Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1673 | 1674 | (Page 1675) | 1676 | 1677 | .... | 1896 | newer

  0 0


  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe (aliyeketi kushoto) na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyechuchumaa) wakizindua kazi ya kutandika reli ya kisasa ya SGR kwenye eneo la Soga, Pwani. Anayeshuhudia katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (katikati) akikagua kipande kilichotandikwa reli ya kisasa ya SGR, Soga mkoani Pwani. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe (wa tatu kulia) akipata maelezo ya namna ya kutengeneza mataruma ya reli ya kisasa ya SGR kwenye kIiwanda cha Soga, Pwani. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye, wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa na wa kawanza kushoto ni Farid Munir Abdallah, Mhandisi Mzalishaji wa Kampuni ya Yapi Merkezi
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe (wa nne kulia) na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kulia) namna kazi ya utandikaji reli ya kisasa ya SGR inavyofanyika kwenye eneo la Soga mkoa wa Pwani 
  Mmoja wa mafundi wakiendelea na kazi ya kutengeneza mataruma ya kujengea reli ya kisasa ya SGR kwenye iwanda cha Soga kilichopo mkoa wa Pwani  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amezindua rasmi kazi ya utandikaji wa reli ya kisasa ya SGR kwenye eneo la Soga lililopo mkoani Pwani ambapo reli hiyo inajengwa kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kwa umbali wa kilomita 300 na kushuhudiwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa.

  Kamwelwe amesema kuwa reli hiyo yenye jumla ya kilomita 300 kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ni kwa ajili ya njia ya reli ambayo itakuwa na umbali wa kilomita 205 na kilomita 95 ni kwa ajili ya reli kupishana ambapo reli hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba mzigo kiasi cha tani milioni 17,000 kwa mwaka ambapo nchi yetu imeingia mkataba wa kujenga reli hiyo na kampuni ya Yapi Merkezi ya kutoka nchini Uturuki na kusimamiwa na mshauri mwelekezi wa kutoka nchini Japan kwa kushirikiana na kampuni ya kizalendo ya hapa nchini kwetu. Reli hiyo itaendeshwa kwa kutumia umeme na itakuwa na spidi ya kilomita 160 kwa saa.

  Ameongeza kuwa Serikali inazalisha mataruma kwenye kiwanda chake yenyewe kilichopo Soga mkoa wa Pwani na vifaa vingine vya ujenzi wa reli hiyo kama vile sementi, mchanga na kokoto vyote vinapatikana hapa nchini. Amefafanua kuwa Serikali iliagiza reli peke yake kutoka nchini Japan ambapo kiasi cha tani 7,250 ziliingizwa nchini katika kipindi cha wiki mbili zilizopita ambapo reli hizo zitatumika kujenga reli hiyo ya kisasa ya SGR kwa ukubwa wa kilomita 60. Amesema kuwa itafika siku ambapo nchi itachimba chuma kutoka kwenye mgodi wa makaa ya mawe ya Mchuchuma na Liganga kwa ajili ya kujenga reli ya kisasa ya SGR badala ya kuendelea kuagiza reli kutoka nje ya nchi

  Kamwelwe amewataka wananchi watambue jitihada za Mhe. Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya kuhimiza wananchi walipe kodi ili Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iweze kukusanya kodi na mapato ambayo yanatuwezesha kama nchi kutumia fedha zetu wenyewe kujenga reli hiyo na tumewajiri wataalam wa kujenga reli hiyo na mkataba umesainiwa mwaka jana kwa ajili ya kujenga kilomita 300 kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro. “tumewaajiri hawa Yapi Merkezi na kazi hii wanatufanyia sisi wenyewe,” amesisitiza Kamwelwe.

  Katika hatua nyingine, Kamwelwe ametoa wito kwa watanzania waliopata nafasi ya kufanya kazi kwenye ujenzi wa reli hiyo watumie utaalamu wao vizuri ili nchi iweze kufanya kazi zake yenyewe na uzalendo uzingatiwe ili tuweze kufikia hatua ya kutumia wakandarasi wetu wa ndani kufanya kila kitu na utaratibu utaangaliwa ili wakandarasi wetu wafanye kazi hizi wao wenyewe kwa kuwa kila kitu kinapatikana hapa nchini.

  Naye Meneja Mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro Mhandisi Maizo Mgedzi amesema kuwa mradi huu umegawanyika katika sehemu kuu tatu ya usanifu, kuchukua ardhi baada ya kufanya tathmini na kulipa fidia na kujenga reli yenyewe ikiwa ni pamoja na kuandaa mfumo wa uendeshaji na matengenezo ya reli hiyo ambapo mitambo na watalaam wa kuendesha reli hiyo vitahitajika. Hadi hivi sasa vijana 60 wazalendo wenye utaalamu na ujuzi wa uhandisi wamepata mafunzo nchini na watapelekwa nje ya nchi kwenye reli na viwanda vinavyofanya kazi ili waweze kuongeza ujuzi na maarifa ya kuendesha reli hii na Shirika litaendelea kuandaa vijana wengine 160 kwa ajili ya uendeshaji wa reli hiyo.

  Ameongeza kuwa reli hiyo itatumia umeme na sio dizeli ambapo TANESCO imepewa jukumu la kutoa umeme kutoka kwenye gridi ya taifa na kuleta kwenye mfumo wa reli ya kisasa ya SGR ambapo jumla ya megawati 160 zitahitajika kuendesha reli hiyo kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro. Shirika la Reli Tanzania litakuwa na jukumu la uhandisi ujenzi, madaraja, mifumo na njia kwa ajili ya kuendesha reli ya kisasa ya SGR.

  0 0

  Serikali imekubali kuongeza muda wa siku 43 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya daraja la nyerere kiunganishi cha barabara ya Kivukoni Kibada wenye urefu wa kilomta mbili ikiwemo kukubaliana na hatua iliyochukuliwa na Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF kumkata asilimia 0.01 mkandarasi wa kampuni ya China Railway construction engeneer Group katika malipo ya makubaliano ya ujenzi huo kutokana na uzembe wa kuchelewesha kukamilika kwa kazi ya ujenzi.

  Waziri wa ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Ajira,vijana,sera bunge na wenye ulemavu) Mh Jenister Mhagama ameridhia wakandarasi hao kuongeza muda huo wa ujenzi kutokana na changamoto za kifusi ambacho awali kilishindikana kupatikana kutokana masuala kadhaa ikiwemo uharibifu wa mazingira katika eneo la Mbutu lilipo Kigamboni .

  “Nimekubali ombi hilo kutokana na changamoto ya kifusi ambapo sasa kimepatiwa ufumbuzi na uongozi wa wilaya ya Kigamboni hivyo nataka katika muda huu niliuongeza barabara hii ikamilike haraka na wakazi wa kigamboni waweze kuondokana na changamoto hii ya barabara”alisema Mh Mhagama.

  Mh Mhagama amesema kuwa barabara hiyo itakapokamilika itaweza kuongeza mapato zaidi kwa daraja na hivyo kukuza uchumi wa nchi kutokana na uwekezaji wa viwanda vingi katika eneo la kigamboni uliopo na unaoendelea kwa hivi sasa.

  Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF ndugu William Erio alimtaka mkandarasi kufanya kazi kulingana na mkataba na kwamba wataendelea kukata tozo ya adhabu ya kutokamilisha mradi kwa wakati na kwamba gharama zote zilizo nje ya mkataba hazitalipwa.

  “Kama shirika tumeamua kumkata mkandarasi huyu kutokana na kushindwa kumaliza kazi kwa wakati kama ilivypangwa awali na kuwa nitahakikisha nafuatilia hatua kwa hatua hadi ujenzi huu ukamilike ndani ya muda uliongezwa”alisema Erio.

  Pia Mkurugenzi huyo wa NSSF alisema kwa sasa shirika hilo litaweka mfumo wa utambuzi wa vyombo vya usafiri kutoka kwa wakala wa serikali ili kuhakikisha mapato ya daraja yanaongezeka kutokana na uhalisia wa tozo halisi ya magari na kuachana na mfumo wa utambuzi kwa kutumia na njia ya kuhisi kwa kutumia macho. Ambapo amesema kuwa mfumo huo utaunganishwa moja kwa moja na mamlaka ya mapato TRA ili kuhakikisha kila gari linatozwa tozo kulingana na thamani ya gari.

  Naye mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mh Sara Msafiri amesema kuwa uongozi wake umeamua kutoa kifusi hicho kilichokwamisha ujenzi huo wa barabara kwa masharti ya wakandarasi hao kuhakikisha uharibifu wa mazingira unadhibitiwa ipasavyo”alisema mh Msafiri.

  Meneja mradi wa kampuni ya ujenzi wa barabara hiyo Bwana Jamal Mruma ameeleza mbele ya waziri kuwa watahakikisha wanamaliza ujenzi kwa haraka kutokana na kumalizwa kwa changamoto ya kifusi .

  Barabara ya daraja la Nyerere ilianza kujengwa mwezi April mwaka jana ambapo mpaka sasa imeshachukua zaidi ya muda wa mwaka mmoja kabla ya kumalizika. 

   MKurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), William Erio (aliyesimama) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Uratibu, Jenista Mhagama wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara katika eneo la Daraja la Kigamboni jana.


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Uratibu, Jenista Mhagama akifafanua jambo kwa watendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Kigamboni wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara katika eneo la Daraja la Kigamboni jana.


  Meneja Mradi wa Kampuni ya China Railway Construction Engineering Group (CRCEG) Jamal Mruma akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Uratibu, Jenista Mhagama (katikati) wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara katika eneo la Daraja la Kigamboni jana, kushoto ni MKurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), William Erio.

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Uratibu, Jenista Mhagama (aliyevaa kitenge) akikagua maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara katika eneo la Daraja la Kigamboni jana .


  Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sara Msafiri (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Uratibu, Jenista Mhagama (katikati) wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara katika eneo la Daraja la Kigamboni mapema jana , kulia ni MKurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), William Erio.

   Eneo la kipande cha barabara katika eneo la Daraja la Kigamboni likiendelea na ujenzi wakatio Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Uratibu, Jenista Mhagama alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara katika eneo la Daraja la Kigamboni mapema jana .

  Picha na MAELEZO


  0 0

  *Yatangaza kuanzia mwaka huu vijana kuanzia miaka 18 hadi 35 kupatiwa elimu ya ufundi bure

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

  CHAMA Cha Mapinduzi(CCM)kimewashukuru Watanzania kwa namna ambavyo wameendelea kukiamini huku kikieleza mambo makubwa yanayofanywa na Rais Dk.John Magufuli watu wanaona na ndio siri ya ushindi wao.

  Pia kimetangaza kwamba kuanzia mwaka huu vijana wenye kuanzia umri wa miaka 18 hadi miaka 35 watapatiwa elimu ya ufundi bure na hiyo  ni fursa kwa vijana.Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Humphrey Polepole wakati anatoa sababu za ushindi wa kishindo ambao Chama hicho wameupata katika uchaguzi mdogo jimbo la Ukonga ,Monduli pamoja na Kata zote ambazo uchaguzi mdogo umefanyika.

  Kuhusu kuaminiwa Polepole amesema kutokana na mambo makubwa ambayo yanafanywa na Serikali ya CCM chini ya Rais Dk.John Magufuli wananchi wanaona na ndio maana kimeendelea kuaminika na kupata ushindi wa kishindo"Yanayofanyika ndani ya nchi yetu watu wanaona.Tumeshinda Jimbo la Ukonga na Monduli.Tumeshinda Kata 23 na kati ya hizo 12 tumepita bila kupingwa.

  "Siri ya kuendelea kuaminika na kushinda chaguzi ni matokeo ya kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya CCM chini ya uongozi madhubuti wa Rais.Dk.John Magufuli," amesema Polepole.Amefafanua kwamba unapozungumzia kupita bila kupingwa kuna sababu mbalimbali na kwamba uchaguzi unasimamiwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria na hasa sheria za uchaguzi.

  "Hivyo wanaoshiriki chaguzi wanatakiwa kuzingatia sheria na taratibu za uchaguzi na kinyume na hapo unapoteza sifa," amesema.Akifafanua zaidi kuwa wanaojiita wapinzani kwa sasa wamebaki na siasa za kubeza mazuri yanayofanyika.Polepole ameeleza pamoja na mambo makubwa yanayofanyika ya kimaendeleo CCM pia imetoa maagizo na maelekezo  kwa mawaziri kushughulika na shida za Watanzania.nakwamba ni marufuku kwa viongozi kujifungia maofisini badala yake watoke kwenda kutatua kero za watu huko waliko.

  Kuhusu kutoa mafunzo ya ufundi,Polepole amesema kuwa kuanzia mwaka huu wanaanza kutoa mafunzo ya ufundi stadi bure Amesema Serikali ya CCM imeamua kwamba vijana wenye umri kuanzia  miaka 18 hadi miaka 35 wapewe elimu ya  ufundi  bure.

  Amesema kila anayetaka kujifunza ni wakati wake sasa na ni fursa kwa vijana kuchangia wakati utakapofika."Watu wanaoana utendaji uliotukuka unaifanywa na serijaki yetu chini ya Rais Magufuli .Kama unabisha nenda Tazara utaona kilichofanyika,sekta ya anga watu wanaona Ndege mpya ambazo zimenunuliwa watu wanaona ,ujenzi wa reli ya kisasa watu wanaona,ujenzi wa vituo vya afya watu wanaona...

  " Hata hao wapinzani wanapanda hizo ndege licha ya kubeza.Uzuri watu wanaona na wao waendelee kubeza,"amesema.Kuhusu  jimbo la Ukonga na Monduli amesema  kwamba wananchi wanaona yaliyofanyika na ndio maana CCM imeshinda kwa kishindo.

  Amesema kwa Monduli kuna uwezeshaji mkubwa kwa wananchi ukiwamo wa kutoa mbuzi bure kwa wananchi na hivyo  wamefanikiwa  kubadilisha maisha yao.Kuhusu malalamiko ya wapinzani kwamba uchaguzi haukuwa huru,Polepole amesema kuwa hayo ni malalamiko ya kila siku na kwamba hawatangaika na kujibu tuhuma ambazo hazina tija

  "Kumekuwa na kawaida ya upinzani kulalamika siku zote na wakishinda wao Tume ya Uchaguzi wanaisifu lakini ikishinda  CCM wanasema Tume mbaya," amesema.Polepole amesema CCM haina muda wa kujibizana nao huku akitoa mfano katika Kata ya Uyole wapinzani wamekwenda na bastola kwenye chumba cha kupigia kura na hakuna aliyesema kuhusu hilo.

  Ameeleza namna ambavyo wanasikitishwa na aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Ukonga kupitia Chadema wa kuonesha vitisho dhidi ya polisi na kufokafoka bila sababu na kutoheshimu mamlaka zilizopo.Amesema kwa namna ambavyo Chadema wamefanya wakati wa kampeni ikiwa pamoja na kutoa vitisho tena mbele ya Polisi na hakuna hatua ambazo zimechukuliwa hakukua na sababu ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kufanya sherehe ya kuwapongeza polisi.

  Ametumia nafasi hiyo kumuomba Msajili wa vyama vya siasa kuendelea kutoa elimu kuhusu namna bora ya kuendesha vyama vya siasa na kuwatumikia wananchi kwa kufuata sheria,kanuni na taratibu.

  0 0


  Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

  MKUU wa Wilaya ya Namtumbo, Sophia Mfaume Kizigo ametoa ufafanuzi kuhusu ziara ambayo ameifanya katika wilaya zote za wilayani humo huku akieleza namna ambavyo imesaidia kusikia changamoto za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

  Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya huyo ni kwamba ziara hiyo  ilikua na malengo makubwa matatu  ambayo yalitofautiana kulingana na kata husika. Akizungumzia ziara hiyo leo amesema utofauti ulikuja kwasababu kuna kata ambazo alikuwa tayari  ameshazitembelea, hivyo ziara hiyo ilikua wakimpokea kwa mara ya pili.

  Wakati kwa Kata zingine alikuwa akipokelewa kwa mara ya kwanza.Ametaja malengo ya  yake  ya ziara hiyo ni kwamba kwa kata ambazo ziara hiyo ni kwa mara ya kwanza,lengo namba moja ilikuwa kujitambulisha. Pia kuhamasisha uhifadhi huku akifafanua alikuwa ameambatana na  wakuu wa idara muhimu kama kilimo, ardhi, ufugaji na uvuvi, misitu, sheria,sanaa utamaduni na michezo pamoja na kamati yote ya ulinzi na usalama ya wilaya.

  Wakuu wa idara za kilimo, ardhi, mifugo na OCD walipata nafasi ya kutoa somo fupi kuhusu uhifadhi. Kila mtaalamu kwa kitengo chake alieleza njia bora zaidi za kufanya shughuli mbalimbali bila kuathiri uhifadhi hasa wa mazingira na hifadhi za misitu tulizonazo.Ameongeza lengo la tatu lilikuwa kusikiliza kero na
  Changamoti za wananchi.

   "Kero karibu zote zilijibiwa palepale kwani wakuu wa idara zote na kamati ya ulinzi na usalama walikuwepo."Kwa kata ambazo nilikua nimekwenda kwa mara ya pili, lengo namba moja lilikua kuhamasisha uhifadhi na lengo namba mbili lilikua kujibu kero na changamoto za wananchi walizotoa katika mkutano uliopita ambazo hazikuwa zimetolewa majibu ya moja kwa moja.

  " Lengo la tatu lilikua kusikiliza kero na changamoto nyingine za wananchi,"amefafanua.Ameeleza kuwa kuna kero ambazo zilitolewa majibu katika ziara iliyopita na kuna nyingine zilihitaji ufuatiliaji ikiwamo ya mgambo na wakulima wa korosho ambapo aliwapatia majibu.

  Kuhusu mgambo Mkuu wa Wilaya Kizigo amesema wananchi wa Magazini katika kijiji cha Magazini walilalamika kwamba wao hawafanyiwi mafunzo ya mgambo hivyo kusababisha wakati wa kazi mbalimbali kama usimamizi wa mitihani wanakosa nafasi hizo. Majibu ndio hayo

  Kwa wakulima wa korosho ambao waliuza korosho zao kupitia Magazini AMCOS mpaka sasa hawajalipwa fedha zao za msimu uliopita.

  "Baada ya kulifuatilia tuligundua wameibiwa na wajanja wachache waliokua viongozi wa hiyo AMCOS. Kwavile Serikali hatuwezi kuingilia shughuli za ushirika bila kibali chao, nilimuagiza Ofisa ushirika aende katika kata hiyo na kufanya nao kikao.

  " Alikwenda na mwisho walikubaliana kwamba wawape muda hao wezi mpaka mwezi wa 12 wawalipe. Walifikia maamuzi hayo kwa kile walichodai kwamba wale wezi ni watoto wao hivyo si busara sana kuwafunga wawape muda,"amesema.Pia amesema katika Kata ya Msisima Vijiji vya Matepwende na Mlalawima pamoja na kata ya Magazini wananchi walilalamika kuhusu kutokufanyika mapitio ya mpango wa matumizi bora ya ardhi (WMAs) kama ilivyopasa baada ya miaka kumi kutimia.

  " Nimewaahidi kuandika barua katika wizara husika ili waje kufanya mapitio hayo kwani ndio wenye mamlaka ya kufanya hivyo,"amefafanua.Baadhi ya wananchi ambao wamepata nafasi ya kuzungumzia ziara hizo wamempongeza Mkuu wa Wilaya na kwamba wamefurahishwa kwa namna ambavyo ameweza kusikiliza shida zao na kuzipatia ufumbuzi.
   MKUU wa Wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo akiwasili kwenye moja ya kata wakati wa ziara yake alioyoifanya hivi karibuni wilayani humo,na kutoa ufafanuzi kuhusu ziara hiyo ikiwemo kusikiliza changamoto za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
   Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza MKUU wa Wilaya ya Namtumbo, Sophia Kizigo (wa tatu kulia) alipokuwa akizungumza nao kwenye moja ya mkutano wake wa hadhara,katika kuzisikiliza changamoto za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

  0 0


  Na Mathias Canal, NFRA-Dodoma

  IKIWA msimu wa kununua mazao umeanza, Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Vumilia  Zikankuba amewataka wakulima kuhakikisha wanazingatia ubora wa mahindi.

  Aidha, amesema nchi inachakula cha kutosha na kusisitiza kuwa katika msimu wa kwanza wa ununuzi wa mahindi bei ya NFRA ni wastani wa Sh 380 hadi Sh 400 kwa kilo.Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Dodoma, Zikankuba alisema NFRA haitaweza kununua mahindi mabovu na kusisitiza wakulima kuwa na mahindi yenye ubora ambayo yatawasaidia kupata masoko ya nje pia.

  " Haiwezekani NFRA itumia fedha za Serikali kununua mahindi yasiyokidhi viwango vya ubora na machafu kutoka kwa wakulima. Hivyo wakulima wanapaswa kuzalisha mahindi kwa kuzingatia viwango vya ubora vinavyokidhi vigezo vya soko..

  Aliongeza: “Lazima chakula tunachonunua kizingatie ubora. Tunataka tubadilishe taswira ya NFRA kwa sababu awali kulikuwa na tatizo la chakula kuharibika kwa kipindi kifupi.”

  Zikankuba alisema ili kuhakikisha mahindi ya wakulima yanaweza kukidhi viwango vinavyotakiwa NFRA tayari imekwishatoa elimu kwa wakulima kupitia vikundi na kwenye vyombo vya habari.Alibainisha kuwa baada ya elimu hiyo wakala umefanikiwa ambapo wakulima kutoka maeneo ya Makambako, Sumbawanga na Mpanda wameanza kuzalisha na kuuza mahindi yenye ubora kwa NFRA.

  “Changamoto iliyopo ni kwa baadhi ya wakulima wachache ambao bado wamekuwa wagumu kubadilika na wale ambao wanaamini wakitumia nafasi zao wanaweza kuuza mahindi yasiyo na ubora,"Alisema kwa mkulima kuwa na mahindi yenye ubora unatoakiwa utasaidia katika kupata soko la NFRA, pia katika taasisi zingine zinazonunua nafaka hiyo za ndani na nje ya nchi.

  "Dhima ya serikali ni kwenda uchumi wa kati kupitia uchumi wa viwanda, kwa mahindi pekee hayatumiki kwa chakula pekee, bali kutengeneza bidhaa mbalimbali. Hivyo hatuwezi kufikia Tanzania ya viwanda endapo wakulima watazalisha malighafi zisizokuwa na ubora,” alieleza.Viwango vinavyopaswa kuzingatiwa na wakulima wa mahindi ni kwamba unyevunyevu usizidi asilimia 13.5, takataka asilimia 0.5 na punje zilizovunjika zisizidi kwa asilimia 2.

  Viwango vingine ni punje zilizoliwa na wadudu na zilizosinyaa zisizidi asilimia moja, punje mbovu asilimia mbili na punje za rangi tofauti zisizidi asilimia 0.5.Zikankuba alitoa msisitizo kwa wakulima kutunza chakula badala ya kukiuza chote.

  “Msimamo wa Rais (John Maguful) wa kutotoa chakula cha msaada upo sahihi kwa sababu kuna maeneo walikwishazoea kupelekewa chakula cha msaada. Msimamo huo umelenga kuwahamasisha wananchi kutunza chakula, haya malalamiko ya hatuna chakula yanachangiwa na uzembe wa wananchi wa kuuza chakula chote,” Vumilia, alibainisha.

  Alisema jukumu la wakala ni kutunza chakula kwa ajili ya dharura kama kumetokea majanga kama mafuriko, njaa, tetemeko  na majanga mengine ambayo wanachi watahitaji msaada wa chakula.Kuhusu bei ya mahindi ambayo NFRA imeanza kununua mahindi kwa wakulima Zikankuba alisema ni wastani wa Sh 380 kwa kilo hadi Sh 400 kwa kilo kulingana na eneo na eneo, na ni bei inayoendana na mwenendo wa bei ya soko.

   “ Mfano bei ya soko ya mahindi mkoani Ruvuma ni Sh 250 kwa kilo, lakini sisi kama NFRA tunanunua kwa bei ya juu ya kuanzia Sh 350 hadi 380 kwa kilo," alisema. Aliongeza: “Mkoani Dodoma NFRA inanunua Sh  420 kwa kilo, Makambako Sh 400, Shinyanga Sh 500, Katavi na Ruvuma Sh 350 hadi 380. Bei hiyo bado ni ya juu ukilinganisha na bei ya soko iliyopo,” alifafanua.

  Aidha, Zikankuba alisema ziada ya mazao yote yaliyozalishwa na wakulima msimu huu imefikia tani milioni 2 huku ziada ya mahindi pekee ni tani 970,000.Zikankuba alisema NFRA imetengewa Sh bilioni 15 kwa ajili ya kununua tani 28,000 kwa awamu ya kwanza ikiwa ni asilimia 2 ya ziada ya mahindi iliyopo.

  Zikankuba alisisitiza kuwa NFRA inazingatia ubora wakati wa kununua kwa kuwa ni haki na muhitaji kupatiwa chakula bora na Salama kwa afya  wakati wa dharula hivyo mahindi ambayo hayana ubora yakituzwa kwa muda mrefu ghalani yanakuwa na nafasi kubwa kupata vimelea vya fangasi ambao husababisha uwepo wa sumu kuvu katika nafaka hiyo. 

  Alisema kuwa Sumu kuvu ni hatari sana kwa afya ya mlaji. Tatizo hili kwa kiasi kikubwa sana, linaweza kuepukika kwa mkulima kufuata mbinu bora za kilimo, mbinu bora za utayarishaji nafaka na mbinu bora za kuhifadhi nafaka baada ya kuvuna. Lengo la NFRA ni kutoa chakula chenye ubora na salama wakati wa dharula.
  Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Vumilia  Zikankuba

  0 0

  Naibu waziri wa Afya Harusi Said Suleiman (kushoto) akipokea msaada wa Vifaa mbalimbali ikiwemo Television kutoka Shirika la kuhudumia watoto Duniani (UNICEF) kwa Mwakilishi wa (UNICEF) Dkt. Maryam Seif Hemed vifaa hivyo vitatumika kutoa elimu na kuimarisha afya za kinamama na watoto.
  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakipatiwa maelezo na Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman baada ya kukabidhiwa Vifaa mbalimbali ikiwemo Television kutoka Shirika la kuhudumia watoto Duniani (UNICEF) huko Wizara ya Afya MmaziMmoja.
  Vifaa vitakavyotumika kwaajili ya matibabu katika Hospitali ya Mnazimmoja.
  Baadhi ya Vifaa vitakavyotumika kwaajili ya matibabu katika Hospitali ya Mnazimmoja. Picha Na Miza Othman – Maelezo Zanzibar.

  0 0

  0 0


  *Yaonya wanaozichezea ,yataka ziheshimiwe na kila mmoja wetu

  Na Said Mwishehe,Globu ya jamii


  BENKI Kuu ya Tanzania(BoT) imewataka Watanzania wote kuhakikisha wanatunza fedha zetu kwani ni mojawapo ya tunu na alama muhimu ya uchumi wa nchi yetu.

  Pia fedha ni alama ambayo inapaswa kuheshimwa kama zilivyo alama nyingine kwa mfano Bendera  ya Taifa. 

   Taarifa ya BoT kwa vyombo vya habar ambayo wameitoa leo inasema utunzaji mzuri wa fedha zetu utapunguza uwezekano wa fedha hizo kuchakaa mapema na kupunguza gharama za uchapishaji."Kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006, kifungu cha 26, BoT ndiyo taasisi pekee yenye mamlaka ya kutoa noti na sarafu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," imesema taarifa hiyo.

   Pia imesema noti na sarafu hizo zina alama muhimu inayolitambulisha taifa la Tanzania ambayo ni nembo ya Bwana na Bibi. Imefafanua alama hiyo inapaswa kuheshimwa kama zilivyo alama nyingine kwamfano Bendera 
  ya Taifa.

  Pia noti na sarafu zote zimetengenezwa kutoa thamani ya kisheria (legal 
  tender) kama ilivyoandikwa juu ya noti au sarafu husika na pia Benki Kuu pekee ndiyo yenye mamlaka ya kuharibu noti na sarafu.

  Taarifa hiyo imefafanua kuhusu hilo kupitia kifungu cha  28 kikisomwa pamoja na kifungu cha 30 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006."Benki Kuu inatoa rai kwa wananchi kuzitunza fedha zetu kwa kuwa ni mojawapo ya tunu na alama muhimu ya uchumi wa nchi yetu. 

  "Vilevile, utunzaji mzuri wa fedha zetu utapunguza uwezekano wa fedha hizo kuchakaa mapema na kupunguza gharama za uchapishaji," imesema taarifa hiyo ya BoT.Imesisitiza kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006, kifungu cha 26, Benki Kuu ya Tanzania ndiyo taasisi pekee yenye mamlaka ya kutoa noti na sarafu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

  Pamoja na mambo mengine imesisitiza umuhimu wa alama hiyo inapaswa kuheshimwa kama zilivyo alama nyingine kwamfano Bendera ya Taifa. Na kwamba Noti na sarafu zote zimetengenezwa kutoa thamani ya kisheria (legal tender) kama ilivyoandikwa juu ya noti au sarafu husika.

  "Na pia Benki Kuu pekee ndiyo yenye mamlaka ya kuharibu noti na sarafu (kifungu cha 28 kikisomwa pamoja na kifungu cha 30 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006) ," amesema.

  0 0


   Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi(UVCCM) Mkoani Tanga,Omari Mwanga akizungumza wakati wa  ghafla ya uzinduzi wa kambi ya Vijana wa chama hicho kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Muheza ambapo  mgeni rasmi Mbunge wa Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu alisema ushirikiano uliofanywa na vijana hao wa kushiriki katika mradi mkubwa kama huo ni jambo la kuigwa nchi nzima.
   Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) Mkoa Tanga Zawadi Nyambo akizungumza katika uzinduzi huo ambapo alisema mpango kazi wa miaka mitano 2017-2022 ambao uliwasilishwa katika Mkutano Mkuu wa UVCCM Mkoa ukiwa na lengo la kuanzisha makambi katika ngazi mbalimbali.
   Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akizungumza


   MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza katika uzinduzi huo
   Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Muheza Like Gugu akizungumza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza Balozi Adadi Rajabu na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Tanga Omari Mwanga kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
   Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Juliaus Mgeni akitoa taarifa ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo
  VIJANA wa UVCCM Mkoani Tanga wakiendelea na ujenzi
   Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu katikati akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Tanga Omari Mwanga
   MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akivalisha taji mara baada ya kuwasili kwenye kambi hiyo ya vijana
   MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu katikati akimaliza kukagua gwaride la vijana mara baada ya kuwasili eneo la mradi wa ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Muheza Lusanga kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoani Tanga Omari Mwanga
   MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu katikati akimsikiliza kwa umakini Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza Like Gugu
   MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu katikati akiwa na Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Tanga kulia Omari Mwanga wakiangalia lori lililoleta saruji kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza inayojengwa eneo la Lusanga
   MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu katika akiwa na Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Tanga Omari Mwanga wakipiga makofi wakati vijana wakiimba nyimbo mbalimbali
  UJENZI wa Hospitali ya wilaya ya Muheza mkoani Tanga umeanza kushika kasi baada ya vijana 300 wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoani Tanga kuungana kwa pamoja kuweka kambi maalumu kwa ajili ya kujitolea kwenye mradi huo.

  Vijana hao wa UVCCM Mkoani Tanga kutoka wilaya zote walianza kambi hiyo Septemba 10 mwaka huu eneo la Lusanga kunapojengwa hospitali hiyo walianza kujitolea na wataalamu katika utekelezaji wa mradi huo kwa awamu ya kwanza kujenga majengo ya utawala,wodi ya wanawake,wodi ya watoto,jengo la maabara,jengo la utakasaji vifaa na jengo la dharura ambayo yatagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 3.

  Akizungumza katika ghafla ya uzinduzi wa kambi hiyo mgeni rasmi Mbunge wa Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu alisema ushirikiano uliofanywa na vijana hao wa kushiriki katika mradi mkubwa kama huo ni jambo la kuigwa nchi nzima.

  Balozi Adadi alisema ipo miradi mingi ambayo inaendelea kutekelezwa katika Halmashauri mbalimbali na ikiwa watawatumia vijana hao wa chama ni wazi wanaweza kujengwa kiuzalendo zaidi na kusaidia kuharikishautekelezaji wake.

  Alisema atahakikisha vijana hao wanapatiwa vifaa muhimu vya kujikingapindi wawapo katika shughuli hiyo ya ujenzi na wanapatiwa chakula chakutosha na mahitaji mengine muhimu ili azma yao ya kuyafikisha majengo hayo uwasa wa lenta Sept 25 iweze kutimia.

  Kwa Upande wa Mkuu wa Wilaya Muheza Mhandisi Hajat Mwanasha Tumbo alisema azimio ni kupata Hospitali ya wilaya hivyo waliona vijana watumike ili kuwajengea uzalendo na kufanya hivyo Serikali inaweza
  kufikia malengo yake.

  Tumbo alisema jambo hilo liwe chachu kwa chama na Serikali kwenye azma ya kutatua kero za wananchi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo haitekelezwi kwa wakati na kusababisha wananchi kuendelea kuteseka.

  “Tunahaja ya kuwatumia vijana hawa sasa hasa katika miradi yetu ya kimaendeleo na si kuwaacha tu na tukifanya hivi tutakuwa tunawajenga kiuzalendo wa kujua chama chao na Serikali nini wanachokifanya kwa ajili ya wananchi wake”Alisema Tumbo.

  Kwa upande wake Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama hicho Mkoa Tanga Zawadi Nyambo alisema mpango kazi wa miaka mitano 2017-2022 ambao uliwasilishwa katika Mkutano Mkuu wa UVCCM Mkoa ukiwa na lengo la kuanzisha makambi katika ngazi mbalimbali.

  Nyambo alisema nguvu itakayotumika kupitia vijana hao ipo imani kubwa ya kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho kitatumika katika shughuli zingine za maendeleo ya kijamii na kuieleza jamii umoja wa vijana hao sio siasa pekee bali ni pamoja na ujenzi wa Taifa.

  Katibu huyo alisema wameazimia kuwatumia vijana kuwajenga katika suala zima la uzalendo kama nguvu kazi katika miradi mbalimbali inayoanzishwa na Serikali”Alisema.

  Awali akisoma taarifa fupi mbele ya mgeni rasmi Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Juliaus Mgeni alisema Wilaya hiyo tangu ianzishwe miaka 45 iliyopita haina Hospitali ya Wilaya na kuitegemea Hospitali 1 ya Teule inayomilikiwa na Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga.

  Alisema Hospitali inazidiwa uwezo kwa sasa mabpo uwezo wake ni kuhudiumia watu 1,500 kwa siku hivyo huduma za rufaa ikijumuisha wagonjwa wenye hali mbaya za kiafya toka vituo vya huduma za msingi wanalazimka kusafirihwa umbali wa km 72 hadi Hospitali ya Rufaa ya Bombo Mkoani Tanga.

  Mgeni alisema Hospitali hiyo inatarajiwa kugharimu kiasi cha zaidi ya shili bilini 11 hadi kumalizika kwake ambapo unategemewa kutekelezwa kwa kipindi cha mika mitatu kuanzia 2017/18 -2019/2020 na itategemea upatikanaji wa fedha

  0 0

   Muonekano wa njia ya juu (flyover) katika makutano ya barabara za Nyerere na Mandela eneo la TAZARA jijini Dar es salaam baada ya magari kuruhusiwa kupita juu yake.Kufunguliwa kwa flyover hio kumepunguza adha ya foleni kwa kiwango kikubwa kiasi ya kwamba safari kutoka katikati ya jiji hadi uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere hivi sasa huchukua si zaidi ya nusu saa badala ya masaa mawili au matatu ya awali. Picha na Muhidin Issa Michuzi
   
   
   
  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda jana  amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya Barabara na Madaraja inayotekelezwa na Serikali kwenye Wilaya ya Kigamboni ambapo kukamilika kwake kutafanya mji wa kigamboni kuwa wa kisasa zaidi.

  Miongoni mwa miradi iliyotembelewa na RC Makonda ni ujenzi wa Barabara ya njia sita za magari kuelekea Daraja la Mwalimu Nyerere yenye urefu wa Km 2 pamoja Mzunguko wa Magari (Round about) yenye ukubwa wa Meter 250 kuelekea Feri Meter 250 kuelekea Kibada ambayo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika October 31 mwaka huu.

  Aidha RC Makonda ametembelea ujenzi wa Barabara ya KKKT na mitaro ya maji yenye urefu wa Mita 275, Barabara ya Hospital ya Vijibweni Mita 800 kutoka Kibada,Barabara ya Kijaka-Mwasonga Km 8, Mwasonga-Kibada Km 16 Kimbiji-Pembamnazi, Daraja la Puna eneo la Buyuni na Daraja la Kibugumo Kata ya Gezaulole ambapo miradi hiyo ipo hatua za mwisho kukamilika. 

  RC Makonda ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo na kuwahimiza TANROAD na TARURA kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati ili wananchi waendelee kufurahia matunda ya serikali ya awamu ya tano.

  Pamoja na hayo RC Makonda amesema wamejidhatiti kuhakikisha Kigamboni inakuwa na Barabara za Lami, Maji ya kutosha na Umeme kwaajili ya Viwanda, Makazi na Showroom kubwa Africa Mashariki na Kati.

  TULIAHIDI NA TUNATEKELEZA.
   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza leo na waandishi wa habari juu ya kuwahimiza Tanroad na Tarura kukamisha miradi kwa wakati katika wilaya ya Kigamboni.
   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akisikiloza kero za wananchi wa wilaya ya Kigamboni leo katika ziara ya kukagua miradi ya barabara katika wilaya hiyo.(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akiwa ameambata na viongizi mbalimbali wakikagua miradi mbalimbali  katika  wilaya  ya Kigamboni.
   Mafundi wakiendelea na kazi.
  Muonekano wa maadhi ya madaraja yanayojengwa katika wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.

  0 0


  Na Veronica Simba – Mara
  Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema Serikali kupitia Wizara anayoisimamia, imejipanga kuhakikisha wawekezaji wote katika sekta ya madini wanatumia umeme katika shughuli zao ili wazalishe kwa tija itakayowawezesha kulipa kodi stahiki kwa Taifa na hivyo kukuza uchumi wa nchi. 

  Alitoa kauli hiyo, Septemba 18, 2018 mkoani Mara, wakati akizungumza na Mkuu wa Mkoa Adam Malima ofisini kwake, kabla ya kuanza ziara ya kazi katika Mkoa huo, kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme.

  “Tunataka migodi izalishe kwa tija ili kusudi ilipe kodi, ushuru na tozo zote stahiki kwa Serikali hivyo kukuza uchumi wa nchi yetu.”

  Kauli hiyo ya Waziri Kalemani, aliitoa kufuatia ombi la Mkuu wa Mkoa kuhusu kuupatia nishati ya umeme Mgodi wa Dhahabu wa Nyamongo uliopo mkoani humo; ambapo Waziri Kalemani alimhakikishia kuwa Wizara yake inakamilisha taratibu za kuunganisha umeme katika Mgodi huo ndani ya muda mfupi, baada ya mwekezaji huyo kukamilisha malipo.

  Alisema kuwa, tayari alishamwagiza Meneja wa TANESCO wa Mkoa wa Mara, Mhandisi Emmanuel Kachewa kuhakikisha Mgodi huo unaunganishiwa umeme kabla ya mwezi huu kuisha.

  Waziri Kalemani alisema kuwa kwa muda mrefu, wengi wa wawekezaji katika sekta ya madini wamekuwa wakitumia mafuta katika kuendesha mitambo hiyo hivyo kulalamika kwamba wanatumia gharama kubwa inayowasababishia hasara katika uzalishaji hivyo kushindwa kulipa kodi stahiki za Serikali kadri ipasavyo.

  Alifafanua kuwa, ni kwa sababu hiyo, Serikali imedhamiria na ilikwishaanza kutekeleza mpango wa kuhakikisha wawekezaji wote wa sekta husika, wakiwemo wakubwa, wa – kati na hata wadogo wanatumia umeme ili kuondoa visingizio vya kuendesha shughuli zao kwa hasara na hivyo kutokulipa kodi ipasavyo.

  Katika hatua nyingine, Waziri Kalemani ametoa wito kwa taasisi zote zinazodaiwa na TANESCO, kuendelea kulipa madeni yao ili kuliwezesha shirika hilo la umma kuwahudumia watanzania kwa viwango na ubora.

  “TANESCO isipolipwa madeni inayozidai taasisi na hata wateja binafsi, inapata shida kuwahudumia wateja wake ambao ni Watanzania. Kwahiyo, tunahamasisha wote ambao bado hawajalipa Ankara za umeme kuendelea kulipa ili kuipunguzia Serikali mzigo,” alisisitiza.

  Katika ziara hiyo, Waziri Kalemani alitembelea maeneo mbalimbali ambapo aliwasha umeme katika vijiji vya Nyakatende, Musoma Vijijini na Bubombi kilichopo Wilaya ya Rorya pamoja na kuzungumza na wananchi. 

  Aidha, alitembelea kijiji cha Nyamohonda kilichopo wilayani Tarime, mpakani mwa Tanzania na Kenya na kuwaahidi wananchi kuwa watapata huduma ya umeme hivi karibuni kwani tayari kazi hiyo imekwishaanza kutekelezwa.

  Awali, akiwasilisha kwa Waziri taarifa ya utekelezaji wa miradi ya umeme katika eneo lake, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Mara, Mhandisi Emmanuel Kachewa alisema kuwa jumla ya vijiji 273 vitapatiwa umeme kupitia Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu, Sehemu ya Kwanza (REA III – Phase 1), ambao umekwishaanza kutekelezwa na unatarajiwa kukamilika ifikapo Juni, 2019.
   Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (kulia), akimweleza jambo Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, muda mfupi kabla ya Waziri kuanza ziara yake mkoani humo kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme na kuzungumza na wananchi, Septemba 18, 2019.
   Mwonekano wa nyumba ya mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Nyakatende, Wilaya ya Musoma Vijijini, muda mfupi kabla ya Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani kuiwashia umeme ikiwa ni ishara ya uwashaji rasmi wa huduma ya nishati hiyo katika eneo hilo. Tukio hilo lilifanyika 18, 2019.
   Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwasha umeme katika nyumba ya mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Nyakatende, Musoma Vijijini, ikiwa ni ishara ya uwashaji rasmi wa nishati hiyo katika eneo hilo. Waziri alikuwa katika ziara ya kazi mkoani humo, Septemba 18, 2018 kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme.
  Meneja wa TANESCO Mkoa wa Mara, Mhandisi Emmanuel Kachewa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya umeme mkoani humo, kwa Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani), alipowasili katika Mkoa huo kwa ajili ya ziara ya kazi Septemba 18, 2018.
   Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kulia), akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Bubombi, Wilaya ya Rorya mkoani Mara, muda mfupi kabla ya kuwasha rasmi umeme katika eneo hilo. Hafla hiyo ilifanyika Septemba 18, 2018.
   Sehemu ya umati wa wananchi wa Kijiji cha Nyakatende, Musoma Vijijini wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), alipokuwa akizungumza nao wakati wa hafla ya uwashaji rasmi umeme katika eneo hilo, Septemba 18, 2018.
  Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, akisalimiana na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mara, alipowasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Septemba 18, 2018 muda mfupi kabla ya kuanza ziara ya kazi mkoani humo kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme.                     

  0 0

  Na Veronica Kazimoto-Tanga

  Wafanyabiashara mkoani Tanga wameelimishwa kuhusu Msamaha wa Riba na Adhabu ya Malimbikizo ya Madeni ya Kodi, Mabadiliko ya Sheria za Kodi ya Mwaka 2018 na Mfumo wa Maadili wa Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kuwawezesha wafanyabiashara hao kujua kwa undani masuala yanayohusu kodi pamoja na kuwahi kuomba msamaha wa riba na adhabu ambapo mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30 Novemba, 2018.

  Akifungua semina ya wafanyabiashara hao mkoani hapa iliyoandaliwa na TRA, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Monica Kinara amesema kuwa, elimu hiyo imekuja wakati muafaka na siyo tu itawasaidia kujua masuala ya kodi bali wale wenye malimbikizo ya madeni ya kodi watanufaika na msamaha huo na hatimaye wataweza kulipa kodi kwa wakati.

  "Ninawashukuru sana TRA kwa kuleta elimu hii hapa mkoani kwetu na ni matumaini yangu kuwa, wafanyabiashara mtatumia fursa hii vizuri ili iwasaidie kuelewa masuala mbalimbali yanayohusu kodi na hasa msamaha wa riba na adhabu ya kodi ili muweze kuomba msamaha huo ndani ya muda uliopangwa," alisema Kinara.

  Naye, Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA Makao Makuu Diana Masalla amewaeleza wafanyabiashara hao kwamba, ni jukumu la kila mwenye malimbikizo ya madeni ya kodi kuwahi kuomba msamaha wa riba na adhabu akiwa ameambatisha dodoso maalum la msamaha huo pamoja na ritani ya taarifa za Mlipakodi.

  "Huu ni msamaha maalumu hivyo ni muhimu mzingatie kutuma maombi kabla ya tarehe 30 Novemba mwaka huu, kinyume na hapa mtaikosa fursa hii muhimu ambayo ina lengo la kuwapunguzia mzigo wa kodi," alisisitiza Masalla.Kwa upande wake Mfanyabiashara wa Nyumba za Kulala Wageni Teti Mathias ameshukuru ujio wa elimu hii mkoani Tanga na kuiomba TRA iwe na utamaduni wa kutoa elimu hizi katika ngazi ya Kata na Tarafa ili wafanyabiashara wengi waweze kupata uelewa wa kutosha kuhusu masuala mbalimbali ya kodi.

  Msamaha maalum wa Riba na Adhabu kwenye Malimbikizo ya Madeni ya kodi unatolewa kwa asilimia 100 kwa wafanyabiashara wenye malimbikizo hayo ambao watakidhi vigezo vilivyowekwa katika utaratibu wa kuomba msamaha huo.
   Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga Masawa Masatu akizungumza wakati wa semina ya wafanyabiashara  iliyofanyika  jijini Tanga kwa lengo la kutoa elimu ya Msamaha wa Riba na Adhabu ya Malimbikizo ya Madeni ya Kodi, Mabadiliko ya Sheria za Kodi ya Mwaka 2018 pamoja na Maadili ambapo takribani wafanyabiashara 150 wamehudhuria semina hiyo.
   Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Monica Kinara akizungumza wakati wa semina ya wafanyabiashara iliyofanyika  jijini Tanga kwa lengo la kutoa elimu ya Msamaha wa Riba na Adhabu ya Malimbikizo ya Madeni ya Kodi, Mabadiliko ya Sheria za Kodi ya Mwaka 2018 pamoja na Maadili ambapo takribani wafanyabiashara 150 wamehudhuria semina hiyo.
   Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi Diana Masalla kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu akiwasilisha mada kuhusu Mabadiliko ya Sheria za Kodi wakati wa semina ya wafanyabiashara iliyofanyika  jijini Tanga kwa lengo la kutoa elimu ya Msamaha wa Riba na Adhabu ya Malimbikizo ya Madeni ya Kodi, Mabadiliko ya Sheria za Kodi ya Mwaka 2018 pamoja na Maadili ambapo takribani wafanyabiashara 150 wamehudhuria semina hiyo.
   Afisa Maadili Mwandamizi Adelaida Rweikiza kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu akiwasilisha mada kuhusu Mfumo wa Maadili wa Watumishi wa TRA wakati wa semina ya wafanyabiashara iliyofanyika  jijini Tanga kwa lengo la kutoa elimu ya Msamaha wa Riba na Adhabu ya Malimbikizo ya Madeni ya Kodi, Mabadiliko ya Sheria za Kodi ya Mwaka 2018 pamoja na Maadili ambapo takribani wafanyabiashara 150 wamehudhuria semina hiyo.
  Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) jijini Tanga kwa lengo la kutoa elimu ya Msamaha wa Riba na Adhabu ya Malimbikizo ya Madeni ya Kodi, Mabadiliko ya Sheria za Kodi ya Mwaka 2018 pamoja na Maadili ambapo takribani wafanyabiashara 150 wamehudhuria semina hiyo. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa ya Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bwana William Erio amefanya mazungumzo na Menejimenti ya baadhi ya Taasisi tatu za Kibenki hapa nchini ambazo ni NMB,CRDB na UBA kwa lengo la kuendeleza na kukuza mahusiano ya kibiashara. 

  Katika mkutano huo wameweza kuzungumza masuala mbali mbali yanayolenga kuimarisha ushirikiano utakaowezesha kukuza maendeleo katika sekta ya uchumi kupitia Benki zao na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF. 

  Wakurugenzi wakuu hao ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bwana Charles Kimei,Bwana Usman Imam Isiaka Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya UBA pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker.
   Wa kwanza pichani kulia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ,Bwana William Erio  akiwa kwenye mazungumzo na Menejimenti ya  Benki ya CRDB ofisini kwake makao makuu jijini DSM ambapo wameweza kuzungumza masuala mbali mbali ya kuimairisha mahusiano baina yao.
   Viongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na viongozi wa Benki ya CRDB wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao  kwenye makao makuu ya NSSF ,katikati Mkurugenzi mkuu wa NSSF Bwana William Erio na pembeni yake ni mkurugenzi mkuu wa CRDB Charles Kimei na pembeni ni viongozi mbalimbali  wa CRDB na NSSF.
   Mkurugenzi Mkuu  wa Benki ya UBA ,Bwana Usman Imam Isiaka akielezea jambo wakati wa mazungmzo yake na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)  Bwana William Erio leo katika makao makuu ya NSSF jijini Dar es salaam.
  Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya NMB Bi.Ineke Bussemaker akipongezana na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bwana William Erio (Kulia) mara baada ya kumalizika kwa  mazungumzo baina yao ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni  Bwana Miichael Mungure amabaye ni MKuu wa kitengo cha akaunti na malipo(NMB), wa kwanza kulia ni Richard Mtapa ambaye ni Meneja Mwandamizi wa Taasisi za Serikali(NMB)

  0 0

  Afisa Masoko na uhusiano wa UTT AMIS Ndg.Waziri Ramadhani akitoa elimu kwa wastaafu watarajiwa kutoka taasisi mbalimbali katika semina iliyo andaliwa na TAGLA katika ukumbi wa JKT Umwema-Morogoro

  Afisa Masoko na uhusiano wa UTT AMIS Ndg.Waziri Ramadhani akitoa elimu kwa wastaafu watarajiwa kutoka taasisi mbalimbali katika semina iliyo andaliwa na TAGLA katika ukumbi wa JKT Umwema-Morogoro

  Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo.

  Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo.

  Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo.


  0 0


  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Kituocha Amani (Amani Center for Street Children ) Meindert Schaap akizungumza wakati wa mahafali ya 12 ya wanafunzi wa Darasa la Saba waliokolewa na kituo hicho kutoka mitaani.


  Mgeni rasmi katika Mahafali hayo ,Mratibu wa Elimu kata ya Karanga,Mercy Mandia akikabidhi zawadi kwa baadhi ya Wanafunzi walihitimu Darasa la Saba waliooklewa kutoka Mitaani na kupata msaada wa Elimu kutoka katika kituo hicho.
  Mzazi Mwakilishi wa watoto wanaolelewa katika kituo hicho ,Editha Cyril akitoa neon la shukrani kwa msaada mkubwa uliotolewa kwa watoto hao.


  Mtoto Getrude Salutary ,mmoja wa Wahitimu wa Darasa la Saba waliokuwa wakilelewa katika kituo hicho akisoma Risalambele ya mgeni rasmi,kushoto kwake ni mwanafunzi mwenzake ,Michael Salutary.


  Kikundi cha Vijana wa Sarakasi wakionyesha umahiri katika mahafali hayo.
  Watoto wanaolelewa katika kituo hicho wakionesha vipaji vyao katika uchezaji wa Muziki.
  Watato hao wakionesha umahiri katika uchezaji wa ngoma za Asili.  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.


  WATOTO 1,200 waliokuwa wakiishi katika mazingra hatarishi mitaani wameokolewa na shirika lisilo la kiserikali la Amani (Amani Center for street Children) na kusaidia upatikanaji wa elimu kwa watoto hao na baadae kuwaunganisha na familia zao.

  Watoto waliookolewa wakiwa katika umri tofati tofauti ,walichukuliwa na kituo cha Amani kutoka katika mitaa ya mikoa ya Singida,Moshi na Arusha ambapo mwaka huu watoto 31 kati ya kundi hilo wamehitimu elimu ya msingi baada ya kupata msaada wa kituo hicho.

  Akizungumza wakati wa mahafali ya 12 ya kuwaaga wanafunzi hao ,Mratibu wa Elimu wa kituo cha Amani Brenda Mzava alisema licha ya kuwaunganisha familia zao baada ya kuwalea watoto hao kwa muda mrefu, kituo bado kinaendelea kuwafuatilia na kuwasaidia hadi hapo watakapoweza kujiendeleza.

  “Kama baadhi yetu tunavyojua watoto hawa walikuwa kwenye mazingira hatarishi na magumu ya mtaani kabla ya kuokoloewa na shirika la Amani, kwa kuwatoa mtaani,kuwapatia huduma na haki za msingi ikiwemo huduma za afya na elimu bora, siyo kazi rahisi hususani kwa motto aliyekuwa mtaani kwa muda mrefu.”alisema Mzava.

  “Kazi hii haikuwa rahisi lakini kwa ushirikiano wa jamii pamoja na serikali hususani Manispaa ya Moshi kupitia shule ya Msingi Shirmatunda na Magereza jambo hili limewezekana hatimaye watoto 31 waliokuwa mtaani wamefanikiwa kuhitimu elimu ya msingi.”aliongeza Mzava.

  Alisema kama shirika wanajivunia watoto hao kwa kuweza kuhitimu elimu yao ya msingi na kuwa ni mafanikio makubwa kwa shirika naTaifa kwa ujumla na kwamba ushirikiano uliopo kati ya shirika la Amani ,jamii na taasisi za Serikali ni wa pekee kwani unaogozwa na uwito pamoja na kujitolea.

  “Kwa namna moja au nyingine tumewawezasha watoto hawa waliohitimu darasa la saba na wale tunaondelea kuwalea katika kituochetu kujenga msingi mzuri wa maisha yao ya baadaye kielimu.”alisema Mzava.

  Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Mratibu wa Elimu kata ya Karanga Mercy Mandia alilipongeza Shirika la Amani kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuwaokoa watoto toka kwenye mazingira hatarishi ya mtaani kisha kuwaweka sehemu salama na kuwapatia huduma za msingi ikiwemo Elimu.

  ”Niwapongeze shirika la Amani kwa kazi nzuri kwa kufanya watoto tunaoita wa mitaani kuwa watoto tena hasa kwa kuwapatia huduma za msingi kama malazi ,Chakula ,huduma za Afya,Elimu pamoja na mchakato mzima wa kuwarudisha kwenye jamii,”alisema Mandia.

  “Nijitihada nzuri naomba kuahidi serikali kuanzia ngazi ya Mtaa,Kata,Manispaa pamoja na Mkoa kwa ujumla tutafanya kazi bega kwa bega kuhakikisha kazi hii inafanikiwa kwa kiasi kikubwa”aliongeza Mandia.

  Mandia alitoa pongezi kwa Mkurugenzi wa kituo hicho ,Meindert Schaap pamoja na wafanayakazi wote kwa kazi nzuri wanaoifanya yakufundisha ,kutunza,na kulea kiroho na kimwili watoto hao na kwamba Mungu ataibariki kazi hiyo na kukumbuka jitihada za kituo hicho.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo cha Amani ,Meindert Schaap alisema ni faraja kubwa kuona idadi kubwa ya watoto waliotoka mitaani wanaelekea kwenye mafanikio makubwa hasa baada ya baadhi yao kuhitimu elimu ya Msingi.

  Akizungumza kwa niaba ya wahitimu wenzake , Joyce Faustine Ngada aliyekuwa akisoma shule ya msingi Magereza alikishukuru kituo cha Amani kwa kuwaokoa kutoka mazingira hatarishi ya mtaani na kuwaleta kituoni ambapo wamefanikiwa kupata huduma mbalimbali za msingi ikiwemo Elimu.

  “Mimi nilichukuliwa nyumbani Bukoba na kuja kufanya kazi za ndani Moshi,baada ya kufika Moshi nilijikuta nafanya kazi tofauti ya ile niliyo ahidiwa wakati natoka nyumbani kwani nilijikuta nafanya kazi ya Baa”alisema Joyce.

  Alisema kupitia muelimishaji mtaani wa Amani (Street Educator) alifanya nae mahojiano na kwamba awali alikuwa akimdanganya lakini nilipogundua anania njema ya kutaka kumuokoa alitoa ushirikiano na kuweza kutoka kwenye kazi ya kuuza Baa na kupelekwa katika kituo cha Shirika la Amani .

  Amani Centre for Street Children ni shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa mwaka 2001 na kusajiliwa baada ya kupewa namba NGO/0766 likifanya kazi ya kuwaokoa watoto wanaoishi mtaani kwa muda wote,katika miji ya Moshi,Arusha na Singida.

  0 0


  Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

  UVUVI na uuzaji wa samaki katika soko la Feri jijini Dar es salaam umezidi kuimarika katika mchakato mzima wa uvuvi wa samaki wenye viwango vinavyotakiwa na uuzwaji wake sokoni umekuwa na tija.

  Akizungumza na blogu ya jamii Kaimu Afisa Uvuvi wa soko la Feri Ahmed Mbarouk ameeleza kuwa upatikanaji wa samaki kwa sasa ni mzuri hasa kwa samaki wakubwa  na hata mauzo yamekuwa mazuri pia kutokana na ubora wa samaki wanaovuliwa kuwa na viwango.

  Kuhusiana na kutokomeza uvuvi haramu Abdallah ameeleza kuwa kwa sasa hakuna matukio hayo ya wavuvi kutumia baruti kuvua samaki na hii ni baada ya kampeni waliyoiendesha na kufanikisha kukamatwa kwa nyavu haramu kubwa 14 aina ya kokoro ambazo ziliteketezwa.

  Akieleza changamoto wanazokabiliana nazo kiutendaji Afisa uvuvi huyo amesema kuwa vifaa vya kazi hasa boti la doria limekosekana hali inayowapelekea kufanya doria kwa miguu licha ya kuwa na askari wa Suma JKT wanaosaidia na kueleza kuwa boti hilo likipatikana litawarahisishia kazi ya kufanya doria nyakati zote na kwa uhuru zaidi.

  Aidha ametoa wito kwa  kwa wavuvi kwa kuvua samaki wenye viwango vinavyofaa na doria hizo ni endelevu hivyo wavuvi wafuate kanuni na taratibu.

  Mmoja wa wavuvi hao Jumanne Ramadhani amesema kuwa wanaushukuru uongozi wa soko hilo hasa maafisa uvuvi kwa kuwapa elimu na kuwasimamia kwani hadi sasa wanajua viwango vya samaki wanaotakiwa kuvuliwa na kupelekwa sokoni na kwa sasa biashara ni nzuri kwani upatikaji wa samaki hasa wakubwa umekuwa mkubwa na soko kwa ujumla limesimama imara.
   . Afisa uvuvi  Msaidizi katika soko la samaki Feri Ahmed Mbarouk akizungumza na blogu ya jamii kuhusiana na hali ya uvuvi na biashara ya samaki sokoni hapo.
   Samaki wakiwa tayari kwa mauzo ambapo samaki mmoja huuzwa kati ya shilingi 45,000 hadi 50,000.(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)
   Mnada wa samaki ukiendelea katika soko la samaki la Feri jijini Dar es Salaam.

  Mwandishi kutoka Michuzi blog akiangalia samaki aina ya kaa mara baada ya kuvuliwa na mmoja wa wavuvi.(Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)

  0 0

  Vyama vya siasa hapa Nchini vimetakiwa kudumisha na kuimarisha demokrasia ndani ya vyama vyao ili viweze kutekeleza majukumu yao kama taasisi imara tofauti na mawazo ya walio wengi kuwa vyama hivyo sio imara kiasi cha kufananishwa na vikundi vidogo vidogo katika Jamii kama vile Saccos.

  Hayo yalisemwa na Msajili wa vyama vya siasa hapa Nchini Jaji Francis Mutungi wakati wa ufunguzi wa kikao kazi na Viongozi wa Kitaifa wa vyama vya siasa kinachoendelea leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuvijengea vyama uwezo wa masuala ya rasimali fedha na rejista ya chama ili viweze kujiendesha kama taasisi.

  Jaji Mtungi aliviambia vyama vya siasa kuwa ni muhimu kujenga vyama kama taasisi imara kwani mtu yeyote kutoka nje anayeitaji kuwekeza katika vyama hawezi kuwekeza katika chama ikiwa chama husika kitakuwa na hati chafu kutoka Ofisi yaMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

  ‘’Mafunzo ya rasimali fedha na regista ya vyama kama vile mali za vyama ni muhimu kwasababu pamoja na vyama kupatiwa mafunzo haya ni vyema mkatambua kuwa vianawajibika kwa wananchi katika suala zima la utendaji wa ndio maana msajili analazimika kufanya ukaguzi katika vyama’’Alisema Jaji Mtungi.

  Aidha Jaji Mtungi aliwaambia wawakilishi wa vyama vya siasa kuwa elimu ya fedha na regista ya chama ni muhimu kwasababu pia zoezi hili linasaidia sana kupunguza migogoro ndani ya vyama vya siasa.

  Wakati huo huo Makamu Mkuu Mstaafu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mkandala ambaye aliwasilisha mada ya Jinsi ya Kuendesha chama kama taasisi,amesema lengo la chama cha siasa chochote ni kujiandaa kushika madaraka au kuwa wapinzani wa serikali hivyo lazima kuhakikisha vinajijenga kama taasisi inayoaminika kwa wananchi.

  Profesa Mkandala amesema siasa vyama vingi hapa Nchini ni matokeo ya ukoloni mamboleo ambao ulianza kushamiri hapa nchini kwa miaka 1990 ambapo nchi ya Tanzania kama zilivyo nchi nyingine Barani Afrika zilikumbwa na mabadiliko ya kiuchumi ya soko huria ikiwemo nchi zilizokuwa za ujamaa kuanza kufuata m asharti ya Shirika la Fedha Duniani IMF.

  Aidha Profesa Mkandala alitaja vigezo vinavyofanya chama kuwa Taasisi muhimu kuwa ni Itikadi, Uongozi bora, Wanachama, Sera na programu za chama, Rasilimali
  Msajili wa vyama vya siasa,Jaji Francis Mutungi akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa kuhusu kudumisha na kuimarisha demokrasia ndani ya vyama vyao leo jijini Dar es Salaam.
  Msajili msaidizi bw. Sisty l.Nyahoza akizungumza na viongizi wa vyama vya siasa katika semina ya siku mbili leo jijini Dar es Salaam.
  Makamu Mkuu Mstaafu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mkandala akizungumza na viongizi wa vyama vya siasa kuhusu jinsi ya kujiendesha chama kama taasisi.

  Semmu ya viongizi wa vyama vya siasa wakiwa katika sema hiyo

  0 0

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) Mwl Raymond Mwangwala akimpa pole mdogo wa marehemu John Guninita Ndg Gerald John Guninita alipowasili nyumbani kwao Ifakara Wilaya ya kilombero.
   Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) Mwl Raymond Mwangwala wakati akiwasili nyumbani kwao marehemu pamoja na mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro Ndg  Innocent Karogelesi.
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) Mwl Raymond Mwangwala akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro Ndg Innocent Karogelesi
  Waombolezaji wakiandamana kutangulia mbele wakati mwili wa Marehemu John Guninita ulipokuwa ukipelekwa eneo la kusaliwa wakati wa mazishi hayo
  Muombolezaji Wakilia kwa uchungu wakati wa mazishi ya marehemu John Guninita  Vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu John Guninita kulipeleka kwenye eneo la kusaliwa wakati wa mazishi hayo
  Mwili wa Marehemu ukiwa umepakizwa kwenye gari kwa ajili ya kupelekwa eneo la ibada
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) Mwl Raymond Mwangwala akitoa mkono wa pole kwa mdogo wa marehemu John Guninita Ndg Gerald John Guninita alipowasili nyumbani kwao Ifakara Wilaya ya kilombero.
  Jeneza Lililobeba Mwili wa Marehemu Ndg John Guninita likiwekwa ndani ya Kaburi na Waombolezaji |(Picha Zote Na Fahadi Siraji Wa UVCCM)

  0 0   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametoa miezi minne kwa waajiri wa Makampuni na Mashirika kuhakikisha wanawaajiri watu wenye ulemavu Kama Sheria ya Walemavu ya 2010 na Mikataba ya kimataifa ya mwaka 2006 iliyoridhiwa na Tanzania mwaka 2009 sura ya 27 unavyowaaagiza kufanya hivyo.

  RC Makonda amesema ifikapo Mwezi January mwakani ataanza ziara ya kutembelea kwenye kila kampuni na taasisi jijini humo kukagua Kama wametekeleza sheria na agizo hilo ambapo watakaobainika kukaidi watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
  1
  Aidha RC Makonda amesema kitendo cha kuwaajiri walemavu itapunguza ongezeko la ombaomba,ukatili, utupwaji wa watoto wenye ulemavu, kuhamasisha walemavu kusoma pamoja na kuwawezesha walemavu kuhudumia familia zao.
  “Hatuwezi kuwa na ndugu zetu wamesoma na wanasifa za kupata Kazi lakini tunawanyima matokeo yake wengine wanaishia kujinyonga, kinamama wanatupa Watoto wenye ulemavu, mila potovu zinaendelea kupoteza haki na mwisho wanabaki wakiwa Masikini na kushindwa hata kumudu gharama za Matibabu, Jambo hili sio la kufumbia macho” alisema Makonda
  2
  Kwa mujibu wa Sheria ya ajira kwa watu wenye ulemavu No. 9 ya mwaka 2010 kifungu cha 31 inamtaka kila mwajiri mwenye wafanyakazi zaidi ya 20 kuhakikisha 3% ya wafanyakazi ni watu wenye ulemavu.

  RAIS MAGUFULI AMEONYESHA DIRA KWA KUTOA KIPAOMBELE CHA AJIRA KWA WALEMAVU, NI WAKATI SASA KWA WAAJIRI KUTEKELEZA SHERIA.

older | 1 | .... | 1673 | 1674 | (Page 1675) | 1676 | 1677 | .... | 1896 | newer