Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1691 | 1692 | (Page 1693) | 1694 | 1695 | .... | 1898 | newer

  0 0
 • 10/07/18--13:06: RUDI TTCL KUMENOGA-MWANRI

 • Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri( wa pili kutoka kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania Waziri Kindamba (kushoto) na viongozi wengine wa Shirika hilo wakiwa na bango lenye maneno ya lugha ya Kinyamwezi yenye maana RUDI NYUMBANI KUMENOGA wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo jana mkoani humo.
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania Waziri Kindamba( wa pili kutoka kushoto) wakionyesha umahiri wa kuzirudi ngoma jana wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya RUDI NYUMBANI KUMENOGA mkoani humo.
  1
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(katikati) akipata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania juu ya huduma mbalimbali zinatolewa na Shirika hilo jana wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya RUDI NYUMBANI KUMENOGA mkoani humo.
  2
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiwapungia mkono wakazi wa Manispaa ya Tabora wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya RUDI NYUMBANI KUMENOGA ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ilifanyika mkoani humo jana .
  3
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kulia walikaa) akiwa na wakazi wa Manisapaa ya Tabora wakisikiza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania Waziri Kindamba( hayupo katika picha) juu ya huduma mbalimbali zinatolewa na Shirika hilo jana wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya RUDI NYUMBANI KUMENOGA mkoani humo.
  4A
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania Waziri Kindamba akitoa maelezo kuhusu huduma mbalimbali zinatolewa na Shirika hilo jana wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya RUDI NYUMBANI KUMENOGA mkoani humo.
  5A
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akipata maelezo  wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya RUDI NYUMBANI KUMENOGA mkoani humo jana.picha na Tiganya Vincent
  RS TABORA  NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA

  WAKAZI wa Mkoa wa Tabora wametakiwa kuliunga mkono Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa kujiunga na huduma mbalimbali wanazotoa ili liweze kuendelea kutoa gawio kubwa kwa Serikali kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi wote hapa nchini.

  Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya rudi nyumbani kumenoga mkoani humo.

  Alisema kuwa kupitia gawio ambalo Shirika hilo linatoa kwa Serikali kati ya fedha hizo zinakuja Mkoani humo kwa ajili ya kuimarisha miundo mbinu ya barabara, huduma za maji, shule , ununuzi wa dawa, ulipaji wa mishahara ya watumishi na shughuli mbalimbali za maendeleo.

  “Ndugu zangu TTCL kumenoga turudi…ukiongeza salio kwenye simu yako hata usipotumia mwezi salio lako liko salama…hivi sasa huduma zao hazihitaji kupanda kwenye mti ndio ufanye mawasiliano, bali popote unawasiliana…hakuna kusema sogea pembeni sikusikii ndio upige simu…hivi sasa hata ukiwa hata porini TTCL inapatikana” alisema.

  Mwanri alisema kwa kuunga mkono huduma za TTCL watakuwa nao wajiwekea akiba ya kurudishiwa sehemu ya huduma walizochangia kwa njia ya Serikali kupata gawio na hatimaye kurejesha sehemu ya fedha hizo katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

  Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwa kuwa huduma zake zinapatikana katika maeneo mengi hapa nchini ni muhimu kwa wakulima na wafanyabiashara kulitumia kwa kutafuta masoko ya mazao.

  Naye Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Waziri Kindamba alisema Shirika hilo hivi sasa limeanza kutoa gawio kwa Serikali ambapo mwezi Juni mwaka huu lilitoa bilioni 1.5 , jambo ambalo lilishindikana kwa kipindi takribani maika 17.

  Alisema juhudi za Shirika hilo linalenga kuhakikisha huduma zake zinapatikana nchini kote na kuwafikia wananchi popote walipo kwa asilimia 100 katika muda mfupi ujao.

  Kindamba alisema lengo ni kusaidia katika kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi wa viwanda , huduma za jamii na maendeleo ya Sekta nyingine kwa kutumia huduma za Shirika hilo.

  Alisema mwelekeo wa Shirika pia ni kusaidia juhudi za Serikali katika kukusanya mapato kupitia malipo yanayofanyika kwa njia ya Mtandao.

  0 0

   Wasanii walioingia Tano Bora wakiwa kwenye picha ya pamoja na chief judge Adam Mchomvu.
   Majaji wa shindano la kusaka wasanii wenye vipaji Tigo Fiesta Supa Nyota mkoani Iringa wakiongozwa na Adam Mchomvu(wapili toka kulia) wengine toka kushoto ni Rodgers Eight, Lord Eyes na kulia Joh Makini mchuano uliofanyika leo mjini Iringa.
  Wasanii wawili walipita kwenye mchujo wa Tigo Fiesta Supa Nyota 2018 mkoani Iringa Ester Queen na TTP ambao itawabidi wapande Leo usiku kwenye jukwaa la Tigo Fiesta kupata mshindi atayeiwakilisha Iringa


  0 0

  0 0  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akipewa maelezo na Rehema Abdalah ambaye amekuwa akiishi karibu na kisima ambacho kiligunduliwa na Wajerumani mnamo karne ya 15 . Maji ya kisima hicho hutumika katika kufanya matambiko kwa wenyeji wa maeneo hayo na pia watu mbalimbali wamekuwa wakifika na kuchota maji katika kisima na kuyanawa wakiamini kuwa ni dawa na yamekuwa yakito mikosi. Naibu Waziri huyo ametembelea eneo hilo ikiwa ni maadhimisho ya urithi wa utamaduni wa Mtanzania pamoja na Siku ya Mikindani lengo likiwa ni kuenzi na kutunza mji huo ambao ni lango la utalii wa mambokale kwa mikoa ya Kusini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akipewa maelezo na Rehema Abdalah ambaye amekuwa akiishi karibu na kisima ambacho kiligunduliwa na Wajerumani mnamo karne ya 15 . Maji ya kisima hicho hutumika katika kufanya matambiko kwa wenyeji wa maeneo hayo na pia watu mbalimbali wamekuwa wakifika na kuchota maji katika kisima na kuyanawa wakiamini kuwa ni dawa na yamekuwa yakito mikosi. Naibu Waziri huyo ametembelea eneo hilo ikiwa ni ,maadhimisho ya urithi wa utamaduni wa Mtanzania pamoja na Siku ya Mikindani lengo likiwa ni kuenzi na kutunza mji huo ambao ni lango la utalii wa mambokale kwa mikoa ya Kusini
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akipewa maelezo na Mzee Mohamedi Kidume kuhusiana na Nyumba aliyofikia na kulala aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwl. Julius Kambarage Nyerere katika nyumba hiyo ambayo kwa sasa imekuwa gofu. Naibu Waziri huyo ametembelea eneo hilo ikiwa ni maadhimisho ya urithi wa utamaduni wa Mtanzania pamoja na Siku ya Mikindani lengo likiwa ni kuenzi na kutunza mji huo ambao ni lango la utalii wa mambokale kwa mikoa ya Kusini
  Baadhi ya maandishi yanayoonesha kuwa Mji Mkongwe wa Mikindani umetangzwa rasmi kwenye gazeti la serikali, Mji huo utafungua milango ya watlii kwa mikoa ya Kusini.
  Baadhi wananchi wakimskiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizindua Mji Mkongwe wa Mikindani ambao umetangazwa kuwa ni kituo cha Urithi wa Taifa na kivutio cha Utalii
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa tatu kushoto) akipewa maelezo na Meneja Mradi wa Trade Aid,Emmanuel Mwambie( wapili kushoto) kuhusiana na ukarabati wa Old Boma la ambayo kwa sasa inatumika kama hoteli na pia kama kituo cha kufundishi vijana zaidi ya 400 kuhusiana na kozi ya ukarimu kwa watalii. Naibu Waziri huyo ametembelea eneo hilo ikiwa ni siku ya urithi wa utamaduni wa Mtanzania pamoja na Siku ya Mikindani lengo likiwa ni kuenzi na kutunza mji huo ambao ni lango la utalii wa mambokale kwa mikoa ya Kusini. Wanne kulia ni Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania, Monica Mussa
  ( PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-WMU)
   
  Wizara ya Maliasili na Utalii imeagizwa ishirikiane na wadau wa utalii wenye nia ya kuwekeza kwenye majengo na maeneo ya kihistoria yaliyopo nchini kwa kuboresha hali ya majengo hayo ili yaweze kudumu kwa muda mrefu zaidi na yaendelee kutumika kama kivutio cha Utalii.

  Pia, Wizara hiyo imeagizwa ianze mara moja ukarabati wa jengo ambalo Mwl.Nyerere alifikia na kulala kwa muda wa siku mbili wakati wa harakati za kupigania uhuru kutoka kwa wakoloni. Maagizo hayo yametolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga wakati kisoma hotuba kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa katika maadhimisho ya siku ya tamasha la urithi wa Mtanzania na siku ya Mikindani iliyofanyika katika Manispaa ya Mtwara Mikindani.

  Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Mhe. Hasunga ameutangaza mji Mkongwe wa Mikindani kuwa ni kivutio rasmi cha Urithi wa Utamaduni na Malikale hapa nchini kufuatia kuhifadhiwa kwake rasmi kisheria kwa tangazo la Serikali namba 308 la mwezi Julai mwaka huu. Kufutia juhudi hizo za Serikali za kutaka kuongeza idadi ya watalii,Waziri huyo amesema juhudi hizo zitasaidia kutangaza na kuhamasisha jamii kupenda na kuenzi utamaduni wao na hivyo kuulinda na kuutumia utamaduni kama fursa ya kukuza utalii kwa mikoa ya kusini.

  Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amesema tamasha hilo limekuwa muhimu kwa Wanamtwara kwa vile linafungua milango kwa watu binfasi pamoja na Mashirika kuwekeza kwenye utalii wa mambokale. Ameongeza kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa utalii wa ukanda wa kusini hali itakayopelekea majengo mengi ambayo yamechakaa sana yaweza kukarabatiwa baadala ya kutegemea Wizara pekee.

  Kwa upande wake, Kaimu Naibu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Andy Karas, ameipongeza Serikali kwa hatua inazozichukua za kuhakikisha maeneo yenye historia yanatunzwa na kuenziwa. Mji mkongwe wa Mikindani ni mojawapo ya maeneo yenye majengo mengi mazuri ya kihistoria yaliyojengwa karne ya 15 na 19 wakati wa utawala wa kikoloni hapa nchini.

  0 0


  Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa Pili kushoto) akizindua huduma ya umeme katika Kijiji cha Madebe wilayani Handeni mkoani Tanga. Wa Pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe.


  Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kushoto) akimkabidhi kifaa cha UMETA, Mbunge wa Bumbuli, January Makamba ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira. Waziri wa Nishati alitoa vifaa vya Umeta 30 kwa Mbunge huyo ili kuwawezesha wananchi kuunganishwa na huduma ya umeme bila kutandaza nyaya ndani ya nyumba.
  Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akiwasalimia wananchi katika Kijiji cha Mahezangulu katika Jimbo la Bumbuli wilayani Lushoto mara baada ya kufika kijijini hapo kukagua kazi ya usambazaji umeme vijijini.
  Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Nkelei wilayani Lushoto ambapo pia alizindua huduma ya umeme katika Kijiji hicho.
  Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizidua rasmi huduma ya upatikanaji wa umeme katika Kijiji cha Mabugai wilayani Lushoto, Mkoa wa Tanga.  Afanya ziara wilayani Handeni, Lushoto na kuwasha umeme katika Vijiji Vitano

  Katika kuhakikisha kuwa adhma ya Serikali ya kusambaza umeme katika vijiji vyote nchini ifikapo mwaka 2021 inatekelezwa, Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amefanya ziara katika Wilaya ya Handeni na Lushoto mkoani Tanga ili kukagua kazi za usambazaji umeme vijijini na kuwasha umeme katika baadhi ya vijiji.

  Akiwa wilayani Handeni, Waziri wa Nishati aliwasha umeme katika Kijiji cha Madebe, Nyasa na Kwamnele na wilayani Lushoto aliwasha umeme katika Kijiji cha Mabugai na Nkelei. Aidha alifanya ziara katika kata na Vijiji mbalimbali ambavyo bado havijasambaziwa umeme ikiwemo Kijiji cha Mahezangulu kilicho katika Jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto ambapo aliagiza kuwa, kiwashiwe umeme ifikapo tarehe 12 mwezi huu.

  Katika ziara yake wilayani Handeni, Viongozi wa Wilaya hiyo walimweleza kuwa, kuna vijiji 10 ambavyo vimepitiwa na miundombinu ya umeme lakini havina nishati hiyo, hivyo kuleta malalamiko miongoni mwa wananchi kuwa walitoa maeneo yao kupisha miundombinu hiyo lakini hawapati umeme. Kuhusu suala hilo, Dkt Kalemani aliagiza kuwa, kuanzia Jumatatu ya tarehe 8 Oktoba, 2018 wataalam wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) waanze utaratibu wa kupeleka umeme katika Vijiji hivyo kwani kinachohitajika ni kusambaza tu umeme kwa wananchi hao kwa kuwa miundombinu ipo.

  Katika hatua nyingine, Dkt Kalemani alitoa onyo kuwa, Meneja yeyote wa TANESCO atakayeonekana anatetea wakandarasi wanaochelewesha kazi kwa kisingizio cha kutokuwa na vifaa atakuwa amejihesabia kuwa kashindwa kazi. “ Hawa wakandarasi tayari wameshalipwa fedha za kuwawezesha kuanza kazi ya usambazaji umeme vijijini, hivyo wanatakiwa kuwa na vifaa vyote vinavyohitajika katika kazi hii,” alisema Dkt Kalemani.

  Vilevile aliwataka watumishi kuwa na lugha ya staha pale wanapohudumia wananchi na kueleza kuwa atakayeshindwa kufanya hivyo ataondolewa katika nafasi yake. Ziara ya Dkt Kalemani wilayani Handeni na Lushoto ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Wilaya hizo, Wabunge, Madiwani na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba.

  0 0

  NAIBU Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Joseph Kakunda amezindua mpango wa mashindano ya mbio za baiskeli na kufanikisha kukusanya Sh milioni 280 kati ya Sh milioni 340 zinazotarajiwa kukusanywa kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu nchini.

  Mashindano hayo yaliyopewa jina la 'Acacia Imara Pamoja Cycle Challenge', yameandaliwa na Kampuni ya Uchimbaji wa Madini nchini -Acacia kwa kushirikiana na Tasisi binafsi kutoka nchini Canada - CanEducate.

  Akizungumza katika uzinduzi wa uchangiaji wa mashindano juzi jijini Dar es Salaam, Kakunda alitoa wito kwa wadau mbalimbali nchini kuchangia mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 3, mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

  Kakunda ambaye alimwakilisha Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo alisema malengo ya mashindano hayo yanaenda sambamba na malengo ya serikali katika kurahisisha mazingira ya utoaji elimu nchini. "Tangu Rais John Magufuli aingie madarakani na kufuta ada za shule pamoja na ada za ziada, hadi mwaka jana kumekuwapo na ongezeko la asilimia 44 la uandikishaji wanafunzi wapya wa elimu ya awali, ongezeko la asilimia 33 la uandikishaji wanafunzi wapya wa darasa la kwanza na wanafunzi wapya wanaojiunga na elimu ya sekondari wameongezeka kutoka 366,396 mwaka 2015 hadi 483,216 mwaka 2017", alisema.

  Alisema hatua hizo zinahitaji ushirikiano wa wadau mbalimbali kama wanavyofanya Acacia katika kufikia malengo ya serikali.Aidha, Mkurugenzi wa Acacia nchini, Asa Mwaipopo alisema kwa mwaka jana pekee kampuni hiyo imejenga madarasa na kukarabati mabweni yenye uwezo wa kubeba wanafunzi 100 wa kike katika Shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo wilayani Kahama.

  Pia imefanikisha ujenzi wa maktaba sita katika shule zinazozunguka migodi ya kampuni hiyo."Tangu tuanze kushirikiana na CaEducate mwaka 2011 katika kuboresha sekta ya elimu nchini, Acacia imetumia zaidi ya sh milioni 450 zilizofikia shule 20 na wanafunzi zaidi ya 5000.

  "Acacia pia imewekeza katika mfumo maalumu wa utoaji wa mafunzo kwa vitendo (IMTT) kwa vibarua au wanagenzi wanaotoka katika vijiji vinavyozunguka migodi yetu."Mafunzo hayo yaliyoanza mwaka 2009 kwa kushirikiana na Veta na Chama cha Wachimbaji wa Madini nchini, Acacia imetumia zaidi ya Sh bilioni 3.3 kutoa mafunzo hayo kwa wanagenzi 744 katika migodi yake mitatu ya Bulyanhulu, North Mara na Buzwagi," alisema.

  Pia alisema tangu mwaka 2008 Acacia imetumia Sh bilioni moja kusaidia wanafunzi wa elimu ya juu wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (MUHAS).Aliongeza kuwa, kwa mujibu wa ripoti ya ukaguzi wa kampuni ya kimataifa ya Ernst and Young iliyotolewa mwaka jana, ilionesha kuwa Acacia imechangia Sh trilioni 1.61 katika uchumi wa Tanzania sawa na asilimia 1.5 ya Pato la Ndani la Taifa.

  "Kutokana na hali tunatoa wito kwa wadau wote kujitokeza kwa wingi kuunga mkono juhudi za Acacia katika kuboresha sekta ya elimu nchini, " alisema.Naye Rais wa taasisi ya CanEducate, Rishi Ghuldu alisema kila mwaka taasisi hiyo huwezesha kielimu wanafunzi 270 na kutoa nafasi 11 za udhamini wa masomo ya elimu ya juu katika vyuo mbalimbali duniani.

  Alisema tasisi hiyo imelenga kuboresha sekta ya elimu ili kusaidia familia maskini kupiga hatua kimaendeleo.Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha alitoa wito kwa Acacia kuelekeza nguvu zaidi katika ujenzi wa mabweni na hosteli ili kuwasaidia wanafunzi wanaotumia umbali mrefu kufika shuleni.

  Wakati mmoja wa wanufaika wa mpango huo wa CanEducate, Yunista Marwa ambaye ni mhitimu wa kidato cha sita, alitoa wito kwa Acacia kuendelea kuwasaidia wanafunzi wanaotoka katika kaya maskini ili waweze kuzisaidia familia zao na jamii kwa ujumla.
  Meneja Mkuu Uhusiano na Uwezeshaji wa Jamiii kutoka kampuni ya Acacia Bi Noleen Dube akiwashukuru wadau waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa kuchangia elimu nchini kupitia mashindano ya baiskeli yanayofahamika ' Acacia Pamoja Imara Cycle Challenge' yanayotarajiwa kufanyika jijini Mwanza mwezi Novemba. Wengine ni pamoja na Naibu Waziri -Tamisemi, Joseph Kakunda (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Acacia, Asa Mwaipopo, (wa tatu kulia) na Rais wa taasisi ya CanEducate ambayo ndio inaratibu mpango huo kwa kushirikiana na Acacia Bw. Rishi Ghuldu.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Acacia, Peter Geleta (wa kwanza kushoto), kulia kwake ni Meneja Uhusiano na Uwezeshaji ya Jamii, Noleen Dube, Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia, Mhandisi Asa Mwaipopo na Naibu Waziri - Tamisemi, Joseph Kakunda pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa mpango wa mashindano ya mbio za baiskeli, "Acacia Imara Pamoja Cycle Challenge" yenye lengo la kukusanya Sh milioni 340 kusaidia wanafunzi wasiomudu gharama za elimu nchini.
  Mkurugenzi wa Acacia, Asa Mwaipopo akizungumza katika hafla ya kuzindua mpango wa kuchangia mashindano ya mbio za baiskeli yanayotarajiwa kufanyika Novemba 3, 2018 katika uwanja wa Kirumba jijini Mwanza kwa lengo la kuchangia huduma za elimu nchini.
  Rais wa Tasisi ya CanEducate, Rishi Ghuldu akizungumza katika hafla ya kuzindua mpango wa kuchangia mashindano ya mbio za baiskeli, 'Acacia Imara Pamoja Cycle Challenge' yanayotarajiwa kufanyika Novemba 3, 2018 katika uwanja wa Kirumba jijini Mwanza kwa lengo la kuchangia huduma za elimu nchini.
  Mmoja wa wanufaika wa Mpango wa kusaidia wanafunzi wasiomudu gharama za elimu katika familia duni zinazonguka migodi ya Acacia, Yunista Marwa akizungumza katika hafla hiyo, namna mpango huo wa CanEducate ulivyomsaidia kuanzia kidato cha pili hadi alipohitimu kidato cha sita.


  Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Joseph Kakunda akizungumza katika hafla ya kuzindua mpango wa kuchangia mashindano ya mbio za baiskeli yanayotarajiwa kufanyika Novemba 3, 2018 katika uwanja wa Kirumba jijini Mwanza kwa lengo la kuchangia huduma za elimu nchini.

  0 0


  Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed kulia akifanya ziara ya kutembelea Hospitali ya Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja kuangalia Miradi na mafanikio mbalimbali yanayo patikana katika hospitali hiyo.
  Daktari wa Hospitali ya Makunduchi Vuai Abdalla (MD) akimuelezea Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed maendeleo na changamoto zinazowakabili katika Hospitali hiyo.
  Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akisalimiana na Mzazi Asia Issa Hassan mkaazi wa Makunduchi aliyekuja kujifungua katika Hospitali hiyo na kumuelezea furaha yake ya kufuata uzazi wa Mpango.
  Muonekano wa Jengo litakalotumika kama Makaazi ya Madaktari kwa ajili ya kuondoa usumbufu wa Madaktari waliokuwa hawana nyumba ya kuishi katika Hospitali hiyo.
  Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akimsikiliza Mpishi wa kituo hicho Suleiman Mohammed Suleiman aliyekuwa akimuelezea changato wanazokabiliana nazo katika kutoa huduma ya chakula.

  Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar

  0 0

  - Wateja kupata fursa kutoa mawazo kuboresha huduma.

  Ikiwa katika shamrashamra ya kuadhimisha miaka 3 ya utoaji wa huduma kwa watanzania, Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel, kwa mara ya kwanza imetangaza mpango wa kutoa huduma ya zawadi kwa wateja wake ambao watatoa mawazo katika kusaidia uboreshaji wa huduma kwa wateja.

  Mpango huo uliopewa jina la “LONGA TUSONGE” pamoja na faida zingine una lengo la kuwashirikisha wateja wote pamoja na wafanyakazi wa Halotel katika kufanya maboresho ya utoaji huduma mbalimbali kupitia mawazo yao wakati huu ambapo kampuni hiyo inapoadhimisha miaka mitatu ya utoaji huduma zake za Mawasiliano hapa nchini.

  Akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa mpango huo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Mhina Semwenda, amesema kuwa, mkakati huo ni sehemu ya kuthamini mchango mkubwa wanaoutoa wateja wake tangu kuanza kutolewa kwa huduma kupitia mtandao huo hapa nchini .

  Amesema tangu kuingia kwa huduma za Mtandao huo wa Halotel, wamekuwa wakipata matokeo mazuri ya wateja wake wanaondeelea kutumia huduma zake mbalimbali hadi wakati huu ambapo wanakuja na mpango huo mpya wa “LONGA TUISONGE”

  Amesema kupitia mpango huo wa mwaka mmoja, wateja wa mtandao huo watapewa nafasi ya kutoa mawazo yao mbalimbali ya kuboresha huduma za Halotel ambayo baadae yatachujwa na kwa yale yatakayokidhi matakwa yatapitishwa na kuwa huduma rasmi ndani ya mtandao huo.

  “Hii fursa kubwa kwa wateja wetu walioko nchi nzima katika kutambua na kuthamini mchango wao mkubwa ambao wamekuwa wakituunga mkono tangu tuanze kutoa huduma za mawasiliano hapa nchini. Lengo letu kubwa ni kuhakikisha wanaendelea kupata huduma bora za mawasiliano zinazotokana na mahitaji yao katika nyanja mbalimbali za kijamii na kiuchumi kupitia Mtandao wa Halotel.” Alisema Semwenda.

  Amesema huo ‘LONGA TUSONGE” ni mpango Shirikishi unaolenga kupokea mawazo mbalimbali ya wateja wake wote ili kujua kitu gani wangependa kiboreshwe au kiongozwe katika huduma zinazotolewa hatua ambayo pamoja na mambo mengine itawasaidia kuendelea kunufahika na huduma za mtandao huo.

  Aidha mkuu huyo wa mawasiliano amesema zawadi hizo zitatolewa kwa wateja watakaotoa mawazo bora kupitia mitandao ya kijamii ya kampuni hiyo, namba ya huduma kwa wateja, maduka ya Halotel yaliyopo nchi nzima, pamoja na barua pepe (callcentre@halotel.co.tz). Zawadi zitakazotolewa kwa washindi wenye mawazo bora ni pamoja na Simu aina ya smatiphone, Muda wa maongezi, 4G router, na fedha Taslimu.

  “Zawadi hizi ni moja ya mikakati ya kutoa motisha kwa wateja wetu na watanzania kwa ujumla ikiwa ni moja ya shukrani yetu kwao katika shamrashamra za kuadhimisha miaka 3 ya kutoa huduma hivyo Halotel ni mtandao wao na wanao uhuru wa kushiriki katika kutoa maoni kuhusu namna ambavyo sisi kama kampuni tunaweza kuboresha huduma. Aliongeza Semwenda.

  “Tunapenda kuwaalika wateja wetu wote walioko nchi nzima kushiriki kikamilifu katika mpango huu, na sisi kama kampuni tuko tayari kuwasilikiza, kuyapokea na kuyafanyia kazi maoni yao ambayo yatazidi kuwa chachu ya kutoa huduma bora”. Alisisitiza Semwenda

  Aidha aliongeza kuwa mtandao wa Halotel ambao huduma zake zinapatikana maeneo mengi nchini itandelea kujikita zaidi na zaidi katika kutoa huduma bora kwa wateja wake wote ikiwa ndiyo sababu kuu ya kuanzishwa kwake hapa nchini.


  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel Mhina Semwenda,(kushoto) akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa mpango wa kutoa ya zawadi kwa wateja wake ambao watatoa mawazo katika kusaidia uboreshaji wa huduma kwa wateja uliopewa jina la Longa Tusonge. Kulia ni Msaidizi wa Mkuu wa kitengo cha Huduma kwa wateja Anthony Thobias.
  Msaidizi wa kitengo cha Huduma kwa wateja Anthony Thobias ( kushoto) akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa mpango wa kutoa ya zawadi kwa wateja wake ambao watatoa mawazo katika kusaidia uboreshaji wa huduma kwa wateja uliopewa jina la “Longa Tusonge”. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel Mhina Semwenda.

  0 0

  Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam
  8 Oktoba, 2018.

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kukusanya jumla ya Shilingi Trilioni 3.84 kwa kipindi cha miezi mitatu ya Mwaka wa Fedha 2018/19 ikiwa ni kuanzia Julai hadi Septemba, 2018 ikilinganishwa na shilingi trilioni 3.65 ambazo zilikusanywa kipindi kama hicho katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Richard Kayombo amesema kiasi hiki ni sawa na ukuaji wa asilimia 5.32 na kuongeza kuwa ukusanyaji wa mapato hayo umekuwa ukiongezeka kila mwezi.

  “Katika mwezi Julai, 2018, TRA ilikusanya jumla ya shillingi trillioni 1.20 sawa na ukuaji wa asilimia 9.20, mwezi Agosti, 2018 jumla ya shilingi trillioni 1.27 zilikusanywa ikiwa ni sawa na ukuaji wa asilimia 5.86 wakati mwezi Septemba, 2018 mamlaka ilikusanya jumla ya shilingi trillioni 1.36 ambayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 1.65,” alisema Kayombo.

  Kayombo amewashukuru walipakodi wanaoendelea kulipa kodi zao kwa hiari na wakati na amewahimiza wale wote ambao bado wanasuasua kujitokeza kulipa kodi hizo na wale wenye changamoto mbalimbali wametakiwa kufika katika ofisi za TRA mikoani na wilayani ili kuonana na mameneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania.

  Aidha, Kayombo amesema TRA inaendelea na zoezi la kupokea maombi ya misamaha ya riba na adhabu katika malimbikizo ya madeni ya kodi za nyuma ambapo ameeleza kuwa mpaka sasa jumla ya walipakodi 1,950 wamewasilisha maombi ya kusamehewa riba na adhabu ambayo yanafikia jumla ya shilingi bilioni 185.4.

  “Mwitikio wa walipakodi kuomba msamaha wa wa riba na adhabu ni mkubwa na unaridhisha na kuna baadhi ya walipakodi waliowasilisha maombi ambao wameshapewa majibu na wengine wako katika hatua mbalimbali za kushughulikiwa maombi yao. Hivyo, nachukua fursa hii kuwakumbusha wafanyabiashara ambao hawajawasilisha maombi wawahi kuwasilisha maombi hayo kabla ya tarehe 30 Novemba, 2018.

  Mkurugenzi Richard Kayombo ametoa wito kwa walipakodi na wananchi wote kwa ujumla kuendelea kulipa kodi kwa hiari na wakati na kuwaasa wale wote wanaojishughulisha na vitendo vya kugushi risiti za kielektroniki za EFD nchi nzima hasa maeneo ya Kariakoo, kuacha mara moja kwa sababu wakibainika watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
   Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo (katikati), akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza makusanyo ya robo mwaka ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2018/19 kuanzia Julai hadi Septemba, 2018 ambapo TRA imefanikiwa kukusanya jumla ya Shilingi Trilioni 3.84. Kulia kwake ni Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi Diana Masalla na kushoto kwake ni Meneja Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Grabriel Mwangosi.
  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano ambao Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo (hayupo pichani) ametangaza makusanyo ya robo mwaka ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2018/19 kuanzia Julai hadi Septemba, 2018 ambapo TRA imefanikiwa kukusanya jumla ya Shilingi Trilioni 3.84.

  0 0


  Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote 2018 limeendelea usiku wa kuamkia jumatatu kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa. Hii ni mara ya tatu mfululizo kwa kampuni ya simu za mkononi Tigo kudhamini tamasha hilo.

  Akizungumza mbele ya umati wa mashabiki waliohudhuria tamasha hilo Mkuu wa wilaya ya Iringa mjini, Richard Kasesela amepongeza kampuni ya Tigo kwa kuwaletea burudani na fursa mbalimbali kwa wakazi wa Iringa. " Hii ni fursa ya pekee kwa wakazi wa mji huu ambayo kampuni ya Tigo imetuletea kwa mara nyingine ndani ya mkoa huu" Ukiondoa Burudani, pia wafanyabiashara wamenufaika sana ndani ya wiki nzima alisema Kasesela.

  Pia mkuu huyo wa wilaya aliweza kupata nafasi ya kumkabidhi zawadi ya Keki kwa msanii Chege Chigunda kwa kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake.

  Kwa upande wa Burudani wasanii wa kundi la Weusi ndio waliofunika kwenye tamasha hilo ilipopelekea mashabiki kuomba wasitoke kwenye jukwaa na kundi la Weusi walifanya hivyo hadi mwisho wa shoo kwa kuimba nyimbo zao nyingi za kuvutia zikiwemo, Madaraka,Swagire, NiCome na nyingine nyingi.

  Mdhamini mkuu wa msimu huu, kampuni ya Tigo imewakumbusha mashabiki wote wa muziki kufurahia promosheni zake tatu murwa katika msimu hii wa vibes. ‘Data Kam Lote inawapa wateja hadi mara mbili ya vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#. Hii itawawezesha wateja wa Tigo kufurahia msimu huu wa vibes kupitia mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+.

  Tigo pia inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Kwa Sumbawanga, tiketi zitakazonunuliwa kwa mfumo wa Tigo Pesa Masterpass QR zitagharimu TSH 5,000 pekee badala ya TSH 7,000 kwa watakaonunua kwa pesa taslim, Wateja wanapaswa kupiga *150*01# na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.

  Wateja wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za kila wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia. 

   Msanii wa Bongo Fleva Chege akiwa kwenye jukwaa la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote usiku wa kuamkia Jumatatu tamasha lililofanyika  kwenye uwanja wa Samora Mjini Iringa
    Mkuu wa Wilaya ya Iringa , Richard Kasesela akilishwa keki na msanii Chege ambaye usiku wa Tigo Fiesta mjini Iringa ilikuwa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa
    Mkuu wa Wilaya ya Iringa , Richard Kasesela (mbele kulia) akicheza pamoja na wasanii waliotoa burudani kwenye Tamasha Kubwa la Tigo Fietsa 2018 Vibe Kama Lote  uwanja wa Samora Mjini Iringa Usiku wa kuamkia jumatatu
   
    Mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota 2018 mkoani Iringa kwa jina la usanii PPT akitoa burudani kwenye jukwaa la Tigo Fiesta
   Baadhi ya mashabiki waliojitokeza kwenye onesho hilo la Tigo fiesta mjini Iringa

  0 0

  NA FREDY MGUNDA,NJOMBE.

  UMOJA wa Wanawake Mkoa wa Njombe chini ya Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Ndugu Rosemary Lwiva na katibu wake Ndugu Angela Milembe wamezindua kadi maalum ya kuwezesha kujiimarisha kiuchumi katika Jumuiya hiyo.

  Uzinduzi huo umezinduliwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Ndugu Theresia Mtewele katika Baraza la UWT Mkoa wa Njombe lililofanyika jumamosi tarehe 6 Oktoba 2018. Kilele cha harambee hiyo kinatarajiwa kufungwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa siku za mbeleni.

  Awali Ndugu Theresia Mtewele amewapongeza UWT Mkoa wa Njombe kwa kuwa wabunifu na namna wanavyofanya kazi kwa umoja.Aidha Ndugu Theresia Mtewele amewaomba Viongozi wa UWT wawe chachu ya kukemea maovu yanayotokana na unyanyaswaji, ukandamizaji na uonevu kwa wanawake na watoto. Pia katika kukuza uchumi wa Jumuiya amewataka UWT kuifanya ajenda ya kujiimarisha kiuchumi kuwa endelevu ili kuifanya jumuiya hiyo kujitegemea kiuchumi waweze kuendesha vizuri shughuli zao za kila siku na kuacha alama katika uongozi wao.

  MNEC amewaomba pia wajikite kuimarisha uhai wa jumuiya kwa kuwa na mkakati maalum wa kuingiza wananchama wapya na kuendelea kushirikiana na wanachama wa zamani ikiwa ni pamoja na ulipaji ada.Katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 amewaomba waweke mkakati kabambe wa kuhakikisha CCM inashinda mitaa yote ya mkoa wa Njombe pia wawahamasishe wanawake kugombea nafasi mbalimbali na kuwaelimisha umuhimu wa kichagua viongozi wanaotokana na chama cha mapinduzi.

  MNEC amewaomba UWT waisemee vizuri serikali na kuwalinda viongozi wao ikiwemo wabunge na madiwani kwa kuwatia moyo na kutoruhusu wasaka vyeo kuwaingilia katika majukumu yao kwa kuanza kampeni mapema.Baraza hilo limehudhuriwa na wabunge wa viti maalum mkoa wa Njombe Mh . Dkt . Suzan Kolimba na Mh. Neema Mgaya . Wabunge hao wameomba wanawake wa Mkoa wa Njombe kuendelea kuwapa ushirikiano ili waweze kutekeleza majukumu yao vema.Mwisho, katika uzinduzi huo MNEC alichangia shilingi 1,000,000/=. Zoezi hilo liliambatana na ugawaji wa hati za pongezi kwa viongozi ambao wamekua na mchango mkubwa kwa Jumuiya katika Mkoa wa Njombe.

  Mbunge viti maalum Neema Mgaya akikabidhiwa hati ya pongezi na Mgeni rasmi MNEC Bi. Theresia Mtewele kwa kutoa mchango mkubwa wa kuijenga jumuiya hiyo
  Mwenyekiti wa UWT (W) Njombe Bi. Angel Mwangeni akikabidhiwa hati ya pongezi na Mgeni rasmi MNEC Bi. Theresia Mtewele
  Mbunge viti maalum Dkt. Suzan Kolimba akikabidhiwa hati ya pongezi na Mgeni rasmi MNEC  Bi. Theresia Mtewele

  0 0

   Maziko ya Mtangazaji wa RTD Ahmed Jongo  yamefanyika leo  makaburi ya Mbagala Charambee Dar es Salaam
   Baadhi ya Ndugu,Jamaa na marafiki wakiwa wamejumuika nyumbani leo mchana kwenye mazishi ya aliyekuwa Mtangazaji mkongwe wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo,nyumbani kwake  kwake Tandika Maghorofani,jijini Dar es Salaam.
    Baadhi ya Ndugu,Jamaa na marafiki wakijadiliana jambo nyumbani kwa marehemu aliyekuwa Mtangazaji mkongwe wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo,nyumbani kwake Tandika Maghorofani,jijini Dar Es Salaam.
   Sehemu ya waombolezaji wakiwamo ndugu,jamaa na marafiki wakijadiliana jambo nyumbani kwa marehemu aliyekuwa mtangazaji nguli wa  Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo,nyumbani kwake Tandika Maghorofani,jijini Dar Es Salaam.
    Miongoni mwa ndugu, jamaa na marafiki wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa nyumbani kwa aliyekuwa Mtangazaji mkongwe wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo Tandika Maghorofani ambaye amefarikia dunia jana.
   Baadhi ya  ndugu, jamaa na marafiki wakiwa katika picha ya pamoja nyumbani kwa marehemu aliyekuwa Mtangazaji mkongwe wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo,nyumbani kwake Tandika Maghorofani,jijini Dar es Salaam.
    Waombolezaji wakijadiliana jambo katika msibani  wa marehemu aliyekuwa Mtangazaji nguli wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo,nyumbani kwake Tandika Maghorofani,jijini Dar es Salaam.
    Baadhi ya  ndugu, jamaa na marafiki wakipata chakula cha mchana nyumbani kwa marehemu aliyekuwa Mtangazaji mkongwe wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo,nyumbani kwake Tandika Maghorofani,jijini Dar es Salaam.
   Ndugu, jamaa na marafiki wakiwa katika picha ya pamoja nyumbani kwa marehemu aliyekuwa Mtangazaji maarufu wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo,nyumbani kwake Tandika Maghorofani Dar es Salaam.

  0 0  The UBA Foundation and Gavi will leverage the United Bank for Africa’s network and expertise to invest in Africa’s health system, starting with Nigeria.


  Dr Seth Berkley, CEO of Gavi, the Vaccine Alliance and Mr. Kennedy Uzoka, UBA Group CEO and Chairman of the UBA Foundation as they announce the partnership agreement between the two institutions towards strengthening health systems and raise awareness of immunisation across Africa, starting in 2018 with Nigeria

  New York, 28 September 2018 - Gavi, the Vaccine Alliance and the UBA Foundation, the Corporate Social Responsibility arm of the United Bank for Africa Group, have joined together to strengthen health systems and raise awareness of immunisation across Africa, starting in 2018 with Nigeria.

  “We are delighted to work with the UBA Foundation to help protect children across Nigeria against some of the world’s deadliest diseases,” said Dr Seth Berkley, CEO of Gavi the Vaccine Alliance. “Strong, sustainable health systems are key to ensuring no child misses out on lifesaving vaccines which is why this partnership will make a real difference, reducing child mortality and helping to meet the Sustainable Development Goals in 2030."

  The partnership with the UBA Foundation aims to raise US$ 1.5 million over the next two years by leveraging UBA’s network of partners to support Gavi’s immunisation programmes in Nigeria. The UBA Foundation will also advocate for immunisation in Nigeria, which has one of the lowest vaccine coverage rates in the world.

  “The United Bank for Africa and the UBA Foundation have been impacting lives positively in Nigeria and across the African continent for several decades, and this is another opportunity to make a difference in the lives of millions of Africans," said Kennedy Uzoka, UBA Group CEO and Chairman of the UBA Foundation. “We are proud of the partnership with Gavi which will run until the end of 2020, with both institutions focused on the overall aim to provide innovative solutions that can increase the capacity of healthcare systems in Nigeria and across Africa."

  In the last five years over 14 million children in Nigeria have been vaccinated against some of the world’s deadliest diseases with support from Gavi. If Nigeria meets its targets for vaccine coverage, it will be able to prevent at least one million deaths by 2028.

  "However, Nigeria needs to invest more domestic resources in health and immunisation,” said Dr Berkley. ”The private sector can be a crucial partner to help leverage expertise and provide new solutions to ensure children across Nigeria have the opportunity to lead long, healthy lives.”


  ABOUT UBA FOUNDATION


  United Bank for Africa (UBA), Africa’s global bank, is committed to being a socially responsible company and role model for all businesses in Africa. UBA recognises the need for a social contract between the bank, the community and its people. To this end, UBA became one of the first banks in Africa to institute a Foundation, the UBA Foundation. UBA Foundation has been impacting lives positively on the African continent for over a decade.

  ABOUT Gavi, the Vaccine Alliance

  Gavi, the Vaccine Alliance is supported by donor governments (Australia, Brazil, Canada, Denmark, France, Germany, India, Ireland, Italy, Japan, the Kingdom of Saudi Arabia, Luxembourg, the Netherlands, Norway, the People’s Republic of China, Principality of Monaco, Republic of Korea, Russia, South Africa, Spain, the State of Qatar, the Sultanate of Oman, Sweden, Switzerland, United Kingdom, and United States), the European Commission, Alwaleed Philanthropies, the OPEC Fund for International Development (OFID), the Bill & Melinda Gates Foundation, and His Highness Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan, as well as private and corporate partners (Absolute Return for Kids, Anglo American plc., The Children’s Investment Fund Foundation, China Merchants Group, Comic Relief, Deutsche Post DHL, the ELMA Vaccines and Immunization Foundation, Girl Effect, The International Federation of Pharmaceutical Wholesalers (IFPW), the Gulf Youth Alliance, JP Morgan, “la Caixa” Foundation, LDS Charities, Lions Clubs International Foundation, Majid Al Futtaim, Orange, Philips, Reckitt Benckiser, Unilever, UPS and Vodafone).

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Watanzania wameombwa kuenzi vitu vya asili ili kudumisha utamaduni na kuvutia watalii wengi kuja nchini.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga alipokua anazungumza na Menejimenti ya Bodi ya Utalii Nchini baada ya kuwatembelea ofisini Kwao. 

  Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Waziri amesema kuwa moja ya vitu ambayo watanzania wanatakiwa kuvidumisha ni utalii wetu ili kuweza kuongeza pato la Taifa.Amesema, kwenye baadhi ya sehemu ambazo zimesahaulika ni Utalii wa Utamaduni kitu kinachopelekea kupotea kwa tamaduni zetu ikiwemo vyakula, mavazi, sanaa za mkono na michoro, michezo pamoja na lugha ya Kiswahili. 

  Amesema, kuanzia mwaka huu wameweka mwezi Septemba kuwa mwezi wa Utamaduni utakaokuwa unajulikana kama Urithi Festival ambapo kutakuwa na maonesho mbalimbali ya vitu vya utamaduni ili kuvutia watu wa nje waje kujionea namna utamaduni wa watanzania ulivyo.Hasunga amesema kuwa, lengo kuu la maonesho hayo ni kuongeza watalii nchini ikiwemo na kuongeza mapato ya ntaifa kutoka Dola Bilioni 1.2 kwa mwaka na kuwa zaidi ya hiyo.

  'Tanzania ina vivutio vingi vua utalii ila vimekuwa vikiharibiwa na watanzania wenyewe na kusababisha Tanzania kushuka kutoka nafasi ya pili hadi ya nane kwenye vivutio vya utalii duniani unaotokana na uvamizi wa wakulima na uvamizi wa mifugo kwenye hifadhi za taifa," amesema 

  " Kwa sasa serikali inataka kuondoa mfumo wote na kurudisha hadhi ya hifadhi zote ili kuboresha utalii ikiwemo wa ndani kutokana na kushuka kutoka watalii laki nane (800,000) kwa mwaka na kufikia watalii laki sita na elfu ishirini na nne (602,400)," amesema Hasunga. 

  Hasunga amesema kuwa kumekuwa na utofauti mkubwa sana kulinganisha na nchi zingine katika kutembelewa na watalii ambapo kwa nchi kama Misri wamekuwa wanapokea watalii Milioni 10 kwa mwaka, Morroco wakipata watalii Milioni 13 huku Afrika Kusini wakipata watalii Milioni 1,500,000. 

  Akisisitiza zaidi, Naibu Waziri amewataka TTB kujitangaza zaidi kwa kila kivutio kilichopo kwenye mkoa, , kutumia Digital Market, kutengeneza makala (video) zinazohusu vivutio, kuweka mabango barabarani ikiwezekana baadhi ya barabara wakabidhiwa kabisa Bodi hiyo. 

  Akijibu hoja za Naibu Waziri, Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Devotha Mdachi amesema kuwa katika upande wa makala wapo katika hatua za kukamilisha na wanatarajia kuzindua mwakani mwezi Machi na utazinduliwa nchini Ujerumani. Amesema kuwa, makala hizo zitaelezea zaidi kuhusu utalii wa ndani, hata hivyo matarajo ya kuongeza watalii wa ndani kwa kuongeza mabalozi ambapo wka sasa wana mabalozi tisa kutoka sehemu mbalimbali nchini. 

  Aidha, ameweka wazi msimamo wa TTB kwenye kutangaza utalii ikiwemo kutumia baadhi ya mashirika ya ndee kama Qatar, ligi kuu ya Uingereza na tayari makampuni mengine kama Emirates wapo kwenye mazungumzo.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea bodi ya Utalii Nchini (TTB) na kuzungumza na menejimenti nzima na kuwataka kutanaza vivutio vya hapa nchini.
  Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Devotha Mdachi akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelewa naNaibu Waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga na kumuahidi kutekeleza yale aaliyowaagiza.

  0 0

  Taasisi ya isiyo ya Kiserikali inayojishughulisha na maswala ya Mazingira pamoja na Utu (HDIECA) , iliandaa maonesho maalum ambayo yaliwakutanisha wajasiliamali mbalimbali ambao wanafanya shughuli zao kwa kutumia mikono yao kwa lengo la kurudisha shukurani zao kwa  jamii kutokana na wananchi kupokea na kushirikiana nao vyema katika kazi zao mbalimbali wanazozifanya kila siku.

  Maonesho hayo yalifanyika katika viwanja vya Azura Kawe Jijini Dar es Salaam na hakukuwa na kiingilio chochote kwa wananchi na wajasiliamali hawakulipia kitu ilikuwa ni Bure kabisa.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti wajasiliamali wengi waliishukuru taasisi hivyo kwa kuwapa fursa hiyo hata ya kuonesha kazi zao na kufahamiana na watumbalimbali na pia kuongeza wigo wa kibiashara kwa kupata wateja wapya.
  Baadhi ya wadau mbalimbali wakiwa wanatazama bidhaa  za wajasiliamali 
  Mmoja wa wajasiliamali (Aliyevaa T-shirt nyeupe) akitoa maelezo ya namna dawa zake za asili zinazofanya kazi.
  Mkurugenzi wa Taasisi ya  HDIECA Bi. Sarah Pima  (aliyevaa kofia) akiwa katika moja ya banda la mjasiliamali kuangalia bidhaa ya unga wa lishe wakati wa maonesho hayo.
  Mmoja wa wajasiliamali (anayenyoosha kidole) akimpa maelekezo mgeni aliyetembelea banda hilo kuhusiana na kazi zao za sanaa wanazozifanya ikiwa ni pamoja na kuchora.
  Mmoja wa wajasiliamali(aliyevaa ushungi) akiwa anamuuzia mteja Juice zake ambapo moja ya Juice iliyokuwapo ni ya Mapalachichi.
   Katika maonesho hayo kulikuwa na wajasiliamali wanaotengeneza vitu mbalimbali kwa mikono yao ambapo pamoja na yote waliomba ikiwezekana watengewe sehemu ambayo watakuwa wanapeleka bidhaa zao na kuziuza hata mara moja kwa mwezi.
  Wananchi wakiendelea kutazama Bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na watanzania 
   Wa kwanza kulia ni Dada mbunifu ambaye yeye anabadili matairi chakavu kuwa mapambo na vitu kw ajili ya matumizi mbali mbali, mfano hawa wadau walio kaa ukiacha (aliyevaa kofia ya njano) vimetengenezwa kwa mataili, vitu hivyo walivyo kalia unaweza weka viatu, Nguo za watoto, kuna stuli za kukalia pia.
  Watu wakendelea kutazama bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na watanzania .
   Wajasiliamali mbalimbali pamoja na waandaaji wa maonesho hayo wakiwa katika picha ya pamoja
   Moja ya Banda la mjasiliamali anayetengeneza Batiki
    Moja ya Banda la mjasiliamali anayetumia chupa chakavu zilizotupwa anaokota na kuziongezea thamani kwa kuviwekea marembo kwa kutumia nyuzi vitambaa na nakshi nakshi zengine
    Moja ya Banda la mjasiliamali anayetengeneza bidhaa zao kwa kutumia mishumaa na maua ya asili
    Moja ya Banda la mjasiliamali anayetengeneza Bangiri, Hereni, Cheni na vitu mbalimbali kwa kutumia Shanga
    Moja ya Banda la mjasiliamali anayetengeneza Note Book kwa kuvalishia kava la kitenge
   Mjasiliamali anayeuza Ubuyu wa nazi
    Moja ya Banda la mjasiliamali anayetengeneza mafuta ya aina mbalimbali
    Moja ya Banda la mjasiliamali anayetengeneza mapambo mbalimbali kwa kutumia kamba na misumali.
  Haya hapa chini yote ni matairi, mjasiliamali huyu anayaongezea thamani yanakuwa  kama yanavyo onekana hapa.
  Aliyevaa kofia ya njano anaitwa Bw. Nzowa yeye baada ya kusikia kuwa kutakuwa na wajasilamali wanafanya maonesho yao na yeye akaja na Gereji yake inayotembea kwa lengo la kuona kama anaweza kupata fursa na kutengeneza Magari lakini pia kutoa elimu ya namna gereji ya kutembea inavyofanya kazi.Picha zote na Fredy Njeje


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza  katika kikao cha kupokea Taarifa ya Maendeleo ya Ujenzi wa Ikulu ya Chamwino Dodoma kutoka kwa wataalamu mbalimbali wanaohusika na ujenzi huo. Wakwanza kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi na wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu Dkt. Moses Kusiluka 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stergomena Tax mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam leo Oktoba 8, 2018  
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stergomena Tax wapili kutoka kushoto mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji  Mnyepe wapili kutoka kulia akifatiwa na  Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara hiyo Bw. Shio. Kushoto ni Msaidizi wa Rais Maswala ya Diplomasia Balozi Zuhura Bundala
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza Balozi wa Kenya nchini Mhe. Dkt. Dan Kazungu baada ya kukutana na  kufanya  naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 8, 2018

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Kenya hapa nchini Mhe. Dkt. Dan Kazungu pamoja na Naibu Balozi wa Kenya Mhe. Boniface Muhia Ikulu jijini Dar es Salaam

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea mfano wa Hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 125 kutoka kwa Balozi wa Kenya hapa nchini Mhe. Dkt. Dan Kazungu  Kwa ajili ya Rambirambi ya nchi hiyo kwa Tanzania kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere huko Mwanza mwezi uliopita. PICHA NA IKULU


  0 0


  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa (CCM), Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Kushoto), akiwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma, Mhe. Felista Bura (Katikati) wakiingia kwenye ukumbi ulipofanyika Mkutano Mkuu Maalumu wa Jimbo la Kondoa ambapo Dkt. Kijaji, aliwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Kipindi cha Miaka 3 ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano katika Jimbo lake
   Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa (CCM), Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi-CCM, katika kipindi cha miaka 3, katika Jimbo la Kondoa, wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Jimbo la Kondoa uliofanyika katika Kata ya Pahi, Kondoa, mkoani Dodoma.

  Mume wa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa (CCM), Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Dkt. Kachwamba, akiwasalimia wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Jimbo la Kondoa, wakati mke wake alipowasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi- CCM, katika kipindi cha miaka 3, katika Jimbo hilo.

  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Mkoa wa Dodoma, Comrade Godwin Mkanwa, akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Jimbo la Kondoa, baada ya kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano katika Jimbo hilo, iliyowasilishwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa (CCM), Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji.

  Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Amina Mollel, akifuatilia kwa makini matukio ya uwasilishwaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Kipindi cha Miaka 3 ya Serikali ya Awamu ya Tano katika Jimbo la Kondoa. Walioketi karibu naye ni wazazi wa Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Mzee Abdallah Kijaji na mkewe Aziza Selemani, katika Kata ya Pahi, Kondoa, Dodoma

  Sehemu ya umati wa wajumbe 1,200 wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Jimbo la Kondoa, wakipokea Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Kipindi cha Miaka 3 ya Serikali ya Awamu ya Tano katika Jimbo la Kondoa, iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, katika Kata ya Pahi, Kondoa, mkoani Dodoma.
  Mkazi wa Kijiji cha Pahi, wilayani Kondoa mkoani Dodoma, Bi. Jezila Jumanne, akisoma kwa makini kitabu cha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Kipindi cha Miaka 3 ya Serikali ya Awamu ya Tano katika Jimbo la Kondoa, kilichotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kondoa, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji.

  …………………..


  Na Mwandishi wetu, Kondoa

  NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa mkoani Dodoma, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo elimu, maji, afya, miundombinu ya barabara na huduma nyingine za kijamii zimeimarika zaidi katika Jimbo la Kondoa katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

  Dkt. Kijaji ameeleza hayo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika Jimbo lake katika Mkutano Mkuu Maalumu wa Jimbo la Kondoa uliowashirikisha zaidi ya wajumbe 1,200, uliofanyika katika Kata ya Pahi, wilayani Kondoa.

  Ameyataja baadhi ya mafanikio makubwa kuwa ni kuchimba na kukarabati visima virefu na vifupi vya maji vipatavyo 56 pamoja na kukarabati visima vingine 4 vilivyoharibika zaidi ya miaka 15 iliyopita ambapo zaidi ya sh. bilioni 1.8 zimetumika, hatua iliyochangia wananchi zaidi ya laki moja katika Jimbo la Kondoa kuanza kupata huduma ya uhakika ya maji.

  Kuhusu Sekta ya Elimu, Dkt. Kijaji ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu, miundombinu ya elimu ikiwemo ujenzi wa shule mbili mpya za Sekondari katika Kata za Hondomairo na Bumbuta kwa gharama ya sh. milioni 140.5, ambazo zitaanza kuchukua wanafunzi kuanzia mwezi Januari, 2019 pamoja na kujenga na kukarabati vyumba ya madarasa, mabweni na nyumba za walimu, kwenye shule mbalimbali za Sekondari na msingi.

  Alisema kuwa hatua hiyo imesababisha kuongezeka kwa ufaulu wa wanafunzi wa shule za msingi kutoka asilimia 37 mwaka 2014 hadi asilimia 68 mwaka jana na kwa upande wa Sekondari, ufaulu umepanda kutoka asilimia 41 hadi asilimia 79.

  Katika Sekta ya Afya, Dkt. Kijaji amebainisha kuwa katika jimbo lake, Serikali inajenga vituo vipya vya afya vinne kwa gharama ya zaidi ya sh. bilioni 2.3 pamoja na zahanati kadhaa hatua ambayo amesema vitakapo kamilika, changamoto za upatikanaji wa huduma za afya zitapungua kwa kiasi kikubwa.

  “Tangu uhuru hadi mwaka 2015, sawa na miaka 54, Jimbo la Kondoa lilikuwa na vituo vya afya vitatu tu, lakini katika kipindi cha miaka mitatu cha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano, tunajenga vituo vya afya vinne, na kupanua huduma za afya katika Kituo kimoja cha afya ili kitoe huduma ya upasuaji, haya ni mafanikio makubwa” alisema Dkt. Kijaji.

  Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi aliyealikwa kwenye Mkutano Mkuu huo maalumu wa Jimbo la Kondoa, Dkt. Bashiru Ally, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma, Bw. Godwin Mkanwa, amempongeza Dkt. Ashatu Kijaji, kwa kutekeleza kwa umakini na umahili mkubwa ahadi za Chama hicho kwa wananchi.

  Bw. Mkanwa ametoa wito kwa watendaji wa Serikali mkoani mwake kuendelea kutatua kero zinazoikabili jamii ikiwemo migogoro ya ardhi na upatikanaji wa huduma muhimu za jamii pamoja na kuwataka viongozi wa Chama na Serikali kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa za mapato na matumizi ya vijiji vyao.

  Baadhi ya wanachama walioshiriki mkutano Mkuu Maalumu huo wa CCM Jimbo la Kondoa, wameeleza kuridhika na utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye maeneo yao na kumpongeza Mbunge wao, Dkt. Ashatu Kijaji kwa kusimamia ahadi zake hatua ambayo imesababisha kuonekana kwa maendeleo kwenye kata zao ikiwemo ubora wa huduma za afya, maji, ujenzi wa barabara na madaraja pamoja na upatikanaji wa mikopo kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

  Jimbo la Kondoa linaundwa na Tarafa tatu, Kata 21, vijiji 84, vitongoji 386 na kuna matawi 172 ya Chama cha Mapinduzi, na kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Jimbo hilo lina idadi ya watu wapatao 234,185

  0 0

   
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakizungumza na Bibi Saura Venant na aliyempakata mwanae, Anord Revocatus (kushoto) na Bibi Dorothea Fidel aliyempakata mwanane Redemta Deobey (wapiki kushoto) wakati awalipotembelea wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya cha Kimeya wilayani Muleba, Oktoba 8, 2018.

  aziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakimjulia hali, Consolata Marios na mwanae Revina Albert wakati walipotembelea wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya cha Kimeya wilayani Muleba, Oktoba 8, 2018.

  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akiwasalimia wananchi wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye Kituo cha Afya cha Kimeya wilayani Muleba, Oktoba 8, 2018.


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wapili kulia) wakipata maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa wilaya ya Muleba, DKt. Modest Buchari (kulia) wakati walipokagau ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kimeya wilayani Muleba (kulia), Oktoba 8, 2018.Wanne kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti.

  Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Kimeya wilayani Muleba, Oktoba 8, 2018

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (watano kushoto) wakitazama ngoma ya asili wakati walipowasili kwenye kituo cha Afya cha Kimeya wilayani Muleba, Oktoba 8, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti na wanne kushoto ni Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka.

  Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa na Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa AnnaTibaijuka (mwenye gauni la bluu) wakicheza ngoma ya asili wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowasili kwenye Kituo cha Afya cha Kimeya wilayani Muleba kuhutubiua mkutano wa hadhara, Oktoba 8, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  ………………….


  * Ifikapo Jumatano awe amepeleka walimu shule ya msingi Rwenzige

  *Ina wanafunzi 216 wa darasa la awali hadi la nne bila mwalimu
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku mbili kwa Kaimu Afisa Elimu (Msingi) wa wilaya ya Muleba, mkoani Kagera Bw. Bukuru Malembo awe amepeleka walimu wawili katika shule ya msingi iliyoko kwenye kitongoji cha Rwenzige kwa kuwa haina mwalimu hata mmoja.

  Shule hiyo yenye madarasa wawili na ofisi moja ya mwalimu ina jumla wanafunzi 216 wa darasa la awali hadi la nne, ilijengwa na wananchi ambapo wanafunzi wake wanafundishwa na mwananchi mmoja aliyemua kujitolea ili kuwapunguzia watoto kutembea umbali wa kilomita 16 kwenda kusoma katika shule ya kijiji cha Kiteme.

  Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana (Jumatatu, Oktoba 8, 2018) baada ya wanafunzi wa shule hiyo kuwasilisha malalamiko yao kwa njia ya bango wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kiwanja cha kituo cha afya Kimeya, baada ya kukagua majengo ya kituo hicho.

  “Haiwezekani watoto wadogo wenye umri wa kuanzia miaka mitano wakatembea umbali wa kilomita 16 kwenda shule wakati katika kitongoji chao kuna shule yenye madarasa mawili na chumba kimoja cha ofisi ya mwalimu na Afisa Elimu hadi sasa hajapeleka walimu na kumuachia mwalimu Benson (kijana ambaye si mwalimu ila anajitolea kufundisha) akifundisha wanafunzi hao peke yake.”

  Waziri Mkuu alimuagiza Afisa Elimu huyo ahakikishe ifikapo Jumatano (Oktoba 10, 2018) saa nne asubuhi awe ameshawapeleka walimu hao katika shule hiyo ya msingi ili waweze kuwafundisha wanafunzi hao na kisha Mkuu wa wilaya hiyo, Mhandisi Richard Ruyango awasilishe taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo ofisini kwake. “Walimu wengi mmewaacha katika shule za barabarani huku za vijijini zikiwa hazina walimu.”

  Kwa upande wake, Bw. Benson Bukerebe (29) maarufu mwalimu Benson alisema yeye kitaaluma si mwalimu bali ni mhitimu wa kidato cha nne, alimua kuanzisha darasa kwa ajili ya kuwafundisha wanafunzi hao kwani alikuwa akiwahurumia kwa sababu baadhi yao hawakuwa na uwezo wa kutembea umbali wa kilomita 16 hadi iliko shule ya msingi ya Kiteme.

  Kijana huyo alisema kwa muda wote huo ameweza kumudu kuwafundisha wanafunzi hao kwa kutumia vitabu vya kuazima kutoka shule mbalimbali za msingi, lengo ni kuhakikisha watoto wenye umri wa kuanza shule katika kitongoji chao wanapata fursa ya elimu ambayo ni haki yao ya msingi.

  Katika hatua nyingine,Waziri Mkuualisema Serikali imeweka sheria kali ili kuwalinda watoto wa kike na wanatakiwa kuheshimiwa katika jamii kwa kuachwa waendelee na masomo yao bila ya usumbufu wa aina yoyote na atakayebainika kukatisha masomo yao atachukulia hatua kali za kisheria.

  Alisema Serikali itatoa adhabu kali ya kifungo cha miaka 30 jela kwa mtu atakayekatisha elimu ya mtoto wa kike iwe kwa kumuoa, kumpa ujauzo na hata ukikutwa naye nyumbani kwako na katika nyumba ya wageni.“Tukikukuta na binti wa shule katika kona isiyoeleweka tunakukamata na kukuchukulia hatua za kisheria. Ole wenuvijana, mkibainika mmewapa mimba mabinti wanaosoma, adhabu yake ni miaka 30 jela.”

  Waziri Mkuu alisema kwa wazazi au walezi watakaowaozesha watoto kike ambao bado ni wanafunzi na kwa upande wa wazazi watakaomsindikiza mtoto wao wa kiume kwenda kuoa mwanafunzi wote watachukuliwa hatua za kisheria.

  0 0

  Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) zimejipanga kuzuia na kudhibiti madhara yanayosababishwa na machafuko ya kisiasa katika jumuiya hiyo na Bara la Afrika kwa ujumla. Wawakilishi wa nchi hizo wamekusanyika nchini Malawi kuanzia tarehe 1 Oktoba hadi 17 Oktoba 2018 kwa ajili ya kufanya mazoezi ya namna ya kutuliza ghasia pamoja na kutoa misaada ya kibinadamu kwa waathirika katika kipindi cha machafuko

  Wawakilishi wa Tanzania kutoka Jeshi la Wananchi, Magereza na taasisi za kiraia ikiwemo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni miongoni mwa watu 600 wanaoshiriki zoezi hilo lililopewa jina la EX UMODZI CPX 2018 na kaulimbiu ya Afrika ni Amani na Maendeleo (Africa for peace and prosperity).

  Katika hafla ya ufunguzi wa mazoezi hayo iliyofanyika leo tarehe 08 Oktoba, 2018 katika Chuo cha Kijeshi cha Malawi kilichopo mji wa Salima takriban kilomita 120 kutoka Lilongwe, Naibu Waziri wa Ulinzi wa Malawi, Mhe. Evaton Chemulirenji alisema mazoezi hayo ni utekelezaji wa maazimio ya SADC na Umoja wa Afrika (AU) wa kuandaa kikosi cha kukabiliana na machafuko barani Afrika (Standby Force-SF) ambacho kinatakiwa kiwe kimekamilika ifikapo Januari 2019.

  Alisema madhumuni ya mazoezi hayo ni kuhakikisha kuwa kikosi cha SF kinapewa mafunzo ya vitendo ya kutosha ili kiwe na ujuzi na mbinu za kushiriki operesheni za kulinda amani na/au kuingilia kati na kuzuia machafuko (peace keeping and enforcement) pale yanapotokea barani Afrika. Aidha, alisema mazoezi hayo ni muhimu kwa kuwa yatasaidia kuimarisha ushirikiano na kuaminiana baina ya nchi wanachama wa SADC.

  Mazoezi hayo yanajumuisha makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na majeshi ya ulinzi, askari polisi, askari magereza na raia wa fani tofauti kama vile za Utawala wa Sheria, siasa, mawasiliano, Utawala, haki za binadamu na jinsia ambao wana mchango mkubwa katila masuala ya operesheni za kulinda amani. 

  Wanajeshi watafanya zoezi la namna ya kutuliza machafuko na raia watajifunza namna ya kusaidia jamii punde tu machafuko yanapodhibitiwa na vikosi vya usalama.

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
  Salima, Malawi

  Naibu Waziri wa Wizara ya Ulinzi wa Jamhuri ya Malawi, Mhe. Evaton Chimulirenji akitoa hotuba wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi wa mafunzo na mazoezi ya namna ya kutuliza ghasia pamoja na kutoa misaada ya kibinadamu kwa waathirika katika kipindi cha machafuko iliyofanyika tarehe 08 Oktoba, 2018 katika Chuo cha Kijeshi cha Malawi kilichopo katika mji wa Salima nje kidogo ya jiji la Lilongwe.Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Sekretarieti ya SADC yanajumuisha makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na majeshi ya ulinzi, askari polisi, askari magereza na raia wa fani tofauti kama vile za Utawala wa Sheria, siasa, mawasiliano, Utawala, haki za binadamu na jinsia ambao wana mchango mkubwa katila masuala ya operesheni za kulinda amani. 

  Mratibu wa Program ya Mafunzo yanayofanyika nchini Malawi akieleza mpangilio wa program ya mafunzo hayo kwa ujumla 

  Mratibu Mkuu wa Mafunzo hayo Meja Jenerali A.B Mhone naye akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo 

  Naibu Waziri wa Ulinzi wa Malawi Mhe. Evaton Chimulirenji (kushoto) akiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Malawi Generali Supini Phiri (kulia) pamoja na Mkuu wa Misheni ya mafunzo hayo, Mhe. Bi. Eunice Lumbia 

  Sehemu ya viongozi wa kijeshi wakifuatilia hotuba zilizokuwa zinatolewa wakati wa ufunguzi huo 

  Kikosi cha Tanzania kinachoshiriki mafunzo hayo kikiwa kimetulia wakati wa gwaride rasmi la ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo. Kikosi hicho kinajumuisha wanajeshi, askari magereza na raia kutoka fani mbalimbali za utawala, siasa na mawasiliano 

  Kikosi cha Malawi ambao ni wenyeji wa mafunzo hayo kikiwa kimetulia wakati wa gwaride la ufunguzi rasmi wa mafunzo 

  Kikosi cha Tanzania kikiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo 

  Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Zakarriya Kera (kushoto) ambaye pia ni kiongozi wa washiriki kutoka kundi la Raia kwenye mafunzo hayo akiwa katika picha na baadhi ya washiriki ambao ni wanajeshi na raia kutoka Tanzania. 

  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe, akifungua kongamano la siku moja la ajira binafsi mjini Morogoro juzi, lililoandaliwa na Taasisi ya WICOF inayojishughulisha na masuala ya kijamii hususani, walemavu na watoto mkoani humo .
  Washiriki wa kongamano hilo.

  Kongamano likiendelea.  Mtoa mada Mogani Isdori akitoa mada kuhusu ulipaji kodi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo akitoa mada kuhusu matumizi ya mitandao.
  Mwanachuo cha Jordan cha mjini Morogoro, Aviva Chrispin akiuliza swali.
  Mjasiriamali, Neema Heri akitoa ushuhuda wa mafanikio yake.
  Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo SUA, Dk.Suleiman Rashid akitoa mada kuhusu umuhimu wa vifungashi kwenye Tangaza na kuongeza thamani ya bidhaa.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza katika kongamano hilo akizungumzia umuhimu wa vifungashio na kuongeza thamani ya bidhaa.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wa kongamano hilo, DC Mchembe pamoja na watoa mada.
  Mjasiriamali, Sara Ngonyani akitoa mada.
  Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Mwajabu Dhahabu, akihutubia.
  Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe, akimkabidhi zawadi ya saa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WICOF, Mwajabu Dhahabu akimkabidhi zawadi ya picha baba yake Mzee Dhahabu.

  Picha ya pamoja.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo, akiwa katika picha ya pamoja na vijana walioshiriki katika kongamano hilo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo, akiwa na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Gairo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo, akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WICOF.


  Na Dotto Mwaibale, Morogoro


  WANAWAKE nchini wametakiwa kuthubutu, kuwa wavumilivu na wabunifu ili waweze kuinuka kiuchumi.

  Mwito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe mjini Morogoro juzi wakati akifungua kongamano la siku moja la ajira binafsi lililoandaliwa na Taasisi ya WICOF inayojishughulisha na masuala ya kijamii hususani, walemavu, watoto na wazee mkoani Morogoro.

  "Ili mjikomboe kiuchumi mnatakiwa kuthubutu, kuwa wavumilivu nawabunifuna uiunga katika vikundi vya ujasiriamali muweze kupata mikopo nakufanyashughuli mbalimbali za biashara" alisema Mchembe.Alisema dhana ya 50 kwa 50 kati ya wanaume na wanawake si kuosha vyombo bali ni mwanamke kuweza kufanya kazi za uzalishaji mali kama wanavyofanya wanaume na kumiliki ardhi.

  Akizungumza wakati akitoa mada katika kongamano hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo aliwataka wanawake hao kutumia mitandao ya kijamii kwa maufaa badala ya kuitumia kwa masuala yasiyo na tija.
  "Jamani wanawake wenzangu tutumie simu zetu kwa ajili ya maendeleo, kama kupeana taarifa, kutafuta masoko ya bidhaa zetu na si vinginevyo" alisema Mgongo.

  Akitoa zawadi ya pekee katika kongamano hilo alisema kwa kutambua umuhimu wa mtoto wa kike Shule ya John The Baptist Girls High School imetangaza fursa ya kusomesha bure wanafunzi watatu wa kidato cha kwanza na watatu wengine hadi cha nne kwa mwaka 2019.

  Alisema anachotakiwa kufanya mwanafunzi ni kufika shuleni hapo siku yoyote ndani ya mwezi wa oktoba 2018 kwa ajili ya kufanya mtihani wa kuchuana na kuwa fursa hiyo imetolewa na Mfuko wa Ndibalema John Mayanja Memorial Scholarship.

  Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Mwajabu Dhahabu alisema kuwa kongamano hilo lenye lengo la kuwajengea uwezo ajira binafsi watoto wa kike ni la kwanza tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo mwaka jana.Alisema kufanyika kwa kongamano hilo ni maandalizi ya kuelekea katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani yatakayofanyika hivi karibuni.s

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka akizungumza katika kongamano hilo alisema serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli imeweka mazingira mazuri ya kuwasaidia wajasiriamali na kuwa imetenga fedha kwa ajili ya kuwakopesha hivyo akato mwito kwa wajasiriamali hao kuongeza thamani ya bidhaa zao kwa kuziweka katika vifungashio vilivyobora.

  Katika hatua nyingine Mtaka aliipongeza kampuni ya Trumark kwa kazi kubwa inayoifanya ya kuwasaidia vijana kuzitambua fursa za maendeleo na akatoa mualiko kwa wajasiriamali hao kwenda Simiyu kwenye maonyesho ya viwanda vidogo vidogo (SIDO) yatakayofanyika kuanzia Oktoba 23 hadi 28.

  Kongamano hilo lilihitimishwa kwa makundi mbalimbali pamoja na watoa mada kupata zawadi na vyeti vya ushiriki.

older | 1 | .... | 1691 | 1692 | (Page 1693) | 1694 | 1695 | .... | 1898 | newer