Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

MAFANIKIO TUNAYOYAPATA NI MABORESHO NA MAONI YA WATEJA - NMB

$
0
0

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya NMB, Omari Mtiga akimkabidhi cheti maalum Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Chasco Traders, Sando Chasco ambaye ni mteja aliyetukuka wa Benki ya NMB kwa muda mrefu sasa. Mteja huyo amepata mafanikio katika biashara yake baada ya kukuwa na huduma za kibenki za NMB, alianza kukopa shilingi 300,000 na sasa anapata mkopo wa zaidi ya milioni 100 kuendesha biashara zake.



Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya NMB, Omari Mtiga pamoja na baadhi ya wateja Benki ya NMB waliojumuika kwenye hafla ndogo ya kuwasikiliza wateja katika tawi hilo wakikata keki maalum ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.


Meneja wa NMB Tawi la Ilala jijini Dar es Salaam, Kidawa Masoud akiandaa keki maalum ya wateja kabla ya kuanza kuwalisha wateja wa NMB Tawi la Ilala walioshiriki katika hafla hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya NMB, Omari Mtiga akimlisha keki Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Chasco Traders, Sando Chasco (kulia) ambaye ni mteja aliyetukuka wa Benki ya NMB kwa muda mrefu sasa.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya NMB, Omari Mtiga (kulia) akimlisha keki mmoja wa wateja wa NMB Tawi la Ilala walioshiriki katika hafla hiyo.
Meneja wa NMB Tawi la Ilala jijini Dar es Salaam, Kidawa Masoud akiwalisha keki baadhi ya wateja wa NMB Tawi la Ilala walioshiriki katika hafla hiyo.








BENKI ya NMB imesema maboresho makubwa iliyoyafanya ni matokeo ya mirejesho kutoka kwa wateja wake. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB, Bw. Omari Mtiga alipokuwa akizungumza na Baadhi ya wateja wa Benki hiyo Tawi la Ilala ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja.

"...Maboresho makubwa tuliyoyafanya ni matokeo ya mirejesho kutoka kwa wateja wetu ambayo tumeyapokea siku za nyuma. Siku zote tunatambua na kushukuru kwa michango na maoni ya wateja wetu, ndio sababu ya kuendelea kuwa nao bega kwa bega," alisema Bw. Mtiga.

Aliongeza kuwa NMB inatambua ushindani mkubwa uliopo na itaendelea kukabiliana nao kwa kadri unavyo kua siku hadi siku. Alisema kwao ushindani wanaupenda na wanachukulia kama fursa ya kufanya vizuri zaidi. "...Ushindani ni fursa nzuri maana inatufanya kubuni bidhaa bora kulingana na mahitaji ya wateja na kufanya vizuri zaidi kwa wateja wetu."

Alisema wiki ya huduma kwa wateja tangu ilipoanza NMB imepata fursa ya kujumuika na wateja wake maeneo mbalimbali na kupata mrejesho kwa masuala mbalimbali juu ya huduma zao na ndio maana inachukulia uzito mkubwa kuzungumza na wateja na kutupa mrejesho ili kuweza kuifanyia kazi.

"...Sisi kwetu tunaiona kama fursa ya pekee kukutana na wateja na kupata maoni yao lengo likiwa ni kuboresha zaidi huduma zetu. Lakini tumekuwa tukifarijika zaidi kwani mbali na mrejesho kuna maeneo ambayo wametutia moyo kwamba tunafanya vizuri hivyo tunawaahidi kuongeza juhudi ili kusonga mbele zaidi."

Tunasema hatubweteki kwa pongezi kwani ushindani ni mkubwa nasi tuna ahidi kufanya vizuri zaidi ili kumfanya mteja afurahiye huduma zetu. Tutaendelea kuboresha na kuangalia mteja wetu anataka nini "Sisi kama taasisi tunasema kwamba tumejipanga na tuko vizuri, tunajiamini na huduma zetu kwa namna tunavyoziboresha.

"...Tunacho waahidi wateja kwa sasa ni kwamba mbali na maboresho tunayoyafanya tutaendelea kukutana nao pia kuchukua mrejesho kutoka kwao...haturidhiki na kudhani tulipofika ni hatua ya mwisho bali tunaendelea kupokea mrejesho siku zote na tunaifanyia kazi hivyo wateja wetu waendelee kutushauri kwani maoni yao ni muhimu kwetu. Tutaendelea kuwapa huduma zile wanazopenda na hata nzuri zaidi ya wanavyoamini, ushahidi wa kufanya hivyo tunao maana mambo mengi wanaotushauri tumeyafanyia kazi kwa maboresho makubwa,"

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Chasco Traders, Sando Chasco ambaye NMB imemtunuki cheti maalum kwa kuwa mteja wa mfano, alisema NMB imemtoa mbali tangu miaka ya nyuma alipoanza na mtaji wa mkopo wa chini kama lakini tatu lakini sasa anaongelea kupata zaidi ya miliomi 100 jambo ambalo anaona ni mafanikio makubwa.

"Kiujumla binafsi NMB ni benki ambayo imenisaidia sana kwani nafanya biashara hadi mikoani na matawi wa benki hiyo yapo kila mahali hivyo inanisaidia kutotembea na mzigo wa fedha hasa dunia ya leo ambapo ni hatari kutembea na fedha. Nafanya mihamala yangu yote ya kuwalipa na kulipwa na wadeni wangu kupitia benki ya NMB. Nimekuwa pia ni balozi mzuri kila ninapofanya biashara zangu kuwashauri kuitumia benki hii kwa usalama wa shughuli zao." alisisitiza mteja huo.

BALOZI KAZUNGU: NINGEPENDA NIONE TAKWIMU ZA BIASHARA, UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA KENYA ZIKIONGEZEKA

$
0
0


 Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (wa pili kushoto) akiangalia mbegu za zao la pamba zinazozalishwa katika Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance (Alliance Ginnery Ltd), kilichopo kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati alipotembelea kiwanda hicho, Oktoba 05, 2018.
PICHA C (2)
Mfanyakazi wa katika Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance (Alliance Ginnery Ltd), kilichopo kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, akitoa maelezo ya namna mbegu za pamba zinavyoandaliwa kwa Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (aliyeshika mbegu katikati), wakati alipotembelea kiwanda hicho, Oktoba 05, 2018.
PICHA D (2)
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiangalia akiangalia mbegu za zao la pamba zinazozalishwa katika Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance (Alliance Ginnery Ltd), kilichopo kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani humo, wakati ziara ya Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (wa nne kulia) kiwandani  hapo, Oktoba 05, 2018.
PICHA E (1)
Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (wa tatu kushoto) akiangalia pamba iliyochambuliwa katika Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance (Alliance Ginnery Ltd), kilichopo kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati alipotembelea kiwanda hicho, Oktoba 05, 2018 (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na (wa pili kushoto) Mkurugenzi wa Kampuni ya Alliance 
PICHA I (1)
Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (wa pili kulia) akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) wakiwa katika Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance kilichopo kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati wa ziara ya Balozi huyo kiwandani  hapo, Oktoba 05, 2018.
PICHA J
Mkurugenzi wa Kampuni ya Alliance Ginnery Ltd, Bw. Boaz Ogola ambaye ni mwekezaji kutoka Nchini Kenya(wa pili kulia), akitoa maelezo kwa  Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (katikati) katika moja ya majengo ya Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance kilichopo kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati wa ziara ya Balozi huyo kiwandani  hapo, Oktoba 05, 2018.
PICHA K
Mkurugenzi wa Kampuni ya Alliance Ginnery Ltd, Bw. Boaz Ogola ambaye ni mwekezaji kutoka Nchini kenya(kulia), akimuongoza Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu (wa pili kulia) na viongozi wengine wa mkoa wa Simiyu, kuelekea katika moja ya majengo ya Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance kilichopo kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati wa ziara ya Balozi huyo kiwandani  hapo, Oktoba 05, 2018.

Na Stella Kalinga, Simiyu.

Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Dan Kazungu amesema angependa kuona  katika kipindi chake atakachokuwepo hapa nchini akiiwakilisha nchi ya Kenya ushirikiano wa kiabishara katika Kenya na Tanzania na unaimarika na takwimu za biashara, viwanda na uwekezaji kati ya nchi hizo zikiongezeka mara dufu.

Balozi Kazungu ameyasema hayo wakati alipotembelea Kiwanda cha Kuchambua pamba cha Alliance (Alliance Ginnery LTD), kilichopo Kata ya Kasoli wilaya ya Bariadi Oktoba 05, 2018 katika ziara yake mkoani Simiyu.

Balozi Kazungu amesema ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji hususani katika viwanda, kati ya Tanzania na Kenya ukiendelea kuimarika zaidi utachangia kuongeza ajira, kuwatoa wananchi katika umaskini pamoja na kuimarika kwa uchumi wa nchi hizo pia.

 “Baada ya miaka minne kazi yangu kama ikiisha hapa, naomba nione takwimu za viwanda, biashara, uwekezaji kati ya Tanzania na Kenya zinaongezeka mara dufu, nafasi za kazi kwa watu wetu zinapatikana na watu wetu wanaondokana na umasikini; kukua kwa Tanzania kuwe ndiyo kukua kwa Kenya hilo ndiyo ombi letu” alisema Mhe. Balozi Kazungu.

Aidha, Mhe. Kazungu ametoa wito kwa  wananchi wa Tanzania na Kenya kuepuka migogoro ya kibiashara ambayo kwa namna moja au nyingine inaweza kuchangia katika kushuka kwa biashara kati ya nchi hizo, huku akiwataka waandishi wa habari kuwa makini na kijiridhisha kabla kuandika habari za kibiashara kwani zisipoandikwa kwa usahihi zinaweza kuchochea migogoro ya kibiashara.

Aidha, Balozi Kazungu amemhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kuwa atakuwa mstari wa mbele kuzungumza na wawekezaji nchini Kenya ili waje kuwekeza, ambapo amebainisha kuwa Sekta binafsi na Shirikisho la watu wenye viwanda hapa nchini wameshaanza kuzungumzia masuala hayo na wenzao wa Sekta binafsi Kenya.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthony Mtaka amemwomba Balozi Kazungu kuwaalika wawekezaji kutoka nchini Kenya na kubainisha kuwa mkoa uko tayari kutoa ardhi bure kwa wawekezaji watakaojenga viwanda vinavyojibu mahitaji ya mkoa, hususani katika kuongeza thamani ya zao la pamba, mazao yatokanayo na mifugo kama ngozi na nyama.

Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu una uwezo wa kuzalisha pamba zaidi ya kilo milioni 400 na hadi sasa umezalisha kilo milioni112 ambazo ni zaidi ya asilimia 50 ya pamba yote nchini; hivyo katika kuiongezea thamani pamba hiyo kiwanda kikubwa cha kuzalisha bidhaa zaidi ya 20 za afya zitokanazo na pamba

“Simiyu tunao uwezo wa kuzalisha zaidi ya kilo milioni 400 za pamba, mpaka sasa tumezalisha kilo milioni 112 ambazo ni zaidi ya asilimia 50 ya pamba yote inayozalishwa hapa nchini; katika kuongeza thamani ya zao la pamba, mwaka huu tutaanza ujenzi wa kiwanda kikubwa kitakachozalisha zaidi ya bidhaa 20 za afya zitokanazo na pamba, kitakachojengwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kwa kushirikiana na wadau wengine na Mkoa wa Simiyu tumetoa ardhi bure” alisema Mtaka.

 Ameongeza kuwa kipaumbele cha pili cha mkoa baada ya kujenga kiwanda hicho ni kuwa na uwekezaji katika viwanda vya nguo(textile industries) ili kupata bidhaa ya mwisho katika zao la pamba, hivyo akaendelea kutoa wito kwa wawekezaji ndani na nje ya nchi kuwekeza katika eneo hili.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Alliance Ginnery Ltd, Bw. Boaz Ogola ambaye ni Mwekezaji kutoka Nchini Kenya amesema lengo la Kampuni hiyo yenye Kiwanda cha kuchambua pamba ni kwenda katika kuongeza thamani ya zao la pamba, ili faida itakayopatikana irudi kwa wakulima kwa kuifanya pamba yao ikanunuliwa kwa bei nzuri itakayowapa motisha ya kuendelea kuzalisha zaidi.

MAJALIWA AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI KAGERA

$
0
0
*Awataka viongozi wa vyama vya ushirika wawe waaminifu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa vyama vya ushirika nchini kutumia vizuri rasimali za vyama hivyo na kwamba Serikali haitalipa deni lolote lililokopwa na vyama hivyo.
 
“Biashara ya kununua madeni yaliyokopwa na vyama vya ushirika haipo kwenye Serikali hii ya awamu ya tano, badala yake itawachukulia hatua wote waliohusika na ubadhilifu huo.”

Pia Waziri Mkuu amepiga marufuku wafanyabiashara kuwaibia wakulima kwa kununua kahawa mbichi ikiwa shambani maarufu kama butura.Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Oktoba 6, 2018) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wafanyabiashara pamoja na wadau wa zao la kahawa baada ya kuwasili mjini Bukoba kwa ajili ya ziara ya kikazi mkoani Kagera.

Waziri Mkuu amesema Serikali itachukua hatua kali kwa viongozi wa vyama vya ushirika ambao si waaminifu na wabadhilifu wa mali za ushirika.”Tunahitaji wakulima wapate fedha.”Amesema Serikali itahakikisha wafanyabiashara wote, hususani wa mazao ya kilimo wanakuwa na mfumo sahihi wa ununuzi wa mazao utakao ongeza tija kwao na kwa wakulima.

Amesema kwa sasa Serikali inataka kuondoa mfumo uliopo wa vyama vya ushirika kufanya biashara na badala yake jukumu hilo libakie kwa wafanyabiashara.Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka wafanyabiashara hao waihakikishie Serikali kwamba watanunua kahawa yote iliyopo kwa wakulima pamoja na kwenye vyama vya ushirika. Wafanyabiashara wameridhia kununua kahawa yote.

Awali, Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba alisema katika msimu wa mwaka huu jumla ya kilo 3,000,464 za kahawa isiyokobolewa na kilo 8,191,86 za kahawa safi bado hazijanunuliwa.Dkt. Tizeba alisema kahawa iliyobakia katika maghala ya vyama vya ushirika ni kama ifuatavyo, chama cha KCU (1990) kina kilo 1,1513 za kahawa isiyokoborewa na kilo 1,936, 367 za kahawa safi.

Pia chama cha KDCU kina kilo 6,012,840 za kahawa safi, Ngara Farmers C.S Ltd kina kilo 592,354 za kahawa isiyokobolewa na kilo 192,660 za kahawa safi.“Nkwenda AMCOS ina kilo 175,553 za kahawa maganda na kilo 50,000 za kahawa safi na Magata AMCOS kina kilo 433,634 za kahawa safi.”

Alisema vyama vya ushirika vinakabiliwa na changamoto ya kiwango kidogo cha kahawa kinachonunuliwa mnadani na wakati mwingine kutonunuliwa kabisa. Hali hii inatokana na kushuka kwa bei katika soko la dunia.Alisema changamoto nyingine ni kuwepo kwa taarifa za upotoshaji kwa wakulima kutoka kwa walanguzi za kuzuia wakulima kukusanya kahawa yao kupitia Vyama vya Ushirika vya Msingi kwa wao watanunua na kuwapatia bei nzuri.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, OKTOBA 6, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kizungumza na wafanyabiashara wa zao la kahawa kwenye ukumbi wa ELCT mjini Bukoba, Oktoba 6, 2018. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba, kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage na wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kizungumza na wafanyabiashara wa zao la kahawa kwenye ukumbi wa ELCT mjini Bukoba, Oktoba 6, 2018. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba, wanne kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijhage na watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali, Marco Elisha Gaguti wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Bukoba kuanza awamu ya pili ya ziara ya mkoa huo itakayodumu kwa siku nne, Oktoba 6, 2018. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama Ngoma ya kikundi cha Kakau Band wakati walipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba kuanza awamu ya pili ya ziara ya mkoa huo itakayochukuwa siku nne, Oktoba 6, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma bango lenye malalamiko ya mmoja wa wananchi wa Bukoba wakati alipowasalimia wananchi kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba baada ya kuwasili kwa ziara ya siku nne mkoani humo, Oktoba , 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti na kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage. 
Baadhi ya wafanyabiashara wa zao la kahawa wa mkoa wa Kagera wakimsikiliza Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa ELCT mjini Bukoba, Oktoba 6, 2018. 

DAWASA YAENDELEA KUTEKELEZA OPERESHENI YA KUZUI UVUJAJI WA MAJI

$
0
0

Mafundi wa Mamlaka ya MajiSafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wakiendelea na Operesheni ya kuziba mabomba yanayovuja maji katika eneo la Magomeni Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya hatua zinazochukuliwa na Mamlaka hiyo kuboresha huduma zake kwa wananchi. Operesheni ya kuzuia maji kuvuja tayari imefanyika Tegeta na leo inaendelea katika eneo la Magomeni Jijini Dar es Salaam.
Mafundi wa Mamlaka ya MajiSafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wakiendelea na Operesheni ya kuziba mabomba yanayovuja maji katika eneo la Magomeni Jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya hatua zinazochukuliwa na Mamlaka hiyo kuboresha huduma zake kwa wananchi. Operesheni ya kuzuia maji kuvuja tayari imefanyika Tegeta na leo inaendelea katika eneo la Magomeni Jijini Dar es Salaam.

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) imeanzisha Operesheni maalum ya kupambana na uvujaji wa maji katika Jiji hilo ikiwa ni moja ya hatua zinazochukuliwa na Mamlaka hiyo kuboresha huduma zake kwa wananchi.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mamlaka hiyo leo , Dhamira ya Mamlaka hiyo ni kuhakikisha kuwa inaondoa kabisa changamoto ya upotevu wa maji kwa kuzuia maji yasivuje kutoka katika mabomba hali itakayoongeza tija katika huduma zinazotolewa kwa wananchi na kuongeza mapato ya Mamlaka hiyo.

“Kazi hii inahusisha mafundi zaidi ya 70 na lengo ni kupunguza tatizo la maji kuvuja kwa asilimia 90 katika maeneo yote DAWASA inayotoa huduma “; Inasisitiza sehemu ya taarifa hiyo

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa Kazi hiyo inayosimamiwa na Idara ya Uzalishaji na Usambazaji Maji itatekelezwa kwa weledi wa hali ya juu ili kufikia lengo la kuzuia upotevu wa maji kutokana na kuvuja.

Katika kuimarisha huduma zake kwa wananchi DAWASA imejidhatiti kuhakikisha kuwa kila mwananchi anafikiwa na huduma ya maji safi na salama kutokana na mikakati madhubuti iliyowekwa na Mamlaka hiyo, yakiendana na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano inayosisitiza utoaji wa huduma bora kwa wananchi hasa wanyonge.

Aidha, Mamlaka hiyo imekwishaendesha Operesheni ya kudhibiti uvujaji wa maji katika eneo la Tegeta na sasa zoezi hilo linaendelea kuanzia leo Oktoba 6, 2018 katika eneo la Magomeni na katika maeneo mengine Jijini Dar es Salaam na Pwani.

Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam DAWASA imefanikiwa katika kuboresha huduma zake kwa wananchi kwa kuhakikisha kuwa upatikanaji wa maji ni wa uhakika na unaendana na mahitaji ya wananchi na dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda.

MAKATIBU WAKUU WA WIZARA 11 WAWASILI MBARALI KUTAFUTA SULUHU YA GN 28 YA MWAKA 2008

$
0
0











Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi cha Makatibu wakuu wa Wizara zinazohusika na suala la Hifadhi ya rasilimali maji na maliasili walipokutana Wilayani Mbarali mkoani Mbeya kwa ajili ya kutembelea maeneo ya shamba la Madibira, Eneo la Ikolojia ya Tindiga la Ihefu na eneo la hifadhi ya Taifa ya Ruaha tarehe O5 Oktoba, 2018.
Baadhi ya Makatibu wakuu wakimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora (hayupo pichani) walipohudhuria Kikao kazi hicho.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dkt.Hamisi Mwinyimvua akichangia hoja wakati wa kikao kazi hicho.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole Gabriel akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha Makatibu Wakuu walipokutana Wilayani Mbarali ili kutembelea shamba la Madibira, Eneo la Ikolojia ya Tindiga la Ihefu na eneo la hifadhi ya Taifa ya Ruaha tarehe O5 Oktoba, 2018 Mkoani Mbeya
Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Bi.Mariam Mtunguja akichangia hoja wakati wa kikao kazi hicho.


Baadhi ya Makatibu Mkuu kutoka Wizara mbalimbali pamoja na Mkoa wa Mbeya Mhe.Albert Chalamila (mwenye fulana nyeusi) wakipokea maelezo kutoka kwa Mwikolojia Hifadhi ya Taifa ya Ruaha Dkt.Halima Kiwango walipotembelea eneo la Ikolojia ya Tindiga la Ihefu Wilayani Mbarali Mbeya.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora akioneshwa maeneo ya Shamba la Madibira na Mhifadhi kutoka TANAPA Bw.Moronda lililopo katika Kijiji cha Mahango Wilayani Mbarali Mbeya.

Baadhi ya Makatibu Wakuu wa Watendaji wa Serikali wakipokea taarifa ya Shamba la Madibira kutoka kwa Mwenyekiti wa MAMCOS L.t.d Bw. Stanford Kisinga walipotembelea eneo hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe.Reuben Mfune akifafanua jambo kwa Baadhi ya Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali waliotembelea eneo la shamba la Madibira lililopo Kijiji cha Mahango Mbarali Mbeya.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)


…………………………

Makatibu Wakuu kutoka Wizara zinazohusika na suala la Hifadhi ya rasilimali maji na maliasili wamewasili Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya kuanzia Oktoba 4 hadi 6, 2018 ikiwa ni ziara ya kikazi kwa ajili ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (RUNAPA) na vijiji vya Wilaya ya Mbarali.

Makatibu wakuu hao ni kutoka Wizara mbalimbali zikiwemo; Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Nishati, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, na Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Lengo la ziara hiyo ni Kuona na kujiridhisha mambo ambayo yanalalamikiwa kuhusiana na tangazo la Serikali namba 28 la mwaka 2008 (GN. 28 ya 2008.), kupata suruhu ya kudumu ya uchepushaji wa maji katika mto Ruaha pamoja uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya mito na mito.

Maeneo yaliyotembelewa na Makatibu Wakuu hao ni pamoja na eneo chepechepe la Ihefu lililopo ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Mashamba ya mpunga ya madibira (MAMCOS), Banio la maji lililopo eneo la Mnazi kijiji cha Warumba kata ya Ubaruku pamoja na mashamba ya Mpunga ya mnazi katika kijiji cha Mwanavala Kata ya Imalilosongwe.

Ziara hiyo iliongozwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera na Uratibu Prof. Faustin Kamuzora na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune.

NHIF TANGA WATUMIA WIKI YA WATEJA KUSIKILIZA MAONI,USHAURI NA KERO ZINAZOWAKABILI KATIKA VITUO VYA HUDUMA ZA AFYA

$
0
0


 MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto wakiwa na wateja wao wa benki ya NMB wilayani Handeni kupata ushauri ,malalamikona changamoto wanazozipata watumishi hao katika kupata huduma za bima ya afya kwenye vituo vya kutolea huduma ikiwa ni wiki ya wateja

Daktari wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Lawi Kupaza akizungumza jambo kushoto ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu Sehemu ya watumishi wa Benki ya NMB wakifuatilia kwa umakini
 MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akiwa na wakiwa na wateja wao wa benki ya NMB wilayani Handeni kupata ushauri ,malalamikona changamoto wanazozipata watumishi hao katika kupata huduma za bima ya afya kwenye vituo vya kutolea huduma ikiwa ni wiki ya wateja
Sehemu ya watumishi wa NMB wilayani Handeni wakimsikiliza kwa umakini Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu

WANANCHI WANAENDELEA KUNUFAIKA NA MFUMO WA USHIRIKI-DKT TIZEBA

$
0
0
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akitoa taarifa ya ukusanyaji, Ukoboaji na uuzaji wa kahawa Mkoani Kagera katika msimu wa mwaka 2018/2019 kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa (Mb) kwenye mkutano wa wadau wa kahawa katika ukumbi wa ELCT Mjini Bukoba. (Picha Na Mathias Canal-WK)

Na Mathias Canal-WK, Bukoba-Kagera

Imebainika kuwa pamoja na changamoto zilizojitokeza katika msimu wa kahawa wa mwaka 2018/2019 lakini bado mfumo wa uuzaji wa kahawa kupitia ushirika umekuwa wa manufaa kwa mkulima kutokana na mkulima kupata uhakika wa kilo za kahawa alizozipeleka chamani tofauti na ilivyokuwa hapo awali. 


Manufaa hayo yamejili kutokana na kuingia mikataba ya kuuza moja kwa moja, ambapo matarajio ya serikali ni kuhakikisha kuwa mkulima analipwa malipo ya awali na kiasi kingine kubaki kwa ajili ya kuendelea kukusanya kahawa na kufanya maandalizi ya malipo ya pili. 


Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba amebainisha hayo Leo tarehe 6 Octoba 2018 wakati akitoa taarifa fupi ya ukusanyaji, Ukoboaji na uuzaji wa kahawa Mkoani Kagera katika msimu wa mwaka 2018/2019 hadi kuishia tarehe 2 Octoba 2018 kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa (Mb) kwenye mkutano wa wadau wa kahawa.


Katika mkutano huo uliofanyika kwenye Ukumbi ELCT Mjini Bukoba na kueleza kuwa ubora wa kahawa umeongezeka kwa kiasi kikubwa tofauti na misimu iliyopita. 


Waziri Tizeba alizitaja changamoto zinazovikabili vyama vya ushirika kwenye zao la kahawa kwa msimu wa mwaka 2018/2019 kuwa ni pamoja na Bei za mnadani, Kahawa kununuliwa kwa kiwango kidogo mnadani na wakati mwingine kutonunuliwa kabisa.


Kuwepo kwa taarifa za upotoshaji kwa wakulima toka kwa Walanguzi za kuzuia wakulima kukusanya kahawa yao kupitia Vyama vya Ushirika vya Msingi kuwa wao (Walanguzi)  watanunua na kuwapatia bei nzuri na Kuwepo kwa katizo la umeme mara kwa mara linalopelekea ukoboaji wa kahawa kutofanyika kwa wakati  (hususani Wilayani Ngara).


Aidha, aliutaja mkakati wa kukabiliana na changamoto hizo kuwa ni pamoja na kuuza kahawa kupitia mnada wa Moshi na mauzo ya moja kwa moja nje ya nchi “Direct Export” ambao umeonesha kuwa na bei nzuri ukilinganisha na ile inayotolewa mnadani Moshi, na Kuomba mkopo wa nyongeza toka TADB kwa ajili ya kuwalipa wakulima malipo yao ya Awali. 


Alisema Chama Cha Ushirika cha Karagwe KCU wanatarajiwa kupata mkopo wa Tshs. 2,000,000,000/= kwa wiki hii na kiasi cha Tshs. 2,000,000,000/= kinaendelea kushughulikiwa ili kiweze  kutolewa wiki ijayo ambapo wanatarajiwa kupata malipo ya mauzo ya kahawa yao kwa wiki ijayo kiasi cha Tshs Bilioni 2.1


Mikakati mingine ya kukabiliana na changamoto ya zao la kahawa ni pamoja na Vyama kuingia mikataba mbalimbali ya kuuza kahawa moja kwa moja nje. KDCU Ltd wana mikataba ya mauzo nje yenye thamani ya Tshs 20,819,815,820.66 ambapo malipo yake yanatarajiwa kulipwa kuanzia wiki hii. Kwa KCU Ltd wana mkataba wa Tshs Bilioni 1.3 na wanatarajia kuingia mikataba mingine na wanunuzi wengine kwa wiki ijayo. 


Dambamba na jitihada za kupatikana kwa umeme wa uhakika katika kiwanda kilichoko Wilayani Ngara zinaendelea kufanyika kwa kushirikiana na mamlaka husika.


Katika hatua nyingine alieleza kuwa mpaka sasa Kahawa iliyoko ghalani ni Kiasi cha Kilo 3,000,464 za kahawa maganda ambayo ilikuwa bado kukobolewa huku Kilo 8,191,867 za kahawa safi kilikuwa bado hakijauzwa na kilikuwepo kwenye maghala ya vyama.


Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa ameanza ziara ya kikazi Mkoani Kagera kuanzia Leo tarehe 6 mpaka tarehe 9 Octoba 2018 ambapo pamoja na mambo mengine lengo kuu la ziara hiyo ni kukagua Maendeleo ya zao la kahawa Mkoani humu.

TCCIA YAJIVUNIA UWEPO WAKE NA MCHANGO WALIOUTOA KWA MIAKA 30 KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI KWA KUSAIDIANA NA SERIKALI

$
0
0


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

CHAMA cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo kinajiandaa kusheherekea miaka 30 tangu kuanzishwa kwake huku kikijivunia mafanikio ambayo yamepatikana katika sekta ya kilimo,biashara na viwanda kutokana na uwepo wao nchini.

Kimeeleza namna ambavyo kimeshiriki kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini n katika kipindi hiki cha kusheherekea miaka 30 ya uwepo wao kabla ya kufikia siku ya kilele Novemba mwaka huu watafanya shughuli mbalimbali katika wilaya na mikoa yote nchini.

Akizungumza Dar es Salaam Kaimu Rais wa TCCIA Octavian Mshiu amesema uwepo wao na mchango wake kwa Taifa mbali na kuwaunganisha vyombo mbalimbali vinavyojihusisha na kilimo,viwanda na biashara wamefanikisha uwepo wa mazingira mazuri ya uwekezaji.

Amesema kimsingi huko nyuma watanzania walikuwa hawashiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi lakini kupitia TCCIA watanzania wameweza kushiriki kwa kuanzisha viwanda na kampuni na hivyo kuwa sehemu ya wawekezaji nchini."Kuna mengi ya kujivunia kama TCCIA ,kadri muda unavyokwenda kuelekea kwenye sherehe ya kutimiza miaka 30 tangua kuanzishwa kw TCCIA mengi tutazungumza kupitia viongozi mbalimbali.

" Baadhi ya viongozi hao wameshastaafu baada ya kuitumikia TCCIA na kutoa mchango wao mkubwa nao watapata nafasi ya kuzungumza na kutoa maoni yao,tulikotoka,tulipo na tunakokwenda,"amesema Mshiu.Kuhusu TCCIA na mchango wake kwa jamii anasema watanzania wengi wanamiliki viwanda ndani na nje ya nje ya nchi na TCCIA imetoa mchango mkubwa nchini Tanzania.

Pia ameahidi TCCIA itaendelea kuunga mkono Serikali katika kusaidia kuboresha sekta ya biashara na Novemba mwaka huu ndio wanatarajia kusheherekea miaka 30 ya TCCIA ambayo ilianza mwaka 1988.Wakati huo huo Kaimu Rais wa TTCIA amesema pamoja na maandalizi ya sherehe hizo,pia wapo katika mchakato wa kuanzisha TCCIA China Diaspora .

Amesema lengo ni kuwasaidia Watanzania wanaofanya biashara China kuwa na mazingira mazuri ya kibiashara na Wachina nao kufanyabiashara na shughuli nyingine za kiuchumi bila usumbufu.Mmoja wa wanachama wa TCCIA amabaye aliyekuwa Mkuu wa msafara wa wafanyabiashara wa Tanzania walioambatana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Alli Iddi, Nelson Ngowi ameeleza namna ambavyo alikutana na wafanyabiashara wa Kitanzania wanaoishi China na namna walivyo na shauku ya kuanzisha TCCIA huko China.

" Pamoja na kushiriki maonyesho ujumbe wetu ulipata heshima ya kukaribishwa na Balozi wa Tanzania nchini china Balozi Mbelwa Kairuki na kubadilishana naye mawazo,”amesema.Kwa upande wake aliyekuwa Rais Mstaafu wa TCCIA David Mwaibula ambaye alikuwa Rais wa pili wa chama hicho amesema kuna mambo mengi ambayo yamefanyika kwa nyakati tofauti na kufafanu huko nyuma hakukuna Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA)lakini walishiriki kuhakikisha chombo hocho cha kukusanya kodi kinaa zishwa na kuwa na mazingira rafiki ya ulipaji kodi.

Pia amesema pamoja na mambo mengine TCCIA wamefanikiwa kuunganisha vyombo mbalimbali na kwamba katika kushughulika na utatuzi wa changamoto au kujadili mambo kadha kazi ya chombo hicho ni kushughulika na taasisi husika na si mtu mmoja mmoja.

Amezungumzia namna ambavyo TCCIA ilivyoshiriki katika kuhakikisha kunakuwa na mazingira mazuri ya ulipaji kodi na pale ambapo haki inawezekana kutotendeka kuna vyombo vyenye mamlaka ya kusikiliza na kutoa uamuzi na hivyo hakuna sababu ya kutoa rushwa ili kupata haki.

"TCCIA tumekuwa tukikaa pamoja na Serikali kujadili mazingira ya uwekezaji .Kwa kweli kuna mambo mengi tunafanya kwa ajili ya kuhakikisha kunakuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji.

"Pia TCCIA imekuwa na jukumu la kutafuta masoko kwa ajili ya mazao ya wakulima.Nakumbuka huko nyuma tumewahi kufanya tafiti kwa kuwashirikisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na lengo ni kutafiti shughuli za kiuchumi," amesema.
 Kaimu Rais wa TCCIA Octavian Mshiu(kushoto) akiwa na aliyewahi kuwa Rais wa TCCIA David Mwaibula wakiwa wameshika cheti
Rais mstaafu wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo nchini(TCCIA)David Mwaibula akifafanua jambo kuhusu Chama hicho ambacho kinatarajia kusheherekea kutimiza miaka 30 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1988

WALIOZEMBEA KUSIMAMIA,KUJENGA MRADI WA MAJI UKALAWA-KITOLE, MKOANI NJOMBE WATAKIWA KUISAIDIA POLISI

$
0
0
Kutokua makini katika uratibu, usimamizi na ujenzi wa mradi wa maji mkoani Njombe kumewaweka matatani baadhi ya watendaji wa serikali na wakandarasi waliopewa dhamana ya kujenga na kufikisha majisafi na salama kwa wananchi. 

Mradi uliotiliwa shaka wa Ukalawa na Kitole umesubiriwa na wananchi kwa zaidi ya miaka mitano na bado umekua butu kukidhi kiu ya wakazi wa vijiji vya Ukalawa na Kitole. Mradi huo umejengwa na kampuni ya Kihanga Farm International iliyolipwa kiasi cha Shilingi Milioni 532 kati ya Shilingi Milioni 562. 

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ameelekeza wahusika walioshiriki katika mradi huo wakiwamo Watalaam wa maji wa Serikali popote walipo, Mhandisi Mshauri wa mradi na Mkandarasi wa mradi wasaidie Jeshi la Polisi kupata undani wa taarifa zinazohusu mradi, ikiwamo malipo yaliyofanyika wakati wananchi hawapati maji. 

Mhe. Aweso (Mb) katika kikao kilichodumu kwa saa sita kilichowakutanisha watalaam wa maji, na baadhi ya walioshiriki katika ujenzi wa mradi wa maji Ukalawa-Kitole, amesema miradi ya maji sio kichaka cha kupitisha fedha na kusisitiza endapo mhusika yoyote atabainika kushiriki kuhujumu mradi huo, hata kama amestaafu utumishi wa umma, atatafutwa popote alipo na kufikishwa katika vyombo vya sheria. Baada ya kikao kumalizika baadhi ya wahusika kutoka kampuni iliyopewa kandarasi ya Kihanga Farm na wataalam wa maji wa serikali walioshiriki walikabidhiwa kwa vyombo husika ili kusaidia zaidi kwa taarifa muhimu. 

Mhe. Aweso (Mb) amesema hakuna faida ya kuwa na mtalaam wa maji anayekabidhiwa mradi bila kujiridhisha na ubora wake kama taratibu zinavyotaka, ambapo imebainika moja ya udhaifu katika mradi wa maji Ukalawa-Kitole ni kwenda kinyume na mkataba, na kutozingatia ushauri wa Mhandisi Mshauri wa mradi na kubadili mfumo wa kusukuma maji kutoka wa kutumia jenereta, kwenda mfumo wa kutumia nishati ya jua (solar) wakati mazingira ya mradi sio rafiki kwa mfumo wa nishati ya jua. 

Mhe. Aweso (Mb) ameagiza kutokana na udhaifu ulioonekana katika mradi huo ameagiza timu aliyoiunda akiwa mkoani Mbeya mwezi Oktoba 2018, ipite katika mradi wa maji Ukalawa na mradi wa Lugenge ambao madakio ya maji mawili yamekamilika lakini mradi bado hauridhishi na ukiwa katika asilimia 60 ya kazi pamoja na Mkandarasi kuongezewa muda. 

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini 
Wizara ya Maji na Umwagiliaji 
06.10.2018 .
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiongea na watalaam wa maji, pamoja na baadhi ya wahusika walioshiriki katika ujenzi wa mradi wa maji Ukalawa-Kitole katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka (kulia). 
1. Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwasikiliza baadhi ya wananchi watakaofaidika na mradi wa maji Lugenge mkoani Njombe. 
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso (Mb ) akipewa maelezo kuhusu kazi iliyoanza ya utandikaji wa mabomba kutoka katika dakio la maji kwenda katika tanki katika mradi wa maji Lugenge,pichani kati ni MKuu wa Mkoa wa Njombe Mh Ole Sendeka.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akipokea mrejesho wa wananchi kuhusu kero ya maji kando ya tanki la maji lililokamilika la mradi wa maji Lugenge. Mkandarasi kapewa mwezi mmoja kuhakikisha maji yanafika katika tanki hilo. 
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiangalia mitambo katika mradi wa maji Kibena.

MAJALIWA: VIWANDA VIMEPUNGUZA TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema changamoto ya upatikanaji wa ajira hususani kwa vijana imeanza kupungua nchini baada ya viwanda vingi kuanza kufanya kazi.

Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kukuza uchumi kutoka wa chini hadi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo mwaka 2025. Aliyasema hayo jana jioni (Jumamosi, Oktoba 6, 2018) alipotembelea kiwanda cha kukoboa kahawa cha BUKOP na cha kusindika kahawa cha Tanica, mjini Bukoba.

Alisema kwa sasa tabia ya vijana wengi kukaa vijiweni imepungua kwenye maeneo mengi nchini baada ya wengi kuajiriwa katika viwanda mbalimbali vilivyoanzishwa na kufufuliwa. Waziri Mkuu alisema viwanda vimekuwa vikitoa ajira nyingi kwa wananchi, ambapo alitolea mfano kiwanda kimoja cha Tanika kilichoajiri watumishi 800.

“Nyie mlioajiriwa kiwandani hapa hakikishe mnafanya kazi kwa bidii, weledi, uaminifu na uadilifu wa hali ya juu ili kukiwezesha kiwanda kuendelea na uzalishaji,” alisisitiza. Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Kagera kwa ziara ya siku nne, inayolenga kufuatilia maendeleo ya viwanda na zao la kahawa, ambalo ni kati ya mazao makuu sita ya biashara. Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Bw. Bernad Limbe kuhakikisha anatafuta eneo kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo.

Aliyasema hayo baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi waliokuwa wakifanya biashara katika eneo bandari na kuondolewa bila ya kupewa eneo lingine. Waziri Mkuu alisema ni marufuku kuwaondoa wananchi katika maeneo yao ya kufanyia biashara bila ya kuwaonesha eneo lingine ambalo watalitumia kwa aliji ya kufanyia biashara zao.

Awali, Meneja Mkuu wa kiwanda hicho, Bw. Linus Leopord alisema kwa mwaka wanazalisha tani 600 za kahawa iliyokaangwa na kusagwa, ambayo inatosheleza kwa mahitaji ya soko. Pia kiwanda cha kahawa cha Tanica kinauwezo wa kuzalisha kahawa ya unga tani 500 kwa mwaka ila kutokana na uchakavu wa miungombinu kinazalisha tani 300 kwa mwaka. Kuhusu masoko Bw. Leopord alisema kwa sasa mauzo yameongezeka, wanauza tani 50 ya kahawa iliyokaangwa na kusagwa kwa mwezi, ambapo awali walikuwa wanauza tani 32.

Kadhalika, Meneja huyo alisema wameimarisha na kuongeza soko la nje ambapo kwa sasa wanauza tani 35 za kahawa ya unga kwa mwezi, awali walikuwa wanauza tani 20. Alisema kiwanda cha Tanika kinamilikiwa na chama cha ushirika cha KCU (53.37 %), KDCU (31.8%), Hazina (7.67), TFC (6.22%) na wafanyakazi wa Tanica (0.92%).

TANZIA: Msiba Ujerumani Wa KONDO MOHAMED MSUMI a.k.a Mguu Mtupu

$
0
0
 Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU e.V) kwa masikitiko makubwa tunawataarifu kifo cha Mtanzania mwenzetu   Kondo mohamed Msumi  ambaye alikuwa akiishi  Bochum,nchini ujerumani.
 Marehemu Kondo Mohamed Msumi amefariki usiku wa 2.kuamikia 3 Oktoba 2018 akiwa hospitalini akipatiwa matibabu,  kamati ya Umoja  wa Watanzania Ujerumani UTU e.V imewasiliana na ndugu wa marehemu waliopo Ujerumani na Tanzania  Tumeazimia kupitisha michango  ili  kutuwezesha kufanikisha  mazishi ya ndugu yetu, bado hatujajua kwamba tutazika hapa Ujerumani au tutasafirisha, tutawaletea taarifa zaidi kadiri tunavyozipata.
 Kamati imechagua Rafiki  wa karibu na familia ya Kondo ili kupokea michango hiyo. Michango yote ipitishwe kwenye acc ifuatayo.

Gls Bank,Jafari Juma Mazangwi. IBAN:DE15 4306 0967 4046 5996 00.Bic: GENODEM1GLSTunawaomba watanzania wote  kutoa michango kwa wingi ili kumuhifadhi ndugu yetu marehemu Kondo Mohamed MsumiAsanteni

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA TANICA NA BUKOP MJINI BUKOBA

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama kopo la kahawa wakati alipotembelea kiwanda cha kusindika kahawa cha TANICA kilichopo mjini Bukoba, Oktoba 6, 2018
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama paketi ya kahawa wakati alipotembelea kiwanda cha kusindika kahawa cha TANICA mjini Bukoba, Oktoba 6, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mtambo kusindika kahawa wakati alipotembelea kwanda cha kusindika kahawa cha TANICA mjini Bukoba, Oktoba 6, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanyakazi wa kiwanda cha kahawa cha TANICA mjini Bukoba baada ya kutembelea kiwanda hicho, Oktoba 6, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha kukoboa kahawa cha BUKOP baada ya kutembelea kiwanda chao kilichopo mjini Bukoba, Oktoba 6, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali, Marco Elisha Gaguti.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Mkuu wa kiwanda cha kukoboa kahawa cha BUKOP, Theobad Mushashu (katikati) kuhusu ukoboaji kahawa wakati alipotembelea kiwanda hicho, Oktoba 6, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Mkuu wa kiwanda cha kukoboa kahawa cha BUKOP, Theobad Mushashu kuhusu ukoboaji kahawa wakati alipotembelea kiwanda hicho, Oktoba 6, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema changamoto ya upatikanaji wa ajira hususani kwa vijana imeanza kupungua nchini baada ya viwanda vingi kuanza kufanya kazi.

Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kukuza uchumi kutoka wa chini hadi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo mwaka 2025.

Aliyasema hayo jana jioni (Jumamosi, Oktoba 6, 2018) alipotembelea kiwanda cha kukoboa kahawa cha BUKOP na cha kusindika kahawa cha Tanica, mjini Bukoba.Alisema kwa sasa tabia ya vijana wengi kukaa vijiweni imepungua kwenye maeneo mengi nchini baada ya wengi kuajiriwa katika viwanda mbalimbali vilivyoanzishwa na kufufuliwa.

Waziri Mkuu alisema viwanda vimekuwa vikitoa ajira nyingi kwa wananchi, ambapo alitolea mfano kiwanda kimoja cha Tanika kilichoajiri watumishi 800. “Nyie mlioajiriwa kiwandani hapa hakikishe mnafanya kazi kwa bidii, weledi, uaminifu na uadilifu wa hali ya juu ili kukiwezesha kiwanda kuendelea na uzalishaji,” alisisitiza.

Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Kagera kwa ziara ya siku nne, inayolenga kufuatilia maendeleo ya viwanda na zao la kahawa, ambalo ni kati ya mazao makuu sita ya biashara.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Bw. Bernad Limbe kuhakikisha anatafuta eneo kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo.

Aliyasema hayo baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi waliokuwa wakifanya biashara katika eneo bandari na kuondolewa bila ya kupewa eneo lingine.Waziri Mkuu alisema ni marufuku kuwaondoa wananchi katika maeneo yao ya kufanyia biashara bila ya kuwaonesha eneo lingine ambalo watalitumia kwa aliji ya kufanyia biashara zao.

Awali, Meneja Mkuu wa kiwanda hicho, Bw. Linus Leopord alisema kwa mwaka wanazalisha tani 600 za kahawa iliyokaangwa na kusagwa, ambayo inatosheleza kwa mahitaji ya soko.Pia kiwanda cha kahawa cha Tanica kinauwezo wa kuzalisha kahawa ya unga tani 500 kwa mwaka ila kutokana na uchakavu wa miungombinu kinazalisha tani 300 kwa mwaka.

Kuhusu masoko Bw. Leopord alisema kwa sasa mauzo yameongezeka, wanauza tani 50 ya kahawa iliyokaangwa na kusagwa kwa mwezi, ambapo awali walikuwa wanauza tani 32.Kadhalika, Meneja huyo alisema wameimarisha na kuongeza soko la nje ambapo kwa sasa wanauza tani 35 za kahawa ya unga kwa mwezi, awali walikuwa wanauza tani 20.

Alisema kiwanda cha Tanika kinamilikiwa na chama cha ushirika cha KCU (53.37 %), KDCU (31.8%), Hazina (7.67), TFC (6.22%) na wafanyakazi wa Tanica (0.92%).


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, OKTOBA 7, 2018.

VIJANA NCHINI WAASWA KUANZISHA MIRADI YA KIMKAKATI

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Iringa mara baada ya kuwasili ofisini hapo kwa ajili ya ziara ya kuhamasisha vijana na kukagua maeneo yaliyotengwa kujenga vitalu nyumba mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akieleza jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara mkoani humo ya kukagua maeneo ya kujenga vitalu nyumba. (Wa kwanza kushoto) ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bw. Fikira Kisimba. 
Baadhi ya Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu waliombatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama katika ziara ya kukagua maeneo ya kujenga vitalu nyumba. (Kulia ni) Afisa Vijana Mwandamizi Bw. Gedfrey Massawe na Afisa Kazi Bi. Neema Moshi. (Kushoto ni) Afisa Elimu wa Mkoa Bw. Richard Mfugale. 
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa Bw. Christopher Magala akielezea jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea Ofisi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akielezea jambo kwa Vijana wa Umoja wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) alipofanya ziara ya kuhamasisha vijana na kukagua maeneo yaliyotengwa kujenga vitalu nyumba mkoani humo.
Mkuu wa Idara ya Uchumi, Uwekezaji na Fedha UVCCM Taifa Bw. Lusekebo Nelson akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama juu ya eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kitalu nyumba lililopo ihemi, wakati akiwa katika ziara ya kukagua maeneo hayo mkoani iringa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akikagua majengo yaliyopo Chuo cha Ihemi ambayo yatatumika kutoa mafunzo ya ujasiriamali na kilimo cha kisasa cha Kitalu nyumba (Green House).
Muonekano wa eneo moja wapo lililotengwa kwa ajili ya kujenga Vitalu nyumba (Green House) lililopo Ihemi. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Vijana wa Umoja wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).




Vijana nchini watakiwa kubadili mtazamo kwa kuanzisha miradi ya kimkakati itakayowawezesha kiuchumi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) alipofanya ziara hiyo Mkoa wa Iringa kwa lengo la Kuhamasisha na kukagua maeneo ya ujenzi wa Vitalu Nyumba (Green House) na uwepo wa miundombinu itakayotumika kwenye maeneo hayo.

Mheshimiwa Mhagama amesema sekta ya kilimo inaajiri na kuchangia katika pato la taifa kwa zaidi ya asilimia 60%, hivyo vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa wakatumie rasilimali ardhi kama mtaji wa kujiajiri na kuweza kuajiri wenzao.

“Lengo letu ni vijana kutumia sekta hii ya umahiri kwa ajili ya kuwaondoa kwenye mitazamo finyu na kuwa na mitazamo chanya ili waweze kunufaika na miradi itakayo buniwa na kutumika kama mfano kwa vijana nchi nzima.” Alisema Waziri Mhagama

Aliongeza kuwa vijana watafundishwa kilimo cha Kitalu nyumba ambavyo vitawawezesha kuongeza thamani kwenye mazao watakayozalisha na mradi huo ukawe sehemu ya ajira zao.Aidha, Waziri Mhagama alitoa rai kwa vijana kuwa chachu ya maendeleo ya uchumi wa taifa kwa kushirikiana kwa pamoja bila kujali itikadi zao ili kutimiza adhima ya vijana wote.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela alisema mradi huo utawawezesha vijana wa mkoa wa Iringa kuweza kuondokana na changamoto ya ajira kwa kuwa Serikali imewaletea teknolojia hiyo itakayo wawezesha vijana kujiajiri.

Naye mmoja wa vijana aliweza kuishukuru Serikali kwa kuanzisha mradi huo wenye tija ya kuwanufaisha vijana wote katika kuwaletea mabadiliko na ukombozi wa kiuchumi.“Mradi huu utatuwezesha sisi vijana kunufaika na teknolojia hii ya kilimo cha kisasa kwa kutumia sehemu ndogo ya mashamba kuzalisha mazao mengi yatakayotusaidia kujipatia mtaji ili tuondokane na umaskini.” Alisema Peter Seni

Katika Ziara hiyo Waziri Mhagama alitembelea Chuo cha Ihemi kwa ajili ya kukagua majengo yatakayokuwa yanatumia kufundishia vijana elimu ya ujasiriamali na kilimo cha kitalu nyumba (Green House).

MOJA BETI YAUTAMBULISHA MCHEZO WA BOOM PESA JIJINI MBEYA .

$
0
0


KAMPUNI ya moja Beti inayojishughulisha na mchezo wa kubahatisha imeutambulisha mchezo mpya wa kubahatisha Jijini Mbeya, unaofahamika kwa jina la ‘BOOM PESA’, na kuwataka wakazi wa Mkoa huo kujitokeza na kununua tiketi ili waweze kujishindia fedha taslimu papo hapo.

Akizungumza leo Jijini Mbeya wakati wa kuutambulisha mchezo huo wa kubahatisha, Msimamizi wa kituo cha huduma kwa Wateja kutoka Moja Beti Florida Mwangosi, amesema mchezo huo ni mpya lakini ni rahisi sana kupata fedha tofauti na michezo mingine .

“ Huu mchezo wetu wa kubahatisha unaofahamika kwa jina la Boom Pesa ni mchezo ambao unachezwa kwenye mitandao yote ya simu za mkononi kwa kununua tiketi , na mara mshindi anaposhinda anapewa fedha zake papo hapo kwenye simu yake , na mchezaji anaweza kununua tiketi kuanzia shilingi 100 na kuendelea” Alisema Florida Mwangosi .

Naye Balozi wa Boom Pesa Sabrina Ibrahimu, alisema mwitikio kwa wakazi wa Jiji la Mbeya kwenye mchezo huo wa kubahatisha ni mkubwa sana , nakwamba wananchi zaidi ya 100 kwa siku moja walijitokeza na kushiriki mchezo huo .

“ Tunawashukuru sana wakazi wa Jiji la Mbeya kwa kuupokea huu mchezo wetu mpya wa kubahatisha , nawapongeza sana maana wamekuja na baadhi wameshinda tunawashukuru sana tunawaomba waendelee kuucheza mchezo huu” Alisema Sabrinma Ibrahimu .

Aidha Baadhi ya washindi wa Boom Pesa kutoka Jijini Mbeya ambao ni Yasinta Ndesabula na Taison John waliliambia gazeti hili kuwa ni mchezo ambao wao hawakutegemea kama wangecheza na kushinda, ambapo wamewahimiza watanzania wengine kucheza ili waweze kujishindia fedha taslimu

Balozi wa mchezo wa kubahatisha wa BOOM PESA kutoka kampuni ya MOJA BET Diana Thomas, akitoa maelekezo kwa moja ya wateja wa kampuni hiyo jinsi ya kushiriki na kucheza huo wakati wa uzinduzi wa BOOM PESA uliofanyika leo jijini Mbeya. Kwa BOOM PESA, washiriki wanajishindia pesa taslimu papo hapo kwa kuweka dau ya kuanzia TZS1000 kupitia simu za mkononi.

KIKWETE AWAPONGEZA BENK YA NMB.

$
0
0
Na Shushu Joel,Chalinze.

MBUNGE wa jimbo la chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani pwani Ridhiwani Kikwete ameipongeza Benk ya Nmb kwa juhudi zao za kutoa misaada kwa jamii ili kutatua changamoto mbalimbali zinazokuwa zikiwakabili wanajamii.

Akitoa pongezi hizo jana, katika kata ya kiwangwa alipokuwa akipokea vifaa mbalimbali vya hospital vilivyotolewa na benk hiyo,Ridhiwani alisema kuwa awali hospital hiyo ilikuwa na changamoto ya vitanda kwa ajili ya kinamama kuweza kujifungulia lakini kutokana na msaada huo tatizo hilo limebaki kuwa ni historia .

“Naipongeza benk ya Nmb kwa kutambua thamni ya kinamama wa chalinze ingawa katika nchi yetu kuna changamoto nyingi sehemu zingine lakini nyie mmeamua kutuletea misaada huu katika halmashauli yetu ya chalinze”Alisema Ridhiwani

“Mimi nawatia moyo tu kwa niaba ya wananchi wa chalinze msichoke kutusaidia kwani mahitaji yetu bado ni mengi ingawa nasi kama serikali tunapambana ili kuihakikisha kinamama wanajifungua bila matatizo ya aina yeyote hile ndio maana hata vifo vya kinamama chalinze wakiwa wanajifungua vinazidi kubaki kuwa historia”

Aliongeza kuwa awali walikuwa wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa viwanda kwa ajili ya kinamama kujifungulia katika hospital hiyo lakini Nmb imewapatia vitanda 10 kwa ajili ya kupunguza tatizo hilo hivyo amewataka wananchi wa kata hiyokwa kushirikiana na watumishi wa hospital hiyo kuhakikisha wanavilinda vifaa hivyo ili viweze kuwasaidia kwa kipindi kirefu.

Kwa upande wake mganga mkuu wa halmashauli ya chalinze Dr Rahim Hangai alisema kuwa kipindi cha nyuma kinamam walikuwa wanapoteza maisha yao wakati wa kujifungua kutokana na changamoto mbalimbali kwa sasa ni wastani ya mama mmoja upoteza maisha kila mwaka kwa watu laki moja wakati wa kujifungua hii ni hatua kubwa sana katika halmashauli yetu ya chalinze.Alisema.

Aidha Dr Hangai alisema kuwa vifaa hivyo vimekuja kwa muda mwafaka kutokana maombi yetu ilikuwa ni kupata vifaa na Nmb wametuletea hivyo chalinze itabaki ni historia vifo vinavyotokana na uzazi kwa kinamama.

“Napenda kuwaomba watumishi wa idara ya afya katika halmshsuli ya chalinze kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha anapambana ili kuwasaidia wagonjwa wanaokuja kupata huduma ili chalinze iendelee kuongoza kwa utoaji wa huduma za kiafya hapa nchini”Alisema De Hangai.

Naye Meneja wa Benk ya Nmb wilaya ya Bagamoyo Bi, Betha Munguli alisema kuwa benk hiyo imetoa msaada wa vifaa mbalimbali katika jimbo la chalinze na vyenye thamani ya shilingi ya milioni kumi ka lengo la kutoa faida wanazozipata kwa jamii ili kuisaidia serikali baadhi ya changamoto zinazokuwa zikiwakabili wananchi.

Aliongeza kuwa benk hiyo itaendelea na kutoa misaada mbalimbali kwa kipindi chote kwani kwa kipindi hiki benk imetenga fedha nyingi za kusaidia katika jamii ili kuweza kulipa fadhila kwa wateja wake.

“Vifaa vilivyotolewa ni vitanda vya kujifungulia 10,vitanda vya kawaida 6,magodoro10,delvery kit 1na Bm Mashine 6 vyote vikiwa na thani ya milioni 10”Alisema Meneja huyo .Aidha amempongeza mbunge wa jimbo hilo kwa ushirikiano anaonyesha katika benk hiyo kwa kuwasisitiza wananchi wake kufungua akaunti katika benk ya Nmb na kuachana na tabia ya kukaa na pesa ndani ya nyumba huku mahali pa kuzihifadhi ipo.
 Mbunge wa jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete  akipokea vifaa vya wagonjwa kwa ajili ya hospital ya kiwangwa vilivyotolewa na benk ya Nmb
 Mbunge wa jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete  akipokea vifaa vya wagonjwa kwa ajili ya hospital ya kiwangwa vilivyotolewa na benk ya Nmb

SERIKALI KUHIFADHI UTAMADUNI WA MAKABILA YALIYO HATARINI KUPOTEA

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Suzan Mlawi akipongeza uongozi wa Four Corner Cultural Programme (4CCP) kwa kuendesha lenye kuenzi Utamaduni,Mila na Desturi za makabila manne yanayopatikana barani Afrika ambayo niyakujivunia leo katika sherehe za kufunga tamasha hilo lililofanyika katika Kijiji cha Hydom Wilaya ya Mbulu Vijijini.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Suzan Mlawi akimkabidhi cheti cha ushiriki muwakilishi wa Taasisi ya Hifadhi ya Ngorongoro Bw.Gibson Ngolongolo leo katika sherehe za kufunga tamasha la saba la 4CCP lililofanyika katika Kijiji cha Hydom Wilaya ya Mbulu Vijijini .
Mbunge wa Mbulu Vijijini Mhe.Flatei Massey na Mratibu wa Kituo cha Four Cultural Programme Bi.Eliminata Awet wakiwa wamejiwekea nyoka mabegani anayetumika kuchezea ngoma ya kikiundi cha wasukuma kutoka Mwanza wakati wa Sherehe za Kufunga Tamasha la Four Corner Cultural Festival liloandaliwa na 4CCP na kufanyika leo katika Kijiji cha Hydom Wilaya ya Mbulu Vijijini,wapili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Suzan Mlawi.
Baadhi ya Vijana kutoka Jamii ya Kidatooga wakicheza ngoma ya asili ya kumkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Suzan Mlawi(hayupo pichani) katika himaya ya nyumba yao iliyopo katika kituo cha makumbusho ya Four Corner Cultural Programme (4CCP) leo katika sherehe za kufunga tamasha la saba la Four Corner Cultural Festival lililofanyika Kijiji cha Hydom,Wilaya ya Mbulu Vijijini.
Jamii ya Wadzabe wakicheza ngoma ya asili mbele ya mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Suzan Mlawi (hayupo pichani) katika sherehe za kufunga Tamasha la Saba la Four Corner Cultural Festival lililoandaliwa na uongozi wa 4CCP na kufanyika leo Kijiji cha Hydom,Wilaya ya Mbulu Vijijini.

…………………….

Na Anitha Jonas – WHUSM – Hydom,Manyara.

Serikali imejipanga kuanzisha programu ya kukusanya na kuhifadhi taarifa jamii za kitanzania ambazo asili ya utamaduni wake upo hatarini kupotea.

Kauli hiyo imetolewa leo katika Kijiji cha Hydom,Wilaya ya Mbulu Vijijini, Mkoani Manyara na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi alipokuwa akifunga Tamasha la Saba la Utamaduni wa Pembe Nne (7th Four Corner Cultural Festival) kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe ambaye ndiye alikuwa afunge tamasha hilo.

Bi.Mlawi alitoa pongezi kwa waandaaji wa tamasha hilo linahusisha makundi manne ya lugha yanayopatikana barani Afrika ila kwa Tanzania yanapatikana mkoani Manyara na jirani ambapo kwa sasa yameanza kupoteza asili yao na utamaduni wake ambayo ni Wahdzabe-Khoisan,Iraqw-Cushits,Datooga-Nilotic na Wabantu-Wanyiramba/ Wanyisanzu.

“Kupitia Idara ya Utamaduni iliyo chini ya Wizara hii nitaunda Kitengo kitakacho kuwa kinashughulikia suala la ukufanyaji wa taarifa za makabila mbalimbali nchini katika mfumo wa picha jongefu pamoja na uandishi wa historia fupi makabila hayo kwa lengo la kuweza kuhifadhi taarifa hizo kwa maslai ya vizazi vijavyo”alisema Bi.Mlawi.

Katibu Mkuu huyo aliendelea kueleza kuwa serikali inatambua changamoto ya utandawazi na elimu ambazo ni moja ya sababu ya baadhi ya tamaduni kuanza kupotea na katika hili serikali itasimamia kuendeleza tamaduni zile zilizo nzuri ila kwa zile zilizo mbaya kama ukeketaji kwa watoto wakike serikali itaendelea kupiga vita.

Kwa upande wa Mratibu wa Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (Four Corner Cultural Programme – 4CCP) Bi.Eliminata Awet alieleza kuwa kituo hicho kilianzishwa kwa lengo la kuhifadhi historia ya makundi ya lugha ya jamii hizo nne ambazo zinapatikana barani Afrika baada kuoneka katika Mkoa wa Manyara umebarikiwa kuwa na jamii zote nne ambapo ni suala la kujivunia na kulitangaza duniani.

“Kituo cha 4CCP kimekuwa kikiandaa tamasha hili kwa mara ya saba sasa ikiwa lengo ni kutangaza tunu hii ya nchi hii kubarikiwa kuwa na makabila haya manne yanayopatikana barani Afrika na yanaonekana kuanza kupotea kufuatia mabadiliko mbalimbali ya kijamii kama elimu na utandawazi,”alisema Bi Awet.

Halikadhalika nae Mbunge wa Mbulu Vijijini Mhe. Flatei Massey aliipongeza wizara hiyo yenye dhamana na masuala ya utamaduni kwa namna inavyojitahidi kuwa karibu na wadau wake wa kisekta kwani hii inatia faraja ya kuona kuwa serikali inajali shughuli zao.

Hata hivyo Katibu Mkuu huyo aliagiza kila mkoa kuanzisha kituo cha kiutamaduni ambacho kitahifadhi historia ya kabila la watu wa mkoa huo pamoja na mila na desturi zao kwa ajili ya vizazi vijavyo kutokana hali ya utandawazi kuanza kupoteza masuala ya kiutamaduni na vituo hivyo vinaweza kutumika kama sehemu ya utalii wa kiutamaduni.

BENKI YA CRDB TAWI LA QUALITY CENTER WASHERHEKEA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA DUNIANI

$
0
0

Keki maalum kwa ajili ya kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani ambapo Benki ya CRDB tawi la Quality Center ilifanya tafrija fupi pamoja na wateja wake.


Baadhi ya wateja wakiweka saini kama kumbukumbu wakati wa hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani iliyofanyika katika tawi la Quality Center.

Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja.

MC wa hafla hiyo Adeline Mushi.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center akiwasalimia baadhi ya wateja wa benki hiyo waliofika katika hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani.


Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementine Kinabo, akizungumza na wateja wa benki hiyo wakati wa hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani.


Wafanyakazi na wateja wa benki wakiwa katika hafla hiyo.

Baadhi ya wateja waliohudhuria hafla hiyo.

Meneja Biashara wa Benki ya CRDB, Joyce Ngarauo, akizungumza kuhusu huduma wanazotoa.

Baadhi ya wateja.

Ofisa wa Benki ya CRDB, Kiwelu Muheza, akizungumza na wateja.

Ofisa wa Benki ya CRDB, Jane John, akisindikizwa na wafanyakazi wenzake wakati akienda kuzungumza na wateja.

Ofisa wa Benki, Jane John, akizungumza na wateja.

Wakala wa Benki ya CRDB akiuliza swali.

Baadhi ya wateja wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.

Ofisa wa Benki ya CRDB, David Nyakubega, akizungumza na wateja.

Mteja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Dk. Judith Mhina, akizungumza wakati wa hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani.

Mteja wa Benki ya CRDB, Ezra Chiwelesa, akizungumza katika hafla hiyo.

Ofisa wa Benki ya CRDB, Adeline Mushi, akifuatilia hotuba ya Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementine Kinabo (hayupo pichani).

Wateja wa Benki ya CRDB wakiwa na furaha.

Clementine akipongezana na Dk. Judith Mhina.

Meneja akipongezana na mteja.
Mteja wa Benki ya CRDB, Godwin Mugisa, akikata keki ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani.

Meneja wa Benki ya CRDB, tawi la Quality Center, Clementine Kinabo (kulia), akikata keki wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki, ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani.

Mteja wa Benki ya CRDB, Godwin Mugisa, akilishwa keki na Clementine Kinabo.

Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementine Kinabo, akilishwa keki na mteja.
Keki ikitayarishwa kwa ajili ya wateja.

Mteja wakilishwa keki.

Dk. Judith Mhina, akilishwa keki katika hafla hiyo.

Mmoja wa wateja akilishwa keki.

Meneja Biashara wa Benki ya CRDB, Joyce Ngarauo, akimlisha keki mteja wa benki hiyo.

Meneja wa Benki ya CRDB, tawi la Quality Center, Clementine Kinabo (kushoto), akijiandaa kumkumbatia mteja wa benki hiyo, Dk. Judith Mhina, wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani.

Kufungua Champagne.

Kufungua Champagne.

Champagne.

Wateja wakipata Champagne.

Wateja wakipata Champagne.

Hafla ikiendelea.

Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center (kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na wateja wa benki hiyo.

Wateja wa Benki ya CRDB wakigonganisha glasi na Meneja wa Tawi la Quality Center Clementine Kinabo (wa pili kushoto) wakati wa hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani.

Wateja wa Benki ya CRDB wakigonganisha glasi na maofisa wa benki hiyo wakiongozwa na Meneja wa Tawi la Quality Center Clementine Kinabo (wa pili kushoto) wakati wa hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani.

Clementine Kinabo (kushoto), akigonganisha glasi na wateja wa benki ya CRDB wakati wa hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani.

Clementine Kinabo (kushoto), akigonganisha glasi na wateja wa benki ya CRDB wakati wa hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani.

Clementine Kinabo (kushoto), akigonganisha glasi na wateja wa benki ya CRDB wakati wa hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani.

Clementine Kinabo (kushoto), akigonganisha glasi na wateja wa benki ya CRDB wakati wa hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani.

Clementine Kinabo (kushoto), akigonganisha glasi na wateja wa benki ya CRDB wakati wa hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani.

Clementine Kinabo (kushoto), akigonganisha glasi na wateja wa benki ya CRDB wakati wa hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani.

Wateja wakijumuika katika chakula cha jioni.

Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementine Kinabo (wa pili kushoto), akipata chakula na wateja wa benki hiyo.

Wafanyakazi na wateja wa Benki ya CRDB wakipata chakula.

Wateja wa Benki ya CRDB wakipata chakula.
Wafanyakazi na wateja wa Benki ya CRDB wakipata chakula.
Wateja wa Benki ya CRDB wakipata chakula.

Wateja wakipata chakula katika hafla hiyo.

Maofisa wa Benki ya CRDB pamoja na wateja wakipata chakula.
Mofisa wa Benki ya CRDB wakipata chakula.

Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakipata chakula.

Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center, Clementine Kinabo (kushoto), akiwa na wateja wake.

Muziki ukichukua nafasi yake.

Baadhi ya wateja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakicheza muziki.

Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Quality Center akionyesha umahili wa kusakataka dansi.

Muziki wa dansi.

Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika picha ya pamoja.

OCD KYERWA ATUHUMIWA KUSINDIKIZA KAHAWA YA MAGENDO

$
0
0
*Waziri Mkuu aagizwa achukuliwe hatua

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi awachukulie hatua askari polisi wote wa wilaya ya Kyerwa wanaotuhumiwa kusindikiza kahawa ya magendo inayouzwa nchi jirani akiwemo Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo, Justin Joseph.

Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Oktoba 7, 2018) baada ya kukagua kiwanda cha kukoboa kahawa cha Nkwenda wilaya Kyerwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi mkoani Kagera. Katika ziara hiyo Waziri Mkuu ameambatana na Mkewe Mama Mary Majaliwa.

“Askari polisi wa wilaya ya Kyerwa pamoja na OCD wao wanatuhumiwa kusindikiza kahawa inayosafirishwa kwa njia ya magendo kwenda nchi ya jirani kupitia njia mbalimbali zisizo rasmi zikiwemo za Kumisongo, Kashaijo na Omukatoma.”

Waziri Mkuu amesema ni jambo la hatari kama askari Polisi wanasindikiza kahawa inayouzwa kwa magendo, hivyo ameagiza jambo hilo lidhibitiwe haraka.”Marufuku kupeleka kahawa nje ya nchi kwa njia ya magendo na polisi msishiriki katika butura.”

Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu amesema kuanzia msimu ujao wa kahawa, minada yote ya kahawa inayozalishwa mkoani Kagera itafanyika ndani ya mkoa huo badala ya kufanyika Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Waziri Mkuu amesema minada yote ya kahawa ikifanyika mkoani Kagera itawawezesha wakulima kulipwa fedha zao kwa muda mfupi na pia itapunguza makato  yasiyokuwa ya lazima ambayo ni kero kwa wakulima.

“Wanunuzi watafuata kahawa ilipo, utaratibu huu utawawezesha wakulima kulipwa fedha zake kwa wakati. Mnada ukifanyika katika maeneo ya uzalishaji utamuwezesha mkulima kujua bei, tofauti na unavyofanyika Moshi kwani ni rahisi mkulima kuibiwa.”

Waziri Mkuu amewataka wananchi kuendelea kuwa na imani na Serikali yao ambayo imedhamiria kuwaletea maendeleo na kwamba itahakikisha kila mmoja anapata haki yake wakiwemo wakulima ambao watasaidiwa katika kutafutiwa masoko ya mazao yao.

 IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, OKTOBA 7, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Kiwanda cha Kukoboa Kahawa cha Kaderes kilichopo eneo la Nyakatuntu wilayani Karagwe Oktoba 7, 2018.  Kulia ni Mkewe Mary na kushoto ni Mkurugenzi  wa kiwanda, Leonard Kachobonaho. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco  Elisha Gaguti. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuui, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia) wakimfariji mtoto , Mathews Martin aliyelazwa katika Kituo cha Afya cha Kayanga wilayani Karagwe, Oktoba 7, 2018. Kushoto ni Mama wa mtoto huyo, Joyce Martin.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimwagilia mti alioupanda baada ya kutembelea Kituo cha Afya cha Kayanga kilichopo Karagwe, Oktoba 7, 2018. Wapili kulia ni mkewe Mary.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakiwapungia wananchi wakati walipowasili kwenye uwanja wa Kayanga Changarawe, Karagwe kuhukutubia mkutano wa hadhara, Oktoba 7, 2018.
 Askari wa akiba wakiwadhibiti  wananchi waliokuwa na shauku ya kumuona Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasili kwenye uwanja wa kayanga Changarawe kuhutubia mkutano wa hadhara, Oktoba7, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MBUNGE MWINGINE WA CHADEMA KUTOK SIMANJIRO JAMES OLE MILLYA ATANGAZA KUACHIA NGAZI CHADEMA NA KUREJEA CCM

$
0
0
 
Mbunge wa jimbo la Simanjiro Mhe. James Ole Millya leo ametangaza kujivua uanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kuomba kurejea ndani ya chama chake cha zamani CCM


BENKI YA CRDB YAAHIDI KUENDELEA KUWASHIKA MKONO SHULE YA WASICHANA YA MARIAN

$
0
0
Benki ya CRDB yaahidi kuendelea kuwashika mkono shule za Marian kwa kutoa kiasi cha tsh milioni 5 ili ziweze kusaidia katika maendeleo ya shule hiyo. Hayo ameyasema Meneja wa Tawi la Bagamoyo Bi. Nitike Nsekela wakati alipohudhuria katika mahafali ya kitado ya nne yaliyofanyika mjini Bagamoyo mjini. 

Bi. Nitike amesema ni jukumu la jamii kwa ujumla kuungana katika malezi ya vijana na si kuachia majukumu walimu. "Niwaombe wazazi tuungane pamoja katika malezi ya watoto wetu maana kipindi hiki cha utandawazi kinaharibu sana kizazi chetu, tuwe walinzi tusiwatupie majukumu walimu tu," amesema.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Bagamoyo mjini Bi. Nitike Nsekela ambaye alikuwa mgeni rasmi akitoa nasaha kwa wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Wasichana Marian wakati wa mahafali yaliyofanyika Bagamoyo-Pwani. Jumla ya wahitimu wapatao 113 wanatarajia kufanya mtihani wa Taifa kumaliza kidato cha nne 2018.
 Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Bagamoyo mjini Bi. Nitike Nsekela ambaye alikuwa mgeni rasmi akimkabidhi Mkuu wa shule ya Wasichana ya Marian ya Bagamoyo Mwalimu Martin Kakwezi hundi yenye thamani ya Tshs milioni 5 ikiwa ni mchango wao katika maendeleo ya shule hiyo. Meneja Msaidizi wa Shule ya Wasichana ya Marian Padre Mugisha akitoa nasaha kwa wahitimu. Mkuu wa shule ya Wasichana ya Marian ya Bagamoyo Mwalimu Martin Kakwezi akitoa wasifu wa shule yao.
  Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Bagamoyo mjini Bi. Nitike Nsekela ambaye alikuwa mgeni rasmi akiwakabidhi wanafunzi vyeti na zawadi zilizotolewa kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao.
Wahitimu wakifuatilia. Wazazi waliohudhuria mahafali hayo.
Burudani toka kwa wanafunzi.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images