Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

UWEKEZAJI KATIKA ELIMU SULUHISHO LA CHANGAMOTO ZA KIUCHUMI AFRIKA

$
0
0
Na. WFM, Bali Indonesia

Nchi za Afrika ikiwemo Tanzania zinatakiwa kuwekeza kwa kiasi kikubwa kwenye maarifa na elimu ili kuendana na soko la ushindani linaloendelea kwa kasi Duniani

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Fedha na Mipango ambaye pia ni mwakilishi wa Tanzania katika Bodi ya Magavana wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Dkt. Philip Isdor Mpango, wakati wa mikutano ya WB na IMF mjini Bali Indonesia.

Dkt. Mpango alisema kuwa, katika mikutano hiyo ya Kimataifa yapo mambo ambayo Tanzania inatakiwa kuyafanyia kazi wakati huu ambao inapiga hatua kuelekea katika uchumi wa kati unaotegemea viwanda ambapo elimu inayotolewa inatakiwa kujikita katika kukuza maarifa na ujuzi .

“Wakati suala la teknolojia likiangaziwa katika bara la Afrika ni vema kuangalia pia namna ya kukabiliana na changamoto zinazotokana na teknolojia hiyo kwa kuwa katika maeneo mengi ajira za watu zimepungua kutokana na mashine kuchukua nafasi za watu”, alisema Dkt. Mpango.

Alisema mikutano ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa imekua na umuhimu mkubwa kwa kuwa wadau wamebadilishana mawazo ambayo yamelenga kukabiliana na changamoto za kiuchumi ambazo zimeendelea kutokea Duniani ikiwa ni pamoja na baadhi ya nchi kuwa juu kiuchumi na nyingine kuendelea kuporomoka kwa kasi. 

Katika mikutano hiyo Tanzania imetajwa kuwa uchumi wake unaendelea kuimarika ambapo kwa sasa unakua kwa takribani asilimia sita hivyo kuwa mfano wa kuigwa barani Afrika na Dunia kwa ujumla.Wajumbe wa mikutano hiyo wametakiwa pia kukabiliana na suala la mabadiliko ya tabia nchi katika nchi zao kwa kuwa yanaathari kubwa katika uchumi hasa katika Sekta ya afya kutokana na kuongezeka kwa magonjwa lakini pia mafuriko na ukame.

Naye Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Rubuka, alisema kuwa suala la amani duniani limejadiliwa kwa kina katika mikutano hiyo kwa kuwa ni chachu ya maendeleo si tu ya kiuchumi lakini pia ya kijamii.

Mikutano ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa inaendelea Mjini Bali Indonesia, ambapo imewakutanisha Mawaziri, Magavana na wadau wa masuala ya Fedha na Uchumi kutoka nchini mbalimbali duniani.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi wa Benki ya Dunia (WB,) anayewakilisha Afrika (Africa group 1 constituency), Bi. Anne Kabagambe, wakati wa mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayoelendelea mjini Bali Indonesia, kushoto kwake ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).
Wajumbe wa Benki ya Dunia (WB) kundi la Afrika (Africa group 1 constituency), wakiwa katika Mkutano Mjini Bali Indonesia.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) wa pili kulia, akijadili jambo na Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga wakati wa mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoelendelea mjini Bali Indonesia.
Waziri wa Fedha na Mipango ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Ushauri wa Masuala ya Fedha wa Benki ya Dunia- WB kwa nchi za Afrika (Africa group 1 constituency) Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akisoma ujumbe wa nchi hizo, wakati wa mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoelendelea mjini Bali Indonesia (kushoto ) ni  na Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango Mjini Bali Indonesia)

HATIMAYE JIMBO LA LIWALE LAPATA MUWAKILISHI BUNGENI

$
0
0
Na. Vero Ignatus, Liwale - Lindi

Hatimaye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Liwale umemalizika kwa huku mgombea wa chama cha mapinduzi (CCM) Zuberi Kuchauka akiibuka mshindi wa kiti cha ubunge

Msimamizi uchaguzi Jimboni hapo Luiza Mlelwa amesema waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 55777 na waliojitokeza kupiga kura walikuwa 40706 kura halali zilikuwa 40,301 kura zilizokataliwa ni 405 

Akimtangaza mshindi wa kiti cha ubunge (6:30usiku ) Jimbo la Liwale msimamizi wa uchaguzi amesema kuwa Zuberi ameshinda kwa kura 34, 582 sawa na asilimia 85.81.Mara baada ya kutangazwa mshindi wa kiti cha Ubunge Zuberi Mchauka amesema ameyapokea matokeo kwa furaha na ameahidi kushirikiana na wananchi wa Jimbo la Liwale kutatua changamoto mbalimbali zilizopo

Aidha Mchauka amesema kuwa changamoto nyingi zilizopo katika Jimbo la Liwaleni pamoja na miundombinu ya barabara, maji, Elimu, mawasiliano na Afya ambapo ameahidi wananchi kuwa atashughulikia changamoto hizo. 

Abdul Kombo Ngakolwa mgombea wa chama cha (AAFP) chama cha wakulima amesema ameridhishwa na ushindi alioupata mgombea wa(CCM) na amempongeza, kwa ushindi huo '' Mara zote mtu unaposhindana lazima mmoja ashinde, asiyekubali kushindwa siyo mshindani'' alisema Abdul

Mwajuma Notey mgombea kutoka (UMD) amewapongeza wanaliwale kwa kufanya maamuzi yao na amesema anayaheshimu, amempongeza mbunge mteule kwa ushindi huo ."Nakupongeza sana kwa ushindi ila namkumbusha tu awakumbuke wapiga kura wako wote waliomchagua na wasiomchagua wote ni wapigakura wako" 

Mchakato wa kumtafuta mbunge wa Jimbo la Liwale ulianza mwezi mmoja uliopita ambapo waliotangaza nia ya kuwania kiti hicho ni wagombea kutoka vyama vifuatavyo AAFP kura 18 sawa 0.2% (UMD 109 sawa 0.49% ACT 285 sawa 0.79%CUF 5207 sawa na 12. 92%.
Msimamizi wa uchaguzi mdogo Jimbo la Liwale Luiza Mlelwa akimkabishi chetu mbunge mteuliwa wa Jimbo la Liwale Zuberi Kichauka. Picha na Vero Ignatus
Wa pili kutoka kulia ni Msimamizi wa Uchaguzi mdogo Jimbo la Liwale Luiza Mlelwa akiniandaa kumtangaza mshindi wa kigi cha ubunge Jimboni hapo. 
Mbunge Mteule wa Jimbo la Liwale akionyesha cheti alichokabidhiwa na msimamizi wa uchaguzi mara baada ya kutangazwa rasmi. Picha na Vero Ignatus

NAIBU WAZIRI OLE NASHA AWATAKA WAHITIMU FEZA KUEPUKA VITENDO VIOVU

$
0
0
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha amewataka wahitimu wa darasa la saba katika shule ya Msingi Feza kuepuka vitendo viovu ambavyo vinaweza kukatisha ndoto zao katika maisha. 

Ole Nasha ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam katika mahafali ya 15 ya darasa la saba ya shule hiyo na kuwataka vijana hao kutambua kuwa kuhitimu katika hatua hiyo ndio mwanzo wa safari ndefu waliyonayo katika Elimu na kuwa nidhamu pekee ndio msingi wa mafanikio.

“Jamii yetu kwa sasa inakabiliwa na mmomonyoko wa maadili vitendo viovu kama vile vijana kujishirikisha katika masuala ya ngono, ulevi, matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii jihadharini navyo sana katika maisha yenu, mkijiingiza tu mtaharibu ndoto zenu mlizojiwekea na matokeo yake mtashindwa kushiriki katika jitihada za kuijenga nchi yenu,” alisisitiza Naibu Waziri Ole Nasha

Alisema Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa Sekta binasfi katika maendeleo ya Elimu nchini kwa kuwaandaa vijana kimaadili na kitaaluma ili kufikia dira ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 inayolenga kuwa na mtanzania aliyeelimika na mwenye maarifa, stadi, umahiri, uwezo na mitizamo chanya ili kuweza kuchangia katika kuleta maendeleo ya Taifa.

“Mtaona Serikali sasa imefuta tozo na kodi ambazo zilikuwa ni kero kwa wamiliki wa Shule binafsi kama vile Tozo ya Uendelezaji Ujuzi (Skills Development Levy-SDL), Tozo ya Zimamoto, Kodi ya Mabango na Tozo ya Usalama Mahali pa Kazi (Occupational Safety and Health Administration-OSHA) hii yote ni kuthamini mchango mkubwa ambao mmekuwa mkiutoa katika kuelimisha vijana wa Taifa hili,” aliongeza Naibu Waziri Ole Nasha.

Hata hivyo amewataka wamiliki wote wa shule nchini kutambua kuwa pamoja na shule kuwa zao wanatakiwa kufuata taratibu, sheria na kanuni katika uendeshaji wa shule hizo kwa ni bado elimu itolewayo ni mali ya umma na watoto ni wa kitanzania. 

Naye Mkurugenzi wa Shule za Feza Ibrahimu Yunus anasema kwa sasa shule hiyo ya Msingi ina jumla ya wanafunzi 770 ambapo wanaohitimu darasa la saba mwaka huu ni jumla ya wanafunzi 75 huku shule hiyo ikijivunia kufanya vizuri kwenye masuala ya Elimu katika ngazi zote zinazotolewa shuleni hapo.

Imetolewa na 
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akihutubia wakati wa mahafali ya kumaliza Elimu ya Msingi Feza yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam. Amewataka wahitimu kuwa na nidhamu, bidii na kutanguliza uzalendo katika yale watakayokuwa wakifanya ili kuweza kufikia malengo yao.
Baadhi ya Wahitimu wa Darasa la Saba katika shule ya Msingi Feza wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Mh William Ole Nasha wakati wa mahafali yao yaliyofanyika jana Oktoba 13,108 jijini Dar es salaam. 1. 
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akigawa cheti kwa mmoja wa wanafunzi aliyehitimu darasa la saba mwaka huu katika shule ya Msingi Feza wakati wa mahafali yao yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Oktoba 13, 2018.

NSSF yatakiwa kutoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Watanzania wote

$
0
0

Serikali imelitaka Shirika la Hifadhi ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii NSSF kutoa elimu zaidi kwa wananchi kuhusiana na faida za kujiunga katika hifadhi za jamii nchini. 

Hayo yameswemwa na Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Sera,Bunge,Ajira ,Vijana na Watu Wenye Ulemavu) Jenister Mhagama kwenye wiki ya Taifa ya maonesho ya wiki ya vijana yanayofanyika katika viwanja vya Tangamano mkoani Tanga ambapo amesema kuwa bado watanzania wengi hawana elimu ya kutosha kuhusiana na kujiwekea akiba ya uzeeni na faida zake hivyo NSSF inaoaswa kuhakikisha inatoe elimu hii. 

“Nawataka NSSF muhakikishe elimu hii mnaitoa ipasavyo na iwafikie watanzania wote nchini ,mwende vijijini huko muelekeze wananchi nao wapate uelewa wa hifadhi za jamii na faida zake”alisema Waziri Muhagama. Mhagama amesema kuwa NSSF ndio inajukumu sasa la kuandikisha wananchi walio kwenye sekta isiyo rasmi hivyo wahakikishe wanawafikia wananchi wengi waliopo kwenye sekta hiyo na hasa wa vijijini na kuwapatia uelewa na waweze kujiunga na kufaika na mafao yote ya NSSF. 

Kwa upande wake kaimu meneja wa NSSF mkoa wa TANGA ,Aisha Nyemba mpaka sasa wameendelea kutoa elimu kwa wananchi kujiandikisha katika mpango wa hiari ambao utawawezesha kufaidika na mafao mbali mbali ikiwemo mafao ya matibabu. Kwa mujibu wa Nyemba mpaka sasa NSSF imeandikisha vikundi vya wajasiriamali idadi ya 47 katika mpango wa hiari na wanachangia michango yao kila mwezi ambapo pia juhudi zinaendelea kuhakikisha wanafikia vikundi vingi vya wajasiriamali katika mkoa wa Tanga. 

Maonyesho haya ya Taifa ya wiki ya vijana yamefikia kilele chake oktoba 14 mwaka huu ambapo yataendana na sherehe za uzimaji wa mwenge kitaifa katika uwanja wa Mkwakwani na kuenzi miaka 19 ya kifo cha Rais wa kwanza Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. 
 Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Sera,Bunge,Ajira ,Vijana na Watu Wenye  Ulemavu) Mhe. Jenister Mhagama, akipata maelezo namna ya kujiunga na uchangiaji wa hiari katika Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa maonesho ya Wiki ya Taifa ya Vijana yanayofanyika katika Viwanja vya Tangamano Jijini Tanga 
Waziri , Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Sera,Bunge,Ajira ,Vijana na Watu Wenye  Ulemavu) Mhe. Jenister Mhagama na Naibu Waziri Mhe. Anthony Mavunde, wakipata maelezo namna ya kujiunga na uchangiaji wa hiari katika Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa maonesho ya Wiki ya Taifa ya Vijana yanayofanyika katika Viwanja vya Tangamano Jijini Tanga .

Mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota Mtwara kupatikana Usiku wa Leo

$
0
0

 Mshiriki aliyeingia wawili Bora kwenye shindano la kusaka vipaji la Tigo Fiesta Supa Nyota toka Mtwara,Mbuta The Swagz akionesha uwezo wake kwenye steji, na jioni ya leo atapanda jukwaa la Tigo Fiesta kupata mwakilishi wa Mtwara.
IMG_20181014_131134
Mshiriki aliyeingia wawili Bora kwenye shindano la kusaka vipaji la Tigo Fiesta Supa Nyota toka Mtwara,Young Ney akionesha uwezo wake kwenye steji, na jioni ya leo atapanda jukwaa la Tigo Fiesta kupata mwakilishi wa Mtwara.
IMG_20181014_133850
Majaji wakiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki waliofika tano Bora 
IMG_20181014_132216 
Msanii Farid Kubanda Fid Q(katikati) akiwa kwenye majukumu ya kufanya mchujo
IMG_20181014_120922
Meza kuu ikiwa kwenye zoezi la mchujo wa kumpata mwakilishi wa Mtwara, kutoka kushoto, Mshindi wa Tigo Supa Nyota 2017, Maarifa Mac, Adam Mchomvu, Fid Q na Edgar Mzoka a.k.a Smarter
IMG-20181014-WA0011
Wasanii wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Duka la Tigo Mtwara leo

MASAUNI ASEMA SERIKALI KUFUNGA CCTV KATIKA MIJI NA MAJIJI

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud

Serikali imesema ipo mbioni kufunga kamera maalum (CCTV camera) kwenye miji na majiji mbalimbali nchini ili kudhibiti masuala ya uhalifu ikiwemo suala la utekaji unaofanywa na watu wasiojulikana.

Aidha Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuph Masauni amewaonya wanasiasa uchwara wanaotumia matatizo yanayotokea nchini kuacha mara moja tabia za kuisema serikali, taasisi na mashirika na wakiendelea watachukuliwa hatua. Masauni aliyasema hayo mapema leo Jijini Arusha wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Murriet jijini Arusha katika ziara yake ya kukagua vituo vya Polisi ikiwemo kujua kama watuhumiwa wanapewa dhamana kwa saa 24 au la na masuala muhimu ya usalama.

Alisema kamera hizo zitafungwa kwaajili ya kubaini wale watekaji na watu wasiojulikana na kusisitiza kuwa ole wao wanasiasa wanaotumia matukio yanayotokea kwaajili ya kujipatia umaarufu wa kisiasa nchini. Alisema suala la ulinzi ni lazima lidhibitiwe haswa maeneo ya mipakani ili kudhibiti wale watu wenye nia ovu ndio maana hivi sasa mkakati wa serikali ni kufunga vifaa vya teknolojia ya kisasa zaidi.

“Hivi sasa serikali inamkakati wa kufunga kamera maalum kwaajili ya kudhibiti matukio ya kihalifu yanatokea katika miji na majiji na natoa onyo kwa wanasiasa kuacha kutumia suala la utekaji wa Mohamed Dewji kama mtaji wao waache vyombo vya dola zifanye kazi yake “ Pia alimwagiza Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha,Almachius Mchunguzi kuhakikisha anatatua changamoto za kihalifu ikiwemo kutoa dhamana kwa washitakiwa kwa makosa yanatistahili dhamana ndani ya saa 24 na kulipobgeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kupunguza uhalifu.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuph Masauni

NAIBU KATIBU MKUU KAILIMA AKABIDHIWA NYUMBA NA TANROAD KWA AJILI POLISI SIMIYU

$
0
0

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhan Kailima (katikati) akikata utepe kuashiria kupokea nyumba za makazi ya Polisi zilizojengwa na Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) mjini Bariadi Mkoani Simiyu. Katika hotuba yake mara baada ya kuzipokea nyumba hizo, Kailima aliishukuru Tanroads na kuwataka wananchi mkoani humo kuendelea kutoa taarifa za uhalifu katika maeneo yao ili kuimarisha ulinzi na usalama. Wapili kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa huo, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga, na kushoto ni Meneja wa Tanroad mkoa huo, Albert Kent.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhan Kailima akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya nyumba za makazi ya Polisi zilizojengwa na Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) mjini Bariadi Mkoani Simiyu. Kailima aliishukuru Tanroads kwa ujenzi wa nyumba hizo na pia aliwataka wananchi mkoani humo kuendelea kutoa taarifa za uhalifu katika maeneo yao ili kuimarisha ulinzi na usalama zaidi. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa huo, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga.
Sehemu ya nyumba za makazi ya Polisi Jeshi la Polisi mkoani Simiyu zilizojengwa na Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS). Nyumba hizo zilipokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhan Kailima (hayupo pichani) katika hafla ya mapokezi iliyofanyika mjini Bariadi mkoani humo. Kailima aliishukuru Tanroads kwa ujenzi wa nyumba hizo na pia aliwataka wananchi mkoani humo kuendelea kutoa taarifa za uhalifu katika maeneo yao ili kuimarisha ulinzi na usalama zaidi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MAZINGIRA BORA YA MIRADI KUIPATIA MIKOPO SEKTA BINAFSI TOKAKA KATIKA MASHIRIKA YA KIMATAIFA

$
0
0


 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwa katika Mkutano na  Mkurugenzi  Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Christine Lagarde (hayupo pichani), mjini Bali Indonesia.
2
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa pili kushoto) akiwa na Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi mbalimbali wakati wa Mkutano na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Christine Lagarde (hayupo pichani), mjini Bali Indonesia ambapo suala la mwenendo wa uchumi wa Afrika uliangaziwa.
3
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Christine Lagarde, akizitaka nchi za Afrika kuboresha uchumi,  wakati wa mkutano kati yake na Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi mbalimbali mjini Bali, Indonesia.
4
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Christine Lagarde (kushoto) akifurahia jambo wakati wa mkutano kati yake na Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za nchi mbalimbali mjini Bali, Indonesia, wakati wa kumalizika kwa mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa.
5
Viongozi wa Shirika la Fedha la Kimataifa wakiwa wamesimama  kwa muda mfupi kukumbuka maafa yaliyotokea kipindi kama hiki mwaka uliopita nchini Somalia, wakati wa  mikutano ya Benki ya Dunia (WB)  na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) mjini Bali Indonesia.
6
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Bi. Christine Lagarde, Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu wa nchi mbalimbali  wakiwa katika Mkutano mjini Bali, Indonesia .
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango mjinin Bali Indonesia)
…………………………..
Na. WFM, Bali Indonesia
Mazingira bora yakutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Sekta Binafsi kutaiwezesha sekta hiyo kupata fedha katika Mashirika ya Kimataifa ambayo yametenga bajeti kwa ajili ya kuimarisha sekta hiyo.
Hayo yameelezwa mjini Bali Indonesia na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango, baada ya kumalizika kwa  mikutano ya mwaka ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) iliyowakutanisha Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu wa nchi mbalimbali.
Dkt. Mpango alisema kuwa, yapo Mashirika ambayo yapotayari kutoa fedha iwapo kuna uhakika wakurudishwa kwa fedha hizo kama zitatolewa kwa mfumo wa  mikopo, hivyo ni vizuri mazingira ya utekelezaji miradi ya Sekta Binafsi yakaboreshwa ili kuwe na urahisi wa upatikanaji wa fedha hizo.
Alisema kuwa, nchi za Afrika ikiwemo Tanzania zinahitaji pia fedha za kuwekeza kwenye miundombinu ya kiteknolojia ili kuweza kuchochea ukuaji wa uchumi
“Kama nchi inatakiwa kuhakikisha  inaongeza mapato ya ndani ya kodi  na yasiyo ya kodi kwa kuwa jambo hilo ni moja ya kigezo chakuweza kupata fedha zaidi kutoka Mashirika ya Kimataifa”, alieleza Dkt. Mpango.
Naye Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Yamungu Kayandabila, alisema kuwa katika mikutano ya mwaka ya WB na IMF, imesisitiza kuondoa vikwazo vya kibiashara kati ya nchi na nchi  kwa kuwa biashara imekuwa na mchango mkubwa katika kukuza pato na uchumi wa nchi unategemea mahusiano mazuri kati ya taifa moja na lingine.
Dkt. Kayandabila alisema kuwa, Mataifa makubwa ikiwemo China na Marekani yanatakiwa kupunguza mvutano unaosababishwa na vikwazo vya kodi baina yao ili kutoathiri nchi ndogo ikiwemo Tanzania inayofanya biashara na nchi hizo.
Mikutano ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa imemalizika mjini Bali Indonesia kwa Mkurugenzi Mtendaji wa IMF Bi. Christine Lagarde na Rais wa Benki ya Dunia Bw. Jim Yong Kim, kukutana na Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu ambapo waliangazia mwenendo wa uchumi wa ulimwengu hasa Afrika ambayo uchumi wa baadhi ya nchi unaenda vizuri na nyingine kutofanya vizuri na kusababisha Bara hilo kuonekana uchumi wake kuonekana kukua kwa kasi ndogo.

MATUKIO KATIKA PICHA SPIKA NDUGAI AKIWA KATIKA MISA MAALUMU YA KITAIFA YA KUMUOMBEA HAYATI BABA WA TAIFA LEO JIJINI TANGA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na waumini (hawapo kwenye picha) wa kanisa kuu la Mtakatifu Antoni wa Padua Jimbo katoliki la Tanga katika Misa Maalumu ya kitaifa ya kumuombea Hayati Baba wa Taifa iliyofanyika leo tarehe 14 Octoba, 2018 Jijini Tanga.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati)akiwa katika picha pamoja na wakimbiza mwenge wa uhuru katika tukio lililofanyika leo tarehe 14 Octoba, 2018 katika uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga, katika kuzima mwenge kitaifa
Waumini wa kanisa kuu la Mtakatifu Antoni wa Padua Jimbo katoliki la Tanga wakiwa katika Misa Maalumu ya kitaifa ya kumuombea Hayati Baba wa Taifa iliyofanyika leo tarehe 14 Octoba, 2018 Jijini Tanga.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiagana na Askofu Mkuu wa kanisa kuu la Mtakatifu Antoni wa Padua Jimbo katoliki la Tanga, Anthony Banzi baada ya kumalizika kwa Misa Maalumu ya kitaifa ya kumuombea Hayati Baba wa Taifa iliyofanyika leo tarehe 14 Octoba, 2018 Jijini Tanga.
 
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (watatu kushoto) aongoza viongozi Mbali mbali wa kitaifa katika Misa Maalumu ya kitaifa ya kumuombea Hayati Baba wa Taifa iliyofanyika leo tarehe 14 Octoba, 2018 katika kanisa kuu la Mtakatifu Antoni wa Padua Jimbo katoliki la Tanga Jijini Tanga.(PICHA NA OFISI YA BUNGE

WAGONJWA WA MACHO 379 KITETO WATIBIWA BURE

$
0
0
Mkazi wa eneo la Kibaya Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, akipatiwa maelezo ya matibabu bure ya ugonjwa wa macho. 
Mganga wa macho wa hospitali ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, akimpima macho mkazi wa mtaa wa Kaloleni, Juma Ally. 
Mganga wa macho wa hospitali ya Wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara, Dk Enock Awary akimpima macho mkazi wa Kibaya, Khadija Hamis ambapo watu 379 walipatiwa vipimo na matibabu bure
Baadhi ya wananchi wa kata ya Kibaya Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, walio na matatizo ya macho wakipewa maelezo ya namna ya kupata matibabu. 


WAGONJWA wa macho 379 wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara wamepatiwa huduma ya vipimo na matibabu ya macho bure kwenye maadhimisho ya siku ya macho duniani.

Katika kuadhimisha siku hiyo wataalamu wa afya kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la ‘Kilimanjaro Center for Community Opthmology ( KCCO) kupitia mradi wa (TRACHOMA SAFE) wametoa huduma ya kupima macho, ushauri, kutoa dawa sambamba na kuwapangia tarehe ya kurudi kwa ajili ya uchunguzi zaidi na upasuaji wagojwa ambao wameonekana kwamba matatizo yao ya macho yanahitaji upasuaji.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Mganga mkuu wa wilaya ya Kiteto Dkt Malkiadi Paschal Mbota alisema ugonjwa wa Trakoma ni tatizo kubwa na idara ya Afya kwa kushirikiana na KCCO wamekuwa wakienda katika maeneo yote ya vijijini kutoa hudumaza ushauri, dawa, upasuaji, kutoa elimu juu ya umuhimu wa kusafisha uso kwa maji safi pamoja na usafi wa mazingira kwa ujumla kwa lengo la kutokomeza ugonjwa huo.

Dkt Mbota alitoa wito kwa jamii, hususani jamii ya kifugaji kujenga tabia ya kunawa uso kwa maji safi mara kwa mara ili kuepuka ugonjwa wa Trakoma. “Mikakati ya wilaya katika kukabiliana na ugojwa huo, kwa kushirikiana na KCCO tumekuwa tukienda kijiji hadi Kijiji kuwatambua wagonjwa na tukishawatambua, madaktari wetu na manesi wamejengewa uwezo wa kutosha kuwapatia huduma zote zinazotakiwa ikiwemo upasuaji, wanaweka mahema hukohuko vijijini wanawafanyia upasuaji,” alisema.

Daktari wa macho wa hospitali ya wilaya ya Kiteto, Dkt Enock Thomas Awary alisema wamejipanga kuhudumia watu wote watakaofika uwanjani hapo kwa lengo la kupata huduma za matibabu ya macho, na wale ambao hawatakuwa wamefikiwa, huduma hiyo itaendelea hadi mwisho wa wiki. 

Dkt Awary alisema huduma wanazotoa ni bure, hivyo watu wote wenye matatizo ya macho wasiache kufika ili wapate huduma hiyo itafika hadi vijijini. Alisema wameandika barua kwa waganga wafawidhi wa vituo vya afya na zahanati zote kuwaelekeza utaratibu, kuhakikisha watu wote wanaohitaji huduma wanafikiwa na huduma hiyo.Mratibu wa mradi wa Trakoma Mkoa wa Manyara, Agnes Lukumay alisema lengo la KCCO kufadhili utoaji wa huduma hizo za matibabu ya macho katika maadhimisho ya siku ya macho duniani ni kuzuia upofu unaozuilika.

Lukumay alisema takwimu zinaonyesha kuwa kwa mkoa wa Manyara ugonjwa huo uko juu zaidi kwa wilaya za Kiteto na Simanjiro.Alitoa wito kwa jamii kujitokeza kupata huduma hizo za matibabu ya macho kwa sababu zinatolewa bure, hivyo wasiache fursa hiyo iwapite.Shirika la Kilimanjaro Center for Community Opthmology’ limeanza kazi zake mwaka 2015, huku mkataba wake ukiwa ni wa miaka mitano. 

Dhima ya shirika hilo ni kutokomeza ugonjwa wa Trakoma ifikapo 2020.

Hadi sasa shirika limeshahudumia kwa kuwafanyia upasuaji wa macho wagonjwa wa Trakoma 600.

Katika maadhimisho hayo wagonjwa 379 wamefika uwanjani hapo kwa lengo la kupata matibabu, ambapo wagonjwa 205 wamehudumiwa na wengine waliobaki wanaendelea kuhudumiwa hadi mwisho wa wiki.

TANESCO YAADHIMISHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE KWA KUPANDA MITI ELFU KUMI (10,000)

$
0
0
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba, Naibu Meya wa Manispaa ya Mji wa Moshi, Mhe. Jombo Koyi, (watatu kushoto), na Mbunge wa Viti Maalum (Vyuo Vikuu), Mhe. Esther Mmasi. (wane kushoto), wakiwa wamebeba miche ya miti na baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Kilimanjaro wakiongozwa na Meneja wao Mhandisi Mahawa Mkaka (wasita kushoto), wakati wa zoezi la upandaji miti Mkoani humo leo Oktoba 14, 2018 
NA SAMIA CHANDE, KILIMANJARO

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeungana na Watanzania katika kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 19 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kupanda miti elfu kumi (10,000) mkoani Kilimanjaro.

Sambamba na upandaji huo wa miti, TANESCO pia imetoa elimu ya uhifadhi wa mazingira ikiwa ni pamoja na kutunza miundombinu ya Shirika hilo ambayo imekuwa ikiathiriwa mara kwa mara na  Miti inayopandwa jirani na miundombinu ya umeme.
Kampeni hiyo ya upandaji miti ilizinduliwa rasmi leo Oktoba 14, 2018.na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Kippi Warioba ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi katika shule ya Msingi Muungano katika Manispaa ya Mji wa Moshi.
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo ya kupanda miti, Mhe.Warioba aliipongeza TANESCO  kwa jitihada zake za dhati za kuungana na wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro katika kutunza mazingira kwa kupanda miti katika wilaya za Moshi, Rombo, Same, Mwanga, Hai na Siha lakini pia kuelimisha wananchi umuhimu wa kutunza mazingira kwa kupanda miti.  
Aidha Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa, aliitaka TANESCO kuendelea kutoa elimu ya upandaji miti ili wananchi waelewe maeneo sahihi ya kupanda miti bila kuathiri miundombinu ya umeme.
 “Ni wajibu wa kila mwananchi kujenga utamaduni wa kutunza mazingira, kwa kupanda miti hususan ya matunda, kwani utafaidi kivutli, matunda na wakati huo huo unakuwa umetunza mazingira.” Aliasa Mhe. Kipi Warioba.
Kwa upande wake Menja wa TANESCO Mkoa wa Kilimanjaro. Mhandisi Mahawa Mkaka akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka alisema kuwa zoezi hilo linalengo la kuelimisha wananchi maeneo  sahihi ya kupanda miti ambayo hayaingiliani na miundombinu ya umeme ili kuepusha madhara mbalimbali kama vile ajali za umeme na upotevu wa umeme pia na uhifadhi wa mazingira.
Mhandisi Mkaka alisema TANESCO ina misongo mbalimbali ya umeme hivyo wananchi wanapaswa kuzingatia sheria inayotaka shughuli za kijamii ikiwemo upandaji wa miti zifanyike umbali wa mita mbili na nusu kutoka kwenye miundombinu ya umeme hii itapunguzi tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara.
Zoezi hil la upandaji miti lilifanywa na wafanyakazi wa TANESCO Mkoani Kilimanjaro na kuhudhuriwa na Mbunge wa viti maalum Bi. Ester Mmasi anae wakilisha Vyuo Vikuu na Naibu Meya Manispa ya Moshi Mhe. Jomba Koyi.
TANESSCO inategemea kutekeleza zoezi hili la upandaji miti nchi zima ili kuhakikisha jamii inapata elimu ya jinsi ya upandaji miti na pia utunzaji wa miundombinu ya umeme, alisema Mhandisi Mkaka kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba, akifanya maandalizi ya kupanda mti leo Oktoba 14, 2018
Meneja wa TANESCO Mkoani Kilimanjaro Mhandisi Mahawa Mkaka akimkabidhi zawadi ya mche wa Matunda  Kaimu Mkuu wa Mkoa Kippi Warioba
Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Kilimanjaro, wakipanda miti leo Oktoba 14, 2018.
 Mbunge wa Viti Maalum (Vyuo Vikuu), Mhe. Esther Mmasi, akimwagilia mti alioupanda.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Mahawa Mkaka, akizungumza wakati wa tukio hilo.

KAMARADI BASHIRU ALLY KATIBU MKUU WA CCM AONGOZA UJUMBE WA VIONGOZI WA CCM KATIKA ZIARA YA KIMKAKATI NCHINI CHINA

$
0
0

Ujumbe wa Viongozi wa CCM umeondoka leo kuelekea nchini China kwa ziara ya kimkakati inayolenga kuongeza mahusiano kati ya CCM na Chama Cha Kikomunisti cha Watu wa China (CPC), Kamaradi Bashiru Ally Katibu Mkuu wa CCM anaongoza ujumbe huo.

Akizungumza kabla ya kuanza safari Kamaradi Bashiru ameelezea safari hiyo kwamba ni ya kimkakati na inalenga kuimarisha mahusiano kati ya CCM na CPC. Aidha amesisitiza safari hiyo pamoja na mambo mengine ujumbe wa viongozi hao utakwenda kubadilisha uelewa, uzoefu na kujifunza mikakati ya kujitegemea kirasilimali ili kuendesha Chama, namna bora na bunifu ya kuendesha Miji na Majiji nchini na namna bora ya kujenga mahusiano kati ya Chama na Serikali katika kutoa maendeleo kwa watu.

Ujumbe wa Chama Cha Mapinduzi umejumuisha kwa uwakilishi viongozi wa Chama Taifa ikiwamo wajumbe wa Baraza la Wadhamini, Jumuia za Chama, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Wajumbe wa Bodi za Kampuni za Chama na Maafisa wa Chama kutoka Ofisi Ndogo ya Makao Makuu. Chama Cha Mapinduzi katika ujumbe huu kimejumuisha maafisa wawili wa Serikali ili nao wakajifunze kama sehemu ya ujumbe huo.

Ujumbe wa CCM utakuwa Nchini China kwa siku 10 na utakuwa na fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali wakiangazia fursa za mashirikiano na uwekezaji kwa maslahi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Taifa.

Wakati uo huo Kamaradi Bashiru ametumia nafasi hiyo kuwashukuru kwa dhati watanzania wakaazi wa Wilaya ya Liwale na Jimbo la Liwale kwa uchaguzi mzuri uliokamilika kwa Amani na usalama na kukiwa na idadi kubwa ya wananchi waliojitokeza kupiga kura ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mgombea wake Zuberi Kuchauka kimeibuka na ushindi wa kishindo.

Huu ni muendelezo wa mikakati ya kukuza mahusiano ya kimataifa, diplomasia ya siasa na uchumi kwa manufaa ya nchi yetu Tanzania.

Imeandaliwa na Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na Idara ya Itikadi na Uenezi na,

KIDUMU CHA CHA MAPINDUZI
Imetolewa na,
 
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Muhimbili Waungana na Watanzania Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere

$
0
0




Wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Hospitali ya Rufaa ya Musoma wakiwa katika kaburi la Baba wa Taifa baada ya kumuombea leo ikiwa ni siku ya kumbikizi yake ambayo hufanyika Oktoba 14 kila mwaka.
Baadhi ya wananchi wakielekea katika eneo la kumuombea Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Kijiji cha Mwitongo mkoani Mara.
Baadhi ya wataalam wa Hospitali ya Rufaa Musoma na Muhimbili wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuelekea kwenye nyumba ambako Baba wa Taifa alikuwa akipumzika enzi za uhai wake na wakati mwingine kukutana na wageni wake.
Dkt. Brighton Mushengezi akiwa katika Makumbusho ya Hayati Mwalimu Nyerere yaliopo kwenye Kijiji cha Mwitongo, Butihama mkoani Mara.
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye maadhimisho hayo leo.
Wataalam wakiwa katika sebule ambako Hayati Mwalimu Nyerere alikuwa akipumzika na Mama Nyerere.
Pichani ni Jengo la Makumbusho ya Hayati Mwalimu Nyerere.

………………………..

Wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) walioko Hospitali ya Rufaa Musoma mkoani Mara wameungana na Watanzania kuazimisha kumbukizi ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Butihama mkoani hapa.

Wataalam hao leo wametembelea Kijiji cha Mwitongo ambako Mwalimu Nyerere amehifadhiwa na kupatiwa maelezo mbalimbali kuhusu histoaria yake. Katika maadhimisho hayo wananchi mbalimbali wamejitokeza wakiwamo wanafunzi, watalam wa afya Muhimbili na kufanyika kwa ibaada ya kumuombea Baba wa Taifa.

Baada ya wataalam hao kushiriki kwenye kumbukizi ya Hayati Mwalimu Nyerere leo, kesho Jumatatu (tarehe 15, 2018) wanaendelea kutoa huduma mbalimbali matibabu kwa wakazi wa mkoa huo na mikoa ya jirani kwa njia ya mkoba pamoja na kujenga uwezo kwa wataalamu wa Hospitali ya Rufaa ya Musoma.

Mwalimu Nyerere alifariki dunia Oktoba 14, mwaka 1999 katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas nchini Uingereza ambako alikwenda kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Madaktari walieleza kwamba kifo chake kilisababishwa na ugonjwa wa saratani ya damu.

Oktoba 14 kila mwaka imefanywa kuwa siku maalam ya kitaifa ili kutoa nafasi ya kumkumbuka na kutafakari mema na mazuri aliyoyafanya enzi za uhai wake.

ARUMERU YAMUENZI MWALIMU NYERERE

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro Leo amewaongoza waumini wa Kanisa la kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Meru Usharika wa MARUVANGO katika Mtaa wa Maruvango katika ibada ya Kuadhimisha miaka 19 ya Kifo Cha Baba wa Taifa hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere 
1
Katika Ibada hiyo pia Mhe Muro aliendesha Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la MARUVANGO na kufanikiwa Kuchangisha Jumla ya Shilingi Milioni 28,331,500 Fedha zilizopatikana Kutokana na Ubunifu na Hamasa ya Mkuu wa wilaya ya Arumeru ambae alilazimika kufanya kazi ya Ziada ya kuhamasisha wananchi na kufikia Malengo.
2
Katika Ibada Hiyo Dc Muro amewataka wananchi wa Arumeru kumuenzi Mwalimu Kwa kuzingatia misingi ya Umoja na Amani ya Nchi, Dc Muro amesema katika Uhai wake Mwalimu Nyerere alipinga vitendo vya Rushwa na Ufisadi, uonevu, ukandamizaji wa Haki za Msingi za wananchi haswa Kina Mama na watoto , Mwalimu Nyerere alisisitiza matumizi bora ya Ardhi ambapo Kwa wilaya ya Arumeru Bado Migogoro ya Ardhi imeendelea kuwa changamoto hatua ambayo imemlazimu Dc Muro kuomba viongozi wa Dini kuendelea kuiombea Wilaya ya Arumeru kuepukana na Migogoro ya Ardhi.
3
Katika Mahubiri yake , Mchungaji wa Usharika Mchg Aminiel Mwenda amesema Kanisa litaendelea kumuenzi Mwalimu Nyerere Kwa kuwasisitiza wananchi kuacha Vitendo viovu vya rushwa , ufisadi, dhuluma na Chuki , ambapo amesema Katika utawala wa awamu ya tano chini ya Mhe , Rais, Dkt. John Pombe Magufuli umeanza kurudisha Mwelekeo na Matendo ya utawala wa Mwalimu Nyerere Kwa kukomesha vitendo vya Rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali ZA nchi ambapo amemuomba Mhe Magufuli kuendelea na jitahada zake za kuitengeneza Tanzania Mpya ya viwanda na yenye uchumi wa kati.
4
Katika Harambee hiyo Dc Muro alialika marafiki, ndugu na Jamaa wanaoishi Arumeru na kutoka katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Dar es Salaam na ARUSHA akiwemo Bw Richard Kashaija kutoka Dar es Salaam ambae ameoa Arumeru.#ArumeruYetu #WakatiWetu #NyerereWetu

SHANGWE ZA HAFLA YA TBL KUMKARIBISHA SAMUEL ETO'O JIJINI DAR

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na Rais wa kitengo cha Masoko cha ABINBEV kanda ya Afrika Mashariki, Roberto Jarrin (Kushoto) akibadilishana mawazo na Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Barcelona na timu ya Taifa ya Cameroon, Samuel Eto’o.
 Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na Rais wa kitengo cha Masoko cha ABINBEV kanda ya Afrika Mashariki, Roberto Jarrin (Kushoto) akibadilishana mawazo na Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Barcelona na timu ya Taifa ya Cameroon, Samuel Eto’o ( Katikati) wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na TBL jijini Dar es Salaam, Eto’o alikuja nchini kwa udhamini wa Castle Lager kuzindua mradi wa ujenzi wa uwanja wa 5-A Side utakaojengwa katika maeneo ya Oysterbay jijini Dar es Salaam, Kulia ni Meneja chapa wa bia ya Castle Lager . Pamela Kikuli
 Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Barcelona na timu ya Taifa ya Cameroon, Samuel Eto’o , akipongezana na Meya wa Kinondoni Benjamini Sitta ,(Kushoto) wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na TBL jijini Dar es Salaam, wa pili kulia ni : Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na Rais wa kitengo cha Masoko cha ABINBEV kanda ya Afrika Mashariki, Roberto Jarrin, Meneja chapa wa bia ya Castle Lager , Pamela Kikuli ( Kulia) na Meneja Udhamini na Mawasiliano ya wateja wa TBL, David Tarimo (wa pili kushoto).
Eto’o akifurahi na wageni waalikwa.Baadhi ya wafanyakazi wa TBL katika picha ya pamoja na Eto’o wakati wa hafla hiyo

Mesen Selekta na Gutta Wapagawisha Tigo Fiesta -Vibe Kama Lote Mtwara

$
0
0


 Msanii Mesen Selekta na Gutta wakionesha uwezo wao wa kutawala jukwaa kwenye Tamasha kubwa la Tigo Fiesta -Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa Nang’wanda Mjini Mtwara usiku wa kuamkia Jumatatu
Supa Nyota Siraji Mbuta
Mshindi atakayeiwakilisha Mtwara kwenye kinyang’anyiro cha kumsaka Tigo Fiesta Supa Nyota, Siraji Mbuta a.k.a Mbuta The Swagx akionesha uwezo wake kwenye jukwaa la Tigo Fiesta usiku wa kuamkia jumatatu.
Bright
Msanii Bright akionesha uwezo wake wa kutawala jukwaa kwenye Tamasha kubwa la Tigo Fiesta -Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa Nang’wanda Mjini Mtwara usiku wa kuamkia Jumatatu
Chege
Msanii Chegge akionesha uwezo wake wa kutawala jukwaa kwenye Tamasha kubwa la Tigo Fiesta -Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa Nang’wanda Mjini Mtwara usiku wa kuamkia Jumatatu
Lulu Diva
Msanii Lulu Diva akionesha uwezo wake wa kutawala jukwaa kwenye Tamasha kubwa la Tigo Fiesta -Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa Nang’wanda Mjini Mtwara usiku wa kuamkia Jumatatu
……………………………
Msanii Jerry Boniface maarufu kama Mesen  Selekta akishirikiana na mdogo wake Gutta waliweza kuwapagawisha mashabiki kwa mtindo wao Singeli.
Msanii huyo alidhihirisha ubora wake uliopelekea uwanja kutimka vumbi kwa nyimbo zake za Kinanda, Kanyaboya, Dab Singeli na nk.

Mji wa Mtwara ulikuwa tofauti na miji mingine kutokana na wasanii kuimba pamoja na mashabiki.
Akizungumza na waandishi wa habari Mesen Selekta alisema ” Hii inanipa mzuka kwa mashabiki kuukubali muziki wangu, nimeona jinsi shangwe la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote walivyolipokea wana Mtwara”.

Msanii mwingine aliyeiteka Mtwara alikuwa Farid Kubanda Fid Q aliwaamsha kwa wimbo wake Fresh, ambao aliurudia mara mbili kutokana na kiu ya mashabiki.

Kivutio kingine kilikuwa kwa MaDj  Zero na Mafuvu waliweza kupiga mziki kwa zamu kama kwa kushindana hii iliweza kuleta ladha na Vibe la aina yake kwa mashabiki.

Kila Tamasha linapopita utafutwa msanii Chipukizi kupitia shindano la kusaka vipaji vya wasanii maarufu Kama Tigo Fiesta Supa Nyota, na kwa mkoa huo msanii, Siraji Mbuta kwa jina la kisanii Mbuta The Swagx aliibuka kidedea kuwakilisha mkoa huo kwenye fainali mwezi ujao.

Kwa upande wa wadhamini Kampuni ya Tigo, Meneja wa Kanda ya Pwani, John Tungaraza alisema ‘Mbali na muziki, wateja wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi mara mbili ya thamani kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia *147*00#. 

Promosheni ya Data Kama Lote itahakikisha kuwa mashabiki wanaweza kufuatilia habari na matukio yote ya msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote; au kufurahia kuperuzi kwenye mtandao wenye kasi zaidi wa 4G+,’ Tungaraza alisema.

Wateja wote wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi TSH 10 millioni, zawadi za kila wiki za TSH milioni moja, ama zawadi za kil asiku za TSH 100,000 kwa kushiriki katika shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo. Ushiriki katika shindano hilo unapatikana kwa kutuma neno MUZIKIkwenda 15571 au kwa kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz.

Walioshusha vibe kama lote mjini Mtwara ni pamoja na kundi la Rostam (Roma and Stamina), Fid Q, Zaid na Weusii (Joh Makini, Niki wa Pili na G-Nako) ambao walikonga mioyo ya wapenzi wa muziki mjini Songea pia. Wengine ni wasanii wa bongo flava Mesen Selekta na Foby, wakongwe Chegge, Barnaba na Mr Blue, pamoja na akina dada Ruby na Lulu Diva.

TIketi za Tigo Fiesta 2018 – zitakuwa zinapatikana  kupitia Tigo Pesa Masterpass QR kwa kupiga *150*01#, kuchagua namba 5 (lipia bidhaa), na kuchagua namba 2 (lipa kwa Masterpass). Tuma kiasi husika  kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.
Ijumaa ijayo Vibe litahamia Moshi Mjini

MANGULA- AZINDUA KAMPENI ZA CCM JANG’OMBE Z’BAR

$
0
0


 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Tanzaia Bara Ndugu Philip Mangulla(katikakati)akimkabidhi bendera ya CCM Mgombea wa nafasi ya Uwakilishi katika uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Jang’ombe ndugu Ramadha Hamza Chande(wa kwanza kushoto) akiwa amesindikizwa na Mbunge wa Jimbo hilo ndugu Ali Hassan King( wa kwanza kulia), katika uzinduzi wa kampeni za CCM katika Jimbo hilo.
DSC_0335
MBUNGE wa Jimbo la Jang’ombe Ndugu Ali Hassan King(kulia) akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwa niaba ya CCM Mgombea wa nafasi ya Uwakilishi katika Jimbo hilo Ndugu Ramadhan Hamza Chande(kushoto), makabidiano hayo yamefanyika mbele ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Philip Mangulla.
DSC_0347
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Tanzaia Bara Ndugu Philip Mangulla(katikakati) akimkabidhi Katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la 2017, Mgombea Uwakilishi wa CCM ndugu Ramadhan Hamza Chande katika Mkutano wa Hadhara wa uzinduzi wa Kampeni za CCM uliofanyika katika uwanja wa Mwembe Matarumbeta uliopo katika Ofisi za CCM jimbo la Jang’ombe.
DSC_0292
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ akizungumza katika mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi Mdogo wa CCM Jimbo la Jang’ombe Zanzibar.
DSC_0393
MGOMBE wa CCM nafasi ya Uwakilishi Jimbo la Jang’ombe akizungumza na kuomba kura kwa Wana-CCM mara baada ya kukabidhiwa miongozo na vitendea kazi vya CCM ambavyo ni Ilani ya Uchaguzi, Katiba ya CCM na Bendera ya CCM mara baada ya kunadiwa na kuombewa kura na viongozi mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi.
DSC_0249
WANACHAMA wa CCM waliohudhuria katika Mkutano huo wakishangilia mara baada ya kupandishwa mgombea uwakilishi wa CCM katika Jimbo hilo.
DSC_0216
MBUNGE wa tiketi ya CCM jimbo la Ukonga,Mwita Waitara akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni za CCM uchaguzi wa Jimbo la Jang’ombe Zanzibar.     
……………………….
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
MAKAMU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangulla amesema CCM inaimarika kisiasa huku Vyama vya upinzani vikiendelea kukosa mvuto ambapo Wabunge na Madiwani wao wanajiunga na CCM kwa nia ya kunufaika na Demokrasia iliyotuka.  

Mwanasiasa huyo mkongwe katika Bara la Afrika na Tanzania kwa ujumla, alibainisha kuwa upinzani umekwisha poromoka na kukosa ridhaa ya kuaminiwa mbele ya Wananchi, jambo linaloifa CCM iendelee kutamba na kuonekana mahili na kinara wa Siasa za maendeleo.

Alisema katika kipindi cha Oktoba mwaka huu Wabunge wa nne  wamekwishavihama vyama vyao hivyo vya upinzani na kujiunga na CCM.
Kauli hiyo ameitoa leo  wakati akizindua rasmi kampeni  za uchaguzi mdogo jimbo la Jangombe katika uwanja wa Mwembe Matarumbeta mjini Unguja ambapo alisema wapo watu wanaosema wabunge hao wananunuliwa lakini ukweli ni kuwa si hivyo.

Alisema aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Liwale ambaye alikuwa CUF, aliulizwa na uongozi wa CCM sababu ya kujiunga na chama ambapo alidai kuwa alikuwa akipata tabu sana wakati wa utekelezaji wake wa maendeleo ya jimboni kwake.
Katika maelezo yake alisema wananchi wanakikubali chama cha CCM lakini jambo lilokuwa linampa tabu ni mipango ya utekelezaji wa ahadi zake ambapo yote ambayo yanafanyika ni kutokana na ilani ya CCM.

“CCM ina historia kubwa na tumekuwa tukitatua shida za wanchi bila ubaguzi, na ndio maana hata viongozi wa Vyama vya upinzania wanajivua uanachama na kujiunga na CCM.”, alisema.Mbali na hilo, alisema katika uchaguzi huo wa jimbo la Jang’ombe wana-CCM wako 8000 huku wapinzani wakiwa 2500 hivyo ni dhahiriushindi ni wa CCM kinachotakiwa ni kuwa ni wanachama kuwashawishi wapinzani kukiunga mkono katika uchaguzi wa Oktoba 27 mwaka huu.

“Ninampongeza Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa kuifanya Zanzibar kuwa na hali ya utulivu na kutokuwa na vurugu hiyo inaonesha kuwa wapinzani ndio wenye vurugu baada ya kususia uchaguzi kwakutoshiriki.Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa upande wa Zanzibar inatekelezwa kwa ufanisi mkubwa na kila tukija katika Visiwa hivi maendeleo tunayaona”alisema.Alisema kwa sasa Baraza la Wawakilishi liko shwari na mambo yote yanakwenda ambapo watu wanajadili kwa hoja maendeleo ya nchi na si kama awali ilivyokuwepo.

Aliwasisitiza wanachama wa CCM na Wananchi kwa ujumla kufanya maamuzi sahihi ya kumchagua Mgombea wa CCM Ramadhan Hamza Chande , ili aweze kuendeleza maendeleo na kutatua kero zitakazojitokeza ndani ya Jimbo hilo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Zanzibar Dk.Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar ,Dk Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ alisema uchaguzi huo mdogo wa jimbo wa Jangombe ni wa kujitathmni na kujipima kuelekea 2020.

 Alisema ni wakati sasa wana-CCM kuungana kwa pamoja na kujitokeza kwa wingi kwenda kuipigia kura CCM Oktoba 27 mwaka huu na kwamba mgombea huyo ana sifa zote zinastahili kuwa mgombea.“Ramadhani Hamza Chande ana sifa na vigezo vyote vya kuiongoza Jang’mbe hadi kufikia mafanikio ya kuwa Jimbo la mfano kwa maendeleo kwani bado ni kijana pia ana upeo na fikra za mikakati ya maendeleo.Kwa upande wake Mbunge wa tiketi ya CCM jimbo la Ukonga,Mwita Waitara alisema kupitia uchaguzi huo mdogo lazima CCM ioneshe kuwa upinzani umekufa kwa upande wa Zanzibar.Aliongeza kuwa ni wakati sasa wanajangombe kutoleta virusi katika Baraza la Wawakilishi ambapo ndio wenye kuleta vurugu kwenye utendaji mzuri wa baraza hilo.

Katika maelezo yake Mbunge Waitara aliongeza kuwa muungano wa vyama vya upinzani UKAWA ni wajanja na wezi kutokana na kuwa  wao wanapinga kila kitu hata kama maendeleo yanafanyika.Waitara alisema vyama vya upinzani havitaki amani wala maendeleo na badala yake wanaleta vurugu hivyo uchagui huo lazima  CCM ioneshe kuwa upinzani wa CUF umekufa. Waitara alisema katika chaguzi zote ndogo CCM imeshinda kwa  kishindo hivyo kwa upande wa Zanzibar jimbo la Jangombe ushindi ni lazima kutokana na kuwa upinzani umeshakufa.

Naye Mwenyenkiti wa CCM,mkoa wa Mjini Talib Ali Talib,alisema uchaguzi  huo wa jimbo la Jangombe unatokana na uamuzi wa CCM  kufanya mabadiliko ya viongozi katika jimbo la Jangombe ambapo imemuondoa kiongozi ambaye ni Mwakilishi wa jimbo hilo na kuamua kumweka kiongozi mwingine.
Alisema CCM katika kampeni hiyo itashinda na kwamba ni kawaida kwa chama kushinda uchaguzi wowote kutokana na utendaji wake mpya wa chama chini ya viongozi wake makini.

Mwenyekiti huyo alisema Oktoba 27 mwaka huu wana-CCM wajitokeze wakampigie kura mgombea wa chama na kwamba ushindi utakaopatikana utakuwa wa asilimia kubwa kutokana na wanajangombe kuwa na uzoefu wa uchaguzi na haijawai kuchukuliwa na upinzani.Naye Mgombea wa jimbo hilo la Jangombe Hamza Ramadhani Chande  aliwahahidi wananchi wa jimbo hilo kutekeleza ilani ya  CCM kwa vitendo na kwamba bila ya kuwepo kwa ubaguzi.

Alisema atashirikiana na wananchi wote kwa makundi ya vijana wanawake na wanafunzi wa vyuo vikuu kwa kujadiliana katika kutekeleza ilani hiyo kwa upande wa afya, elimu, miundombinu na vikundi vya Ujasiriamali.
“Nakuombeni mnipe kura hakika sitokuangusheni bali nitashirikiana nanyi na kutumia uwezo wangu kuhakikisha Jang’ombe inaendelea kuwa imara kimaendeleo katika sekta zote.

Pamoja na hayo aliongeza kuwa atabuni mikakati mbadala katika ya kuhakikisha kila changamoto itakayojitokeza inatafutiwa ufumbuzi wa kudumu kwa haraka kabla haijaleta madhara kwa jamii.

Wadau wataka Kiswahili kitumike kama Lugha ya Kufundishia

$
0
0







Na Shamimu Nyaki – WHUSM

Wadau mbalimbali wameishauri Serikali kufikiria namna ya kutumia lugha ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia shuleni ili kukuza na kuendeleza lugha hiyo ambayo ndio utambulisho wa Taifa letu.

Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dodoma katika Mdahalo wa Kumbukizi ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius K.Nyerere uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha ST.Jonhs of Tanzania ambapo mada mbalimbali ziliwasilishwa na kujadilia na washiriki.

Awali Mhe.Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Mwakyembe akifungua mdahalo huo alisema kuwa lugha ya Kiswahili ndio lugha kuu ya mawasiliano hapa nchini na ndio lugha inayowatambulisha watanzania Ulimwenguni. “Kiswahili hivi sasa ni lugha kubwa sana duniani na inazungumzwa na watu wengi hivyo ni lazima watanzania wakawa mstari wa mbele kukikuza na kukiendeleza kwa kukizungumza kwa ufasaha”.Alisema Dkt Mwakyembe.

Aidha Dkt. Mwakyembe amemuagiza Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw.Godfrey Muingereza kuhakikisha kuwa katika mashindano yajayo ya ulimbwende washiriki wanatumia lugha ya Kiswahili katika mashindano ya ndani na watakapoiwakilisha nchi kimataifa.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Susan Mlawi ameongeza kuwa mdahalo huo ni muendelezo wa Kampeni ya Uzalendo na Utaifa inayotarajiwa kufikia kilele chake Disemba 08 mwaka huu ambapo itatanguliwa na matukio tofauti kiwemo Mijadala,makongamano na nyimbo mbalimbali na kauli mbiu mwaka huu ni “Kiswahili Uhai wetu,Utashi wetu.”

Pia katika mdahalo huo Kaimu Mkuu wa Chuo cha St. Johns University of Tanzania Prof.Yohana Msanjila aliiomba Serikali kuona umuhimu wa kutumia lugha ya Kiswahili katika somo la Uraia kwakua ndio somo linalozungumzia Utamaduni wa nchi pamoja na Uzalendo jinsi mtu anayoweza kuipenda na kuilinda nchi yake.

Vilevile mwanafunzi Edmund Kakoi kutoka shule ya Sekondari Dodoma alieleza kuwa ni lazima vijana kutambua kuwa luga ya Kiswahili sio lugha iliyopitwa na wakati bali ni lugha ambayo inaipa heshima nchi katika mataifa mbalimbali.

Katika mdahalo huo mada tatu ziliwasilishwa ikiwemo “Maisha na Uongozi wa Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius K.Nyerere yanavyoakisi Uzalendo na Utaifa” iliyowasilishwa na Dkt. Alfred Sebahene kutoka Idara ya Taaluma na Rushwa ya chuo hicho.

Mada nyingine “Mchango wa Lugha ya Kiswahili katika kukuza Uzalendo na Utaifa” iliyowasilishwa na Dkt. Stella Faustine kutoka Idara ya Kiswahili chuo kikuu cha Dodoma na mada ya tatu ilikua “Dhima ya Uzalendo na Utaifa katika Maendeleo ya Uchumi wa Viwanda” iliyowasilishwa na Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Dodoma.
 .Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Mwakyembe 

KAMPENI YA DCB DIGITAL YAZIDI KUPASUA ANGA

$
0
0
 Mbunge wa Kondoa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (kulia), akifurahi na Mkuu wa Masoko wa Benki ya Biashara ya DCB, Rahma Ngassa (wa pili kushoto), Meneja wa DCB Tawi la Dodoma, Joseph Njile (kushoto) pamoja na Ofisa Mikopo wa DCB Dodoma,  Nuru Ashraf, wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Jimbo la Kondoa ambapo benki hiyo ikiwa kama mdau wa maendeleo ilienda kuhamasisha wananchi wa Kondoa kujiunga na huduma yao mpya ya DCB Digital ili kupata  huduma za kibenki kwa kupitia simu ya mkononi katika hafla iliyofanyika katika Kata ya Pahi, wilayani Kondoa, Dodoma jana. Ndani ya DCB Digital mteja anaweza kujiunga na akaunti ya muda maalum (Digital FDR) , Akaunti ya malengo (Kibubu Digital Account), huduma ya Malipo ya Nusu Mshahara (Digital Salary advance) na huduma ya ATM bila kutumia kadi ya benki. Wa pili kulia ni mjumbe wa mkutano huo, Shamte Kapesa.
 Mbunge wa Kondoa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (kulia), akisalimiana na Mkuu wa Msoko wa Benki ya Biashara ya DCB, Rahma Ngassa, huku Meneja Tawi wa DCB Dodoma, Joseph Njile (kushoto) na Nuru Ashraf, Ofisa Mikopo wa DCB  Dodoma  wakiangalia, wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Jimbo la Kondoa ambapo benki hiyo kama mdau wa maendeleo ilienda kuhamasisha wananchi wa Kondoa kujiunga na huduma yao mpya ya  DCB Digital ili kupata  huduma za kibenki kwa kupitia simu ya mkononi katika hafla iliyofanyika katika Kata ya Pahi, wilayani Kondoa, Dodoma. Ndani ya DCB Digital mteja anaweza kujiunga na akaunti ya muda maalum (Digital FDR) , Akaunti ya malengo (Kibubu Digital Account), huduma ya Malipo ya Nusu Mshahara (Digital Salary advance) na huduma ya ATM bila kutumia kadi ya benki.

 Mbunge wa Kondoa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (kulia), akisalimiana na Ofisa Mikopo wa Benki ya Biashara ya DCB Tawi la Dodoma, Nuru Ashraf huku Mkuu wa Masoko wa DCB, Rahma Ngassa (wa pili kushoto) na Meneja Tawi wa DCB Dodoma, Joseph Njile (kushoto) wakiangalia, wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Jimbo la Kondoa ambapo benki hiyo kama mdau wa maendeleo ilienda kuhamasisha wananchi wa Kondoa kujiunga na huduma yao mpya ya  DCB Digital ili kupata  huduma za kibenki kwa kupitia simu ya mkononi katika hafla iliyofanyika katika Kata ya Pahi, wilayani Kondoa, Dodoma . Ndani ya DCB Digital mteja anaweza kujiunga na akaunti ya muda maalum (Digital FDR) , Akaunti ya malengo (Kibubu Digital Account), huduma ya Malipo ya Nusu Mshahara (Digital Salary advance) na huduma ya ATM bila kutumia kadi ya benki. Wa pili kulia ni mjumbe wa mkutano huo, Shamte Kapesa.
 Mfanyabiashara ndogondogo mkazi wa Kata ya Pahi wilayani Kondoa, Subira Mohamed Ngwata (kulia), akifungua akaunti ya DCB Digital kwa kutumia simu yake ya mkononi huku maofisa wa benki hiyo, Vicent Speratus (kushoto) na Chuki Jarufu wakimpa maelekezo wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Jimbo la Kondoa ambapo benki hiyo kama mdau wa maendeleo ilienda kuhamasisha wananchi  kujiunga na huduma yao mpya ya  DCB Digital ili kupata  huduma za kibenki kwa kupitia simu za mkononi katika hafla iliyofanyika Pahi, Kondoa, mkoani Dodoma. Ndani ya DCB Digital mteja anaweza kujiunga na akaunti ya muda maalum (Digital FDR) , Akaunti ya malengo (Kibubu Digital Account), huduma ya Malipo ya Nusu Mshahara (Digital Salary advance) na huduma ya ATM bila kutumia kadi ya benki.
 Meneja wa Benki ya Biashara ya DCB Tawi la Dodoma, Joseph Njile (wa pili kulia) akiwaelekeza wakazi wa Kata ya Pahi jinsi ya kujiunga na DCB Digital wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Jimbo la Kondoa ambapo benki hiyo kama mdau wa maendeleo ilienda kuhamasisha wananchi  kujiunga na huduma yao mpya ya  DCB Digital ili kupata  huduma za kibenki kwa kupitia simu za mkononi katika hafla iliyofanyika Pahi, Kondoa, mkoani Dodoma. Ndani ya DCB Digital mteja anaweza kujiunga na akaunti ya muda maalum (Digital FDR) , Akaunti ya malengo (Kibubu Digital Account), huduma ya Malipo ya Nusu Mshahara (Digital Salary advance) na huduma ya ATM bila kutumia kadi ya benki.
  Mbunge wa Kondoa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (kulia), akisalimiana na Meneja wa Benki ya Biashara ya DCB Tawi la Dodoma, Joseph Njile huku Mkuu wa Masoko wa DCB, Rahma Ngassa (wa pili kushoto) na Ofisa Mikopo wa DCB Dodoma, Nuru Ashara wakiangalia, wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Jimbo la Kondoa ambapo benki hiyo kama mdau wa maendeleo ilienda kuhamasisha wananchi wa Kondoa kujiunga na huduma yao mpya ya  DCB Digital ili kupata  huduma za kibenki kwa kupitia simu ya mkononi katika hafla iliyofanyika wilayani katika Kata ya Pahi, Kondoa mkoani Dodoma jana. Ndani ya DCB Digital mteja anaweza kujiunga na akaunti ya muda maalum (Digital FDR) , Akaunti ya malengo (Kibubu Digital Account), huduma ya Malipo ya Nusu Mshahara (Digital Salary advance) na huduma ya ATM bila kutumia kadi ya benki. Wa pili kulia ni mjumbe wa mkutano huo, Shamte Kapesa.
Mchuuzi wa mbogamboga na mkazi wa Kata ya Pahi wilayani Kondoa, Hadija Iddi (kulia) akipewa maelezo na Ofisa Mahusiano wa DCB Dodoma, Chuki Jarufu jinsi ya kujiunga na huduma ya DCB Digital  wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Jimbo la Kondoa ambapo benki hiyo kama mdau wa maendeleo ilienda kuhamasisha wananchi  kujiunga na huduma yao mpya ya  DCB Digital ili kupata  huduma za kibenki kwa kupitia simu za mkononi katika hafla iliyofanyika wilayani humo mkoani Dodoma. Ndani ya DCB Digital mteja anaweza kujiunga na akaunti ya muda maalum (Digital FDR) , Akaunti ya malengo (Kibubu Digital Account), huduma ya Malipo ya Nusu Mshahara (Digital Salary advance) na huduma ya ATM bila kutumia kadi ya benki.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU OKTOBA 15,2018

Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>