Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1676 | 1677 | (Page 1678) | 1679 | 1680 | .... | 1897 | newer

  0 0  NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

  SIKU moja baada ya kupinduka kwa kivuko cha MV Nyerere chanzo kilichosababisha cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni simu ya mkononi na kuzidisha uzito wa mizigo na abiria.

  Katika ajali hiyo hadi jana (alhamisi) usiku majira ya saa 2:36 miili 40 ikiwemo ya watoto sita ilikuwa imeopolewa kutoka ndani ya kivuko hicho huku watu wengine 38 wakiokolewa kwenye ajali hiyo mbaya ya pili kwa ukubwa kutokea katika Ziwa Victoria.

  Aidha, zoezi la uokoaji lililazimika kusitishwa juzi usiku kutoka na giza hali ambayo ilizidisha sintofahamu ya kuwaokoa abiria walionasa ndani ya kivuko hicho ambacho kimepinduka na kuzama sehemu kubwa ya juu ikiwa majini.

  Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela miili 42 hadi asubuhi leo ilikuwa imeopolewa na wengine 44 walikuwa bado miili yao haijapatikana huku watu 40 wakiripotiwa kuwa hai miongoni mwa walipata ajali.Akizungumza kwa simu jana usiku mmoja wa abiria walionusurika kwenye ajali hiyo kwa sharti la hifadhi ya jina alisema kabla ya kivuko hicho kupinduka kilipoteza uelekeo kutokana na nahodha ku-chart kwenye simu kabla ya ajali kutokea.

  “ Kabla ya ajali wakati tukielekea kwenye ghati nahodha alikuwa akichart kwa simu alijikuta amepoteza uelekeo na wakati anakata kona kivuko kulalia upande mmoja na kusababisha shehena ya mizigo wa nafaka kuelemea upande na kupinduka,”alisema mtoa habri huyo. 

  Alisema kuwa kivuko hicho kilikuwa kimebeba shehena ya magunia 100 yenye uzito wa tani 10.8, lori moja aina ya Fusso nalo likiwa na magunia ya mahindi, saruji na magari madogo mawili moja aina ya Toyota Hilux lilikoluwa limebeba vyuma (vifaa vya umeme) yote ikikadiriwa kuwa na uzito zaidi ya tani 30.Kivuko hicho kilipinduka juzi majira kati ya saa 7:30 na saa 8:00 mchana umbali wa mita 100 kaba ya kufika kwenye ghati la Bwisya kikitokea katika ghati la Bugorola  katka kisiwa kisiwa cha Ukerewe.  

  Juzi mmoja wa manusura wa ajali hiyo aliyefahamika kwa jina moja la Michael alisema kuwa kabla ya kufika kwenye ghati kutia nanga kivuko hicho kilikata kona na kilijikita chini ambapo nahodha wake alitoka nje kuangalia nini kimetokea.“Nahodha alikata kona chombo kikajikita chini na alitoka nje kuangalia nje  kabla ya kuipeleka darajani lakini kutokana na kona kuwa kubwa aliyokata ilialia upande mmoja na kusababisha mizigo ielemee upande huo na haikuweza kurudi upande wa pili kikapinduka,”alisema Michael.

  Alisema baada ya kivuko hicho kulalia upande mmoja baadhi ya abiria waliokuwa wamekaa nje eneo la mizigo walirushwa majini na ambao hawakuwa na kitu cha kuwasaidia kujiokoa walikufa maji.“Abiria walikuwa wengi pamoja na shehena ya mizigo na baada ya kupinduka abiria waliokuwa ndani hawakuweza kutoka na wote wamekufa maji, yaani waliokufa ni wengi mno isipokuwa wachache waliokuwa wamekaa mbele kwenye eneo la mizigo,”alisema manusura huyo ambaye alishuhudia kivuko hicho kikipinduka.

  Hata hivyo kivuko hicho kudaiwa kuzidiwa uzito na wingi wa abiria na kusababisha kupinduka hakijazama bado kinaelea jambo linalofanya uwezekano wa kuokolewa kwa abiria waliopo ndani kwa kuwa watakuwa hai.Shuhuda huyo alisema kivuko hicho kimepinduka na kusababisha kibinuke mgongo juu na eneo la juu kuzama majini na kufanya uokoaji kuwa mgumu na kwamba hadi muda huo alikuwa ameshuhudia miili 16 ikiopolewa kutoka majini.

  Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa uwezekano wa kuwapata abiria wakiwa hai utategemea miujiza ingawa vikosi vya ulinzi na uslama vikishirikiana na wananchi vinaendelea kuopoa miili ya marehemu kutoka ndani ya kivuko hicho .

  “hali ni mbaya na hakuna uwezekano wa kuwapata abiria wakiwa hai ni kuomba miujiuza ya Mungu il sina takwimu za miili iliyopolewa kwa sasa tangu zoezi hili lianze asubuhi baada ya kusitishwa usiku jana kutoka giza ila ni wengi waliokufa.Kuweni na subira hadi jioni takwimu zitakuwa tayari,”alisema mmoja wa waokoaji.


  0 0  WANAHISA wa benki ya Azania wameonyesha kuridhishwa na mwenendo, ufanisi pamoja na mafanikio ya benki hiyo licha ya uwepo wa changamoto kadhaa zinazoikabili sekta ya benki hapa nchini, huku wakionesha kuridhishwa zaidi na namna benki hiyo ilivyoweza kukabiliana na changamoto ya mikopo isiyolipika.(Non- performing Loans)

  Wakizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa benki hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo, wadau hao wamesema baada ya kupitia ripoti ya mwaka ya mwaka 2017 kuhusu mwenendo wa biashara wa benki hiyo wamebaini kuwa benki hiyo imepiga hatua kubwa kwenye nyanja kadhaa ikiwemo ongezeko la rasilimali (asset growth), kukidhi matakwa ya sheria za kibenki pamoja na kufanikiwa kukwepaji changamoto ya mikopo isiyolipika.

  “Kwa mujibu wa ripoti hii ongezeko la rasilimali yaani asset growth ni asilimia 15 na zaidi kinachovutia zaidi ni kuona kwamba benki yetu imejitahidi sana kukabiliana na tatizo la mikopo isiyolipika kwa kuwa na asilimia 8 tu ya mikopo na wito wangu kwa uongozi wa benki ya Azania ni kuhakikisha asilimia hizi zinashuka hadi kufikia chini ya asilimia 6,’’ alisema mmoja wa wanahisa hao Bw Misheck Ngatunga.

  Awali, akisoma taarifa yake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw Charles Itembe alisema ufanisi wa benki hiyo umethibitishwa zaidi mwaka huu baada ya kutoa gawio la kiasi cha Sh. Mil 633 kwa wanahisa wake ikiwa ni mara ya kwanza tangu benki hiyo ianzishwe mwaka 1995.

  Alisema mafanikio hayo ya kiutendaji yameiwezesha benki hiyo kupata faida baada ya kodi kiasi cha Sh Bilioni 1.81 kutoka hasara ya sh. Bilioni 6.04 iliyoikumba benki hiyo mwaka 2016.

  “Aidha katika kipindi cha mwaka 2017 benki ya Azania imeweza kukupata faida itokanayo na riba (interest income) ya Sh bilioni 41.9 ikilinganishwa na kiasi cha sh bilioni 39.5 kilichopatikana mwaka 2016.’’ Alisema Bw Itembe huku akiainisha wazi kuwa mkakati wa benki hiyo ni kujitanua kwa kuongeza matawi kwenye mikoa mbalimbali ambapo kwa mwaka huu imeweza kufungua matawi yake mkoani Dodoma na Morogoro.

  Akizungumza kwenye mkutano huo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa benki hiy, Makamu Mwenyekiti Bw Eliudi Sanga alisema kwa kiasi kikubwa mafanikio hayo yamechangiwa na mabadiliko iliyoyafanya mwaka 2017 yakilenga kubadilisha masuala mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya muundo wa utendaji ili kuboresha utoaji wa huduma, kuwekeza kwenye ubora na usimamiaji wa masuala ya fedha.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Bw Charles Itembe, (kushoto) akizungumza na wadau wa benki hiyo kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa benki ya Azania uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni pamoja naMakamu Mwenyekiti wa Bodi  ya wakurugenzi wa benki hiyo, Bw  Eliudi Sanga (katikati) na Mkurugenzi wa Masuala ya kisheria wa benki hiyo Bw Charles Mugila.
   Makamu Mwenyekiti wa Bodi  ya wakurugenzi wa benki ya Azania Bw  Eliudi Sanga (kushoto) akizungumza na wadau wa benki hiyo kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa benki ya Azania uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Bw Charles Itembe.
   Baadhi ya wadau wa benki ya Azania wakifuatilia mkutano huo.
   Makamu Mwenyekiti wa Bodi  ya wakurugenzi wa benki ya Azania Bw  Eliudi Sanga (katikati) akiongoza mkutano huo.

  0 0

  *Ni kutokana na ajali ya kivuko cha MV Nyerere

  WAZIR MKUU Kassim Majaliwa amekatisha ziara ya mkoa wa Dodoma na kuelekea Ukerewe Mwanza kuwafariji wananchi waliopatwa na maafa kutokana na ajali ya kivuko cha MV Nyerere.

  Waziri Mkuu ambaye alikuwa na ziara ya kikazi ya siku saba katika mkoa wa Dodoma, ametangaza uamuzi huo leo mchana (Ijumaa, Septemba 21, 2018) wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chandama, wilayani Chemba ambao walisimamisha msafara wake ili wamweleze kero kubwa ya maji inayowakabili.

  “Nimelazimika kukatisha ziara yangu na wala sitaenda Kwa Mtoro ili niende kuwafariji wenzetu waliopatwa na msiba wa kupoteza ndugu zao kutokana na ajali iliyotokea jana usiku. Idadi ya waliopoteza maisha imefikia 91, ni msiba mkubwa kwa Taifa letu,” amesema Waziri Mkuu kwa masikitiko.

  Waziri Mkuu alikuwa akitokea kijiji cha Itolwa kata ya Jangalo ambako alikuwa na mkutano wa hadhara, aliwaeleza wananchi wa vijiji vya Itolwa, Mapango na Chandama kwamba Serikali imetenga sh. bilioni 5.6 kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji kwenye wilaya hiyo.

  Akijibu kero kuhusu ubovu wa barabara, Waziri Mkuu alisema amebaini ukubwa wa tatizo la barabara hiyo yenye urefu wa km.10.3 lakini imetengewa sh. milioni 833 ambazo alisema hazitoshi.

  “Mhandisi wa TARURA nenda ukakae na timu yako, inabidi mfanye upya mahesabu yenu kwa sababu barabara hii ni ndefu na ina madaraja mengi lakini pia inapita kwenye vijiji vingi. Wenzenu Kondoa wamepata sh. bilioni saba, sasa hii sh. milioni 800 hata sijui itaanzia wapi,” alisema.

  “Barabara hii inapita kwenye vijiji vingi vikubwa na wakazi wa huku ni wengi. Hata kama kwa sasa hatuwezi kuijenga kwa kiwango cha lami, inapaswa ijengwe vizuri kwa kiwango kinachoweza kupitika kwa mwaka mzima,” alisema.

  Aliwasisitiza watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba waache tabia ya kupenda kukaa ofisini na badala yake waende vijijini ili wakawasikilize wananchi na kutatua kero zao.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  41193 - DODOMA.
  IJUMAA, SEPTEMBA 21, 2018.

  0 0


  Ziara ya Mjukuu wa  Malkia wa Uingereza nchini, (Prince William)
  Mjukuu wa Malkia wa Uingereza “Prince” William anatarajiwa kufanya ziara nchini kuanzia tarehe 26 hadi 29 Septemba 2018.  Ziara hiyo inakuja kufuatia maombi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alipofanya naye mazungumzo wakati wa mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola uliofanyika Uingereza mwezi Aprili 2018.

  “Prince” William atakapowasili nchini pamoja na mambo mengine atafanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Aidha, atatembelea kikosi cha Maji cha Jeshi la Polisi; Bandari ya Dar es Salaam; Jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii (Mpingo House); Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi iliyopo mkoani Tanga na Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori cha Mweka kilichopo mkoani Kilimanjaro.

  “Prince” William ni mmoja wa wanaharakati duniani wanaopinga biashara haramu ya bidhaa za wanyamapori na Uingereza imekuwa ikisifu juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kupambana na vitendo vya ujangili.

  “Prince” William ataondoka nchini tarehe 29 Septemba 2018 kuelekea nchini Kenya. 

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
  Dar es Salaam, 21 Septemba 2018

  0 0


  Rais Dkt Magufuli ametangaza kuanzia leo Bendera ya Taifa kupepea nusu mlingoti kwa siku nne ikiwa ni sehemu ya maombolezo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kuhusiana na ajali ya kuzama kwa Kivuko cha MV Nyerere kilichokuwa kikifanya safari zake  kati ya kisiwa cha  Bugolora na Ukara katika ziwa Victoria  Wilayani Ukerewe mkoani Mwanza ambapo  watu 131 wanahofiwa kupoteza maisha. Pia Rais Dkt. Magufuli ametangaza siku nne za Maombolezo kuanzia leo tarehe 21 Septemba 2018. PICHA NA IKULU

  0 0

  Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

  NAIBU Waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah Ulega amefungua rasmi mafunzo ya ufugaji wa kuku kibiashara katika jiji la Dar es salaam na kueleza mikakati ya Wizara inayolenga kuongeza uzalishaji wa sekta ya mifugo na uvuvi hasa katika kuangalia suala la chakula na lishe kwa mifugo ili kuweza kuinua kipato kwa wananchi.

  Akizungumza katika ufunguzi huo Ulega ameeleza ķuwa sekta ya ufugaji wa kuku ni moja ya shughuli muhimu za kiuchumi zinazogusa wananchi wa mjini na vijijini na zaidi ya asilimia 72 ya kaya zote nchini hufuga kuku kwa malengo ya kuboresha lishe na kipato.

  Na amewataka wanawake na vijana kujikita katika ufugaji wa kuku kwani huhitaji mtaji mdogo na sekta hiyo huchangia asilimia 53 ya kipato cha kaya za wafugaji wa kuku ukilinganisha na vyanzo vingine vya mapato.

  Aidha kuhusiana na mada zitakazojadiliwa katika mafunzo hayo Ulega amesema yatakayojadiliwa ni pamoja na utengenezaji na matumizi ya vyakula vya kuku, uzalishaji na upatikanaji wa vifaranga bora, uthibiti wa magonjwa na matumizi ya dawa za kuku, ujasiriamali na masoko ya kuku na mazao yake.

  Sambamba na hayo kutakuwa na fursa ya uanzishwaji vyama vya ushirika, majukwaa na mitandao ya wafugaji wa kuku nchini pamoja na upatikanaji wa mikopo hususani kupitia mfuko wa vijana, wanawake,wazee na wenye ulemavu katika halmashauri zote kama mpango wa serikali unavyoeleza.

  Ameeleza kuwa baada ya mafunzo hayo maarifa ya wafugaji hao yataongezeka na kupelekea kuongezeka kwa kiwango cha uzalishaji wa kuku wa mayai hivyo hali ya kipato itaongezeka zaidi.

  Aidha amesema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi 2015-2020 pamoja na mpango wa maendeleo wa taifa kwa miaka mitano yaani 2015/206 hadi 2020/2021 na amewataka wafugaji watumie fursa ipasavyo na kulipeleka taifa kwenye uchumi wa kati.  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wafugaji wa kuku leo katika katika mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo wafugaji hao yaliyoandaaliwa na Wizara hiyo.


  Kaimu Mkurugenzi wa utafiti, mafunzo na Ugani wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt Angello Mwilawa akizungumza na wafugaji wa kuku wakati ya utolewaji wa mafunzo hayo katika kuhakikisha sekta hiyo inakuwa bora zaidi.


  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwasikiliza na kujibu maswali ya wafugaji waliohudhuria mafunzo ya ufugaji wa kuku yaliyoandaliwa na Wizara hiyo.


  (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)

  0 0

  Na Zanab Nyamka, Globu ya Jamii.

  NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt  Faustine Ndugulile amewataka Wizara ya Afya kuongeza idadi ya mikoa iliyopo katika programu ya huduma ya TB kupitia teknlojia ya simu za mkononi ili kila mwananchi aweze kupata huduma hiyo.

  Hayo yamesemwa leo wakati wa uzinduzi wa huduma ya TB kupitia kupitia teknolojia ya simu za mkononi unaojulikana kama TAMBUA TB  kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kufahamu kuhusu dalili za Kifua  pamoja na mpango labambe wa kudhibiti kifua kikuu nchini.

  Dkt Ndugulile amesema kuwa pamoja na kuwa na programu hiyo lazima Wizara watoe elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Kifua Kikuu ambapo inakadiriwa zaidi ya vifo 27,000 vinasababishwa na uginjwa huo.

  Amesema, katika kuboresha na kudhibiti ugonjwa wa Kifua Kikuu, wameweka mifumo ya tambua ambapo imeongeza mashine 209 zinazoweza kutambua mgonjwa ndani ya masaa mawili.

  Dkt Ndugulile amesema, kupitia Wizara mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma inatekeleza mpango mkakati wa miaka mitano 2015-2020 lengo likiwa ni kupunguza maambukizi mapya ya TB kwa asilimia 20 na idadi ya vifo vinavyotokana na TB kwa asilimia 35.

  Amesema, kuwa kutokana na mpango wa Wizara wamewekea mkakati wa kuboresha zaidi huduma  na kutoa rai ya kuongeza idadi ya mikoa kwani wananchi wote wanahitaji huduma hiyo ili kupunguza kasi ya maambukizi.
  NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt  Faustine Ndugulile  akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya huduma ya TB kupitia teknlojia ya simu za mkononi  uliojulikana kwa jimba TAMBUA TB akiwataka kuongeza  idadi ya mikoa ili wananchi wapate huduma hiyo nchini kote.
  Meneja wa mradi wa ya huduma ya TB kupitia teknlojia ya simu za mkononi  Dk Beatrice Mutayoba akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu hiyo akielezea namna mfumo utakavyosaidia kutambua wagonjwa kwa njia rahisi na kwuashauri kufika katika kituo cha afya kwa ajili ya kupata matibabu.
  Baadhi ya washiriki mbalimali wakiohudhuria uzinduzi wa programu ya huduma ya TB kupitia teknlojia ya simu za mkononi  uliojulikana kwa jimba TAMBUA TB.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt  Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja madaktari kutoka sehemu mbalimbali na mashirika yalityosaidia kufanikisha mradi huo.


  0 0   Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Mohammed Ally Ahmed  akisisitiza jambo kwa viongozi wa vyama vya siasa wakati wa  mkutano wa Msajili wa Vyama vya Siasa na viongozi hao mapema hii leo jijini Dar es Salaam.  

  Na Monica Laurent  

  Viongozi wa kitaifa wa vyama vya Siasa nchini wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa maslahi mapana ya taifa kuepuka kuanzisha vyama kwa maslahi binafsi.Hayo yalisemwa Jana na  Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Mhe. Mohammed Ally Ahmed wakati wa kufunga mafunzo kwa viongozi wa kitaifa ya vyama vya Siasa yaliyofanyika kwa siku mbili  katika ukumbi mdogo wa Ofisi za Bunge Septemba 19 na 20 , 2018 kwa lengo la kuwajengea uwezo viongozi hao ili kuendesha vyama vyao kama taasisi.

  “Linapotokea zuri basi tuseme hili ni zuri na linapotokea baya tuseme hili lina tatizo kwa maslahi mapana ya taifa letu, utitiri wa vyama vya siasa pekee hautasaidia taifa kama vyama hivyo havitakuwa na nguvu ya kufanya kazi ama kuonyesha uzalendo wa kuendesha taifa”. Alisisitiza Mhe. Ahmed.

  Kiongozi huyo wa vyama vya sias pia ametoa angalizo kwa jamii kuwa chama cha siasa kinapoanzishwa kiwe  ni kwa ajili ya maendeleo ya taifa kwa kuweka mstakabali mzuri wa vizazi vilivyopo na zijavyo.Mhe.Ahmed ametoa wito kwa viongozi hao kuunga mkono jitihada za Serikali kupitia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa za kuvijengea uwezo vyama hivyo,  na kuongeza kuwa mafunzo ya aina hiyo yatasaidia kubadili mawazo na mitazamo ya kiutendaji wa shughuli za vyama vya siasa nchini ili  kujielekeza katika mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kisiasa.

  Baadhi ya mada zilizotolewa nia pamoja na jinsi ya kuendesha chama kama taasisi,utaratibu wa kukagua hesabu za fedha a vyama vya siasa na mambo muhimu ambayo vyama vinapaswa kuzingatia,jinsi ya kuandaa taarifa za fedha kwa ajili ya ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali.

  Viongozi wa kitaifa wa vyama pia walipata fursa za kufahamu jinsi ya kuandaa rejista ya mali za chama na kuandika taaarifa za mali, jinsi ya kuandaa bajeti ya chama cha siasa na taarifa ya utekelezajii wake na  pia wajibu  na majukumu ya kufanya marejesho ya wadhamini RITA.

  Mafunzo hayo yalikuwa mwendelezo wa Mafunzo ambayo Ofisi ya Msajili inaendelea kuyatoa kwa vyama vya siasa ili kusaidia vyama hivyo kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa na kujiendesha kama taasisi.

  0 0


  Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akikabidhi Vyeti vya Kuhitimu Mafunzo ya masuala ya Manunuzi kwa Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Zabuni Wizara ya Madini wakikabidhi
  Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akikabidhi Vyeti vya Kuhitimu Mafunzo ya masuala ya Manunuzi kwa Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Zabuni Wizara ya Madini wakikabidhi
  Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akikabidhi Vyeti vya Kuhitimu Mafunzo ya masuala ya Manunuzi kwa Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Zabuni Wizara ya Madini wakikabidhi
  Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akikabidhi Vyeti vya Kuhitimu Mafunzo ya masuala ya Manunuzi kwa Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Zabuni Wizara ya Madini wakikabidhi
  Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Zabuni Wizara ya Madini wakiwa wakijadiliana wakati wa mafunzo kuhusu masuala ya manunuzi kwa wizara hiyo.
  Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akijadiiana jambo na Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni na Mkurugenzi w Utawala na RasilimaliWatu Issa Nchasi na Mjumbe wa Bodi na Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Athony Tarimo. Wengine ni Maafisa kutoka PPRA waliotoa mafunzo hayo.

  Na Asteria Muhozya, Morogoro

  Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amewataka Wajumbe wa Bodi ya Zabuni Wizara ya Madini kuhakikisha kwamba wizara hiyo haipati hoja kutokana na kukikukwa kwa taratibu za manunuzi baada ya wajumbe hao kupatiwa mafunzo kuhusu Sheria na Kanuni za Manunuzi ya Umma.

  Pia, wajumbe hao wametakiwa kuhakikisha wanafamu kwa weledi Sheria na Kanuni za manunuzi ili waweze kutoa maamuzi sahihi.

  Naibu Waziri Nyongo aliyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya Wajumbe wa Wizara hiyo yaliyofanyika katika ofisi za Madini Mkoa Morogoro tarehe 21 Septemba,2018.

  Naibu Waziri Nyongo alisema hitaji la kuwapatia mafunzo wajumbe hao linafuatia upya wa wizara hiyo ikiwemo wajumbe wa bodi hiyo ambao wengine wametoka katika sekta mbalimbali hivyo mafunzo hayo yatakuwa chachu ya kuzingatia sheria na kanuni za manunuzi zilizoanishwa.

  “Masuala ya manunuzi yanalalamikiwa sana kutokana na ucheleweshaji wa maamuzi. Lakini pia, manunuzi ya umma yamekuwa na matatizo kutokana na kuwepo Mikataba mibovu kwa hiyo baada ya ninyi kupatiwa mafunzo haya, sitarajii vitu kama hivi kujitokeza. Pia, Naibu Waziri Nyongo aliwataka wajumbe wa bodi kuhakikisha kuwa, mafunzo waliyoyapata yanawasaidia kuepukana na vitendo vya rushwa wakati wa kusimamia shughuli za manunuzi ya wizara.

  “Ukiiba mali ya umma kuna siku wengine watakuja na watahoji. Siku zote mali ya umma ni ya kuogopa,” alisisitiza Naibu Waziri nyongo. Naye, Mwenyekiti wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala na RasilimaliWatu Wizara ya Madini, Issa Nchasi, alisema kuwa, wakati wa mafunzo wajumbe hao walipata nafasi ya kujifunza kuhusu Sheria, Mikataba na Kanuni za Manunuzi ikiwemo kupata uzoefu wa shughuli za manunuzi na namna zinavyofanyika.

  Akizungumzia manufaa ya mafunzo, Nchasi alisema kuwa yamekuwa na manufaa makubwa kwa kuwa yatawawezesha wajumbe kutoa maamuzi sahihi ikiwemo kumshauri Afisa Masuhuli kufuata Sheria na Kanuni ili kuepuka ununuzi ambao hauzingatii sheria. Aliongeza kuwa, mafunzo hayo yalilenga kuwawezesha wajumbe kuelewa Sheria ili kufanya kazi zao kwa weledi.

  Kwa upande wake, Mkufunzi kutoka Wataalam kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Paschal Komba aliipongeza wizara ya Madini kwa kutoa mafunzo hayo kwa wajumbe wa bodi hiyo na kuelea kuwa, yatawawezesha kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria na taratibu za ununuzi wa umma.

  Mafunzo hayo yalitolewa na Wataalam kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma (PPRA)

  0 0

  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia) akifafanua jambo kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid wakati wa kikao cha kupokea maoni ya wajumbe wa Baraza hilo ya rasimu ya kanuni ya Miundombinu ya Kimkakati ya Mawasiliano, Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mtandao wa TEHAMA na mapitio ya Sera ya Taifa ya Posta, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Baraza hilo, Zanzibar.
  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Mohammed Ahmed Salum wakati wa kikao cha kupokea maoni ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ya rasimu ya kanuni ya Miundombinu ya Kimkakati ya Mawasiliano, Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mtandao wa TEHAMA na mapitio ya Sera ya Taifa ya Posta, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Baraza hilo, Zanzibar.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Hamza Hassan Juma (wa kwanza kushoto) akitoa maoni yake wakati wa kikao cha kupokea maoni ya wajumbe wa Baraza hilo ya rasimu ya kanuni ya Miundombinu ya Kimkakati ya Mawasiliano, Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mtandao wa TEHAMA na mapitio ya Sera ya Taifa ya Posta, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Baraza hilo, Zanzibar. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye na katikati ni Naibu Spika wa Baraza hilo Mhe. Mgeni Hassan Juma.
  Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakisikiliza kwa makini wasilisho na maoni ya wajumbe wa Baraza hilo wakati wa kikao cha kupokea maoni yao ya rasimu ya kanuni ya Miundombinu ya Kimkakati ya Mawasiliano, Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mtandao wa TEHAMA na mapitio ya Sera ya Taifa ya Posta kilichofanyika kwenye ukumbi wa Baraza hilo.

  Baadhi ya wakurugenzi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wakisikiliza kwa makini maoni ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar ya rasimu ya Kanuni ya Miundombinu ya Kimkakati ya Mawasiliano, Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mtandao wa TEHAMA na mapitio ya Sera ya Taifa ya Posta kilichofanyika kwenye ukumbi wa Baraza hilo.

  Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amepokea maoni ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya rasimu ya kanuni ya Miundombinu ya Kimkakati ya Mawasiliano kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ambapo kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Baraza hilo

  Nditiye amewaeleza wajumbe wa Baraza hilo kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeona ni vema iwasilishe rasimu ya kanuni hizo ili ziweze kupata maoni ya wajumbe hao kwa kuwa mawasiliano ni suala la muungano. Aidha, amefafanua kuwa wajumbe walishiriki na kutoa maoni yao wakati Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walishirikiana kutunga Sheria iliyoanzisha Shirika la Mawasiliano Tanzania na kufuta Kampuni ya Simu Tanzani ili kuiwezesha Serikali kumiliki Shirika hilo kwa asilimia 100 na liweze kujiendesha kwa faida kwa kuzingatia maslahi mapana ya taifa letu na ulinzi na usalama ambapo Shirika limeweza kutoa gawio kwa Serikali katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa Serikali.

  Mhandisi Nditiye amewashukuru wajumbe wa Baraza hilo kwa ushirikiano wao wakati wa utungaji wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ambapo Serikali imezingatia na kutekeleza maoni waliyoyatoa wakati wa utungaji wa sheria hiyo ikiwemo suala la uwakilishi wa Zanzibar kwenye Bodi ya Shirika na Ofisi Zanzibar

  Amefafanua kuwa katika kifungu cha 7 (2) (b) cha sheria ya Shirika hilo, sheria imeelekeza wazi kuwa lazima wajumbe wawili wa Bodi ya Shirika watoke Zanzibar na muundo wa Shirika umezingatia uwepo wa Ofisi ya Shirika Zanzibar badala ya kuwa na tawi tu.

  Katika hatua nyingine, Nditiye amewajulisha wajumbe wa Baraza hilo kuwa, katika kifungu cha 24 cha sheria ya Shirika hilo, inampa mamlaka Waziri mwenye dhamana kuandaa kanuni ambazo zitarahisha utekelezaji wa majukumu ya Shirika ambapo amewaeleza wajumbe kuwa wawe huru na wazi kutoa maoni yao ili kuweza kufanikisha utungaji wa Kanuni ya Miundombinu ya Kimkakati ya Mawasiliano. Kanuni hiyo itatoa maelekezo kwa Shirika ya namna ya kuendesha miundombinu ya Mawasiliano ikiwemo Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Data.

  Pia, wajumbe walipata fursa ya kutoa maoni yao kwa ajili ya Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mtandao wa TEHAMA na mapitio ya Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003 ili kuweza kuwa na sera mpya inayokwenda na wakati kutokana na mabadiliko ya ukuaji wa teknolojia. “Kwa mujibu wa Ibara ya 5 ya Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, inazitaka nchi wanachama kuwa na mashirikiano yanayohusiana na masuala ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kitamaduni na kiteknolojia ambapo itifaki hii ikiridhiwa itatuwezesha nchi yetu kuwa na ushirikiano na nchi za jirani kwenye nyanja ya mawasiliano na hivyo kurekebisha muingiliano wa mawasiliano ya wananchi wetu waishio mipakani na matumizi ya pamoja ya miundombinu ya mawasiliano na masafa,” amesema Nditiye.

  Naye Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Mohammed Ahmed Salum ameishukuru Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa utayari na ushirikiano unaoendelea katika nyanja ya masuala ya mawasiliano ambayo yanahusu muungano.

  Mhe. Salum amefafanua kuwa huu ni muendelezo na anaipongeza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa ushirikiano huu wa masuala yanayohusu muungano ambapo tangu mwaka 2016 tumekuwa tunashirikiana vizuri, sheria yoyote inaletwa kwa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Wizara yetu ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji na hatimaye Barazani. “Tunashukuru walileta sheria ya TTCL na semina ilitolewa na ikapendekezwa na kuridhiwa kuwe na wajumbe wawili kwenye Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania badala ya mmoja na sasa zimeletwa kanuni ili tuzipitie na kutoa maoni yetu ili Mhe. Waziri mwenye dhamana aweze kutunga kanuni hizi kwa kuwa ndiye mwenye dhamana,” amesema Mhe. Salum

  Naye Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Mgeni Hassan Juma ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kushirikiana na Baraza kupitia na kutoa maoni yao kuhusu sheria, kanuni na itifaki mbali mbali zinazohusu sekta ya mawasiliano na zinazogusa masuala ya mmungano. Mhe. Juma amekiri kuwa Baraza la Wawakilishi Zanzibar lina uwakilishi mzuri kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na amewataka wabunge wa Baraza kufanya vizuri zaidi katika kuwakilisha wananchi kwa kwenda kwenye maeneo yao, kupata mahitaji na changamoto zinazowakabili na kusimamia masuala yanayogusa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwa ni masuala ya muungano ili kuondoa mambo madogo madogo ambayo yanagusa muungano

  Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hamza Hassan Juma amesema kuwa sheria nyingi zilikuwa zinapitishwa Bungeni tunasikia tu, ila katika kipindi cha Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, sheria zote zinazoenda Bungeni ambazo zinahusu muungano zinafika Barazani na zinatolewa maoni na sasa yanatekelezwa.

  Pia, katika hatua nyingine, wawakilishi wa taasisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wamepata nafasi ya kutoa maoni yao kuhusu nyaraka husika baada ya kupata wasilisho linalohusu nyaraka hizo kutoka kwa watendaji wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambapo Mkurugenzi wa Mawasiliano, Mhandisi Clarence Ichwekeleza, Mkurugenzi wa TEHAMA, Munaku Mulembwa, Afisa Sheria, Eunice Masigati na Mkurugenzi Msaidizi wa Masuala ya Mtandao, Mhandisi Steven Wangwe wamewasilisha mada za nyaraka husika na kupokea maoni ya wajumbe wa Baraza na watendaji wa taasisi ili ziweze kujumuishwa na kuboresha nyaraka tajwa.


  Imetolewa na:
  Prisca J. Ulomi
  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
  Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  0 0


  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu leo akiongea na wananchi walioshiriki kwenye Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  DSC_0783Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu leo akikata utepe kuzindua kitabu cha mpango mkakati wa udhibiti wa ugonjwa wa Ebola usiingie nchini, baada ya kufanya Matembezi ya Hiyari yaliyoanzia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja na kumalizikia Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuhamasisha wananchi kujikinga na ugonjwa wa Ebola.
  DSC_2006Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Lawrence Thobias akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu, Bw. Richard Mayongela akiongea na wananchi walioshiriki Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kwa kuanzia kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja na kumalizikia kwenye Viwanja vya Karimjee.
  DSC_0608Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu (watatu kulia) leo akiongoza Matembezi ya Hiyari kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yaliyoanzia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja na kuishia Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Mohamed Kambi.
  DSC_1935Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakiwa miongoni mwa wananchi walioshiriki Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yaliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  IMG_0274Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakiwa miongoni mwa wananchi walioshiriki Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yaliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  IMG_0293
  Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu baada ya kumalizika kwa Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yaliyofanyika leo kuanzia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja na kuishia Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  taa1Wadau mbalimbali wakipiga picha mbele ya bango lenye ujumbe kuhusiana na ugonjwa wa Ebola la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), mara baada ya kumalizika kwa Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa huo usiingie nchini yaliyofanyika leo kwa kuanzia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja na kumalizikia Viwanja vya Kariamjee jijini Dar es Salaam.
  taaWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu leo akitembea mbele ya bango la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakati wa Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yaliyofanyika leo kuanzia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja na kuishia Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
  taa4
  Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) walioshiriki kwenye Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa wa Ebola usiingie nchini yaliyofanyika leo kuanzia kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja na kuishia Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu.

  Na Mwandishi Wetu
  WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeipongeza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kwa kuchukua hatua za haraka za kudhibiti ugonjwa wa Ebola usiingie nchini, imeelezwa.

  Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Ummy Mwalimu katika hotuba yake kwa wananchi walioshiriki Matembezi ya Hiyari ya kuelimisha na kuhamasisha Jamii kuzuia ugonjwa huo usiingie nchini yaliyoanzia kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja na kuishia Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, ambapo imesharipotiwa ugonjwa huo umeingia nchi jirani ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.

  Mhe. Mwalimu amesema TAA inafanya jambo jema kwa kuhakikisha wasafiri wote wanaoingia nchini kupitia viwanja vya ndege wanafanyiwa ukaguzi na kutoa taarifa za afya zao kwa wale ambao watabainika kuwa na joto la mwili lisilokuwa la kawaida.

  “Nawapongeza sana tena sana Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania kwa kuhakikisha nchi inakuwa salama bila kupata maambukizi ya ugonjwa huu wa Ebola, imeripotiwa sasa huu ugonjwa upo Kivu Kaskazini, ambapo ni karibu na nchini na Wavuvi wanakuwa na muingiliano kwa kutoka huko na kuja nchini,” amesema Mhe. Mwalimu.

  Hatahivyo, amesema pamoja na ugonjwa huo kutoingia nchini, lakini kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), tayari imeripotiwa wananchi 111 wa Kongo wamepata maambukizi na kati yao 75 sawa na asilimia 67 wamefariki, hivyo inakisiwa endapo Tanzania ikiwa na wagonjwa 100 anaweza kusababisha vifo vya watu 50.   

  “Ebola bado haujaingia nchini Tanzania, lakini ni kweli kwamba tupo katika hatari kubwa zaidi kupata ugonjwa huu, hii inatokana na mlipuko wa ugonjwa huu kuwepo katika eneo la Kivu Kaskazini na imesharipotiwa kuua watu na sisi hatupo mbali na eneo la Kivu, hivyo tusikubali ugonjwa huu kuingia nchini na tutoe elimu juu ya ugonjwa huu,” amesisitiza Mhe. Waziri Ummy Mwalimu.

  Aidha, Mhe. Mwalimu aliwaomba Viongozi wa Dini kutumia majukwaa yao katika mahubiri yao kutoa tahadhari kwa wananchi kuhusiana na ugonjwa huu wa Ebola, ambapo pia awaomba wasanii wa muziki na viongozi wa Siasa nchini kutumia majukwaa yao ili kufikisha taarifa kwa wananchi juu ya ugonjwa huu.
  Naye Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa TAA, Bw. Lawrence Thobias aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu, Bw. Richard Mayongela amesema viwanja vya ndege vimekuwa na mikakati ya muda mrefu kwa kushirikiana na Wataalamu wa Afya ya kudhibiti magonjwa ya kuambukiza ukiwemo Ebola.

  Bw. Thobias amesema sasa viwanja vyote hususan vilivyopo katika mipaka ya nchi zimefungwa mashine maalum (thermos scanner) za kutambua joto la mwili wa binadamu, na ikibainika limezidi nyuzi joto 38, abiria huyo anapelekwa katika chumba maalum na kufanyiwa mahojiano ya kina juu ya afya yake na pia abiria wanaowasili na ndege zinazofanya safari nchi jirani na Kongo nao hunawa mikono kwa dawa maalum kabla ya kutoka nje ili kuendelea na safari zao.

  “Kwa upande wetu tumeweka mikakati kamambe ili huu ugonjwa usiweze kuingia nchini, mbali na abiria kunawa kwa dawa maalum anapoingia tu ndani ya mlango wa wasafiri wanaotoka nje ya nchi, pia kuna mashine maalum (thermo scanners) ambazo zinaonesha joto la mwili wa kila abiria anapoingia kwenye lango hilo, na kimetekwa chumba maalum cha mahojiano kwa wale wanaobainika kuwa na joto la juu, na pia katika hospitali ya Temeke napo kipo chumba maalum endapo atabainika mgonjwa aliyepatikana kupitia viwanja vyetu anapelekwa huko,” amesema Bw. Thobias.

  Mbali na kuweka mashine mbalimbali kwenye viwanja vya ndege nchini, pia TAA ikiwa ni mmoja wa wadhamini imechangia Tshs. Milioni 5 kwa ajili ya kampeni ya kutoa elimu juu ya ugonjwa wa Ebola kwa wananchi.

  Ugonjwa wa Ebola unasambazwa na virusi vya Ebola na husababisha homa kali inayoweza kuambatana na kutokwa damu mdomoni, puani, masikioni, machoni na sehemu nyingine za wazi na unaenea kwa haraka, na namna ya kujikinga na ugonjwa huu ni pamoja na kuepuka kugusa damu, machozi, jasho, matapishi, kamasi, mkojo au kinyesi cha mtu mwenye dalili za ugonjwa; pia mtu hatakiwi kugusa, kuosha au kuzika maiti ya aliyekufa kwa Ebola; pia usiguse au kula wanyama kama popo, sokwe au swala wa msituni.Dalili za Ebola ni pamoja na homa kali, maumivu ya kichwa na misuli, mwili kulegea, kutapika, kuharisha, vipele na kutokwa damu maeneo mbalimbali ya mwili.

  0 0

   MKURUGENZI wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Akson, akimsikiliza Mbunge wa Busega, Dkt. Chegeni, walipokuwa wakitambulishwa, madiwani wa CCM wa Mkoa wa Mbeya walioteuliwa katika uchaguzi mdogo uliopita,  wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018, lililofanyika kwenye Uwanja wa Tandale Wilayani Rungwe mji wa Tukuyu mkoani Mbeya jana Sept 21/ 2018.
   WASANII wa Kikundi cha ngoma cha Makandana, wakishambulia jukwaa wakati wa mashindano ya ngoma katika Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018, lililofanyika kwenye Uwanja wa Tandale Wilayani Rungwe mji wa Tukuyu mkoani Mbeya jana Sept 21/ 2018.
   WASANII wa Kikundi cha ngoma cha Bagamoyo cha Wilayani Rungwe, wakishambulia jukwaa wakati wa mashindano ya ngoma katika Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018, lililofanyika kwenye Uwanja wa Tandale Wilayani Rungwe mji wa Tukuyu mkoani Mbeya jana Sept 21/ 2018. 

  WASANII wa Kikundi cha ngoma cha Zanzibar, akishambulia jukwaa wakati wa mashindano ya ngoma katika Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018, lililofanyika kwenye Uwanja wa Tandale Wilayani Rungwe mji wa Tukuyu mkoani Mbeya jana Sept 21/ 2018. (Picha na Muhidin Sufiani)

  0 0

  Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

  KATIKA hali ya kustaajabisha mkazi mmoja katika kijiji cha Magoza Wilayani Mkuranga amemuua mkewe na kumfukia.

  Imeelezwa kuwa katika  kijiji cha magoza  Kata ya Kiparang'anda Wilayani Mkuranga  Selemani Juma amemuua mkewe Bi Selina Sulubu kwa madai ya mgogoro wa mapenzi uliodumu kwa muda mrefu na kisha kumfukia kwa siri katika shamba la jirani yake.

  Tukio hilo limebainika leo baada ya siku kumi kupita tangu kufukiwa kwa mwili huo.

  Michuzi blog ilifika eneo la tukio na kushuhudia jeshi la polisi kwa kushirikiana na wataalam wa afya  kutoka hospitali ya Wilaya na wananchi wakifukua mwili wa marehemu.

  Kwa upande wake Mganga mkuu wa Hospitali ya Mkuranga Dkt. Steven Mwandambo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo  kwa kuuona mwili wa marehemu na wamekabidhi jeshi la polisi ili waweze kuendelea na hatua nyingine.

  Aidha kaka wa marehemu  bahati Mabubu amesema; baada ya kupata taarifa kwa shemeji yake kuhusu kutoroka kwa dada yake nyumbani aliamua kufunga safari kuja Mkuranga ili kumtafuta dada yake.

  Mabubu ameongeza kuwa alipofika Mkuranga katika kijiji cha magoza alibaini shemeji ya kuwa na hali ya wasiwasi,ndipo alipompeleka kituo cha polisi na kukiri kufanya mauji ya mke wake.

  Ikumbukwe kuwa ni miezi minne tu imepita tangu kutokea kwa mauaji ya nesi wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga yaliyosabishwa na wivu wa mapenzi kutoka katika wilaya ya Mkuranga.
  Polisi na wataalamu wa afya kwa kushirikiana na wananchi wakisaidiana kufukua mwili wa Selina Sulubu aliyeuwawa na mumewe katika kata ya Kiparang`anda Wilaya ya Mkuranga mkoa Pwani. (picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii)

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani mheshimiwa Kangi Lugola ameagiza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa watu wanaosambaza picha za watu waliopoteza maisha kwenye ajali ya kivuko cha MV Nyerere iliyotokea juzi Septemba 20,2018.

  Waziri Lugola ameviagiza vyombo vinavyohusika kufuatilia wanaosambaza picha hizo kwa ni kinyume cha sheria za makosa ya mtandao.

  Tangu jana kumezuka tabia kwa baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii ikiwemo whatsapp,instagram na facebook wamekuwa wakisambaza picha za watu waliofariki kwenye ajali ya kivuko cha MV Nyerere kwenye magroup na wengine kupost kwenye kurasa zao kitendo ambacho ni kinyume cha sheria,utu na maadili.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Askari wa Usalama barabarani (Trafiki),alipopata nao chai ya asubuhi mara baada ya kutoka kushiriki Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Osterybay Jijini Dar es salaam.Septemba 23,2018. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata chai ya asubuhi na baadhi ya Askari wa Usalama barabarani (Trafiki) Ikulu Jijini Dar es salaam mara baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Osterybay Jijini Dar es salaam.Septemba 23,2018. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Waziri mkuu Mama Mary Majaliwa walipoungana na waumini wengine kusali Ibada ya jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam.Septemba 23,2018.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono wa amani na mmoja wa  Masista wakati wa Ibada ya jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam.Septemba 23,2018.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipewa mkono wa pole na Paroko msaidizi Padre Batholomeo Bachoo kwa niaba ya Waumini wa Parokia hiyo kufutia ajali ya Kivuko cha Mv Nyerere iliyotokea katika Ziwa Victoria Septemba 20,2018.Wakati wa Ibada ya jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam.Septemba 23,2018.

   Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Janeth Magufuli akipewa mkono wa pole na Paroko msaidizi Padre Batholomeo Bachoo kwa niaba ya Waumini wa Parokia hiyo kufutia ajali ya Kivuko cha Mv Nyerere iliyotokea katika Ziwa Victoria Septemba 20,2018.Wakati wa Ibada ya jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam.Septemba 23,2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Paroko msaidizi Padre Asis Mendonca mara baada ya kushiriki Ibada ya jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam.Septemba 23,2018.

  PICHA NA IKULU  0 0

  *Waziri asema uwezo wa kivuko ilikuwa kubeba watu 101 lakini siku ya tukio kilibeba watu 265

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  WAZIRI wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe amesema hadi sasa idadi ya miili ya watu waliokufa kutokana na kuzama kwa kivuko cha MV.Nyerere imefikia 224.

  Pia amesema uwezo wa kivuko hicho ni kubeba watu 101 lakini kimebainika kuwa watu ambao walikuwa kwenye kivuko hicho walikuwa 265 ambayo ni kubwa ukilinganisha na uwezo wa kivuko hicho.

  Waziri Kamwelwe amesema hayo leo mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa maziko ya miili tisa ambayo imezikwa na Serikali kati ya miili 224 iliyopatikana baada ya tukio hilo.Amefafanua kati ya miili hiyo 224 ambayo imepatikana wanawake ni 126,wanaume 71.Pia watoto wa kike ni 17 na watoto wa kiume ni 10

  Pia amesema miili ambayo imetambuliwa ni waliotambuliwa ni 219 na wote wamechukuliwa na ndugu na miili ambayo bado haijatambuliwa ni watu wanne ambao hao watazikwa na Serikali leo.Ameongeza kuna miili ya watu watano ambayo hiyo itazikwa pamoja na miili ya watu wanne na kufanya jumla ya miili ambayo itazikwa leo ni tisa.

  Waziri Kamwelwe amesema miili ambayo haijatambuliwa imechukuliwa DNA na kisha kukabidhiwa kwa ndugu au vyovyote itakavyoamriwa.

  Wakati huo huo amesema kwamba baada ya kutokea kwa tukio hilo watanzania wote wamonesha ushirikiano mkubwa na kwamba michango ambayo imepatikana ni Sh.Milioni 190 na tayari wamefungua akaunti maalum ya maafa inayofahamika Mv.Nyerere.
  Baadhi ya Masanduku yenye miili ya Marehemu waliofariki kufuatia kivuko  cha MV Nyerere kupinduka na kuzama

  0 0

  * Ni katika tukio la kuzama kivuko cha MV.Nyerere, Mbunge wa Ukerewe aomba kivuko cha uhakika

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  MKUU wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema msiba huo ni mkubwa na wa kitaifa huku akieleza kuwa wananchi wamefanya kazi kubwa kwani wao ndio wamefanikisha kupata kwa watu 40 walio hai.

  Mongella amesema hayo leo mchana huu wakati akitambulisha viongozi mbalimbali kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye ameongoza maziko ya Watanzania waliopoteza maisha kutokana na tukio la kupinduka kwa kivuko cha Mv.Nyerere.

  Mkuu huyo wa Mkoa amemwambia Waziri Mkuu kwamba Septemba 20 mwaka huu saa nane mchana walipata taarifa za kuwa kivuko hicho kinazama na wao wakafika eneo la tukio saa 11 jioni.

  Amesema baada ya kufika walikuwa wananchi wa eneo hilo tayari wamefanikiwa kuokoa watu walio hai 40 na hakika wananchi hao wamefanya kazi kubwa."Watu 40 wameokolewa na wananchi wa maeneo haya.Sisi wengine wote tumeokoa mtu mmoja tu jana.Hivyo wananchi hawa wamethibitisha uwezo mkubwa na tunao watu wananchi wenye uwezo mkubwa," amesema.

  Wakati huo huo Mongella amesema kwamba tukio hilo limeacha majonzi na masikitiko makubwa lakini wanashukuru ushiriki wa makundi mbalimbali kwa namna ambavyo wameshiriki katika tukio hilo.Pia wamesema  viongozi mbalimbali nao wamefika katika eneo la tukio hilo na uwepo wao umekuwa faraja kubwa.

  "Kwa namna ambavyo watu wameshiriki katika tukio hilo ni vema tukashukuru makundi yote na si mtu mmoja mmoja," amesema Mongella.


  MBUNGE WA UKEREWE

  Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ukerewe Joseph Mkundi (Chadema) amemwambia Waziri Mkuu kwamba amejawa na simanzi kutokana na tukio hilo.Pia amesema katika maisha yake hakuwahi kushuhudia vifo vya idadi kubwa kwa mara moja kama ambavyo imetoke huku akieleza  na tukio hilo ni janga ambalo tayari limetokea.

  Amesema kutokana na  janga hilo kuna jambo la kujifunza kuhakikisha halitokei tena tukio la aina hiyo huku akiomba Watanzania kushikamana kama Taifa."Faraja ambayo tunayoweza kuipata sisi wananchi wa Ukerewe na ukanda huu ni kupata chombo ambacho kitakuwa madhubuti na kuhakikisha wananchi wa eneo hili maisha yao kuwa salama.

  " Tuwaombee marehemu wetu roho zao Mwenyezi Mungu azilaze mahala pema peponi.Amina,"amesema Mbunge huyo.

  VIONGOZI WA DINI

  Kabla ya kuipumzisha miili hiyo Katika nyumba zao za milele viongozi wa dini zote wameleza kusikitishwa na tukio hilo na kuomba dua na sala kwa Mwenyezi Mungu kutokana na tukio hilo.ia viongozi hao pamoja na kumuomba Mungu awape faraja wafiwa ambao wameondokewa na wapendwa wao wameeleza kwamba tukio limeleta masikitiko makubwa lakini wanaamini kila jambo jambo hupangwa na Mungu.

  Wamefafanua watu wamekusanyika hapo ili kushuhudia tukio kubwa la kuwasitiri wapendwa wetu ambao leo wanarudi mavumbi.Pia wamuomba Mungu awape faraja viongozi wa ngazi mbalimbali katika kipindi hiki kigumu ambacho Taifa linapitia.

  Viongozi hao wamesema wanawaombea wote walioaga dunia wasamehewe zambi zao.Wameomba Mungu aliupushe Taifa na majanga ambayo yanaweza kutokea.

  0 0
  Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akitoa neno wakati wa hafla ya kuwaaga rasmi Majaji Wastaafu wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, walioketi ni sehemu ya Majaji Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam pamoja na Divisheni walioshiriki katika hafla hiyo.
  Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akitoa neno wakati wa hafla ya kuwaaga rasmi Majaji Wastaafu wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, walioketi ni sehemu ya Majaji Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam pamoja na Divisheni walioshiriki katika hafla hiyo.
  Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu, Mhe. Sekieth Kihio akipokea zawadi kutoka kwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi, (katikati) ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Jaji Munisi.
  Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akimpatia zawadi, Jaji Mstaafu Mhe. Laurence Kaduri ikiwa ni ishara ya pongezi kwa kumaliza utumishi wa Mahakama salama.
  Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akimpatia zawadi, Mhe. Jaji Mstaafu Gadi Mjemmas
  Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akimpatia zawadi, Mhe. Jaji Mstaafu Fredrica Mgaya
  Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, Mhe. Ibrahim Mipawa akitoa neno la shukrani
  Jaji Kiongozi, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi (katikati) pamoja na baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu waliohudhuria katika hafla ya kuwaaga Majaji Wastaafu wakiwa katika picha ya pamoja na Majaji hao.
  Jaji Kiongozi, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi (katikati) pamoja na baadhi ya Majaji wengine wa Mahakama Kuu waliohudhuria katika hafla wakiwa katika picha ya pamoja na Majaji Wastaafu, wa kwanza kushoto ni Jaji Mstaafu, Mhe. Sekieth Kihio, wa pili kushoto ni Jaji Mstaafu, Mhe. Laurence Kaduri, wa pili kulia ni Jaji Mstaafu, Mhe. Fredrica Mgaya, wa kwanza kulia ni Jaji Mstaafu, Mhe. Ibrahim Mipawa. Waliosimama wa pili kulia ni Jaji Mstaafu, Mhe. Gadi Mjemmas, wa pili kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Beatrice Mutungi, wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Jaji Munisi na wa kwanza kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Ilvin Mugeta.  Na Mary Gwera, Mahakama

  JAJI Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi amewahakikishia Majaji Wastaafu kuwa Mahakama itaendelea kushirikiana nao katika masuala mbalimbali licha ya kuwa wamemaliza muda wao wa kazi.

  Mhe. Jaji Feleshi aliyasema hayo, Septemba 22 jijini Dar es Salaam, katika hafla fupi ya kuwaaga jumla ya Majaji Wastaafu tisa (9) kutoka Mahakama Kuu- Masjala Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi na Kazi.

  “Napenda kuwapongeza kwa Utumishi wenu uliotukuka kwa Mahakama hadi kufikia siku ya leo, nipende kuwahakikishia kuwa Mahakama itaendelea kuwa pamoja nanyi kwa kila hali, iwe kwa shida au raha,” alisema Jaji Kiongozi.

  Aidha; Mhe. Jaji Kiongozi aliwataka Majaji hao kutosita kushiriki katika shughuli mbalimbali za Mahakama ili kuendeleza maboresho ambayo Mahakama inakusudia kufikia kupitia Mpango Mkakati wake.

  Aliongeza kwa kuwasihi Majaji hao Wastaafu kutosita kutoa ujuzi wao kwa Majaji ambao bado wapo kwenye Utumishi wa Umma pindi wanapohitajika kutoa elimu katika Mafunzo mbalimbali yanayofanyika ndani ya Mahakama.

  Kwa upande wake, Jaji Mstaafu, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, Mhe. Fredrica Mgaya ameushukuru Uongozi wa Mahakama kwa kuwaandalia hafla hiyo kwani wamefurahi na kujisikia kuwa wao bado ni sehemu ya Wanafamilia wa Mahakama.

  Kwa ujumla Majaji hao Wastaafu kila mmoja kwa nafasi yake waliishukuru Mahakama ya Tanzania kwa kuwalea na kufanya kazi kwa ushirikiano katika kipindi chote cha utumishi wao.

  Vilevile wametoa wito kwa Watumishi wa Mahakama ambao bado wapo kazini kufanya kazi kwa bidii na kupenda kazi zao.

  Majaji Wastaafu walioagwa ni pamoja na Mhe. Sekieth Kihio, Mhe. Projestus Rugazia, Mhe. Augustine Shangwa, Mhe. Laurence Kaduri, Mhe. Gadi Mjemmas, Mhe. Fredrica Mgaya, Mhe. Ibrahim Mipawa, Mhe. Aghaton Nchimbi, na Mhe. Pelagia Khaday.

  0 0


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiendesha Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Zanzibar kichofanyika Leo katika ukumbi wa CCM Ofisi Kuu Kisiwandui Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 23/09/2018.

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiteta na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Samia Suluhu Hassan wakati wa kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Zanzibar kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akiendesha Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Zanzibar kichofanyika Leo katika ukumbi wa CCM Ofisi Kuu Kisiwandui Mjini Unguja,(kulia)Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Juma Abdalla Sadala na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Samia Suluhu Hassan (kushoto)
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Wajumbe wa Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Zanzibar kichofanyika Leo katika ukumbi wa CCM Ofisi Kuu Kisiwandui Mjini Unguja,wakisimama kwa dakika moja kuwakumbuka Wananchi waliofariki katika ajali ya Meli MV Nyerere huko Mwanza,ilioyotokea tr 20 mwezi huu, (kushoto).
  Baadhi ya Viongozi na Wajumbe wa Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akiendesha kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Juma Abdalla Sadala alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo alipohudhuria katika Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 23/09/2018.

  0 0

  Na Ismail Ngayonga-MAELEZO

  DAR ES SALAAM

  SERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo inatekeleza Programu ya Kuendeleza Sekta ya kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) ambayo ni utekelezaji wa Mpango wa Uwekezaji katika Sekta ya Kilimo Nchini (TASFIP) unaolenga kukuza kilimo kwa asilimia 6 kwa mwaka.

  Kwa kuzingatia hatua hizo, Wizara ya Kilimo imekusudia kuleta mageuzi ya kilimo kutoka mtazamo uliopo wa kilimo cha kujikimu hadi kufikia uendeshaji wa kilimo kwa mfumo wa kibiashara.

  Aidha upatikanaji wa chakula cha kutosha unategemea kwa kiasi kikubwa ongezeko la uzalishaji katika sekta ya kilimo, hususan mazao ya nafaka, ambayo upatikanaji wake hupunguza gharama za maisha kwenye chakula.

  Inaelezwa kuwa asilimia 80 ya Watanzania wote wanaishi vijijini, kati yao wakulima wadogo wanakadiriwa kufikia Milioni 20 wanaopaswa kuguswa na mageuzi ya kiuchumi kama inavyoelezwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.

  Pamoja na Tanzania kuwa rasilimali za kutosha zinazoweza kusaidia kuleta mabadiliko ya uchumi na kuinua hali za maisha ya wananchi, sekta ya kilimo inaelezwa kukabiliwa na changamoto mbalimbali.

  Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na pembejeo zisizotosheleza kama vile mbegu bora, mbolea na dawa za kilimo, mfumo wa kizamani wa uoteshaji mazao na ucheleweshaji wa maendeleo ya miundombinu kama vile, skimu za umwagiliaji, miundombinu ya masoko.

  Katika mwaka 2015/2016 makadirio ya mahitaji ya pembejeo za kilimo nchini yalikuwa tani 485,000 za mbolea, tani 60,000 za mbegu bora, miche ya chai 1,700,000, miche ya kahawa 5,000,000, viuatilifu vya korosho tani 25,000 na viuatilifu vya pamba ekapaki 1,500,000.

  Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2018/19, Waziri wa Kilimo, Dkt Charles Tizeba anasema Serikali imeendelea msukumo pia umewekwa katika kuimarisha upatikanaji wa pembejeo za kilimo ikiwemo mbegu bora na Viuatilifu nchini.

  Anasema katika mwaka 2017/18 upatikanaji wa mbegu bora ulifikia tani 51,700.51 ikilinganishwa na tani 28,278.2 za mwaka 2016/2017, ambapo tani 26,112.69 zilizalishwa nchini na tani 16,277.7 ziliagizwa kutoka nje na wafanyabiashara.

  “2018/2019, Wizara itachangia upatikanaji wa tani 40,000 za mbegu bora mbalimbali; miche bora ya chai milioni 10 na miche bora ya kahawa milioni 12; kusambaza tani 8,600 na lita 9,800 za viuatilifu” anasema Waziri Tizeba.

  Dkt. Tizeba anasema Wizara kwa kushirikiana na Taasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation itakamilisha Mfumo wa Taifa wa kuimarisha upatikanaji wa mbegu bora ikiwemo uboreshaji wa uzalishaji wa mbegu mama katika vituo vya utafiti pamoja na kujenga uwezo wa Taasisi ya Uthibiti wa Ubora wa Mbegu (TOSCI).

  Waziri Tizeba anasema Serikali kupitia Bodi ya Korosho Tanzania kwa kushirikiana na Vyama Vikuu vya Ushirika wa Korosho na Benki ya NMB imekamilisha mchakato wa uagizaji wa pembejeo za korosho ikiwemo kuingia mikataba na wazabuni ambao kwa ujumla wao wataleta salfa ya unga tani 35,000 na viuatilifu vya maji lita 520,000.

  Kilimo ni sekta muhimu katika maendeleo ya uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla hususani katika wakati huu tunapojidhatiti kufikia uchumi wa viwanda, ambapo asilimia 65 ya malighafi hutegemea mazao ya kilimo.

  Uamuzi wa Serikali wa kujenga uchumi wa Viwanda unalenga kuleta maendeleo jumuishi na endelevu kwa kutumia rasilimali zilizopo na hivyo kuchangia katika kukuza pato la taifa, kutoa nafasi za ajira na kuzalisha bidhaa bora kwa masoko ya ndani na nje ya nchi.

  Ili kufanikisha azma hiyo, ni wajibu wa Serikali kuimarisha nguvu ya uwezeshaji na uwekezaji katika kundi kubwa la wakulima wadogo waliopo vijijini.
   

older | 1 | .... | 1676 | 1677 | (Page 1678) | 1679 | 1680 | .... | 1897 | newer