Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

IGP AKUTANA NA BALOZI WA KOREA NCHINI

$
0
0

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na Balozi wa Korea nchini Song, Geum-young wakati balozi huyo alipotembelea Makao makuu ya Polisi Dar es Salaam ambapo walizungumza mambo mbalimbali ya kuimarisha Uhusiano. (Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akimkabidhi jarida la Polisi Balozi wa Korea nchini Song, Geum-young baada ya kufanya mazungumzo ya kuimarisha uhusiano Makao makuu ya Polisi Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Polisi).

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI OKTOBA 18,2018

TAASISI YA USTAWI WA JAMII BADO INAENDELEA KUPOKEA MAOMBI YA UDAHILI AWAMU YA NNE KWA MWAKA WA MAOSOMO 2018/19

Baraza la Biashara Mkoa wa Dodoma Laaswa Kuongeza Ushiriki wa Sekta Binfasi

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge akifungua  mkutano wa kuhakiki mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na binafsi  uliofanyika leo Jijini Dodoma.
????????????????????????????????????
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith akiteta jambo na Katibu Tawala Msaidizi wa mkoa huo anayeshughulikia Sekta za Uchumi na Uzalishaji Bi Aziza Mumba mara baada ya mkutano wa kuhakiki mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na binafsi  katika mkoa huo.
????????????????????????????????????
Mhadhiri  kutoka Chuo  kikuu Mzumbe Prof. Honest   Ngowi akiwasilisha rasimu ya mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na binafsi  wakati wa kikao cha kujadili muongozo huo leo Jijini Dodoma.
????????????????????????????????????
Sehemu ya wakuu wa Wilaya wa mkoa wa Dodoma wakifuatilia mkutano wa kuhakiki mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na binafsi  uliofanyika leo Jijini Dodoma.
????????????????????????????????????
Sehemu ya washiriki  mkutano wa kuhakiki mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na binafsi  uliofanyika leo Jijini Dodoma.
(Picha zote na MAELEZO)
……………………
Frank Mvungi- MAELEZO,

Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge, ameongoza mkutano wa majadiliano ya Baraza la Biashara la mkoa huo ili kupitia na kuhakiki mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ili usaidie kukuza ushiriki wa sekta binafsi na kuchochea ukuaji wa sekta zinatoa ajira kwa wananchi walio wengi kama kilimo.

Akizungumza na wajumbe wa baraza hilo  leo Jijini Dodoma  na wadau wengine, Dkt. Mahenge amesema kuwa, mkutano huu una lengo la kuhakiki mwongozo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ngazi ya Mikoa na Wilaya.

“Tunategemea utakuwa rejea thabiti kwa viongozi na watendaji ambao wamekuwa wakibadilika mara kwa mara kutokana na uteuzi au chaguzi”. Alisisitiza Dkt. Mahenge

Akifafanua zaidi, mkuu huyo wa mkoa wa Dodoma amesema mkutano huo wa majadiliano una lengo la kuhakikisha ushiriki wa sekta binafsi unaongozeka ili kuchochea maendeleo ya mkoa na taifa.

Aliongeza kuwa, majadiliano hayo yatasaidia kutatua changamoto zinazojitokeza mara kwa mara ambazo zimekuwa zikifubaza upatikanaji wa fursa za kiuchumi na kijamii na yanategemewa kutoa ufumbuzi wa changamoto  hizo kwa kuzingatia maandalizi ya majadiliano, kanuni za majadiliano na utekelezaji baada ya majadiliano.

“Ninatambua kuwa Mabaraza ya biashara yapo katika Wilaya zote mkoani hapa hivyo naamini yatatumika ipasavyo  na yatawezesha kuchochea Maendeleo katika Mkoa na Wilaya zetu kwa kushawishi ongezeko la biashara na uwekezaji”. Alibainisha Dkt. Mahenge.

Pia aliwahimiza  viongozi wa kisiasa na watendaji wote wahakikishe mabaraza ya biashara yanakuwa hai katika maeneo yao ili kuchochea maendeleo na ustawi wa wananchi.

Aidha, aliwataka viongozi katika ngazi za Wilaya kuboresha mazingira ya biashara yatakayowezesha wananchi  kutoa mchango kwenye pato la mkoa na taifa kwa ujumla.  

Michango ya wadau itakuwa imejumuishwa ifikapo mwishoni mwa mwezi wa 10. Baada ya Mwongozo kukamilika utazinduliwa rasmi na Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani kwa tarehe itakayopangwa.

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KUONGEZA KASI YA MATIBABU YA MOYO KWA WATOTO KWA KUWA NA WODI YA WATOTO

$
0
0
 Katika kuimarisha na kuboresha matibabu ya magonjwa ya moyo kwa watoto, Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeendelea kuboresha wodi ya watoto iliyopo katika jengo la watoto ili ifikapo Desemba mwaka huu wodi hiyo ianze kutoa huduma zote kwa watoto.

Wodi hiyo inatarajiwa kuwa na vitanda 32 ambapo vitanda nane vitakuwa katika chumba cha kulaza watoto wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) na vitanda 24 katika wodi za kawaida za watoto, vyumba vitatu kwa ajili ya kliniki za watoto pamoja na vyumba kwa ajili ya ofisi .

Kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2015 hadi 2018 Taasisi imeona jumla ya watoto 8,000 wenye matatizo mbalimbali ya kuzaliwa nayo na yasiyo ya kuzaliwa nayo. Kwa upande wa upasuaji wa moyo jumla ya watoto 889 wamefanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua na upasuaji wa bila kufungua kifua

Watoto 519 walifanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua na kati ya hao watoto 238 walifanyiwa upasuaji na madaktari wetu bingwa wa magonjwa ya moyo huku watoto 281 walifanyiwa upasuaji wakati wa kambi maalum zilizowaunganisha madaktari wetu na madaktari kutoka shirika la Mending Kids International, SACH, na mashirika mengine. Upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cathlab ulifanyika kwa watoto 370

Kwa upande wa kliniki ya watoto kila siku inatoa huduma ya kati ya watoto 30 hadi 40 na kulaza mtoto mmoja hadi wawili. Tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2018 jumla ya watoto 95 wamefanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua watoto 60

Zaidi ya asilimia 75 ya watoto wanaofanyiwa upasuaji ni wale wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ambayo ni matundu na magonjwa yanayoshambulia milango ya mishipa mikubwa na midogo ya moyo. Asilimia 25 ni wale ambao walizaliwa salama na kupata matatizo hayo baada ya kuzaliwa.
 
Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
18/10/2018

RC GAMBO:MTUMISHI ALIYECHUKUA PESA ZAIDI(YA MWANANCHI) YA KUUNGANISHA UMEME AIREJESHE HARAKA

$
0
0
Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Mkuu wa Wilaya ya Karatu Bi Theresia Mahongo wakipata maelezo kutoka kwa wahandisi wa TARURA wilaya ya Karatu juu ya maendeleo ya ujenzi wa daraja la Getamong wilayani humo. Picha na Vero Ignatus
Meneja wa TANESCO Wilaya ya Karatu Edward Mwakapaju akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo juu ya hali ya utekelezwaji wa mradi wa umeme vijijini REA wilayani humo.Picha na Vero Ignatus
Wananchi wa eneo la Kilimamoja wilayani Karatu wakiwa katika mkutano wa hadhara kutoa kero zao kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. Picha na Vero Ignatus 

Na. Vero Ignatus, Karatu. 

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amemwagiza Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)Wilaya ya Karatu, Edward Mwakapaju kuhakikisha mtumishi wa shirika hilo aliyechukua pesa kiasi cha Sh. 70,000/= kwa mmoja kati ya mwananchi wa eneo la Mang'ola badala ya Sh. 27,000/= za kuunganishiwa umeme wa REA kuzirudisha mara moja.

Gambo  amesema kuwa haridhishwi na kasi ya usambazwaji umeme unaofanywa na Kampuni ya NIPO Group Ltd kwenye vijiji na vitongoji mbalimbali vya wilaya hiyo na kumpa agizo Meneja wa Tanesco Mkoa wa Arusha, Henry Mhina kuhakikisha anachukua hatua ili wananchi waweza kuunganishiwa umeme.

RC Gambo  aliyasema hayo katika ziara yake ya siku tatu kwaajili ya kukagua miradi ya umeme wa Vijijini ( REA) miradi ya maji  na barabara inayosimamiwa na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA).

Alisema mtumishi huyo wa Tanesco (jina hakumtaja) alichukua fedha kwa mwananchi wa Man'gola kiasi cha Sh. 70,000 ili amuunganishie umeme wa REA ilihali akijua kuwa gharama ya kuunganisha umeme huo ni Sh. 27,000/= huku wananchi wengine wa vijiji vya Tloma na Ganako wakitozwa Sh. 177,000/= badala ya Sh. 27,000/=. 

Alisema ingawa mtumishi huyo wa Tanesco amefukuzwa kazi lakini hela alizochukua Sh. 70,000/= kutoka kwa mwananchi huyo haijarudishwa hivyo ni vyema sasa hela hizo zikarudishwa kwa mwananchi huyo mara moja huku akiziagiza vyombo vya ulinzi na usalama kushughulikia tatizo hilo mara moja.

Pia alimwagiza Meneja wa Tanesco Mkoa wa Arusha, Mhina kuhakikisha anakaa na watendaji wa NIPO Group Ltd kuhakikisha wanakaa kwa pamoja ili kutatua changamoto za  msambazaji wa umeme wa kampuni ya Lesheya Investment Ltd  aliyeingia mkataba na kampuni ya NIPO Group Ltd kwaajili ya kusambaza nguzo hadi eneo husika ili kufunga umeme kwa wananchi.

"Nataka huyu mtumishi wa Tanesco arejeshe hela ya huyu mwananchi mara moja na pia lazima hatua zichukuliwe kwa hao wanaowachukulia wananchi kiasi kikubwa cha kuwaunganishia umeme wananchi huko vijijini pia siridhishwi na kasi ya usambazwaji umeme unaofanywa na kampuni ya NIPO Group Ltd na naomba hii kampuni kama mnaona wakala anawakwamisha chukueni hatua " Alisema Gambo.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Bi. Theresia Mahongo alisema kuwa suala la mwananchi huyo kuchukuliwa kiasi cha Sh. 70,000/= ni la kweli na lipo mezani kwake hivyo vyombo vya ulinzi na usalama vinalishughulikia suala hilo.

Awali Mhandisi wa kampuni ya NIPO Group Ltd, Hussein Said alisema kuwa kampuni hiyo inaendelea na kazi katika wilaya hiyo pamoja na vijiji mbalimbali lakini changamoto kubwa ni mahitaji ya nguzo ambapo hadi sasa mahitaji ya nguzo hizo ni makubwa kuliko usambazwaji wa umeme wanaofanya kwani mahitaji ya nguzo kubwa ni 1,661 hadi sasa nguzo zilizopo ni 795 huku nguzo ndogo zikiwa zimekuja 257.

Pia wana changamoto kubwa ya usambazwaji wa Transfoma zilizopo ni 21 badala ya 70 kutoka Kiwanda cha kutengeneza Transfoma cha Tanelec huku akisisitiza kuwa endapo watasanbaziwa vifaa hivyo ikiwemo nguzo na transfoma kwa wakati wataweza kusambaza umeme kwa kasi.

Awali wananchi wa kijiji cha Kibaoni na Kilimamoja akiwemo Yusuph Said na Elizabeth Sabaha waliomba kero hiyo ya maji kushughulikia mara moja kwani hivi sasa badala ya wananchi hao kulipia Shilingi 20 kwa ndoo moja ya maji ya kijiji wao wanalipa Sh. 100 kwa ndoo moja.

Gambo anaendelea na ziara yake ya siku tatu katika wilaya za Karatu na Ngorongoro ambapo anakagua maendeleo ya miradi ya barabara na maji katika wilaya hizo.

TAASISI YA CORNELL ALLIANCE FOR SCIENCE YA MAREKANI YAWATUNUKU VYETI WAANDISHI WA HABARI KILIMO SAYANSI

$
0
0

 Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Tekonolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu, akimkabidhi cheti, Mwandishi wa Habari Suleiman Msuya, baada ya kushiriki mafunzo ya kuandika habari za Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO), yaliyofanyika New Dodoma Hoteli mkoani Dodoma na kuibuka Mshindi wa Pili katika Mashindano ya uandishi wa habari  juu ya teknolojia hiyo kwa kundi la Waandishi wa habari za magazeti. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Jukwaa la Wazi la Kilimo na Teknolojia Afrika (OFAB) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Cornell cha Marekani, Cornell Alliance For Science na African Agricutural Technology Foundation (AATF).
Mshindi wa  Kwanza kwa upande wa Waandishi wa Habari za Magazetini Bw. Daniel Mkate akipokea cheti.
 Mshindi wa kwanza wa kuandika habari hizo kwa njia ya redio katika mafunzo hayo, Kemsi Fadhil akipokea cheti.

 Mshindi wa pili wa kuandika habari za GMO kwa njia ya Televisheni, Vumilia Kondo akipokea cheti.
 Mshindi wa kwanza wa kuandika habari za GMO kwa njia ya Televisheni katika mafunzo hayo, Doreen Mlay akipokea cheti.
 Meza kuu wakati wa utoaji wa vyeti hivyo.
 Mshindi wa jumla wa kuandika habari za GMO kwa njia ya magazeti katika mafunzo hayo, Rose Milondo akikabidhiwa cheti.










 Mwanahabari Dotto Mwaibale akipokea cheti cha ushiriki.



























 Picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.

WAZIRI MWAKYEMBE ATEUA WAJUMBE WATANO WA BODI YA BASATA,YUMO MSANII MWANA FA NA SINGLE MTAMBALIKE


Black Friday 2018 is coming: Top Deals We can expect on Jumia Tanzania.

$
0
0
Black Friday 2018 is coming: Top Deals We can expect on Jumia Tanzania.

Black Friday is the name given to the shopping day after Thanksgiving. It is reported that the term was originally coined by the Philadelphia Police Department in the USA to describe the chaos surrounding the congestion of pedestrian and vehicular traffic. This was because, on the day after Thanksgiving, many people went out to shop causing traffic accidents and even violence.

What is Black Friday?

Black Friday, is an event that was once considered popular only in the US but has equally gained popularity in African countries. Black Friday marks the beginning of Christmas shopping, with different stores offering huge discounts on everything including TVs, Laptops, cellphones, Kitchen appliances, gaming products and a whole lot of other products. Today, Black Friday is a global feature, and everyone is searching for discounts and deals that they otherwise not get on a regular day.

Jumia Tanzania's Black Friday is no different, it is the season to shop for as many items as you want online and enjoy the greatest discounts. Top products with the greatest discounts include flat-screen TVs, electronics, mobile phones, fashion and cosmetics. But that’s not all, as there will be even greater deals on stylish dresses, shoes and accessories. 

What Happens on Black Friday

Globally, retail stores offer shocking discounts on lots of products like television sets, home theatres, microwaves, toasters, blending machines, refrigerators, washing machines, clothes, smartphones and even flights and hotels. Shoppers will usually scramble for the best offers and will spend a great amount of time online on the biggest retail stores like Amazon and in walk-in stores like Walmart. In the past, sites have crashed and fights broke out.

In the previous years, Jumia has hit an all-peak in sales during the Black Friday event. This not only means that Africa's disposable income and online consumption is growing but at a very high rate too. This year's Black Friday sale is not going to be any different, there will be reduced prices Jumia Tanzania and huge Jumia Travel Black Friday deals. Get your shopping list ready as there will be massive discounts on a huge range of products on Jumia Tanzania. Also, since Black Friday is only a month to Christmas, you can plan and book for holiday getaways with Jumia Travel Black Friday deals. Get excellent discounts on different destinations and Hotels in Tanzania. All the amazing offers and deals will be taking place online on the Jumia Tanzania official website.

When is Jumia’s Black Friday in Tanzania

This year, Jumia is introducing ‘Black Fridays’, set to begin on November 16th to December 7th. Yes, four whopping Fridays! Jumia Tanzania is planning on having discounts of up to 70% off on more than 1 million products. These products include mobile phones with discounts that go as far as 50% on all types of smartphones including iOS and Android smartphones. Also, if you are planning to buy home appliances and electronics, hold on until Black Friday on Jumia Tanzania kicks off. There will be fantastic deals on appliances like coffee makers, toasters, Juicers and blenders, cookers and irons. Other deals will be on fashion items including shoes, clothes and accessories for men, women and children.

While traditionally, offers are done on physical stores prompting huge waiting lines, cashier lines, pushing and shoving, Jumia Tanzania's Black Friday is purely online. Good thing is, you can shop conveniently without leaving your desk. Pure bliss, no shoving and scrambling for your favourite items. You can also pay securely online and have your many orders delivered to an address of your choice.
What else to watch out for during these Black Fridays

Apart from the fun and the thrill of shopping for your favourite items at highly discounted prices, Black Fridays come with other amazing goodies all wrapped up uniquely and it’s up to you to unravel the mystery. Among them includes:
Daily Flash Sale: There will be new amazing deals on top products every Friday between November 16th - December 7th. This means that online shoppers get to enjoy new deals every Friday.

Treasure Hunt: This is a feature where a highly discounted product is hidden across the Jumia Tanzania website, which when found should be purchased by the customer as quickly as possible as only the fastest shopper gets it. Wheel of fortune: This is a wheel on Jumia’s website which you spin and win every day. It has 500, 000 vouchers up for grabs

SERA YA DIPLOMASIA YA UCHUMI INAVYOLETA MAGEUZI YA UWEKEZAJI

$
0
0
Na. Immaculate Makilika.MAELEZO

KATIKA miaka ya 1960 hadi 1980 malengo ya ziada katika Sera ya mambo ya nje ya Tanzania yalikuwa ni ukombozi wa Bara la Afrika kutoka kwa makucha ya ukoloni na ubaguzi wa rangi.

Baada ya kukamilisha juhudi hizo, Tanzania ilifanya mageuzi makubwa katika Sera ya Mambo ya Nje iliyoweka msisitizo wa diplomasia ya uchumi ili kusukuma maendeleo ya Taifa. Diplomasia ya uchumi ni msisitizo wa Sera ya Mambo ya Nje yenye mikakati, malengo, mbinu na maarifa yanayoelekeza taifa kupata na kuvuna rasilimali na utaalam kutoka jumuiya ya mataifa ili kuleta na kuchochea maendeleo ya taifa husika.

Mwaka 2001 Tanzania ilipitisha sera hiyo ili kuharakisha maendeleo hasa katika mageuzi ya kiuchumi kupitia uwekezaji, ambapo katika mwendelezo huo Serikali ya Awamu hii ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli imeongeza kasi ya utekelezaji wa sera ili kuifanya Tanzania kufikia nchi ya kipato cha uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Azma hii inamaanisha kuwa diplomasia ya uchumi lazima iongeze mkakati wa Diplomasia wa viwanda ili kutekeleza maono na mawazo ya Rais Dkt. Dkt. John Pombe Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kupitia malighafi za mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi.

Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahriki kwa mwaka 2018/2019, Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga anasema kuwa sera ya diplomasia ya uchumi imeweka vipaumbele katika uwekezaji, miundombinu ikiwa ni pamoja na nishati, biashara na masoko ya bidhaa kutoka viwandani, kilimo, utalii na madini

Aidha, Balozi Mahiga anasema kuwa Serikali imeendelea kufanya jitihada mbalimbali ili kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka 2025, ambapo hivi karibuni Wizara hiyo imeratibu maonesho ya bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya Tanzania, yaliyofanyika mjini Nairobi nchini Kenya.

“Katika maonesho hayo ya kipekee kuwahi kufanywa na Tanzania huko nchini Kenya jumla ya kampuni 27 zinazozalisha bidhaa za viwandani kutoka Tanzania zilishiriki ili kutangaza bidhaa na kuvutia utalii, ambapo yaliyotoa fursa kwa wafanyabiashara wa Tanzania kutafuta masoko nchini humo na kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili” anasema Waziri Mahiga. 

Aidha, Balozi Mahiga anasema kupitia sera ya diplomasia ya uchumi, Serikali za Tanzania na Misri, zimeratibu majadiliano ya pamoja hatua iliyosaidia kuondoleana ushuru wa forodha kwa kiwango cha asilimia 100, huku Tanzania ikiondoa ushuru kwa kiwango cha asilimia 96.89, ambapo kiwango kilichosalia kitaondolewa katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Katika kuchagiza sera hiyo, Dkt. Mahiga anasema mwezi Februari, mwaka huu, Serikali za Tanzania na Korea Kusini ziliandaa kongamano la biashara na uwekezaji kati ya mataifa hayo mawili, kufuatia mazungumzo baina ya viongozi wa kampuni ya Hyundai na Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC).

Aidha, Balozi Mahiga anasema aliwataka wadau wanaosimamia masuala ya biashara na uwekezaji kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wawekezaji wanaoonesha nia ya kuwekeza nchini

DC MURO AVIONYA VYAMA VYA SIASA KUTODUMAZA MAENDELEO

$
0
0
Na Imma Msumba, Arumeru

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe.Jerry Muro amevitaka vyama vya siasa kuacha  malumbano na mvutano isiyokuwa na tija kwa wananchi wa Arumeru na badala yake amewataka kuungana na serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Arumeru.

Mh. Muro ameyasema hayo baada ya kuingilia kati mgogoro wa umiliki wa jengo ambalo awali lilikuwa likitumiwa na chama cha ushirika kata ya Ilikiurei hatua iliyosababisha kufungwa kwa ofisi ya serikali ambayo ilikuwa ikihudumia wananchi wa vitongoji viwili.

Kwa upande wao wananchi wanaoishi katika vitongoji hivyo mbali na kumpongeza Dc Muro kwa kuchukua hatua kwa haraka kuwa ofisi hizo zifunguliwe wamesema uamuzi huo utawasaidia kupata huduma ambazo wamekuwa wakizikosa kwa muda mrefu kutokana na mvutano wa umiliki wa jengo hilo kutoka kwenye vyama viwili vya siasa.

Baadhii ya Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe.Jerry Muro alipokuwa akizungumza nao

GLOBAL COMPACT NETWORK TANZANIA CHALLENGES COMPANIES TO DISRUPT THE BUSINESS-AS-USUAL MINDSET

$
0
0
A panelist from Regulatory Scientific Affairs Marsha Yambi presents during the Global Compact Network Tanzania (GCNT) AGM today. From (left) are other panelists,  UNGCNT National Coordinator, Emmanuel Nnko, ILO Senior Programme Officer Anthony Rutabanzibwa and Sustanability Practice, Strategist Mesiya Mwangoka. (Prepared by Robert Okanda)
A section of participants of the Global Compact Network Tanzania (GCNT) First Annual General Meeting (AGM) follow the presentation in Dar es Salaam October 18 2018. 
A section of participants of the Global Compact Network Tanzania (GCNT) First Annual General Meeting (AGM) follow the presentation in Dar es Salaam October 18 2018. 
A section of participants of the Global Compact Network Tanzania(GCNT) First Annual General Meeting (AGM) exchanges views in Dar es Salaam October 18 2018. 
A section of participants of the Global Compact Network Tanzania(GCNT)  First Annual General Meeting (AGM) follow the presentation in Dar es Salaam October 18 2018. 
A section of participants of the Global Compact Network Tanzania(GCNT) First Annual General Meeting (AGM) follow the presentation in Dar es Salaam October 18 2018. 
A section of participants of the Global Compact Network Tanzania(GCNT) First Annual General Meeting (AGM) follow the presentation in Dar es Salaam October 18 2018. 
A section of participants of the Global Compact Network Tanzania(GCNT) First Annual General Meeting (AGM) keenly follow the proceeding of the meeting in Dar es Salaam October 18 2018. 
Ernest Salla , UNDP representative , delivers his speech before welcoming the chief guest to address the participants,  during the Global Compact Network Tanzania (GCNT) AGM 2018  
The Deputy Permanent Secretary in the Ministry of Industry, Trade and Investment, Ludovick Nduhiye delivers his speech at AGM. 
UNGCNT National Coordinator, Emmanuel Nnko responds to issues raised by the panel members during the AGM today. 
A section of participants of the Global Compact Network Tanzania(GCNT) First Annual General Meeting (AGM) pose for a souvenir photo with Vice  Chair for Global Compact, Dr Aggrey Mlimuka (seated second row centre) in Dar es Salaam October 18 2018. 
Global Compact Network Tanzania Vice Chair elected , Dr Aggrey Mlimuka (centre) gives votes of thanks to members after being elected during the  Global Compact Network Tanzania(GCNT)  AGM in Dar es Salaam today. Together with him are news elected leaders. 
Vice Chair  for Global Compact, Dr Aggrey Mlimuka (second seated second row) poses for memorable photo with other elected members and delegates during the climax of meeting. 

MPINA AWATAKA VIONGOZI WOTE WA SERIKALI KUSHIRIKI KIKAMILIFU KWENYE ULINZI WA RASLIMALI ZA MIFUGO.

$
0
0



Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akikata utepe kufungua Mnada wa Kimataifa wa Mifugo Kirumi ulioko wilayani Butiama mkoani Mara juzi, wengine wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima{kushoto},Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi}kulia} na Katibu Mkuu Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel.Picha na Mpiga Picha Wetu

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akifunua kitambaa katika jiwe la msingi  la ufunguzi  wa Mnada wa Kimataifa wa Mifugo Kirumi ulioko wilayani Butiama mkoani Mara juzi, wengine wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima{kulia} na Katibu Mkuu Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel }kushoto}.Picha na Mpiga Picha Wetu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina aliyenyanyua mkono akiwa na Katibu Mkuu Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel (kulia kwake)  wakati wa ufunguzi wa Mnada wa Kimataifa wa Mifugo Kirumi ulioko wilayani Butiama mkoani Mara juzi. Picha na Mpiga Picha Wetu


NA JOHN MAPEPELE, MARA

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amewataka viongozi wote wa serikali kuanzia ngazi za vijiji,wilaya kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa rasilimali za mifugo badala ya hali ilivyo sasa ya kuiacha ikitoroshwa kwenda nchi za nje kwa kuamini kwamba jukumu la ulinzi wa rasilimali hizo ni la Wizara ya Mifugo na Uvuvi peke yake na ikosesha serikali mapato.

Waziri Mpina ameyasema hayo wakati akizundua mnada wa mpakani wa Kimataifa wa Mifugo katika eneo la Kirumi Wilayani Butiama mkoani Mara ambapo ameagiza kufungwa kwa minada yote ya mifugo iliyofunguliwa kinyemela kwani imekuwa kichocheo cha upotevu wa mapato wa Serikali na kuonya wanaoanzisha minada hiyo bila kufuata taratibu zilizopo watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.

Aidha amemuagiza Katibu Mkuu Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel kuanza mara kuihakiki minada yote iliyopo nchini ili kuibaini ambayo imeanzishwa kinyume cha sheria iweze kufutwa.

“wako watu wanafungua minada kila sehemu wanaamua tu wakati taratibu za ufunguzi wa minada wanazijua kabisa ya kwamba ni lazima wizara iridhie kufunguliwa kwa mnada huo”alisisitiza Waziri Mpina

Amesema Serikali inapotaka kuanzisha mnada inakuwa na malengo ya kuhakikisha biashara ya mifugo inafanyika vizuri na kwamba uanzishaji holela wa minada unadhoofisha mipango inayowekwa na Serikali jambo ambalo haliwezi kukubalika.

Naye Katibu Mkuu Mifugo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Profesa Elisante Ole Gabriel alisema kufunguliwa kwa mnada huo kutasaidia usimamizi na kudhibiti utoroshaji wa mifugo na kuongeza mapato ya Serikali ambapo amesema mnada wa Kirumi umewekwa kimkakati na unatarajia kuvuta wafanyabiashara wa mifugo kutoka katika nchi za jirani na kuliingizia taifa mapato makubwa.

Waziri Mpina amewataka viongozi wa Serikali kuhakikisha wanapanga matumizi bora ya ardhi na kuwawezesha wafugaji kupata huduma zinazostahili ikiwemo malisho na maji badala ya hali ilivyo sasa ambapo kila kiongozi anaona mifugo ni laana kwa taifa.

Pia Waziri Mpina pia alimuagiza Katibu Mkuu Mifugo kuanzisha haraka ofisi itayotoa huduma ya vibali kwa watu wanaotaka kusafirisha mifugo nje ya nchi tofauti na ilivyo sasa ambapo wafanyabishara hao hulazimika kwenda hadi jijini Mwanza kufuatilia vibali hivyo.

Ameagiza kupelekwa kwa mitungi ya kupandikiza mbegu bora ya mifugo katika Mkoa wa Mara na kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo kwa gharama isiyozidi sh 5,000 tofauti na ilivyo sasa ambapo hulazimika kugharamia hadi sh, 100,000 kupata huduma hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima alisema Serikali ngazi ya mkoa huo itaendelea kuwachukulia hatua kali watu wote wataoshiriki vitendo vya utoroshaji mifugo nje ya nchi huku akiwaonya watu wanaondeleza vitendo vya wizi wa mifugo kwamba hawatapata tena nafasi katika kipindi hiki cha utawala wa Serikali ya awamu tano.

Malima alisema tayari mkoa huo umepokea mwekezaji wa kiwanda cha maziwa kitakachokuwa na uwezo wa kusindikiza tani 200,000 kwa siku na kusema kuwa itakuwa ni ukombozi mkubwa kwa wafugaji wa mkoa huo kupata soko la uhakika la maziwa yao.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Mkoa wa Mara, Mrida Mshoja amesema ngombe zilikuwa zinatoroshwa kwenda Kenya na kwamba kufunguliwa kwa mnada huo kutawezesha wafugaji kupata soko la uhakika la mifugo yao na kumshukuru Waziri Mpina kwa kufanikisha azma ya kuanzisha mnada huo.



MTANGAZAJI ISAAC GAMBA AFARIKI DUNIA NCHINI UJERUMAN, POLISI WAFANYA UCHUNGUZI WA KIFO CHAKE

$
0
0

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MTANGAZAJI maarufu nchini Isaac Muyenjwa Gamba ambaye alikuwa akitangaza Idhaa ya Kiswahiliya DW ya Ujeruman amefariki dubia leo akiwa nyumbani kwake mjini Bonn nchini humo.

Taarifa ambazo Michuzi Blog imezipata kutoka kwa wafanyakazi wa DW ambao walikuwa wakifanya naye kazi kabla kifo kumkuta wanasema kwa sasa wanaendelea kufanya mawasiliano na familia yake ili kupata maelekezo.

Wamesema kifo cha Gamba kimewasikitisha na kimewashangaza kwani baada ya kuona hakufika ofisini juzi,jana na leo waliamua kutoa taarifa Polisi na walipoenda nyumbani kwake walivunja mlango na baada ya kuingia ndani walimkuta akiwa tayari amefariki dunia.

Wamesema baada ya Polisi wa nchini humo kuingia ndani waliukuta mwili wa Gamba kwenye kochi.Hivyo wakati wakifanya mawasiliano na familia pia wanasubiri uchunguzi wa Polisi kwanza na kisha waendelee na taratibu nyingine.

"Kwa upande wetu huku Ujeruman tunaendelea kuwasiliana na familia yake wakati tukiendelea kusubiri majibu ya taarifa za uchunguzi wa Polisi," amesema mmoja wa wafanyakazi wa DW aliyeomba jina lake lihifadhiwe kwa nia njema tu.

Gamba wakati wa uhai wake pia amewahi kutangaza Redio One na ITV na kabla ya hapo pia amewahi kutangaza Redio Uhuru na RFA ambapo aina ya utangazaji wake na sauti yake vilimfanya kuwa maarufu nchini Tanzania.

Mungu amlaze mahala pema peponi. Ameen
MTANGAZAJI maarufu nchini Isaac Muyenjwa Gambaa akiwa kazini enzi za uhai wake.

NDITIYE AKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA UJENZI A BANDARI KAVU, KWALA VIGWAZA

$
0
0

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa bandari kavu, Kwala eneo la Vigwaza mkoani Pwani. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Uhandisi, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Mhandisi Charles Otare na wa kwanza kulia ni Meneja wa Mradi huo kutoka SUMA JKT Raymond Kweka
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyesimama katikati) akipata maelezo kuhusu maendeleo ya mradi wa ujenzi wa bandari kavu, Kwala mkoani Pwani kutoka kwa Mkurugenzi wa huduma za Uhandisi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mhandisi Charles Ogare (anayetoa maelezo). Wa kwanza kulia ni Meneja wa Mradi huo kutoka SUMA JKT, Raymond Kweka
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akipitia ramani ya mpangilio wa matumizi ya eneo la bandari kavu, Kwala mkoani Pwani wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa bandari hiyo. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Uhandisi, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mhandisi Charles Ogare
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa bandari kavu, Kwala kuhusu eneo la njia ya reli itakayoingia bandarini humo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa bandari hiyo mkoani Pwani. Wa kwanza kulia Kaimu Meneja wa Badari ya Dar es Salaam, Fred Liundi na wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Uhandisi, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Mhandisi Charles Ogare
Muonekano wa eneo linaloandaliwa kujenga njia ya reli kwa ajili ya kusafirisha mizigo inayoingia na kutoka bandari kavu, Kwala mkoani Pwani wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo

Onesho la Tigo Fiesta Latua Moshi na Ofa kabambe ya Data Kama Lote Inayowapa Wateja Hadi Mara Mbili ya Thamani Ya Intaneti Watakayonunua Kutoka Tigo

$
0
0

Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Nancy Bagaka(katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo jinsi wapenzi wote wa muziki mjini Moshi watakavyofurahia promosheni tatu murwa katika msimu huu wa vibes. ‘Data Kama Lote inawapa wateja hadi mara mbili ya vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#. Pembeni yake kutoka kushoto ni Hamisi Mandi B12, Mr. Blue, Rosa Ree na Kennedy The Lemedy.
Mjumbe wa Tamasha la Tigo Fiesta toka Clouds Media, Hamisi Mandi Maarufu kama B12 (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Moshi jinsi tamasha hilo litakalofanyika kesho uwanja wa Majengo mjini Moshi kuwa litakuwa lenye ubora wa hali ya juu. Wengine pichani toka kushoto ni Mr. Blue, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Nancy Bagaka, Rosa Ree na Kennedy The Lemedy.

Waziri wa Ladha na Vibe wa Tigo Fiesta 2018,Kennedy The Lemedy akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Moshi, Ambapo kesho tamasha la Tigo Fiesta litaendelea Mjini Moshi mkoa Kilimanjaro .
Msanii Rapa wa Kike Tanzania, Rosa Ree akizungumza na wanahabari kwenye hoteli ya Panama leo mjini Moshi

…………………. 

Vibe Kama Lote imewasili mjini Moshi na ahadi ya kuwapagawisha mashabiki wa muziki kwa vibe asilimia 100% za nyumbani pamoja na promosheni tatu kabambe zitakazoendana na fursa kubwa za kibiashara kwa wakaazi wote wa mji huo.

Mdhamini mkuu wa msimu huu wa Tigo Fiesta 2018, kampuni ya Tigo imewakumbusha mashabiki wote wa muziki mjini Moshi kufurahia promosheni zake tatu murwa katika msimu huu wa vibes. ‘Data Kama Lote inawapa wateja hadi mara mbili ya vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#. Hii itawawezesha wateja wa Tigo kufurahia msimu huu wa vibes kupitia mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+,’ Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Kaskazini, Nancy Bagaka alisema.

Tigo pia inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Kwa tamasha la Moshi litakalofanyika katika viwanja vya Majengo, tiketi zitakazonunuliwa kwa mfumo wa Tigo Pesa Masterpass QR zitagharimu TSH 8,000 pekee badala ya TSH 10,000 kwa watakaonunua kwa pesa taslim, Wateja wanapaswa kupiga *150*01# na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.

Wateja wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za kila wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia.

Huu ni mwaka wa 17 wa tamasha la muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ambapo mwaka huu linashirikisha 100% wasanii wa nyumbani wanaozuru mikoa 15 ya nchi ikiwemo; Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Singida, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku kilele kikifanyika Dar es Salaam.

Ripoti ya Taifa ya Takwimu za Mazingira 2017 kusaidia Serikali kupambana na Uharibifu wa Mazingira

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akikata utepe kuzindua Ripoti ya Taifa ya Takwimu  za Mazingira ya mwaka 2017 leo Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wan chi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba.
1
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akizungumza na washiriki wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Taifa ya Takwimu za Mazingira ya mwaka 2017 leo Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January  Makamba.
3
Mtakwimu mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)  Bw. Pius Kasikana akiwasilisha mada wakati wa hafla ya kuzindua Ripoti ya Taifa ya Takwimu  za Mazingira ya mwaka 2017 leo Jijini Dodoma.
4
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akionesha Ripoti ya Taifa ya Takwimu  za Mazingira ya mwaka 2017 leo Jijini Dodoma mara baada yakuizindua leo Jijini Dodoma.
5
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima akimkabidhi Ripoti ya Taifa ya Takwimu  za Mazingira ya mwaka 2017 Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Irenius Ruyobya leo Jijini Dodoma.
6
Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira Bi Ruth Minja akiwasilisha mada wakati wa hafla ya kuzindua  Ripoti ya Taifa ya Takwimu za Mazingira ya mwaka 2017 leo Jijini Dodoma.
7
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Ardhi Dkt. Anes Mahenge akiwasilisha mada wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Taifa ya Takwimu  za Mazingira ya mwaka 2017 leo Jijini Dodoma.(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO
…………………….

Na; Mwandishi wetu
Ripoti ya Taifa ya Takwimu za Mazingira ya mwaka 2017 iliyozinduliwa leo Jijini Dodoma imetajwa kuwa ya kihistoria na itasaidia Serikali katika kuchukua hatua stahiki kupambana na uharibifu wa mazingira.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Naibu Waziri wa Ofisi hiyo Mhe. Mussa Sima (Mb) wakati akizindua ripoti hiyo leo Jijini Dodoma amesema kuwa ripoti hiyo ni ya kuhistoria na itasaidia katika kuchukua hatua mbalimbali kukabiliana na uharibifu wa mazingira hapa nchini.

Matokeo yanaonesha kuwa kuna upotevu wa misitu takribani hekta 372,000 tangu mwaka 1995 hadi 2010 hivyo ni muhimu kuchukua hatua stahiki kuondokana na changamoto za uharibifu wa mazingira”. Alisisitiza Mhe. Sima
Akifafanua amesema kuwa ripoti hiyo inaonesha kuwa miji 10 tu ndio yenye miundo mbinu ya maji taka ambayo inanufaisha wananchi takribani asilimia 10.
Aliongeza kuwa Serikali imejipanga kikamilifu kukabiliana na changamoto za uharibifu wa Mazingira kwanza kwa kuweka mfumo wa kisheria unaosimamia suala hilo na pia kuweka Taasisi mahususi inayosimamia masuala yote ya mazingira hapa nchini.

Pia alitoa wito kwa Wizara na Idara zinazojitegemea kutenga Bajeti kwa ajili ya vitendea kazi,uchakataji wa takwimu za mazingira katika maeneo yao ili kushiriki kikamilifu katika kutunza mazingira na kuchochea maendeleo endelevu yanayoenda sambamba na utunzaji wa mazingira.

Aliongeza kuwa Serikali kwa kuthamini umuhimu wa uwekezaji imeweka mazingira mazuri yanayowawezesha wawekezaji kupata cheti cha Tathmini ya mazingira ndani ya siku 70 kutoka siku 149 za awali ili kuharakisha mchakato wa uwekezaji na kuvutia wawekezaji.

Pia aliwataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kutenga maeneo ya uwekezaji  na kuyapima ili wawekezaji wanapojitokeza wapatiwe maeneo hayo yakiwa yamepimwa ili kuharakisha maendeleo.Uzinduzi wa Ripoti ya Takwimu za Mazingira ya mwaka 2017 ni kichocheo cha maendeleo kwa kuwa inatoa taswira halisi ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kulinda mazingira na kutekeleza miradi yote kwa kuzingatia sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na Kanuni zake.

RC Wangabo Amtaka DED Kuhamishia Ofisi Zake karibu na Wananchi

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (mbele) akikongoza ukaguzi wa jengo lililojengwa kwa madhumuni ya kuhamia ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (mbele kulia) pamojana na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule wakikagua jengo lililojengwa kwa madhumuni ya kuhamia ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. 
jengo lililojengwa kwa madhumuni ya kuhamia ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo 


……………………….

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo amemtaka Mkurugenzi wa Halmauri ya Wilaya ya Sumbawanga kuhakikisha anahamishia ofisi zake karibu na wananchi ambao wanishi katika mipaka ya halmashauri yake na sio kubaki mjini.

Amesema kuwa kwa kufanya hivyo mji utatanuka na maendeleo yatapatikana na pia kupunguza gharama za kuwahudumia wananchi pindi majanga yanapotokea kwani kuwa nao karibu kutasababisha kutotumia pesa nyingi kuwafuata na wao kupata urahisi wa kufika katika ofisi hizo.

“Rai yangu mkurugenzi mtafute mahala kwingine kwa kujenga ofisi za halmashauri ya wilaya, mahala pengine ambapo ni ndani ya halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga na sio ndani ya manispaa, ofisi hii inapaswa iwe nje ya eneo la manispaa, faida yake ni kupanua huduma kuliko kila kitu kufikiria manispaa,” Alisema

Ameyasema hayo alipokwenda kukagua jengo jipya la halmashauri hiyo ambalo lilianza kujengwa mwaka 2012 na kutegemewa kumalizika mwaka 2013 japokuwa bado kukamilika ambapo serikali ilitenga shilingi bilioni 2.3 lakini hadi kufikia katika hatua ya sasa, tayari shilingi bilioni 1.6 zimeshatumika kupitia fedha za Ruzuku ya Miradi ya Maendeleo (CDG) ambapo kwa sasa imefutwa.

Awali akitoa taarifa ya jengo hilo Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga John Msemakweli amesema kuwa halmashauri tayari imekwisha tuma andiko maalum na kupeleka wizara ya fedha na OR – TAMISEMI ili kuwezeshwa kumalizia jengo hilo litakalokuwa na ofisi 76 na kumbi 2.

“Hadi sasa tumeandika andiko maalum la jumla ya shilingi 716,933,989 ili kukamilisha mradi huu, tunategemea jengo hili likikamilika litakuwa na ofisi 76 na kumbi 2 ambazo zitakuwa zinatosheleza mahitaji ya ofisi za watumishi wote walio katika makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya,” Alibainisha.


Jengo hilo ambalo lipo karibu na jengo la Manispaa ya Sumbawanga halijatengewa fedha za kuliendeleza tangu mwaka wa fedha 2015/2016 hadi sasa.


Katika hatua nyingine, Mh. Wangabo alimuagiza Mkurugenzi huyo kuunda timu ya kuhakikisha wanapambana na mifugo inayoharibu barabara kwani serikali inatumia mabilioni kuzitengeneza na kuzikarabati na hivyo si vyema uharibifu huo ukaendelea.

Tigo Yamwaga Zawadi Kibao Kwenye Shindano la Tigo Fiesta 2018 Chemsha Bongo Trivia

$
0
0


 Mshindi wa Shindano la Tigo Fiesta 2018 Chemsha Bongo Trivia toka Mkoa wa Tanga, William Alloyce Mganga(katikati)akikabidhiwa zawadi ya simu aina ya Tecno Camon X toka kwa Meneja Mauzo wa Tigo mkoa wa Tanga, Robert Kasulwa(kulia) na kushoto ni Msimamizi wa Duka la Tigo mkoa wa Tanga Hassani Nkua.Ili kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya  http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia.
3I8A1491
Mshindi wa Shindano la Tigo Fiesta 2018  Chemsha Bongo Trivia , Zam Mohammed Zam wa Mombasa Unguja akipokea shilingi milioni moja kutoka kwa Msimamizi wa Kampuni ya Tigo tawi la Zanzibar, Adolph Mapenzi baada ya kushinda katika promosheni hiyo, makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za Tigo ziliopo Malindi Unguja

MAGAZETI YA LEO IJUMAA OKTOBA 19,2018

Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>