Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1678 | 1679 | (Page 1680) | 1681 | 1682 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Bw. Paul Mtango ambaye ni Mkulima wa Kijiji cha Mpirani Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro akiwaonyesha Wajumbe wa Bodi ya Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) mfumo alioutumia kupanda Maharage katika shamba lake kwa kutumia Kilimo hifadhi, mfumo unaowafanya wakulima kupata mazao mengi tofauti na walivyokuwa wakilima awali.
  Bw. Paul Mtango ambaye ni Mkulima wa Kijiji cha Mpirani Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Bodi ya Baraza la Kilimo Tanzania waliofika shambani kwake kujionea namna anavyonufaika na mradi wa kilimo hifadhi unaoratibiwa na ACT/TAP ambapo amewaeleza kwa kutumia Kilimo Hifadhi anaweza kupata gunia 12 za maharage kwa heka moja tofauti na awali alipokuwa akipata gunia 3 kwa hekari..
  Bw. Paul Mtango ambaye ni Mkulima wa Kijiji cha Mpirani Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro akisisitiza jambo kwa Wajumbe wa Bodi ya Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) waliofika shambani kwake kujionea namna anavyonufaika na mradi wa kilimo hifadhi unaoratibiwa na ACT/TAP, kuhusu namna kilimo hifadhi kinavyohifadhi ardhi vizuri kwa kizazi kijacho.


  UONGOZI wa Halimashauri ya Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro umeonyesha kuridhishwa kwake na namna Mradi wa Kilimo Hifadhi unaotekelezwa wilayani humo na Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) chini ya Mradi wake wa Ubia wa Kilimo Tanzania ulivyoweza kuwasaidia wakulima kwa kupata mavuno mengi ukilinganisha na hapo awali.

  Kauli hiyo imetolewa Jana na Kaimu Mkurugenzi wa halimashauri hiyo
  John Nnko ,Wakati alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) waliofika wilayani humo kujionea utekelezaji wa Mradi wa kilimo Hifadhi unaotekelezwa na Baraza la Kilimo Tanzania chini ya Mradi wake wa Ubia wa Kilimo Tanzania.

  Alisema kuwa mpaka sasa kumekuwa na mwikitio mkubwa wa wakulima kutaka kujifunza zaidi namna ya kulima kilimo hifadhi hasa katika mazao ya mahindi na maharage ambapo alilishukuru Baraza la Kilimo kwa kutekeleza Mradi huo wilayani Same ambao unawafanya kupata mavuno mengi na kutokuwa na hofu ya ukame.

  “Mpaka sasa Mradi huu wa Kilimo Hifadhi umekwisha kuwafikia zaidi ya wakulima 1,300 na uko katika vijiji tisa pekee, lakini tunaona mwitikio wa wakulima unazidi kuwa mkubwa wa kutaka kujua namna ya kulima kwa kutumia teknolojia hii, kwakweli ACT tunawashukuru sana kwa sababu pia hata watalaamu mmetuletea nyie” Alisema.

  Miongoni mwa vijiji vinavyotekeleza mradi huo wilayani humo ni pamoja na Saweni, Hedaru,Kisiwani, Njiro, Mpirani na Ishinde ambapo wakulima waliueleza ujumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya ACT iliyofika katika mashamba yao kuwa tangu mradi huo wa Kilimo hifadhi ulipoanza mwaka 2011 vipato vyao vimeimarika huku gharama za uandaaji wa mashamba zikipungua.

  “Awali kabla ya mafunzo tulikuwa tunapanda robo heka ya Maharage kwa kutumia kilo 25 za Mbegu, na ukija kuvuna unaambulia debe tatu au nne tu, lakini kwa kutumia kilimo hifadhi robo heka hiyo hiyo tunapanda kwa kutumia kilo sita pekee za mbegu na mavuno yake tunapata gunia tatu hadi nne kwa kweli tunawashukuru sana hawa watu wa ACT kwa kutuletea hiki kilimo hifadhi” Alisema Bi Agnes Tumaini Mkulima wa Kilimo hifadhi kijiji cha Mpirani wilayani Same.

  Wakulima wameieleza bodi hiyo kuwa licha ya mavuno mengi wanayoyapata kwa sasa changamoto kubwa inayowakabili ni uwepo wa bei ndogo ya mazao hasa ya mahindi pamoja na Pembejeo za kilimo na kuomba wadau wa kilimo kujitokeza kuwekeza katika kilimo hicho.

  “Kwa sasa nimeona Kilimo hifadhi kinamaana tulikuwa tunalima kienyeji bila mpangilio lakini baada ya watalamu wa ACT kuja hapa kutuelimisha kuhusu kilimo hiki kwakweli nimenufaika sana, situmii muda mwingi shambani, natumia mbegu kigodo, sina shaka kuhusu ukosefu wa mvua lakini hatimaye kwakutumia kilimo hifadhi Napata mavuno mengi tofauti na wenzangu.”alisema Bw. Paul Mtigi Mkulima wa Kilimo Hifadhi Kata ya Maole Wilayani Same.

  “Pamoja na mafanikio tunayoyapata lakini bado tunakabiliwa na changamoto ya LIPA (Jembe maalum la kulimia kilimo hifadhi) Mkulima anatakiwa alime kibiashara kwa hivyo tunaomba wadau wengine wa kilimo watuwezeshe kupata LIPA kwa sababu ndio pembejeo muhimu inayomrahisishia mkulima hasa kwenye kilimo hifadhi lakini mpaka sasa hakuna na ndio changamoto kubwa katika kilimo hiki cha hifadhi” alisema

  Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa Bodi ya ACT, Bw Enock Ndondole alisema bodi imeridhishwa na namna mradi huo unavyotekelezwa wilayani Same na kuwapongeza wakulima kwa kuitikia kwa wingi teknlojia hiyo ya Kilimo hifadhi.

  “Kikubwa tunachowamba jitahidini kuwafikishia wakulima wenzeni hii teknlojia ili nao wanufaike kama mnavyonufaika ninyi, wakija hapa wakiona mnavyofanya kazi wengi zaidi wataanza kulima kwa teknlojia hii, kwa sababu dhamira yetu ni kuona wakulima wengi wanatumia kilimo hifadhi na kuachana na kilimo cha kizamani na nyie ndio mnanafasi ya kuwaelimisha wakulima ambao bado hawaja anza kutumia teknolojia hii alisema Bw Ndondole.

  Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kilimo Tanzania (ACT) Bi Janeth Bitegeko alisema ACT tangu kaunzishwa kwake imekuwa na mchango mkubwa katika kuinua sekta ya kilimo ambapo alitaja masuala muhimu yaliyoasisiwa na ACT kuwa ni pamoja na uanzishwaji wa Benki ya Kilimo, Program ya Kilimo kwanza na kwamba tayari serikali imekwisha ondoa kodi nyingi ambazo zilikuwa kero kwa mkulima baada ya kazi kubwa iliyofanywa na Baraza la Kilimo Tanzania.


  0 0

  NA DANIEL MBEGA, KISARAWE

  KUWEKWA kwa jiwe la msingi la kiwanda kidogo cha kuchakata zao la muhogo katika Kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe kumetoa fursa kubwa kwa kikundi cha akinamama wanaojihusisha na kilimo cha zao hilo pamoja na wananchi wengine.

  Kiongozi wa Kikundi cha akinamama cha Kitanga Green Voices, Mama Abia Magembe, anasema uwekaji wa jiwe hilo la msingi uliofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jumamosi, Septemba 15, 2018 umefufua matumaini si ya akinamama pekee, bali hata wananchi wengine ambao walikuwa wamekata tamaa ya kulima muhogo kutokana na kutokuwepo kwa soko la uhakika.

  “Matumaini sasa yapo ingawa bado tunayo safari ndefu ya kufikia malengo, tunataka kuchakata na hatimaye kutengeneza bidhaa mbalimbali zaidi ya 300 kwa kutumia zao la muhogo,” anasema Mama Magembe, Ofisa Kilimo mstaafu ambaye amefufua upya matumaini ya wakulima wa eneo hilo.

  Tayari amekwishawafundisha akinamama zaidi ya 60 kijijini hapo ambao wanaweza kutengeneza bidhaa mbalimbali zinazotokana na zao la muhogo na anaendelea kuwafundisha wengine, kwani anasema, mahali kilipo kiwanda hicho patakuwa kituo cha kudumu cha mafunzo kwa wote, wanaume kwa wanawake.

  Wakati wa uzinduzi huo, DC Mwegelo aliahidi kuwasaidia akinamama hao pamoja na wakulima wengine kukuza zao la muhogo, ambalo alisema ni miongoni mwa mazao mawili ya kipaumbele wilayani humo, likiwemo zao la korosho.

  Alisema atawasaidia akinamama hao kuwaunganisha na wadau mbalimbali ili kupata mikopo nafuu, ikiwemo mikopo isiyo na riba huku pia akiahidi kwamba, changamoto ya umeme na maji zitatatuliwa haraka.

  Pengine unafahamu faida tatu au nne tu za muhogo ambazo ni kuutafuna mbichi, kuuchemsha au kuuchoma; unga wake kwa ajili ya lishe, majani yake kama mboga ya kisamvu na dawa pamoja na miti yake inapokauka kutumika kama kuni.

  Inawezekana hujui kama maganda ya mihogo baada ya kumenywa ni chakula bora cha mifugo yakikaushwa au mabichi.Siyo ajabu pia hujui kwamba muhogo ukitwangwa mbichi na kuchujwa, maji yake yake yanatoa wanga (starch) ambao hutumika kutengeneza dawa za madoa, gundi katika samani, rangi za awali za ukuta na sukari (sugar syrup) na pia ni lishe nzuri.

  Lakini zao la muhogo ni zaidi ya linavyofikiriwa kwa sababu licha ya faida hizo chache, lakini pia linazalisha bidhaa zaidi ya 300 kama ambavyo akinamama wa Kijiji cha Kitanga, Kata ya Msimbu wilayani Kisarawe wameamua kufanya.

  Akinamama hao kupitia kikundi chao cha Kitanga Green Voices mbali ya kuzalisha unga pamoja na chips, sasa wanatengeneza bidhaa lukuki zenye ubora kama chapatti, maandazi, skonzi, biskuti, tambi, cassava chop, na nyinginezo nyingi.

  Hatua hiyo imekuja baada ya kupatiwa mafunzo kupitia mradi wa Green Voices unaofadhiliwa na taasisi ya maendeleo ya wanawake wa Afrika inayojulikana kama Women of Africa Foundation, ambayo iko chini ya Makamu wa Rais mstaafu wa Hispania, María Teresa Fernández de la Vega.

  Kuanzishwa kwa mradi huo wa kusindika muhogo pamoja na bidhaa zake kumeliokoa zao hilo ambalo licha ya kuwa na manufaa makubwa kwa jamii, lakini limekuwa likidorora hata katika soko la vyakula.

  “Tangu tumeanzisha kikundi hiki miezi mitatu iliyopita hivi sasa muhogo hauwezi kuozea shambani na wananchi wanaona umuhimu wa zao hilo,” anasema Mama Magembe, ambaye ni mratibu wa mradi huo.

  Mama Magembe, ambaye yeyé pamoja na akinamama wengine tisa walipatiwa mafunzo nchini Hispania kwa nia ya kuanzisha shughuli za ujasiriamali unaoendana na utunzaji wa mazingira pamoja na kupambana na mabadiliko ya tabianchi, anasema kwamba zao la muhogo sasa limepata thamani kubwa kijijini hapo na wana uhakika wakulima wa wilaya ya Kisarawe wanaweza kugeukia miradi kama hiyo ili kuongeza mnyororo wa thamani.

  Akinamama 10 wanaofanya miradi mbalimbali ya ujasirimali kutpia mradi wa Green Voices wanatoka mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Kigoma, Kilimanjaro, Pwani na Mwanza.Silvera Mujuni, Ofisa Chakula na Lishe wa Wilaya ya Kisarawe, anasema kwamba wilaya hiyo ina fursa kubwa ya kusindika na kuchakata mazao mengi yatokanayo na muhogo kwa kuwa zao hilo ndilo kuu kwa chakula na biashara.

  Anasema kwamba, ardhi katika vijijini vingi vya wilaya hiyo inastawisha muhogo kwa wingi, hivyo ikiwa wananchi watajizatiti na kujifunza namna ya kuchakata bidhaa za muhogo wanaweza kupata faida kubwa kiuchumi.

  “Muhogo ndilo zao kuu katika maeneo mengi ya wilaya hii ambayo haiwezi kustawisha mazao mengine kama mahindi, hivyo ni vyema wananchi wakajifunza utengenezaji wa bidhaa mbalimbali zinazotokana na zao hilo,” anasema Bi. Silvera aliyemwakilisha mkurugenzi wa wilaya hiyo na ambaye ndiye alikuwa akiwafundisha akinamama hao namna ya kutengeneza bidhaa mbalimbali.

  Awali Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Wazir Yakoub Wazir, aliwataka akinamama hao wajipange wasajiliwe rasmi ili waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na serikali na taasisi nyingine za binafsi.

  “Ofisi yangu iko wazi wakati wote, mkitaka kwenda kusajiliwa wilayani hata leo niko tayari kuwasaidia, nawaombeni mje niwasaidie hata namna ya kuandaa katiba ya kikundi pamoja na taratibu nyingine,” alisema.

  Naye Diwani wa Kata ya Msimbu, Anna Lilomo, amesema atajitahidi – kwa kushirikiana na diwani mwenzake wa viti maalum Mossy Sultan Kufurumbaya – kuwapigania akinamama hao kwenye vikao vya Baraza la Madiwani ili waweze kupatiwa misaada na mikopo hata kupitia katika asilimia 10 ya bajeti ya halmashauri ambayo hulenga kuwasaidia wanawake na vijana.

  “Bahati nzuri sisi hapa ni madiwani wanawake, kwa hiyo tutalipeleka suala la akinamama hawa kwenye Baraza la Madiwani na kuelezea umuhimu wa kuongeza thamani kwenye zao letu la muhogo ili limkomboe mkulima,” alisema Diwani Lilomo.

  Mratibu wa Mradi wa Green Voices nchini Tanzania, Bi. Secelela Balisidya, anasema kwamba anafarijika anapoona wanawake wakihamasika kushiriki shughuli za maendeleo, hasa ujasiriamali unaolenga kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.

  “Suala la kuhakikisha usalama wa chakula, kutokomeza umaskini, kuwawezesha wanawake kiuchumi na mapambano dhidi ya tabianchi ni mambo yaliyopewa kipaumbele katika Malengo Endelevu ya Dunia, hivyo wanawake wanaotekeleza miradi ya Green Voices wanayatekeleza malengo hayo kwa wakati mmoja,” anasema Secelela.


  Zao lililotelekezwa, sasa mkombozi

  Muhogo ni zao linalochukuliwa na wengi kama la ziada hasa kwenye ukame, lakini wengi hulifanya kama mlo wa hamu bila kutambua kwamba zao hilo lina manufaa makubwa kwa lishe na kibiashara.Wengi wanauchukulia muhogo kama chakula cha maskini, hawa wale wanaojitiahidi kulima zao hilo, huyapa kipaumbele mazao mengine kuliko muhogo.

  Lakini muhogo ni zao mojawapo ambalo linaweza kuiepusha jamii na baa la njaa huku katika baadhi ya mataifa likitumika kama chanzo cha nishati ili kukabiliana na bei ya mafuta na nishati nyinginezo.Baa la njaa ni tatizo kubwa linalozikumba nchi nyingi barani Afrika, Tanzania ikiwa miongoni mwazo, lakini licha ya watu kuhimizwa kulima muhogo, bado wanalipuuza zao hilo na kuliona kama zao fulani la mizizi tu.

  Katika mikoa kama Lindi na Mtwara ambayo kwa miaka mingi inalima kwa wingi muhogo, chakula chao kikuu kilikuwa ugali wa muhogo.Licha ya kudharauliwa kwa zao hilo, lakini siyo ajabu ukakuta mlo wa siku hiyo umetokana na muhogo kasoro chumvi na nazi, kwani inawezekana kuni zilizopikia ni matawi ya muhogo, ugali wa muhogo na kisamvu cha muhogo!

  Na wakulima wengi katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara wanakula ugali wa muhogo pale wanapokoa unga wa mahindi, ambapo wanaokula ugali huo wa muhogo (Wazaramo wanasema ‘bada’ na Wamakua wanauita ‘matamba’) huonekana maskini wa kutupa.

  Leo hii wanapohamasishwa kulima muhogo kwa sababu ya kustahimili ukame, bado wengi wanasuasua, lakini watakapoambiwa kwamba unga wa muhogo unatoa bidhaa nyingi zenye faida kubwa, huenda wengi wakaligeukia zao hilo na kulima kibiashara.

  Inafurahisha sana siku hizi kuona watu wengi wakikimbilia ugali wa muhogo hata hotelini, lakini hiyo bado haijatosha kulirasimisha zao hilo ili liwe na tija kubwa.

  Akinamama wa Kijiji cha Kitanga wanaweza kuwa mabalozi wazuri wa zao hilo, kwa sababu tayari wameanza kutengeneza bidhaa mbalimbali ambazo hata wananchi wa kijiji hicho wameshangazwa nazo baada ya kuzionja na kuona ubora wake.

  Kilimo cha muhogo siyo tu kitasaidia kukuza pato la mkulima, lakini kinaweza pia kuokoa mazingira pamoja na kuisaidia Tanzania kuokoa karibu Dola za Marekani 20 milioni sawa na Shs. 42 bilioni zinazotumika kuagiza chakula nje, jukumu ambalo kikundi cha Kitanga Green Voices kimeamua kulibeba. 

  Faida za muhogo ni nyingine kama zilivyoelezwa hapo juu, lakini kwa msisitizo ni kwamba, unga wake hutumika kutengeneza vyakula mbalimbali, baadhi ni uji na ugali, vitafunwa kama keki, mikate, skonzi, biskuiti, mandazi, mafuta ya lishe, sabuni ya unga, kuni, mboga, huksi pamoja na bidhaa nyingine nyingi.

  Mazao yanayopatikana katika mzizi wenyewe, miti na majani huweza kuzalisha bidhaa anuwai za viwandani kama vifaa vya nguo, karatasi, mafuta, kilevi, dawa za binadamu na plastiki wakati ambapo wanga (starch) hutumika kutengeneza dawa za madoa, gundi katika samani, rangi za awali za ukuta na sukari (sugar syrup). 

  Takwimu za kilimo cha muhogo duniani zinaonyesha kuwa, Afrika ni bara la tatu duniani kwa kuzalisha zaidi muhogo ambapo huzalishaji takriban tani milioni 102.6 kila mwaka.

  Tanzania ni nchi ya nne kati ya wazalishaji wakubwa wa muhogo barani Afrika baada ya Nigeria, Ghana na Kongo DRC ambapo inaelezwa kwamba karibu ekari 670,000 za ardhi ya kilimo zinatumika kuzalisha muhogo, zao linalochangia karibu asilimia 15 za chakula kwa nchi nzima ambapo karibu kaya 1,213,958 huzalisha muhogo nchini.

  Mikoa inayozalisha muhogo kwa wingi ni Mwanza, Mtwara, Lindi, Shinyanga, Tanga, Ruvuma, Mara, Kigoma, Pwani na maeneo yote ya Zanzibar. Ukanda wa Ziwa ni wazalishaji wakubwa zaidi ikifuatiwa na ukanda wa kusini. Mkoa wa Ruvuma huzalisha kati ya 5-10% ya uzalishaji wote Tanzania. 

  Muhogo ndilo zao la pili kwa kuchangia pato la taifa kwa asilimia 19 baada ya mahindi. Taarifa ya Shirika la Utafiti wa Viwanda na Maendeleo ya Mazao ya Chakula Tanzania (TIRDO) inaonyesha kuwa zao la muhogo linastawi kirahisi.Hii ni pamoja na kuvumilia ukame na halishambuliwi na magonjwa au wadudu wanaoathiri mazao mengine na pia muhogo unaweza kutoa mazao mengi katika ardhi duni ambayo mazao kama mahindi hayawezi kustawi.

  Kwa mujibu wa TIRDO, muhogo ni zao la pili kuwa na wanga mwingi baada ya viazi vitamu ambavyo vina asilimia 20 hadi 30 ya wanga na kwamba asilimia 84 ya zao hilo hutumika kama chakula cha binadamu.

  Kiongozi wa Kikundi cha akinamama cha Kitanga Green Voices, Mama Abia Magembe, akitoa maelezo ya utengenezaji wa bidhaa mbalimbali zinazotokana na zao la muhogo kwa wageni mbalimbali, akiwemo mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, na Balozi Getrude Mongella.

  0 0

  Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na wakulima wa zao la Mkonge kwenye Shamba la Mgombezi lililopo katika Kijiji na kata ya Mgombezi katika Wilaya ya Korogwe wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga jana tarehe 24 Septemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK, Tanga)
  Kikao kazi wakulima wa zao la Mkonge na Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba kilichofanyika katika kijiji na kata ya Makuyuni Wilaya ya Korogwe  wakati wa ziara ya waziri huyo ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga, jana tarehe 24 Septemba 2018. 
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martin Shigela akitoa maelezo mafupi Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba kuhusu zao la Mkonge mkoani humo mbele ya wakulima wakulima katika kijiji na kata ya Makuyuni, Wilayani Korogwe jana tarehe 24 Septemba 2018. 
  Wakulima wa zao la Mkonge kwenye Shamba la Mgombezi lililopo katika Kijiji na kata ya Mgombezi wilaya ya Korogwe wakifatilia kwa makini mkutano wa Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba wakati wa mkutano wa pamoja kujadili zao la Mkonge Mkoani Tanga jana tarehe 24 Septemba 2018. 
  Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na wakulima wa zao la Mkonge kwenye Shamba la Mgombezi lililopo katika Kijiji na kata ya Mgombezi wilaya ya Korogwe wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tanga jana tarehe 24 Septemba 2018. 


  Na Mathias Canal-WK, Tanga

  Wakulima wadogo wa zao la mkonge Wilayani Korogwe mkoa wa Tanga, wameiomba Serikali kuweka utaratibu wa kuanzisha soko huria kwa ajili ya ununuzi wa zao hilo ili malengo yaliyowekwa na serikali ya kuzalisha tani 100,000 kwa mwaka yafikiwe.

  Wakulima hao wameilalamikia Kampuni ya Katani Ltd. kwamba inachukuwa asilimia 54 na kumuachia mkulima asilimia 46 jambo walilodai ni unyonyaji unaofanywa na kampuni hiyo kinyume na utaratibu wa kiutendaji.

  Wakulima hao wametoa malalamiko yao mbele ya waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba wakati akizungumza na wananchi katika maeneo tofauti wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili kutekeleza maagizo aliyopewa hivi karibuni na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa ya kutembelea mashamba ya Mkonge mkoani humo na kutatua changamoto zinazowakabili wakulima.

  Katika mkutano huo pia wakulima hao walijadili suala la bei na namna ambavyo sera iliyowekwa na serikali inayoelekeza kuwa kila mwaka mkonge uzalishwe tani 100,000 na kwamba sera hiyo haisimamiwi ipasavyo kwani endapo kama ikisimamiwa ipasavyo zao hilo litaingia kwenye zao kuu la kibiashara nchini.

  Akizungumza katika mikutano hiyo Waziri wa Kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba alisema kuwa Tanzania ilikuwa ndiyo nchi pekee barani Afrika kupokea zao la mkonge kutoka Jimbo la Yucatan, nchini Mexico mwaka 1893. Mkoa wa Tanga ndio ulikuwa kinara wa kulima zao hilo kwa wingi kwa kuwa na mashamba makubwa ikifuatiwa na Morogoro.
  Hadi kufikia mwaka 1964, uzalishaji wa mkonge nchini ulikuwa ni tani 235,000 kwa mwaka, hivyo kuifanya Tanzania kuwa ndiyo nchi pekee iliyokuwa ikifanya vizuri katika zao la mkonge barani Afrika.
  Aliongeza kuwa Kutokana hali hiyo, sekta ya kilimo hicho ndiyo sekta ambayo ilikuwa imeajiri watu wengi hususani katika maeneo ya mashambani. Hivyo Mkoa wa Tanga ulikuwa na maendeleo makubwa ya kiuchumi kutokana na faida ya uwapo wa zao hilo ukitoa viwanda vilivyokuwepo enzi hizo.
  Licha ya zao hilo kuwa na manufaa ya kiuchumi, ni bidhaa ya nyuzi pekee ndiyo ilikuwa ikisafirishwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kuuzwa katika masoko ya dunia. Hata hivyo, ujio wa kamba mbadala za nailoni katika miaka ya 1970 uliweza kuua soko la mkonge kwa kiasi kikubwa hali iliyolazimu kushusha uzalishaji na kufikia tani 32,000 pekee kwa mwaka.
  Dkt Tizeba alisisitiza kuwa zao la Mkonge ni miongoni mwa mazao muhimu ya kibiashara hivyo serikali inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli imejidhatiti kuhakikisha zao hilo linaendelea kukua na kuongeza uzalishaji maradufu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanufaikaji wakubwa ni wakulima na sio vinginevyo.

  Akijibu malalamiko ya wananchi ambao ni wakulima wa mkonge katika Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Dkt Tizeba alisema kuwa serikali haiwezi kuchukua hatua za haraka katika kutatua mgogoro huo badala yake inaendelea kujiridhisha ili kubaini ukweli kuhusu uendeshaji wa zao hilo kupitia kampuni ya Katani LTD na ndani ya wiki mbili itatoa maelekezo ya serikali.

  Dkt Tizeba ameitaka kampuni ya Katani LTD pamoja na wakulima wa katani kutunza kumbukumbu zao zote ili ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) itakapoanza kazi ya ukaguzi iweze kupata taarifa za uhakika.

  0 0

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
  MKUU wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi amewataka Madaktari wanaopatiwa mafunzo ya jinsi ya kufanya tathmini kwa mfanyakazi aliyeumia au kuugua mahala pa kazi, kutenda kazi kwa weledi na kwa haraka ili kuharakisha utoaji wa fidia.
  Mkuu wa Mkoa alitoa rai hiyo leo Septemba 24, 2018 wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa madakatari na watoa huduma za afya kutoka mikoa ya Singida, Dodoma, Kigoma na Tabora kwenye chuo cha Uhasibu Singida.
  “Katika kutoa fidia kwa mfanyakazi aliyepata madhara mahala pa kazi hakuna njoo kesho….njoo kesho, bali ni kumhudumia Mfanyakazi huyo kwa haraka ili aweze kupata fidia yake kutokana na madhara aliyoyapata kwa wakati na ninyi madaktari ndio wenye jukumu kubwa la kuhakikisha mnafanya kazi kwa weledi na kwa haraka.” Alisema.
  Dkt. Nchimbi alisema, katika suala la utoaji fidia, Madaktari ni sawa na mahakimu, na wanayo dhamana kubwa sana kwani mapendekezo yao ndiyo yatatoa muongozo kwa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, kuamua ni kiwango gani ambacho muathirika anapaswa kufidiwa au kutofidiwa kabisa.
  “Kwa nafasi yenu Madaktari na kwa taaluma yenu mnafahamu sana namna ya kuwahudumia wahitaji wenu, lakini vile vile mnavyofanya katika tiba nyingine, huwezi kumtibu au kuwa na uhakika ni tiba ya namna gani mgonjwa anapaswa kupewa mpaka uwe na uelewa sahihi na ndio maana leo mko hapa ili muwe na uelewa sahihi, mtakapotoka hapa hatutarajii mseme sijui, sina uhakika, hayo siyo maneno ambayo tunataka yatoke kwenye vichwa vyenu baada ya mafunzo haya.
  Alisema ni jambo zuri kwa madaktari wote baada ya kupatiwa mafunzo wawe na uelewa sahihi na wa namna moja, ili wote wakibadilishana uzoefu au taarifa, wakute kwamba wote wanapata huduma ambayo ina uelewa mmojana hayatakuwa maamuzi ya utashi binafsi wa daktari bali yawe maamuzi ya kitaalamu nay a haki.
  Akizungumza wakati wa ukaribisho, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi WCF, Masha Mshomba alisema, mafunzo haya ya madaktari ni muendelezo wa mpango wa Mfuko kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali kuhusu shughuli za Mfuko na miongoni mwa wadau wakubwa wa Mfuko ni Madaktari.
  “Jukumu kuu la Mfuko ni kupokea madai na kulipa mafao ya Fidia na hadi sasa tuna mwaka wa pili tukitekeleza jukumu hilo la msingi na nikuhakikishie kwamba tumekuwa tukilitekeleza na limeleta tofauti sana kati ya hali iliyokuwepo kabla ya kuanzishwa kwa Mfuko kwa maana ya malipo ya fidia yameongezeka sana na katika miaka miwili tu hii malipo ya fidia kwa wafanyakazi yamefikia shilingi Bilioni 4.5.” Alisema Bw. Mshomba.
  Alisema, mafunzo haya yanalengo la kujenga uwezo kwa madaktari katika kufanya tathmini ya Mfanyakazi aliyeumia au kuugua mahala pa kazi ili hatimaye Mfanyakazi aweze kulipwa fidia stahiki.
  Naye Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Raskazi Muragila, alisema Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi una muda mfupi sana, umeanzishwa mwaka 2015 na utendaji rasmi umeanza mwaka 2016 kwa hivyo una miaka miwili tu hadi sasa, na ni wazi kwamba katika kipindi hiki kifupi, wafanyakazi wengi bado hawana uelewa kuhusu Mfuko huu, lakini pia wale wanaofanya tathmini (Madaktari) nao pia hawana uelewa wa kutosha kuhusu namna wanavyoweza kutimiza wajibu wao katika suala zima la ulipaji fidia.
  “Naupongeza Mfuko kwa hatua iliyochukua ya kuendelea kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali na ningeuomba Mfuko uwatembelee pia wafanyakazi wenyewe na waajiri ili wote wawe na uelewa wa pamoja.” Alisema.
  Mafunzo hayo yanaendeshwa na wataalamu mkutoka Taasisi ya Tiba Moi na Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi, yatahusu Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi na shughuli za Mfuko kwa ujumla, mchakato wa kupokea madai ya fidia, jinsi ya kufanya tathmini ya Mfanyakazi aliyeumia au kuugua kutokana na kazi.

  Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi, (aliyesimama), akitoa hotuba wakati akifungua mafunzo ya siku tano ya madaktari kutoka mikoa ya Singida, Dodoma, Tabora na Kigoma kuhusu namna ya kufanya tathmini ya Mfanyakazi aliyeumia au kuugua mahala pa kazi. Mafunzo hayo yameandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF). Wengine pichani kutoka kulia ni Daktari bingwa na mbobezi wa magonjwa ya mifupi kutoak MOI, Dkt. Robert Mhina, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskazi Muragila, na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini WCF, Dkt. Abdulsalaam Omary.
  Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akitoa neon la ukaribisho kwenye mafunzo hayo.


   Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi, (kushoto), akipeana mikono na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, wakati wa mapunziko ya mafunzo hayo. Kulia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya mifupa, na kionbgozi w atimu ya wataalamu wa kutoa mafunzo hayo, Dkt. Robert Mhina.
   Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo.
   
    Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo.
   Mkuu wa kitengo cha huduma za kisheria WCF, Bw. Abraham Siyovelwa akitoa mada kuhusu Sheria ya Fidia 
  Dkt. Abdulsalaam Omary, Mkurugenzi wa Huduma za tiba na tathmini WCF akitoa mada kuhusu mchakato wa madai ya Fidia na jinsi ya kiutoa tathmini kwa mfanyakazi aliyeumia, kuugua au hata kufariki mahala pa kazi.
  Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter akitoa mada kuhusu shughuli za Mfuko.
  Meneja Madai na Tathmini WCF, Dkt. Ali Mtulia, (kushoto), akizungumza mwanzoni mwa mafunzo hayo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasikliano na Uhusioano WCF, Bi. Laura Kunenge.
  Dkt. Pascal Magessa kutoka Idara ya Madai na Tathmini WCF, akizungumza na mmoja wa washiriki.

   Watoa mada wakiongozwa na Dkt. Robert Mhina (kulia)
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasikliano na Uhusioano WCF, Bi. Laura Kunenge, akiongoza taratibu za mafunzo hayo.

   Mgeni rasmi na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na madaktari kutoka Kigoma.
    Mgeni rasmi na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na madaktari kutoka Dodoma.
    Mgeni rasmi na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na madaktari kutoka Tabora
    Mgeni rasmi na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na madaktari kutoka Singida.  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, akizindua jiwe la msingi la kiwanda kidogo cha kuchakata zao la muhogo katika Kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe.


  NA DANIEL MBEGA, KISARAWE


  MKUU wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, amepongeza jitihada za akinamama katika kubuni miradi ya maendeleo na kuongeza kuwa Serikali iko tayari kuunga mkono jitihada zao, na hasa katika miradi ya kilimo ambayo inaleta uhakika wa chakula.

  DC Mwegelo amesema hayo leo, Jumamosi, Septemba 15, 2018 wakati akiweka jiwe la msingi la kiwanda kidogo cha kuchakata muhogo katika Kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe, ambacho kinamilikiwa na akinamama wapatao 30 wanaoongozwa na Ofisa Kilimo mstaafu, mama Abia Magembe.

  Mkuu huyo wa wilaya aliweka jiwe hilo la msingi kwa niaba ya Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, ambaye pia ni Mbunge wa Kisarawe.Alisema anapongeza jitihada kubwa zilizofanywa na akinamama hao siyo tu katika kubuni miradi ya maendeleo, bali pamoja na kuwasaidia wengine na kusema kwamba, kiwanda hicho ni cha mfano ambapo kinakwenda sanjari na kauli mbiu ya Serikali ya kuifanya Tanzania ya Viwanda.

  “Nawapongeza sana akinamama, pamoja na kiongozi wenu Mama Magembe, hakika hizi ni jitihada zinazotakiwa kuungwa mkono na serikali yangu itafanya kila njia kuona kwamba mnasimama,” alisema.
  Aliwapongeza pia wafadhili wa Mradi wa Green Voices waliotoa mafunzo kwa akinamama 15 huko Hispania, ambapo akinamama 10 kati yao, akiwemo Mama Magembe, walianzisha miradi ya aina hiyo baada ya kurejea nchini huku wakiwafundisha akinamama wengine.

  Mradi wa Green Voices, ambao unalenga kupambana na mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa mazingira pamoja na kujikita katika uhakika wa chakula unafadhiliwa na taasisi ya Women for Africa Foundation inayoongozwa na Makamu wa Rais mstaafu wa Hispania, Maria Thereza de la Vega, ambapo kwa Tanzania akinamama 10 wanaendesha miradi mbalimbali katika mikoa sita.

  Miradi mingine ni utengenezaji wa majiko banifu, ufugaji wa nyuki, kilimo cha uyoga, kilimo nyumba (green house) cha mboga mboga, ukaushaji wa matunda na mbogamboga kwa kutumia umeme-jua, kilimo cha matunda, kilimo cha viazi lishe pamoja na utengenezaji wa majiko ya umeme-jua.Miradi hiyo iko katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Kilimanjaro, Morogoro, Kigoma na Mwanza.

  DC Mwegelo aliahidi kuwaunganisha akinamama wa kikundi hicho cha Kitanga Green Voices na taasisi mbalimbali za fedha ili kupatiwa mikopo isiyo na riba au yenye masharti nafuu, ambapo alisema tayari kikundi kimojawapo kilichopatiwa mafunzo na Mama Magembe tayari kilikwishapokea kiasi cha shilingi milioni moja kutoka Halmashauri ya Wilaya.

  Alisema, wilaya yake ina mpango wa kuanzisha kiwanda cha kuchakata muhogo ili kutengeneza wanga (starch), lakini kwa kuanzishwa kwa kiwanda hicho cha akinamama, anaamini kinaweza kuwa cha mfano katika kutekeleza maazimio hayo ya serikali.“Tumepanga kuanzisha kiwanda cha kuchakata muhogo ili kutengeneza wanga, lakini kwa kuwa kiwanda hiki kipo, nadhani ni mwanzo mzuri wa kuona kwamba tunaweza kuongeza nguvu ili azma yetu itimie maana wilaya hii inaongoza kwa kuwa na mihogo mingi,” alisema.

  Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya, Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Mtera Mwampamba, alisema kwamba muhogo na korosho ni mazao ya kipaumbele katika wilaya hiyo na kwamba ujio wa kiwanda hicho unaakisi malengo yao.Awali, Mratibu wa Kikundi hicho, Mama Magembe, alisema kwamba, fedha walizopewa na wafadhili zilikuwa takriban shilingi milioni 12 ambazo walizitumia kununulia mashine na kujenga jengo moja, na familia yake binafsi iliamua kuchangia shilingi milioni nane ambazo zimejenga jengo la pili pamoja na kununulia matanki mawili ya kuvuna maji ya mvua.

  Hata hivyo, jengo hilo la pili bado halijakamilika ambapo aliomba serikali iangalie uwezekano wa kuwasaidia ikiwa ni pamoja na kusaidia kupatiwa mashine kubwa za kisasa pamoja na umeme.“Mbali ya changamoto ya vitendea kazi na majengo, lakini pia kuna changamoto ya umeme ambapo tunatumia mashine zinazotumia nguvu kazi za watu, jambo linalokwamisha uzalishaji wake. Tungekuwa na umeme tunaamini kwamba tungeweza kuzalisha tani nyingi za unga wa muhogo, lakini pia tukipata mashine kubwa tunaweza kuchakata muhogo na kuusaga na shughuli nyingine zote zikaishia hapa hapa kuliko ilivyo sasa ambapo tunalazimika kubeba chenga na kwenda kusaga mjini,” alisema.

  Aliitaja changamoto nyingine kuwa ni ukosefu wa maji safi na salama, hali inayokwamisha shughuli nyingi.
  Hata hivyo, DC Mwegelo alisema kwamba, mpango wa kupeleka umeme kwenye kijiji hicho upo katika awamu ya tatu ya Umeme wa REA, lakini akaahidi kufuatilia ili kuona uwezekano wa awamu hiyo kuanzia kijijini hapo ili kusukuma mbele maendeleo.

  Kuhusu suala la maji, alisema, hivi sasa kuna mpango wa kuleta maji wilayani Kisarawe kutoka Ruvu, lakini akasema, kwa kuwa maji yatakayozalishwa kila siku kutakuwa na ziada za lita takriban 2000, wataangalia uwezekano wa kusambaza majji hayo katika vijiji vingine kikiwemo Kijiji cha Kitanga.

  Kuhusu changamoto ya masoko, DC Mwegelo aliahidi kushirikiana na akinamama hao na wadau wengine na kuhimiza kwamba, uzalishaji wa bidhaa zitokanazo na muhogo ndio utakaotoa fursa ya kupatikana kwa masoko mengi.DC Mwegelo alishuhudia bidhaa mbalimbali kama keki, maandazi, tambi, vitumbua, biskuti na chapatti ambazo zimetengenezwa kwa kutumia unga wa muhogo huku akisema kwamba, kilimo hicho kikiendelezwa siyo kitakuwa na tija kibiashara tu, bali kitakuwa na uhakika wa chakula.

  Mratibu wa Mradi wa Green Voices nchini Tanzania, Secelela Balisidya, aliwashukuru wafadhili wa mradi huo na kuwapongeza akinamama wote ambao walipata mafunzo na kuja kuanzisha miradi.Alisema kwamba, akinamama hao wameweza kuwapatia mafunzo wanawake wenzao zaidi ya 600 ambao wako katika vikundi mbalimbali na kwamba miradi mingi imeonyesha mafanikio makubwa.

  Naye Balozi Getrude Mongella, ambaye ni Mjumbe wa Bosi ya taasisi ya Women of Africa Foundation, aliwataka wanawake kote nchini kubuni miradi endelevu na kuwahimiza wanaume kuwaunga mkono akinamama ili miradi hiyo iweze kufanikiwa.Kwa upande wake, mwakilishi wa taasisi ya Women for Africa Foundation, Alicia Cedaba, alisema kwamba wamefurahishwa na mafanikio katika miradi mingi iliyoanzishwa na akinamama chini ya ufadhili wao na kwamba wataangalia uwezekano wa kuendelea kufadhili.


  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, mara baada ya kuzindua jiwe la msingi la kiwanda kidogo cha kuchakata zao la muhogo katika Kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe kwa niaba ya Waziri wa Ofisi ya Rais (Tamisemi), Selemani Jafo, ambaye pia ni Mbunge wa Kisarawe. Kushoto ni Kiongozi wa Kikundi cha akinamama wa Kitanga Green Voices, Abia Magembe na kulia ni Balozi Getrude Mongella.
  Kiongozi wa Kikundi cha akinamama wa Kitanga Green Voices, Abia Magembe, akimwelekeza jambo Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, na Balozi Getrude Mongella mara baada ya mkuu huyo wa wilaya kuweka jiwe la msingi la kiwanda kidogo cha kuchakata zao la muhogo katika Kijiji cha Kitanga wilayani humo.
  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo, na Balozi Getrude Mongella, wakisikiliza maelezo kutoka kwa Kiongozi wa Kikundi cha akinamama wa Kitanga Green Voices, Abia Magembe, kuhusu namna muhogo unavyochakatwa.

  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, akiangalia unga wa muhogo uliofungashwa huku akipata maelezo kutoka kwa Kiongozi wa Kikundi cha akinamama wa Kitanga Green Voices, Abia Magembe.
  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, akiangalia baadhi ya wanakikundi cha Kitanga Green Voices wakiweka mihogo kwenye mashine tayari kwa kuichakata ili kupata chenga pamoja na wanga.

  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, akiangalia bidhaa mbalimbali zinazozalishwa kutokana na unga wa muhogo huku akipata maelezo kutoka kwa Kiongozi wa Kikundi cha akinamama wa Kitanga Green Voices, Abia Magembe.
  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, pia alipanda mti wa matunda katika eneo la kiwanda hicho kidogo kwenye Kijiji cha Kitanga wilayani Kisarawe.
  Mratibu wa Mradi wa Green Voices kutoka taasisi ya Women for Africa Foundation, Alicia Cedaba, akiwa na Mama Abia Magembe, Kiongozi wa Kikundi cha akinamama wa Kitanga Green Voices.

  0 0

  Wateja wa Jumia kulipia bidhaa kwa Masterpass
  Kurudishiwa 10% ya kiasi cha pesa watakacholipia bidhaa walizoziagiza.
  Ni salama, rahisi na salama zaidi ambapo wateja hawatakiwi kulipia kwa pesa taslimu.

   Katika jitihada za kurahisisha huduma za manunuzi ya bidhaa kwa njia ya mtandao nchini, Jumia imewawezesha wateja wake kulipia bidhaa zozote watakazonunua kwenye mtandao wake kwa kutumia huduma ya Masterpass.
  Maboresho haya ya kufanya malipo yamekuja ikiwa ni njia ya kuwarahisishia wateja kuwa na machaguo salama, rahisi na haraka zaidi kulipia bidhaa zao. Lengo la Jumia ni kuhakikisha Watanzania wanafanya huduma zao kwa kidigitali ili kurahisisha maisha yao ya kila siku. Na huduma ya Masterpass ambayo haimuhitaji mteja kubeba kiwango cha fedha ni suluhisho tosha kwa nyakati hizi za maendeleo ya sekta ya fedha kidigitali.

  Akizungumzia juu ya huduma hii mpya ya njia ya malipo ambayo imetambulishwa na Jumia, Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Bw. Albany James amebainisha kuwa, “huu ni mwendelezo wa Jumia katika kuhakikisha kuwa Watanzania wanaweza kufanya manunuzi kwa usalama na urahisi mahali popote walipo. Kabla ya kuja na njia hii mpya ya malipo kwa kutumia huduma ya Masterpass, wateja wanalipia kwa Tigo Pesa au pesa taslimu. Tunaamini njia hii imekuja kufanya mapinduzi kwa wateja ambao wanakwenda na wakati kwa kuhifadhi fedha zao kidigitali.”

  “Sio kila mtu anapenda kutembea na pesa taslimu siku za hivi karibuni. Ukiachana na sababu za kiusalama kwa wateja kutembea na kiwango kikubwa au kwa wafanyakazi wetu ambao hupokea malipo hayo kwa niaba ya kampuni, lakini njia hii mpya hurahisisha mchakato mzima. Hii ina maana kwamba badala ya mteja kutoa pesa, mteja atatumia simu yake ya mkononi kufanya malipo kwa ‘QR Code’ ya Jumia ndani ya muda mfupi tu!” alifafanua zaidi Bw. James.

  Huduma hii mpya ya njia ya malipo imekuja wakati ambapo Jumia inaendesha kampeni ya ‘Electroshock.’ Kampeni hii ni ya kipekee ambayo inatoa fursa kwa wateja kununua bidhaa mbalimbali za vifaa vya umeme kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, ofisini, shuleni, na binafsi. Lakini pia wateja wanapatiwa vocha za punguzo la bei mpaka shilingi 50,000 pamoja na ofa ya kupelekewa bidhaa zao mpaka mahali walipo kwa zitakazozidi shilingi 200,000 na kuendelea kwa jijini Dar es Salaam pekee!
  “Jumia imekuja kufanya mapinduzi katika namna ambayo Watanzania wanafanya manunuzi yao ya kila siku. Kwa miaka mingi wamekuwa wakipoteza muda na gharama kwenda na kurudi madukani kufuata bidhaa, muda ambao ungepaswa kuelekezwa katika shughuli zingine za maendeleo. Katika kulipatia ufumbuzi suala hili, sisi tumekuja na suluhisho kwa kuyakusanya maduka yote na kuyaweka sehemu moja mtandaoni. 


  Hii inamrahisishia mteja kuweza kuperuzi bidhaa kutoka kwa wafanyabiashara tofauti ndani ya wakati mmoja mahali na muda wowote alipo na kisha kufanya manunuzi na kupelekewa bidhaa zake mpaka pale alipo. Kwa mfano, wakati huu wa kampeni ya ‘Electroshock’ mteja anaweza kuperuzi bidhaa zaidi ya 1000 za vifaa vya umeme,” alihitimisha Meneja Masoko wa Jumia Tanzania.

  Katika kunogesha kampeni ya ‘Electroshock‘ ambayo inatarajiwa kufika kikomo Oktoba 7, Jumia imewapatia Watanzania ambao ni wapenzi wa mchezo ‘Playstation’ kununua bidhaa mpya ya ‘FIFA19’ ambayo haijaingia sokoni bado ikitarajiwa kuzinduliwa mnamo Septemba 28 duniani kote. Kupitia mtandao wa Jumia wateja wanaweza kuweka oda ya bidhaa hiyo na kuwa wa kwanza kuimiliki mara tu ikiingia sokoni. Lakini kama hiyo haitoshi kuna simu za bure ambazo zitakuwa zinashindaniwa kwenye mtandao huu kwa kupitia programu yao ya simu ya ‘Jumia App.

  0 0

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  WAZIRI wa Nishati D.Medradrd Kaleman amesema Serikali imeweka mikakati madhubuti kuhakikisha Watanzania wanakuwa wanafuika namba moja katika miradi mikubwa inayoendelea nchini.

  Pia amesema katika kuhakikisha sekta ya nishati na gesi inawanufaika Watanzania wa makundi yote Serikali imeweka sera na mikakati madhubuti itakayosimamia vema maslahi ya nchi.

  Waziri Kalemani amesema leo jijini Dar es Salaam baada ya kuzungumza kwenye Kongamano la Pili la mafuta na gesi ambapo wadau zaidi 300 kutoka mataifa 75 duniani wameshiriki na kutoa maoni yao.

  Akifafanua zaidi kuhusu namna ambavyo Serikali imejiandaa katika kuhakikisha sekta ya mafuta na gesi Waziri Kaleman amesema kikubwa ambacho wanahamasisha ni wananchi kushiriki katika sekta hizo na hasa miradi mikubwa inayoendelea ili waweze kunufaika.

  “Tumewaambia wawekazaji wote ambao wamefika hapa na wale ambao wanayo miradi mikubwa wanayoendelea kuitekeleza kuhakikisha wananchi wetu wanashirikishwa na kunuifaka.“Kuna kazi ambazo hazina sababu ya kufanywa na watu wa nje.Tunafahamu Watanzania wamesoma kwa viwango tofauti lakini kila mmoja lazima ashiriki kwa nafasi yake na anufaike na uwepo wa miradi inayoendelea nchini,”amesema Waziri Kalemani.

  Amefafanua katika kushiriki huko ni matarajia ya Serikali kuwa kampuni ambazo zinahusika na chakula basi vitauza chakula, kampuni za kisheria basi nazo zitatoa ushauri wa kisheria na kwamba kila kampuni, kikundi au mtu mmoja mmoja lazima ashiriki na tayari Serikali imeweka mazingira mazuri.

   Pia amezungumzia hisa ya asilimia 25 kwa ajili ya wazawa na kwamba muwekezaji yoyote ambaye anataka kuja kuwekeza nchini katika gesi na mafuta basi lazima asilimia 25 ya uwekezaji iwe ya watanzania.

   Amewahakikisha Watanzania kuwa Serikali imejipanga vema kuhakikisha rasilimali zilizopo nchini zinawanufaisha.Wakati huo huo amesema mkutano huo umedhihirisha namna ambavyo sekta binafsi wanashirikiana na Serikali katika kutoa muelekeo kuhusu sekta hiyo.

  0 0


   MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kulia akimfariji mama wa dereva wa bodaboda aliyeuwawa Mohamed Ally alimaarufu Sharo anayefanya kazi zake Pangani mjini ambaye inadaiwa alikodisha na watu wasiojulikana na kufanya mauaji hayo
   MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kushoto akimpa pole mama wa bodaboda aliyeuwawa Mohamed Ally alimaarufu Sharo anayefanya kazi zake Pangani mjini ambaye inadaiwa alikodisha na watu
  wasiojulikana na kufanya mauaji hayo
   MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah katikati akiteta jambo na ndugu wa marehemu kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Nyange Hassani katikati ni Afisa Tawala wa wilaya hiyo Gipson


   MKUU wa wilaya ya Pangani Mkoani Tanga Zainabu Abdallah ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo kufanya uchunguzi wa kina ufanyike ili kuweza kubainika sababu za mauaji ya dereva wa bodaboda Mohamed Ally alimaarufu Sharo anayefanya kazi zake Pangani mjini.

  Inadaiwa mauaji ya bodaboda huyo yalitokea jioni ya Septemba 22 mwaka hu na mwili wake kupatikana Jumapili na kuzikwa juzi mara baada ya kukodiwa na watu wasiojulikana ambao walitaka awapeleka Tanga mjini na walipofika njiani wakatekeleza mauaji hayo kwa kumnyonga hadi umauti ulipomkuta na kuchukua pikipiki yake kutokomea kusikojulikana.

  Akizungumza mara baada ya kuitembelea familia ya marehemu na kutoa pole, Mkuu huyo wa wilaya alisema wamepokea kwa masikitiko makubwa na mshtuko wizi huo na mauaji hayo ya bodaboda ambaye ni kijana mjasiriamali.

  “Kijana huyui mkazi wa Pangani ameuwawa kikatili sana kwa kunyongwa na watu wasiokuwa na utu na kuchukua pikipiki aliokuwa akifanyia biashara ….inaumiza kijana asie na hatia anayejitafutia riziki kujikwamua kimaisha ndoto zake zinakwamishwa”Alisema.

  Aidha alisema wanalaani vikali vitendo hivyo huku akiviagiza vyombo husika kufanya uchunguzi wa tukio hilo haraka ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua kwa kupelekwa kwenye vyombo vya kisheria.

  Hata hiyo alisema wanatarajia kukutana na kuongea na chama cha waendesha BodaBoda wilaya ya humo kuhusu jambo hili na mustakabali wao hasa kwenye masuala ya ulinzi na usalama.

  0 0
  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mh. Jerry Muro ameendelea kutatua kero na changamoto zinazowakabili wananchi wa Wilaya ya Arumeru ikiwemo kero sugu ya changamoto ya migogoro ya ardhi.

  Dc Muro kupitia mkakati wake wa kutatua kero za wananchi ( PAPO KWA PAPO ) amefanikiwa kutatua kero ya utapeli wa kuuziwa viwanja vyenye migogogoro kwa kuamuru baadhi ya wamiliki wa makampuni yanayojishughulisha na biashara ya viwanja ( REAL ESTATE ) kurudisha fedha za wananchi waliouziwa viwanja vyenye matatizo ndani ya mwezi mmoja.

  Aidha Dc Muro amezipiga marufuku kampuni zoote zinazojihisisha na udalali wa viwanja kutokufanya kazi katika Wilaya ya Arumeru mpaka hapo watakapopata maelekezo rasmi kutoka katika Ofisini ya Mkuu wa Wilaya lengo likiwa ni kukabiliana na ongezeko la uuzwaji wa ardhi za vijiji pasipo kufuata taratibu.

  DC Muro anaendelea na zoezi lake lakushughulikia kero za Wananchi kwa mtindo wa PAPO KWA PAPO.
  Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mh. Jerry Muro akizungumza na na baadhi ya wamiliki wa makampuni yanayojishughulisha na biashara ya viwanja ( REAL ESTATE ),ambapo amezisimamisha kampuni hizo kufanya shughuli hiyo na kuwata kurudisha fedha za wananchi waliouziwa viwanja vyenye matatizo ndani ya mwezi mmoja. 
  Baadhi ya Wakazi wa Arumeru wakimsikiliza Mkuu wa wilaya hiyo ya Arumeru Mh. Jerry Muro alipokuwa akizungumza nao kuhusu kero na changamoto mbalimbali walizonazo,kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi na majibu ya papo kwa papo.

  0 0  0 0

  Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ambapo alimueleza umuhimu wa kutangaza na Kuitetea mafanikio ya Serikali kutokana na manuaa yake kwa wananchi, jana Mkoani Geita.
  Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akimueleza Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na Viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) namna walivyojipanga kuendelea kuhakikisha namna mapato ya madini kutoka katika makampuni yanatumika kuondoa adha za wananchi katika sekta muhimu za Afya, Elimu na Wjasiriamali.

  Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw. Pascal Shelutete akimueleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel na kumuhakikishia ushirikiano wa kutosha katika eneo la mawasiliano lengo ni kufanya taarifa za Serikali zinawafikia wananchi.
  Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akiwa katika Picha ya Pamoja na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas pamoja na Viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO).
  Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel mara baada ya kumaliza mazungumzo jana  25/09/2018 Mkoani Geita.  Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel kwa utendaji wake wa ubunifu na unaolenga kuboresha maisha ya Watanzania.

  Dkt. Abbasi ameyasema hayo jana jumanne  Septemba 25, 2018 akiambatana na viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikali (TAGCO) alipofika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huyo katika ziara ya kufuatilia utendaji wa sekta ya habari.

  Katika mazungumzo hayo Dkt. Abbasi amemueleza Mhandisi Gabriel kuwa mafanikio hayo ya Geita na mengine ambayo Serikali kwa ujumla inayatekeleza umuhimu yanapaswa kutangazwa na kutetewa kwa kuwa yana manufaa nakubwa kwa wananchi. Katika mazungumzo RC Gabriel alisema mkoa wake umehakikisha mapato kutoka kwa makampuni ya madini yanatumika kuondoa adha za wananchi katika sekta muhimu kama afya, elimu na wajasiriamali.

  Alisisitiza kuwa katika sekta ya Afya wamepanga kuwa kufikia Mei, 2019 zahanati zote mkoani Geita zitakuwa zimekamilika. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikali (TAGCO), Bw. Pascal Shelutete amemuhakikishia Mhandisi Gabriel ushirikiano wa kutosha katika eneo la mawasiliano lengo ni kuhakikisha taarifa za Serikali zinawafikia wananchi.

  Aidha, Bw. Shelutete pia amempongeza RC huyo kwa utendaji wake makini na wa kimageuzi unaowagusa na kuwafunza wengi nchini.

  0 0

  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ametoa muda wa mwezi mmoja kwa mkandarasi wa mradi wa maji Tunduma kukamilisha kazi hiyo. 

  Mhe. Aweso (Mb) ametoa muda huo mjini Tunduma baada ya kukagua mradi huo ambao umekamilika kwa asilimia 93 na kusisitiza atarudi kuufungua baada ya muda aliotoa kukamilika. Amesema wananchi wanasubiri majisafi na salama kutoka katika mradi huo ambao Serikali imetoa kiasi cha Shilingi milioni 895 kuhakikisha huduma inawafikia wananchi. 

  Wakati huohuo, Mhe. Aweso (Mb) amewaelekeza Wahandisi wa Maji mkoani Mbeya kufanya kazi kwa weledi na kuepuka vishawishi ambavyo vinaharibu taaluma yao na kazi. Mhe. Aweso amesema hayo katika kikao kazi kilichowakutanisha Wahandisi wa maji wa mkoa wa Mbeya, jijini Mbeya. Amewaelekeza moja ya kazi wanayotakiwa kufanya ni kutembelea miradi na kujiridhisha na ubora wake, pia kujua kinachofanyika katika ujenzi na sio kukaa maofisini. 

  Mhe. Aweso (Mb) amesema mradi ukijengwa katika kiwango bora na wananchi wakapata huduma nzuri jambo hilo ni moja kati ya kumbukumbu muhimu kwa wote waliofanya kazi, na kusisitiza wahandisi wote wanaofanya vizuri watatambuliwa kwa ubora wa kazi walizosimamia. 

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini 
  Wizara ya Maji na Umwagiliaji 
  25.09.2018

  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Jumaa Aweso (Mb), akiongea na vyombo vya habari katika eneo la mradi wa maji Tunduma. Mkandarasi wa mradi huo kapewa mwezi mmoja kukamilisha kazi. 
  Watumishi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira jijini Mbeya wakiwa katika kikao na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Jumaa Aweso (Mb), hayupo pichani, jijini Mbeya.
  Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo (kushoto) akimkaribisha Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) kuongea na watumishi wa Mamlaka ya Maji jijini Mbeya.
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Jumaa Aweso (Mb), akiongea na Wahandisi wa Maji wa mkoa wa Mbeya kuhusu uwajibikaji katika miradi ya maji.
  Wahusika walioshiriki katika kusimamia mradi wa Maji Galijembe mkoani Mbeya, Wahandisi wa majina na mkandarasi-kampuni ya Black Dot, wakiwa katika gari la Polisi ili kusaidia kuhusu mkandarasi kulipwa na mradi kutokamilika. 
  Mhusika kutoka kampuni ya Black Dot iliyopewa kandarasi ya mradi wa maji Galijembe mkoani Mbeya, na kuutelekeza, pamoja na Mhandisi aliyehusika katika mradi huo, wakitoa maelezo yao kwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso (Mb), hayupo pichani.
  Mmoja kati ya wahusika wa kampuni ya Black Dot iliyopewa kandarasi ya ujenzi wa mradi wa maji Galijembe mkoani Mbeya akitoa maelezo ya kutokamilika mradi kwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso, MB, (hayupo pichani) . 
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Jumaa Aweso (Mb), akipanda kukagua moja ya tanki la kuhifadhi maji la mradi wa Mlowo mkoani Mbeya.
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Jumaa Aweso (Mb), akiangalia maendeleo ya ujenzi wa chujio la maji katika mradi wa maji wa Vwawa mkoani Mbeya.

  0 0

   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, leo 26, 09, 22018 amemjulia hali Wazirii wa Maliasili na Utalii, Dk. Khamis Kingwangalla nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam. Dk. Kigwangalla alipata ajali Augusti 4 mwaka huu wakati akiwa kwenye ziara yake ya kikazi

  0 0

  WILAYA ya Namtumbo mkoani Ruvuma kupitia Mkuu wake wa Wilaya Sophia Mfaume Kizigo imesaini mkataba wa lishe bora, ambapo wamedhamiria malengo, vipaumbele na majukumu yote wanayotakiwa kuyatimiza yanatimia.

  Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Kizigo amesema mkataba huo ni wa miaka 4 (2018 hadi 2021).

  Amefafanua kwamba licha ya kwamba Ruvuma ni mkoa unaozalisha chakula kwa wingi sana na kulisha taifa lakini Ruvuma hiyohiyo ipo katika mikoa 5 ambayo ina hali mbaya sana ya lishe bora.

  "Ruvuma kama mkoa kuna udumavu (stunting) asilimia 44, utapiamlo mkali asilimia 2.6, uzito pungufu asilimia 13.7, Upungufu wa damu (anaemia) na uzito mkubwa asilimia 21.1," amefafanua.

  Pia ameongeza mkataba huo unaelekeza mpango mkakati wa lishe bora, kutoa elimu kwa wananchi ili wabadili tabia katika ulaji unaofaa, elimu ya lishe kwa jamii na mkakati wa kutengeneza chakula dawa.

  Mkuu huyo wa Wilaya ameelezea namna ambavyo mkataba huo ukisimamiwa vema utakavyoleta mabadiliko kwa kufanikisha Wilaya ya Namtumbo inafanikiwa katika suala la lishe bora. 
  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme akiimkabidhi Mkuu wa Wilaya Sophia Mfaume Kizigo mkataba wa kufanikisha lishe bora kwa Wananchi mapema jana,mkoani humo
  Pichani kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume Kizigo ikisaini mkataba wa lishe bora kwa Wananchi,kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,katika mkataba huo Wialaya ya Namtumbo wamedhamiria malengo, vipaumbele na majukumu yote wanayotakiwa kuyatimiza yanatimia.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kulia) akizungumza wakati Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe, Asia Abdallah (kushoto) alipotembelea Makao Makuu ya Benki hiyo kuzungumzia fursa mbalimbali za kilimo zilizopo wilayani Kilolo.
  Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe, Asia Abdallah (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na uongozi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB). Anayemsikiliza ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kulia).
  Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha akizungumza wakati wa kikao hicho.

  ……………………………

  Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imesema ipo tayari kusaidia mapinduzi ya kilimo wilayani Kilolo mkoani Iringa kupitia ujenzi wa viwanda vya kimkakati vyenye kulenga kunyanyua maisha ya mkulima mdogo wilayani humo.

  Ahadi hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine wakati akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe, Asia Abdallah aliyetembelea Makao Makuu ya Benki hiyo.

  Bw. Justine amesema kuwa TADB ipo tayari kusaidia juhudiza wilaya ya Kilolo za kujenga kiwanda kisasa cha chai na mazao mengine ya kimkakati ili kuongeza kipato cha wakulima wilayani.“Benki ipo tayari kutoa mtaji wa kujenga viwanda vya kimkakati ili kupata soko la mazao ya wakulima wadogo wadogo hasa wakulima wa chai,” alisema.

  Bw. Justine aliongeza kuwa Benki imelenga kutekeleza kwa vitendo dhana ya Tanzania ya Viwanda kwa kujielekeza katika uwekezaji wa viwanda vitakavyotoa ajira kwa vijana na wanawake wilayani humo.Akieleza fursa zilizopo wilayani humo, Mkuu wa Wilaya, Mhe. Asia Abdallah alisema kuwa wilaya yake ina hekari zaidi ya 3,000 zilizotengwa kwaajili ya kilimo cha mazao ya kimkakati ikiwemo zao la chai.“Tunafarijika kwa utayari wa Benki kusaidia uwekezaji wa kimkakati hasa katika ujenzi wa kiwanda cha chai wilaya kwetu,” alisema.

  Mheshimiwa Abdallah aliongeza kuwa wilaya ya kilolo ina fursa za kilimo ikiwemo uwepo wa ekari zaid ya 20,000 kwa ajii ya shughuli za kilimo cha mazao mbalimbali ikiwemo maparachichi, ufugaji wa samaki na nyuki.

  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Dkt,Ally Saleh Mwinyikai akimkaribisha Waziri wa Habari Utalii na Michezo Mahmoud Thabit Kombo (hayupo pichani)katika hafla ya Kukabidhi Leseni za Utangazaji (TV ONLINE)ambapo jumla ya Tv Online Nane na Kebol mbili zilipatiwa hafla Iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii na Michezo Kikwajuni Zanzibar.
  Waziri wa Habari Utalii na Michezo Mahmoud Thabit Kombo akitoa hotuba katika hafla ya Kukabidhi Leseni za Utangazaji (TV ONLINE)ambapo jumla ya Tv Online Nane na Kebol mbili zilipatiwa hafla Iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii na Michezo Kikwajuni Zanzibar.
  Waziri wa Habari Utalii na Michezo Mahmoud Thabit Kombo kulia akimkabidhi Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Hassan Hatibu Leseni ya Utangazaji (TV ONLINE)katika hafla ya kukabidhi leseni Iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii na Michezo Kikwajuni Zanzibar.
  Waziri wa Habari Utalii na Michezo Mahmoud Thabit Kombo kulia akimkabidhi Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Leseni ya Utangazaji (TV ONLINE)katika hafla ya kukabidhi leseni Iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii na Michezo Kikwajuni Zanzibar.
  Waziri wa Habari Utalii na Michezo Mahmoud Thabit Kombo katikati akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na Waliopatiwa Leseni za Utangazaji(TV ONLINE)Katika hafla ya kukabidhi leseni Iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii na Michezo Kikwajuni Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANIZBAR.

  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt. Aziz P. Mlima (kulia) akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni Ikulu jijini Kampala, Uganda tarehe 25 Septemba 2018. 
  Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt. Aziz P. Mlima akiwa pamoja na Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho 
  Picha ya Pamoja

  0 0


  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani ) kuhusu kuhusu kampeni ya Uzalendo na Utaifa, ambayo maadhimisho  yake yatafanyika Desemba 8, 2018 Jijini Dodoma  Huku kauli mbiu ikiwa ni  “Kiswahili, uhai wetu, utashi wetu” kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bi. Leah Kihimba na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fisoo
  PIX 01 (6)
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Waandishi wa (pichani) kuhusu kampeni ya Uzalendo na Utaifa, ambayo maadhimisho  yake yatafanyika Desemba 8, 2018 Jijini Dodoma  Huku kauli mbiu ikiwa ni “Kiswahili, uhai wetu, utashi wetu”
  PIX 03 (6)
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani ) kuhusu kuhusu kampeni ya Uzalendo na Utaifa, ambayo maadhimisho  yake yatafanyika Desemba 8, 2018 Jijini Dodoma  Huku kauli mbiu  ikiwa ni“Kiswahili uhai wetu, utashi wetu” kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fisoo.(Picha na Paschal Dotto-MAELEZO)

  Na Fatma Salum-MAELEZO
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amebainisha kuwa lugha ya Kiswahili inatarajiwa kuwa lugha kuu ya mawasiliano katika bara la Afrika ifikapo mwaka 2063.

  Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Kampeni Ya Uzalendo na Utaifa kwa mwaka 2018 yanayotarajiwa kufanyika Desemba 8 Jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais John Pombe Magufuli.

  Alisema kuwa kampeni hiyo kwa mwaka huu imejikita katika kuhamasisha matumizi ya lugha ya Kiswahili ambayo ni kielelezo kikubwa cha utashi na uhai wa taifa la Tanzania na inakua kwa kasi sana barani Afrika na duniani kote kwa ujumla.“Sasa hivi Kiswahili ni lugha ya kumi kati ya lugha elfu 6 zinazoongelewa na watu wengi duniani na kwa mujibu wa Tafiti za Umoja wa Afrika zinaonesha kuwa ifikapo mwaka 2063 Kiswahili kitakuwa lugha kuu ya mawasiliano katika bara la Afrika na utambulisho wa mtu mweusi duniani,” alisema Mwakyembe.

  Alieleza kuwa dunia yote inatambua kwamba Tanzania ndio chimbuko la lugha adhimu ya Kiswahili hivyo watanzania wanapaswa kujivunia lugha hiyo na kuitangaza kwa kuwa ni sehemu ya utamaduni wa taifa na msingi wa uzalendo na utaifa.Waziri Mwakyembe alibainisha kuwa kampeni hiyo mwaka huu imejikita katika kuhamasisha matumizi ya lugha ya Kiswahili ili kuwasisitiza watanzania kuthamini lugha yao na utamaduni wao na kurejea kwenye misingi ya maadili ya taifa lao.

  Alisema kuwa sasahivi kuna changamoto kubwa ya mmomonyoko wa maadili inayosababishwa na baadhi ya watu hasa vijana kuiga tamaduni za nje kutokana na utandawazi hivyo kupelekea kudharau utamaduni wao ikiwemo lugha ya Kiswahili jambo ambalo lisipochukuliwa hatua madhubuti litaleta athari kwa jamii.Pia Waziri Mwakyembe alitoa pongezi kwa Rais John Pombe Magufuli kwa mchango wake mkubwa anaoonesha katika kutumia, kukuza na kuitangaza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi hivyo amekuwa ni mfano wa kuigwa.

  Aidha alitoa rai kwa watanzania wote na wadau mbalimbali kuunga mkono kampeni hiyo kwa hali na mali ili Tanzania iweze kufanikiwa kulinda misingi ya utamaduni na utaifa hususan lugha ya Kiswahili.Kampeni ya Uzalendo na Utaifa ilianza rasmi mwaka jana 2017 na itakuwa ikiadhimishwa kila mwaka ambapo kwa mwaka huu kauli mbiu yake ni ‘Kiswahili Uhai Wetu, Utashi Wetu’.  

  0 0

  Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ipo katika mpango mkakati wa kuungana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) katika kuwawezesha wakulima na wafanyabiashara wa mazao ya kilimo kuchangamkia fursa za uwepo wa soko la uhakika la mazao ya kilimo nchini China ili kuongeza tija katika kilimo biashara nchini.

  Hatua hii ya TADB ni kuitikia wito wa fursa za uwepo wa soko la uhakika wa mazao ya kimkakati yaliyomwayo nchini kama ilivyobainika wakati wa maonyesho ya 15 ya ASEAN (CAEXPO) 2018 yaliofanyika wiki iliyopita huko Nanning, Guangxi nchini China ambako Tanzania ilipewa heshimiwa kuwa mshirika maalum wa maonyesho kutoka barani Afrika.

  Akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya TADB na TANTRADE kilicholenga kujadilia namna Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania itakavyoweza kuwawezesha wakulima na wafanyabiashara wa mazao ya kilimo kuchangamkia fursa za uwepo wa soko la uhakika la mazao ya kilimo nchini China, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine amesema TADB ipo tayari kuwawezesha kwa kuwapa mikopo ya gharama nafuu ili kupata mtaji wa uhakika katika kuongeza tija shughuli za kilimo.

  “Tumejipanga kuitikia wito huu kwa vitendo kwa kuzingatia kuwa moja kati ya majukumu ya benki ni kusaidia kuwaunganisha wakulima na masoko ili kuinua uzalishaji wenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini,” alisema.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade,, Bw. Edwin Rutageruka amesema TanTrade ilipeleka sampuli mbalimbali za mazao na bidhaa za Tanzania katika Maonesho ya Kimataifa ya CAEXPO 2018 ambapo Tanzania imepata fursa ya soko kwa mazao zaidi ya 10 ikiwemo korosho, kahawa, mbaazi, choroko, degu, chai, tangawizi, asali na mhogo.

  “Wakati wa CAEXPO 2018  bidhaa zilizosindikwa kutoka Tanzania zilipata soko kubwa hivyo tunadhani ujio wa TADB utsaidia kuongeza nguvu za kimtaji ili kuweza kukidhi mahitaji ya kimtaji kwa wakulima na wafanyabiashara wa mazao ya kilmo,” alisema.

  Bw. Rutageruka aliongeza kuwa maonyesho hayo yaliwashirikisha zaidi ya wafanyabiashara wakubwa 50 kutoka China ambao wameonesha nia ya kufanya biashara na Tanzania hasa katika mazao ya kilimo.

  kwa mujibu wa taarifa ya mwaka 2017 ya Benki Kuu ya Tanzania, China ni nchi ya nne katika nchi zinazonunua bidhaa kutoka Tanzania ambapo ilinunua takribani asilimia 8 ya bidhaa zote zilizouzwa nje ya Tanzania kwa mwaka 2016/2017.
   Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Bw. Edwin Rutageruka (kushoto) akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kulia) wakati walipokutana katika kikao cha pamoja kati ya TADB na TANTRADE kilicholenga kujadilia namna Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania itakavyoweza kuwawezesha wakulima na wafanyabiashara wa mazao ya kilimo kuchangamkia fursa za uwepo wa soko la uhakika la mazao ya kilimo nchini China.
   Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Bw. Edwin Rutageruka (kulia) akizungumza juu ya fursa za masoko nchini China wakati wa kikao cha pamoja kati ya TADB na TANTRADE. Anayemsikiliza ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kushoto).
   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine akifafanua jambo wakati wa kikao.
   Washiriki wa majadiliano hayo wakiwa katika picha ya pamoja.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Bw. Edwin Rutageruka (kulia) mara baada ya kikao cha pamoja kati ya TADB na TANTRADE kilicholenga kujadilia namna Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania itakavyoweza kuwawezesha wakulima na wafanyabiashara wa mazao ya kilimo kuchangamkia fursa za uwepo wa soko la uhakika la mazao ya kilimo nchini China.

older | 1 | .... | 1678 | 1679 | (Page 1680) | 1681 | 1682 | .... | 1898 | newer