Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

TADB Board meets African Development Bank Delegation

0
0



Board Chairperson, Madam Rosebud Kurwijila insists on something while talking with members of the visiting delegation AFDB (not in picture), during a joint meeting between TADB and AFDB.
IMG_6162
AFDB’s Chief Financial Sector Development Officer, Grace Kyokunda (second left) elaborates something during a joint meeting between TADB and AFDB. Others in picture are AFDB’s Senior Investment Officer, Trade Finance, Mkola Tambwe-Mlima (left), TADB’s, Acting Managing Director, Mr. Japhet Justine (right) and second right is Bank’s Head of Legal Service, Neema Christina John.
IMG_6163
TADB’s Acting Managing Director, Mr. Japhet Justine makes a point during a joint meeting between TADB and AFDB. The meeting held at TADB’s Board Room, Dar es Salaam.
IMG_6164
AFDB’s Senior Investment Officer, Trade Finance, Mkola Tambwe-Mlima (left) talks during the meeting with TADB’s Board of Directors. Looking on are AFDB’s Chief Financial Sector Development Officer, Grace Kyokunda (centre) and TADB’s Head of Legal Service, Neema Christina John.
IMG_6160
TADB’s Board Chairperson, Madam Rosebud Kurwijila (centre) chairs a joint meeting between TADB and AFDB. The meeting held at TADB’s Board Room, Dar es Salaam.
IMG_6165 (1)
The delegation from African Development Bank (AFDB) having a group photo with TADB’s Board of Directors and Bank’s management.
The Tanzania Agricultural Development Bank’s Board of Directors has met with the delegation from African Development Bank (AFDB), which is in official engagements pertaining to AFDB’s projects supervision in the country.
During the visit the delegation met with TADB’s Board Chairperson, Madam Rosebud Kurwijila, board members and management team of the Bank, which was led by Acting Managing Director, Mr. Japhet Justine.
The delegation was led by AFDB’s Chief Financial Sector Development Officer, Grace Kyokunda.

NAIBU WAZIRI ULEGA AKAGUA UJENZI WA MACHINJIO YA NG’OMBE MKOANI LINDI UNAOGHARIMU ZAIDI YA BIL.1

0
0


 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (mwenye miwani), akimsikiliza Kaimu Afisa Mifugo wa Manispaa ya Lindi, Fadhili Chamasi (kushoto), wakati akikagua ujenzi wa machinjio ya ng’ombe utakaogharimu zaidi ya bilioni moja katika eneo la  Ngongo mkoani Lindi jana katika ziara yake mkoani Lindi. PICHA: MPIGAPICHA WETU
IMG_6196
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (mwenye miwani), akimsikiliza Kaimu Afisa Mifugo wa Manispaa ya Lindi, Fadhili Chamasi (kushoto), wakati akikagua ujenzi wa machinjio ya ng’ombe utakaogharimu zaidi ya bilioni moja katika eneo la  Ngongo mkoani Lindi jana katika ziara yake mkoani Lindi. PICHA: MPIGAPICHA WETU
IMG_6165
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (mwenye miwani), wakati akikagua ujenzi wa machinjio ya ng’ombe utakaogharimu zaidi ya bilioni moja katika eneo la  Ngongo mkoani Lindi jana katika ziara yake mkoani Lindi.
IMG_6183
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (mwenye miwani), wakati akikagua ujenzi wa machinjio ya ng’ombe utakaogharimu zaidi ya bilioni moja katika eneo la  Ngongo mkoani Lindi jana katika ziara yake mkoani Lindi.

Bikosports yampa bonasi ya sh milioni 5 mkazi wa Kigamboni

0
0



Msemaji wa BIKOSPORTS Tanzania, Jeff Lea kulia, akikabidhi hundi ya sh Milioni 5 kwa mshiriki wa bahati nasibu ya kubashiri matokeo ya michezo ya mpira wa miguu, Salum Juma wa pili kutoa kulia, aliyepewa bonasi ya kiasi hicho baada ya kubashiri mechi 11 badala ya 13 ambayo ndio droo kubwa ya sh milioni 97 hali iliyowavutia biko sports kumpa bonasi hiyo kama sehemu ya kuwajali wateja wao. Wengine ni Maulid Kitenge Balozi wa Bikosports pamoja na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Saleh wakati kushoto kwake ni Meneja Uendeshaji wa Bikosports Tanzania Lucas Kiangi.

MKAZI wa Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Salum Juma, ameibuka kidedea baada ya kukabidhiwa Sh Milioni 5 kutoka kampuni ya michezo ya kubashiri matokeo ya bikosports, baada ya mdau huyo wa michezo ya kubahatisha kutabiri michezo 11 ya mpira wa miguu duniani, jambo lililowavutia Bikosports na kuamua kumpa bonasi kama sehemu ya kuwajali wachezaji wa bahati nasibu yao.

Akizungumza katika Mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Biko sports, Jeff Lea alisema kitendo cha shabiki huyo kubashiri michezo 11 kimewafanya waone haja ya kumpa bonasi, akiamini kuwa haitawavunja nguvu wasahiriki wao badala yake itawapa mwamko katika kushiriki mbio za kuwania Sh Milioni 97 kwa mtu atakayeibuka shujaa wa kubashiri michezo 13 kama droo yao kubwa inavyotaka.

Leya alisema licha ya wadau mbalimbali kuendelea kuvuna fedha mbalimbali kwa kubashiri na Kampuni yao ambayo namba ya kampuni ni 101010, ambapo mchezo huo unaweza kuchezwa kwa kutuma jamvi kwa *149*89# bila kusahau kwa kuingia kwenye mtandao wao moja kwa moja kujionea mpangilio mzima wa mchezo wao unaoweza kuchezwa bila kuwa na akaunti huku ushindi ukipatikana moja kwa moja kwenye simu ya mkononi.

“Biko Sports tunawajali sana wateja wetu ndio maana leo tumeamua kwa dhati kabisa kumpa bonasi ya Sh Milioni tano ndugu yetu Juma kwa sababu amejitahidi kwa kubashiri michezo 11, akishindwa miwili tu ili avune Sh Milioni 97 kutoka kwetu, ambapo bikosports ina machaguo Zaidi ya 125.

“Biko Sports ni rahisi kubashiri na kushinda bila kusahau jinsi tunavyojali wateja, hivyo kwa pamoja tunaamini watanzania wataendelea kubashiri kwakupitia kampuni yetu kwa sababu tumeboresha mno huduma zetu na fedha zetu zinalipwa muda mfupi tu baada ya kufanikiwa kushinda kwenye jamvi husika,” Alisema.

Naye Balozi wa Biko Sports Tanzania ambaye ni mwandishi nguli wa michezo nchini hapa nchini, Maulid Kitenge, alimpongeza Juma kwa kuonyesha shauku ya kuzitafuta Sh Milioni 97 za Bikosports, huku akiwataka Watanzania wote na wapenda michezo ya kubashiri matokeo kucheza kwa kupitia kampuni yao yenye uhuru wa mechi nyingi na za kutosha.

“Ukiwa ni mdau wa michezo hii ya kubashiri matokeo, hapana shaka Bikosports ndio mahala sahihi na tulivu mno kwa kushinda zawadi mbalimbali pale mtu anapofanikiwa kushinda jamvi lake, hivyo hata kwa hatua hii ya kutoa bonasi kwa watu wanaofanya vizuri kutabiri kwetu ni shauku ile ile ya kuwajali wateja wetu.

“Watanzania wachangamkie kubashiri kwenye kampuni ya Biko Sports kwa sababu kuna mpangilio mzuri na yoyote anaweza kubashiri matokeo hata kwa kutumia simu ya tochi au kwa kupitia mtandao wetu wa www.bikosports.co.tz, “Alisema.

Akizungumzia hatua ya kupewa bonasi yake ya Sh milioni tano, mshindi huyo aliishukuru bikosports kwa kumpa bonasi hiyo akisema kuwa itaendelea kumfanya aendelee kuziwinda fedha nyingi kutoka bikosports hususan sh milioni 97 ambazo zitatoka mtu akifanikiwa kubashiri michezo 13.

“Lengo langu ni kupata hizo zawadi za juu kabisa, hivyo kupewa bonasi hii ni jambo zuri kwangu, ila nitahakikisha nashinda dau hilo kubwa, nikiamini kuwa linawekea mwangaza mzuri wa kimaisha kwa kupitia bahati nasibu hii ya kubashiri matokeo kutoka kwenye kampuni ya bikosports,” Alisema Juma na kuwataka Watanzania waendelee kubashiri kwa kupitia bikosports ili wavune zawadi mbalimbali.

Bikosports ni mchezo mzuri na rahisi unaotoa nafasi nyingi Zaidi ya ushindi, ukichezeshwa nchini Tanzania, ambapo wateja wanaweza kubashiri kuanzia mchezo mmoja na kuendelea, ambapo kwa wale watakaofanikiwa kubashiri michezo 13 kwa pamoja, watajishindia jumla ya Sh Milioni 97, huku kianzio cha fedha cha kubashiri kikianzia Sh 500 na kuendelea.

WAZIRI LUGOLA AWASILI TABORA AKIELEKEA MKOANI KIGOMA KIKAZI

0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akipokelewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Emmanuel Nleyi (kushoto) alipowasili mkoani humo, leo. Waziri Lugola yupo safarini akielekea mkoani Kigoma kikazi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Emmanuel Nleyi (kulia), pamoja Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani humo, SP Nestory Didi. Waziri Lugola yupo safarini akielekea mkoani Kigoma kikazi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

WAFANYABIASHARA SAME WAFURAHIA ELIMU YA KODI

0
0
Na Veronica Kazimoto

Wafanyabiashara Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro wamefurahia elimu ya kodi iliyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ikiwa na lengo la kuwaongezea uelewa juu ya Msamaha wa Riba na Adhabu kwenye Malimbikizo ya Madeni ya Kodi, Mabadiliko ya Sheria za Kodi kulingana na Sheria ya Fedha ya Mwaka 2018 na Mfumo wa Maadili kwa Watumishi wa TRA.

Wakizungumza mara baada ya kumaliza semina hiyo, wafanyabiashara hao wamesema kuwa, wamefurahishwa na elimu waliyoipata kutoka TRA na kwamba itawasaidia katika shughuli zao za kila siku.

"Binafsi nimefurahi sana kupata elimu ya kodi ambayo kwa hapa Same tuna takribani mwaka mzima bila kupatiwa elimu hii, kwa kweli ninaomba TRA watupatie semina hizi mara kwa mara ili tuweze kuendesha biashara zetu kwa ufanisi", alisema Regina Msuya ambaye ni Mfanyabiashara wa Vifaa vya Shule na Ofisi.

Msuya ameongeza kuwa, ni muhimu Mamlaka ya Mapato Tanzania iangalie namna ya kuongeza muda wa semina hizo ili waweze kuyapata kwa undani masuala yote yanayohusiana na kodi.

Kwa upande wake Mfanyabiashara anayemiliki Baa wilayani hapa Tizinga Mbogo, mbali na kufurahishwa na elimu ya kodi aliyoipata, ameiomba TRA kushirikiana na ofisi ya Afisa Biashara ili kuondoa changamoto zinazowakabili ambazo utatuzi wake hutegemea ofisi hizo mbili.

"Kwanza kabisa naomba elimu hii iendelee maana tumejifunza mambo mengi mazuri kutoka kwa wenzetu wa TRA, aidha naomba Afisa Biashara ashirikiane na Mamlaka ya Mapato Tanzania hapa wilayani kwetu kwa ajili ya kututalia kero ambazo zinategemea maamuzi ya ofisi hizi mbili," alieleza Mbogo.

Awali akifungua semina hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Senyamle, amewahimiza wafanyabiashara wote wenye malimbikizo ya madeni ya kodi yanayotokana na riba na adhabu kuwahi kutuma maombi ya msamaha pamoja na kuwataarifu wenzao wenye madeni kama hayo.

Elimu ya kodi inaendelea kutolewa katika Mikoa ya Kaskazini ambapo baada ya kumaliza Mkoa wa Tanga, sasa elimu hiyo inatolewa katika Mikoa ya kilimanjaro, Arusha na Manyara.
 Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Senyamle akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya wafanyabiashara iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu kodi. Semina hiyo imefanyika Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.
 Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Diana Masalla akitoa elimu ya kodi wakati wa semina ya wafanyabiashara iliyofanyika Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.
  Afisa Maadili Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Adelaida Rweikiza akiwasilisha mada kuhusu Mfumo wa Maadili kwa Watumishi wa TRA wakati wa semina ya wafanyabiashara iliyofanyika Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.
 Afisa Kodi Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Shaban Makumlo akiwasilisha mada kuhusu Msamaha wa Riba na Adhabu kwenye Malimbikizo ya Madeni ya Kodi wakati wa semina ya wafanyabiashara iliyofanyika Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya wafanyabiashara wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa mada mbalimbali wakati wa semina ya wafanyabiashara hao iliyofanyika Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).

NEWZ ALERT;TAARIFA YA KUZAMA KWA KIVUKO CHA MV NYERERE.

0
0


SERIKALI YAKABIDHI PIKIPIKI 32 KWA MAAFISA ELIMU KATA ,KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOSHI.

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi pikipiki 32 kwa Maafisa Elimu kata waliopo katika wilaya ya Moshi.
Baadhi ya Mafisa Elimu Kata katika Halmashauri ya wilaya ya Moshi wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mkuu wa wilaya ya Moshi ,katika hafla fupi ya kukabidhi pikipiki kwa ajili ya kusaidia katika Sekta ya Elimu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi ,Michael Kilawila akiungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
Baadhi ya Maafisa Elimu kata waiwa katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Tatu Kikwete akizungumza katika hafla hiyo.
Kaimu Afisa Elimu Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Abdalah Komesha akisoma taarifa kuhusu makabidhiano ya pikipiki hizo ambazo zimetolewa kwa Maafisa Elimu kata hao.
Baadhi ya Maafisa Elimu kata wakiwa katika hafla hiyo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Brabarani mkoa wa Kilimanjaro,Meja Hilda Mlay akitoa elimu ya usalama barabarani kwa Maafisa Elimu kata ambao wamekabidhiwa pikipiki kwa ajili ya kurahisisha kazi zao.
Mkaguzi wa Magari wa Polisi ,Francis Arthur akitoa elimu namna ya kutumia pikipiki kwa watendaji hao.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akikabidhi funguo ya  pikipiki kwa mmoja wa Maafisa Elimu kata wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya pikipiki hizo ambazo zitasaidia katika kukuza Elimu kupitia mradi wa KKK.kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila na mwisho ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Tatu Kikwete. 
Maafisa Elimu kata wakiwa wamevalia kofia ngumu ,tayari kuanza safari mara baada ya kukabidhiwa pikipiki kwa ajili ya kurahisisha utendaji kazi wao.
Sehemu ya pikipiki zilizokabidhiwa kwa Maafisa Elimu kata ,katika Halmashauri ya wilaya ya Moshi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
MKUU wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba amesema hatarajii kupokea taarifa ya ajali, wala mwaliko wa kwenda hospitalini kumjulia hali, ofisa wa serikali aliyelazwa wodini au chini ya uangalizi maalumu (ICU) kutokana na ajali iliyosababishwa na ‘munkari’ wa kukimbiza pikipiki za umma, zaidi ya spidi 150.
Warioba aliyaeleza hayo juzi, wakati akizungumza na Waratibu wa Elimu Kata 32 waliokabidhiwa pikipiki aina ya Honda TVS, kwa ajili ya kutekeleza Mpango wa Kukuza Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu unaotambuliwa kama KKK.
“Na kwa kweli nitasikitika sana, kualikwa kumtembelea mmoja wa maofisa wetu akiwa ameumia ama amepoteza maisha, tunawahitaji kweli kweli, jamii imewekeza kwenu, serikali imewekeza kwenu mpaka mkafikia hapo mlipo kwa uwezo mlionao,
“Kada hii ya watumishi haifanyi mambo ya kihuni barabarani, na wala sitaki kusikia mara umekamatwa umebeba mkaa au umeazima pikipiki inatumika na watu wasiohusika, sijaona hata mmoja mwenye umri wa kwenda kuchezea maisha yake. Wako ambao wakiendesha wakisikia muungurumo anaamsha hisia, anaona kama ana paa, wako ambao wakiendesha na kupigwa upepo wanahisi uhuru zaidi, na ndio maana hatizami anakwenda spidi 50 hadi 150.”
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Tatu Kikwete akitoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya vyombo hivyo, alisema pikipiki hizo kwa kuwa ni mali ya serikali zipo taratibu lazima zifuatwe katika uendeshaji na ndio maana amaemua kumwita Mwakilishi wa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Kilimanjaro (RTO, Meja Hilda Mlay na Mkaguzi wa magari, Francis Arthur na maofisa wa Bima.
Kaimu Ofisa Elimu ya Msingi, Abdalah Komesha alisema halmashauri hiyo yenye jumla ya shule za msingi 274, imepokea pikipiki hizo zilizotolewa kupitia mradi wa Lanes kwa ajili ya kufanya ufuatiliaji wa utendaji kazi katika shule zilizopo katika kila kata.
“Hizi pikipiki ni lazima zitumike ndani ya kata husika na kama ni nje ya kata, iwe kwa kibali maalumu kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji, lakini pia itatakiwa kutumika siku za kazi tu na kama ni nje ya utaratibu ni lazima kuwe na kibali na wala hazitakiwi kutumika kubeba mizigo mizito na abiria,”alisema Komesha
Ili kuepukana na ajali hizo kwa watumishi wa umma, Meja Mlay kutoka Ofisi ya RTO Kilimanjaro, aliwataka waratibu hao wa elimu wa kata kuomba kibali kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Tatu Kikwete kujiunga na darasa maalumu la mafunzo ya usalama barabarani yanayotolewa na kikosi hicho.
Julai 2 mwaka huu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Seleman Jaffo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, walikabidhi pikipiki 2,894 kwa ajili ya waratibu wa elimu katika kata za nchi nzima kwa ajili ya kuboresha sekta hiyo.
Mwisho

UTT AMIS YATOA ELIMU YA MIFUKO YAO KWA WANANCHI MBALIMBALI NA WASHIRIKI WA SEMINA JIJINI MOROGORO

0
0
Afisa Masoko na uhusiano wa UTT AMIS Ndg.Waziri Ramadhani akitoa elimu kwa wastaafu watarajiwa kutoka taasisi mbalimbali katika semina iliyo andaliwa na TAGLA katika ukumbi wa JKT Umwema-Morogoro
Afisa Masoko na uhusiano wa UTT AMIS Ndg.Waziri Ramadhani akitoa elimu kwa wastaafu watarajiwa kutoka taasisi mbalimbali katika semina iliyo andaliwa na TAGLA katika ukumbi wa JKT Umwema-Morogoro
Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo.

NAIBU SPIKA TULIA AKSON AWAKABIDHI KOMBE NA PIKIPIKI WASHINDI WA MICHUANO YA TULIA, TIMU YA NETIBOLI YA LUPEPO

0
0


Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Akson, akiwakabidhi Kombe na Pikipiki wachezi wa timu ya Netiboli ya Lupepo baada ya kuibuka washindi katika mchezo wa fainali za michuano ya Tulia dhidi ya Mpuguso uliochewa jana Sept 19 2018 katika Uwanja wa Tandale mji wa Tukuyu Wilaya ya Rungwe. Katika mchezo huo Lupepo walishinda kwa mabao 28 – 14 na kutwaa ubingwa. (Picha  na Muhidin Sufiani)
03
MCHEZAJI wa timu ya Netiboli ya Kata ya Mpuguso, Tusajigwe Mwansasu, akidaka mpira huku akizongwa na Razia Joel wa timu ya Lupepo, wakati wa mchezo wa fainali wa Michuano ya Tulia uliochewa jana Sept 19 2018 katika Uwanja wa Tandale mji wa Tukuyu Wilaya ya Rungwe. Katika mchezo huo Lupepo walishinda kwa mabao 28 – 14 na kutwaa ubingwa. (Picha  na Muhidin Sufiani)
05
MCHEZAJI wa timu ya Netiboli ya Mpuguso, Sofia Mahala (kulia) akiwania mpira na Razia Joel, katika mchezo wa fainali za michuano ya Tulia dhidi ya Mpuguso uliochewa jana Sept 19 2018 katika Uwanja wa Tandale mji wa Tukuyu Wilaya ya Rungwe. Katika mchezo huo Lupepo walishinda kwa mabao 28 – 14 na kutwaa ubingwa. (Picha  na Muhidin Sufiani)
04 (1)
2 (25)
BEKI wa timu ya Mbande Fc, Bariki Mwaijotele (kulia) akijaribu kuwania mpira na Niko Celion wa Ndanto Fc, wakati wa mchezo wa fainali wa Michuano ya Tulia uliochewa jana Sept 19 2018 katika Uwanja wa Tandale mjiwa Tukuyu Wilaya ya Rungwe. Katika mchezo huo Mbande Fc walishinda kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya kumalizika dakika 90 kwa kufungana bao 1-1. Katikati yao ni Nahodha wa Ndanto fc, Ringo mwalenje. (Picha  na Muhidin Sufiani)
7 (7)
 
MSHAMBULIAJI wa timu ya Ndanto Fc, Anard Amoni akijaribu kumtoka Ezekia Mwakisole Mbande Fc, wakati wa mchezo wa fainali wa Michuano ya Tulia uliochewa jana Sept 19 2018 katika Uwanja wa Tandale mjiwa Tukuyu Wilaya ya Rungwe. Katika mchezo huo Mbande Fc walishinda kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya kumalizika dakika 90 kwa kufungana bao 1-1. (Picha  na Muhidin Sufiani)

TatuMzuka yazindua ‘jackpots’ mbili kubwa za kubadili maisha kila wiki

0
0
Wiki hii TatuMzuka imezindua jackpot ya Jumatano ikiwa ni jackpot ya pili ndani ya wiki moja. Watanzania sasa watapata fursa ya kuwa washindi wa jackpots mara mbili na hivyo kutengeneza washindi wengi zaidi kupitia jackpots.
Jackpot ya jumatano ambayo itahusisha wachezaji wote waliocheza tangu jumapili itakuwa inaonyeshwa saa 3 usiku kupitia Clouds TV na EATV.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni hiyo, Bwana Sebastian Maganga alisema kampuni ya The Network ambao ni wamiliki wa mchezo wa namba wa TatuMzuka imekuwa ikiangalia namna ya kuongeza nafasi za Watanzania kushinda kwa wingi na kwa kiasi ambacho kinabadilisha maisha yao.

“Tangu tulipoanza mwaka mmoja uliopita tumetoa jackpot ya kihistoria ya milioni 300, na sasa kwa kuongeza jackpot ya jumatano watanzania hawatahitaji kusubiri wiki nzima kushinda, itakuwa sasa jumatano na jumapili” Alisisitiza Maganga

Baada ya uzinduzi huu, Tatumzuka sasa itaondoa jackpot ya kila siku ya Mzuka Deile na kuibadilisha na droo za vipindi maalumu ndani ya siku moja. Droo hizi zitatengeneza mamilionea wengi kwa haraka na kuufanya TatuMzuka kuwa mchezo unaotengeneza mamilionea wengi zaidi kuliko mchezo mwingine katika soko.

Akiongea wakati wa uzinduzi, balozi wa TatuMzuka Mussa Hussein (pichani) alisema hii ni fursa kubwa kwa watanzania kubadili maisha yao kupitia jackpots mbili kubwa kila wiki.

“Kwa tiketi moja ya shilingi 500 sasa Watanzania watakuwa wanasubiri kwa siku 3 tu kushinda kupitia jackpot za jumatano na jumapili. Hii itakata kiu ya wachezaji wetu wapendwa ya kusubiri muda mrefu kushinda kiasi kikubwa” Aliongeza Hussein

Ili kuongeza nafasi ya watanzania wengi kutazama shoo za jackpots Bwana Maganga alisisitiza kwamba The Network imeiongeza TBC1 kati ya vituo vitakavyokuwa vinaonyesha mubashara shoo ya jackpot ya jumapili.

WAZIRI UMMY MWALIMU APOKEA MSAADA WA DAWA,VIFAA TIBA KUTOKA SERIKALI YA INDIA

0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amepokea msaada wa dawa na vifaa tiba wenye thamani ya Sh.Bilioni mbili kutoka Serikali ya India.

Msaada huo wa dawa na vifaa tiba wa Serikali ya India umekabidhiwa kwa Waziri Mwalimu na Balozi wa India nchini Tanzania na kwamba dawa na vifaa tiba hivyo ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ambayo imedhamiria kuboresha sekta ya afya.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa msaada huo Waziri Mwalimu ameishukuru Serikali ya India kwa kutoa msaada huo ambao umetokana na ombi la Rais Dk.John Magufuli kwa Waziri Mkuu wa India ambaye alikuja nchini.

"Wakati Waziri Mkuu wa India alipokuja nchini,Rais Dk.John Magufuli alitoa ombi la kuomba dawa muhimu na vifaa tiba.Hivyo tunatoa shukrani kwa Serikali ya India kwa msaada huu.Tunatoa shukrani kwa Waziri Mkuu wa India," amesema Waziri Mwalimu.

Akizungumzia zaidi msaada huo,Waziri Mwalim amesema miongoni mwa dawa ambazo zimetolewa na Serikali ya India  ni dawa aina ya Amoxline kwa ajili ya watoto na zipo dozi 19800.
Pia kuna dawa ya kuzuia wajawazito kuvuja damu baada ya kujifungua na kwamba kuna dawa za chanjo ya homa ya ini.
Waziri Mwalim amesema kuwa dawa na vifaa tiba vitapelekwa kwenye Hospitali za umma na kwamba pamoja na msaada huo Serikali imefanikiwa kuboresha sekta ya afya ikiwemo ya kuongeza dawa na vifaa tiba.

"Dawa ambazo zimetolewa zitatolewa bure.Hii imedhihirisha mahusiano mazuri kati ya Tanzania na India.Kwa kukumbusha tu baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani tumekuwa tukinunua dawa kutoka viwandani badala ya watu binafsi.

" Tunaomba Balozi wa India uendelee kuhamasisha wawekezaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba waliopo India kuja kuwekeza nchini kwa kujenga viwanda vya dawa,"amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Wakati huo huo Waziri Mwalimu amezungumzia namna ambavyo Serikali imefanikiwa kuongeza dawa muhimu nchini ambazo kwa sasa zipo za kutosha.

Amefafanua  kuwa taarifa ya Bohari ya Dawa nchini(MSD) ni kwamba kuna ongezeko kubwa la  dawa muhimu hadi  kufikia asilimia 85 kutoka asilimia 36 huko nyuma.

Pia amesema Serikali imeendelea kuhakikisha dawa zote zinakwenda katika maeneo yote ili wananchi wenye mahitaji ya dawa wazipate.

"Kati ua muhimu ya dawa ambazo zimepewa kipaumbele ni dawa ya kumuwezesha mama mjazito kutojifungua mtoto mwenye kichwa kikubwa na mgongo wazi," amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Kwa upande wake Balozi wa India nchini Tanzania Sandeep Arya amesema thamani ya msaada ambao umetolewa na Serikali yao una thamani ya Sh.bilioni mbili na lengo ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya kuboresha sekta ya afya.
"Dawa na vifaa tiba hivyo unalenga kusaidia kuboresha sekta ya afya nchini Tanzania.Pia msaada huu unathibitisha ushirikiano na uhusiank mzuri kati Serikali hizi mbili," amesema Balozi Arya.

TUME YA UCHAGUZI YA TAIFA YAKANUSHA TUHUMA ZA CHADEMA

0
0
 
Na Idara ya Habari-NEC

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt. Athumani Kihamia (pichani) amekanusha Tuhuma zilizotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Freeman Mbowe dhidi ya Tume kutokana na uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Monduli na Ukonga.
Uchaguzi mdogo katika Jimbo la Monduli, Mkaoni Arusha na Ukonga Jijini Dar es Salaam ulifanyika Tarehe 16, Septemba mwaka huu pamoja na Kata 23 za Tanzania Bara.
Dkt. Kihamia akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo (20.09.2019) amesema tuhuma zilizotolewa na Mbowe dhidi ya Tume na dhidi yake binafsi hazina ukweli wowote.
Dkt. Kihamia aliwathibitishia waandishi wa habari kwamba tuhuma kwamba kulikuwa na vituo ‘fake’ 16 kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Ukonga ni za uongo na kwamba vituo vilivyotumika ni 673 ambavyo ni vilevile vilivyotumika kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
“Vituo vilevile 673 vilivyotumika kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 ndio hivyohivyo vilivyotumika kwenye uchaguzi mdogo wa Septemba 16 Jimbo la Ukonga. Hakujapunguzwa kituo hata kimoja wala kuongozwa kituo hata kimoja…,” alisema.
Dkt. Kihamia aliongeza kwamba wakala wa Chadema wa kujumlisha matoke, Bi. Asia Msangi ambaye pia alikuwa mgombea wa chama hicho Jimbo la Ukonga alisaini fomu ya matokeo jambo ambalo linaonyesha kwamba chama hicho kiliridhia mchakato huo.
Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi alisisitiza kwamba ni vyema chama hicho kikawaeleza wananchi ukweli juu ya sababu zilizowapelekea kushindwa kwenye chaguzi hizo badala ya kuizushia Tume uongo kila mara.
“Watanzania wasipotoshwe, wanasiasa wasitafute sababu za kushindwa kwa kuzungumza mambo yasiyokuwa na ukweli na kama tuhumu za Chadema ni za ukweli basi ni bora wakaenda mahakamani. Hizi ni tuhuma za uongo zenye lengo la kujiosha,” alisema.
Kuhusu Monduli na tuhuma kwamba kuna mawakala wa Chadema waliozuiliwa, Dkt. Kihamia amesema kwamba wapo watu wasiokuwa mawakala wanaotambulika kisheria walitaka kukiwakilisha chama hicho na hivyo walizuiliwa.
“Sio kweli kwamba mawakala walikataliwa na kutolewa nje ila kilichotokea ni kwamba wapo watu ambao walifika kituoni kwenye vituo vinne tofauti wakidai kwamba ni mawakala wakati hawajaapa kufanya kazi hiyo kwa hiyo watu kama hao hawawezi kuruhusiwa,” alisema.
Mkurugenzi aliongeza kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliwatuma Makamishna na Maofisa wake kwenye maeneo yote ambayo yalikuwa yanafanya uchaguzi ili kufuatilia mwenendo wa uchaguzi kwa hiyo Tume ina taarifa za uhakika juu ya yale yote yaliyojiri.
Kuhusiana na kujitokeza kwa wapiga kura wachache, Dkt. Kihamia alisema kwamba kwa kawaida chaguzi ndogo huwa hazina msisimko mkubwa kwa wapiga kura kwa hiyo idadi ya wapiga kura waliojitokeza sio ya kushangaza.
“Ukifanya utafiti duniani kote utagundua kwamba chaguzi ndogo huwa hazina wapiga kura wengi, kwa hiyo hili sio jambo la kushangaza,” alisema.
Katika hatua nyingine, Dkt. Kihamia alimtaka, Mhe. Mbowe kumuomba radhi kwa kumtuhumu kuwa yeye ndio anahusika na mambo yaliyokinyume na sheria ndani ya Tume.
“Mhe. Mbowe sijawahi kukutana naye na yeye hajawahi kukutana na mimi, kwa maana hivyo hatujawahi kugombana, hivyo anatakiwa achague maneno ya kusema…..mimi sipendi kulumbana na wanasiasa na wanasiasa wengine wote waelewe hivyo, nipo hapa kuhakikisha kwamba Tume inatimiza wajibu wake,” alisema.

WAZIRI MKUU AAGIZA WATAFITI WA ZAO LA UFUTA WAPELEKWE MAKUTUPORA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba apeleke wataalamu kwenye kituo cha utafiti kilichopo Makutupora, Dodoma ili wazalishe mbegu bora za ufuta kwa ajili ya mikoa ya kanda ya kati.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Alhamisi, Septemba 20, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Mauno, wilayani Kondoa ambako alienda kukagua ujenzi wa kituo cha afya. Waziri Mkuu leo ameanza ziara ya kikazi ya siku saba katika mkoa wa Dodoma.

Alikuwa akijibu ombi la mbunge wa viti maalum, Bi. Mariam Ditopile ambaye alisema mkoa wa Dodoma ni wa pili kwa uzalishaji wa ufuta hapa nchini lakini aina ya ufuta inayozalishwa ni ya daraja la chini kwa sababu hawana mbegu za ufuta mweupe.

“Ili mradi mikoa ya kanda ya kati inazalisha ufuta, ninamuagiza Waziri wa Kilimo ahamishe watumishi kutoka kokote ili wakae Makutupora na kuwasaidia wakulima wawe na mbegu bora zenye kutoa mafuta mengi,” alisema.

Amesema kila mwaka Serikali inatumia zaidi ya dola za Marekani milioni 267 kuagiza mafuta ya kula kutoa nje ya nchi na kwamba hivi sasa imeamua kufufua mazao ya mbegu za mafuta ili mafuta ya kula yazalishwe kwa wingi hapa nchini.

 “Sasa hivi tumeanza kufufua mazao ya mbegu za mafuta ni nilianza mkoa wa Kigoma kwa kuhimiza kilimo cha michikichi. Sasa hivi niko Dodoma nahimiza ufuta na alizeti na nitaenda Singida kwa ajili ya zao hilo la alizeti,” amesema.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza wananchi wa Kata ya Mauno wilayani Kondoa, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi Mkoani Dodoma, Septemba 20, 2018.  
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, akizungumza na wananchi wa Kata ya Mauno Kondoa Mkoani Dodoma, Septemba 20, 2018.
 Wananchi wa Kata ya Mauno wilayani Kondoa, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipowasili katika kata hiyo akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Dodoma, Septemba 20, 2018.

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia chumba cha kuhifadhia maiti, wakati alipokagua ujenzi wa kituo cha afya cha kata ya Mauno Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma, Septemba 20, 2018, kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Godwin Mkanwa, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dk. Ikaji Rashid.

Major Lazer waachia nyingine wakiwa na staa wa SA, Babes Wodumo

0
0



MAJOR LAZER WAMSHIRIKISHA STAA WA AFRIKA KUSINI, BABES WODUMO KWENYE ‘ORKANT/BALANCE PON IT’ARTWORK Orkant2 4000x4000 300dpi.jpg
Major Lazer wameachia wimbo mpya, Orkant/Balance Pon It wakimshirikisha muimbaji wa Afrika Kusini, Babes Wodumo. Wimbo huo umekuja na video mpya ya ushirikiano kati Major Lazer na muongozaji wa Afrika Kusini, Adriaan Louw. Video hii imefanyika huko jijini Durban.
 “Orkant/Balance Pon It” imekuja baada ya kuachiwa kwa “All My Life” ikimshirikisha nyota wa Nigeria, Burna Boy na ni wimbo wa pili wa wa ushirikiano na wasanii wa Afrika kutoka kwa Major Lazer.
Major Lazer hivi karibuni pia walizindua Afrobeats Mix mpya, yenye mchanganyiko wa nyimbo toka barani na kutumia jukwaa lao la kimataifa kuonesha uwezo wa wasanii wa Afrika.
Pia, bendi hiyo itaanza ziara yake ya Afrika kuanzia mwezi huu hadi October kwa kupita nchini Afrika Kusini, Malawi, Kenya, Ethiopia na  Uganda.

UVCCM YAMJIBU MWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWE

0
0


Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) umesema unaamini Juhudi anazofanya Rais John Magufuli ndani ya serikali yake ndio siri ya cha chama hicho kushinda kwenye uchaguzi wa marudio uliomalizika hivi karibuni.

Hayo yamebainishwa jijini Dar na Katibu wa chipukizi na uhamasishaji wa Umoja huo,Hassan Bomboko,wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano alipokuwa akijibu tuhuma zilizotolewa na Mwenyekiti Taifa wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema,Freeman Mbowe kuwa CCM walishinda kutokana na wizi wa kura.

Bomboko amesema madai hayo sio ya kweli kwani chama hicho kimeshinda kutokana kile anachodai ni kasi ya utendaji wa Rais magufuli katika kuwatumikia wananchi.

Amesema kwa sasa serikali ya Rais Magufuli imefanya mambo mengi mazuri ambayo yamewapendeza wananchi mpaka yakawafanya wachague wagombea wa Chama cha mapinduzi.

Ameongeza kuwa miradi mbali ya ujenzi wa Reli,Barabara,Madaraja Miundombinu ya Umeme pamoja kudhibiti rushwa, madwawa ya kulevya na kuleta nidhamu katika utumishi wa Umma ni vitu pekee vinavyokipa nguvu chama hicho kuaminika kwa wananchi.

Amemtaka Mbowe kuacha visingizio na badala yake atafute sababu ya kushindwa kwa chama chake.

Hata hivyo,Mwanasiasa huyu amesema kama chama chochote hakiridhiki na matokeo hayo kifuate sheria ikiwemo kwenda kufungua kesi mahakamani .

IDADI YA MIILI ILIYOOPOLEWA YAFIKIA 44, WATU WALIO HAI 37 KATIKA AJALI YA KUZAMA KWA KIVUKO CHA MV.NYERERE KATIKA ZIWA VICTORIA

0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya kamii

IMEELEZWA kuwa hadi sasa jumla ya miili ya maiti ya watu 44 imetolewa ndani ya maji ya Ziwa Victoria huku pia watu waliokuwa hai 37 wameokolewa baada ya kutokea ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorora na Ukara katika wilayani y
Ukerewe mkoani Mwanza.

Hata hivyo juhudi za kuendelea kuokoa watu waliokuwa ndani ya kivuko hicho ambacho kilizama ziwani jana mchana zinaendelea huku vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wadau wengine wa ukoaji wakiendelea kufanya jitihada za kutafuta miili na watu waliomo ndani ya kivuko hicho.

Akizungumza asubuhi kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ameiambia Michuzi Blog kwamba wanaendelea nq juhudi za kuokoa watu waliokuwa wanasafiri na kivuko hicho na kazi inakwenda vizuri.

Alipoulizwa idadi ya watu ambao wamefainikiwa kuokolewa hadi sasa wakiwa hai amejibu idadi yao imefikia watu 37 na juhudi zinaendelea.

Kuhusu watu waliokufa kutokana na ajali hiyo ,Kamanda amejibu kuwa wamefanikiwa kupata miili ya watu 44.

Hata hivyo alipoulizwa kuhusu idadi ya watu waliokuwa wakisafiri na kivuko hicho ambacho kimepata ajali ,amejibu kwamba kwa sasa ni ngumu kupata idadi yao na kikubwa ambacho wanaendelea nacho ni kuendelea na ukoaji ambalo ndilo muhimu kwa sasa."Tunaendelea na ukoaji wa watu ambao wamezama ,hivyo suala la idadi ya watu tuliweke kando.Tunachoweza kueleza tunaendelea na ukoaji ikiwamo kuwaondoa watu waliokuwa ndani ya meli(kivuko).

Hata hivyo wakati Kamanda akielezea kinachoendelea ikiwemo juhudi za ukoaji,baadhi ya mashuhuda wamedai kivuko hicho kilikuwa na idadi kubwa ya watu pamoja na mizigo.Imedaiwa kuwa idadi ya watu ndani ya kivuko ni zaidi ya 150 huku wengine wakidai walikuwa watu zaidi ya 200.Mbali ya idadi ya watu pia kulikuwa na mizigo mingi hali iliyosababisha kivuko kuzidiwa na kuelemea upande mmoja.

Kivuko cha Mv.Nyerere kabla ya kuzama ziwani inaelezwa kiliondoka Bugorora kwenda Ukara kati ya saa 6 na saa 7.30 mchana na kilizama dakika kama 5 kabla ya kufika kwenye ghati ya Ukara.

Michuzi Blog itaendelea kukujuza kila kinachoendelea katika shughuli za uokoaji.Pia inaungana na Watanzania wote katika kutoa pole kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wananchi wa Mkoa Mwanza ,ndugu,jamaa na marafiki kutokana na tukio hilo ambalo limesababisha kupoteza roho za Watanzania wenzetu.
Juhudi za uokoaji zilipokuwa zikifanyika hapo jana kufuatia Kivuko cha MV. Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorora na Ukara katika wilayani ya Ukerewe mkoani Mwanza kuzama.

Bonde la Wami Kuwachukulia Hatua Wasiolipa Ada za Maji

0
0
Na Grace Semfuko-MAELEZO

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imewataka wakazi wanaotumia maji ya bonde hilo kuhifadhi mazingira na kulipia ada za matumizi ya maji hayo ili waweze kupata huduma na kulisaidia bonde hilo kuzalisha maji mengi yatakayowezesha wakazi wake kuyatumia.

Hatua ya bodi hiyo inatokana na kuwepo kwa baadhi ya wakazi ambao hutumia maji bila kuyalipia hali inayosababisha hasara na bodi kushindwa kutoa huduma inavyostahili na kusababisha wananchi kulalamikia upatikanaji mdogo wa maji.

Hayo yamebainishwa na Afisa Maji wa Bonde la Wami Ruvu, Simon Ngonyani, wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar Es Salaam.

Ngonyani alisema kuwa ulipaji wa ada za matumizi mbalimbali ya maji na utiririshaji wa maji taka ni jambo la kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji.

“Tupo katika zama za uchumi wa viwanda ambapo maji yanahitajika kwa wingi ili kuendesha shughuli za kila siku za kijamii, hivyo basi wale wote wanaoiba maji wanasababisha hasara na sisi hatutawavumilia,” alisema Ngonyani.

Aidha aliwataka wakazi wanaosimamiwa na bonde hilo wenye visima vya maji kufika Wizara ya Maji na Umwagiliaji ili waweze kupewa elimu juu ya namna ya kuvihifadhi visima hivyo ikiwa ni sehemu ya utunzaji wa mazingira.

“Wenye visima wote wanatakiwa waje kujiandikisha Wizara ya Maji ili tuweze kuvihakiki visima vyao na kuangalia namna bora ya utunzaji wake ili kuepukana na magonjwa na milipuko yatokanayo na matumizi ya maji kwenye visima visivyo salama,” alisema Ngonyani.

Aidha alisisitiza kuwa licha ya kuvihakiki pia wamiliki hao wanatakiwa kulipa ada za umiliki na atakaekiuka agizo hilo au kuficha visima hivyo atachukuliwa hatua za kisheria. 

MAGAZETI YA LEO SEPTEMBA 21,2018

0
0



















Serikali Yafuta Baadhi ya Tozo za Kikanuni zilizokuwa Zikitozwa na OSHA Kuvutia Wawekezaji

0
0

MFALME WA REGGAE JAH KIMBUTE AFARIKI DUNIA

0
0
Habari zilizotufikia katika chumba chetu cha habari usiku wa kuamkia leo zinaeleza kwamba gwiji wa muziki wa reggae nchini Jah Kimbute amefariki dunia nyumbani kwake Msasani jijini Dar es salaam, mshirika wa karibu wa marehemu David Msitta Manju, amethibitisha.

Akiongea nasi kwa njia ya simu kutoka Mwanza aliko kikazi, Manju amesema amepata habari usiku huu kwamba Jah Kimbute amefariki dunia Alhamisi jioni nyumbani kwake.

Amesema kwamba amepata taarifa hizo toka kwa mkewe aliyeko jijini Tanga na kwamba mipango ya mazishi itajulikana leo asubuhi baada ya ndugu kukusanyika.

Mke wa marehemu pia alithibitisha habari hizo akiwa Tanga, na kusema kila kitu kitafahamika baada ya ndugu wa Jah Kimbute kukutana.

Amesema marehemu alikuwa akiishi na mwanae nyumbani kwake Msasani na kwamba jana jioni alipokwenda chumbani kwake alimkuta amefariki.

"Hizi habari tumezipata usiku huu na sasa ndugu wa marehemu ambao wengi wako Lushoto wanakusanyika tayari kwa safari ya Dar es salaam kesho kukamimlisha mipango yote.

Jah Kimbute, ambaye jina lake halisi alikuwa Samwel Mleteni, alitamba sana katika anga ya muziki na kuitwa Mfalme wa Reggae wa Tanzania miaka ya 80 akiwa na kundi lake la Roots and Culture lililokuwa na makaazi yake jijini Dar es salaam.
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images