Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 167 | 168 | (Page 169) | 170 | 171 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Nani atatwaa taji laMiss Universe Tanzania, jibu la swali hilo litajulikana leo (Ijumaa) wakati warembo 15 kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania watakapochuana kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini kuanzia saa moja kamilli usiku.

  Warembo hao mbali ya kuwania taji la Miss Universe Tanzania ambalo kwa sasa linashikiliwa na Winfrida Dominique, pia watawania taji la Miss Earth Tanzania na kupata tiketi ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa.

  Warembo hao kwa nyakati tofauti waliokuwa wakitambiana huku kila mmoja akisema atatwaa taji hilo na kuiwakilisha nchi katika mashindano ya dunia yaliyopangwa kufanyika  Novemba 9 jijini Moscow, Russia.

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications inayoandaa mashindano hayo, Maria Sarungi alisema kuwa kila kitu kimekamilika na warembo wamepania kufanya makubwa jukwaani . Maria alisema kuwa warembo wote wana ari ya juu na kila mmoja akiwa na shauku ya kutwaa taji hilo.

  “Kwa upande wetu, kila kitu kipo tayari, warembo wamejiandaa vilivyo na tumeandaa shoo bora na fupi, hivyo mashabiki wa masuala ya urembo wanatakiwa kufika mapema ili kuona nani anatwaa taji na kupata tiketi ya kuiwakilisha nchi kimataifa,” alisema Maria.

  0 0


  We are taking this opportunity to thank our entire fans around the globe
  for your support to this band. 
  It is your support that makes the Ngoma Africa band prosper, without
  you there will be no success!

   Please, we ask you again to keep on supporting and let the band be on
  the top most position in every event, festival, media etc.
   Let others around you join the band at www.ngoma-africa.com , here
  they will have the opportunity to enjoy music at www.ngoma-africa.com

  Your Band !
  THE NGOMA AFRICA BAND

  0 0

   Masalia ya msitu uliopo kwenye kijiji cha Luvulunge wilaya ya Makete mkoa wa Njombe mara baada ya moto kuuteketeza msitu huo ambao mbali na kuwa na miti pia nyaya za umeme wa gridi ya taifa unaotoka mkoa jirani wa Mbeya kuja Makete zimepita katika eneo hili lililoungua
   Nguzo za umeme zikiwa zimeponea chupuchupu kuteketezwa na moto huo.
   
   
   
  Mojawapo ya nguzo zilizopo kwenye msitu huo kama unavyoziona, na sipati picha kama zingeungua nini kingetokea?(Picha zote na Edwin Moshi, Makete)

  0 0

   Kiongozi wa Kundi la Ngoma za asili la Albino Revolution,akiimba moja ya nyimbo zao za kuhamasisha amani pamoja na kuwaombea watu wenye Ulemavu,wakati wa Muendelezo wa Tamasha la 32 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo,linaloendelea kwenye Ukumbi wa Chuo Kukuu cha Sanaa,Bagamoyo Mkoani Pwani.Tamasha hilo lilaloonekana kuwa na wapenzi wengi kutoka sehemu mbali mbali,linatarajiwa kumalizika Septemba 28,2013.
  Mmoja wa Wasanii wa Kundi la Ngoma za asili la Albino Revolution akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma hizo kwa namna yake.
   Burudani imekolea huku shangwe zikisikika ukumbi mzima.
   Umoja ni Nguvu.
   Hii namna ya kumaliza burudani kwa Wasanii hawa.
   Pichani ni kivuli cha Msanii wa Maigizo wa Kundi la Mapoloni Cultural Group aliekuwa akiigiza Jukwaani wakati wa Muendelezo wa Tamasha la 32 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni,linaloendelea kwenye Ukumbi wa Maonyesho wa Chuo Kikuu cha Sanaa,Bagamoyo Mkoani Pwani.
   Wasanii wa Maigizo na Ngoma za asili wa Kundi la Mapoloni,wakionyesha umahiri wao wa kuigiza Jukwaani wakati wa Muendelezo wa Tamasha la 32 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni,linaloendelea kwenye Ukumbi wa Maonyesho wa Chuo Kikuu cha Sanaa,Bagamoyo Mkoani Pwani.
   Wachezaji wa Ngoma za Asili wakionyesha Umahizi wao jukwaani.

  0 0

   Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu kushoto akifuatilia kwa umakini jinsi Afisa Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude, anavyomuelekeza Bw. Mweusi Mohamed Mweusi, namna ya kifaa cha kuchajia simu kwa kutumia umeme wa Jua (Readset Solar Charger)kinavyounganishwa na kuanza kufanya kazi  leo  Katika banda la kampuni ya Vodacom lililoko katika  maonesho ya Wiki ya Huduma za kifedha na uwekezaji yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam. 
  Mmoja wa maofisa wa Vodacom akitoa maelezo kwa baadhi ya wajasiriamali wanaopata mafunzo katika maonesho ya Wiki ya Huduma za kifedha na uwekezaji yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam, Kampuni ya Vodacom imetoa mafunzo kwa wajasiriamali hao ya namna ya kujiunga na kunufaika na fursa ya mikopo isiyokuwa na riba inayotolewa kwa wanawake wajasiriamali  wadogowadogo MWEI.


  0 0

   4793 Wakili wa serikali Mkuu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Frederick Manyanda (kulia) akieleza kwa waandishi wa (hawapo pichani) mkakati wa kuhakikisha kuwa huduma ya usimamizi na utoaji wa haki inawafikia wananchi wote kwa karibu kwa kufungua ofisi zaidi Mikoani, Katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam,katikati ni Afisa Habari toka ofisi hiyo Bi. Asiatu Msuya na Kulia kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Bi. Georgina Misama. 

  4793 Wakili wa serikali Mkuu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Frederick Manyanda (kulia) akieleza kwa waandishi wa (hawapo pichani) mkakati wa kuhakikisha kuwa huduma ya usimamizi na utoaji wa haki inawafikia wananchi wote kwa karibu kwa kufungua ofisi zaidi Mikoani, Katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam,katikati ni Afisa Habari toka ofisi hiyo Bi. Asiatu Msuya na Kulia kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Bi. Georgina Misama. 

  =========  =====  ====

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI  OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFUNGUA OFISI  23 KATIKA MIKOA MBALIMBALI KUFANIKISHA MPANGO WA UTENGANISHWAJI WA SHUGHULI ZA UPELELEZI NA UENDESHAJI WA MASHTAKA NCHINI

  ______________________________


  Utangulizi

  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imefanikiwa kufungua Ofisi 23 katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Kilimanjaro (Moshi), Arusha, Mwanza, Kagera (Bukoba) Mara (Musoma), Shinyanga, Tabora, Singida, Iringa, Mbeya, Mtwara, Lindi, Dodoma, Rukwa (Sumbawanga),Ruvuma (Songea), Njombe, Manyara,Morogoro,Kigoma,Geita  na Pwani. Aidha jumla ya Ofisi mbili (2) za zimefunguliwa katika Wilaya za Temeke na Monduli. Kwa mwaka wa fedha 2012/2013 pekee jumla ya Ofisi tano (5) zimefunguliwa katika mikoa ya Pwani, Kigoma, Morogoro, Manyara, Njombe na Geita ikiwemo pia Ofisi mbili za Wilaya.


  Lengo

  Lengo kuanzishwa na kuimarishwa kwa Ofisi hizi za Mikoa na Wilaya ni kuhakikisha kuwa huduma ya usimamizi na utoaji wa haki inawafikia wananchi wote kwa karibu zaidi. Baadhi ya huduma zinazotolewa ni pamoja na kuendesha Mashtaka mahakamani, kushughulikia malalamiko na kero za wananchi kuhusiana na kesi za jinai na madai zinazowakabili, kutembelea mahabusu na kuratibu upelelezi wa kazi za upelelezi wa makosa ya jinai zinazofanywa na vyombo pelelezi/chunguzi ikiwemo Polisi, Magereza, Uhamiaji,TAKUKURU.


  Utekelezaji wa Mpango wa kutenganisha Upelelezi na Mashtaka nchini

  Serikali kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeendelea kutekeleza mpango huu wa Utenganishwaji wa Upelelezi na Mashtaka kwa mujibu wa Sheria ambapo mfumo wa Sheria ambao uliwezesha kutungwa kwa Sheria ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, 2005 na Sheria ya Usimamizi wa Uendeshaji Mashtaka nchini, 2008 umeboreshwa; pamoja na kuanzishwa kwa Jukwaa la Ki-taifa la Haki-Jinai (National Criminal Justice Forum) Desemba 2009 linaloviunganisha pamoja vyombo vyote vinavyosimamia utolewaji wa Haki-Jinai nchini;


  Serikali pia imeboresha  Muundo wa Divisheni ya Mashtaka kwa kuweka Sehemu (Section) mahsusi inayosimamia utekelezaji wa mchakato wa utenganishaji wa kazi za upelelezi na Mashtaka na uratibu wa kazi za ki-pelelezi; pamoja na kuanzishwa kwa huduma ya Mashtaka ya moja kwa moja ambako Mawakili wa Serikali wanaendesha kesi;  Hii imepelekea idadi ya kesi zinazofunguliwa Mahakamani ambako Mawakili wa Serikali wanaendesha Mashtaka kupungua ikilinganishwa na kipindi cha nyuma; Kuongezeka kwa ubora wa huduma zitolewazo na kupungua kwa kesi za kubambikizwa.


  Utekelezaji wa Programu ya Utenganishwaji wa Mashtaka na Upelelezi (Civilianization) imetoa msukumo mkubwa kwa Ofisi kuingia uanachama na makubaliano ya mashirikiano na vyama vinavyohusiana na kazi za Uendeshaji Mashtaka duniani, kama vile-IAP, HOPAC, APA, EAAP, na ARINSA; Serikali itaendelea kupanua wigo wa uendeshaji wa Mashtaka kwa kuanzisha na kuimarisha Ofisi katika Wilaya zote nchini pamoja na Mikoa miwili iliyobaki ya Katavi na Simiyu.


  Tunapenda kuwakumbusha Wadau wetu wote na Wananchi kwa ujumla kuwa mstari wa mbele katika kutoa taarifa za uhalifu au jinai yoyote katika jamii kwa vyombo husika kupitia utaratibu unaofaa; na kutoa ushahidi Mahakamani pale unapohitajika kwa kuwa hizi  ni nguzo muhimu katika uendeshaji wa kesi mbalimbali. Aidha tunatoa wito kwa umma, wadau wetu na wananchi wote kwa ujumla pamoja na vyombo vya habari nchini kufuatilia mtiririko, hoja zinazowalishwa Mahakamani na uamuzi uliotolewa na Mahakama katika kesi mbalimbali zinazoendelea kuwa na taarifa sahihi ya kuhusu kesi hizo.


  Imetolewa Na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

  Ijumaa, Septemba 27, 2013


   Kwa mawasiliano zaidi

  OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

  SLP 9050

  KIVUKONI FRONT

  DAR ES SALAAM

  SIMU: +255 22 21181778

  NUKUSHI: +255 22 2113236

  BARUA PEPE: info@agctz.go.tz 

  TOVUTI:            www.agctz.go.tz

  0 0

  ZAIDI ya  washiriki 100 kutoka ndani na nje ya nchi watashiriki kwenye tamasha la Sanaa na utamaduni la Jambo Festival litakalofanyika oktoba 23 hadi 27 mwaka huu katika viwanja vya Suye vilivyopo mjini hapa.


   Mwenyekiti wa tamasha hilo, la Jambo Festival 2013 ,Augustine Namfua alisema kuwa , tamasha hilo ni la pili kufanyika mkoani Arusha ambapo wamekuwa wakifanya kila mwaka lengo likiwa ni kuwawezesha  washiriki mbalimbali kuweza kuonyesha bidhaa zao za kitamaduni kutoka ndani na nje ya nchi.


  Alisema kuwa, tamasha hilo ambalo ni la kimataifa pia litawashirikisha washiriki kutoka nchi za Ufaransa,na Angentina ambao wataweza kuonyesha matamasha mbalimbali ya kitamaduni sambamba na kuonyesha bidhaa zao za kitamaduni  .


  Alisema kuwa, tamasha hilo litaenda sambamba na matukio mbalimbali ya kiasili ikiwemo maonyesho  ya mavazi ya kiasili,pamoja na tamasha la kiasili kutoka vikundi jijini Tanga, Arusha,  na Dar es Saalamu .

   Namfua aliongeza kuwa, pia kutakuwepo na tamasha la muziki wa kisasa    pamoja na onyesho la  mavazi , na ubunifu wa mavazi ambapo  katika tamasha hilo kwa siku hizo kila siku kutakuwa na matamasha mbalimbali ambayo yatakuwa yakionyeshwa .


   Aliongeza kuwa, tamasha hilo limekamilika kwa asilimia 50 huku watu mbalimbali wakiwemo binafsi, mashirika na taasisi mbalimbali zinazohusika na maswala ya sanaa na tamaduni wanaendelea kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kushiriki katika tamasha hilo .


   ‘tamasha la mwaka jana lilifana sana kwani tuliweza kupata washiriki wengi sana kutoka ndani na nje ya nchi na lilikuwa na mwitiko mkubwa sana , huku watu mbalimbali wakipata fursa ya kuonyesha sanaa zao na tamaduni mbalimbali na kuweza kujifunza kutoka kwa wenzetu wan je ya nchi ndio maana tumeamua kufanya tena mwaka huu mwezi wa kumi hivyo tunatarajia  watu mbalimbali kushiriki kikamilifu katika tamasha hilo’alisema Namfua.


   Aidha aliwataka watu mbalimbali kufika katika tamasha hilo na kuonyesha  bidhaa zao za kitamaduni zinazotengenezwa kwa mikono pamoja na kutangaza tamaduni zao za kiafrika , huku akiwataka wadau mbalimbali kuonyesha  moyo katika kusaidia matamasha hayo  ili yaendelee kufanyika mara kwa mara.

  0 0


  Mfadhili wa shirika lisilo la kiserikali la Ilula Orphan Program(IOP) la Iringa, Yokes na Klaas wakimkabidhi moja ya vifaa mganga mkuu wa hospitali ya Ilula Dk. Erasto Rite alivyoikabidhi hospitali teule ya Ilula makabidhiano yaliyofanyika katika hospitali hiyo ilula
   iliyoko wilaya ya Kilolo mkoani Iringa2. Mfadhili wa shirika lisilo la kiserikali la Ilula Orphan Program(IOP) la Iringa, Klaas akionyesha moja ya vifaa vya kuongeza joto kwa watoto alivyoikabidhi hospitali teule ya Ilula makabidhiano yaliyofanyika katika hospitali hiyo ilula iliyoko wilaya ya Kilolo mkoani Iringa3. Mfadhili wa shirika lisilo la kiserikali la Ilula Orphan Program(IOP) la Iringa, Klaas akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Ilula na wafanyakazi wa IOP. (Picha zote na Denis Mlowe)
  =========  =======   ==========
  HOSPITALI TEULE YA ILULA YAPATIWA MSAADA


  Na Denis Mlowe,Ilula  MFADHILI  wa shirika lisilo la kiserikali la Ilula Orphan Program(IOP) la Iringa, Yoker n Klaas ametoa msaada wa vifaa tiba na ukarabati  wa majengo ya hospitali teule ya Ilula iliyoko katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa  vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 32  kwa ajili ya kuwasaidia mama wajawazito na watoto wanaozaliwa kabla ya muda(njiti).  Akizungumza wakati akikabidhi msaada wa vifaa tiba kwa mganga mkuu wa hospitali hiyo Dk. Erasto Rite katika makabidhiano yaliyofanyika katika hospitali hiyo, Klaas alisema lengo ni kupunguza vifo wa watoto na kusaidia kutoa huduma bora kwa wananchi wasio na uwezo walioko katika wilaya hiyo na   sehemu za jirani.  Alisema watoto wachanga wanategemea sana misaada kutoka kwa wakubwa hivyo msaada wa huduma bora ni jukumu la kitu mwanajamii kuweza kutoa kile ambacho anaweza kuasaidia katika jamii.  "Tutajitahidi kuweza kuwalinda kwa njia yoyote na moja ya malengo ya IOP ni kuweza kulinda afya za watanzania na kuwaletea maendeleo hivyo msaada huu ni mwanzo tu wa kuwapatia vifaa vya kazi" alisema Klaas  Klaas alisema msaada huo ni ishara ya kuendelea kuimarika kwa ushirikiano baina ya hospitali hiyo na asasi hiyo na kuahidi kuendelea kutoa misaada kuimarisha huduma za afya kwa wananchi wa wilaya ya Kilolo.  Kwa upande wake, Dk. Erasto Rite alisema msaada wa vifaa tiba utaisaidia hospitali hiyo kuhudumia watoto wengi zaidi na kwa uhakika na kuwashukuru shirika hilo lisilo la kiserikali kwa msaada huo uliowafikia kwa wakati.    Alisema hospitali hiyo ina upungufu mkubwa wa vifaa tiba, ukosefu wa maji, chumba cha maiti na   ukosefu wa gari la kubebea wagonjwa  Alisema lengo la Hospitali hiyo ni kuongeza viwango vya matibabu kuweza kufikia hadhi ya kitaifa kwa kuwa na vifaa bora na kuongeza huduma nyingi zaidi ambazo hazipatikaniki katika hospitali hiyo.  Rite alisema lengo la hospitali hiyo kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wanaozaliwa kabla ya muda (njiti) kuimarisha miundo mbinu ya hospitali hiyo kwa kujenga idara mbalimbali na kujenga  sehemu za kulaza wagonjwa .

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (katikati) akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu matokeo ya utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa.
  Afisa Mwandamizi wa Benki ya Dunia Bw. Richard Martini (katikati) akitoa salaam za Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Bw. Phillipe Dongier, ameipongeza Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kuzingatia vigezo vya tafiti vya kimataifa katika kutoa matokeo ya Mapato na Matumizi ya Kaya nchini.

  Na. Aron Msigwa – MAELEZO,Dar es salaam.

  Uwezo wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi  nchini kwa mwaka 2011/2012  unaonyesha kuongezeka kutokana  na  maboresho  mbalimbali  yaliyofanyika katika sekta ya elimu, afya, umiliki wa biashara, shughuli za kilimo, umiliki wa Vifaa na Rasilimali , makazi bora, ongezeko la shughuli za kiuchumi na ajira.

   Akitoa taarifa ya Utafiti  ulioendeshwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kuangalia tathmini ya kiwango cha umasikini wa kaya kwa kutumia kipato na masuala mengine yasiyo ya umasikini wa kipato leo jijini Dar es salaam , Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile amesema kuwa kukua kwa kiwango cha elimu, matumizi ya nishati ya umeme, hali ya makazi na umiliki wa rasilimali ni miongoni mwa sababu za kuongezeka kwa uwezo wa mapato na matumizi ya kaya.


  0 0

   Salha israel mrembo alieng'ara miaka ya 2011 katika mashindano ya urembo nchini,akiongea na washiriki wa Tanzania Top Model 2013 namna ya kujiamini wakiwa katika jukwaa na kujibu maswali endapo watakabiliana na vyombo vya habari.
  Washiriki wakimsikiliza kwa makini Salha Israel wakati akiongea nao.
   Washiriki wakiwa katika picha ya paoja na Salha israel.
    Mrembo Salha Israel atembelea kambi ya washiriki wa sindano la Tanzania Top model iliopo katika hoteli ya Jb Belmont iliyopo maeneo ya posta kwa lengo la kuwapa mbinu mbalimbali za kufanya vizuri jukwaani kwani shindano hilo lina upinzani mkali kwa washiriki wenyewe kwa wenyewe.

    Salha alitoa mbinu mbalimbali za kujiamini kwa mwanamitindo awapo jukwaani pamoja na mbinu za kujibu maswali kiusahihi kwa wanahabari ambapo imezoeleka kwa washiriki wengi hushindwa kujibu maswali kiusahihi kitu ambacho hupunguza ari ya shindano.

    Fainali za mashindano haya zitafanyika desemba 7,pia washiriki watapigiwa kura na wananchi ambapo namba maalumu itaolewa hivi punde kumpigia mshiriki umpendae ili kumuongezea alama amabazo zitamwezesha mshiriki wako ashinde.

  0 0

  MwanaFA3
  Mwanamuziki maarufu wa kizazi kipya Hamisi Mwinjuma a.k.a Mwana Fa a.k.a Binamu ambaye hivi sasa yuko nchini Marekani kwa ziara maalum anatarajiwa kuwa mgeni katika kipindi cha Live Talk katika idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika (VOA). Kipindi hicho ambacho hurushwa moja kwa moja na radio washirika kinaanza saa moja na nusu saa za Afrika Mashariki na saa kumi na mbili na nusu jioni saa za Afrika ya kati na Washington itakuwa ni saa tano na nusu asubuhi . 

  Katika matangazo ya Ijumaa hii VOA itazungumzia suala zima la Muziki wa Bongo Flava unakoelekea na changamoto zake kwa ujumla. Kipindi hiki kitarushwa kwa muda wa saa moja ambapo nusu ya kwanza itakuwa kwenye radio washirika na ili usikie kwa saa nzima ungana na VOA kwenye mtandao . www.voaswahili.com

  0 0

  E83A4423
  Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Katala Beach hoteli mjini Singida.
  E83A4411
  Mjumbe wa bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Lyidia Choma (kulia) akitoa taarifa yake kwenye siku ya wadau wa Mfuko huo na ule wa Afya ya Jamii (CHF).Mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Katala Beach Hotel mjini Singida. Kushoto (aliyeshika mike) ni Meneja wa NHIF mkoa wa Singida, Agnes Chaki.
  E83A4406
  Mkurugenzi wa takwimu na uhai wa mfuko wa NHIF makao makuu, Michael Mhando akitoa nasaha zake kwenye mkutano wa wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Katala Beach Hotel mjini Singida. Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, Wa kwanza kulia ni kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Mussa Kamala, Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi na katibu tawala mkoa wa Singida,Liana Hassan.
  E83A4435
  Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, (wa pili kulia) akifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano wa siku ya wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii. Wa kwanza kulia ni Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bi. Lyidia Choma.Wa tatu kulia ni Katibu Tawala mkoa wa Singida, Liana Hassan na,Mkuu wa Wilaya ya Singida,Queen Mlozi na kaimu Mganga Mkuu mkoa wa Singida,Dk.Mussa Kimala.


  Na Nathaniel Limu
  Zaidi ya asilimia 73 ya kaya za mkoa wa Singida, hazijajiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF), hali inayochangia wanafamilia watibiwe bila utaratibu maalum.

  Hayo yamesemwa na mkuu wa moa wa Singida, Dk. Parseko Kone, wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa mkutano wa siku ya wadau wa Mfuko wa Taifa Bima ya Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii (NHIF) wa mkoa wa SIngida.
  Akifafanua, amesema kati ya kaya 259,251 za mkoa wa Singida, ni kaya 45,575 tu, ndizo zilizojiunga na mfuko wa afya ya jamii kati ya mwaka 1998 na Septemba 30 mwaka huu. Hii ni sawa na asilimia 17.6 tu.

  “Hata hivyo,wilaya ya Iramba imekuwa ikifanya vizuri katika uandikishaji wa wananchi, kwani takwimu zinaonyesha hadi Septemba 30 mwaka huu, wamekwisha andikisha asilimia 50.3 ya kaya zilizolengwa. Hali hii inaonyesha kuwa viongozi bado hatujatimiza wajibu wetu wa kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko huu”, amesema Dk.Kone.

  Aidha, mkuu huyo wa mkoa, amesema pia inawezekana watoa huduma wamekuwa ni chanzo cha kuwakatisha tama wananchi waliojiunga na hivyo, kuwafanya wananchi wengine wasite kujiunga na Mfuko huu.
  “Kwa kuwa wadau wote tumekutana hapa leo, ni nafasi yetu kuangalia nini sababu ya kuzorota kwa utaratibu huu ambao katika baadhi ya halmashauri hapa nchini, umeimarika zaidi",amesema Dk.Kone.

  Awali mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Lyidia Choma, alisema Mfuko huo umeidhinisha shilingi bilioni 10, ili zitolewe kwa watoa huduma kuwawezesha kupata vifaa tiba na kukarabati maeneo yao ya kutolea huduma.

  “Utaratibu huu ni mikopo ya bei nafuu ambayo hairejeshwi kwa fedha taslimu, isipokuwa kwa kukatwa katika madai ambayo mtoa huduma anawasilisha kwa Mfuko”,amefafanua. Alifafanua kuwa kwa mkopo wa vifaa tiba, mkopo hurudishwa kwa makato ya asilimia 10 ambayo hulipwa ndani ya miezi 24 na mikopo ya ukarabati wa maeneo ya kutolea huduma, ni miezi 36. Kauli mbiu ya mwaka huu, ni Afya Bora kwa wote sasa kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akitolea ufafanuzi wa kina kwa Wakazi wa kijiji cha Nakapanya Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma mapema leo jioni,kuhusiana na tatizo sugu la bei ya zao la Korosho kwa wakulima,ambao wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu,Kinana aliwahakikishia Wanachi hao kuwa tatizo hilo watalifanyia kazi ipasavyo na kufikia hatua ya kulimaliza kabisa. 

  Aidha tatizo hilo ni kubwa kwa upande wa mikoa ya Kusini,ikiwemo Mtwara,Lindi na Ruvuma.Kinana alibainisha kuwa CCM kitahakikisha suala la hilo linashughulikiwa kwa umakini  mkubwa ikishirikiana na Serikali sambamba na sambamba na taasisi zinazohusika na zao hilo,ili kukomboa uchumi wa Wananchi wa eneo hilo hasa kwa kuhakikisha viwanda vya kubangua korosho vinajengwa na vile ambavyo vimebinafsishwa na havifanyi kazi kunaandaliwa utaratibu ambao utawafanya wawekezaji wengine kupewa ili vifanye kazi na kutatua tatizo la bei ndogo ya zao hilo inayolipwa na wanunuzi. 

  Katika ziara hiyo hiyo Kinana ameongozana na Katibu wa NEC siasa,Itikadi na uenezi Ndugu Nape Nnauye na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dkt.AshaRose Migiro. 
   Baadhi ya Wakazi wa kijiji cha Nakapanya Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wakishangilia jambo mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,kuzungumzia na kufafanua vyema kuhusiana na tatizo kubwa lililopo kwenye zao la Korosho,ambako kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi ikiwemo suala la bei ya ununuzi wa Korosho kuwa ndogo,malipo kutokulipwa kwa wakati kwa wakulima na mengineyo.
  Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini ,Mh.Ramo Matalla Makani akielezea baadhi ya matatizo yanayoisumbua Wilaya hiyo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana  (pichani kulia) mapema leo,katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Nakapanya,Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.Kinana na ujumbe wake wataanza ziara yao rasmi leoo Wilayani humo mkoani Ruvuma kwa madhumuni ya kuimarisha chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa Ilani ya CCM,katika Mikoa ya Ruvuma na Mbeya.
  Baadhi ya Wakazi wa kijiji cha Nakapanya Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wakiwa wamekusanyika mapema jana wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,alipokuwa akizungumza nao kuhusiana na ufumbuzi wa matatizo yao mbalimbali ikiwemo suala la huduma za afya,Barabara,Maji sambamba na tatizo sugu la zao la Korosho wilayani humo.

  0 0

  Tanzania Financial Services for Underserved Settlements (TAFSUS

  Tanzania Financial Services for Underserved Settlements (TAFSUS) is a Local Finance Facility which provides credit enhancement to Community Driven Settlement Upgrading Projects in the form of Guarantee or bridge finance. 

   TAFSUS is a not-for-profit organization registered on 27th January 2009 with registration No 69478 as a Company limited by guarantee, located within TAWLAT offices, NIC Life House, 5th Floor at the Sokoine Drive/Ohio Avenue.

  The Objectives of TAFSUS are:
  ·         To bring together key players involved in cities and national level settlement upgrading strategies to address the challenge of financing;
  ·         To catalyze the integration of commercial finance into settlement upgrading;
  ·         To provide mechanisms to blend different forms of funding to maximize affordability for the poor;
  ·         To provide a financial mechanism to support the implementation of city-based settlement upgrading strategies; and
  ·         To advocate for sound policies, enforcement of laws and proactive planning to prevent further growth/generation of unplanned areas.
  TAFSUS is looking at supporting community initiatives through development of Bankable projects to access funds from commercial financial institutions with leverage of community contribution and Government subsidy. TAFSUS also offers technical support for developing and upgrading projects which include low cost housing, accesses to portable water and titling of properties in informal settlements.

  TAFSUS has currently entered into Agreement with Azania Bank Limited to provide Credit Guarantee Facility to finance upgrading of unplanned settlements.

  TAFSUS  now invites Associations, NGOs, Registered Communities or Groups to submit brief Concept Notes of maximum of 3 pages indicating name of organisation, nature of project, location, problem to be solved, beneficiaries, estimation of revenue and expenditures, Project costs and any other aspects that they feel should be known to enhance the acceptability of the project (Technical and Financial).

  Budget Limit
  The value of the Project should not exceed Tshs.100 Million per applying Organization or Group.
   
   Submission of the Concept Note

  The Concept Note should be submitted to TAFSUS by 20th November 2013. Mode of submission is in Hard copy and Soft copy to;
  TAFSUS Manager,
  Tanzania Financial Services for Underserved Settlements,
  P O Box 79603
  Dar es Salaam- Tanzania

  Tel No.  022-2120285

   NOTE:
  ·                     While preparing projects, the following aspects are inclusive:
  Ø  Access to improved water supply;
  Ø  Access to impoved sanitation;
  Ø  Sufficient living areas;
  Ø  Durability of housing; and
  Ø  Security of tenure.
  ·         For more information on services and type of projects supported by TAFSUS, visit www.tafsus.co.tz
  • TAFSUS is not providing Grants or Loans but is providing Credit Enhancement
  • Late proposals will not be accepted

  DELIVERED BY TAFSUS  November, 2013

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injnia Stella Manyanya akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni nane (8) Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa Wafugaji wa Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa Ndugu Pancras Maliyatabu kama fedha ya kianzio kwa Kongano la umoja wa wafugaji hao zilizotolewa na Tume ya Sayansi na Teknolojia nchini (COSTECH) kwa lengo kuendeleza ufugaji wa kisasa usioathiri mazingira na kumnufaisha mfugaji kiuchumi. Kulia ni Ndugu Festo Maro Afsa Utafiti Mkuu wa COSTECH na kushoto ni Katibu wa Umoja wa Wafugaji hao Ndugu Jisena Biliya.
  Viongozi wa Umoja wa Wafugaji wa Wilayani Nkasi wakionyesha hundi yenye thamani ya shilingi milioni nane waliyopewa na COSTECH kama "Seed Fund" kwa ajili kuendeleza kongano la wafugaji Wilayani humo. Kulia wanaoshuhudia ni Ndugu Festo Maro Afsa Utafiti Mkuu wa COSTECH na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na Wanakongano wa Umoja wa Wafugaji wa Wilayani Nkasi (hawako pichani) katika Mkutano uliofanyika Kalambo Ranch  Wilayani humo tarehe 14 Novemba 2013. Mkuu huyo Mkoa aliwataka wafugaji kufuga kisasa bila kuathiri mazingira kwa kufuga mifugo michache inayoendana na maeneo husika, aliwataka pia wafugaji kuwaendeleza watoto wao kielimu tofauti na ilivyo hivi sasa amabao wengi wao hufanyishwa kazi za uchungaji wa mifugo. Katika hotuba yake fupi alitoa agizo kwa halmashauri zote Mkoani Rukwa kuweka kipaombele katika kutenga maeneo kwa ajili ya wafugaji na wakulima katika kila kijiji na kujiwekea mkakati wa idadi ya mifugo itakayofugwa kulingana na ukubwa wa eneo la malisho.
  Ndugu Festo Maro Afsa Utafiti Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Nchini COSTECH akizungumza na wanakongano wa Umoja wa Wafugaji wa Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa jana tarehe 14 Novemba 2013. Katika maelezo yake alisema kuwa sio kila Kongano hupewa fedha za kianzio bali hushindanishwa na kwamba Kongano la Umoja wa Wafugaji wa Wilayani Nkasi likiwa na wanachama 167 limeibuka washindi kwa kuwa na mipango thabiti ya kuendeleza shughuli zao za ufugaji kisasa kwa kuwainua kiuchumi, kielimu, kiafya na kubwa zaidi bila kuathiri mazingira. Alisema Lengo la COSTECH kutoa misaada kama hiyo ni kuwawezesha wadau wafanye shughuli zao kisayansi zaidi.
  Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aweze kuzungumza na Wanakongano wa Umoja wa Wafugaji wa Wilayani humo ambao yeye ndie muasisi wa umoja huo. Katika neno lake la awali alimtaarifu Mkuu huyo wa Mkoa kuwa Umoja huo ulianzishwa mwaka jana 2012 tarehe 29 Agosti na kusajiliwa rasmi tarehe 30 Agosti 2013 ukiwa na wanachama 167 na lengo kuu likiwa ufugaji bora wa kisasa usioathiri mazingira na utakaomnufaisha mfugaji.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa Wafugaji wa Wilayani Nkasi Ndugu Pancras Maliyatabu Cheti rasmi cha usajili wa umoja huo uliosajiliwa rasmi tarehe 30 Agosti 2013. Katikati anaeshuhudia ni Katibu wa umoja huo ndugu Jisena Biliya.
  Picha ya pamoja. (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

  0 0

  ________________

  MUDA

  TUKIO


  LEO, NOVEMBA 15, 2013 – UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU JK NYERERE  Saa 12:50 jioni

  Kuwasili kwa mwili wa Marehemu – Uwanja wa Ndege wa Mwalimu JKN  KESHO, NOVEMBA 16, 2013 – VIWANJA VYA KARIMJEE


  Saa 2:00 – 3:30 asubuhi

  Kuwasili kwa Wageni, Wananchi na Waombolezaji


  Saa 3:30 asubuhi

  Kuwasili Mwili wa Marehemu


  Saa 4:00 – 5:45 asubuhi

  Ibada ya Misa Takatifu, Viwanja vya Karimjee


  Saa 5:45 – 6:55 mchana

  Salaam za Rambirambi na Neno la Shukurani  Saa 6:55 – 8:40 Mchana

  Kuaga Mwili wa Marehemu  Saa 9:00 Alasiri

  Msafara kupeleka mwili wa marehemu Kibamba Msakuzi  KESHO KUTWA, NOVEMBA 17, 2013 – NYUMBANI KWA MAREHEMU - KIBAMBA, MSAKUZI


  Saa 2:30 – 4:30 asubuhi

  Ibada ya Misa nyumbani kwa marehemu


  Saa 5:00 asubuhi

  Kuanza safari ya kwenda Chanjale, Kisangara Juu, Mwanga, Kilimanjaro

  0 0

   Muuguzi katika kituo hicho cha St. Laurent Diabetes Centre, akimpima Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Ask. Dk. Alex Malasusa huku Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi akishuhudia.
   Wananchi mbalimbali wakipata huduma ya kupimwa ugonjwa wa sukari katika kituo hicho cha St. Laurent Diabetes Centre
  Burudani kutoka Mjomba Band ikitolewa
  ******
  Ugonjwa wa Kisukari umekuwa tishio kwa mataifa mengi duniani, Tanzania ikiwemo. Inasemekana kuwa nchi maskini na zinazoendelea duniani ndio zinazongoza kwa ugonjwa wa Kisukari. Aidha, kwa sasa ugonjwa wa Kisukari unashika nafasi ya tatu duniani kueneza vifo.

  Katika makala hii, Mtaalam  wa Maradhi  ya Kisukari , Dkt. Mary Mayige , kutoka kituo cha Kisukari cha St. Laurent Diabetes Centre, jijini Dar es Salaam anaeleza kwa ufasaha dalili za ugonjwa huu, kinga na tiba yake.

  Dkt. Mary Mayige  anafafanua kuwa Kisukari kwa kifupi (na kwa lugha ya kueleweka) ni ugonjwa unaotokana na kuwa na kiasi kikubwa cha sukari kwenye damu.  Aliongezea kuwa sukari inapokuwa nyingi kwenye damu ya binadamu, hapo ndipo mtu huyo husumbuliwa na maradhi hayo.

  Mkurugenzi  Mtendaji wa kituo cha Kisukari yaani St. Laurent Diabetes Centre, Dkt. Mary Mayige aliwakaribisha watanzania wote katika upimaji wa bure wa Kisukari na pressure katika kituo chao kilichopo Msasani karibu na CCBRT, Dar es Salaam tarehe 10/11/2013. Kabla ya uzinduzi rasmi wa kituo hicho, watanzania walijitokeza kwa wingi kupima na kujua afya zao siku hiyo na kujipatia ushauri wa bure kutoka kwa madaktari na wauguzi wa kituo hicho.

  Watu wengi walinufaika na huduma zilizotolewa na kitu hicho cha St.Laurent Diabetes Centre.

  Siku moja kabla ya maadhimisho ya siku ya Kisukari Duniani, kituo cha St. Laurent Diabetes Centre walifanya uzinduzi rasmi wa kituo chao Wakiongozwa na mgeni rasmi Mkuu wa Kanisa la KKKT Askofu Dkt. Alex G. Malasusa, pamoja na Waziri  wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt .Hussein Mwinyi, na  Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mhe. January Makamba na waheshimiwa wageni waalikwa wawakilishi kutoka serikalini, kwenye  sekta binafsi , za umma na sekta za afya.

  0 0

  Mohamed-deji31
  Once again a Tanzanian-born Mohammed ‘Mo’ Dewji has been mentioned as one of the Africa’s successful young businessmen at Forbes Magazine. He is the CEO of METL, a large Tanzanian conglomerate with activities in distribution, Textiles, Manufacturing, Agriculture and Real estate.

  As young brilliant Tanzanian entrepreneur ‘Mo’ his father, Gulam Dewji, started their family business as a commodities trading. After Mo finished studying business at Georgetown University, he returned home and took the reins of the family business, transforming it into a manufacturing player. He is also a Member of Tanzania’s parliament and has a net worth estimated at USD 500 million.

  It is an amazing story that tells a long walk of 12 years in business competition in Tanzania, East Africa and Africa at large.

  0 0

  Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Uingereza, Prince Charles ambaye pia ni Mtoto wa Malkia wa nchi hiyo, Malkia Elizabeth II ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa hatua zake za dhati za kulinda wanyamapori na kupambana na ujagili dhidi ya tembo na faru. 

   Aidha, Prince Charles amesema kuwa yuko tayari kuunga mkono juhudi hizo za Tanzania kwa kushirikiana na mtoto wake, Prince William ambaye amechagua shughuli za kulinda wanyamapori na kupambana na ujangili duniani kama moja ya shughuli zake kuu. 

   Moja ya hatua ambazo Prince Charles ameamua kuchukua ni kukabiliana na soko la bidhaa kuu za ujangili duniani, na hasa meno ya tembo na faru, na kufanya kampeni kubwa duniani dhidi ya biashara hiyo haramu. 

   Prince Charles ametoa pongezi hizo na msimamo wake wa kuunga mkono jitihada za Tanzania wakati alipokutana kwa mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. Viongozi hao wamekutana kwenye Jumba la Tintagel mjini Colombo, Sri Lanka, ambako amefikia wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) ambao Prince Charles ameufungua rasmi asubuhi ya leo, Ijumaa, Novemba 15, 2013, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mahinda Rajapaksa. 

  Rais Kikwete naye yuko Sri Lanka kuhudhuria Mkutano huo. Wakati wa mazungumzo hayo, Rais Kikwete ametumia muda mrefu kumwelezea Prince Charles kuhusu hatua ambazo zimekuwa zinachukuliwa na Serikali yake kupambana na ujagili dhidi ya tembo na faru ikiwamo Operesheni Maalum – Operesheni Tokomeza -ambayo ilifanyika hivi karibuni kuwasaka na kukabiliana na wafanya biashara haramu ya meno ya tembo.

   Rais Kikwete amemwambia Prince Charles kuwa pamoja na kuchunguza malalamiko yaliyotolewa na makundi mbali mbali ya watu kuhusu operesheni hiyo ya kwanza, bado operesheni hiyo itaendelea kwa sababu ni muhimu kulinda wanyamapori dhidi ya majangili. “Imefika mahali ambako tunahitaji kuchukua hatua kali. 

  Wakati wa Uhuru wetu kulikuwepo na tembo kiasi cha 350,000 lakini ilipofika mwaka 1989 idadi hiyo ilikuwa imepungua na kubakia 55,000. Hata hivyo, baada ya operesheni maalum na kubwa, idadi hiyo ilikuwa imeongezeka hadi kufikia 110,000 kabla ya kuanza wimbi jipya la ujangili mwaka 2010. Operesheni lazima iendelee,” Rais Kikwete amemwambia Prince Charles. 

   “Tusaidie kufunga na kuvuruga hili soko la bidhaa za wanyampori. Operesheni ya sasa imethibitisha kuwa mtandao wa uwindaji haramu na biashara haramu ya meno ya tembo na faru ni mkubwa na watu wengi wanahusika, lakini kinachovuruga zaidi ni kwamba lipo soko la uhakika la meno ya tembo.” 

   Prince Charles amemweleza Rais Kikwete kuhusu hatua ambazo anakusudia kuzichukua kukabiliana na hali hiyo, ikiwa ni pamoja na kuandaa mkutano mkubwa wa wakuu wa nchi na Serikali Februari 13, mwakani na kufanya mkutano mwingine mkubwa na vyombo vya habari kutoka pote duniani mwakani. 

   “Nakusudia pia kutumia wasanii nyota mbali mbali duniani kuendesha kampeni ya kuielimisha dunia kuhusu athari za biashara hiyo haramu kwa sababu asilimia kubwa ya mapato ya ujangili inasaidia kugharimia vikundi vya kigaidi duniani.” 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwana wa Malkia  Elizabeth II wa Uingereza, Prince Charles,  jijini Colombo, Sri Lanka, leo Novemba 15, 2013 pembeni ya mkutano wa Wakuu wa nchi za Junuiya ya Madola (CHOGM 2013) ambako Prince Charles, maarufu zaidi kama His Royal Highness the Prince of Wales, anamwakilisha mama yake mwenye umri wa miaka 87 ambaye hakuhudhuria kwa mara ya kwanza katika miaka 40 ya historia ya mkutano huo unaofanyika kila baada ya miaka miwili katika nchi itayoteuliwa mwishoni mwa mkutano. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe Peter Kallaghe.

  Malkia Elizabeth wa II alihudhuria CHOGM kwa mara ya kwanza mwaka 1973 jijini Ottawa, akiwa kakosa kikao cha mwaka 1971, na tokea hapo hajakosekana tena hadi safari hii. Alikuwepo pia katika mkutano wa mwisho uliofanyika mwaka 2011 jijini  Perth, Australia. 

  Na hii ni mara ya kwanza kwa Prince Charles kumwakilisha mama yake ambaye imesemekana hakwenda Sri Lanka kutokana na ushauri wa kutosafiri umbali mrefu. Ila katika CHOGM 2007 iliyofanyika Kampala, Uganda, yeye na mama yake walihudhuria pamoja.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika kikao cha ufunguzi cha wakuu wa nchi za Jumuiya ya Madola jijini Colombo Srilanka leo asubuhi.kushoto ni Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete asubuhi ya leo, Ijumaa, Novemba 15, 2013, alikuwa miongoni mwa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola 53 walioshiriki katika sherehe kubwa na za kufana za Mkutano huo wa siku tatu.

  Sherehe hizo zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Nelum Pokuna Mahinda Rajapaksa mjini Colombo, Sri Lanka, ziliendelea kwa karibu saa mbili kuanzia saa nne kamili asubuhi.

  Miongoni mwa viongozi ambao walizungumza kwenye sherehe hiyo ya ufunguzi ni Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kisoshalisti ya Sri Lanka, Mheshimiwa Mahinda Rajapaksa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mheshimiwa Kamalesh Sharma.


  Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Uingereza Prince Charles ndiye amefungua rasmi Mkutano huo kwa niaba ya Mama yake, Malkia Elizabeth ambaye ni Mkuu wa Jumuiya ya Madola. Malkia Elizabeth hakuweza kuhudhuria Mkutano huo.


  Mara baada ya ufunguzi huo uliopambwa na ngoma za kuvutia sana ukiwamo muziki wa vijana na maonyesho ya watoto wa shule ambao walizunguka Ukumbi wa Mikutano, wakuu hao walihamia kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kumbukumbu wa Bandaranaike kwa ajili ya kuanza vikao rasmi.


  Wakati wa chakula cha mchana, viongozi hao walihudhuria hafla rasmi iliyoandaliwa na Mheshimiwa Sharma na baadaye jioni wamehudhuria Chakula cha Usiku kilichoandaliwa na Prince Charles na mkewe, The Duchess of Cornall kwenye Hoteli ya Cinnamon Lakeside.


  Imetolewa na; 
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, 
  Ikulu, DAR ES SALAAM. 
   15 Novemba, 2013


  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiana na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk Asha-Rose Migiro  kujenga daraja la mto Munjapu wilayani Tunduru.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyeshwa jinsi barabara itakavyokuwa baada ya kukamilika kwa daraja la mto Munjapu,lililopo kijiji cha Mnemasi, Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kuimarisha chama,kusimamia ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 katika mkoa wa Ruvuma akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa kwenye kijiji cha Mchoteka kwa staili ya aina yake ya kukimbia mchaka mchaka mpaka kwenye miradi ya ujenzi wa madarasa,maabara na nyumba za walimu katika shule ya Sekondari ya Mchoteka wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa moja ya nyumba za walimu wa shule ya Sekondari Mchoteka,wilayani Tunduru.
  Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akishiriki uchimbaji wa msingi wa vyumba vya maabara ya shule ya sekondari Mchoteka wilayani Tunduru.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na umati wa wananchi wa kijiji cha Mchoteka wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Mchoteka waliofurika kutaka kumsikiliza, Katibu Mkuu alikuwa na ratiba ya kuonana na kumsalimia balozi wa nyumba kumi lakini kwa namna wananchi walivyojaa ilibidi ahutubie wananchi kwanza kabla ya kuonana na Balozi wa nyumba kumi.
  Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa KImataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Mchoteka wilayani Tunduru.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Mchoteka waliojitokeza kwa wingi kuja kuwapokea viongozi wao wa kitaifa.
  Babu Akuilaya (Babu Mkuu) kama heshima aliyopewa na Machifu wa Mchoteka,Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na wananchi wa kijiji cha Mchoteka na kuwashukuru kwa heshima waliyompa.
  Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi kwa wanachama wapya wa CCM ambapo zaidi ya wanachama 100 wamejiunga na CCM katika kata ya Mchoteka.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata mapokezi mazuri wakati akiwasili katika kata ya Nalasi,kijiji cha Nalasi wilaya ya Tunduru.
  Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiimba na akina mama wakazi wa kata ya Nalasi waliojitokeza kwa wingi kuupokea ugeni .
  Umati wa wakazi wa Kijiji cha Nalasi ukiwa umejaa kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara katika mkoa wa Ruvuma.


   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kataNalasi ,wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma ambao walijitokeza kwa wingi kumsikiliza .
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Mkina kijiji cha Mkina ,wilaya ya Tunduru mkoa wa Ruvuma.
   Baadhi ya wananchi wakisikiliza hotuba za viongozi wao wa CCM Taifa wakiwa juu ya miti.
  Sehemu ya wakazi wa kata ya Mkina wakisikiliza hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya mikoa ya Ruvuma na Mbeya.Wananchi hao wamemueleza Katibu Mkuu wa CCM kuwa hawapo tayari kuuza korosho kwa mkopo,pia hawapo tayari kupangiwa bei na wanunuzi, wananchi hao waliitupia lawama bodi ya korosho pamoja na vyama vya ushirikia kwani vimeonekana havina msaada kwa wakulima.

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mkina wilayani Tunduru mkoani Ruvuma ,Katibu Mkuu aliahidi kushirikiana nao katika kuhakikisha tatizo la zao la Korosho linapatiwa ufumbuzi kwani ni zao pekee linaloweza kuinua uchumi wa eneo hilo.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha moja ya leseni za dereva wa Boda Boda ambazo zilitolewa baada ya madereva hao kupata mafunzo ya kuendesha ya usalama barabarani yaliosimamiwa na mbunge wa Tunduru Kusini Mtutura Abdallah Mtutura.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa kata ya Mbesa ,kijiji cha Mbesa wilayani Tunduru ,Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya mkoa wa Ruvuma ambayo ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
  Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye akitoa ufafanuzi kwa wananchi wa kata ya Mbesa, kijiji cha Mbesa juu ya mpango wa serikali katika kuhakikisha wananchi hao wanapata maji,Kushoto Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma kitabu kinachoonyesha Mbesa ipo kwenye mpango wa kupata maji.

older | 1 | .... | 167 | 168 | (Page 169) | 170 | 171 | .... | 1896 | newer