Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1675 | 1676 | (Page 1677) | 1678 | 1679 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), Waziri wa kilimo akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Mradi wa utafiti na kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania hafla iliyofanyika katika ukumbi wa ESRF Jijini Dar es salaam Leo tarehe 19 Septemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
  Baadhi ya washiriki wa mkutano wa uzinduzi wa Mradi wa utafiti na kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania hafla iliyofanyika katika ukumbi wa ESRF Jijini Dar es salaam Leo tarehe 19 Septemba 2018 wakifatilia kwa umakini mkubwa hotuba ya Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), Waziri wa kilimo.
  Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), Waziri wa kilimo (kulia) akikata utepe ishara ya kuzindua Mradi wa utafiti na kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania hafla iliyofanyika katika ukumbi wa ESRF Jijini Dar es salaam Leo tarehe 19 Septemba 2018. Mwingine pichani ni Dkt Tausi Mbaga Kida, Mkurugenzi wa Taasisi ya tafiti za kiuchumi na kijamii ESRF.
  Picha ya pamoja Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) Waziri wa kilimo akiwa na washiriki wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa utafiti na kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania hafla iliyofanyika katika ukumbi wa ESRF Jijini Dar es salaam Leo tarehe 19 Septemba 2018.

  Na Mathias Canal-WK, Dar es salaam

  Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) Waziri wa kilimo, ameitaja Programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (Agricultural sector Development Programme ASDP II) kwamba italeta mageuzi makubwa katika sekta hiyo zikiwemo sekta zingine ya Mifugo na Uvuvi kwa kuongeza uzalishaji, tija na kufanya kuwa na matokeo makubwa yatakayopelekea kupungua kwa madhara ya mabadiliko ya tabia nchi.

  Dkt Tizeba ameyasema hayo Leo tarehe 19 Septemba 2018 wakati wa uzinduzi wa Mradi wa utafiti na kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika nyanja za kilimo na mfumo wa chakula nchini Tanzania hafla iliyofanyika katika ukumbi wa ESRF Jijini Dar es salaam.

  Alisema kuwa ASDP II ni Programu ya miaka 10 itakayotekelezwa kuanzia mwaka wa 2017/2018 hadi 2027/2028 katika vipindi viwili vya miaka mitano mitano. Awamu ya kwanza itaanza kutekelezwa 2017/2018 hadi 2022/2023 ambayo ni muendelezo wa awamu ya kwanza ya ASDP 1 iliyotekelezwa kuanzia mwaka 2006/2007 hadi 2013/2014.

  Alieleza kuwa Programu hiyo imezingatia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025, Mpango wa Maendeleo wa muda mrefu 2012-2021, Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano 2016-2021, Mkakati wa kuendeleza sekta ya kilimo 2015 na Mpango wa uwekezaji katika kilimo na lishe (Tanzania Agriculture and Food Security Investment Plan -TAFSIP 2011). 

  Pia alisema kuwa Wizara ya kilimo inaendelea kukuza na kulinda Maendeleo ya sekta ya kilimo yaliyo endleevu kwa kuongeza uzalishaji, kubiresha mifumo inayokwenda sambamba na tabia nchi kwa kuzingatia mabadiliko ya tabia ya nchi kwa umakini mkubwa sana kwani Tanzania ni miongoni mwa nchi chache ambazo zimefanikiwa kuendeleza Mpango mkakati wa kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi ili kwenda sambamba na Dira ya maendeleo ya Taifa 2025. 

  Alisema kuwa serikali inatambua juhudi zitakazotolewa na mradi wa utafiti wa kujenga uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya nchi katika nyanja za kilimo na Mfumo wa chakula nchini Tanzania CCRF-AFRICAP katika kuelewa mustakabali wa sekta ya kilimo.
  Mradi huo wa CCRF-AFRICAP ni mradi wa kikanda utakaojumuisha nchi nne Barani Afrika ambazo ni Tanzania, Malawi, Afrika kusini, na Zambia ambapo kwa upande wa Tanzania Mradi huo utasimamiwa na ESRF ambazo ni wawakilishi wa mtandao wa Taasisi zinazojihusisha na uchambuzi wa sera katika nyanja za chakula, kilimo, na maliasili Barani Afrika (FANRPAN) ukijumuisha watafiti katika nyanja za mifumo ya kilimo ikiwemo sayansi ya udongo, sayansi ya mimea, sayansi ya Mifugo na ikolojia, kisiasa na sayansi ya jamii.
  Kwa mujibu wa Dkt Tausi Mbaga Kida, Mkurugenzi wa Taasisi ya tafiti za kiuchumi na kijamii ESRF, alisema kuwa lengo la mradi huo ni kuainisha na kutekeleza Sera zinazotokana na uthibitisho wa kisayansi kupitia utafiti katika kuendeleza Maendeleo endelevu, uzalishaji, mifumo ya kilimo inayozingatia mabadiliko ya tabia nchi ili kuwezesha kufikia usalama wa chakula na Maendeleo ya kiuchumi.
  Mabadiliko ya tabia nchi ni miongoni mwa changamoto inayoikabili mataifa ya Afrika katika karne ya 21 kwani inakadiriwa kuwa idadi ya watu watakaokuwa hatarini kwa njaa itaongezeka maradufu Barani Afrika pia kupelekea ongezeko la ukame , kupungua kwa uzalishaji na kubadilika kwa Nyakati za hali ya hewa yatakayopelekea kupungua kwa uzalishaji wa Mazao mengi ya chakula yanayostawi sana.


  0 0

  Mwezeshaji mkaguzi wa polisi Elifuraha Kukudi akizungumza mjini Babati Mkoani Manyara kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo askari wa dawati la jinsia na watoto. 
  Mkuu wa mtandao wa askari polisi wa kike chuo cha polisi Moshi, Grace Lyimo (kulia) akiwa na wakuu wa dawati la jinsia na watoto wa wilaya za Mkoa wa Manyara kwenye mafunzo yaliyofanyika mjini Babati kwa kuandaliwa na jukwaa la Utu wa mtoto (CDF) kwa ufadhili wa shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya idadi ya watu (UNFPA). 

  Baadhi ya wakuu wa dawati la jinsia na watoto wa wilaya za Mkoa wa Manyara, wakifuatilia mafunzo yaliyotolewa na jukwaa la Utu wa mtoto (CDF) chini ya udhamini wa wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya idadi ya watu (UNFPA) Mjini Babati Mkoani Manyara.
  ………………………
  JUKWAA la Utu wa mtoto (CDF) la jijini Dar es salaam, limewajengea uwezo askari polisi wa dawati la jinsia wa Mkoa wa Manyara, juu ya namna ya kuzifanyia kazi kesi za unyanyasaji wa kijinsia kwenye maeneo yao. 

  Akizungumza mjini Babati mkoani Manyara, afisa msaidizi wa idara ya ushiriki wa wanaume na wavulana wa jukwaa la utu na mtoto (CDF) Yared Bagambilana, alisema wamekuwa wakishirikiana na polisi katika kukomesha ukatili wa watoto. Bagambilana alisema kupitia mafunzo hayo anatarajia wakuu hao wa dawati ya jinsia watafanikisha kupunguza matukio ya ukatili kwa watoto kwenye maeneo yao. 

  “Matukio ya ukeketaji yapo kwa wingi kwenye mkoa wa Manyara hivyo wakuu hawa wa dawati la jinsia watatumia mafunzo ,” alisema Bagambilana. 

  Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Grace Lyimo ambaye ni mkuu wa mtandao wa askari polisi wa kike chuo cha polisi Moshi, alisema mafunzo hayo wanawajengea uwezo zaidi wakuu hao wa dawati. 

  Lyimo alisema wamewajengea uwezo zaidi wakuu hao wa dawati namna nzuri ya kutunza takwimu za makosa yanapotokea na jinsi ya kuyashughulikia. Akifungua mafunzo hayo, mkuu wa upelelezi wa wa makosa ya jinai wa mkoa wa Manyara (RCO) Joshua Mwafulango alisema wakuu hao wa dawati watafanikisha majukumu yao zaidi kwani wapo tayari kuwapa msaada wowote watakaouhitaji.
  Mwafulambo alisema wanategemea kiwango cha ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto katika vituo vyao vya kazi utapungua baada ya mafunzo hayo. 

  Mkuu wa dawati la jinsia wa wilaya ya Simanjiro, Happy Miyeye alisema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika kushughulikia kesi zinazoletwa kwenye dawati lao. Miyeye alisema matukio ya ubakaji na ukatili kwa watoto yamekidhiri kwa jamii hivyo wanajitahidi kuhakikisha wanakomesha hayo. 

  Mafunzo hayo ya siku sita yanawashirikisha wakuu 20 wa dawati la jinsia na watoto wa wilaya za Babati, Mbulu, Simanjiro, Hanang’ na Kiteto.

  0 0   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza wananchi wa Kata ya Mauno wilayani Kondoa, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi Mkoani Dodoma, Septemba 20, 2018.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
  ……………………..

  *Akerwa na tabia ya kupokea fedha na kutopeleka vifaa, dawa

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hataki kuona tabia ya kupokea fedha na kuchelewa kupeleka vifaa inayofanywa na Bohari ya Madawa (MSD) ikiendelea.

  “MSD ninawatahadharisha wasirudie kosa la kupokea fedha na kutopeleka dawa na vifaa tiba. Ofisi zao ziko hapo Dodoma mjini, ni kwa nini mnachelewa kuleta vifaa hivyo,” amehoji.Ametoa onyo hilo leo mchana (Alhamisi, Septemba 20, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mauno, wilayani Kondoa ambako alienda kukagua ujenzi wa kituo cha afya na kuelezwa kuwa MSD imekuwa ikichelewa kuleta dawa. Waziri Mkuu jana ameanza ziara ya kikazi ya siku saba katika mkoa wa Dodoma.

  Amesema Serikali ilitoa sh. milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho cha afya na kwamba baada ya ukaguzi ameridhika na kazi inayofanyika. Hata hivyo, amemtaka Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo pamoja na madiwani wahakikishe wanatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa wodi mbili za wagonjwa wa kawaida wa kike na wa kiume.

  “Hapa mna kituo cha afya, hospitali ya wilaya iko Kondoa mjini ambako ni km.62 kutoka hapa. Tengeni fedha za kujenga hizo wodi ili watu walazwe hapahapa. Halmashauri mnao uwezo wa kujenga hizo wodi mbili. Nataka nione mnaanza na nipate taarifa kuwa mmeanza ujenzi huo,” 
  amesisitiza.

  “Mwenyekiti wa Halmashauri na madiwani kaeni na mfanye hiyo kazi. Nikisema muanze maana yake ni kuanza. Tunataka wana-Mauno watibiwe hukuhuku na hakuna haja ya kuwasumbua wananchi kwenda hadi Kondoa mjini. Mkimaliza ujenzi, mtuambie, tutaleta sh. milioni 250 za kununua vifaa vya ndani.”

  Amesema Serikali inaimarisha huduma za afya kwa kujenga zahanati na kuimarisha vituo vya afya ambapo hadi kufikia Agosti mwaka huu, jumla ya vituo vya afya 209 vilikuwa vimekwishajengwa hapa nchini.Amesema kila mwezi, Serikali inapeleka wilayani humo sh. milioni 25 kwa ajili ya ununuzi wa dawa kuanzia hospitali ya wilaya, vituo vya afya na zahanati na akawaonya waganga na wauguzi wasiziguse dawa hizo kwa sababu zimelenga kuwasaidia wananchi.

  Mapema, akizungumza na wananchi hao, Naibu Waziri wa Fedha, Dk. Ashatu Kijaji ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kondoa, aliishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuimarisha huduma za afya wilayani humo ambapo katika kipindi cha miaka mitatu, wameweza kuwa na vituop vya afya vitano.

  “Katika kipindi cha miaka 40, tulikuwa na vituo vya afya vitatu tu lakini ndani ya miaka mitatu, tumefikisha vituo vya afya vitano. Alivitaja vituo hivyo kuwa ni Mauno, Busi, Bereko, Kalamba na Thawi.Waziri Mkuu anaendelea na ziara yake wilayani Kondoa ambako atazungumza na wananchi.

  0 0


  Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi John Kijazi akizungumza katika Kikao Kazi cha siku tatu cha Makatibu Wakuu, Makatibu Tawala wa Mikoa na Manaibu Katiku Wakuu wa wizara kilichoanza jana tarehe 19 Septemba 2018 jijini Dodoma.(Picha na: Frank Shija - MAELEZO)
  Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhandisi, Balozi John Kijazi(kushoto) akiteta jambo na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzabar, Dkt. Adulhamid Yahya Mzee wakati wa Kikao Kazi cha siku tatu cha Makatibu Wakuu, Makatibu Tawala wa Mikoa na Manaibu Katiku Wakuu wa wizara kilichoanza jana tarehe 19 Septemba 2018 jijini Dodoma.
  Baadhi ya washiriki wa Kikao Kazi cha siku tatu cha Makatibu Wakuu, Makatibu Tawala wa Mikoa na Manaibu Katiku Wakuu wa wizara wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi, Mhandisi John Kijazi (hayupo pichani) wakati wa kikao hicho kilichoanza jana tarehe 19 Septemba 2018 jijini Dodoma. (Picha na: Frank Shija –MAELEZO).

  Na:Frank Mvungi- MAELEZO

  Miundombinu mipya ya Wizara na Taasisi za Serikali kuongeza ufanisi na kupunguza gharama za uendeshaji wa Serikali hali inayoongeza kasi ya kutoa huduma Bora kwa wananchi hasa wale wanyonge.

  Akizungumza wakati wa Kikao Kazi cha Makatibu Wakuu, Makatibu Tawala wa Mikoa na Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara kinachofanyika Jijini Dodoma, Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeazimia kujenga uchumi wa Viwanda utakaowanufaisha wananchi wote.

  “ Mikutano hii itakuwa ikifanyika kila mwaka baada ya kutofanyika mwaka 2016 na mwaka 2017 kutokana na zoezi lililokuwa linaendelea la kupanga upya safu ya watendaji Wakuu ndani ya Serikali na Taasisi zake katika Serikali mpya ya Awamu ya Tano, pamoja na kuboresha mifumo ya uendeshaji wa Serikali” ; Alisisitiza Balozi Kijazi.

  Akifafanua Balozi Kijazi, amesema kuwa kwakuzingatia dhamira ya Serikali ni dhahiri kuwa lengo la kufikia uchumi wa kati litafikiwa katika muda uliopangwa.

  Aliongeza kuwa, Watendaji wote Serikalini wanapaswa kusoma na kuelewa mazingira ya sasa na kutekeleza majukumu yao kulingana na mipango, maelekezo na mahitaji ya wakati huu wa Serikali ya Awamu ya Tano, na azma ya Kiongozi wetu Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Pia Balozi Kijazi aliwaasa washiriki wa Kikao Kazi hicho kuepuka tabia ya kufanya kazi kwa mazoea kama ilivyozoeleka huko nyuma kwa kuzingatia sheria , Kanuni na Taratibu za Serikali ya Awamu ya Tano kwa maslahi ya wananchi.

  Katika Kikao Kazi hicho mada mbalimbali zinawasilishwa ikiwemo ; Uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo, Matumizi ya TEHAMA Serikalini, Utawala Bora na Mapambano Dhidi ya Rushwa, Ulinzi na Usalama, Mkakati, Mwongozo na Mwelekeo kuhusu agenda ya Tanzania ya Viwanda na mifumo ya Udhibiti wa ndani Serikalini na jumuiya za Kiraia.

  Kikao Kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinafanyika Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya mikakati ya Serikali kuimarisha utendaji wa Serikali na utoaji wa huduma bora kwa wananchi hasa wanyonge ili kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kujenga Tanzania mpya.Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee.

  0 0

   MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kwakibuyu Kata ya Kipumbwi wilayani Pangani wakati wa ziara yake ambapo aliwataka kuacha kushiriki kwenye vitendo vya biashara haramu za magendo na uingizaji wa dawa za kulevya
   NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso akizungumza katika ziara hiyo ya mkuu wa mkoa
   MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah  Issa akizungumza katika ziara hiyo
   Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Pangani Hamis Mnegero akizungumza katika ziara hiyo
   Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwl Hassani Nyange akizungumza katika ziara hiyo
   Mwenyekiti wa Halmashuri ya wilaya ya Pangani  akizungumza katika ziara hiyo
   MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katika akiteta jambo na Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gipson kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa
   MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katikati akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa wakati wa ziara yake wilayani humo kushoto ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji na Mbunge wa Jimbo la Pangani  (CCM) Jumaa Aweso
   AFISA Tawala wa wilaya ya Pangani Gipson kulia akiwa na wananchi wa Kijiji
  cha Kwakibuyu kata ya Kipumbwi wakimsikiliza kwa umakini mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Kata ya Kipumbwi wilayani Pangani wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wakati wa ziara yake
   Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikilizaa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
  Sehemu ya wananchi wa Kijiji cha Kwkibuyu wilayani Pangani wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) ambao hawapo pichani wakati wa ziara ya Mkuu wa mkoa huyo


  MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella amewaonya wananchi wa Kijiji cha Kwakibuyu kata ya Kipumbwi wilayani Pangani wanaojishughulisha na uingizwaji wa dawa za kulevya ,wahamiaji haramu na biashara za magendokuacha mara moja vitendo hivyo kabla hawajakumbana na mkono wa sheria huku akiwataka wananchi kuwafichua watu hao.  Eneo la Kipumbwi limekuwa likitajwa kuwa ni miongoni mwa maeneo ambayo kumekuwa bandari bubu ambayo imekuwa ikitumika kwenye matumizi mbalimbali ikiwemo kuingiza bidhaa za magendo, wahamiaji haramu jambo
  ambalo alisema linapaswa kukomeshwa.

  Shigella aliyasema hayo jana wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali ikiwemo kuzungumza na wananchi kwenye mikutano ya hadhara wilayani Pangani ambapo alisema Bandari hiyo bubu zimekuwa tatizo
  kwenye kutumika kwenye matumizi ambayo yasiyokuwa salama.

  “Hapa Kipumbwi mmekuwa na tatizo kubwa la bandari bubu ambayo imekuwa kutumika kwenye matumizi yasiyosalama biashara haramu ya kupitisha wahamiaji, dawa za kulevya ama kusafirisha wahamiaji haramu lakini wapo  baadhi yenu wanadhamira njema ya kuleta bidhaa kutoka maeneo mengine  ikiwemo mkoani Tanga wakati mwengine kivuko kikiwa kimefungwa
  kinawaongeze gharama watumiaji wa mwisho”

  Mkuu huyo wa mkoa wa Tanga alisema pia yapo baadhi ya maombi ya muda mrefu ambayo viongozi wa wilaya hiyo walikwisha kuwasilisha akiwemo Mbunge wa Jimbo hilo Jumaa Aweso ambaye ni Naibu Waziri wa Maji na
  Umwagiliaji na Mkuu wao wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa.

  “Hivyo wataona uwezekano wa kuanzishwa mchakao wa eneo hilo kuwa bandari ndogo na sasa wameanza mchakato kuifanya Kipumbwi iwe bandari ndogo na Meneja wa Bandari ya Tanga alifika kufanya mkutano na DC kuanza mchakato wa kuirasimisha”Alisema

  Alisema baada ya kumalizika mchakao wa kuanzishwa bandari ndogo eneo hilo wananchi wapaswa kuhakikisha wanawafichua wale wanaopitisha bidhaa haramu za magendo na kuichafua sura ya kipumbwi kwa kupitisha
  dawa za kulevya.

  “Kwani tukifanya hivyo tutakuwa tumepiga hatua na dhamira ya kuanzishwa bandari hiyo itakuwa imekamilika lakini ikibainika eneo hilo bado wanapitisha wahamiaji haramu, bidhaa za magendo na dawa za
  kulevya hawatasita kuifunga”Alisema RC Shigella.

  Naye kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso alisema katika kipindi chake cha miaka miwili amesaidia Jimbo hilo ambalo lina kata 14 kupata umeme wa uhakika ambao ndio wilaya ya kwanza Tanzania ambayo kuna umeme kwenye karibia ya maeneo yote isipokuwa machache tu.

  Alisema pia Jimbo hilo miaka ya nyumba lilikuwa likipokea bajeti ya maji milioni 500 mwaka mzima lakini hivi sasa imepanda na kufiikia Bilioni 2 hali ambayo ni jambo jema kwao kwa ustawi wa sekta hiyo muhimu.

  “Pamoja na mambo hayo waswahili wanasema lakini niwaambie mpango tulionao kukabiliana na changamoto ya maji tutachimba visima virefu zaidi ya kiwanja cha mpira Kipumbwi na Sakura kuhakikisha wananchi

  wanaondokana na tatizo la maji”Alisema.

  0 0

   WASANII wa kikundi cha ngoma cha Ilopa, wakishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 lililoanza jana Sept 20/2018 katika Uwanja wa tandale mji wa Tukuyu Wilayani Rungwe.
  MKURUGENZI wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Akson, akimtunza pesa msanii wa muziki wa kizazi kipya Hip Hop akapela, Meshack Ngemela, aliyetoa burudani katika Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 lililoanza jana Sept 20/2018 katika Uwanja wa tandale mji wa Tukuyu Wilayani Rungwe. 

   MSANII wa muziki wa kizazi kipya Hip Hop akapela, Meshack Ngemela, akighani mashairi ya akapela huku akipongezwa na Machief wa Mkoa wa Mbeya waliohudhuria katika Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 lililoanza jana Sept 20/2018 katika Uwanja wa tandale mji wa Tukuyu Wilayani Rungwe.
   WASANII wa kikundi cha ngoma cha Katembo, wakishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 lililoanza jana Sept 20/2018 katika Uwanja wa tandale mji wa Tukuyu Wilayani Rungwe.

   Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hip Hop akapela, Meshack Ngemela, akitoa burudani katika Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 lililoanza jana Sept 20/2018 katika Uwanja wa tandale mji wa Tukuyu Wilayani Rungwe.
   WASANII wa kikundi cha ngoma cha Songela, wakishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 lililoanza jana Sept 20/2018 katika Uwanja wa tandale mji wa Tukuyu Wilayani Rungwe.

   WASANII wa kikundi cha ngoma cha Lupaso, wakishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 lililoanza jana Sept 20/2018 katika Uwanja wa tandale mji wa Tukuyu Wilayani Rungwe.
   MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Dogo Ditto, akiimba jukwaani na Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Akson, wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 lililoanza jana Sept 20/2018 katika Uwanja wa tandale mji wa Tukuyu Wilayani Rungwe.
   WASANII wa kikundi cha ngoma cha Kawetele, wakishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 lililoanza jana Sept 20/2018 katika Uwanja wa tandale mji wa Tukuyu Wilayani Rungwe.

  MKURUGENZI wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania, Dkt. Tulia Akson akisalimiana na waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harison Mwakyembe.

  (Picha na Muhidin Sufiani)

  0 0

  Mwenyekiti wa Jumuiya za Tawalaza Mikoa (ALAT) Gulamhafeez Mukadamu (kulia) akipokea mfano wa hundi ya Sh milioni 100 kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Kati - Nsolo Mlozi, hundi hiyo iliyotolewa na Benki ya NMB Nchini kama udhamini wa mkutano Mkuu wa Mwaka wa ALAT unaotarajiwa kufanyika kuanzia wiki ijayo Jijini Dodoma.

  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Angelina Mabula akizungumza kwenye ufunguzi wa maonyesho ya Nyumba day yaliyofanyika jana viwanja vya tawi la NMB Kambarage Jijini Dodoma. Benki ya NMB imeandaa siku ya Nyumba maalum kwaajili ya kuwakutanisha wateja wa mikopo ya nyumba wa NMB na makampuni ya ujenzi wa nyumba ambayo benki hiyo inamkataba nayo.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Angelina Mabula akitembelea mabanda ya Wadau wa vifaa vya ujenzi kwenye maonyesho ya nyumba day yaliyoandaliwa na Benki ya Nmb Jijini Dodoma jana. Benki ya NMB imeandaa siku ya Nyumba maalum kwaajili ya kuwakutanisha wateja wa mikopo ya nyumba wa NMB na makampuni ya ujenzi wa nyumba ambayo benki hiyo inamkataba nayo.
  Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja kutoka benki ya NMB, Omary Mtiga (kulia) akizungumza katika tukio hilo. 

  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Angelina Mabula akitembelea mabanda ya Wadau wa vifaa vya ujenzi kwenye maonyesho ya nyumba day yaliyoandaliwa na Benki ya Nmb Jijini Dodoma jana. Benki ya NMB imeandaa siku ya Nyumba maalum kwaajili ya kuwakutanisha wateja wa mikopo ya nyumba wa NMB na makampuni ya ujenzi wa nyumba ambayo benki hiyo inamkataba nayo.

  NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anastazia Mabula amezitaka taasisi za fedha pamoja na waendelezaji milki binafsi kushirikiana na Serikali ili kutatua changamoto iliyopo ya uhaba wa nyumba na makazi nchini.


  Akihutubia katika ufunguzi wa maonyesho ya nyumba yaliyoandaliwa na benki ya NMB jana na kufanyika katika viwanja vya Kambarage jijini Dodoma, Mabula amesema serikali inauhaba wa nyumba za watumishi hususani baada ya serikali kuhamia jijini Dodoma.


  Amesemakuwa Tanzania inaupungufu wa nyumba 3,000,000, hivyo ili kutatua changamoto hiyo, kunatakiwa kujenga nyumba zaidi ya laki mbili kila mwaka hivyo hawana budi kuwashirikisha wadau kikamilifu kama benki ya NMB ilikuziba pengo hilo.


  Akizungumzia upande wa Dodoma, Mabula amesema mahitaji ni kuwa na nyumba zaidi ya elfu 23 lakini zilizopo ni nyumba 1329 tuhivyo maonyesho hayo yaliyowakutanisha wateja wa benki ya NMB, waendelezaji milki pamoja na wauzaji wa vifaa vya ujenzi yana tija kubwa kwani yanalenga kuiunga mkono serikali katika suala la maendeleo.


  “Makazi bora ni haki ya kila mwananchi, na tukiri kuwa tuna changamoto ya uhaba wa nyumba nchini, lakini kupitia maonyesho haya tunaweza kukutana na wadau mbalimbali kama vile taasisi za fedha waendelezaji miliki na pia wauzaji wa vifaavya ujenzi ili kumaliza changamoto hiyo,” Alisema Mabula.


  Amesema Serikali imeshaweka mazingira wezeshi yanayoruhusu taasisi za serikali pamoja na waendelezaji milki binafsi kushiriki katika kuzalisha nyumba ambazo wananchi wanaweza kununua kupitia mikopo inayotolewa na benki za biashara hivyo kuzitaka benki hizo kutoa mikopo kwa riba nafuu ambayo hata mwananchi wa kipato cha chini ataweza kuimudu.


  “Taasisi za fedha ziangalie viwango vya riba, tusiwaumize wananchi, lakini kwa upande wa wadau wengine naomba msogeze huduma zetu karibu na jamii, sambamba na kujenga nyumba kwa kuzingatia mahitaji ya walaji, kuna wa chini, wa kati na wa juu, wote muwape huduma kulingana na halizao,” Alisisita Waziri huyo.


  Naye Meneja wa NMB Kanda ya Kati - Nsolo Mlozi amesema lengo la maonyesho hayo ya sikumbili ni kuwakutanisha wateja wa benki hiyo pamoja wadau mbalimbali wa nyumba ili kuweza kutatua changamoto ya uhaba wa nyumba na makazi iliyopo kwa sasa kwa kuzingatia kuwa sekta hiyo inakuwa kwa kasi.


   “NMB tumeona hii ni nafasi ya kuhakikisha tuna uwezo wa kuwapa mikopo wateja lakini pia tuwalete karibu na wauzaji wabidhaa mbalimbali kwenye sekta hii ili wateja waweze kuona na kulinganisha,…hii ni katika ushindani wa kibiashara ili wateja waweze kupata kitu bora,” Alisema Mlozi.


  Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja kutoka benki ya NMB, Omary Mtiga amewataka wateja wa benki hiyo kutumia fursa hiyo kwani wanatoa mikopo rahisi na yenye masharti nafuu na muda wa kurejesha ni mrefu.


  Amesema tayari wameshatoa mkopo wa zaidi ya shilingi Bilioni 13 nchi nzima, na kwa mkoa wa Dodoma wametoa mkopo wa zaidi ya shilingi milioni 700 na wanaendelea kutoa mikopo hiyo ili kuiunga mkono serikali katika azma yakustawisha makao makuu ya Serikali.

  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Angelina Mabula akitembelea mabanda ya Wadau wa vifaa vya ujenzi kwenye maonyesho ya nyumba day yaliyoandaliwa na Benki ya Nmb Jijini Dodoma jana. Benki ya NMB imeandaa siku ya Nyumba maalum kwaajili ya kuwakutanisha wateja wa mikopo ya nyumba wa NMB na makampuni ya ujenzi wa nyumba ambayo benki hiyo inamkataba nayo.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Angelina Mabula akitembelea mabanda ya Wadau wa vifaa vya ujenzi kwenye maonyesho ya nyumba day yaliyoandaliwa na Benki ya Nmb Jijini Dodoma jana. Benki ya NMB imeandaa siku ya Nyumba maalum kwaajili ya kuwakutanisha wateja wa mikopo ya nyumba wa NMB na makampuni ya ujenzi wa nyumba ambayo benki hiyo inamkataba nayo.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi - Angelina Mabula akitembelea mabanda ya Wadau wa vifaa vya ujenzi kwenye maonyesho ya nyumba day yaliyoandaliwa na Benki ya Nmb Jijini Dodoma jana. Benki ya NMB imeandaa siku ya Nyumba maalum kwaajili ya kuwakutanisha wateja wa mikopo ya nyumba wa NMB na makampuni ya ujenzi wa nyumba ambayo benki hiyo inamkataba nayo.

  0 0


   Mkuu wa Utawala na Rasilimali Watu wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF),  Bw. Deodatus Sagamiko akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi wa ESRF Dk Tausi Kida wakati wa Mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
   Mchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Lorah Basolile Madete akitoa neno la ufunguzi wakati wa Mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
   Mratibu wa Maabara inayoshughulikia mabadiliko kuelekea miji Tanzania (TULab) kutoka ESRF, Mussa Martine akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
   Bw. Anton Cartwright wa Kituo cha Afrika cha miji kutoka nchini Afrika Kusini akiwasilisha Muhtasari wa tafiti tatu zilizofanyika chini ya Maabara inayoshughulikia mabadiliko kuelekea miji Tanzania (TULab)  na kuongoza majadiliano kuhusu athari za kisera katika tathmini ya kitaifa ya mabadiliko kuelekea miji (National Urbanization Transition Assessment -NUTA) wakati wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
   Yash Ramkolowan wa DNA Economics kutoka Afrika Kusini akiwasilisha Utafiti wa kuoanisha athari za kiuchumi kwa kuangalia njia mbili zinazotumika Tanzania kuelekea uchumi wa kati wa viwanda wakati wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
   Gemma Todd kutoka Ifakara Health Institute (IHI), akiwasilisha matokeo ya awali ya utafiti wa mipango miji wakati wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
   Mratibu wa Maabara inayoshughulikia mabadiliko kuelekea miji Tanzania (TULab) kutoka ESRF, Reshian W. Kanyatila akielezea masharti ya ushiriki katika shindano la utoaji huduma katika majiji.
   Mtafiti Msaidizi na Mratibu wa Miradi wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Bw. Emmanuel Njavike (katikati) akiwasilisha waliyojadili katika kikundi kazi wakati wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jana jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya washiriki wakitoa maoni wakati wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jana jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wataalam walioshiriki mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jana jijini Dar es Salaam.
  Mchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Lorah Basolile Madete (kushoto), Mshehereshaji wa mkutano ambaye pia ni Mtafiti Mshiriki wa ESRF, Dr. Jane Mpapalike (katikati) pamoja na Bw. Anton Cartwright wa Kituo cha Afrika cha miji kutoka nchini Afrika Kusini wakijadiliana jambo wakati wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
  Msanii wa Bongo Flava, Beka Flava akitoa burudani ya wimbo maalum wakati wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
  Picha ya pamoja


  IMEELEZWA kuwa katika mazingira ya sasa ya kuipeleka Tanzania katika uchumi wa kati kwa kuwa na viwanda ni lazima taifa litakuwa na mabadiliko katika makazi na kwamba miji mingi itachipuka.
  Aidha serikali inapotekeleza mpango wake wa pili wa maendeleo  2016/17-2020/21 katika mpango wa muda mrefu wa maendeleo kwa lengo la kuwezesha mabadiliko ya kiuchumi kwa maendeleo ya watu uwepo wa miji ni wa lazima.
  Aidha mazingira duni ya maisha katika vijiji kunafanya watu kuhamia katika maeneo yenye shughuli mbalimbali na hivyo kukuza miji iliyopo.
  Hayo yalisemwa na Dk Lorah Basolile Madete, Mchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha kwenye mkutano wa mkutano wa 5 wa jukwaa la ukuaji wa miji Tanzania (Tanzania Urbanisation Laboratory - TULab) ulioambatana na uwasilishaji wa tafiti tatu zilizofanywa na TUlab kuanzia mwaka jana.
  Pia alisema tofauti kubwa ya kipato iliyopo vijijini na mijini inafanya maeneo ya jirani na vijiji kubadilika na kuanza kuchukua muonekano wa miji.
  “Ndio kusema ni lazima kujiandaa kwa mabadiliko hayo na kuwa na  mpangilio wa kudhibiti ukuaji wa miji, kinyume chake Tanzania haitaweza kuvuna faida katika uchumi, kijamii na kimazingira kama miji itakua ghafla bila mipango mathubuti” alisema Dk Madete.
  Katika mkutano huo ilielezwa kuwa kudhibiti miji ni kitu muhimu ikiwa mataifa yanataka kuwa na maendeleo endelevu ya kiuchumi na ustawi wa jamii.
  Miji hiyo inatakiwa kupangwa na kukua kwa mujibu wa makubaliano ya dunia kama  yale ya Paris na maendeleo endelevu yaliyokubaliwa na Umoja wa Mataifa.
  Pia makubaliano mengine yanayotakiwa kuzingatiwa ni New Urban Agenda, Ajenda ya maendeleo ya Afrika ya 2063, Mikataba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na ule wa Ushirikiano wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
  Kwa kutekeleza makubaliano hayo Tanzania itakuwa inajiweka sawa katika uendelezaji wa miji yake katika hali ambayo inaleta tija na kuongeza ufanisi kwa yale yanayofanyika katika mji.
  Katika mpango wa pili wa Maendeleo serikali ya Tanzania imesema wazi kwamba inakuwa na miji iliyopangwa na inayotoa huduma kwa ufanisi kama ya utunzaji wa mazingira, uondoaji wa taka na maji taka, mambo ya usafirishaji na nishati safi ya kuaminika.
  Hata hivyo imeelezwa kuwa kazi ya kuendeleza miji haiwezi kufanywa na serikali pekee bali na wadau wengine ambao wanatambua thamani ya upangaji miji.
  Katika suala la ushirikiano ndilo linafanya uwepo wa Jukwaa la Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) kuwa la muhimu ili kuwa na uhakika wa maendeleo ya miji kwa kuisaidia Serikali kufanya maamuzi yenye uhakika na tija.
  TULab ilianzishwa Agosti 2017 na Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na  ESRF na Coalition for Urban Transitions (CUT) na kufanya tafiti tatu zilizowasilishwa na Bw. Anton Cartwright wa Kituo cha Afrika cha Miji, Afrika Kusini.
  Bw. Anton aliwasilisha  Muhtasari wa tafiti tatu zilizofanyika chini ya Jukwaa hilo linaloshughulikia mabadiliko kuelekea miji bora Tanzania au kwa ufupi TULab  na jinsi tafiti hizo zitakavyosaidia kuandaa mwongozo wa ukuaji bora wa miji Tanzania (National Urbanisation Roadmap).
  Naye Bw. Yash Ramkolowan  kutoka  Afrika Kusini aliwasilisha Utafiti utakao angalia uhusiano kati ya viwanda na ukuaji wa miji Tanzania huku Gemma Todd kutoka Ifakara Health Institute (IHI) aliwasilisha matokeo ya awali ya utafiti wa mipango miji.
  Naye Mratibu wa TULab. Reshian W. Kanyatila, alizungumzia Shindano la Utoaji Huduma Bunifu zitakazosaidia kuboresha Jiji la Dar es salaam na masharti ya jinsi ya kushiriki katika shindano hilo.
  Awali akifungua mkutano kwa niaba ya Mkurugenzi wa ESRF Bw. Deodatus Sagamiko alisema kwamba tangu mwaka jana kuanzishwa kwa TUlab, tafiti tatu zimefanyika ambazo zinafungua ukurasa wa kuanza uandaaji wa mwongozo wa ukuaji bora wa miji Tanzania. Bw. Deodatus Sagamiko, Mkuu wa Utawala na Raslimali Watu wa ESRF, alielezea umuhimu wa tafiti hizo na haja ya kuongeza utafiti mwingine ili kukamilisha maandalizi ya mwongozo huo.
  Kutokana na hatua iliyofikiwa TULab inafanya utafiti unaohusisha maendeleo ya viwanda na ukuaji wa miji. Pia TULab inaangalia uwezekano wa kuendesha shindano la ubunifu katika utoaji huduma kwa jiji la Dar es Salaam kabla mwongozo wa ukuaji bora wa miji kuzinduliwa hapo mwakani.

  0 0

  Mratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania Mkoani Tanga TAWLA Latifa Ayoub akisisitiza jambo wakati wa mdahalo wa wadau wa masuala la ardhi mkoani Tanga leo mjini Tanga kuhusu changamoto zinazowakabili wanawake kwenye kumiliki ardhi uliofanyika leo kwenye ukumbi wa YDC Jijini Tanga ukihusisha wadau kutoka maeneo mbalimbali ulioandaliwa na chama hicho Mratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania Mkoani Tanga TAWLA Latifa Ayoub kulia akisisitiza jambo wakati wa mdahalo wa wadau wa masuala la ardhi mkoani Tanga leo mjini Tanga.kuhusu changamoto zinazowakabili wanawake kwenye kumiliki ardhi kushoto ni Mwanasheria wa TAWLA Mkoani Tanga Mwanaidi Kombo ambapo mdahalo huo uliandaliwa na chama hichoMwanasheria wa TAWLA Mkoani Tanga Mwanaidi Kombo akisisitiza jambo kwenye mdahalo huo Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba Tanga Doris Wilson Mangwe akizungumza katika mdahalo huo MWANASHERIA wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza mkoani Tanga katika Sigisbert Akwilini akiwa na wadau wengine wakifuatilia mdahalo huo ambao uliandaliwa na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) mkoani Tanga Madiwani wa Kata za Chumbangeni Saida Gadafi CCM) kushoto akiwa na Diwani wa Kata ya Majengo (CUF) Suleimani Mbaruku wakifuatilia mdahalo huo MWANASHERIA wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza mkoani Tanga Sigisbert Akwilini akichangia kwenye mdahalo huo Afisa Mipango wa wilaya ya Muheza mkoani Tanga Rehema Akida akizungumza katika mdahalo huo Afisa Mtendaji wa Kata ya Mabokweni Salim Mdoe akizungumza katika mdahalo huo Afisa Mtendaji wa Kata ya Masiwani Jijini Tanga Sheria Salame akizungumza katika mdahalo huo
  Baadhi ya wadau wa mdahalo huo wakizungumza Mwansiti Bashiru kutoka kata ya Mbaramo wilayani Muheza akizungumza katika mdahalo huo
  Diwani wa Kata ya Majengo (CUF) Suleimani Mbaruku

  0 0

  MKURUGENZI wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Akson, akimtunza pesa msanii wa muziki wa kizazi kipya Hip Hop akapela, Meshack Ngemela, aliyetoa burudani katika Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 lililoanza jana Sept 20/2018 katika Uwanja wa tandale mji wa Tukuyu Wilayani Rungwe.
   WASANII wa kikundi cha ngoma cha Songela, wakishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 lililoanza jana Sept 20/2018 katika Uwanja wa tandale mji wa Tukuyu Wilayani Rungwe. 
   WASANII wa kikundi cha ngoma cha Lupaso, wakishambulia jukwaa wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 lililoanza jana Sept 20/2018 katika Uwanja wa tandale mji wa Tukuyu Wilayani Rungwe.
   MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Dogo Ditto, akiimba jukwaani na Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Akson, wakati wa Tamasha la Tulia Traditional Dances Festival 2018 lililoanza jana Sept 20/2018 katika Uwanja wa tandale mji wa Tukuyu Wilayani Rungwe.(Picha na Muhidin Sufiani)


  0 0

  Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS Bw. Daudi Mbaga akiielezea mifuko ya uwekezaji itolewayo na UTT AMIS ni suluhisho la maisha baada ya kustaafu kwa wastaafu watarajiwa wa wizara ya fedha kutoka mikoa mbalimbali katika semina iliyofanyika katika ukumbi wa wizara ya fedha Morogoro.
  Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo.

  Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo.

  Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo.  0 0

   MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kwakibuyu Kata ya Kipumbwi wilayani Pangani wakati wa ziara yake ambapo aliwataka kuacha kushiriki kwenye vitendo vya biashara haramu za magendo na uingizaji wa dawa za kulevya
   NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso akizungumza katika ziara hiyo ya mkuu wa mkoa
   MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah  Issa akizungumza katika ziara hiyo
   Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Pangani Hamis Mnegero akizungumza katika ziara hiyo
   Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwl Hassani Nyange akizungumza katika ziara hiyo
   Mwenyekiti wa Halmashuri ya wilaya ya Pangani  akizungumza katika ziara hiyo
   MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katika akiteta jambo na Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gipson kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa
   MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katikati akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa wakati wa ziara yake wilayani humo kushoto ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji na Mbunge wa Jimbo la Pangani  (CCM) Jumaa Aweso
   AFISA Tawala wa wilaya ya Pangani Gipson kulia akiwa na wananchi wa Kijiji
  cha Kwakibuyu kata ya Kipumbwi wakimsikiliza kwa umakini mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella Wananchi kutoka maeneo mbalimbali Kata ya Kipumbwi wilayani Pangani wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wakati wa ziara yake
   Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikilizaa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
  Sehemu ya wananchi wa Kijiji cha Kwkibuyu wilayani Pangani wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) ambao hawapo pichani wakati wa ziara ya Mkuu wa mkoa huyo

  MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella amewaonya wananchi wa Kijiji cha Kwakibuyu kata ya Kipumbwi wilayani Pangani wanaojishughulisha na uingizwaji wa dawa za kulevya ,wahamiaji haramu na biashara za magendokuacha mara moja vitendo hivyo kabla hawajakumbana na mkono wa sheria huku akiwataka wananchi kuwafichua watu hao.


  Eneo la Kipumbwi limekuwa likitajwa kuwa ni miongoni mwa maeneo ambayo kumekuwa bandari bubu ambayo imekuwa ikitumika kwenye matumizi mbalimbali ikiwemo kuingiza bidhaa za magendo, wahamiaji haramu jambo
  ambalo alisema linapaswa kukomeshwa.

  Shigella aliyasema hayo jana wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali ikiwemo kuzungumza na wananchi kwenye mikutano ya hadhara wilayani Pangani ambapo alisema Bandari hiyo bubu zimekuwa tatizo
  kwenye kutumika kwenye matumizi ambayo yasiyokuwa salama.

  “Hapa Kipumbwi mmekuwa na tatizo kubwa la bandari bubu ambayo imekuwa kutumika kwenye matumizi yasiyosalama biashara haramu ya kupitisha wahamiaji, dawa za kulevya ama kusafirisha wahamiaji haramu lakini wapo  baadhi yenu wanadhamira njema ya kuleta bidhaa kutoka maeneo mengine  ikiwemo mkoani Tanga wakati mwengine kivuko kikiwa kimefungwa kinawaongeze gharama watumiaji wa mwisho”

  Mkuu huyo wa mkoa wa Tanga alisema pia yapo baadhi ya maombi ya muda mrefu ambayo viongozi wa wilaya hiyo walikwisha kuwasilisha akiwemo Mbunge wa Jimbo hilo Jumaa Aweso ambaye ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji na Mkuu wao wa wilaya ya Pangani Zainabu Issa.

  “Hivyo wataona uwezekano wa kuanzishwa mchakao wa eneo hilo kuwa bandari ndogo na sasa wameanza mchakato kuifanya Kipumbwi iwe bandari ndogo na Meneja wa Bandari ya Tanga alifika kufanya mkutano na DC kuanza mchakato wa kuirasimisha”Alisema

  Alisema baada ya kumalizika mchakao wa kuanzishwa bandari ndogo eneo hilo wananchi wapaswa kuhakikisha wanawafichua wale wanaopitisha bidhaa haramu za magendo na kuichafua sura ya kipumbwi kwa kupitisha
  dawa za kulevya.

  “Kwani tukifanya hivyo tutakuwa tumepiga hatua na dhamira ya kuanzishwa bandari hiyo itakuwa imekamilika lakini ikibainika eneo hilo bado wanapitisha wahamiaji haramu, bidhaa za magendo na dawa za
  kulevya hawatasita kuifunga”Alisema RC Shigella.

  Naye kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso alisema katika kipindi chake cha miaka miwili amesaidia Jimbo hilo ambalo lina kata 14 kupata umeme wa uhakika ambao ndio wilaya ya kwanza Tanzania ambayo kuna umeme kwenye karibia ya maeneo yote isipokuwa machache tu.

  Alisema pia Jimbo hilo miaka ya nyumba lilikuwa likipokea bajeti ya maji milioni 500 mwaka mzima lakini hivi sasa imepanda na kufiikia Bilioni 2 hali ambayo ni jambo jema kwao kwa ustawi wa sekta hiyo muhimu.

  “Pamoja na mambo hayo waswahili wanasema lakini niwaambie mpango tulionao kukabiliana na changamoto ya maji tutachimba visima virefu zaidi ya kiwanja cha mpira Kipumbwi na Sakura kuhakikisha wananchi
  wanaondokana na tatizo la maji”Alisema.

  0 0

  Uongozi wa Benki ya NBC umetembelea Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu yenye lengo la kuendeleza na kukuza uhusiano mzuri uliopo baina ya Benki na shirika hilo.

  Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Bwana Theobald Sabi katika mazungumzo alisema benki hiyo ni miongoni mwa taasisi ambayo serikali imeweka hisa zake na inajivunia kufanya kazi na NSSF,kwani alisema Benki yake inaendeshwa kisasa zaidi ambapo katika kuhakikisha wanahudumia wananchi kwa haraka NBC wana huduma ya “mobile banking” inayoweza kuwafikia wananchi wengi waliopo vijijini wakiwemo wastaafu wa NSSF.

  Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa NSSF Bwana William Erio aliishukuru NBC kwa kuifanya NSSF kuwa mteja wake mkubwa zaidi katika huduma za kibenki na kuwashukuru kwa kuwa tayari kutoa ushauri wa kitaalamu utakaohitajika na Shirika kwa sasa katika boresha huduma zao.

  Hata hivyo Bwana Erio aliwahakikishia uongozi wa NBC kwamba ushirikiano uliopo utaendelea kuimarika chini ya uongozi wake na alissitiza kuhakikisha mifumo ya fedha za wananchama inaendelea kuwa salama na kutumika kwa maendeleo ya Taifa. Pia alishukuru NBC kwa kuendelea kutoa riba ya asilimia tano kwenye akaunti ya makusaanyo kutoka kwa wanachama wa NSSF.

  NBC imekuwa Benki ya nne kuweza kutembelea katika Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambapo benki nyingine ni pamoja na CRDB,NMB na UBA ambazo wote kwa pamoja wamekutana na NSSF na kupanga namna ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara.
  Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF na ujumbe wake (kushoto) akiwa na ujumbe wa Menejimenti ya Benki ya Taifa ya Biashara nchini NBC(kulia) ulioongozwa na Mkurugenzi mtendaji Theobald Sabi wakifurahia jambo kwenye mazungumzo yao yaliyofanyika katika makoa makuu ya NSSF jijini Dar es salaam ambapo kwa pamoja wamekubaliana kuendeleza mahusiano yao ya kibiashara.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) , Bwana William Erio( katikati) akiwa na Menejimenti ya Benki ya Taifa ya Biashara,kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Theobald Sabi na wajumbe nane wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mazungumzo makuu ya NSSF jijini Dar es salaam.(Watatu kulia ni Mkurugenzi wa Fedha wa NSSF Bwana Gambamala Luchunga na wa kwanza kushoto ni Meneja kiongozi wa Masoko na Uhusiano wa NSSF Bi.Lulu Mengele.)

  0 0


  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker akizungumza


  Na Mwandishi Wetu, Morogoro

  SERIKALI mkoani Morogoro imewahimiza Wafanyabiashara wakubwa eneo hilo kukitumia Kituo cha Biashara kilichofunguliwa na Benki ya NMB ili kutambua fursa zilizopo katika kituo hicho pamoja na kuunganishwa na masoko ya ndani na nje hatua itakayo saidia kukuza uchumi wa mkoa huo.

  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Kebwe Steven Kebwe alisema hayo wakati akizindua kituo hicho cha kibiashara mkoani Morogoro kilichoanzishwa na Benki ya NMB kwa lengo la kuwasaidia wafanyabiashara wa mkoa huo.

  Katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo, alisema NMB imeamua kuanzisha kituo hicho cha kibiashara baada ya Mkoa wa Morogoro kuwa na fursa nyingi za kiuchumi ikiwemo shughuli za kilimo, uchimbaji madini na masuala ya kiutalii.

  Alisema kuwa NMB kupitia fursa hizo imeona iwasaidia Wafanyabiashara wa Morogoro kwa kuanzishia kituo maalumu ambacho licha ya kupata elimu na kuunganishwa na masoko ya ndani na nje pia watapatiwa huduma anuai za mikopo.

  Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker alisema kituo cha Biashara cha Morogoro ni kituo cha kumi nchini na kimeanzishwa mahususi kwa ajili ya Wafanyabiashara wa Mkoa wa Morogoro waweze kukuza uchumi wao.

  Alisema kuwa kuanzishwa kwa kituo hicho kumetokana na kuwepo kwa fursa nyingi ikiwemo viwanda vya sukari vya kilombero na Mtibwa pamoja na fursa za uwepo wa migodi ya madini na shughuli za utalii ambapo kama wafanyabiashara watazitumia ipasavyo basi wataweza kukuza uchumi wa mkoa huo.

  Mkurugenzi huyo alisema Benki ya NMB imekuwa ikiiunga mkono Serikali katika jitihada zake mbalimbali ikiwemo kusaidia kukusanya kodi zake na sasa, kuelekea uchumi wa viwanda imeamua kuwasaidia Wafanyabiashara kwa kuanzishia kituo chao maalumu ambapo watakutana na maofisa wa Benki hiyo kuweza kupata ushauri wa kibiashara na kuunganishwa na klabu 35 zenye jumla ya wanachama 2000 wenye uzoefu wa biashara na masoko ya ndani na nje ya nchini.

  Naye Mkuu wa kitengo cha Biashara NMB Makao makuu, Donatus Richard, alisema Benki hiyo inajivunia kuwaona Wafanyabiashara waliochukua mikopo ya chini lakini leo wamekuwa matajiri wakubwa baada ya kupata ushauri katika vituo tisa vya kibishara vilivyopo katika mikoa mbalimbali na kutaka wafanyabiashara wa Morogoro kuchangamkia fulsa hiyo.

  Uzinduzi wa kituo hicho cha kibiashara umekwenda sambamba na Benki hiyo kutoa msaada wa madawati yenye thamani ya sh milioni 10 kwa shule za sekondari za Lupanga na Kilakala zilizopo Manispaa ya Morogoro.

  0 0

  Na Stella Kalinga, Simiyu

  Waziri wa nishati Dkt Medard Kalemani amemuondoa Meneja wa TANESCO wilaya ya Meatu mkoani Simiyu Bw.Amos  Mtae katika nafasi ya umeneja baada ya kushindwa kusimamia usambazaji wa umeme kupitia Mradi wa Umeme vijijini (REA) wilayani humo na amemwagiza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO kumpangia kazi nyingine.

  Waziri KALEMANI amechukua hatua hiyo katika mkutano wa hadhara mjini Meatu  akiwa katika ziara yake ya kukagua  kazi zinazofanywa na wakandarasi wa mradi wa Umeme vijijini REA awamu ya tatu Septemba 20, 2018, ambapo anaanzia katika uzinduzi wa mradi wa umeme  katika ofisi ya kijiji cha Dakama wilaya ya Meatu.

  Dkt. Kalemani ameoneshwa kutoridhishwa na kasi ya mkandarasi anayesambaza umeme wilayani Meatu ambaye ni kampuni ya White City, kutokana na kutokuonekana katika vituo na kutokuwa na vifaa vya kutosha na vituo vya kutosha.

  “Kasi ya mkandarasi hapa ni mbovu niliteegemea nione wakandarasai wanachakarika maana kote nilikotoka nimekuta wanachakarika, pili nilitegemea nione yadi ya vifaa vya wakandarasi wetu”

  “Huyu meneja ndiye msimamizi wa wakandarasi, namuuliza anasema hajui leo wakandarasi wako wapi sasa anasimamia nini? Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO pokea maelekezo, kuanzia sasa huyu Meneja wa TANESCO Wilaya mtoe, weka Meneja mwingine kuanzia kesho hapa, wananchi wanataka umeme hapa” alisema Dkt. Kalemani.

  Katika hatua nyingine Dkt. Kalemani amewahakikishia wananchi wa vijiji 36 vya wilaya ya  MEATU kupata umeme kupitia Mradi wa Umeme Vijijini (REA) Awamu ya tatu na akawasisitiza kuwa umeme utakapowafikia wautumie kwa ajili ya maendeleo.
   Aliyekuwa Meneja wa Meneja wa TANESCO wilaya ya Meatu mkoani Simiyu Bw.Amos  Mtae (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani (wa tatu kulia), wakati wa ziara yake wilayani humo Septemba 20, 2018.
    Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Umeme wa REA Awamu ya Tatu katika Kijiji cha Dakama wilayani Meatu mkoani Simiyu, Septemba 20, 2018.
  Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akiwaonesha wananchi wa Kata ya  Mwamishali kifaa cha Umeme kiitwacho UMETA , alipozungumza nao wakati wa ziarayake wilayani Meatu mkoani Simiyu, Septemba 20, 2018.
   Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani(kulia) akiteta jambo na Mkuu wa  Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa ziara yake wilayani Meatu Mkoani Simiyu, Septemba 20, 2018.
  Baadhi ya wananchi wa Kata ya Mwamishali wilayani Meatu wakishangilia baada ya Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani kuwatangazia kuwa vijiji vyote katika wilaya yao vitapata umeme kupitia mradi waWakala wa Nishati  Vijijini (REA) Awamu ya tatu, baada ya uzinduzi wa zoezi hilo katika Kijiji cha Dakama wilayani Meatu, Septemba 20,2018.

  0 0


  Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd (anayekabidhi) pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo akimkabidhi Mtendaji wa Soko la Samaki Feri, Mkuu Hanje (anayepokea kulia) vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi katika soko hilo. Wafanyakazi wa NMB leo wamejitolea kufanya usafi katika soko hilo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya usafi.
  Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd (anayekabidhi) pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo akimkabidhi Mtendaji wa Soko la Samaki Feri, Mkuu Hanje (anayepokea kulia) vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi katika soko hilo. Wafanyakazi wa NMB leo wamejitolea kufanya usafi katika soko hilo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya usafi.
  Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd (anayekabidhi) pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo akimkabidhi Mtendaji wa Soko la Samaki Feri, Mkuu Hanje (anayepokea kulia) vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi katika soko hilo. Wafanyakazi wa NMB leo wamejitolea kufanya usafi katika soko hilo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya usafi.
  Wafanyakazi wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam wakishiriki kufanya usafi katika soko la Feri lililopo jijini Dar es Salaam.
  Wafanyakazi wa Benki ya NMB Mkoa wa Dodoma wakitoa msaada kwenye wodi ya akinamama Kituo cha Afya cha Makole cha jijini Dodoma walipofika hapo mwisho wa wiki kufanya usafi pamoja na kutoa misaada ya vitu mbalimbali.
  Wafanyakazi wa Benki ya NMB Mkoa wa Dodoma wakitoa msaada kwenye wodi ya akinamama Kituo cha Afya cha Makole cha jijini Dodoma walipofika hapo mwisho wa wiki kufanya usafi pamoja na kutoa misaada ya vitu mbalimbali.
  Wafanyakazi wa Benki ya NMB Mkoa wa Dodoma wakitoa msaada kwenye wodi ya akinamama Kituo cha Afya cha Makole cha jijini Dodoma walipofika hapo mwisho wa wiki kufanya usafi pamoja na kutoa misaada ya vitu mbalimbali.
  Wafanyakazi wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam wakishiriki kufanya usafi katika ufukwe wa soko la Feri lililopo jijini Dar es Salaam.
  Wafanyakazi wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam wakishiriki kufanya usafi katika eneo la soko la Feri lililopo jijini Dar es Salaam.
  Wafanyakazi wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam wakishiriki kufanya usafi katika ufukwe wa soko la Feri lililopo jijini Dar es Salaam.
  Wafanyakazi wa Benki ya NMB Makao Makuu jijini Dar es Salaam wakijitolea kufanya usafi eneo la Coco Beach Dar es Salaam.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB Makao Makuu jijini Dar es Salaam wakijitolea kufanya usafi eneo la Coco Beach Dar es Salaam.
  Wafanyakazi wa Benki ya NMB mkoani Kyela Mkoa wa Mbeya wakishiriki kufanya usafi katika eneo la kituo cha mabasi kuungana na jamii.

  WAFANYAKAZI wa Benki ya NMB Tanzania jana walijitokeza kufanya usafi pamoja na jamii maeneo mbalimbali Tanzania Bara na Visiwani pamoja na kutoa msaada wa vitu kwa wahitaji na vifaa vya kufanyia usafi katika baadhi ya maeneo.

  Kwa jijini Dar es Salaam wafanyakazi hao wakiongozwa na viongozi waandamizi wa benki hiyo walifanya usafi eneo la Coco Beach pamoja na Soko la Samaki la Feri kwa kushirikiana na wananchi waliojitokeza kufanya usafi kwenye maadhimisho ya usafi duniani.

  Hata hivyo mbali na kufanya usafi katika Soko la Feri walitoa msaada wa vifaa vya kufanyia usafi katika soko hilo, ikiwa ni kuhamasisha usafi kwa jamii na kuunga mkono shughuli hizo ambazo ni muhimu kwa jamii yoyote.

  Akikabidhi vifaa vya kufanyia usafi Soko la Feri, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd alisema huo ni utaratibu wa kawaida wa benki hiyo kujitolea ama msaada au kushiriki moja kwa moja katika shughuli za kijamii ili kujenga ushirikiano kwa jamii wanayoihudumia.

  Alisema Soko la Feri linahudumia watu mbalimbali ambao ni wateja wa Benki hiyo hivyo wana kila sababu kusaidia kuboresha huduma katika soko hilo. Vifaa alivyokabidhi kwa uongozi wa Soko hilo mara baada ya kuwasili ni pamoja na mifagio, reki, makoleo, mifuko maalum ya kuhifadhia na kuzolea taka na vifaa vya kujikinga wakati wa kufanya usafi.

  Wakati zoezi hilo likifanyika Dar es Salaam na mikoa mbalimbali pia wafanyakazi wa Benki hiyo walifanya usafi maeneo mbalimbali pamoja na kutoa misaada kwa wahitaji hasa wagonjwa hospitalini. miko unga mkonopamoja na wafanyakazi wa benki hiyo akimkabidhi Mtendaji wa Soko la Samaki Feri, Mkuu Hanje vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi katika soko hilo.

  Mkoani Dodoma wafanyakazi wa benki hiyo mbalimna kufanya usafi walitembelea wodi ya akinamama Kituo cha Afya cha Makole na kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa kituoni hapo. Mkoani Mbeya wafanyakazi walifanya usafi katika vituo vya mabasi pamoja a eneo la Kasumulo mpaka wa Tanzania na Malawi.  Wafanyakazi wa Benki ya NMB mkoani Kyela Mkoa wa Mbeya wakishiriki kufanya usafi katika eneo la kituo cha mabasi kuungana na jamii.


  Wafanyakazi wa Benki ya NMB mkoani Mbeya eneo la Kasumulo mpakani mwa Tanzania na Malawi wakishiriki kufanya usafi kuungana na jamii.

  Wafanyakazi wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam wakishiriki kufanya usafi katika ufukwe wa soko la Feri lililopo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na Veronica Kazimoto

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaendelea kutoa elimu ya maadili na namna bora ya kuhudumia wateja kwa watumishi wake nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi hao na kuwaongezea weledi katika majukumu yao ya kila siku.

  Akiwasilisha mada kuhusu Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma kwa Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania katika ofisi ya TRA Moshi mkoani Kilimanjaro, Afisa Maadili Mwandamizi wa mamlaka hiyo Adelaida Rweikiza amesema kuwa  ni wajibu wa watumishi wote wa TRA kuwahudumia wateja kwa usawa na kwa kiwango cha hali ya juu.

  "Ni wajibu wetu sisi watumishi wa TRA kuhakikisha tunatoa huduma bora pamoja na kutumia lugha nzuri kila tunapowahudumia wateja wetu," alisema Rwikiza.

  Rweikiza ameongeza kuwa, maadili katika Utumishi wa Umma  ni jambo la msingi hivyo amewasisitiza watumishi hao kuwa waadilifu na kuepuka vitendo vya rushwa na mienendo mibaya ambayo inaweza kuharibu taswira ya TRA.

  Naye, mmoja wa watumishi hao ambaye ni Afisa wa Kodi Robert Mlay amefurahishwa na kitendo cha Mamlaka ya Mapato Tanzania kutoa elimu kwa watumishi wake na kufafanua kuwa, elimu hiyo itawasaidia katika kuongeza ufanisi na kutimiza malengo ya mamlaka.

  "Nimejisikia vizuri sana kupata elimu hii ya maadili na namna bora ya kuwahudumia wateja kwasababu itatusaidia sisi kama watumishi wa TRA kutoa huduma kwa haki bila upendeleo wowote," alieleza Mlay.
   Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kilimanjaro Msafiri Mbibo akizungumza wakati wa utoaji elimu kwa wafanyakazi wa TRA Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro  iliyofanyika leo kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi hao ili waendelee kutoa huduma bora na stahiki kwa wateja wao.
    Afisa Maadili Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Adelaida Rweikiza akiwasilisha mada kuhusu Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma wakati wa utoaji elimu kwa wafanyakazi wa TRA Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro  iliyofanyika leo kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi hao ili waendelee kutoa huduma bora na stahiki kwa wateja wao.
    Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Diana Masalla akijadiliana jambo na Afisa Kodi Mwandamizi wa mamlaka hiyo Shaban Makumlo wakati wa utoaji elimu kwa wafanyakazi wa TRA Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro  iliyofanyika leo kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi hao ili waendelee kutoa huduma bora na stahiki kwa wateja wao.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wakisikiliza kwa makini mada kuhusu Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma wakati wa utoaji elimu kwa wafanyakazi hao iliyofanyika leo kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi hao ili waendelee kutoa huduma bora na stahiki kwa wateja wao


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke.

  Pamoja na mambo mengine Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke alimpa taarifa Makamu wa Rais juu ya ziara ya Mwanamfalme William wa Uingereza, atakayewasili nchini wiki ijayo kwa ziara yake ya siku tatu yenye lengo la kujifunza mambo ya uhifadhi wa wanyamapori kama sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa Dunia unaohusu masuala ya Uhifadhi wa Wanyamapori utakaofanyika London, Uingereza mwezi Oktoba. 

  Aidha Balozi Cooke alimjulisha Mhe. Makamu wa Rais utekelezaji wa makubaliano mbalimbali yaliyofikiwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi za Jumuiya ya Madola uliofanyika Aprili 2018, jijini London, Uingereza.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(kulia) akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke leo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(kulia) akimsikiliza  Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke(kushoto) alipokuwa anafanya mazungumzo naye leo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.  
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke leo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mshindi wa droo ya kwanza wa promosheni ya Shinda Zaidi na SportPesa inayoendeshwa na kampuni ya kubashiri Tanzania SportPesa amepatikana leo Ijumaa 21, Septemba 2018.Ntale Lusalula Rajabu (21) ambaye pia ni dereva bodaboda mkazi wa Mwera, Pangani ameweka rekodi kwa kufungua dimba na kuwa mshindi wa kwanza kwa kushinda bajaji mpya kutoka SportPesa.
  Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumtangaza mshindi huyo Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas alisema “Kupitia promosheni ya kwanza kuliyoifanya mwaka jana tulitoa bajaji 100 na tumekuwa tukiwafatilia washindi wetu na kusema ukweli masiha yao si ya kuigiza tena, ni maisha halisi, bora zaidi na wanawe kujikimu kimaisha mfano waliokuwa wanapitia changamoto ya kuwapeleka watoto shuleni kutokana na ada ama vifaa vya shule wamefanikisha hilo, na waliokuwa wanapata changamoto kuendesha familia zao kwa sasa wanaendelea vizuri.”


  Baada ya sisi kuona kwamba tumewasaidia familia zaidi ya 100 na Tanzania tunaishi familia nyingi tumeona turudishe tena shindano kama hili ili na leo tumefanya droo ya kwanza na mshindi ametoka sehemu za Mwera Mkoa wa Tanga wilaya ya Pangani. Hii maana yake ni kwamba wanaoshiriki kucheza na SportPesa ambapo pia ni burudani”Hii inatutia moyo sisi kama kampuni kwamba promosheni yetu inasikika na inajulikana sehemu kubwa ya nchi na watu wa aina tofauti na hata washindi tuliowapata kwenye promosheni iliyopita asilimia kubwa walipatikana kutoka mikoani”
  Safari hii mteja wa SportPesa anapaswa kuweka ubashiri wake na moja kwa moja ataingia kwenye droo ya kuwania bajaji mpya”.Mtumiaji wa mitandao yoyote ya simu anaweza kucheza kupitia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupiga *150*87# kwa USSD, APP, njia ya mtandao(WEBSITE) na kupitia ujumbe mfupi yaani SMS.

  0 0   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Skuli mpya Sekondari ya Kinuni Jimbo la Pangawe Wilaya ya Magharibi”B” Mkoa wa Mjini Magharibi,sambamba na Skuli 9 za Sekondari za Zanzibar sherehe zilizofanyika leo,akiwepo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pemba Juma,[Picha na Ikulu.] 21/09/2018.
  DSC_6117
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimsikiliza Mkandarasi wa Kampuni ya Ujenzi ya Salem Construction LTD Nd,Aziz M.Qurban (katikati) alipokuwa akitoa maelezo baada ya kuweka  jiwe la msingi ujenzi wa Skuli mpya Sekondari ya Kinuni Jimbo la Pangawe Wilaya ya Magharibi”B” Mkoa wa Mjini Magharibi leo ,sambamba na Skuli 9 za Sekondari za Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 21/09/2018.
  DSC_6416
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa kitoa hutuba yake kwa Wananchi na Wanafunzi leo katika sherehe ya  uwekaji wa   jiwe la msingi ujenzi wa Skuli mpya Sekondari ya Kinuni Jimbo la Pangawe Wilaya ya Magharibi”B” Mkoa wa Mjini Magharibi,sambamba na Skuli 9 za Sekondari za Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 21/09/2018.
  DSC_6388
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akitoa hutuba yake kwa Wananchi na Wanafunzi   katika sherehe ya  uwekaji wa   jiwe la msingi ujenzi wa Skuli mpya Sekondari ya Kinuni Jimbo la Pangawe Wilaya ya Magharibi”B” Mkoa wa Mjini Magharibi,sherehe zilizofanyika leo sambamba na Skuli 9 za Sekondari za Zanzibar,(kulia) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma(kushoto)Waziri Kiomgozi Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Kijito Upele Mhe.Shamsi Vuai Nahodha na Naibu katibu Mkuu CCM Zanzibar Dk.Juma Abdala Sadala(wa pili kushoto),[Picha na Ikulu.] 21/09/2018. 
  DSC_6430
  Baadhi ya Wanafunzi waliohudhuria katika sherehe ya uwekaji wa   jiwe la msingi ujenzi wa Skuli mpya Sekondari ya Kinuni Jimbo la Pangawe Wilaya ya Magharibi”B” Mkoa wa Mjini Magharibi,sambamba na Skuli 9 za Sekondari za Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake kwa   Wanafunzi hao leo katika sherehe Skuli hapo, [Picha na Ikulu.] 21/09/2018.
  DSC_6220
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono  Wananchi na Wanafunzi mara baada ya kuweka   jiwe la msingi ujenzi wa Skuli mpya Sekondari ya Kinuni Jimbo la Pangawe Wilaya ya Magharibi”B” Mkoa wa Mjini Magharibi,sherehe zilizofanyika leo sambamba na Skuli 9 za Sekondari za Zanzibar,(katikati) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pemba Juma,[Picha na Ikulu.] 21/09/2018.
  DSC_6046
  Miongoni mwa madarasa mapya ya Skuli ya Sekondari ya Kinuni  Wilaya ya Magharibi”B” Mkoa wa Mjini Magharibi,yaliyowekwajiwe la msingi na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)  sherehe zilizofanyika leo sambamba na Skuli 9 za Sekondari za Zanzibar.
  DSC_6054
  Miongoni mwa madarasa mapya ya Skuli ya Sekondari ya Kinuni  Wilaya ya Magharibi”B” Mkoa wa Mjini Magharibi,yaliyowekwajiwe la msingi na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)  sherehe zilizofanyika leo sambamba na Skuli 9 za Sekondari za Zanzibar.

  NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein amesema mafanikio yaliyopatikana katika Sekta ya Elimu nchini yanatokana na Utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020.
  Kauli hiyo ameitoa wakati akiweka jiwe la msingi katika Skuli ya Sekondari ya Kinuni iliyopo Wilaya ya Magharibi ‘’B’’ Unguja, amesema ujenzi wa skuli hiyo ya Ghorofa ambayo ni ya kisasa ni hatua kubwa ya kimaendeleo katika sekta ya elimu.

  Alisema CCM kupitia Ilani yake imeahadi kuimarisha Sekta ya Elimu kwa kuimarisha miundombinu ya upatikanaji wa elimu ikiwemo kujenga majengo ya kisasa yanayoendana na kasi ya maendeleo katika zama za sasa.
  Alibainisha kuwa Serikali ya awamu ya saba inaendeleza kwa vitendo falsafa ya elimu bila ya malipo iliyoasisiwa na Marehemu Mzee Abeid Aman Karume kwa lengo la kukuza kiwango cha elimu.

  Alisema serikali ya ASP ilitangaza elimu bure kwa lengo la kuwakomboa watoto wa Waafrika waliokoseshwa fursa ya elimu kwa makusudi na utawala uliokuwa ukitawala kabla ya Mapinduzi ya mwaka 1964.Dk.Shein alisema pamoja na maendeleo yanayopatikana katika sekta za elimu bado zipo changamoto zinazoendelea kutatuliwa zikiwemo upungufu wa madarasa, madawati pamoja na upungufu wa walimu hasa wa masomo ya Sayansi.

  Alisema Zanzibar kwa sasa imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo katika sekta ya elimu ikilinganishwa na kabla ya Mapinduzi kwani na skuli za msingi 62 na skuli za sekondari nne lakini kwa sasa idadi imekuwa ni kubwa hadi hatua ya kuwa na Vyuo vikuu vinavyozalisha wataalamu wa kada tofauti kila mwaka.

  Alisema serikali inawasomesha walimu wa masomo ya Sayansi kupitia Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA) ili watakapohitimu masomo yao wafundishe katika skuli mbali mbali za msingi na sekondari kwa lengo la kumaliza tatizo la kutofaulu masomo ya Sayansi kutokana na upungufu wa walimu kwa baadhi ya Skuli.
  Pamoja na hayo alieleza kuwa katika juhudi za kutatua changamoto ya upungufu wa madawati serikali imeagiza Madawati 22,000 kutoka nchini China,  yatakayogawiwa katika Skuli zenye changamoto hiyo nchi nzima.

  “Elimu ndio msingi wa maendeleo ya mwanadamu yeyote na ndio maana baada ya waasisi wetu kufanya Mapinduzi ya Mwaka 1964, kwa lengo la kuondosha vitendo vya ubaguzi na kuwapatia elimu vijana wa makundi yote bila ubaguzi.”, alisema Dk. Shein.Dk.Shein alipiga marufuku ya tabia ya kuchangishwa fedha kwa wanafunzi na kueleza kwamba mwalimu au kiongozi yeyote atakayebainika kufanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

  Pia ameziagiza Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar kujenga barabara ya lami ya Kinuni ndani inayofika katika Skuli hiyo.  
  Akizungumza Waziri wa Elimu Zanzibar  Riziki Pembe Juma, alisema Wizara hiyo inaendelea na mikakati endelevu ya kufanya mageuzi makubwa ya kimaendeleo katika sekta ya elimu nchini.

  Waziri Riziki alieleza kuwa katika Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 Serikali imeahidi kujenga skuli 10 za Ghorofa na kwa sasa tayari tisa zinajengwa ambapo skuli ya kumi nayo itaanza kujengwa siku za hivi karibuni.Awali akizungumza Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Zanzibar  Dkt. Idrissa Muslim Hija amesema ujenzi wa skuli hiyo mpya ya Sekondari ya Kinuni ni miongoni mwa Skuli Tisa zinazojengwa nchini ambapo kwa upande wa Unguja zinajengwa tano na kwa upande wa Pemba zinajengwa nne.

  Alisema Skuli hizo zinajengwa kwa ushirikiano wa karibu baina ya SMZ na wadau wa maendeleo ambapo jumla ya Dola milioni 10.2 zimetolewa na shirika la Opec Fund for internation Development kati ya hizo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa asilimia 11.17 na zaidi ya bilioni 2.8 zitatumika katika ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Kinuni.

  Pamoja na hayo alisema Skuli ya Kinuni itakuwa ya Ghorofa moja yenye Madarasa 14, Maabara tatu, Maktaba moja, Ofisi za Walimu pamoja na miundombinu ya Watu wenye ulemavu.Dkt. Idrissa alifafanua kwamba lengo la ujenzi wa Skuli hizo ni kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani ili wapate mazingira rafiki ya kujifunza na kufaulu vizuri katika mitihani.
  Akizitaja skuli tisa zinazojengwa kupitia mradi huo Unguja ni Skuli za Sekondari Kinuni, Fuoni, Mwembe shauri, Chumbuni na Bububu kwa upande wa Pemba ni Skuli za Wale,mwambe, Kizimbani na Micheweni.

  Uwekaji wa Jiwe la msingi katika skuli ya Kinuni ni miongoni mwa maadhimisho ya sherehe za miaka 54 ya Elimu bila malipo Zanzibar, na Skuli zote tisa zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi katika sherehe za kilele cha Maadhimisho ya miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar  Januari 12, mwaka 2019.

older | 1 | .... | 1675 | 1676 | (Page 1677) | 1678 | 1679 | .... | 1898 | newer