Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1707 | 1708 | (Page 1709) | 1710 | 1711 | .... | 1903 | newer

  0 0


  Mkurugenzi wa NMB – Bi. Ineke Bussemaker akichangia kwenye mdahalo ulioandaliwa na KPMG juu ya nafasi ya Tekinolojia kwenye ukuaji wa Biashara Nchini uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi wa Tehama, Wizara ya Kazi, Usafirishaji na Mawasiliano – Melembwa Munaku, Mkurugenzi wa Selcom – Sameer Hiurji na Mkurugenzi wa Tehama kutoka KPMG – Anthon Nzamu.
  Mkurugenzi wa NMB – Bi. Ineke Bussemaker akichangia kwenye mdahalo ulioandaliwa na KPMG juu ya nafasi ya Tekinolojia kwenye ukuaji wa Biashara Nchini uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi wa Tehama, Wizara ya Kazi, Usafirishaji na Mawasiliano – Melembwa Munaku, Mkurugenzi wa Selcom – Sameer Hiurji na Mkurugenzi wa Tehama kutoka KPMG – Anthon Nzamu.
  Mkurugenzi wa NMB – Bi. Ineke Bussemaker akichangia kwenye mdahalo ulioandaliwa na KPMG juu ya nafasi ya Tekinolojia kwenye ukuaji wa Biashara Nchini uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi wa Tehama, Wizara ya Kazi, Usafirishaji na Mawasiliano – Melembwa Munaku, Mkurugenzi wa Selcom – Sameer Hiurji na Mkurugenzi wa Tehama kutoka KPMG – Anthon Nzamu.

  BENKI ya NMB imesema itaongeza kiwango cha mikopo inayoitoa kwa kampuni ndogo na za kati mara mbili zaidi na kufikia Shilingi trilioni tatu kwa miaka mitatu ijayo. Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtengaji wa benki hiyo Bi – Ineke Bussemaker wakati akizungumzia udhamini wa NMB kwa hafla ya Kampuni Bora 100 zamwaka 2018/2019 (Top100 Mid-sized Companies' Survey).

  Kwa miaka mitatu iliyopita, NMB imetoa mikopo yenye thamani ya Shilingi trilioni 1.5 kwa kampuni ndogo na za kati. Akizungumza katika uzinduzi wa utafiti wa Kampuni Bora 100 za mwaka 2018/2019 jijini Dar es Salaam jana, Bi. Bussemaker alisema kampuni zinazowekeza katika kufanya biashara kidigitali zipo katika nafasi nzuri zaidi ya kufanya vizuri kibiashara.

  "Hatima ya uchumi wa nchi upo katika kufanya biashara kidijitali ili kuhakikisha mifumo ya utendaji inakwenda kwa kasi,” alisema na kuongeza kuwa kampuni zilizoweza kuweka mifumo sawa ya dijitali zipo katika nafasi bora zaidi ya kupata mikopo kutoka katika benki yake.

  Alisema Benki ya NMB inazidi kuwekeza katika mifumo ya utoaji huduma kwa njia za kidijitali ili kuwafikia wananchi wengi zaidi wanaohitaji huduma zake nchini kote. Kampuni Bora 100 Tanzania ni shindano linaloendeshwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited kwa kushirikiana na KPMG.

  Mbali na NMB, wadhamini wengine wa Kampuni Bora 100 za mwaka 2018/2019 ni pamoja na Soko la Hisa la Dar es Salaam na Azam Media na Hoteli ya Hyatt Regency.


  Akitoa matokeo ya utafiti wa Kampuni Bora 100 za mwaka 2018/2019, Mtafiti kiongozi wa kampuni ya AZ Advisory, Dk. Remidius Ruhinduka, alisema asilimia 23 ya Kampuni za kati nchini zinaona mwenendo wa uchumi nchini kwa kipindi cha miezi sita iliyopita sio mzuri huku asilimia 62 ya kundi hilo iko na kuimarika kwa uchumi kwa kipindi cha miezi sita ijayo.

  Mkutano huo wa utafiti umefanyika ikiwa imesalia siku moja kufikia fainali za shindano la Top100 ambayo itafanyika Oktoba 25, katika fainali hizo kampuni bora 100 za kati zitatangazwa. Dk. Ruhinduka alisema asilimia kubwa ya wafanyabiashara wanamatumaini ya kuimarika kwa uchumi licha ya changamoto walizonazo katika biashara zao.

  "Mtazamo wa wafanyabiashara kwa kipindi cha miezi 6 iliyopita asilimia 55 wanasema biashara inaimarika, asilimia 22 wanasema iko sawa na asilimia 23 wanasema mwenendo sio mzuri. Hata hivyo kwa kipindi cha miezi sita ijayo Asilimia 60 wanasema uchumi utaimarika, asilimia 28 itakuwa sawa na asilimia 12 itakuwa mbaya," amesema Dk. Ruhinduka.

  Pia utafiti huo ulihoji mtazamo wa wafanyabiashara hao kuhusu mwenendo wa sekta ya wafanyabiashara wakati nchini ambapo kwa kipindi cha miezi sita iliyopita aslimia 62 walisema hali imeimarika asilimia 20 walisema iko sawa na asilimia 18 walisema hali ni mbaya.

  Mwenendo wasekta kwa kipindi cha miezi sita ijayo utafiti huo ulibainisha kuwa asilimia 66 ya wafanyabiashara walisema mwenendo utaimarika asilimia 20 walisema itakuwa sawa na asilimia 14 walisema utakuwa sawa.

  0 0
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wafanyakazi wa NSSF alipotembelea banda hilo katika maonesho ya SIDO mkoani Simiyu.(wa pili kushoto ni Afisa matekelezo wa NSSF Simiyu Mr Khalid Omar, wa Tatu kushoto ni Stara Masatu ambaye ni Afisa mwandamizi wa NSSF Shinyanga,Katikati ni Abasi Cothema, Afisa mwandamizi sekta isiyo rasmi, na wa kwanza kulia ni Nuhu Ramadhani ambaye ni Mkuu wa Kituo cha NSSF Simiyu.Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Mtaka ametoa wito kwa NSSF kuwekeza nguvu kubwa katika kuhakikisha wajasiriamali wadogowadogo wanajiunga na NSSF
  Afisa matekelezo wa NSSF Bwana Abdul- Aziz Abed akitoa elimu kwa wageni waliotembelea Banda la NSSF wakati wa maonesho ya SIDO yanayoendelea Mkoani Simiyu

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira nchini(JET) John Chikomo akifafanua jambo kwenye semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu sekta ya uhifadhi wa mazingira na wanyamapori inayoendelea wilayani Bagamoyo mkoani Pwani
   Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET) wa kwanza kushoto pamoja na waandishi wengine wa vyombo vya habari wakisikiliza mada kwenye semina ya mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi kuhusu sekta ya uhifadhi wa wanyamapori
   Mwanasheria kutoka Timu ya Wanasheria  waliobobea katika  mazingira (LEAT) Stanslaus Nyembea akitoa mada kwenye semina ya waandishi wa habari za mazingira inayoendelea wilayani Bagamoyo mkoani Pwani
   Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mjadala kwenye semina ya waandishi wa habari za mazingira nchini inayoendelea wilayani Bagamoyo mkoani Pwani .Semina hiyo imeandaliwa na JET
   Mwakilishi kutoka USAID Protect Symphrose Makungu akizungumza kwenye semina ya Waandishi  wa habari za mazingira ambayo imeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET) nchini ya ufadhili wa USAID Protect
   Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET) na watoa mada
   Mwandishi wa gazeti la Mtanzania Sidi Mgumia(kulia) pamoja na mtangazaji wa Radio Clouds Sophia Kesi wakifuatilia mada wakati wa semina ya waandishi wa habari za mazingira.
  Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye semina ya mafunzo ya waandishi wa habari za mazingira

  0 0


  Na mathias Canal-WK, Bariadi-Simiyu

  Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) leo Alhamisi Octoba 2018 amewataka wajasiriamali kote nchini kuchangamkia fursa ya kutembelea katika Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.

  Katika maonesho hayo ambayo yalianza Oktoba 23 mwaka huu, Dkt Tizeba amesema kuwa hiyo ni fursa kwa wananchi kuweza kujielimisha katika maeneo mbalimbali ya teknolojia za viwanda hususani viwanda vidogo, lakini pia wajasiriamali kupata nafasi ya kujifunza kutoka kwa wenzao wa maeneo mengine nchini na nje ya nchi.

  "Nitoe wito kwa wananchi wa mkoa wa Simiyu na mikoa ya jirani kama Mara, Mwanza na Shinyanga wajitokeza kwa wingi kushiriki maonesho haya maana hii ni fursa muhimu kwao katika kuakisi kwa vitendo Tanzania ya viwanda" Alisema Dkt Tizeba

  Dkt Tizeba amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka kwa kubuni jambo hilo sambamba na kumpongeza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage kwa kuwaalika wajasiriamali, na wataalamu waoneshaji wa teknolojia mbalimbali kwani jambo hilo litatoa fursa kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu na mikoa mingine kuona ushindani katika uongezaji wa thamani wa mazao mbalimbali na fursa kwa wajasiriamali kujifunza kutoka kwa wenzao.

  Aidha, Dkt Tizeba amesema kuwa Maonesho hayo ya SIDO ambayo ni ya kwanza kufanyika Kitaifa yatawasaidia wajasiriamali kote nchini kupanua masoko ya bidhaa zao.Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO) yakiwa na Kauli Mbiu isemayo PAMOJA TUJENGE VIWANDA KUFIKIA UCHUMI WA KATI”. yalifunguliwa rasmi na Waziro Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa (Mb) siku ya Jumanne Oktoba 23, 2018 na yanatarajiwa kuhitimishwa siku ya Jumapili Oktoba 28, 2018.
  Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza jambo mara baada ya kuwasili kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu, Leo alhamisi tarehe 25 Octoba 2018.
  Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza jambo wakati akikagua mashine zinazotengenezwa na SIDO TDC kwa ajili ya uchakataji wa mazao mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu, Leo alhamisi tarehe 25 Octoba 2018.
  Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akiwa ameambatana na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka kutembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yanayofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu Leo alhamisi tarehe 25 Octoba 2018.

  0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Garib Bilal alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam kumjulia hali.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akifafanua jambo kwa Makamu wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Garib Bilal alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam kumjulia hali..
   Makamu wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Garib Bilal akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam kumjulia hali.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) (kulia) akiagana na Makamu wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mohammed Garib Bilal alipomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam kumjulia hali.

  0 0

  SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limepanga kufunza wanafunzi 200 kutoka shule sita nchini namna ya kutengeneza mfumo wa alama zinazotumiwa katika maandishi ya kompyuta na matumizi yake.

  Wanafunzi hao 200 watakuwa miongoni mwa vijana zaidi ya 2,489 waliofunzwa kuendeleza utaalamu wa kidijiti kwa ajili ya maendeleo.Kwa mujibu wa taarifa ya UNESCO, katika kuadhimisha siku ya Umoja wa Mataifa yenye kauli mbiu “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu” mafunzo yalifanyika katika shule ya sekondari ya Chazinge.

  Hatua hizo zimelenga kuwezesha njia ya kuelekea uchumi wa viwanda nchini Tanzania.Pamoja na shule ya sekondari ya Chazinge na Kimani iliyopo Kisarawe mkoani Pwani nyingine ni Jamhuri, Gerezani na Benjamin Mkapa zilizopo Ilala mkoani Dar es Salaam.

  Katika mafunzo hayo UNESCO watahakikisha kwamba vijana wanakuwa wavumbuzi, wabunifu na hivyo kutumiwa kuboresha namna bora ya kufanya biashara miongoni mwa vijana wa kike na wakiume.
  Taarifa hiyo imesema kwamba lengo kuu ni kuwezesha vijana hasa wanawake kutumia kikamilifu mifumo ya tehama kujiendeleza katika masomo ya  Sayansi, Tehama, Uhandisi na Mahesabu (STEM).

  Alisema mafunzo hayo yataongeza pia uwezo wa vijana kujiajiri na kuajiriwa kwa kuwa na ujuzi zaidi.
  Mradi wa mafunzo hayo ni sehemu ya mradi wa UNESCO unaofanyiwa kazi katika nchi zaidi ya 25 unatambuliwa kama Youth Mobile Initiative kwa lengo la kuboresha hali za uchumi za mataifa hayo kupitia matumizi ya kompyuta.

  UNESCO katika kuendeleza vijana imeshirikiana na Apps and Girls kuendesha tamasha la nne la Africa Code Week linalofanyika katika nchi 36 za Afrika tangu lianzishwe mwaka 2015.Imeelezwa katika taarifa hiyo kwamba jumla ya vijana milioni 1.8 wamefunzwa masuala ya dijiti kuelekea karne ya 21.
  Mafunzo hayo yamalenga kuhakikisha kwamba wanakuza uwezo wao wa kutumia alama za siri kutengeneza programu mbalimbali kwa matumizi anuai.
   Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Nancy Kaizilege akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Chanzige iliyopo wilayani Kisarawe kuhusu nafasi ya vijana katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu wakati wa maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week” yaliyoambatana na sherehe za maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia  Malengo ya Maendeleo Endelevu”  ambapo mafunzo  hayo yamefanyika jana shuleni hapo.
   Mkufunzi Kiongozi kutoka Shirika lisilo la kiserikali la Apps and Girls, Bw. Wilhelm Oddo akitoa utangulizi wa elimu ya Tehama kwa baadhi ya wasichana wa Shule ya Sekondari Chanzige wilayani Kisarawe. Haya ni moja kati ya mafunzo ya Tehama yameandaliwa na Shirika hilo lisilo la kiserikali la Apps and Girls likishirikiana na UNESCO  wakati wa maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week” yenye lengo la kuongeza ushiriki wa mtoto wa kike katika masomo ya Sayansi, Tehama, Uhandisi na Mahesabu (STEM) yaliyoambatana na sherehe za  maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu”  ambapo mafunzo  hayo yamefanyika jana shuleni hapo.
   Wakufunzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Apps and Girls, Balbina Gulam (kushoto) na Raymond Benedict (kulia) wakiendesha mafunzo ya Tehama kwa vitendo kwa baadhi ya wasichana wa Shule ya Sekondari Chanzige wilayani Kisarawe wakati wa maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week” yaliyoenda sambamba na sherehe za maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu”  ambapo mafunzo hayo yamefanyika jana shuleni hapo.

   Baadhi ya wasichana wa Shule ya Sekondari Chanzige wilayani Kisarawe wakishiriki mafunzo ya Tehama kwa vitendo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Apps and Girls likishirikiana na UNESCO wakati wa maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week” yaliyoenda sambamba na sherehe za maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu”  ambapo mafunzo hayo yamefanyika jana shuleni hapo.
   Afisa kutoka kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Justin Mori akifafanua jambo kwa baadhi ya wasichana wa Shule ya Sekondari Chanzige wilayani Kisarawe walioshiriki mafunzo ya Tehama kwa vitendo yalioandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Apps and Girls likishirikiana na UNESCO wakati wa maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week” yaliyoenda sambamba na sherehe za maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu”  ambapo mafunzo hayo yamefanyika jana shuleni hapo.
    Baadhi ya wasichana wa Shule ya Sekondari Chanzige wilayani Kisarawe walioshiriki mafunzo ya Tehama kwa vitendo yaliyoandaliwa na Shirika la Apps and Girls likishirikiana na UNESCO wakati wa maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week” yaliyoenda sambamba na sherehe za maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa Mataifa yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu” ambapo mafunzo hayo yamefanyika jana shuleni hapo.
   Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Nancy Kaizilege na Mwanzilishi wa Shirika lisilo la kiserikali la Apps and Girls, Bi. Carolyne Ekyarisiima wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasichana wa Shule ya Sekondari Chanzige wilayani Kisarawe walioshiriki mafunzo ya Tehama kwa  vitendo yaliyoandaliwa na Shirika la Apps and Girls likishirikiana na UNESCO wakati wa maadhimisho ya tamasha la nne la “Africa Code Week” yaliyoenda sambamba na sherehe za maadhimisho ya miaka 73 ya Umoja wa  Mataifa yaliyobeba kauli mbiu ya “Uwezeshaji Vijana Kiubunifu ili Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu” ambapo mafunzo hayo yamefanyika jana shuleni hapo.  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea ripoti ya uchunguzi wa  ajali ya kivuko cha MV Nyerere kutoka kwa kamati iliyoundwa na Serikali kwa ajili ya kuchunguza ajali hiyo.

  Amepokea ripoti hiyo leo (Alhamisi, Oktoba 25, 2018) kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati  hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstafu, Jenerali George Waitara,kwenye makazi ya Waziri Mkuu, jijini Dar es Salaam.

  Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuishikuru kamati hiyo kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli kwa kazi kubwa waliyoifanya ambayo imethibitisha umakini wao.

  Pia ameipongeza kamati hiyo kwa namna walivyotumia muda wao vizuri kwa kufanya kazi hiyo na kutoa mapendekezo kwa Serikali juu ya mambo waliyoyabaini.“Nimepokea taarifa kwa niaba ya Serikali, Serikali itafanya mapitio ya taarifa yote na viambatisho vyake na itapitia kwa kina mapendekezo mliyoyatoa ambayo yote yatafanyiwa kazi.”

  Waziri Mkuu ameongeza kuwa Serikali inaamini mambo yote yaliyosheheni katika taarifa hiyo ni yale ambayo Watanzania wanasubiri kuona yakifanyiwa kazi.MV Nyerere ilipindika na kuzama Septemba 20, mwaka huu katika ziwa Victoria ambapo Watanzania zaidi 200 walipoteza maisha na wengine Zaidi ya 40 waliokolewa.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea Ripoti ya Kamati iliyoundwa na Serikali Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha MV Nyerere kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati  hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstafu, Jenerali George Waitara, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha  Ripoti ya Kamati iliyoundwa na Serikali Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha MV Nyerere  baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali George Waitara (kushoto) kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018.  
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati iliyoundwa na Serikali Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha MV Nyerere baada ya kupokea Ripoti ya Kamati hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018. Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera na Uratibu, Profesa Faustin Kamuzora na  wapili kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali George Waitara.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati  iliyoundwa na Serikali Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha MV Nyerere  baada ya kupokea Ripoti ya Kamati hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018. Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera  na Uratibu) Profesa Faustin Kamuzora na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali George Waitara.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiagana na Mwenyekiti wa Kamati  iliyoundwa na Serikali  Kuchunguza Ajali ya Kivuko cha Mv Nyerere, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali, George Waitara  baada ya kupokea Ripoti ya Kamati hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 25, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akisalimiana na Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN) hapa Zanzibar Bibi.Dorothy Temu-Usiri (katikati) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na ujumbe aliofuatana nao,[Picha na Ikulu.] 25/10/2018. 
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akimsikiliza  Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN) hapa Zanzibar Bibi.Dorothy Temu-Usiri walipokuwa katika mazungumzo wakati  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akiwa na ujumbe aliofuatana nao (hawapo pichani),[
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na ujumbe wa Mratibu wa Umoja wa Mataifa (UN) hapa Zanzibar Bibi.Dorothy Temu-Usiri (wa pili kulia) walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo

  0 0

  Naibu Waziri , Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Injinia Stella Manyanya akiwahutubia washiriki wa kongamamano la uwekezaji na biashara (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo uliofanyika mapema leo Jijini Dar es Salaam.

  Baadhi ya washiriki wa kongamano la uwekezaji baina ya Makampuni 41 kutoka Ubelgiji na Sekta binafsi 200 kutoka Tanzania wakifuatilia mazungumuzo ya kongamano hilo yaliyofanyika mapema leo Jijini Dar es Salaam  Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),John Mnali akiwasilisha maada kwa washiriki wa kongamano, kuhusu fursa zinazopatikana nchini pamoja na huduma zinazotolewa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania kwa wawekezaji .  Washiriki kutoka Tanzania wakifuatilia mazungumuzo katika kongamano la uwekezaji na biashara yalifanyika mapema leo katika ukumbi wa Serena Hoteli Jijini Dar es Salaam.


  Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),John Mnali akisisitiza jambo kwa washiriki wa kongamano ( hawapo pichani), kuhusu fursa zinazopatikana nchini pamoja na huduma zinazotolewa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania, katika kongamano linalofanyika Jijini Dar es Salaam. (Picha na Paschal Dotto-MAELEZO)

  …………………………………………………………………………..

  Na  Paschal Dotto-MAELEZO

  Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara imezitaka sekta binafsi na makampuni kuchangamkia fursa za uwekezaji na biashara ili kuweza kuimarisha mitaji yao pamoja na kupanua wigo wa masoko na kutangaza fursa za uwekezaji kwa kushirikiana na makampuni ya nchi za nje.

  Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika kongamano la kibiashara linalohusisha makampuni zaidi ya 41 kutoka nchini Ubelgiji na sekta binafsi 200 kutoka Tanzania, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Injinia Stella Manyanya, amesema kuwa Tanzania na Ubelgiji zimekuwa na mashirikiano ya siku nyingi katika masuala ya kiuchumi.

  “Nchi ya Ubelgiji tunashirikiana nayo kwenye masuala ya bandari za Dar es Salaam na Zanzibar, lakini pia natambua kuwa Ubelgiji wana mahusiano na nchi za Rwanda na Congo kwa hiyo ni rahisi kuunganisha ukanda huu kwa kutumia bandari zetu na kufungua biashara katika ukanda huo”, alisema Injinia Manyanya.

  Aidha, Injinia Manyanya alibainisha kuwa kongamano hilo litafungua ukurasa mpya kwa jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kwani amekuwa akisisitiza masuala ya uwekezaji ili kujenga Tanzania ya Viwanda ambapo ameweza kuzuia rushwa, urasimu na ufisadi kitu ambacho kimevuta wawekezaji wengi kuja kuwekeza hapa nchini.

  Alieleza kuwa fursa za uwekezaji zimefunguliwa Tanzania na kuwasihi wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali duniani kuja kuwekeza kwenye sekta mbalimbali.

  “Tanzania kuna fursa nyingi sana za uwekezaji ikiwemo fursa za kilimo, masuala ya umeme, madini, utalii pamoja na uvuvi, kwa ujumla sasahivi viwanda vinaweza kujengwa katika maeneo mbalimbali nchini”, alisema Injinia Manyanya.

  Pia alitoa wito kwa makampuni na sekta binafsi za Tanzania kushirikiana na makampuni hayo ya Ubelgiji ili kuingia ubia wa kuwekeza na kufanya biashara kwa lengo la kuimarisha sekta ya uwekezaji na biashara kwa manufaa ya Watanzania.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), John Mnali, alisema kuwa ugeni huo umekuja kutafuta fursa mbalimbali za uwekezaji pamoja na kufanya biashara kwenye sekta za utalii, umeme, viwanda na kilimo.

  “Tumepata mwitikio mkubwa kwa sekta na makampuni binafsi kuja kushiriki kwenye kongamano na mazungumzo haya, kwa hiyo napenda kuwaomba Watanzania wenye makampuni kunapokuwa na makongamano kama haya wasibaki nyuma na sisi TIC jukumu letu ni kuwasaidia, hivyo basi watakaokubaliana watapata vibali na leseni za uwekezaji pamoja na biashara”, alisisitiza Mnali.

  Kongamano la kibiashara kati ya Tanzania na Ubelgiji linafanyika Jijini Dar es Salaam kwa siku tatu na limezinduliwa na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Injinia Stella Manyanya.

  0 0  Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Hassan Musa Kabeke akizungumza na wajumbe wa halmashauri ya BAKWATA mkoani Mwanza, masheikhe wa wilaya, Kata na Misikiti ya wilaya zote za Mwanza jana, kwenye ukumbi wa mikutano wa baraza hilo Mbugani katika Wilaya ya Nyamagana jana. Picha na Baltazar Mashaka

  Kiamu sheikh wa Mkoa wa Mwanza Hassan Musa Kabeke akiweka saini kwenye kitabu cha wageni kwenye ofisi za Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza jana tangu ateuliwe kushika wadhifa huo. Wanaoshudia wa kwanza ni Mwenekiti wa Halmashauri ya baraza hilo Amran Batenga, aliyekuwa akikaumu nafasi hiyo Hamis Almas na Kaimu Katibu wa baraza hilo mkoani humu Sina Mwagalazi.
  Kaimu Katibu Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza, sina Mwagalazi akizungumza na wajumbe wa Halmashauri kuu ya baraza hilo, masheikhe wa wilaya na kata wa wilaya za mkoani humu.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya BAKWATA Mkoa wa Mwanza Amran Batenga akizungumza na wajumbe wa halmashauri hiyo, masheikhe wa wilaya na kata za mkoani humu jana kwenye ukumbi wa baraza hilo Mbugani katika Wilaya ya Nyamagana.
  Kaimu Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza Hassan Musa Kabeke akiteta jambo na mtangulizi wake Sheikh Hamis Almas muda mfupi baada ya kumvisha joho.


  NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

  KAIMU Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza Hassan Musa Kabeke amesema moja ya vipaumbele vyake ni kuimarisha uchumi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na elimu ya dini.

  Sheikhe Kabeke alitoa kauli hiyo jana kwenye ukumbi wa ofisi za BAKWATA zilizopo Mbugani katika Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri ya mkoa, masheikh wa wilaya na kata mkoani humu.

  Alisema miongoni mwa mambo yanayomkera ni hali duni ya maisha na udhalili (unyonge) hivyo ameweka mikakati na mipango ya kuimarisha uchumi wa BAKWATA ili kubadilisha maisha ya walimu wa madrasa, masheikhe na maimamu wa misikiti ambao ni zao la uislamu (kiwanda) na misingi ya dini hiyo ya Kiislamu.

  Kaimu Sheikhe huyo wa mkoa alisema madrasa na msikiti ndio eneo dhaifu kutokana na walimu na masheikhe kushindwa kufundisha elimu ya dini na hata ujira wao ni mdogo wanazidiwa na watumishi wa ndani jambo ambalo linamkera na hivyo ameamua kulitafutia tiba.

  Sheikhe Kabeke alieleza kuwa ili kuboresha hali za walimu wa madrasa,masheikhe na maimu na waumini wa kiislamu lazima kuwe na vyanzo vya mapato yatakayosaidia Waislamu na haiwezekani kuendelea kuwa na BAKWATA ombaomba.

  “Niwaondoe hofu maana wapo watu wanaosema mimi ni mkali la hasha, mimi nina msimamo kwenye haki.Sote tunachukia ufisadi, wizi na umaskini na hata Mufti wa Tanzania kilio chake ni kutaka kuwatoa waislamu kwenye udhalili (unyonge).Katika hili la kuimarisha uchumi hata mkinilaumu niko radhi na Mwenyezi Mungu atanihukumu,”alisema Sheikhe Kabeke.

  Alisema waislamu hawana sababu ya kuwa wanyonge na wasimuone mkali bali atautumia na kuendelea na ukali huo kuwaondoa kwenye unyonge wao kuwataka viongozi dini ya kiislamu na waumini kutumia neema waliyopewa na Mungu kutafuta pepo na nyumba ya ahera.

  Aliongeza kuwa BAKWATA ina hali mbaya kiuchumi na ni taasisi pekee isiyo na wanachama wanaolipa ada wakati chombo hicho kinawapa heshima hivyo kwa Mkoa wa Mwanza dira na mipango yake ya kuleta maendeleo viongozi wa ngazi ya mkoa watachangia sh.8,000 mwezi sawa na sh. 2,000 kwa wiki fedha ambazo zitawekwa kwenye akaunti maalumu.

  “Tunataka kujenga uchumi kwa kuangalia rasilimali watu na kuanzia Oktoba viongozi watachanga sh. 8,000 kwa ngazi ya mkoa, wilaya sh. 4,000 , kata sh. 500 na tayari akaunti imefunguliwa kwa usalama wa fedha hizo ili ndani ya miaka tujenge jengo la kitega uchumi, kulipa mishahara ya walimu wa madrasa na masheikhe na kutatua kero zao,” alifafanua Sheikhe Kabeke.

  Aidha,kuhusu elimu ambayo imegawanyika sehemu tatu, aliwawataka waislamu kuacha kulalamika kuwa taasisi yao inahujumiwa na kuchafuliwa pamoja na kupoteza akidi yao ilhali wenye dhamana ya kufundisha elimu ya dini shuleni hawatimizi wajibu wao na kusababisha vijana waliolelewa kwa misingi ya dini kiislamu wakosekane.

  Alisistiza kuwa kama huo ni ukali basi hana budi kuacha hali iendelee ili uislamu ufe na kutoweka kwa sababu masheikhe na walimu hawaoni umuhimu wa kufundisha elimu ya dini shuleni licha ya kutengwa kwa vipindi vya dini.

  Kaimu Sheikh huyo wa mkoa alimshukuru Mufti wa Tanzania Abubakar Zuberi bin Ali kwa na Baraza la Ulamaa kwa kumteua, kumuona na kumuamini kuwa anafaa kumsaidia kwenye nafasi hiyo kubwa ambayo si ya kukimbiliwa na kuahidi kuwa kwenye uongozi wake hatabadilika na atakubali kushauriwa.

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya watu wa China Mhe. Wang Ke, katika mazungumzo hayo yaliyojikita katika kuimarisha mahusiano kwenye sekta mbalimbali zikiwemo Elimu, biashara, kilimo na teknolojia. Pamoja na mambo mengine Dkt. Ndumbaro amemshukuru Mhe. Wang Ke, kwa kuendelea kuliwakilisha Taifa lake vyema hapa nchini. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara ya Mambo ya Nje jijini Dar es Salaam Tarehe 25 Octoba, 2018 
  Maafisa Mambo ya Nje wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Dkt. Ndumbaro na Mhe. Wang Ke 
  Sehemu ya maafisa wa Ubalozi wa China wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Dkt. Ndumbaro na Mhe. Wang Ke. 
  Balozi Wang Ke akimwelezea Dkt. Ndumbaro zawadi ya sahani yenye mchoro wa maua 
  Dkt. Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Wang Ke (wa tatu kutoka kushoto), kulia ni maafisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kushoto ni Maafisa Ubalozi wa China.

  0 0


  Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin mkapa akifungua majada wa mazungumzo ya kusaka amani ya nchi ya Burundi kwenye ukumbi wa mikutano wa Ngurdoto Mountain Lodge leo wilayani Arusha

   Na Ahmed Mahmoud Arusha

  Serikali yashindwa kushiriki licha ya juhudi za msulushi, kundi kubwa la viongozi washiriki wakiwemo marais wastaafu, majadala wa mapitio ya kayanza na enteber kutoka na azimio moja

  Mchakato wa mazungumzo ya kusaka amani nchini burundi yameanza rasmi leo ambapo Makubaliano ya Kayanza 1 ,2 na ,makubaliano ya Enteber yanaendelea kujadiliwa ili kuweza kupata taarifa moja ambayo msuluhishi ataipeleka kwenye kikao cha wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika mashariki.

  Pamoja na jitihada za Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamini Mkapa ambaye ni msimamizi wa msuluhishi wa amani ya Burundi za kuitaka serikali ya nchi hiyo kuja katika meza ya maungumzo hadi sasa hawajtoa majibu yeyote kama waja au la Juhudi hizo zimepelekea wadau wengine katika mazungumzo ya amani kuendelea na mazungumzo hayo ikiwemo kujadiliana kuhusiana na baada ya serikali kutotuma mwakilishi hadi sasa huku wakiwa hawajatoa majibu kama wanakuja au la.

  Akifungua mazungumzo hayo mh.Mkapa akiwa anamaanisha kile alichosema kuwa hadi sasa hakupata maelezo sahihi kutoka kwenye serikali ya Burundi kwani hadi muda huu hawajatoa maelekezo yoyote kama watakuja au hawaji katika mazungumzo hayo. Amesema serikali hiyo imekuwa ikitoa maagizo ya kutaka kusijadiliwe baadhi ya vipengele ikiwemo suala la uchaguzi

  Amesema kuwa atapeleka maelekezo yake kwa msuluhishi wa mazungumzo hayo pamoja kikao cha viongozi wakuu wan chi za jumuiya ya Afrika mwezi November mwaka huu ili watoe maamuzi kwani wao ndio walimtuma kuifanya kazi hiyo.

  “Nimejitahidi kadiri ya uwezo wangu kuita serikali ya burundi lakini imeshindikiana kwa kuwa haya ni mazungumzo ya mwisho nasubiria mazimio haya ya kikao hichi niwasilishe kwenye kikao cha wakuu wa mataifa ya Afrika mashariki november”

  Amewataka viongozi hao kutoka makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo Asasi za kiraia,viongozi wa dini na wa kisiasa,vijana ,kinamama na wazee kuja na muongozo kwa kupîtia ,miongozo hiyo ili kusaidia kwenda kwenye uchaguzi 2020 .

  Amesema kuwa serikali ya Burundi Hata kama wasiposhiriki haiwezi kuathiri mazungumzo hayo kwani walishatoa msimamo wao tokea awali tunao hivyo wajadili na kupitia miongozo hiyo ilikufikia kwenda katika uchaguzi .

  Msimamo wa serikali ya Burundi kuhusu mkataba wa Kayanza unaona ndio dira ya kuelekea kwenye uchaguzi huru ambapo vyama vya upinzani wao wanaona kuwa muda sasa umefika kukaa mezani kujadili kwa pamoja mustakabali wa nchi yao na suala zima la uchaguzi utakao kuwa huru sanjari na makundi yote kuwa huru kushiriki kuijenga nchi yao.

  Msuluhishi wa mazungumzo hayo Rais mstaafu Benjamin Mkapa ameona kuwa viongozi hao wazingatie miongozo hiyo miwili ili aweze kuipitia na baadae kuweza kuja na moja ambayo itapelekwa kwenye vikao vya wakuu wa nchi za EAC.

  Wapinzani wa nje na ndani ya nchi wameshatoa miongozo yao kakiao chao cha Enteber cham waka 2018 kinaonyesha jinsi miongozo yao waliopitisha hivyo tuapitia tupate muongozo mmoja huu utakuwa ndio yatakuwa mapendekezo yatakayo saidia kusukuma

  0 0


  Muonekano wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Magoma lililopo katika hatua za mwisho za ujenzi.
  Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Mhe. Amiri Rajabu Mruma (kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Fundi wa Kampuni ya SUMA JKT alipokuwa akikagua ujenzi wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Magoma Wilayani Korogwe.
  Mhe. Jaji Mruma akiendelea na ukaguzi.
  Jaji Mruma akitoa elimu kwa Wajumbe wa Kamati ya maendeleo ya Kata ya Hale Wilayani Korogwe.
  Mhe. Jaji Mruma (wa tano kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya maendeleo ya kata ya Hale. Mstari wa kwanza kulia ni Afisa Tawala wa Mahakama ya Wilaya ya Korogwe, Bw. Emmanuel Machimo akifuatiwa na Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Tanga, Bw.Ahmed Ng’eni.
  (Picha na Amina Ahmad, Mahakama Kuu, Tanga)  Na Amina Ahmad, Mahakama Kuu, Tanga

  Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Mhe. Amir Mruma amemuhimiza Mkandarasi SUMA JKT kuharakisha ukamilishaji wa ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Magoma iliyopo Wilayani Korogwe ili ianze kutumika mara moja.

  Akiwa katika ziara ya kikazi Wilayani Korogwe; Mhe. Jaji Mruma alipata fursa ya kutembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Mahakama hiyo Oktoba 23 ambapo hata hivyo aliridhishwa na hatua iliyofikiwa.

  Katika ziara yake Wilayani humo, Mhe. Jaji Mfawidhi alifanikiwa pia kukutana na Kamati za Maendeleo za Kata ya Magoma na Mashewa na kutoa elimu juu ya haki na wajibu wa wananchi katika migogoro ya ardhi, kesi za ubakaji, mimba za utotoni na usimamizi wa Mirathi.

  Kwa upande wao; Wajumbe wa Kamati za Maendeleo (WDC) walitoa shukrani zao za dhati kwa Jaji Mfawidhi kwani ilikuwa ni mara yao ya kwanza kukutana na Jaji na kupewa elimu ya kisheria, hali iliyowapelekea kumuomba Jaji Mfawidhi aendelee na utarabu wa kukutana nao mara kwa mara kuwajengea wigo na uelewa mpana wa masuala ya kisheria ili kufanikisha majukumu yao.

  Sambamba na hilo, wajumbe hao walipongeza pia huduma zinazotolewa na Watumishi wa Mahakama na kukiri kwamba hakuna malalamiko yoyote juu ya huduma za Mahakama katika vituo vyao.

  Mhe. Jaji Mruma anatarajia kuendelea na ziara hiyo kwa kuongea na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Korogwe, kukagua Mahakama ya Wilaya Korogwe, Mahakama za Mwanzo Old Korogwe, Manundu, Bungu na Vugiri.

  Vilevile atazungumza na Watumishi wa Mahakama hizo, Kamati za maendeleo za Kata zilizomo Mahakama husika pamoja na wafungwa na Mahabusu wa Gereza la Manundu na Gereza la kilimo Kwa Mgumi lengo likiwa ni kuboresha huduma ya utoaji haki kwa ujumla.

  0 0

  Diwani wa kata ya Idodi Onesmo Mtatifikolo ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa utoaji wa hati hizo katika kijiji cha Kitisi ambapo jamii ya wabarbaigi wanaishi maeneo hayo nao walipewa hati miliki za kimira na kuanza kukomesha hama hama ya kabili hilo la wafugaji
  Wabarbaigi wanaoishi katika kijiji cha Kitisi kata ya Idodi wilaya ya Iringa wameanza kuondokana na mfumo dume baada ya kukubali wanawake kupatiwa hati miliki za kimila za maeneo ambayo wanamiliki mara baada ya kupata elimu kutoka mradi wa LTA wa feed the future
  JAMII ya Wabarbaigi wanaoishi katika kijiji cha Kitisi kata ya Idodi wilaya ya Iringa wakiwa kwenye picha na viongozi mara baada ya kupatiwa hati miliki za kimila za maeneo ambayo wanamiliki mara baada ya kupata elimu kutoka mradi wa LTA wa feed the future

  NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

  JAMII ya Wabarbaigi wanaoishi katika kijiji cha Kitisi kata ya Idodi wilaya ya Iringa wameanza kuondokana na mfumo dume baada ya kukubali wanawake kupatiwa hati miliki za kimila za maeneo ambayo wanamiliki mara baada ya kupata elimu kutoka mradi wa LTA wa feed the future unaotekelezwa katika wilaya za mkoa wa Iringa na Mbeya.

  Wakizungumza wakati wa kukabidhiwa hati za kimira wanawake wa kibarbaigi walisema kuwa awali walikuwa hawaruhusiwi kumiliki mali yoyote ile bali mali zote zilikuwa zinamilikiwa na wanaume.

  “Kwenye kabila letu mila zinawapa sana nafasi wanaume kumiliki mali na vitu vingine na kumfanya wanamke kuwa tegemezi jambo ambalo miaka ya nyuma limerudisha maendeleo nyuma ya wanawake” walisema wanawake hao wa Kibarbaigi

  Wanawake hao walisema kuwa baada ya kupata elimu ya upimaji wa ardhi na kuifanya ardhi kuwa na hati miliki imesaidia wanaume wa kabila hilo kuanza kuitambua nafasi ya mwanamke na kumuwezesha mwanamke naye kumiliki mali sawa na wanaume wa kabila la wabarbaigi.

  Tunaishukuru serikali na mradi wa LTA kwa elimu waliyoitoa kwa wanaume wa kabila la Barbaigi kwa kukubali wanawake wamiliki ardhi kwa kupewa hati miliki za kimira bila elimu hiyo wanawake sisi tungeendelea kuwa wakina mama wa nyumbani tu.

  Naye mwenyekiti wa kabila hilo la wafugaji Shabani Ntasham alisema kuwa kupatikana kwa hati miliki za kimira kumekomesha hamahama ya jamii hiyo pamoja na kumuwezesha mwanamke wa jamii hiyo kumiliki ardhi.

  “Sisi kabila letu ni watu wa kuhama hama hivyo baada ya kupata hati miliki za kimira sasa hatuwezi kuhama tena kwa kuwa tunamiki ardhi kisheria zinazotuwezesha kuboresha makazi yetu na kutufanya tuishi na kufanya shughuli zetu sehemu moja” alisema Ntasham

  Ntasham alisema Mradi wa LTA wa feed the future unaofadhiwa na USD umetoa elimu kwa kabila la barbaigi na kusaidia kuanza kuondokana kwa kiasi chake mfumo dume kwa kuwawezesha wanaume wa kabila hilo kuwagawaia wanawake ardhi na kuzikatia hati miliki za kimila.

  “Saizi umeona wanawake na wanaume wanafuraha kwa pamoja kwa kuwa kila mmoja anamiliki ardhi yake ambayo inamuwezesha kufanya jambo analolitaka kwa wakati wake tofauti kama ilivyokuwa hapo zamani” alisema Ntasham

  Akizungumza na wanakijiji hao baada ya kukabidhi hati hizo diwani wa kata ya Idodi Onesmo Mtatifikolo alisema kuwa hati hizo zitawasaidia kutenga maeneo kwa ajili ya matumizi mbalimbali kwa kuzingatia uwezo wa ardhi kuhimili idadi hiyo na kasi ya ongezeko la watu na mifugo kwa miaka mingi ijayo.Mtatifikolo aliongezea kuwa,hatua hiyo itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi kwa kuimarisha usalama wa miliki za ardhi na kuongeza thamani ambayo itawawezesha hata kukopesheka katika taasisi za kifedha zikiwemo benki.

  “Usajili wa ardhi ni muhimu kwasababu unaongeza ulinzi wa umiliki wa ardhi, unawezesha uwekezaji, unaongeza thamani ya ardhi na unapunguza migogoro ya ardhi,” alisema Mtatifikolo.Aidha Mtatifikolo aliwaomba Feed The Future wautanue mradi huo angalau ufike umalize kupima vijiji vyote vya kata hiyo huku akivikumbusha vijiji vyote vya kata hiyo kuendelea kutoa ushirikiano kwenye miradi ambayo inasaidia kukuza maendeleo ya nchi. 

  “Tunataka katika kipindi ambacho Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) tuhakikishe tunapima ardhi na mipango ya matumizi bora na ipimwe ili kila mwenye kipande chake cha ardhi awe na hati yake,” alisema Mtatifikolo.

  Mtatifikolo aliwataka wanakijiji wa kijiji hicho ambao hawajapimiwa maeneo yao kwa sababu mbalimbali ikiwemo ubishi na migogoro ya kifamilia kutumia vizuri muda ambao bado mradi huo upo katika wilaya hiyo na kuhakikisha nao wananufaika na zoezi hilo.

  Awali naibu mkurugenzi wa Mradi wa LTA, Malaki Msigwa aliwapongeza wataalamu wa mradi huo kwa kuhakikisha wanawasaidia wananchi wa kijiji cha Kitisi kupima maeneo yao na kupata hati miliki za kimila ambazo zitakuwa msaada mkubwa kwenye maendeleo ya kiuchumi.

  “Baadhi ya miradi imeibuliwa wakati wa upimaji wa ardhi hivyo ni fursa sasa kwa wananchi wenyewe kuitumia vizuri ardhi waliyopimiwa na kupewa hati miliki za kimila na kwa kuwa asilimia fulani kijiji hiki kimepimwa hivyo wanaweza kuwa kijiji cha mfano kwa kuwapa maendeleo hata wawekezaji wazuri kwa faida yao” alisema Msigwa

  0 0


  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu (katikati), akimfafanulia jambo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Arnold Kihaule, wakati walipokua wanatoka katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika Bungeni, jijini Dodoma leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhan Kailima.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu (kulia), akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Arnold Kihaule, wakati walipokua wanatoka katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika Bungeni, jijini Dodoma leo.
  Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Marlin Komba (kulia) wakifurahia jambo na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara hiyo, Wanja Mtawazo, wakati walipokua wanatoka katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika Bungeni, jijini Dodoma leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0


  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akitoa taarifa kuhusu usimamizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii jijini Dodoma kushoto ni Niabu wake Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akitoa maelezo kuhusu usimamizi wa uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kusaidia makundi maalum nchini wakati Wizara ilipokuwa ikiwasilisha taarifa kuhusu usimamizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo jijini Dodoma kushoto ni Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba akitoa maoni yake kwa Viongozi na Watendaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto walipowasilisha taarifa ya usimamizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mbele ya Kamati yake jijini Dodoma.
  Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu akitoa maelezo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo jijini Dodoma kuhusu Marekebisho ya Kanuni za Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na itakavyosaidia kuweka uwazi na uwajibikaji kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile.
  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Leornad Baraka akifafanua kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Usajili na Uratibu wa Mashirika hayo nchini mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii jijini Dodoma.
  Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii na watendaji kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakisikiliza hija mbalimbali wakati Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu ilipowasilisha taarifa kuhusu usimamizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mbele ya Kamati hiyo jijini Dodoma.
  Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii na watendaji kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakisikiliza hija mbalimbali wakati Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu ilipowasilisha taarifa kuhusu usimamizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mbele ya Kamati hiyo jijini Dodoma.

  Picha na Kitengo cha Mawasiliano- WAMJW

  …………………………………………………………………………………….

  Na Mwandishi Wetu- Dodoma

  Serikali imesema Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa mwaka 2005 imeweka masharti kwa mashirika yaliyokuwa yamesajiliwa katika Sheria nyingine na yanasifa za kusajiliwa kama Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, kuomba Cheti cha Ukubalifu chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.

  Hayo yamesema mapema leo mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiwasilisha taarifa ya usimamizi wa Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Maendeleo ya Jamii.

  Waziri Ummy Mwalimu amesema kimsingi Cheti cha Ukubalifu kinatolewa ili kuyaweka Mashirika yote Yasiyo ya Kiserikali chini ya usimamizi mmoja ili kuondokana na changamoto za awali ambapo mashirika hayo yalikuwa yakiratibiwa chini ya Sheria na Mamlaka zaidi ya moja.

  Waziri Ummy aliwaambia wajumbe wa Kamati hiyo kuwa kutokana na kutungwa kwa Sera na Sheria hii kwa mara ya kwanza Tafsiri ya “Shirika Lisilo la Kiserikali” ilipatikana rasmi akiongeza kuwa Tafsiri hii inayotofautisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Asasi nyingine za kiraia kama vile Jumuia za kijamii zinazosajili Wizara ya Mambo ya Ndani, Makampuni yanayosajiliwa BRELA na Bodi za wadhamini zinazosajiliwa na RITA.

  Aidha Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa kufuatia marekebisho ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mwaka 2005, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yalipewa hadhi ya utu inayoyawezesha kumiliki na kuuza mali, kutengeneza faida, kushitaki na kushitakiwa katika vyombo vya Sheria.

  Waziri Ummy amesema hadi kufikia Machi, 2018, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali 4,868 tayari yamefanyiwa uhakiki kati ya Mashirika 8,716 ambapo Taasisi 513 zenye sifa za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambazo zilikuwa zimesajiliwa katika Sheria nyingine zilielekezwa kuzingatia matakwa ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa kusajiliwa chini ya Sheria husika.

  Pamoja na uhakiki huo Waziri Ummy amesema bado yapo baadhi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo yamesajiliwa chini ya Sheria nyingine lakini hawakuja kuhakikiwa na wala bado hawajasajili kwenye Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002.

  Ameiambia Kamati hiyo kuwa taratibu za kuyaondoa kwenye Regista Mashirika ambayo yamesajiliwa chini ya Sheria hii na hayakujitokeza kwenye zoezi la uhakiki zinaendelea ikiwa ni pamoja na kuyafutia usajili.

  Akiongea kuhusu changamoto za kijamii kwa Mashirika hayo Waziri Ummy alisema uzoefu katika nchi nyingine unaonyesha kuwa baadhi ya Mashirika yametumika kufanikisha vitendo mbalimbali vya kihalifu na hivyo kuhatarisha usalama wa nchi.

  Amevitaja baadhi ya vitendo vya kihalifu ambavyo vinaweza kutumika kupitia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuathiri usalama wa nchi kuwa ufadhili wa ugaidi, Utakasishaji wa fedha haramu, Ujasusi, Usafirishaji wa binadamu, Kuhamasisha chuki dhidi ya Serikali, Kuhamasisha vitendo vinavyokinzana na mila na desturi za Kitanzania ikiwa ni pamoja na matendo ya Ushoga na Usagaji.

  Kwa upande wake Naibu Waziri amesema kuwa wanaendelea na uandaaji wa kanzi data ambayo itasaidia kuhainisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kwa sehemu yanapofanyia kazi na kuwezesha Serikali kuratibu vyema shughuli za Mashirika hayo kwa maendeleo ya Taifa.

  Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba amesema kuwa Serikali inawajibu wa kuyaratibu vyema na kuyalea Mashirka hayo kwa mustakhabali wa taifa.

  Akichangia wasilisho hilo mmoja wa wajumbe wa Kamati Mhe. Salma Kikwete amesema kuwa Serikali inatakiwa kuwekewa utaratibu mzuri kwa Mashirika hayo kufanya kazi sehemu ambazo zinachangamoto nyingi.

  Pia Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. John Jingu ameiambia Kamati kuwa lengo la kufuatilia fedha zinazoingia kupitia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali sio baya bali ni kuweze kujua mchango wa Mashirika hayo katika kuwaletea wananchi maendeleo.

  Wizara katika tamko lake la Mwezi wa tisa iliyataka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kuwasilisha ripoti ya mwaka 2016/17 yenye taarifa za mapato na matumizi na kutaja chanzo cha fedha kwa shirika husika.

  0 0


   
  (POINT OF IMPACT) ENEO AMBALO LORI LA MAFUTA MALI YA KAMPUNI YA MOUNT MERU LOGISTIC NA GARI NDOGO AINA YA PAJERO YENYE NAMBA STK.8925 MALI YA WIZARA YA KILIMO YALIGONGANIA
  PIX 2
  KAMANDA MUSILIMU AKIPOKEA MAELEZO TOKA KWA MKUU WA USALAMA BARABARANI WA WILAYA YA MANYONI-INSP JOHN (WA KATI) AMBAYE ALIAMBATANA NA MKUU WA USALAMA BARABARANI WA MKOA WA SINGIDA-ASP. EDSON (ALIYEVAA KHAKI) KATIKA ENEO LA TUKIO LA AJALI LILILOHUSISHA WATUMISHI WA WIZARA YA KILIMO
  PIX 3
  ALAMA ZA BREKI ZA LORI KATIKA USO WA BARABARA(SKEEDMARKS) KUTOKEA ILIPOANZIA HADI ILIPOKUJA KUGONGANA NA GARI DOGO MALI YA WIZARA YA KILIMO NA KUSABABISHA VIFO VYA WATUMISHI WA WIZARA HIYO.
  PIX 4
  MUONEKANO WA MBELE WA LORI LILILOGONGANA NA GARI DOGO MALI YA WIZARA YA KILIMO WILAYANI MANYONI MKOANI SINGIDA NA KUSABABISHA VIFO VYA WATUMISHI HAO
  PIX 5
  KAMANDA WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI(T), SACP FORTUNATUS MUSILIMU AKIKAGUA NAMNA AMBAVYO GARI AINA YA LORI LILILOGONGANA NA GARI NDOGO MALI YA WIZARA YA KILIMO LILIVYOHARIBIKA MARA BAADA YA AJALI HIYO ILIYOSABABISHA VIFO VYA WATUMISHI WATANO WA WIZARA HIYO.

  0 0

  NA MWAMVUA MWINYI, CHALINZE 

  SERIKALI imewahakikishia wananchi wa jimbo la Chalinze ,mkoani Pwani kuwa wataondokana na tatizo la maji na kubaki historia ifikapo mwezi april mwakani. 

  Tatizo la maji limekuwa likiwapa shida wananchi hao kwa miaka mingi hali iliyokuwa ikiondoa imani na serikali yao. Akizungumza na wakazi wa Chalinze, makamu wa Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu alisema ,shida ya maji Chalinze imekuwa kubwa ambapo wamekuwa wakikosa huduma hiyo ya maji safi na salama ya uhakika. 

  "Faraja inakuja, naimani ifikapo 2019 kero hii itakuwa historia, "alisisitiza. 
  Pamoja na hayo, Samia amewataka akinamama wajawazito wakiwa tayari kujifungua wakimbilie hospital ama vituo vya afya badala ya kuendekeza masuala ya kishirikina suala linalosababisha vifo kwa mama na mtoto. 

  Aliwaomba ,watumie vituo vya afya kunusuru vifo vya akinamama na watoto. Akizungumzia tatizo la mgogoro wa wakulima na wafugaji aliwaasa waheshimiane. Akitolea ufafanuzi juu ya kudhibiti tatizo hilo, naibu waziri wa mifugo na uvuvi, Abdallah Ulega alisema, NARCO inaanzisha maeneo ya wafugaji na imetenga heka 100,010 ambapo ng'ombe watahamishia malisho ndani ya Narco.

  "Miezi mitatu ng'ombe mmoja atalipiwa sh. 10,000 na ukiisha muda huo unaanza mkataba upya"alielezea.Ulega alifafanua, njia hiyo itapunguza ongezeko la mifugo hiyo.Mkurugenzi mkuu wa DAWASA Cyprian Luhemeja alieleza wanaendelea kufanyia kazi miradi mbalimbali na wanatarajia italeta jibu ndani ya jamii na kuondokana na kero hiyo. 

  Awali mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete anasema ,uchelewaji wa hatua za kupata huduma ya maji inaleta sura ya kufanya siasa kwa wananchi ambao bado wanaiamini serikali yao. Ridhiwani aliiomba, serikali kuendelea kusukuma na kuusimamia mradi wa CHALIWASA ili uanze kazi haraka na kuondoa kero hiyo. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakiteta jambo na ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) na Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi Abdallah Ulega katika ziara ya kukagua shughuli za kimaendeleo Bagamoyo na Chalinze. (Mwamvua Mwinyi

  0 0   Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akifafanua jambo kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu wakati wa ziara yake kwenye eneo la ujenzi wa bandari, Bagamoyo mkoani Pwani
  JPEG. NA. 2
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akigusa  eneo la ujenzi wa bandari, Bagamoyo kwenye mchoro huo wakati wa ziara yake mkoani Pwani. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye
  JPEG. NA. 3
  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Mhandisi Karim Mataka (wa kwanza kushoto) akimuonesha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu (wa pili kushoto) mchoro unaoonyesha eneo la ujenzi wa bandari, Bagamoyo wakati wa ziara yake mkoani Pwani. Wa tatu kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye
  JPEG. NA. 4
  Muonekano wa mchoro wa eneo la ujenzi wa bandari, Bagamoyo wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu (hayupo pichani) mkoani Pwani

  0 0

  Mhandisi wa Wilaya ya Madaba, Jonas Maganga akitoa maelezo kwa Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa kuhusu ujenzi wa chanzo cha Mradi wa Maji wa Maweso, mkoani Ruvuma.
  Afisa Maji wa Bonde la Ziwa Nyasa, Mhandisi Elise Englebert akitoa taarifa kwa Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa kuhusu ujenzi wa ofisi ndogo za Bonde la Ziwa Nyasa na Bonde la Ruvuma na Pwani ya Kusini, Songea Mjini.
  Waziri wa Maji, Profesa Mbarawa (aliyevaa kofia) akiwa na viongozi wa Halmashauri ya Madaba akisikiliza taarifa kuhusu Mradi wa Maji wa Lilondo akiwa juu ya tenki la mradi huo uliopo wilayani Madaba, mkoani Ruvuma.
  Waziri wa Maji, Profesa Mbarawa akipita kukagua maendeleo ya ujenzi wa tenki la Mradi wa Maji wa Madaba, mkoani Ruvuma.
  Mafundi wakiendelea na ujenzi wa tenki la Mradi wa Maji wa Madaba, mkoani Ruvuma.

  …………………………..

  Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa ametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Madaba na kukagua miradi ya maji ya Madaba, Lilondo na Maweso.

  Miradi hiyo ambayo ujenzi wake unaendelea inalenga kuimarisha huduma ya upatikanaji wa maji kwa maeneo ya vijiji hivyo, mkoani Ruvuma.

  Akizungumza na wananchi wa Lilondo, Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amepongeza juhudi za wakazi wa kijiji hicho wa kukabiliana na tatizo la maji kwa kujenga tenki la maji na kuahidi wizara yake itatoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa mabmba na kazi ya ulazaji wa mabomba hayo kwa ajili ya kusambaza maji kwa wananchi.

  Amesema wananchi hao ni mfano wa kuigwa na kuwashukuru kwa nia yao njema ya kuinga Serikali mkono katika kuleta maendeleo ya Sekta ya Maji. Akitoa ahadi kwa viongozi wa Halmashauri hiyo kuwa atalipa fedha zilizobaki kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya Lilondo na Maweso ili waweze kumaliza kazi ya ujenzi.

  Aidha, Profesa Mbarawa ameanzisha zoezi la upandaji miti katika chanzo cha maji Maweso na kuitaka Serikali ya Kijiji na wananchi wapande miti ya kutosha na zoezi hilo liwe endeevu kwa lengo la kuwa na chanzo cha uhakika cha maji kwa miaka mingi. Mradi wa maji wa mtiririko wa Lilondo umefikia asilimia 65 ya ujenzi, lengo la mradi likwa ni kutoa huduma kwa wakazi 5,919 ifikapo 2024 katika Kijiji cha Lilondo, utagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 1.048.

  Huku mradi wa maji wa mtiririko wa Maweso ukiwa umefikia asilimia 65 ya ujenzi, lengo la mradi ni kutoa huduma ya maji kwa wakazi 2,876 ifikapo 2023 katika Kijiji cha Maweso, utagharimu zaidi ya Silingi Milioni 546. Profesa Mbarawa amemaliza ziara yake ya siku 6 mkoani Ruvuma ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya maji

older | 1 | .... | 1707 | 1708 | (Page 1709) | 1710 | 1711 | .... | 1903 | newer