Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

SHILINGI BILIONI 3/- ZATENGWA KWA AJILI YA UJENZI MACHINJIO YA VINGUNGUTI

$
0
0

Na Mwandishi Wetu,Globu ya jamii

SHILINGI bilioni tatu zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa  machinjio ya Vingunguti jijini Dar es Salaam ambapo ujenzi unatarajia kuanza  Novemba mwaka huu.

Uamuzi wa kutengwa kwa fedha hizo ni katika jitihada za kuondoa changamoto zinazoikabili machinjio hayo.

Hayo ameelezwa jana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam  mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalah Ulega.

Ulega alifanya ziara fupi katika machinjio hiyo akiambata na viongozi wengine wa serikali wakiwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Nyama, Dk wa Mifugo na Mkurugenzi Msaidizi wa  Masoko na uzalishaji toka Wizarani.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Ulega alielezwa changamoto zinazoikabili machinjio hiyo ikiwa ni pamoja na  wafanyabiashara wa nyama kutozwa ushuru mkubwa kwa mazao ya mifugo, ukosekanaji wa  soko la uhakika la ngozi, ambapo Ulega amesema Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi ina mkakati  kabambe wa kukabiliana na changamoto hizo.

Ulega amefafanua  kwa kuanza na ujenzi wa machinjio mpya ya kisasa utakaofanyika kwa gharama hizo za fedha za Serikali.

“Wasimamizi wote wa ujenzi wa machinjio hii  nawataka muhakikishe kuwa ujenzi huu unafanyika kwa haraka na ubora ili machinjio hii iweze kuchinja ng’ombe, mbuzi, kondoo na kuku kwa kuwa machinjio nyingi zilizojengwa hazijazingatia suala la uchinjaji wa kuku,” amesisitiza Ulega.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega(katikati)  akiwasili kwenye eneo la machinjio ya Vingunguti kwa ajili ya kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wadau wa machinjio hayo jana jijini  Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akikagua eneo linalotumika kuuza nyama ya Ng`ombe na Mbuzi.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega  akizungumza na wananchi (wadau) wa machinjio ya Vingunguti  kuhusu kero zao mbalimbali wazipatazo kuhusu eneo hilo la Mchinjio.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega  akizungumza na wananchi(wadau) wa machinjio ya Vingunguti ambapo amewahakikishi serikali ya awamu ya tano ipo pamoja nao na amewaomba kulipa kodi ili kuinua uchumi wa Taifa.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega jana  katika machinjio ya vingunguti  jijini Dar es Salaam.
 Wadau wa machinjio ya Vingunguti wakiendelea na kazi.(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)


MKUU WA MAJESHI JWTZ AIPONGEZA NMB KUKUZA MCHEZO WA GOLF

$
0
0

Mgeni rasmi na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Yakub Mohamed (wa pili kulia) kwenye Mashindano ya NMB Kombe la Mkuu wa Majeshi mchezo wa Golf akimkabidhi kikombe mshindi wa jumla katika mashindano hayo, Richard Mtweve (kulia). Kutoka kushoto wanaoshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara NMB, Donatus Richard, Mwenyekiti wa Klabu ya Golf Lugalo, Brigedia Jenerali mstaafu, Michael Luwongo.
Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Yakub Mohamed akizungumza lipokuwa akiyafunga Mashindano ya NMB Kombe la Mkuu wa Majeshi kwa mchezo wa Golf yaliyofanyika kwenye Klabu ya Golf ya JWTZ Lugalo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard (kushoto) akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi katika Mashindano ya NMB Kombe la Mkuu wa Majeshi kwa mchezo wa Golf yaliyofanyika kwenye Klabu ya Golf ya JWTZ Lugalo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard (kushoto) akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi katika Mashindano ya NMB Kombe la Mkuu wa Majeshi kwa mchezo wa Golf yaliyofanyika kwenye Klabu ya Golf ya JWTZ Lugalo jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Yakub Mohamed (wa pili kulia) katika Mashindano ya NMB Kombe la Mkuu wa Majeshi mchezo wa Golf akimshukuru Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard (Wa pili kushoto) kwa udhamini wa Mashindano hayo. Mgeni rasmi na Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Yakub Mohamed (wa pili kulia) kwenye Mashindano ya NMB Kombe la Mkuu wa Majeshi mchezo wa Golf akimshukuru Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard (kushoto) kwa udhami ni wa Mashindano ya NMB Kombe la Mkuu wa Majeshi kwa mchezo wa Golf mara baada ya kufunga mashindano hayo. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali Mirisho Sarakikya akishuhudia.
Mshindi wa jumla katika Mashindano ya NMB Kombe la Mkuu wa Majeshi kwa mchezo wa Golf, Richard Mtweve akizungumza kwa furaha mara baada ya kupokea vikombe vya ushindi.
Rais wa Chama cha Mchezo wa Golf Tanzania (TGU), Chris Martin (kuliaa) akimkabidhi kitabu cha mwongozo wa mchezo wa golf Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard ili naye aendelee kuwa mdau wa mchezo huo.
Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali Mirisho Sarakikya (kulia) akijisajili eneo la kuanzia kabla ya kuanza kushiriki michuano ya Mashindano ya NMB Kombe la Mkuu wa Majeshi (JWTZ) kwa mchezo wa Golf.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard (kulia) akiitambulisha timu ya NMB kwenye hafla hiyo.

Mmoja wa wachezaji katika Mashindano ya NMB Kombe la Mkuu wa Majeshi kwa mchezo wa Golf akiendelea na mchezo.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard akizungumza katika hafla ya kufunga Mashindano ya NMB Kombe la Mkuu wa Majeshi kwa mchezo wa Golf yaliyofanyika kwenye Klabu ya Golf ya JWTZ Lugalo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Chama cha Mchezo wa Golf Tanzania (TGU), Chris Martin (kulia) akimkabidhi kitabu cha mwongozo wa mchezo wa golf Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali Mirisho Sarakikya (kushoto) ambaye ni mchezaji wa mchezo huo.








MKUU wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo ameipongeza Benki ya NMB nchini kwa juhudi zake za kuendelea kuukuza mchezo wa Golf Tanzania.

Jenerali Mabeyo ametoa pongezi hizo jana kupitia kwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Yakub Mohamed alipokuwa akimwakilisha katika hafla ya kufunga Mashindano ya NMB Kombe la Mkuu wa Majeshi kwa mchezo wa Golf yaliyofanyika kwenye Klabu ya Golf ya JWTZ Lugalo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwa niaba ya Jenerali Mabeyo, Luteni Jenerali Mohamed alisema jamii ya mchezo wa Golf Tanzania inatambua mchango mkubwa unaotolewa na NMB katika kudhamini mchezo huo mara zote jambo ambalo linaendeleza kukua kwa mchezo huo nchini, hivyo wataendelea kushirikiana na benki hiyo.Alisema NMB wamedhamini mashindano hayo kwa mwaka wa tatu mfululizo huku yakizidi kukua na mchezo huo kuwa maarufu nchini, na yamekuwa yakishirikisha wachezaji vijana na wameanza kufanya vizuri jambo ambalo ni mafanikio kwa taifa kimichezo.

Akizungumza katika hafla hiyo, mwakilishi wa NMB alisema benki hiyo itaendelea kushirikiana na jamii katika kuendeleza na kukuza michezo yote pale inapopata fursa kwani mbali ya kujenga mahusiano mazuri na jamii pia ni afya na sasa ni sehemu ya ajira kwa jamii. Alisema NMB itaendelea kushirikiana na Klabu ya Golf ya JWTZ Lugalo kwani ni shukrani kwa mahusiano waliyonayo kikazi.

Aidha aliwakaribisha maofisa wa juu na wateja wengine maalum kuungana katika kujipatia huduma za kibenki zinazotolewa kwao kama wateja maalum ikiwemo mikopo nafuu na ya haraka, ushauri wa kifedha na kadi maalum za kupata huduma za kibenki popote.Kwa upande wake Rais wa Chama cha Mchezo wa Golf Tanzania (TGU), Chris Martin alisema chama hicho kimejipangia kufikisha wachezaji 3000 wamchezo huo ifikapo 2020, huku idadi ya wachezaji kwa sasa haifiki 1000.

Alisema Klabu ya Golf Lugalo imekuwa ikifanya vizuri kwani hadi sasa inawachezaji vijana (watoto) takribani 60 na 22 kati yao wameshiriki katika Kombe la NMB Mashindano ya Golf ya Mkuu wa JWTZ, jambo ambalo linaleta matumaini ya kuendelea kukua kwa mchezo huo.

Washindi katika mashindano hayo, yalioshirikisha wachezaji wa ridhaa 79, wakulipwa 19 na watoto 22 walijipatia fedha taslimu, vikombe na zawadi za vifaa mbalimbali kama friji, TV, radio, baskeli, dish za ving'amuzi na vinginevyo.NMB ilidhamini mashindano hayo kwa kuchaangia shilingi milioni 26 pamoja na vifaa mbalimbali zikiwemo jezi zilizotumiwa katika mashindano hayo.
Makamu Rais wa Umoja wa Klabu za Golf Tanzania, Luteni Canali David Luoga akiwakaribisha wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.
Baadhi ya wachezaji (kulia) wakijisajili kushiriki Mashindano ya NMB Kombe la Mkuu wa Majeshi mchezo wa Golf.

Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali Mirisho Sarakikya (kulia) akishiriki michuano ya Mashindano ya NMB Kombe la Mkuu wa Majeshi (JWTZ) kwa mchezo wa Golf.

A RECORD TURNOUT FOR THE ROTARY DAR MARATHON AS IT MARKS 10 YEARS

$
0
0
(From Left to right) The Rotary Dar Marathon 2018 committee chair, Ms. Catherinerose Barretto, The Rotary Dar Marathon Chair of the Board, Ms. Sharmila Bhatt and SBC Tanzania’s CEO Avinash Jha wave their flags to officially start the Rotary Dar Marathon 2018 which took place yesterday during the Nyerere Day at the Green grounds Oysterbay in Dar es salaam. PHOTO COURTESY OF ROTARY DAR MARATHON.
A cross section of runners take part in the 10th edition of the 2018 Rotary Dar Marathon which takes place annually in Dar es Salaam. More than 15,000 people have turned up to participate in this year’s Marathon where the event marked its 10th anniversary in a fashionable style in Dar es Salaam yesterday. PHOTO COURTESY OF ROTARY DAR MARATHON.
Faraja Lazaro Damas of Tanzania crosses the finish line to win the 2018 Rotary Dar Marathon Men’s 21.1km race at the Green grounds in Dar es Salaam yesterday. The Marathon marks its 10th anniversary since its inception in 2009. 
A Competitor in the Men's 21.1km cycling leads the pack at the start of the 2018 Rotary Dar Marathon held in Dar es Salaam yesterday during the Nyerere Day at the Green grounds Oysterbay in Dar es Salaam.
Rotary Dar Marathon Patron, His Excellency the former President Al-Haj, Ali Hassan Mwinyi hands over a fully paid ticket to Beruit Marathon to the winner of Men’s 42.2km full Marathon a Tanzanian resident, Samson Ntandu during the 2018 Rotary Dar Marathon which took place at the Green grounds Oysterbay in Dar es Salaam yesterday. The runner will have the opportunity to participate in the Beirut Marathon with everything fully sponsored by Pepsi. Through this initiative, Pepsi aims to raise the profile of Tanzanian runners on the global stage.
Winner of Women’s 42.2km full Marathon a Tanzanian resident, Sara Ramadhani poses for a photo with her counterparts Dorcas Chesano (left) who emerged second and Doris Fisha (right) who emerged third in the 2018 Rotary Dar Marathon which took place at the Green grounds Oysterbay in Dar es Salaam yesterday. PHOTO COURTESY OF ROTARY DAR MARATHON.



Dar es Salaam. The Rotary Dar Marathon had one of its biggest turnouts this year as it marks ten years of its existence since it was started in 2009. An estimated total of 15,000 people participated in the event which included a full marathon of 42.2km, a half marathon 21.1km, including cyclists, and a 9km and 5km family walk. This year, the Rotary Marathon was also held in Bukoba and Karagwe where over 1,400 participants ran and walked.

The Rotary Dar Marathon, considered as one of the biggest marathons in the country and a prime event in the Country’s sporting and social calendars, had participants from all walks of life, different ages and a number of professional marathon runners Kenya, Rwanda, Uganda, and Malawi. This year’s event, as has been the case in the past 9 years, was generously sponsored by various companies such as Pepsi, Ashton Media, Toyota, ALAF, Minet, Zoom Tanzania, Resolution Insurance, Clouds Media Group, Azam, Plasco, Insignia, Knight Support, Ashers Industries, Exim Bank, KLM, CSI Construction and Soft Tech.

The event kicked off in the early morning hours of Sunday as the various runners were flagged off starting with the long-distance runners 42.2 km runners, followed by the half marathon 21.1 km runners and cyclists. The route which saw runners and cyclists go through the peninsula into the heart of the city had the first runners back at The Green around 8.30am where the full marathon was dominated by professional athletes and the male winners being Samson Ntandu from Tanzania for the full marathon, followed by Peter Sule from Tanzania for the second place and thirdly Dushimukiza Thomas from Rwanda.

Winners amongst the female runners were Sara Ramadhani from Tanzania seconded by Dorcas Chesano from Kenya and thirdly Doris Fisha from Malawi.The Tanzania winning runner in the full marathon is Samson Ntandu for the men and Sara Ramadhani for the women who have won a full sponsorship to represent Tanzania in the Beirut Marathon this year, courtesy of SBC Pepsi.

Speaking during the event, the winner Samson Ntandu, expressed how grateful he was to the organizers who did a great job and had this to add, “It was an exciting route and it’s great to see that the months of training that I put into this, have finally paid off.’

Giving out the prizes this year was the patron of the Rotary Dar Marathon, former president Ali Hassan Mwinyi called on Tanzanians to exercise and take part in such events as they not only promote a healthy lifestyle but through their participation and contribution they support very worthy causes that go a long way in helping the underprivileged. He commended the Rotary Clubs in Dar es Salaam for continuing to organize the Rotary Dar Marathon and raising funds for various high impact community service projects.

The Chair of the Board of the Rotary Dar Marathon, Mrs Sharmila Bhatt, could not hide her excitement due to the turnout this year, “I’m overwhelmed by your support and more so that we have had a historic turnout this year and I would like to thank all the people that have made this possible from the sponsors, volunteers, our fellow Rotarians and every single one of you who has taken part. This wouldn’t be possible without your generous support and belief in our efforts and cause” said Mrs Bhatt. 

She continued to remind people that each individual participating has surely touched on a lot more people through Rotary Marathon’s continued efforts.
Rotary Dar Marathon Chair, Catherinerose Barretto, expressed “an event that started humbly in 2009 with 700 participants, today, as Rotarians, we are proud of what we have achieved with the strong support of our community and will continue to serve above self for the years to come”

Other winners from this event included:-


MEN’S 21.1KM
1 FARAJA LAZARO (TANZANIA)
2 DONALD MUSSA (KENYA)
3 JOSEPH PANGA (TANZANIA)

WOMEN’S 21.1KM 
1 CATHERINE SYOKAO (KENYA)
2 NANCY JERAGAT (KENYA)
3 MARATHA YANKURINJE (RWANDA)

CYCLING 21.1KM (MEN)
1 MOHAMED SHAMU (TANZANIA)
2 MUSA WAER (TZ)
3 HASSAN AMIR (TZ)


CYCLING 21.1KM (WOMEN)
1 HAMIDA ACKLAND (TZ)
2 UPENDO NCHOME (TZ)
3 TASMEEN HASSAN (TZ)

Rock City Marathon yazidi kuwavutia washiriki wa kimataifa

$
0
0
Rock City Marathon yazidi kuwavutia washiriki wa kimataifa
Zikiwa zimebaki wiki chache kabla ya kufanyika  kwa mbio za Rock City Marathon, idadi kubwa ya wanaridha wa kimataifa wameonyesha nia ya kuja nchini  ili kushiriki katika mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo wanariadha walioonyesha nia ya kushiriki mbio hizo wengi wanatoka katika nchi za Ethiopia, Ghana, Afrika Kusini, Marekani, Canada, China, Rwanda, Burundi, DRC Congo huku Kenya ikiendelea kuongoza katika orodha ya mataifa ya nje yanaoleta washiriki zaidi katika mbio hizo.
“ Zikiwa zimebaki takribani wiki mbili kabla ya kufanyika kwa mbio hizo tayari zaidi wa washiriki 200 kutoka nje ya nchi wameonyesha nia ya kushiriki mbio hizi na kinachosubiriwa kwasasa ni wao tu kufuata taratibu kupitia Shirikisho la Riadha Taifa (RT). Lengo letu ni kupata washiriki zaidi ya 5000 katika msimu huu,’’ alisema Ngowi katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari mapema leo.
“Ni taarifa njema kwetu kuona kwamba baada ya muda mrefu sasa si watanzania bali ulimwengu mzima umeanza kutuelewa nini tunakifanya Kanda ya Ziwa hususani katika jiji la Mwanza…ni ushindi pia kwa sekta ya utalii katika kanda hii.’’alibainisha
Kwa mujibu wa Ngowi, katika kuhakikisha kwamba mbio hizo zinalitangaza vyema  jiji la Mwanza, njia ambazo zimekuwa zikitumika kwa wakimbiaji zinahusisha alama muhimu za jiji hilo ikiwemo jiwe la Bismarck lililopo kwenye fukwe ya Ziwa Victoria, makutano ya mzunguko wa  samaki (The Vic Fish Roundabout), jengo la Rock City Mall pamoja na Daraja la Furahisha na hatimaye kuishia Uwanja wa CCM Kirumba.
Hata hivyo, alishukuru jitihada zinazofanywa na vyombo vya habari nchini kwa kutangaza mbio hizo.
“ Kwa mfano matangazo ya moja kwa moja yaliyofanywa katika kilele cha mbio hizi msimu uliopita yaliwezesha maelfu wa watanzania kuweza kufuatilia mbio hizi wakiwa majumbani kwao nchini kote…mwaka huu pia mbio zitaoneshwa moja kwa moja kupitia telesheni,’’
 “Zaidi kupitia uwekezaji wa jitiahada zetu kwenye mitandao ya kijamii umetuwezesha kuwa karibu na wadau wengi wa mchezo wa riadha hususani nje ya nchi hatua ambayo imetusaidia kuweza kuwavuta kwa urahisi kuja kushiriki katika mbio hizi zinazolenga kutangaza utalii katika kanda ya Ziwa,’’
  “Mipango yetu ya muda mrefu kwa kushirikiana na wadau wetu wakiwemo Puma Energy Tanzania, Tiper, Tanapa, Ttb, Nssf, Gold Crest, New Mwanza Hotel,  Cf Hospital, Dasani,  CocaCola, Metro Fm, Ef Outdoor,  Kk Security, Belmont Fairmount Hotel , Bigie Customs na Global Education Link zinatupeleka tulipotarajia,’’ aliongeza.
Bw Ngowi alivitaja vituo vinavyoendelea na usajili huo kwasasa kuwa ni pamoja na New Mwanza Hotel , Rock City Mall, The  Gym Buzuruga, Nyakato  mecco sokoni, Buzuruga Stand, Biggie co. ltd Mwanza,  Ladies  Collection shop –Kirumba Sokoni, Magu Simiyu, Viwanja vya Nyamagana, Radio Metro Fm, Semira  Eletronics, Lake Radio na Nyegezi  Stand.
Alisema usajili huo pia utahusisha ofisi zote za riadha mikoa ya Geita, Simiyu na Shinyanga huku akiongeza : “Kwa upande wa Dar es Salaam Fomu za ushiriki pia zinapatikana katika jengo la SHAMO Tower, Mbezi Beach , jijini Dar es, Salaam ”

 Baadhi ya washiriki wa mbio za Rock City Marathon mwaka jana.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU MWAKA HUU WA 2018 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea taarifa kutoka kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama walioongozana na wakimbiza Mwenge wa Uhuru mwaka huu wa 2018 alipokutana na kufanya nao mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 15, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama pamoja na wakimbiza Mwenge wa Uhuru mwaka huu wa 2018 alipokutana na kufanya nao mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 15, 2018
PICHA NA IKULU

NDALICHAKO ASHIRIKI KONGAMANO LA ELIMU PANGANI,ASEMA WANAFUNZI WANAOTUMIA MTAALA MPYA WATAENDELEA KUSOMA KWA KIPINDI CHA MIAKA SABA

$
0
0
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknologia Proffesa Joyce Ndalichako akizungumza katika kongamano la Wadau wa elimu wilayani Pangani ambalo lilikwenda sambamba na harambee ya kuchangia ujenzi wa mabweni shule ya Sekondari Mwera kulia ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM0 kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallahhalfa iliyofanyika mjini Pangani
 NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso akizungumza katika halfa hiyo kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknologia Proffesa Joyce Ndalichako
 Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah akizungumza katika kongamano hilo kulia ni
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknologia Proffesa Joyce Ndalichako na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwalimu Hassani Nyange
 Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwalimu Hassani Nyange akizungumza katika kongamano hilo
 Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gipson George akizungumza katika kongamano hilo
 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza katika kongamano hilo
 WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknologia Proffesa Joyce Ndalichako kulia akitoka kukagua mabweni ya moja ya shule ya Sekondari wilayani Pangani kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kushoto ni Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani nyuma ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso
 Sehemu ya wadau wa elimu wilayani Pangani wakiwa kwenye Kongamano hilo
 WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknologia Proffesa Joyce Ndalichako wa pili kutoka kushoto akiwa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso wakirufahia jambo wakiwa kwenye kivuko wakielekea ng'ambo ya pili ya mto Pangani kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassan Nyange
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknologia Proffesa Joyce Ndalichako akishuka kwenye kivuko akiwa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kushoto na Mkuu wa wilaya ya Pa ngani Zainabu Abdallah

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknologia Proffesa Joyce Ndalichako amesema kwamba wanafunzi wanaosoma kupitia mtaala mpya watasoma kwa kipindi cha miaka saba kama ilivyokuwa awali.

Proffesa Ndalichako aliyasema hayo  mjini Pangani wakati wa Kongamano la Elimu wilayani Pangani lililoenda sambamba na harambee ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya wanafunzoi shule ya sekondari Mwera mbapo alisema suala la muda wa elimu msingi lipo kwa mujibu wa sheria ya elimu ya mwaka 1982.

Alisema sheria hiyo imeweka bayana kwamba muda wa elimu ya msingi ni miaka saba na bado sheria hiyo haijafanyiwa marekebisho hivyo wanafunzi wanaosoma kupitia mtaala mpya watasoma miaka saba.

Akitolea ufafanuzi suala hilo alisema ikifika mahali kama kutakuwa na ulazima wa kubadilisha miaka ya kwenda shule kitakachotanguliwa ni kufanya marekebisho ya sheria kwa sababu jambo linalokuwa ndani ya sheria huwezi kulifanyia mabadiliko bila kuanza kufanya marekebishi ya sheria husika.

“Niwatoe hofu watanzania kwamba suala la kisheria huwezi kubadilika kwa tamko wala waraka wa kamishna wa elimu au kubadilika kwa maelekezo mengine yoyote bali linaweza kubadilika pale sheria ya elimu 1982 kwenye kipengine kinachoeleza muda wa elimu ya msingi miaka 7 kitakapofanyiwa marekebisho”Alisema Waziri Proffesa Ndalichako

Alisema baada ya kufanyiwa marekebisho ndio inaweza kubadilika na haitakuwa kinyumenyume na itaweka bayana kwa sababu badiliko kama hilo ni kubwa la sera na kisheria hivyo watu watafahamu mapema.

“Kumekuwa na mchanganyika kwa sababu sera ya elimu ya mwaka 2014 imeonyesha serikali itakuja kuweka utaratibu lakini haikusema itaweka lini kwamba elimu ya msingi iwe lazima mpaka sekondari”Alisema.

Alisema bado hatujawa tayari kuwa elimu ya msingi na sekondari kwa wanafunzi wote hivyo tunaendelea kuboresha elimu ya msingi na sekondari kuhakikisha mazingira mzuri ya kufundisha na walimu wa kutosha.

Alisema watakapoona wamefika mahali na kuona haja ya kufanya hayo watu wamekuwa wakiulizia serikali itawashirikisha wadau wote kwamba tunakwendaje huku akieleza mkakati ni serikali kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa alimueleza Waziri huyo kwamba namna walivyohamasisha suala la elimu wilayani humo ili kuwapa uelewa wananchi juu ya umuhimu wa elimu ikiwemo kutoa wimbo wa kuhamasisha.

“Mh Waziri kutokana na awali kuwa na hali ambayo sio nzuri kwa elimu wilayani hapa mimi na Mbunge wa Jimbo la Pangani Jumaa Aweso tulikwenda studio kurekodi nyimbo ya kuhamasisha elimu tunashukuru Mungu hali imebadilika na suala la elimu limekuwa likipewa kipaumbele”Alisema.

RC MAKONDA AAGIZA KUKAMATWA KWA VIGOGO WALIOHUJUMU SOKO LA KARIAKOO

$
0
0


 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ameagiza kukamatwa kwa waliokuwa viongozi wa Soko la Kimataifa Kariakoo kwa kusababishia serikali hasara ya zaidi ya Shilingi Bilioni 1.3.Vigogo walioagizwa kukamatwa ni aliekuwa Mkuu wa idara ya fedha, Mkuu idara ya utumishi, mkuu idara ya manunuzi na aliekuwa mkuu idara ya mipango na biashara ambao wameagizwa kufikishwa mahakamani Mara moja.
index
RC Makonda ametoa maagizo hayo wakati wa mkutano wa utatuzi wa kero za wafanyabiashara Soko la Kariakoo ambapo pia ametoa siku tano kwa watendaji kupitia upya sheria zote za ushuru mdogomdogo baada ya kubaini uwepo wa ushuru mkubwa unaoumiza na kuwarudisha Nyuma wafanyabiashara.
“Hatuwezi kuwa na shirika linaloongeza kero kwa wafanyabiashara na kuwarudisha Nyuma, haiwezekani mtu alipie kodi ya pango, ushuru wa kuingiza mzigo 600, ushuru wa Siku 1,700, muuza kahawa alipe 1,000 na bado mtu huyohuyo analipa ushuru wa Choo na Bafu 500, hili haliwezekani” Alisema RC Makonda.
2
Aidha RC Makonda ameagiza kuvunjwa kwa mkataba wa makusanyo ya ushuru baina ya mbia na soko na badala yake ameagiza kazi ya ukusanyaji wa ushuru ifanywe na uongozi wa soko.
Pamoja na hayo RC Makonda ameagiza soko kuu la kariakoo kurejeshwa kwenye hadhi ya kimataifa na sio kuendeshwa kiholela Kama ilivyo sasa ambapo linapokea bidhaa za rejareja kutoka mitaani badala ya kuwa soko la kuuza bidhaa za jumla.
3
Miongoni mwa kero zilizolalamikiwa na wafanyabiashara ni uhusiano mbovu baina ya viongozi na wafanyabiashara, kodi ya pango, vyanzo vingi vya ushuru, mikataba, mikopo, soko kupoteza mwelekeo, mkanganyiko kwenye viwango vya vipimo, kadi ya kizimba na ukamataji ambapo RC Makonda ameahidi kuzifanyia kazi.

UCHAGUZI MDOGO SERENGETI, SIMANJIRO NA KATA 21 ZA TANZANIA BARA

$
0
0
Idara ya Habari-NEC

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza Tarehe mbili Desemba (Desemba 2, 2018) kuwa siku ya Uchaguzi Mdogo kwenye Jimbo la Simanjiro, Serengeti na kata 21 za Tanzania Bara.

Akitoa taarifa kwa umma Jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu Oktoba 15, 2018), Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa Semistocles Kaijage amesema fomu za Uteuzi wa Wagombea zitatolewa kati ya tarehe 28 Oktoba hadi 03 Novemba mwaka huu.

“Uteuzi wa Wagombea utafanyika tarehe 03 Novemba mwaka huu. Kampeni za Uchaguzi zitafanyika kuanzia tarehe 04 Novemba hadi tarehe 01 Desemba mwaka huu na siku ya Uchaguzi itakuwa ni tarehe 2 Desemba, mwaka huu,” Jaji Kaijage amesema.

Mwenyekiti huyo wa Tume amesema kwamba Tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, aliitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge katika Majimbo mawili (2), Jimbo la Serengeti lililopo Halmashauri ya Serengeti Mkoani Mara na Jimbo la Simanjiro katika Halmashauri ya Simanjiro Mkoani Manyara.

Jaji Kaijage alisema kwamba barua hiyo imepokelewa kufuatia Wabunge wa Majimbo hayo Waheshimiwa Marwa Ryoba Chacha, na James Ole Millya kujiuzulu na kutoka kwenye Chama vyama vyao vya awali.

Amesema Tume pia imepokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa ambaye kwa kutumia mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, aliitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata 21 za Tanzania Bara. Nafasi hizo wazi zimetokana na sababu mbalimbali ikiwemo vifo na kujiuzulu.

“Tunapenda kuvikumbusha Vyama vya Siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia Sheria, Kanuni, Maadili ya Uchaguzi, Taratibu, Miongozo na maelekezo yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa kipindi chote cha Uchaguzi huu mdogo,” alisema.

Kata zenye uchaguzi nah almashauri zao kwenye mabano ni pamoja na Ilboru, Mlanfarini na Oldonyosambu (Wilaya ya Arusha), Engutoto na Olasiti (Manispaa ya Arusha), Hazina (Manispaa ya Dodoma), Chinugulu (Wilaya ya Chamwino), Kasharu, Nyakimbili, Kishongo (Wilaya ya Bukoba), Chonyonyo, Ihanda (Wilaya ya Karagwe).

Nyingine ni pamoja na Muhindawa, Mnanila (Wilaya ya Buhigwe), Mnerongongo (Wilaya ya Nachingwea) Ngarenairobi (Wilaya ya Siha), Kyanyari (Wilaya ya Butiama), Namilembe (Wilaya ya Ukerewe), Lukanga, Beta (Wilaya ya Mkuranga) na Chikola (Wilaya ya Manyoni).

WAANDISHI WA HABARI ZA KILIMO SAYANSI WAPIGWA MSASA JIJINI DODOMA

$
0
0

Mwanaharakati na Mwandishi wa Vitabu kuhusu Sayansi ya Kilimo kutoka nchini Uingereza Mark Lynas (kulia), akitoa mada kwenye mafunzo ya uandishi wa habari za kilimo  Sayansi kuhusu Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) kutoka mikoa mbalimbali na nje ya nchi yaliyofanyika jijini Dodoma leo.
 Wanahabari wakiwa kwenye mafunzo hayo.

 Mafunzo yakiendelea.


 Muonekano wa ukumbi katika mafunzo hayo.




 Mratibu wa OFAB nchini Tanzania, Dk.Philbert Nyinondi, akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
 Mtafiti wa Kilimo, Justin Ringo,  kutoka Kituo cha Utafiti cha TARI-Ilonga mkoani Morogoro, akichangia jambo.
 Mwanahabari Dino Mgunda akichangia jambo.
 Mwanahabari David Rwenyagila akichangia jambo.
 Mwanahabari Benson Eustace akiuliza swali. 
 Mafunzo yakiendelea.

 Ofisa Mwandamizi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Thomas Chali, akielezea kuhusu kanuni za matumizi ya GMO hapa nchini.
Mhariri Mtendaji wa Taasisi ya Cornell Alliance for Science Bi. Joan Conrow kushoto), akielezea jinsi ya kuandika habari zinazohusu GMO. Kulia ni Mwanaharakati na Mwandishi wa Vitabu kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na mazingira kutoka nchini Uingeleza Bw.  Mark Lynas.
Muonekano wa ukumbi wa mafunzo hayo.
Na Dotto Mwaibale, Dodoma

WAANDISHI wa Habari nchini  wametakiwa kutumia taaluma zao kuelimisha jamii kuhusu  Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) hasa katika sekta ya kilimo.


Akitoa mada katika mafunzo  kwenye mafunzo ya uandishi wa habari wa kilimo sayansi kuhusu GMO kutoka mikoa mbalimbali na nje jijini Dodoma leo Ofisa Mwandamizi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Thomas Chali alisema waandishi wa habari ni wa muhimu katika kutoa mafunzo kupitia taaluma zao.

Katika hatua nyingine Chali alisema pamoja na kuwepo kwa Sheria ya uwepo Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) nchini bado zipo changamoto kuu tano katika usimamizi wa teknolojia hiyo ya kisasa.


Alisema Sheria ya Tanzania inaruhusu matumizi na kufanyika kwa tafiti mbalimbali zinazohusu GMO ila kinachohitajika ni taratibu kufuatwa ili kuhakikisha usalama unakuwepo.  


Alisema pamoja na kuwepo kwa sheria hiyo changamoto ya uelewa mdogo, uchache wa wataalam, uhaba wa miundombinu, uwepo wa mfumo wa uwajibikaji na wasiwasi wa baadhi ya watu ni mambo ambayo wanayafanyia kazi ili kuhakikisha tekonolojia hiyo inakuwa na manufaa nchini na kwa wananchi.


Ofisa huyo alisema ili kuhakikisha wanaenda pamoja katika kutatua changamoto hiyo wamekuwa wakitoa elimu, kuwajengea uwezo watu mbalimbali kuhusu teknolojia hiyo.


Chali alisema Serikali inatambua fursa zilizopo katika matumizi ya bioteknolojia ya kisasa kwenye kuendeleza sekta ya kilimo nchini ambayo ni mkombozi wa wananchi kwa asilimia kubwa.


Akichangia Mada kuhusu GMO, Mwanaharakati na Mwandishi wa Vitabu kuhusu Sayansi ya Kilimo kutoka nchini  Uingereza,Mark Lynas   alisema waandishi wa habari ni watu muhimu katika  mafanikio ya jamii yeyote hivyo wanawajibu wa kutumia taaluma yao kuwabadilisha na kuelezea teknolojia hiyo ya kisasa.


"Mimi ni mmoja ya watu ambao nilikuwa napinga GMO lakini baada ya kupata elimu ya kutosha nikaelewa na sasa nimekuwa mwanaharakati mzuri ambaye nimeandika vitabu vya kilimo sayansi,"alisema.


Alisema GMO  kwa sasa imethibitishwa na taasisi na mashirika mbalimbali  duniani kama American Association for the Advancement Science (USA), National  Academia of Science (USA), Royal Society (UK), African Academia of Science na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa haina madhara  katika  kilimo.


Mwanaharakati  huyo alisema kwa sasa bidhaa za GMO  zinatumika kwa binadamu na mifugo kote duniani hivyo  hakuna namna ya kuikwepa.


Aidha Mwandishi huyo alisema GMO  inaonesha matokeo chanya kwa wakulima ambapo wanavuna mazao kwa asilimia 200 tofauti na awali.


Pia aliongeza kuwa teknolojia hiyo imekuwa mkombozi katika maeneo yaliyoathirika kwa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.


Lynas alisema hoja za baadhi ya watu kuwa GMO inasababisha magonjwa ya saratani na vichwa vikubwa haina mashiko katika ulimwengu  wa sasa.


Mafunzo hayo yameandaliwa na Jukwaa la Wazi la Kilimo na Teknolojia Afrika (OFAB) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Cornell cha Marekani, Cornell Alliance for Science na African Agricutural Technology Foundation (AATF). 


SUKOS YAKABIDHI VIFAA VYA ZIMA MOTO IDARA YA URATIBU WA MAAFA NCHINI

$
0
0


Mkurugenzi wa Taasisi ya Maafa, Majanga na Uokoaji -SUKOS, Suleiman Kova (kulia) akikabidhi Hati ya Shukrani kwa Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kanali Jimmy Said Matamwe walipomtembelea kukabidhi vifaa vya zima moto Ofisini kwake Dodoma.


Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kanali Jimmy Said Matamwe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa SUKOS Foundation walipotembelea Idara hiyo ili kukabidhi Vifaa vya Zima Moto pamoja na hati ya shukrani kwa namna Taasisi yake inavyoshirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, kulia kwake ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Suleiman Kova.


Mkurugenzi wa Taasisi ya Maafa, Majanga na Uokoaji -SUKOS, Suleiman Kova (kulia) akizungumza jambo wakati wa kukabidhi vifaa vya zima moto pamoja na hati ya shukrani kwa Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kanali Jimmy Said Matamwe (katikati) na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi (Mipango na Utafiti) Idara hiyo Bw.Bashiru Taratibu walipotembelea Oktoba 15, 2018.


Mkurugenzi wa Taasisi ya Maafa, Majanga na Uokoaji – SUKOS, Suleiman Kova akimkabidhi vifaa vya zima moto Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kanali Jimmy Said kwa ajili ya kutoa huduma ya uokoaji endapo itatokea majanga ya moto katika maeneo ya kazi.


Mkurugenzi Msaidizi Mipango na Utafiti Idara ya Uratibu wa Maafa Bw.Bashiru Taratibu akiangalia vifaa vya zima moto vilivyokabidhiwa na Taasisi ya Taasisi ya Maafa, Majanga na Uokoaji –SUKOS Oktoba 15, 2018 kwa ajili ya kutoa huduma ya uokoaji endapo itatokea majanga ya moto.


Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kanali Jimmy Said Matamwe (katikati) akipokea maelezo kutoka kwa Meneja wa Oparesheni Bi.Rahma Kova wakati wa kukabidhi cheti cha Shukrani ya ushirikiano uliopo kati ya SUKOS na Ofisi ya Waziri Mkuu.

PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

WAKAZI WA MKOA WA TANGA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MRADI MPYA WA BOMBA LA GESI

$
0
0
 Afisa Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) Ayubu Masenza katikati akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda lao kwenye eneo la Tangamano kulikokuwa kunafanyika maonyesha ya wiki ya vijana Kitaifa
 Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Malik Munis kushoto akiwaonyesha wananchi maeneo bomba la mafuta litapita  waliojitokeza kwenye banda lao
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) Eugene Isaya akiwaonyesha kitu wananchi waliojitokeza kwenye banda lao



WAKAZI wa Mkoa wa Tanga wametakiwa kuchangamkia fursa ikiwemo kupokea mradi mpya wa bomba la gesi toka Tanga-Tanzania hadi nchini Uganda mradi ambao utakwenda sambamba na mradi mkubwa wa Bomba la Mafuta.

Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mwandamizi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) Ayubu Masenza wakati alipozungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mradi mkubwa wa bomba la Mafuta wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya vijana kwenye viwanja vya Tangamano Jijini Tanga

Alisema mbali ya uwepo wa mradi huo wa bomba la Mafuta toka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga-Tanzania Serikali ya Uganda ipo katika mchakato mkubwa wa Ujenzi wa mradi wa bomba la gesi litakaloanzia Jijini hapa hadi nchini Uganda.

Alisema Jiji hilo litakuwa miongoni mwa Majiji ambayo yanakuwa kwa kasi kutokana na uwepo wa miradi mikubwa barani Afrika ambayo inatarajiwa kutekelezwa na Serikali ya Tanzania na ile Uganda kutokana na ushirikiano mwema wa kiuchumi.

Aidha alisema ujio wa bomba la mafuta utakuwa na manufaa makubwa kwa wakazi wa Jiji hili la Tanga kutokana na Uganda kuhitaji gesi ya hapa nchini hivyo itakapokuwa ikitokea Mkoani Mtwara itafika mkoani hapa na itakwenda sambamba na bomba hilo hadi Uganda.

Masenza alisema uwepo wa gesi Jijini Tanga kutaongeza fursa za
wawekezaji kutokana na viwanda vingi kuhitaji matumizi ya gesi katika shughuli zote za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.

Alisema mbali na uwepo wa ajira kupitia miradi hiyo pia ongezeko la matumizi ya gesi litakuwa kubwa hasa katika viwanda, mashule,taasisi za kijeshi,Hospitali,na mwananchi mmoja mmoja jambo ambalo linaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira.

Alisema hatua zote muhimu za utekelezaji wa miradi hiyo mikubwa umekwisha anza na zipo katika hatua nzuri huku jambo la msingi kwa wananchi kuwa na utayari ili kunufaika na fursa hizo.

“Nijukumu la wananchi wa Tanga sasa kuweza kunufaika mbali na Serikali lakini mwamanchi mmojammoja wananafasi kubwa kunufaika na miradi hii itakayoweza kubadilisha maisha yao kwa ujumla.

Hata hivyo alisema mradi huo wa bomba la mafuta utapitia mikoa
nane,wilaya 24,kata 184 na Vijiji 270 huku matarajio ya maeneo hayo ni kupitia wa mradi wa bomba hilo la gesi kutokana na ujenzi wake utakwenda sambamba.

TATIZO LA VYOO MAHAKAMA ZA MWANZO KANDA YA SHINYANGA SASA KUWA HISTORIA

$
0
0
Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Shinyanga, Mhe. Richard Kibella akikagua kujionea hali ya choo.




Na Emmanuel Oguda-Mahakama Kuu, Shinyanga

Mahakama Kanda ya Shinyanga imedhamiria kuhakikisha kuwa kila Mahakama ya Mwanzo inakuwa na vyoo bora ambavyo vitatoa huduma kwa Wananchi na wateja wa Mahakama pamoja na Watumishi wa Mahakama za Mwanzo waliopo katika Kanda hiyo.

Akikagua baadhi ya Mahakama ambazo tayari zimeanza kutekeleza agizo la ujenzi wa vyoo bora wakati wa ziara ya ukaguzi wa Mahakama mapema mwezi Oktoba, 2018, Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu, Kanda ya Shinyanga, Mhe. Jaji Richard Kibella amepongeza Mahakama ambazo tayari zimetekeleza agizo ambalo alilitoa mwezi Julai, 2018.Mhe. Jaji Kibella aliagiza kwa mara nyingine kwa Mahakama ambazo bado kuanza kutekeleza agizo hilo kufikia mwezi Desemba, 2018.

“Mahakama za Mwanzo zinahudumia Wananchi wengi hivyo ni vyema kila Mahakama kuhakikisha inatunza mazingira yake kwa kuwa na huduma ya vyoo bora ili wananchi waweze kujisitiri pindi wawapo Mahakamani,” alisisitiza Mhe. Jaji Kibella.

Mhe. Jaji Mfawidhi huyo aliongeza kuwa Mahakama zote za mwanzo zilizopo ndani ya Kanda ya Shinyanga zinatakiwa kuanza mara moja ujenzi wa vyoo ili kutimiza azma ya utunzaji bora wa mazingira sambamba na kutoa huduma kwa wananchi.

Mahakama za Mwanzo ambazo tayari zimetekeleza ujenzi wa vyoo ni pamoja na Mahakama ya Mwanzo Kilago, Mahakama ya Mwanzo Mpunze na Mahakama ya Mwanzo Ukune na zote za Wilayani Kahama.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE OKTOBA 16,2018

JAJI MKUU ATAKA KESI ZIMALIZIKE KWA WAKATI

$
0
0











Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwasili katika kisiwa cha Ukerewe kuanza ziara yake ya kukagua shughuli za Mahakama katika Mkoa wa Mwanza. Leo Jaji Mkuu alitembelea Mahakama ya wilaya ya Nansio- Ukerewe, Mahakama za Mwanzo za Nansio mjini na Ilangala pamoja na Ofisi ya Mkuu wa wilaya. Katikati ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza Mhe. Mary Moyo.



Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akielezea kuhusu Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama baada ya kumkabidhi kitabu cha Mpango huo Kaimu Mkuu wa wilaya ya Ukerewe ambaye ni Katibu Tawala wa wilaya (DAS) Bwana Focus Majumbi.



Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Ilangala mara baada ya kuzungumza nao.wakati Jaji Mkuu alipotembelea ofisi ya Mkuu wa wilaya



Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa katika picha ya pamoja na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Pius Msekwa na Mkewe mama Anna Abdalah alipowatembelea nyumbani kwao Nansio Ukerewe. Wa kwanza kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza Mhe. Sam Rumanyika pamoja na watumishi wengine wa Mahakama ya Tanzania.



Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa katika picha ya pamoja na Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Pius Msekwa na Mkewe mama Anna Abdalah alipowatembelea nyumbani kwao Nansio Ukerewe


Na Lydia Churi- Mahakama, Mwanza

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka watumishi wa Mahakama katika wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza hususan Mahakimu kutimiza wajibu wao kikamilifu kwa kuhakikisha wanamaliza kesi ili wananchi waweze kupata haki kwa wakati.

Akizungumza na Watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Nansio-Ukerewe pamoja na Mahakama za Mwanzo za Ilangala na Nansio mjini, Jaji Mkuu pia amewakumbusha Mahakimu kuhakikisha hukumu zinatolewa ndani ya siku 90 baada ya shauri kusikilizwa na endapo siku zitazidi basi zisizidi siku ishirini na moja.

Alisema Mahakama ya Tanzania inafanya kila jitihada ili kuhakikisha wananchi wanapata haki kwa wakati huku akitolea mfano wa nakala za hukumu kutolewa bure. Alisema Mahakama imeingia mkataba na shirika la Posta ili kusambaza nakala za hukumu pamoja na nyaraka nyingine za mahakama.

“Suala la hakimu kuchelewesha hukumu bila sababu za msingi halikubaliki na ni utovu wa nidhamu, jiwekeni kwenye nafasi ya wanaocheleweshewa hukumu ndipo mtaona ni kwa namna gani wanaumizwa na suala hili”, alisema Jaji Mkuu.

Awali akizungumza na Kaimu Mkuu wa wilaya ya Ukererwe Bwana Focus Majumbi, Jaji Mkuu alitoa wito kwa viongozi wa serikali kusaidia kuwaelimisha wananchi taratibu za Mahakama ili wapate haki kwa wakati kwa kuwa haki ni kwa mujibu wa Sheria.

Alisema wananchi wengi hawafahamu taratibu za Mahakama ambapo badala ya kudai haki zao Mahakamani huenda kwa watu wasiohusika na kusababisha haki zao kuchelewa.

Naye Kaimu Mkuu wa wilaya ya Ukerewe aliiomba Mahakama ya Tanzania kuanza kuitumia Mahakama ya Mwanzo ya Irugwa ambayo hivi sasa haijaanza kutumika kutokana na ukosefu watumishi. Mkuu huyo wa wilaya pia aliiomba Mahakama kusaidia ili wilaya yake isaidiwe kupata Mwenyekiti wa kudumu wa mabaraza ya kata.

Jaji Mkuu wa Tanzania anaendelea na ziara yake ya siku nne mkoani Mwanza ambapo atakagua utekelezaji wa shughuli za Mahakama.

GOOD FOOD AFRIQUE TARGETS TO PROMOTE AGRO-PROCESSING FOR INDUSTRIALIZATION

$
0
0
As we mark this year’s World Food day with the slogan ‘Zero hunger’ which is goal number 2 on the sustainable development goals (SDGS) Good Food Afrique is specializing in promoting smallholder farmers and entrepreneurs who are involved in agro-industry especially food processing in push for industrialization.

The new organization wants to achieve this through creating markets, provision of suitable processing premises, processing facilities and equipment, training, mentorship and build good value supply chain in the industry.

“My idea is in sync with Tanzania’s current socio-economic growth policy through industrialization,” said the organization’s CEO, Ms Juliana Mataba.Ms Mataba who is the promoter of the good food concept was selected among the 12 young entrepreneurial women from East African countries to attend a fellowship programme which she now wants to share the experiences.

The programme named “Advance young women in agribusiness, entrepreneurship and innovators fellowship programme” was held at the Michigan State University (MSU) in the US under the sponsorship of the US State Department of Education and Culture.

During the five-week programme, she was attached to the university’s product centre where she was trained on assisting food processors with processing ideas and the mechanism of building such ideas into business and ultimately business set-ups.

The exposure she acquired from this programme has motivated her to launch her mission of reaching out and fostering small-scale agroindustry entrepreneurs, according to her.“The good food concept seeks to incubate food processing projects and simultaneously promote value chains for agroindustry in furtherance of value addition to agricultural products. Good food processing will help to reduce post-harvest losses as well as linking the local agriculture to the international markets,” she said.

Agriculture is Tanzania’s economic mainstay accounting for about 30 per cent of the gross domestic product (GDP). The sector also provides employment to over 65 per cent of Tanzanians and in favorable seasons, it covers more than 100 per cent of the domestic food needs.

However, there is little value addition and small and medium agro processors have not been able to produce, brand and market Tanzanian products well and hygienically resulting into failure to penetrate both local and international markets.“Food processing is an opportunity to increase entrepreneurship, create jobs, potential for improving export earnings, widening tax base as well as developing the sector in general,” said Ms Mataba.

Good Food Afrique intends to bring together all food stakeholders including vendors, food processors, supermarkets, fresh produce, farmers, food agents, distributors and all stakeholders in the value chain who are dealing with food and agriculture in Tanzania.

“Our aim is to see the food industry moving forward in the thriving manner,” she adds
Juliana Mataba, CEO of Good Food Afrique addressing a meeting while in the US recently.

TFDA yatoa Elimu ya Madhara yatokanayo na vipodozi yenye viambato sumu

Halotel kuwekeza dola za kimarekani 700 katika sekta Umma na mawasiliano

$
0
0
Na Karama Kenyunko Globu ya jamii
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Halotel inakusudia kuwekeza dola za kimarekani (USD) 700 katika sekta Umma na  mawasiliano nchini ikiwa na malengo ya kuwafikia wateja zaidi ya milioni Sita katika kipindi cha miaka mitano toka kuanzishwa kwake.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Halotel Tanzania, Nguyen Van Son, amesema hayo leo Oktoba 16,2018 wakati wa maadhimisho ya miaka mitatu ya Halotel yaliyofanyika katika ofisi zao.

Son amesema, pamoja na mipango hiyo ya kuwekeza, kampuni hiyo pia imekusudia kuboresha zaidi Huduma ya utumaji wa pesa kwa njia ya mtandao, 'Halopesa' kwa ajili ya Wateja binafsi, mashirika na serikali kwa ujumla.

 "Mpaka sasa tunatimiza miaka mitatu Halotel inefanya uwekezaji wa dola za kimarekani (USD) 500 ikiwa ndio kampuni inayoongoza kwa kwa kuwekeza miuondombinu ya mawasiliano katika sehemu mbalimbali nchini inayowafikia asilimia 95 ya wananchi wote ikiwa n vituo 4400 vya kupokea mawasiliano" amesema Son.

Kampuni hiyo imepanga kuimarisha mtandao wake wa 4G ili kuwafikia Wateja wengi zaidi hadi wale walioko pembezoni mwa miji na kuwapa gharama nafuu za mawasiliano ambapo mpaka sasa Wateja zaidi ya milioni tatu na wengine zaidi ya milioni moja waliojiunga na Halopesa.

Ameongeza, kuwa, kupitia Huduma hio wanaamini watakuwa wameisaidia serikali na taasisi zote za kibiashara kuendeleza Utoaji wa Huduma zao kwa ufanisi ukizingatia Halotel imekuwa ikishiriki katika shughuli mbali mbali za kijamii zinazoliwezesha taiga kufikia malengo yake mbali mbali.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Halote, Mhina Semwenda kulia akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuadhimisha miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake hapa nchini. kushoto ni Naibu mkurugenzi Mkuu wa Halotel, Nguyen Van Son.

Naibu mkurugenzi mkuu wa Halotel Nguyen Van Son akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kusheherekea miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake hapa nchini kulia ni katibu wa kampuni hiyo Nguyen Thi Thuy Linh.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza Naibu mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Van Son jijini Dar es Salaam leo Oktoba 16.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya jamii

TAARIFA

Rais Magufuli ateua Makamishna wa Tume ya Kurekebisha Sheria na NARCO

MBUNGE AZZA HILAL AKABIDHI VIFAA TIBA VYA MILIONI 36.5 KWENYE VITUO VYA AFYA WILAYANI KAHAMA

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) amekabidhi msaada wa Vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 36.5 kwa ajili ya vituo vya afya na zahanati sita zilizopo katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Msalala na Kahama Mji wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Mheshimiwa Azza amekabidhi vifaa tiba hivyo leo Jumanne Oktoba 16,2018 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Anamringi Macha wakati wa Kikao cha Baraza la UWT wilaya ya Kahama uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kahama.
Vifaa tiba hivyo ni pamoja na shuka 100,mashine za kupima damu,wingi wa damu,sukari,joto,mapigo ya moyo na vifaa vya kusaidia kujifungua kwa akina mama ambavyo kupatikana kwake kumetokana na jitihada za mbunge huyo kuhakikisha vifo vya mama na mtoto vinapungua mkoani Shinyanga.
Awali akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa tiba hivyo,Mheshimiwa Azza Hilal alisema kupitia Kampeni yake ya ‘Afya Yangu Mtaji Wangu’ na kuwajali akina mama aliamua kutafuta wadau kwa ajili ya kusaidia kumaliza changamoto ya uhaba wa vifaa tiba katika vituo vya afya na zahanati.
“Nawashukuru sana Bahari Pharmacy Ltd na Brett &Beileys kwa kunishika mkono na kuchangia kupatikana kwa vifaa hivi ambavyo leo navikabidhi ili vikatumike kwenye zahanati na vituo vya afya kwani hatutaki kuona vifo vya mama na mtoto”,alieleza Azza.
“Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Jemedari,Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiria kuboresha huduma za afya,na tutaendelea kushirikana ili kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya bora ili washikiriki katika shughuli za uchumi”,aliongeza.
Alivitaja vituo vya afya vitakavyonufaika na msaada huo kuwa ni Mwendakulima,Mbika na Lunguya na zanahati ambazo ni Ngogwe,Kisuke na Bulige.
Akipokea vifaa tiba,Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha alimshukuru mbunge huyo kwa msaada huo na kubainisha kuwa ameunga mkono kwa vitendo ilani ya CCM na juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli katika kuboresha sekta ya afya.
“Nikupongeze sana kwani umetumia cheo chako kwa faida ya wote badala ya kujinufaisha wewe mwenyewe,lakini nikushukuru pia kwa kuendelea kujitoa kwa hali na mali katika kukitumikia chama na wananchi,umekuwa kiungo mzuri sana”,alisema Macha.
Kwa Upande wake Mbunge wa Jimbo la Ushetu,Mheshimiwa Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi aliahidi kumuunga mkono mheshimiwa Azza kwa kutoa msaada wa vifaa tiba katika vituo vitatu vya afya wilayani Kahama.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza wakati akikabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 36.5 kwa ajili ya zanahati na vituo vya afya wilayani Kahama leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kahama.Kushoto ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kahama,Telephora Saria,kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Myonga.  - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 36.5 kwa ajili ya zanahati na vituo vya afya wilayani Kahama vilivyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) kwa kushirikiana na wadau wake Bahari Pharmacy Ltd na Brett &Beileys.
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha(aliyevaa miwani) akiangalia vifaa tiba vilivyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad.
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha akimshukuru Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad kwa kuleta vifaa tiba wilayani Kahama. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Ushetu,Mheshimiwa Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi. 
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi vifaa tiba kwa  Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi shuka ikiwa ni sehemu ya shuka 100 alizotoa kwa ajili ya vituo vya afya na zahanati wilayani Kahama.
Wa pili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha akiwa ameshikilia boksi lenye mashine ya kupimia sukari mwilini. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Myonga.Wa kwanza kushoto ni  Mbunge wa Jimbo la Ushetu,Mheshimiwa Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi akifuatiwa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiwa ameshikiliwa vifaa tiba.
Mwakilishi wa Mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya Ushetu,Dk. Joseph Mugizi akisoma maandishi katika mashine/kifaa cha kupimia sukari baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha.
Kushoto ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Kahama,Dk.  David Lucas akipokea mashine/kifaa cha kupimia wingi wa damu.
Mwakilishi wa Mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya Msalala,Dk. Martine Dotto akipokea kifaa cha kupimia mapigo ya moyo.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Kahama,Dk.  David Lucas akiwa ameshikilia kifaa cha vifaa vya kujifungulia kwa akina mama.Katikati ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akifafanua kuhusu vifaa vya kujifungulia.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa UWT halmashauri ya wilaya ya Ushetu
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa UWT halmashauri ya wilaya ya Kahama Mji.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa UWT halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha akizungumza baada ya kupokea vifaa tiba vilivyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad.Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kahama,Telephora Saria.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu,Mheshimiwa Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi akizungumza wakati Mheshimiwa Azza Hilal akikabidhi vifaa tiba.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live


Latest Images