Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

Mdau Mahmoud Shoo na Leila (Jennifer) Kakolaki walivyomeremeta jijini dar

$
0
0
 Mdau Mahmoud Shoo na Mai Waifu wake,Leila (Jennifer) Kakolaki wakiwa na nyuso za bashasha na raha tele wakati wa tafrija yao ya kuwapongeza mara baada ya kumeremeta,iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Shengeni,Mbezi Beach jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Maharusi Mahmoud Shoo na Mai Waifu wake,Leila (Jennifer) Kakolaki wakijadiliana jambo kwa furaha wakati wa tafrija yao ya kuwapongeza mara baada ya kumeremeta,iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Shengeni,Mbezi Beach jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wakipata kinywaji kwa namna yao.
Maharusi wakiwa na wapambe wao wakati wa tafrija yao ya kuwapongeza mara baada ya kumeremeta,iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Shengeni,Mbezi Beach jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


KINANA AWAUNGURUMIA WATENDAJI WA VYAMA VYA MSINGI USHIRIKA NA BAADHI YA WATENDAJI WA SERIKALI MKOANI RUVUMA.

$
0
0
 Ndugu Kinana na Ujumbe wakienda kukagua ujenzi wa jengo la Wodi ya Wazazi ya akina mama na Watoto,kwenye hospitali ya Wilaya ya Namtumbo.
Pichani kulia ni Mbunge wa jimbo la Namtumbo,Mh.Vita Kawawa,Katibu wa NEC,Siasa Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye,Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt.ASharose Migiro wakishiriki katika ujenzi wa msingi wa Wodi ya Wazazi na Watoto katika hospitali ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

 Pichani shoto ni Mbunge wa jimbo la Namtumbo,Mh Vita Kawawa pamoja na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana  wakishiriki kuchanganya sementi kwa ajili ya ujenzi wa Wodi ya Wazazi ya akina mama na Watoto inayojengwa kwenye hospitali ya Wilaya ya Namtumbo kwa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete.
 Jengoo la Utawala wa hospitali hiyo ya wilaya ya Namtumbo.
 Pichani shoto ni Mbunge wa jimbo la Namtumbo,Mh Vita Kawawa akimuongoza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake walipokuwa wakikagua majengo ya hospitali  hiyo.
 Barabara ya kuelekea kwenye hospitali hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM akiwa ameongozana na Ujumbe wake wakipata taarifa ya mtambo wa kufua umeme katika kituo cha kufua Umeme ndani ya Wialaya ya Namtumbo. 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akifungua shina la Wakereketwa la Waendesha Bodaboda Wilayani namtumbo,Kinana aliwachangia vijana hao kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya kuwafungulia akaunti ya benki,ili waweze kupata mikopo  ya kununua piki piki kwa ajili ya shughuli zao.
Katibu wa NEC Siasa,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa wa Lwinga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Namtumbo kwenye uwanja wa Taifa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Lwinga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Namtumbo kwenye uwanja wa Taifa mkoani Ruvuma.Ndugu Kinana na ujumbe wake wapo kwenye ziara ya kikazi mkoani Ruvuma,Mbeya na Njombe katika kukagua Utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha CCM,kusikiliza matatizo ya Wananchi ikiwa ni pamoja na kuwahimiza kushiriki katika shughuli mbalimbali za kujiletea maendeleo. Katika Ziara hiyo ya Tunduru na Namtumbo wananchi wamelalamikia kuhusu bei ya zai la Korosho na Tumbaku,kama vile haitoshi wanancho hao walikwenda mbali zaidi kwa kulalamikia suala zima la Mbolea.
21
Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Mh. Vita Kawawa akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara mjini Namtumbo, mkutano huo umefanyika kwenye uwanja wa Taifa.Vita Kawawa amewatuhumu baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika na Ofisa Ushirika wa mkoa huo wa kuwambambikizia madeni wakulima wa Tumbaku kupitia ruzuku ya mbolea,ambapo makadirio ya mbolea inayohitajika kwa wakulima huongezwa kinyemela na Wananchi kuachiwa mzigo mkubwa wa kulipa madeni ambayo hayawahusu,hali inayowapelekea wakulima hao kutokuwa na imani na baadhi ya viongozi wa chama na serikali.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya Mchomoro Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma mara baada kupokelewa vyema na wananchi ya Wilaya hiyo ya Namtumbo.
 Mbunge wa jimbo la Namtumvo,Vita Kawawa akifafanua jambo kwa Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt.ASharose Migiro pamoja na Katibu wa NEC Siasa,Itikadi na Uenezi,Nnape Nnauye ndani ya Kata ya Mchomoro Wialayani Namtumbo mkoani Ruvuma.
 Katibu Mkuu wa CCM,ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakipata chai nyumbani kwa balozi wa shina,Said Husein mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Mchomoro wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.Kinana na ujumbe wake kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama na kukagua uhai wa chama katika mkoa wa Ruvuma.

ILO YAENDESHA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI NA KUJIKINGA NA VVU KWA WANAWAKE CHALINZE

$
0
0
SONY DSC
Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi ILO Bi. Getrude Sima akisisitiza jambo kwa washiriki kuhusiana na mafunzo waliyoyapata yakawe chachu ya kuleta maendeleo.
SONY DSC
Picha juu na chini ni baadhi ya wakinamama wa Chalinze wakifuatilia mafunzo hayo yaliyomalizika mwishoni mwa wiki.
SONY DSCSONY DSC 
Mgeni rasmi Kaimu Afisa Tarafa ya Chalinze kata ya Pera Bw. Rashid Kiwamba akikabidhi vyeti kwa mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo.
SONY DSC 
Mwanamke wa Kimasai Paspen Kisota akipokea cheti chake baada ya kuhitimu mafunzo hayo.
SONY DSC
Picha juu na chini mgeni rasmi Kaimu Afisa Tarafa ya Chalinze kata ya Pera Bw. Rashid Kiwamba na Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi ILO Getrude Sima wakiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu.
SONY DSCSONY DSC
Fundi Sanifu wa Maabara ya Afya Bw. Rwezahura Merehiory akichukua damu kwa ajili ya vipimo vya VVU kwa mmoja wa washiriki wa semina ya mafunzo ya Ujasiriamali na Kupambana na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi iliyoratibiwa na shirika la Kazi duniani (ILO) wilaya ya Chalinze mwishoni mwa wiki.


SONY DSC
Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi ILO Getrude Sima (kushoto) akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Kaimu Afisa Tarafa ya Chalinze kata ya Pera Bw. Rashid Kiwamba (kulia) kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya siku sita kuhusu maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa Wanawake wasiokuwa kwenye ajira rasmi na wanaoishi pembezoni katika juhudi za kudhibiti maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.
.Zaidi ya wanawake 220 wafikiwa na mradi huo wa Shirika la Kazi Duniani

Na Damas Makangale, Chalinze Moblog.

SHIRIKA LA KAZI DUNIANI (ILO) limeendesha mafunzo ya siku sita kuhusu maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa Wanawake wasiokuwa kwenye ajira rasmi na wanaoishi pembezoni katika juhudi za kudhibiti maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi. Moblog inaripoti. Mradi huo wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) unalenga wanawake wote ambao wapo pembezoni wa barabara na mipakani kwa sababu wapo katika hali ya hatarishi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoa Pwani Wilayani Chalinze, Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) Getrude Sima amesema ndani ya siku sita mradi wa mapambano ya Ukimwi chini ya ILO umewafikia wanawake 120 katika kata za Pera, Chamakweza, Mpingo, Bwilingu, Msolwa na Mdaula.
SONY DSC
Mshauri wa Biashara wa shirika lisilokuwa la Kiserikali (NGO) TAPBDS Bi. Theresia Kato akifundisha wakinamama wa Chalinze (hawapo pichani) jinsi ya kuandika na kuandaa mchanganuo wa biashara katika mafunzo hayo ya siku sita yaliyoandaliwa na Shirika la kazi Duniani (ILO).

Amesema tangu mradi uanze kutekelezwa hapa nchini wakutoa mafunzo ya ujasiriamali na kujikinga na Virusi vya Ukimwi wameweza kuwafikia wanawake 220 nchi nzima katika maeneo ya pembezoni na mpakani kama vile Tunduma, Kyela na Namanga.

“Unajua wanawake wengi wanakuwa katika kundi hatarishi pale wanapokuwa katika maeneo ya mpakani na pembezoni mwa barabara kwa mfano Chalinze kwa sababu ya muingiliano wa watu hasa Madereva na Wafanyabiashara,” amesema Sima.

Sima ameongeza kuwa katika mradi huu wa mapambano ya Ukimwi malengo ni kumuelimisha Mwanamke ili ajitambue na aweze kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa kumfundisha stadi za maisha pamoja na ujasiriamali.

Amesema mradi unalenga wanawake wasiokuwa katik ajira rasmi ili kuongeza muamuko miongoni mwa wakinamama mitaani na vijijini ili waweze kukabiliana na vishawishi katika sehemu zao wanazoishi.
SONY DSCBi. Theresia Kato akiwaelekeza washiriki namna ya kujaza fomu za kuombea mikopo kwa taasisi mbalimbali.

Kwa upande Mshauri wa Biashara toka shirika lisilo kuwa la Kiserikali TAPBDS, Theresia Kato amesema kuwa biashara ndogo ndogo ni muhimu katika kumjengea mwanamke uwezo wa kujiamini na kujitegemea.
“lazima wanawake waamuke ili waweze kuanzisha biashara zao na kuandika mchanganuo wa biashara na kutafuta mitaji kupitia taasisi mbalimbali za fedha hapa nchini,” amesema.

Dr Donald Thomas alipohojiwa na Jamii Production

$
0
0
Katika kipengele hiki cha HUYU NA YULE, wiki hii utasikia mahojiano niliyowahi kufanya na Dr Donald Thomas. Mhandisi na mwanaanga wa Marekani.
 Ilimchukua miaka 33 kutimiza ndoto zake za kuelekea kwenye Orbit. Na baada ya kwenda kwenye Orbit mara nne, akastaafu na sasa anahimiza wanafunzi wa chekechea kujiunga na masomo ya Sayansi na Hesabu kwa manufaa ya kizazi kijacho
Nilipata fursa ya kuhojiana naye ambapo alieleza mengi mema

Kwa maoni, ushauri, nk usisite kutuandikia jamiiproduction@gmail.com

LG TO FOCUS ON NEW PREMIUM PRODUCTS

$
0
0
Global electronics giant LG Electronics has announced plans to focus on its premium range of products, from smartphones to TV sets and refrigeratorsduring the peak holiday season as it works towards stamping its position in the market.

Among the premium products that LG will be focusing on are: the LG G2 smartphone, as well as maximizing 3G and mid-tier mass devices such as the L II Series and F Series under the mobile phone segment.


In the home appliances segment, it will also be looking to focus more on OLED TVs and Ultra HD TVs.


The new strategic direction that will be rolled out globally follows impressive results posted by the firm in the third quarter of 2013 in which it recorded US$12.51 billion in consolidated revenues. In recent months, LG Electronics has been ramping up its position in the smartphone market. During the third quarter of 2013, it shipped a total of 12 million smartphones.


The focus on premium products and mid-tier mass devices is expected to appeal to the Tanzanian market as LG increases its competitiveness and marketing investments.


At the same time, the global leader and technology innovator in consumer electronics, mobile communications and home appliances noted that increased research and development investments and weak global market conditions continue to impact the business.



However, the Air Conditioning and Energy Solutions division will continue to focus on growing its market share of non-seasonal products and higher margin products such as new commercial air conditioning system that will later this month be introduced to the Tanzanian market.

MSAMA ATANGAZA UZALENDO TAMASHA LA KRISMAS

$
0
0
MKURUGENZI wa Tamasha la Krismasi, Alex Msama amewataka wafanyakazi wake wa makampuni yake kutangaza uzalendo wa hali ya juu kwa sababu tamasha hilo nia yake ni kutangaza amani na upendo.
Akizungumza na wafanyakazi wake hivi karibuni, Msama alisema tamasha hilo litakuwa na wageni wengi kutoka nchi mbalimbali sambamba na viongozi wa Tanzania.    
Msama aliyasema hayo katika maandalizi ya tamasha hilo ambalo linatarajia kufanyika Desemba 25 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na baadaye mikoa ya Morogoro, Dodoma, Arusha na Kilimanjaro.
“Kila mmoja mfanyakazi awe askari kwa mwenzake ili kufanikisha maendeleo ya Tamasha hilo ambalo litakuwa na dhamira ya kusaidia wanaoishi katika mazingira hatarishi,” alisema Msama.
Aidha Msama alisema umakini utaongezeka zaidi katika suala la tiketi ambazo zitatoka nje ya Tanzania kwa sababu ya kukwepa wizi unaofanywa na baadhi ya wasilolitakia mema tamasha hilo.
“Tunajipanga kutengeneza tiketi kutoka nje ya nchi ambazo zimepiga hatua zaidi kimaendeleo ili kukwepa wizi unaofanywa na wajanja wachache wasiolitakia mema tamasha hilo lenye lengo la kusaidia wenye uhitaji maalum,” alisema Msama.

Nape awawakia live Mawaziri wasio wajibika kutatua kero za Wananchi .

Serikali kuendelea kutumia rasilimali kukabiliana na umasikini.

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha  Saada Mkuya  Salum (kulia)akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu  mkutano wa kupitia  utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali (GBS) ulioshirikisha  na  Washirika wa Maendeleo(DPS) na wadau mbalimbali kutoka serikalini uliofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dares Salaam. Kushoto ni  Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Profesa Adolph  Mkenda.
 Mwenyekiti  wa Washirika  wa Maendeleo  Balozi wa Sweden , Lennarth  Hjeimaker (kulia)akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu  mkutano wa kupitia  utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali (GBS) ulioshirikisha  na  Washirika wa Maendeleo(DPS) na wadau mbalimbali kutoka serikalini uliofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dares Salaam (kulia) Naibu Waziri wa Fedha  Saada Mkuya  Salum .

Na Magreth Kinabo 

 Serikali imesema kwamba itaendelea kuelekeza rasilimali  katika masuala  ya  elimu,  afya,  kilimo ikiwa ni hatua ya kuweza kupunguza umasikini  kwa haraka ikiwa ni pamoja  na  kukabiliana  na changamoto zilizopo katika sekta mbalimbali .

 Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Fedha  Saada Mkuya  Salum wakati  akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu  mkutano wa  mwaka  2013 wa kupitia  utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali (GBS) ulioshirikisha  na  Washirika wa Maendeleo(DPs) na wadau mbalimbali kutoka serikalini uliofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dares Salaam.

 “Changamoto inayotukabili ni kuleta maendeleo kwa haraka.  Uchumi wa nchi unakuwa kwa asilimia 7 lakini umasikini umepungua kwa asilimia 2,”alisema Waziri huyo.

 Alisema  changamoto inayoikabili serikali ili kukabiliana na umasikini nchini ni kuhakikisha inaelekeza rasilimali zake  ili ziweze kuzalisha ajira .Pia  kuangalia idadi ya watu  kulingana na uchumi wa nchi.

 Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri huyo kufuatia  Mwenyekiti  wa Washirika  wa Maendeleo Balozi wa Sweden ,  Lennarth  Hjeimaker  kueleza  kuwa    hatua za  kupunguza  umasikini  na upatikanaji wa huduma za jamii  bado ni ndogo  ,kiwango cha ufaulu kwa shule za sekondari na msingi kushuka na  uwiano wa walimu na wanafunzi bado mdogo,  zaidi ya nusu ya watu vijijini wahapati maji safi na salama na upatikanaji wa nishati vijijini bado ni changamoto.

 Wadau hao pia wameishauri Serikali kuendelea kupambana na tatizo la rushwa nchini.

 Katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita 2012/2013  wadau hao walichangia Dola za Marekani milioni 560 na mwaka huu wa fedha  waliahidi kutoa Dola za Marekani milioni  561 hivyo hadi sasa Serikali imeshapokea Dola za Marekani milioni 290.2.

BEATRICE MROKI APATA KIPAIMARA KANISA LA KKKT UKONGA

$
0
0
Novemba 17, 2013 ilikuwa siku ya furaha sana kwa Beatrice Mroki (kushoto) kwa kupata sakrementi yake ya Kipaimara baada ya kuhitimu mafunzo ya miaka miwili katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Ukonga jijini Dar es Salaam. Pichani ni Beatrice akigonganisha glasi na msimamizi wake Neema Steven wakati wa tafrija maalum ya kumpongeza iliyofanyika katika ukumbi wa Samunge Ukonga Mazizini.
 Hapa ilikuwa Kanisani wakisubiri kupokea Kipaimara katika KKKT Ukonga
 Baada ya Kipaimara baba na mama yake Beatrice wakilamba picha na Binti yao.



 Nasisi tulijipiongeza kwa malezi bora Mungu aliyotujalia

 Bibi zake Beatrice wakijipongeza na kumtakia heri Mjukuu wao.

 Beatrice na wapambe wake...

Pongezi kutoka kwa wazazi...

 Dada Kilave akimpongeza mdogo wake

 Kikundi cha Ligimilo wakicheza kwaito...

 Keki ilikuwa hiviii ...

 na ilikatwa hivi....

 Ikaliwa hivi... Hapa Beatrice akimlisha mdogo wake Glory.


 Father Kidevu wakati wa zawadi alimpa gwala binti yake

 Muongezaji maarufu wa filamu za Kibongo Leah Mwendamseke nae alikuwepo.


 Ligimilo wakitangaza zawadi yao..

 Weee...!! Tulia nami nimsaidie baba leo...Glory Mroki akimfotoa dadayake picha.

 Kazawadi haka jamani... siku moja nitavaa shati lake.

 Huko jikoi mambo yalikuwa hivi

 Mwisho lilishuka sebene kali kutoka kila aina ya muziki kuanzia injili hadi katika kiduku namna hii.

KINANA NA UJUMBE WAKE AWASILI MJINI SONGEA LEO

$
0
0
 Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana ukipita leo katika 'mkeka' wa barabara, ulipokuwa ukitokea wilayani Namtumbo kwenda wilayani Songea mkoani Ruvuma.Ndugu Kinana yuko katika ziara mkoani Ruvuma, kukagua utelekezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kushirikiana nao kupata njia za kuzitatua, barabara hiyo ni miongoni mwa barabara kadhaa zilizojengwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM na kuwaondolea wananchi kero ya kusafiri kwenye barabara mbovu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki shughuli za ujenzi katika Zahanati ya Mahilo wilayani Songea mjini .
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya mwalimu kwenye shule ya sekondari Mdandamo wilayani Songea mjini
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi wa nyumba ya maabara katika shule ya sekondari Mdandamo wilayani Songea mjini
 Katibu wa NEC, Itikati na Uenezi Nape Nnauye akishirikiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wai Ruvuma, kuondosha gogo kwenye eneo la ujenzi wa Zahanati katika Kata ya Mahilo, Songea mkoani Ruvuma.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na waasisi wa CCM wilaya ya Songea mjini, kutoka kushoto ni Mzee Hashimu Gawaza na kulia kwa Katibu Mkuu ni Mzee Clemenci Nyoni ambao walikaa kikao cha kwanza na Mwalimu Nyerere tarehe 12 Agosti 1957 wakati wa harakati za kuikomboa nchi,anayefuatia kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho.
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akiwa na Wazee hao.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wazee waasisi pamoja na wananchi wa kata ya Matogoro ambapo alitaka wana CCM kuenzi kazi zilizofanywa na waasisi wetu kwa kudumisha mshikamano ,umoja na amani.


 Ofisi ya Kata ya Matogoro  CCM ambayo iliwekwa jiwe la msingi tarehe 20 Desemba 1986 na Mzee Rashid Mfaume Kawawa,Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ameahidi kutoa bati za kuezeka ofisi  hiyo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchama wa Shina namba 1tawi la Ambachai kata ya Mfaranyaki nyumbani kwa Balozi wa Shina Ndugu Magreth Mchula,Katibu Mkuu alisisitiza viongozi wa ngazi za chama kuwa na mazoea ya kutembelea mabalozi wao kwani ndio msingi wa wanachama.
 
 Wanachama wa Shina namba 1 wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,pichani Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa amejumuika na wanachama kukaa nao pamoja kwenye mkeka.

 Mzee Mustafa Mohamed Songambele akionyesha furaha yake alipokutana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana , Mfaranyaki Songea,Katibu Mkuu ameanza leo ziara ya kuetembelea wilaya ya Songea mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na viongozi mbalimbali wa CCM waliofika kumlaki alipowasili kwenye eneo maarufu linalojulikana kama Nonga Nonga wilaya ya Songea mjini.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisalimiana na Mzee Mustafa Songambele mmoja wa waasisi wa Tanu na mwanasiasa wa muda mrefu.
 Mlezi wa Vijana wajasiriamali wa Mfaranyaki Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimu vijana hao baada ya kufunguliwa kwa Shina lao na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia ngoma ya kutoka kikundi cha ngoma cha Mfaranyaki baada ya kuzindua shina la vijana wajasiriamali wa Mfaranyaki.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishirikiana na wananchi wa Kata hiyo kusafisha eneo kwenye ujenzi wa Zahanati ya kata hiyo. Wanne kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
Wazee pekee wawili walisosalia kati ya waliokuwepo kwenye mkutano wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere wakati wa harakati za TANU, mwaka 1957 katika eneo la Matogolo, Songea mkoani Ruvuma, Hashim Gawaza (92) na Clemence Simon Nyoni (93), wakivishwa vazi la heshima na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipowasili eneo hilo leo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kushoto) akiwa na wanachama wa Shina namba noja, waliokuwa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipotembelea nyumbani kwa Mjumbe wa Shina namba moja, Magreth Mtiula, eneo la Mfaranyaki mjini Songea.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimsalimia mama huyu, Mkazi wa mtaa wa Mfaranyaki mjini Songea, baada ya kumuona kuwa mwenye shangwe kubwa wakati msafara wa Kinana ulipopita karibu na nyumbani kwa mkazi huyo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akifungua Shina la Vijana Wajasiriamali wa CCM la Dk. Asha-Rose Migiro, katika mtaa wa Mfaranyaki mjini Songea leo
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akisalimia baada ya kuzinduliwa shina hilo.

WABUNGE WA EALA KUTOKA TANZANIA WAMPONGEZA RAIS KIKWETE, WASISITIZA MAZUNGUMZO KUTATUA MIGOGORO

$
0
0
Kimbisa akizungumza na wanahabari Ukumbi wa Idara ya habari Maelezo.
WABUNGE wanaoiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki wamesema suluhisho la matatizo ya nchi za Maziwa Makuu yatapata ufumbuzi wa kudumu iwapo kutakuwa na utaratibu wa kukaa meza moja kwa pande zote husika na kufanya mazungumzo ya kuleta amani.

Hayo yalisemwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa wabunge hao, Adam Kimbisa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam ambapo pia alipongeza hotuba ya Rais Jakaya Kikwete alioitoa Bungeni Dodoma Novemba 7 mwaka huu juu ya Jumuiya hiyo.

“Sisi tunaamini amani ni jambo la msingi katika Afrika Mashariki na hasa katika nchi zilizo katika Maziwa Makuu. Tunawapongeza wanajeshi wetu na wanajeshi Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa kazi nzuri walioifanya iliyowezesha mafanikio kupatikana” alisema.

Akielezea juu ya baadhi ya nchi wanachama wa EAC ambao ndio waanzilishi wa vurugu mbalimbali na migogoro Mwenyekiti huyo alisema kuwa Tanzania imekomaa kisiasa hivyo hawawezi kuwaondoa wale wanaoleta chokochoko kwa kuwa dawa ni kuzungumza na sio kuwatoa.
Mtangamano.

Aidha Kimbisa amesema misingi ya Utengamano wa kiuchumi ikijengeka vizuri na kufanya kazi ipasavyo wananchi wote wa Afrika Mashariki watafaidika na hivyo suala la kuruka hatua yoyote ni jambo lisilokubalika.

“Tunaungana na kauli ya Rais kwamba Tanzania ni kati ya nchi zinazotaka ngazi zote za mchakato wa Mtangamano zitekelezwe moja baada ya nyingine bila kuruka hatua yoyote. Hatua ya kwanza ni Umoja wa Forodha inafuata soko la Pamoja kasha Umoja wa Fedha na hatimaye shirikisho la Kisiasa” alisema.

Alisema hadi sasa ni hatua mbili zilizotiwa saini na mchakato wa kuweka saini Umoja wa fedha unatarajiwa kutiwa saini baada ya kikao cha Juu cha Marais kinachotarajiwa kufanyika mjini Kampala Novemba 30 iwapo masuala yote muhimu ya mchakato huo yatakuwa yamekamilika.

 “Jambo la msingi ambalo hata Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya imesema wazi kwamba Jumuiya lazima iwe ni ya wananchi kwa manufaa ya wananchi na isiwe ya viongozi. Wananchi washirikishwe katika kila hatua na kila ngazi ili iweze kushiriki kikamilifu kwa ajili ya maslahi yao” alisema. 


 Kuhusu VISA alisema kuwa wao wanaruhusu nchi nyingine kuendelea lakini Tanzania bado hawajafikia muafaka kwa kuwa wanaangalia maslahi ya nchi kwanza. Katika Hatua nyingine, Wabunge hao walimpongeza Rais Kikwete kupeleka kikosi cha Wanajeshi katika Brigedia Maalum iliyoundwa na Umoja wa Mataifa ili kuongeza nguvu ya kudhibiti waasi Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA),Adam Kimbisa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati wabunge hao wakitoa pongezi kwa Rais Jakaya Kikwete kwa hotuba yake aliyoitoa Bungeni hivi karibuni. Kushoto ni Katibu wa Wabunge hao, Shy-Rose Bhanji.
wanahabari wakifuatilia hotuba hiyo..
Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA),Adam Kimbisa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati wabunge hao wakitoa pongezi kwa Rais Jakaya Kikwete kwa hotuba yake aliyoitoa Bungeni hivi karibuni. Kushoto ni Katibu wa Wabunge hao, Shy-Rose Bhanji. Kulia ni Mkurugezni Msaidizi wa MAELEZO, Zamaradi Kawawa.
<!--[if gte mso 9]>

Serikali yatoa ufafanuzi wa vifaa vya kutoa risiti za kieletroniki.

$
0
0

Naibu Waziri wa Fedha  Saada Mkuya  Salum (kulia)akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu utata wa vifaa vya kieletronik vya kutoa risiti(EFD)
========  =======  ========
Na Magreth Kinabo

Serikali imesema imeshaelekeza wasambazaji wa vifaa vya eletroniki vya kutoa risiti (EFD) kuuzwa  kwa bei tofauti kulingana  na ubora wake.

Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Fedha  Saada Mkuya  Salum wakati  akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam.

 Naibu Waziri huyo ,alitoa ufafanuzi huo  baada kuulizwa swali na waandishi wa habari kufutia mgomo wa wafanyabiashara unaoendelea katika baadhi ya mikoa kufutia kifaa hicho kuuzwa kwa bei ya Sh. 700,000 na 800,000 ambayo wanadai  ghali.

“ Utumiaji wa EFD si kumkomoa mfanyabiashara bali ni kuongeza mapato ya Serikali katika kuendeleza maendeleo ya nchi".

Kwa mujibu wa  Naibu Waziri huyo alisema vifaa hivyo vipo vinavyouzwa kuanzia bei ya 100,000 na kuendelea,hivyo na kuwataka wasambazaji kuuza vifaa hivyo kulingana na bei iliyopangwa kulingana na ubora.

NBS KUENDELEA KULINDA UBORA WA TAKWIMU ZAKE BARANI AFRIKA.

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa shughuli za kitakwimu Bi.Aldegunda Komba akitoa ufafanuzi wa ushiriki wa Tanzania katika maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika kwa mwaka 2013. Maadhimisho hayo yatafanyika Novemba 20 jijini Dar es salaam.
 =========  =======  ======
NBS KUENDELEA KULINDA UBORA WA TAKWIMU ZAKE BARANI AFRIKA.
 
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imesema kuwa itaendelea na jukumu la kukusanya na kutoa takwimu Bora zinazokidhi mahitaji na viwango vinavyokubalika kimataifa ili kuiwezesha serikali na wadau mbalimbali kufanya maamuzi sahihi katika mipango ya maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi wa shughuli za kitakwimu Bi.Aldegunda Komba wakati akitoa ufafanuzi wa ushiriki wa Tanzania katika maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika kwa mwaka 2013.

Bi. Aldegunda amesema  maendeleo ya serikali yoyote ile duniani yanategemea uwepo wa takwimu Bora ambazo hurahisisha utungaji wa sera sahihi na upangaji wa mipango ya maendeleo ya wananchi kwa kufuata vipaumbele na fursa zilizopo.

Ameongeza kuwa takwimu bora huiwezesha serikali kufanya maamuzi sahihi na kutathmini mwenendo na mafanikio ya mipango mbalimbali inayopangwa na kukidhi mahitaji ya wadau mbalimbali kwa kuwapatia taarifa za Afya, kilimo, watu na makazi, taarifa za mapato na matumizi ya kaya.

Amesema Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi zinazothamini mchango wa takwimu kwa maendeleo ya taifa inaungana na mataifa mengine barani Afrika kuadhimisha Siku ya Takwimu Afrika ambayo huadhimishwa tarehe 18 Novemba.

Ameeleza kuwa hiyo nchini Tanzania itaadhimishwa tarehe 20 jijini Dar es salaam chini ya kauli mbiu isemayo “Takwimu Bora kwa Maendeleo ya Afrika” ikilenga  kuifahamisha jamii juu ya umuhimu wa matumizi ya Takwimu bora katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii barani Afrika.

Kuhusu ufanisi wa ukusanyaji wa takwimu Bora wa Tanzanzania ikilinganishwa nan chi nyingine barani Afrika Bi. Aldegunda amefafanua Ofisi ya Taifa ya Takwimu hutoa takwimu zake kwa kuzingatia sifa mbalimbali za upataji wa takwimu bora zikiwemo za matumizi ya mbinu na viwango vinavyokubalika kimataifa.

Pia ameongeza kuwa takwimu zote zinazotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu huakisi hali halisi ya eneo husika pia takwimu hizo  hutolewa kwa wakati maalum.

MARKETERS NIGHT ILIVYOFANA JIJNI DAR

$
0
0
 Mkurugenzi wa masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Ephraim Mafuru akitoa neno kwa wageni waalikwa(hawapo pichani)katika usiku wa Wanamasoko uliofanyika mwishoni mwa wiki katika hotel ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wageni waliohudhuria Marketers Night Out
 Wageni waalikwa walipata nafasi kuonja na kufurahia bidhaa za Kampuni ya bia ya Serengeti, mmoja ya wageni akimiminiwa kinywaji cha Johnie Walker kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti.
 Msemaji mkuu wa Marketers Night Steve Gannon ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti akitoa somo kwa wanamasoko waliohudhuria katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam. 



 Msemaji mkuu wa Marketers Night Steve Gannon ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti akitoa somo kwa wanamasoko waliohudhuria katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam. 
  Burudani pia ilikuepo
 Mshiriki wa Tusker Project Fame aliyetolewa wiki chache zilizopita Angella Karashani(Angel) akitoa burudani katika hafla ya usiku wa wanamasoko mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam
  Baadhi ya wageni waliohudhuria Marketers Night wakiwa katika picha ya pamoja
wageni waalikwa wakipata chakula

KACHUKUE FOMU NA UJIANDIKISHE SASA


NEWZ LIVE KUTOKA IRINGA

$
0
0
Wauzaji wa magazeti katika manispaa ya iringa wameto pongezi kwa vyombo vya habari kwa kupunguza changamoto zinazowakabili ikiwemo baadhi ya watu kusoma magazeti bila kununua.
 
Wakizungumza na nuru fm wauzaji hao wamesema vyombo vya habari vimewasaidia kuhamasisha wananchi kununua magazeti .  wauzaji hao wamesema tabia ya baadhi ya watu kusoma magazeti bila kununua ingendelea kuwepo bila waandishi wa habari kuzungumzia suala hilo.
 
Aidha wametoa wito kwa wananchi kusoma magazeti kwa ukawaida ili kupata habari mbalimbali.

===========  =======   ======
Wananchi manispaa ya Iringa wapewa elimu ya kujinga na ugonjwa wa malaria.
 
Wananchi katika manispaa ya Iringa wamepewa elimu ya jinsi ya kujikinga  na ugonjwa wa maralia pamoja na kusisitizwa kutumia  dawa pindi wagudulikapo na ugonjwa huo ambao huuwa binadamu mmoja kila baada ya dakika tano.
 
Akitoa elimu hiyo Dkt.NICOLAS NTABAYE amesema kuwa mgojwa anapofika katika huduma ya matibabu ni vyema akapata ushauri wa daktari kwanza kabala ya kuanza matibabu.
 
Dkt. amesema ugonjwa wa malaria unaendalea kuongoza kwa  vifo vingi tofauti na magonjwa mengine,ambapo hata katika takwimu za magonjwa yanayoua malaria imeonesha kuwa na takwimu kubwa.
 
Aidha amezitaja takwimu za wagonjwa wa malaria kwa watoto chini ya miaka mitano kuwa ni watoto elfu therathin mia saba tisin na tano kati ya wagonjwa tisini na nne elfu na hamsini na saba ambayo ni sawa na asilimia 32.7.

========  ======  ======
Mtihani wa darasa la nne kufanyika Novemba 20.
 
Mtihani wa darasa la nne unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 20 na 21 mwezi huu katika shule za msingi kitaifa. Akizungumza na nuru fm afisa elimu wa shule za msingi katika manispaa ya iringa ANGELUS KISIGA amesema maandalizi yamekamilika na mitihani imeshafikishwa katika kila shule.
 
Amesema wanafunzi wameandaliwa vizuri katika mitiani hiyo kwa njia ya kuwapa majaribio ya kila wiki na mitihani ya kujipima ili kujua uwezo wao kitaaluma. Ameongeza kuwa alama za ufauru zinazotakiwa kwa wanafunzi wa darasa la nne ni 125 kwa masomo ya darasa la nne.
  
Aidha KISIGA ametoa wito kwa wazazi kuwapa watoto wao muda wa kujisomea pindi wawapo nyumbani huku akiwataka wanafunzi kuwa watulivu wakati wa mtihani.

Mbunge wa Namtumbo,Vita Kawawa na vita ya ufisadi jimboni mwake,afunguka live

KINANA AKUTANA NA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU SONGEA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu vya SAUT, St.Joseph na Chuo cha Ualimu Matogoro kwenye ukumbi wa Songea Club.
 Wanafunzi wapatao 650 wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye ukumbi wa Songea Club.
 Mkuu wa Wilaya ya Songea mjini Ndugu Joseph Joseph Mkirikiti(wa kushoto) akiwa pamoja na wadau wa elimu wa Wilaya ya Songea wakimsikiliza Karibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimu wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo Songea .
 Katibu wa Mkoa wa Vyuo vya Elimu ya Juu Ndugu Christopher Ngubiagai akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu vya mjini Songea wakati wa kikao cha wanafunzi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Klabu ya Songea
Baadhi ya wanafunzi wakisikiliza kwa makini masuala mbalimbali yaliyokuwa yanajadiliwa kwenye kikao kilichowahisusha wanafunzi wa vyuo vikuu na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye ukumbi wa klabu ya Songea.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO AANZA ZIARA KATIKA MKOA WA MOROGORO KWENYE MIRADI YA UMEME

$
0
0
 Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akizungumza na watendaji wa  shirika la umeme nchini (Tanesco) ikiwa ni pamoja na wadau wa umeme mjini Morogoro kabla ya kuanza rasmi ziara yake kwenye miradi ya umeme.
 Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akitoa maelekezo kwa meneja wa Tanesco mkoa wa Morogoro Deogratius Ndamugoba mara baada ya kujionea moja ya transfoma iliyojengwa kwa ajili ya kupeleka umeme katika kijiji cha Matombo kilichopo katika wilaya ya Morogoro Vijijini.
 Kazi ya kuweka umeme ikiwa ni pamoja na kufunga mita ikiendelea kwenye moja ya nyumba zilizopo katika kijiji cha Mtombozi kilichopo katika wilaya ya Morogoro Vijijini.
 Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mtombozi kilichopo katika wilaya  ya Morogoro Vijijini wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya umeme.
 Meneja wa Tanesco mkoa wa Morogoro Deogratius Ndamugoba akitoa  ufafanuzi wa maendeleo ya miradi ya umeme katika kijiji cha Mtombozi mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo. 
 Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akisalimiana na mmoja wa wakazi wa kijiji cha Ngong’oro kabla ya kusikiliza kero zao ikiwa ni pamoja na kuzungumza nao
Mwenyekiti wa kijiji cha Ngong’oro Mahamba Shukuru  akiwasilisha changamoto katika upatikanaji wa huduma ya umeme katika kijiji hicho kwa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter  Muhongo ambapo Waziri huyo ameahidi kufanyia kazi mara moja kupitia kwa watendaji wake. 

MAJI NI UHAI

$
0
0
Wananchi wa kiji cha Nalasi wilayani Tunduru wakichota maji kutoka kwenye moja ya Visima kijijini hapo,Wananchi hao walimueleza mpiga picha wetu Adam Mzee kuwa maji hayo yanawasaidia kupunguza umbali wa safari kwani yamesogezwa karibu na pia wanalipia shilingi elfu moja kwa mwezi.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images