Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1704 | 1705 | (Page 1706) | 1707 | 1708 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Naibu Spika wa Bunge Mh. Dkt. Tulia Ackson akimwakilisha Spika wa Bunge Mh. Job Ndungai aliongoza Harambee ya changizo la fedha kwa ajili ya maendeleo  chuo cha St. Mark’s ambacho kipo Buguruni Malapa Jijini Dar es Salaam.

  Katika harambee hiyo Dkt. Tulia aliwezesha kuchangisha Tsh Milioni 284 kwa umahili mkubwa ambapo alitumia njia mbalimbali pamoja na  mistari  ya Bibilia ambayo iliwahamasisha watu wengi kuchangia jambo ambalo wengi hawakutarajia.

  Katika harambee hiyo pamoja na waumini na wageni mbalimbali kuhamasishwa kuchangia fedha hizo  na  Dkt. Tulia, lakini pia bila woga aliwabana Maaskofu, wachungaji na wainjilisti ili wapate kuchangia katika harambee  hiyo.

  Naibu Spika wa Bunge Mh. Dkt Tulia Ackson akizindua rasmi harambee ya kuchangia maendeleo ya chuo cha St. Mark's ambapo alisema kuwa yeye hato ongea mengi zaidi ya kukusanya fedha kwa kuwa jambo hilo ni muhimu.
   Baba Askofu Afidh abeid (aliyeshika kipaza sauti) akiomba kwa ajili ya ufunguzi wa Harambee ya kuchangia fedha za maboresho chuo hicho
  Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Dkt. Maimbo Mdolwa akitoa neno la Shukurani kwa Mgeni rasmi Naibu Spika wa Bunge Mh. Dkt Tulia Ackson  kwa kukubali kuungana nao katika harambee ya kuchangia fedha  kwa ajili ya maendeleo ya chuo hicho.
  Kaimu Mkuu wa Chuo cha St. John Prof. Emmanuel Mbennah akizungumzia kuhusu maudhui na nia ya kufanya harambee ya kupata fedha kwa ajili ya maendeleo  ya chuo cha St. Mark's
  Mwenyekiti wa Kamati ya kuchangisha fedha za maboresho ya Chuo cha ST. Mark's Jaji Mkuu Mstaafu Mh. Agustino Ramadhani akielezea historia ya chuo cha St. Mark's tangia kilipo anzia hadi sasa.
  Mgeni rasmi  Naibu Spika wa Bunge Mh. Dkt Tulia Ackson(Kushoto) akipokea zawadi kutoka chuo cha St. Mark's
   Mgeni Rasmi Naibu Spika wa Bunge Mh. Dkt Tulia Ackson pamoja na Meza kuu wakitoa mkono wa salam wakati waumini na wageni waalikwa walipokuwa wakitoa sadaka.
  Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha St. Mark's Dkt. Peter Kopweh akizungumza jambo wakati wa Harambee ya kuchangiza fedha za Maboresho ya chuo hicho.
  Mh. Balozi Lupia akizungumza jambo wakati wa Harambee ya kuchangia maendeleo ya chuo hicho
  Baadhi ya watu wakitoa ahadi pamoja na michango yao
  Sr. akitoa neno pamoja na maombi wakati wa harambee ya kuchangisha  fedha kwa ajili maboresho ya chuo hicho.
  Mgeni Rasmi Naibu Spika wa Bunge Mh. Dkt Tulia Ackson akionesha picha ambayo allichorwa na mmoja muumini wa Kanisa la Anglikana.
  Mgeni Rasmi Naibu Spika wa Bunge  Mh. Dkt Tulia Ackson, akipokea kwa niaba picha ya Spika wa Bunge Mh. Job Ndungai.
  Baadhi ya Wachungaji pamoja na watumishi wengine ambao wanasomea Uchungaji wakiwa katika Harambee hiyo.
  Waumini, Waalikwa  mbalimbali pamoja na watumishi wa Chuo cha St. Mark's wakiwa katika Harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya maboresho ya Chuo hicho.
  Kwa ambao wangependa kuchangia wanaweza kutumia njia zifuatazo

  TIGO PESA : 0677058716

  CRDB BANK: 0150237155300 (HOLLAND BRANCH)

  TIB : 004600000860601 (SAMORA DAR ES SALAAM)

  (Picha zote na Fredy Njeje)

  0 0

  Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

  MEYA  Mstaafu  wa Manispaa ya Kinondoni Yusufu Mwenda amempongeza Rais John Magufuli kwa kuruhusu mfumo wa elimu ya bure  katika shule za Msingi na Sekondari na kuwataka wazazi kushirikiana na shule hizo katika maendeleo mbalimbali.

  Akizungumza katika mahafali ya kwanza ya  Shule ya Sekondari ya Mikocheni,Mwenda alisema hatua hiyo ya Rais Magufuli imesaidia wanafunzi pamoja na wazazi wengi kunufahika na elimu hiyo.

  Alisema ukilinganisha na miaka ya nyuma,hivi sasa wanafunzi wengi  wanapata elimu tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma ambapo wengi waliikosa kutokana na kushindwa kulipia ada za shule.Mwenda alisema katika kipindi kifupi cha uongozi wake tangu aingie madarakani, amejenga shule nyingi katika kata mbalimbali, jambo lililowawezesha wanafunzi wengi na jamii kunufahika.

  "Kinachotakiwa kwa sasa ni wazazi kutoa ushirikiano kwa shule hizo ili ziweze kupata nguvu ya kusonga mbele kimaendeleo na kuinua kiwango cha elimu nchini alisema Mwenda.Aliwataka wazazi pia kutambua kuwa licha ya Serikali kutoa elimu  bure, bado wanapata kuchangia maendeleo ya shule hizo hatua itakayozisaidia kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo kuongeza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi.

  Aidha aliwapongeza wahitimu katika mahafali hayo na kuwataka kuwa mfano kwa kufanya vizuri katika mtihani wao mwisho na hivyo kufungua njia yao ya kimaisha lakini pia kuwapa hamasa wanafunzi waliobakia shuleni hapo. Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Salama Ndyetabura alisema shule hiyo iliyoanzishwa miaka minne iliyopita pamoja na mafanikio baadhi iliyoyafikia,bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa maabara.

  Alisema pamoja na changamoto hiyo,pia shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madras pamoja na walimu wa masomo ya sayansi suala aliliiomba Serikali kulitatua.Jumla ya wanafunzi 158 walihitimu katika mahafali hayo wakiwemo wavulana 79 na wasichana 79.

  0 0   Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe, Anthony Mtaka akizungumza na Waandishi wa Habari(hawapo pichani) , juu ya ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa, yatakayofanyika Oktoba 23-28, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
  PICHA B
  Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uwekezaji wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Shoma Kibende akizungumza katika Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe. Anthony Mtaka na Waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa, yatakayofanyika Oktoba 23-28, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
  PICHA C
  Baadhi ya Waandishi wa Habari na Maafisa na Mameneja wa SIDO wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe, Anthony Mtaka katika mkutano wake na Waandishi wa Habari, juu ya ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa, yatakayofanyika Oktoba 23-28, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
  PICHA D
  Baadhi ya Mameneja wa SIDO wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe, Anthony Mtaka katika mkutano wake na Waandishi wa Habari, juu ya ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa, yatakayofanyika Oktoba 23-28, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
  PICHA E
  Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Seif Shekalaghe  akizungumza katika Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe. Anthony Mtaka na Waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa, yatakayofanyika Oktoba 23-28, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
  PICHA F
  Meneja wa SIDO Mkoa wa Kagera  Richard Mahela  akizungumza katika Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe. Anthony Mtaka na Waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya ufunguzi wa Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa, yatakayofanyika Oktoba 23-28, 2018 katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu.
  ………………………….
  Na Stella Kalinga, Simiyu
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa wananchi mkoani humo na maeneo mengine nchini kujitokeza kwa wingi kushirikia katika  Maonesho ya Kitaifa ya Viwanda Vidogo (SIDO), yatakayofanyika kuanzia Oktoba 23-28, mwaka huu katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani humo na kubainisha kuwa Maandalizi yote yamekamilika.
  .Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Mtaka amesema Maonesho haya yatafunguliwa rasmi siku ya Jumanne Oktoba 23, 2018 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.
  Ameongeza kuwa katika maonesho hayo wajasiriamali, waoneshaji wa teknolojia mbalimbali wamealikwa na kusisitiza kuwa hii ni fursa kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu na mikoa mingine kuona ushindani katika uongezaji wa thamani wa mazao mbalimbali na fursa kwa wajasiriamali kujifunza kutoka kwa wenzao.
  “ Nitoe wito kwa wananchi wa mkoa wa Simiyu kujitokeza kushiriki maonesho haya maana hii ni fursa kwao ya kuweza kujielimisha katika maeneo mbalimbali ya teknolojia za viwanda hususani viwanda vidogo, lakini pia wajasiriamali watapata nafasi ya kujifunza kutoka kwa wenzao wa maeneo mengine nchini na nje ya nchi” alisema Mtaka.
  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uwekezaji wa  Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), Shoma Kibende amesema tayari wajasiriamali kutoka mikoa mbalimbali wamethibitisha kushiriki  maonesho hayo na baadhi yao wameanza kuwasili.
  “Wajasiriamali zaidi ya 1000 kutoka mikoa yote nchini wanatarajia kushiriki maonesho haya na baadhi yao wameshaanza kuwasili, lakini pia kuna taasisi mbalimbali ambazo ni taasisi shirikishi na SIDO, huduma za kupata ubora hii ni fursa pekee kwa Watanzania” alisema.
  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe amesema zaidi ya wajasiriamali 51 kutoka wilayani humo watashiriki katika kuonesha bidhaa mbalimbali ambazo wametengeneza na kuzalisha kupitia viwanda vidogo.
  Naye Meneja wa SIDO Mkoa wa Kagera,Richard Mahela amesema maonesho ya SIDO ambayo ni ya kwanza kufanyika Kitaifa  yatawasaidia wajasiriamali kote nchini kupanua masoko ya bidhaa zao kwa kuwa wameandaa vipeperushi vya bidhaa zao ambavyo  vitasambazwa kwa lengo la kusaidia kuwaunganisha na wanunuzi.
  Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa ambayo ni ya kwanza kufanyika ngazi ya Kitaifa yatafunguliwa rasmi Jumanne Oktoba 23, 2018 na kuhitimishwa siku ya Jumapili Oktoba 28, 2018 yakiwa na Kauli Mbiu: PAMOJA TUJENGE VIWANDA KUFIKIA UCHUMI WA KATI”.

  0 0


   Beatrice Mbawala (wa pili kushoto) akiangalia bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali kutoka kikundi cha Gogoni Vicoba Investor, wakati alipomwakilisha mkuu wa wilaya ya Ubungo jijini Dar es salaam, katika uzinduzi wa kikundi hicho, kilichopo kata ya Kibamba ,(wa kulia) ni mkufunzi wa vicoba kutoka taasisi ya Pamoja Entrepreneurship Support for Community  Development (Pescode) Enethlena Wadelanga
  IMG-20181021-WA0023
  Beatrice Mbawala akizungumza wakati alipomwakilisha mkuu wa wilaya ya Ubungo jijini Dar es salaam, katika uzinduzi wa kikundi cha Gogoni Vicoba Investor, kilichopo kata ya Kibamba.Picha na Mwamvua Mwinyi
  ……………………….
   
  NA MWAMVUA MWINYI,KIBAMBA.
   
  TAASISI mbalimbali za kifedha zimeaswa kutoa elimu kwa wajasiriamali kuhusiana na nidhamu ya matumizi ya fedha katika biashara zao ,kabla ya kuwakopesha ili waweze kunufaika na mikopo wanayowapatia.
   
  Pamoja na hayo, wajasiriamali hao wametakiwa kuwa wabunifu kwa kuzalisha bidhaa zilizo bora na kuhifadhiwa vizuri ili kuendana na soko la ushindani wa kibiashara.Hayo yalisemwa na Beatrice Mbawala ambae alimwakilisha mkuu wa wilaya ya Ubungo jijini Dar es salaam, wakati wa uzinduzi wa kikundi cha Gogoni Vicoba Investor, kilichopo kata ya Kibamba .Alieleza, elimu juu ya fedha wanazokopa wajasiriamali ni muhimu kwani baadhi yao wamekuwa wakifilisika kutokana na matumizi yasiyo sahihi ya fedha .
   
  Beatrice alisema kuwa ,baadhi ya wajasiriamali wameshindwa kufikia mafanikio  na kuwa wajasiriamali wakubwa kutokana na kushindwa kuwa na nidhamu ya fedha wanazokopa .“Akinamama ,wajasiriamali mliopo hapa mhakikishe mnakuwa waaminifu na kuwajali wateja wenu,kuzalisha bidhaa bora na kuacha kutumia mikopo mnayochukua kutafuta kiki mitaani,kwa kufanya ufahari”alieleza Beatrice.
   
  Nae mkufunzi wa vicoba kutoka taasisi ya Pamoja Entrepreneurship Support for Community  Development (Pescode) Enethlena Wadelanga alisema ,wanawapa mafunzo ya ujasiriamali kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi na kifikra na kujitetea kwa kuunganisha nguvu ujuzi na uzoefu.Alifafanua ,jamii inapaswa kuamka ili kuleta maendeleo kwa kuungana kwani vita ya kiuchumi ni ya pamoja kwa ajili ya kuboresha maisha kupitia shughuli zao za kila siku za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za kila mwanachama.  
   
  Enethlena alifafanua, wanatarajia kujenga ofisi kwa ajili ya kufanyia shughuli zao na kuanzisha ufugaji wa kuku na kuwaomba wadau kuwaunga mkono hasa taasisi za kifedha ili waweze kujiinua kiuchumi.Mwanachama Mariam Kawawa alisema kuwa wangehitaji kutengewa eneo kwa ajili ya wajasiriamali kufanyia kazi kuliko kila mtu kufanyia sehemu yake ambapo baadhi ya bidhaa huzalisha uchafua na kutupwa holela.
   
  Mariam alibainisha, kutokana na kujiunga kwenye vicoba hiyo ameweza kunufaika na mafunzo mbalimbali ambapo kwa sasa anazalisha bidhaa mbalimbali na kuweza kujikwamua kiuchumi huku akiwa ametoa ajira kwa watu wengine ambao anashirikiana nao.Gogoni Investor ilianzishwa mwaka mmoja uliopita na ina wanachama 50 ambao kuna makundi mawili A na B ikiwa na malengo ya kujikwamua kiuchumi .

  0 0

  SUALA la kujitambua na kutambua nini mahitaji yako ni moja ya chanzo cha mabadiliko yanayohitajika katika maisha, Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira-UNEP, Joyce Msuya amebainisha.

  Alisema hayo akizungumza na wanawake mbalimbali waliofika kusikiliza historia yake na jinsi alivyoweza kumudu maisha ya mama, mke na mfanyakazi katika mashirika mbalimbali ya kimataifa na kupanda ngazi.
  Aidha alisema pamoja na kujitambua mtu anatakiwa kufanya kazi kwa kuwajibika, kujisukuma zaidi katika kazi na kufanya maamuzi ya kushirikisha familia hasa patna.

  Msuya ambaye alianza kazi ya UNEP mwaka huu mwezi wa nane baada ya kupitia Benki ya dunia na mashirika mengine kadhaa alisema mfumo wa Tanzania wa shule, malezi ndiyo iliyofanya kuunganisha nguvu, uwezo na ujasiri wa kuweza kufanya mambo ambayo yamemfanya kupata nafasi kubwa zaidi.

  Alisema mfumo wa Tanzania wa maisha umekuwa msukukumo mkubwa kwake kwani  aliweza kuishi na watu tofauti na kuvumilia huku akitekeleza wajibu wake kwa kujiongeza zaidi.Alisema kutokana na juhuzi za wazazi wake katika kusimamia malezi aliweza kupata maarifa zaidi ya kuishi kwa kuhudhuria shule za umma za Forodhani, Jangwani na Weruweru kisha kuchukua mafunzo ya kijeshi katika kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa ( JKT) Mafinga na kumalizia mafunzo hayo Mlalakua.

  “Ukweli ni kuwa wazazi wangu walitaka tuishi maisha ya kawaida kama watanzania wengine ndiyo maana walinipeleka shule za bweni na kuhakikisha naenda jeshini. “ alisema Mkurugenzi huyo ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi.

  Anasema malezi ya kujitegemea yamemfanya awe na uwezo wa kufanya bajeti hali ambayo ilimwezesha kuishi vyema Scotland na hata alipoenda kuchukua shahada yake ya pili nchini Canada.“Kusema ukweli  Baba na mama walinitengenezea mfumo mzuri wa kuishi hasa pale walipojenga na kunihimiza kufanya kazi na kusoma wakati nikiwa mdogo.” Alisema Msuya.
  Anasema amevuka vigingi vingi hasa kwenye muwashawasha wa masomo lakini kama walivyo watu wote alifanya maamuzi makini kuzingatia ushauri na kile anachokipenda.

  Akiulizwa nini hasa kinamsukuma, alisema kwamba familia ni kitu muhimu kwake na kwamba amefanya mambo mengi akiwa na familia yake kuanzia mume wake ambaye wamo katika ndoa kwa miaka 20 na kujaliwa kuwa na watoto wawili.
   Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira-UNEP, Bi. Joyce Msuya akizungumza viongozi wanawake vijana kwenye mdahalo ambapo aliutumia kuhamasisha wanawake wengine kujituma uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bi. Natalie Boucly. 
   Mkurugenzi wa uendeshaji wa Doctors’ Plaza, Bi. Sophia Byanaku akiuliza swali kwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira-UNEP, Bi. Joyce Msuya (hayupo pichani) wakati wa mdahalo maalum kwa viongozi wanawake vijana ambapo walipata fursa ya kuhamasishwa kujituma na kujitambua uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya viongozi wanawake vijana walioshiriki kwenye mdahalo ulioendeshwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira-UNEP, Bi. Joyce Msuya (hayupo pichani) ambapo aliutumia kuhamasisha wanawake wengine kujituma uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam
  Baadhi ya viongozi wanawake vijana wakiuliza maswali kwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira-UNEP, Bi. Joyce Msuya (hayupo pichani) wakati wa mdahalo maalum uliotumika kuhamasisha wanawake wengine kujituma na kujitambua ambapo umefanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam
  Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira-UNEP, Bi. Joyce Msuya katika picha ya pamoja na viongozi wanawake vijana mara baada ya kumalizika kwa mdahalo huo uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam. 

  0 0

  Wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania PLC, kupitia mpango wake wa Pamoja na Vodacom leo wametoa msaada wa vifaa vya kusomea kwa Wanafunzi zaidi ya 150 wenye ulemavu katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya shule hiyo iliyoko Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam.

  Elimu bora kwa wote ni moja kati ya nguzo kuu za asasi ya Vodacom Tanzania Foundation hivyo msaada huu wa nyenzo za kujifunzia pamoja na vifaa mbalimbali vya elimu kwa ajili ya wasioona pamoja na wale wenye uoni hafifu utaisaidia shule kukabiliana na matakwa mbalimbali ya kuhudumia wanafunzi wenye mahitaji maalum.

  Upatikanaji wa vitabu vya nukta nundu (vitabu maalum kwa Wasioona) pamoja na maandiko mengine, ni hafifu na msaada huu utasaidia katika kupunguza ukubwa wa tatizo hili. Msaada huu kutoka kwa Wafanyakazi wa Vodacom unahusisha mashine kumi na karatasi maalum za kuchapia maandishi ya nukta nundu (Maandishi maalum kwa Wasioona), viti, faili za plastiki (maalum kwa ajili wasioona), vifaa hivi vitasaidia zaidi ya wanafunzi 67 wenye shida ya macho katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko. Kwa sasa Walimu wataweza kuandaa lesoni na vifaa maalum vya kufundishia kwa ajili ya wanafunzi wenye uoni hafifu. Zaidi ya hayo, Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC wamejitolea nguo, sabuni na vyakula mbalimbali ili kuwasaidia wanafunzi hao.

  Akizungumza kwa niaba ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom, Mkurugenzi wa Kanda ya Dar es Salaam na Pwani George Lugata alisema, “elimu ni haki ya msingi na kipengele muhimu cha malengo endelevu ya milenia, tunatambua mchango muhimu wa shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko katika kuwalea Watoto walio pembezoni wenye ulemavu kwa kuwapa elimu bora inayoendana na mahitaji ya wanafunzi.” 

  Asasi ya Vodacom Tanzania Foundation imekuwa ikitumiwa na wafanyakazi wa Vodacom kurejesha fadhila kwa jamii na kuwainua walio pembezoni wa jamii. Pamoja na Vodacom ni mojawapo kati ya mpango unaotumika, na kupitia mpango huu wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom wameweza kuwa mawakala wa mabadiliko kwa kuwasilisha changamoto zilizoko katika jamii yao. 

  “Tuna shauku ya kuisaidia jamii yetu, na huu umekuwa ni utaratibu wetu kwa miaka zaidi ya 12 kupitia Vodacom Tanzania Foundation,” alisema Lugata huku akiongeza kwamba hii ni mara ya pili kwa Vodacom kutoa msaada kwa shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ambapo mwaka 2011 walitoa msaada wa Shilingi 12 milioni ili kujenga mabweni na vyoo kwa ajili ya wanafunzi hao. 

  Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Naibu Waziri wa nchi, ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu (anayeshughulikia Walemavu) Stella Ikupa Alex aliishukuru kampuni ya Vodacom kwa msaada huo na kufafanua namna ambavyo msaada huo utasaidia kupunguza mzigo ambao serikali imekuwa ikiubeba kuihudumia shule hiyo huku akiomba taasisi zingine kufuata nyayo za Vodacom. 

  “Zaidi ya nusu ya watoto wenye ulemavu nchini hawaendi shule hii ikisababishwa na hali zao, kwa sasa Tanzania kuna Watoto 4.2 milioni wenye ulemavu,” alisema Naibu Waziri Stella Ikupa, “pamoja na maendeleo mazuri yaliyofanyika kutokana na juhudi mbalimbali lakini bado kuna watoto wenye ulemavu hawapelekwi shule, ila kwa msaada wa taasisi kama Vodacom Foundation tumeweza kuhakikisha kuwa idadi kubwa ya watoto wenye ulemavu hawaachwi pembezoni katika ulimwengu wa elimu,” aliongeza. 

  Mkuu wa shule hiyo, Anna Mshana alielezea furaha yake kwa niaba ya wanafunzi, “tumefurahishwa sana na ukarimu wa Wafanyakazi wa Vodacom, Zawadi zao zitatusaidia sana katika kufundisha na pia kuwawezesha wanafunzi wetu kuelewa kwa haraka yale wanayofundishwa maana wengi wa wanafunzi hawa wanatoka katika familia zenye kipato cha chini, alisema.


  Kamishna msaidizi watu wenye ulemavu, ofisi ya waziri mkuu, sera, bunge, ajira na watu wenye ulemavu, Beatrice Fungamo (Kushoto) akipokea moja ya mashine maalum za kuandikia maandishi ya nukta nundu (Braille) zilizotolewa jana na taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC wakiongozwa na mkurugenzi wa kanda ya Pwani George Lugata, vifaa hivyo vitaleta ufanisi katika kutoa elimu bora kwa wasioona na wale wenye uoni hafifu. 

  0 0

  Msanii Khery Sameer Rajabu maarufu kama Mr. Blue jana alimpandisha msanii Ali Kiba kwenye jukwaa la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga kwa kushirikiana nae kwenye wimbo wao uitwao MBOGA SABA . Mr Blue alianza kwa kusema "nataka niwape 'surprise"leo toka kwa ndugu yangu mwenye roho ya pekee aje apande hapa juu awasalimie na niimbe nae,". 
  Ndipo Kiba akapanda na kuulipua uwanja Mkwakwani kwa mayowe, baada ya kumalizika kwa wimbo huo Kiba alisalimia na kushuka jukwaani kitu ambacho mashabiki walitamani aendelee kuimba lakini hakuwa kwenye orodha.
  Kwa upande wa wasanii wengine Rostam na Maua Sama waliendeleza "Remix" yao ya IOKOTE na kuwapa mashabiki Vibe Lote. Nao kundi la Weusi kushirikiana na Nandy waliweza kuimba pamoja na kukonga nyoyo za mashabiki uwanja wa Mkwakwani.

  Tamasha la Tigo Fiesta linaambatana na shindano la kusaka vipaji lijulikanalo kama Tigo Fiesta Supa Nyota na kwa mkoa wa Tanga, msanii Faraji Majimoto aliibuka mshindi atayeiwakilisha mkoa wa Tanga. 

  Wadhamini wa Tamasha hilo Kampuni ya Tigo, wamewaletea wateja wao ofa kabambe ya intaneti wanaweza kuvuna hadi mara mbili ya thamani kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia *147*00#. Promosheni ya Data Kama Loteitahakikisha kuwa mashabiki wanaweza kufuatilia habari na matukio yote ya msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote; au kufurahia kuperuzi kwenye mtandao wenye kasi zaidi wa 4G+.

  Wateja wote wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi TSH 10 millioni, zawadi za kila wiki za TSH milioni moja, ama zawadi za kil asiku za TSH 100,000 kwa kushiriki katika shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo. Ushiriki katika shindano hilo unapatikana kwa kutuma neno MUZIKIkwenda 15571 au kwa kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz

  Tamasha hilo litaendelea ijumaa hii kwenye uwanja wa Kiruma mkoani Mwanza.
  0 0

   Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere akizungumza leo na watumishi wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi waliopo TRA Makao Makuu jijini Dar es Salaam juu ya uboreshaji wa huduma mbalimbali za walipakodi.
   Meneja wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Bw. Gabriel Mwangosi (katikati) akitoa maoni wakati wa kikao na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere kilichofanyika leo TRA Makao Makuu jijini Dar es Salaam.
   Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Bi. Agnes Kitwanga akifafanua jambo wakati wa kikao na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere kilichofanyika leo TRA Makao Makuu jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).

  0 0


  MUOGELEAJI nyota wa klabu ya kuogelea ya Morogoro, (Mis Piranha) , Dennis Mhini amepata nafasi ya kusoma na kujifunza mchezo wa kuogelea kwenye klabu maarufu ya St Felix ya Uingereza.

  Dennis aliyeiwakilisha Tanzania katika michezo ya Olimpiki ya Vijana nchini, Argentina amepata nafasi hiyo baada ya kufikiwa viwango vilivyowekwa na shule hiyo chini ya kocha maarufu, Sue Purchese.

  Kigezo cha kwanza ni ubora wake katika mchezo kuogelea baada ya kufikia muda unaotakiwa na pili uwezo wake wa darasani.

  Baba wa mchezaji huyo, Hamis Mhini alisema kuwa mwanaye pamoja na kutoweza kutwaa medali Argentina, alifanikiwa kupunguza muda wake wa kuogelea, jambo ambalo limewavutia sana walimu na kocha maarufu wa mchezo wa kuogelea nchini uingereza, Sue Purchase.

  Mhini alisema kuwa hatua hiyo ni kubwa katika maendeleo ya mchezo wa kuogelea nchini kwani anaamini kuwa mwanaye ataiva na kuwa muogeleaji bora Tanzania na dunia.

  Alisema kuwa Dennis anapenda sana mchezo wa kuogelea na ndiyo maana waliamua kumpa nafasi ya kufanya kile ambacho anakipenda na kufikia kiwango cha kufuzu michezo ya Olimpiki ya Vijana iliyofanika mjini Buenos Aires.

  Katika michezo hiyo, Dennis aliweza kushika nafasi ya tatu katika kundi la kwanza kweye staili ya freestyle ya mita 100 kwa kupata muda wa sekunde, 58.53 na pointi 514 na vile vile kumaliza katika nafasi ya tatu kwa upande staili ya backstroke kwa mita 50 kwa kutumia sekunde 29.79 na kupata pointi 525.
  Dennis alisema kuwa amefurahi sana kupata nafasi hiyo na kuahidi kufanya mambo makubwa kwa Taifa lake.

  Alisema kuwa atahakikisha anakuwa na kiwango cha kufuzu katika mashindano mbalimbali duniani ikiwa pamoja na Mashindano ya Dunia, Jumuiya ya Madola na Olimpiki ya wakubwa.Dennis Mhini (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na kocha Michael Livingstone (wa kwanza kulia) mara baada ya kuwasili kutoka Argentina. Wengine katika picha ni wanamichezo na viongozi.
  Kocha wa mchezo wa riadha, Mwinga Mwanjala (kulia) akimkabidhi shada la maua, Dennis Mhini (wa tatu kushoto) mara baada ya kuwasili kutoka Argentina kwa ajili ya mashindano ya Olimpiki ya vijana.
  Muogeleaji, Dennis Mhini (wa tatu kushoto) katika picha ya pamoja na wazazi wake, Hamis Mhini (wa kwanza kushoto), Bhoke Mukoji Mhini ( wa pili kushoto) mara baada ya kuwasili kutoka Argentina kwa ya mashindano ya vijana ya Olimpiki. Wa nne kushoto ni kocha wa timu ya Taifa, Michael Livingstone ambaye anafuatiwa na Eugenia Kaitesi, Derick Mhini. Pia katika picha ni Deborah Mhini (katikati).
  Timu ya Tanzania iliyoshriki katika mashindano ya vijana ya Olimpiki katika picha ya pamoja na makocha wao na mkuu wa msafara.

  0 0


  Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akiteta jambo na mtunzi wa kitabu Maida Waziri


  WATANZANIA wametakiwa kuwa na msukumo wa kuthubutu kuanzisha shughuli za ujasiriamali ambazo zitakua na kuleta tija kwake yeye mwenyewe na kwa taifa kwa ujumla.Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama katika hotuba iliyowasilishwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha ujasiriamali mwishoni mwa wiki.

  Mkuu wa itifaki Aman Christopher akiwaongoza Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulege (katikati) na mtunzi wa kitabu Maida Waziri .
  Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akisalimiana na mtunzi wa kitabu Maida Waziri katika Red Carpet .
  Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulege akiongozana na Maida na waziri na waalikwa wengine wanazuoni Dk Goodluck Urasa (kulia),Godfrey Sembeye na Kaimu Rais wa TCCIA Octavian Mshiu (kushoto) wakiiingia ukumbini tayari kwa uzinduzi .Alisema Serikali inahimiza watu kutumia fursa zilizopo nchini ambazo ni nyingi, kufanya ujasiriamali ili kukuza na kuuendeleza uchumi ambao unahitaji viwanda vidogo vya kati na vikubwa.

  Akizungumza kabla ya kuzindua kitabu cha Sauti ya Mjasiriamali: Kesho yako ni uthubutu kilichoandikwa na Mjasiriamali mmliki wa kampuni ya ujenzi ya Ibra Contractors, Naibu waziri Ulega alisema historia ya Maida kama ilivyoelezwa katika kitabu inaweka bayana kwamba wananchi wakithubutu wataweza kuibadili Tanzania kuwa ya viwanda.
  Naibu Waziri akiwa katika meza

  Wageni wakiwa katika ukumbi wakifuatilia yanayojiri


  “Tumeona kupitia wasomi, video iliyooneshwa hapa na hata katika majadiliamoya wanazuoni hakuna njia rahisi ya kufikia mafanikio bali ni kule kuthubutu kuanzisha kitu hata kama huna mtaji “ alisema. Alitaka wananchi kuondokana na uwoga na kutumia raslimali zilizopo kujipambanua na kuupiga vita umaskini.

  “ Ukisoma maandishi yake utabaini kwamba wote tunaweza kuwa wajasiriamali kinachotukwamisha ni uwoga wetu wa kuthubutu kama mwenzetu Maida alivyofanya kuanzia kuuza mitumba,kumiliki boti za uvuvi, kuuza maziwa hadi kuwa mkandarasi mwenye sifa hapa nchini “ alisema Ulega. Alisema kwa kuwa ujasiriamali ni chanzo kikuu cha bidhaa na huduma mbalimbali wananchi wanaweza kuufahamu ukweli wa kusonga mbekle kwa kupata maarifa kutoka kwenye kitabu hicho ambacho kinahimiza ujasiriamali endelevu.

  Abbysolo akiwa katika hafla akitumbuiza akili ya fedha
  Naibu Waziri akiteta jambo na Maida

  Kitabu hicho chenye sura 12 kina historia kimegawanyika awamu tatu ya kwanza ikiwa ni wasifu wa Maida waziri, pili mapambano yake ya kujijenga kijasiriamali na tatu kanuni na tabia za mijasirimali.

  Naibu Waziri Ulega pamoja na kumpongeza Maida Waziri kushirikisha Watanzania maisha yake kupitia kitabu ili kila anayemwangalia aweze naye kufanya ujasiriamali na kujipatia mbinu na weledi kutoka katika kitabu hicho, atafikisha hoja kwa wenzake kuona namna bora ya kufikisha kitabu hicho kwa wanafunzi ili waelewe ujasiriamali kutoka wakiwa wadogo. Katika hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho, wanazuoni walipata nafasi ya kukijadili kitabu kwa njia ya mdahalo na washiriki kupata nafasi ya kuuliza maswali.

  Dk Donath Olomi akizungumza

  Akizungumzia fikira muhimu za kitabu Dk Donath Olomi kutoka taasisi ya IMED alisema kwamba amekuwa mwalimu wa ujasiriamali kwa miaka zaidi ya 30 na katika muda wote huo hajawahi kupata kusoma kitabu chenye uhalisia kama cha Maida waziri kuhusu ujasirimali. Alisema Maida Waziri ameonesha njia ya kwamba katika ujasiriamali unaanza na kile kinachowezekana kama yeye alivyoanza na sh Elfu kumi kununulia mitumba na sasa anamiliki kampuni tano ikiwamo ya ukandarasi ya Ibra Contractors.

  Alisema kutokana na kitabu hicho taifa linatakiwa kuona umuhimu wa kuanza kufundisha ujasiriamali katika shule ili kuongeza ufahamu na mbinu za kuushiriki. “Maida amekuwa mwalimu, mtafiti na mshauri mkubwa katika tasnia ya ujasiriamali kupitia kitabu chake akitoa mchango mkubwa katika ajenda ya kujenga ujasirimali nchini “ alisema Dk Olomi.
  Dk Goodluck Urasa akizungumza

  Naye Dk Goodluck Urassa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alimsifu Maida kwa kuandika kitabu hicho ambacho kina nguvu kubwa kutokana na kuelezea maisha yake na jinsi alivyothubutu katika ujasiriamali. “Vitabu vinaandikwa vya namna mbili. Moja kinaandikwa maisha ya watu wengine kupitia utafiti na kusoma na mbili ni kuandika kitabu kueleza maisha yanayokugusa. Hii aina ya pili ina nguvu kubwa na dada Maida ameweza” alisema Dk Goodluck.

  Mtaalamu huyo alisema kitabu kimeeleza na kuonesha kwamba hakuna njia ya mkato katika kukabvili umaskini na kufanya ujasirimali bali ni kuthubutu na kuchukua hatua. Aidha Dk Goodluck alitaka wazazi kuanza kutambua umuhimu wa malezi kwani yanachangia mtu kuwa mbunifu. “Unashangaa mtoto mkubwa katika nyumba hajui wapi alipoweka begi lake la shule dada anaagizwa amtafutie” alisema Dk Goodluck ambaye alisema tabia hiyo inachochea uvivu na udumavu wa maamuzi.
  Maida Waziri akizungumza


  Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akiangalia kitabu baada ya kukizindua

  Tabasamu baada ya kazi nzito kitabu kikioneshwa kwa washiriki wa hafla

  Naye mtunzi wa Sauti ya Mjasiriamali: Kesho Yako Ni Uthubutu, Maida Waziri amewataka watanzania kuchota maarifa na weledi kutoka kwenye kitabu hicho ambacho kimeelezea historia ya maisha yake na jinsi alivyopambana katika ujasiriamali. Aidha alisema katika kitabu hicho ameeleza sifa za mjasiriamali na kanuni anazostahili kuzifuata ili kuwa na mafanikio.
  Naye Mhariri mzalishaji wa magazeti ya serikali Beda Msimbe ambaye alipitia kitabu hicho aliwataka wale wanaopenda kuupiga vita umaskini kuhakikisha kwamba wanakisoma kwa kuwa kimejaa maarifa na kutia moyo.Kitabu hicho kinapatikana kupitia www.maidawaziri.com

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimjulia hali Mbunge wa Makete Profesa Norman Sigala King ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
  Mbunge wa Makete Profesa Norman Sigala King ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam akizungumza mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumjulia hali leo tarehe 22/9/2018.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda anawaalika vijana wote wenye utaalamu wa Teknolojia yani IT kufika Ofisini kwake Tar 01/11/2018 Asubuhi kwaajili ya kuunda Mfumo wa kuratibu Uwajibikaji wa Watendaji wa Umma ilikuhakikisha kero na malalamiko ya wananchi yanashughulikiwa kwa uharaka.

  Mfumo huo utakuwa ukipokea malalamiko ya watendaji wasiowajibika kuanzia ngazi ya Mitaa, Kata, Wilaya, Mkoa na viongozi Wakuu akiwemo Mkuu wa mkoa,Katibu tawala Mkoa, Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi, Makatibu tawala wilaya na wakuu wa idara Watakuwa wakiona ni mtendaji gani asiewajibika kutatua kero za wananchi.

  RC Makonda amesema hataki kuona wananchi wanafika kwenye ofisi za umma na kuambia "Njoo kesho" kila siku pasipokujua kuwa wanatumia nauli na kupoteza muda.

  Mfumo utampa mwananchi uwezo wa kueleza malalamiko yake endapo amefika ofisi ya umma na watendaji kushindwa kushughulikia kero zake kwa uzembe.

  SHAUKU YA RC MAKONDA NI KUONA UWAJIBIKAJI NA UTENDAJI KWENYE OFISI ZA UMMA UNAONGEZEKA ILI KUPUNGUZA KERO KWA WANANCHI.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Sheikh Hasani Bin Mussa Kabeke wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza  Oktoba 22, 2018 akiwa njiani kwenda mkoani Simiyu ambako kesho anatarajia kufungua maonesho ya wajasiriamali.   Sheikh huyo amechaguliwa hivi karibuni kushika wadhifa huo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella  (katikati) wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza akiwa njiani kwenda mkoani Simiyu ambako kesho anatarajia kufungua maonesho ya wajasiriamali. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ushirikiano mzuri baina ya taasisi mbalimbali za dini nchini na Serikali ni jambo la muhimu katika kuboresha na kuimarisha amani.

  Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Oktoba 22, 2018) alipowasili jijini Mwanza akiwa njiani kwenda mkoani Simiyu ambako kesho anatarajia kufungua maonesho ya wajasiriamali.Alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza, Waziri Mkuu amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakiwemo wa Serikali na wa dini mbalimbali.

  Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua mkakati wa viongozi wa dini wa kuunda kamati za amani nchini ambapo walianzia kwenye ngazi ya mkoa na sasa wamefikia katika kata.“Viongozi wa dini mnadhamana kubwa katika kulifanya Taifa liendelee kudumisha amani, utulivu na mshikamano, hivyo ushirikiano wenu na Serikali ni muhimu.”

  Amesema viongozi wa Serikali wakati wote wamekuwa tayari kufanyakazi na viongozi pamoja na taasisi mbalimbali za dini, lengo ni kuimarisha amani na utulivu uliopo nchini.Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza inawajibu wa kuhakikisha kwamba maeneo ya mkoa huu yanaendelea kuwa salama.

  Pia, Waziri Mkuu amempongeza Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Sheikh Hassan Bin Mussa Kabeke kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo.“Nakupongeza kaimu sheikh wa mkoa kwa kuteuliwa na ninakutakia kila la heri katika kazi yako na kwamba dhamana yako kubwa ni kuwaunganisha waislamu na waumini wa dini zote.”


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  41193 – Dodoma
  JUMATATU, OKTOBA 22, 2018.

  0 0

  Mamlaka ya chakula na Dawa TFDA kanda ya Kati Dodoma imeanza kutoa elimu kwa wasindikaji wa mazao ya Nafaka baada ya kubaini baadhi ya bidhaa wanazozalisha hususani unga wa mahindi na siagi ya karanga kuwa na vimelea vya ugonjwa wa sumukuvu ambao ni hatari kwa afya ya watumiaji na wakati mwingine husababisha vifo. 

  Mafunzo hayo yanatokana na ripoti ya ufuatiliaji wa usalama na ubora wa bidhaa zitokanazo na unga mchanganyiko na siagi ya karanga uliofanywa na mamlaka hiyo ya mwaka 2015-2018 na kubaini mazo hayo huzalishwa kwa wingi mkoani humo yana dalili ya uwepo wa fangasi na sumukuvu. 

  Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya kati DK.Englbert Bilashoboka amesema kuwa  Mamlaka imeanza kutoa elimu kwa wasindikaji wa mazao ya Nafaka baada ya kubaini baadhi ya bidhaa wanazozalisha hasa Unga wa Mahindi na Siagi ya Karanga kuwa na vimelea vya ugonjwa wa Sumukuvu.

  Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw.Maduka Kessy amesema kuwa ugonjwa huo hujitokeza baada ya mlaji kutumia bidhaa zenye vimelea vyake kwa kiasi kikubwa huathiri Ini,kusababisha Saratani na hata vifo kwa watumiaji ambao ni nguvukazi ya Taifa. 

  Kessy amesema kuwa mwaka 2015 hadi 2016 na mwaka 2017 hadi 2018 TFDA ilifanya ufuatailiaji wa bidhaa za unga,unga mchanganyiko na siagi za karanga zilizokuwa zikiuzwa katika soko nchini. 

  “Katika ufuatiliji huo ilibainika kuwa bidhaa hizi zilikuwa na dalili ya uwepo wa sumukuvu,hususani katika bidhaa zitokanazo na mahindi na karanga hizi ndizo wajasiliamali wengi wanauza”amesema Bw.Kessy 

  Kwa upande wa baadhi ya Wasindikizaji wamekiri kutokuwa na uelewa juu ya sumukuvu kwani awali walikuwa wakisindika Nafaka Kienyeji bila kuchagua mazao ambayo mengine yana dalili za uwepo wa vimelea vya ugonjwa huo. 
  Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Ndugu Maduka Kessy akizungumza na wajasiriamali hawapo pichani, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wasindikaji wadogo wa bidhaa za unga,unga mchanganyiko ( Composite Flour) na siagi ya karanga yanayofanyika Jijini Dodoma. 
   
  Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya wasindikaji wadogo wa bidhaa za unga,unga mchanganyiko ( Composite Flour)na siagi ya karanga wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa katika semina hiyo 
  Meneja wa Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya kati DK.Englbert Bilashoboka akitoa ufafanuzi mbalimbali husiana semina hiyo kwa waandishi wa habari ( hawapo Pichani) wakati wa Mafunzo ya wasindikaji wadogo wa bidhaa za unga,unga mchanganyiko ( Composite Flour) na siagi ya karanga yanayofanyika  jijini Dodoma. 
  Washiriki wa Mafunzo ya wasindikaji wadogo wa bidhaa za unga,unga mchanganyiko ( Composite Flour)na siagi ya karanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi waliokaa kwenye viti kulia ni Meneja wa Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya kati DK.Englbert Bilashoboka na kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw.Maduka Kessy 

  0 0


  0 0


  0 0

  Na Beatrice Lyimo - MAELEZO, CHINA 

  Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki amezitaka Taasisi zenye dhamana ya kutafuta masoko ya bidhaa mbalimbali nchini ikiwemo TANTRADE , Bodi ya Kahawa, Bodi za Chai, Korosho, Nafaka na Mazao mchanganyiko kushiriki kwenye maonesho mbalimbali yatakayofanyika nchini China ili kutafuta masoko mapya ya bidhaa zao.

  Balozi Kairuki ameyazungumza hayo alipokutana na ujumbe wa Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi walipotembelea nchini China kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu baina ya China na Tanzania katika tasnia ya habari na mawasiliano.

  "Uzoefu wa hivi karibuni umekuwa wa kukatisha tamaa kutokana na Ubalozi kutafuta fursa mbalimbali kwa ajili ya bidhaa za Tanzania kutangazwa lakini wadau wameshindwa kushiriki" ameongeza Balozi Kairuki.

  Aidha, Balozi Kairuki amesema kuwa kumekuwepo na ongezeko la matumizi ya kahawa miongoni mwa Watu wa Jamhuri ya China na kahawa ya Tanzania ni miongoni mwa kahawa zinazopendwa sana na watu hao hivyo hiyo ni nafasi ya kupata soko la uhakika nchini humo endapo itafanyika kampeni mahususi ya kuitangaza kahawa ya Tanzania.

  Vilevile amesema kuwa Madini mbalimbali na vito kutoka Tanzania yana nafasi ya kupata soko nchini China endapo patakuwepo na mifumo mizuri ya kisasa ya kuendesha mnada ya madini.Mbali na hayo, Balozi Kairuki ametaja baadhi ya matarajio ya Ubalozi wa Tanzania nchini China katika kipindi cha miaka minne ijayo ikiwepo kuongeza idadi ya sasa ya watalii toka China kutoka 30,000 hadi 100,000 ifikapo mwaka 2020.

  Aidha, amesema kuwa Ubalozi unatarajia kuongeza uwekezaji kutoka China hususani kwenye ujenzi wa viwanda ikiwa na lengo la kati ya sasa hadi 2021 kuvutia viwanda 100 ili kufanya ongezeko la uwekezaji kutoka dola za Kimarekani Bilioni 3.6 za sasa hadi kufika dola za Kimarekani bilioni 7 ifikapo 2021.

  "Pia Ubalozi unatarajia kuongeza idadi ya fursa za mafunzo kwa Watanzania katika fani mbalimbali hususani uhandisi ikiwa na lengo kuu la kuhakikisha watanzania 1,000 wapate mafunzo ya uhandisi ifikapo mwaka 2021.

  Dkt. Abbasi ameambatana na baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Habari na Uhusiano Serikalini wa Wizara na Taasisi za Serikali kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu baina ya Tanzania na China katika sekta ya mawasiliano.

  0 0  0 0

  *Tanzania ni kati ya nchi 160 zinazoshiriki Kongamano la Kimataifa la Uwekezaji.

  Kongamano la Kimataifa la Uwekezaji (World Investment Forum) limefunguliwa tarehe 22 Oktoba 2018 Geneva, Uswisi na Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) Dkt. Mukisa Khitui na litaendelea mpaka Oktoba 26,2018. 

  Kauli mbiu ya kongamnao ni ‘uwekezaji kwa maendeleo endelevu’ (investing for sustainable development) ambapo majadiliano yatajikita kwenye changamoto za uwekezaji katika mazingira mapya ya utandawazi na mapinduzi ya viwanda (Globalization and Industrialization). 

  Kongamano hili la aina yake huandaliwa kila baada ya miaka miwili na UNCTAD kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa masuala ya Uwekezaji. Takribani washiriki zaidi ya 5,000 wanashiriki kutoka nchi 160 duniani ikiwemo Tanzania na ujumbe wake unaongozwa na Balozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa Geneva, Dkt. James Alex Msekela. 

  Washiriki wa kongamnao hilo ni kutoka katika nyanja mbalimbali za umma na sekta binafsi ikiwamo Wakuu wa nchi, Mawaziri Wakuu, Mawaziri, Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi za Uwekezaji. Wengine ni Watendaji wa Makampuni ya Kimataifa na Ushirikiano wa Hisa, Wasimamizi wa Mifuko ya Fedha, Wakurugenzi Wakuu wa Mashirika ya Sekta Binafsi, Wataalam wa eneo la Uwekezaji wa Kimataifa,Wabunge,Wawakilishi wa Vyama vya Kiraia, Wasomi Maarufu, na vyombo vya Habari vya Kimataifa. 

  Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kama mdau wa masuala ya uwekezaji nchini kinashiriki katika kongamano hili ambapo Mkurugenzi Mtendaji Bw. Geoffrey Mwambe atashiriki katika vipindi/midahalo na majadiliano mbalimbali kwa lengo la kuinadi Tanzania kuwa ni nchi bora ya kuwekeza Afrika kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo amani, uchumi imara unaokua kwa kasi, uwepo wa rasilimali, uwepo wa miundo mbinu na uongozi bora. 

  Vilevile kupitia mikutano hiyo Bw. Mwambe atanadi fursa za uwekezaji zinazopatikana Tanzania katika sekta mbalimbali pamoja na kuelezea mazingira ya uwekezaji. Bw. Mwambe pia atatumia mwanya huo kupambanua zaidi namna ambavyo Tanzania wa sasa inafanya mapinduzi ya kiuchumi hususani kuendeleza viwanda ili kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025. 

  Sambamba na kongamano hilo, Kituo kwa kushirikiana na Ubalozi kinaiwakilisha nchi katika maonesho ya uwekezaji (World Investment Village) kupitia banda la Tanzania ambapo takribani nchi arobaini zinashiriki. Lengo la maonesho hayo ni kueleza washiriki wa kongamano hali ya uchumi wa nchi husika, majukumu ya taasisi inayosimamia masuala ya uwekezaji, sababu za kuwekeza katika nchi husika, fursa za uwekezaji zilizopo, na namna ambavyo wawekezaji wanasaidiwa kuanzisha uwekezaji wao nchini. 

  Vilevile maonesho hayo ni njia pekee inayotoa fursa kwa nchi washiriki kujifunza mbinu/mikakati na kubadilishan auzoefu katika kuvutia uwekezaji zaidi. Baadhi ya nchi zinazoshiriki maonesho hayo ni Rwanda, Namibia, Gaboni, Malawi, Nigeria, Burkina, Faso, Siera Leone, Madagascar, Botwasana, Zimbabwe, Kongo, Burundi, Cote Devour, Mauritius na Zambia. 

  Kuwepo kwa washiriki wengi kutoka katika nyanja mbalimbali kwenye maeneo ya uwekezaji, ni wazi kwamba Kituo kitajifunza mengi kuhusiana na masuala ya uwekezaji ambayo yatatumika kama chachu ya kuleta maboresho katika sekta ya uwekezaji nchini. Ni imani yetu kubwa kwamba ushiriki wa Kituo katika kongamano hili utakuwa wa manufaa makubwa si tu kwa Kituo bali pia kwa Taifa ikiwa ni pamoja na kutoa mapemdekezoya Kisera kuhusu masuala ya uwekezaji.
  Mhe Balozi Dkt. James Msekela (wa tatu kutoka kulia) na Mkuregenzi wa TIC Bw. Geoffrey Mwambe (wa ili kutoka kulia) wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa uwekezaji Geneva,Uswisi.
  Rais wa Namibia Mhe.Dkt Hage Geingob akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Bw. Geoffrey Mwambe katika Banda la Tanzania kwenye kongamano la kimataifa la Uwekezaji.
  Ufunguzi wa kongamano la Kimataifa la Uwekezaji.

  0 0


  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa mkutano wa kumnadi mgombea wa Uwakilishi jimbo la Jang`ombe kwenye viwanja vya Baja.
  26
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi pamoja na Katiba ya Chama mgombea wa CCM nafasi ya Uwakilishi Jimbo la Jang`ombe Bw. Ramadhan Hamza Chande wakati wa mkutano wa kumnadi mgombea wa Uwakilishi jimbo la Jang`ombe kwenye viwanja vya Baja. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
  1
  Wahamasishaji wakiwa wamebeba picha ya mgombea wa nafasi ya uwakilishi kupitia CCM jimbo la Jang`ombe Bw. Ramadhan Hamza Chande wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Baja ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
  8
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Dkt. Abdulla Juma Sadala wakati wa mkutano wa kumnadi mgombea wa Uwakilishi jimbo la Jang`ombe kwenye viwanja vya Baja.12
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo wakati wa mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa Uwakilishi jimbo la Jang`ombe kwenye viwanja vya Baja kushoto ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid.
  16
  Bendi ya Muziki wa Taarab ya Big Star ya CCM Zanzibar ikitumbuiza wakati wa mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa CCM wa jimbo la Jang`ombe kwenye viwanja vya Baja.
  ………………………
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo alikuwa mgeni rasmi katika mkutano wa kampeni jimbo la Jang`ombe ambapo Chama Cha Mapinduzi kimemsimamisha Bw. Ramadhan Hamza Chande kugombea nafasi ya Uwakilishi katika jimbo hilo.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa, Makamu wa Rais amewataka wakazi wa Jang`ombe kufuata nyayo walizoachiwa na Wazazi wao.Mheshimiwa Samia amewambia wakazi wa jimbo hilo kuwa atatoa ushirikiano wa kutosha kwa kufanya kazi pamoja na Viongozi wa Jimbo hilo katika kuboresha huduma za afya na elimu.
  Pamoja na Viongozi wengine Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Mbunge mteule wa jimbo la Liwale kutoka mkoani Lindi Bw. Zuberi Kachauka ambaye aliwaambia wakazi wa Jimbo la Jang`ombe kuwa upinzani umekufa kwa kukosa sera na viongozi bora.
  Kampeni za Uwakilishi jimbo la Jang`ombe zilianza tarehe 14 Oktoba na zinatazamiwa kukamilika tarehe 25 Oktoba  2018 na tarehe 27 Oktoba wananchi watapiga kura kumchagua Mwakilishi wa jimbo hilo.

older | 1 | .... | 1704 | 1705 | (Page 1706) | 1707 | 1708 | .... | 1898 | newer