Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 170 | 171 | (Page 172) | 173 | 174 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwafokea wafanyakazi wawili wa kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China baada ya kufumwa na msafara wake wakiiba mafuta ya Diesel kwenye tanki la lori la la kumwagilia maji (Boza) la kampuni hiyo tarehe 19 Novemba 2013 Katika kijiji cha Ntendo Manispaa ya Sumbawanga. Mkuu huyo wa Mkoa alikemea tabia hiyo ya wafanyakazi wezi na kusema umekua ni ugonjwa wa mda mrefu unaozorotesha kukamilika kwa ujenzi wa barabara za lami zinazoendelea kujengwa Mkoani Rukwa.

  Wafanyakazi hao waliokamatwa ni dereva William Ebron (kulia pichani)
  na kibarua Isaya Godwin  ambao walifumwa majira ya saa nne asubuhi wakinyonya mafuta kwenye tanki la Lori hilo lenye namba za usajili T-518 BDV mali ya kampuni hiyo kwa kutumia mpira wa kupitishia maji na kumuwekea mteja kwenye dumu la lita tano, hata hivyo mteja huyo alifanikiwa kukimbia. Baada ya kuhojiwa walidai kuwa mteja wao huyo angelipia lita hizo tano kwa Tsh. 3500/= bei ambayo kihalali haiwezi kununua japo lita mbili za mafuta hayo katika soko. 
   Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ulikua ukielekea katika kata ya Mtowisa kwa ajili ya shughuli za kuhamasisha maendeleo ambapo ulikumbana na mkasa huo njiani katika Kijiji cha Ntendo. Barabara ya Sumbawanga - Namayere inajenga kwa kiwango cha lami na mkandarasi Jiangxi Geo-Engineering (Group) Corporation kutoka China chini ya Mhandisi Mshauri Nicholas O’Dwyer and Company Limited kutoka Ireland akishirikiana na Apex Engineering Ltd. kutoka Tanzania kwa gharama ya Sh. bilioni 78.8 ambazo ni fedha za ndani.
  Watuhumiwa William Ebron (kulia) na kibarua Isaya Godwin (kushoto) muda mfupi baada ya fumanizi wakiwa hawana cha kujitetea.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwakabidhi wezi hao kwa vyombo vya usalama ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
  Watuhumiwa wakiwa mikononi mwa Polisi.
  Mashuhuda wa tukio hilo.
  Baada ya kuanza ziara yake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akimuapisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Adam Misana (wapili kulia) na baadhi ya watendaji wa Kata ya Mtowisa na Kijiji cha Muze juu ya utekelezaji wa maazimio na makubaliano waliowekeana. Maazimio hayo ni pamoja na kutenga maeneo maalum kwa ajili ya shuguli za maendeleo ya vijana, kutenga maeneo maalum kwa ajili ya wakulima na wafugaji katika kila kijiji kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji, kuwekeana utaratibu maalum wa idadi ya mifugo inayotakiwa kufugwa kulingana na ukubwa wa maeneo husika, uhifadhi wa mazingira hususani ujenzi wa vyoo kuepukana na maradhi ya milipuko pamoja na maagizo mengine mbalimbali yaliyotolewa na Mkuu huyo wa Mkoa. 
  Katika ziara yake hiyo alifanya mikutano minne ikiwepo miwili ya nje na miwili ya ndani ambapo maagizo mbalimbali kwa ngazi ya Wilaya, Halmashauri na vijiji yalitolewa kwa watendaji husika.
  (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili jijini Warsaw, Poland, kuhudhuria mkutano wa Nchi wanachama wa Mkataba wa Kyoto kuhusu mabadiliko ya Tabia Nchi unaoanza leo Jumanne Novemba 19, 2013. PICHA NA IKULU.


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa sita mstari wa tatu nyuma) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika wakati alipohudhuria katika Mkutano wa mkuu wa tatu wa nchi za Kiarabu, 'Afro Arab' uliofanyika leo Nov 19, 2013 nchini Kuwait.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihudhuria mkutano mkuu wa tatu wa nchi za Kiarabu, 'Afro Arab' uliofanyika leo Nov 19, 2013, nchini Kuwait.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika, wakati wakiwasili kwenye ukumbi wa Mkutano wa Tatu wa nchi za Kiarabu 'Afro Arab', uliofanyika nchini Kuwait, leo Nov 19, 2013. Picha na OMR.

  0 0

  Askofu Damian Dallu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Geita akiongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba marehemu Dkt. Sengondo Mvungi katika makaburi ya familia kijijini Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Jumatatu, Novemba 18, 2013.
  Mke wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba marehemu Dkt. Sengondo Mvungi, Bi. Anna Mvungi akiweka shada la maua katika kaburi la mume wake wakati wa mazishi kijijini Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Jumatatu, Novemba 18, 2013.
  Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi wakati wa mazishi kijijini Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro JUmatatu, Novemba 18, 2013.


  Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi likishushwa kaburini wakati wa mazishi yaliyofanyika kijijini Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro JUmatatu, Novemba 18, 2013.
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda, mkewe Mama Tunu, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba na viongozi wengine wakifuatilia ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi. Mazishi hayo yalifanyika kijijini Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro JUmatatu, Novemba 18, 2013.
  Familia ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi ikifuatilia ibada ya mazishi iliyofanyika katika kijijini cha Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro Jumatatu, Novemba 18, 2013.
  Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha Josephat Lobullu (kulia) na Askofu wa Jimbo la Same Rogath Kimaryo wakiongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi. Ibada hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chanjale wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro na kuhudhuriwa pia na Askofu Damian Dallu (katikati) wa Jimbo la Geita JUmatatu, Novemba 18, 2013.

  0 0

  093

  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Nchini (CTI) Bi Christine Kilindu (Mwisho Kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya viwanda nchini na mchango wa sekta hiyo katika kupambana na tatizo la ajira katika kilele cha Siku ya Viwanda Afrika, (Kati Kati) ni Kaimu Katibu Mkuu Odilo Otieno (Kushoto) Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) Emmanuel Kalenzi .

  .Kesho ni kilele cha Siku ya Viwanda Afrika wananchi waombwa kujitokeza kwa wingi .Tanzania yapiga hatua viwanda 700 vyaanzishwa ndani ya miaka mitano .UNIDO yaifagilia serikali ya JK kwenye kuhamasisha uwekezaji kwenye sekta ya viwanda .Ujasiriamali kufundishwa kuanzia mashuleni


  Na Damas Makangale, Moblog
  MKURUGENZI Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Nchini (CTI) Bi Christine Kilindu amesema moja ya vikwazo katika ukuaji wa sekta ya viwanda na biashara ni uwepo wa wadhibiti wengi (Regulators) na tozo ya ushuru wa asilimia 0.2 ni kizingiti kwa maendeleo ya viwanda Tanzania. Moblog inaripoti.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha siku ya Viwanda Afrika ukumbi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, amesema moja ya mambo ambayo yanawakwaza wawekezaji na wafanyabiashara ni uwepo wa wadhibiti wengi katika sekta ya viwanda.
  “Sisi hatujakataa kudhibitiwa ila tulikwenda kumuona Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu na tulimweleza juu ya matatizo ya kuwa na wadhibiti wengi na kila mtu ana taka asilimia zake (percent) hiki ni kikwazo katika ukuaji wa sekta ya viwanda hapa nchini,” amesema Bi Kilindu
  Amesema kwamba pamoja na hayo lakini kwa siku za hivi karibuni hali ya kutegemaa kwa nishati ya umeme kumefanya sekta ya viwanda kupiga hatua kubwa kwani kwa sasa wanachangia asilimia 10 ya ajira na asilimia 20 ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi.
  Kilindu amesema shirikisho la viwanda linaunga mkono kwa dhati kabisa dhana ya ujasiriamali katika kusukuma gurudumu la maendeleo pamoja na kuanza kufundisha elimu ya ujasiriamali mashuleni kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari.
  102
  Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda toka Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko Bi Elli Pallangyo akizungumzia ukuaji wa viwanda kwa miaka ya hivi karibuni ambapo amesema jumla ya viwanda 700 vimeanzishwa nchini.

  “Tunataka elimu ya ujasiriamali katika shule za msingi na sekondari ili vijana wetu waanze kufundishwa kuhusu ujasiriamali na waondokane na dhana ya kuajiriwa na waweze kujiajiri,” aliongeza.Naye Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) Emmanuel Kalenzi amesema katika siku ya Viwanda Afrika ni muhimu kwa nchi na wadau wote wa maendeleo duniani ksuhirikiana katika kukuza hali ya ujasiriamali miongoni mwa jamii.

  Amesema kuwa sekta ya viwanda ni mhimili mkubwa katika kutokomeza tatizo la ajira kwa vijana kupambana na umaskini na ni chachu ya ukuaji wa uchumi na pato la taifa. Kalenzi alilisitiza kuwa shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda limejikita katika kufanya utafiti na kuhamasisha uwekezaji wenye tija kwenye sekta ya viwanda lakini viwanda vyenye kutoa ajira rasmi na inayoheshimika.

  “Ongezeko la watu wasio kuwa na ajira Afrika ni ushahidi tosha kwamba bara la Afrika linatakiwa kujikita zaidi katika kuanzisha viwanda vipya na vinavyotoa ajira kwa sababu asilimia 63 ya watu walioajira Afrika wako katika ajira hatarishi,” amesema Kalenzi.

  Kwa Upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko Odilo Majengo amesema kwamba viwanda vya uzalishaji ambavyo vipo nchini Tanzania vinaweza kuinua uchumi wa taifa na kukuza pato la nchi.
  “Kesho ni kilele cha siku ya viwanda Afrika na ni muhimu kwa watanzania wote kushiriki katika maonyesho hayo yanayoendelea katika viwanja vya saba saba ukumbi wa PTA kwani wafanyabiashara wengi wataonyesha bidhaa zao,” amesema Majengo
  104
  Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko Odilo Majengo akisisitiza jambo katika siku ya Viwanda Afrika ambayo kilele chake ni kesho hapa nchini. Kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) Emmanuel Kalenzi na Mwisho Kulia Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Nchini Bi Christine Kilindu.
  Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda toka Wizarani, Bi Elli Pallangyo amesema kwa kipindi cha miaka mitano mpaka sasa taifa limeweza kupata viwanda vipya 700 na pato la taifa kupitia vianda kufikia asilimia 9.
  Bi Pallangyo aliongeza sekta ya viwanda kwa miaka hivi karibuni imepiga hatua kubwa za kimaendeleo na kuchangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa na mauzo nje ya nchi.
  Wakati huo huo pamoja na serikali kutamba kwa uanzishwaji wa viwanda vipya lakini Kuna baadhi ya viwanda vilivyokuwa vikifanya kazi miaka ya nyuma hasa katika serikali ya awamu ya kwanza na ya pili, lakini sasa havipo tena baada ya watu waliokabidhiwa kushindwa kuviendeleza.
  Baadhi ya viwanda hivyo ni kama kiwanda cha nguo cha Urafiki Garments kilichopo ubungo, Tanzania Dairies limited ambacho kilikuwa cha maziwa, Ubungo Spining mill, pamoja na cha Zana za kilimo (UFI) ambacho kilikuwa maalum kwa ajili ya kutengeneza zana za kilimo. Vingine ni Tanzania Sewing Thread na Poly Sacks. Viwanda hivyo hivi sasa havifanyi kazi.
  Viwanda hivyo vilikuwa vinafanya kazi katika awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere, lakini sasa vimekufa kutokana na uzembe na kuridisha nyuma sekta ya viwanda nchini.
  Hivi Karibuni, Waziri wa Viwanda na Biashara Dk Abdallah Kigoda, alitoa ripoti inayoonyesha jinsi hali ya viwanda ilivyo barani Afrika.
  Ripoti hiyo ilijikita zaidi kwa nchi ya Tanzania ikionyesha jinsi viwanda vyake vilivyodorora.
  Kigoda anaelezea kwamba ripoti hiyo imejikita zaidi kutatua matatizo mbalimbali ambayo yameikumba sekta ya viwanda.Anasema wanajipanga jinsi ya kutatua matatizo yaliopo kwenye sekta hiyo ili kufufua viwanda na kuleta maendeleo nchini.
  Dk Kigoda anasema Serkali itaweka mazingira bora kwa ajili ya kuvutia wawekezaji, kuboresha na kulegeza masharti kwa wawekezaji, kuboresha miundo mbinu, na kupambana pamoja na urasimu.
  120
  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) Bw. Emmanuel kalenzi akihojiwa na mwandishi wa MOblog.
  “Ripoti hii imejikita zaidi jinsi ya kutatua matatizo mbalimbali zinazoikumba sekta ya viwanda nchini, naamini kwa kufanya hivi sekta ya viwanda itainuka upya,” anasema Kigoda.
  Dk Kigoda:Tufufue viwanda vyetu
  Kutokana na hali hiyo Serikali na sekta binafsi zinatakiwa kuungana ili kufufua uchumi kupitia viwanda na siyo kutegemea kilimo tu kama uti wa mgongo wa taifa.
  “Mageuzi ya fikra zetu yanahitajika kuitazama upya sekta ya viwanda na kuacha kusema kwamba kilimo pekee ndio uti wa mgongo wa taifa letu kwani hata nchi zilizoendelea zinathamini viwanda pia,” anasema Kigoda.
  Waziri huyo anafafanua kwamba vitendo vinahitajika zaidi kufufua sekta ya viwanda.
  “Lazima tuondokane na nadharia na kujikita kwenye vitendo ili Wizara ya Viwanda na biashara ipanue soko la ndani na nje, lakini hili litafanikiwa baada serikali na sekta binafsi kuungana pamoja,”amesema Kigoda.
  Anabainisha kwamba tatizo kubwa linaloikumba sekta ya viwanda nchini ni ukosefu wa mitaji na tatizo la kupatikana kwa soko la uhakika la kuuza bidhaa za viwandani.
  Anafafanua kwamba matatizo hayo yanasababisha kudorora kwa biashara katika nchi za Afrika.
  “Ukosefu wa mtaji kwa wafanyabiashara ni changamoto kuu inayowafanya washindwe kuwekeza kwenye viwanda, hadi kufikia biashara katika nchi.
  Kutokana na kuwapo kwa tatizo hilo biashara imedorora kwa sababu imekuwa ikifanyika kwa asilimia 10 tu ukulinganisha na nchi nyingine duniani.
  Viwanda vinatumia mitambo duni
  Katika hatua nyingine wizara husika kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO), imeandaa ripoti ambayo imechambuliwa kiundani kuhusu maendeleo ya viwanda Tanzania ili kuonyesha matatizo yanayokabili viwanda nchini.

  0 0  Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Bw. Chaha Nyaikabwe  akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mpango wa Mfuko huo kuanza kukopesha nyumba kwa wanachama wake kwa ajili ya kuboresha huduma zake na kutatua changamoto za makazi kwa wanachama,wakati  wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari( MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Mawasiliano, Masoko na Uenezi Bi. Hawa Kikeke.


  Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa iliyotolewa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Bw. Chaha Nyaikabwe, katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari   (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.  (Picha na Hassan Silayo)  Na Frank Mvungi-Maelezo

  Mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma (PSPF) waanza kukopesha nyumba wanachama wake ikiwa ni moja ya hatua za kuboresha huduma zake kwa wanachama.

  Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi wa uendeshaji na Meneja kumbukumbu wa mfuko wa Resheni kwa watumishi wa umma  Bw. Chacha Nyaikwabe wakati wa mkutano na waandishi wa habari .

  Akifafanua zaidi alisema mfuko huo umejenga nyumba katika mikoa ya Shinyanga nyumba 50,Mtwara nyumba 50 na Morogoro nyumba 25 ambapo lengo la Mfuko huo ni kufika mikoa yoye hapa nchini.

  Aliongeza kuwa nyumba hizo zinakopeshwa kwa wanachama wa mfuko huo ambao wanatakiwa kulipa mkopo wa Nyumba hizo kwa muda wa miezi 300.

  Alibainisha kuwa hata wananchi wasio wanachama wanaweza kununua nyumba hizo ambazo kila moja inagharimu  kuanzia milioni 59 hadi milioni 80 kutegemeana na ukubwa wa nyumba.

  Alitoa  rai kwa wananchi wote kujiunga na mfuko huo bila kujali wako katika sekta rasmi au isiyo rasmi ili waweze kunufaika na mafao mbalimbali yanayotolewa na mfuko huo ikiwemo fao la elimu,Kifo, kujitoa na Ugonjwa.

  Aliongeza kuwa katika kuboresha huduma zake mfuko huo sasa umeanza kusajili wanachama katika mpango wa hiari kwa raia na asiye raia wa Tanzania ambapo mwanachama anaweza kuwasilisha michango yake kwa wiki, mwezi au msimu.


  Katika hatua nyingine Mfuko huo umeanzisha utaratibu unaowawezesha hata wasio wananchi walio nje ya Tanzania kujiunga na mfuko huo ilimradi tu wawe watanzania.

  0 0

  MWIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili Solomon Mukubwa atashiriki Tamasha la Krismasi lililopangwa kufanyika Desemba 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema jana kuwa tayari wamemalizana na Mukubwa, ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya.

  “Pia tumemalizana na mwimbaji wa hapa nchini anaitwa John Lissu ambaye ni mmoja kati ya waimbaji mahiri na wenye mashabiki wengi.

  “Dhamira yetu ni kuwa na wasanii wote wanaokubalika na mashabiki,” alisema Msama na kuongeza kuwa Desemba 26 mwaka huu tamasha hilo litafanyika Uwanja wa Jamhuri Morogoro.

  Mukubwa ametamba na albamu mbalimbali ikiwemo Usikate Tamaa, ambayo ina nyimbo kama Mungu Wangu Nitetee, Niko na Yesu, Mke Si Nguo, Moyo Tukuza Bwana, Chunga Ahadi Yako na Yesu Jina Zuri na Usikatae Tamaa. Pia Mukubwa amewahi kutoa albamu mbili ambazo ni Sijaona Rafiki na Mungu Mwenye Nguvu.

  Sijaona Rafiki Kama Yesu ambayo ni albamu yake ya kwanza ina nyimbo za Uwe Nami Bwana, Sijaona Rafiki Kama Yesu, Nitayainua Macho, Matendo ya Mungu, Bwana Wastahili na Yesu Kimbilio. 

  Wasanii wengine ambao tayari wamethibitisha kushiriki tamasha hilo la nyimbo za kusifu na kuabudu ni Watanzania, Rose Muhando, Upendo Nkone na Upendo Kilahiro wakati wa nje ni Ephraim Sekeleti wa Zambia.

  0 0

  MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa (CCM) Lita Kabati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake mwishoni mwa wiki.(picha na Denis Mlowe).
  ========  ======  =======
  MBUNGE AVITAKA VYOMBO  VYA DOLA KUTENDA HAKI
  Na Denis Mlowe,Iringa
  MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa (CCM) Lita Kabati amevitaka vyombo vya sheria hususan mahakama na Jeshi la Polisi kutenda haki kwa watuhumiwa wanaofika katika idara hizo wanapopatwa na matatizo na kesi mbalimbali.

  Akizungumza na mwandishi wa habari Ofisini kwake Kabati alisema hayo baada ya kutembelea Idara ya Magereza ya Mkoa wa Iringa na kukutana na wafungwa na mahabusu walimpatia kero zao kwa lengo la kuzifikisha katika mamlaka husika.

  Alisema watuhumiwa wengi wamevitupia lawama vyombo hivyo kwa kuwasingizia kesi mbalimbali hususani jeshi la polisi na kwa upande wa mahakama kutoa vifungo ambavyo wengi wao wamembakiwa na jeshi hilo.


  kabati alisema mahakama na jeshi la polisi vinatakiwa kufanya uchunguzi wa kina katika kubaini makosa ya watuhumiwa na kutenda haki kwa kufata sheria za nchi kuliko ilivyo sasa wengi walioko katika kifungo na mahabusu wanalalamika kutondewa haki na kubambikiwa kesi ambazo haziwahusu.

   "Mahakama ni moja ya vyombo vya vinavyotetea haki ya mtuhumiwa hivyo kama mtu ametenda uhalifu kwa namna yoyote lazima uchunguzi wa kina ufanyike kwa lengo la kutenda haki kwa watuhumiwa, wengi wao wametoa malalamiko kuhusu jeshi la polisi na mahakama kuwa rushwa inatawala katika vifungo vyao na wanaomba msaada wa kusaidiwa kutendewa haki" alisema Kabati

  Alisema viongozi wako kwa ajili ya kutetea haki za msingi za mwananchi na rasilimali zake na kumletea maendeleo hivyo mahakama na jeshi la polisi waepuke kuwabambikia kesi wananchi.
  Kabati alisema lazima tuwe wakweli  jeshi la polisi limekuwa likielemewa kwa kiwango kikubwa tuhuma za kuwanyanyasa na kuwakandamiza watuhumiwa kutokana  na malalamiko kutoka kwa wafungwa na mahabusu wenyewe kwa hili linatakiwa kubadilika.

  "Imenisikitisha sana kwa kuwa kuna watu wanajifanya Miungu mtu katika hizi Idara za mahakama, na jeshi la polisi kuweza kuwabambikia kesi watu hivyo kusababisha mrundikano mkubwa wa kesi mahakamani na kujaza watu katika magereza zetu, mie naomba kabisa wazifatilie na hili jambo sitalifumbua macho kuanzia sasa na nitalivalia njuga na nitahakikisha kwamba katika ubunge wangu nilionao hizi changamoto zinatatuliwa kwa wakati" alisema Kabati.

  alisema atapigia haki ya wananchi wa Iringa kutoendelea kunyanyasika na vyombo hivi vya dola  kwa kupakaziwa kesi ambazo haziwahusu na kila mwananchi ana haki ya kutendewa yaliyo mazuri kwa kufuata sheria za nchi.

  0 0


  Katika hali ya kuonyesha kwamba wafanyabiashara wa eneo la kariakoo hawataki wala kusikia kuhusu mashine za T.R.A,Wafanyabiashara hao wameamua kufunga mabango katikati ya mitaa yakiwa na ujumbe wa kupinga matumizi ya mashine hizo.

  Leo ni siku ya pili kwa wafanyabiashara hao kugoma kufanya biashara,Swali la msingi je Serikali inaonaje hali hii ya wanainchi kukosa huduma?na pia huu ni mkoa wa nne sasa baada ya Mbeya,Morogoro na Mtwara.PICHA NA DJ SEK

  0 0

  Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil Colaso akielezea jinsi Airtel inavyowathamini wateja wake kwa kuwawezesha kushinda tiketi za kuweza kujionea mechi mojawapo ya Timu ya Manchester United.
   Baadhi ya wadau mbalimbali wakifuatilia kwa umakini uzinduzi wa promosheni hiyo mpya ya ‘MIMI NI BINGWA’ uliofanywa na Airtel Tanzania kwa ushirikiano na klabu ya Manchester United.
   Meneja Uhusiano wa Timu ya Manchester United, Bw. Michael Higham akielezea faida za muungano kati ya Airtel Tanania na  Manchester kuwa utaongeza hata idadi ya mashabiki wa klabu hiyo kwa Watanzania.
   Mkurugenzi wa Kitengo cha Masoko kutoka Airtel Tanzania, Bw. Levi Nyakundi (kushoto) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Kitengo cha Masuala ya Fedha Airtel Tanzania, Bw. Kalpesh Mehta wakifuatilia kwa umakini kabisa uzinduzi wa promosheni hiyo mpya.
   Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde ambaye alikuwa ni mshehereshaji wa uzinduzi wa promosheni ya ‘MIMI NI BINGWA’ akizungumzia promosheni mpya ya Airtel iliyozinduliwa jana katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam. Kutoka kulia ni Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo,  Bw. Leornad Thadeo, Mkurugenzi wa Airtel Tanzania  Sunil Colaso pamoja na Meneja Uhusiano wa Timu ya Manchester United, Bw. Michael Higham. 
   Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil Colaso akimkabidhi jezi ya Timu ya Manchester UnitedMkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bwana Leornad Thadeo jezi mpya ya  Manchester United. 
   Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil Colaso akimkabidhi jezi ya Timu ya Manchester United, raisi mpya wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania Bw. Jamal Malinzi. 
   Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akimkabidhi jezi ya Timu ya Manchester United mtangazaji wa Clouds FM, Bw. Ephraim Kibonde ambaye alichukua kwa niaba ya wapenzi wa mpira.
  Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil Colaso (wa pili kutoka kushoto) akiwa pamoja na Meneja Uhusiano wa Timu ya Manchester United, Bw. Michael Higham  (wa kwanza kushoto). Kutoka kulia niMkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Bw.  Leornad Thadeo, Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na  Mtangazaji wa Clouds FM, Bw. Ephraim Kibonde muda mfupi baada ya uzinduzi wa promosheni ya ‘MIMI NI BINGWA’ iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam.

  ===========  =========  ==========
  Wateja wa Airtel 10 kila mwezi kushinda tiketi za kwenda Old Trafford kushuhudia mechi LIVE
  Dar es Salaam. KAMPUNI ya mawasiliano ya Airtel Tanzania imetangaza ushirikiano na klabu nguli ya mpira wa miguu ya Manchester United ya nchini Uingereza utakaowezesha wateja wa kampuni Airtel 10 kila mwezi kujishindia safari za kwenda kushuhudia mechi za klabu hiyo moja kwa moja (live) katika uwanja wa Old Trafford. ‘Mimi Ni Bingwa’ inalenga kuwazawadia wateja zawadi zenye thamani za zaidi ya shilingi milioni 500.

  Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa promosheni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso alisema ubia huo mpya unadhihirisha nia ya kampuni ya kufurahisha na kutosheleza mahitaji ya wateja wake.

  “Kampuni ya Airtel Tanzania tunaingia ubia mpya na klabu ya Manchester United ambao utawapa na nafasi wateja wetu wote na wapenzi wa Mpira fursa za kuangalia mechi za timu ya Manchester United live katika uwanja wa Old Trafford.

  “ Natoa wito kwa wateja wetu kuchangamkia fursa hii na kushiriki kikamilifu ili kujishindia zawadi mbali mbali za kila siku, kila wiki na zawadi nono ya shilingi milioni 50 itakayotolewa mwishoni mwa promosheni hii,” aliongeza.

  Aidha Colaso alisema kuwa kampuni yake imekuwa chachu ya maendeleo ya michezo mbali mbali ikiwemo mpira wa miguu kupitia mkakati madhubutu wa kuendeleza mpira wa miguu maarufu kama Airtel Rising Stars.

  “Tunajivunia kuwa mpango wetu wa Airtel Rising Stars imeanza kuvumbua vipaji nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla. Pia tunajivunia kuwa Tanzania imefanya vizuri katika mashindano ya Airtel Rising Stars ya Afrika ya vijana chini ya miaka 17 yaliyofanyika nchini Nigeria miezi michache iliyopita,” aliongeza.

  Naye, Meneja Mahusiano wa Klabu ya Manchester United Michael Higham wakati wa hafla hiyo alisema ubia wa klabu yake na kampuni ya Airtel ya Tanzania umelenga kuongeza uwakilishi wa klabu hiyo nchini Tanzania.

   “Tunafaraja kupata ubia huu mpya na tuna matumaini kuwa hii itakuwa fursa nzuri ya kuwapatia na kujionea mechi kali moja kwa moja. Bila shaka, tunategemea kuwa ushirikiano huu utatusaidia kuongeza mashabiki hapa Tanzania,” alisema Higham.

  Aidha, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Leonard Tadeo wakati wa hafla hiyo aliipongeza kampuni ya Airtel kwa kuendelea kusaidia maendeleo ya sekta ya michezo nchini.

   “Nachukua nafasi hii kuishukuru kampuni ya Airtel Tanzania kwa jitihada zake za kuendelea kusaidia maendeleo ya michezo nchini hususani Airtel Rising Stars ambayo imeibua vipaji kama Serengeti Boys na Timu ya Tanzanite kwa wasichana ambao wamekuwa wakiiwakilisha nchi vizuri katika michezo ya kimataifa,” alisema Tadeo.

  Wakati huo huo, Rais wa Shiriko la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi wakati wa tukio hilo naye aliishukuru Airtel kwa uhusiano wake wa muda mrefu na shirikisho na kuyaasa makampuni mengine kusaidia maendeleo ya michezo nchini.
  “Kampuni ya Airtel Tanzania imekuwa ni chombo muhimu katika maendeleo ya michezo ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu kupitia mpango wake wa Airtel Rising Stars ambao umetuletea heshima kubwa kimataifa miezi michache iliyopita.

  “TFF itaendelea kufanyakazi kwa ukaribu na wadau mbali mbali ili kuhakikisha tunaupeleka mchezo wa mpira wa miguu nchini katika ngazi ya juu zaidi,” alisema.
  Zawadi za thamani ya zaidi ya milioni 500 zitashindaniwa katika promosheni ya ‘Mimi ni Bingwa’ na Airtel Tanzania.

  Washindi katika promosheni hiyo watajishindia jezi halisi za timu ya Manchester United, fedha taslim kila siku na kila wiki na zawadi kubwa ya shilingi milioni 50 mwishoni mwa promosheni.

  Ili kushiriki  kwenye promosheni ya Airtel MIMI NI BINGWA mteja anatakiwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) ukiwa na neno “BINGWA”  kwenda namba 15656 .

  0 0


  The Leed Central Seventh-day Adventist church is organising a Special Day of Prayer for the Philippines at 169 Meanwood Road, Leeds LS7 1JW, on the 23rd of November 2013 to remember Philippines and all those who were affected by the Typhoon Haiyan.

  A special collection will be made for ADRA, a charity working in the Philippines at the moment.  The service will begin at 11am-1pm, which will be followed by fellowship meal in the church hall.

  We would like to extend this invitation to you and request that if possible, we could have your presence at the occasion. 

  Please pass the message along and if you can't make it, then join us in prayer on the day wherever you are.

  Regards,

  Pastor Ikwisa Mwasumbi.

  0 0  HAYA SASA KAMA KAWAIDA YAO, AK CLASSIC COSMETICS WAMEWASHUSHIA MZIGO WA VITU VYA TOFAUTI KABISA!!  KUANZIA PRODUCTs ZA KUPUNGUA,TIBA ZA CHUNUSI,PRODUCTs ZA KUNG'ARISHA NGOZI YAKO,DAWA ZA KUONDOA STRETCH MARKS, ...NA  KUNA MADINI MENGINE LUKUKI MAPYAAAAAA!!EM TUONGOZANE HAPA.. MADUKA YAPO KINONDONI KWA MANYANYA NA SINZA KUMEKUCHA!!

   KWA MAELEZO NA PICHA ZAIDI WATEMBELEE www.akclassic.blogspot.com
   KUWEKA ODA NA KUFIKISHIWA BIDHAA MPAKA ULIPO PIGA  0753-482909/0713-468393
  0 0

  Karibu katika mahojiano kamili na Dr Donald Thomas.
  Mhandisi na mwanaanga wa Marekani
   Katika mahojiano haya, Dr Thomas anaeleza historia yake na namna ambavyo ALIHANGAIKA NA KUVUMILIA kabla hajapata nafasi ya kufanya kile alichokuwa akikipenda zaidi. Ilimchukua miaka 9 tangu ajaribu kwa mara ya kwanza mpaka achaguliwe, na katika miaka hiyo, alituma maombi mara nne.

  Ili kuongeza nafasi yake kufanikiwa akaamua kuchukua madarasa ya urubani, scuba diving, kufundisha, kuongeza elimu na mengine ili kufanikisha kile alichotaka kufanya japo hakukuwa na uhakika wa hilo.
  Lakini aliamini katika atendalo.

  Pia ameeleza maandalizi wanayofanya na mafunzo wanayopitia kuanzia wanapochaguliwa mpaka wanapoenda kwenye mission hizo, hisia na uoga wake siku ya kwanza alipanda space shuttle. Amezungumzia safari nzima na shughuli kuanzia wanavyoondoka mpaka wanavyofika angani pamoja na changamoto za kuishi kwenye orbit. Kuanzia kupika mpaka kutumia choo. Na pia, namna alivyopokea taarifa za kulipuka kwa space shuttle Columbia. Shuttle aliyoitumia mara tatu kati ya nne alizokwenda kwenye orbit.

  Baada ya miaka 20 aliyofanya kazi kama mwanasayansi wa NASA, na safari nne kwenye Orbit, akastaafu na sasa ni Mkurugenzi wa Willard Hackerman Academy katika chuo kikuu cha Towson hapa Maryland ambapo anahimiza wanafunzi wa chekechea kujiunga na masomo ya Sayansi na Hesabu kwa manufaa ya kizazi kijacho
  Nilipata fursa ya kuhojiana naye mwaka 2011


  Kwa maoni, ushauri, nk usisite kutuandikia jamiiproduction@gmail.com

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Ndugu Jestina Mhagama mara baada ya kuwasili katika eneo la Seminari Kuu wilaya ya Peramiho.
   Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akisalimiana na Mbunge wa Peramiho Ndugu Jenista Mhagama .
   Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye mavazi ya jadi yajulikanayo kama Mgolole na kukabidhiwa silaha za jadi alipowasili katika kijiji cha Peramiho B.
   Wanachama wa shina namba 28 wakishangilia hotuba ya  Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara ya kukagua uhai wa chama katika Mkoa wa Ruvuma.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akinywa chai nyumbani kwa Balozi wa Nyumba 10 Issa Said,Katibu Mkuu amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha mabalozi wa nyumba 10 wanatembelewa na viongozi wa ngazi zote.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi na wananchi wa Peramiho wakishiriki kubeba matofali ya ujenzi wa Zahanati ya Kahegwa,Kinana aliahidi kutoa mifuko ya sementi 100 pamoja na bati 100 kukamilisha suala la ujenzi wa zahanati hiyo inayojengwa kwa nguvu za wananchi.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya Kahegwa baada ya kushiriki shughuli za kubeba matofali kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya Kahegwa,Katibu Mkuu aliwaeleza wananchi hao kuimarisha moyo wa kujitegemea  kwani maendeleo ya Tanzania yataletwa na Watanzania wenyewe na si wahisani.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akizungumza na mmoja wa wananchi aliyefarijika sana kwa kumsikia Katibu Mkuu akizungumza maneno ya msingi na yenye kutia moyo sana hasa katika suala la kujitegemea.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti kwenye zahanati ya Lusonga ambayo kwa asilimia kubwa imejengwa kwa nguvu za wananchi.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,akiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Ndugu Jenista Muhagama ,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho na wakikata utepe wa kufungua jengo la Zahanati ya   Lusonga.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisiliza taarifa ya kikundi cha akina mama wajasiriamali  watengeneza sabuni ambayo ilisomwa na Fransisca Andrea.
   Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi la jengo la  Ofisi ya tawi la Mlandizi, Peramiho wilaya ya  Songea vijijini.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Peramiho ,wilaya ya Songea Vijijini  mkoani Ruvuma.
   Mbunge wa Jimbo la Peramiho  Ndugu Jestina Muhagama akihtubia wakazi wa Peramiho na kuzungumzia matatizo sugu yanayo wasunbua wananchi wa jimbo lake, hasa ukosefu wa Pembejeo na kutolipwa pesa wanayoidai serikali kwa wakati.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Peramiho ambapo aliwapongeza kwa kuwa wakulima wazuri wenye kujituma kwa bidii katika suala zima la kilimo.

   Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Tarafa Ndugu Salima Mapunda baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara.
   Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya kufungua jengo la CCM Tawi la Masangu.
   Katibu Mkuu wa CCm Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na masista  kutoka kanisa katoliki la Chikole,jimbo la Peramiho.

  0 0

   Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akizindua rasmi mradi wa umeme wa Berega.Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo amezindua mradi mkubwa wa umeme uliopo katika kata Barega iliyopo katika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro. Aidha alitembelea miradi mingine inayotekelezwa na MCC na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wananchi. Pia alitembelea nyumba ambayo amewahi kuishi mwaka 1979 wakati akifanya utafiti wa miamba huko Kibaoni katika wilaya ya Mvomero ikiwa ni pamoja na kuonana na mwenyeji wake ambaye wameishi katika nyumba moja mwaka 1979-
   Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa umeme wa Berega. Mradi huu umefadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
   Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Elias Tarimo akisoma  taarifa ya hali ya umeme katika wilaya ya Kilosa kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo. 
  Mtaalam kutoka Shirika la Umeme Nchini Mhandisi Lawrance Maro akimpa maelezo Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo juu ya mradi wa umeme unaopeleka umeme katika kijiji cha Bunduki kilichopo katika wilaya ya Mvomero huko Morogoro.
   Wakazi wa kata ya Berega iliyopo katika wilaya ya Kilosa wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo ( hayupo pichani)
   Kikundi cha ngoma za asili  kutoka katika kata ya Berega kikitumbuiza kwenye uzinduzi wa mradi huo.
   Waziri wa Nishati na Madini  Prof. Sospeter Muhongo akiwa ameketi mbele ya nyumba aliyowahi kuishi  mwaka 1979 wakati akifanya utafiti na uchoraji wa ramani za miamba.
   Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akimzungumzia rafiki yake Bw. Chrispin Gaudence Mkunde ( wa kwanza kulia kwake mwenye suti nyeusi) ambaye waliwahi kuishi pamoja mwaka 1979 katika kijiji cha Msumba katika kata ya Kibaoni.

  0 0


  0 0


  0 0


  DSC05297
  Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene (kushoto) akiwasili katika Hoteli ya New Palm Tree iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani kufungua mkutano wa nne wa Mtandao wa vyombo vya habari vya Kijamii nchini (COMNETA) akiwa ameongozana na wenyeji wake Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari na mratibu wa miradi ya UNESCO , Yusuph Al-Amin (wa pili kulia), Mwenyekiti wa COMNETA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Redio ya Jamii ya Wilayani Karagwe ya FADECO Bw.Joseph Sekiku (wa pili kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa COMNETA ambaye pia ni Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Telecentre Sengerema FM mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye.

  Na.Mwandishi wetu
  SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni,(UNESCO), limeiomba Serikali kutambua mchango wa redio za jamii katika maendeleo nchini na hivyo kufanya nao kazi kwa karibu.

  Ombi hilo limetolewa jana na Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari na mratibu wa miradi ya UNESCO , Yusuph Al-Amin wakati wa mkutano wa Mtandao wa vyombo vya habari vya Kijamii nchini (Community Media Network of Tanzania – COMNETA)unaofanyika mjini Bagamoyo.

  Akizungumza kwenye mkutano huo, Al-Amin aliwapongeza COMNETA kwa kufanikiwa kuanzisha umoja huo ambao awali kulikuwa na vituo viwili tu vilivyokuwa vikitambuliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), huku kwa sasa vikifikia vituo zaidi ya 27, kwa nchi nzima ikiwemo Tanzania Bara na Visiwani.
  DSC05299
  Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene akibadilishana mawazo na wenyeji wake kabla ya kufungua mkutano wa nne wa COMNETA unaoendelea Bagamoyo mkoa wa Pwani.
  Akifafanua zaidi, Al-Amin alisema UNESCO imekuwa ukiisaidia COMNETA kufikia malengo yake kwa kutambua kuwa radio hizo zinafanya kazi katika jamii na zina uwezo mkubwa wa kuifikia jamii inayoizunguka.
  “Zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania wako vijijini na hawa wanafikiwa kwa karibu zaidi na radio jamii, kwa kupata taarifa za kina na za haraka” alisema Al-Amin.

  Alitoa mfano wa Radio ya jamii iliyoko Micheweni, Pemba ambayo uwepo wake umesaidia sana kuleta mabadiliko ya maendeleo wilayani hapo tofauti na ilivyokuwa huko nyuma ambapo wilaya hiyo likuwa nyuma sana kimaendeleo.

  ‘Vipindi mbalimbali vya kuhamasisha maendeleo vinavyorushwa na redio hii vimesaidia sana kuhamasisha wananchi na sasa mwamko wa maendeleo umekuwa mkubwa hapo Micheweni” alisema, Al-Amin. Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0

  WANARIADHA kutoka nchi 21 wanatarajiwa kushiriki mbio ndefu za Uhuru, Uhuru Marathon, zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Desemba 8, mwaka huu.

  Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, Katibu wa Kamati ya Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema, kujitokeza kwa wanariadha kutoka mataifa mbalimbali kumeongeza hamasa kubwa ya mbio hizo.

  Melleck alisema, wanariadha kutoka mataifa hayo ndio ambao wamejiandikisha mpaka sasa na wanaamini wengi wataendelea kujitokeza ili kufanikisha lengo lake.

  Alitaja nchi wanazotoka wanariadha waliojiandikisha mpaka sasa ni Tanzania, Uganda, Kenya, Afrika Kusini, Ethiopia, Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Malawi na Marekani.

  Wanariadha wengine wanatoka Ujerumani, Jamaica, Urusi, China, Japan, Venezuela, Comoro, Nigeria, Italia, Canada, Madagascar na Uturuki.

  “Hii ni faraja kubwa kwetu, kwani inaonyesha kwa kiwango kikubwa lengo letu la kupigania amani, umoja na mshikamano miongoni mwetu linakubalika na watu wengi duniani,” alisema.

  Aidha Melleck alise,a usajili bado unaendelea kwa wale wanaotaka kushiriki ambapo fomu zitakazotolewa kwa mshiriki wa kilomita 3 atalipa Sh 100,000 yule wa kilomita 5 Sh 2,000 na washiriki wa kilomita 21 na 42 watalipia Sh 6,000.

  “Tunachukua nafasi hii pia kuziomba kampuni au taasisi mbalimbali zinazotaka kudhamini mbio hizo zijitokeze na kufanya hivyo, kwani nafasi bado ipo na tukumbuke bila amani hakuna chochote kinachoweza kufanyika,” alisema.

  0 0


older | 1 | .... | 170 | 171 | (Page 172) | 173 | 174 | .... | 1897 | newer