Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

China na Tanzania Kushirikiana Katika Mafunzo kwa Wanahabari

$
0
0
Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, CHINA


Kansela wa Idara ya Habari, Wizara ya Mambo ya Nje katika Jamhuri ya Watu wa China, Bw. Gong Anmin amemuahidi Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi kushughulikia suala la mafunzo kwa Wanahabari wa Tanzania kwa lengo la kuwajengea uwezo katika sekta ya mawasiliano.

Bw.Gong ameyasema hayo wakati wa mkutano maalumu baina yake na ujumbe kutoka Tanzania ulioongozwa na Dkt. Abbasi uliolenga kujifunza na kubadilishana uzoefu katika sekta ya habari na mawasiliano na wataalamu wa Serikali ya China. Bw. Gong aliongeza kuwa: "suala la kuongeza uwezo kwa wanahabari ni muhimu kwani itasaidia kuongeza taaluma waliyonayo hivyo nitajitahidi kufanikisha mafunzo kwa wanahabari wa Tanzania ambayo ni nchi rafiki na China kwa miaka mingi"

Mbali na hayo Dkt. Abbasi pia amekutana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje anayeshughulikia Idara ya Masuala ya Afrika Bw. WAN Li. Katika Mazungumzo yao Bw. Wan amesema kuwa urafiki wa Tanzania na China ni wa muda mrefu na ulianzishwa na waasisi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Mwenyekiti Mao Zedong hivyo kuahidi kutunza na kudumisha urafiki huo.

Bw. Wan anaongeza kuwa katika miaka 54 iliyopita uhusiano wa kibalozi baina ya nchi hizo umezidi kuimarishwa ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika. Aidha, Bw. Wan alieleza kufurahishwa na mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii yanayoendelea nchini Tanzania na kusema wanayaunga mkono. Kwa upande wake, Dkt. Abbasi ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa kuzidi kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sekta mbalimbali za maendeleo.

Dkt. Abbasi aliongeza kuwa baada ya mikataba mingi ya ushirikiano kuasisiwa miaka ya nyuma Serikali ya sasa ya Tanzania pia ilisaini mkataba mpya wa ushirikiano katika sekta za utamaduni na habari na Serikali ya China mwaka 2016 unaoshadidisha zaidi urafiki kati ya mataifa hayo mawili. Aidha Dkt. Abbasi amesema kuwa kuna miradi mbalimbali inayoendelea Tanzania ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa nchini Tanzania (SGR) hivyo amewakaribisha wawekezaji kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kuwekeza katika miundombinu ya sekta ya reli lakini pia kuwaalika Wachina kutembelea Tanzania na kufaidika na maeneo mbalimbali ya utalii.

Black Friday 2018: Top Deals We can expect here in Tanzania

$
0
0
The countdown has begun! You know it is near and it can be seen everywhere. The excitement is building, the spirits are rising. Yes, it is time for the biggest shopping event of the year, it is Black Friday 2018. This is a shopping haven for everyone as you can find everything you could possibly need at the lowest possible prices. This year, Black Friday falls on the 23rd of November’.
Why is called Black Friday?

There have been a few theories regarding why this biggest shopping event is termed Black Friday. Given the different theories, we cannot say for sure why. However, we’d share these theories for you to think over. According to an article on Thebalance.com, "It was originally called Black Friday because so many people went out to shop that it caused traffic accidents and sometimes even violence. The Philadelphia Police Department coined the phrase to describe the mayhem surrounding the congestion of pedestrian and auto traffic in the downtown area."

Wonderopolis.org shares a different theory: “Black Friday is the day when retailers finally begin to turn a profit for the year. In accounting terms, operating at a loss (losing money) is called being “in the red" because accountants traditionally used red ink to show negative amounts (losses). Positive amounts (profits) were usually shown in black ink. Thus, being “in the black" is a good thing because it means stores are operating at a profit (making money).”Who is Hosting Black Friday Sales in Tanzania?

On the 16th November 2018, Jumia will be hosting one of the largest Black Friday Sales of all time. This year, for Jumia’s customers it will be Black Fridays as it will be Black Friday every Friday from November 16th to December 7th. The day is fast approaching and many people have already started making a list of what they want to buy on this auspicious occasion. Everyone is looking forward to the huge discounts being offered on almost all products. So grab your own paper and pen and think of all that you have ever wanted to buy as you can’t miss out on this golden opportunity.

During the Black Friday Sale, anything and everything that you could ever imagine buying will be right in front of you at the best prices you can ever think of. Mind-blowing discounts being offered on all items available up to 70% off!. Buyers are in for a treat this year because very high-end brands’ products are on sale. Everything offered will be of excellent quality and very authentic. Make your shopping spree exciting this year because of Black Friday.

Top Deals To Expect This Black Friday 2018

With the exceptional deals and marvellous discounts that come with Black Friday, here is a list of super hot deals we think you should look out for:
Electronics:

If you’ve been thinking of getting world-class electronics for your living room, bedrooms, offices, hotels, and so on. You are just in luck as the best electronics from your favourite brands would be sold at the lowest prices. There are multiple categories to choose from. The most sought-after electronics can be gotten from top brands like LG, Panasonic, Samsung, Sony, and a lot more. You get to shop for the latest range of, LCD televisions, speakers, chargers, home theatres, DVDs, electronics accessories and what not will be at your fingertips.
 
Fashion:

What you wear represents the real image of your whole personality. The imaginative and enduring collection of dresses, pants, shirts, trousers, lingerie and other fashion items would be brought to you on Black Friday to amuse your day. All the clothes and accessories you want will be just a click away. If you are looking to get a footwear to make your day, this could be the right time. Black Friday sale will be covering the ultimate array of splendid footwear that varies in colours, designs, and materials. 
 
Both genders, male and female, would have the elite opportunities to enhance the splendour of their gait and alter the style of their personality. Look amazing while going for that important business meeting with that classy office wears that would be sold during this event. Sunglasses have a way of giving you a totally different look. Eyewear differs in colours and shapes depending on the environment where it is worn. 
 
Are you looking to get a timepiece that will add the glamour trait to your personality and will also act as a bracelet? Black Friday is the right time to get that watch you have always desired at a low cost. The watches will be for both female and male buyers. From water resistance watches, luxury watches, sport watches to mechanical watches, everything will be encompassed in the sale
Games & Gadgets:

During Black Friday, expect lots and lots of amazing discounts on all smartphones, laptops, PlayStation games, cameras, headphones, speakers, Beats by Dre, chargers as well as other accessories. If you are looking to get mobile phones for your family and friends or even for yourself, then you are in luck. Samsung, one of the largest electronics giants in the world has produced quite a number of high-class trending flagship devices. Samsung mobile phones come with the best features and amazing looks that you can think of. Every phone will offer you superior picture quality, long-running battery times, faster processing speeds and so much more. 
 
The newly launched Samsung Galaxy S9, Samsung Galaxy Note 9, Samsung Galaxy S8, Samsung Galaxy Note 8 and a lot more would be sold at ridiculously low prices during Black Friday. Beats Audio products are taking the world by storm. Developed by the rapper and artist, Dr Dre, they are a sensation among the youth especially. Their headphones are known for having a special emphasis on the bass and are the best for playing hip-hop, rap, soul, pop etc. The Beats Pill is one of the most used speakers as they are portable and easy to carry around while they provide the best music quality experience.

Apple, one of the leading multinational mobile phone companies in the world recently launched the iPhone X, iPhone Xs, and iPhone Xmax. The new flagship devices are a combination of sophistication, technology, class, and exquisite designs. These smartphones have unique features that distinguish it from other smartphones. You should look out for these devices as they would be sold at an extremely low cost.

There you have it, Top deals to look out for during Black Friday. So go ahead and shop till you drop folks! Hope you have an amazing shopping experience and get everything that you always wanted.

AWESO AAGIZA WATALAAM WA MAJI NA WAKANDARASI WA MIRADI YA MAJI YA TSAMAS NA DARAKUTA-MINJINGU WAITWE POPOTE WALIPO

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ameelekeza Watalaam wa maji walioshiriki katika kusimamia ujenzi wa miradi ya maji ya Tsamas na mradi wa maji Darakuta-Minjingu pamoja na Wakandarasi waliopewa kandarasi katika miradi hiyo kufika katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Babati bila kukosa asubuhi ya tarehe 23.10.2018.

Mhe. Aweso (Mb) ambaye yuko mkoani Manyara katika ziara ya kikazi ametoa maelekezo hayo baada ya kubaini kasoro katika utekelezaji wa miradi hiyo ambapo pamoja na Serikali kutoa fedha, bado wananchi hawajapata huduma ya majisafi na salama.

Mradi wa maji wa Darakuta-Minjingu ambao hadi sasa umetumia kiasi cha Shilingi Bilioni 1.7 ulisanifiwa mwaka 2009 na ulitakiwa kuhudumia vijiji vya Minjingu, Mwada, Ngoley, Olasiti, Masaini, Maramboi na Eluwai. Aidha, mradi wa maji wa Tsamas mkandarasi amelipwa zaidi ya Shilingi milioni 100, hata hivyo mabomba yaliyotumika katika chanzo cha maji yanapasuka hivyo kusababisha ukosefu wa huduma ya majisafi ya uhakika kwa wananchi.

Naibu Waziri Aweso (Mb), pamoja na hayo,  amepongeza utekeleza wa mradi wa maji wa Haraa unaozalisha lita elfu 21 kwa saa kwa kukamilika vizuri, na kuagiza fedha za mradi ziwekwe benki ili kuwezesha kamati ya watumia maji  kuendesha mradi.

Hadi mwezi Septemba 2018 mkoani Manyara, huduma ya upatikanaji maji vijijini ilikua asilimia 52 na Babati mjini asilimia 75.
 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiongea katika eneo la mradi wa maji wa Bonga, uliopo kata ya Bonga Babati  mkoani Manyara. Mradi huo utakapokamilika utatoa maji lita elfu 40 kwa saa na kufikisha kiwango cha upatikanaji majisafi na salama katika mji wa Babati kuwa asilimia 95. Aidha, vijiji vya jirani navyo vitapata huduma ya majisafi na salama kupitia mradi huo. Waziri Aweso (Mb) amesema wote watakaostahili fidia kupisha mradi Serikali itawalipa.
 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb)-kushoto, akimsikiliza Mbunge wa Babati vijijini Mhe. Jitu Soni –kulia, akimweleza kuhusu hali ya mradi wa maji wa Tsamas. Katikati ni MKuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Elizabeth Kitundu. 
 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb)  aliyenyoosha mkono, akitoa maelekezo kuitwa popote walipo kwa Watalaam wa maji waliosimamia miradi ya maji ya Tsamas na mradi wa maji Darakuta –Minjingu, pamoja na Wakandarasi wa miradi hiyo mara moja.  Miradi hiyo imebainika kuwa na kasoro nyingi za kitalaamu, na haitoi maji ingawa Serikali imewalipa Wakandarasi
 Baadhi ya wanakijiji wa Kijiji cha Tsamas mkoani Manyara wakijadili kuhusu maji  katika kikao kifupi katika shamba la migombawakati wa ziara ya kikazi ya  Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) haonekani pichani.
 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiangalia maji yanayochotwa  katika mto Tsamas kwa matumizi mbalimbali na wananchi. 
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akikagua ubora wa bomba zilizotumika katika mradi wa maji Darakuta-Minjingu. Mradi huo ulisanifiwa mwaka 2009, na umeshatumia kiasi cha shilingi Bilioni 1.7, hatahivyo wananchi bado hawajapata huduma ya majisafi na salama, hivyo wahusika wote, wakiwamo watalaam wa maji na wakandarasi wa mradi wameelekezwa kufika  katika kikao kitakachofanyika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Babati. 

MAWAKALA WA NMB KANDA 7 WANUFAIKA NA MAFUNZO YA KIBENKI KUBORESHA BIASHARA ZAO

$
0
0
BENKI ya NMB imetoa mafunzo ya kibenki kwa mawakala wake kutoka Kanda saba nchini ili kuboresha huduma kwa wateja na kukuza biashara zao. Mafunzo hayo yaliotolewa kwa mawakala wa NMB, ambao wanasaidia kutoa huduma za kibenki kwa wateja, yametolewa kwenye Kanda 7, ambazo ni pamoja Nachingwea, Newala, Tandahimba, Mbeya, Dodoma, Morogoro, Arusha, Tabora na Mwanza.

Benki ya NMB iliamua kuwajengea uwezo mawakala wake ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja pindi wanapowahudumia. Katika mafunzo hayo, mawakala walipata elimu kutoka kwa wataalam wa masuala ya kibenki pamoja na timu ya mtandao wa kanda husika. Miongoni mwa mafunzo hayo ni pamoja na uelewa juu ya huduma na bidhaa mbalimbali za benki,

Pamoja na hayo, NMB ilitoa motisha na kutambua michango ya mawakala waliofanya vizuri katika kutoa huduma hizo. Baadhi walipata zawadi mbalimbali na vyeti maalum kwa wakala aliyefanya vizuri kwa kila Kanda. Ujuzi huo utaendelea kutolewa kwa maeneo yaliosalia. Benki ya NMB kwa sasa ina zaidi ya mawakala 6000 nchi nzima.
Meneja wa NMB kanda ya ziwa - Abraham Augustino, akizungumza na mawakala wa benki hiyo kwenye kongamano la mawakala lililofanyika Jijini Mwanza jana. NMB inaendesha semina ya mawakala zaidi ya 6,000 ili kuwajengea uwezo na kutambua mchango wao katika kutoa huduma za kibenki nchini. 
Mmoja wa wakala akitunukiwa cheti baada ya kufanya vizuri katika biashara yake. 
NMB inaendesha semina ya mawakala zaidi ya 6,000 ili kuwajengea uwezo na kutambua mchango wao katika kutoa huduma za kibenki nchini. Baadhi ya mawakala wakiwa katika kongamano la mafunzo. 
Wakala wa NMB kutoka wilayani Chato Mkoani Geita - Suleiman Rweikondo, akionesha cheti cha mshindi wa wakala bora namba moja kwa kanda ya ziwa wakati wa kongamano la mawakala liliofanyika jijini Mwanza jana.NMB inaendesha semina ya mawakala zaidi ya 6,000 ili kutambua mchango wao katika kutoa huduma za kibenki nchini.

RAIA WA USWISI AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILIONI 34 AMA JELA MIAKA 20

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii

MKURUGENZI wa Fairme NGO, Rene Staheli (62) ambaye pia ni raia wa Uswis leo Oktoba 23, 2018 amehukumiwa kulipa faini ya Sh Sh. Milioni 34 ama kutumikia kifungo cha miaka 20 gerezani baada ya kukiri kosa la kukutwa na vipande vitatu vya meno ya Kiboko.

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile wa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Rwizile amesema mahakama imemtia hatiani mshtakiwa kufuatia yeye mwenyewe kukiri kosa lake.

Kufuatia kukiri kutenda kosa linalokukabiki na kukubali vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapa,mahakama inakutia hatiani na inakuhukumu kulipa faini ya Sh 34,036,188 na iwapo utashindwa basi utatumikia kifungo cha miaka 20 gerezani", amesema Hakimu Rwizile.

Kabla ya hukumu hiyo kutolewa, wakili wa serikali Mwandamizi, Patrick Mwita aliiomba mahakama kutoa adhabu Kali kwa mshtakiwa huyo kwa kukutwa na maliasili yetu ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.Katika utetezi wake, ameiomba mahakama impe adhabu ndogo kwa kuwa hili ni kosa lake la kwanza, haijaisumbua mahakama ndio maana amekiri kosa lake na pia anafamilia kubwa inayomtegemea huko kwao Uswisi. 

Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi, mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa Oktoba 16, mwaka huu katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere alikamatwa akiwa na nyaraka za Serikali ambazo ni vipande vitatu vya meno ya Kiboko vyenye uzito wa kilogeamu tano na thamani ya USD 1,500 ambazo ni sawa na Sh 3, 403, 618.80 Mali ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa wanyama pori.

Hadi MICHUZI BLOG inaondoka katika mahakama ya Kisutu mshtakiwa alishindwa kulipa faini na amepelekwa gerezani.
Mkurugenzi wa Fairme NGO, Rene Staheli (62) ambaye pia ni raia wa Uswis leo Oktoba 23.2018 akitoka katika Mhakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kuhukumiwa kulipa faini ya Sh Sh. Milioni 34 ama kutumikia kifungo cha miaka 20 gerezani baada ya kukiri kosa la kukutwa na vipande vitatu vya meno ya Kiboko.

MATOKEO YA DARASA LA SABA HAYA HAPA

DCP LIBERATUS SABAS AZUNGUMZA NA WANAVIJIJI MKOA WA MTWARA, AKAGUA VIPENYO WANAVYOTUMIA WAHALIFU KUKIMBILIA NCHINI MSUMBIJI.

$
0
0
 Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas akitoa Elimu kwa wanakijiji wa Chikong’o, Wilayani Tandahimba, Mkoa wa Mtwara juu ya kukabiliana na wageni wanaoingia maeneo hayo wakitokea sehemu mbalimbali za Nchi na Nchi jirani ya Msumbiji hiyo itasaidia kupunguza uhalifu katika maeneo na makazi yao.
 Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas akitoa Elimu kwa wanakijiji cha Mkaha Wilaya ya Tandahimba Mkoa wa Mtwara, juu ya kukabiliana na wageni wanaoingia maeneo hayo wakitokea sehemu mbalimbali za Nchi na Nchi jirani ya Msumbiji hiyo itasaidia kupunguza uhalifu katika maeneo na makazi wanayoishi.
Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas akiwa katika kijiji cha Chikong’o wilayani Tandahimba mkoani Mtwara akikagua moja ya vipenyo wanavyotumia wahalifu kuvuka kutoka nchini Tanzania kwenda Nchini Msumbiji moja ya vipenyo hivyo ni Mto Ruvuma. (Picha na Jeshi la Polisi)

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA NNE DKT. KIKWETE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara alipowasili leo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2018.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza  Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 23, 2018.  PICHA NA IKULU


KAMATI ZA BUNGE ZAFANYA VIKAO JIJINI DODOMA

$
0
0
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma leo. Wajumbe hao wakiongoozwa na Mwenyekiti Mhe. Naghenjwa Kaboyoka wamekutana na Mwenyekiti wa Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari  (TPA). 
 Viongozi wa Mamlaka ya Bandari (TPA) wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati Kamati hiyo ilipokutana nao katika kikao kilichofanyika Jijini Dodoma Leo. Wa kwanza ni Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Ndugu Deusdedit Kakoko na Mwenyekiti wa Bodi ya TPA, Profesa Ignas Rubaratuka.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC)  Mhe. Abdallah Chikota akizungumza katika kikao cha Kamati  hiyo kililchofanyika Jijini Dodoma leo ambapo walikutana na Halmashauri ya Kilwa.pembeni ni Katibu wa Kamati Ndugu Victor Mhagama.
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma leo. Wajumbe hao wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mhe. Abdallah Chikota wamekutana na Halamshauri ya Wilaya ya Kilwa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilwa Ndugu Renatus Mchau akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) wakati Halmashauri hiyo ilipokutana na Kamati hiyo katika kikao kilichofanyika leo Jijini Dodoma.

DKT TIZEBA ALITAKA JESHI LA POLISI KUTOA TAARIFA SAHIHI ZA AJALI YA WATUMISHI WATANO ILIYOTOKEA MKOANI SINGIDA

$
0
0
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akiongoza zoezi la kuaga miili ya watumishi watano wa wizara ya kilimo waliofariki kwa ajali ya gari juzi tarehe 21 Octoba 2018 katika kijiji cha Njiri Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida, Wengine pichani ni Waziri wa fedha na Mipango Mhe Philiph Mpango, Naibu Waziri wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa, na Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah Ulega. (Picha Na Mathias Canal, WK)
Sehemu ya waombolezaji walioshiriki kuaga miili ya watumishi watano wa wizara ya kilimo waliofariki kwa ajali ya gari juzi tarehe 21 Octoba 2018 katika kijiji cha Njiri Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza wakati wa kuaga miili ya watumishi watano wa wizara ya kilimo waliofariki kwa ajali ya gari juzi tarehe 21 Octoba 2018 katika kijiji cha Njiri Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akiwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wakati wa kuaga miili ya watumishi watano wa wizara ya kilimo waliofariki kwa ajali ya gari juzi tarehe 21 Octoba 2018 katika kijiji cha Njiri Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Katibu Mkuu wa wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akitoa taarifa za miili ya marehemu wakati wa zoaezi la kuaga miili ya watumishi watano wa wizara ya kilimo waliofariki kwa ajali ya gari juzi tarehe 21 Octoba 2018 katika kijiji cha Njiri Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na rasilimali watu Bi Hilda Kinanga akieleza hatua zilizochukuliwa na wizara ya kilimo tangu kutokea ajali iliyoua watumishi watano wa wizara hiyo katika kijiji cha Njiri Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.

Na Mathias Canal-WK, Dodoma


Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) leo Jumanne tarehe 23 Octoba 2018 ameongoza mamia ya waombolezaji kuaga miili ya watumishi watano wa wizara ya kilimo waliofariki kwa ajali ya gari juzi tarehe 21 Octoba 2018 katika kijiji cha Njiri Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida wakiwa safarini kutokea Jijini Dodoma kuelekea mkoani Shinyanga na Mwanza kikazi.


Ajali hiyo iliyolihusisha Lori la mizigo na gari ya serikali STK 8925 iliyokuwa na watumishi hao watano ambao walikuwa safarini kuungana na Ujumbe wa Benki ya Maendeleo ya afrika (AFDB) kwa maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa kuanzisha viwanda vya kusindika mazao (Stage Agro Processing Zone).


Dkt Tizeba amelitaka jeshi la Polisi Mkoa wa Singida kutoa taarifa zilizo sahihi tofauti na taarifa walizozitoa awali za ajali hiyo kwani zinakinzana na maelezo ya dereva wa Lori ambaye amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni vilevile kukinzana na maelezo yanayotolewa na mashuhuda waliopo katika eneo la ajali hiyo.


“Naomba Kauli iliyotolewa na jeshi la polisi irudiwe tena waende wakafanye utafiti wa kweli kwani kumekuwa na lawama kwa dereva wa serikali ambazo hazistahili maana taarifa zinasema kuwa dereva wa Lori alikuwa anaingia barabarani pasina kufuata taratibu jambo lililopelekea kutokea kwa ajali hiyo”


“Ninaomba sana jeshi la polisi kutenda haki katika tukio hili lenye kuacha maumivu kwa familia, wizara na Taifa zima” Alikaririwa Dkt Tizeba


Waziri Tizeba amewataka wananchi kuacha kulaumu na kutoa hukumu kwa dereva wa serikali kwa kusababisha ajali hiyo badala yake kuwaombea marehemu wapumzike kwa amani kwani hakuna binadamu anayeweza kusababisha ajali na vifo vya watu wengi kwa makusudi.


Watumishi hao walioagwa kwa kupoteza maisha kwa ajali ya gari ni Dereva Mwandamizi wa wizara ya kilimo Ndg Abdallah Seleman Mushumbusi (53), Afisa kilimo wa Wizara Ndg Charles Joseph Somi (33), Mkemia daraja kwanza Ndg Erasto Isack Mhina (43), Mtakwimu daraja la kwanza Bi Ester Tadayo Mutatembwa (36) na Mhasibu daraja la pili Bi Stella Joram Ossano (39).


Aidha, Mhandisi Tizeba ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na watumishi wote wa wizara ya kilimo kwa kupoteza nguvu kazi ya Taifa tena watumishi hao wakiwa safarini kutekeleza majukumu ya kiserikali.


Vilevile amewashukuru wabunge wa kamati ya kudumu ya maji, kilimo na mifugo kwa kuacha kikao kazi ili kuungana na waombolezaji kuaga miili ya watumishi hao.


Viongozi wengine walioshiriki katika zoezi la kuaga miili hiyo ni pamoja na waziri wa fedha na Mipango Mhe Philiph Mpango, Waziri wa Viwanda, Bishara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage, Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah Ulega na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya kilimo Prof Siza Tumbo.


Kwa upande wake katibu Mkuu wa wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe amewataja watumishi hao waliofariki kuwa walikuwa wachapakazi hodari, wapole, wacheshi na waadilifu hivyo kufuatia mauti iliyowakumba Wizara imepata pengo kubwa.


Alisema kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma mwajiri anagharamia misiba hiyo na kuahidi kushirikiana na ndugu wa marehemu kwa ajili ya taratibu nyingine za kupata haki na mafao yao.

WAZIRI MKUU AITAKA SIDO KUBUNI TEKNOLOJIA RAFIKI

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameliagiza Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO)lijielekezekatika kubuni teknolojia na mitambo rafiki inayolenga kutatua changamoto za wajasiriamali kulingana na mazingira yao. 

Amesema Serikali inaendelea kuimarisha shughuli za SIDO lakini bado kuna  changamoto za wajasiriamali wadogo ambazo lazima zishughulikiwe kwa kasi kubwa ili kufungamanisha shughuli za SIDO na uchumi wa Viwanda

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Oktoba 23, 2018) wakati akifungua Maonesho ya SIDO kitaifa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Nyakabindi vilivyoko wilayani Bariadi mkoani Simiyu na kuhudhuriwa na wajasiriamali 500.

Amesema ili kufikia uchumi wa kati inambidi kila Mtanzania mahali alipo afanye kazi kwa bidii, maarifa na ubunifu. “Tusipoteze wakati kwa kufanya mambo yasiyo na tija. Tuzingatie falsafa ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Hapa Kazi Tu.”

“Mfano kwa hapa Bariadi, tunatarajia SIDO watuletee teknolojia na mitambo inayoweza kurahisisha ukamuaji wa mafuta yanayotokana na mbegu za alizeti na pamba, kwa Dodoma taknolojia na mitambo kwa ajili ya kuchakata zabibu.”

“Kigoma pelekeni teknolojia na mitambo kwa ajili ya kuchakata mbegu za michikichi na kwenye maeneo yanayolimwa korosho teknolojia na mitambo  ya kubangua korosho na maeneo kama Ilula ambayo yanazalisha nyanya kwa wingi wapate teknolojia na mitambo ya kusindika na kuhifadhi nyanya na mbogamboga.”
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Maonesho ya Shirika la  Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, Oktoba 23, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Badhi ya wananchi wa  mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kufungua Maonesho ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO)  kwenye uwanja wa Nyakabindi.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) kitanzania ili wakue na kuwa wawekezaji wakubwa. Pia kuwawekea mazingira wezeshi ya kufanya shughuli zao.”
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama chaki zilizotengenezwa wilayani Maswa katika maonesho ya Shirika la Kuhudumia  Viwanda Vidogo (SIDO) kwenye  uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, Oktoba 23, 2018 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea jembe la asili kutoka mhunzi,  Mashaka Daniel wa  Bukoba katika Maonesho ya Shirika la Kuhudumia  Viwanda Vidogo (SIDO)  aliyoyafungua kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, Oktoba 23, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa  Ufundi wa Shirika la Kuhudumia  Viwanda Vidogo (SIDO), Prosper Godfrey (kulia)  kuhusu majiko makubwa yanayotengenezwa na SIDO wakati alipofungua Maonesho ya SIDO kwenye uwanja wa Nyakabindi  mkoani Simiyu Oktoba  23, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simyu, Anthony Mtaka na watatu kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi  Stella Manyanya.

SERIKALI YAAINISHA DAWA MUHIMU ZINAZOPATIKANA MSD

$
0
0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akifafanua hali ya upatikanaji wa dawa nchini kwa wajumbe wa kamati ya Bunge ya Huduma za jamii nchini hawapo pichani wakati wa kikao cha kamati ya hiyo kinachoendelea katika ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , katikati aliyekaa ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akichangia mada wakati wa kikao cha kamati ya Bunge ya Huduma za jamii nchini kinachoendelea katika ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , wa kwanza kulia aliyekaa ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Huduma za jamii nchini na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Bw. Peter Serukamba akitoa mwongozo kwa wajumbe wa kamati ya Bunge ya Huduma za jamii nchini wakati wa kikao cha kamati ya hiyo kinachoendelea katika ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,wa kwanza kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.


Katibu Mkuu Wizara ya afya Dkt. Mpoki Ulisubisya aliyesimama akichangia mada wakati wa kikao cha kamati ya Bunge ya Huduma za jamii nchini kinachoendelea katika ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , waliokaa kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na katikati ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari Kambi aliyesimama akielezea jambo kwa wajumbe wa kamati ya Bunge ya Huduma za jamii wakati wa kikao cha kamati ya hiyo nchini kinachoendelea katika ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .

…..

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa nchini (MSD) Bwa. Laurean Bwanakunu akichangia mada wakati wa kikao cha kamati ya Bunge ya Huduma za jamii nchini kinachoendelea katika ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyekaa kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile. PICHA NA WIZARA YA AFYA.

………………
WAMJW, BUNGENI DODOMA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imeainisha dawa aina 135 kama dawa muhimu na za kipaumbele cha wizara kwa lengo la kuhakikisha kuwa zinapatikana nyakati zote katika bohari zote za kanda za MSD.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Janii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akitoa taarifa ya utendaji ya Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) aliyowasilisha katika kamati ya kudumu ya Bunge huduma na maendeleo ya jamii jijini Dodoma.

Waziri Ummy alisema tathimini ya upatikanaji wa dawa hizo ni wa hadi mwezi Julai 2018 ambapo ni sawa na asilimia 93 hivyo Wizara yake imeitaka MSD kuongeza idadi ya dawa muhimu 177 na kufikia dawa za kipaumbele 312 ambapo upatikanaji wa dawa hizo ni asilimia 73 kufikia robo mwaka ya kwanza ya mwaka wa fedha 2018/2019.

“Hali ya upatikanaji dawa muhimu umeimarika kuanzia mwaka 2016/2017 na kufikia asilimia 93 nchi nzima katika mwaka 2017/2018 na hivyo kuweza kufanikiwa katika maeneo mengi na kufikisha dawa moja kwa moja katika vituo vya kutolea huduma za afya nchi nzima”.Alisema Waziri Ummy Mwalimu. Aidha, Waziri Ummy alisema MSD imeweza kusambaza dawa moja kwa moja hadi vituo vya kutolea huduma za afya vinavyofikia 5,432 nchi nzima kwa kutumia magari 215 na hivyo kusambaza dawa zenye thamani za shilingi bilionini 600 kwa mwaka kupitia mfumo wa ugavi ulio enea nchi nzima.

Hata hivyo Waziri Ummy amesema kuwa hivi sasa MSD inapeleka dawa mara 6 kwa mwaka na pale kwenye mahitaji ya dharura tofauti na zamani ambapo ilikua inapeleka dawa mara nne kwa mwaka. Mbali na hayo Waziri Ummy alisema Bohari ya dawa imeendelea kuimarika kifedha katika kipindi cha miaka mitano iliyopita hususan katika mwaka wa fedha 2017/2018 ambapo Serikali iliongeza bajeti ya dawa, vifaa na vifaa tiba na kuweza kutoa kiasi cha shilingi bilioni 80.1 na kwa mwaka wa bajeti 2018/2019 kwa robo hii ya mwaka imepokea shilingi bilioni 20.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewataka wafamasia wote wa Hospitali na vituo vya afya kupeleka orodha ya dawa zilizopo kwenye stoo kwa madaktari kila mwanzo wa wiki. “Wafamasia wote wa Hospitali na zahanati za Serikali wanatakiwa kuwapelekea madaktari orodha ya dawa zilizopo kwenye stoo ili kama dawa ya ugonjwa Fulani haipo Daktari awe na uwezo wa kuandika dawa mbadala kwa mgonjwa” amesema Dkt. Ndugulile.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya dawa nchini Bw. Laurean Bwanakunu amesema kuwa katika kuhakikisha upatikanaji wa dawa unadumu nchini wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi kujenga kiwanda cha dawa nchini. “Tunatarajia mpaka kufikia Machi 2019 kukamilisha ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi kujenga kiwanda cha dawa nchini ambapo utafanyika kwa haraka ili kukamilikia mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2019” alisema Bw. Bwanakunu.

GEKUL AIKACHA CHADEMA,ALA KIAPO KUITUMIKIA CCM

$
0
0
Na John Walter-Babati

Aliyekuwa Mbunge Wa Jimbo La Babati Mjini Kupitia Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo [CHADEMA] Paulina Gekul Amepokelewa Rasmi Na Chama Cha Mapinduzi Pamoja Na Aliyekuwa Diwani Wa Kata Ya Maisaka Kupitia Chama hicho Abrahamani Kololi,Mara Baada Ya Kujivua Uanachama Huo kwa kile Walichokieleza ni kuchoshwa na Mambo yanayofanywa na  Chadema.


Akizungumza Na Wananchi  Na Wanachama Wa Ccm Paulina Gekul Alieleza Kuwa Kama Mbunge  Ambaye Yupo  Kwa Ajili Ya Kuwatumikia Wananchi Amefikiri Ni Muda Muafaka Wa Kukiri Ukweli Hadharani Yale Mazuri Ambayo Yanafanywa Na Rais Wetu Lakini Pia Yale Mazuri Yalikuwa Yakifanywa Na Chama Cha Mapinduzi Chama Ambacho Ndio Kina Dola Na Ndio Kina serikali.
“Ni Mengi Mazuri Yamefanywa Katika Jimbo Letu Na Serikali Kuu Haya Mambo Ndio Yaliyonifariji Na Kuonakuwa Kwanini Nisiwe Pamoja Na Hawa Watu Ambao Nikiwa Nao Hapo Nakuwa Na Mh.Rais Na Viongozi Na Wanachama Wa Ccm Ili Kuwaletea Wananchi Maendeleo Na Zile Ndoto Ambazo Mh.Rais Akiwaza Kwa Ajili Ya Watanzania”alisema Gekul
 “Sababu Ya Kujiuzulu Ni Kwamba Yale Aliokuwa Akiyapigania Kwaajili Ya Wananchi  Machache Yake Yalikuwa Yakikubalika  Na Yale Ambayo  Na Mengine Kuachwa   Hivyo Ili Kuweza  Kutimizia Wanachi Yale  Aliyowaahidi  Ni Wakati Wa Kuungana Na Viongozi Wa Ccm Kwa Ajili Ya Babati Ambapo Yatakuwa Mepesi Kuliko Vile Ambavyo Walikuwa Wakitofautiana.”

‘’ Kwa Mzigo nilionao Kwa ajili Ya Wananchi Wa Babati niliona mimi Nisiwe Sababu Ya kuwakosesha Haki yenu Kwa Sababu Nipo Upinzani Naamini baada ya Jitihada hizi na Mapokezi Haya Makubwa Babati Yetu Itakuwa Mpya tena,itasonga mbele,na Babati Yetu itasonga mbele na kubadilika kwa sababu tutakuwa tunaongea lugha moja hakuna atayaweza kuzuia’’alisema Gekul.
Kwa upande wake katibu wa siasa na mahusiano ya kimataifa  Kanali Mstaafu Ngemera Lubinga,alisema kwa sasa tayari wamepata watu wa kulinda usalama wa chama na kuzijua njia za adui yao kwa kuwa wale wote wanaotoka upinzani wanazijua njia wanazotumia kwa ajili ya kuharibu mipango ya Ccm.

‘’Niwapongeze wale wote waliorudi Ccm kwani wamerudi wakati ambao tanzania inasema ccm mpya na Ccm mpya hivyo ni wakati wa kutekeleza  majukumu kwa pamoja kwani huwezi kutengeneza jamii mpya kama huna nidhamu ya hali ya juu’’alisema Lubinga. Aidha aliwataka wote waliujiunga  na ccm waendane sawa na hitaji la nchi ambalo ni kuwaongoza wananchi kulingana na ilani ya chama cha mapinduzi ikiwa ni pamoja na kuzingatia usiri wa dhamana  ya  uongozi ndani ya  chama ,hivyo basi kwa  kuwa Paulina anataarifa nyingi za adui ni wakati wake wa kupewa majukumu ili aweze  kwenda kupambana na maadui kwa kuwa yeye ndio anajua madaraja ya adui.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti alikipongeza chama cha Mapinduzi  kwa kukubali kuwapokea wanachama wenye akili huku akieleza kuwa unaweza kuwa na chama kikubwa lakini wanachama ni mzigo hivyo kwa kuwa gekul  tayari tupo nae ni matumaini yetu tutafikia tuliyokuwa tunaitaka.‘’Kuna Taarifa  Kuwa Kuna Watu Wanataka Kujiunga Na Chama Cha Mapinduzi Lakini Tufike Mahali Tuseme Inatosha Kwani Kuna Wanaotaka Kujiunga Na Chama Hiki Kwa Ajili Ya Kutaka Kukivuvunga Na Kuna Taarifa Ambazo Zipo  Kuwa Wanasema Tutawafuata Hukohuko Kuwavuruga Ndio Mana Mi Nasema Tuishie Hapa Hapa Inatosha Kwasababu Tayari Tumeshalamba Madume Magarasha Yabaki Huko Huko Yatatuvuruga Ndo Maana Nasema Inatosha Tumechukua Madume’’alisema Mnyeti.

Naye Mbunge Wa Jimbo La Babati Vijijini Kupitia Chama Cha Mapinduzi Jitu Son Alimpongeza Mbunge huyo Kwa Kujiunga  Ccm Huku akieleza kuwa awali walikuwa wakikutana kwa siri na kufanya mawasiliano kwa siri  kwa ajili ya kujadili masuala ya maendeleo kwa kuhofia lakini kwa sasa itakuwa ni hadharani kwa kuwa lengo ni moja na chama ni kimoja.

Ujerumani Yampongeza Rais Magufuli Kupambana na Rushwa – Balozi Waechter

$
0
0
Na Judith Mhina – MAELEZO

Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Dkt Detlef Waechter amempongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa kufanikiwa kupambana na rushwa nchin Tanzania na kupata mafanikio makubwa ndani ya kipindi kifupi.

Hayo amesema Balozi Waechter alipofanya mahojiano na Idara ya Habari MAELEZO mapema jana katika hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro Dar-es-salaam Kempinski katika barabara ya Sokoine Jijini Dar-es –salaam.

Akielezea jinsi rushwa ilivyoota mizizi sehemu nyingi ikiwemo Ujerumani amesema “Tatizo la rushwa sio la Tanzania peke yake, hata pale Ujerumani lipo japo si kwa kiasi kikubwa, bali kila mara serikali inapaswa kujiangalia na kuhakikisha inapambana na mfumo wa rushwa mahala popote. Ili raia wako wawe na imani na serikali yako”

Kwa dhati kabisa nampongeza Rais Magufuli kwani hali ilikuwa sio nzuri kulingana na ripoti tuliyoisikia wakati wa Mkutano wa 38 wa Bara la Afrika wa Kuthibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya miezi mawili iliyopita. Uwepo wa rushwa Tanzania ilikuwa ni eneo linalotumiwa katika kupitisha madawa hayo ambapo sasa suala hili limepungua kwa kiasi kikubwa kutokanana juhudi za Rais Magufuli.

Akielezea ubaya wa rushwa Balozi Waechter amesema kuwa matatizo ya rushwa yanarejesha nyuma maendeleo kwa kuwa watu hawapati huduma wanazostahili kwa kuwa tu kuna wengine wanatumia rushwa. Halikadhalika uwepo wa rushwa unaondoa uaminifu kutoka Taifa moja kwenda linguine au nchi moja kwenda nyingine.

Ukiangalia maeneo ambayo hayana utulivu na amani, inatokana na kushamiri kwa rushwa na kuwa na serikali ambazo hazisimamii vema huduma kwa wananchi wake. Hili ni tatizo kubwa lililokumba nchi za kiafrika ambazo raia wake kila siku wanatafuta njia ya kuelekea Ulaya.

Raia hao wanakwenda ulaya sio kwa kupenda ni kwa sababu wamekosa utulivu na amani katika nchi zao, kinachopatikana nchini kwao ni kwa ajili ya wajanja wachache wanaoweza kutoa rushwa na kuhodhi utajiri wa nchi badala ya kuhudumia umma wa nchi nzima. Amesema Balozi Waechter.

Pia Balozi Waechter ameongeza kwa kusema kuwa nimefurahishwa na Tanzania kuona umuhimu wa viwanda katika kujenga uchumi wa nchi ya Tanzania, kwani sio rahisi uwe mzalishaji wa malighafi alafu umtehgemee mtu mwingine anunue na nchi yako ipate faida. Nadhani ni uamuzi wa busara kabisa walioufanya Tanzania kuelekea katika nchi ya viwanda.

Nchi zote zilizoendelea kama Ujerumani zimefika hapo zilipo baada ya kufanya mageuzi ya hali ya juu katika suala zima la viwanda na tekinolojia, Ujerumani ipo tayari kushirikiana na Tanzania pale ambapo itahitajika katika kuendeleza juhudi za kufanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda,

Aidha mpaka sasa wapo wawekezaji kadhaa wa Ujerumani ambao wamewekeza katika masuala ya Uzalishaji cement Mfano ni kiwanda cha cement cha Tanga, Pia kuna mradi mkubwa wa kupeleka maji safi na salama katika Mji wa Kigoma ambapo maji yanatolewa katika ziwa Tanganyika kwa ajili ya matumizi ya watanzania,

Mahusiano ya Tanzania na Ujerumani ni mazuri sana na tunatarajia kuendelea kushirikiana katika masuala mbalimbali ya kijamii, kiuchumi, na kimaendeleo kwa faida ya nchi zetu mbili. Pamoja na hayo tunauhusiano wa muda mrefu sana kati ya Ujerumani na Tanzania mara tu baada ya uhuru wa Tanganyika hadi sasa.

Akielezea suala zima la nchi zote mbili kujifunza kutoka kwa mwenzake amesema Ujerumani inajifunza kitu kikubwa sana hapa Tanzania ambacho chimbuko lake ni Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere suala zima la Amani na Utulivu ambao mimi binafsi sijawahi kuuona sehemu yeyote ambayo nimeweza kuishi.

Wito wangu ni kuwa kwa kuwa mmeamua kuijenga Tanzania ya viwanda itategemea sana hali yenu ya amani na utulivu mlionao ambao sina shaka kwa kuwa ni mabingwa wa hali yote Barani Afrika na duniani nina hakika mtafanikiwa kutimiza azma yenu . Muungeni mkono Rais Dkt Magufuli mtafanikiwa.

WAKULIMA SKIMU YA UYOLE WAOMBA KUTEMBELEWA NA WAKALA WA VIPIMO

$
0
0
Katika picha ni Miundombinu mfereji wa maji unaopeleka maji katika skimu ya umwagiliaji Iganjo Uyole mkoani Mbeya, pembeni yake ni shamba la mahindi yanayomwagiliwa kwa kutumia maji yanayopita katika mfereji huo.


Bwana John Soda mkulima katika skimu ya Iganjo Uyole Mkoani Mbeya akizungumza kuhusu ukarabati uliyofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika skimu hiyo, inayoonekana kwa nyuma ni sehemu ya miundombinu hiyo.
Katika Picha ni banio linaloruhusu maji toka chanzo cha maji cha mto Nkwanana kupeleka katika skimu ya umwagiliaji ya iganjo iliyopo Uyole mkoani Mbeya.
…………………………

Na Mwandishi Maalum.

Wakulima, katika skimu ndogo ya kilimo cha mbogamboga ya Iganjo Iliyopo Iliyopo Uyole nje kidogo ya jiji la Mbeya, wameomba wataalam kutoka wakala wa vipimo kuwatembelea ili kuweza kusaidia tatizo la vipimo halisi vya mazao yao ambavyo vinafanywa katika hali ya udanganyifu na kuwasababishia hasara.

Hayo yemeelezwa na Mwenyekiti wa chama cha Wamwagiliaji Iganjo Bw. John Soda alipokuwa akizungumza katika eneo hilo mbapo alisema kuwa suala la kuzidisha ujazo unaotakiwa (lumbesa) bado ni tatizo jambo ambalo linawasababishia wao kama wakulima kuuza mazao yao kwa bei ya hasara.

Bwana Soda alisema kuwa kumekuwa na tatizo la upimaji wa mazao katika magunia ambapo magunia yanayokaguliwa yanakuwa na vipimo halisi lakini magunia yanayokwenda sokoni yanakuwa hayana uhalisia.

“Tunawaomba wakala wa vipimo waweze kuja kututembelea na kusimamia kwa ukaribu swala hili la udanganyifu katika vipimo, jambo ambalo kwa kiasi fulani limekuwa likitusababishia hasara sisi wakulima wa mboga mboga hasa katika zao la viazi, vitunguu na karoti, Pamoja na hilo naiomba serikali iweke utaratibu wa kuuza mazao na kutoa bei elekezi.” Alisema Bwana Soda.

Kwa Upande wake Bwana Solomon Soda Mkulima katika skimu hiyo aliishukuru Serikali kwa ukarabati na ujenzi wa miundombinu katika skimu hiyo na kuiomba iendelee kuwasaidia waweze kupata pembejeo kwa bei ya ruzuku, na kumalizia kuboresha miundombinu katika sehemu iliyobakia.

Aidha Bw. Solomon alisema kuwa, katika skimu hivyo ambayo ipo pembezoni mwa mto Nkwanana kumekuwa na upandaji wa miti ya mikaratusi ambayo inafyonza maji na kusababisha mto huo kukauka maji hivyo “ Naiomba Serikali itusaidie tuitoe miti hii na kupanda miti mingine ambayo ni rafiki kwa mazingira maaana miti ya mikaratusi inatabia ya kunyonya maji na inaweza kusababisha mto huu kukauka au kupelekea upungufu wa maji.”

Sambamba na hilo Bw. Solomon aliiomba serikali na mamlaka husika kufanya ukaguzi katika maduka yanayouza madawa ya kilimo mkoani Mbeya kwani kuna wasiwasi kuwa madawa mengi yanakuwa yamepitwa na wakati.

Kwa upande mwingine wakulima hao wameeleza kuwa kilimo cha umwagiliaji kimewapa manufaa makubwa ikiwa ni pamoja na kujenga na kuishi katika nyumba za kisasa, kuwasomesha watoto na kuongeza kipato familia na kuchangia katika maendeleo ya eneo hilo kwa ujumla.

Skimu ya kilimo cha umwagiliaji Uyole imekarabatiwa kwa fedha za serikal kupitia mfuko wa kuendeleza kilimo cha umwagiliaji Wilayani Mbeya.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO OKTOBA 24,2018

UMOJA WA MATAIFA KUADHIMISHA MIAKA 73 TOKEA KUANZISHWA

$
0
0
Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza na Waandishi jana katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere ikiwa ni matayarisho ya kusherehekea miaka 73 ya Siku ya Umoja wa Mataifa ambapo tarehe 24 Oktoba husherehekewa Duniani kote na kwa Tanzania yataadhimishwa jijini Dar es Salaam na Zanzibar, kushoto ni Bw. Alvaro Rodriguez Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na kulia Bw. Deusdedit B. Kaganda Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa. 
Bw. Deusdedit B. Kaganda Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano  wa Kimataifa kulia akimkaribisha Bw. Alvaro Rodriguez Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kushoto kuzungumza na waandishi wa habari katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Mkutano huo ulifanyika kufuatia tarehe 24 Oktoba, Umoja wa Mataifa utaadhimisha Miaka 73 ya tokea kuanzishwa kwake. Katikati Mhe. Dkt. Damas Ndumaro (Mb) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Bw. Alvaro Rodriguez, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania aliyekaa kushoto alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere akilelezea juu ya maendeleo ya Umoja huo na kaulimbiu ya mwaka huu katika kuadhimisha siku ya Umoja wa Mataifa tarehe 24 Oktoba iliyobeba ujumbe wa "Uwezeshaji Vijana na Ubunifu kwa ajili ya malengo ya maendeleo endelevu" 
Baadhi wa waandishi wa Habari walioshiriki katika mkutano wa Waandishi wa Habari katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

WACHIMBAJI WA MADINI WAPEWA ELIMU KUHUSU TAHADHARI YA MIONZI.

$
0
0

Proff Lazaro Busagala Mkurugenzi Tume ya nguvu za atomic Tanzania akizungumza na washiriki wa mafunzo.Picha na Vero Ignatus
Denis Mwalongo muwezeshaji wa mafunzo maalumu kwa wataalamu.
Washiriki wa kiwa katika Mafunzo




Na Vero Ignatus Arusha.

Zaidi ya wataalamu 20 kutoka katika kampuni mbalimbali za uchimbaji madini nchini wanatarajiwa kuwa mabalozi chanya katika kutoa elimu kuhusu tahadhari na matumizi sahihi ya mionzi kwa wachimbaji pamoja na jamii.

Akizungumza na wataalamu hao mkurugenzi wa tume ya nguvu za mionzi (Atomic) Profesa Lazaro Busagala nchini amesema niwakati muafaka kwa jamii kuwa na elimu,uelewa kuhusu mionzi hususani katika maeneo ya migodi na jamii inayo pakana na migodi ya uchimbaji madini.

Denis Mwalongo ni muwezeshaji wa mafunzo maalumu kwa wataalamu hao amesema kuwa katika migodi mingi nchini wafanyakazi wamekuwa wakiathirika zaidi kwa kufanya kazi zao bila vifaa vya kujikinga kiafya.

Amesisitiza kuwa endapo mionzi ikiingia Zaidi mwilini kwa muda mrefu mtu anaweza kupoteza maisha kwa kuugua hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari kabla ya madhara kutokea katika maeneo ya kazi na jamii inayozunguka migodi ya uchimbaji madini.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema matarajio yao baada ya kupata elimu zaidi juu ya matumizi na tahadhari kwa wafanyakazi na jamii kwa ujumla,ambapo wamesisitiza kuwa watakuwa mabalozi katika kutoa elimu hiyo ilikuokoa maisha ya wananchi na wafanyakazi wengine.

Mafunzo hayo yenye lengo la kuwajengea uwezo zaidi wataalamu hao pamoja nakuinusuru jamiii nayo inayopakana na maeneo ya migodi ilikuokoa vizazi vya sasa na vijavyo.

Maandalizi ya Rock City Marathon yakamilika.

$
0
0

Maandalizi ya mbio za Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika Octoba 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza yamekamilika huku zaidi ya washiriki elfu tano (5,000) kutoka ndani na nje ya nchi wakitarajiwa kushiriki katika mbio hizo.

Tayari Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw John Mongella pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt Philis Misheck Nyimbi wamekwisha thibitisha ushiriki wao kwenye mbio hizo ambazo pia zitahusisha ushiriki wa baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali, wabunge na washiriki kutoka mashirika na taasisi mbalimbali.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Mwanza jana, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi alisema kamati yake imejiandaa kupokea washiriki zaidi ya 5,000 wa mbio hizo kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo wakimbiaji wa kimataifa.

“Tunatarajia kuwa na mbio zenye mafanikio makubwa mwaka huu. Maandalizi kwa kiasi kikubwa yamekwisha kamilika na kinaochoendelea kwa sasa ni usajili wa washiriki kutoka ndani na nje ya nchi na tunatarajia kufunga zoezi hilo siku ya Jumamosi Oktoba 27,’’ alibainisha.

Akizungumzia kuhusu zawadi, Ngowi alisema pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 4 kila mmoja, sh.mil 2/- kwa washindi wa pili na sh. Mil 1/- kwa washindi wa tatu, huku washindi wanne hadi kumi nao pia wakiibuka na medali na pesa taslimu.

Kwa upande wa mbio za Kilomita 21, Ngowi alisema, pamoja na medali washindi wa kwanza kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 3/- kila mmoja, sh. Mil 1/- kwa washindi wa pili na sh. 750,000/- kwa washindi wa tatu huku pia washindi wanne hadi wa kumi wakiibuka na zawadi za pesa taslimu na medali kila mmoja.

Aliwataja wadhamini ambao pia watashiriki katika mbio hizo kuwa ni pamoja na kampuni za Puma Energy Tanzania, Tiper,Rock City Mall, NSSF, Gold Crest, New Mwanza Hotel, CF Hospital, Coca Cola, Metro Fm, EF Outdoor, KK Security, Belmont Fairmount Hotel , Bigie Customs na Global Education Link.

Alibainisha kuwa mbio za Km 5 zitahusisha watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino ambapo washindi kwa upande wa mashirika watapatiwa zawadi za utambuzi ikiwemo medali na vyeti vya ushiriki huku pesa zikielekezwa kwa washiriki wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino.

Bw Ngowi alivitaja vituo vinavyoendelea na usajili huo kwasasa kuwa ni pamoja na Igoma, Buzuruga, Airport Mwanza, Rock city mall, Chuo Kikuu cha Saut, Nyegezi Stand, Mwanza hotel, Nyamagana Stadium, Dampo pamoja na Nyakato.

Alisema usajili huo pia utahusisha ofisi zote za riadha mikoa ya Geita, Simiyu na Shinyanga huku akiongeza : “Kwa upande wa Dar es Salaam Fomu za ushiriki pia zinapatikana katika jengo la SHAMO Tower, Mbezi Beach , jijini Dar es, Salaam ”.

Mwanariadha Alphonce Simbu akionyesha tabasamu baada ya kukabidhiwa fedha taslimu ikiwa ni zawadi baada ya kuibuka mshindi kwanza katika mbio za km 21 katika mashindano ya Rock City Marathon mwaka 2013.

AMANI NA UTULIVU ULIOJENGWA NA NYERERE NI FUNZO KWETU UJERUMANI - BALOZI DKT DETLEF WAECHTER

$
0
0
Na Judith Mhina-MAELEZO
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Dkt Detlef Waechter, amesema hajawahi kuona amani anayoiona hapa Tanzania.

Amesema maneno hayo wakati wa mahojiano maalum na Idara ya Habari MAELEZO mapema wiki hii katika Hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro Dar-es-salaam Kempinski katika barabara ya Sokoine Jijini Dar-es –salaam.

Mheshimiwa Balozi Waechter amesema “Hayati, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni kiongozi ambaye hatasahaulika kwa kuwa amani aliyojenga Tanzania ni ya pekee haipatikani mahali popote duniani”. 

Kwa kutambua hilo Balozi amesema kuwa Ujerumani imeona umuhimu wa Baba wa Taifa la Tanzania kama mfano wa kuigwa duniani kwa kujenga amani na usalama wa binadamu. Ambapo watu wa dini tofauti, makabila tofauti na asili tofauti wanakaa pamoja na kushirikiana kujenga nchi. Huu ni urithi na funzo kubwa kwetu ambapo Julius Nyerere ametuachia.

Kutokana na amani na usalama wa binadamu alioujenga, Serikali ya Shirikisho ya Ujerumani imejifunza jambo kubwa sana kutoka kwa Mwalimu Nyerere na kuona ni busara kufadhili jengo la Makao Makuu la Umoja wa Afrika pale Adiss Ababa Ethiopia. Linaloitwa The Julius Nyerere Peace and Security Building.

“Jengo lile ni kielelezo tosha kuwa vizazi na vizazi vitakavyofika pale Addiss Ababa Ethiopia watatambua uwepo wa Mwalimu Nyerere duniani na pia, anakumbukwa kwa Amani na Utulivu alioujenga akiwa hapa duniani na kamwe hatasahaulika” Amesisitiza Balozi Waechter.

Balozi Waechter amesema kuwa kwa muda nilioishi hapa Tanzania, tangu 2016 ninashangazwa kuambiwa watanzania ambao walio wengi ni Wakristu na Waislamu wanaoishi pamoja na kushirikiana kwa upendo na mambo yanaendelea kama kawaida. 

Ameongeza kwa kusema kuwa, Watanzania walio wengi hawajui hili la kuwaweka watu wenye asili tofauti, dini tofauti mahala pamoja ni vigumu sana na haliwezekani katika nchi nyingine. Nimeambiwa hapa Tanzania watu wanaoishi mchanganyiko wa makabila tofauti, dini tofauti na Itikadi tofauti kwa kweli alichokifanya Nyerere kitabakia kama kumbukumbu ya dunia na ni lazima dunia iige mfano huu.

Balozi Waechter amesema kuwa imani za dini hapa duniani zinaleta mgongano mkubwa katika jamii nyingi. Huwezi kuwaweka wakaishi katika eneo moja na ni lazima kila mara kuwa na tahadhari ili kuepuka mgongano wa aina yeyote ile.

Mara nyingi pale Ujerumani tumekuwa tukishuhudia migongano ya mara kwa mara kwa Wakimbizi walioingia Ujerumani kutokana na tofauti za kimazingira walikotoka na imani zao za dini. Hii ni changamoto kwetu, lakini nina hakika sisi Ujerumani tutajifunza mengi hapa Tanzania kutokana na amani na utulivu mlionao.

Lakini kwa Baba wa Taifa la Tanzania Hayati Mwalimu Nyerere kwake sio shida kabisa amekaa na Wakimbizi bila shida Taifa lina watu wa imani tofauti kweli sio tatizo wanashirikiana na kutekeleza mambo ya taifa na ya kila siku kwa pamoja kama vile ni watu wa kundi moja hakika hii ni ajabu. Ameshangaa Balozi Waechter

Ujerumani inamtambua Mwalimu Julius Nyerere kuwa ni kiongozi muhimu sana katika Bara la Afrika, pamoja na Rais wa kwanza wa Weusi waliowengi Afrika ya Kusini Hayati Rais Nelson Mandela. Hii imepelekea serikali ya Ujerumani kuona umuhimu wa Amani na Usalama na kufadhili kwa kutoa fedha za walipa kodi wa Ujerumani ambao wamefanikisha ujenzi wa Makao Makuu ya Umoja wa Afrika. 

Nyerere ni Baba wa Amani na Usalama Barani Afrika na dunia kwa ujumla, kwa kulitambua hilo Ujerumani imeona iko haja ya kuunga mkono juhudi za Umoja wa Afrika ya kuhakikisha Afrika inakuwa na Amani na Usalama, ili kuweza kuwaweka raia wake ndani ya Bara husika badala ya kukimbilia Ulaya ambapo wanatumia njia ambazo sio salama kwa uhai wa binadamu.

Pia, serikali ya Shirikisho la Ujerumani umejitahidi kufanya jitihada ya kutembelea nchi za Afrika Magharibi ambazo zinaweza kusaidia kupunguza wimbi la Wakimbizi kwenda Ulaya kwa kujaribu kushirikiana nao ili wajenge uchumi Imara. Tunafahamu sio kwamba Wakimbizi hawapendi kukaa kwao ila hali halisi ya amani na usalama inapokosekana, rushwa inaposhamiri hivyo kubaki katika nchi zao ni kuhatarisha maisha yao. 

Wito wangu kwa Watanzania wasisahau mambo muhimu ambayo Nyerere amewaaasa kuhusu Amani na Usalama. Nchi nyingi zinatamani mlichonacho Tanzania lakini najua kazi aliyoifanya Mwalimu Nyerere haikuwa ndogo ni kubwa na kama kweli mnamheshimu, itunzeni Amani yenu na Utulivu ili mumuenzi kwa vitendo. Amesisitiza Balozi Waechter.

Sisi Ujerumani hatuchoki kusema ukweli kuhusu Amani na Utulivu wa Tanzania tunawaasa mataifa mengine kwa kuwaambia kuwa waangalie mfano wa Tanzania ni nchi ambayo imetambua Amani na Utulivu utaleta mambo mengine yote. Nadhani hakuna faida ya kuwa na maendeleo ambayo watu wako hayawafaidishi kutokana na kukosa amani. Sasa unatafuta maendeleo kwa ajili ya nani? Aliuliza Balozi Waechter.

Eneo hili la Amani na Utulivu mnaweza kulitangaza sana na kuwaambia watu mbalimbali duniani waje waone mfano kwa kutembelea maeneo mnayoishi kuangalia nyumba zenu za ibada unakuta msikiti, makanisa ndani ya jamii na kila mmoja anaabudu kwa muda wake, angalia mikusanyiko ya sherehe za kijamii hazibagui na Mtanzania yupo huru kuishi mahala popote ndani ya nchi yenu.

Hivyo Watanzania msikate tamaa katika suala zima la uchumi kwa kuwa mmepata uongozi wenye nia ya kulipelekea Taifa lenu mahali pazuri tumieni fursa mliyoipata kujenga nchi yenu kwa manufaa ya Taifa lenu na dunia kwa ujumla.

Balozi Waechter, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa ushirikiano mzuri unaoendelea kati ya Tanzania na Ujerumani na ameahidi kutumia ushirikiano huo kwa manufaa ya nchi zote mbili.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>