Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1701 | 1702 | (Page 1703) | 1704 | 1705 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza jana na wananchi kuhusu athari za ukataji miti ovyo kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Isalalo kata ya Wasa wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe.
  Baadhi ya Watendaji aliokuwa ameongozana nao katika mkutano huo wa hadhara katika kijiji cha Isalalo.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akimsikiliza huku akiwa anaandika swali analoulizwa na zungumza Ester Mwakanja kuhusiana athari za ukataji miti ovyo kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Isalalo kata ya Wasa wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akisoma karatasi katika mkutano wa hadhara ulioufanya katika kijiji cha Isalalo kata ya Wasa wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe .( PICNA NA LUSUNGU HELELA)


  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga amewaonya watu wenye tabia ya kukata miti ovyo kuwa Serikali hatosita kuwachukulia hatua za kisheria kutokana na kushamiri kwa uharibifu wa misitu mkoani Songwe.

  Ametoa onyo hilo wakati alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Isalalo kata ya Wasa wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe. Amesema kufuatia kasi ya ukataji miti ovyo unaoendelea kwa ajili ya mbao na nishati ya mkaa katika maeneo hayo kunatishia kutoweka kwa mvua wanayoitegemea kwa ajili kilimo cha mazao ya kahawa, mahindi pamoja na mazao mengine.

  Amewaeleza Wananchi hao kuwa uharibifu huo ukiendelea utaawathiri wao wenyewe kwa vile mvua itakoma kunyesha katika maeneo yao. Amewataka wakikata mti wapande miti na wale wanaokata miti kwa ajili ya Nishati ya mkaa wafuate kanuni na sheria ili kuepuka kukabiliana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)

  Aidha, Mhe. Hasunga Amewataka Wananchi hao kuwa hata pale inapotokea wanataka kukata mti wa mwembe uliopo katika nyumba zao wanatakiwa kuomba kibali kutoka TFS. Pia, Waziri Hasunga amewaagiza TFS itoe miche 10,000 kwa Kata ya Wasa msimu wa mvua utakapokaribia kufuatia ombi la mwanakijji Kasian Mwanjala alilowasilisha kwa Mhe. Hasunga kuwa wanataka kupanda miti ili wanakosa miche.

  Katika hatua nyingine, Mhe.Hasunga ambaye ni Mbunge katika jimbo la Vwawa lililopo mkoani hapo amewahakikishia wananchi wake kuwa ifikapo mwakani kata ya Wasa itapata umeme wa REA hali itakayosaidia kuboresha maisha kwa wananchi wake. “Moja ya ahadi yangu niliyoitoa kwenu ni kuhakikisha katika jimbo langu wananchi mnapata umeme, hadi sasa tayari nguzo za umeme zimeanza kuwekwa ” amesema Mhe Hasunga.

  0 0

  HATIMAYE Canada imeandika historia baada ya kuwa nchi ya pili duniani baada ya Uruguay kwa kuhalalisha rasmi matumizi ya bangi hadharani kama dawa na starehe. 
   
   
  Jarida la Times nchini humo limeeleza kuwa baada ya miaka 95 ya kuzuiliwa kwa matumizi ya bangi hatimaye Canada imetangaza rasmi matumizi ya bangi na soko la kuuza bangi lilifunguliwa rasmi usiku wa kuamkia jumatano. Na hiyo imekuja baada ya watu zaidi ya milioni 15 kutoa maoni yao katika sanduku la posta na kupendekeza uhalalishaji wa matumizi ya bangi. 

  Imeelezwa kuwa mwaka 2001 bangi iliruhusiwa kutumika kama dawa na hiyo ni baada ya shinikizo kutoka kwa wabunge nchini humo na kwa sasa watatununua na kutumia bangi hadharani bila bughudhi na polisi watahakikisha na kukabiliana na visa vya uendeshaji magari wakiwa wamelewa bangi. Uhalalishwaji huo umekuja baada ya ahadi ya waziri mkuu wa nchi hiyo Justin Trudeau wa Liberal Party of Canada katika kampeni zake za mwaka 2015. 

  Na baadhi ya wananchi wameonekana kununua bidhaa hiyo huku wakipewa risiti ambazo zimekatwa kodi. Historia inaeleza kuwa mwaka 1923 matumizi ya bangi yalipigwa marufuku nchini humo na kufikia mwaka 2001 bangi iliruhusiwa kwa matumizi ya dawa pekee na Oktoba 17 mwaka huu bangi imehalalishwa rasmi kwa matumizi ya dawa na starehe.

  0 0

  Mhandisi wa Maji Wilaya ya Nanyamba, Moses Msuya akimuonyesha Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa mpango ya utekelezaji wa mradi wa Nanyamba-Mlanje.
  Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akikagua matenki ya mradi wa Nanyamba-Mlanje katika Wilaya ya Nanyamba, mkoani Mtwara.
  Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akiwa kwenye mradi wa Mkwiti, katika wilaya Tandahimba, mkoani Mtwara.
  Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Newala, akiongozwa na Mkuu wa Wilaya, Aziza Mangosongo.
  Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akisikiliza taarifa inayosomwa na Mhandisi wa Maji Wilaya, Nsajigwa Sadiki. 


  Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amekerwa na wakandarasi wababaishaji ambao wamekuwa wakichangia miradi mingi ya maji kuchelewa kukamilika au kujenga miradi yenye viwango duni na kuisababishia Serikali matatizo na wananchi wake.

  Hali hiyo imetokana na kukosekana kwa mkandarasi katika eneo la kazi kwenye mradi wa Nanyamba-Mlanje, katika Wilaya ya Nanyamba mkoani Mtwara wakati alipofika kukagua mradi, kitendo ambacho hakukifurahia.

  Profesa Mbarawa amesema alitegemea kumkuta mkandarasi huyo site ili aweze kuzisikia changamoto zinazomkabili na kuzipatia ufumbuzi ili mradi huo uweze kukamilika mara moja na kutoa huduma.Akiongea na wakazi wa Mlanje, Profesa Mbarawa amesema ametoka kuidhinisha malipo ya Shilingi Milioni 93 kwa mkandarasi huyo wiki iliyopita lakini ameshangazwa na kutomkuta akifanya kazi, na kuwaambia wakandarasi wasiokaa site ni wababaishaji na hawafai.

  “Wakandarasi wa namna hii ni wababaishaji hawatufai na siwataki kwa sababu wanaigombanisha Serikali na wananchi, wakikwamisha mipango ya Serikali na wananchi wakiendelea kukosa maji bila sababu za msingi. Sitaki wakandarasi wa aina hii na ndio maana tumewafukuza waliokuwa kwenye miradi ya Kigoma na Lindi kutokana na tabia za ubabaishaji’’, amesema Profesa Mbarawa.

  “Ni lazima popote kwenye miradi ya maji nitakapotembelea nikute mkandarasi akiwa site, sitaki jambo hili lijirudie tena. Nataka wakandarasi wanaothamini kazi tunazowapa na kumaliza kwa wakati”, amesisitiza Profesa Mbarawa.

  Akiwa katika Wilaya ya Tandahimba, Profesa Mbarawa ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya vijiji 10 wilayani humo, ambapo miradi ya vijiji 6 vya Likolombe, Kidoo, Malamba, Matogoro, Mihambwe na Mkupete imekamilika baadhi ya miradi hiyo ikiwa ni mipya na mingine imefanyiwa upanuzi.

  Wakati miradi iliyobaki ya vijiji 4 vya Chaume-Mkonjowano ukarabati wake umekamilika, Mahuta ukarabati na upanuzi umekamilika, Jangwani-Maheha ukarabati wake umefikia asilimia 95 na Litehu-Libobe ukarabati na upanuzi wake umefikia asilimia 95.

  Pia, Serikali inatekeleza mradi wa Mkwiti wilayani Tandahimba ambao utaongeza huduma ya maji kwa wananchi wapatao 21, 384 katika vijiji 14, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP II) ambao kwa sasa ujenzi wake umefikia asilimia 66 na utagharimu Shilingi Bilioni 8.5.

  0 0


  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini katika kijiji cha Saza kilichopo wilayani Songwe mkoani Songwe ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili katika mkoa huo yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini tarehe 18 Oktoba, 2018.
  Msimamizi wa uchimbaji madini katika Mgodi wa Dhahabu wa Sunshine uliopo katika kijiji cha Mbangala wilayani Songwe mkoani Songwe, Evarist Lukuba (kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa tatu kushoto mbele) mara alipofanya ziara katika mgodi huo.
  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa New Luika uliopo katika kijiji cha Mbangala wilayani Songwe mkoani Songwe, Honest Mrema (wa pili kulia mbele) akielezea majukumu ya mgodi huo kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo pamoja na msafara wake mara alipofanya ziara katika mgodi huo.
  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (mbele) pamoja na msafara wake wakiendelea na ziara katika Mgodi wa Dhahabu wa New Luika uliopo katika kijiji cha Mbangala wilayani Songwe mkoani Songwe.
  Kutoka kushoto, Afisa Madini Mkazi katika Mkoa wa Mbeya, Sabai Nyansiri, na Afisa Madini kutoka Ofisi hiyo, Godfrey Nyanda, wakinukuu maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani) kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya.
  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mary-Prisca Mahundi, (wa pili kushoto) mara baada ya kuwasili katika Wilaya hiyo kabla ya kuanza ziara yake rasmi.  ………………………..

  Na Greyson Mwase, Songwe  Serikali kupitia Wizara ya Madini imepiga marufuku usafirishwaji wa kaboni kwa ajili ya kuchenjulia madini ya dhahabu kutoka mkoa mmoja hadi mwingine na kusisitiza kuwa haitasita kumchukulia hatua za kisheria mchimbaji wa madini atakayekiuka agizo hilo.

  Agizo hilo limetolewa leo tarehe 18 Oktoba, 2018 na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo katika mkutano wake na wachimbaji wadogo wa madini katika kijiji cha Saza kilichopo wilayani Songwe mkoani Songwe ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili katika mkoa huo yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

  Katika ziara yake Nyongo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Samwel Jeremeah, Afisa Madini Mkazi katika Mkoa wa Mbeya, Sabai Nyansiri, Afisa Madini anayesimamia wilaya za Songwe na Chunya, Athuman Kwariko, Maafisa Madini kutoka Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Mbeya, Ndege Bilagi na Mhandisi Godfrey Nyanda, vyombo vya ulinzi na usalama vya Wilaya pamoja na waandishi wa habari.

  Akizungumza na wachimbaji hao, Naibu Waziri Nyongo alisema kuwa lengo la Serikali kupitia Wizara ya Madini kupiga marufuku usafirishwaji wa kaboni kutoka katika mkoa mmoja kwenda mwingine tangu Juni mosi mwaka huu lilikuwa ni kuhakikisha kila mkoa unapata mapato stahiki kupitia ujenzi wa mitambo ya kuchenjua madini kwa kutumia kaboni.

  “Kama Serikali tunataka kuhakikisha kila mkoa unajenga mitambo ya kuchenjua madini badala ya kwenda kuchenjulia katika mikoa ya jirani kwa kutumia kaboni na kukosa mapato stahiki,” alifafanua Nyongo. Alisisitiza kuwa, Serikali haitasita kutaifisha kaboni itakayokamatwa ikisafirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine ikiwa ni pamoja na kuwachukulia wahusika hatua za kisheria.

  Akielezea mikakati ya Wizara ya Madini katika kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini, Nyongo alisema kuwa Wizara imeshaanza kutenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo nchini na kuwataka kuunda vikundi na kuomba leseni ili waweze kufanya shughuli zao za uchimbaji wa madini kwa kufuata sheria na kanuni za madini.

  Aliongeza kuwa, Wizara ya Madini imeanza kujenga vituo vya umahiri kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini kuhusu namna bora ya kubaini, kuchimba na kuchenjua madini na kueleza zaidi kuwa moja ya kituo kinachotarajiwa kujengwa ndani ya kipindi cha miezi sita kitakuwa katika Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.

  Aidha, Nyongo aliwataka wachimbaji wadogo kuhakikisha wanalipa mrabaha na kodi mbalimbali zinazotakiwa Serikalini na kuwataka maafisa madini nchini kuhakikisha wanasimamia vyema ukusanyaji wa mapato hayo.

  Pia, aliwataka wachimbaji wadogo wa madini kuepuka uchenjuaji wa madini kwa kutumia zebaki kwani ina madhara makubwa katika uharibifu wa mazingira na binadamu.

  Akielezea namna bora ya usimamizi wa viwanda vitakavyojengwa kwa ajili ya kuchenjua madini ya dhahabu kwa kutumia kaboni, Nyongo alisema mbali na kuhakikisha wamiliki wanakuwa na leseni za uchenjuaji wa madini, wataalam wa mazingira kutoka Wizara ya Madini watapita na kukagua ili kuhakikisha kuwa viwanda vinajengwa katika mazingira mazuri ambayo hayatakuwa na athari katika makazi ya wananchi.

  Awali wakizungumza katika mkutano huo kwa nyakati tofauti wachimbaji wadogo waliwasilisha kero mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa maeneo kwa ajili ya kuendesha shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini, ushuru na tozo nyingi, pamoja na kutoshirikishwa katika mikataba baina yao na wawekezaji wakubwa wa madini.

  0 0  Eliafile Ndossi ambaye ni mwezeshaji kutoka Shirika la Tanzania Mindset Network akitoa elimu juu ya madhara ya kupinga Ukeketaji kwa viongozi wa Vitongoji, Vijiji pamoja na wazazi na walezi katika kijiji Cha Pemba na Kyoruba.


  Christina Edward mkazi wa kijiji cha Nyabisaga kata ya Pemba akibainisha changamoto wanazokumbana nazo kama wazazi katika suala zima la kupinga Ukeketaji baada ya kutembelewa Nyumbani kwake na watoa elimu ya kupinga Ukeketaji kupitia Shirika la Tanzania Mindset Network.
  Ghati Samweli ambaye ni mwezeshaji kutoka Shirikala Tanzania Mindset Network akitoa elimu ya kupinga Ukeketaji baada ya kutembelea moja ya familia katika kijiji cha Nyabisaga Wilayani Tarime Mkoani Mara ambapo watoa elimu hiyo wameamua kufika Nyumba kwa Nyumba lego ni kunusuru mtoto wa kike hasiweze kukeketwa.
  Picha ya Pamoja baada ya kutolewa kwa elimu ya kupinga Ukekeytaji katika kijiji cha Nyabisaga.
  Eliafile Ndossi ambaye ni mwezeshaji kutoka Shirika la Tanzania Mindset Network akitoa elimu juu ya madhara ya kupinga Ukeketaji kwa viongozi wa Vitongoji, Vijiji pamoja na wazazi na walezi katika kijiji Cha Pemba na Kyoruba.
  Rouben Makuri mwenyekiti wa kijiji cha Kyoruba akichangia hoja juu ya kupinga ukeketaji kwa mtoto wa kike ambapo amewasihi wazazi na walezi kuondokana na sula la kupeleka watoto ili kukeketwa.

  0 0

  NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

  MBUNGE wa viti maalum Mkoani Pwani, Subira Mgalu ,ametoa msaada wa taa za kisasa, zinazotumia umeme wa jua katika zahanati zaidi ya hamsini ,kati ya 121 ambazo zinatoa huduma ya kuzalisha akinamama Mkoani humo .

  Lengo la kusambaza taa hizo ni kupunguza changamoto ya ukosefu wa umeme wa uhakika katika zahanati hizo .Akielezea juhudi hizo alizozichukua ,wakati akizungumza na wananchi wa Ngolongo na Mloka ,wilayani Rufiji ,Subira alisema alifanya tathmini na tafiti na kubaini zipo zahanati 121 mkoa mzima ambazo zinatumia solar ama hakuna umeme kabisa .

  Alieleza kufuatia tathmini hiyo ,alifanya jitihada za kupata taa hizo ,zenye uwezo wa kuongeza umeme kwenye simu ,kuwasha tochi na taa ili kusaidia kuboresha huduma ya afya."Kwa sasa nimeshazifikia zahanati karibia 50 na natarajia kuzimaliza zahanati 121 ,kwa kuzipatia taa mbili mbili kila zahanati ifikapo mwishoni mwa mwezi huu" alifafanua .

  Wakati huo huo":; baadhi ya wakazi akiwemo Issa Kabandika alisema ,umeme ukifika Mloka utakuwa kichocheo cha maendeleo yao lakini bado haujafika mitaani kwani nguzo zipo barabara kuu .Sultan Mbena na Hiyari Puga walimshukuru Rais Dk.John Magufuli na serikali kwa hatua ya mradi huo wa stigo ,na wanaomba uendelee kwa maslahi yao na nchi .

  Akijibu malalamiko ya wananchi hao, kuhusu kutofikiwa na umeme ,mbunge huyo ambae pia ni naibu waziri wa nishati alilitaka ,shirika la umeme (Tanesco ) kwamba umeme usiishie barabarani ufike kwa wananchi .

  "Serikali inatekeleza mradi mkubwa wa hydro power (stigo) wilayani hapa ,hivyo nawahakikishia wananchi vipo vijiji vimetajwa kufikishiwa umeme kupitia mradi huu""Vijiji vitapata umeme kila mtaa ikiwemo Ngolongo Mashariki ,Ngolongo Magharibi ,Kilimani Mashariki ,Kilimani Magharibi ,Mloka, Nyamwinyili,Ndundunikanza,Msona,Kipugila ambavyo vimetajwa kwenye andiko la mradi kitaifa na kimataifa ," alifafanua Subira .

  Alieleza, lakini wale wenye mahitaji ya umeme wa haraka Tanesco iwaunganishie na kuwawekea nguzo na wengine wasubiri umeme wakati mradi ukitekelezwa.
  Mbunge wa viti maalum Mkoani Pwani ,Subira Mgalu akikabidhi taa za kisasa kwa ajili ya zahanati ya Ngolongo wilayani Rufiji Mkoani Pwani.(picha na Mwamvua Mwinyi)

  0 0


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametoa kiasi cha Milioni 50 kwa timu ya Taifa ya Tanzania.

  Fedha hizo ni  kwa ajili ya safari ya mchezo wa marudiano baina ya Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' dhidi ya Lesotho utakaochezwa Novemba 16.

  Akiwa anazungumza na wachezaji na viongozi katika hafla ya chakula cha Mchana Ikulu Jijini Dar es Salaam, Dkt Magufuli amesema kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya safari na sio kwa wasindikizaji.

  “Nawapa Millioni 50 kwa ajili ya safari ya Lesotho, fedha hizi zitumike kwa ajili ya wanaotakiwa kusafiri tu, sio mambo ya wachezaji 15, viongozi wasindikazaji 30. Haya mambo yafikie mwisho.” amesema Dkt Magufuli.

  Mbali na hilo amewataka wachezaji kujituma na kuacha mambo ya kihuni, "Wachezaji wasipoacha uhuni watakuwa wanafunga magoli mengine ila ya uwanjani watashindwa"

  Taifa Stars  katika mchezo uliopita dhidi ya Cape Verde walifanikiwa kuondoka na ushindi wa goli 2-0 mechi iliyopigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa na kufikisha jumla ya alama 5 akishika nafasi ya pili nyuma ya Uganda.

  0 0


  Pichani ni daraja la Kijiji cha Getamok linalosuasua kukamilika kwake kutokana na changamoto mbalimbali

  Na, Vero Ignatus, Karatu

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameiagiza kampuni ya Kiure Engineering Ltd kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa daraja uliogharimu Sh. milioni 250 fedha zilizotolewa na serikali kwaajili ya ujenzi wa daraja hilo eneo la Getamok.

  Gambo aliyasema hayo wakati alipokuwa akikagua ujenzi wa daraja hilo ambalo ni muhimu kwaajili ya wakazi wa maeneo hayo.

  Alisema kampuni ya Kiure Engineering Ltd imekuwa kikwazo kikubwa cha kutokamilisha ujenzi wa daraja hilo kwa muda uliopangwa hali iliyopelekea kuongezewa muda wa miezi nane ili wamalize ujenzi huo.

  Amesisitiza kuwa lazima wakandarasi wazawa wakajithamini pale wanapoomba kazi za ujenzi wa aina mbalimbali za miradi ya maendeleo na kama hawana uwezo huo wa kufanya kazi ni vyema wakaacha kuepusha kuingia matatani kwani serikali inapotoa fedha kwaajili ya jambo fulani ni lazima likamilike kwa wakati.

  "Tunawapa hadi Oktoba 23 mwaka huu daraja hili liwe limeshakamilika, na ikifika saa kumi jioni Mkuu wa Wilaya hii atakuja na OCD kuangalia kama mmekamilisha kinyume na hapo tutatumia nguvu za ziada kusukuma jambo hili''alisema Gambo

  Pia niwaonye nyinyi wakandarasi wazawa mjitathimini maana mnaomba kazi halafu mnaleta ubabaishaji wa mara kwa mara na hamkamilishi kazi zenu kwa wakati, kama hamuwezi kazi acheni " alisema Gambo.

  Naye Msimamizi wa Mradi huo kutoka kampuni ya Kiure Engineering Ltd, Said Idd alikiri ni kweli wamechelewesha kukabidhi daraja hilo kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo mvua kubwa kunyesha mwezi Machi mwaka huu pia walipokuwa wakichimba udongo walikumbana na chemchem kubwa ya maji hali iliyopelekea kuchelewa kutekeleza ujenzi wa daraja hilo.

  Alisema kwa sasa daraja hilo limekamilika kwa asilimia 90 na kazi iliyobaki hivi sasa ni kusambaza mawe na kuweka kingo za maji ikiwemo kurekebisha kasoro mbalimbali kwaajili ya kukabidhi kwa DC wa Karatu Bi. Theresia Mahongo.

  Naye DC, Mahongo alisema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa daraja hilo na mara kwa mara alikuwa anaenda eneo hilo kuangalia ujenzi wake na kusisitiza kuwa ni vyema sasa wakandarasi wakapima uwezo wa kazi wanazotaka kuzifanya kwani uzembe wa mkandarasi huyo umepelekea kukatwa fedha zake za mradi huo baada ya kuzembea kazini.

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Japan hapa nchini Shinichi Goto Ikulu jijini Dar es Salaam.
  2-Japan
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Balozi wa Japan hapa nchini Shinichi Goto mara baada ya kupokea Hati zake za Utambuliso Ikulu jijini Dar es Salaam.
  3-Japan
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Japan hapa nchini Shinichi Goto mara baada ya kupokea Hati zake za Utambuliso Ikulu jijini Dar es Salaam.
  4-Japan
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Japan hapa nchini Shinichi Goto mara baada ya kupokea Hati zake za Utambuliso Ikulu jijini Dar es Salaam.
  5-Geogia
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Georgia hapa nchini Zurab Dvalishivili Ikulu jijini Dar es Salaam.
  7-Georgia
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi mteule wa Georgia hapa nchini Zurab Dvalishivili  mara baada ya kupokea Hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  8-Georgia
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Balozi wa Georgia hapa nchini Zurab Dvalishivili  mara baada ya kupokea Hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  9-Georgia
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Georgia hapa nchini Zurab Dvalishivili  mara baada ya kupokea Hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  10-Geoargia
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Georgia hapa nchini Zurab Dvalishivili  mara baada ya kupokea Hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

  0 0


   MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akizungumza wakati wa mahafali ya 8 ya Darasa la Saba katika Shule ya Kana Eglish Medium Central  School ya Jijini Tanga ambapo alitumia nafasi hiyo kuhamasisha mpango wa Toto Afya Kadi kwa watoto na wazazi.
   Afisa Uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Nico Kasebwa kushoto akisisitiza jambo kwa mmoja wa wananchi wa Jiji la Tanga aliyefika kwenye banda lao kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko huo uli kuweza kunufaika na huduma za matibabu wakati wanapougua kushoto ni Afisa Uanachama NHIF Jesca Nyau
   Afisa Uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Nico Kasebwa akimuonyesha kitu kwenye kipeperushi chenye maelezo ya Mpango wa Toto Afya Kadi mkazi wa Jiji la Tanga Daudi Mbisco mara baada ya kutembelea banda lao
   Sehemu ya wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo
   Sehemu ya Wazazi na Walezi wakiwa kwenye Mahafali hayo

  MFUKO wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) umewapa mbinu bora za wazazi na walezi kuwapa zawadi muhimu watoto wao katika maisha yao ni kuwaingiza kwenye mpango wa Toto Afya kadi ili waweze kunufaika na huduma za matibabu.

  Hayo yalisemwa na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga Ally Mwakababu wakati akizungumza na wanafunzi na walezi kwenye mahafali ya nane ya darasa la Saba katika shule ya Kana Central English Medium Primary School.

  Alisema wakati wa ukuaji wa watoto wamekuwa wakikumbana na magonjwa mbalimbali ambayo yanaweza kupelekea kukwamisha ndoto zao lakini wanapokuwa wameandikishwa kwenye mpango wa Toto Afya Kadi wanaweza kupata matibabu kwenye vituo mbalimbali vya Afya.

  “Nimekuja hapa kwa lengo kuu moja kuhamaisha umuhimu wa wazazi na walezi kuwapa zawadi ya Bima watoto wao kupitia mpango wa Toto Afya Kadi kwani hakuna anayweza kuelezea gharama za matibabu wakati mtoto wake anayweza kuungua”Alisema.

  Hata hivyo alisema kwamba wazazi wanapowaingiza watoto wao kwenye mpango huo unawapa uhakika wa matibabu na wanaweza kuwa na kumbukumbu nzuri ya maisha yao .

  0 0


  Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), (katikati) akikagua mtambo wa kuchakata nyanya akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard kasesela (Kulia) wakikagua kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Iringa jana Alhamisi Octoba 19, 2018. Mwingine Pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha Darsh Ndg Bhadresh Pandit. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
  Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wakifatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), alipotembelea na kukagua kiwanda cha Darsh jana Alhamisi Octoba 19, 2018.
  Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), (katikati) akikagua mitambo ya kuchakata nyanya akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard kasesela (Kulia) wakikagua kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Iringa jana Alhamisi Octoba 19, 2018.
  Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), akikagua mitambo ya kuchakata nyanya akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard kasesela wakikagua kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Iringa jana Alhamisi Octoba 19, 2018.

  Na Mathias Canal-WK, Mseke-Iringa


  Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), amewataka wakulima wa nyanya Mkoani Iringa kuchangamkia fursa ya kuongeza uzalishaji wa nyanya ili kuakisi uhitaji wa viwanda vya nyanya ikiwa ni pamoja na kiwanda cha Darsh chenye uwezo wa kusindika Tani 250 za nyanya kwa siku.


  Waziri Tizeba ametoa mwito huo jana Octoba 18, 2018 wakati akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.


  Kiwanda hicho kinafanya shughuli za ukusanyaji wa nyanya kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Iringa na mikoa ya jirani na kufanya usindikaji wa nyanya ambapo hupeleka kiwanda cha Arusha kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na nyanya ambazo huuzwa ndani na nje ya nchi.


  Waziri Tizeba, aliwataka wakulima hao kujiunga kuanzisha kikundi cha ushirika ili kuwa na urahisi wa mikopo ili kuwezesha uwezo wa uwekezaji kupitia kilimo cha umwagiliaji kitakachoongeza tija katika kipato chao na jamii kwa ujumla.


  “Wakulima wa nyanya hapa Igwachanya na hata katika maeneo mengi nchini wanalima kwa kutegemea mvua na uzalishaji huwa mdogo na usiokidhi mahitaji ya soko hivyo nawasihi kuongeza uzalishaji wa nyanya kwani soko la uhakika lipo” Alikaririwa Dkt Tizeba


  Kadhalika, Waziri wa kilimo aliutaka uongozi wa kiwanda hicho kuongeza wigo wa ununuzi wa nyanya katika mikoa mingine ya uzalishaji ikiwemo mkoa wa Dodoama na Singida.


  Awali akisoma taarifa ya kiwanda hicho mbele ya mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha Darsh Ndg Bhadresh Pandit ameishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuhimiza sera ya uchumi wa viwanda kwa kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuendelea kuzitafutia ufumbuzi changamoto chache zinazojitokeza hivyo kuendelea kulinda maslahi mapana ya Taifa.


  Alisema uanzishwaji wa kiwanda hicho ulitokana na ushawishi uliopatikana kutoka kwenye muunganiko wa wajasiliamali vijijini (MUVI) na Techno Serve walipotembelea kiwanda cha Darsh Mkoani Arusha.


  Naye Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela alimpongeza waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba kwa kutenga muda wake na kukubali kufanya ziara Wilayani Iringa ili kubaini changamoto zinazowakabili wakulima wa nyanya nchini.

  0 0

  NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Saadalla ‘Mabodi’ (kulia), akimnadi na kumuombea kura mgombea wa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Jang’ombe Ramadhan Hamza Chande(kushoto) katika kampeni za CCM Uchaguzi wa Jang’ombe zilizofanyika Uwanja wa Kwaalinatu.
  BAADHI ya Wana –CCM walioudhuria katika Mkutano huo wa kampeni uliofanyika Kwaalinatu.
  Mgombea uwakilishi wa CCM Jimbo la Jang’ombe Ramadhan Hamza Chande akiomba kura kupitia mkutano huo wa kampeni uliofanyika uwanja wa Kwaalinatu.
  MKE wa Rais mstaafu wa awamu ya nne ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete akimuombea kura Mgombea wa tiketi ya CCM Uchaguzi wa Jang’ombe Ramadhan Hamza Chande.

  NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

  NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ amewatahadharisha wanachama wa chama hicho, kuwa makini kwa kuepuka propaganda na njama chafu zinazofanywa na viongozi wakuu wa CUF waliotengeneza migogoro bandia ili waweze kupata huruma ya wananchi kuingia madarakani.

  Tahadhari hiyo aliitoa wakati akimnadi mgombea wa nafasi ya Uwakilishi kwa tiketi ya CCM Ramadhan Hamza Chande katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Jang’ombe huko katika Uwanja wa Kwaalinatu.

  Alisema CUF wametengeneza mgogoro bandia wenye lengo la kuiyumbisha CCM mwaka 2020 mbinu dhaifu ambazo hazitoweza kufanikiwa mbele ya CCM ya sasa iliyokuwa imara na inayokwenda sambamba na ulimwengu wa siasa za Kisayansi.

  Dk. Mabodi alisema ushahidi pekee wa kuonyesha kuwa viongozi wa CUF hawana uadui kwa upande wa Zanzibar na Tanzania bara ni pale waliposhirikiana kumnadi mgombea wa Chama hicho katika kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Liwale ambao mgombea wa CCM ameibuka mshindi.

  Akimnadi na kumuombea kura Mgombea wa CCM katika Uchaguzi wa mdogo wa Jimbo la Jang’ombe Ramadhan Hamza Chande, Dk. Mabodi aliwasihi Wana-CCM na wananchi wa Jimbo hilo kumchagua mgombe huyo ili aendeleze mambo mema yaliyoasisiwa na viongozi wa waliopita wa nafasi hiyo.

  Alisema CCM imempitisha Ramadhan ikiamini kuwa ana uwezo na anafaa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwa kasi kubwa.

  “Mgombea huyo ni mbunifu, mchapakazi na mwenye uzalendo wa kweli nakuombeni wananchi wa Jang’ombe mfanye maamuzi sahihi ya kumpa kura nyingi za ndio aweze kuwatumikia kwa uadilifu.

  Pia Ramadhan Hamza nakusisitiza kuwa ukipewa nafasi ya Uongozi wewe utakuwa ni kiongozi na mwakilishi wa Wananchi wote na sio CCM hivyo utatakiwa kuwatumikia bila upendeleo wala ubaguzi”, alisisitiza Dk.Mabodi.

  Akieleza namna Chama kilivyojipanga kuwaletea maendeleo Wananchi, Dk.Mabodi alisema CCM inafanya siasa za kuimarisha maendeleo katika sekta zote Mijini na Vijijini ili kumaliza ahadi zote zilizotolewa katika Uchaguzi mkuu uliopita kabla ya mwaka 2020.

  Dk.Mabodi aliongeza kuwa Chama kimekuwa kikishuka kwa wananchi wa makundi yote kwa lengo la kuratibu changamoto na kuzitatua kwa wakati.

  Naye Mgombe wa tiketi ya CCM katika Uchaguzi mdogo wa Jang’ombe Ramadhan Hamza Chande, aliwaomba wananchi na wanachama wa CCM wa jimbo hilo kukichagua Chama Cha Mapinduzi kupitia mgombe huyo aweze kuwatumikia na kuharakisha maendeleo ya Jang’ombe.

  Katika maelezo yake Ramadhan alisema atakapopewa rdhaa na wananchi hao ya kuwa kiongozi atashirikiana nao kupanga mikakati ya kupanga mikakati yenye tija ndani ya Jimbo hilo.

  Awali Mke wa Rais mstaafu wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Tanzania Mama Salma Kikwete, alisema matunda yanayotokana na sera na mipango endelevu ya CCM yanaonekana wazi wazi kwani Zanzibar na Tanzania bara zote zinang’ara kwa miundombinu ya kisasa ya barabara na kuimarika kwa Sekta za Elimu, Afya pamoja na Maji safi na Salama.

  Alisema CCM imekuwa ikiendeleza misingi ya maendeleo iliyoasisiwa na Vyama vya ukombozi vya ASP na TANU vilivyoungana na kuunda taasisi hiyo kwa nia ya kuongeza nguvu za kusimamia ufanisi sera na mipango ya maendeleo kwa wananchi wote.

  Akizungumza katika Mkutano huo wa kampeni aliyekuwa kiongozi wa ngazi za juu wa CUF Julius Mtatiro aliyejiunga na CCM, aliwaomba wananchi wa Jang’ombe kumchagua mgombea wa CCM kwani vyama vya upinzani hasa CUF vina matatizo na migogoro isiyoweza kutatulika kutokana na ubinafsi na sera za ubaguzi za viongozi wa vyama hivyo.

  Mtatiro alitumia mkutano huo kuwaomba radhi Watanzania hasa Vijana wa CCM kuwa kipindi yupo upinzani alitumiwa vibaya na CUF kukwamisha mipango ya maendeleo iliyokuwa ikitekelezwa na Serikali zote mbili za Chama Cha Mapinduzi.

  Alisema kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 aliyohudumu katika CUF, hakuna hata siku moja Chama cha CUF ama UKAWA waliyoweza kushauri ama kupongeza mambo mema yanayofanywa na CCM badala yake waliponda na kupotosha umma kwa makusudi.

  “Nakuombeni vijana wenzangu mnisamehe sana nilipoteza muda na nguvu nyingi kwa upinzani lakini baada ya kuona kasi ya maendeleo katika CCM ya sasa nikaona bora nitoke kule na kujiunga na CCM ili niwatumikie Watanzani ’’, alieleza Mtatiro.

  Akizungumza Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Abdallah Hasnuu Makame, akimuombea kura mgombea wa CCM katika mkutano huo wa kampeni alisema mafanikio makubwa yaliyopatikana yametokana uwepo wa tunu za Taifa ambazo ni Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 pamoja na Muungano wa Serikali mbili.

  Alisema wananchi wa Jimbo la Jang’ombe hawatojutia maamuzi yao endapo watamchagua mgombea wa CCM aweze kuwaongoza kwa kipindi cha miaka miwili kufika 2020, kwani historia ya siasa za Tanzania toka mwaka 1992 ulipoasisiwa mfumo wa vyama vingi CCM ndio Chama pekee kilichoweza kutimiza kwa vitendo matakwa ya wananchi katika mfumo wa vyama vingi.

  Akizungumza Mwakilishi wa Viti Maalum CCM Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Faida Mohamed Bakari, aliwaomba wanawake na vijana wa Jang’ombe kumchagua Ramadhan awe mwakilishi kwani ana uwezo mkubwa wa kusimamia maslahi ya makundi hayo sambamba na kuanzisha miradi mbali mbali itakayoweza kuwanufaisha wananchi.

  Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Jang’ombe unatarajiwa kufanyika Octoba 27, mwaka 2018, kufuatia aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo Abdallah Diwani kuvuliwa uanachama kwa makosa ya ukiukaji wa maadili ya Chama Cha Mapinduzi.

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya kuchangisha fedha za maboresho ya majengo ya Chuo cha ST. Mark's Jaji Mkuu Mstaafu Mh. Agustino Ramadhani akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam kuhusiana na Harambee itakayofanyika kesho tarehe 20.10.2018 chuoni hapo ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Spika wa Bunge Mh. Job Ndungai. Kiasi cha Tsh Milioni 800 zinahitajika katika ukarabati wa kituo hicho.
  Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha St. Mark's Dkt. Peter Kopweh akifafanua jambo kuhusiana na harambee hiyo.

  Jaji Mkuu mstaafu, Agustino Ramadhani ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya kuchangisha fedha za kuboresha majengo ya Chuo cha St. Mark’s kilichopo Buguruni Marapa amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza ili kusaidia harambee kwa ajili ya kuboresha majengo ya chuo hicho kiasi cha fedha tsh Milioni 800.

  Hayo yalisemwa wakati alipokuwa na mkutano na waandishi wa habari chuoni hapo ambapo alisema  uamuzi wa kuboresha majengo hayo umetokana na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Kuagiza wafanye hivyo.

  “Nimewaiteni waandishi wa Habari kwa lengo la kuwataka kutusaidia kuutangazia umma kuwa siku ya jumamosi Octoba 20, 2018 tutakuwa na harambee kwa ajili ya kuchangisha fedha za kuboresha majengo yetu kama tulivyo agizwa na TCU” alisema Jaji Ramadhani.

  Zaidi ya Tsh Milioni 800 zinatarajiwa kuchangishwa katika harambee hiyo itakayofanyika chuoni hapo kuanzia saa nane mchana na mgeni rasmi anatarajia kuwa Spika wa Bunge Job Ndungai. 

  Kwa ambao hawatoweza kufika katika harambee hiyo wanaweza pia kuchangia katika njia zifuatazo

  TIGO PESA : 0677058716

  CRDB BANK: 0150237155300 (HOLLAND BRANCH)

  TIB : 004600000860601 (SAMORA DAR ES SALAAM)
  0 0

   Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson leo ametembelea Benki ya CRDB na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, AbdulMajid Mussa Nsekela.Dkt. Tulia alisema dhumuni la Mkutano huo ni kumpongeza, Nsekela kwa uteuzi wake wa kuwa Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Benki ya CRDB na kufanya mazungumzo juu ya masuala mbalimbali ya kiuchumi na maendeleo.
   Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki wa Benki ya CRDB, AbdulMajid Mussa Nsekela, walipokuwa wakizungumza ofisini kwake, Azikiwe jijini Dar es salaam.
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson akifurahi jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki wa Benki ya CRDB, AbdulMajid Mussa Nsekela wakati alipokuwa akisaini kitabu cha wageni.

  0 0

  Msanii Chin  Beez akimkabidhi simu aina ya Tecno R6 na Tiketi ya kwenda kushuhudia Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote mteja wa Tigo, Lole Kway. Ndani ya msimu huu wa Tigo Fiesta wateja wanaoenda kupata huduma kwenye maduka wanapata zawadi mbalimbali.
  IMG_20181019_134418
  Msanii, Dogo Janjaroo akigawa vipeperushi kwa wateja ndani ya Duka.
  IMG_20181019_143726
  Meza ya Majaji ikiongozwa na Adam Mchomvu(katikati) na kulia, Joh Makini na kushoto ni Evans Lyatuu toka Moshi Fm kwenye kinyang’anyiro cha kumpata mwakilishi wa Tigo Fiesta Supa Nyota toka mkoa wa Kilimanjaro leo.
  IMG_20181019_142648
  Msanii atakaye uwakilisha mkoa Kilimanjaro kwenye fainali za Tigo Fiesta Supa Nyota 2018, Samson Msweta maarufu kama Samson Classic akiimba kwa staili ya kufokafoka kwenye kinyang’anyiro cha kumpata mwakilishi huo leo kwenye viwanja vya Hugo.
  IMG_20181019_134921
  Msanii Richie Mavoko akisaidia kutoa Huduma kwa mteja wa Tigo Pesa, Bi. Gloria Mushi kwenye Duka la Tigo lililopo barabara ya Mawenzi mjini Moshi
  IMG_20181019_134452
  Msanii Rose Ree akisaidiana na mtoa Huduma wa  Duka laTigo barabara ya Mawenzi mjini Moshi, Felister Tarimo leo mara baada ya wasanii kutembelea Duka hilo.
  IMG_20181019_134312
  Msanii Chin Beez akitoa hiduma kwa wateja walioenda kupata huduma ndani ya Duka la Tigo lililopo barabara ya Mawenzi mjini Moshi leo.

  0 0


   
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemkabidhi Waziri wa Nchi, OR-TAMISEMI, Selemani Jafo orodha ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ili awachukulie hatua baada ya kugoma kuhamia katika kituo chao cha kazi na kuendelea kuishi jijini Dodoma.
   
  *Ni wa halmashauri ya wilaya ya Bahi waliogoma kuhamia kituo cha kazi


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemkabidhi Waziri wa Nchi, OR-TAMISEMI, Selemani Jafo orodha ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ili awachukulie hatua baada ya kugoma kuhamia katika kituo chao cha kazi na kuendelea kuishi jijini Dodoma.

  Amemkabidhi orodha hiyo leo (Ijumaa, Oktoba 19, 2018) baada ya mkuu wa wilaya hiyo Bibi Mwanahamisi Mukunda kusoma taarifa ya wilaya, ambayo pamoja na mambo mengine alieleza kuwa watumishi wote wameshamia kwenye kituo chao cha kazi na wanaishi. Waziri Mkuu alikuwa katika kikao na Watumishi wa Halmashuri hiyo.

  “Mkuu wa wilaya umedanganywa watumishi bado wanaishi jijini Dodoma, walichokifanya baadhi wamejiunga watatu na wamekodi chumba kimoja. Namkabidhi Waziri wa TAMISEMI orodha ya watumishi hawa ambao wamegoma kuishi kwenye kituo chao cha kazi ili uwashughulikie”

  Waziri Mkuu amesema watumishi hao wamegoma kuhamia katika kituo chao cha kazi licha ya Serikali kuwataka kufanya hivyo.”Maelekezo hatuyatoi kwa ajili ya kujifurahisha, bali tunataka utekelezaji ufanyike ili wananchi waweze kuhudumiwa ipasavyo.”
  Jumatano, Juni 27, mwaka huu, Waziri Mkuu wakati akizinduavituo 51 vya kufuatilia taarifa za hali ya hewa, vituo 15 vya haidrolojia, kanzidata ya taarifa za hali ya hewa na kituo cha operesheni na mawasiliano ya dharura wilayani Bahi, aliwaagiza watumishi wa Halmashauri hiyo wanaoishi nje ya kituo chao cha kazi wahamie kituoni kwao.

  Waziri Mkuu alisema Serikali inataka watumishi wa umma wawajibike na waishi katika vituo vyao vya kazi. “Nawataka watumishi wote wa wilaya hii wanaoishi jijini Dodoma wawe wamehamia hapa ifikapo Julai 30 mwaka huu na wasiohamia nipewe majina yao.”

  Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka viongozi na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Bahi wakiwemo madiwani na wakuu wa idara wahakikishe wanamaliza tofauti zao na washirikiane katika kufanyakazi kwa lengo la kuboresha maendeleo ya wananchi.

  Awali, Waziri Mkuu alikagua mradi wa ujenzi wa nyumba ya walimu katika shule ya sekondari ya Mpalanga yenye uwezo wa kukaliwa na walimu sita, ambapo amesema ameridhishwa na ujenzi huo. Mradi huo unagharimu zaidi ya sh. milioni 140.

  Pia Waziri Mkuu amezindua daraja la Chipanga ambalo ujenzi wake umegharimu sh. bilioni 2.18 na kisha alitembelea kituo cha Afya cha Bahi ambako alikagua wodi ya wazazi na kuzungumza na akinamama ambao waliishukuru Serikali kwa kuboresha huduma za afya.

  0 0   Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Dkt. Detlef Waechter akibadilishana nyaraka za mkataba wa ufadhili na Mheshimiwa Simai Mohamed Said (Mwakilishi Jimbo la Tunguu),  Mwenyekiti wa  Bodi ya Wadhamini ya Busara Promotion katika Ubalozi wa Ujerumani Dar es Salaam jana Oktoba 18,2018.
  DSC010
  Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Dkt. Detlef Waechter akiagana baada ya kutiliana saini mkataba wa ufadhili na Mheshimiwa Simai Mohamed Said (Mwakilishi Jimbo la Tunguu),  Mwenyekiti wa  Bodi ya Wadhamini ya Busara Promotion katika Ubalozi wa Ujerumani Dar es Salaam jana Oktoba 18,2018.
  DSC005
  Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Dkt. Detlef Waechter akitiliana saini mkataba wa ufadhili na Mheshimiwa Simai Mohamed Said (Mwakilishi Jimbo la Tunguu),  Mwenyekiti wa  Bodi ya Wadhamini ya Busara Promotion katika Ubalozi wa Ujerumani Dar es Salaam jana Oktoba 18,2018.


     

  …………………
  DAR ES SALAAM.
  Serikali ya Ujerumani kupitia kwa Balozi wake Nchini Tanzania, Dkt. Detlef  Waechter imetiliana saini ya ufadhili na Taasisi ya Busara Promotions waandaaji wa tamasha la Sauti za Busara linalofanyika kila mwaka visiwani Zanzibar.
  Ujerumani imekubali kuchangia fedha ambazo zitaenda kufanikisha shughuli za tamasha hilo msimu wa 16, mwakani 2019.
  Hafla hiyo imefanyika Oktoba 18, 2018  katika ofisi za Ubalozi huo Jijini Dar es Salaam.
  Tukio hilo la kutiliana saini, limewahusisha Balozi huyo wa Ujerumani nchini Dkt. Detlef  Waechter  pamoja na Mwenyekiti wa Tamasha hilo la Sauti za Busara, Mheshimiwa Simai Mohammed Said ambaye pia (Mwakilishi jimbo la Tunguu).
  Ufadhili huo ni juhudi za Wizara ya Mambo ya Nje ya nchini Ujerumani  katika kuunga mkono utamaduni wa Tanzania kwa kufadhili Tamasha hilo la kimataifa la Muziki ambalo limekuwa pia kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi visiwani Zanzibar.
  Balozi Dkt. Detlef Waechter amemwakikishia  Mwenyekiti wa Bodi wa Busara Promotions kuwa wataendelea kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza utamaduni wa Mtanzania kwa kuongeza fursa na tija zitokanazo na zao la ushirikiano wa Nchi hizo mbili.
  Kwa upande wao Busara Promotions wamesema kuwa maandalizi ya tamasha hilo lenye kauli mbiu “Where African Music Stars Shine Brightly”, yanaendelea na tayari wamechapisha majina ya Wasanii na bendi pamoja na Nchi wanazotoka miongoni mwao ni Staa wa muziki wa Hip Hop Fareed Kubanda maarufu kama “Fid Q” kutoka Tanzania.
  Pia wapo: Mokoomba (Zimbabwe), Afrigo Band (Uganda), Fadhilee Itulya (Kenya), Ifrikya Spirit (Algeria), Rajab Suleiman & Kithara ( Zanzibar), Tune Recreation Committee, (Afrika Kusini), Ithrene (Algeria).
  Wengine ni: Hoba Hoba Spirit (Morocco), M’Toro Chamou (Mayotte/Reunion), Trio Kazanchis +2 (Ethiopia/Switzerland), Faith Mussa (Malawi), Shamsi Music (Kenya), Sofaz  (Reunion), Dago Roots( Reunion), Lydol  (Cameroun), Jackie Akello (Uganda).
  Wamo pia: S Kide & Wakupeti Band (Tanzania), Tausi Women’s Taarab (Zanzibar), Mkubwa na Wanawe Crew (Tanzania), Damian Soul (Tanzania) na  Wamwiduka Band (Tanzania).
  Tamasha  hilo la 16 litafanyika Mji Mkongwe Zanzibar kuanzia tarehe 7 – 10 February 2019 huku  majukuwaa 3 tofauti yatawaka moto kwa muziki wa moja kwa moja ‘live’ kwa muda wa siku zote za tamasha kuanzia asubuhi, mchana na Usiku.

  0 0


  Na Grace Semfuko –MAELEZO

  Serikali ya Marekani imesema inatambua juhudi za Serikali ya Tanzania za kuvutia wawekezaji na kwamba Mazingira mazuri ya uwekezaji yanayofanywa na Serikali yatasaidia kufikia Uchumi wa kati na wa Viwanda.

  Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Dkt Inmi Patterson amesema kufuatia juhudi hizo Serikali yake inaungana na Tanzania katika kuwezesha wawekezaji wengi wa Kimarekani kuja kuwekeza Nchini. Balozi Patterson ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Geoffrey Mwambe alipomtembelea Ofisini kwake na kuzungumzia masuala mbalimbali ya uwekezaji ikiwemo namna bora ya kuvutia wawekezaji wa nje.

  Kaimu Balozi huyo ameihakikishia Serikali ya Tanzania kwamba itatoa kila aina ya ushirikiano ili kufanikisha Tanzania ya viwanda. “Ubalozi wa Marekani,nchi ya Marekani na Wamarekani wote waliopo nchini Tanzania wapo tayari kusaidiana na serikali katika kuhakikisha nchi ya viwanda inafanikiwa,” amesema.

  Pia ametoa ushauri kwa Serikali ya Tanzania kuwa ili ifanikiwe kwenye uchumi wa viwanda ni vema ikaendelea kushirikiana ba sekta binafsi katika kufanikisha uwekezaji na kwamba amefurahishwa na mazungumzo ambayo ya Serikali ya Tanzania inafanya kati yake na sekta binafsi. “Hakuna nchi ambayo inaweza kufikia uchumi wa viwanda bila kushirikisha sekta binafsi pamoja na wawekezaji wa ndani na nje.Hivyo ni vema sekta binafsi zikapewa fursa katika uwekezaji ili kufikia Serikali ya Viwanda ambayo sisi tunaiunga mkono kwa nguvu zote,” amesema.

  Kuhusu mazungumzo yao amesema yamejikita katika kukuza biashara ,uwekezaji na kukuza uchumi na kwamba kutokana na mazingira mazuri yaliyopo ni imani yao Tanzania itafikia kuwa nchi ya viwanda. Kwa upande wake Mwambe amesema TIC jukumu lao ni kukutanisha sekta mbalimbali za Serikali na binafsi ambapo mabalozi wa Tanzania waliopo nchi mbalimbali wanahakikisha wanashiriki kikamilifu kuvutia kuvutia wawekezaji.

  Amefafanua ni hivyo hivyo kwa ubalozi wa Marekani nchini kupitia Kaimu Balozi wake wamekuwa na wajibu wa kuhamasisha uwekezaji baina ya nchi hizo mbili. “Ni jukumu lake kuhamasisha wawekezaji wa Marekani kuja Tanzania kuwekeza.Tunafahamu juhudi za Serikali ya Marekani katika kuisaidia Tanzania kwa kuhakikisha inajiimarisha kiuchumi.

  Amesema jitihada za Kaimu Balozi zimesaidia kufanikisha kwa ujio wa kundi la wafanyabiashara wa Florida kuja nchini kwa ajili ya kuangalia mazingira ya uwekezaji na kwamba wanatarajia kuja siku za karibuni. ” Tumezungumza maeneo mbalimbali ambayo tunaweza kushirikiana ili kutimiza malengo ya Serikali ya kutekeleza uwekezaji nchini. Kama nchi tunataka kuendelea,lazima tutafute njia sahihi za kuendeleza mifumo ya uwekezaji.

  “Tunataka kujenga nchi,hivyo tuna jukumu kubwa la kujenga sekta binafsi na tukiwa na private sekta tutakwenda vizuri kama Taifa.Sisi TIC tutahakikisha sekta binafsi inaimarika na maamuzi ya Serikali ni kuijenga sekta binafsi na mjumbe wa bodi yangu ni mtu mmoja kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi Bw.Godfrey Simbeye,” amefafanua.

  Ameongeza Serikali yenye rushwa huwa haikusanyi kodi huo ni msemo wa Mwalimu Nyerere, hivyo jukumu lililopo ni kuhakikisha rasilimali zilizopo zinatunufaisha wote.”TIC tunataka kutengeneza umoja na mazingira yanayokubalika kwenye uwekezaji zaidi”.

  0 0   Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza na Mgeni wake Mheshimiwa Prof. Lou Jiwei ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la China (CPPCC) alipomtembelea hii leo na kufanya nae mazungumzo kwenye Ukumbi wa Spika Jijini Dodoma.
  PIC 2
  Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akisalimiana na Balozi wa China hapa nchini Mheshimiwa Wang Ke alipomtembelea na kufanya nae mazungumzo hii leo kwenye Ukumbi wa Spika Jijini Dodoma. Balozi huyo aliambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la China (CPPCC) kutoka nchini ChinaMheshimiwa Prof. Lou Jiwei.
  PIC 3
  Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akimvalisha vazi la Kimasai mgeni wake ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la China (CPPCC) Mheshimiwa Prof. Lou Jiwei kama ishara ya Utamaduni wa Kitanzania walipokutana na kufanya mazungumzo kwenye Ukumbi wa Spika Jijini Dodoma hii leo.

older | 1 | .... | 1701 | 1702 | (Page 1703) | 1704 | 1705 | .... | 1897 | newer