Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1696 | 1697 | (Page 1698) | 1699 | 1700 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Na Estom Sanga-Zanzibar

  Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- Ksiwani Unguja Bw. Ayoub Mohamed Mahmoud amepongeza jitihada zinazofanywa na Mfuko huo katika kutekeleza maelekezo ya serikali ya kusaidia jitihada za kuwandolea kero ya umaskini wananchi. 

  Bwana Mahmoud ambaye pia ndiye Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi amesema TASAF imekuwa kielelezo sahihi na cha kujivunia katika kutekeleza wa sera za kupambana na umaskini kwa kushajihisha wananchi kujiletea maendeleo kwa kutumia nguvu na raslimali zilizoko kwenye maeneo yao. 

  Kiongozi huyo ameyasema hayo wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kianga unatekelezwa na Wananchi kwa kushirikiana na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF kupitia utaratibu wa Mfuko huo wa kuendeleza miundombinu ya Afya,Elimu na Maji kwenye maeneo ya Walengwa. 

  Mkuu huyo wa Mkoa wa Mjini Magharibi amesema miradi iliyoibuliwa na Wananchi kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na TASAF imeleta mageuzi makubwa katika maeneo mengi ya visiwa hivyo kufikia hatua ya baadhi yao kuzalisha bidhaa za kilimo kama vitunguu maji na hivyo kujiongezea kipato na kuukimbia umaskini uliokuwa unawakabili. 

  Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga amesema tangu Mfuko huo ulipoanzishwa na Serikali, umetoa mchango mkubwa katika kusaidia jitihada za kuboresha maisha ya wananchi huku akisisitiza kuwa mafanikio hayo yametokana na sera sahihi za kupambana na umaskini zinazoratibiwa na serikali. 

  Bwana Mwamanga amesema TASAF imekuwa ikizingatia kwa kina maelezo ya Serikali yanayotilia mkazo pamoja na mambo mengine umuhimu wa wananchi wakiwemo Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kufanya kazi kwa bidii ili waweze kuondokana na adha ya umaskini na kujiongezea kipato chao. 

  Mkurugenzi Mtendaji huyo wa TASAF amesema licha ya mafanikio makubwa yaliyopatikana katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, Serikali kupitia Mfuko huo imeamua kubosheresha kuboresha zaidi utekelezaji wa Mpango huo ili uweze kuwafikia wananchi wote wanaokabiliwa na Umaskini nchini huku msisitizo ukiwa ni kuibua shughuli za uzalishaji mali kwa kufanya kazi na kisha kulipwa kulingana na kazi watakayokuwa wameifanya. 

  Kwa Upande wao wananchi wa shehia ya Kianga wameishukuru Serikali kwa kuuwezesha Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF kutekeleza miradi kadhaa ya maendeleo kwenye shehia yao ukiwemo mradi huo mkubwa wa ujenzi wa Kituo cha Afya kitakachowapunguzia adha ya kufuata huduma hiyo mbali na eneo lao.
  Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,bw. Ladislaus Mwamanga (aliyesimama) akihutubia wananchi wa Shehia ya Kianga,wilaya ya Magharibi A mkoa wa Mjini Magharibi kisiwani Zanzibar (hawapo pichani) baada ya kukagua ujenzi wa kituo cha Afya unaotekelezwa na TASAF kwa kushirikiana na Wananchi wa eneo hilo.

   Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi ,Unguja Bw. Ayoub Mohamed  Mahmoud (aliyesisima nyuma ya meza) akiwahutubia wananchi wa Shehia ya Kainga baada ya kukagua ujenzi wa jengo la kituo cha Afya cha shehia hiyo unaojengwa na TASAF kwa kushirikiana na wananchi.
   Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Bw. Mahmoud akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw.Mwamanga na maafisa wa serikali baada ya kukagua ujenzi wa jengo la Kituo cha Afya-Kianga (nyuma yao)
   Baadhi ya wananchi wa Shehia ya Kianga kisiwani Unguja wakisikiliza hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga( hayupo pichani) baada ya kukagua jengo la kituo cha Afya kinachojengwa na TASAF kwa kushirikiana na Wananchi.
   Sehemu ya jengo la Kituo cha Afya Kianga katika mkoa wa Mjini Magharibi kinachoendelea kujengwa TASAF na Wananchi wa eneo hilo ambacho kitapunguza tatizo la kufuata huduma za Matibabu mbali na eneo lao.

  0 0

  Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja aitwaye ASAJILE JUMA @ MWANDIGA [28] Dereva Tax na Mkazi wa Nzovwe Jijini Mbeya kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha pamoja na kupatikana na mali za wizi.
  IMG_3201
  Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 10/10/2018 majira ya saa 15:30 alasiri huko Ndanyela, Kata ya Nzovwe, Tarafa ya Iyunga ndani ya Jiji na Mkoa wa Mbeya baada ya kufanyika msako mkali katika maeneo hayo.
  IMG_3198
  Aidha mtuhumiwa alifanyiwa upekuzi kwenye gari analolitumia na kwenye makazi yake na alikutwa na mali mbalimbali zidhaniwazo ni za wizi zikiwemo mali zilizoibiwa na taarifa yake kufunguliwa katika kituo cha Polisi Mbalizi ambazo ni:-
  1. Hair dryer moja aina ya Equatol 3000 rangi nyeupe
  2. Camera aina ya NIKON D.3100 rangi nyeusi
  3. Video camera aina ya Sony
  4. Video camera aina ya Sony PD.175
  5. Betri 3 za camera
  6. Video audio AMP splitter
  7. Video mixer aina ya data video
  8. Video projector aina ya EPSON
  9. DVD Disk empter
  10. Nyanya 8 za kusafirishia picha(USB)
  11. Nyaya 1 ya Picha na taa
  12. Taa 1 aina ya simplex
  13. Video light aina ya TRIOPO

  IMG_3165

  Baada ya Upekuzi huu, Jeshi la Polisi lilifanya mahojiano ya kina na mtuhumiwa kulikopelekea kutaja matukio ambayo amehusika nayo ambayo ni wizi wa mali pamoja na watuhumiwa wenzake waliokamatwa ambao ni washirika wa mtuhumiwa ASAJILE JUMA @ MWANDIGA katika matukio ya wizi:-
  Watuhumiwa hao ni pamoja na:-
  1. ANNA FERIKI [20] Mfanyabiashara na Mkazi wa Kalobe
  2. EPHRASIA HOSEPH [44] Mkazi wa Kalobe
  Mali zilizokamatwa kwenye upekuzi mara baada ya kukamatwa ASAJILE JUMA @ MWANDIGA baadhi zilitambuliwa na mlalamikaji bwana DAHIL MOHAMED kuwa ni mali zilizoibiwa katika tukio alilolitolea taarifa.
  Pia katika Upekuzi huo Jeshi la Polisi lilikamata kombati za Jeshi mashati 03 na suruali 03 zikiwa ni sare za majeshi ya DRC –CONGO, KENYA na CHINA.
  Pamoja na hayo ilikamatwa Gari aina ya Noah yenye namba T.215 CHF kwa mtuhumiwa ambayo ilikuwa ikitumika kubebea mali za wizi.
  Pamoja na mali hizo Jeshi la Polisi lilikamata tairi 1 ya gari, betri 2 za gari, Guard boot pair 60 za rangi mbalimbali zilizokutwa kwa mtuhumiwa ambazo zinahusishwa na tukio la wizi lililoteka tarehe 04/10/2018 huko eneo la mlima Iwambi Wilaya ya Mbeya Vijijini kwenye gari lenye namba T.849 AUL aina ya FUSO lililokuwa likitokea mkoa Rukwa kuja Mbeya likiendeshwa na EUSEBIUS MWALONGO.
  Awali mnamo tarehe 21/09/2018 majira ya saa 22:00 usiku mtu mmoja aitwaye DAHIL MOHAMED [35] Video shooter na Mkazi wa Sokomatola Jijini Mbeya akiwa anaendesha gari lenye namba T.834 AKB aina ya Toyota Dyna akiwa anasafiri akitokea Sokomatola kwenda Kiwila Wilayani Tukuyu alipofika eneo la Mlima Igawilo alivamiwa na watu sita wasiojulikana wakiwa na silaha za jadi yaani mapanga na nondo na kumpiga sehemu ya paji la uso juu ya jicho la kulia kwa kutumia nondo baada ya kuvunja kioo cha dirisha la gari na kuiba vifaa mbalimbali ambazo ni:-
  1. Camera aina ya NIKON D.3100 rangi nyeusi
  2. Video camera aina ya Sony
  3. Video camera aina ya Sony PD.175
  4. Video mixer 1
  5. Betri 3 za camera
  6. Video audio AMP splitter
  7. Video mixer aina ya data video
  8. Video projector aina ya EPSON
  9. DVD Disk empter
  10. Nyanya 8 za kusafirishia picha(USB)
  11. Nyaya 1 ya Picha
  12. Taa 1 aina ya simplex
  13. Video light aina ya TRIOPO
  14. Begi moja lenye camera 2
  15. Begi lenye laptop 2(compact na HP core –i5
  Mali zote zilikuwa na thamani ya Tshs 17,350,000/=. Tukio hili liliripotiwa kituo cha Polisi Inyala huko Wilaya ya Kipolisi Mbalizi na kufunguliwa kesi ya Unyang’anyi wa kutumia Silaha. Baada ya tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya liliendesha msako mkali katika maeneo mbalimbali na kufanikiwa kumkamata ASAJILE JUMA @ MWANDIGA ambaye baadae aliwataja washirika wenzake. Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
  Katika tukio jingine Jeshi la Polisi Mkoa wa mbeya linawashikilia watuhumiwa watatu wakiwa na samaki wanaosadikiwa kuwa wa wizi.
  Watuhumiwa waliokamatwa wamefahamika kwa majina ya:-
  1. NIKOLAUS CHARLES [25] Mkazi wa Kalobe
  2. VENANCE ISACK [27] Mkazi wa Ruanda
  3. MUSA EDSON NSWIMA [22] Mkazi wa Kalobe
  Watuhumiwa kwa pamoja walikamatwa mnamo tarehe 12.10.2018 majira ya saa 07:00 asubuhi huko maeneo Kalobe Juakali, Kata ya Nzovwe, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya wakiwa na samaki kg 100 wakiwa wamehifadhiwa kwenye mifuko ya sandarusi samaki wanaosadikiwa kuibiwa katika tukio la wizi lililotokea huko eneo la mlima Iwambi Mkoani Mbeya.

  0 0


  Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

  NAIBU Waziri wa kilimo na uvuvi na Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega amezindua rasmi maonesho ya nne ya ndege wafugwao katika viwanja vya maonesho (sabasaba) jijini Dar es salaam.

  Akizungumza katika uzinduzi huo Ulega ameeleza kuwa maonesho ya mwaka huu yamehusisha makampuni mengi ya ndani na nje ya nchi kama Kenya, Poland na China na amewakaribisha kuwekeza nchini kutokana na kuwepo kwa fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali.

  Aidha ametoa pongezi kwa vyama vyote vya wadau wa ndege wafugwao chini ya chama mama cha Tanzania Poultry show (TPS) kwa kutoa kipaumbele katika suala la ufugaji wa kuku.Pia amewataka kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja  na wao kama serikali wapo pamoja kama walezi wao, katika kuhakikisha wanasonga mbele zaidi na amewapongeza kwa ushirikiano wao kupitia vyama vyao.

  Ulega amesema kuwa Rais Magufuli ameendelea kusimamia maendeleo ambapo hadi sasa tozo zilizokuwa kero kwa wafugaji, wakulima na wavuvi zimeondolewa ili kuweza kuendeleza shughuli za hizo.Kuhusiana na changamoto zilizotolewa na wafugaji hao hasa katika mashudu na soya ambazo huagizwa kutoka nje Ulega amesema kuwa maandalizi yameanza katika nyanda za juu kusini ambako soya zimelimwa na wanavutia uwekezaji katika usindikaji ili kuweza kuvutia uwekezaji wa kuchakata soya na kupunguza gharama za kuagiza bidhaa hizo kutoka nje.

  Kuhusiana na machinjio zinazochinja kuku Ulega amesema kuwa sehemu hizo zimekuwa na ubora wa chini sana na amewataka wahakikishe wanaboresha machinjio hayo yanayosimamiwa na halmashauri na manispaa hasa kwa kuzingatia wanaweka  sehemu ya machinjio ya kuku ili kuleta thamani.

  Mwenyekiti wa chama cha ndege wafugwao Harko Bhaghat amemshukuru Naibu waziri na wizara kwa ujumla kwa kutoa kipaumbele kwa wafugaji na kusema kuwa hadi sasa wamepata mafanikio makubwa na kubwa zaidi ni baada ya serikali kuondoa tozo katika bidhaa za mifugo.

  Bhaghati amewataka wafugaji kujisajili ili waweze kupata fursa mbalimbali za kuendeleza soko la ndege wafugwao hasa kuku.
  Naibu Waziri wa  Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wafugaji wa ndege wafugwao, katika ufunguzi wa maonesho ya nne ya ndege wafugwao nchini jana jijini Dar es Salaam . (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu  ya Jamii)
   Mwenyekiti wa chama cha wafugaji wa ndege Harko Bhaghati akisoma risala mbele ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Abdallah Ulega.
   Mtaalamu na mshauri wa mifugo kutoka kampuni ya Animal Care Dkt. Bakari Mwanga akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega  kuhusu uzalishaji na utunzaji wa mifugo unaofanywa na kampuni yao.

   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akitembelea mabanda mbalimbali katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam
  Sehemu ya wafugaji waliojitokeza ili kupata semina na mafunzo kuhusiana na ufugaji wa kuku.

  0 0  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ( wa kwanza mbele) akiendelea na ziara katika mgodi wa makaa ya mawe wa Edenville International (T) Limited uliopo katika kijiji cha Nkomolo II Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa.
  Meneja wa mgodi wa makaa ya mawe wa Edenville International (T) Limited, Jamhuri Mbamba (kushoto) akimwonesha Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia) moja ya makaa ya mawe kwenye mgodi huo.

  Meneja wa mgodi wa makaa ya mawe wa Edenville International (T) Limited, Jamhuri Mbamba (katikati) akielezea hali ya uzalishaji wa makaa ya mawe katika mgodi huo kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) katika ziara hiyo.


  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) akibadilishana mawazo na Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (kulia) kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kabla ya kuanza ziara ya siku moja katika mkoa huo yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini tarehe 12 Oktoba, 2018.  ……………………….

  Na Greyson Mwase, Sumbawanga

  Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini ipo tayari kuwasaidia wawekezaji kwenye shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini ili uchimbaji wao ulete manufaa kwa nchi.

  Aliyasema hayo leo tarehe 12 Oktoba, 2018 mara baada ya kumaliza ziara yake katika mgodi wa makaa ya mawe wa Edenville International (T) Limited uliopo katika kijiji cha Nkomolo II Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja katika mkoa huo yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

  Katika ziara yake Nyongo aliambatana na Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Katavi, Mhandisi Giliard Luyoka, Katibu Tawala Msaidizi – Sehemu ya Miundombinu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Happiness Shayo, Wataalam wa Madini, Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na waandishi wa habari.

  Alisema kuwa katika kuhakikisha watafiti na wachimbaji wa madini wanafanya kazi katika mazingira mazuri, Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini imeanza kusogeza huduma zake kwa kuhakikisha kuwa inaanzisha ofisi za maafisa madini wakazi katika mikoa yote ambapo mkoa wa Rukwa unatarajiwa kupata ofisi kwa mara ya kwanza.

  Katika hatua nyingine Naibu Waziri Nyongo aliushauri uongozi wa mgodi huo kujikita kwenye uzalishaji wa makaa ya mawe ambayo ni bora na kuuza katika nchi za jirani kwa kuwa mahitaji ya makaa ya mawe ni makubwa.

  Aliwataka maafisa madini wakazi wa mikoa yote nchini kuhakikisha wanashirikiana na ofisi za wakuu wa wilaya, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wawakilishi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika zoezi la usimamizi wa upakiaji wa madini kabla ya kusafirishwa ili kudhibiti mianya ya utoroshwaji wa madini mbalimbali.

  Wakati huohuo Naibu Waziri Nyongo aliwataka wachimbaji wa madini nchini kufuata kanuni na sheria za madini katika kuhakikisha kuwa wanalipa kodi stahiki serikalini ili fedha ziweze kuwanufaisha wananchi kupitia uboreshwaji wa huduma za jamii.

  Awali akielezea hali ya uzalishaji wa makaa ya mawe katika mgodi wa makaa ya mawe wa Edenville International (T) Limited, meneja wa mgodi huo Jamhuri Mbamba alisema kuwa, uzalishaji unazingatia mahitaji ya soko na kusisitiza kuwa kwa sasa mahitaji ni takribani tani 3000 kwa mwezi na kuendelea kusema kuwa mgodi unatarajia kuongeza uzalishaji hadi kufikia tani 15,000 za makaa ya mawe kwa mwezi.

  Aliendelea kusema kuwa kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Oktoba 2018 jumla ya tani takribani 9941.78 za makaa ya mawe yalioshwa na kuuzwa kwa wateja wa ndani na nje ya nchi .Akielezea changamoto za mradi Mbamba alisema kuwa, awali lengo kuu la mradi lilikuwa ni uzalishwaji wa umeme lakini mchakato wake umekuwa ukichukua muda mrefu pasipo mafanikio.

  Alisema hadi sasa maongezi kati ya kampuni na Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) yamekuwa yakiendelea kwa kipindi kirefu na kwa sasa kampuni inaandaa zabuni kama ilivyoainishwa hapo awali.

  Aliongeza kuwa pia mradi ulilenga ujenzi wa njia ya umeme ya Mbeya hadi Kigoma hadi Nyakanazi ambao haujaanza kujengwa.

  0 0

   Msanii Elias Barnaba akiwa kwenye Jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea usiku wa kuamkia jana.
    Msanii Mr Blue akiwa kwenye Jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea usiku wa kuamkia jana.
    Msanii Chege akiimba mbele ya mashabiki wake kwenye Jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea usiku wa kuamkia jana.
    Msanii wa Hip Hop Fid Q akiwaimbisha mashabikiwa wake kwenye Jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea usiku wa kuamkia jana.
    Msanii Lulu Diva akiimba  kwenye Jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea usiku wa kuamkia jana.
   Wasanii waliopanda jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote kwenye uwanja wa Majimaji Songea usiku wa kuamkia jana kwa pamoja wakiweka mishumaa juu kumkumbuka Mtayarishaji wa muziki Joshua Magawa a.k.a Pancho Latino aliyefariki hivi karibu kwenye kisiwa cha Mbudya jijini Dar Es Salaam
   Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mhe.Pololite Mgema akiongea na wanachi waliojitokeza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea usiku wa kuamkia jana. Pembeni ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Christina Mndeme ns Mratibu wa Tamasha hilo Shafii Dauda.

  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Christina Mndeme akiongea na wananchi waliojitokeza kwenye Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea usiku wa kuamkia jana.
    Msanii Rubby akiimba kwenye Jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea usiku wa kuamkia jana.


  Likiwa limeingia mkoa wanne Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote limefana na kuacha alama kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani  Ruvuma usiku wa kuamkia jana, Kabla ya kuingia mkoani humo Tamasha hilo lililoanzia Mkoa wa Morogoro limepita  mikoa ya Rukwa, Iringa, Songea na kuelekea Mtwara jumapili hii.

  Akifungua Tamasha hilo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme aliyeongozana na mkuu wa wilaya ya Songea Mjini Mhe. Pololite  Mgema alisema Tunawashukuru Kampuni ya Tigo na Clouds Media kwa kutuletea tamasha hili kubwa mkoani kwetu. “ Hii si kwa burudani pekee bali ni fursa kwa wakaazi wa mkoa huu kwa kuwawezesha kwa kuwaongezea kipato kwa kipindi hiki chote cha wiki nzima”. Niendelee kuwapongeza tena Tigo  na Clouds Media na kuwaomba mwakani msiache kuja tena kwenye mkoa wetu.

  Kwa upande wa burudani, ilianza kwa kumpata mshindi wa shindano la kusaka vipaji la Tigo Supa Nyota kwa kumuibua Msanii Single Baba atakayeiwakilisha Ruvuma kwenye fainali zitakazofanyika jijini Dar Es Salaam mwezi ujao.

  Shoo rasmi ilianza kwa Msanii Mesen Selekta kufuatiwa na Rubby huyu ni msanii aliyeibuliwa kwenye Supa Nyota miaka kadhaa iliyopita, kwa kweli ni msanii wa aina yake aliweza kuteka hisia za mashabiki kwa kuimba nyimbo tofauti tofauti zikiwemo Niwaze,Ntade, Na Yule,Forever na nyingine.

  Jumla ya wasanii kumi na mbili walipanda jukwaani wakiwemo Rostam, Weusi, Ruby, Mr. Blue, Barnaba, Zayd, Fid Q, Masen Selekta,  Lulu Diva,Chege, Foby ambao wasanii hao ndio watapanda kwenye jukwaa jumapili uwanja wa Nangw’anda Mtwara.

  Mdhamini mkuu wa msimu huu, kampuni ya Tigo imewakumbusha mashabiki wote wa muziki mjini Sumbawanga kufurahia promosheni zake tatu murwa katika msimu hii wa vibes. ‘Data Kama Lote inawapa wateja hadi mara mbili ya vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#. Hii itawawezesha wateja wa Tigo kufurahia msimu huu wa vibes kupitia mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+.

  Tigo pia inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Kwa Sumbawanga, tiketi zitakazonunuliwa kwa mfumo wa Tigo Pesa Masterpass QR zitagharimu TSH 5,000 pekee badala ya TSH 7,000 kwa watakaonunua kwa pesa taslim, Wateja wanapaswa kupiga *150*01#  na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.

  Wateja wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za kila wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya  http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia.

   Huu ni mwaka wa 17 wa tamasha la muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ambapo mwaka huu linashirikisha 100% wasanii wa nyumbani watakaozuru mikoa 15 ya nchi ikiwemo; Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Singida, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku kilele kikifanyika Dar es Salaam.  0 0

  Imeelezwa kuwa maboresho ya miundombinu ya skimu ya kilimo cha umwagiliaji ya Igomelo iliyopo wilayani Mbarali Mkoani Mbeya, imewanufaisha kwa namna mbalimbali wakulima wanaojishughulisha na kilimo cha mbogamboga. 

  Hayo yameelezwa jana na Mhandisi wa kanda ya Mbeya wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Elibariki Mwendo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea skimu hiyo.

  Mhandisi Mwendo alisema kuwa, Serikali imetumia kiasi cha shilingi Milioni mia mbili hamsini (250Milioni) kukarabati miundombinu ya skimu hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa banio kubwa linalotoa maji katika chanzo cha maji cha mto Mbarali na mifereji inayopeleka maji mashambani.

  “katika skimu hii wakulima wanajikita zaidi katika kilimo cha mbogamboga kama vile vitunguu, nyanya, matango, na hata zao la mpunga, ambapo kabla ya marekebisho na maboresho ya miundombinu hii, hali haikuwa nzuri kwani wakulima walikuwa wanajichotea maji kiholela ili kuweza kumwagilia mazao yao, lakini kwa sasa kama mnavyoona, maji yanakwenda moja kwa moja mashambani kwa utaratibu maalum ulivyopangwa ambapo kila mkulima ana zamu yake ya kuingiza maji mashambani tayari kwa kilimo, jambo ambalo limepelekea wakulima hawa kuongeza uzalishaji katika mazao wanayolima na kujiongeza pato la familia.” Alisisitiza Mhandisi Mwendo.

  Mmoja wa wakulima wanaojishughulisha na zao la kilimo cha vitunguu katika skimu hiyo Bw. Yohana Mbuna (52) amesema amekuwa akijishughulisha na kilimo katika skimu hiyo kwa takribani miaka ishirini sasa, “ Kabla ya maboresho katika skimu hii hali ilikuwa mbaya kwanza tulikuwa tunalima bila kufuata utaratibu, tulikuwa tunagombania maji na hata mavuno hayakuwa mengi kwa heka moja nilikuwa napata magunia 30 lakini kwa sasa kwa heka moja ninaweza kupata zaidi ya magunia 100 na hii hunisaidia kupata fedha za kusomesa watoto wangu, na ninalima vitunguu kama zao la biashara, pamoja na hilo mazao mengine ya chakula kama mpunga ninalima kwa ajili ya familia yangu.” Alisema Bw. Mbuna.


  Katika Picha Mhandisi Elibariki Mwendo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji akizungumza kuhusu maboresho yaliyofanywa katika banio (halipo pichani) lililopo katika chanzo cha maji cha mto Mbarali kinachopeleka maji katika skimu ya umwagiliaji ya Igomelo, nyuma pichani ni mto Mbarali.
  Bibi Victoria Kinyega akifanya kazi ya kuchambua vitunguu katika skimu ya umwagiliaji wa Igomelo.
  Vijana wanaofanya kazi katika shamba la vitunguu kwenye skimu ya Igomelo iliyopo Mbarali Mkoani Mbeya wakijaza vitunguu katika gunia maarufu kwa jina la net, tayari kwenda sokoni kuuzwa.
  Kulia Afisa Kilimo Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kanda ya Mbeya, Bw. Mnadi Taribo akimuelezea mgeni aliyetembelea shamba la mpunga katika skimu ya Umwagiliaji Igomelo, kuhusu teknolojia ya kisasa ya kilimo cha mpunga inayotumia kiasi kidogo cha maji, yaani kilimo shadidi.
  moja ya ghala la kuifadhia vitunguu linalotumiwa na wakulima katika skimu ya umwagiliaji ya Igomelo.
  Miundombinu inayopeleka maji katika mashamba ya mazao ya mbogamboga na mpunga katika skimu ya umwagiliaji ya Igomelo.  0 0

  Shirika la Hifadhi ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii NSSF ni kati ya Tasisisi za serikali iliyoshiriki kwenye maonyesho ya wiki ya Taifa ya Vijana yanayofanyika katika viwanja vya Tangamano wilaya ya Tanga mjini Mkoani Tanga ambapo wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye mpango wa hiari . 

  Kaimu meneja wa mkoa waTanga Bi Aisha Nyemba amesema kuwa katika maonyesho haya wananchi wote wanaotaka kujiunga kwa hiari na kujiwekea akiba wanaweza kufanya hivyo na kwamba NSSF itawatambua na kuweka katika rekodi za wananchama wapya. 

  “Ukija hapa katika banda letu utaweza kuandikishwa na kutambulika kwenye rekodi zetu hivyo ni fursa ya pekee kwa wananchama wapya kujiandikisha katika maonyesho haya”alisema bi Aisha. Bi Aisha amesema kuwa tangu maonyesho haya yaanze Oktoba 8 mwaka 2018 wananchi wengi wamejitokeza kujiandikisha na kupata elimu kuhusiana na umuhimu wa mafao ya NSSF na kuvutiwa hasa hasa katika eneo la matibabu bure. 

  Wananchi wanaojiandikisha kwenye mpango wa hiari ni wale waliopo kwenye sekta isiyo rasmi kama vile waendesha bodaboda,mama lishe, wajasiriamali na wengine wengi. 

  Maonyesho haya ya Taifa ya wiki ya vijana yaatafikia kilele oktoba 14 mwaka huu ambapo yataendana na sherehe za uzimaji wa mwenge kitaifa katika uwanja wa Mkwakwani.
  Kaimu meneja wa mkoa NSSF mkoa wa Tanga bi Aisha Nyemba akitoa maelekezo kwa mkazi wa Tanga ,Yahaya Katubu alipofika kwenye banda la NSSF,wakati wa maonesho  wiki ya vijana yanayofanyika katika viwanja vya Tangamano mkoani Tanga
  OFisa madai wa shirika la Taifa ya Hifadhi ya Jamii NSSF Athuman Bakari akitoa amelekezo kwa wananchi wa mkoa wa TANGA waliotembelea kwenye maonesho ya wiki ya kitaifa ya Vijana yanayofanyika katika viwanja vya Tangamano Tanga
  Ofisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF Bi Aisha Sango akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea katika banda la NSSF kwenye maonesho ya wiki ya Kitaifa ya Vijana inayofanyoka katika viwanja vya Tangamano mkoani TANGA
  Ofisa mikopo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF Athuman Bakari akitoa maelekezo kwa wananchi waliofika kwenye viwanja vya Tangamano yanapofanyika maonyesho ya wiki ya vijana.


  0 0   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiweka saini katika daftari la wageni baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), tayari kwa ziara ya kikazi jijini Arusha.Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Kilimanjaro,Mrakibu Msaidizi Zauda Mohamed na katikati ni Mkuu wa Kituo cha Polisi KIA,Mrakibu Msaidizi Abel Mgode
  PIX 2
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), tayari kuelekea jijini Arusha kwa ziara ya kikazi.Katikati ni Mkuu wa Kituo cha Polisi KIA, Mrakibu Msaidizi Abel Mgode na kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Kilimanjaro, Mrakibu Msaidizi Zauda Mohamed.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

  0 0

   Waziri Dkt. Kigwangalla na Waziri Prof. Kabudi wakiwa katika mkutano huo.
  IMG867
  Waziri Dkt. Kigwangalla na Waziri Prof. Kabudi wakiwa wakibadilishana mawazo na wadau wa masuala ya wanyama kwenye muda wa mijadala wakati wa mkutano huo
  IMG920
  Waziri Dkt. Kigwangalla akizungumza katika mkutano
  ………………………
  Na  Mwandishi Wetu, London
  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mawaziri wake Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla na Wazirri wa Katika na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi wameweza kuhutubia mkutano mkubwa na wa Kimataifa juu ya upigaji vita biashara haramu ya nyara, uliokuwa wa siku mbili Oktoba 11 na 12, 2018, Jijini London, Uingereza.

  Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla na Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi wamuwakilisha  Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano  huo wa Kimataifa  na kuandaliwa na Serikali ya Uingereza chini ya Uenyekiti wa Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William.

  Mwaka huu mkutano huo  ni wa Nne wa Ngazi ya juu kuhusu Biashara haramu ya nyara ambao huku ukiwakutanisha  viongozi wakuu wa nchi, mawaziri na wataalam kutoka zaidi ya nchi 60 Duniani pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali, wasomi na wafanyabiashara.

  Mkutano huo una lengo la kuimarisha jitahada zinazofanywa na Serikali mbalimbali duniani katika kupambana na kuzuia biashara haramu ya nyara.
  Mawaziri hao wa Tanzania kwa nyakati tofauti wameweza kusoma hotuba zao zenye malengo ya na jitihada za Serikali ya Tanzania katika uhifadhi wa Maliasili na kupambana na biashara haramu ya nyara hususani katika hifadhi zake za taifa na maeneo yote ya mapori ya hakiba sambamba na shoroba zilizopo.

  Imeelezwa kuwa, Tanzania ni moja ya nchi ambayo imetenga asilimia 32.5% ya eneo lake kwa ajili ya uhifadhi na inasifika kwa uwingi wa bayoanuai.
  Jitiada za kuzuia ujangili zimepelekea kupungua kwa ujangili kwa asilimia 50 na hii imejidhihirisha kwa kuongezeka kwa Tembo kutoka 43330 mwaka 2014 hadi kufikia tembo 59830 mwaka 2015. Kwa zaidi ya Asilimia 60
  Wakati akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Mkutano huo Prince William wa Uingereza alisifu jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika uhifadhi na upambanaji wa Biashara haramu ya nyara.

  Prince William alipongeza jitihada alizozishuhudia wakati wa ziara yake nchini Tanzania zikiwemo kutoka Elimu ya uhifadhi kwa wanafunzi pamoja na vyuo vizuri vya Elimu ya uhifadhi kikiwemo Chuo cha Elimu ya Uhifadhi wa Wanyamapori Mweka.

  Madhumuni ya mkutano huo ni kujenga ushirikiano baina ya nchi, taasisi binafsi na za kiserikali, NGOs na Wanataaluma, pia unalengo la kubadilishana uzoefu na mbinu za kupunguza mahitaji ya soko la nyara kwa nia ya kulifunga soko hilo duniani.

  0 0

   Mdhamini wa Chama cha Skauti Tanzania na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Skauti Mkuu Mhe. Mwantumu Mahiza ambaye amemtembelea nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es salaam kumwamkia na kujitambulisha leo Jumamosi Oktoba 13, 2018
   Mdhamini wa Chama cha Skauti Tanzania na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akimsikiliza Skauti Mkuu Mhe. Mwantumu Mahiza akimtambulisha wajumbe alioongozana nao nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam kumwamkia na kujitambulisha.
   Mdhamini wa Chama cha Skauti Tanzania na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akimsikiliza Skauti Mkuu Mhe. Mwantumu Mahiza akimtambulisha wajumbe alioongozana nao nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam kumwamkia na kujitambulisha.
   Mdhamini wa Chama cha Skauti Tanzania na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akipokea zawadi ya kigoda maalumu cha kuwekea Kurani Tukufu kutoka kwa  Skauti Mkuu Mhe. Mwantumu Mahiza ambaye amemtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam kumwamkia na kujitambulisha akiwa ujumbe wake. Wengine kutoka kushoto ni Kamishna Mkuu wa chama hicho Mhe. Abdulkarim Shah, Mjumbe wa Bodi ya Skauti Kennedy Ndosi, Kamishna Mtendaji wa chama hicho Eline Kitaly na Mjumbe wa Bodi ya Skauti Omar Ilyas.  
  Mdhamini wa Chama cha Skauti Tanzania na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na   Skauti Mkuu Mhe. Mwantumu Mahiza ambaye amemtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam kumwamkia na kujitambulisha akiwa ujumbe wake. Wengine  ni Kamishna Mkuu wa chama hicho Mhe. Abdulkarim Shah, Mjumbe wa Bodi ya Skauti Kennedy Ndosi, Kamishna Mtendaji wa chama hicho Eline Kitaly na Mjumbe wa Bodi ya Skauti Omar Ilyas. 

  0 0  Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Augustino Mrema(kushoto) akiongoza kikao cha kujadili Wafungwa waliopendekezwa kunufaika/kutonufaika katika mpango wa Parole. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike ambaye pia ni Katibu wa Sekretarieti ya Bodi ya Taifa ya Parole. Kikao hicho cha siku mbili  kimefanyika leo Oktoba 13, 2018, katika Bwalo la Gereza Kuu Isanga, Jijini Dodoma.
  PIX 2
  Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike ambaye pia ni Katibu wa Sekretarieti ya Bodi ya Taifa ya Parole akitoa taarifa fupi ya Sekretarieti  kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Augustino Mrema(kushoto meza kuu) katika kikao hicho.
  PIX 3
  Wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Parole wakipitia majalada ya wafungwa waliopendekezwa kunufaika/kutonufaika katika mpango wa Parole leo Oktoba 13, 2018 jijini Dodoma.
  PIX 4
  Sekretarieti wakifuatilia kwa makini majadiliano katika kikao hicho.
  PIX 5
  Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Augustino Mrema(kushoto) akiteta jambo na Katibu wa Bodi ya Taifa ya Parole ambaye pia ni Kamishna  Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike katika kikao hicho(Picha na Jeshi la Magereza
  ………………………..
  Na Lucas Mboje, Dodoma;
  Kikao cha 39 cha Bodi ya Taifa ya Parole kimeanza leo  Oktoba 13, 2018 chini ya Uenyekiti wa Mhe. Augustino Mrema katika Ukumbi wa Gereza Kuu Isanga, Jijini Dodoma.

  Kikao hiki cha siku mbili  kwa mujibu wa Sekretarieti ya Bodi ya Taifa ya Parole kitajadili Wafungwa waliopendekezwa kunufaika/kutokunufaika katika mpango wa Parole.Utaratibu huu wa Parole hapa nchini ni mojawapo ya adhabu mbadala wa kifungo ambao ni matokeo ya mfumo uliobuniwa na jamii katika nchi nyingi ikiwa ni njia mojawapo ya kupunguza ongezeko la wafungwa ndani ya magereza hivyo kuipunguzia Serikali na wananchi ambao ndio walipa kodi mzigo mkubwa wa kuwahudumia wafungwa wawapo magerezani.

  Lengo Kuu la Sheria ya Bodi ya Parole ya Mwaka 1994 ambayo ilifanyiwa marekebisho Mwaka 2002 ni kuweka masharti maalum kuhusu utaratibu wa urekebishaji wa wahalifu nje ya kuta za magereza baada ya Mfungwa kutumikia sehemu ya kifungo chake na kuonesha mwelekeo wa kurekebika unaokubalika kwa mujibu wa Sheria hii na Kanuni zake.

  Pamoja na utekelezaji wa Sheria hii hapa nchini  kumekuwepo  na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wake ikiwemo  ufinyu au wigo mdogo wa kisheria uliowekwa na Sheria yenyewe ambapo kutokana na wigo mdogo uliopo wa kisheria takwimu zilizopo zinaonesha kuwa wafungwa wengi hawawezi kujadiliwa kwa kuwa hawana sifa zinazotakiwa kwa mujibu wa Sheria iliyopo.

  Kwa mujibu wa Sheria hiyo mfungwa anayestahili kunufaika na mpango wa Parole ni yule anayetumikia kifungo cha miaka minne(4) na kuendelea na awe ametumikia theluthi moja (1/3) ya kifungo chake na kuonesha mwelekeo wa kurekebika unaokubalika kwa mujibu wa Sheria hii na Kanuni zake.

  Hiki ni Kikao cha 5  kufanyika chini ya Uenyekiti wa Mhe. Augustino Mrema  tangu ateuliwe na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli  kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Julai 16, 2016.

  0 0

   Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akisalimiana na Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Cameroon na vilabu vya Barcelona, Chelsia na Intermilan ambaye sasa anakipiga katika Klabu ya FC Qatar, Samuel Etoo, aliyemtembelea leo ofisini kwake, Masaki jijini Dar es salaam. 
   Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Cameroon na vilabu vya Barcelona, Chelsia na Intermilan ambaye sasa anakipiga katika Klabu ya FC Qatar, Samuel Etoo, aliyemtembelea leo ofisini kwake, Masaki jijini Dar es salaam. 
   Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi yenye jina la Mchezaji huyo ambaye pia ni Balozi wa Bia ya Castle Lager, Samuel Etoo, aliyemtembelea leo ofisini kwake, Masaki jijini Dar es salaam.

  Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akipeana mkono na Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Cameroon na vilabu vya Barcelona, Chelsia na Intermilan ambaye sasa anakipiga katika Klabu ya FC Qatar, Samuel Etoo, aliyemtembelea leo ofisini kwake, Masaki jijini Dar es salaam. 
   Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Cameroon na vilabu vya Barcelona, Chelsie na Intermilan ambaye sasa anakipiga katika Klabu ya FC Qatar, Samuel Etoo (kulia kwake)  na Balozi wa Bia ya Castle Lager hapa nchini, Ivo Mapunda (kushoto kwake), pamoja na ukumbe walioambayana nao. 
   Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akikiwa ameambatana na Mgeni wake Mchezaji Samuel Etoo na ujumbe wake wakati akiwasindikiza baada ya mazungumzo yao leo ofisini kwake, Masaki jijini Dar es salaam. 
   Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiagana na Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Cameroon na vilabu vya Barcelona, Chelsia na Intermilan ambaye sasa anakipiga katika Klabu ya FC Qatar, Samuel Etoo, aliyemtembelea leo ofisini kwake, Masaki jijini Dar es salaam. 
  Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Msanii Dokii kwa Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Cameroon na vilabu vya Barcelona, Chelsie na Intermilan ambaye sasa anakipiga katika Klabu ya FC Qatar, Samuel Etoo, aliyemtembelea leo ofisini kwake, Masaki jijini Dar es salaam. 

  0 0


  Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akikagua mfereji wa maji wa Mkombozi na Mboliboli Tarafa ya Pawaga Mkoani Iringa kwa ajili ya umwagiliaji wa mashamba ya mpunga katika ziara ya kikazi ya kukagua hali ya upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya Nyanda za juu kusini Jana tarehe 12 Octoba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
  Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akikagua mashamba ya mpunga alipotembelea Tarafa ya Pawaga Mkoani Iringa katika ziara ya kikazi ya kukagua hali ya upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya Nyanda za juu kusini jana tarehe 12 Octoba 2018.
  Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Iringa kukagua hali ya upatikanaji wa mbolea kuelekea msimu wa kilimo wa mwaka 2018/2019.


  Na Mathias Canal-WK, Iringa


  Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba amewaagiza wataalamu wa umwagiliaji kuzuru Tarafa ya Pawaga ili kutembelea na kukagua mfereji wa maji wa Mkombozi na Mboliboli Tarafa ya Pawaga ili kuanzisha skimu ya umwagiliaji.


  Waziri Tizeba ametoa agizo hilo Jana tarehe 13 Octoba 2018 wakati alipotembela eneo la mashamba ya mpunga wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Iringa ya kukagua hali ya upatikanaji wa mbolea katika mikoa ya Nyanda za juu kusini.


  Alisema kuwa mfereji huo unaohudumia wakulima wa mpunga katika vijiji vya mboliboli, Usolanga, Mbugani na Mkumbwani unapaswa kuwekewa mkakati wa haraka ili kujengwa skimu ya umwagiliaji kwa ajili ya mashamba ya wakulima yanayotajwa kuwa na ukubwa wa hekari 11,000.


  "Kwa bahati nzuri Tume ya umwagiliaji sasa rasmi imehamishiwa kwangu haina hata siku tano nitawasimamia kweli kweli ili kuwa na matokeo makubwa na ya haraka kwenye kilimo ambacho ndicho mkombozi wa mkulima" Alikaririwa Dkt Tizeba


  Aidha, aliwashauri wakulima katika Tarafa hiyo ya Pawaga kuingia katika kilimo cha pamoja ili pindi wanapovuna waweza kuuza kwa pamoja jambo litakalowafanya kuwa na maamuzi ya kupanga bei waitakayo ya Mazao.


  Waziri Tizeba ameitaka Tume ya umwagiliaji kufanya uhakiki wa maeneo yote ya mashamba hayo ya wakulima kwa kuyapima kabla ya kuingia katika kilimo cha pamoja ikiwa ni pamoja na kuainisha gharama za ukamilifu wa mfereji huo wa Mkombozi na Mboliboli.


  Alisema kuwa faida ya kulima kwa pamoja wakulima wanapata fursa ya kukopeshwa kirahisi na Mabenki kuliko kufanya kuomba mkopo kwa mkulima mmoja mmoja kwani masharti yake yanakuwa magumu zaidi. 


  Kadhalika, Waziri Tizeba amemuagiza Mshauri wa Kilimo wa Mkoa wa Iringa Bi Grace Macha kuanisha uhitaji wa mbegu katika Mkoa huo ili taarifa zitolewe haraka kwa Wakala wa Taifa wa Mbegu (ASA) ili waweze kutoa mbegu punde msimu unapoanza.


  0 0


  Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora Janath Kayanda akitoa maelezo ya awali kabla ya ufunguzi wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa huo jana cha kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora Hassan Wakasuvi akifungua Kikao maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa huo jana cha kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ( wa pili kutoka kulia) akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi jana katika Kikao maalumu cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Tabora.
  Baadhi ya Wajumbe wa Hamashauri Kuu ya Cahama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora wakiwa katika kikao maalumu jana kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
  Mbunge wa Urambo Margaret Sitta akiomba ufafanuzi jana wakati kikao maalumu jana Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora cha kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Haruna Kasele akitoa maoni yake jana wakati kikao maalumu jana cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora cha kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.


  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora-Uyui Saidi Ntahondi akitoa maoni yake jana wakati kikao maalumu jana cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora cha kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM. picha na Tiganya Vincent

  ……………………………….

  NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA

  HALMASHAURI kuu ya CCM Mkoa wa Tabora imeipongeza Serikali ya Awamu ya tano kutokana na kutekeleza kwa vitendo Ilani yake ya miaka mitano tangu ulipofanyika uchaguzi Mkuu uliopita mwaka 2015 hadi sasa.

  Pongezi hizo zimetolewa jana kwenye kikao maalumu cha wajumbe wa Halmashauri hiyo iliyokutana kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kutoka serikali ya Mkoa wa Tabora.

  Wajumbe hao walisema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dokta John Pombe Magufuli iliahidi miradi mbalimbali kwa wakazi wa Mkoa huo ikiwemo ya maji, afya, barabara na kilimo ambapo utekelezaji wake unaonekana kwa macho. Waliitaja miradi ambayo utekelezaji wake umeanza na unaendelea kwa kasi mkoani humo kuwa ni wa maji kutoka ziwa Victoria kwa ajili ya wakazi wa Wilaya za Nzega, Tabora na Igunga.

  Miradi mingine ni ujenzi wa barabara za kiwango cha lami kuunganisha Mkoa huo na mikoa jirani ambapo ujenzi unaendelea. Katika hatua nyingine wajumbe hao wamezitaka Halmashauri za wilaya mkoani humo kuhakikisha kiasi cha fedha inachotenga kutokana na mapato ya ndani kwa ajili ya vijana, akinamama, walemavu na ile ya miradi ya Maendeleo zinatumika kama ilivyokusudiwa.

  Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Ccm Mkoa Hassan Wakasuvi alisema kuwa asilimia kumi ya mapato ya ndani inayotengwa na kila Halmashauri kwa ajili ya makundi hayo ziwafikie walengwa bila kuwa na riba. Alizitaka Halmashauri hizo kuweka utaratibu wa kupitia vikundi vyote vinavyopewa fedha hizo ili iweze kuvisaidia kukuza mitaji yao na waweze kuzirejesha zinufaishe wengine.

  Aidha kikao hicho kiliwaagiza wajumbe wa Hamashauri kuu wa kila Wilaya kutembelea na kukagua miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yao kutokana na fedha zinazotokana na asilimia 40 ya mapato ya ndani ya kila wilaya. Hatua ilifikiwa baada ya kubainika baadhi ya Halamashuri za Wilaya zimekuwa zikiandika kwenye makaratasi kuwa zimetenga fedha zilizotokana na mapato ya ndani kwa ajili ya miradi lakini hakuna kitu kilichofanyika

  0 0


  Na. WFM, Bali Indonesia

  Nchi za Afrika ikiwemo Tanzania zinatakiwa kuwekeza kwa kiasi kikubwa kwenye maarifa na elimu ili kuendana na soko la ushindani linaloendelea kwa kasi Duniani

  Hayo yalibainishwa na Waziri wa Fedha na Mipango ambaye pia ni mwakilishi wa Tanzania katika Bodi ya Magavana wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Dkt. Philip Isdor Mpango, wakati wa mikutano ya WB na IMF mjini Bali Indonesia.

  Dkt. Mpango alisema kuwa, katika mikutano hiyo ya Kimataifa yapo mambo ambayo Tanzania inatakiwa kuyafanyia kazi wakati huu ambao inapiga hatua kuelekea katika uchumi wa kati unaotegemea viwanda ambapo elimu inayotolewa inatakiwa kujikita katika kukuza maarifa na ujuzi .

  “Wakati suala la teknolojia likiangaziwa katika bara la Afrika ni vema kuangalia pia namna ya kukabiliana na changamoto zinazotokana na teknolojia hiyo kwa kuwa katika maeneo mengi ajira za watu zimepungua kutokana na mashine kuchukua nafasi za watu”, alisema Dkt. Mpango.

  Alisema mikutano ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa imekua na umuhimu mkubwa kwa kuwa wadau wamebadilishana mawazo ambayo yamelenga kukabiliana na changamoto za kiuchumi ambazo zimeendelea kutokea Duniani ikiwa ni pamoja na baadhi ya nchi kuwa juu kiuchumi na nyingine kuendelea kuporomoka kwa kasi. 

  Katika mikutano hiyo Tanzania imetajwa kuwa uchumi wake unaendelea kuimarika ambapo kwa sasa unakua kwa takribani asilimia sita hivyo kuwa mfano wa kuigwa barani Afrika na Dunia kwa ujumla.

  Wajumbe wa mikutano hiyo wametakiwa pia kukabiliana na suala la mabadiliko ya tabia nchi katika nchi zao kwa kuwa yanaathari kubwa katika uchumi hasa katika Sekta ya afya kutokana na kuongezeka kwa magonjwa lakini pia mafuriko na ukame.

  Naye Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Rubuka, alisema kuwa suala la amani duniani limejadiliwa kwa kina katika mikutano hiyo kwa kuwa ni chachu ya maendeleo si tu ya kiuchumi lakini pia ya kijamii.

  Mikutano ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa inaendelea Mjini Bali Indonesia, ambapo imewakutanisha Mawaziri, Magavana na wadau wa masuala ya Fedha na Uchumi kutoka nchini mbalimbali duniani.

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  Wizara ya Fedha na Mipango
  Mjini Bali Indonesia

  Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Benki ya Dunia (WB,) anayewakilisha Afrika (Africa group 1 constituency), Bi. Anne Kabagambe, wakati wa mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayoelendelea mjini Bali Indonesia, kushoto kwake ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).
  Wajumbe wa Benki ya Dunia (WB) kundi la Afrika (Africa group 1 constituency), wakiwa katika Mkutano Mjini Bali Indonesia.
  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) wa pili kulia, akijadili jambo na Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga wakati wa mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoelendelea mjini Bali Indonesia.
  Waziri wa Fedha na Mipango ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Ushauri wa Masuala ya Fedha wa Benki ya Dunia- WB kwa nchi za Afrika (Africa group 1 constituency) Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akisoma ujumbe wa nchi hizo, wakati wa mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoelendelea mjini Bali Indonesia (kushoto ) ni  na Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango Mjini Bali Indonesia)

  0 0

   Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile (wa pili kushoto), akimkabidhi kadi ya matibabu Mwanamuziki Mkongwe, Mzee Makassy jijini Dar es Salaam leo wakati wa mkutano wa fursa kwa Wanaumoja wa Muziki Tanzania (TAMUFO) ambapo pia alitoa kadi za matibabu za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa wanamuziki mbalimbali kupitia Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NNSF). Kutoka kushoto ni  Rais TAMUFO, Dk.Donald Kisanga, na Mlezi wa TAMUFO , Mhandisi Juliana Pallangyo .
   Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile (wa pili kushoto), akimkabidhi kadi ya matibabu Mwanamuziki, Kikumbi Mwanza Mpango 'King Kiki.

   Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile (wa pili kushoto), akimkabidhi kadi, Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stellah Joel.   Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile (wa pili kushoto), akimkabidhi kadi, Mkurugenzi Mtendaji wa Bendi ya African Stars (Twanga Pepeta), Asha Baraka.
   Wadau wa muziki wakiwa katika mkutano huo.
   Mkutano ukiendelea.
   Mshereheshaji MC wa mkutano huo akiwa katika vazi la Kinaigeria.

   Wadau wa mkutano.
   Ofisa Mkuu Mwandamizi Kitengo cha Sekta Isiyo Rasmi kutoka NNSF, Abbas Cothema, akitoa mada.
   Meza kuu.
   Mwanamuziki Salim Mohamed Zahoro akizungumza.
   Mzee Makassy akizungumza.
   Mwanamuziki King Kiki, akizungumza.
   Mlezi wa TAMUFO, Mhandisi Dk. Juliana Pallangyo, akiteta jambo na wadau wa muziki.
   Wanamuziki wakiserebuka wakati wakimkaribisha Mhe.Ndugulile kuzungumza nao.

   Katibu Mkuu wa TAMUFO, Stellah Joel, akizungumza.
   Rais wa TAMUFO, Dk.Donald Kisanga, akizungumza.
   Wadau wa muziki wakiwa kwenye mkutano huo.

  Mkaguzi wa Jeshi la Polisi, Dk. Ezekiel Kyogo akitoa mada kwenye mkutano huo.
   Waimbaji wa Kwaya ya Sayuni wakiwa kwenye mkutano huo.
   Maombi yakifanyika.
   Mheshimiwa Ndugulile, akizungumza na wanamuzi hao.
   Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile, akimkabidhi kadi, Maria Joseph.

  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile, akimkabidhi kadi,  Hellen Makundi.

   Kadi zikiendelea kutolewa.
   Mhe.Ndugulile, akipiga picha na viongozi wa TAMUFO.
   Mhe.Ndugulile, akimkabidhi kadi mwanamuziki wa Injili, Boniface Mwaitege.
   Picha ya pamoja.

  Na Dotto Mwaibale

  WASANII wametakiwa kutumia sanaa yao kutoa elimu ili jamii iachane na vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vimeshamiri nchini.

  Mwito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile Dar es Salaam leo wakati akizungumza katika mkutano wa fursa kwa Wanaumoja wa Muziki Tanzania (TAMUFO) ambapo pia alitoa kadi za matibabu za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kupitia Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NNSF).


  "Siku hizi kumekuwa na matukio mengi ya ukatili wa kijinsia ukihusisha masuala ya mapenzi na mambo mengine tuna waomba ninyi wasanii kupitia sanaa yenu tungeni nyimbo zitakazotoa elimu ya jamii kuachana na vitendo hivyo" alisema Ndugulile.

  Alisema Serikali inatambua TAMUFO na ndio maana amefika kushiriki nao katika mkutano huo kutokana na mchango mkubwa wa wanamuziki katika taifa letu.

  Alisema sanaa ni ajira na kuwa inachangia pato la taifa kutokana na kodi wanaliyolipa. 

  Aliongeza kuwa wajibu wa serikali ni kuhakikisha kila mtu anakuwa na afya bora wakiwemo wanamuziki na katika kutekeleza hilo inajenga vituo vya afya 67 katika kila wilaya na kuwa bajeti yake imepanda kutoka sh.bilioni 31 hadi kufikia sh.bilioni 270 kwa mwaka huu wa fedha wa 2017/2018 na kuwa mpango wa serikali ni kila mtanzania kuwa na kadi ya NHIF.

   Rais wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO), Dk.Donald Kisanga alisema mkutano huo ni muhimu kwao kwa kuwa unawahamasisha wanamuziki kujiunga na mfuko huo wa bima ya afya wakiwa na lengo la kuwasaidia pale wanapoumwa waweze kutibiwa tofauti na ilivyo sasa .

  Akitoa mada kwenye mkutano huo Ofisa Mkuu Mwandamizi Kitengo cha Sekta Isiyo Rasmi kutoka NNSF, Abbas Cothema alisema ni muhimu kwa wanamuziki kujiunga na mfuko huo ambao ni mkombozi kwao siku za usoni.

  Alisema kupitia NSSF wameweza kuwaunganisha wanamziki kadhaa na NHIF ambapo walikuwa wakikabidhiwa kadi zao za matibabu.


  Mkaguzi wa Jeshi la Polisi, Dk. Ezekiel Kyogo akitoa mada kwenye mkutano huo alisema ni muhimu kwa wanamuziki kuzijua sheria na kuwepo uzimamizi mzuri wa sheria hizo ili kulinda kazi za wasanii ili ikitokea mtu yeyote kuzikiuka akamatwe na sheria ichukue mkondo wake. 

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wakiungana na waumini wengine katika Ibada Maalumu ya kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Oktoba 14, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wakitoa sadaka walipoungana na waumini wengine katika Ibada Maalumu ya kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Oktoba
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinunua Rosari baada ya kuhudhuria Ibada Maalumu ya kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Oktoba 14, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wakiwa na Mama Maria Nyerere na mwanae Makongoro Nyerere walipomtembelea nyumbani kwao Msasani jijini Dar es salaam baada ya kungana na waumini katika Misa Maalumu kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Oktoba 14, 2018

     
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mjane wa Baba Taifa, Mama Maria Nyerere, aliyemtembelea nyumbani kwake Msasani baada ya kutoka katika Ibada Maalumu ya kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Oktoba 14, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wakiwa na Mama Maria Nyerere walipomtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam baada yakuhudhuria Misa Maalumu kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Oktoba 14, 2018
   
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wakisindikizwa na Mama Maria Nyerere pamoja na mwanae Makongoro Nyerere na wajukuu wake walipomtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam baada yakuhudhuria Misa Maalumu kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Oktoba 14, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na aliyekuwa Katibu Myeka wa Mwalimu Nyerere, Mzee Masoi wakati yeye na mkewe mama Janeth Magufuli walipomtembelea Mama Maria Nyerere Mzee Samwel Kasori nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam baada yakuhudhuria Misa Maalumu kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Oktoba 14, 2018

  PICHA NA IKULU

  0 0


  Katibu Mkuu Shirika la HHRD la Marekani Ayoub Mohd akimkabidhi hati ya mkabidhiano ya vifaa vilivyotolewa na Shirika hilo katika hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja, Mjini Zanzibar.
  Meneja Mkaazi wa Shirika la HHRD Ofisi ya Nairobi Musa Ibrahim akieleza kuridhishwa na watendaji wanpopkea misaada wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya Hospitali iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja.
  Katibu Mkuu Shirika la HHRD Ayoub Mohd akizungumza baada ya kumkabidhi Waziri wa Afya msaada wa vifaa vilivyotolewa na Shirika hilo katika hafla iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
  Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akitoa shukrani zake kwa Shirika la HHRD kwa msaada waliotoa kwa ajili ya wananchi wa Zanzibar.
  Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akimkabidhi mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu Zanzibar Haidar Hassan Madoea moja ya baskeli zilizotolewa msaada na Shirika la HHRD .Picha na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar

  ………………………..

  Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar

  Msaada wa Dawa na Vifaa Tiba unaotolewa na wafadhili mbali mbali unaweza kupunguza matumizi ya Serikali yaliyopangwa katika bajeti ya mwaka 2018/19 iwapo Wafanyakazi wa Wizara ya Afya watachukua juhudi ya kuilinda na kuitunza misaada hiyo.

  Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed alieleza hayo Ofisini kwake Mnazimmoja wakati wa hafla ya kupokea msaada wa vifaa tiba na vitendea kazi vya Hospitali kutoka Shirika linalotoa misaada ya Kijamii la Marekani la HHRD kupitia Jumuiya ya Muzdalifa ya Zanzibar.

  Alisema Serikali inaendeleza mashirikiano na Mashirika na Taasisi za ndani na nje ya nchi ili kuona huduma za Afya zinaimarika na wananchi wanapata huduma bila usumbufu. Waziri Hamad alilipongeza Shirika la HHRD kwa msaada huo na kulishauri kuangalia uwezekano wa kusaidia zaidi katika maeneo ya mama na mtoto na kuwapatia mafunzo wafanyakazi wa Hospitali.

  Alikumbusha kuwa pamoja na misaada inayotolewa na wafadhili, Serikali imeweka Bajeti ya kutosha kwa ajili ya dawa na amewataka wafanyakazi wanaosimamia uagiziaji wa dawa kuwa waangalifu kuepuka kununua dawa ambazo zipo kwa wingi katika Hospitali na vituo vya afya.

  Amewashauri watendaji hao kuangalia maeneo ambayo yanaupungufu wa dawa na mahitaji yake ni makubwa na kuepuka kuingiza dawa ambazo matumizi yake ni madogo na hatimae kuharibika. Meneja Mkaazi wa Shirika la HHRD Ofisi ya Nairobi Musa Ibrahim alieleza kuridhishwa na uwajibikaji wa Serikali wanapoleta misaada kwa kusimamia na kuhakikisha inafika kwa waliokusudiwa.

  Alisema kutokana na uaminifu na juhudi zinazochukuliwa na watendaji mbali mbali wanakusudia kuongeza misaada mengine yenye lengo la kupunguza matatizo katika jamii. Katibu Mkuu wa Muzdalifa Sheikh Farouk Hamad Khamis alisema Taasisis hiyo itaendelea kufanya juhudi ya kutafuta mashirika yenye nia ya kutoa misaada ya kibinadamu isiyokuwa na masharti ili kuwapatia wanaoihitaji.

  Amewahakikisha wananchi kuwa msaada hasa wa dawa na chakula unaotolewa na Taasisi hiyo Uko salama kwa ajili ya matumizi ya binadamu hivyo wasiwe na shaka kuitumia. Katibu Mkuu wa HHRD Ayoub Mohd alimkabidhi Waziri wa Afya msaada wa mafriji matano ya kuhifadhia damu, vigari vya walemavu 17, gloves boksi 20, mipira ya wazazi boksi 20 na vyakula vya lishe kwa ajili ya watoto vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi 33 milioni.

  0 0

  Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wakulima wa Pareto katika kijiji cha Ikanga kilichopo kata ya Mdabulo Wilayani Mufindi kwenye mkutano wa hadhara akiwa katika muendelezo wa ziara ya kikazi Mkoani Iringa, Jana tarehe 13 Octoba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)
  Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akikagua shamba la Pareto la mkulima Bahati Mhapa, katika kijiji cha Ikanga Wilayani Mufindi kwenye mkutano wa hadhara akiwa katika muendelezo wa ziara ya kikazi Mkoani Iringa, Jana tarehe 13 Octoba 2018. 
  Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza na wakulima wa Pareto katika kijiji cha Ikanga kilichopo kata ya Mdabulo Wilayani Mufindi kwenye mkutano wa hadhara akiwa katika muendelezo wa ziara ya kikazi Mkoani Iringa, Jana tarehe 13 Octoba 2018. 
  Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akikagua kiwanda cha Pareto Mafinga (PCT) kilichopo mamlaka ya Mji wa Mafinga wakati akiwa katika muendelezo wa ziara ya kikazi Mkoani Iringa, Jana tarehe 13 Octoba 2018.   Na Mathias Canal-WK, Mufindi-Iringa


  Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) amewataka wakulima wa Pareto kote nchini kujiunga na mfumo rasmi wa vyama vya msingi vya ushirika.

  Dkt Tizeba ametoa Mwito huo Jana tarehe 13 Octoba 2018 wakati akizungumza na wakulima wa Pareto katika kijiji cha Ikanga kilichopo kata ya Mdabulo Wilayani Mufindi kwenye mkutano wa hadhara akiwa katika muendelezo wa ziara ya kikazi Mkoani Iringa.

  Alisema kuwa ushirika ni dhana ya kuleta maendeleo kwa kushirikiana ambapo dhana hiyo imefanikiwa kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kijamii katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita. 

  “Kutokana na changamoto mbalimbali zilizoikumba sekta hii ya ushirika watu wengi wamekosa imani na vyama hivi na baadhi ya vyama vimeshindwa kufanya kazi vizuri hivyo nawahakikishia serikali inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli imerejesha nidhamu kwenye ushirika” Alikaririwa Dkt Tizeba na kuongeza kuwa

  Alisema kuwa Ushirika maana yake ni muungano wa watu ambao wanafanya kazi pamoja kwa hiari ili kufanikisha mahitaji yao ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni kupitia shughuli ya biashara inayomilikiwa kwa pamoja na kudhibitiwa kidemokrasia. Ushirika unazingatia maadili ya kujisaidia wenyewe, jukumu binafsi, demokrasia, usawa na mshikamano.

  Wanachama wa Ushirika wanaamini katika misingi ya uaminifu, uwazi, uwajibikaji kwa jamii na kuwajali wengine. Muundo wa Ushirika kwa ujumla unategemea uimara wa chama cha msingi cha Ushirika, hivyo kuna umuhimu wa kuhakikisha vyama imara vya msingi vinaanzishwa.

  Wakulima wa Pareto katika Mikoa ya Nyanda za juu Kusini na maeneo yote nchini wanapaswa kulima kwa wingi zao hilo ili waweze kuinua kipato chao na kuondokana na umaskini kutokana na kuwepo kwa uhakika wa soko la zao hilo.Aidha, Waziri Tizeba amesimamisha utendaji kazi wa Wakala wa ununuzi wa Pareto Wilayani Mufindi Ndg Nilbet Kabonge badala yake amemtaka mwenyekiti wa kijiji kuitisha mkutano wa kijiji ili kuchagua wakala mwingine atakayesimamia maslahi ya wakulima.

  “ Tena Mkurugenzi wa Halmashauri unapaswa kuhakikisha kuwa unanunua mzani maalumu kwa ajili ya kupima ubora wa zao la Pareto kwani kufanya hivyo kutaondoa udanganyifu wa muda mrefu kwenye zao hili” Alisema

  Kadhalika, aliutaka uongozi wa Wilaya ya Mufindi na uongozi wa Mkoa wa Iringa kusimamia ipasavyo upimaji wa ubora wa zao la Pareto ili kuepusha wizi na udanganyifu kwa wakulima wanaouza Pareto yao kupitia mawakala wenye vipimo ambavyo havijathibitishwa na wakala wa vipimo nchini.

  Pareto ni moja kati ya zao ambalo hulimwa Tanzania, na huwa ni zao jamii ya ua ambalo hutumika kutengenezea dawa za kuuwa wadudu shambani (insecticide) hujulikana kama pyrethtin.

  0 0
 • 10/14/18--01:52: Article 4

older | 1 | .... | 1696 | 1697 | (Page 1698) | 1699 | 1700 | .... | 1898 | newer