Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1695 | 1696 | (Page 1697) | 1698 | 1699 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Muwakilishi wa Tasisi ya Msichana Initiative, Eugine Shao, akizungumza na waandishi wa habari umuhimu wa kuhadhimisha siku ya Msichana Duniani na Malengo ya Tasisi yao katika kumlinda Mtoto wa Kike hili aweze kufikia malengo sanjari na kupata elimu.
   Mourine Richard Kutoka Tasisi ya Her Initiative akizungumza umuhimu wa Mtoto wa kike kujiamini na kuwataka wanaume kuondoa dhana ya kuwanyanyapaa Wanawake kwa umri.
   Dada Viola akitoa mada kwa wasichana waliohudhuria kongamano katika kuadhimisha siku ya Msichana Duniani kwa kuwataka waweze kujiamini.
   Mmoja wa wadau walioshiriki katika Kongamano la siku ya Msichana Duniani lililofanyika katika Ukumbi wa Nafasi Art Space jijini Dar es Salaam
  Baadhi ya Wasichana walioshiriki katika Kongamano siku ya Msichana Duniani katika Ukumbi wa Nafasi Arts Space.
  --

  0 0
 • 10/11/18--23:00: Article 1
 • Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto, Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la kitaifa la ustawi wa Jamii ,katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi.
  Baadhi ya Washiriki wa Kongamano hilo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa kongamano la kitaifa la ustawi wa Jamii.
  Mwenyekiti wa Chama cha Wataalamu wa Ustawi wa Jamii Tanzania (TASWO) ,Zena Mabeyo akizungumza wakati wa kongamano hilo.
  Baadhi ya Washiriki katika kongamano hilo.
  Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto, Ummy Mwalimu ,akiteta jambo na Kamishna wa Ustawi wa Jamii nchini Dkt Naftali Ng’ondi wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo.
  Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto, Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo lililofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi .


  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini ,Moshi

  Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto, Ummy Mwalimu amesema kukamilika kwa mchakato wa sheria ya kusimamia kada ya maafisa ustawi wa jamii nchini itasaidai kurudisha hadhi na heshima kwa kada hiyo likiwemo suala la maadili pamoja na utendaji kazi.

  Waziri Mwalimu  amesema kukosekana kwa sheria hiyo kumepelekea baadhi ya maafisa ustawi wa jamii kukosa uadilifu ikiwemo kujihusisha katika vitendo vya rushwa pamoja na kushindwa kutoa haki kwa usawa.

  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa  kungamano la Kitaifa la ustawi wa jamii, lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hospitali ya rufaa ya KCMC Mjini Moshi, amesema kupatikana kwa sheria hiyo pia kutawezesha ufutaji wa leseni kwa wale watakaoenda kinyume na sheria..

  Katika Kongamano hilo lililobeba kauli mbiu ya mchango wa taaluma ya ustawi wa jamii katika kuelekea uchumi wa viwanda na maendleo endelevu,Waziri Mwalimu alisema sheria hiyo itajumuisha suala la usajili wa kwa maafisa ustawi wa jamii ili kusimamia maadili na weledi katika kazi zao .

   Alisema kuwa wapo baadhi ya wananchi wenye kipato cha chini wameshindwa kufika katika ofisi za ustawi ngazi za Halmashauri kwa sababu imeshajengeka dhana kuwa mwenye fedha ndiye anaesikilizwa na kupewa haki.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha wataalamu wa ustawi wa jamii Tanzania (TASWO) ,Zena Mabeyo amesema kuwa kuwepo kwa chombo maalumu kwa ajili ya kada hiyo kitakuwa na nafasi kubwa katika kusimamia masuala mazima ya maadili na kuchukua hatua kwa wasiofuata sheria.

  Naye Kamishna wa ustawi wa jamii nchini Dkt Naftali Ng’ondi amesema ni muhimu uwepo wa sheria mahsusi itasaidia kuchukua hatua kwa baadhi ya watendaji wanaofanya kazi za ustawi wa jamii huku wakiwa hawajasomea taaluma hiyo.

  0 0
  HAKUNA kuchelewesha pale mtu anapotupia ubashiri wake na SportPesa anaingia kwenye Droo ya bajaj Re na unapopigiwa simu ya ushindi kuwa umeshinda bajaj utapelekewa mpaka ulipo bila kutoa hata shilingi.

  Ni kwa wakati Mwingine Tena SportPesa inamkabidhi mshindi wa Droo ya saba ya Shinda zaidi na SportPesa bajaj yake huyu ni Magita Mbwega kutoka Kahama aliipokea timu ya ushindi ikiwa na Mzigo wake mpya wa bajaj ilioupeleka mpaka nyumbani kwake.

  Mbwega anasema aliweka ubashiri wa shilingi elfu moja pekee na baada ya mechi akashinda shilingi elfu tano lakini habari njema kwake ilikuwa kupokea simu kutoka SportPesa kuwa ameshinda bajaj, Anadai kuwa wakati ameambiwa ameshinda hakuamini kabisa mpaka alipoona timu imefika nyumbani kwake.

  shindi huyu wa droo ya Saba ambaye ni mjasiriamali wa kuuza nafaka anaeleza kuwa ili kubashiri sio lazima uwe maskini wala Tajiri bali hii ni Fursa kwa kila mtanzania.

  "Unajua jambo ambalo nimejifunza tangu nimeanza kucheza na SportPesa ni kwamba mchezo huu hauchagui maskini wala tajiri mimi nina biashara yangu lakini bado kupitia ubashiri na Sportpesa ninaongeza kila siku mtaji wangu pale naposhinda ubashiri lakini mbali ya hilo leo nimeshinda bajaji naenda kuongeza tena mtaji wangu na pesa nyingine ntakayopata kupitia bajaj hii itaingia kwenye matumizi ya ujenzi wa nyumba yangu nyingine". Alisema Mbwega.

  Kwa upande wake mke wa Bwna Mbwega alisema kwake anaona kama neema Ya Mungu imewashukia kutokana na ushindi huo mkubwa kutoka SportPesa huku akiamini baadhi ya changamoto ambazo walishindwa kuzitatua kutokana labda na wingi wa majukumu zitatatuliwa na kipato kitachotokana na bajaj hiyo.

  Huu ndio Mchongo wa Maana hivi sasa kwa watanzania kwani kwa kutumia simu Yeyote ya Mkononi unaweza piga *150*87# ukajisajili na SportPesa na kuanza kucheza , au unaweza kucheza kupitia tovuti yani www.sportpesa.co.tz kumbuka kuweka pesa kuanzia buku au zaidi ili uanze kucheza namba ya kampuni ni 150888 na kumbukumbu namba ni 888 kumbuka kucheza mara nyingi ndio kuongeza nafasi ya kushinda bajaj.

  0 0


  Mkurugenzi na Mmiliki wa eneo la uwekezaji la Kilua lililopo Kijiji cha Disunyala Kata ya Kilangalanga Mlandizi Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani Bw.Mohammed Kilua (aliyesimama) akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa huduma kwa wawekezaji wa TIC Bw.Ayoub Sizya (aliyekaa kushoto kwake), wengine ni baadhi ya walioonyesha nia ya kuwekeza viwanda kwenye eneo hilo lenye ekari 1,000.

  Mkurugenzi na Mmiliki wa eneo la Kilua la ukanda wa uwekezaji wa viwanda lenye ekari elfu moja lililopo Kijiji cha Disunyala Kata ya Kilangalanga Mlandizi Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani Bw.Mohammed Kilua akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na kulikabidhi eneo hilo kwa kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC kwa ajili ya kuvutia wawekezaji,TIC imechukua eneo hilo na kuwataka wawekezaji kujitokeza kujenga viwanda. Picha na Jacline Amos-MAELEZO

  Mmoja wa Wawekezaji Kampuni ya KAMAKA kwenye eneo la Uwekezaji la Kilua lililopo Kijiji cha Disunyala Kata ya Kilangalanga Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani Bw. Jurijs Matinovs (Kati kati)akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi wa huduma kwa wawekezaji kutoka TIC Bw.Ayoub Sizya (aliyevaa suti na shati jeupe) kuhusiana na uwekezaji wanaotaka kuufanya wa ujenzi wa kiwanda kwenye eneo hilo. (Picha na Jackline Amos-MAELEZO)
  Sehemu ya Kiwanda cha vyuma cha Kilua kilichopo Kibaha Mkoani Pwani, kiwanda hicho kipo kwenye eneo la ekari 1,000 eneo ambalo limekabidhiwa kwa kituo cha uwekezaji Tanzania TIC kwa ajili ya kuvutia wawekezaji wengi zaidi wa ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kujenga viwanda vingine vingi. (Picha na Jackline Amos-MAELEZO).  Wenye Maeneo Makubwa ya Uwekezaji Watakiwa Kushirikiana na TIC.

  Na Grace Semfuko-MAELEZO

  Wananchi wenye viwanja na maeneo makubwa nchini ambayo yanafaa kwa uwekezaji wameshauriwa kwenda katika kituo cha uwekezaji Tanzania TIC ili kuona ni kwa namna gani wataweza kuyatumia maeneo hayo kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda.

  Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa huduma kwa wawekezaji kutoka katika Kituo cha uwekezaji Tanzania TIC Bw. Ayoub Sizya wakati akitembelea na kukagua eneo la ukanda wa uwekezaji na mauzo ya ndani na nje ya nchi la Kilua lililopo kijiji cha Disunyala Kata ya Mlandizi Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani.

  TIC imeingia makubaliano na Mmiliki wa eneo la ukanda wa uwekezaji kwa ajili ya mauzo ya ndani na nje ya nchi la Kilua lililopo Kijiji cha Disunyala Kata ya Mlandizi Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani lenye zaidi ya ekari 1000 ambalo ni maalum kwa ajili ya ujenzi wa Viwanda.

  “Sisi TIC tumeingia makubaliano na Ukanda huu wa uwekezaji wa Kilua lengo letu ni kuimarisha shughuli za uwekezaji,tunafanya hivi ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi,kama unavyojua eneo hili linamilikiwa na mtu binafsi,na ni eneo kubwa ,hivyo tukiungana tutaleta wawekezaji wengi zaidi na Tanzania ya Viwanda itazidi kusonga mbele” alisema Ayoub Sizya Kaimu Mkurugenzi wa huduma kwa wawekezaji TIC.

  Mmiliki wa eneo hilo la ukanda wa uwekezaji Bw. Mohammed Kilua amesema watarajia kujenga viwanda zaidi ya 70 na kwamba mpaka sasa kiwanda kimoja kimekamilika ujenzi wake huku vingine saba vikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi ambapo ifikapo mwishoni mwa mwaka huu viwanda 20 vitakuwa vimeanza ujenzi.

  “Tutajenga viwanda vingi, ni zaidi ya 70 na kwenye eneo hili tayari tumepata maombi ya zaidi ya ujenzi wa viwanda 20 kwa mwaka huu, Tanzania ya Viwanda itafanikiwa tu,lengo letu ni kuunga mkono juhudi za Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli” alisema Mohammed Kilua Mkurugenzi wa eneo la ukanda wa uwekezaji la Kilua Bw.Mohammed Kilua.

  Kampuni ya Kamaka ni moja ya makampuni yanayowekeza kiwanda katika eneo hilo la Kilua, kwa upande wao wamesema ushirikiano baina ya kilua na TIC utaleta tija ya uzalishaji wa viwanda na kufikia malengo ya Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ya uchumi wa viwanda na kufikia uchumi wa kati.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo ya KAMAKA Bw. Jurijs Matinovs amesema wamejiandaa kuwekeza kwa nguvu zao zote na kwamba watahakikisha wanaendeleza juhudi za Rais Dkt John Pombe Magufuli.

  Eneo hilo maalum la uwekezaji mpaka sasa litatumia zaidi ya shilingi bilioni 15 za kitanzania kwa ajili ya kuweka miundombinu ya umeme,maji na barabara ambazo zitawezesha kufikika kirahisi kwenye viwanda vitakavyojengwa.

  0 0


  Meneja Mwandamizi Wateja Binafsi wa NMB, Ally Ngingite (wa pili kushoto) akimkabidhi Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Phares Magesa moja ya jezi zilizotolewa na NMB kwa ajili ya timu za mpira wa kikapu za Savio (wanaume) na Lioness (wanawake) kama sehemu ya udhamini wa timu hizo ambazo ni mabingwa wa ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam.
  Meneja Mwandamizi Wateja Binafsi wa NMB, Ally Ngingite (wa pili kushoto) akimkabidhi Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Phares Magesa moja ya mabegi yaliyotolewa na NMB kwa ajili ya timu za mpira wa kikapu za Savio (wanaume) na Lioness (wanawake) kama sehemu ya udhamini wa timu hizo ambazo ni mabingwa wa ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam.
  Meneja Mwandamizi Wateja Binafsi wa NMB, Ally Ngingite (wa pili kushoto) akimkabidhi Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Phares Magesa moja ya mipira iliyotolewa na NMB kwa ajili ya timu za mpira wa kikapu za Savio (wanaume) na Lioness (wanawake) kama sehemu ya udhamini wa timu hizo ambazo ni mabingwa wa ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam.
  Baadhi ya wachezaji wa timu za mpira wa kikapu za Savio na Lioness za Don Bosco Upanga wakiwa katika tukio hilo.
  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Phares Magesa (kushoto) akikabidhi sehemu ya vifaa vya michezo kwa mchezo wa mpira wa kikapu kwa wachezaji wa timu za mpira wa kikapu za Savio (wanaume) na Lioness (wanawake) kama ufadhili wa timu hizo. Benki ya NMB imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu hizo ikiwa ni ufadhili wa timu hizo. Anaye shuhudia ni Meneja Mwandamizi Wateja Binafsi wa NMB, Bw. Ngingite (wa pili kushoto) waliotoa vifaa hivyo.  BENKI ya NMB imekabidhi msaada wa vitabu na udhamini wa jezi, mabegi ya michezo na mipira kwa kituo cha vijana cha Don Bosco Upanga cha jijini Dar es Salaam kinachomiliki timu mbili za mchezo wa mpira wa kikapu kwa wanaume na wanawake ambazo ni mabingwa wa ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa mchezo huo.

  Msaada huo na udhamini wa vifaa hivyo kwa kituo hicho kinachosaidia vijana umegharimu kiasi cha shilingi milioni 15, ambapo akikabidhi Meneja Mwandamizi Wateja Binafsi wa NMB, Ally Ngingite alisema benki hiyo itaendelea kuchangia katika shughuli za kusaidia jamii pamoja na kuinua michezo nchini.Akifafaanua katika ufadhili huo, Bw. Ngingite alisema ufadhili huo umejumuisha vitabu mbalimbali kwenye maktaba ya kituo cha Don Bosco Upanga pamoja na vifaa vya michezo vitakavyotumiwa na timu ya mpira wa kikapu wanaume ya Savio na timu ya mpira wa kikapu wanawake ya Lioness zote zikilelewa na kituo hicho.

  Alisema NMB imetenga takribani shilingi bilioni moja ikiwa ni maalum kusaidia shughuli za kijamii ikiwemo sekta za afya, elimu na majanga endapo yanaikumba jamii. Alisema michezo mbali na kuwa ajira kwa vijana pia inawajenga kiafya na kuwawezesha kufanya vizuri hata kwenye elimu.Timu za mpira wa kikapu za Savio na Lioness ambazo zipo chini ya kituo cha Don Bosco Ukonga ni mabingwa wa ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa mchezo huo, na kwa udhamini wa NMB wao wamenufaika kupata jezi za kisasa, mipira ya mchezo huo pamoja na mabegi maalum ya michezo kujiandaa na mashindano aanuai.

  Kwa upande wake Mlezi wa Kituo cha Don Bosco Upanga, Padre Michael Muia aliishukuru Benki ya NMB kwa ufadhili na msaada walioutoa kwa kituo hicho na kuahidi wataitumia vizuri iwe chachu ya mafanikio zaidi kwa vijana.
  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Phares Magesa (kulia) akizungumza kuishukuru NMB kwa ufadhili huo. Kulia ni Meneja Mwandamizi Wateja Binafsi wa NMB, Ally Ngingite.
  Baadhi ya maofisa kutoka Benki ya NMB na vijana wa Kituo cha Don Bosco Upanga pamoja na wanahabari wakiwa katika hafla ya makabidhiano.
  Mlezi wa Kituo cha Don Bosco Upanga, Padre Michael Muia akizungumza kuishukuru Benki ya NMB kwa ufadhili na msaada walioutoa kwa kituo cha Vijana Don Bosco Dar es Salaam.

  0 0

   Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Uzuri, Bw. Sifuni Mbwambo (kushoto) akiongozana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe Jacqueline Mengi (wa pili kushoto) pamoja na Mratibu wa Miradi wa Taasisi hiyo, Bw. Francis Bazil (wa pili kulia) kuelekea ofisini kwa mkuu wa shule hiyo mara baada ya kuwasili kwa ajili ya hafla fupi ya kuzindua maktaba katika shule hiyo, iliyopo Kata ya Manzese , Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe Jacqueline Mengi akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Uzuri, Bw. Sifuni Mbwambo mara baada ya kuwasili shuleni hapo katika hafla fupi ya kuzindua maktaba ya shule hiyo iliyokarabatiwa na kuwekwa vitabu kwa hisani ya taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe jana jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe Jacqueline Mengi akiwasalimia wanafunzi wa shule ya Msingi Uzuri kabla ya kuelekea kwenye eneo husika kwa ajili ya kuzindua maktaba iliyokarabatiwa na kuwekwa vitabu kwa hisani ya taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe katika shule hiyo, iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo jana jijini Dar es Salaam.
    Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe Jacqueline Mengi akiimba na kucheza pamoja na wanafunzi wa shule ya Msingi Uzuri kabla ya kuelekea kwenye eneo husika kwa ajili ya kuzindua maktaba iliyokarabatiwa na kuwekwa vitabu kwa hisani ya taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe katika shule hiyo, iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo jana jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe  Jacqueline Mengi akitabasamu wakati akitambulishwa kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Uzuri kabla ya kuelekea kwenye eneo husika kwa ajili ya kuzindua maktaba iliyokarabatiwa na kuwekwa vitabu kwa hisani ya taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe katika shule hiyo, iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo jana jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe Jacqueline Mengi akikata utepe kuzindua maktaba iliyokarabatiwa na kuwekwa vitabu kwa hisani ya taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe katika shule hiyo, iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo jana jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Uzuri, Bw. Sifuni Mbwambo (kulia), Mwenyekiti wa Kamati ya shule  Bw. Yassin Shaaban Bakari (katikati), Mratibu wa Elimu kata ya Manzese, Laura Tesha (kushoto) pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakiwakilisha wenzao.
   Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Uzuri, Bw. Sifuni Mbwambo akizungumza na kuwatambulisha wageni wa meza kuu wakati wa hafla fupi ya kuzindua maktaba iliyokarabatiwa na kuwekwa vitabu kwa hisani ya taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe katika shule hiyo, iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo jana jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe Jacqueline Mengi na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya shule  Bw. Yassin Shaaban Bakari.
   Mgeni rasmi Afisa Elimu wa Manispaa ya Ubungo Chausiku Masegenya akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuzindua maktaba iliyokarabatiwa na kuwekwa vitabu kwa hisani ya taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe katika shule hiyo, iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo jana jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe Jacqueline Mengi (kushoto) akizungumza na wanafunzi pamoja na walimu wa shule ya Msingi Uzuri (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kuzindua maktaba iliyokarabatiwa na kuwekwa vitabu kwa hisani ya taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe katika shule hiyo, iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo jana jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Uzuri, Bw. Sifuni Mbwambo na kulia ni Mratibu wa Elimu kata ya Manzese, Laura Tesha.
   Baadhi ya wawakilishi wa wanafunzi wa shule ya msingi Uzuri wakimsikiliza Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe Jacqueline Mengi (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kuzindua maktaba iliyokarabatiwa na kuwekwa vitabu kwa hisani ya taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe katika shule hiyo, iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo jana jijini Dar es Salaam.
    Mwenyekiti wa Kamati ya shule Bw. Yassin Shaaban Bakari akitoa neno la shukrani kwa taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe kwa kukarabati jengo la maktaba pamoja na kuweka vitabu wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa maktaba hiyo iliyofanyika katika shule hiyo, iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo jana jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya walimu na wanahabari walioshiriki hafla fupi ya uzinduzi wa maktaba iliyokarabatiwa na kuwekwa vitabu kwa hisani ya taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe katika shule hiyo, iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo jana jijini Dar es Salaam.
   Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Uzuri, Bw. Sifuni Mbwambo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe Jacqueline Mengi pamoja na Mratibu wa Elimu kata ya Manzese, Laura Tesha wakitazama picha za maktaba ilivyokuwa hapo awali kabla ya kufanyiwa ukarabati na taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe wakati wa hafla ya kuzindua jengo la maktaba hiyo iliyofanyika katika shule hiyo, iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo jana jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe Jacqueline Mengi akikata utepe kuzindua eneo la maktaba iliyokarabatiwa na kuwekwa vitabu kwa hisani ya taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe katika shule hiyo, iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo jana jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Uzuri, Bw. Sifuni Mbwambo (kulia), Mwenyekiti wa Kamati ya shule Bw. Yassin Shaaban Bakari (katikati), Mratibu wa Elimu kata ya Manzese, Laura Tesha (kushoto) pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakiwakilisha wenzao.
   Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe Jacqueline Mengi na Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Uzuri, Bw. Sifuni Mbwambo wakifunua pazia kwenye kibao maalum cha wafadhili ambao ni taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe waliohusika kukarabati na kuweka vitabu kwenye jengo la maktaba hiyo shuleni hapo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa maktaba hiyo iliyofanyika katika shule hiyo, iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo jana jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa Kamati ya shule Bw. Yassin Shaaban Bakari (kulia).
   Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Uzuri, Bw. Sifuni Mbwambo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe Jacqueline Mengi pamoja na Mratibu wa Elimu kata ya Manzese, Laura Tesha wakikagua shelfu za vitabu vya maktaba katika shule hiyo, iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo wakati wa hafla fupi iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
  Wanafunzi wa shule ya Msingi Uzuri wakitoa burudani ya Igizo la usomaji wa vitabu wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa maktaba ya shule iliyokarabatiwa na kuwekwa vitabu kwa hisani ya taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe uliyofanyika katika shule hiyo, iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo jana jijini Dar es Salaam.
   Mgeni rasmi Afisa Elimu wa Manispaa ya Ubungo, Chausiku Masegenya na Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe, Jacqueline Mengi katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wa shule ya msingi Uzuri  iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo wakati wa hafla fupi iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe Jacqueline Mengi, Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Uzuri, Bw. Sifuni Mbwambo, Mratibu wa Elimu kata ya Manzese, Laura Tesha wakiwa katika picha ya pamoja baadhi ya wanafunzi wa hiyo mara baada ya kuhitimisha zoezi la uzinduzi wa maktaba hiyo shuleni hapo jijini Dar es Salaam.

  Na Mwandishi wetu,
  Wanafunzi nchini wametakiwa kujibidisha kusoma vitabu mbalimbali sio kwa malengo ya kufaulu mitihani pekee, bali  pia kwa ajili kupata elimu na maarifa mapya yatakayowasaidia kukabiliana na changamoto za maisha.
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe Jacqueline Mengi ametoa wito huo jijini Dar es salaam wakati akizindua maktaba ya shule ya Msingi Uzuri, iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo, ambayo imekarabatiwa na kuwekwa vitabu kwa hisani ya taasisi hiyo.
  Mkurugenzi huyo pia amewashawishi wanafunzi wa shule za msingi nchini wa kuanzia darasa la nne hadi la saba kushiriki shindano la Andika Challenge la kuandika na kubuni hadith zenye mafundisho, lililoanzishwa na Taasisi hiyo,  na kuwahakikishia kuwa kila mkoa utatoa washindi.
  Wakizungumza katika hafla hiyo Afisa Elimu wa Manispaa ya Ubungo Chausiku Masegenya, na Mwenyekiti wa Kamati ya shule Bw. Yassin Shaaban Bakari wameipongeza Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe kwa ufadhili huo unaounga mkono jitihada za serikali za kuboresha utoaji wa elimu nchini.
  Aidha Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bw. Sifuni Mbwambo na Mwanafunzi Vivian Herbeth wameipongeza taasisi ya Dr Ntuyabaliwe na kusisitiza kuwa shule hiyo ina maendeleo mazuri kitaalum ingawa inakabiliwa na changamoto mbalimbali, zikiwemo upungufu wa samani hasa kwa walimu,  uchakavu wa majengo, na ukosefu wa uzio.


  0 0

  WAFANYAKAZI wa benki ya TIB Corporate  wamtembelea Mkurugenzi Mkuu wa bohari ya dawa (MSD) Laurean Rugambwa jijini Dar es Saaam leo.

  Uamuzi wa wafanyakazi wa benki hiyo kwenda MSD nimwendelezo wa kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja kwa namna ya kutembelea wateja wao kwaajili ya kutoa shukurani kwa wateja.

  Mkurugenzi Mkuu wa bohari ya dawa (MSD) Laurean Rugambwa amewashukuru benki hiyo kwani wamefanya kitu cha tofauti pia amewatia moyo kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na kujituma.


  Wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate wakitembelea bohari ya dawa (MSD)mara baada ya mazungumzo na mkurugenzi mkuu wa bohari ya dawa jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni kusheherekea wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika Oktoba kila mwaka.
  Mkurugenzi Mkuu wa bohari ya dawa (MSD) Laurean Rugambwa akizungumza na wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate mara baada ya kumtembelea ofisini kwake ikiwa kushehereka wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika Oktoba kila mwaka.   Wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa bohari ya dawa (MSD) mara baada ya kumtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.  Wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa bohari ya dawa (MSD)  mara baada ya kumtembelea  ofisini kwake.
   Wafanyakazi wa bohari ya Dawa (MSD) wakimsikiliza mfanyakazi wa benki ya TIB Corporate hayupo pichani jijini Dar es Salaam leo.
  Wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate wakimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa bohari ya dawa (MSD)  mwenye tisheti ya bluu leo mara baada ya kutembelewa na wafanyakazi hao ofisini kwake.
  Mfanyakazi wa benki ya TIB Corporate akiangalia boksi la dawa mara baada ya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa bohari ya dawa (MSD) Laurean Rugambwa kuwaonesha jinsi bohari hiyo ilivyo.
  Mkurugenzi Mkuu wa bohari ya dawa (MSD) Laurean Rugambwa  akiwaonesha baadhi ya maboksi ya dawa wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate wakiwa  kutembelewa na wafanyakazi hao  jijini Dar es Salaam na kuangalia mteja wao anavyofanya kazi.
  Wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate wakipata maelezo mara baada ya kufika kitengo cha usafirishaji dawa.

  Wafanyakazi wa benki ya TIB Corporate akiangalia jinsi bohari ya dawa (MSD) wanavyofanya kazi zao.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaweka mikakati madhubuti kwa lengo la kuimarisha matumizi ya fukwe kama sehemu ya kivutio cha utalii ili kongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini na kutengeneza ajira kwa wananchi sambamaba na kukuza uchumi wa Taifa.

  Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Oktoba 12, 2018) wakati alipomuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye ufunguzi wa onesho la Kimataifa la Utalii la Swahili International Tourism Expo, katika  Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar ES Salaam.

  Onesho hilo linalofanyika kwa siku tatu nchini linahudhuriwa na wafanyabishara wakubwa wa utalii takriban 170  kutoka nchi mbalimbali duniani pamoja na wauzaji wa bidhaa za utalii takriban 300 kutoka ndani na nje ya nchi.

  Waziri Mkuu amesema sekta ya utalii nchini inachangia zaidi ya asilimia 25 ya mauzo yote ya nje na takriban ajira 1,500,000, ambapo kati ya ajira zote za moja kwa moja na zile ambazo si za moja kwa moja.

  Amesema kutokana na juhudi za utangazaji wa vivutio vya utalii nchini unaoratibiwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), wageni wengi maarufu duniani wanakuja kuona vivutio hivyo wakijua kwamba Tanzania ni nchi ya amani, yenye utulivu na Watanzania ni watu wakarimu. 

  Amsema kati ya wageni hao waliokuja hapa nchini kwa mwaka huu ni pamoja Rais Mstaafu wa Marekani, Bw. Barack Obama aliyekaa siku nane; Rais wa Uswisi Bw. Alain Berset aliyekaa siku 10 pamoja na mchezaji wa golf mstaafu kutoka Marekani, Bw. Jack Nicklaus.

  Kadhalika, Waziri Mkuu amesema kuwa  mbali na watu hao maarufu duniani kuja nchini pia makundi makubwa ya watalii yenye zaidi ya watu 300, wameingia nchini tangu mwanzoni mwa mwaka huu kutoka nchi za Israel, Australia na Hispania. “Hii ni ishara njema kwa maendeleo ya kasi ya sekta hii.”

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa mchango wake mkubwa kwenye maendeleo ya sekta ya utalii nchini kutokana na hatua mbalimbali anazozichukua katika kukuza sekta hiyo.

  Amesema miongoni mwa hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. Magufuli katika kuimarisha sekta ya utalii ni pamoja na kuboresha usafiri wa anga nchini, ambao kwa sasa umeongezeka kwa sababu ya uwekezaji mkubwa wa Serikali.

  “Ununuzi wa ndege saba mpya za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ambapo ndege nne tayari zimeshawasili na kuanza kutoa huduma ni kielelezo tosha cha juhudi za Serikali. Kati ya ndege hizi zipo ambazo hivi karibuni zitaanza kutoa huduma ya usafiri kati ya Tanzania na nchi za India na China.”

  Waziri Mkuu ametaja hatua nyingine kuwa ni ujenzi wa jengo la abiria yaani “Terminal 3”kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, ambapo baada ya kukamilika na kuanza kutumika jengo hilo linatarajiwa kutoa huduma zenye viwango vya kimataifa kwa abiria na kuruhusu ndege nyingi zaidi kuingia na kutoka nchini. Ujenzi wake umekamilika kwa zaidi ya asilimia 80.

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wadau wa utalii, kwenye ufunguzi wa maonesho ya Swahili International Tourism Expo, yaliyofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere Dar es salaam, Oktoba 12, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania Jaji Thomas Mihayo, wakati akiwasili kwenye ukumbi wa Julius Nyerere Dar es salaam, kufungua maonesho ya Swahili International Tourism Expo Oktoba 12, 2018, katikati ni Naibu Waziri wa maliasili na Utalii Josephat Hasunga , kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema. 
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la ndege Tanzania (ATCL) Ladiclaus Matindi, alipotembelea mabanda, kwenye ufunguzi wa maonesho ya Swahili International Tourism Expo, yaliyofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere Dar es salaam, Oktoba 12, 2018, kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, Naibu Waziri wa maliasili na Utalii Josephat Hasunga, Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania Jaji Thomas Mihayo. 
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia bidhaa za Tanzania zinazotolewa ndani ya ndege ya ATCL, kwenye ufunguzi wa maonesho ya Swahili International Tourism Expo, yaliyofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere Dar es salaam, Oktoba 12, 2018, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika la ndege Tanzania (ATCL) Ladiclaus Matindi na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania Jaji Thomas Mihayo. 

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  MAOFISA wanaosimamia madawati ya mikopo vyuoni wametakiwa kutokuwa chanzo cha migogoro ili kuhakikisha wanafunzi wanapata huduma bora isiyokuwa na urasimu na badala yake wahakikishe wanaimarisha madawati hayo ili kuhakikisha wanafunzi wenye sifa na uhitaji wanufaika na mikopo kama ilivyokusudiwa na Serikali.

  Agizo hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa James Mdoe wakati akizungumza katika kikao kazi cha siku mbili cha maafisa hao kilichoanza mjini Bagamoyo.

  Amesema dhamira ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha wanafunzi wengi wanapata Elimu ya juu bila kikwazo.

  Profesa Mdoe amesema kwa mwaka wa fedha 2018/19 serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 427. 5 ambapo jumla ya wanafunzi 124 watanufaika na mkopo huo, na kuwa ugawaji wa mikopo hiyo uzingatie haki, vigezo, kanuni na sheria.

  “Nataka twende vizuri tukahakikishe huduma bora inatolewa katika mwaka huu mpya wa masomo ikiwa ni pamoja kutoa huduma bora,kusimamamia kumbukumbuku na kuhakikisha mawasiliano ya mara kwa mara yanakuwepo kati ya maafisa mikopo na bodi ya mikopo na kwa haipendezi maafisa mikopo kuwa chanzo cha migogoro,”amesisitiza Profesa Mdoe.

  Profesa Mdoe pia ameitaka bodi hiyo kuimarisha mifumo ya TEHAMA ili kuboresha utendaji kazi, ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya kuwasaka waajiri warejeshe fedha ambazo wafanyakazi wao walisoma kwa mkopo, ili fedha hizo zitumike kwa wanafunzi wengine.

  Akizungumza katika kikao kazi hicho Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya mikopo Abdul- Razq badru amesema kuwa maagizo yote yaliyolewa na Naibu katibu Mkuu watayasimamia katika utekelezaji wa ugawaji wa mikopo kwa wnanafunzi huku akikiri kuongezeka kwa idadi ya wanufaika wa mikopo hiyo inayotolewa na serikali.

  “Bodi ya mikopo inaahidi kusimamia haki, vigezo, kanuni na sheria katika utoaji wa mikopo hiyo kwa wanafunzi kama ambavyo sheria zinavyoelekeza, niwasihi sana maafisa mikopo kufanya kazi kwa weledi na kuacha mazoea ili kuondoa migogoro inayoweza kujitokeza,”alisisitiza Badru.
  Mkurugenzi wa Elimu ya Juu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adam Mwakalobo akizungumza kuhusiana na ofisi yake inavyoratibu masuala ya elimu ya juu nchini kwa kushirikiana na vyuo vikuu,katika mkutano wa maafisa wa mikopo vyuo vikuu ulifanyika mjini Bagamoyo.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe akizungumza wakati akifungua mkutano wa kikao kazi cha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kwa maafisa wa mikopo katika vyuo vikuu uliofanyika mjini Bagamoyo, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya mikopo Abdul- Razq Badru.
  Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB )Abdul- Razq Badru akitoa taarifa ya bodi hiyo katika mkutano wo katika bodi na maafisa wa mikopo katika vyuo vikuu nchini katika mkutano uliofanyika mjini Bagamoyo.
  Ofisa Mikopo wa Chuo cha Uhasibu Arusha Esther Mwigune akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasimi katika kikao cha HESLB na Maafisa Mikopo katika Mkutano uliofanyika Mjini Bagamoyo
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa mikopo wa vyuo vikuu.

  0 0

  Every 14 October is Nyerere Day in Tanzania, a day to honour the memory of the nation’s first president and the number one leader in its independence movement and the solicitor for the union of Tanganyika and Zanzibar into the single nation of Tanzania.

  The late Julius Nyerere played an instrumental role in setting standards by which African countries rendered brotherly assistance to refugees. The late Nyerere was decorated with a famous Nansen Award in 1983 being the second Africa leader to be awarded the Nansen Medal after the then Botswana President, the late Sir Seretse Khama who received it in 1978.The former late president of Tanzania ‘Baba wa Taifa’ used the funds that accompanied the Nansen Award to build a primary school for Burundian refugees at Katumba settlements in Mpanda district, Rukwa region and set up basic needs structures.

  The award to the late Nyerere come in the awake of a gloomy refugee situation in Africa in 1983, at the time when, out of the ten million refugees in the world, five million were from the African continent.In his Nansen medal acceptance speech, the late Nyerere noted “we have boarders with eight countries, from only one of them have we never, throughout our 22 years of independence life, received any refugee. From two others we have received only small numbers, and these mostly intellectuals or former political leaders.”The late Nyerere at a time, reiterated Tanzania’s policy of providing refugees with the opportunity to earn their living without any sort of discrimination.

  In his effort to champion the rights of refugees, the late Nyerere stressed the importance of providing them with new means of livelihood saying “only when a person is earning his or her own living, or contributing in some way to the society he finds himself in, can he or she regain the self –respect which is an essential part of the human dignity”The late father of the Tanzanian Nation in his key note address notified the international community, that Africa was not responding to refugee problems simply by appealing for external help but was doing a lot more than was visibly noticed. He reiterated his deep rooted belief that refugees should be given the means to support themselves. 

  In his speech, Mr. Poul Hartling, United Nations High Commissioner for Refugees then, on the occasion said that “I think we all admire the highly significant national emblem of Tanzania which represents a man and woman holding upright a shield on which figures the torch of freedom - this is the greatest of all human values for which the brave people of your country strove for many years under your enlightened leadership.”It is no accident, Mr. President that measures based on granting durable solutions for refugees were initiated by the founding rather of the United Republic of Tanzania. 

  Their implementation required courage and perseverance, skill and wisdom combined with an intimate knowledge of the African scene and - above all - true “love of man” which forms part of Nansen’s motto engraved in the Medal. At a time of tension when the most elementary human rights of innocent people are violated, when defenseless men, women and children fall victim to ruthless aggression and blind vengeance, it is comforting to find that a Statesman like you, Mr. President, have so much at heart the rescue of some of the neediest among suffering humanity - the refugees.

  The late Nyerere become the facilitator of the Burundi Peace Negotiations after being approached by a number of world leaders who wanted him to become more actively involved in the search for solutions to the conflict in the region. As a first peace facilitator of the Peace Talks in Burundi in April 1999 he visited Mtendeli and Muyovosi refugee camps in Kigoma and Lukole camp in Kagera region to hear refugee views on the piece initiatives and to brief refugees on the progress of the talks he was facilitating in Arusha.During his visit, the late Nyerere recalled that both the Tanzania Government and UNHCR were bound by the convection to protect all refugees and, if they were to falter, the International community would be extremely critical.

  The late Nyerere has been remembered by various leaders across the world and within UNHCR for his enormous contribution for refugees. The former Assistant High Commissioner for refugees, Mr. Soren Jessen Petersen commented that “UNHCR recognized Mwalimu’s role in Africa since day one of his leadership. UNHCR’s Nansen medal, awarded to Mwalimu in 1983 was in recognition of his exemplary support to refugees.”

  The former President of Tanzania, Benjamin Mkapa commented that “Mwalimu Nyerere was acutely sensitive to the plight of refugees and displaced persons. Under Mwalimu leadership, Tanzania was not only peaceful, thereby not generating refugees, but he made Tanzania home to everyone seeking political and personal refuge.”

  The former United Nations High Commissioner for refugees, Ms. Sadako Ogata described Mwalimu as a legendary leader who will forever be held in the highest esteem as a great statesman, untiring advocate for social justice and peace and champion of the cause of the world underprivileged. “Personally I will retain fond memories of Mwalimu as a strong supporter of refugees and other displaced victims of armed conflict. In recognition he was awarded the UNHCR Nansen medal in 1983.”

  Currently, Tanzania remains generous to more than 300,000 refugees and asylum-seekers in the country. The majority of refugees in Tanzania are from Burundi and the Democratic Republic of the Congo, with 87 per cent living in three camps in the Kigoma Region. The Nansen Award was introduced by a Norwegian Fridjtof Nansen, for the purpose of serving global refugee problems. Nansen was a pioneer of international humanitarian aid, who become the first League of Nations High Commissioner for refugees in 1921. This year the Nansen award was granted to a South Sudanese surgeon Dr. Evan Atar Adaha for his outstanding 20 -year commitment in providing medical services to people forced to flee conflict in Sudan.


  0 0


  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akielezea maboresho ya sheria ya takwimu inayowafanya watafiti waweze kufanya tafiti zao kwa urahisi kwa maendeleo ya taifa, wakati wa Mkutano kati yake na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeziwakilisha nchi za Afrika Bw. Andrew Bvumbe (hayupo pichani), wakati wa mikutano ya mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF na Benki ya Dunia (WB) mjini Bali Indonesia, kushoto ni Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania- TRA Bw. Charles Kichere.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeziwakilisha nchi za Afrika Bw. Andrew Bvumbe (wa pili kushoto) akifurahia jambo kwenye mkutano na wajumbe wa Tanzania walioshiriki mikutano Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF na Benki ya Dunia (WB) mjini Bali Indonesia. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikali Wizara ya Fedha na Mipango- Bali Indonesia) .
  Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohamed (kulia), akieleza kuhusu mpango wa kuboresha Sekta ya uvuvi ili kureta tija wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anayewakilisha nchi za Afrika Bw. Maxwell Mkwezalamba (hayupo pichani), wakati wa mikutano ya mwaka ya IMF na Benki ya Dunia (WB) mjini Bali Indonesia.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anayewakilisha nchi za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba, akiipongeza Tanzania kwa hatua iliyochukua ya kukuza uchumi, wakati wa Mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) uliofanyika Mjini Bali Indonesia.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeziwakilisha nchi za Afrika, Bw. Andrew Bvumbe (kulia), akieleza jambo wakati wa Mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kushoto), wakati wa mikutano ya mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa- IMF na Benki ya Dunia (WB) mjini Bali Indonesia, wa tatu kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohamed na kushoto ni Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania- TRA, Bw. Charles Kichere.  ………………………  Na. WFM Mjini Bali Indonesia

  Marekebisho ya Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2018, hayawazuii wadau wa takwimu kutoa takwimu kwa ajili ya matumizi yao bali marekebisho hayo yanaweka misingi ya kuzingatiwa wakati wa utoaji wa takwimu hizo.

  Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango, alipofanya mkutano na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha (IMF) anayewakilisha Tanzania na nchi nyingine (Africa Group 1 Constituency), Bw. Maxwell Mkwezalamba, katika Mikutano ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) mjini Bali Indoneshia.

  Dkt. Mpango amesema kuwa lengo la marekebisho ya sheria hiyo ni kurahisisha ufanyaji wa tafiti na utoaji wa matokeo ya tafiti na sio kuwabana wadau katika ukusanyaji wa taarifa za kitakwimu au kuzuia mijadala ya uchambuzi wa kisera wa matokeo ya takwimu rasmi.

  “Tumekubaliana kutumia fursa ya kuboresha Kanuni za Takwimu kwa ajili ya kuweka mazingira ya utekelezaji mzuri wa vipengele vya sheria vilivyorekebishwa kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali ili kuelewa lengo la marekebisho hayo”, alieleza Dkt. Mpango.

  Marekebisho hayo ya kanuni za takwimu yatawezesha utekelezaji mzuri wa vifungu vya sheria vilivyorekebishwa ambapo ametoa wito kwa wadau kushiriki katika mchakato wa marekebisho hayo.

  Aidha, Waziri alieleza kuwa mwezi Novemba mwaka huu Serikali itakutana na wadau wa maendeleo, ili kutoa fursa kwa wadau hao kuelewa kwa kina dhumuni la Serikali kufanya marekebisho yaliyofanyika na kupitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwezi Septemba 2018.

  Vilevile, Waziri Mpango, alimueleza Mkurugenzi Mtendaji wa IMF kuwa marekebisho makubwa ya kiuchumi ambayo yamefanywa na Serikali ya Awamu ya Tano yameambatana na mabadiliko ya sheria mbalimbali hususan sheria za za madini kwa lengo la kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha wananchi lakini pia wawekezaji wanaowekeza fedha zao nchini.

  Aidha, alisema kuwa Bw. Kwezilamba, ni mwakilishi wa Tanzania kwenye Bodi ya Magavana wa IMF, hivyo ni muhimu aelewe maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanayofanyika nchini Tanzania ili aweze kueleza uhalisia kwenye mikutano ya Bodi hiyo.

  Naye Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Florens Luoga, alisema kuwa BoT imeendelea kuboresha Sera ya Fedha ya Mwaka 2017 ili kutatua changamoto za Sekta ya Fedha zinazoibuka zikiwemo za uhaba wa mikopo hasa katika Sekta binafsi.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha (IMF) anaeiwakilisha Tanzania, Bw. Maxwell Mkwezelamba, aliipongeza Tanzania kwa hatua mbalimbali za maendeleo ya uchumi kwa kuwa imeendelea kuwa nchi inayopiga hatua kubwa ya maendeleo na kuwa mfano katika nchi za Afrika.

  Ameishauri Tanzania kutumia ofisi yake ili Washirika wa Maendeleo waelewe dhumuni la marekebisho ya kiuchumi yanayoenda sambamba na maboresho ya sheria mbalimbali ili maendeleo hayo yawe endelevu.

  Vilevile Dkt. Mpango, alifanya mkutano na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia (WB) anayewakilisha Tanzania na nchi nyingine (Africa Group 1 Constituency), Bw. Andrew Bvumbe, wakati wa mikutano ya mwaka ya WB na IMF inayofanyika mjini Bali Indonesia na kupongeza ushirikiano wa kimaendeleo na taasisi hizo.

  0 0  Mwenyekiti  kamati ya kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Mhe. Oscar Mukasa akiongoza kikao cha pamoja baina ya Wajumbe wa kamati hiyo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo na watendaji wake wakati wa kupokea na kujadili taarifa ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuhusu hatua iliyofikiwa katika utafiti wa upatikanaji wa chanjo ya Ukimwi nchini kilichofanyika leo katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
  V25A0198
  Mwenyekiti  kamati ya kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Mhe. Oscar Mukasa akizungumza na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo na watendaji wake (hawapo kwenye picha) wakati wa kupokea na kujadili taarifa ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuhusu hatua iliyofikiwa katika utafiti wa upatikanaji wa chanjo ya Ukimwi nchini katika kikao kilichofanyika leo katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kushoto ni Mjumbe wa kamati, Mhe. Dkt. Haji Mponda na kulia ni katibu wa kamati hiyo, Ndg. Happy Ndalu
  V25A0161V25A0173V25A0183
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Dkt. Faustine Ndugulile akitoa ufafanuzi  mbele ya Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi katika majadiliano ya taarifa ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuhusu hatua iliyofikiwa katika utafiti wa upatikanaji wa chanjo ya Ukimwi nchini katika kikao kilichofanyika leo katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
  V25A0090
  Mjumbe wa Mwenyekiti  kamati ya kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Mhe. Godfrey Mgimwa akizungumza jambo katika majadiliano na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo na watendaji wake wakati wa kupokea taarifa ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuhusu hatua iliyofikiwa katika utafiti wa upatikanaji wa chanjo ya Ukimwi nchini kilichofanyika leo katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kulia ni Mjumbe wa kamati, Mhe. kemirembe Lwota
    V25A0067
  Mjumbe wa Mwenyekiti  kamati ya kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Mhe. Albert  Ntabaliba Obama akizungumza jambo katika majadiliano na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo na watendaji wake wakati wa kupokea taarifa ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuhusu hatua iliyofikiwa katika utafiti wa upatikanaji wa chanjo ya Ukimwi nchini kilichofanyika leo katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
  V25A0128
  Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza na wajumbe kamati ya kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi wakati wa majadiliano ya taarifa ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuhusu hatua iliyofikiwa katika utafiti wa upatikanaji wa chanjo ya Ukimwi nchini katika kikao kilichofanyika leo katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoo, Dkt. Faustine Ndugulile
  (PICHA NA OFISI YA BUNGE

  0 0


  Akipokea msaada wa mabati , mkuu wa mkoa wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto )kutoka kwa mkuu wa kitengo cha mahusiano cha kampuni ya Sayona fruits iliyopo Mboga Chalinze ,Abubakar Mlawa (kulia) ,msaada ambayo umeelekezwa kuimarisha sekta ya elimu .( picha na Mwamvua Mwinyi )


  NA MWAMVUA MWINYI,PWANI 

  SEKTA ya elimu mkoani Pwani, inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa 3,678 katika shule za msingi pamoja na nyumba za walimu 5,188.

  Kufuatia changamoto hiyo ,kampuni ya Sayona fruits ,iliyopo Mboga huko Chalinze imetoa mabati 1,000 yenye thamani ya sh.mil 24 ,kwa ajili ya umaliziaji wa majengo mbalimbali ya shule za msingi mkoani humo .

  Akipokea mabati hayo ,kutoka kwa mkuu wa kitengo cha mahusiano cha kampuni hiyo ,Abubakar Mlawa , mkuu wa mkoa wa mkoa huo mhandisi Evarist Ndikilo alisema ,wanakabiliana na changamoto hizo kwa kushirikiana na halmashauri,jamii na wadau wa elimu . “Miundombinu ya shule za sekondari na hasa shule za msingi bado kuna upungufu ,ambapo mkoa una jumla ya shule za msingi 613 huku za serikali zikiwa ni 562 na 51 ni za watu binafsi “

  “Shule za msingi pekee mahitaji ya vyumba vya madarasa ni 700,671, yaliyopo 3,993 na upungufu ni vyumba vya madarasa 3,678 ” alifafanua Ndikilo.
  Ndikilo alitaja pia tatizo la nyumba za walimu ili waweze kuishi vizuri hivyo kuna mahitaji ya nyumba hizo 6,779 . Alisema ,nyumba zilizopo ni 1,591 na upungufu ni nyumba za walimu 5,188.#

  “Mtaona ni namna gani bado tuna changamoto za miundombinu kwenye sekta ya elimu ambapo inasababisha baadhi ya wanafunzi kushindwa kusoma kwenye mazingira bora na walimu kufundisha katika mazingira yasiyo ridhisha ” alisisitiza. Hata hivyo akimshukuru mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Sayona Shubash Patel ,Ndikilo alisema ni mdau mkubwa kimkoa kwani amekuwa akisaidia kwenye sekta mbalimbali . Alielezea kati ya mabati hayo,yataanza na shule yetu ya msingi Mkoani kwani ina mahitaji mengi na kumalizia majengo mengine katika shule nyingine.

  Awali akikabidhi mabati hayo , Abubakar Mlawa alisema ,msaada huo utawezesha kuezeka baadhi ya vyumba vya madarasa ,matundu ya vyoo na nyumba za walimu. Alieleza ,licha ya kuwekeza lakini pia wanashiriki kusaidia huduma za kijamii ikiwemo kuboresha sekta ya elimu . “Sayona lengo lake kubwa ni kuweka mazingira bora ya kusoma kwa wanafunzi wetu ,hivyo tumekuja kukukabidhi mabati haya 1,000”; alisema Mlawa . Nae ,ofisa elimu wa mkoa wa Pwani ,Abdul Maulid aliwashukuru Sayona kwa msaada huo ambao unakwenda kuimarisha sekta ya elimu .

  Alitoa rai na kuwaomba wawekezaji wengine kujitoa kusaidia sekta ya elimu kwa kuiga mfano wa kampuni ya Sayona.

  0 0


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Uganda Mhe.Dk.Aziz Ponary Mlima ayefika kumuaga Rais Ikulu Mjini Zanzibar leo,Balozi aliteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli
  DSC_2420
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na  Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Uganda Mhe.Dk.Aziz Ponary Mlima  alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kumuaga Rais,Balozi aliteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli
  Picha na Ikulu

  0 0

   Mmoja wa mgonjwa aliyelazwa katika Hospitali ya Rufaa Musoma akionwa na Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani wa Muhimbili, Dkt.  Brighton Mushengezi kwa kushirikiana na Mtaalam wa magonjwa ya ndani, Farbian Gabriel Beyesigwa  wa Hospitali ya Rufaa Musoma.
  004
  Daktari bingwa wa macho wa Muhimbili, Dkt. Neema Kanyaro akitoa huduma ya macho kwa wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa macho leo katika Hospitali ya Rufaa Musoma.
  005
  Mmoja wa watoto wenye tatizo kwenye koo akifanyiwa upasuaji leo na daktari bingwa Muhimbili, Dkt. Raymond Leiya.
  006
  Wataalam wa upasuaji wa Hospitali ya Rufaa Musoma wakifanya upasuaji kwa kushirikiana na wataalam wa Muhimbili Dkt. Athuman Mbalamula na Dkt. Helen Mrina.
  001
  Wataalam wa Muhimbili na wa Hospitali ya Rufaa Musoma wakifanya upasuaji wa macho jana katika Hospitali ya Mkoa wa Musoma.
  007002
  Dkt. Athuman Mbalamula wa Muhimbili akifanya upasuaji kwa mgonjwa mwenye tatizo sehemu ya tumbo kwa kushirikiana na mtaalamu wa upasuaji, Joram Laurent wa Hospitali ya Rufaa Musoma.
  008
  Baadhi ya wagonjwa wakisubiri majibu katika maabara ya Hospitali ya Mkoa wa Musoma jana.
  Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
  ……………………………..
  Na John Stephen, Musoma

  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeongeza siku saba zaidi kwa watalaam wake walioko Hospitali ya Rufaa Musoma ili kuhakikisha wanahudumia idadi ya wananchi wengi waliojitokeza kwa wingi kupata huduma katika kambi maalumu iliyoanza Oktoba 7, 2018 mkoani Mara.

  Kambi hiyo ilitarajiwa kuisha leo Oktoba 12, 2018, lakini kutokana na hitaji kubwa la wananchi waliojitokeza kupata huduma, uongozi wa hospitali umeamua kuongeza siku hadi Ijumaa ijayo tarehe 19 Oktoba, 2018 ambapo watahitimisha na kurejea jijini Dar es  Salaam.

  Hadi kufikia jana Alhamisi jumla ya wananchi  1210 walikuwa wamejiandikisha kupata huduma mbalimbali za matibabu kati hao   wananchi 1155 wameonwa na watalaamu  wa Muhimbili wale wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Musoma.

  Kati ya hao, kinamama watano wamefanyiwa upasuaji, 36 wenye matatizo ya macho wamepatiwa huduma ya upasuaji, wagojwa wanane wamepatiwa huduma ya upasuaji wa mfumo wa mkojo, 14 upasuaji wa magonjwa mbalimbali (general surgery), 10 upasuaji wa masikio, koo na pua na  233 wamefaniwa uchunguzi wa kawaida.

  Baadhi ya wagonjwa wamepewa rufaa za kwenda kutibiwa Muhimbili na wengine Hospitali ya Bugando ambako watafanyiwa uchunguzi zaidi na hatimaye kupata tiba stahiki kutokana na mazingira ya ugonjwa.

  Hospitali ya Taifa Muhimbili ilipeleka watalaam wake 14 mkoani Mara katika Hospitali ya Rufaa ya Musoma mapema wiki hii ili kujenga uwezo wa watalaam na kutoa huduma kwa wananchi wenye matatizo mbalimbali  ya afya.

  Philipo Jackson Mayunga mkazi wa Wilaya ya Busega mkoani Simiyu ameomba uongozi wa Muhimbili kuongeza muda kwa wataalam wake kuendelea kutoka huduma kwa kuwa wametoka mbali kufuata huduma.

  “Wataalam wamepewa muda mchache sana hivyo naomba waongezewe muda kwani watu wengi wanahitaji huduma za madaktari bingwa na wengine wamekata tamaa kwamba hawatatibiwa,” amesema Mayunga.

  Kutokana na mahitaji ya wananchi mbalimbali wa Mkoa wa Mara, Muhimbili imelazimika kuongeza muda kwa wataalamu wake ili kuhakikisha hakuna mtu yeyeyote atakayekosa huduma baada ya matibabu.

  0 0

   Meza ya Majaji wakiongozwa na Chief Judge, Adam Mchomvu (wapili kushoto) wengine toka kushoto ni Chege,Man C na Joh Makini.
   Msanii Chipukizi aliyeingia Mbili Bora almaarufu, Single Baba akinyanyua mikono juu mara baada ya kutangazwa kupanda jukwaa la Tigo Fiesta jioni ya leo uwanja wa Majimaji Songea, jumla ya wasanii wawili watachuana kumpata mwakilishi wa mkoa wa Ruvuma.
   Wasanii waliongia mchujo wa mwisho utaofanyika jioni ya leo kwenye jukwaa la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote uwanja wa Majimaji, kushoto ni Single Baba na Yatosha.
   Baadhi ya wateja wa Tigo wakipokea zawadi toka kwa wasanii mbalimbali
   Baadhi ya wateja wa Tigo wakipokea zawadi toka kwa wasanii mbalimbali
   Msanii Ruby akimkabidhi zawadi mteja wa Tigo, Fatuma Komba leo
   Wasani watakaopanda jukwaa la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote uwanja wa Majimaji Songea jioni ya leo wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Duka la Tigo lililopo mtaa Itundu Songea
  Majaji wakiwa kwenye picha ya pamoja na  washindi wawili nyuma waliosimama na chini toka kushoto ni jaji Man C toka Jogoo Fm, Adam Mchomvu, Chege na Joh Makini.


  0 0  0 0

  Mkurugenzi wa Tume ya uchaguzi Taifa (NEC) Dkt. Athumani Kihamia akiwa Liwale leo na kuzungumzia maandalizi ya Uchaguzi ndani ya jimbo hili. Picha na Vero Ignatus.
  Mkurugenzi wa huduma za Kisheria Tume ya Taifa ya Uchaguzi Emmanuel Kawishe. Picha na Vero Ignatus.
  Na. Vero Ignatus, Liwale,-Lindi

  Maandalizi ya uchaguzi mdogo Jimbo Liwale Mkoani Lindi na kata nne Tanzania Bara yamekamikika kwa asilimia 100

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Tume ya uchaguzi Taifa (NEC) Dkt. Athumani Kihamia kwamba vifaa vimefika wakati hivyo amewataka wananchi wa Liwale watambue kuwa uchaguzi siyo vita bali ni sera ya nchi ya kupata viongozi kwa kuchaguliwa,

  "Vifaa vya uchaguzi vimefika kwa wakati, watendaji wa uchaguzi wamepatiwa mafunzo ya kutosha pia ulinzi na usalama umeimarishwa hivyo wananchi msiogope kuja kupiga kura hapo kesho".'' Kwa upande wa kampeni zipo salama hakuna mtu aliyejeruhiwa wala kurupushani, hakuna malumbano yeyote makubwa ambayo yanaashiria ubunjifu wowote wa Amani''Amesema Kihamia.

  Amesema vituo vya kupiga kura vitafunguliwa kesho saa moja asubuhi na vitafungwa majira ya saa kumi jioni 13oktoba 2018, hivyo wananchi wamejitokeze kwa wingi kutimiza haki yao ya msingi ya Kikatiba ya kupiga kura.Aidha wananchi wametakiwa wakishapiga kura warudi manyumbani mwao na kuendelea na shughuli zao za kihalali zinazotekelezwa kila siku.

  '' Hakuna haja ya kusema kuwa kuna mwananchi anayelinda kura maana tayari wana mawakala wao kayika mchakato mzima wa upigaji kura hadi kuhesabu hadi kumtangaza mshindi'',Mkurugenzi wa huduma za kisheria kutoka NEC Emmanuel Kawishe amesema hakuna changamoto ila baadhi vyama ambao hawakupata taarifa sahihi kuhusiana na maswala ya mawakala, hadi kufikia kusema tume imekataa wakati ilishakubaliana na vyama hivyo.

  Ikumbukwe kuwa uchaguzi huo mdogo unafanyika katika jimbo la Liwale kutoka na aliyekuwa mbunge Zuberi Kuchauka wa awali kuhama kutoka chama cha CUF na kuhamia CCM

  0 0

   Meneja wa Mradi Kinyerezi II, Mhandisi Stephens S.A.Manda (wakwanza kulia), akimtembeza Naibu Mkurugenzi wa TANESCO (usambazaji) Mhandisi Raymond Seya, (wapili kulia), kujionea maendeleo ya mradi w aumeme wa Kinyerezi II jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Oktoba 12, 2018. 

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
  SHIRIKA la Umeme Nchini TANESCO limesema liko tayari kupokea uwekezaji wa viwanda vya aina zote kwani hivi sasa kuna umeme wa kutosha, bora na wa uhakika.Hayo yamesemwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO (Ugawaji), Mhandisi Raymond Seya, baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa umeme  Kinyerezi II jijini Dar es Salaam, Ijumaa Oktoba 12, 2018. 

   “Mradi unafikia mwisho sasa, kwasababu mashine zote zimeshafungwa na uwezo wa mashine hizi ni kuzalisha  Megawati 240, tunamalizia mambo madogo madogo kama ujenzi wa barabara na kupaka rangi lakini pia kujenga ofisi za wafanyakazi.” 

  Alifafanua Mhandisi  SeyaTunataka kuwahakikishia wananchi uwekezaji huu mkubwa wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 750 zote zikiwa zimetolewa na serikali umekamilika na tayari umeingizwa kwenye Gridi ya taifa.“Tunapenda kumshukuru sana Mhe. Rais wa serikali ya awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuridhia kufadhili mradi tunawahakikishia sera ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa viwanda itatekeelezwa kikamilifu na sisi kama TANESCO tuko tayari kupokea uwekezaji wa viwanda vya aina zote.” Alisema. 

   Alisema, tayari umeme huo umeingizwa kwenye gridi ya taifa na hadi sasa kwa ujumla kuna kiasi cha umeme kwenye gridi ya taifa Megawati 1500 na ukiangalia repoti za matumizi ya umeme kila siku tunakiuwa na ziada ya Megawati 250 hadi 160, Wikiendi inakuwa zaidi kwa sababu matumizi ya umeme yanapungua kwa hivyo yunapoongeza vyanzo hivi vya uzalishaji umeme tuanzidi mkuwa na uwezo wa kuunganisha wateja zaidi na kutoa huduma iliyo bora.” Alisema. 

   Mhandisi Seya pia alitembelea mradi mwingine wa upanuzi wa Kinyerezi I ambapo miundombinu ya kusimika mashine iko tayari na kwamba zoezi la kufunga mashine hizo litaanza wakati wowote luanzia sasa.Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo, Meneja wa Mradi Kinyerezi II, Mhandisi Stephens S.A.Manda Alisema miradi yote miwili ni miradi ya kimkakati na kwamba wakati mradi wa Kinyerezi II tayari umekamilika, mradi wa upanuzi wa Kinyerezi I, umefikia asilimia 70.“Mradi wa upanuzi wa Kinyerezi I, utakuwa na Megawati 185 ambapo Kinyerezi I yenyewe inazalisha umeme Megawati 150 na hivyo utafanya jumla ya Megawati 335 utakapokamilika Agosti mwakani. 

   “Kwa hiyo miradi yote hii itakapokamilika tunazungumzia jumla ya Megawati 575 zitakuwa zinazalishwa hapa Kinyerezi.” Alifafanua Mhandisi Mmanda.“Sasa hivi kwenye Gridi ya Taifa tunatosheleza mahitaji yote na tuna ziada, kwa hiyo tunachosema kama Shirika la umeme tunao umeme wa mkutosha na wawekezaji waje ili tuweze ili twende na falsafa ya Rais wetu ya kuwa na nchi yenye uchumi wa kati lakini zaidi sana nchi yenye uchumi wa viwanda.” Alsiema.Mhandisi Mmanda alibainisha kuwa Mradi wa upanuzi wa Kinyerezi I utakamilika Agosti mwakani.
   Meneja wa Mradi Kinyerezi II, Mhandisi Stephens S.A.Manda (wapili kulia), akimpatia maelezo Naibu Mkurugenzi Mtedaji wa TANESCO (usambazaji), Mhandisi Raymond Seya, kuhusu namna mitambo katika chumba cha udhibiti (Control room) inavyofanya kazi
   Meneja Miradi Mwandamizi  TANESCO, Mhandisi Emmanuel Manirabona, akikagua mitambo kwenye chumba cha udhibiti (Control room) cha Kinyerezi II leo Ijumaa Oktoba 12, 2018.
   Mhandisi Seya (kushoto), akiteta jambo na Mhandisi Mmanda.
   Naibu Mkurugenzi Mtedaji Shirika la Umeme nchini TANESCO anayeshughulikia usambazaji, Mhandisi Raymond Seya, (katikati), kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, akitembelea mradi wa umeme wa Kinyerezi II kujionea maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo leo Ijumaa Oktoba 12, 2018. Kulia ni Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Stephenes S.A Mmanda (kulia) na Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika hilo, Bi. Leila Muhaji,.
   Moja ya mitambo ambayo tayari imewasili ili kutekeleza mradi mwingine wa upanuzi wa Kinyerezi I.
  Muonekano wa eneo itakapofungwa mitambo kwenye eneo la upanuzi wa mradi wa umeme Kinyerezi I hadi kufikia leo Ijumaa Oktoba 12, 2018.

older | 1 | .... | 1695 | 1696 | (Page 1697) | 1698 | 1699 | .... | 1897 | newer