendaji Serikalini wanatumia vibaya jina lake kwamba lazima wahusika wote watachukuliwa hatua. 

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bw. Gelasius Byakanwa na Mkuu wa mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi walilalamikia kitendo cha Prof. Magigi kuvuruga mfumo wa uuzaji wa korosho.Pia walisema licha ya kumshauri kiongozi huyo juu ya namna bora ya kuendesha minada ya uuzaji wa korosho hakuwasikiliza na kwamba hakuwa tayari kushirikiana nao na pia alikuwa akidharau mamlaka zao. 

Pia alikuwa akiingiza askari na kuwatisha na kukamata viongozi wa ushirika bila ya wao kujua jambo ambalo walisema limezua taharuki kwa watendaji wa ushirika.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, OKTOBA 26, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wakuu wa Mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na Ruvuma ambao mikoa yao imeanza kuuza korosho, Wenyeviti wa Vyama Vikuu vya Ushirika na Watendaji Wakuu wa Bodi ya Korosho kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Oktoba 26, 2018. Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba.
Washirki wa Mkutano ulioitishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa uliowajumuisha Wakuu wa Mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Pwani ambao mikoa yao imeanza kuuza korosho, Wenyeviti wa Vyama Vikuu vya Ushirika na Watendaji Wakuu wa Bodi ya Korosho wakimsikiliza Waziri Mkuu wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Oktoba 26, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

MBIO ZA NAMTUMBO SELOUS MARATHON ZAZINDULIWA JIJINI DAR,KUFANYIKA NOVEMBA 10, 2018

$
0
0
Kwa mara nyingine tena zile mbio ambazo zimekuwa zikisubiriwa kwa hamu na shauku kubwa na wakazi wa mkoa wa Ruvuma na vitongoji vyake hususan wilaya ya Namtumbo maarufu kama Namtumbo Selous Marathon zimewadia ambapo tarehe rasmi ya kufanyika kwa mbio hizo imetangazwa kuwa tarehe10 Novemba2018. 

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa mbio hizo jijini Dar EsSalaam, Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mh. Sophia Kizigo amesema kuwa mbio hizo zilizoanza rasmi mwaka jana chini ya udhamini wa kampuni ya madini ya Uranium one na kampuni ya Nyuklia ya Rosatom ya Urusi zinalenga kukusanya kuchangisha fedha na vifaa vya ujenzi kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Namtumbo ambapo ujenzi wa baadhi ya majengo umekwisha anza tangu mwaka jana na kwamba unatarajiwa kuendelea tena mwaka huu. 

Nina kila sababu ya kuwashukuru sana wadhamini wa mbio hizi wenzetu Uranium One na Rosatom kwa jinsi ambavyo wamekuwa wakijitolea kuhakikisha kuwa mbio hizi sio zinafanyika lakini pia malengo yake kufanikiwa kwa kiasi kikubwa sana pia tunawashukuru wadau mbalimbali wakiwemo chama cha riadha, wafanyakazi na uongozi wote wa hospitali ya wilaya ya Namtumbo na wananchi wa Namtumbo kwa ujumla kwa michango mbalimbali. 

Naomba pia ni shukuru makampuni na wale wote waliokwisha kuchangia ujenzi wa hospitali hii ya Namtumbo. Makampuni hayo ni MMI, FB Attorney, Namis Corporate, Tanesco, BOT, ITV/Radio One, Halotel, Tulia Trust, wabunge wa mkoa wa Ruvuma, Ma DC na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma. 

Kwa upande wake kampuni Uranium One na mwakilishi wa Rosato amesema kuwa mbio hizo pamoja kulenga kuboresha miundombinu ya afya katika wilaya ya Namtumbo, mbio hizo pia zinaleta umoja na mshikamano mzuri baina ya serikali sekta binafsi na wananchi kwa ujumla huku ikihamasisha afya kwa njia ya mazoezi. 

Nao waratibu wa mbio hizo wamewataka watanzania wanaopenda michezo wajitokeze kwa wingi kushiriki katika mbio hizo za KM 21, KM 10, KM 5, na KM 2.5 ambapo walitaja njia nzuri ya kujisajili kuwa ni kutuma ujumbe kwenda runselous2018@gmail.com ambapo kuanzia miaka 16 na kuendelea watashiriki KM 21 na KM 10 lakini KM5 na 2.5 zitawahusu wazee na watoto 

Mbio hizo zinatarajiwa kudhuriawa na wakimbiaji kutoka mataifa mbalimbali kama Marekani, Japan na Urusi ambako wafanya kazi wa kampuni ya Uranium nao watakuja kushiriki mbio hizo. 

Kujisajili: kupitia ofisi ya mganga mkuu wa wilaya ya Namtumbo na barua pepe runselous2018@gmail.com

Mahala: Mbio zote zitaanzia na kuishia Hospitali ya Wilaya ya Namtumbo 
Muda: Mbio zitaanza saa 12 asubuhi 


“PAMOJA TUNAWEZA” 


Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mh. Sophia Mfaume Kizigo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Namtumbo Selous Marathon zitakazofanyika Namtumbo,Mkoani Ruvuma Novemba 10 mwaka huu.Kulia ni mwakili kutoka Mantra(Uranium One) Tanzania Mrs Khadija Pallangyo, na kushoto ni katibu wa afya wilaya ya Namtumbo.
Mwakilishi kutoka Chama cha Riadha Tanzania RT Iddi Muhunzi (kushoto) akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Namtumbo Selous Marathon zitakazofanyika Namtumbo mkoani  Ruvuma Novemba 10 mwaka huu. Katikati ni Mkuu wa wilaya ya Namtumbo na kulia ni mwakili kutoka Mantra(Uranium One) Tanzania Mrs Khadija Pallangyo.
Mwakilishi kutoka Chama cha Riadha Tanzania RT Ombeni Zavala akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Namtumbo Selous Marathon zitakazofanyika Namtumbo mkoani  Ruvuma Novemba 10 mwaka huu.

MWANZA KUFURIKA NA VIBE KAMA LOTE LA TIGO FIESTA 2018

$
0
0
Mkuu wa Mkoa Wa Mwanza, Mhe. John Mongella akizungumza na waandishi wa habari leo kufungua rasmi pazia la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote litakalofanyika jumamosi hii uwanja wa CCM Kirumba Mkoani humo. Wengine pichani kushoto ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa,Uthman Madati na Msanii Nikki Wa Pili.
Beatrice
Mkuu wa Hifadhi ya Kisiwa cha Saanane kilichopo mkoani Mwanza, Beatrice Kessy akizungumza na waandishi wa habari na Wasanii watakaopanda jukwaa la Tigo Fiesta kesho jumamosi kuhusu umuhimu wa watalii na watanzania kutembelea kisiwa hicho.
Nikki
Msanii wa Bongo Fleva, Nikki Wa Pili akizungumza na wanahabari jinsi alivyojipanga kutoa burudani kwenye tamasha la Tigo Fiesta kesho Jumamosi.
Picha ya pamoja
Mkuu wa Mkoa Wa Mwanza, Mhe. John Mongella akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tigo na wasanii wataopanda kwenye jukwaa la Tigo Fiesta uwanja wa CCM Kirumba kesho.
Uthman
Mkuu wa Mkoa Wa Mwanza, Mhe. John Mongella akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tigo na wasanii wataopanda kwenye jukwaa la Tigo Fiesta uwanja wa CCM Kirumba kesho.
Wa Kazi
Msanii wa Bongo Fleva, Wakazi akizungumza na wanahabari jinsi alivyojipanga kutoa burudani kwenye tamasha la Tigo Fiesta kesho Jumamosi uwanja wa CCM Kirumba.
………………………………………………………………………
Wakaazi wa Mwanza kufurahia ofa murua ya Data Kama Lote inayowapa wateja hadi mara mbili ya thamani ya intaneti watakayonunua kutoka Tigo

 Jumamosi hii, jiji la Mwanza linatarajiwa kufurika na vibe kama lote kutoka kwa wasanii 100% wanaokonga nyoyo za mashabiki wa msimu huu wa Tigo Fiesta 2018- Vibe Kama Lote.Baada ya wiki saba ambazo zimeshuhudia msimu huu mkubwa zaidi wa kitamaduni katika ukanda wa Afrika ya Masahariki na Kati ukizuru miji ya Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Njombe, Mtwara, Songea na Moshi, Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote sasa imetua katika fukwe za Ziwa Victoria na ipo tayari kutifua vumbi katika viwanja vya CCM Kirumba leo Jumamosi tarehe 27 Oktoba.

Waandaaji wa tamasha hilo, kampuni ya Clouds Media group wamesema vibes katika jiji la Mwanza zitaongozwa na msanii Fid-Q ambaye ni mzaliwa wa jiji hilo, akisindikizwa na kundi la Weusi, Rostam, Wakazi na Rich Mavoko. Wasanii wengine watakaopagawisha siku hiyo ni Jux, Barnaba, Whozu, Nandy, Aslay, Country Boy, Nedy Music, Nkunda Star pamoja na Jay Melody. Mwanza pia itashuhudia vibes kutoka kwa Mchama the Best, Jolie, Benson watakaotanguliwa na washindi wa shindano la kusaka vipaji la Tigo Fiesta Supa  Nyota.

Akiashiria kuanza kwa msimu huu wa vibes jijini Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alizungumzia uwepo wa fursa za biashara zinazoambatana na msimu huo. “Wamiliki wa kumbi za starehe, hoteli na nyumba za kulala wageni, mam ntilie, wauza maji na wamiliki wa vyombo vya usafiri ikiwemo bodaboda wote wana fursa kubwa ya kujiongezea kipato kwa sababu tunaratajia maelfu ya wageni kufurika jijini Mwanza katika kipindi hiki,’ alisema.

Hali kadhalika, kampuni ya Tigo imewakumbusha wakaazi wa Mwanza wazikose kufurahia promosheni murwa ya Data Kama Lote itakayowapa bonasi ya hadi mara mbili kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#. ‘Hii itawawezesha wateja wa Tigo kufurahia msimu huu wa vibes kupitia mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+,’ Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Ziwa, Uthman Madati alisema.

Tigo pia inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Kwa tamasha la Mwanza litakalofanyika, tiketi zitakazonunuliwa kwa mfumo wa Tigo Pesa Masterpass QR zitagharimu TSH 8,000 pekee badala ya TSH 10,000 kwa watakaonunua kwa pesa taslim, Wateja wanapaswa kupiga *150*01#  na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.

Wateja wa Tigo pia wanaweza kujaribu umahiri wao wa kujibu maswali yanayohusiana na msimu wote wa vibes kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia.  Washindi wanajinyakulia zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya  http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia.

Huu ni mwaka wa 17 wa tamasha la muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ambapo mwaka huu linashirikisha 100% wasanii wa nyumbani wanaozuru mikoa 15 ya nchi. Baada ya Mwanza, tamasha hilo linahamia Musoma kabla ya kutua  Muleba, Kahama, Arusha Singida na Dodoma, huku kilele kikifanyika jijini Dar es Salaam.

MATUKIO KATIKA PICHA SPIKA NDUGAI AKIFUNGA MAONYESHO YA ASASI ZA KIRAIA 2018 YALIYOFANYIKA JIJINI DODOMA

$
0
0

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto)akimkabidhi tuzo ya Mshindi wa kwanza Mwenyekiti wa taasisi ya uhamasishaji uwazi na uwajibikaji katika raslimali za madini, mafuta na gesi asilia Bw. Ludovick Utoh alieipokea kwa niaba ya Haki Ardhi katika maonyesho ya wiki yaAsasi za Kiraia 2018 yenyekaulimbiu “Tanzania ya Viwanda: Watu, Sera na Utekelezaji” katika tukio lililofanyika leo tarehe 26 Octoba, 2018 katika ukumbi wa African Dream Jijini Dodoma. Katikati ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mhe. Fatma Toufiq

Spikawa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wasabakushoto) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mbali mbali kutoka Asasi za kiraia baada ya kufunga maonyesha ya Asasi za kiraia 2018 yenye kauli mbiu “Tanzania ya Viwanda: Watu, Sera na Utekelezaji” yaliyofanyika leo tarehe 26 Octoba, 2018 katika ukumbi wa African Dream Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na washiriki mbali mbali kutoka Asasi za kirai (hawapo kwenye picha) wakati akifunga maonyesho ya Asasi za Kiraia 2018 yenye kauli mbiu“Tanzania yaViwanda: Watu, Sera na Utekelezaji” yaliyofanyika leo tarehe 26 Octoba, 2018 katika ukumbi wa African Dream Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kushoto mbele) akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society (FCS), Bw. Francis Kiwanga (wa pili kulia) wakielekea katika ukumbi wa African Dream kwa ajili ya kufunga maonyesho ya Asasi za Kiraia 2018 yenye kauli mbiu “Tanzania ya Viwanda: Watu, Sera na Utekelezaji” yaliyofanyika leo tarehe 26 Octoba, 2018 Jijini Dodoma

Washiriki Mbali mbali kutoka Asasi za kiraia wakiwa katika ufungaji wa maonyesho ya Asasi za Kiraia 2018 yenye kauli mbiu “Tanzania ya Viwanda: Watu, Sera na Utekelezaji” yaliyofanyika leo tarehe 26 Octoba, 2018 katika ukumbi wa African Dream Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society (FCS), Bw. Francis Kiwanga wakati alipowasili katika ufungaji wa maonyesho ya Asasi za Kiraia 2018 yenye kauli mbiu “Tanzania yaViwanda: Watu, Sera na Utekelezaji” yaliyofanyika leo tarehe 26 Octoba, 2018 katika ukumbi wa African Dream Jijini Dodoma.(PICHA NA OFISI YA BUNGE

Mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota apatikana na wasanii watembelea Duka Mwanza

$
0
0

 Wasanii wakipata maelezo mbalimbali kwenye Duka la Tigo lililopo barabara ya Nyerere mjini Mwanza

 Meza ya Majaji kutoka kushoto ni Richard Mavoko, Asam Mchomvu, Fid Q,Roofer na Dj Frank
Mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota 2018 mkoa wa Mwanza, Elisayo akifanya yake kwenye Steji na kuibuka mshindi wa kuwakilisha mkoa huo kwenye fainali zitakazofanyika Dar Es Salaam


SAMIA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA BARABARA YA LAMI YA MKURANGA - KISIJU

$
0
0


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha kutengenezea Gypsum Board kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Knauf kilichopo Mwanambaya Mkuranga Bw. Zachopolous Georgions. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
810
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua ujenzi wa barabara Mkuranga – Kisiju inayojengwa kwa kiwango cha lami ikiwa siku ya tatu ya ziara yake ya siku sita ya kukagua na kuhimiza shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
111213
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya mpango wa kuborsha barabra za Mkuranga kutoka kwa Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (katikati) wakati akikagua ujenzi wa barabara Mkuranga – Kisiju inayojengwa kwa kiwango cha lami ikiwa siku ya tatu ya ziara yake ya siku sita ya kukagua na kuhimiza shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani kulia pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
19
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia moja ya vifungashio vinavyotumika kufungashia vigae vya marumaru (tiles) alipotembelea kiwanda cha Goodwill Ceramic ltd kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Robin Huang. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
20
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ya vigae (tiles) moja alipotembelea kiwanda cha Goodwill Ceramic ltd kilichopo Mkuranga mkoani Pwani, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Robin Huang. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
21

WAZIRI LUKUVI AAGIZA WALIOKUWA WAFANYAKAZI WA USHIRIKA KUTOONDOLEWA ENEO LA LAMBO ESTATE NA KUPATIWA EKARI MBILI KILA MMOJA

$
0
0
HAI, KILIMANJARO-

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amekata mzizi wa fitna ambapo ameagiza waliokuwa wafanyakazi wa chama cha ushirika katika eneo la Lambo Estate Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro kutoondolewa katika eneo hilo na kila mmoja kupatiwa ekari mbili kwa ajili ya kuendesha shughuli zao za kimaisha.

Uamuzi huo wa Lukuvi wa kutoa ekari mbili kwa wananchi 78 unafanya kutolewa kwa jumla ya ekari 156 kati ya ekari 1600 na unatokana na mgogoro wa muda mrefu baina ya waliokuwa wafanyakazi wa ushirika na uongozi .Mgogoro uliibuka baada ya wafanyakazi hao kutakiwa kuondoka katika makazi yaliyopo kwenye eneo la shamba kutokana na utumishi wao kukoma.

Waziri Lukuvi alitoa maamuzi hayo katika wilaya Hai ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya kutembelea wilaya za Hai, Moshi na Same kushughulikia migogoro ya ardhi katika wilaya hizo mkoa wa Kilimanjaro. Mhe Lukuvi ameshangazwa na ushirika wa watu wachache kutaifisha ardhi na kuamuru watu waliokuwepo muda mrefu katika eneo la lambo estate kuondoka na kusema kuwa safari hii serikali itawanyoosha wale wote wanaofanya ujanja wa kuwaonea wanyonge. *”Sijawahi kuona ushirika wa namna hii ambapo wenye rasilimali hawanufaiki na ardhi iliyopo katika kijiji chao halafu ardhi hiyo inakodishwa kwa wanachama wa ushirika wanaotoka vijiji vingine”* alisema Waziri Lukuvi.

Huku akishangiliwa na wananchi wakati akitoa maamuzi hayo, Mhe. Lukuvi alisema amekwenda katika eneo hilo la Lambo Estate kushughulikia mgogoro wa ardhi. Suala la ushirika litashughulikiwa na waziri mwenye dhamana na vyama vya ushirika ambae ataamua iwapo ushirika huo unafaa. Waziri Lukuvi alisisitiza kuwa, serikali haiwezi kuwaondoa wazee walioishi kwa muda mrefu. Waziri wa Ardhi ametoa maagizo kwa wananchi watakaopewa ekari mbili kuwa maeneo watakayopatiwa ni kwa ajili ya kufanyia shughuli zao na hawaruhusiwi kuuza na kwa yeyote atakayeamua kuondoka eneo hilo basi eneo hilo litabaki kuwa la serikali.

Kufuatia maelekezo hayo Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai kuanza mara moja zoezi la kuwagawia wananchi ekari hizo kama ilivyoagizwa na mhe Lukuvi.

Awali Katibu wa jumuiya ya wanaushirika Edward Chedi alimueleza Mhe Waziri Lukuvi kuwa mgogoro wa eneo hilo ulianza mara baada ya shamba hilo kutaifishwa na ajira za walikuwa wafanyakazi wa ushirika kukoma mwaka 2001 na kuwepo mfululizo wa kesi uliofikia ngazi ya Mahakama Kuu na kuagizwa waliokuwa wafanyakazi kulipwa mafao na kukabidhiwa vyeti vya kutambuliwa pamoja na ekari hamsini za kujikimu kwa kipindi watakachokaa hapo kabla ya kuondolewa.

TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inathamini uwepo wa sekta binafsi nchini na kwamba inaendelea kushirikiana nayo katika kuboresha maendeleo ya Taifa.

Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Oktoba 27, 2018) wakati alipokutana na bodi mpya ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania kwenye makazi wa Waziri Mkuu, jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ampongeza Mwenyekiti wa taasisi hiyo Bw. Salum Shamte na wajumbe wa bodi hiyo kwa kuchaguliwa kuingoza taasisi hiyo. Bodi hiyo mpya ilikwenda kujitambulisha.

“Serikali inadhamira ya dhati ya kushirikiana na taasisi hii kwa sababu ndio muwezeshaji wa kuifanya Tanzania kufikia uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo 2025,” amesema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa taasisi hiyo Bw. Shamte amesema sekta binafsi inatambua juhudi za Serikali katika kuboresha mazingira ya biashara nchini Tanzania.

“Sisi tupo tayari kushirikiana na Serikali kwa kuwabana wafanyabiashara ambao wanaenda kinyume na maadili na sheria, ila tunaomba Serikali ishirikiane nasi katika utekelezaji wake.”

Pia, Bw. Shamte ameiomba Serikali iendelee kutoa vivutio kwa biashara zinazoanza ili kuhamasisha uwekezaji kwa kuwa baadhi yake zimeonesha gharama kubwa za uzalishaji.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Bodi Mpya ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dsr es salaam Oktoba 27, 2018.  Kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa Faustin Kamuzora na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Salum Shamte. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi Mpya ya Taasisi  ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) baada ya mazungumzo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, jijini Dar es salaam, Oktoba 27, 2018. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa Faustin  Kamuzora  na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Salum Shamte.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mwenyekiti wa Bodi Mpya ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Salum Shamte  baada ya kukutana na wajumbe wa Bodi hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAKAMU WA RAIS ,SAMIA SULUHU HASSAN AZIMWAGIA SIFA WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI NA DAWASA.

$
0
0
Makamu wa Rais ,Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa ziara yake mkoani Pwani alipotembelea mradi wa tenki la kuhifadhia maji linalojengwa katika wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani ,Tenki lenye uwezo wa kuhifadhi lita Milioni sita za maji .
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Pwani,wakiwa katika eneo la mradi wa tenki l Maji katika wilaya ya Kisarawe ambalo linajengwa chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) .
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Prof Makame Mbarawa akitoa taarifa juu ya Miradi mbalimbali ya maji inayoendelea hivi sasa ikiwa na lengo la kuondoa chanagmoto ya upatikanaji wa huduma ya maji katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Waziri wa Nchi, ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ,Seleman Jafo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kisarawe akizungumza wakati wa ziara ya Makamu wa Rais ,Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara katika wilaya ya Kisarawe Mapema leo. 
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe,Jokate Mogelo akifanya utamburisho wa wageni wakati wa ziara hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam ( DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akimuonesha Makamu wa Rais ,Samia Suluhu Hassan kupitia ramani ,maeneo ambayo mradi wa maji kutoka tenki la Maji la Kibamba hadi Kisarawe utapita. 
Waziri wa Nchi, ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ,Seleman Jafo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kisarawe akimueleza jambo Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja .
Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Prof Makame Mbarawa akizungumza jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja .
Sehemu ya ujenzi wa tenki hilo unavyoonekaana katika wilaya ya Kisarawe.
Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassan akiagana na Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Prof Makame Mbarawa mara baada ya kutembelea eneo hilo la mradi wa tenki la Maji.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kisarawe.

Na Dixon Busagaga,Kisarawe.

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu ameimwagia sifa Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Waziri wake ,Makame Mbarawa kwa utendaji wake wa kazi nzuri inayofanya kwa kasi ili kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa uhakika.

Mbali na Wizara ya Maji na Umwagiliaji ,Mama Samia pia ameupongeza uongozi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kwa hatua kubwa wanayoifanya ya kutimiza azma ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama katika  mkoa wa Pwani .

Makamu wa Rais ametoa pongezi hizo leo alipotembelea Mradi wa tenki la Kuhifadhia Maji yatakayosukumwa kutoka Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu kupitia tenki la Maji la Kibamba ,mradi ambao utagharimu zaidi ya Sh Bilioni 10.4 huku akiwataka wananchi wa Kisarawe kulinda miundo mbinu ya maji .

Amesema  awali kulikuwa na tabia kwa miradi kusuasua  na kwamba  kwa usasa chini ya usimamizi wa Waziri Mbarawa Miradi hiyo itaenda vizuri na maji yatapatikana.

"Kuja kwa mradi huu mkubwa wa maji utawapatia vijana ajira katika viwanda baada ya wawekezaji kuja na najua umeme upo na wa gesi unakuja,"amesema Mama Samia.

Kwa upande wa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa amesma  mradi huo unajengwa chini ya kampuni ya Chico na utadumu kwa miezi minane na kwamba hadi kufikia Julai 2019 utakuwa umekamilika ikiwa ni pamoja uwekaji wa bomba la Km 5 kwenda Vigungu na Km 14 kwenda Viwandani,

“Katika kutekeleza miradi mbalimbali ,DAWASA imetengwa akaunti maalumu ambapo asilimia 35  ya mapato inawekwa kwenye akaunti hiyo kwa ajili ya kuendesha miradi mbalimbali.na kwa mradi huu mbali na ujenzi wa tenki la kuhifadhi maji pia zitafungwa pampu nne kubwa kwa ajili ya kusukuma maji kwa wananchi wa Kisarawe “alisema Mbarawa.

Naye Waziri wa TAMISEMI na Mbunge wa Kisarawe Seleman Jafo ameshukuru kwa mradi wa maji kufika Wilaya ya Kisarawe na kupitia mradi huu wana kisarawe watakuwa wamenufaika kwa asilimia kumi.

Ameyataja maeneo ya Mzenga na Mwanalumango kuwa na shida kubwa ya maji na watu wa Kisarawe wanaishukuru sana serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kufanikisba mradi huu kwani ni mara ya kwanza toka kupata kwa uhuru.

Rock City Marathon kufanyika kesho

$
0
0
Mbio za Rock City Marathon msimu wa tisa zinatarajiwa kufanyika kesho jijini Mwanza. Maandalizi ya mbio hizo zinazotarajiwa kuanzia kwenye Daraja la Furahisha na kuishia kwenye viwanja vya Rock City Mall jijini humo yamekamilika huku zaidi ya washiriki elfu tano (3,000) kutoka ndani na nje ya nchi wakitarajiwa kushiriki katika mbio hizo.

Tayari Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw John Mongella pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt Philis Misheck Nyimbi wamekwisha thibitisha ushiriki wao kwenye mbio hizo ambazo pia zitahusisha ushiriki wa baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali, wabunge na washiriki kutoka mashirika na taasisi mbalimbali.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Mwanza leo, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi alisema kamati yake imejiandaa kupokea washiriki zaidi ya 3,000 wa mbio hizo kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo wakimbiaji wa kimataifa.

“Tunatarajia kuwa na mbio zenye mafanikio makubwa mwaka huu. Maandalizi kwa kiasi kikubwa yamekwisha kamilika na kinaochoendelea kwa sasa ni usajili wa washiriki kutoka ndani na nje ya nchi na tunatarajia kufunga zoezi hilo siku ya Jumamosi Oktoba 27,’’ alibainisha.

Akizungumzia kuhusu zawadi, Ngowi alisema pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 4 kila mmoja, sh.mil 2/- kwa washindi wa pili na sh. Mil 1/- kwa washindi wa tatu, huku washindi wanne hadi kumi nao pia wakiibuka na medali na pesa taslimu.

Kwa upande wa mbio za Kilomita 21, Ngowi alisema, pamoja na medali washindi wa kwanza kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 3/- kila mmoja, sh. Mil 1/- kwa washindi wa pili na sh. 750,000/- kwa washindi wa tatu huku pia washindi wanne hadi wa kumi wakiibuka na zawadi za pesa taslimu na medali kila mmoja.

Aliwataja wadhamini ambao pia watashiriki katika mbio hizo kuwa ni pamoja na kampuni za Puma Energy Tanzania, Tiper,Rock City Mall, NSSF, New Mwanza Hotel, CF Hospital, Coca Cola, Metro Fm, EF Outdoor, KK Security, Belmont Fairmount Hotel , Bigie Customs na Global Education Link.

Alibainisha kuwa mbio za Km 5 zitahusisha watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino ambapo washindi kwa upande wa mashirika watapatiwa zawadi za utambuzi ikiwemo medali na vyeti vya ushiriki huku pesa zikielekezwa kwa washiriki wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino.

Bw Ngowi alivitaja vituo vinavyoendelea na usajili huo kwasasa kuwa ni pamoja na Igoma, Buzuruga, Airport Mwanza, Rock city mall, Chuo Kikuu cha Saut, Nyegezi Stand, Mwanza hotel, Nyamagana Stadium, Dampo pamoja na Nyakato.
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio  za Rock City Marathon Bw Zenno Ngowi (katikati) akionesha mbele ya waandishi wa habari baadhi ya zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika kesho jijini Mwanza. Wengine ni pamoja na Mratibu Mtaalamu wa mbio za Rock City Marathon Bw John Bayo (kulia) na  Mwakilishi wa Kampuni ya Ulinzi ya KK Security ambao ni moja wa wadau wa usalama katika mbio hizo, Bw Andrew Maiga ndio
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio  za Rock City Marathon Bw Zenno Ngowi (katikati) akionesha mbele ya waandishi wa habari baadhi ya zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika kesho jijini Mwanza. Wengine ni pamoja na Mratibu Mtaalamu wa mbio za Rock City Marathon Bw John Bayo (kulia) na  Mwakilishi wa Kampuni ya Ulinzi ya KK Security ambao ni moja wa wadau wa usalama katika mbio hizo, Bw Andrew Maiga ndio
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio  za Rock City Marathon Bw Zenno Ngowi (katikati) akionesha baadhi ya zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika kesho jijini Mwanza.
 Mratibu Mtaalamu wa mbio za Rock City Marathon Bw John Bayo akizungumza kuhusu maandalizi ya mbio hizo.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images