Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1706 | 1707 | (Page 1708) | 1709 | 1710 | .... | 1903 | newer

  0 0

   Mtawala wa Ras al khaima Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi akipeana mikono na Viongozi mbalimbali alipokua  akiondoka Zanzibar na kurejea nyumbani.
   Mtawala wa Ras al khaima Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi akipita katika zulia kuelekea kwenye ndege tayari kwa kuiondoka Zanzibar na Kurejea nyumbani.
   Mtawala wa Ras al khaima Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi akiagana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Ussi(Gavu)alipokua akiondoka Zanzibar na kurejea nyumbani.
  Mtawala wa Ras al khaima Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi akipunga mkono ikiwa ni ishara ya kuaga wakati akipanda ndege na kuondoka Zanzibar na kurejea nyumbani.

  PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

  Na Baltazar Mashaka, Mwanza.

  SERIKALI mkoani Mwanza imepokea msaada wa vifaa tiba na upasuaji kwa walemavu wa macho vilivyotolewa na The Desk & Chair Foundation (TD & CF) Tawi la Tanzania.

  Vifaa hivyo vitakavyotumika kwenye kambi ya upasuaji wa mtoto wa jicho wakati wa maadhimisho ya Siku ya Fimbo Nyeupe yanayofanyika kitaifa jijini humu, vilipokelewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dk. Philis Nyimbi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela.

  Akikabidhi msaada huo Mwenyekiti wa The Desk & Cir Foundation Sibtain Meghjee alisema wanaunga mkono juhudi za serikali za kuhudumia jamii kwa kuwa taasisi hiyo inatambua watu wenye ulemavu wana changamoto nyingi zikiwemo kushindwa  kumudu gharama za matibabu.

  “Taasisi hii inafanya shughuli za kusaidia jamii (walemavu,wagonjwa na masuala ya elimu),kulingana na mahitaji.Kwa changamoto za walemavu wa macho ni kushindwa kumudu gharama za tiba sababu ya ugumu wa kipato hivyo serikali iangalie jinsi ya kuwasidia wapate Bima ya Afya,”alisema Meghjee.

  Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo Mongela alisema maadhimisho ya ya Fimbo Nyeupe ni kielelezo kuwa walemavu wana mchango mkubwa na ndiyo maana TEHAMA inawaelekeza kwenye Uchumi wa Viwanda kama ilivyo kauli mbiu.

  Alisema vifaa hivyo vitahudumia wilaya saba za Mkoa wa Mwanza  na hivyo serikali imejipanga wananchi watakaojitokeza hawatakosa huduma kwenye maadhimisho hayo na kambi ya uchunguzi wa macho, watakaobainika watatibiwa kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou Toure.
   Mwenyekiti wa The Desk Chair Foundation Sibatain Meghjee akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa tiba vya macho na upasuaji kwa serikali ya Mkoa wa Mwanza. Kushoto wa kwanza ni Katibu Tawala Msaidizi Seif Rashid, wa pili ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagan Dk. Philis Nyimbi.
   Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Silas Wambura akizungumza kuhusu ubora wa vifaa hivyo kabla ya kukabidhiwa.
    Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dk. Philis Nyimbi,akipokea vifaa tiba na upasuaji pamoja na fimbo nyeupe kutoka kwa Mwenyekiti wa Desk & Chair Foundation Sibtain Meghjee (kulia) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela.
   Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dk. Philis Nyimbi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akizungumza baada ya kupokea msaada wa fimbo nyeupe, vifaa tiba vya macho na upasuaji vilivyotolewa an The Desk & Chair Foundation.


  0 0


  WAZIRI wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amezindua mradi mkubwa wa uboreshaji wa huduma ya maji mjini Mbinga akiwa katika ziara yake kikazi mkoani Ruvuma.

  Akizungumza katika uzinduzi huo, Profesa Mbarawa amesema mradi huo ni hatua ya Serikali kufikia lengo la kufikia asilimia 90 kwa miji mikuu ya wilaya itakapofika mwaka 2020, na imepanga kutumia Silingi Bilioni 1.2 kwa ajili ya kuboresha huduma ya maji kwa miji mingine 25 Tanzania Bara na Visiwani.

  Amesema mradi huo utabadilisha kwa kiasi kikubwa maisha ya wananchi wa Mbinga sio tu kwa kutoa huduma ya majisafi na majitaka kwa wananchi.  Pia, ni muhimu kwa shughuli za kila siku za kiuchumi zinazofanyika katika mji huo.

  Vilevile, Profesa Mbarawa ameipongeza Mamlaka ya Maji ya Songea Mjini (SOUWASA) kwa kazi nzuri ya kusimamia mradi huo mpaka umekamilika.
  Mradi huu upo chini ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya mji wa Mbinga (MBIUWASA) ulianza kujengwa Mei, 2017 chini ya mkandarasi Almasi General Supplies Ltd ya Songea na kuanza kutoa huduma ya maji kwa mji wa Mbinga Februari, 2018 umegharimu   Shilingi Bilioni 1.029.

  Naye Meneja wa MBIUWASA, Patrick Ndunguru amesema kukamilika kwa mradi kumeleta ongezeko la uzalishaji wa maji kutoa wastani wa lita 700,000 wakati wa kiangazi na lita 1,600,000 wakati wa masika, ikichangia kuongeza mapato kutoka Shilingi Milioni 18 hadi Milioni 25 kwa mamlaka hiyo.

  Wizara ya Maji kwa kutumia Kampuni ya Don Consult ilisanifu mradi huu kwa lengo la kumaliza tatizo la maji katika mji wa Mbinga, pamoja na mfumo wa uondoaji salama wa majitaka.
    Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa  akizindua mradi mkubwa wa maji wa uboreshaji wa huduma ya maji mjini Mbinga uliogharimu Sh. Bilioni 1.029 akiwa na DC Mbinga, Cosmas Nshenye.
    Sehemu ya mradi wa maji wa uboreshaji wa huduma ya maji mjini Mbinga.
   Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akifungua maji katika mradi wa maji Kagugu, wilayani Mbinga katika mkoa wa Ruvuma kuashiria kukamilika kwake.
    Sehemu ya watu waliohudhuria hafla ya kusheherekea kukamilika kwa mradi wa maji wa Kagugu, wilayani Mbinga, mkoani Ruvuma.

  0 0

  Na Margareth Chambiri.

  TUME ya Taifa ya Uchaguzi imewaonya Wasimamizi wa Uchaguzi ambao ama kwa kujua au kwa makusudi wataharibu au kukiuka taratibu za Uchaguzi kutokana na kutofuata sheria na taratibu za Uchaguzi.

  Onyo hilo limetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Mbarouk Salum Mbarouk wakati akifungua mafunzo kwa Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi jijini Dodoma.

  Mheshimiwa Mbarouk ambaye amewataka Wasimamizi hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea amesema Sheria ya Taifa ya Uchaguzi na ile ya Serikali za Mitaa zinaunda kosa la jinai na kutoa masharti ya adhabu kwa Afisa yeyote wa Uchaguzi ambaye atasababisha kuharibu uchaguzi.

  Makamu Mwenyekiti huyo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  amesema madhara ya kutozingatiwa kwa taratibu za Uchaguzi ni kusababisha kesi nyingi za Uchaguzi na kuitumbukiza Serikali katika gharama ambazo zingeweza kutumika katika shughuli nyingine za maendeleo.

  Amewataka Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kuyaelewa vyema maeneo wanayofanyia kazi na kujiamini ambapo pia amewakumbusha jukumu walilo nalo la kuimarisha imani ya wananchi na wadau wengine wa Uchaguzi kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

  Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt Athumani Kihamia amewataka washiriki wa mafunzo hayo kutoa ushirikiano kwa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki Uchaguzi Mdogo ikiwa ni pamoja na kuvishirikisha katika kila hatua muhimu wakati wa mchakato wa Uchaguzi.

  Dkt. Kihamia amesema Watendaji wote wa Tume wanapaswa kuwapo katika maeneo yao ya kazi wakati wote hususan kipindi cha Uteuzi, kufungua ofisi hadi muda wa kisheria na Vyama vyote ambavyo vimefuata taratibu vipewe fomu za Uteuzi na Wagombea wao wateuliwe kama wamekidhi vigezo.

  Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi ameongeza kusema kuwa kutozingatiwa kwa mambo hayo husababisha kuharibu imani ya Wadau na kusababisha malalamiko ya kutoridhishwa na mchakato wa Uchaguzi na hatimaye mashauri ya Uchaguzi kufikishwa mahakamani.

  Kadhalika Dkt Kihamia amewataka Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi hao wa Uchaguzi kutojihusisha na migogoro ya ndani ya Vyama na iwapo Vyama vitakuwa na malalamiko vielekezwe kuwasilisha malalamiko yao kwenye Kamati za Maadili na si mahali pengine popote.

  Kwa mujibu wa Dkt. Kihamia chaguzi zote duniani ni kielelezo cha demokrasia na kwamba Uchaguzi huru na wa haki hutokana na Wasimamizi wa Uchaguzi wanaozingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zinazosimamia Uchaguzi husika.

  Jumla ya Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi 210 kutoka katika Majimbo manne ya Serengeti, Simanjiro, Ukerewe na Babati Mjini pamoja na Kata 47 zinazotarajiwa kufanya Uchaguzi Mdogo Desemba 3, mwaka huu wanashiriki katika mafunzo hayo yatakayodumu kwa siku tatu jijini Dodoma. 
  Mkuu wa Idara ya Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Irene Kadushi, akifafanua jambo wakati wa mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi. 
  Mkuu wa Idara ya Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Emmanuel Kawishe akifafanua hoja katika mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi.
  Afisa Uchaguzi Meshack Mgovano, akieleza jambo kwenye mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi.
  Picha zote na NEC.

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  KATIKA jitihada za kuijengea Jamii uelewa na hamasa juu ya umuhimu wa kutunza afya na Kufanya Mazoezi, Kampuni ya E World (Events World) kwa kushirikiana na wadau mbali mbali inawaletea mbio za Kigamboni International Marathon, mbio hizi zitaambatana na zoezi la Upimaji wa afya katika kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani ambayo huazimishwa tarehe 1 mwezi wa 12 kila mwaka.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Ndg. Dimo Debwe Mitiki Mwenyekiti wa mbio hizo ambaye pia ni kocha wa michezo ya riadha na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo ya Riadha ya Walemavu Tanzania alisema, Lengo kuu la “Kigamboni International Marathon” ni kuchochea shughuri za kiuchumi kwa kutangaza fursa za uwekezaji,Biashara na vivutio vya kitalii Vilivyopo Kigamboni na maeneo ya karibu, Kuimarisha Afya pia Kuhamasisha michezo ya Riadha kwa maendeleo ya Taifa letu.

  Aidha “Kigamboni Marathon” inafanyika kuunga mkono kampeni ya Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha Watanzania kufanya mazoezi ili kuimarisha afya.

  Pia Kwa siku za hivi karibuni Tumeshuhudia Viongozi wetu wakihamasisha wafanyabiashara na wadau mbali kuwekeza ndani ya wilaya yetu mpya ya kigamboni, hivyo ni imani yetu kuwa kufanyika kwa „kigamboni International Marathon‟ kutawavutia watu mbali mbali kufika Kigamboni na kujionea uzuri pamoja na fursa zilizopo kigamboni.

  Ni ukweli ulio wazi ya kuwa Kigamboni imezunguukwa na maeneo mazuri zaidi ya kimichezo, Utalii na Uwekezaji kuliko sehemu yeyote ile Jijini Dar es saalam na hiyo ni sababu moja wapo inayotupelekea kuamini kuwa „Kigamboni International Marathon‟ ni miongoni mwa mbio bora Tanzania yenye lengo la wakimbiaji wazuri watakao watakaoleta ushindani mkubwa katika Mchezo huu wa riadha Duniani kote.

  Kigamboni International Marathon itafanyika tarehe 2 mwezi wa 12, 2018 Katika sehemu yenye mandhari nzuri nay a kipekee kabisa Afrika Mashariki ‘Fun City – Theme and Water Park’ ili kutoa nafasi kwa washiriki kuburudika na michezo mbali mbali ikiwemo kuogelea baada ya mbio. ikiwa na Mbio za urefu wa kilomita 21(Half Marathon), Kilomita 10 na Mbio kwaajili ya watoto, wazee na hata wale wasio na mazoezi ya mara kwa mara (Fun Run) pia zawadi mbali mbali kushindaniwa zikiwemo Medali za dhahabu, Silver na Gold pia Pesa Taslimu kwa washindi.

  Kwa niaba ya Kamati ya maandalizi ya „kigamboni International Marathon‟ natanguliza Shukrani kwa wadau wote waliojitokeza kuunga mkono katika Jambo hili lenye tija kwa Maendeleo ya Taifa letu wakiwemo Viongozi wetu ndani na nje ya Kigamboni, wanahabari, Taasisi Mbali mbali, Makampuni na Jamii kwa Ujumla.

  Tunakaribisha Ushiriki/ Udhamini wa Makampuni mbali mbali kutoka ndani na nje ya Kigamboni na kunatoa fursa kwa wafanyabiashara waliyopo Kigamboni kuitumia fursa hii kujumuika pamoja na kuonyesha walichonacho lakini pia kufahamiana na kuongeza Marafiki wenye tija.
  Muandaaji wa Mashindano ya Riadha ya Kimataifa ya Kigamboni Dimo Debwe akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Mkutano wa kutambulisha Mbio hizo zitakazo fanyika Desemba 2 Mwaka hu kuanzia eneo la Fun City Mpaka Daraja la Kigamboni.
  Mmoja wa Wafadhili wa Mashindano ya Riadha ya Kimataifa, Sunil Rodrigues akieleza kwanini mbio hizo zitafanyika katika eneo la Fun City Kigamboni.
  Mratibu wa Masuala ya Habari wa Mbio za Kigamboni, mwani Nyangasa akizungumza na Waandishi wa Habari Juu ya ushiriki wa Wanahabari Kumi katika Mashindano hayo.
  Uongozi wa Mashindano ya Riadha ya Kigamboni Marathoni wakionyesha Flana zitakazotumika katika Mbio za Kigamboni Intenational Marathon.

  0 0

  Benki TIB Corporate ikiwa ni mdau wa karibu wa maendeleo imechangia kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa wilaya ya Bariadi ili kuwezesha mradi wa upimaji wa viwanja kwaajili ya kujengwa Viwanda. 

  Benki ya TIB corporate imetoa mchango huo wakati wa maonyesho ya SIDO ya Kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi katika mkoa wa Simiyu. Maonyesho hayo yalizinduliwa jana Oktoba 23 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kuudhuriwa pia na viongozi wengine pamoja na waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo na Naibu Wazir wa Viwanda na Biashra Dkt. Stella Manyanya. 

  Kauli Mbiu ya maonyesho ya mwaka huu 2018 ni “Pamoja Tujenge Viwanda kufikia Uchumi wa Kati” Kwa sasa Benki yaTIB Corporate inashirikiana na SIDO ili kuvumbua fursa ambazo benki itaweza kuwapatia wajasiriamali wa viwanda vidogo na kukuza biashara zao

  TIB Corporate Bank ni Benki ya biashara na inatoa huduma zote za kibenki kwa watu binafsi, Makampuni Binafsi, Taasisi za serikali , NGOs na watanzania wote kwa ujumla. Lengo ni kuhakikisha kuwa watanzania wengi wanaweza kupata huduma bora za kibenki kwa ufanisi Zaidi. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa TIB Corporate Bank, Frank Nyabundege mara baada ya kutembelea banda la TIB Corporate wakati wa maonyesho ya SIDO ya Kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi ktk mkoa wa Simiyu. 
  Mkurugenzi wa matawi na masoko TIB Corporate Bank, Theresia Soka akimkabidhi mkoba kutoka benki ya TIB Corporate mara baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutembelea banda la Benki ya TIB Corporate wakati wa maonyesho ya SIDO ya Kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi ktk mkoa wa Simiyu. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi wa matawi na masoko TIB Corporate Bank, Theresia Soka mara baada ya kutembelea banda la benki ya TIB Corporate wakati wa maonyesho ya SIDO ya Kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi ktk mkoa wa Simiyu.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa matawi na masoko TIB Corporate Bank, Theresia Soka mara baada ya kutembelea banda la benki ya TIB Corporate wakati wa maonyesho ya SIDO ya Kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi wilayani Bariadi ktk mkoa wa Simiyu.

  0 0

   Wafanyabiashara ndogondogo wa Mbagala  jijini Dar es Salaam wakiuza bidhaa zao nje ya kituo cha mabasi leo (Picha na Emmanuel Massaka wa MMG)

   Wafanyabiashara ndogondogo wa Mbagala  jijini Dar es Salaam wakiuza bidhaa zao nje ya kituo cha mabasi leo (Picha na Emmanuel Massaka wa MMG)
  Ajali kazini

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akieleza kuhusu Serikali kuwa na Dawati linaloshughulikia bajeti ya maendeleo ya watoto wakati wa Mkutano na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika Bi. Leila Pakkala (hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.

  Ujumbe kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ukiongozwa na Mkurugenzi wa Shirika hilo Bi. Leila Passala (katikati), wakifatilia kwa makini maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango, (hayupo pichani) kuhusu elimu, lishe na sheria ya mtoto, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dodoma.
  Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango na Ujumbe wa UNICEF ukiongozwa na Mkurugenzi wa Shirika hilo Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika Bi. Leila Pakkala katika Mkutano Jijini Dodoma.  Na: WFM – Dodoma


  Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto ( UNICEF), wameonesha nia ya kuisaidia Serikali ya Tanzania kufanya tafiti mbalimbali kuhusu maendeleo ya mtoto ili kukabiliana na changamoto zinazomkabili.

  Hayo yamebainishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango, baada ya mkutano wake na Mkurugenzi wa UNICEF Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Leila Pakkala, uliofanyika ofisi za Wizara hiyo Jijini Dodoma.Dkt. Mpango alisema kuwa Shirika la UNICEF, lina nia yakushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), ili kuweza kufanya tafiti katika mikoa mbalimbali, kuzichapisha na kuzisambaza ili kuongeza uelewa wa watu kuhusu maendeleo ya watoto.

  “Watu wengi wanajua uwekezaji kwa maana ya barabara na miundombinu mingine mikubwa lakini katika mazungumzo yetu tumesisitiza kuendelea kuwekeza katika maendeleo ya watu hasa katika umri mdogo kwa kuwa usipowekeza katika umri huo na kuwekeza katika umri mkubwa matokeo yake hayawi mazuri.”, alisema Dkt. Mpango.

  Alisema kuwa, maeneo ambayo ni muhimu kuyafanyia kazi kwa kushirikiana na UNICEF ni pamoja na udumavu, elimu kwa ajili ya watoto hasa ambao hawajafikia umri wa kwenda shule na sheria ya mtoto katika kuhakikisha anakua salama kwa lengo la kulitumikia taifa kwa siku za usoni, hivyo alisisitiza kuwekeza mapema kwa mtoto katika afya, lishe, elimu, uhuru wao na usalama hivyo kuwa na uwezo mkubwa wa kulitumikia Taifa kwa wakati ujao.

  Aidha Dkt. Mpango alisema kuwa, Serikali inafanya jitihada kubwa kusimamia maendeleo ya uchumi kwa ujumla, kwa kuwa Taifa lisipokuwa na uchumi imara haliwezi kuwekeza katika maendeleo ya watoto.Alisema bajeti zinatakiwa kuweka umuhimu wa kuwekeza katika mtoto hivyo kuna Kitengo kinachohakikisha bajeti ya Serikali Kuu na Halmashauri zinazingatia mambo ya msingi ambayo yatasaidia watoto wa Tanzania kuwa na maendeleo stahiki.

  Kwa Upande wake Mkurugenzi wa UNICEF Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika Bi. Leila Pakkala, amesema kuwa Tanzania imepiga hatua katika maendeleo ya mtoto jambo ambalo linastahili pongezi na pia ameipongeza Serikali kwa ukuaji wa uchumi, kupambana na rushwa, ujenzi wa miundombinu na kuongeza mapato ya ndani kupitia kodi.

  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango, amelipongeza Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto- UNICEF, kwa juhudi zinazofanywa kuhakikisha maendeleo ya mtoto nchini Tanzania na Bara la Afrika kwa ujumla kwa kuwekeza katika lishe na elimu ili kuwa na kizazi kijacho chenye uelewa wa kutosha ili kuleta tija katika Sekta za Maendeleo.

  0 0


   Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo  jijinini Dodoma ambapo alisema wachangiaji wa mfuko huo wameongezeka kutoka wanachama 164,706 mwaka 2001/2002 hadi wanachama 873,012 septemba mwaka huu.
  IMG-20181024-WA0025
  Mkurugenzi wa NHIF Bw.Bernad Konga akijibu maswali kutoka kwa wajumbe wa kamati ambapo alisema mfuko wake upo tayari kuanza mara moja kutoa huduma kupitia vifurushi vipya vitakavyojulikana kama JIPIMIE ili watanzania waweze kupata huduma za matibabu kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini
  IMG-20181024-WA0028
  Wakurugenzi wa NHIF wakipitia taarifa ya mfuko huo wakati ikiwasilishwa kwenye kamati mapema leo
  IMG-20181024-WA0029
  Waziri Ummy Mwalimu akiwasilisha taarifa ya NHIF kwa kamati na kusema kuwa Mpango wa Wizara ni kuhakikisha wagonjwa wa mfuko huo wanapata huduma nzuri kupitia vituo vyote vya afya 7,142 vinavyotoa huduma za NHIF vikiwepo vile vya binafsi.
  IMG-20181024-WA0030
  Katibu Mkuu Afya Dkt.Mpoki Ulisubisya(wa kwanza kulia),Mkurugenzi wa NHIF Bw.Benard Konga(anayefuata)pamoja na wakurugenzi  wengine wa Wizara na NHIF wakifuatilia taarifa hiyo.
  IMG-20181024-WA0032
  .WazirinUmmy Mwalimu akifafanua jambo mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo jijini Dodoma.
  IMG-20181024-WA0033
  Waziri Ummy Mwalimu akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Idara Kuu Afya Dkt.Mpoki Ulisubisya(mwenye miwani)na Mkurugenzi wa NHIF Bernad Konga
  IMG-20181024-WA0034
  Baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo wakimsikiliza Waziri wa Afya(hayupo pichani)akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mfuko wa bima wa NHIF(Picha zote na Wizara ya Afya)
  IMG-20181024-WA0035
  Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe.Peter Serukamba akichangia taarifa hiyo


  Na.WAMJW,Bungeni,Dodoma
  Idadi ya wanachama wachangiaji wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya imeongezeka kutoka wanachama 164,708 waliokuwa wameandikishwa  mwaka 2001/2002 hadi wanachama 873,012 mwezi Septemba 2018.
  Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiwasilisha  taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mfuko huo kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Bungeni jijini Dodoma.
  “Ongezeko hili limetokana na kanuni na misingi  inayotumika katika kuendesha utaratibu wa mfuko huu ikiwa ni pamoja na uchangiaji wenye usawa kwa kuzingatia viwango vya mshahara,usawa katika kupata huduma na ushiriki wa Serikali katika usimamizi kwa faida ya wanachama” alisema Waziri Ummy.
  Waziri Ummy amesema kuwa kwa upande wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), jumla ya kaya zilizojiunga hadi Septemba mwaka huu ni 2,220,953 ikiwa ni sawa na wanufaika wapatao 13,506,330 sawa na asilimia 25 ya watanzania wote’ kwa hiyo mifuko hii yote inatoa huduma kwa watu 17,656,697 sawa na asilimia 33 ya watanzania wote kwa mujibu  wa idadi ya makadirio ya watanzania kwa sasa.
  Idadi ya wanufaika imeongezeka  kutoka 691,774 mwaka 2001/2002 hadi wanufaika 4,150,367 sawa na asilimia 8 ya watanzania wote” alisema Waziri Ummy.
  Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa mpaka sasa idadi ya wanachama wengi waliojiunga  asilimia 67 ni watumishi wa umma ambao wanajiunga kwa mujibu wa sharia.
  Hata hivyo Waziri Ummy alisema mfuko unaendelea kutoa elimu na kubuni vifurushi mbalimbali vitakavyovutia wananchi wengi kujiunga na kufaidika  na mfuko ambapo utawawezesha wanachama wengi zaidi kujiunga hasa wale wa sekta isiyo rasmi na kujiwekea malengo ya kuwafikia watanzia asilimia 50 mwaka 2020.
  “Mfuko umekamilisha uandaaji wa vifurushi vya michango na mafao kulingana na uwezo wa wananchi kulipia bima  ya afya,suala hili lipo katika hatua za mwisho kabla ya kuanza kwa utekelezaji”. Alisisitiza Waziri Ummy.
  Waziri Ummy amesema kuwa mpango huo utamwezesha mwananchi kuchagua vifurushi vya aina mbalimbaliu vya huduma  anayoitaka kwa utaratibu utakaojulikana kama ‘JIPIMIE’ na wanachama watalipa kidogo kidogo kwa utaratibu ujulikanao kama ‘DUNDULIZA’ ambao tayari umeshakamilika.
  Kwa upande wake Mwenyekiti wa kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba amesema kuwa NHIF wanatakiwa kuweka mfumo wa kutoa huduma za bima ya afya kwa mashirika makubwa ya hapa nchi na yale ya nje kwa kuwauliza  huduma zipi wangependa kuhudumiwa katika hospitali za hapa nchini hususan zile za binafsi na hivyo kuweza kuongeza idadi kubwa ya wateja watakaohudumiwa na NHIF.
  Naye Mkurugenzi wa NHIF Bw. Bernad Konga akijibu maswali ya wajumbe wa kamati hiyo alisema kwamba NHIF imekubali kuboresha huduma zao na hivyo wapo tayari kuanza huduma za vifurushi za  ‘JIPIMIE’ mara moja ili wananchi waweze kupata huduma za afya kulingana na vipato vyao.
  Aidha, alisema hivi sasa wameajiri madaktari wapatao kumi na nane  na kuwaweka kwenye hospitali kubwa za Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutatua changamototo za wateja wa huduma za bima hiyo zikiwemo za kunyanyapaliwa  pamoja na kukagua fomu zinazojazwa na wataalam wa hospitali hizo ili kupunguza malalamiko ya wateja wa huduma za bima ya NHIF na kuahidi wataongeza hospitali zingine awamu inayofuata

  0 0

  Kamishna wa Maadili Mhe. Harold Nsekela (kulia) akiwaapisha Kiapo cha Uadilifu Viongozi Wakuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi nchini (NACTE) katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili jijini Dar es Salaam. Wa pili kutoka kulia ni Katibu Mtendaji (NACTE) Dkt Adolf Babiligi Rutayuga, Mkurugenzi wa Habari, Utafiti na Mipango Dkt. Marcelina Aloyce Baitilwake na Mkurugenzi wa Ushauri na Usaidizi wa Vyuo vya Ufundi Mhandisi Dkt. Gemma Kishari Modu.
  Viongozi Wakuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi nchini (NACTE) Wakila Kiapo cha Uadilifu mbele ya Kamishna wa Maadili Mhe. Harold Nsekela (hayupo pichani). Kutoka kulia ni Katibu Mtendaji (NACTE) Dkt Adolf Babiligi Rutayuga, Mkurugenzi wa Habari, Utafiti na Mipango Dkt. Marcelina Aloyce Baitilwake na Mkurugenzi wa Ushauri na Usaidizi wa Vyuo vya Ufundi Mhandisi Dkt. Gemma Kishari Modu.

  Viongozi Wakuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi nchini (NACTE) wakisaini Hati zao za Ahadi ya Uadilifu baada ya kuapishwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Harold Nsekela (hayupo pichani). Kutoka kulia ni Katibu Mtendaji (NACTE) Dkt Adolf Babiligi Rutayuga, Mkurugenzi wa Habari, Utafiti na Mipango Dkt. Marcelina Aloyce Baitilwake na Mkurugenzi wa Ushauri na Usaidizi wa Vyuo vya Ufundi Mhandisi Dkt. Gemma Kishari Modu.  Kamishna wa Maadili Mhe. Harold Nsekela wa pili kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Wakuu wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi nchini (NACTE). Wengine Kutoka kulia ni Katibu Mtendaji (NACTE) Dkt Adolf Babiligi Rutayuga, anayefuata baada ya Kamishna wa Maadili ni Mkurugenzi wa Habari, Utafiti na Mipango Dkt. Marcelina Aloyce Baitilwake na Mkurugenzi wa Habari, Utafiti na Mipango Dkt. Marcelina Aloyce Baitilwake

  …………………………..

  Kamishna wa Maadili Mhe. Harold Nsekela amewataka viongozi wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kujiepusha kupokea zawadi wakati wanapotekeleza majukumu yao.

  Wito huo aliutoa wakati akiwaapisha Kiapo cha Uadilifu Viongozi wakuu wa Baraza hilo wakiongozwa na Katibu Mtendaji Dkt. Adolf Babiligi Rutayuga katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili jijini Dar es Salaam.

  Mhe. Kamishna alisema kuwa Sekretarieti ya Maadili ipo katika mchakato wa kulifanyia kazi jambo hilo ambapo viongozi wa umma watatakiwa kutamka katika fomu zao zawadi wanazopokea ili kuwapa urahisi Sekretarieti kufuatilia jambo hilo kwa ukaribu zaidi.

  Akinukuu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya 1995, kifungu cha 12(2) kinachosema kuwa Kiongozi wa umma pale atakapopokea zawadi yenye thamani inayozidi shilingi 200,000/= atatakiwa kutaja zawadi aliyopokea na thamani yake na kukabidhi zawadi hiyo kwa Afisa Mhasibu wa Ofisi inayohusika ambaye atatoa maagizo kwa maandishi kuhusu matumizi ya zawadi hiyo au jinsi ya kuishughulikia kwa njia nyingine yeyote. Alifafanua Mhe. Nsekela. Hata hivyo Mhe. Nsekela aliwaasa viongozi hao kujiepusha kupokea zawadi kwa namna yeyote ile.

  Kuhusu Kiapo cha Uadilifu ambacho aliwaapisha viongozi hao, Mhe. Nsekela aliwaasha viongozi hao kuzingatia vipengele vyote 12 ambavyo walikiri mbele yake na kwamba hizo ni taratibu za ajira zao na sio mageni katika utumishi wa umma. Aidha, Mhe. Nsekela aliwataka viongozi hao kujiepusha kutumia vibaya madaraka yao na badala yake wafanye kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zinazowaongoza.

  Pia, Mhe. Nsekela aliwakumbusha viongozi hao kutoa Matamko ya Rasilimali na Madeni yao, ya Wenza wao pamoja na Watoto wao ambao wana umri chini ya miaka 18 kwa mujibu wa Sheria. Sambamba na hilo, Kamishna wa Maadili alitumia fursa hiyo kuwaomba wenza wa viongozi hususani wanaume kutoa ushirikiano wakati wa zoezi la uhakiki wa Rasilimali na Madeni ya Viongozi linapofanyika.

  Viongozi wengine walioapishwa Kiapo cha Uadilifu na Kamishna wa Maadili ukiacha Dkt. Adolf Babiligi Rutayuga ambaye ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo ni Mkurugenzi wa Habari, Utafiti na Mipango Dkt Marcelina Aloyce Baitilwake na Mkurugenzi wa Ushauri na Usaidizi wa Vyuo vya Ufundi Mhandisi, Dkt. Gemma Kishari Modu.

  0 0


  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari na wajumbe wa Baraza hilo, ambapo aliwataka madereva wa magari ya Serikali kufuata sheria za barabarani na atakaye vunja sheria hizo atakamatwa, atawekwa mahabusu, kuwapeleka mahakamani  pamoja na kuwaondolea sifa za madaraja C na E kwenye leseni zao na hivyo na hivyo kukosa sifa za kuendesha magari hayo. Kushoto meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Elius Kwandikwa. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambaye pia ni Katibu wa Baraza hilo, Fortunatus Musilimu. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma, jana.
  PIX 2
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari na wajumbe wa Baraza hilo, ambapo aliwataka madereva wa magari ya Serikali kufuata sheria za barabarani na atakaye vunja sheria hizo atakamatwa, atawekwa mahabusu, kuwapeleka mahakamani  pamoja na kuwaondolea sifa za madaraja C na E kwenye leseni zao na hivyo na hivyo kukosa sifa za kuendesha magari hayo. Kushoto meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Elius Kwandikwa. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambaye pia ni Katibu wa Baraza hilo, Fortunatus Musilimu. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma, jana.
  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  ……………………..

  Na.Alex Sonna,Dodoma

  Kufuatia ongezeko  la magari yanayoendeshwa na madereva wa Serikali kupata ajali, Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Tanzania limeibuka na  kutoa tamko la kufuatilia na kuhakikisha madereva wanaoendesha magari ya viongozi wa Serikali wanapata mafunzo ya kuwaendesha viongozi hao.

  Akizungumzana na waandishi wa habari Jijini Dodoma Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo,Hamadi Masauni wakati akitoa tamko la kwanza mara baada ya kuchaguliwa kwa baraza hilo  huku akiwa ameongoza na Makamu Mwenyekiti wa baraza,Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Elias Kwandikwa na wajumbe wengine wa Baraza hilo.

  Mhe.Masauni amesema kuwa baraza lilopita lilifanya kazi nzuri ila baraza jipya lina malengo yake ya kupunguza ajali nchini hasa za viongozi wa Serikari kwa kuwafuatilia na kuhakikisha madereva wanaoendesha magari hayo wanapata mafunzo ya kuwaendesha viongozi hao.

  Aidha amesema kuwa kwa sasa wanaishauri Serikali kutoa waraka maalum utakaosaidia kuwadhibiti viongozi ambao wanatoa maelekezo kwa madereva wakimbize magari kwa mwendokasi na malengo ya baraza hilo ni kuimarisha utendaji wa kamati za usalama za mikoa na kuweka mikakati ya pamoja ya utendaji na usimamiaji wa majukumu ya kamati hizo.

  “Kudhibiti mwendokasi na kuovateki kunakofanywa na madereva wa magari kwa kuwakamata,kuwaweka mahabusu na kuwaondolea sifa za madaraja C na E kwenye leseni zao hivyo kukosa sifa ya kuondesha magari hayo,”amesema Masauni

  Amesema kuwa baraza hili lina malengo mengi ya kufanya utafiti na kutoa ushauri kwa Serikali kuhusu ukaguzi wa alama za magari,kuongeza muda wa kutoa huduma,kwa mabasi ya abiria ya masafa marefu.Mhe.Masauni amesema kuwa Pikipiki za kubeba abiria kuwa na tela,ushauri ambao unazingatia matumizi ya vyombo hivyo barabarani,mazingira ya barabara yanayotumika na madhara ambayo yanaweza kujitokeza.

  Naibu Waziri amesema kuwa kazi kubwa ya mwendelezo wa baraza jipya ni kufanya utafiti wa vyanzo vya ajali na kuchukua hatua na kuishauri Serikali hatua mbadala za kuchukua.Kwa upande wake Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini,Fortunatus Muslim,aliwashangaa wale wanaohoji utendaji kazi wa Trafiki nchini katika kupiga tochi, huku akidai kwamba wao huwa hawapangiwi wafanyaje kazi kinachotakiwa ni madereva kufuata sheria
  Hivyo amesema kuwa Trafiki hatakiwi kupangiwa kazi kwani wao wanafanya kazi kubwa na kuwashangaa watu wana hoji hoji tu,nawaambia nyakua nyakua inaendelea nchini kwa wale wanaokiuka sheria za barabarani.

  Aidha amesema kuwa kuhusiana na misafara ya viongozi kukimbia,misafara hiyo inataratibu zake ikiwemo kuweka askari katika kingo za barabara za kuingia barabara kuu hivyo inakuwa rahisi kuzuia watu wenye magari na pikipiki kuuvamia msafara huo

  0 0

  NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO 

  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema serikali itafuatilia baadhi ya wafanyabiashara wanaodaiwa kuingiza bidhaa feki na kuuuza kwa gharama nafuu hali inayosababisha kushusha soko la ndani. 

  Akizindua kiwanda cha African Dragon kinachotengeneza malighafi ya mabati, Zinga wilayani Bagamoyo mkoani Pwani kilichojengwa kwa thamani ya bilioni 11 ,alisema kuwa suala hilo amelichukua na kuahidi kulifanyiwa kazi.

  Alieleza, kwa hali hiyo inakatisha tamaa na jitihada za wawekezaji wa ndani katika juhudi za serikali kuhamasisha wawekezaji kuwekeza nchini. Samia alielezea ,sekta ya viwanda kwa sasa ndiyo mpango wa serikali wa kihakikisha nchi inakuwa kwenye uchumi wa kati kupitia viwanda."Ofisi yangu imelichukua suala hilo na italishughulikia "alisisitiza Samia. 

  Hata hivyo Samia, aliwaasa wazazi na walezi kusimamia vijana wao kupata elimu ya ujuzi wa kuweza kuajiriwa ili kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira. 
  Alipongeza mkoa wa Pwani kwa kuongoza kwa kusheheni viwanda kitaifa, amewaomba kujipanga na kuvutia wawekezaji katika mkoa, kwani sio kazi rahisi. 

  "Katika utekelezaji wa Uchumi wa viwanda ,mtoe ushirikiano kwa wawekezaji ili kuweza kutimiza malengo ya serikali ya kuelekea uchumi wa kati "alieleza Samia. Akimkaribisha makamu wa Rais, Mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo alisema mkoa huo, una jumla ya viwanda 429 ikiwemo vya kati, vikubwa na vidogo ,na kutengeneza ajira za moja kwa moja zaidi ya 20,000 na kunufaika na ushuru na kodi inazolipa viwanda hivyo. 

  Ndikilo alieleza, moja ya changamoto ni ukosefu wa soko ambapo kwa Bagamoyo tayari viwanda viwili ikiwemo cha nguzo za zege za umeme kimefungwa na kiwanda cha viungo macho kimesimamisha uzalishaji. Alieleza umeme uliopo ni megawatts 62 mahitaji ni 79 kimkoa, wanapengo la megawatts 17 ili kupata umeme wa kutosha .

  Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Siling Soun alisema ,kilianzishwa 2015 ,kimegharimu bilioni 11 ikiwa ni gharama za mitambo na ujenzi. Alisema, kwasasa wameshatoa ajira 50 za moja kwa moja na kulipa ushuru wa halmashauri milioni 30 mwezi june mwaka huu. 

  Soun alitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na kukatika kwa umeme na kusababisha hasara ya milioni mbili pamoja na soko kuwa sio la uhakika kutokana na uingizwaji wa bidhaa feki zinazonunuliwa na kuingizwa kutoka nje ya nchi na kuuzwa kwa gharama nafuu. 

  Alitaja ,changamoto nyingine ni miundombinu mibovu hali inayosababisha usafirishaji kuwa sio rafiki. Akijibu changamoto za umeme, Naibu waziri wa nishati,Subira Mgalu alisema katika kutatua changamoto kiwandani hapo, wanatarajia kupunguza tatizo hilo kupitia ujenzi wa umeme kutoka Tegeta hadi eneo la uwekezaji (EPZA )Bagamoyo. 

  Alisema, kwenye masuala ya miundombinu ya umeme wameshaanza kutatua changamoto hizo kwa kuanzishwa miradi mikubwa ya umeme nchini ikiwemo stiglers gorge huko kwenye maporomoko ya mto Rufiji. Samia yupo kwenye ziara ya kikazi ya siku sita mkoani Pwani, oktoba 24 alikuwa Bagamoyo na oktoba 25 ataendelea Bagamoyo na Chalinze ambapo oktoba 29 itamalizika. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi waliojitokeza kumsikiliza alipotembelea eneo la Mbegani itakapojengwa Bandari Mpya ya Bagamoyo ikiwa siku ya kwanza ya ziara yake ya siku sita ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyeshwa mchoro na kupata maelezo ya itakavyokuwa Bandari Mpya ya Bagamoyo kutoka kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Mhandisi Karim Mataka ikiwa siku ya kwanza ya ziara yake ya siku sita ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0  0 0

  Ahmed Mahmoud Arusha

  Taasisi ya mfuko wa mgunduzi wa madini ya Tanzanite inatarajia kufanya Tamasha na maonyesho ya madini ya Tanzanite lengo likiwa ni kumuenzi mgunduzi wa madini hayo Mzee Jumanne Ngoma.

  Hayo yameelezwa na mwenyekiti mtendaji wa Taasisi hiyo Bi Asha Ngoma alipokuwa akiongea na wadau wa sekta ya madini mkoani hapa na kueleza kuwa katika tamasha hilo watashiriki kuonyesha zana mbalimbali alizokuwa akitumia mgunduzi huyo pamoja na madini aliyowahi kupata.

  Amesema kuwa lengo la kikao kuongea na wadau kuhusu uandaaji wa tamasha la madini hayo ambapo maonyesho hayo kutangaza nchi ili madini hayo yajulikane yanatoka hapa nchini kwani sekta hiyo na wadau wake watanufaika kutokana na maonyesho hayo.

  “Tunaenda kukutana na Serikali kwani wadau wamefurahia kuaandaa tamasha hili kutimiza miaka 50 tokea kugunduliwa kwa madini ya tanzanite na maonyesho hayo yatafanyika mwezi wa 12 tarehe 6-8 mwaka huu”alisema Ngoma.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wa madini na vito hapa nchini(Tamida) Sammy Mollel alisema kuwa tamasha hilo limekuja wakati muafaka na kuunga mkono uwepo wa tamasha hilo kwani litasaidia ukuaji wa kiuchumi na udhibiti wa madini ya Tanzanite ambapo madini haya yanatoka hapa nchini pekee amhali yalipogunduliwa madini hayo.

  Amesema kuwa kutakuwa na maonyesho ya uzaji na ununuzi wa madini ya vito na pia kutembelea sehemu ambayo yaligunduliwa madini hayo ambapo tunatarajia kujenga mnara wa kuenzi ugunduzi wa madini hayo eneo hilo na tunaendelea kumpongeza mh.Rais kwa kujenga ukuta ambao unadhibiti madini hayo.

  Aidha kwa upande mwingine Makamu mwenyekiti wa wafanyabiashara wa madini ya vito Tamida Thomas Munnisi alisema kuwa ni jambo jema kwa tamasha hilo kuweza kuenzi kazi nzuri ya Mzee Jumanne Ngoma na wadau wa madini ya Tanzanite wana wajibu mkubwa kuweza kuonyesha kwa vitendo kuunga mkono kazi hiyo kwa kufanya Harambee kuunga mkono juhudi zake kama mh.Rais Dkt.John Magufuri alipoweza kumchangia million 100.

  Alieleza jusikitishwa kwake na wachimbaji na wafanyabiashara wa madini hayo kumsahau mgunduzi hiyo Mzee jumanne ngoma kwa mchango wake kwani alitumia uwezo na rasilimali zake katika kugundua madini hayo ambayo yameweza kuwatajirisha watu wengi ilhali yeye akibakia maskini.

  “Naipongeza Taasisi hii ya mgunduzi wa madini ya Tanzanite kwa uamuzi wao wa kuaandaa tamasha hilo ambalo litakuwa na maslahi mapana kwa taifa na wadau wa sekta ya madini ya vito nchini napenda kuishauri tamasha hilo likafanyika eneo la merelani ndani ya ukuta au nje ya ukuta lengo ni serikali kupata mapato yake”alisisitiza Munisi

  0 0

  Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ameelekeza timu ya wataalam wa maji kutoka Wizara ya Maji kukagua miradi yote ya maji katika wilaya ya Mbulu mkoani Manyara na kuainisha changamoto za miradi hiyo na namna ya kuzimaliza ili wananchi wapate huduma ya majisafi na salama kama Serikali ilivyopanga. 

  Mhe. Aweso ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara ya kikazi katika Wilaya ya Mbulu ambapo amekagua mradi wa maji wa Arri, mradi wa maji Mongahay – Tumati, na mradi wa maji Dongobesh. 

  Mhe. Aweso (Mb) amesema miradi hiyo imechukua muda mrefu kukamilika wakati wananchi wanapata adha ya kutokua na uhakika wa majisafi na salama kwasababu mahitaji yameongezeka. Amesema baadhi ya miradi wamepewa wakandarasi wasio na uzoefu wa kutosha hivyo kushindwa kuikamilisha kama kwa mujibu wa mikataba waliyopewa. 

  Waziri Aweso (Mb) akiongea na wakazi wa Mbulu amesema hatavumilia kuona rasilimali za serikali zinatumika vibaya katika sekta ya maji, na kuainisha kuwa wakandarasi wanaoharibu miradi ya maji, watachukuliwa hatua za kisheria, pamoja na kufungiwa kushiriki kazi yoyote inayohusu sekta ya maji hapa nchini. 

  Pamoja na hilo, Mhe. Aweso (Mb) ameelekeza Jumuiya za Watumia Maji nchini zisajiliwe, na ziweke mikakati ya kutunza miradi ya maji ili idumu na kuwa endelevu. Aidha, viongozi wawashirikishe waanchi kulinda vyanzo vya  maji na watoe elimu zaidi ili kuzuia kazi ya aina yoyote katika vyanzo vya maji ndani ya umbali wa mita 60. Aidha, Mhe. Aweso (Mb) ameagiza fedha za dharura kiasi cha shilingi milioni 60 zitumike kuchimba kisima cha maji kwa wakazi wa Haydom. 
   Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb), anayetizama kamera, akiwa katika mradi wa maji wa Mongahay – Tumati wilayani Mbulu, ameagiza wataalam wa maji kutoka Wizara ya Maji kukagua miradi yote ya maji wilayani Mbulu ili kubaini changamoto za kitaalam na kutoa ushauri kuhusu namna ya kukamilika kwa miradi hiyo mara moja ili huduma ya majisafi iwafikie wananchi kwa uhakika. 
   Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiangalia upatikanaji majisafi na salama kwa wananchi katika kioski cha Kwa Zacharia mjini Hanang’. Hata hivyo, Waziri Aweso ameelekeza miradi ya maji ikaguliwe kwasababu kiwango chaupatikanaji maji wilayani Mbulu hakitoshi. 
  Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akipewa maelezo kuhusu mradi wa maji wa Dongobesh kutoka kwa mtalaam wa maji wa wilaya ya Mbulu Onesmo Mwakasege.
  Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akishiriki kazi ya kuchimba mtaro kupata nafasi ya kukarabati bomba linalosambaza maji kwa wananchi katika mtaa wa Stendi ya zamani, mjini Haydom Mbulu. 
  Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb), watatu kushoto mstari wa mbele-meza kuu, akiwa katika moja ya mkutano wa hadhara wilayani Mbulu. Pichani ni katika uwanja wa kata wa Haydom
  .

  0 0

  Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, CHINA

  Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi Jumatano Oktoba 24, 2018 ametembelea magazeti ya People's Daily Online na China Daily nchini China kwa lengo la kujifunza na kujadiliana namna bora zaidi ya kushirikiana katika sekta ya habari.

  Akiwa katika vyombo hivyo, Dkt. Abbasi amesema kuwa China na Tanzania zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu kwenye masuala mbalimbali hivyo ni muda sasa wa kufanyia kazi mkataba wa ushirikiano wa Tanzania na China kwenye masuala ya utamaduni na habari uliosainiwa mwaka 2016

  "Lengo la ziara yetu ni kujifunza wenzetu mnavyofanya kazi na pia kutafuta namna ya kuweza kufanya kazi kwa pamoja katika sekta ya habari," ameongeza Dkt. Abbasi akiwa People's Daily. Amelitaka gazeti hilo linalomilikiwa na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na linalofikisha habari zake kwa wasomaji milioni 700 duniani kupitia mitandao mbalimbali kuenzi ushirikiano huo wa muda mrefu kwa kuzipa nafasi pia habari za maendeleo za Afrika na Tanzania.

  Kwa upande wake Meneja Mawasiliano wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Bw. Pascal Shelutete amewakumbusha viongozi wa chombo hicho kuzipa fursa habari za utalii hasa vivutio vingi vilivyoko Tanzania. Akiwa katika gazeti la China Daily lililoanzishwa na Serikali ya China zaidi ya miongo mitatu iliyopita, Dkt. Abbasi aliwaeleza wahariri wanaohusika na toleo maalum la Afrika kuzingatia kuwa nchi nyingi za Afrika hasa Tanzania zina maendeleo na vivutio vya uwekezaji vinavyopaswa kujulikana kwa wekezaji wengi wa China maombi ambayo wahariri wa gazeti hilo waliyakubali.

  Dkt. Abbasi anaendelea na ziara yake ambapo atatembelea television za China za CCTV na CGTN na baadaye kufanya mahojiano na Idhaa ya Kiswahili ya Redio China.

  Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi Jumatano akifafanua jambo wakati kwenye kikao cha pamoja mara baada ya kutembelea waendeshaji wa magazeti ya People's Daily Online na China Daily nchini China kwa lengo la kujifunza na kujadiliana namna bora zaidi ya kushirikiana katika sekta ya habari.

  Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi sambamba na Ujumbe wake wakiwa kwenye kikao cha pamoja na baadhi ya Waendeshaji wa magazeti ya People's Daily Online na China Daily nchini China kwa lengo la kujifunza na kujadiliana namna bora zaidi ya kushirikiana katika sekta ya habari.
  Baaadhi ya waendeshaji wa magazeti ya People's Daily Online na China Daily nchini China wakifafanua jambo kwa wageni wao kutoka nchini Tanzania (hawapo pichani) wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi,wakati wa kikao chao cha pamoja na kuzungumza mambo mbalimbali kwa kwa lengo la kujifunza na kujadiliana namna bora zaidi ya kushirikiana katika sekta ya habari.
  Picha ya pamoja
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi ( wanne pichani) akiwa na ujumbe wake ambapo Jumatano Oktoba 24, 2018 walitembelea magazeti ya People's Daily Online na China Daily nchini China kwa lengo la kujifunza na kujadiliana namna bora zaidi ya kushirikiana katika sekta ya habari.

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mhe. Mwanamvua Mlindoko, wakati alipowasilia wilayani Uvinza Tarafa ya Nguruka mkoani Kigoma Jana 24/10/2018, kwa lengo la kuzungumza na wananchi kufuatia tukio la kushambuliwa na kuuawa kwa askari wawili na wingine mmoja kujeruhiwa wakati wakitekeleza zoezi la kuwaondoa wananchi waliovamia eneo la Ufugaji Ranchi ya Taifa NARCO kwa kuendesha shughuli za kilimo kinyume cha sheria na taratibu za nchi. Picha na Jeshi la Polisi.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akizungumza na wananchi (hawapo Pichani) wa Tarafa ya Nguruka wilayani Uvinza mkoani Kigoma Jana 24/10/2018, na kuwataka kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kufichua uhalifu na wahalifu pamoja na watu wanaojihusisha na matukio ya mauaji ili waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria. Picha na Jeshi la Polisi.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akiondoka baada ya kumaliza mkutano na wananchi wa Tarafa ya Nguruka wilayani Uvinza mkoani Kigoma Jana 24/10/2018, ambapo IGP Sirro, aliwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa sahihi zitakazofanikisha kukamatwa kwa watu waliojihusisha na tukio la kuwashambulia na kuwaua askari wawili na wananchi wawili wilayani humo.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akiondoka baada ya kumaliza mkutano na wananchi wa Tarafa ya Nguruka wilayani Uvinza mkoani Kigoma Jana 24/10/2018, ambapo IGP Sirro, aliwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa sahihi zitakazofanikisha kukamatwa kwa watu waliojihusisha na tukio la kuwashambulia na kuwaua askari wawili na wananchi wawili wilayani humo. Picha na Jeshi la Polisi.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Hai, Bw. Lengai Ole Sabaya akizindua rasmi duka la Vodacom Tanzania jana wilayani hapo ikiwa ni mpango wa kuhahakikisha wanafikia wateja wao wote, popote walipo. Kando yake ni Agripina Boisafi, Mkuu wa Duka hilo. 
  Picha 3648: Mkuu wa Wilaya ya Hai, Bw Lengai Ole Sabaya akisaini kitabu cha kumbukumbu baada ya kuzindua duka la Vodacom Tanzania wilayani hapo jana. Wa tatu kulia ni Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kazkazini, Brigita Steven na Mkuu wa duka hilo, Bi Agripina Boisafi (wa kwanza kushoto) pamoja na wafanyakazi wa Vodacom.

  0 0

  Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.

  Hatimaye Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa anayekabiliwa na kesi ya uchochezi pamoja na viongizi wenzake nane wa Chadema, leo amepata wakili wa kumtetea dhidi ya kesi hiyo inayounguruma katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, 

  wakili Jamuhuri Johnson amejitambulisha leo Oktoba 25.2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri wakati kesi hiyo ilipokuja leo kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali (PH).Hatua hiyo imefikwa baada ya Wakili aliyekuwa akimtetea Msigwa, Jeremiah Mtobesya kujitoa Agosti 23, mwaka huu.

  Wakili Jamuhuri amedai kulingana na umuhimu wa kesi hiyo ameomba ahirisho ili apate muda wa kupitia jalada la kesi hiyo na na pia ameomba kupatiwa mwenendo mzima wa kesi tangia ilipoanza ili aweze kumwakilisha mteja wake huyo vizuri.

  Wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi aliiomba mahakama kutupilia mbali maombi hayo ya wakili Jamuhuri na kudai kuwa wanapinga kwa sababu kwa kuangalia mwenendo wa kesi hiyo ni wazi katika kesi ya msingi hakuna hatua yoyote iliyopigwa zaidi ya washtakiwa kusomewa mashtaka yanayowakabili.

  Katika kuwasomea washtakiwa Maelezo ya awali (PH) wahusika wakuu ni washtakiwa ambao wakisomewa ndiyo wanawajibu wa kujibu kipi wanakubali na kipi hawakikubali. Baada ya Nchimbi kueleza hayo, wakili wa Msigwa, Jonson alieleza kuwa mteja wake siyo mwanasheria kuna maelezo ambayo amempatia hayaelewi vizuri ndiyo sababu aliomba kupitia jalada.

  Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba Mosi, mwaka huu asubuhi kwa ajili ya PH.Mbali na Msigwa washtakiwa wengine ni ambao wanatetewa na Wakili Kibatala ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika, mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, mbunge wa bunda, Esther Bulaya, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko na katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji.

  Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari 1 na 16, 2018, Dar es Salaam.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila (wa pili kushoto) akikabidhi cheti cha shukrani kwa Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Kusini, Salema Kileo kutokana na udhamini wa benki hiyo katika maonyesho ya mifuko ya uwezeshaji, programu na vikundi vya kifedha yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) katika hafla ya ufungaji rasmi wa maonyesho hayo katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe mjini Mbeya leo. Kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa huo, Mariam Mtunguja. 
  Mkuu wa Uhai wa Wateja wa NBC Tanzania, Gaudence Shawa (kulia) akizungumza na Mshauri wa Kilimo na Huduma za Fedha Vijijini wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT), Samora Lupalla (katikati) huku Ofisa Habari wa mfuko huo, Victor Kyando akiangalia katika hafla ya ufungaji rasmi wa maonyesho hayo katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe mjini Mbeya leo. Kushoto ni Meneja Mahusiano wa NBC Tanzania, William Kallaghe. 
  Baadhi ya wafanyakazi wa NBC Mkoa wa Tawi la Mbeya wakihudhuria hafla ya ufungaji wa meonyesho hayo katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe mjini humo leo.

older | 1 | .... | 1706 | 1707 | (Page 1708) | 1709 | 1710 | .... | 1903 | newer