Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1677 | 1678 | (Page 1679) | 1680 | 1681 | .... | 1897 | newer

  0 0  Mkutano wa  kwanza wa Baraza la Nne la  Wafanyakazi wa  Taasisi ya Tiba ya Mifupa, ajali na upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) leo Septemba 23,2018 umefikia tamati kwa wajumbe wa mkutano huo kupitisha maazimio 11 ya kimkakati.

  Mkutano huo umehitimishwa na Mwenyekiti wake Dkt. Respicious Boniface ambaye pamoja na mambo mengine amewashukuru wadau walioshirikiana na MOI katika maandalizi ya Baraza hilo na pia kuwapongeza na kuwashukuru wajumbe kwa kushiriki kikamili kwa kuchangia mada mbalimbali zilizowasilishwa na kutengeza maazimio ya kuboresha huduma za Taasisi.

  Kwa upande wake Katibu mpya wa Baraza hilo Bwana Ngina Mitti amefurahishwa na ushirikiano ambao ameupata kutoka kwa wajumbe wa Baraza hilo ambapo pia wamemwahidi kuendelea kushirikiana nae katika kuboresha huduma za Taasisi.“Tumemaliza kikao cha kwanza cha baraza la nne la wafanyakazi MOI leo tukiwa na maazimio 11 ambayo nikiwa kama katibu natakiwa kuhakikisha maazimio hayo yanatekelezwa kabla ya kikao cha pili ambacho kitafanyika kabla ya bajeti ijayo.

   Kwa ushirikiano mzuri niliouona kutoka kwa Mkurugezi Mtendaji, wakurugenzi wengine, wakuu wa vitengo na wafanyakazi kwa ujumla ni imani yangu kuwa kila kitu kitatekelezwa kwa wakati kwa manufaa ya taasisi na taifa kwa ujumla” ameeleza Katibu huyo mpya  Bwana Ngina Mitti.
  Maadhimio hayo yamelenga kutoa huduma za Afya kwa Watanzania ili kuahakikisha huduma zote za matibabu ya mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu zinatolewa hapa nchini na kumaliza kabisa rufaa za nje ya Nchi pia kuhakikisha wagonjwa wanaofika MOI wanapata huduma bora na kwa wakati.

  Akifunga vikao vya Baraza hilo, Dkt. Boniface amesema Taasisi ipo kwenye mpango kabambe wa kuboresha huduma hususani kwenye upande wa utunzaji wa kumbukumbu kwenye mfumo maalum (Data Base).  “Tunataka tuanzishe ‘propper data base’ ya uhakika yaani kila anayeingia anajulikana na anaonekana ili kuondoa ili suala la wagonjwa kuwahi namba hapa ambapo wanakuja kuanzia saa 12  alfajili hii sasa itakoma.

  Mfumo huu utasaidia sana hivyo kwa sasa tunajipanga kwa hilo” alimalizia Dkt. Boniface.
  Baraza hilo la Wafanyakazi limehudhuliwa na wajumbe zaidi ya 70 huku pia pia wadau mbalimbali wakiwemo SSRA ambao walitoa mada juu ya kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi ya Jamii sambamba na Benki ya NMB ambao ni waadu wakubwa wa MOI ambao walitoa elimu na mafunzo namna ya benki hiyo inavyoweza kuwasaidia wateja wake wakiwemo wafanyakazi wa MOI.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, ajali na upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dk Respicious Lwezimula Boniface (Kulia) ambaye alikuwa mgeni rasmi akimpongeza na kumkaribisha Katibu mpya wa Baraza la Wafanyakazi wa MOI, Bwana Ngina Mitti baada ya kuchaguliwa kwenye Baraza hilo la Nne.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokete Mwegelo akizungumza jambo wakati wa halfa iliyoandaliwa kwa ajili ya uchagiaji katika sekta ya elimu yenye lengo la kutokomeza ziro kwa wanafunzi wa shule za sekondari.
  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo akiwa na na wadau mbali mbali wa maendeleo katika halfa hiyo iliyofanyika katika shule ya Sekondari Minakaki.
  Diwani wa kata ya Kibuta Mohamed Kilumbi akizungumza jambo wakati wa halfa hiyo ya uchangiaji kwa ajili ya kutokomeza ziri katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe .PICHA NA VICTOR MASANGU  VICTOR MASANGU,KISARAWE

  WADAU mbali mbali wa maendeleo hapa nchini katika kuunga juhudi za Rais wa awamu ya tano Dk John Pombe Magufuli katika kuboresha sekta ya elimu wamempongeza na kumuunga mkono mkuu mpya wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo kwa kuweza kuanzisha kampeni maalumu kwa ajili kutokomeza ziro kwa wanafunzi wa shule za sekondari kwa lengo la kuweza kuongeza kasi ya kiwango cha ufaulu.

  Pongezi hizo wamezitoa wakati wa halfa fupi ambayo iliandaliwa na mkuu huyo wa wilaya kwa lengo la kuweza kuchangia fedha katika sekta ya elimu ambazo zitaweza kuwa mkombozi mkumbwa katika kuwasaidia wanafunzi kuweza kufanya vizuri katika masomo yao husaani pindi wanapomaliza katika kidato cha nne.

  Wakizungumza katika hafla fupi ya uchangiaji wadau wa maendeleo akiwemo Mohameda Kilumbi ambaye pia ni diwani wa wa kata ya Kibuta pamoja na Hamisa Mobeto wamesema kwamba wameamua kuchangia kwa hali na mali katika sekta ya elimu kwa lengo la kuweza kuborsha sekta ya elimu kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakifanya vibaya katika mitihani yao.

  “Kwa kweli sisi kama wadau wa maendeleo tumeona umhumimu wa kushiriki katikam zoezi hili la kumuunga juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuchangia sektaya elimu, na pia kwa pamoja tumeungana kumuunga mkono mkuu wa wilaya wetu ambaye ameteuliwa hivi karibuni lakini lengo letu kubwa ni kuhusina na hii kampeni ya kutokomeza Ziro katika wilaya ya Kisarawe,”waliwema wadau hao.

  Pia Diwani Kilumbi alisema kwamb lengo lake kubwa ni kuendelea kushirikiana kwa dhati na viongoz mbali mbali i wa serikali kwa lengo la kuweza kuimarisha miundimbinu ya majengo ya madarasa mbayo yataweza kuwa ni rafiki zaidi kwa wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri ambayo yatawafanya wanafunzi kuongeza bidii katika masomo yao.

  Naye Hamisa Moteto ambaye pia ni mwigizaji maarufu hapa nchi alisema kwamba ameguzwa na suala hususana kwa wanafunzi wa kike hivyo atahakikisha anaendelea kutoa michango mbali mbali ambayo itaweza kusaidia kwa kisi kikubwa kuboresha miundombinu ya majengo ya madarasa ili kuweza kuwapa fursa wanafunzi hao kusoma katika mazingira mazuri na kuongeza kiwango cha ufaulu.

  “Mimi nimeamua kuungana na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe katika kuhakikisha kwamba tunamuunga mono Rais wetu katika kuboresha setkta ya elumu hiyo kwa upende wangu licha ya harambee hii kusogezwa mbele kutokana na maafa ambayo yametokea uko ukerewe lakini tumeamua kutoa michango mbali mbali mimi na wezangu ambayo itaweza kuwasaidia wanafunzi katika suala zima la kukuza kiwango cha elimu,”alisema Mobeto.

  Kwa upande wake Mkuu huyo wa Wilaya alisema kwamba lengo lake kubwa ki kuhakikisha anapambana vilivyo katika kukuza sekta ya elimu hivyo amewaomba wadau mbali mbali wa maendeleo kumpa sapoti Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli katika kuleta mabadiliko chanya katika suala zima la maendeleo katika sekta mbali mbali hususan elimu.

  Katika halfa fupi hiyo ya uchangiaji wadau mbali mbali waliweza kuahidi na kutoa pesa taslimu ambapo kiasi cha shilingia zaidi ya milioni 125 ziliweza kuahidiwa na shilingi milioni 13 ziliweza kutolewa kwa lajili ya kampeni ya kutomeza ziro katika Wilaya ya Kisarawe iliyopo Mkoani Pwani.

  0 0
  Afisa Tawala wa Wilaya ya Kasulu,Bw.Titus Mguha, mweye shati la kitenge akishirikiana na Meneja wa Miradi ya Maji kutoka taasisi ya Poul Due Jensen Foundation,Bw.Nils Thorup kukata utepe kuzindua mradi wa maji sai na salama katika kata ya Zeze wilayani Kasulu ambao umetekelezwa na Water Mission Tanzania, kwa udhamini wa taasisi ya Poul Due Jensen Foundation.
  Afisa Tawala wa Wilaya ya Kasulu, Bw.Titus Mguha (wa pili kutoka kulia) akifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wa kata ya Zeze ambao umejengwa na taasisi ya Water Mission Tanzania,kwa udhamini wa taasisi ya, Poul Due Jensen Foundation,wengine pichani ni Mkurugenzi wa Water Mission Tanzania Benjamin Filskov (wa kwanza kushoto),Mkurugenzi wa water Mission wa kanda ,Will Furlong (katikati) na Meneja wa Miradi ya Maji kutoka taasisi ya Poul Due Jensen Foundation,Bw.Nils Thorup
  Baadhi ya wakazi wa Zeze wakicheza ngoma kufurahia kupata maji.
  Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika hafla hiyo ya uzinduzi wakifuatilia matukio Wakazi wa Kata ya Zeze iliyopo wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, kuanzia sasa wana uhakika wa kupata maji safi na salama kutokana na kuzinduliwa kwa mradi mpya wa kusambaza maji katika eneo lao.Mradi huo wenye uwezo wa kuhudumia watu karibu 5,100,umefanikishwa na Shirika lisilo la Kiserikali la kimataifa la Water Missions International Tanzania.
   
   Serikali ya Tanzania,Water Missions International Tanzania na Poul Due Jensen Foundation ,kwa pamoja tunatambua kuwepo mahitaji ya maji safi na salama katika kanda hii na tunashirikiana pamoja na jamii zinazoishi maeneo ya miradi tumehakikisha tunaanzisha miradi endelevu ya maji safi na salama ambayo imeleta suluhisho la tatizo hili kwenye nchi za Afrika Mashariki.”
   
   Aliendelea kusema “Tunayo furaha kusheherekea uzinduzi wa mradi wa maji wa kata ya Zeze,ikiwa ni kuienzi,siku ya Niels Due Jensen,kutimiza miaka 75 ya kuzaliwa na miaka 50 ya kutoa mchango wake wa kuhudumia miradi ya kijamii kupitia taasisi ya Poul Due Jensen Foundation na kampuni ya Grundfos,” Mwakilishi kutoka taasisi ya Poul Due Jensen Foundation,ambaye ni Meneja wa miradi ya maji,Bw. Nils Thorup alisema “Niels Due Jensen, mwenyewe ndiye alitoa maagizo kuwa pesa za msaada kutoka taasisi yake zisaidie kufanikisha miradi ya maji karibu na moja ya eneo lililopo karibu kambi za wakimbizi nchini Tanzania”.
   
  Niels siku zote anasema kufanya kazi peke yako mafanikio yake yana mipaka ila kushirikiana na watu wengi kunaweza kufanikisha kila jambo. Ni wakati wenu wakazi wa jamii ya Zeze kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha mradi huu tunaosheherekea kuzinduliwa kwake siku hii ya leo unakuwa endelevu.Hakuna anayeweza kufanikisha hilo peke yake bali unahitajika ushirikiano na mkifanikisha hilo mradi huu utanufaisha Watoto wenu,wajukuu mpaka vizazi vya mbele vijavyo”. 
   
  Mkurugenzi wa Water Mission Tanzania nchini,Bw.Benjamin Filskov, alieleza jinsi taasisi hiyo ilivyofanikisha miradi mbalimbali ya maji nchini Tanzania “Niels Due Jensen amekuwa mfano wa kuigwa kwangu kwa kuwa ameniwezesha kuielewa vizuri miradi endelevu ya maji na jinsi ya kuifanikisha.Ninayo furaha kuienzi dhamira yake hiyo kupitia mradi huu.” Wakazi wa kata ya Zeze idadi yao inakaribia watu 5,100,ikiwemo watu wengine zaidi 410 ambao wanakuja kwenye taasisi za kihuduma zilizopo kwenye kata hiyo (Shule na Zahanati) ambao wanafanya idadi ya watu kufikia 5,510.
   
  Kata ya Zeze inazo shule za msingi 2,shule ya sekondari moja,zahati ndogo na makanisa.Wakazi wa Zeze wamekuwa wakipata maji kwenye visima na wengi wao wamekuwa wakitayumia kwa kunywa bila kuyaweka katika mazingira ya usafi zaidi. Kwa upande wake,Afisa Tawala wa Wilaya ya Kasulu,Titus Mguha ,amesema mradi huu ni wa kihistoria kutokana na eneo hilo kuwa na changamoto ya maji kwa muda nrefu “Kwa niaba ya Serikali napenda kuzishukuru taasisi za Water Mission Tanzania, the Niels Due Jensen Foundation na Grundfos kwa jitihada zao ambazo zimefanikisha wakazi wa eneo hili wanapata maji safi na salama”alisema. Alisema,kabla ya kuanzishwa mradi huu,wanawake walikuwa wakisafiri umbali mrefu kutafuta maji na maji waliyokuwa wakiyapata hayakuwa salama ambapo yalisababisha kuwepo kwa milipuko mbalimbali ya magonjwa kwenye jamii hiyo. 
   
  Alitoa wito kwa wanufaika wa mradi huo kuwa sehemu ya mradi huo na siku zote kuwa mstari wa mbele kulinda miundombinu ya mradi na kuwapa ushirikiano wataalamu wanaosaidia kuufanikisha “Kama Serikali ya wilaya tuko tayari kushirikiana na Water Mission Tanzania,kuhakikisha mradi huu unakuwa endelevu katika eneo hili ambalo linakua kwa kasi,”alisema.

  0 0

  *Awataka Watanzania waiache Serikali na dola vifanye kazi yake
  *Asema tume ya uchunguzi itatangazwa karibuni, wahusika kuchukuliwa hatua *Waziri Mhagama atangaza namba ya tigopesa kupokea michango

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza maelfu ya wakazi wa wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza na mkoa jirani wa Mara katika mazishi ya kitaifa ya watu waliopoteza maisha kwenye ajali ya MV Nyerere Septemba 20, mwaka huu.

  Waziri Mkuu ambaye ameongoza mazishi hayo leo (Jumapili, Septemba 23, 2018) kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, amewataka Watanzania waiache Serikali na vyombo vya dola viendelee kufanya kazi yake.

  “Wito wa Serikali kwenu wote, ni kuwasihi tushikamane na wenzetu waliopoteza ndugu zao, wakiwemo wazazi, kaka, dada na watoto. Ninaomba tuiache Serikali na vyombo vya dola viendelee kufanya kazi yake. Tuendelee kuwa wavumilivu,” amesema.

  Akiwasilisha salamu za rambirambi kutoka kwa Rais Magufuli mbele ya wafiwa na waombolezaji, Waziri Mkuu amesema: “Mheshimiwa Rais alipokea tukio hili kwa mshtuko mkubwa na anawapa pole sana wafiwa wote pia anawaombea majeruhi wote wapate ahueni mapema.”

  Amesema jumla ya watu 224 walipoteza maisha kutokana na ajali hiyo. Kati ya hao, miili 214 kati ya 219 iliyotambuliwa, ilichukuliwa na ndugu zao. Miili minne haikuweza kutambuliwa lakini ipo miili mitano ambayo ilitambuliwa na ndugu zao na hao ndugu wakaona ni vema wazikwe hapa eneo la tukio. Kwa hiyo leo tutawazika ndugu zetu tisa katika eneo hili,” amesema.

  Waziri Mkuu amesema Serikali imechukua hatua ya kuunda tume ya uchunguzi na kuahidi kwamba tume hiyo itatangazwa wakati wowote. “Tume ikikamilisha kazi yake, wote watakaobainika kuwa wamehusika watachukuliwa hatua mara moja,” amesema.

  Ili kukabiliana na tatizo la usafiri lililopo, Waziri Mkuu amesema meli ya MV Nyehunge imeanza kutoa huduma ya usafiri wa muda badala ya MV Nyerere iliyokuwa ikitoa huduma kati ya bandari ndogo ya Bugolora, Ukerewe na kisiwa kidogo cha Ukara.

  Amesema jitihada za kuivuta meli ya MV Nyerere iliyopinduka zinaendelea na kwamba maafisa wote wanaohusika na usafiri wa majini ambao walizembea kwenye suala hilo, wamekamatwa na wameanza kuhojiwa.

  Akigusia chanzo cha ajali hiyo, Waziri Mkuu amesema inasadikiwa kivuko cha MV Nyerere kilibeba mizigo mingi kuliko uwezo wake ambao ni wa kubeba tani 25 za mizigo, magari matatu na abiria 101. “Hadi sasa inaonesha kulikuwa na watu zaidi ya 260, yaani 41 waliookolewa na 224 waliopoteza maisha,” amesema.

  Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi wote wa Ukara waliojitokeza kusaidia kazi ya uokoaji tangu ajali hiyo ilipotokea. Pia aliwashukuru wote waliotoa michango mbalimbali, watumishi wa hospitali za Bugando, Sekou Toure, Ukerewe, kituo cha afya cha Bwisya na timu nzima inayofanya kazi ya uokoaji na uopoaji wa miili kwa kazi kubwa waliyoifanya.

  Wakati huohuo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Jenista Mhagama ametangaza namba ya tigopesa ambayo wananchi wanaweza kuitumia kutuma michango yao kwa ajili ya waliopatwa na maafa hayo.

  “Tumefungua akaunti ya maafa kwenye Benki ya NMB tawi la Kenyatta lakini ili kurahisisha upokeaji wa michango kutoka kwa wananchi wa kawaida, tumesajili namba ya tigo yenye namba 0677-030-000 kwa jina la RAS Mwanza. Naomba wale wasioweza kwenda benki watumie namba hiyo,” amesema.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMAPILI, SEPTEMBA 23, 2018.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye kaburi  la mmoja wa wananchi walifariki katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama katika katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe. Majaliwa aliwaongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi yaliyofanyika kwenye kijiji hicho Septemba 23, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima kwenye kaburi  la mmoja wa wananchi walifariki katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama   katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe. Majaliwa aliwaongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi yaliyofanyika kwenye kijiji hicho Septemba 23, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa pole wafiwa katika mazishi ya mwananchi waliofariki katika ajali ya Kivuko cha MV Nyerere kilichozama  katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe. Majaliwa aliwaongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi yaliyofanyika kwenye kijiji cha Bwisa  kisiwani Ukara Septemba 23, 2018. 
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipewa maelezo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kuhusu juhudi zinazofanywa  na wahandishi za kukivuta kivuko cha MV Nyerere kilichozama katika Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe wakati aliposhiriki katika mazishi ya wananchi waliokufa katika ajali ya kivuko hicho kwenye kijiji cha Bwisa kisiwani Ukara Septemba 23, 2018.
  Askofu wa Jimbo Katoliki la Bunda, Renatus Nkwande akiomba katika  mazishi ya wananchi waliofariki dunia katika ajali ya Kivuko cha MV  Nyerere kilichozama katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe. Mazishi hayo yaliyoongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa yalifanyika katika kijiji cha Bwisa kisiwani Bukara, Septemba  23, 2018.  
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Abood  (wapili kulia) akiungana na Masheikh katika  sala kwenye mazishi ya wananchi waliofariki dunia katika ajali ya Kivuko cha MV Nyerere kilichozama katika Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe. Mazishi hayo yaliongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika kijiji cha Bwisa  kisiwani Bukara, Septemba 23, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0  0 0

   


   
   


  0 0

  NA MWAMVUA MWINYI, KIBITI 

  NAIBU Waziri wa Nishati ,Subira Mgalu amesema serikali inaendelea kujenga gati la Nyamisati, Kibiti, mkoani Pwani na haina mpango wa kulihamisha ambapo linatarajiwa kugharimu sh. bilioni 14 hadi kukamilika kwake. 

  Amewatoa shaka hiyo baada ya wananchi hao kuhisi ujio wa ujenzi wa mradi mkubwa wa uzalishaji umeme katika maporomoko ya mto Rufiji, Hydro Power (Stigilers Gorge )utasababisha athari za ujenzi wa gati hilo kwenda kisiwa cha Mafia. 

  Subira aliyasema hayo, wakati akizungumza na wananchi wa Nyamisati, mara baada ya kutembelea ujenzi wa gati hilo .Alisema mradi wa ujenzi wa gati hilo umefanyiwa utafiti wa kina na kubaini hautakuwa na athari zozote za kimazingira .Subira alieleza, baadhi ya watu wanadai kuwa eneo hilo la gati kina cha maji kitapungua suala ambalo sio la kweli ."Wataalamu wa mradi wa Hydro Power na gati walikaa kubadilishana uzoefu, na ripoti yao inaonyesha hakutakuwa na athari za kimazingira "

  " Wataalamu walifanya upembuzi yakinifu na hakujaonyesha kuwa kutakuwa na athari ya kimazingira," alisisitiza Subira .Alisema ,miradi yote hiyo ina faida kubwa kwa wananchi na Taifa na serikali imetumia wataalamu kufanya utafiti ili kujiridhisha .Pamoja na hilo, Subira alieleza serikali imedhamiria kuufungua ukanda wa Kisiwa cha Delta kwa kupeleka nishati ya umeme ambapo inatarajia kuanza na umeme wa jua. 

  Pia imetengwa kiasi cha sh. bilioni. Nne kwa ajili ya ujenzi wa daraja Mbwera na mil. 400 imetengwa kwa kujenga kituo cha afya Mbwera. Nae meneja wa ujenzi wa mradi wa gati la Nyamisati kutoka mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Erick Madinda alisema maji hayawezi kupungua mara litakapojengwa bwawa kubwa la uzalishaji umeme la Stigilers Gorge.

  Alieleza, eneo hilo ni sehemu ambapo kuna mwingiliano wa mto na bahari hivyo maji hayawezi kupungua na kuleta athari kwenye gati.Mbunge wa Kibiti Ally Ungando, aliomba kasi ya ujenzi wa gati iongezeke kwakuwa imekuwa ndogo.
  Naibu waziri wa nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Nyamisati wilayani Kibiti.(picha na Mwamvua Mwinyi)

  0 0

  MAREKEBISHO YA TAARIFA KWENYE MAOMBI YA MIKOPO HESLB


  Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda kuwataarifu waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019 na umma kwa ujumla kwamba imetangaza orodha ya baadhi ya waombaji mikopo ambao fomu zao za maombi ya mikopo zina upungufu ili waweze kufanya marekebisho kwa njia ya mtandao https://olas.heslb.go.tz kwa siku saba (7) kuanzia Jumatatu  Septemba 24 hadi Jumapili  Septemba 30, 2018.

  Katika kipindi hicho waombaji wote wa mikopo ambao fomu zao zina upungufu wa baadhi ya taarifa na nyaraka zao ama za wadhamimi wao, watapaswa kusoma majina yao kwenye orodha iliyowekwa kwenye tovuti ya HESLB www.heslb.go.tz na kisha kuingia kwenye mtandao wa maombi ya mikopo ili kufanya masahihisho kwa kufuata hatua zilizowekwa na baada kukamilisha, waziwasilishe ndani ya muda uliopangwa bila kutuma kwa njia ya EMS.

  Nyaraka zote zinazokosekana ikiwa ni pamoja na vyeti vya kuzaliwa au vya vifo vya wazazi, kurasa za taarifa na saini za mwombaji na/au mdhamini wake zinapaswa kujazwa kwa ukamilifu, kuwa ‘scanned’ na kisha kupakiwa kwenye mtandao baada ya kuthibitishwa na mamlaka husika.

  Zoezi la Uhakiki wa Taarifa za Waombaji wa mikopo
  Baada kukamilika kwa muda wa kupokea maombi ya mikopo Julai 31, 2018, HESLB ilikuwa imepokea jumla ya maombi 78,833 ambapo baada ya uhakiki, HESLB ilibaini jumla ya waombaji zaidi ya 25,000 fomu zao za maombi zikiwa na upungufu wa nyaraka na uthibitisho wa kuwezesha kuendelea na hatua inayofuata ya kupangiwa mikopo katikati ya mwezi Oktoba, 2018.
    
  Hitimisho
  Kwa taarifa hii pia tunapenda kuwakumbusha waombaji wa mikopo ambao wamo katika orodha hiyo yenye upungufu wa taarifa kusoma kwa umakini na kurekebisha kasoro hizo ili waweze kupangiwa mikopo. Aidha tunawatahadharisha dhidi ya matapeli wanaoweza kutumia taarifa hiyo kuwalaghai waombaji mikopo kuwa wanaweza kuwasaidia kupata mikopo. Tangazo maalum na mwongozo wa marekebisho vinapatikana katika tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz).

  Iwapo wana maswali, wawasiliane nasi kupitia:

  Simu:                     0736665533 au 022 5507910
  Barua pepe:          adcp@heslb.go.tz au info@heslb.go.tz

  Taarifa hii pia inapatikana kwenye tovuti ya HESLB www.heslb.go.tz

  Imetolewa na:
  Mkurugenzi Mtendaji
  Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
  DAR ES SALAAM


  0 0  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa AllyRich Sanaa Arts LTD,Aliko Richard akizungumza na wageni mbalimbali na wakazi wa mkoa wa mbeya alio walika kuja kushuhudia wazo la Ndoto yake ya Niache Nichore katika Ukumbi wa Tughimbe Jijini Mbeya.
   Mkurugenzi wa Parick Mission Ndele Mwaselela akizungumza na wadau juu ya umuhimu wa kutumia maharifa tuliyopata kwa faida ya jamii kama alivyofanya Ally Rich.
   Mratibu wa Ndoto ya Ally RICH ya Niache Nichore, Mc Mwakyusa akizungumzia kwa upana juu ya umuhimu wa ndoto hiyo katika kizazi kijacho kwenye taaluma ya uchoraji na ubunifu.
   Mchoraji Mkongwe mkoani Mbeya , Furaha Mwaibandi akizungumzia uzoefu wake katika uchoraji na umuhimu wa jamii kuthamini Sanaa ya uchoraji.
   Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya , ACP.Hamisi Sungu akizungumza na wadau umuhimu wa michoro katika usalama wa maisha yetu kuanzia Viwandani mpaka Barabarani hivyo aksema ni vyema kila mmoja akatahimini ndoto ya Ally Rich.
   Mzee Mwampashi akikabidhi zawadi ya moja ya bidha zitakazotolewa katika programu ya niache nichore kwa wachoraji wa mkoa wa Mbeya.
   Wageni Maalum wakionyesha Madaftari ya kuchorea ambayo yanatokana na ndoto ya Niache nichore ya Ally Rich
   Afisa Biashara Mkoa wa Mbeya , Stanley Kibakaya akizungumzia umuhimu wa uwekezaji katika Jiji la Mbeya kaama alivyofanya Ally Rich.
  Sehemu ya wadau walioshiriki katika Mkutano huo wakifatiliakwa makini yanayozungumzwa

  0 0

  Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

  MKUUwa Wilaya ya Biharamulo Sada Malunde amewataka wote wanaoendesha shughuli za kilimo na ufugaji katika misitu ya hifadhi ya Biharamulo na msitu wa Nyantakara wilayani humo kuondoka mara moja kabla ya kuwachukulia hatua za kisheria.

  Malunde ametoa agizo hilo jana Septemba 23 akiwa kwenye msitu wa Nyantakara ambako alienda na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na maofisa wa Wakala wa Misitu (TFS) kwa ajili ya kuona uvamizi na uharibifu mkubwa unaoendelea katika hifadhi za misitu iliyopo wilayani humo.

  “Misitu huu unavamiwa kwa kasi kubwa na kuharibiwa na watu wanaoendesha shughuli za kilimo na ufugaji kinyume cha sheria, hali hii inatishia zaidi baada ya Serikali kupandisha hadhi mapori tengefu ya Kimisi, Burigi na Biharamulo kuwa Hifadhi za Taifa ambapo kuna sheria kali zinazowabana wananchi kufanya shughuli za kibinadamu.

  "Nikiwa kama kiongozi mwenye dhamana ya kusimamia utekelezaji wa sheria. Sitakubali hali hii iendelee, nawataka muondoke kwa hiari na kwenda kuishi kwenye vijiji vinavyotambulika kisheria kabla selikali hajatumia nguvu kuwaondoa,” amesema Malunde.Aidha Malunde alisema ni wakati muafaka sasa kwa serikali kuangalia uwezekano wakurekebisha sheria za misitu na kuzifanya ziwe kali zaidi ili kuepuka uharibifu wa hifadhi za misitu nchini.

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Professa Dos Santos Silayo amesema kuwa vijiji ambavyo vinaanzishwa katika maeneo ya misitu bila kufuata taratibu ni kosa kisheria na kuahidi kushirikiana kikamilifu kudhibiti uvamizi na uharibifu wa misitu wilayani huo.Kwa upande wa Meneja Misitu wa Kanda ya Ziwa Cosmas Ndakidemi amewataka wakazi wanaoishi maeneo ya jirani na misitu ya hifadhi ya Biharamulo na msitu wa Nyantakara wilayani humo kuheshimu mipaka na taratibu zilizopo ili kuepuka kuingia kwenye mkono wa sheria.

  Tayari kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo ilishatoa maagizo kuwa watu wote wanaoishi katika maeneo ya hifadhi ya misitu kuondoka kabla ya mwisho wa mwezi Septemba mwaka huu.
  Kulia ni Meneja Misitu ya Hifadhi wilayani Biharamulo Emmanuel Komba akimweleza Mtendaji Mkuu wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS Dos Santos Silayo (aliyeshika kiunx) jinsi wavamizi wa maeneo ya msitu wa Nyantakara wilayani humo wanavyathiri uhifadhi na kuhujumu uchumi wa Taifa walipotembelea situ huo na kujionea uharibifu mkubwa wa msitu huo unaosababishwa na shughuli za uchomaji mkaa . Pembeni ni Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Mhe. Sada Malunde
  Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Mhe. Sada Malunde (mwenye kofia) akiwataka wananchi wote wanaoendesha shughuli za kilimo na ufugaji katika misitu ya hifadhi ya Biharamulo na msitu wa Nyantakara wilayani humo kuondoka mara moja kabla ya kuwachukulia hatua za kisheria alipokuwa kwenye Kijiji cha Mpago kilichopo ndani ya msitu wa Nyantakara wilayani Biharamulo jana. Kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS Professa Dos Santos Silayo mwenye dhamana ya kusimamia msitu huo.
  Mmoja kati ya wavamizi wa msitu (hakuweza kufahamika jina lake) wanaoendesha shughuli za kilimo na ufugaji katika msitu wa Nyantakara wilayani Biharamulo akiendelea na shughuli zake katika msitu huo licha ya kutakiwa kuondoka mara moja kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria kama alivyokutwa na mpiga picha wetu katika Kijiji cha Nyamagana kilichopo ndani ya msitu huo.

  0 0

  Na Ripota Wetu,Michuzi Blog

  MBUNGE wa Mtama Nape Nnauye(CCM) amenusurika kifo baada ya gari aliyokuwa akisafiria kupata ajali.

   Nape amepata ajali hiyo leo asubuhi katika Kijiji cha Kibutuka akiwa njiani kuelekea Liwale kwa ajili ya kushiriki kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Mkoa.

  Taarifa ambazo Michuzi Blog imezipata asubuhi zinaeleza kuwa ndani ya gari hiyo Nape alikuwa ameambatana na watu wengine wanne ambao wote ni wazima na hamna aliyedhurika. 
  Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi amepata ajali akiwa safarini kuelekea wilayani Liwale kushiriki kikao cha kamati kuu ya siasa ya mkoa wa Lindi ikiwa ni pamoja na kuungana  na ziara ya Katibu mkuu wa CCM Taifa Bashiru Ally anayoifanya wilayani Liwale. Katika ajali hiyo hakuna kifo
  Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kibutuka wakilitazama Gari lenye namba za usajiri T 349 DEL likiwa limepinduka 

  0 0


  MKUUwa Wilaya ya Biharamulo Sada Malunde amewataka wote wanaoendesha shughuli za kilimo na ufugaji katika misitu ya hifadhi ya Biharamulo na msitu wa Nyantakara wilayani humo kuondoka mara moja kabla ya kuwachukulia hatua za kisheria.

  Malunde ametoa agizo hilo jana Septemba 23 akiwa kwenye msitu wa Nyantakara ambako alienda na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na maofisa wa Wakala wa Misitu (TFS) kwa ajili ya kuona uvamizi na uharibifu mkubwa unaoendelea katika hifadhi za misitu iliyopo wilayani humo.

  “Misitu huu unavamiwa kwa kasi kubwa na kuharibiwa na watu wanaoendesha shughuli za kilimo na ufugaji kinyume cha sheria, hali hii inatishia zaidi baada ya Serikali kupandisha hadhi mapori tengefu ya Kimisi, Burigi na Biharamulo kuwa Hifadhi za Taifa ambapo kuna sheria kali zinazowabana wananchi kufanya shughuli za kibinadamu. 

  "Nikiwa kama kiongozi mwenye dhamana ya kusimamia utekelezaji wa sheria. Sitakubali hali hii iendelee, nawataka muondoke kwa hiari na kwenda kuishi kwenye vijiji vinavyotambulika kisheria kabla selikali hajatumia nguvu kuwaondoa,” amesema Malunde.Aidha Malunde alisema ni wakati muafaka sasa kwa serikali kuangalia uwezekano wakurekebisha sheria za misitu na kuzifanya ziwe kali zaidi ili kuepuka uharibifu wa hifadhi za misitu nchini.

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Professa Dos Santos Silayo amesema kuwa vijiji ambavyo vinaanzishwa katika maeneo ya misitu bila kufuata taratibu ni kosa kisheria na kuahidi kushirikiana kikamilifu kudhibiti uvamizi na uharibifu wa misitu wilayani huo.Kwa upande wa Meneja Misitu wa Kanda ya Ziwa Cosmas Ndakidemi amewataka wakazi wanaoishi maeneo ya jirani na misitu ya hifadhi ya Biharamulo na msitu wa Nyantakara wilayani humo kuheshimu mipaka na taratibu zilizopo ili kuepuka kuingia kwenye mkono wa sheria.

  Tayari kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo ilishatoa maagizo kuwa watu wote wanaoishi katika maeneo ya hifadhi ya misitu kuondoka kabla ya mwisho wa mwezi Septemba mwaka huu.
  Kulia ni Meneja Misitu ya Hifadhi wilayani Biharamulo Emmanuel Komba akimweleza Mtendaji Mkuu wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS Dos Santos Silayo (aliyeshika kiunx) jinsi wavamizi wa maeneo ya msitu wa Nyantakara wilayani humo wanavyathiri uhifadhi na kuhujumu uchumi wa Taifa walipotembelea situ huo na kujionea uharibifu mkubwa wa msitu huo unaosababishwa na shughuli za uchomaji mkaa . Pembeni ni Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Mhe. Sada Malunde
  Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Mhe. Sada Malunde (mwenye kofia) akiwataka wananchi wote wanaoendesha shughuli za kilimo na ufugaji katika misitu ya hifadhi ya Biharamulo na msitu wa Nyantakara wilayani humo kuondoka mara moja kabla ya kuwachukulia hatua za kisheria alipokuwa kwenye Kijiji cha Mpago kilichopo ndani ya msitu wa Nyantakara wilayani Biharamulo jana. Kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS Professa Dos Santos Silayo mwenye dhamana ya kusimamia msitu huo.
  Mmoja kati ya wavamizi wa msitu (hakuweza kufahamika jina lake) wanaoendesha shughuli za kilimo na ufugaji katika msitu wa Nyantakara wilayani Biharamulo akiendelea na shughuli zake katika msitu huo licha ya kutakiwa kuondoka mara moja kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria kama alivyokutwa na mpiga picha wetu katika Kijiji cha Nyamagana kilichopo ndani ya msitu huo.

  0 0

  NA MWAMVUA MWINYI, KIBITI .

  NAIBU Waziri wa Nishati ,Subira Mgalu amethibitisha kuwa serikali inaendelea kujenga gati la Nyamisati, Kibiti, mkoani Pwani na haina mpango wa kulihamisha ambapo linatarajiwa kugharimu sh. bilioni 14 hadi kukamilika kwake. 

  Amewatoa shaka hiyo wananchi ambao walikuwa wakidai ujio wa ujenzi wa mradi mkubwa wa uzalishaji umeme katika maporomoko ya mto Rufiji, Hydro Power (Stigilers Gorge )unaweza kusababisha athari za ujenzi wa gati hilo kwenda kisiwa cha Mafia. 

  Subira aliyasema hayo, wakati akizungumza na wananchi wa Nyamisati,  mara baada ya kutembelea ujenzi wa gati hilo .Alisema  mradi wa ujenzi wa gati hilo umefanyiwa utafiti wa kina na kubaini  hautakuwa na athari zozote za kimazingira .

  Subira alieleza, baadhi ya watu wanadai kuwa eneo hilo la gati kina cha maji kitapungua suala ambalo sio la kweli ."Wataalamu wa mradi wa Hydro Power na gati walikaa kubadilishana uzoefu, na ripoti yao inaonyesha hakutakuwa  na athari za kimazingira "

  " Wataalamu walifanya upembuzi yakinifu na hakujaonyesha kuwa kutakuwa na athari ya kimazingira," alisisitiza Subira .Alisema ,miradi yote hiyo ina faida kubwa kwa wananchi na Taifa na serikali imetumia wataalamu kufanya utafiti ili kujiridhisha .

  Hata hivyo, Subira alieleza serikali imedhamiria kuufungua ukanda wa Kisiwa cha Delta kwa kupeleka nishati ya umeme ambapo inatarajia kuanza na umeme wa jua. Pia imetengwa kiasi cha sh. bilioni. Nne kwa ajili ya ujenzi wa daraja Mbwera na mil. 400 imetengwa kwa kujenga kituo cha afya Mbwera.  

  Nae meneja wa ujenzi wa mradi wa gati la Nyamisati kutoka mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Erick Madinda alisema maji hayawezi kupungua mara litakapojengwa bwawa kubwa la uzalishaji umeme la Stigilers Gorge.Alieleza,  eneo hilo ni sehemu ambapo kuna mwingiliano wa mto na bahari hivyo maji hayawezi kupungua na kuleta athari kwenye gati.

  Mbunge wa Kibiti Ally Ungando, aliomba kasi ya ujenzi wa gati iongezeke kwakuwa imekuwa ndogo.
    Naibu waziri wa nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Nyamisati wilayani Kibiti.
  Naibu waziri wa nishati, Subira Mgalu (wa pili kutoka kulia)  akimuelekeza jambo meneja wa ujenzi wa mradi wa gati la Nyamisati kutoka mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Erick Madinda (kushoto) kabla ya waziri huyo kuzungumza na wananchi wa Nyamisati wilayani Kibiti

  0 0

   KUTUPA MTOTO – JIJINI MBEYA. 

  JESHIi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mwanamke mmoja ambaye amefahamika kwa jina la INES MTUNDU [19] Mwanafunzi wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Isengo kwa kosa la kumtupa chooni mtoto mchanga wa masaa kadhaa. 

  Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 23.09.2018 majira ya saa 09:53 asubuhi huko maeneo ya Isengo – Airport ya zamani, Kata ya Iyela, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Inadaiwa kuwa mwanafunzi huyo alikuwa mjamzito na mara baada ya kujifungua chooni ndipo alimtupa mtoto huyo. 

  Mara baada ya taarifa kulifikia Jeshi la Polisi, jitihada za haraka zilifanyika kwa kushirikiana na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji na kufanikiwa kumuokoa mtoto huyo akiwa hai. Mama na mtoto huyo wote wapo Hospitali ya Wazazi – Meta wakipatiwa matibabu. Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani. 


  KUPATIKANA NA BHANGI – KYELA. 
  Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja ambaye amefahamika kwa jina la GOLIATH EMANUEL [43] Mkazi wa Kasumulu Wilaya ya Kyela akiwa na dawa za kulevya aina ya bhangi debe sita nyumbani kwake. 
  Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 22.09.2018 majira ya saa 23:47 usiku huko Kasumulu, Kata ya Ngana, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela katika msako uliofanyika maeneo hayo. Mtuhumiwa alikuwa ameificha bhangi hiyo katika mifuko ya salfeti nyumbani kwake. Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani. 

  MAUAJI – CHUNYA. 

  Mnamo tarehe 22.09.2018 majira ya saa 15:00 alasiri huko katika kitongoji cha kasisi, kijiji cha nkwangu, kata ya upendo, tarafa ya kipembawe, wilaya ya chunya, mtu mmoja aitwaye LUTONJA LUKELESHA [33] Mkazi wa Kasisi alifariki dunia akiwa anajipatia matibabu kienyeji nyumbani kwake. 

  Inadaiwa kuwa marehemu alipigwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na kukanyagwa kwa miguu kifuani na tumboni siku ya tarehe 12.09.2018 majira ya saa 12:09 mchana huko kijiji cha Kasisi na kaka yake aitwaye MASANILA LUKELESHA [45] Mkazi wa Kasisi akiwa na wenzake wawili. 

  Chanzo cha tukio hili ni tuhuma za wizi wa radio ndogo yenye thamani ya Tshs 15,000/= ya mmalila mchoma mkaa ambaye jina lake halisi bado kufahamika. Mtuhumiwa mmoja MASANILA LUKELESHA amekamatwa na msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa wengine wawili waliokimbia unaendelea. 

  Katika kudhibiti ajali za barabarani, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na doria katika maeneo ya mlima nyoka [barabara kuu ya Mbeya-Njombe-Iringa], mlima iwambi [barabara kuu ya Mbeya – Tunduma], mlima Igawilo [barabara kuu ya Mbeya – Tukuyu] na Kawetele [barabara kuu ya Mbeya – Chunya]. Aidha katika operesheni ya kukamata bajaji zinazokiuka sheria za usalama barabarani ndani ya Jiji la Mbeya kuanzia mwezi Julai hadi Septemba 2018 jumla ya bajaji 170 zimekamatwa, madereva 31 wamefikishwa Mahakamani na bajaji 91 zimelipa tozo sawa na Tshs.2,730,000/= na bajaji 75 bado zipo kituoni kwa hatua zaidi za kisheria na watuhumiwa 14 wapo rumandewakiendelea na mashauri yao. 

  Imesainiwa na: 
  [ULRICH O. MATEI - SACP] 
  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

  0 0

   
  Energy solutions services provider, Dalbit has secured two major petroleum products supply contracts with the World Food Programme (WFP) in Gulu, Northern Uganda and Goma, in the Eastern part of the Democratic Republic of Congo (DRC).

  Valued at approximately US$ 6.8 million and US$1.1 million, respectively, the two tenders secured following competitive bidding processes will see Dalbit International South Sudan supply Jet fuel to the WFP bases in Gulu and Goma.

  In Gulu, the firm has additionally completed the construction of a brand new operating depot with a capacity to hold more than 720,000 litres of Jet A1 products. The firm is additionally building and will operate a depot to world-class standards in Goma to facilitate the smooth execution of the tender. The operations will include a compact refuelling bowser configured to serve various types of aircraft.

  The WFP is the world's largest humanitarian agency fighting hunger worldwide, delivering food assistance in emergencies and working with communities to improve nutrition and build resilience. Each year, WFP assists some 80 million people in around 80 countries.

  At the Dalbit Goma depot, engineering works are at an advanced stage to complete the fabrication of two petroleum products holding tanks. Each of them, with a capacity of 1 million litres, will be connected to ancillary infrastructure including a purpose-built fuelling bay with a further two storage tanks for Jet A1 and Gasoil fuels.

  The company operates four depots in Juba, Rumbek, Wau and Bor with a storage capacity of over 6 million litres for Gasoil and Jet-A14. 

  “We are excited that Dalbit has secured the contract to supply WFP in Gulu and Goma and this works well with our commitment to fuelling regional growth across the social and economic development fronts,” said Dalbit International South Sudan Country Business Manager, John Paul Ogondi.  He also added “In such remote areas, Dalbit is deploying tailor-made solutions including customised product delivery options to enable WFP to meet its humanitarian mandate efficiently and cost-effectively.”

  In a news communiqué issued earlier this year, the WFP announced that it had scaled up its operations in the Democratic Republic of Congo's Kasai Region to stem severe hunger. The communiqué issued in February confirmed that recent airlifts from France of Plumpy’Sup, a micronutrient-rich, ready-to-use supplementary food, have allowed WFP to treat 9,000 malnourished children in January.

  Established in 2004, Dalbit has carved an enviable niche as the reliable and dependable energy solutions provider of choice in the frontier regions. Using its state of the art facilities, it has established itself as a progressive petroleum supply company delivering competitive and cost-efficient energy solutions across the continent.

  The firm provides efficient, innovative and responsible energy solutions to clients in the development, humanitarian and economic sectors in the urban and remote regions of South Sudan. The firm has developed a fleet of operating trucks customised to traverse the challenging terrain within its areas of operation, providing a responsible and distinct market differentiation.

  Dalbit South Sudan, is also a keen investor in people and communities; developing human skills and investing in projects and initiatives that offer equal opportunities to its people. In partnership with the community in Rumbek, Dalbit continues to support Bishop Mazzolari School, building classrooms and amenities that have helped to provide continuous education and a sense of normalcy to the children and the community.


  0 0

   
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametangaza tume ya kuchunguza ajali ya kivuko cha MV Nyerere yenye wajumbe saba ambayo itaongozwa na Jenerali mstaafu, George Waitara.

  Akitangaza majina hayo kwenye kijiji cha Bwisya katika kisiwa cha Ukara, wilayani Ukerewe, mkoani Mwanza leo (Jumatatu, Septemba 24, 2018), Waziri Mkuu amesema wajumbe hao wanapaswa kuikamilisha kazi hiyo ndani ya mwezi mmoja.

  Amewataja wajumbe wengine kuwa ni Mbunge wa Ukerewe, Bw. Joseph Mkundi, Mhandisi Marcelina Magesa, Wakili Julius Kalolo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Bi. Queen Mlozi.

  Wengine ni SACP Camillus Wambura na Mkurugenzi wa Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Bashiru Taratibu Hussein.

  Amemwagiza Mkuu wa Majeshi, Jenarali Venance Mabeyo asimamie uundaji wa tume hiyo na kuainisha ni mahitaji gani yanatakiwa kwa haraka na pia afuatilie utekelezaji wake. 

  MV Nyerere ilipinduka na kuzama Septemba 20, mwaka huu ambapo hadi sasa jumla ya watu 41 wameokolewa na wengine 227 wamepoteza maisha baada ya miili mingine mitatu kupatikana leo asubuhi. Jana yalifanyika mazishi ya kitaifa ambapo miili tisa ilizikwa kwenye eneo la uwanja wa shule ya msingi Bwisya. Miili 214 ilitambuliwa na kuchukuliwa na ndugu zao.

  Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza itangazwe zabuni ya haraka ya kutengeneza kivuko kingine kipya chenye uwezo wa kubeba tani 50 za mizigo na abiria zaidi ya 200.

  “Hili ni agizo la Mheshimiwa Rais, na mimi ninamuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe aitishe zabuni hiyo haraka sana. Kazi hiyo ifanywe mara moja ili kivuko kipya kiweze kutengenezwa na kusaidia wananchi wa eneo hili kwa haraka,” amesema.

  Amesema kivuko kipya kikikamilika, itabidi kipangiwe ratiba za safari nyingi zaidi badala ya kwenda mara moja kwa siku ili kuondoka kero ilikuwa ikiwakabili wananchi hao.

   IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMATATU, SEPTEMBA 24, 2018.

  0 0

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya watu walionusurika  katika  ajali ya kivuko cha MV Nyerere wakati alipotembelea Kituo cha Afya cha Bwisya  kisiwani humo Septemba 24, 2018. Wengine ni mwananchi ambao bado wamepotelewa na  ndugu na jamaa katika ajali hiyo wakisubiri kutambua miili endapo itaonekana.

   Gari la wagonjwa  likiwa limeegeshwa kwenye jengo la Kituo cha Afya cha Bwisya katika kisiwa cha Ukara wilayani  Ukererwe ili kuteremsha mwili wa mtoto  ambao waokoaji  waliupata katika kivuko cha MV Nyerere Septemba  24, 2018. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alitembelea kituo hicho leo asubuhi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia wakati Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akikabidhi  kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi, Isaack Kamwelwe mchango wa sh. milioni 10 zilizotolewa na CCM kwa ajili ya kusaidia katika  ajali ya Kivuko cha MV Nyerere  kilichozama ktika kisiwa cha Ukara wilayaniu Ukerewe, Septemba 20, 2018.  Makabidhiano hayo yalifanyika  katika kijiji cha Bwisya kisiwani Ukara, Septemba 24, 2018.

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali, Venance Mabeyo  baada ya kumkabidhi jukumu kuwa msimamizi mkuu wa operesheni ya uokoaji katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kwenye kijiji cha Bwisya katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe, Septemba 24, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (katikati)  na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa Faustine Kamuzora kwenye kijijii cha Bwisya katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe baada ya Waziri Mkuu kutembelea eneo kilipozama kivuko cha  MV Nyerere kijijini hapo Septemba 24, 2018.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi waandamizi wa serikali wanaosimamia utekelezaji wa mradi wa kufua umeme katika Mto Rufiji wa Stiegler's Gorge wakisimama kwa dakika kadhaa kuwakumbuka marehemu waliopoteza maisha kwenye ajali ya kivuko cha MV Nyerere huko Ukara wilayani Ukerewe mkoa wa Mwanza Septemba 20, 2018. Hii ilikuwa ni kabla ya kuanza kwa kikao kazi ambapo alipokea taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 24, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na viongozi waandamizi wa serikali wanaosimamia utekelezaji wa mradi wa kufua umeme katika Mto Rufiji wa Stiegler's Gorge pamoja na wataalamu wakati wa kikao kazi ambapo alipokea taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 24, 2018.

  0 0

   Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Diana Masalla akitoa elimu ya Msamaha wa Riba na Adhabu kwenye Malimbikizo ya Madeni ya Kodi wakati wa semina ya wafanyabiashara iliyofanyika leo mkoani Manyara.
   Afisa Maadili Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Adelaida Rweikiza akiwasilisha mada kuhusu Mfumo wa Maadili kwa Watumishi wa TRA wakati wa semina ya wafanyabiashara iliyofanyika leo mkoani Manyara.
   Afisa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Manyara Nicodemus Massawe akijibu baadhi ya maswali ya wafanyabishara wakati wa semina ya wafanyabiashara hao iliyofanyika leo mkoani Manyara.
  Baadhi ya wafanyabiashara wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa mada mbalimbali wakati wa semina ya wafanyabiashara hao iliyofanyika leo mkoani Manyara. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).

  Na Veronica Kazimoto Manyara
  MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa elimu ya Msamaha wa Riba na Adhabu ya Malimbikizo ya Madeni ya Kodi kwa wafanyabiashara, washauri wa wafanyabiashara na wakaguzi wa hesabu mkoani Manyara ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha wale wote wenye madeni ya kodi yanayotokana na riba na adhabu kuomba msamaha kabla ya tarehe 30 Novemba, 2018.

  Akiwasilisha mada kuhusu msamaha huo, Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA Makao Makuu Diana Masalla amesema kuwa, lengo la kutoa elimu hiyo ni kuhakikisha kwamba, kila mfanyabiashara mwenye malimbikizo ya madeni ya kodi anapata taarifa na kufuata taratibu za kuomba msamaha huo.

  "Mpaka sasa TRA imeshatoa elimu hii ya msamaha wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya kodi katika mikoa mingi nchini na lengo letu ni kuwahamasisha wafanyabiashara wote wenye malimbikizo hayo kuomba msamaha ili waweze kupata unafuu na kulipa kodi ya msingi tu isiyo na riba wala adhabu," alisema Masalla.

  Aidha, pamoja na washiriki hao kupewa elimu ya msamaha wa riba na adhabu ya kodi, pia wameelimishwa kuhusu Mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya Mwaka 2018 pamoja na Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma kwa Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania.

  Afisa Maadili Mwandamizi wa mamlaka hiyo Adelaida Rweikiza akizungumza na washiriki hao wakati akiwasilisha mada ya maadili amesema kuwa, ni haki ya wateja wote wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kuhudumiwa vizuri na kwa usawa bila upendeleo.

  "Ninyi wateja wetu mna haki ya kupata huduma bora na pia mnatakiwa kupewa haki sawa bila upendeleo wowote na pale ambapo mtumishi yeyote wa TRA akionyesha dalili zozote za uvunjifu wa maadili ikiwa ni pamoja na vitendo vya rushwa, mnatakiwa kutoa taarifa kwa viongozi wake ili hatua zichukuliwe," alieleza Rweikiza.

  Mamlaka ya Mapato Tanzania imejipanga kuhakikisha kuwa, wafanyabiashara wenye malimbikizo yenye madeni ya kodi wanapata taarifa na kuomba msamaha huo lakini pia wanapata elimu ya mabadiliko ya sheria za kodi pamoja na namna wanavyopaswa kuhudumiwa na watumishi wa TRA.

older | 1 | .... | 1677 | 1678 | (Page 1679) | 1680 | 1681 | .... | 1897 | newer