Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

WATOA HUDUMA ZA AFYA WATAKIWA KUTOWASAHAU WATOTO KATIKA KUWAKINGA NA MAAMBUKIZI YA VVU

$
0
0

Naibu waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikata utepe kuashiria uzinduzi wa muongozo wa Mkakati wa wauguzi na wakunga kusogeza huduma za VVU na UKIMWI karibu na jamii uliofanyika Kitaifa Mkoani Njombe .
Naibu waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wananchi waliojitokeza kupima VVU katika viwanja vya Turbo mkoani Njombe mapema leo wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa wauguzi na wakunga kusogeza huduma za VVU na UKIMWI karibu na jamii uliofanyika Kitaifa Mkoani Njombe .



Naibu waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisikiliza maelezo kutoka kwa mtoa huduma wakati alipotembelea mabanda ya kupima VVU na kutoa ushauri nasaha katika viwanja Turbo mkoani Njombe wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa wauguzi na wakunga kusogeza huduma za VVU na UKIMWI karibu na jamii uliofanyika Kitaifa Mkoani Njombe.


Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka kitabu cha muongozo wa utoaji huduma kwa wauguzi na wakunga nchini wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa wauguzi na wakunga kusogeza huduma za VVU na UKIMWI karibu na jamii uliofanyika Kitaifa Mkoani Njombe

……………………..

Na WAJMW-NJOMBE

Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na watoto imewataka watoa huduma za afya nchini kutokuwasahau watoto na vijana katika kuwakinga na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa wauguzi na wakunga kusogeza huduma za VVU na UKIMWI karibu na jamii ikiwemo ushauri nasaha, kupima VVU na kufuatilia maendeleo ya afya za walengwa uliofanyika mapema leo mkoani Njombe.

“Bado tuna changamoto kwa watoa huduma wetu wa afya kwa baadhi ya maeneo ikiwemo kutokuwapima watoto hali ya maambukizi, kutoa dawa kwa watoto na kuwapa elimu vijana hivyo natoa rai kwa wahudumu wa afya tuweze kuweka mkakati wa kufikia makundi hayo” alisema Dkt. Ndugulile.

Aidha Dkt. Ndugulile amewasisitiza Wauguzi na Wakunga kutoa huduma kwa kuzingatia miiko na maadili hususan katika kutoa huduma za VVU kwa jamii inayowazunguka ikiwemo kutumia lugha nzuri na kuwa wanyenyekevu kwa wananchi.Sambamba na hilo Dkt. Ndugulile amewaasa wanaume nchini kuacha uoga na kujitokeza kupima VVU ili kutambua afya zao na kuanza matibabu mara moja iwapo watakutwa na maambukizi.

“Tutawafuata wanaume popote walipo hususan waliopo kwenye mikusanyiko yao ikiwemo kwenye sehemu za starehe, viwanja vya mipira , Migodini na sehemu za uvuvi ili kutoa elimu na kuwashauri wapime ili kujua afya zao” alisema Dkt. Ndugulile.Aidha Dkt. Ndugulile amesema kusudio la kufanya hivyo ni kuhakikisha kufikia malengo ya 90 90 90 ya kutokuwa na maambukizi mapya ifikapo mwaka 2030. Ambapo asilimia 90 ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi wawe wanajua hali zao za maambukizi.

Ili kutimiza malengo ya serikali katika kupambana na maambukizi, Dkt Ndugulile amesema Serikali imekuja na utaratibu wa dawa kinga ambapo dawa hizo zitatumika kwa makundi maalumu ambayo yako hatarini kupata maambukizi. “Lakini vile vile tumekuja na utaratibu unaoitwa dawa-kinga ambazo kuna makundi ambayo tumebaini, ambayo yako kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi ya UKIMWI.

Makundi haya kuna dawa ambayo tunataka tuwape zisaidiane na kinga nyingine ili kusaidia watu wasipate maambukizi ya virusi vya UKIMWI lakini hatusemi kwamba tumeshapata kinga”. Dkt Ndugulile.Sambamba na hayo Dkt. Ndugulile amewataka watoa huduma waende wakatoe msisitizo na kuelimisha jamii katika maeneo ambayo dawa-kinga zimeanza kufanyiwa majaribio ili kuleta matokeo chanya.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka amesema ukanda wa nyanda za juu kusini ni ukanda ambao una maambukizi makubwa ya VVU na serikali ya mkoa ilianza kampeni ya tohara kwa wanaume, na sasa inaelekea kwa watoto wa sekondari na shule ya msingi ikiwa ni njia mojawapo ya kupambana na maambukizi mapya.

“Takwimu zinaonesha sisi tuna kiwango kikubwa cha maambukizi kuliko katika ukanda ule ambao tohara kwa wanaume inaanzia katika umri mdogo kiwango cha maambukizi kiko chini lakini pia kuna mahusiano kati aya tohara ya wanaume na maambukizi ya VVU kwahiyo kama mkoa kampeni hii tumeivalia njuga chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na TAMISEMI”. Alisema Ole Sendeka.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Waganga Wakuu wa mikoa na Wafawidhi wa mikoa mbalimbali pamoja na wauguzi na wakunga waliopata muongozo wa kusogeza huduma za VVU na UKIMWI karibu na jamii ikiwemo ushauri nasaha, kupima VVU na kufuatilia maendeleo ya afya za walengwa.

CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA CHAMPONGEZA RAIS MAGUFULI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Skauti Mkuu wa Tanzania Ndg. Mwantumu bakari Mahiza Ikulu jijini Dar es salaam Oktoba 3, 2018.

Chama cha Skauti Tanzania tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Mheshimiwa John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuthamini na kuafiki kuwa Mlezi wa Chama na kumuapisha Skauti Mkuu wetu Bi. Mwantumu B. Mahiza.

Shukrani zetu kwa Mheshimiwa Rais kwa kuthamini mchango unaotolewa na wanachama pamoja na Viongozi wa Chama cha Skauti Tanzania.

Shukrani zetu zingine ni kwa Mdhamini wa Chama cha Skauti Tanzania, Mheshimiwa DK. Ali Hassan Mwinyi, Rais mstaafu wa awamu ya pili kwa mchango wake mkubwa kwa Chama cha Skauti, yeyé pamoja na Wadhamini wenzake DK. Salim Ahmed Salim, Waziri Mkuu mstaafu, na Askofu Nestori Timanywa (Marehemu) wamefanya kazi kubwa sana kuifikisha Skauti hapa tulipo.

Daima tutaendelea kuwaenzi Viongozi wetu kwa kulinda Heshima zao kwa kuwajibika na kufuata maelekezo yote watakayoyatoa kwa maslahi ya Chama na Taifa kwa ujumla.

Aidha tumehamasika sana na kufarijika na kauli ya Mlezi wetu kuwa anatambua shughuli za Skauti katika Taifa letu na kuthibitisha kuwa anafahamu changamoto zinazokabili Chama na kuahidi kuzishughulikia kwa uwezo wake wote na kwamba yupo pamoja nasi bega kwa bega.

Tunapenda kuwashukuru Viongozi wetu wote wa Kitaifa, kuanzia Mlezi, Wadhamini, Rais wa Chama cha Skauti, pamoja na Makamu Rais wa Chama. Skauti Mkuu, Wajumbe wa Bodi, Makamishna Wakuu Wasaidizi Makao Makuu, pamoja na Makamishna wote wa Skauti wa Mikoa na Wilaya zote Tanzania kwa kuratibu na kusimamia program za vijana skauti siku hadi siku.

Tunashukuru sana umma wa Watanzania hasa wazazi na walezi wa vijana skauti kwa kushirikiana nasi na kutuamini kuwalea watoto wao na vijana kwa kuwafundisha kuwa Wazalendo, Wakakamavu na wenye maadili mema ili kupata TAifa bora lenye Viongozi Wazalendo wenye kuipenda Nchi yao.


MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU KIBARIKI CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA.


ELINE KITALY

KAMISHNA MTENDAJI.

mbelea Chuoni hapo.

WAZIRI UMMY AUAGIZA UONGOZI WA HOSPITALI YA ST FRANCIS KUSHUSHA BEI ZA MATIBABU MARA MOJA

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy amwalimu akikagua vifaa vya mmoja kati ya wagonjwa waliopata Rufaa ya kwenda kutibiwa katika Hospitali ya St. Francis pindi alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika kituo cha Afya cha Kibaoni.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimjulia hali mtoto aliefika na mama yake kupata huduma katika kituo cha Kibaoni.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya viongozi wa Mkoa wa Morogoro walioongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ifakara James Lihunyo (hayupo kwenye picha)
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikagua cheti cha mgonjwa katika kituo cha Afya cha Kibaoni wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma kisha kuelekea Hospitali ya Rufaa ya St. Francis.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimjulia hali mtoto aliefika na mama yake kupata huduma katika kituo cha Kibaoni.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jisnsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akieleza umuhimu wa Bima ya Afya kwa watoto kwa mmoja kati ya wamama waliofika kupata huduma za Afya katika kituo cha Afya cha Kibaoni.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maelekezo kwa Baba Askofu wa jimbo la Ifakara Salutaris Libenaambae baada ya kikao cha kuboresha hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali hiyo.

Upande wa mbele wa Hospitali ya Rufaa ya St. Francis.



Na WAMJW – IFAKARA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameuagiza uongozi wa Hospitali ya Dini ya St.Francis kupunguza gharama za matibabu kwa wananchi ndani ya mwezi mmoja kabla hajarudi kufanya ukaguzi wa mara ya pili.

Ameyasema hayo wakati akiwa katika ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika Hospitali ya St Francis iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Ifakara Mkoa wa Morogoro kufuatia taarifa isiyoridhisha juu ya gharama za matibabu iyoripotiwa siku ya Octoba 3 na Televisheni ya Taifa (TBC).

Waziri Ummy alisema kwamba, Serikali inatoa Jumla ya Watumishi 243 sawa na Asilimia 68% katika Hospitali hiyo, lengo ni kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini kupata huduma za bora za afya na zenye unafuu ikiwa ni moja kati ya ahadi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati anaingia madarakani.

“Kati ya Watumishi 352, watumishi 219 wanalipwa mshahara na Serikali Kuu, ambapo kila mwezi tunalipa shilingi milioni 153.7, bila kuhesabu gharama za watumishi 12 walioshikizwa kutoka Wizara ya Afya, Watumishi 12 kutoka Halmashauri ya Kilombero, Katibu tawala Morogoro ameleta watumishi 2, jumla watumishi 243, ambao ni sawa na Asilimia 68% wanalipwa mshahara kutoka Serikali kwa Asilimia 100%”. Alisema Mhe. Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa mwaka wa bajeti 2015/2016 Serikali ilipeleka dawa zenye thamani ya shilingi Millioni 119.5, bajeti ya mwaka 2016/2017 shilingi milioni 177.9 huku kwa mwaka 2017/2018 dawa zenye thamani ya shilingi milioni 118.7 zilinunuliwa hospitalini hapo.

Kwa upande mwingine Waziri Ummy alisema kuwa mwongozo wa Wizara ya Afya, unazitaka Hospitali zote kuhakikisha kuwa wanawake wajawazito, wazee wasio na uwezo na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano kupata huduma za matibabu bila malipo. bali na hayo Waziri Ummy alitoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Morogoro kujiunga na mifuko ya Bima ya Afya bila kuwasahau watoto walio chini ya umri wa miaka 18 ambao hupata bima ya afya kwa shilingi 50,400/=

“Wakati umefika wa Watanzania kujenga utamaduni wa kuwa na uhakika wa matibabu kabla ya kuugua, na uhakika huo ni wa kupitia Bima ya Afya”, alihimiza Waziri Ummy kwa msisitizo. aziri Ummy, aliendelea kusema kuwa, Serikali inaelekea kutunga sheria ambayo itamlazimu kila Mtanzania kupata Bima ya Afya, ili aweze kupata huduma za matibabu ya Afya bila kikwazo chochote cha fedha.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mhe. Peter Ambrose Lijualikali amemuomba Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu kuikumbuka Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero kwa kujenga Hospitali ya Wilaya, jambo litaloimarisha hali ya utoaji huduma za Afya kwa wananchi. Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya St. Fransis, Baba Askofu Salutaris Libena ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kufika hospitali hapo na kuahidi kutekeleza maelekezo yote ambayo yametolewa na Serikali.

” Tunaahidi kwamba tumeelewa na tutatekeleza maelekezo yote, katika lengo la kuboresha huduma za Afya kwa wananchi “, alisema Baba Askofu Libena.

BENKI YA STANBIC YATOA ZAWADI NA UJUMBE WA SHUKRANI KWA WATEJA

$
0
0

Mteja wa Benki ya Stanbic, Ruth Bura akifurahia kupokea chupa ya kinywaji chake pendwa cha ‘champagne’ kama zawadi kutoka kwa mhudumu wake wa Benki ya Stanbic, Edward Nyerere wakati wa sherehe za wiki ya huduma kwa wateja katika tawi la Centre.
Ruth Bura mteja wa Benki ya Stanbic akifungua chupa ya ‘champagne’ na wafanyakazi wa benki hiyo, Edward Nyerere (kushoto), Jacquiline Michael (wa pili kushoto) na Elikaneny Uloto (kulia) wakati wa sherehe za wiki ya huduma kwa wateja katika Tawi la Centre.
Mteja wa Benki ya Stanbic, Aisha Sykes akimshukuru Bw. Fredrick Mushi, mhudumu wake wa benki, baada ya kumpatia ujumbe wa kumshukuru kwa kuwa mteja wa benki ya Stanbic. Benki ya Stanbic imesherehekea wiki hii ya huduma kwa wateja kwa kuwapa zawadi wateja wao na kuwashukuru kwa kuendelea kuwa wateja wa benki hiyo.
Mshauri wa wateja wa Benki ya Stanbic akimpa mteja wake ujumbe wa shukurani kwa kufanya miamala yake ya kibenki na Stanbic wakati wa sherehe za wiki ya huduma kwa wateja katika Tawi la Centre.
Meneja wa Benki ya Stanbic Tawi la Centre, Bw. Adelhem Msiagi akimpa mteja wao ujumbe wa shukurani kwa kuchagua kufanya miamala yake ya kibenki na benki ya Stanbic wakati wa sherehe za wiki ya huduma kwa wateja katika tawi la Centre.

IGP AKUTANA NA BALOZI WA UTURUKI NCHINI

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Balozi wa Uturiki nchini Mhe. Ali Davutoglu wakati balozi huyo alipomtembelea ofisini kwake Makao Mkauu ya Polisi Dar es Salaam ambapo walijadiliana mambo mbalimbali ya kuimarisha uhusiano. ( Picha na Jeshi la Polisi)
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiongea na Balozi wa Uturiki nchini Mhe. Ali Davutoglu wakati balozi huyo alipomtembelea ofisini kwake Makao Mkauu ya Polisi Dar es Salaam ambapo walijadiliana mambo mbalimbali ya kuimarisha uhusiano. 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiongea na Balozi wa Uturiki nchini Mhe. Ali Davutoglu wakati balozi huyo alipomtembelea ofisini kwake Makao Mkauu ya Polisi Dar es Salaam ambapo walijadiliana mambo mbalimbali ya kuimarisha uhusiano. ( Picha na Jeshi la Polisi)

MAKATIBU KAMATI WAANDAA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ZIARA ZA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO.

$
0
0

Katibu kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Ndg. Pamela Pallangyo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ziara za ukaguzi wa miradi ya Maendeleo mbele ya Makatibu Kamati katika kikao kilichofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma.
V25A9349
Mkurugenzi wa Kamati za kudumu za Bunge, Ndg. Athuman Hussein (katikati) akizungumza na Makatibu Kamati (hawapo kwenye picha) wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa ziara za ukaguzi wa miradi ya Maendeleo yaliyozingatia mwongozo wa ziara za kamati, katika kikao kilichofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Ndg. Grace Bidya na kulia ni Katibu kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Ndg. Pamela Pallangyo
V25A9317
Katibu kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Ndg. Grace Bidya akiteta jambo wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa ziara za ukaguzi wa miradi ya Maendeleo yaliyozingatia mwongozo wa ziara za kamati mbele ya Makatibu Kamati (hawapo kwenye picha) katika kikao kilichofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma.
V25A9344
Mkurugenzi Msaidizi Kamati za Huduma na Maendeleo ya Jamii, Ndg. Dickson Bisile akizungumza na Makatibu Kamati wakati wa kikao cha uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa ziara za ukaguzi wa miradi ya Maendeleo yaliyozingatia mwongozo wa ziara za kamati kilichofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Ndg. Hosiana John
V25A9194
Makatibu Kamati, kamati za kudumu za Bunge wakimsikiliza Katibu kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Ndg. Pamela Pallangyo (aliesimama) akiwasilishaji taarifa ya utekelezaji wa ziara za ukaguzi wa miradi ya Maendeleo yaliyozingatia mwongozo wa ziara za kamati katika kikao kilichofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma.
V25A9235
Makatibu Kamati wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa ziara za ukaguzi wa miradi ya Maendeleo yaliyozingatia mwongozo wa ziara za kamati katika kikao kilichofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma. Kuanzia kushoto ni Katibu kamati ya kudumu ya Bunge ya Maliasili na Utalii, Ndg. Gerald Magiri, Mkurugenzi Msaidizi Kamati za Masuala ya Jumla, Ndg. Angelina Sanga na Katibu Kamati ya Katiba na Sheria, Ndg, Stanslaus Kagisa

TRA YAKAMATA WATU WAWILI KWA KOSA LA KUGUSHI RISITI ZA EFD

$
0
0


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewakamata watu wawili mwanamke na mwanaume kwa kosa la kugushi Risiti za Kielektroniki za EFD katika maeneo ya Sinza Mori jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa mamlaka hiyo Richard Kayombo, amesema kuwa, watuhumiwa hao ni Doreen Urassa (40) mkazi wa Kunduchi na Raymond Alexander (31) mkazi wa Kinondoni Mkwajuni jijini hapa.

"Tarehe 4 Oktoba, 2018 majira ya saa 1 jioni, tulifanikiwa kuwakamata watu wawili maeneo ya Sinza Mori wakiwa wanagushi risiti za EFD. Watuhumiwa hawa tutawafikisha mahakamani kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria", alisema Kayombo. 

Kayombo ametoa wito kwa watu wote wanaojishughulisha na makosa hayo kuacha mara moja kwa kuwa TRA itaendelea kufanya msako mkali na mtu yeyote akibainika anagushi risiti, atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.Aidha, Mkurugenzi Kayombo amewaomba wasamalia wema waendelee kutoa taarifa za kuwafichua wanaogushi risiti na kuwahakikishia kuwa, majina yao hayatatajwa popote.

“Mamlaka haitamvumilia mtu yeyote anayejaribu kukwamisha ukusanyaji mapato ya serikali iwe kwa kugushi risiti au biashara ya magendo au njia nyingine yoyote ya udanganyifu. Hivyo, tunawaomba wasamalia wema waendelee kutupa ushirikiano kwa kuwafichia watu wadanganyifu na tunawahakikishia kutunza siri kwa kutoyataja majina yao popote pale”, alifafanua Kayombo.

Mamlaka ya Mapato Tanzania inaendelea na zoezi la kuwasaka watu wote wanaojishughulisha na vitendo vya kugushi risiti ikiwa ni pamoja na kukamata biashara za magendo ambapo wanaobainika hufikishwa mahakamakani kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

Rais Magufuli amteua Bw. Habbi Gunze kuwa Mwenyekiti wa BASATA


DIAMOND AWEKA HISTORIA TANDALE... AREJESHA SHUKRANI KWA WANANCHI

$
0
0

*RC Makonda aongeza muda wa kupiga muziki
*Asema mwisho iwe saa nane usiku,atoa maagizo

Na Khadija Seif ,Globu ya jamii

NI upendo wa aina yake ambao msanii Nassem Abdull 'Diamond'ameamua kuufanya kwa wananchi wa Kata ya Tandale jijini Dar es Salaam.
Unajua kwanini?Iko hivi msanii huyo leo ameamua kusheherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kujumuika na wananchi hao na kubwa zaidi ametumia nafasi hiyo kurejesha ahsante kwa wananchi hao.

Katika sherehe hizo Diamond ameamua kufanya mambo yenye kugusa jamii kutokana na aina ya misaada ambayoa ameitoa kwa wananchi hao ambapo ameamua kugawa bodaboda kwa vijana wa Tandale na kugawa kadi za bima 1000 kwa wananchi wa Tandale.

Pia msanii huyo ameamua kutoa msaada wa bajaji kwa mama mwenye ulemavu baada ya kuona anahitaji msaada kwa kumpatia chombo hicho ambacho kitamsaidia mama huyo.Wakati wa sherehe hiyo ikiendelea Diamond hakusita kueleza changamoto ambazo amezipitia katika maisha yake hadi kufika hapo alikofikia.

Pamoja na yote Diamond ametoa ombi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuondoa zuio la kufanya muziki mwisho saa sita usiku."Tunaomba Mkuu wa Mkoa hili zuio la mwisho saa sita usiku uliondoe kwani limetubana sana.

"Watu wa Dar ikifika saa sita ndio wanataka kutoka kwenda kwenye kumbi za sterehe, lakini kwa katazo lililopo inakuwa ngumu.Hivyo tunaomba ulitazame hili ili tuendelee kudamshi,"amesema Diamond.Pia ameomba kwa Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam kuwapatia eneo WCB ili wajenge studio kwa ajili ya wasanii wa muziki wa Tandale.

Kwa upande wa watu waliokuwa eneo hilo wengi wao wameonesha kufurahishwa na kitendo cha Diamond na kumpongeza kwa uamuzi wake wa kusaidia jamii.Hata hivyo Makonda akizungumza kwenye tukio hilo ametoa maagizo ya kuhakikisha linapatikana eneo kwa ajili ya ujenzi wa kiwanja cha mpira pamoja na kiwanja ambacho kitajengwa shule ya msingi kwa ajili ya wananchi wa Tandale.

Kuhusu kuongezwa muda kwa ajili ya burudani Makonda amesema suala hilo lipo kisheria na la muda mrefu kidogo na kufafanua zaidi kuwa kuna sheria ya mazingira, ambapo kelele nazo ni sehemu ya uchafuzi wa mazingira.Hata hivyo baada ya maelezo mengi ametangaza kuanzia leo ameongeza muda wa kupiga muziki ambapo sasa watapiga hadi saa nane usiku badala ya saa sita usiku kwa kila wikend.

Hivyo ametoa maagizo kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kutowakamata watu wanaopiga muziki hadi saa nane usiku na kwamba Jiji la Dar ndio jiji la starehe na ushauri wake ni vema watu wakajenga kumbi za ndani.

Wasanii mbalimbali nao wamepata nafasi ya kuzungumza na kutoa maoni yao na kubwa zaidi ni namna ambavyo Diamond amethibitisha wananchi wa Tandale ni sehemu ya maisha yake.
 Msanii wa Bongo Fleva Naseeb Abdull a.k.a Diamond Platnumz akizungumza na mashabiki wake wakati wa sherehe za kumbukizi ya kuzaliwa kwake ambapo tukio linakwenda sambambamba na msanii huyo kurejesha shukrani kwa wananchi wa Kata ya Tandale.
 Mkuu ya Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambaye pia ni Mlezi wa kundi la Wasanii WCB ,akizungumza wakati wa sherehe za kumbukizi ya kuzaliwa kwa Msanii Naseeb Abdul ' Diamond'  ambapo tukio linakwenda sambambamba na msanii huyo kurejesha shukrani kwa wananchi wa Kata ya Tandale.
Msanii Nyota wa Bongofleva Nasseb Abdul a.k.a Diamond akimsikiliza mmoja wa akina Mama ambaye ni mlemavu,alipokuwa akimshukuru huku akitoa machozi na kutoamini kwa kile kilichotokea,kwa kupewa zawadi ya Bajaji ili aweze  kujikimu kimaisha na kuisaidia familia yake,Mama huyo mkazi wa Tandale amemshukuru Diamond kwa kumpa zawadi hiyo kwani hakutegemea na kwamba agalau sasa ataweza kuwa na ahuweni ya maisha.
Mama mlemavu wa miguu ambae ni dereva wa Bajaji akiwa ndani ya Bajaji aliyopewa zawadi na Msanii Diamond mbele ya umati wa wakazi wa Tandale ukishuhudia sambamba na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh Paul Makonda.
Daimond akimkabidhi nyaraka za gali aliyomnunulia mpiga picha wake aliyemtaja kwa jina moja la Lukamba,kama zawadi kwa jitihada na kujituma katika kazi ambazo amekuwa akizifanya kila siku 
Aliyewahi kuwa Miss Tanzania Jacqueline Mengi akiwasalimia wananchi wa Tandale  wakati wa sherehe za kumbukizi ya kuzaliwa kwa Msanii Naseeb Abdul ' Diamond'  ambapo tukio linakwenda sambambamba na msanii huyo kurejesha shukrani kwa wananchi wa Kata ya Tandale.
Msemaji wa Simba Haji Manara akizungumza jambo kwenye hafla hiyo iliyofanyika Tandale 
Msanii wa Hip Hop nchini Rashid Makwiro 'Chid Benz' akitoa burudani kwenye hafla hiyo 
Baadhi ya wananchi wa Tandale wakiwa katika sherehe za kumbukizi ya kuzaliwa kwa Msanii Naseeb Abdul ' Diamond'  ambapo tukio linakwenda sambambamba na msanii huyo kurejesha shukrani kwa wananchi wa Kata ya Tandale.















NHIF KAGERA WAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUTOA MSAADA WA MASHUKA YA WAGONJWA HOSPITAL YA RUFAA YA MKOA WA KAGERA

$
0
0
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera

KATIKA kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja mwaka 2018 uongozi wa bima ya afya Mkoa wa Kagera(NHIF) wameahadhimisha wiki hii kwa kwa kutoa msaada wa mashuka 60 yenye thamani ya shilingi 720,000 kwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Bukoba.

Meneja wa mfuko wa bima ya afya (NHIF)Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo amesema wiki hii wameitumia kuwa karibu na wanachama wao kwa kutembelea vituo vya tiba na kupata maoni kutoka kwa wanachama wao.

"Tumetumia wiki hii kutembelea vituo mbalimbali vya kutolea huduma na kushuhudia upatikanaji wa huduma kwa wanachama wetu na kupata maoni yao, katika kuwa karibu na wanachama wetu kwa wiki hii mrejesho tumeupata toka kwa wanachama wetu unaonyesha wanachama wetu wamekuwa wakipata huduma nzuri na bora"alisema Odhiambo

Odhiambo aliishukuru serekali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli kwa kusimamia nidhamu kwa watumishi pamoja na kuondoa tatizo la uhaba wa dawa na vitendanishi kwani hivi sasa vituo vingi vina dawa za kutosha.

Meneja huyo pia amehaidi kuyafanyia kazi maoninyote yaliyotolewa na wanachama wa mfuko huo kwa kushirikiana na watoa huduma.Maofisa wa hao wa mfuko wametembelea vituo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa pamoja na Bukoba town Health.mwingine,Odhiambo amehadi kuyafanyia kazi kwa haraka maoni yaliyotolewa na wanachama kwa kushirikiana na watoa huduma.

Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kagera Dkt John Mwombeki ameshukuru mfuko wa bima ya afya (NHIF) kwa msaada kwakuwa utasaidia kuboresha huduma kwa wagonjwa wanaolazwa hapo.Alisema hospitali inafanya jitihada mbali mbali za kutatua changamoto ya muda wa upatikani wa huduma ikiwa ni pamoja na kuajiri madaktari wa muda.
Meneja wa mfuko wa bima ya afya Mkoa wa Kagera akiongea na wagonjwa waliolazwa katika hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera katika wiki ya maadhimisho ya huduma kwa wateja 
Meneja wa NHIF Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo akiongea na wanachama wa mfuko huo waliofika hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kwaajili ya kupata matibabu.
Uongozi wa mfuko wa bima ya afya(NHIF)Kagera wakikabidhi mashuka 60 kwa uongozi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya huduma kwa wateja.

MHE.NAPE AMNADI BW.MOHAMED MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA LIWALE KWA TIKETI YA CCM

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Mh. Nape Nnauye akimnadi Bw. Zuber Mohamed Mgombea ubunge jimbo la Liwale mkoani Lindi kwa tiketi ya CCM katika moja ya mikutano ya kampeni uliofanyika leo jimboni humo, Bw. Zuber Mohamed alijivua uanachama wa CUF na kujiunga na CCM na ameteuliwa na Chama hicho kugombea tena ubunge jimbo la Liwale

1
Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Mh. Nape Nnauye akizungumza na wananchi wa jimbo la  Liwale wakati wa  kampeni ya kumnadi, Bw. Zuber Mohamed alijivua uanachama wa CUF na kujiunga na CCM na ameteuliwa na Chama hicho kugombea tena ubunge jimbo hilo
2
Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Mh. Nape Nnauye  akimnadi mgombea ubunge kupitia CCM Bw.Zuber Mohamed  wananchi wa jimbo la  Liwale
3
Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Mh. Nape Nnauye akiwa na baadhi ya viongozi na wabunge wa CCM wakicheza wimbo wakati wa Kampeni ya kumnadi mgombea ubunge kupitia CCM Bw.Zuber Mohamed kwa  wananchi wa jimbo la  Liwale 
4
Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Mh. Nape Nnauye akiwasikiliza kwa umakini wananchi wa jimbo la Liwale wakati wa Kampeni ya kumnadi mgombea Ubunge kupitia CCM Bw.Zuber Mohamed 
………………………

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KOZI MBALIMBALI KATIKA CHUO CHA USTAWI WA JAMII

BENKI YA AZANIA YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA.

$
0
0
Benki ya Azania yenye matawi yake sehemu mbali mbali nchini imeadhimisha wiki ya huduma kwa mteja, lengo kuu likiwa ni kuwashukuru wateja wake kwa kuwa nao bega kwa bega katika ukuaji wa benki hiyo.



Katika maadhimisho hayo benki ya Azania imewatembelea wateja kwenye sehemu zao za kazi lengo likiwa ni kuona namna gani wanaweza kuboresha huduma zao, mbali na hilo waliweza kutoa zawadi na vyeti kwa wateja wao lengo likiwa ni kuwashukuru kwa kuichagua benki hiyo.


Baadhi ya wateja waliopatiwa Vyeti na Zawadi kwenye maadhimisho ya Wiki ya huduma kwa mteja.Benki ya Azania imeelekeza nguvu zake katika kuhakikisha kila mteja anapata huduma bora kulingana na mahitaji yake.

Baadhi ya wateja wakipata maelezo kutoka kwa watoa huduma. bali na kutoa huduma hizo Watoa huduma kwenye matawi mbali mbali ya benki hiyo waliweza kuvaa mavazi ya kitenge kuonyesha Utanzania wao.



Katika kuonyesha ushirikiano na wateja Watoa huduma wa benki ya Azania waliweza kulishana keki na wateja.


Benki ya Azania inaendelea kuwahimiza wananchi wote kujiunga na benki yao ili waweze kupata huduma bora na zenye ufanisi wa hali ya Juu.
Azania Bank bega kwa bega!

WAKAZI WA SUMBAWANGA WAKUNWA NA TAMASHALA TIGO FIESTA VIBE KAMA LOTE

$
0
0

 Msanii Barnaba akionesha umahiri wake kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote yake lililofanyika jana kwenye uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga.
 Burudani mbalimali zilitolewa kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote yake lililofanyika jana kwenye uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga.
 Msanii wa Hip Hop atambulika kwa jina la kisanii Fid Q akiwaimbisha wakazi wa Sumbawanga kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote yake lililofanyika jana kwenye uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga.
  Msanii wa Hip Hop kutoka kundi la Weusi Joe Makini  akiwaimbisha wakazi wa Sumbawanga kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote yake lililofanyika jana kwenye uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga.


 MMoja wa wasanii wa kike,ambaye amekuwa akifanya vyema kwenye anga ya muziki wa bongofleva atambulikae kwa jina la Nandy akionesha umahiri wake wa kuimba na kucheza mbele ya wakazi wa Sumbawanga kwenye  Msanii wa Hip Hop atambulika kwa jina la kisanii Fid Q akiwaimbisha wakazi wa Sumbawanga kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote yake lililofanyika jana kwenye uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga.





Wakazi wa manispaa ya Sumbawanga na vitongoji vyake usiku wa kuamkia leo walipata burudani ya aina yake ya msimu wa tamasha kubwa nchini la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote.

Hili ni tamasha la pili kwa mkoa huo baada ya ufunguzi uliofanyika mkoa wa Morogoro.

Msimu huu si kwa burudani tu, bali huwa na fursa mbalimbali kwa wafanyabiasha na waendesha bodaboda.
 
Kwenye steji ndio kunaacha gumzo kwa wakazi wa miji mbalimbali ambapo tamasha linafanyika.
Akifungua pazia la tamasha hili msanii Nedy Music alianza kuwapasha joto mashabiki akifuatiwa na msanii WhoZu ambaye aliwapagawisha kwa kibao chake kiitwacho "uendi mbiguni".

Msanii mkongwe Farid Kubanda Fid Q nae alichota hisia za mashabiki kwa kushusha nyimbo zake tofauti tofauti ukiwemo Fresh.Ben Pol ambaye miaka yote huwa mbunifu kwenye jukwaa, alipanda na wenyeji 6 wa mji huo kwa kuonyesha namna ya wakaazi wa Sumbawanga wanaishi katika mazingira tofauti kulingana na anachofanya kwa siku.

Kwa upande wa mdhamini mkuu wa Tigo Fiesta 2018, Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za Juu Kusini, Henry Kinabo alisema msimu kampuni ya Tigo imekuja ofa kabambe kwa wateja wao. 
 
" Huu ni msimu wa aina yake kama utannunua tiketi kwa Tigo Pesa Master Pass QR utaweza kupata tiketi kwa shilingi elfu tano ambapo ukinunua kawaida unapata kwa elfu saba, kadhalika wateja wa Tigo waingia kwenye shindano la Tigo Fiesta 2018 Chemsha Bongo Trivia, ambapo zawadi za kila siku za shilingi laki moja na za will za milioni 1 utolewa. Pia wateja wa Tigo wataweza kufutahi Huduma ya intaneti kupitia promosheni ya Data Kama Lota kwa kununua kifurushi na kupata mara mbili ya ulichonunua kupitia menu ya *147*00#.

Kesho jumapili Vibe la Tigo Fiesta litahamia mkoani Iringa kwenye uwanja wa Samora na itapandisha wasanii akiwemo Fid Q, Ben Pol,Maua Sama, WhoZu, Marioo, Nandy, Chege,Barnaba, Billinas, Weusi na wengine wengi.

MKANDARASI NA MHANDISI WA MAJI WATAKIWA KUJIELEZA MRADI KUTOFANYA KAZI, NJOMBE

$
0
0

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso (Mb), akisikiliza maelezo kuhusu mradi wa maji wa Ukalawa, katika jimbo la Lupembe mkoani Njombe. Mradi huo bado haujaanza kutoa huduma ya majisafi na salama kwa wananchi.

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) leo ametoa muda wa saa kumi na mbili (12) kwa Mkandarasi, pamoja na Mhandisi wa maji aliyesimamia mradi wa maji wa Ukalawa mkoani Njombe kueleza sababu za kukwama kwa mradi huo ambao serikali imeshalipa fedha.

Mhe. Aweso (Mb) ambaye ameanza ziara ya kikazi mkoani Njombe ya kukagua mradi kwa mradi inayohusu sekta ya maji amesema itakapofika saa mbili kasoro asubuhi, tarehe 06.10.2018 wahusika hao wakutane nae katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe bila kukosa, kabla ya kutafutwa.

Mhe. Aweso (Mb) ameainisha kuwa kumbukumbu zinaonyesha mkandarasi aliyepewa kandarasi ya mradi huo wenye thamani ya shilingi Milioni 562, tayari ameshachukua malipo kiasi cha Shilingi Milioni 532 wakati wananchi bado hawapati majisafi na salama kama serikali ilivyopanga.

Mhe. Aweso (Mb) akiongea na wananchi wa vijiji vya Ukalawa na Kitole ambao wanategemea majisafi na salama kutoka katika mradi huo amesema serikali ikitoa fedha maana yake ni wananchi kupata huduma ya maji, na si vinginevyo, na suala la kuoneana haya katika kazi halina nafasi kwasababu maji hayana mbadala.

Mhe. Aweso (Mb) amewakumbusha wataalam wa maji kuwashirikisha wananchi katika miradi ya maji ili wajue kazi inavyofanyika, pia kulinda miradi hiyo. Mradi wa maji Ukalawa una vituo vya maji 13 ambavyo havitoi maji.

Huduma ya majisafi na salama kwa Mkoa wa Njombe ni asilimia 55.7 kwa mjini na asilimia 65.5 vijijini.

UBALOZI WA SWEDEN WATOA ZAIDI YA BILION 14 ZA KITANZANIA KWA FCS

$
0
0

Balozi wa Sweden nchini Bw. Anders Sjoberg akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Bw. Krancis Kiwanga wakati wa kusaini Ruzuku kwa ajili ya kusaidia AZAKI za hapa nchini.
 Balozi wa Sweden nchini Bw. Anders Sjoberg  akisaini Ruzuku kwa ajili ya kusaidia AZAKI za hapa nchini.

Balozi wa Sweden nchini Bw. Anders Sjoberg akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Bw. Krancis Kiwanga wakati wa kusaini Ruzuku kwa ajili ya kusaidia AZAKI za hapa nchini.
Kwa kipindi hiki ambacho tunahitaji kuelekea katika sera ya uchumi wa viwanda Tanzania inahitaji jamii iliyo
huru, yenye demokrasia na inayofuata haki katika juhudi zake za kuwaleletea maendeleo wananchi wake.


Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Bw. Francis Kiwanga wakati akipokea Ruzuku ya shilingi billion 14.3 za kitanzania ambayo ni sawa dola za kimarekani milioni 6.25 kutoka katika Ubalozi wa Sweden wa hapa Tanzania kwa ajili ya kuwezesha kazi za Asasi za Kiraia (AZAKI).

Ruzuku hiyo itatumika katika kujenga demokrasia na utawala bora kwa kuboresha AZAKI,kuongeza ushawishi na ushiriki wa wananchi katika maswala ya sera za maendeleo pamoja na mafunzo kwa kipindi 2018 – 2020.

Makubaliano hayo yamefanyika jana oktoba 5, 2018 katika ubalozi wa Sweden hapa nchini Tanzania uliopo posta jijini Dar es salaam na kutiwa saini na Balozi wa Sweden nchini Bw. Anders Sjoberg pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Bw. Francis Kiwanga.

Akiongea baada ya zoezi la kusaini Ruzuku hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society Bw. Francis Kiwanga amesema kuwa Taasisi hiyo imejikita katika kuwasaidia watanzania na imeweka nguvu kubwa katika kuimiza uwajibikaji na utawala bora pamoja na kuwajengea uwezo vijana, wanawake na makundi mengine ili kusaidia maendeleo yao na ya  nchi kwa ujumla.

“Sekta ya Asasi za Kiraia (AZAKI) nchini sasa ni jukwaa madhubuti la kuhabarisha, kuwezesha na kuhamasisha wananchi  kufuatilia,kuhoji na kushiriki katika jitihada za serikali katika ngazi zote. Ruzuku hii kwa kiwango kikubwa sana itatuongezea
nguvu katika kufanikisha hilo”. amesema Bw. Kiwanga

  
Balozi wa Sweden nchini Bw. Anders Sjoberg akisaini mkataba na Taasisi ya FCS wa kusaidia AZAKI za hapa nchini, mkataba huo uliosainiwa jana katika ubalozi wa Sweden hapa Tanzania.

Ameongeza kuwa kwa miaka 16 sasa uwezeshaji wa FCS kwa azaki umefikia wilaya zote za Tanzania bara na Zanzibar, kupitia utoaji Ruzuku na huduma za kujenga uwezo kwa Asasi zaidi ya 5000, Na nyingi ni za ngazi ya chini na katika jamii zilizopo vijijini.

Kwa upande wake balozi wa Sweden nchini Bw. Anders Sjoberg alisema kuwa Sweden imeamua kushirikiana na Foundation for Civil Society kutokana na uwezo pamoja na kujituma kwake katika kuwezesha sekta ya asasi za kiraia ili kushiriki kikamilifu katika kujenga utawala bora nchini Tanzania.

“Kuwezesha asasi za kiraia kunatoa nafasi ya kujenga uwajibikaji na uwazi katika jamii” alisema Balozi Sjoberg

WAZIRI MKUU MAJALIWA MGENI RASMI MAONESHO YA SIDO KITAIFA SIMIYU

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari na Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa,yatakayofanyika mkoani SIMYU katika Viwanja vya nane nane Nyakabindi, kuanzia tarehe 23-28 Oktoba, 2018.
Baadhi ya na Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa,yatakayofanyika mkoani SIMYU katika Viwanja vya nane nane Nyakabindi, kuanzia tarehe 23-28 Oktoba, 2018 , wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ,katika mkutano uliofanyika Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari na Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa,yatakayofanyika mkoani SIMYU katika Viwanja vya nane nane Nyakabindi, kuanzia tarehe 23-28 Oktob, 2018 .
Baadhi ya waandishi wa habari na Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) Kitaifa,yatakayofanyika mkoani SIMYU katika Viwanja vya nane nane Nyakabindi, kuanzia tarehe 23-28 Oktoba, 2018 , wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ,katika mkutano uliofanyika Mjini Bariadi.

Na Stella Kalinga, Simiyu

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maonesho ya Kwanza ya Viwanda vidogo (SIDO) ambayo Kitaifa yatafanyika mkoani SIMYU katika Viwanja vya nane nane Nyakabindi, kuanzia tarehe 23-28 Oktoba, 2018.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka katika kikao cha maandalizi ya maonesho hayo kilichowashirikisha baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na mameneja wa Shirika la Viwanda vidogo (SIDO) kutoka mikoa ya Simiyu, Dodoma ,Mwanza, Kagera ,Mara, Shinyanga na Arusha.



Mtaka amewakaribisha wananchi wa mkoa mwenyeji Simiyu Watanzania wote kwa ujumla kuja kushiriki maonesho ya SIDO yatakayobebwa na Kauli Mbiu “Pamoja Tujenge Viwanda Kufikia Uchumi wa Kati” na kubainisha kuwa mkoa wa Simiyu unaamini kuwa maonesho hayo yatakuwa ni maonesho darasa, mahali ambapo watu watajifunza na kufanya biashara.

Ameongeza kuwa maonesho ya SIDO yanabeba ajenda ya Serikali ya awamu ya tano na matamanio ya Mhe. Rais ya kuwa na Tanzania ya Viwanda na kuifikisha nchi katika Uchumi wa Kati, hivyo akaawaalika wadau wote wenye teknolojia mbalimbali kushiriki maonesho haya.

“Ninawaalika wadau wote wenye teknolojia mbalimbali waweze kushiriki maonesho haya , nayaalika makampuni, taasisi na mashirika yenye vitu vinavyoweza kuwafaa wajasiriamali na Watanzania ambao wangehitaji kuwekeza kwenye viwanda, waweze kuleta teknolojia zao”

“Ninawaaalika Wajasiriamali wote kushiriki maonesho haya maana yatatoa nafasi kila mjasiriamali kujifunza kwa mwenzake, kupata elimu na kubadilisha ujuzi ili waweze kuzalisha bidhaa bora zaidi” alisema Mtaka

Aidha, ametumia mkutano huo kuzialika taasisi za fedha ili ziweze kujitangaza kwa wajasiriamali nao wakaona ni namna gani wanaweza kupata mitaji, huku akisisitiza na kuzialika taasisi za kitaaluma na vitivo vya uhandisivya Vyuo vikuu pamoja na mashirika mbalimbali ya Kimatifa yanayofanya kazi hapa nchini.

Akizungumzia ada ya ushiriki Mtaka amesema wajasiriamali wenye mahitaji maalum watashiriki bure, wajasiriamali wadogo watashiriki bila kulipia gharama yoyote isipokuwa watalipa shilingi elfu kumi (10,000/=) kwa ajili ya sare, wajasiriamali wa kati watachangia shilingi laki mbili (200,000/=) taasisi, makampuni na mashirika ambayo hayapo katika makundi la wajasiriamali wadogo , wa kati na wadhamni watatakiwa kuchangia shilingi milioni mbili (2000,000/=) kama ada ya ushiriki.

Kwa upande wa udhamini Mtaka amesema kuwa kwa taasisi, mashirika au kampuni zitakazo dhamini maonesho hayo, kiwango cha juu kitakuwa shilingi milioni thelethini (30,000,000/=), kiwango cha kati shilingi milioni kumi (10,000,000/= ) na kiwango cha chini kitakuwa milioni tano (5,000,000/=) huku akisisitiza kuwa wadhamini hawa watambuliwa kwa vyeti na watapewa kipaumbele cha mgeni rasmi kutembelea mabanda yao.

Jumla ya wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa 1000 wanatarajia kushiriki Maonesho haya ya Viwanda Vidogo SIDO Kitaifa pamoja na taasisi, mashirika na makampuni ya Umma na binafsi yatashiriki pia.

IGP SIRRO AWASHUKURU WANANCHI

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud Arusha

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro amewashuru wananchi kwa ushirikiano uliopelekea matukio ya uhalifu nchini kupungua kwa kiasi kikubwa ikiwemo matukio ya matumizi ya silaha.

Akizungumza na vyombo vya habari Jijini hapa Siro amesema kuwa matukio mengi ya uhalifu hapa nchini yamepungua ambapo amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano utakaosaidia kuondoa uhalifu nchini. Amesema kuwa Dhamana ipo kisheria na kila mmoja na haki ya kuipatahivyo inategemea na kosa ulilofanya ndio linepelekea kupewa dhamanatena kwa siku yoyote na muda wowote.

“Swala la dhamana lipo kwa mujibu wa sheria na dhamana inatolewawakati wowote ila inategemea na makosa ya mtuhumiwa”alisema siro Amesema Hali ya ulinzi na usalama hapa nchi kwa sasa ni shwari kuanzia hapa Arusha na mikoa mengine isipokuwa kwa kigoma wameongeza askari kuendelea kudhibiti matukio kwa kuwa mkoa huo ni miongoni mwa mikoa ya mipakani ina ina muingiliano.

Aidha amesema kuwa matukio ya mauaji ya mapenzi yamekuwachangamoto kubwa na yanalisumbua jeshi hilo hususani masuala ya ubakaji lazima tuwe wastaarabu kuepuka matukio yatakayopelekea mauaji na familia kuteseka. “Suala la mauaji ya wapenzi kwa wapenzi ikiwemo kufumaniana limekuwa changamoto kwetu tumejipanga kuyashughulikia na kuwataka viongozi wa madhehebu ya dini kulishughulikia hilo lipo kwenye uwezo wao”alitanabisha Sirro

Amesema kuwa ushamba ndio unaopelekea mtu kumuua mpenzi wake hivyo kuifanya familia kuteseka na kuwasihi watanzania kuweza kuepuka matukio hayo kwa kuwa wastaarabu na kuvumiliana.

MAJAMBAZI SUGU WAWILI HATARI WANASWA MWANZA

$
0
0
Jambazi sugu Peter Thomas Nyanchiwa anayedaiwa kuiba gari na kumjeruhi dereva wa gari hilo kwa risasi akionyeshwa kwa waandishi wa habari na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza (RPC) ACP Jonathan Shanna (kushoto). Picha na Baltazar Mashaka.

Mtuhumiwa wa Ujambazi Jackson Elias akitambulishwa wkwa waandishi habari jana baada ya kutiwa mbaroni na polisi kuhusiana na tukio la uhalifu.Kushoto ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza (RPC) Kamishna Msaidizi wa polis (ACP) Jonathan Shanna. wengine ni maofisa na askari wa jeshi hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza (RPC) Jonathan Shanna akiwasomea waandishi wa habari majina ya hati ya kusafiria ya mtuhumiwa wa ujambazi Peter Thomas Nyachiwa.

Kamanda Jonathan Shanna akiwaonyesha wana habari gari T 122 DLY lilioibwa na majambazi kabla ya kukamatwa huko Runzewe mkoani Geita.



· Mmoja anaswa na bastola,risasi 42 na magazine mbili, fedha tasilimu sh. milioni 1.3 za hongo barabarani, simu tatu na kadi nane za mitandao tofauti.
· Mwingine anaswa na Bendera ya Taifa, king’amuzi cha Startimes

NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

MAJAMBAZI sugu wawili hatari wamenaswa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza waiwa na silaha na vitu mbalimbali baada ya kufanya uhalifu katika matukio mawili tofauti.

Majambazi hao Peter Thomas Nyanchiwa au Smart Boy mkazi wa jijini Dar Es Salaam, alikamatiwa eneo la Runzewe mkoani Geita huku Jackson Elias maarufu Longoko (20) mkazi wa Shamaliwa Igoma katika Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza akikamatwa Oktoba 3, majira ya saa 11:00 alfajiri akiwa nyumbani kwake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza (RPC) Kamishna Msaidizi (ACP) Jonathan Shanna alisema majambazi hao walikuwa wakiwatesa wananchi kutokana na uhalifu wa kutumia silaha wakiwavunjia nyumba na kuwapora mali na fedha .

Alisema tukio la kwanza jambazi Peter akiwa na wenzake wawili walikodisha gari hilo jijini Mwanza kutoka kwa mmiliki wake kwenda kuwachukua watalii wakidai wameharibikiwa gari lao katika mbuga ya wanyama Serengeti ili kuwawezesha kuendelea na safari ya kutalii kwenye mbuga hiyo.

Alieleza kuwa mtuhumiwa na wenzake wawili wakiwa njiani katika eneo la Kijiji cha Nata wilayani Serengeti walimshusha dereva wa gari hilo jina linahifadhiwa na kumkalisha chini kabla ya kumpiga risasi mbili moja kichwani upande wa kulia ambayo ilitokea kwenye taya kushoto na kung’oa meno matatu ambapo nyingine ilimparaza kwenye shavu la kulia.

“ Watuhumiwa hao baada ya kumshusha dereva na kumketisha chini aliwaomba asali kwanza, baada ya kumaliza kusali walimpiga risasi kichwani (mbele karibu ya sikio la kulia) kisha wakaondoka na gari wakiamini kuwa amefariki dunia,”alisema ACP Shana na kuongeza kuwa :

“Dereva aliokolewa na wananchi waishio jirani na eneo hilo baada ya kusikia milio ya risasi, walifika na kumkimbiza Hospitali ya Wilaya ya Serengeti kwa matibabu na kisha walitoa taarifa polisi ambapo majeruhi huyo anaendelea vizuri,”

Alieleza zaidi kuwa baada ya kufanya uhalifu huo Peter na majambazi wenzake waliondoka na gari kurudi walipotoka wakipitia katika barabara ya Lamadi-Bariadi-Maswa hadi Shinyanga-Kahama wakielekea nchini Uganda ambako walitarajia kuliuza gari hilo.

“ Wakati wakiendelea na harakati hizo Jeshi la Polisi Mwanza tulipata taarifa n kwa kutumia kikosi kamambe chenye weledi wa hali ya juu na kwa kushirikiana na wenzetu wa mikoa ya Mara na Geita tulianza kufuatili kwa kina na kulifukuzia gari hilo,”alisema.

Kamanda huyo wa polisi aliongeza kuwa walifanikiwa kulilipata eneo la Runzewe na kuwaamuru majambazi hao wasimame wakagoma na kuanza kuwarushia askari risasi lakini polisi waliwakabili vilivyo na kwa umahiri mkubwa waliwazi nguvu na kuwadhibiti.

Hata hivyo baada ya kuzidiwa majambazi wawili walifanikiwa kutoka kwenye gari na kutokomea porini ambapo mmoja wao (Peter) alikamatwa akiwa na bastola moja na risasi 12 na polisi walifanikiwa kukamata vitu mbalimbali baada ya kufanya upekuzi kwenye gari hilo.

Alivitaja vitu hivyo kuwa ni magazine mbili moja ikiwa na risasi 30 silaha aina ya Karashinkov (AK 47),vibao viwili vyeupe vikiwa na namba bandia T 876 DMB Toyota, bastola aina ya Barreta namba H44780Y na leseni yake namba 00097399 , hati ya kusafiria namna AB362201 mali ya Peter Thomas Nyanchiwa, hati ya dharura ya kusafiria ya Rashid Rashid na cheti cha VETA namba 35912 cha Abdallah Omary Shaaban.

Vingine ni kivuli cha kadi bandia namba 6032015 ya gari T 876 DMB Toyota, leseni ya udereva ya Peter Thomas,fedha tasilimu sh. 1,330,000, kadi tatu za ATM za benki za NMB (2) na CRDB,simu mbili aina ya Tecno,Sumsung moja, Fero moja ,kadi nane za mitandao mbalibali ya simu, vifaa vya kuvunjia (pries, pipe ranger, spanner moja na nyundo).

Kamanda huyo alifafanua kuwa fedha hizo kwa mujibu wa mtuhumiwa walikuwa wakizitumia kutoa hongo barabarani kwa askari wasio waaminifu na kwamba kadi za simu walikuwa wakizibadilisha kukwepa kukamatwa na polisi wanapofanya uhalifu na kufuatiliwa.

Pia mtuhumiwa huyo ambaye amekuwa kitafutwa kwa muda mrefu na polisi alikiri kufanya matukio mbalimbali ya uhalifu kwenye nchi jirani na kuwataka wenzake waliotoroka wajisalimishe wenyewe vinginevyo watakiona cha moto wasipofanya hivyo kwani msako wa kuwatafuta unaendelea.

Aidha, ACP Shanna alisema wanashikilia jambazi mwingine Jackson Elias au Longoko anayetuhumiwa kuvunja jengo la mashine ya kusaga katika Kijiji cha Lugeye wilayani Magu na kuiba motor tatu usiku akishirikiana na wenzake watatu.

Alidai kuwa mtuhumiwa alitoroka baada ya kufanya uhalifu huo Septemba 28, mwaka huu majira ya 5:00 usiku huku wenzake watatu wakikamatwa wakiwa na motor hizo walizoiba lakini alikamatwa siku tatu baada ya tukio.

“Tuliendelea na msako na ilipofika Oktoba 3, mwaka huu majira ya saa 11:00 alfajiri alikamatwa na polisi akiwa nyumbani kwake na kwenye upekuzi alikutwa akiwa na Bendera ya Taifa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, king’amuzi cha Startimes, mkasi mkubwa wa kukatia vyuma, bisbisi, pries moja, tindo ya kufungulia makufuli na kipande cha chuma kimoja (nondo) kilichochongwa,”alisema.

ACP Shanna alitoa onyo kwa vijana na watu wenye tabia na wanaojishusisha na uhalifu wa aina yoyote wanajihatarishia usalama wao na hivyo waache na kufanya kazi halali za kuwaingizia vipato na kusisitiza Mwanza si eneo la kuchezea watakao beep watapigiwa.ssssss

ABAMBWA KWA KUJIFANYA DK BINGWA HOSPITALI YA BUGANDO

$
0
0
Daktari bandia wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando (BMC) Joseph Samwel au Nkwabi Samwel maarufu Kabinza (26) akiwa kwenye kituo cha Polisi Kati Nyamagana, kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ACP Jonathan Shanna wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa daktari huyo bandia.

NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

DAKTARI Bingwa bandia wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando (BMC) ya jijini Mwanza Joseph Samwel au Nkwabi Samwel maarufu Kabinza (26) anayedaiwa kujifanya daktari atafikisha mahakamani muda wowote.

Samweli aliangukia mikononi mwa jeshi la polisi jijini Mwanza akituhumiwa kujifanya daktari bandia ambapo alikamatwa Oktoba 3,mwaka huu majira ya saa 11:30 jioni katika Hospitali ya BMC akiwa katika chumba cha upasuaji.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa kutokana na malalamiko ya baadhi ya wagonjwa waliyotaoa kwa uongozi wa hospitali hiyo pamoja na jeshi la polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza (RPC) Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shanna akizungumza na waandihi wa habari jana alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kuwekewa mtego na kunaswa akiwa kwenye chumba cha upasuaji atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Alisema kabla ya kutiwa mbaroni mtuhumiwa huyo alikuwa akijifanya ni daktari bingwa na alifanikiwa kuwatapeli baadhi ya wagonjwa wanaotaka kupata huduma za upasuaji na matibabu kwa njia za mkato kwa kuwatoza kati ya sh. 100,000 na 200,000 ili awapangie tarehe za karibu wapate huduma hizo.

Kwa mujibu wa ACP Shanna mtuhumiwa huyo tapeli ni mkazi wa Mtaa wa Pasiansi katika Manispaa ya Ilemela ingawa awali alipohojiwa kwenye Hospitali ya BMC alidai ni mkazi wa wilayani Magu.

“Jeshi la polisi tulipokea malalamiko ya wagonjwa kutapeliwa na kuibiwa mara kwa mara wodini na hivyo tuliwaelekeza wayafikishwe kwa uongozi wa hospitali.Tuliweka mtego tukishirikiana na na uogozi wa hospitali hiyo ya rufaa BMC tukafanikiwa kumnasa akiwa kwenye chumba cha upasuaji akiwa amevalia sare zinazovaliwa na madaktari wakiwa theater,” alisema ACP Shanna.

Alisema daktari bingwa huyo bandia alipohojiwa alikiri hakuwahi kupata elimu ya taaluma hiyo wala kufanya kazi ya utatibu. “ Polisi bado tunaendelea kuchunguza ili kubaini sare hizo alizipata wapi na aliingiaje kwenye chumba cha upasuaji.Pia wagonjwa waliotapeliwa na kuchukuliwa fedha zao wafike polisi kumtambua kwani tapeli huyu anachafua sifa ya hospitali ya BMC na baada ya upelelezi atafikishwa mahakamani,”alisema. ACP Shanna.

Aidha, kutoka na tukio hilo kamanda huyo wa polisi alitoa onyo kwa wananchi wenye tabia ya kujifanya watumishi wa umma waache vinginevyo watakumbana na mkono wa sheria. Juzi Afisa Uhusiano wa Hospitali hiyo ya BMC Lucy Joseph Mogele akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutoka hospitalini hapo alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya malalamiko ya wagonjwa ikiwa ni pamoja na kutiliwa shaka na madaktari pamoja na wauguzi wa hospitali hiyo.

Alisema kuwa likuwa akijifanya muuguzi na wakati mwingine daktari na baada ya kumshitukia mbinu mbalimbali za kimtego ziliwekwa ili kuweza kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo lakini akawa anakwepa hadi alipokamatwa juzi majira ya saa 11:30 jioni akiwa kwenye wodi ya wagonjwa wa mifupa (J5).

Mogele alieleza kuwa baada ya kubaini hakuwa na taaluma ya utabibu wala uuguzi madaktari wakishirikiana na wauguzi waliweka mtego wa kumnasa ikiwemo kumuomba kitambulisho cha kazi lakini mara zote alikuwa akikwepa na kutoweka kwenye eneo la hospitali. “Mtuhumiwa huyo alishitukiwa na wataalamu (madaktari na wauuguzi) yapata mwezi sasa na kutokana na taratibu zao wataalamu hao wa hospitali walimtambua kuwa hakuwa na ujuzi wa kitabibu kama alivyokuwa akijitambulisha,”alisema na kuongeza;

“ Mtu huyu alijitambulisha kuwa ni mkazi wa Magu na alikuwa akibadilisha maelezo kila mara.Hata kuhusu taaluma yake alisema ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha SAUT na anasoma kozi ya uuguzi ambayo kwenye mtaala haipo na pia chuo hakipo Dodoma.” Kwa mujibu wa Mogele maelezo yake Samwel (dk. bandia) yalikuwa yakijichanganya na hata taaluma yake hadi wanamkabidhi kwa polisi haikuwa imefahamika na alijitambulisha kuwa ni mkazi wa Magu na haijulikani kama ana familia (mke na watoto).

Hata hivyo Mogele alisema hadi mtuhumiwa huyo anatiwa mabaroni idadi ya wagonjwa waliotapeliwa ama kuhudumiwa naye hospitalini hapo kwa kipindi cha mwezi haijafahamika ambapo tukio ni la kwanza kutokea katika hospitali hiyo kubwa katika Mkoa wa Mwanza na Kanda ya Ziwa

Kwa upande Mwanasheria wa Hospitali ya BMC Anaclet Kamala alisema hospitali hiyo inapakwa matope na watu kujifanya ni watumishi wakati si kweli na kuwataka wagonjwa na ndugu kufuata na kuzingatia taratibu zilizowekwa ili kuepuka kutapeliwa.

Alitoa rai kwa wagonjwa kupata msaada kutoka kwa wahudumu wa hospitali hiyo ambao huvalia sare zenye maandishi “ Niulize Nikusaidie” ili kuepuka usubufu na kutapeliwa na watu wasio watumishi wa taasisi hiyo.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images