Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 168 | 169 | (Page 170) | 171 | 172 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Badra Masoud akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kuwepo kwa upungufu wa umeme kwenye gridi ya Taifa kuanzia tarehe 16 hadi 26 November, 2013 kutokana na upungufu wa gesi kutoka katika Kisiwa cha Songosongo kilichopo Wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi Unaosababishwa na Matengenezo ya Kiufundi kwenye visima vya gesi unaofanywa na Kampuni ya Pan Afrika ili kuboresha upatikanaji wa gesi ya kutosha kwenye visima hivyo.

  0 0

  Jeneza lenye mwili wa marehemu Dkt.Sengondo Mvungi, likiwasili kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo kwa ajili ya kuagwa
   Jeneza likipelekwa sehemu iliyoandaliwa
   Mashada ya maua na picha ya marehemu
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza kutoka salamu za rambi rambi za serikali wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi,kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Katiba Jaji Joseph Sinde Warionba akiongea machache wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi,kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.
   Makamu wa Rais Dkt Gahlib Bilali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Katiba Jaji Joseph Warioba, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Mhe Angela Kairuki na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mhe James Mbatia wakiwa katika shughuli za kuaga mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi,kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo. 
  Misa wakati wa shughuli hiyo
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuagwa mwili huo iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.
  Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda  akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuagwa mwili huo iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo. Picha na OMR


  0 0

   
  Picha ya Marehemu Dkt.Sengondo Mvungi enzi za uhai wake.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza wakati wa kutoka salamu za rambi rambi katika shughuli ya kutoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi,iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Ibada ilkiendelea wakati wa shughuli ya kutoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi,iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Taratibu za Kumuombea Marehemu Dkt.Sengondo Mvungi ikiendelea leo kwenye Viwanya vya Karemjee,Jijini Dar es Salaam.
  Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Dkt.Sengondo Mvungi likiwekwa sawa tayari kwa kuaza kwa zoezi la kutoa Heshima za Mwisho.
  Viongozi wa Dini wakitoa heshima za mwisho
  Watawa wa Kanisa Katoliki wakitoa heshima kwa Mwili wa Marehemu Dkt.Sengondo Mvungi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt. Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt. Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Mh. Seif Sharrif Hamad akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt. Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Mh. Benjamin Mkapa, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt. Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.


  Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Cleopa Msuya akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt. Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Tume ya Katiba,Mh. Jaji Joseph Warioba akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt. Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Katika na Sheria,Mh. Angella Kairuki akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt. Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Katiba,Mh. Jaji Augustine Ramadhan akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt. Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Dkt. Salim Ahmed Salim akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt. Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Fredrick Sumaye akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt. Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Ulinzi,Mh. Shamsi Vuai Nahodha akiambatana na Mh. Hamad Rashid wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt. Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi,Mh. James Mbatia na Mkewe wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt. Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Mh. Stephen Wassira akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt. Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nishati na Madini,Mh. Prof. Sospeter Muhongo akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt. Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara,Mh. Mwigulu Nchemba.
  Waziri wa Uchukuzi,Mh. Mwakyembe.
  Inspekta Jenerali wa Polisi,Said Mwema.
  Kamanda Kova.
  Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenela Mukangara
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick.
  Mwenyekiti wa Chama cha CUF,Prof. Ibrahim Lipumba akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt. Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa CHADEMA,Mh. Freeman Mbowe akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt. Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

  Familia ya Marehemu.

  0 0

  Bunduki ya plastiki iliyotengenezwa kwa mashine ya 3D ikifyatua risasi wakaati wa majaribio
  Photo credits: Screenshot from ATF Video
  Kama tulivyoripoti katika ripoti hii ya Septemba 21, mauaji ya kutumia bunduki ni kati ya matatizo makubwa nchini Marekani.
  Lakini pia, uwezo wa nchi hiyo katika teknolojia umesaidia kupunguza madhara ya vifo hivyo kwa kuwezesha kukamatwa kwa silaha kabla hazijafanya madhara.

  Hii inajumuisha pia kutumia vifaa maalum vya kugundua vitu vya chuma ambavyo mtu anaweza kuwa ameficha. Hata hivyo, kukua huko kwa teknolijia pia kuna athari katika mapambano dhidi ya uhalifu.

  Wiki hii, kitengo kinachojishughulisha na udhibiti wa Pombe, Tumbaku, Bunduki na Milipuko nchini Marekani (ATF) kimetoa ripoti kuhusu athari ama madhara yanayoweza kusababishwa na bastola za plastiki zinazochapishwa katika umbo halisi (3D Guns)

  Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).
  Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC
  Hii ilikuwa ripoti ya Novemba 16, 2013

  Kwa maoni, ushauri, nk usisite kutuandikia jamiiproduction@gmail.com

  0 0

  Bidhaa feki zimekuwa moja kati ya tatizo kubwa linaloikumba soko la Tanzania tatizo linaloletwa na kile kinachoitwa soko huria, wateja wa bidhaa mbalimbali wamekuwa wakipata hasara kutokana na bidhaa kushindwa kufanya kazi kutokana na uwezo mdogo au bidhaa hiyo kuharibika mapema mara baada ya kununuliwa dukani na kumuacha manunuzi akilalamika bila ya msada wowote ama kwa kutojua nini cha kufanya au kwa kutakuwa na matumaini ya kupata msaada kutoka kwa mamlaka husika.

  Sekta mbalimbali zimeshaanza juhudi za kukabiliana na tatizo la bidhaa feki kwa kuvumbua mbinu na mikakati itakayokabiliana na tatizo lilopo sokoni hivi sasa. Makampuni makubwa hasa yale yanayotengeneza simu za mkononi yameshaanza kutoa huduma Maalum za kubaini simu halisi mara mtu anaponunua katika maduka mbalimbali. Kuongezwa kwa muda wa huduma ya mkataba wa bidhaa kwa lugha ya kigeni  “Warranty” mara mtu anaponunua ni moja kati ya mbinu hizo pamoja na kusajili simu mpya mara inaponunuliwa, huduma hizi zote zinalenga kupambana na simu feki.

  Kwa kutumia mbinu za kipekee katika kuhamasisha watu kutonunua bidhaa feki au iliyoibiwa na kumpa mteja nafasi ya kuangalia uhalisia wa bidhaa husika aliyonunua, kampuni kama Samsung imetambulisha huduma yake ya “E-Warranty” ya miezi 24 kutoka miezi 12. Mteja aliyejisajili na huduma ya E-warranty mara baada ya kuinunua bidhaa ya Samsung atapata huduma za ukarabati wa bidhaa yake ndani kwa miaka bure mara tatizo lolote linapotokea, iwe tatizo hilo linalotokana na bidhaa yenyewe au mtuamiaji wake kuharibu bidhaa hiyo.     

  Huduma hii ya kusajili bidhaa yako kwenye e-warranty imerahisishwa zaidi, mara mteja anaponunua bidhaa halisi anaweza kujisajili kwa kutumia simu yake kupitia mitandao yote hapa nchini. Katika bidhaa za simu mteja wa Samsung anatakiwa kusajili simu yake katika huduma ya e-warranty kwa kutuma ujumbe wenye namba maalum zenye uwezo wa kujua mahala simu hiyo iliponunuliwa (IMEI) kwenda 15685, namba hizi Maalum ambazo ni 15 zinapatikana nyuma ya kasha la simu au nyuma ya simu yenyewe. 

  Katika kuhamasisha Watanzania wananunua bidhaa halisi na kuzisajili, Samsung Tanzania imetangaza kuanza kwa promosheni yake kubwa katika msimu huu wa mwisho wa mwaka kwa kuwazawadia wateja watakaonunu bidhaa halisi na kuzisajili, wateja hao wataingia kwenye droo ya kila wiki  na kuwa na nafasi ya kujishindia bidhaa mbalimbali za Samsung.

  “Hofu yetu kubwa imekuwa katika madhara wanayowapata Watanzania kwa kutumia bidhaa feki, bidhaa feki zipo sokoni na ili kuonyesha tunawajali wateja ni Lazima tupambane na tatizo hili, tumetambulisha huduma ya e-warranty ambayo inampa nafasi mteja kwa kuangalia uhakika wa bidhaa aliyonunua kwamba si feki” alisema Bw. Kishor Kumar, Meneja wa Samsung Tanzania Kitengo cha Simu na Teknolojia ya Habari.

  Pambika na Samsung ni promosheni ya nchi nzima ambayo imeanza Novemba 7 mpaka Decemba 23, 2013. Promosheni hii inalengo la kuwazawadia wateja wapya wa Samsung wakati huo huo ikihamasisha wateja kuinunua bidhaa halisi na kuzisajili katika huduma ya e-warranty ili kufaidi huduma zake bure ndani ya miaka miwili.


  0 0

  IMG_4434

  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko Maria Bilia akizungumza na waandishi wa habari kuhusu siku ya Viwanda Afrika ambapo alielezea mafanikio na changamoto katika sekta ya viwanda nchini na Afrika kwa ujumla. Kulia ni Afisa mipango wa Taifa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) Bw. Gerald Runyoro.
  IMG_4451
  Afisa Mipango wa Taifa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) Bw. Gerald Runyoro akizungumzia ushiriki wa shirika hilo katika kukuza viwanda nchini.
  IMG_4459
  Kaimu Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Nchini (CTI) Dr. Samwel Nyantahe akizungumzia umuhimu wa kuongeza thamani za bidhaa zinazozalishwa hapa nchini kwa minajiri ya kupambana na tatizo la ajira.


  IMG_4483
  Mkurugenzi wa Viwanda vidogo vidogo kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko Dakta. Consolatha Ishebadi (katikati) akifafanua changamoto wanazokutana nazo wafanyabiashara wazawa katika kutengeneza vifungashio vyenye ubora (Packaging) kwenye bidhaa zao.
  IMG_4478
  Mwandishi kutoka gazeti la The Citizen akiuliza swali wakati wa mkutano huo wa siku ya Viwanda Afrika.
  IMG_4440
  Sehemu ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali waliohudhuria mkutano huo.


  Na Damas Makangale, Moblog
  SERIKALI imesema haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria wafanyabiashara wote kutoka nje wanaofanya biashara au kufungua viwanda vidogo vidogo bila kufuata taratibu, kanuni na sheria za nchi. Moblog inaripoti.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari katika kuadhimisha Siku ya Viwanda Afrika jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Bi. Maria Bilia amesema kuna baadhi ya wafanyabiashara toka nje ambao hawataki kufuata taratibu za uwekezaji na sheria za nchi.

  “Matokeo ya kutokufuata sheria za nchi katika uwekezaji au ufanyaji wa biashara ni uanzishwaji wa viwanda vinavyozalisha bidhaa ambazo hazikidhi viwango na ni hatari kwa Afya za walaji,”

  “Sheria za nchi zipo wazi kwamba lazima Kituo cha Uwekezaji (TIC) na Brela msajili wa biashara wahusishwe kwenye mchakato mzima wa uwekezaji au biashara yeyote ndani ya nchi,” Bilia amesema.

  Amesema vile vile Wizara ya Viwanda kwa kushirikiana na Wizara zingine na taasisi za Serikali wanaendelea kurahisisha urasimishaji wa biashara kwa wanyonge kupitia mradi wa Mkurabita Mkakati wa Kurasimisha Biashara kwa Wanyonge ili kuwawezesha wazawa kufanya biashara zenye tija kwao na taifa kwa ujumla.

  Bi. Bilia aliendelea kusema kuwa siku ya viwanda Afrika ilianzishwa mwaka 1989 na Tanzania ilijiunga rasmi mwaka 1990 katika kuhamasisha ukuaji wa viwanda katika kukuza uchumi wa nchi za Afrika. Amesema sekta ya viwanda ikishirikishwa na sekta zingine inaweza kufanya mabadiliko haraka katika maisha ya mtu mmoja mmoja hususani ajira na hutoa bidhaa bora kwa matumizi ya binadamu.

  Alisisitiza kuwa mwaka huu Serikali imepanga kuwa na maonyesho ya wiki nzima yatakayofikia kilele tarehe 20 mwezi huu ambapo wafanyabiashara mbalimbali watapata fursa ya kuonyesha bidhaa zao katika ukumbi wa PTA saba saba.

  Amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni “ Ni Ajira na ujasiriamali, Fursa ya Kuharakisha Maendeleo ya Viwanda Afrika katika juhudi za kupunguza makali ya umaskini na tatizo la ajira kwa vijana.

  Kwa upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda Nchini (CTI) Dkt. Samwel Nyantahe amesema shirikisho la viwanda linaunga mkono juhudi za serikali katika kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ili kuongeza mapato ya nchi.
  “Sisi Shirikisho la Viwanda kwa kushirikiana na serikali na watu binafsi tutaendelea kuhamasisha jamii umuhimu wa viwanda katika kuongeza thamani ya bidhaa na kupambana na tatizo la ajira nchini,” amesema.

  Bw. Gerald Runyoro kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) amesema umoja wa mataifa kwa kushirikiana na serikali na wadau wengine wataendelea kusisitiza watu kuwekeza na kufungua viwanda ili kuharakisha maendeleo ya kiuchumi Afrika.
  Amesema wafanyabiashara lazima wawe na ujasiri wa kufungua biashara au kiwanda katika juhudi za kuongeza thamani bidhaa zitokazo Afrika na kutafuta fursa za uwekezaji nje ya Afrika.

  0 0
 • 11/16/13--08:34: TOYOTA PASSO FOR SALE
 •  MAKER: TOYOTA
  MODEL: PASSO
  YoM: 2004
  ODO: 56247
  COLOR: MAROON
  HAIJATUMIKA BONGO.......
  PRICE: MIL 8 NEGOTIABLE
  MAWASILIANO 0713 344 399

  0 0

  Mabingwa watetezi wa michuano ya taifa ya kikapu (Taifa Cup) kwa mwaka jana, bado hawajathibitisha ushiriki wao katika michuano ya mwaka huu kutokana na ukata wa fedha.

  Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari kutoka kwa mabingwa hao wa mwaka jana ambao ni Mkoa wa Tanga, mpaka sasa timu yao inafanya mazoezi bila matumaini ya kuelekea mjini Mbeya itakapofanyika michuano hiyo kwa mwaka huu mwishoni mwa mwezi wa 11.

  “Michuano hii ya kikapu taifa kwa mwaka jana ilifanyika mkoani hapa (Tanga), hivyo ikawa rahisi kwetu kuweka kambi na kupata mahitaji mengine, ndiyo maana tukaibuka mabingwa, lakini mwaka huu hali katika kambi si nzuri kwani bajeti inatubana mpaka sasa hatujui mustakabali wetu,” kilisema chanzo hicho.

  Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Tanga (TRBA), Carlistus Zakaria timu hiyo inahitaji kiasi cha Sh mil 11, ili kuweza kusafiri mpaka Mbeya. Vilevile kiasi hicho cha fedha kitaweza kuhudumia kambia kwa malazi na chakula pamoja na vifaa vya michezo kwa muda wote watakaokuwa Mbeya.

  “Timu yetu ina wachezaji 24 Wavulana na Wasichana pamoja na viongozi wanane hivyo kufanya idadi ya watu 32, tunahitaji kiasi cha Sh mil 3.5 za nauli kuenda na kurudi, Sh mil 5.2 za chakula kwa siku zote tutakazokuwa Mbeya pamoja na Sh mil 8.8 za vifaa vya michezo na fedha za dharura,” ilisema sehemu ya barua hiyo.


  Aidha kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari ambacho kimetaka hifadhi ya jina lake mpaka sasa Mkoa wa Tanga, haujaonyesha nia ya kuwasaidia mbali ya kuwapelekea barua kutoka Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), ambayo inaweka wazi kila kitu juu ya ushiriki wetu.

  “Kinachotutia uchungu juu ya kupuuzwa huku ni kuwa, mwaka jana tulipouletea heshima Mkoa wetu kila mtu alitusifia, lakini hawakujua kama vizuri vyataka gharama. Sasa ili tuendelee kuuletea vikombe mkoa wetu tunawaomba wadau wa mchezo huu watusaidie tufike Mbeya.

  “Tumeamua hatuhitaji fedha, hata wakitokea watu wakitudhamini usafiri, wengine wakatupa vifaa na wengine wakatuhakikishia chakula hatuna matatizo, kikubwa tunahitaji kushiriki michuano hii kwa hali na mali, tukishindwa kushiriki itakuwa aibu kubwa kwa mkoa wetu,” kilisema chanzo hicho.

  Hata hivyo, kwa mujibu wa barua ya TBF, iliyotolewa Aprili mwaka huu na kutiwa saini na Katibu Mkuu Msaidizi wa shirikisho hilo Michael Maluwe, imeweka wazi kuwa Serikali ya Mkoa inawajibika moja kwa moja kuhakikisha timu hizo zinashiriki michuano ya Taifa Cup.

  “Ni wajibu wa kila mkoa kuhakikisha unawajibika katika maandalizi na kuipeleka timu ya mkoa kwenye kituo cha mashindano,” imesema sehemu ya barua hiyo na kuongeza kuwa. “Mambo muhimu ya kuzingatia ni gharama za nauli kwa timu, gharama za malazi na chakula vilevile usafiri wa ndani, posho na ada ya ushiriki ambayo ni Sh 100,000.”

  Aidha timu ya kikapu ya Tanga imeweka wazi kuwa mtu binafsi, kampuni ama taasisi ambayo itaguswa na matatizo ya kambi hiyo, ambayo inapigana kuhakikisha inatetea ubingwa wake ilioupata mwaka jana wanafungua milango kupokea msaada wowote utakaowawezesha kuishi mjini Mbeya kuanzia Novemba 30 mpaka Disemba 8 mwaka huu itakapokamilika michuano hiyo.

  Wamebainisha kuwa wapo tayari kutangaza biashara ya mfadhili yeyote atakayewasaidia ama mtu aliyeguswa anaweza kuwatumia fedha katika akaunti ya benki namba 4172506984 NMB Bank (badaraka Branch).

  0 0

  Na Swahili TV
  Kwa niaba ya Familia, Kamati ya Mazishi Marekani na Tanzania na ndugu na jamaa wote kwa ujumla tumeona ni vyema nanyi mkaona matukio yote kwani mlishiriki katika msiba huu. Kwa mara nyingine tena tunatoa shukrani zetu za dhati kwa wote mliofanikisha Shughuli zote Usafiri, Maandalizi mbalimnbali na hatimaye kuuhifadhi mwili wa mpendwa wetu, dada yetu, rafiki na kipenzi chetu Bi. Martha Shani.Mazishi yalifanyika Puma Sindiga siku ya Alhamisi ya Octoba 31, 2013. Video ya matukio yote tutaiweka soon hapa hapa Swahili TV Blog.

  PICHA ZA MATUKIO YOTE
  Alex akipewa pole na Shangazi wa Martha

  Kushoto; Vincent Mughwai, Joseph, Alex akimshikia mtoto Chris beleshi akiweka udongo katika kaburi la Mama yake, huku Mchungaji Peter Ihema wa Kanisa la Pentekoste Puma akitazama . Mazishi yalifanyika Alhamis Oktoba 31, 2013 Puma-Singida.
  Alex, Joseph, DMK, Muddy wakiwafuatilia shughuli za Mazishi Alhamis Oktoba 31, 2013 Puma-Singida.
  AU INGIA


  0 0

  Msimamizi wa Kiwanda cha Korosho,Korosho Africa Ltd akifafanua namna ya Korosho zinavyobanguliwa kwa kutumia mashine za kisasa kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa ameambatana na ujumbe wake,Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye pamoja na  Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro,Kinana na Ujumbe wake wanamalizia ziara yao leo ndani ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma na kesho kuwasili ndani ya Wilaya ya Namtumbo kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo ya chama na wananchi sambamba na miradi. 
  Maeleoz yakitolewa namna ya Korosho zinavyochambuliwa mara baada ya kubanguliwa na mashine ya kisasa,ampapo zao hilo la biashara linalotegemewa na wakulima wa Wilaya ya Tunduru wamekuwa wakilalamikia suala la bei kuwa ndogo inayopangwa na Wanunuzi hali inayowapelekea Wakulima wa zao hilo kukata tamaa na maisha yao kuendelea kuwa duni siku hadi siku.
  Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye akizungumza na akina mama wanaofanya kazii ya kuchambua Korosho ndani ya kiwanda cha Korosho Africa,ambao baadhi ya akina mama hao walilamika suala la ujira wanaolipwa kuwa ni mdogo na haukidhi mahitaji yao ya kila siku.
  Baadhi ya akina mama wanaofanya kazi ya kuchambua Korosho ndani ya kiwanda cha Korosho Africa,wakiendelea na kazi yao ya kuchambua Korosho,ambapo imeelezwa kuwa mtu mmoja huchambua korosho kwa wastani wa kilo kumi mpaka 15.
  Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro,akizungumza na akina mama wanaofanya kazi ya kuchambua Korosho ndani ya kiwanda cha Korosho Africa mapema leo mchana walipokwenda kutembelea kiwandani hapo na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa kiwandani hapo.
  Uchambuzi wa Korosho ukiendelea.
  Tahadhari ya maandishi ndani ya kiwanda cha Korosho kwa wafanyakazi.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa tarafa ya Jakika mapema leo mchana,ikiwa sambamba na kuweka jiwe la msingi kwenye Ofisi ya CCM ya kata ya Jakika,Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma,Ndugu Kinana ameambatana na ujumbe wake,Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye pamoja na  Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi nje ya Zahanati ya kijiji cha Matemanga,Ndugu Kinana aliweka jiwe la msingi nyumba mbili za Waganga ikiwemo na kushiriki ujenzi wa mradi wa nyumba hizo akiwa sambama na ujumbe wake,Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye pamoja na  Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro.
  Moja ya nyumba za watumishi wa Zahanati ya kijiji cha Matemanga ambayo Ndugu Kinana aliweka jiwe la msingi.
  Pichani kulia Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana sambamba na ujumbe wake Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye pamoja na  Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro,wakishiriki ujenzi wa nyumba mbili za Waganga katika zahanati ya Matemanga wilayani Tunduru mkoani Ruvumma.
  Baadhi ya akina mama wakifurahia jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake Wilaya ya Tunduru mapema leo jioni kwenye uwanja wa Baraza la Iddi,Wilayani humo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.
  Sehemu ya wakazi wa Tunduru mjini  wakishangilia  jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake mapema leo jioni kwenye uwanja wa Baraza la Iddi,Wilayani humo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.
  Pichani kulia Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana  akihitimisha ziara yake mapema leo jioni kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Baraza la Iddi,Wilayani Tunduru mkoani Rukwa na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.Kinana na Ujumbe wake kesho ataelekea Wilayani Namtumbo kuendelea kukagua miradi ya mbalimbali ya Wananchi na chama kwa ujumla.
  Baadhi ya Mafundi wakiendelea na ujenzi kwenye moja ya darasa ikiwe ni sehemu ya mradi wa ujenzi wa madarasa na maabara katika shule ya sekondari ya kata ya Mgomba,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameambatana na ujumbe wake,Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye pamoja na  Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro walishiriki ujenzi -
  Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrhman Kinana akiwa ameambatana na ujumbe wake,Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye pamoja na  Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro wakiishiriki ujenzi kwenye moja ya darasa ikiwa ni sehemu ya mradi wa ujenzi wa madarasa na maabara katika shule ya sekondari ya kata ya Mgomba,iliopo Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.Anaeshuhudia ni Mkoa wa Ruvuma,Mh Said Thabit Mwambungu. 

  0 0
 • 11/16/13--12:14: ZIARA YA MWANA FA VOA
 • IMG_4606Mwana Fa mara tu alipowasili ofisi za VOA Washington Dc na kupokelewa na mkuu wa idhaa hiyo Mwamoyo Hamza siku ya Ijumaa Novemba 15 kati kati ni Khadija Riyami na watangazaji wa idhaa (hawapo pichani ) kabla ya kuingia kwenye kipindi cha Live Talk kinachorushwa kila Ijumaa na VOA. IMG_4630Mkuu wa idhaa ya Kiswahili ya VOA Mwamoyo Hamza kushoto na Mwana Fa na mwenyeji wake Dj.Rich Mwandemane. IMG_4626Khadija Riyami kushoto akiwa na Mwana Fa na Dj Rich. IMG_4628Wakiwa na prodyuza wa idhaa ya Kiswahili Duane Collins.Kwa picha zaidi ungana na sundayshomari.com

  0 0

  Katibu wa Waziri Mkuu Jimbo Ndugu Charles Kanyanda akimkabidhi Sister Scholastica Mwembezi wa Masista Maria Mtakatifu Malkia wa Afika ambao ni wamiliki wa kituo cha kulea mayatima cha Katandala Mkoani Rukwa viatu pea sitini zilizotolewa na Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Tunu Pinda ikiwa ni ahadi aliyoitoa alipotembelea kituo hicho mapema mwaka huu. Aidha Sister Mwembezi amemuomba Katibu Kanyanda kumfikishia salamu za shukrani Mama Pinda ikiwa ni pamoja kumkumbusha ahadi ya gari aliyoitoa kwa kituo hicho.  
   Ndugu Charles Kanyanda akimvisha viatu mmoja ya watoto yatima katika kituo hicho baada ya kukabidhi zawadi hizo kutoka kwa Mama Tunu Pinda. Mzee Kanyanda amewataka wadau mbalimbali kuonyesha moyo wa upendo katika kusaidia mahitaji mbalimbali kwa watoto na kituo hicho.
  Katibu wa Waziri Mkuu Jimbo Ndugu Charles Kanyanda akiimba moja ya wimbo na watoto wa kituo cha kulea mayatima cha Katandala.
  (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

  0 0

   Mradi wa maji uliopo Matamba.
  =====
  Kutokamilika kwa baadhi ya miradi ya maji na mingine kujengwa chini ya kiwango kumeonekana kuwa mwiba mchungu kwa wananchi na baadhi ya viongozi wapenda maendeleo wilayani Makete mkoani Njombe

  Hayo yamebainika hii leo kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya (DCC) kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Makete wilayani hapo

  Akizungumza kwenye kikao hicho, mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mh. Daniel Okoka amesema kwa upande wa tarafa ya Matamba amesema yeye kama mtia saini mikataba ya ujenzi wa miradi hiyo hataipokea mpaka akatapofanya ukaguzi hatua kwa hatua

  "Mimi nitakwenda Matamba na kuwafuata wananchi tunakwenda hatua kwa hatua na kuzungumza nao wakati wa ukaguzi na wakiridhika na ujenzi huo wa mradi, mimi nitaupokea wakikataa sitaupokea" alisema Okoka

  Amesema kwa kiasi kikubwa anashangazwa na baadhi ya viongozi wa Matamba ambao hakuwataja kumwambia kuwa hana mamlaka ya kufanya mikutano kwenye maeneo hayo, na kufafanua kuwa yeye kama mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete ana uwezo wa kufanya mikutano sehemu yeyote ile ndani ya wilaya yake bila kizuizi, na hivyo viongozi hao wasimkwamishe

  Akichangia hoja hiyo, katibu wa CCM wilaya ya Makete Miraji Mtaturu amesema ni aibu kwa viongozi pindi miradi ya maji inapoonekana kutokamilika ilihali taarifa zinazotolewa zinaonesha kuwa miradi hiyo imefanyika na imekamilika 

  Akizungumzia mradi wa Matamba amesema hali ni mbaya kwani mradi huo hautoi maji licha ya taarifa kudai kuwa umekamilika, na kudai kuwa huu si muda wa kulumbana kumtafuta mchawi na badala yake kinachotakiwa ni maji yawafikie wananchi na si kitu kingine

  Naye mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro ameagiza kuwa tatizo hilo la ukosefu wa maji katika maeneo mbalimbali yenye changamoto ikiwemo Matamba lifanywe haraka iwezekanavyo ukizingatia kuwa serikali imetoa kipaumbele kwa miradi hiyo ya maji


  0 0
 • 11/17/13--04:54: changamkia fursa hiyo mdau.
 • Hii ni blogu ya magari ambapo kutakuwa na list pamoja na picha za magari yanayouzwa hapa Tanzania na Mawasiliano ya wauzaji pamoja na bei. Lengo ni kukupa urahisi wa kupata kile ukitakacho kwa urahisi na unafuu tu na bure kabisa.

  Pia Unaweza kututumia picha za magari unayouza au kuuza kupitia e-mail yetu hapo chini bure kabisa bila gharama yoyote na sisi tutaweka muda huo huo kupitia mtandao wetu huu wa Magari Tanzania
  Tutumie sasa Picha za magari unayouza na sisi tutakuwekea bure kabisa
  Tutembelee Kupitia link hii http://magaritanzania.blogspot.com/
  E-mail yetu ni magaritanzaniablog@gmail.com

  0 0

   MKALI wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando, ni miongoni mwa Watanzania watakaotumbuiza Tamasha la Krismasi Desemba 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
   
  Msanii huyo anayetamba na albamu zake mbalimbali ikiwemo ya Utamu wa Yesu, pia atatumbuiza Desemba 26 mwaka huu kwenye Tamasha la Krismasi litakalofanyika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
   
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Krismas, Alex Msama alisema jana kuwa hatua ya kamati yake kumalizana na Muhando imewapa faraja kubwa, kwani huyo ni miongoni mwa waimbaji ambao Watanzania wanawapenda.
   
  “Mungu ni mwema, kila tunalolipanga anatusaidia sana, karibu waimbaji wote ambao mashabiki wanawapenda, wamekuwa na ushirikiano mkubwa na sisi. Hawana matatizo na si watu wenye tamaa, bali wanaweka mbele kutoa huduma.
   
  “Tayari hivi sasa waimbaji watatu wa Tanzania tumeshakubaliana nao ambao ni Upendo Nkone, Upendo Kilahiro na huyo Rose Muhando, kwa nje tumeshamalizana na Ephraim Sekeleti. Bado tunaendelea na mazungumzo na wasanii wengine wa ndani ya Tanzania na nje ya nchi ili wote waje kutumbuiza,” alisema Msama.
   
  Albamu ya Utamu wa Yesu ya Rose Muhando inabeba nyimbo saba ambazo ni Utamu wa Yesu, Raha Tupu, Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia.
   
  Mbali na Utamu wa Yesu, Rose Muhando pia amewahi kutamba na albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi) na Jipange Sawasawa.

  Pia amepata kung’ara katika wimbo wa Vua Kiatu, alioshirikiana na Anastazia Mukabwa wa Kenya katika albamu ya Vua Kiatu, ambayo ilikuwa na nyimbo kama  Vua Kiatu, Ee Mungu, Usiwe Manamba, Nzizilela, Nishike Mkono Bwana, Wanaokudharau na Mfalme.

  0 0
  Tshs. Milioni 5 kushindaniwa....

  Yamebaki masaa machache sana apatikane Mama Shujaa wa Chakula Mtandaoni - Mpendekeze sasa..!!

  Kama unamfahamu mkulima yeyote mwanamke, mtanzania, mwenye umri wa miaka 18 na zaidi, anayelima mazao ya chakula, huu ni wakati wako sasa wa kumpa zawadi ya kufungia mwaka.

  Kampeni ya Grow inayoendeshwa na shirika la kimataifa la Oxfam kupitia balozi wake Shamim Mwasha (Blogger 8020fashions) inatoa zawadi ya vifaa vya kilimo vyenye thamani ya Tshs. Milioni 5 pamoja na nafasi ya ushiriki katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2013 litakalofanyika sambamba na Maisha Plus.

  Mpendekeze ashinde sasa kwa kubofya hapa na kujaza nafasi zote surveymonkey.com/s/growtanzania


  Kumbuka; leo ni siku ya mwisho ya kupokea mapendekezo. Usiache nafasi hii ikupite.

  Wekeza kwa wakulima wadogo wanawake. Inalipa.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokutana na Waziri wa Maendeleo ya Minazi na Maendeleo ya Shamba la Janatha wa Sri Lanka, Mheshimiwa Jagath Pushpakumara (shati jeupe) na ujumbe wake mjini Colombo, Sri Lanka, kuzungumzia njia za kushirikiana kukabiliana na maradhi ya mazao likiwamo zao la mnazi ambalo linakabiliwa na tatizo la mnyauko.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi inayotokana na zao la mnazi toka kwa Waziri wa Maendeleo ya Minazi na Maendeleo ya Shamba la Janatha wa Sri Lanka, Mheshimiwa Jagath Pushpakumara (shati jeupe) na ujumbe wake mjini Colombo, Sri Lanka, kuzungumzia njia za kushirikiana kukabiliana na maradhi ya mazao likiwamo zao la mnazi ambalo linakabiliwa na tatizo la mnyauko.
  Picha ya pamoja ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati na Waziri wa Maendeleo ya Minazi na Maendeleo ya Shamba la Janatha wa Sri Lanka, Mheshimiwa Jagath Pushpakumara (shati jeupe) na ujumbe wake mjini Colombo, Sri Lanka, kuzungumzia njia za kushirikiana kukabiliana na maradhi ya mazao likiwamo zao la mnazi ambalo linakabiliwa na tatizo la mnyauko. PICHA NA IKULU

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

  0 0

  Millen Happiness Magese (kulia) akikagua baadhi ya miradi yake manispaa ya Mtwara.
   Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Millen Happiness Magese amewataka watu binafsi na makampuni mbalimbali kujitokeza kwa wingi katika kusaidia tasnia ya elimu hasa katika maeneo yasiyopewa kipaumbele ili kuwaokoa watoto wa maeneo hayo kutotumbukia katika vitendo visivyo vya kimaadili. Rai hiyo ameitoa wakati alipotembelea miradi yake aliyoifadhili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na utengenezaji wa madawati.
  Millen Happiness Magese akiwa amepozi na wanafunzi huku wakiwa wamekalia madawati aliyochangia katika shule hiyo.
  Sehemu ya madawati yaliyotolewa na mrembo huyo katika shule  ya Msingi Mjimwema.
  Millen akizidi kukagua miradi hiyo leo.
  Ujenzi wa madarsa unaendelea katika shule ya msingi Mjimwema iliyopo manispaa ya Mtwara ambapo mradi wa kutengeneza madawati ulikabidhiwa kwa vikundi mbalimbali vya wajasiriamali mkoani hapo kwa mpango maalum kupitia ofisi ya mkuu wa Wilaya, Mheshimiwa Wilman Ndile. Jumla ya madawati hamsini na tano (55) yenye thamani ya shilingi milioni tano yalikuwa tayari yameshatengenezwa kama walivyoahidi wajasiriamali hao wakati wakikabidhiwa kazi ya utengenezaji wa madawati hayo.
  Millen akiwa pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mjimwema iliyopo manispaa ya Mtwara ambapo madarasa yanajengwa na pia pia aliwanunulia wanafunzi hao madaftari kama waonekanavyo pichani.
  Madawati hayo yalikabidhiwa rasmi na Millen yalikabidhiwa kwa wanafunzi wa shule ya msingi Lilungu. Kwa upande wa afisa elimu wa manispaa ya Mtwara Frola Aloys amewataka wadau wa elimu kuonesha uzalendo wa hali ya juu kwa maeneo ya Kusini mwa Tanzania huku mkuu wa shule ya msingi Lilungu Abdul Nangomwa akielezea changamoto zinazoendelea kuikumba sekta ya elimu katika shule za msingi wilayani Mtwara.

  Millen akipozi na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mjimwema nje ya darasa jipya linalojengwa na mrembo huyo.
  Mbali na kukabidhi madawati Millen aligtembelea ujenzi unaoendelea shule ya msingi Mjimwema na kutoa zawadi ya madaftari napenseli kwa wanafunzi hao ambapo mpaka sasa shule in mikondo mitatu ambayo ni kuanzia darasa la awali mpaka darasa la pili.
  Ziara hiyo ya mrembo huyo aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania mwaka 2001, ni mwendelezo wa shughuli za kijamii anazozifanya nchini Tanzania hasa katika kusaidia makundi yenye mahitaji maalumu na yale yasiyopewa kipaumbele.
  Mwanzoni mwa mwaka huu Millen Magese alitoa kiasi cha shilingi milioni kumi na tano katika kusaidia huduma hiyo ya elimu katika manispaa ya Mtwara.

  0 0

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiteta jambo na Mama Marianne Lwanetzki  raia wa Ujerumani alipomtembelea nyumbani kwake jana kujionea maisha ya mama huyo ambae kwa sasa anaishi Mkoani Rukwa katika nyumba yake inayoitwa 'Kinder House" na watoto yatima 12 ambao aliamua kuwachukua kutoka katika mazingira magumu na kuishi nao kama watoto wake huku akiwapatia huduma mbalimbali za chakula, malazi, elimu na tiba. Watoto hao yatima wapo wanaume sita na wanawake ni sita.

  Katika historia yake fupi Mama huyo alifika Mkoani Rukwa kwa shughuli za kitalii na ndipo alipomuona mtoto mmoja katika moja ya kituo cha kulelea mayatima akiwa na hali mbaya ya kiafya huku akiwa mgojwa sana, Aliamua kumchukua mtoto huyo na kuishi nae hadi akapona ndipo aliposhawishika na kuamua kuhamia Tanzania na kuchukua watoto wengine yatima hadi kufikia 12 ambao kwasasa amesema wanatosha kulingana na uwezo alionao.

   Aliongeza kuwa katika kuwalea watoto hao anatumia uwezo wake yeye binafsi pamoja na misaada  mbalimbali kutoa kwa ndugu, jamaa na marafiki wa nchini kwake Ujerumani.
  Mtoto Kastory Mabruki ambaye ametajwa kuwa na sifa mbalimbali ikiwemo Uongozaji wa kwaya kama inavyoonekana pichani na hata uongozaji wa midahalo"debate" mbalimbali shuleni kwao zikiwemo za wanafunzi wa madarasa ya juu zaidi ya lile analosoma na kuzimudu vizuri. Katika watoto hao 12 kila mmoja anaonekana kuwa na kipaji cha aina yake ambapo Mama yao Mlezi anajitahidi kuviendeleza na kuvipa nafasi.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiongea kumpongeza Mama Marianne kwa juhudi alizozichukua ambapo ameguswa sana na mpango huo wa mtu binafsi kulea watoto kama familia moja tofauti na sehemu nyingine nyingi ambazo taasisi ndizo zinazojishughulisha na vituo vya kulelea mayatima.Mkuu huyo wa Mkoa amewaasa watanzania wenye uwezo kuiga mfano huo kusaidia jamii kuondokana na kero za watoto wa mitaani.
  Picha Ndani:Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (katikati mbele waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mama Marianne Lwanetzki (wapili kushoto mbele waliokaa) raia wa Ujerumani na watoto yatima 12 alioamua kuwachukua na kuwalea kama watoto wake wakitokea katika mazingira magumu na ambao anaishi nao katika nyumba yake anayoiita "Kinder House" iliyopo katika Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa. Mama huyo anawapatia watoto hao mahitaji yao yote ikiwemo chakula, malazi na elimu. Kulia ni Katibu wa Mhe. Manyanya Frank Mateni. 
   Picha Nje:Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (watatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mama Marianne Lwanetzki (watatu kulia) raia wa Ujerumani na watoto yatima 12 alioamua kuwachukua na kuwalea kama watoto wake wakitokea katika mazingira magumu na ambao anaishi nao katika nyumba yake anayoiita "Kinder House" iliyopo katika Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa. Mama huyo anawapatia watoto hao mahitaji yao yote ikiwemo chakula, malazi na elimu. Wapili kulia ni Hamza Temba - Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa.
  Handshaking.
  Nyumba hii inajulikana kama "KINDER HOUSE" ambapo kwa mujibu wa Mama mwenye nyumba hii Marianne Lwanetzki ambae ni raia wa Ujerumani alisema neno "kinder" kijerumani lina maana ya watoto. Mama Marianne amesema nyumba hiyo ambayo ni kubwa ikiwa na eneo la kutosha ameshaiandikia kisheria na kwamba ni urithi kwa watoto hao 12 anaowalea hata kama hatokuwepo tena duniani basi hapo ndipo nyumbani kwao.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akiagana na familia ya Mama Marianne Lwanetzki yenye watoto yatima 12 pamoja na wafanyakazi wake wanaomsaidia kwenye shughuli za malezi. (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

older | 1 | .... | 168 | 169 | (Page 170) | 171 | 172 | .... | 1898 | newer