Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

TWANGA PEPETA KUSHEREHEKEA MIAKA 20 TANGU KUANZISHWA KWAKE


NEWS ALERT:BASI LA NEW FORCE LATUMBUKIA MLIMA KITOGA LIKIWA NA ABIRIA,MAJERUHI 12 WATAJWA MAJINA YAO

$
0
0
Leo tarehe 16/10/2018 majira ya saa 13:00 mlima Kitonga katika barabara kuu ya Iringa – Morogoro Wilaya ya Kilolo na Mkoa wa Iringa . Gari lenye namba za usajili T 852DHA aina ya ZHONGTONG BUS mali ya NEWFORCE wa Dsm likiendeshwa na IDD s/o BAKARI MALULI , kabila Mhehe, miaka 38 na mkazi wa Dsm akikwepa gari lenye namba za usajili T.623DMG, likiendeshwa na RAMADHAN S/O SALIMIN ambapo basi hilo la kampuni ya New force kwa kuepuka kugongana uso kwa uso liliacha barabara na kupinduka hatimaye kusababisha majeruhi 12 ambao ni .

1.LEONARD s/o POTES, KYUSA, 32 YRS WA MPANDA 
2.JAMES s/o NDUNGURU, MNGONI, 49YRS, WA DSM, 
3.IDD s/o BAKARI MALULI, MHEHE, 38YRS, DEREVA WA DSM 
4.BAKARI s/o ZAYUMBA, MBONDEI, 27YRS WA MBEYA 
5.NDEKE S/o MWAIFUSE 53YRS, WA DSM
6.TABIA d/ o FRANCIS, KYUSA, 65YRS, WA MBEYA 
7 .GRACE D/o BONIPHACE, MCHAGA 24YRS, WA MOROGORO 
8.GRORY D/o BONIPHACE MCHAGA 24YRS, WA MOROGORO 
9.ANNA D/o ALEX 22YRS, MUHAYA, WA DSM
10.AZIZA D/o MUHINA, MZIGUA, 43YRS WA DSM 
11.SAWA s/o MTINGALA MAKUA, 52YRS, WA DSM
12.IAN D/o EVANCE 2YRS, KYUSA WA MBEYA

Waliolazwa hospitali teule ya Itunda wilaya ya Kilolo. Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa gari namba T623 kulipita gari lingine bila kuchukua tahadhari..Amedhibitisha Kaimu Rpc Kamishna msaidizi wa Polisi. DEUSDEDIT KASINDO.
 Mmoja wa wasamaria wema akimsaidia mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo
 Baadhi ya abiria walionusurika kifo wakitoka kwenye basi hilo mara baada kupata ajali 

UBUNGO NA KIGAMBONI KUNUFAIKA NA MRADI MKUBWA WA KUTEKETEZA TAKA

$
0
0



Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa uteketezaji wa taka kwa njia salama bila kuathiri mazingira. Warsha hiyo ya siku moja imefanyika katika ukumbi wa NIMR jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwakilishi wa Shirikika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uendelezaji wa Viwanda (UNIDO) Dkt. Stephen Kagbo.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi. Magdalena Mtenga akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa warsha ya mradi wa uteketezaji wa taka kwa njia salama bila kuathiri mazingira. Mradi huo kwa nchi ya Tanzania utatekelezwa katika Wilaya za Kigamboni na Ubungo.
????????????????????????????????????
Wataalamu kutoka Taasisi za Serikali, Sekta binafsi na Asasi zinazojishughulisha na masuala ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine (wa nne kutoka kulia) mara baada ya uzinduzi wa warsha ya uteketezaji wa taka kwa njia salama bila kuathiri mazingira, jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………..
Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na UNIDO hii leo wamezindua warsha ya Mradi wa kudhibiti kemikali zitokanazo na uchomaji wa taka katika maeneo ya wazi. Akizindua warsha hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa NIMR jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine amesema kuwa mradi huo unatarajia kuja na mapendekezo ya namna ya kupunguza athari za uchomaji taka katika mazingira.

Balozi Sokoine amesema kuwa lengo kubwa la warsha hiyo ya wataalamu ni kujadili mbinu bora za uchomaji taka bila kuathiri mazingira. “Tunategemea mradi huu utatusaidia sana sisi watu wa mazingira katika kudhibiti uchomaji hovyo wa taka, uchomaji unaofanyika maeneo ya wazi unazalisha kemikali ambazo zinadumu kwa muda mrefu katika mazingira.” Alisisitiza Balozi Sokoine.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi. Magdalena Mtenga amesema kuwa jamii inapaswa kufahamu kuwa taka ni mali na ni vema zikabadilishwa kuwa fursa, ikiwa ni njia bora ya kusukuma mbele agenda ya uchumi wa viwanda.  “Uchomaji wa taka unasababisha uzalishaji wa kemikali hatarishi kwa mazingira ambazo hudumu kwa muda mrefu na sisi lengo letu ni kudhibiti hii hali ndio maana tumekuja na huu mradi ili  taka zirejerezwe na kutumika kwa matumizi mengine” Mtenga alisisitiza.

Kwa upande mwingine Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uendelezaji wa viwanda (UNIDO)  Dkt. Stephen Kagbo amesema uchafuzi wa mazingira ni suala linalozikabili nchini nyingi barani Afrika hivyo ujio wa mradi huu utatoa fursa ya kuja na teknolojia ya kisasa ya kuteketeza taka kwa namna bora bila kuathiri mazingira.

Utekelezaji wa Mradi huo utaanza katika Wilaya za Ubungo na Kigamboni na nchini nyingine zinazonufaika na mradi kama huu ni pamoja na Botswana, Lesotho, Madagascar, Mozambique, Swaziland na Zambia.

DC Uyui Atoa Mkono wa Pole kwa Wananchi Walioathiriwa na Uvamizi wa Tembo

$
0
0








Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Gift Msuya akitoa mkono wa pole kwa mmoja wa wananchi walioathirika na uvamizi wa tembo katika kijiji SawMill Kata ya Migiri Wilayani humo. (Picha zote na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Uyui)


Na  Mwandishi wetu- Uyui

Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora Mhe. Gift Msuya amewatembealea na kuwapa pole wananchi walioathirika na uvamizi wa Tembo katika Kijiji cha SawMill Kata ya Migiri.

Akizungumza na wananchi hao mara baada ya kuwatembelea na kuwafariji amesema kuwa ameshawaagiza Askari wanyamapori kufika katika kijiji hicho na kuwaondosha tembo hao ili wasiendele kuleta madhara katika eneo hilo ikiwemo kuharibu mali na kudhuru wananchi .

“Jukumu la Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa salama na wanaendelea na shughuli zao za uzalishaji kama kawaida ndio maana nimewaagiza askari wanyamapori kufika hapa mara moja na kuwaondosha tembo hawa” ; Alisisitiza Msuya

Akifafanua amesema kuwa tembo hao ambao idadi yao haikufahamika waliingia katika kijiji hicho na kuanza kuharibu mazao ya chakula yaliyokuwa yamehifadhiwa na wananchi hao katika vihenge.

Pia aliwataka wananchi katika maeneo hayo kuishi kwa tahadhari kwa kutoa taarifa haraka pale watakapoona wanyama hao wameingia katika makazi yao ili Serikali ichukue hatua stahiki kwa haraka kuepusha maafa.

Tembo hao ambao idadi yao haikufahamika mara moja walivamia makazi ya watu usiku wa kumakia tarehe 15 Oktoba na kusababisha uharibifu wa wa mazao ya chakula yaliyokuwa yamehifadhiwa na wananchi hao.

MRADI WA UPANUZI WA BANDARI YA DAR ES SALAAM WAFIKIA ASILIMIA 42

$
0
0


 Naibu Waziri wa Uchukzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akikagua maendeleo ya mradi wa upanuzi wa bandari, ujenzi wa magati na kuongeza kina cha sehemu ya kupakia na kupakua mizigo wakati wa ziara yake kwenye Bandari ya Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mhandisi Karim Mataka
JPEG. NA. 2
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akipata maelezo kutoka kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mhandisi Karim Mataka (aliyenyoosha mkono) kuhusu maendeleo ya mradi wa upanuzi wa bandari, ujenzi wa magati na kuongeza kina cha kupakia na kupakua mizigo wakati wa ziara yake kwenye bandari ya Dar es Salaam
JPEG. NA. 3
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mhandisi Karim Mataka (wa kwanza kulia) kuhusu utengenezaji wa zege maalumu kwa ajili ya kujengea magati ya bandari wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi wa upanuzi wa bandari, ujenzi wa magati na kuongeza kina cha kupakia na kupakua mizigo kwenye Bandari ya Dar es Salaam
JPEG. NA. 4
Picha ya muonekano wa maendeleo ya mradi wa upanuzi wa bandari, ujenzi wa magati na kuongeza kina cha kupakia na kupakua mizigo bandarini wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani)  kwenye Bandari ya Dar es Salaam

………………………..
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa upanuzi wa bandari, ujenzi wa magati na kuongeza kina cha kupakia na kupakua mizigo kwenye Bandari ya Dar es Salaam

Nditiye amesema kuwa ameridhishwa na hatua iliyofikiwa ya maendeleo ya mradi huo kwa kufikia kiwango cha asilimia 42 ya mradi huo ambapo mradi huo ulitegemewa ukabidhiwe mwezi Oktoba mwaka huu 2018. Amefafanua kuwa ilibidi  mradi huo ufanyiwe maboresho ili kuendana na matakwa ya mradi ili uweze kubeba mizigo mizito na utakamilika mwezi Juni mwakani, 2019.

Pia, ameongeza kuwa, ili kuweza kwenda sambasamba na muda wa mkataba wa mradi huo, ujenzi wa gati namba moja ulikuwa unaendelea na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka huu, 2018 badala ya mwezi Aprili mwakani 2019, “hivyo tuko ndani ya muda wa mkataba,” amesema Nditiye.

Naye Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Karim Mataka amemweleza Nditiye kuwa maendeleo ya mradi ni mazuri japo walikumbana na changamoto ya kukukutana na udongo laini baharini kwenye eneo la ujenzi wa mradi huo ambapo iliwalazimu kuimarisha eneo hilo ili bandari iweze kubeba mzigo wa kontena mpaka tano zikiwa zimepandana kutokea chini kwenye eneo la kupakia na kupakua mizigo
Mataka ameongeza kuwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania imejipanga ili kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika kwa wakati ndani ya kipindi cha miezi 36 kuendana na matakwa ya mkataba wa mradi huo ambao ulianza rasmi tarehe moja Julai mwaka 2017 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka 2020. Mataka amesema kuwa mradi huo unagharimu jumla ya shilingi bilioni 336 na unajengwa na mkandarasi wa kampuni ya kutoka China ya CHEC (LYU wei)

Amefafanua kuwa mradi wa upanuzi wa bandari, ujenzi wa magati na kuongeza kina cha kupakia na kupakua mizigo, utaiwezesha bandari kuhudumia meli kubwa zaidi ambapo hivi sasa hamna kina cha mita 12 ambapo inazifanya meli nyingi kuwa kwenye foleni na kulazimika kusogeza meli moja moja ambapo mradi huu ukikamilika, bandari itakuwa na uwezo wa kushusha mizigo ya kutoka kweye meli kubwa saba kwa wakati mmoja

TAA Yasaidia Mafuta Kinga Jua Kwa Walemavu Wa Ngozi

$
0
0

Katibu Mkuu wa Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) Bw. Mussa Kabimba (aliyesimama) akizungumia changamoto wanazokutana nazo watu wenye Ualbino. Katikati ni Kaimu Meneja Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bi. Naomi Semadio na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Jeshi la Wokovu, Bw. Masoud Babu (kushoto).

Kaimu Meneja Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bi. Naomi Semadio akitoa hotuba fupi, kabla ya zoezi la ugawaji wa mafuta kinga jua ya Ngozi kwa watoto wenye Ulemavu wa ualbino. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Jeshi la Wokovu, Bw Masoud Babu.

Kaimu Meneja Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bi. Naomi Semadio (katikati) akimkabidhi chupa ya mafuta kinga jua ya Ngozi kwa mmoja wa watoto wenye ulemavu wa Ualbino. Wengine ni Katibu Mkuu wa Chama cha Watu wenye Ulemavu Ualbino Tanzania (TAS) , Bw. Mussa Kabimba (kulia) na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Jeshi la wokovu Mwl. Masoud Babu (kushoto).
Akitoa neno la Shukrani mmoja wa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi, Joyce Mahona akiishukuru Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kwa msaada huo mkubwa waliotoa wa mafuta kinga jua ya Ngozi, ambayo yatawasaidia tofauti na awali walikuwa wakitumia mafuta ya kawaida.

……………………….

Na Mwandishi Wetu

WAKATI Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ikisaidia mafuta maalum chupa 55 ya ngozi kwa walemavu wa ngozi, imetoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kuwasaidia mahitaji hayo na mengine yanayowakabili.

Akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Kaimu Meneja Rasilimali Watu na Utawala, Bi. Naomi Semadio, amesema Mamlaka kupitia sera yake ya kusaidia jamii (Corporate Social Responsibility Policy) imechangia mafuta kinga jua ya ngozi kwa Chama cha Watu wenye Ulemavu wa ngozi (TAS), kama sehemu ya mchango wake kwa chama hicho katika kuwajali na kuwahudumia Watanzania wenye ualbino katika kukabiliana na changamoto ya afya ya ngozi.

Semadio amesema kufuatia maombi hayo kwa kushirikiana na TAS wametoa mafuta hayo aina ya Infinity care SPF 30 Sunscreen yenye thamani ya Tshs 1,375,000 kwa watoto wa shule za msingi Uhuru Mchanganyiko na Jeshi la Wokovu (Salvation Army), lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba watoto hawa wanapata fursa ya elimu katika mazingira mazuri kwa kuhakikisha hali nzuri ya afya ya Ngozi.

« Mamlaka inatambua wajibu wake katika kuhakikisha inaboresha maisha ya watanzania, kwa kusaidia wahitaji katika jamii na inawajali watu wote wenye ulemavu bila ya kuwabagua na kwa kudhihirisha hilo imekuwa na wafanyakazi walemavu mbalimbali na wanawajali kama walivyo watu wazima wasiokuwa na ulemavu, » amesema.

Amesema moja ya msingi mkuu wa Mamlaka ni kuwajali wateja wake na wadau wake, TAA ipo kwa ajili ya kutoa huduma kwa watu wa hali zote, kwa kuzingatia hilo Mamlaka itaendelea kuwasaidia wadau wake mbalimbali wenye uhitaji.

Tayari Mamlaka imeshatoa misaada kwa watu mbalimbali ukiwemo Umoja wa Wabunge Wanawake wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kujenga vyoo vya mfano vya watoto wa kike wenye ulemavu kwa majimbo yote Tanzania nzima, pia imefanikisha tamasha la Urithi Wetu lililofanyika Jijini Dar es Salaam.

Dira ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ni kuwa mtoaji wa huduma za viwanja vya ndege kwa kiwango cha Kimataifa; wakati Dhima yetu inasema Kutoa huduma bora na viwezeshi katika viwanja vya ndege kwa kuzingatia ufanisi katika matumizi ya rasilimali zilizopo.

Mamlaka inasimamia na kuendesha viwanja 58 vilivyopo chini ya serikali, ambapo katika hivyo viwili ni vya Kimataifa ambavyo ni Julius Nyerere (JNIA) na Kilimanjaro (KIA). Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania inatoa shukrani kwa wadau wetu na serikali, ambapo kwa namna moja au nyingine wanamchango katika kusaidia watu wenye ulemavu.

Hatahivyo, Semadio ametoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo nchini kujitokeza kusaidia walemavu kulingana na mahitaji yao. Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TAS, Mussa Kabimba amesema asilimia 70 ya walemavu wa ngozi wanapoteza maisha wakiwa wadogo kutokana na kushambuliwa na ugonjwa wa saratani ya ngozi.

Kabimba amesema mazingira ya familia za wanaozaliwa na ulemavu wa ngozi, zinatokana na wakulima na wafugaji, ambapo upatikanaji wa mafuta kinga jua ya ngozi, kofia pana na miwani kwa ajili ya kuboresha afya zao ni changamoto kubwa. «Ninaomba wadau wengine waguswe ili kutoa msaada kwa vijana wetu ili waweze kuboresha afya zao, tunawashukuru sana Mamlaka kwa namna ambavyo mlivyosaidia mafuta haya, pia nawashukuru walimu kwa kusaidia kuwaweka wanafunzi kuwa na afya nje, » amesema

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Jeshi la Wokovu (Salvation Army), Masoud Babu ameishukuru TAA kwa kusaidia wanafunzi wao, ambao sasa hawatashambuliwa na maradhi mbalimbali ikiwemo saratani ya ngozi, ambayo imekuwa ikikwamisha jitihada zao za kujiendeleza kielemu. Akitoa neno la Shukrani mmoja wa wanafunzi, Joyce Mahona alishukuru kwa msaada huo mkubwa ambayo utawasaidia kwa kuweka ngozi zao katika afya bora, kwani awali walikuwa wakipaka mafuta ya kawaida pekee.

Chaneli ya Utalii Kuzinduliwa Disemba Mwaka Huu

$
0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Susan Mlawi akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kamati inayoshughulikia uanzishwaji wa Chaneli ya Runinga ya Utalii leo jijini Dodoma. Chaneli hiyo inaanzishwa kufuatia agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipotembelea studio za Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) mnamo tarehe 16, Mei, 2017. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Profesa Adolf Mkenda.

………………………..

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO

Serikali imeazimia kuzindua Chaneli ya Utalii inayotegemewa kurushwa kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) mnamo mwezi Disemba mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Susan Mlawi wakati wa Kikao cha Kamati inayofuatilia uanzishwaji wa chaneli hiyo.

Bi. Susan amesema kuwa vikao vya wadau na wataalam mbalimbali vitakavyowezesha uanzishwaji wa chaneli hiyo vinaendelea ambapo katika kikao hicho imetolewa taarifa ya hatua zilizofikiwa ambazo zimeonekana kuleta mafanikio makubwa. “Tumekusudia kuifanya chaneli hii ambayo tunatarajia uzinduzi wake utafanyika mwezi Disemba mwaka huu kuwa na vipindi bora vyenye kugusa utalii wa kila aina. Aidha, tunategemea kuweka lugha mbalimbali ambazo zitasaidia watu wengi kutoka mataifa mbalimbali kuweza kuitazama.”

Ameongeza kusema kuwa hadi kufikia muda huu tayari fedha za mitambo itakayoweza kuanzisha chaneli hiyo zimeshapatikana na ametoa rai kwa TBC kutoa kipaumbele katika maandalizi ya chaneli hiyo na kuandaa utaratibu maalum wa kusimamia matangazo yake. Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa ni muhimu chaneli hiyo ionekane sehemu mbalimbali duniani ili kupata wadau wengi watakaoweza kuweka matangazo yao na kuiwezesha chaneli hiyo kujiendesha.

Amefafanua kuwa matangazo kupitia chaneli hiyo itakayotangaza utalii wa Tanzania yataingiza fedha nyingi ambazo zitasaidia kujiendesha badala ya nchi kutumia fedha nyingi kuutangaza utalii nje ya nchi. “Kupitia chaneli hii, tunataka utalii uchukue sura mpya katika kuvutia uwekezaji kwani itawezesha Tanzania kujitangaza kiutalii katika nchi mbalimbali duniani na kuongeza Pato la Taifa,” alisema Prof. adolf Mkenda.

Naye Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo amesema, nchi ikiwa na chaneli yenye maudhui ya utalii itasaidia Watanzania kufahamu kwa urahisi vivutio vilivyopo nchini pia itawafanya wadau mbalimbali kufahamu sio tu utalii bali pia masuala ya kiutamaduni. Vile vile chaneli hii itawawezesha wadau kufahamu maeneo mahususi ya upigaji picha za mnato na jongefu ambazo zitaifanya nchi kujulikana zaidi nje ya nchi kupitia picha.

Uanzishwaji wa chaneli ya utalii kupitia TBC ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa wakati alipotembelea shirika hilo mnamo mwaka 2017.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO OKTOBA 17,2018


HALOTEL TANZANIA YAADHIMISHA MIAKA MITATU YA HUDUMA TANGU IANZISHWE HAPA NCHINI TANZANIA

$
0
0
Naibu Mkurugenzi wa Halotel Tanzania Nguyen Van Son, akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za makao makuu ya Halotel wakati wa hafla fupi ya kusherekea maadhimisho ya miaka mitatu ya kampuni hiyo kutoa huduma za mawasiliano Tanzania tangu ilipozinduliwa nchini mwaka 2015. (kushoto) ni Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa Kampuni hiyo Mhina Semwenda.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel Mhina Semwenda, akizungumza na waandishi wa Habari, katika ofisi za makao makuu ya Halotel ambapo akielezea mafanikio waliyoyapata kwa kuwafikishia huduma za mawasiliano wananchi waliopo vijijini ndani ya miaka mitatu ya utoaji huduma. wakati wa hafla fupi ya kusherekea maadhimisho ya miaka mitatu ya kampuni hiyo, Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Halotel Tanzania Nguyen Van Son na katibu wa kampuni hiyo Nguyen Thi Thuy Linh
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel Mhina Semwenda, akijibu maswali ya wanahabari wakati alipozungumza nao katika ofisi za makao makuu ya Halotel ambapo ameelezea mafanikio waliyoyapata kwa kuwafikishia huduma za mawasiliano wananchi waliopo vijijini ndani ya miaka mitatu ya utoaji huduma. wakati wa hafla fupi ya kusherekea maadhimisho ya miaka mitatu ya kampuni hiyo, Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Halotel Tanzania Nguyen Van Son
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel Mhina Semwenda, akizungumza na waandishi wa Habari, katika ofisi za makao makuu ya Halotel ambapo akielezea mafanikio waliyoyapata kwa kuwafikishia huduma za mawasiliano wananchi waliopo vijijini ndani ya miaka mitatu ya utoaji huduma. wakati wa hafla fupi ya kusherekea maadhimisho ya miaka mitatu ya kampuni hiyo, Katikati ni Naibu Mkurugenzi wa Halotel Tanzania Nguyen Van Son na kushoto katibu wa kampuni hiyo Nguyen Thi Thuy Linh


Kampuni ya Simu za mkononi ya Halotel Tanzania inaadhimisha miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa huduma za Kampuni hiyo ya mtandao wa simu za mkononi hapa nchini. 

Hayo yamezungumzwa na Naibu Mkurugenzi wa Halotel Tanzania Bw. Nguyen Van Son wakati akizungumza na waandishi wa habri kuhusu siku hii ili kuonyesha mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na Kampuni hiyo kwa kipindi chote tangu ilipoanza kutoa huduma hapa nchini 

Nguyen Van Son amesema kuna mikakati mipya kuanzia sasa ambapo Halotel Tanzania inakusudia kuwekeza kiasi cha Dola za Marekani Milioni 700 katika sekta ya mawasiliano nchini Tanzania ikiwa na malengo ya kuwa nafasi ya pili na kuwafikia wateja zaidi ya Milioni 6 katika kipindi cha miaka mitano ya kwanza.

Pamoja na mipango hiyo , Halotel Tanania imekusudia kuendelea kuiboresha huduma ya utumaji wa pesa kwa njia ya Mtandao ijulikanayo kama ‘Halopesa’ sambamba na kitengo cha teknolojia ya mawasiliano ‘ICT’ kwa ajili ya wateja wa Mashirika Binafsi na Serikali kwa ujumla.

Ameongeza kuwa “Katika kipindi cha miaka mitatu tunapoadhimisha siku hii, Halotel Tanzania tayari imefanya uwekezaji unaofikia Dola za Marekani Milioni 500, ikiwa ndiyo kampuni inayoongoza kwa kuwekeza miundombinu ya Mawasiliano sehemu mbalimbali nchini inayowafikia asilimia 95 ya wananchi wote ikiwa na vituo 4,400 vya kupokea mawasioliano (BTS’s) kwa umbali wa Kilomita 18,300”.

Bw.Nguyen Van Son ameongeza kuwa mpango wa biashara wa Halotel zaidi umelenga kuwafikia watu walioko pembezoni mwa miji kwa kuwapa gharama nafuu za mawasiliano huku ikiwa tayari imewafikia wananchi zaidi ya Milioni tatu sambamba na Milioni moja wengine waliojiunga na mtandao wa Halopesa

Hivi karibuni pia Halotel Tanzania itawekeza kiasi cha Dola za Marekani Milioni 200 kwa ajili ya kuboresha huduma za mtandao na zaidi kuhakikisha inaimarisha mtandao wa 4G kwa wateja wake kote nchini.Amesongeza kuwa Kampuni hiyo itaboresha huduma zake mbalimbali ikiwa na lengo la kuwafikia wateja zaidi ya Milioni 6 pamoja na watumiaji Milioni 3 wa huduma ya Halopesa baada ya miaka mitano kuanzia mwaka ujao , pamoja na kuboresha huduma kwa wateja wake wakubwa kutoka Taasisi mbalimbali za kibiashara za Binafsi na Serikali.

Kampuni hiyo inaamini kuwa kupitia huduma hizi itakuwa tumeisaidia Serikali na taasisi zote za kibiashara kuendeleza utoaji wa huduma kwa ufanisi wakati huu ambao pia inatarajia kuandaa mfumo maalumu kwa wateja wake utakaowawezesha kufanya biashara zao kwa ufanisi.Kupitia mikakati mbalimbali ya Kampuni hiyo, itaweza kufikia lengo la kuwa kampuni namba mbili inayotoa Mawasiliano yenye tija hapa nchini.

Mbali na hiyo Halotel imekuwa ikishiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii inayoliwezesha Taifa kufikia malengo yake mbalimbali

TANZANIA YAJITOSHELEZA KWA CHAKULA MIAKA MITANO MFULULIZO-DKT TIZEBA

$
0
0
Waziri wa Kilimo, Dkt Charles Tizeba (Mb) akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani Kitaifa ambayo yamefanyika kwenye viwanja vya JK Nyerere katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma Leo tarehe 16 Octoba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal,WK)
Kikundi cha ngoma ya asili cha Mkoani Songwe kikitumbuiza mara baada ya waziri wa Kilimo, Dkt Charles Tizeba (Mb) kuwasili kuhitimisha kilele cha maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani Kitaifa ambayo yamefanyika kwenye viwanja vya JK Nyerere katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma Leo tarehe 16 Octoba 2018.
Waziri wa Kilimo, Dkt Charles Tizeba (Mb) akitoa salamu za Rais John Pombe Magufulu wakati akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani Kitaifa ambayo yamefanyika kwenye viwanja vya JK Nyerere katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma Leo tarehe 16 Octoba 2018.
Sehemu ya wananchi wakifatilia hotuba ya waziri wa Kilimo, Dkt Charles Tizeba (Mb) kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani Kitaifa ambayo yamefanyika kwenye viwanja vya JK Nyerere katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma Leo tarehe 16 Octoba 2018.

Na Mathias Canal-WK, Tunduma-Songwe


Tanzania imeendelea kuwa ghala la chakula kwa nchi za jirani kwa kipindi kirefu baada ya kujitosheleza kwa chakula takribani kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo. 


Tanzania imeweza kuuza ziada ya mazao mbalimbali ya chakula katika nchi za nje. Kulingana na takwimu zilizotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kipindi cha mwezi Juni 2017 hadi Juni 2018 yameuzwa mahindi kiasi cha Tani 64,477.95  zenye thamani ya Shillingi Billioni 90.6  za kitanzania na maharage  Tani 99,434.45 zenye thamani ya shillingi Bilioni 222.0 za Kitanzania. 


Hayo yamebainishwa na Waziri wa Kilimo Dkt Charles Tizeba (Mb), Leo tarehe 16 Octoba 2018 wakati akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani Kitaifa ambayo yamefanyika kwenye viwanja vya JK Nyerere katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma.


Dkt Tizeba alisema kuwa mazao hayo yamekuwa yakiuzwa zaidi katika nchi za Kenya, Uganda, DRC, Rwanda, Burundi, Sudani Kusini na Uarabuni. 


"Pamoja na kuuza mazao nje ya nchi, nchi yetu imekuwa ikitegemea kuagiza zao la ngano kutoka nje ya nchi kutokana na uzalishaji mdogo wa zao hilo hapa nchini. Serikali inatoa wito kwa wakulima hususani wa maeneo ambayo zao hili linalimwa na kukua vizuri waweze kuongeza maeneo ya uzalishaji na tija ili nchi iweze kupunguza utegemezi wa zao hili kutoka nchi za nje" Alikaririwa akisema


Alisema, Pamoja na uzalishaji mzuri wa chakula nchini, Lishe duni (utapiamlo) kwa jamii na kwa baadhi ya maeneo inaendelea kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuathiri maendeleo ya wananchi kiafya, kielimu na kiuchumi.


Aidha, ili kuyafikia malengo endelevu ya maendeleo (Sustainable Development Goals), alisema , Lishe ni moja ya muhimili muhimu wa kuwezesha kufikiwa kwa malengo yote 17 hivyo Serikali kwa kulitambua hilo, imeamua kujumuisha masuala ya lishe kuwa mojawapo ya maeneo ya kimkakati katika Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21. 


Kadhalila, aliwataka wadau wote wa lishe nchini kushiriki na kuonyesha bayana mchango wao katika kukabiliana na utapiamlo. 


Tarehe 16 ya mwezi Oktoba kila mwaka, Tanzania na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, huadhimisha Siku ya Chakula Duniani ambapo lengo la maadhimisho ya siku hiyo ni kukumbushana wajibu wa kila mmoja katika kupambana na njaa, kuanzia ngazi ya kaya hadi Taifa. 


Maadhimisho ya mwaka huu yamebeba kaulimbiu inayosema “ Matendo yetu ni hatima yetu. Dunia bila njaa ifikapo 2030 inawezekana”. "Kaulimbiu hii inatutaka kufanya kazi kwa umahiri mkubwa ili tujitosheleze kwa chakula na kuwa na akiba ya kutosha kuendesha maisha yetu ya kila siku." Alisisitiza Dkt Tizeba na kuongeza kuwa


"Pia kaulimbiu hii inatukumbusha kuacha kufanya mambo kwa mazoea na badala yake tutumie utalaamu katika kuongeza kuzalisha mazao  ya kilimo, mifugo na uvuvi."


ZAWADI ZATAJWA KICHOCHEO CHA UKEKETAJI TARIME

$
0
0
NA BALTAZAR MASHAKA, TARIME

ZAWADI zimetajwa kuwa chanzo na kichocheo kikubwa cha vitendo vya ukeketaji na tohara kwa watoto wa kike na kiume wilayani Tarime katika Mkoa wa Mara.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wanafunzi walioshiriki tamasha la kupinga Ukatili wa kijinsia lililoandaliwa na Shirika la ATFGM Masanga na kufanyika katika Shule ya Sekondari Kemambo kwa ufadhili wa Terre des Homes tamasha ambalo lilishirikisha shule 10 mbili za msingi na nane za msingi wilayani Tarime.

Wanafunzi hao walieleza kuwa kipindi cha ukeketaji mabinti (watoto wa kike) wanapotoka kukeketwa huzunguka kwenye jamii inayowazunguka ili kupatiwa zawadi ya fedha, nguo na vitu vingine jambo ambalo huwashawishi wengine ambao hawajakeketwa kwenda kufanyiwa vitendo hivyo vya ukatili ili nao wapatiwe zawadi.

Pia waliishauri serikali kusimamia Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 na kanuni zake kupiga marufuku vishawishi vya zawadi za nguo na fedha ili kudhibiti uketetaji wa watoto wa kike na tohara isiyo salama kwa vijana wa kiume.

“Mtoto mmoja anaweza kupata nguo (vitenge) na fedha nyingi ambazo huzibana kwa pini kichwani hivyo wale ambao ni wadogo kama hawajakeketwa wakiona hizo zawadi wanatamani na kushawishika kukeketwa, hivyo serikali ipige vita zawadi hizo kwa kusimamia Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 na kanuni ” alisema ( Maria Marwa jina la linahifadhiwa) mwanafunzi huyo wa Shule Msingi Nyabusara.

Aidha, mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kemambo Mussa Issack alisema kipindi cha tohara kwa wanaume, vijana hutembea umbali mrefu baada ya kutahiriwa huku baadhi yao wakitokwa damu nyingi na wengine kukimbizwa hospitalini jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao.

“ Jambo hili ingawa linaonyesha ujasiri na ushujaa lakini ni hatari kimaisha hivyo suala tohara kwa vijana wa kiume niombe lifanyike kitaalamu ili kunusura watoto wasipoteze maisha kwa kutokwa na damu nyingi baada ya tohara.Pia sehemu inayotumika kutahiria na vifaa vyake si salama kwa afya yao,”alisema mwanafunzi huyo.

Akifunga tamasha hilo jana mgeni rasmi Mkuu wa Shule ya Sekondari Kemambo, Matinde Gimonge alisema elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia inayotolewa kwa watoto hao tawanya waendelee kuwa mabalozi kwa kuelimisha jamii inayowazunguma ili kukomesha mila na tamaduni hizo potofu.

“Ni muhimu elimu hii inayotolewa kwa watoto ikawa chachu ya kuachana na vitendo vya ukatili na hivyo waendelee kuwa mabalozi ili kuifanya jamii salama isiyo na ukatili,”alisema Gimonge.

Kwa upande wake Mratibu wa Haki za Watoto wa Shirika la ATFGM Masanga Emmanuel Omenda alieleza kuwa matokeo hanya (faida) yaliyopatikana tangu kuundwa kwa klabu za kupinga ukatili kwa watoto wa shule za sekondari na msingi ni matukio mbalimbali ya ukatili kuripotiwa na kufanyiwa kazi pamoja na baadhi ya wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria.

Aliongeza kuwa zaidi ya watoto 1,500 wa shule 40 kabla na baada ya kufanyika kwa tamasha hilo wamepatiwa elimu ya kupinga Ukatili wa Kijinsia, Ukeketaji, Ndoa na Mimba za utotoni na anaamini watakuwa mabalozi wazuri katika kufikisha elimu hiyo kwa jamii wilayani Tarime na maeneo mengine ya Mkoa wa Mara ili kutokomeza vitendo hivyo vya ukatili. 
Mgeni rasmi, Mkuu wa Shule ya Sekondari Kemambo Matinde Gimonge akifungua tamasha la kupinga Ukatili wa Kijinsia na kuwataka wanafunzi kuwa mabalozi wazuri wa kufikisha elimu kwa jamii, elimu ambayo wanaipata kupitia kwenye matamasha ya namna hiyo.
 
 Mwanasheria wa Shirika la Kupinga Ukatili wa Kijinsia la ATFGM Masanga wilayani Tarime, Dora Luhimbo akitoa elimu ya kupinga masuala ya ukeketaji na ndoa za utotoni lililoandaliwa na shirika hilo na kukutanisha shule 10 za msingi na sekondari ambalo lilifanyika katika Shule ya Sekondari Kemambo wilayani humo.
 Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za kata za Matongo na Kemambo wakiwa katika tamasha la elimu ya kupinga Ukatili wa Kijinsia, Ukeketaji, Ndoa na Mimba za utotoni lililoandaliwa na shirika la ATFGM Masanga Tarime.
 Mwanasheria wa Shirika la Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Tarime, Mara ( ATFGM Masanga) Dora Luhimbo akicheza muziki na baadhi ya wanafunzi katika tamasha hilo la kupinga ukatili wilayani humu.

"Ushiriki wa Wananchi Katika Miradi ya Kimkakati Kuchochea Ukuaji wa Uchumi"-Waziri Jenista

OLE NASHA:VETA NI CHOMBO MUHIMU KATIKA UJENZI WA VIWANDA NCHINI

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha amesema kuwa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ni chombo muhimu katika kuzalisha mafundi watakaohudumia viwanda vinavyojengwa nchini.

Ole Nasha ameyasema hayo jana wakati alipotembelea Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ikiwa ni kujua utendaji wa mamlaka hiyo katika uzalishaji wa ujunzi kwa vijana nchini, amesema kuwa serikali ya awamu ya tano imejipambanua kuwa ni nchi viwanda hivyo licha ya kuwepo kwa wahandisi ni lazima kuwepo kwa mafundi.

Amesema kuwa VETA ni lazima waonyeshe njia katika uzalishaji wa vijana wenye ujuzi ambao watatumika katika viwanda na miradi mbalimbali ya serikali inayojenga wakiwemo mafundi wa reli.

“Wahandisi kazi yao kuweka michoro lakini kazi ya kujenga ni mafundi hivyo ni wajibu wenu VETA wa kuzalisha rasimali hiyo katika ujenzi wa taifa na kazi yenu inaonekana baadhi ya vijana wamemaliza shahada ya kwanza na sasa wanajiunga mafunzo ya ufundi stadi”.amesema Ole Nasha.

Ole Nasha amesema kuwa vyuo vyote vinatakiwa kuangaliwa mitaala na VETA na visivyo na vigezo wavifungie .Nae Mwenyekiti wa Bodi ya VETA , Peter Maduki amesema kuwa wanajenzi wa vyuo vya VETA kata Mikoa Mitatu na Wilaya moja moja ambavyo vitagharimu sh. bilioni 38.

Amesema Mikoa vitavyojengwa vyuo vya ufundi Geita , Simiyu , Rukwa pamoja wilaya ya Chato ikiwa kuhakikisha kila mkoa unakuwa na chuo cha ufundi stadi. Nae Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dk.Pancras Bujulu amesema kuwa changamoto yake ni kutafuta fedha kwa ajili ya kuismamamisha Vete.



Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akizungumza na Menjejimenti ya VETA pamoja na Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Peter Maduki akizungumza kuhusiana na mipango ya bodi katika ujenzi wa vyuo katika Mkutano wa Menejimenti na wafanyakazi.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dkt Pancras Bujulu akizungumza katika Mkutano wa Menejimenti na wafanyakazi kuhusiana mikakati ya VETA leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi na Menejimenti katika Mkutano na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha

WAANDISHI HABARI ZA KILIMO SAYANSI WATEMBELEA SHAMBA LA MAJARIBIO LA GMO MAKUTUPORA MKOANI DODOMA

$
0
0


Mkurugenzi wa Kituo cha Mjaribio ya Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) cha  Makutupora mkoani Dodoma, Dkt. Cornell Massawe, akizungumza na Waandishi wa Habari za Kilimo Sayansi walipotembelea shamba hilo kwa ziara ya mafunzo mkoani humo jana.
Mtafiti wa Kilimo Dkt. Justin Ringo kutoka Tari-Ilonga, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mahindi ya GMO na yale yaliyopandwa kwenye ukame.
Mkurugenzi wa Kituo cha Majaribio ya Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) cha  Makutupora mkoani Dodoma, Dkt. Cornell Massawe, akiwaonesha Waandishi wa Habari mahindi yaliyopandwa kwa mbegu za kienyeji jinsi yalivyoshambuliwa na wadudu.
Mtafiti wa Kilimo Dkt.Justin Ringo kutoka Tari-Ilonga, akizungumza na Waandishi wa Habari.
Mtafiti wa Kilimo Dkt.Justin Ringo kutoka Tari-Ilonga, akitoa maelezo kwa Waandishi wa Habari juu ya namna mtego wa kunasa wadudu aina ya Bungua wa mahindi   unavyofanya kazi.
Mahindi yaliyoliwa na wadudu aina ya Bungua wa mahindi na Viwavi Jeshi yanavyoonekana.
Waandishi wakiuliza maswali.
Hapa Waandishi wa habari wakielezwa jinsi mahindi yaliyokwisha fanyiwa utafiti yanavyoteketezwa katika shimo maalumu.
Muonekano wa shamba hilo la majaribio.
Wanahabari wakisubiri kuingia katika shamba hilo la majaribio.
Safari  kuelekea kwenye shamba hilo.
Mtafiti wa Kilimo Dkt.Justin Ringo kutoka Tari-Ilonga, akionesha waandishi wa habari (hawamo pichani) namna wadudu aina ya Bungua wa mahindi walivyoshambulia mmea wa mahindi katika shamba hilo la majaribio.

ZAIDI YA KAYA 200 KATA YA MNYANJANI JIJINI TANGA KUNUFAIKA NA MRADI WA UJENZI WA MTARO

$
0
0
 MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kushoto akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea mradi wa Ujenzi wa Mradi wa Mfereji utakaopitisha maji kutoka kwenye makazi ya watu nyakati za mvua na kupelekea baharini 
 MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akishiriki kuchimba mtaro eneo la Mnyanjani Jijini Tanga ambao utasaidia kuondoa kero ya kutuama maji kwenye makazi ya wananchi wakati wa mvua wakati alipofanya ziara ya kuutembelea
Mtaro utakaopitisha maji kwenye eneo la Mtaa wa Mnyanjani Jijini Tanga ya mvua na kupelekea baharini ili kuwaepusha wananchi na mafuriko nyakati za mvua
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku kulia aakimuonyesha kitu Mhandisi toka Wakala wa Usimamizi wa barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoani Tanga Omari Saidi wakati alipotembelea ujenzi wa mradi wa Mtaro 


ZAIDI ya kaya 200 katika mtaa wa Mnyanjani kata ya Myanjani Jijini Tanga zitanufaika na mradi wa ujenzi wa mtaro kwa ajili ya kuondoa tatizo la mafuriko linalotokea kila nyakati za msimu wa mvua. 

Hayo yamebainishwa na Mhandisi toka Wakala wa Usimamizi wa barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoani Tanga Omari Saidi wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya jitihada za kuzinusuru kata hizo. 

Mhandisi Saidi alisema mradi huo unaokadiriwa kutumia Shilingi Milioni 170 umeelekezwa katika eneo hilo lililokuwa na hali ya kutuama kwa maji kila mwaka nyakati zote za mvua na kusababisha mafuriko na kupelekea wananchi kulazimika kuyahama makazi yao. Alisema mradi wa mtaro huo ambao utakuwa na urefu wa mita 512 utakuwa na uwezo wa kusukuma maji kuelekea bahari na kuzifanya kaya hizo na maeneo ya pembezono mwa mtaa huo kuishi kwa amani hasa nyakati za mvua. 

“Ni kweli hali ya mtaa huu haikua ya kuridhisha sisi tarura ambao tunamamlaka sasa tumeona hiki ndio kipindi cha kurekebisha miundombinu ya mifereji namea mvua zitakapo nyesha kaya hizi zitakuwa sehemu salama”Alisema Saidi. Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Tanga(CUF) Alhaj Mussa Mbaruku ambae alitembelea mradi huo jana alisema matumaini makubwa yanaonekana ya kuwanusuru wananchi hao na mafuriko yanayotokea kila mwaka. Alhaj Mbaruku alisema eneo hilo limekuwa kero kwa wananchi hao ambao kila nyakati za mvua maisha yao yanakuwa hatarini kutokana na hofu ya mafuriko yanayosababishwa na mvua za misimu na kulazimika kutafuta makzi mapya. 

“Taratibu hali ya maeneo yaliyokuwa yanakumbwa na mafuriko ndani ya Jiji yanaanza kuwa na hali nzuri baada ya taasisi hiyo kuwa makini na utekelezaji wa ujenzi wa mifereji hasa katika maeneo yanayotuama maji”Alisema Alhaj Mbaruku. Hata hivyo aliiomba taasisi hiyo kuendeleza kasi yao na mbali ya miradi ya mifereji pia ihakikishe kuwa barabara zote ndani ya Jiji hili zinaweza kutumika nyakati zote na zinajengwa kwa kiwango cha lami huku akiongeza kusema kuwa ulazima wa uwepo wa barabara za lami ndani ya jiji lazima uzingatiwe. 

Awali akizungumzia kero hiyo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Bakari Haule alisema tatizo la mafuriko katika eneo hilo lililkua ni kubwa mbali ya nyumba hizo kujengwa katika mpangilio lakini adha kubwa ilikuwa ni kutuama kwa maji nyakati za mvua.

TFDA YATOA UFAFANUZI KUHUSU DAWA ZINAZODAIWA KUTIBU MAGONJWA YA FIGO NA HOMA YA INI

SHIRIKA LA MARIE STOPES TANZANIA LARUHUSIWA KUENDELEA KUTOA HUDUMA ZAKE HAPA NCHINI

SPIKA ATEMBELEWA NA WAGENI KUTOKA TAASISI YA KIMATAIFA YA KIDEMOKRASIA (NDI)

$
0
0
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akimsikiliza Mkurugenzi wa Taasisi  ya Kimataifa ya Kidemokrasia (NDI) Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Dkt. Keith Jennings wakati Mkurugenzi huyo pamoja na baadhi ya viongozi wa Taasisi hiyo  walipomtembelea Ofisini kwake leo Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na viongozi wa Taasisi  ya Kimataifa ya Kidemokrasia (NDI), katikati ni Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Dkt. Keith Jennings na wa mwisho ni Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi hiyo Ndg. Sandiy Quimbaya. Wageni hao walimtembelea Mhe. Spika leo Ofisini kwake Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na  viongozi wa Taasisi  ya Kimataifa ya Kidemokrasia (NDI), kushoto kutoka kwa Mhe. Spika  ni Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Dkt. Keith Jennings na kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi hiyo Ndg. Sandiy Quimbaya. Wageni hao walimtembelea Mhe. Spika leo Ofisini kwake Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Mkurugenzi wa Taasisi  ya Kimataifa ya Kidemokrasia (NDI) Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Dkt. Keith Jennings wakati Mkurugenzi huyo pamoja na baadhi ya viongozi wa Taasisi hiyo  walipomtembelea Ofisini kwake leo Jijini Dodoma.

Wizara Zakutana kujadili Kamera za kudhibiti Uhalifu

$
0
0

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Radhiya Rashid Haroub (kushoto), wakati wa Kikao cha kubadilishana uzoefu juu ya suala la ufungaji wa kamera maalumu za kuzuia na kudhibiti  uhalifu ambazo tayari zimeshafungwa Visiwani Zanzibar. Wengine ni ujumbe kutoka Jeshi la Polisi ulioongozana na Naibu Waziri, ukiongozwa na Kaimu Kamishna wa Jeshi la Polisi, SACP Saleh Mohamed Saleh (watatu kushoto)
PIX 2
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Radhiya Rashid Haroub  akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa Kikao cha kubadilishana uzoefu juu ya suala la ufungaji wa kamera maalumu za kuzuia na kudhibiti uhalifu ambazo tayari zimeshafungwa Visiwani Zanzibar. Wengine ni ujumbe kutoka Jeshi la Polisi ulioongozana na Naibu Waziri, ukiongozwa na Kaimu Kamishna wa Jeshi la Polisi, SACP Saleh Mohamed Saleh (watatu kushoto)
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
………………………
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimekutana kujadili suala la ufungaji kamera maalumu za kudhibiti na kuzuia uhalifu.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alisema Serikali inatambua umuhimu wa ulinzi na usalama kwa raia wake na iko katika mpango wa kufunga kamera hizo katika miji yote mikuu nchini.
Waziri Masauni alisema lengo la kufunga kamera hizo ni kuiwezesha serikali kupambana na matukio ya uhalifu ya utekaji, makosa ya barabarani, uporaji wa fedha katika taasisi za fedha.
“Tumekuja kuchukua uzoefu kwa wenzetu wa Zanzibar ambao tayari wameshafunga kamera hizi katika maeneo mbalimbali na nimeona jinsi zinavyofanya kazi za kubaini wahalifu.
“Teknokolojia haiepukiki katika kudhibiti, Serikali tumejipanga na hivi karibuni tutaanza kufunga kamera za CCTV  katika miji mikuu na maeneo ya mikoa iliyoko mipakani ili  kudhibiti wahalifu kutoka nje ya Tanzania,” alisema Masauni
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Radhiya Rashid Haroub alisema tayari washafunga kamera hizo ambazo zilizinduliwa Oktoba 3, mwaka huu.
Alisema uzinduzi wa kamera hizo ulifanywa na Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein.“Mfumo huo ni muhimu na tumehakikisha unaimarisha usalama katika mji wa Zanzibar ili wananchi waweze kufanya shughuli zao kwa amani na salama na tayari ushaanza kufanya kazi katika maeneo mbalimbali hapa Zanzibar,” alisema.

RAIS WA ZANZIBAR DKT ALI MOHAMED SHEIN AFUNGUA MAONESHO YA KWANZA YA UTALII ZANZIBAR

$
0
0


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohamed Shein kushoto akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya kale Khadija Bakari mara baada ya kuwasili katika ufunguzi wa Maonesho ya kwanza ya Utalii yaliofanyika Hotel Verde Maruhubi Zanzibar.Katikati ni Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo. 
????????????????????????????????????
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohamed Shein katikati akiwapamoja na Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya kale Mahmoud Thabit Kombo kulia na Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud walipotembelea mabanda mbalimbali ya maonesho katika ufunguzi wa maonesho hayo ya kwanza ya Utalii yaliofanyika Hotel Verde Maruhubi Zanziba
????????????????????????????????????
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohamed  Shein kushoto akipata maelezo kuhusiana na Vitu mbalimbali vya kizamani ikiwemo Pishi katika ufunguzi wa maonesho  ya kwanza ya Utalii yaliofanyika Hotel Verde Maruhubi Zanzibar.
????????????????????????????????????
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohamed Shein wapili kushoto akiuliza maswali kwa Meneja Mkuu  wa Kampuni ya Com Net Keith McCormick alipotembelea Banda hilo katika ufunguzi wa maonesho  ya kwanza ya Utalii yaliofanyika Hotel Verde Maruhubi Zanzibar.
????????????????????????????????????
Baadhi ya Viongozi wa Serikali waliohudhuria katika ufunguzi wa maonesho  ya kwanza ya Utalii yaliofanyika Hotel Verde Maruhubi Zanzibar.
????????????????????????????????????
Baadhi ya Wageni Waalikwa mbalimbali  waliohudhuria katika ufunguzi wa maonesho  ya kwanza ya Utalii yaliofanyika Hotel Verde Maruhubi Zanzibar.
????????????????????????????????????
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo akitoa hotuba ya makaribisho kwa mgeni Rasmi katika ufunguzi wa maonesho  ya kwanza ya Utalii yaliofanyika Hotel Verde Maruhubi Zanzibar.
????????????????????????????????????
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein akisisitiza jambo wakati akitoa Hotuba ya Ufunguzi wa maonesho  ya kwanza ya Utalii yaliofanyika Hotel Verde Maruhubi Zanzibar.
????????????????????????????????????
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt,Ali Mohamed Shein kulia  alipotoa hotuba  ya Ufunguzi wa maonesho  ya kwanza ya Utalii yaliofanyika Hotel Verde Maruhubi Zanzibar.katikati ni Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Samia Suluhu Hassan na Mwisho kushoto ni Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya kale Mahmoud Thabit Kombo.
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images